Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 20 | 21 | (Page 22) | 23 | 24 | .... | 1904 | newer

  0 0


  Afisa Mawasiliano wa Kampuni ya magari ya Be Forward Tanzania, Mashariki na Kati Oliver Philbert akizungumzia kuzinduliwa rasmi kwa Kampuni ya Be Forward hapa Tanzania na pia tukio la kampuni hiyo kukabidhi zawadi kubwa ya gari kwa mmoja wa wateja wake kutoka Uganda aliyeibuka mshindi wa shindano la photo contest..

  Amesema Be Forward ni kampuni inayojihusisha na uuzaji magari nchini Japan kwa njia ya mtandao wa Internet, na ili kuongeza ufanisi na Imani kwa wateja wetu tumefungua kampuni Tanzania ambayo inajishughulisha na huduma kwa wateja. Be forward Tanzania itatengeneza ajira zaidi ya 1,000 kwa watanzania hivyo kuipunguzia mzigo serikali na kuongeza kipato kwa watanzania.

  Kampuni hiyo iliendesha ‘Photo Contest’ ambapo wateja wake walitakiwa kutuma picha za magari walionunua kutoka katika kampuni hiyo, na kisha ziliwekwa katika mtandao wa Be Forward na katika ‘Kurasa yao ya Facebook na watu kuzi’like’.

  Rais wa kampuni ya Be Forward kutoka Japan Bw. Hironori Yamakawa akimkabidhi mfano wa funguo ya gari Mshindi wa shindano la gari lililoendeshwa na kampuni ya Be Forward Bw. Kakuru Adnan (kushoto).

  Mshindi wa shindano la gari lililoendeshwa na kampuni ya Be Forward Bw. Kakuru Adnan akitoa shukrani kwa washiriki wote wa nchi mbalimbali walioshiriki na hatimaye yeye kuwa mshindi na pia kampuni ya Be Forward kwa kubuni shindano la “photo Contest’ na kuwataka wananchi wa Afrika Mashariki hasa Tanzania ambapo kampuni ndio imefunguliwa wasisite kujitokeza na kufika kwenye ofisi zao kujipatia huduma.

  Hili ndio gari aina ya Toyota Corolla alilozawadiwa mshindi huyo Bw. Kakuru Adnan.

  Rais wa kampuni ya Be Forward kutoka Japan Bw. Hironori Yamakawa akizungumza machache ambapo amewataka watanzania kujisikia huru kufika na kufanya kazi na kampuni hiyo, pia amempongeza mteja wao kutoka Uganda aliyeibuka kuwa mshindi wa zawadi ya gari na kuahidi kuwa wanafanya maandalizi ya kuendesha kitu kingine tena kwa ajili ya wateja wao..

  Rais wa kampuni ya Be Forward kutoka Japan Bw. Hironori Yamakawa ( wa pili kulia) na baadhi ya wageni waalikwa wakimsikiliza mshindi wa shindano hilo Bw. Kakuru Adnan (hayupo pichani) wakati wakati akitoa shukrani zake kwa kampuni hiyo.
  Pichani Juu na Chini ni Rais wa kampuni ya Be Forward kutoka Japan Bw. Hironori Yamakawa akikabidhi zawadi kwa wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo.

  Rais wa kampuni ya Be Forward kutoka Japan Bw. Hironori Yamakawa (wa pili kushoto waliochuchuma) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kampuni hiyo ofisi ya Tanzania na wageni waalikwa.

  Rais wa kampuni ya Be Forward kutoka Japan Bw. Hironori Yamakawa akimkabidhi rasmi mshindi wa shindano la picha ambaye pia ni mteja wa kampuni hiyo gari aina ya Toyota Corolla Bw. Kakuru Adnan kutoka nchini Uganda.

  Mshindi wa shindano la gari lililoendeshwa na kampuni ya Be Forward Bw. Kakuru Adnan akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Kampuni hiyo pamoja na baadhi ya wakuu wa vitengo na idara mbalimbali za kampuni hiyo kutoka nchini Japan.

  Rais wa kampuni ya Be Forward kutoka Japan Bw. Hironori Yamakawa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa kampuni hiyo ofisi za Tanzania na wa makao makuu nchini Japan.

  Bw. Kakuru Adnan akitoa tabasamu bashasha baada ya kuliwasha gari hilo.


  Bw. Kakuru Adnan akiondoka na gari lake alilojishindia tayari kuanza safari ya kurudi nchini Uganda. Hafla hiyo imeandaliwa na kampuni ya EndePa event planners waliopo Mikocheni B, Mlandege Street.

  0 0  Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi Nape Nnauye ametembelea Kijiji cha Rungwe Mpya kilichopo kata ya Rungwe Mpya Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma na kufanya shughuli mbalimbali za Chama ikiwa ni pamoja na Kuweka jiwe la Msingi la Ofisi ya CCM kijijini hapo na kuhutubia mkutano wa hadhara wa wananchi wa Kata hiyo pamoja na Kata ya Asante Nyerere.

  Baada ya kuweka Jiwe hilo la Msingi, Nnauye alikabidhi kadi kwa wanachama wapya wa Chama hicho kutyoka katika kata za Asante Nyerere pamoja na Rugwe Mpya, wanachama ambao wamerejea CCM kutoka vyama vya upinzani hasa NCCR Mageuzi na Chadema.

  Aidha Nape pia alipata fursa ya kuzungumza na Wajumbe wa Nyumba Kumi wa chama hicho, Wazee pamoja na Vijana waendesha Bodaboda mjini Kasulu.
  Pichani juu ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Rungwe Mpya na Asante Nyerere katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Rungwe Mpya kilichopo Kata ya Rungwe Mpya Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma.
   Nape akikabidhi kadi kwa wanachama wapya.


  Akina mama wakishangilia ujio wa Nape kijiji cha Rungwe Mpya.
  Nape akiwa na Mjumbe wa NEC, Kasulu, Daniel Nsanzugwanko.


   Baadhi ya Kadi zilizorejeshwa.
  Mkuu wa Wilaya Kasulu, Danny Makanga akicheza ngoma wakati wa mapokezi hayo ya Nape Kijijini hapo.
   Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akiweka jiwe la Msingi la Ujenzi wa Ofisi ya CCM Kijiji cha Rungwe Mpya Wilayani Kasulu.
   Nape akiangalia jengo hilo la CCM
  Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi Kata ya Asante Nyerere, Yohana Seif akizungumza katika mkutano wa hadhara mara baada ya kurejea CCM.
  Katibu Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye (katikati) akisalimiana na Diwani wa Kata ya Rungwe Mpya, Moris Mahabula wakati wa Mapokezi ya Katibu huyo. Kushoto ni Katibu wa Mwenezi wa Mkoa wa Kigoma, Zubery Mabie.
  Kutoka kulia ni Katibu Mwenezi wa CCM, Mkoa wa Kigoma, Zubery Mabie, Mjumbe wa NEC Kasulu, Daniel Nsanzugwanko, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kasulu wakisikiliza kwa makini maswali kutoka kwa wajumbe wa Shina wa CCM Kasulu.
  Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akisikiliza hoja mbalimbali za wajumbe hao.
  Wajumbe hao wakifuatilia kikao hicho na Katibu wa Itikadi na Uenezi.
  Wanachama wakila Kiapo cha CCM Kata ya Rungwe Mpya.
  Burudani ya ngoma kutoka kikundi cha akina mama.

  0 0

  katibu mkuu wa chama cha CCM, Abdurahman Kinanan akifungua pazia kuzindua tawi jipya la chama hicho ndani ya kata ya Bunyambo,Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma mapema leo jioni.
  Jiwe la Msingi lililowekwa na Ndugu Kinana.  Ndugu kinana akishiriki ujenzi wa ofisi ya tawi jipya la chama cha CCM  kata ya Bunyambo,Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma mapema leo jioni.

  Ndugu Kinana akisomewa taarifa kutoka kwa wanachama wa chama cha CCM,mapema leo jioni.
  Ndugu Kinana akizungumza na wanachama wa chama hicho sambamba na wananchi wa kata hiyo ya Bunyambo,Ndugu Kinana aliahidi kutoa kiasi cha shilingi milioni mbili kukamilisha ujenzi wa tawi hilo jipa la chama hicho.
  Ndugu Kinana akizungumza na Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Kumwambu,Wilaya ya Kibondo,Ndugu Kinana alikwenda shuleni hapo kukagua maendeleo ya ujenzi wa shule hiyo na pia kushiriki ujenzi wake,pia aliahidi kutoa Solar Pannel kwa ajili ya kuzalisha umeme ofisi za walimu,Kompyuta moja,seti ya jezi mbili sambamba na mipira miwili kwa ajili ya shule hiyo.

  Ndugu Kinana akishiriki ujenzi wa shule ya sekondari ya Kumwambu akiwa sambamba na baadhi wa viongozi wa Wilaya na mkoa kutoka chama cha CCM.
  Wazee wa chama wa shina,Matawi,kata,Madiwani Wilaya,Wazee pamoja na Jumuiya kwa ujumla wakishangilia jambo kwenye mkutano wao wa ndani uliofanyika kwenye ukumbi wa Vijana,wilayani Kibondo.
  Ndugu Kinana akizungumza na Wazee wa chama wa shina,Matawi,kata,Madiwani Wilaya pamoja na Wazee,lengo ikiwa ni kuwasilisha taarifa ya kazi za chama na serikali,Ndugu Kinana ameahidi kutoa kiasi cha shilingi milioni kumi kwa ajili ya kusaidia shunguli mbalimbali za Vijana sambamba na hilo Kinana ameahidi kutoa kiasi cha shilingi Milioni tatu kwa ajili ya kuwasaidia Walemavu.Mkutano huo umefanyika leo kwenye ukumbi wa Vijana,wilayani Kibondo,Mkoani Kigoma.
  Ndugu Kinana akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kibondo,Emmanuel Gwegenyeza,pichani kati ni Mkuu wa Wilaya ya Kibondo,Venance Mwamoto pamoja na Kada wa chama hicho,Matoni Nyobeye,mara baada ya kuwasili kijiji cha Kilemba,wilayani Kibondo mapema leo jioni.
  Msafara wa Ndugu Kinana pamoja na baadhi ya viongozi wa juu wa chama cha CCM,Mkoa na Wilaya.

  0 0

  Ofisa wa Kampuni ya Tigo, David Sekwao (katikati), akongea na mshindi wa droo ya promotioni ya Tigo smart card, Dar es Salaam leo. Anayeshuhudia kulia ni Ofisa Mkaguzi kutoka Bodi ya Taifa ya Kusimamia Michezo ya Kubahatisha na mfanyakazi wa Tigo (kulia).
  ---
  Tigo Tanzania leo imetangaza mshindi wa droo kubwa ya promosheni ya smartcard kuwa ni Bwana Julius Raphael Kanza ambaye ni mkazi wa jiji la Dar es Salaam.

  Bwana Kanza ameshinda zawadi kuu ambayo ni tiketi ya bure ya kwenda na kurudi Madrid Uhispania pamoja na kulipiwa gharama zote za safari kwenda kutizama  mechi  ya soka kati ya Real Madrid na FC Barcelona.

  Alivyojulishwa kuhusu ushindi wake Bwana Kanza alifurahishwa sana na kusema “Sikutegemea kabisa kuwa mshindi wa droo hii, nimefurahi sana na ninajiona wa muhimu sana. Napenda kuwashukuru Tigo kwa zawadi hii na nina hamu sana siku ziwadie niende kushuhudia mechi hii kubwa kati ya Real Madrid na FC Barcelona”.

  “Droo hii ni mwendelezo wa droo za promosheni ya smartcard ambazo zinaendelea kufanyika  kila mwezi, robo mwaka, na kila mwaka. Promosheni ya smartcard ilizinduliwa Septemba 2012 hususan kwa ajili ya wateja wa Tigo ambao wanatumia smartphones kama Blackberry, Android na iphone.” Alisema Bwana David Sekwao meneja wa ubunifu wa ofa za Tigo.


  Bwana Sekwao aliendelea kwa kusema kuwa "Mbali na zawadi kuu ya droo hii, washindi 42  watabahatika  kujishindia zawadi mbalimbali zikiwemo tiketi 12 za sinema, tiketi 12 za klabu, tiketi 12 za kuangalia mechi za mpira kwenye klabu ya hapa nchini, vocha 3 za kununua bidhaa mbalimbali na vocha 3 za chakula cha jioni.” Aliongeza kuwa “mshindi wa leo bwana Kanza atapatiwa tiketi ya bure ya kwenda na kurudi Madrid Uhispania na kulipiwa gharama zote za safari kwenda kuangalia mechi  ya soka kati ya Real Madrid na FC Barcelona ambazo ndio timu kuu za ligi ya Hispania La Liga"

  Kushiriki katika shindano hili, mteja alitakiwa awe amejiunga na kifurushi cha Smartcard chenye thamani ya Tshs 30,000 kwa mwezi na awe ametumia huduma hii kwa miezi mitatu mfululizo na vilevile awe amejiunga na jamii ya smartcard kupitia www.tigo.co.tz/smartcardcommunity.

  Zawadi nyingine kuu za mwaka za droo hii ni pamoja na  tiketi ya ndege ya kwenda na kurudi Dubai, malazi ya siku 5 pamoja na hela ya matumizi kiasi cha shilingi laki moja na nusu kwa siku na vilevile tiketi na gharama za kwenda na kurudi Uingereza kuangalia mechi kati ya Arsenal na man United mwezi Aprili mwaka 2013.

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji, wa wateja binafsi na wajasiliamali wa Ecobank Africa, Patrick Akinwuntan (katikati) akisisitiza jambo katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam Januari 31, alipoongea nao kuhusu upatikanaji wa huduma za kibenki bila kufika matawini nchini TanzaniaDar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo nchini,Enoch Osei-Safo na Mkuu wa Wateja wa binafsi na Wajasiriamali wa benki hiyo, Joyce Malei
  Mshauri wa maswala ya mahusiano wa Ecobank Daisy Mumbi akiwatambusha wakurugenzi kwa waandishi wa habari kabla ya kuanza kwa mkutano na waandishi wa habari. 
  Mkurugenzi Mtendaji, wa wateja binafsi na wajasiliamali wa Ecobank Africa, Patrick Akinwuntan (katikati) akiwa pamoja na maofisa wengine wa benki hiyo wakielekea kwenye warsha iliyofanyika Hoteli ya Serena Dar es Salaam Januari 31 2013.

  0 0


  Pamoja na habari njema za maelewano kupatikana baina ya Serikali na wenyeji wa Mtwara kuhusiana na swala la gesi asilia ya Mtwara kutumika Dar es Salaam badala ya huko huko Mtwara kwa ajili ya uzalishaji wa umeme, ukweli ni kwamba bado hilo sio jibu kwa watanzania wengine wengi ambao bado wanaona kwamba gesi ya Mtwara ilibidi izalishe umeme huko huko Mtwara badala ya Dar es Salaam ili kuwezesha taifa kupata faida kubwa zaidi.


  Ukweli ni kwamba upembuzi yakinifu ulikuwa ni muhimu sana ili kubaini faida na hasara za matumizi yote mbada ya gesi asilia ya Mtwara kwa ajili ya uzalishaji wa umeme ili kuwezesha ule mbada wenye faida kubwa zaidi kwa taifa kwa kipindi chote cha uhai wa mradi kuchaguliwa.

  Hii ni kuzingatia kwamba, uzalishaji wa umeme tarajiwa kutokana na gesi asilia ya Mtwara ni mradi mkubwa unaogharimu fedha nyingi sana na wa muda mrefu na kwamba matumizi mbadala ya gesi asilia ya Mtwara kwa ajili ya uzalishaji umeme ni mingi na inayotofautiana sana kwa gharama na faida kwa vipindi vyote vya uhai wake. Miongoni mwa matumizi hayo mbadala ni yale ya gesi asilia ya Mtwara kuzalisha umeme huko huko Mtwara na gesi asilia ya Mtwara kuzalisha umeme Dar es Salaam ambayo hutofautiana sana kwa gharama na manufaa kwa taifa kwa vipindi vyote vya uhai wake.

  Pia maamuzi ya Serikali kuhusu ni mbadala upi miongoni mwa matumizi ya gesi ya Mtwara mbadala kwa ajili ya uzalishaji wa umeme utumike hapa Tanzania yalibidi yahusishe wataalamu kutoka wizara zote, sekta binafsi na watanzania wote kupitia Bunge lao tukufu kwani matarajio na matakwa ya sekta mbalimbali za kiuchumi hapa nchini kutokana na matumizi mbada ya gesi asilia kwa ajili ya uzalishaji umeme yanaweza kutofautiana na kupingana sana.

  Hivyo, ilibidi upembuzi yakinifu ufanywe kwa kuzingatia mapendekezo ya wataalamu kutoka Wizara zote, sekta binafsi na watanzania wote kwa kupitia Bunge lao tukufu ili kuwezesha kubaini gharama na faida za matumizi yote mbadala ya gesi asilia ya Mtwara kwa ajili ya uzalishaji wa umeme kwa kuzingatia matarajio na matakwa ya wote kitaifa ili kuwezesha kuchaguliwa kwa ule mbadala wa matumizi ya gesi asilia ya Mtwara kwa ajili ya uzalishaji mkubwa wa umeme unaozingatia matarajio na matakwa ya wote na ulio na manufaa makubwa zaidi kwa wote na kwa taifa lote kwa ujumla kwa kipindi chote cha uhai wake.

  Ni vizuri serikali ikaweka bayana vipengele vilivyozingatiwa na taratibu zote zilizofuatwa kuwezesha kuamuliwa na Serikali gesi asilia ya Mtwara izalishe umeme Dar es Salaam badala ya Mtwara.

  0 0
 • 01/31/13--20:28: kumbukumbu ya Mzee matovu

 • Gration H. Matovu
  YOU LIVE ON,
  IN THE HEARTS YOU TREASURED.
  REST IS THINE AND
  SWEET REMEMBRANCE OURS.
   
         YOU ARE GREATLY MISSED
  BY YOUR LOVED ONES.
   
  UNAISHI KATIKA MIOYO YA ULIOWAHIFADHI.
  PUMZIKO NI LAKO KATIKA BWANA NA
  KUMBUKUMBU NZURI NI YETU.
   
        TUNAKUKOSA SANA TUKUPENDAO.

  0 0


  Ndugu zangu,

  Wanadamu tunahangaika sana kutaka kutunza siri. Niwaambie, katika maisha hakuna siri. Na kama zipo, ni chache sana.

  Inasemwa, kuwa siri ni ya mmoja. Lakini ona, hata mmoja huyo anaweza kuweweseka na siri ya moyoni mwake. Na mara ile atakapomnon'oneza mwenzake, basi, kuna unafuu atauona.

  Ukweli ni huu, kuwa kwenye maisha haya tunayoishi, siri ni chache sana. Ndio, ni wanadamu wachache sana wenye siri na wakazitunza. Hivyo, wanadamu tunapoteza muda na nguvu zetu nyingi sana katika kujifanya tunatunza siri. Ni kazi bure.

  Duniani kuna wenye kusema wasiyomaanisha, na kuna wasiomaanisha wanayosema. Haya ni mawili tofauti. Na wenye kuyatenda wanadhani kuna wanachoficha. Kuwa wana siri. Hapana, wanajidanganya. Hivyo, ni waongo tu.

  Mara nyingi nakutana na watu wenye kutamka; " E bwana ee, jambo nililokueleza ni siri, usimwambie mtu!" Na jambo hilo hilo unaweza kuambiwa na mwingine, kwa staili hiyo hiyo, kuwa ni la siri!

  Wanachoshindwa wengi kutofautisha ni hiki; muhimu na siri. Lililo la muhimu, na pengine nyeti, si lazima liwe la siri.

  Na hilo ni Neno La Leo.

  Maggid Mjengwa,

  Iringa.

  0788 111 765


  0 0  "HABARE NJEMA KWA WOTE WANAOSUMBULIWA NA STRETCH MARKS HASA WAKATI WA MIMBA NA BAADA YA KUJIFUNGUA,SASA UNAWEZA KUZUIA UWEZEKANO WA KUPATA STRETCH MARKS WEWE MAMA MJAMZITO KWA KUTUMIA TRILASTIN MATERNITY STRETCH MARK PREVENTION!!!

  DAWA HII ITAIFANYA NYAMA YA NGOZI YAKO NYORORO NA LAINI MUDA WOTE HII ITAISADIA KUEPUSHA KUTENGENEZA MICHIRI YA HATARI AMBAYO HUTOKEZA BAADA YA NGOZI KUWA KAVU KUPINDUKIA WAKATI WA UJAUZITO.
   "USISUBIRI TATIZO LIKUKUTE NDIO UANZE KUANGAIKA"WAHI MAPEMA KWANI KINGA NI BORA KULIKO TIBA.
   
   TRILASTIN MATERNITY STRETCH MARK PREVENTION ZINAPATIKANA @AK CLASSIC COSMETICS KINONDONI & SINZA.
  KWA MAELEZO ZAIDI ZAMA www.akclassic.blogspot.com
  PIA WANAPATIKANA 0713468393/0753482909

  0 0

   
  Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama cha Mapinduzi (CCM) Nape Nnauye akiangalia matunda ya Mchikichi ambayo yanaoteshwa kwenye mapipa kwa ajili ya kukamua mafuta ya mawese katika Kijiji cha Ilagala, Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma.
   Wana CCM wa Igalula wakiwa katika kikao cha ndani na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.
  Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama cha Mapinduzi (CCM) Nape Nnauye akikagua maendeleo ya ujenzi katika Kituo cha afya Ilagala.
   Nyumba ya Daktari wa Ilagala
   
  Wakazi wa Ilagala wakimsikiliza Nape Nnauye
   Nape akihutubia wakazi wa Ilagala ambao walitoa kilio chao kuhusiana na mgogoro wa ardhi baina ya Kijiji na Magereza .

  0 0

  Wakazi wa Kijiji wa Bunyambo wakichota maji ya kisima,Wilayani Kibondo Mkoa wa Kigoma.
   Samaki mkunje angali mbichi yaani ile mapemaaa,mpango mzima wa kilimo kwanza,ni kilimo tu
   Sehemu ya soko la pamoja wakati ule ya wakimbizi.
   Sehemu ya eneo la Kibondo mjini.
   Usafiri kama kawa ndani ya Kibondo na nje.
   Sehehemu ya eneo la soko ndani ya Wilaya ya Kibondo
   Shamba la mahindi
   Shamba la Migomba
  Shamba la Karanga

  0 0
 • 02/01/13--06:18: KUMBUKUMBU

 • Mzee Mbonea Kazeni Mshana.

  Leo ni miaka 10 tangu ulipochukuliwa kukaa na Baba yetu wa Mbinguni Milele Tarehe 1/02/2003. Tunakumbuka, busara, hekima, kujali, malezi bora ya kwako uliyotupa. Tunakumbuka bidii, juhudi na uchapa kazi wako. Lakini tunaamini kuwa umepumzika na taabu za dunia hii vizuri.

  Unakumbukwa na mkeo mpendwa Rahel Mshana, Wanao wapendwa Joyce, Felix, Joseph, Judith na Brian, pia wakwe zako Godlisten, Stephen na Neema na wajukuu zako Innocent, Rachel, Sarah, Daniel, Gideon, Elisha, Reinhard, Rachel na Jonathan.

  Pia unakumbukwa na mkweo Naizihijwa Joseph Mritha, na Ndugu Zako na jamaa na marafiki tulioishi nao kwa upendo Mwadui -Shinyanga na Arusha.

  Ufunuo 14: 13...."Heri wafu wafao katika Bwana Tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao"

  0 0


         THE UN SECRETARY-GENERAL,BAN KI-MOON
  --
  MESSAGE FOR INTERFAITH HARMONY WEEK
  New York, 1 February 2013

  For billions of people around the world, faith is an essential foundation of life.  
  It provides strength in times of difficulty and an important sense of community.  The vast majority of people of faith live in harmony with their neighbours, whatever their creed, but each religion also harbours a strident minority prepared to assert fundamentalist doctrines through bigotry and extreme violence.


  These acts are an affront to the heritage and teachings of all major religions.  They also contravene the Universal Declaration of Human Rights, which affirms the right of all to freedom of thought, conscience and religion.  It is imperative that the moderate majority is empowered to stand firm against the forces of extremism.  But, this can only be achieved through strong leadership.    

  Next month at its forum in Vienna, the Alliance of Civilizations will continue its efforts to unite faiths and cultures.  Whether on the world stage or in their communities, religious and cultural leaders have a responsibility to speak the language of tolerance and respect.  This is a central message of World Interfaith Harmony Week.   

  We must also reach out to young people with a message of hope.  Too often marginalized, jobless and facing a future of uncertainty, youth can be easy prey for fanatics offering a sense of cause and community.  We need to expose the invalidity of this lure and offer a compelling alternative. 


  This cannot be achieved by words alone.  Young people need jobs and a meaningful stake in a future that they can believe in.  The United Nations is currently engaged in defining a post-2015 sustainable development agenda.  Our goal is to eradicate extreme poverty in our lifetime and promote equitable economic opportunity for all while protecting the environment.  To do that, we need the engagement of all actors – including young people and communities of faith.    

  We live in times of turmoil and transformation – economic, environmental, demographic and political.  These transitions bring both hope and uncertainty.  Our job is to ensure that hope wins, and our task will be made easier if the followers of all faiths collaborate in common cause.  Let us never forget that what divides us is minuscule compared with what unites us.  Working together, we can achieve all our goals for peace, prosperity and physical and spiritual well-being. 

  0 0

  Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Tuzo za Mwanamichezo bora wa TASWA, Haji Manara, akizungumza na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam, leo mchana, wakati wakitangaza kuhusu kusogezwa mbele kwa shughuli hiyo ya utaoji tuzo ambapo sasa hafla hiyo itafanyika April 27, 2013, ambapo pia alizungumzia kwa ujumla maandalizi hayo. Katikati ni Katibu Mkuu wa TASWA, Amir Mhando, (kulia) ni Mjumbe wa TASWA, Turo Chambo.
  Baadhi ya waandishi wa Habari waliohudhuria mkutano huo, leo.
  *********************************
  TUZO za Wanamichezo Bora wa Tanzania wa mwaka 2012 zinazoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) zitafanyika Aprili 27 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

  Kamati inayoratibu tuzo hiyo ilifanya kikao chake cha kwanza Jumanne wiki hii, ambapo wajumbe wa kamati hiyo walikubaliana mambo mbalimbali ya kimsingi kuhakikisha tuzo zinakuwa na mvuto kama ilivyokuwa miaka iliyopita na pengine ziwe bora zaidi.

  Kutokana na hali hiyo vyama vyote vya michezo vilivyosajiliwa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT), ambavyo vipo hai na vinaendesha mashindano vitaandikiwa barua kwa ajili ya kutoa mependekezo yao ya wanamichezo waliofanya vizuri kwa mwaka jana upande wa michezo yao na yawasilishwe kabla ya Februari 28, mwaka huu.


  Tunaomba ieleweke kuwa vyama vitatoa mapendekezo na hivi sasa Kamati ya Tuzo inafanya mazungumzo na kampuni mbalimbali zinazohusika na mambo ya mawasiliano ili kuona namna zitakavyoshirikiana na wadau katika kuchambua majina hayo, ambapo kila chama kimetakiwa kiwasilishe majina matano ya wanamichezo wao kwa kila jinsia kama ni mchezo unaochezwa na jinsia mbili, lakini kama ni mchezo wa jinsia moja watatakiwa kuwasilisha majina matano ya jinsia husika tu.

  Yapo marekebisho kadhaa yamefanyika ikiwa ni pamoja na kuongeza idadi ya tuzo kutoka 36 za mwaka jana hadi kufikia 42 mwaka huu na idadi inaweza kuongezeka ama kupungua kulingana na sifa za wanamichezo ambazo vyama vitaleta.

  Tunaomba wadau watupe ushirikiano wa kutosha katika jambo hili ili kuzifanya tuzo ziwe bora na kuhakikisha kila anayestahili kupata tuzo anazawadiwa kwa kuthamini kile alichokifanya, ambapo ukumbi utakapofanyika tuzo hizo utatangazwa hivi karibuni baada ya kukamilisha baadhi ya mambo.

  Idadi ya michezo itakayopewa tuzo pamoja na aina nyingine ya tuzo zitakazotolewa ikiwemo Tuzo ya Heshima tutaendelea kujulishana kadri siku zitakavyokuwa zinasonga mbele. Washindi wa kila tuzo ndiyo mmojawapo ataibuka kuwa Mwanamichezo Bora wa Tanzania Mwaka 2012.

  Dhamira ya kamati yangu ni kutaka kuhakikisha kuwa TASWA haikukosea kututeua na tutaleta wanammichezo sahihi na hatimaye kumpata yule bora ambaye ataungana na wengine waliopata kutwaa tuzo hiyo miaka ya nyuma.

  Wanamichezo ambao wamepata kutwaa Tuzo ya Mwanamichezo Bora Mwaka wa Tanzania ni Samson Ramadhan (2006),  Martin Sulle (2007) na Mary Naali (2008) wote wakiwa wanariadha, wakati mwaka 2009 alikuwa Mwanaidi Hassan na mwaka 2010 alikuwa pia Mwanaidi Hassan ambaye ni mcheza netiboli na mwaka 2011 alikuwa mwanasoka Shomari Kapombe.

  Haji Manara
  Mwenyekiti Kamati ya Tuzo za TASWA

  01/02/2013


  0 0


  Na Mroki Mroki, FK BLG Kigoma.
  Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara Komred Philip Mangula amewasili mkoani Kigoma asubuhi hii kwa ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) na kupongeza mabadiliko makubwa yaliyopo mkoani humo hasa Uwanja huo wa Ndege ambao unaonekana sasa kuwa wa kisasa.

  Mangula ambaye amepata mapokezi makubwa yaliyoongozwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nappe Nnauye pamoja na mjumbe wa Sekretarieti ya chama hicho ambaye ni Katibu wa Siasa na Mahusiano ya Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kanali Mstaafu. Issa Machibya pamoja na viongozi mbalimbali wa chama na serikali.

  Mangula amesema Kigoma ya sasa si Kigoma aliyo ijua miaka iliyopita na viongozi wanastahili pongezi kwa maendeleo hayo ya sekta mbalimbali.

  “Kigoma ya leo sio Kigoma ile ya zamani ..uwanja huu wakati ndege inataka kutua nilitaraji nitasikia matairi ya kihangaika lakini nikashangaa tunakwenda vizuri tu” alisema Mangula akishangiliwa na wakazi wa Kigoma.

  Aidha amewaambia wakazi wa Mkoa wa Kigoma kutembea kifua mbele kutoka na mafanikio makubwa yaliyofikiwa hasa katika ujenzi wa uwanja wa ndenge wa kigoma ambao zamani haukuwa na tabaka la lami ambapo sasa uwanja huo umewekewa tabaka la lami na kuondoa usumbufu waliokuwa wakiupata zamani wananchi wa Kigoma.

  Pia Mangula amewataka wakazi wa mkoa huo kuendelea kupuuza kejeli zinazoendelea kutolewa na wanasiasa wa upinzani kuwa mkoa wa kigoma umesahaurika kitu ambacho amesema hakina ukweli kwani mkoa huo sasa umefunguka kwa miundombinu ya barabara.
  Wakati huo huo, katika kuadhimisha miaka 36 ya kuzaliwa kwa chama cha mapinduzi ccm, mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwasili kesho mkoani hapa kwa ajili ya maadhimisho hayo yanayotarajiwa kufanyika Jumapili Februari 3, 2013 katika uwanja wa Michezo wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.

  Maandalizi ya sherehe hizo yanaendelea ambapo sasa yamefikia asilimia zaidi ya themnini na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye pamoja na wajumbe wa NEC na viongozi wengine wa CCM wanataraji kwenda kukagua maandalizi hayo jioni ya leo.
  Mangula akiteremka katika ndege.
  Akisalimiana na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye
   Mangula akisalimiana na Katibu wa Siasa na Mahusiano ya Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro.
   
   
  Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara Komred Philip Mangula akisalimiana na viongozi mbalimbali wa CCM waliofika kumpokea Uwanja wa Ndege Mjini Kigoma hii leo.
  Makamu Mwenyekiti wa UWT, Dogo Mabruk (kushoto) na Mjumbe wa NEC-Wilaya ya Uvinza, Asha Baraka pamoja na wanachama wengine wa CCM wakimsikiliza Mangula.

  Vijana wa CCM waliofika kumpokea Makamu Mwenyekiti CCM Bara.


  0 0              WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII


  TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UPATIKANAJI WA DAWA ZA KUTIBU MALARIA.


  Utangulizi

  Kumekuwepo na taarifa kupitia baadhi ya vyombo vya habari kwamba kuna upungufu mkubwa wa dawa mseto za kutibu malaria aina ya ALU katika vituo vya kutolea huduma za afya hapa nchini.Taarifa hizo zilimnukuu Mkurugenzi wa shirika lisilo la serikali la SIKIKA, katika mkutano na wahariri wa vyombo vya habari uliofanyika mjini Dar es Salaam hivi karibuni.


  Ufafanuzi

  Taarifa alizotoa Mkurugenzi wa SIKIKA, chanzo chake kimetokana na kunukuu taarifa zinazopatikana kutoka katika mfumo wa kielektroniki wa wizara ambao unafuatilia takwimu za dawa za malaria katika vituo vya huduma ujulikanao kama ‘SMS for Life’.

  Mfumo huu unatoa taarifa za upatikanaji wa dawa za kutibu malaria aina mbili tu ambazo ni Alu na Quinine, na sio dawa nyingine za kutibu Malaria.


  Hivyo basi, dawa zingine zote pamoja na zile za msaada, ambazo zinapokelewa na kusambazwa katika hospitali zote nchini hazitolewi taarifa kwa kutumia mfumo huu wa “SMS for Life”. Hivyo kusababisha wakati mwingine kuonekana hakuna dawa wakati dawa hizo  zipo vituoni.


  Hali halisi


  Dawa za Alu zilizopokelewa mwezi Januari 2013;-

  ·         Vidonge vya watoto  dozi  2,400,000 ambazo zitatosheleza kwa miezi 5

  ·         Vidonge vya watu wazima dozi 5,688,720 zinatosheleza matumizi ya miezi 14


  Shehena nyingine za dawa za Alu zinatarajiwa kufika nchini mwezi Machi, 2013.


  Aidha, kufikia tarehe 31 Disemba 2012 kulikuwa na dawa za Alu za watoto dozi 1,315,967 ambazo zilitosha matumizi ya miezi 2.  Vile vile, kulikuwa na dozi za Alu 2,283,610 za watu wazima ambazo zinatosha matumizi ya miezi 2 na nusu.


  Hitimisho


  Wizara inapenda kuwahakikishia wananchi kwamba kwa sasa kuna dawa za kutibu malaria vituoni za kutosha. Vile vile, Bohari kuu ya Dawa (MSD) inaendelea na usambazaji wa dawa hizi katika vituo vyote nchini. Aidha, taratibu za kuagiza na kuleta shehena zaidi ya dawa za malaria kutoka nje ya nchi zinaendelea ili kuhakikisha kuwa dawa za kutibu malaria zinapatikana kwa muda wote.  Regina L. Kikuli

  KAIMU KATIBU MKUU

  01/02/2013


  0 0


  Mwakilishi wa Jumuiya ya Wazanzibari wanaoishi nchini Canada (ZANCANA) Bishara Al Masroori akizungumza na Wazazi wa watoto wenye ulemavu hawapo pichani katika hafla ya kukabidhi msaada kwa watu hao,kushoto ni Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Fatma Abdulhabib Fereji huko  Makao Makuu ya Jumuiya ya watu wenye ulemavu Zanzibar Weles.
  Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Fatma Fereji akiwa na Mwakilishi wa Jumuiya ya Wazanzibari wanaoishi nchini Canada Bishara Al Masroori wakimkadhi baskeli ya walemavu Mtumwa Hamadi Khamis mkaazi wa Tomondo huko Weles Makao Makuu ya Jumuiya ya watu wenye ulemavu Zanzibar.  Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

  =====  ======  ======
  Na Ali Issa-Maelezo Zanzibar 1/2/2013

  Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa kwaza wa Rais Fatuma Abdullhabibu Fereji amesema kuna kila sababu za kuwasaidia Vipando watu wenye ulemavu ili waweze kufikia katika Shughuli zao na kuungana na wenzao katika harakati za maisha.

  Hayo ameyasema leo huko Makao makuu ya Jumuiya ya watu wenye ulemavu Zanzibar Welesi alipokuwa akikabidhi Baskeli za kutembelea na vifaa mbali mbali kwa Watoto wenye ulemavu, ukiwa ni msada kutoka Jumuiya ya Wazanzibari wanaoishi nchini Kanada (ZANCANA).

  Amesema msaada wa Jumuiya ya ZANCANA unafaa kuigwa na kupigiwa mfano kwani utawawezesha Walemavu hao kukabiliana na majukumu yao ya kila siku kwa wepesi.

  Waziri Fereji amesema Walemavu wanahitaji kufanya mambo mengi ya msingi lakini kuna wakati hushindwa kutokana na ukosefu wa usafiri ikiwa ni pamoja na Baskeli na vifaa vingine vinavyoweza kuwasaidia kufanya mambo yao ipasavyo.

  “wana hitaji kwenda skuli,kutembea, kuchanganyika na wenzao,hivyo wanapo kosa vifaa kama hivi husindwa watoto wetu kuyafikia mahitaji yao muhimu hivyo msada huu ni furaha kwao na kwetu” Alisema Waziri Fereji.

  Aidha waziri huyo asema kuwa watu wenye ulemavu wanahitaji kutunzwa na kupewa haki za msingi ikiwemo elimu,afya, malazi, chakula na mengineo kitu ambacho mtu yoyote anaweza kuwawezesha watu hao si lazima wazee .

  Amesema mpaka hivi leo kuna badhi ya Wazazi wanawafungia ndani walemavu na kuwakosesha haki zao za msingi kwa madai kuwa ni hawataweza kufikia masafa ambayo huduma zinatolewa.

  Waziri Fereji amekemea tabia hiyo ya kuwafungia Walemavu na kusisitiza kuwa ulemavu si sababu ya kumkosesha mtoto elimu kwani jambo hilo liko katika milki ya Mwenyezi mungu Muumba.

  Nae Mzazi wa mtoto Mtumwa Hamad Khamis wakati akitoa shukrani alisema Msaada huo umekuja wakati muafaka kwao kutokana na kukosa Baskeli ambazo watoto wao walikuwa wanazihitaji kwa muda mrefu.

  Ameongezea kuwa mtoto wake amekuwa akipata wakati mgumu wakati wa kwenda Skuli kutokana na kukosa usafiri wa uhakika ambao unamuwezesha kwenda na kurudi Skuli anayosoma.

  Aidha mzazi huyo amegusia suala la unyanyapaa linalomkabili Mtoto wake Skulini kwao kutokana na Skuli hiyo kutokuwa ya mchanganyiko kati ya Wanafunzi Walemavu na wasiokuwa Walemavu jambo ambalo linamfanya afikirie kubadilisha Skuli.

  Jumuiya ya Wazanzibari wanaoishi nchini Kanada (ZANCANA) imetoa msaada kwa Watu wenye ulemavu ikiwa ni pamoja na Bskeli za kutembelea, Viti, vifaa watoto vya kuchezea ikiwa ni jitihada za kusaidia ndugu zao wanaoishi katika mazingira magumu .

  IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR.

  0 0  VIONGOZI wa mataifa mbalimbali duniani, kila mara wanakutana katika vikao vya kimataifa kusaka amani, bila amani hakuna kitu chochote kinachoweza kufanya nchi isonge mbele.
   
  Utasongaje mbele wakati kila saa ni migogoro na vita? Lakini Watanzania tumejaliwa kwa kiasi kikubwa kuwa na amani, ambayo kwa sasa kuna baadhi ya watu wanataka kuichezea. Ni kama vile wamechoka nayo.
   
  Lakini wakati kukiwa na migogoro mingine ambayo haina tija, kuna kitu ambacho kimeanzishwa ili kuwakumbusha Watanzania kuhusu misingi halisi tuliyowekewa na waasisi wa Taifa hili.
   
  Hiki si kingine isipokuwa ni mbio za Uhuru Marathon, ambazo zitafanyika mwishoni mwa mwaka huu huku Rais Jakaya Kikwete kwa kuona umuhimu wake naye ameamua kushiriki kama kinara na jemedari wa Taifa hili ambapo mara kwa mara amekuwa akiwakumbusha wananchi juu ya umuhimu wa kuenzi amani iliyopo..
   
  Akithibitisha hilo, Mratibu wa Uhuru Marathon, Innocent Melleck, anasema lengo la mbio hizo ni kuwakumbusha Watanzania umuhimu wa kukumbuka, kuzingatia na kuuenzi urithi waliaochiwa na viongozi waliopigania uhuru wa nchi.
   
  Anasema urithi huo ambao utakuwa ukikumbukwa kila mwaka kupitia mbio hizo, ni upendo, mshikamano, umoja na amani iliyopo. Melleck anasema mbio hizo zitakuwa zikifanyika kila mwaka na zitaanza rasmi siku ya tarehe 08/12/2013 na zitatanguliwa na shamrashamra za kanda zote za Nchi yetu.
   
  Hilo lilithibitishwa pia na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara , ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati zinazinduliwa jijini Dar es Salaam.
   
  Uzinduzi wa mbio hizo ulienda sambamba na kuzinduliwa rasmi kwa mtandao wa Uhuru Marathon ambao utakuwa na habari za kila aina kuhusu mbio hizo na washirika wake.
   
  Dk. Mukangara alipongeza wazo la kuanzishwa mbio hizo ambazo zitakuwa zikifanyika kila mwaka, lengo likiwa ni kudumisha umoja, amani na upendo miongoni mwa Watanzania na kuuenzi uhuru wetu.
   
  Waziri alikiri, kwa sasa kuna mbio nyingi za marathon hapa nchini, lakini hakuna ambaye alikuja na wazo zuri la kuanzisha mbio kama hizo za kuuenzi uhuru wetu na kudumisha amani nchini.
   
  “Nawapongeza waandaaji wa mbio hizi ambao ni vijana wa Kitanzania waliokuja na wazo hili zuri la kuanzisha mbio za uhuru. Tunazo mbio nyingi sana hapa nyumbani, lakini hatukuwa tumewaza kuanzisha mbio zinazolenga kuuenzi uhuru wetu na kudumisha amani yetu.
   
  “… Kwa niaba ya Serikali, napenda kusema wazi kuwa tumefurahishwa sana na wazo hili la kuanzisha mbio hizi za Uhuru na nichukue fursa hii kuwaomba wadau na wapenda maendeleo ya michezo kuungana na taasisi hii kufanikisha mpango huu ili uweze kuwa na mafanikio.
   
  “Serikali bado itaendelea kuweka miongozo na mazingira rafiki ya kushirikiana na wadau wenye nia nzuri ya kuendeleza michezo nchini. Nina hakika waheshimiwa mawaziri, wabunge, viongozi mbalimbali wa Serikali, mashirika binafsi na viongozi wa dini wote watajitokeza kushiriki mbio hizi,” alisema.
   
  Hapa ndipo tunapoweza kusema kwamba, fikiria mbio zozote kubwa duniani kama vile London Marathon nchini Uingereza, Paris Marathon, Ufaransa au zile zingine zenye kupendwa na wengi zaidi duniani za Berlin Marathon zinazofanyika Ujerumani kila mwaka, lakini Uhuru Marathon ni zaidi ya mbio.
   
  Kwani mashindano yote haya ni ya kutukuka, kutokana na kushirikisha wanariadha wenye majina makubwa duniani, huku kukiwa na ushindani mkubwa zaidi miongoni mwa washiriki.
   
  Lakini kwa sasa Tanzania ina cha kujivunia zaidi kwa ujio wa mashindano ya mbio Uhuru Marathon.
   
  Upekee wa shindano hilo la Uhuru Marathon ni kutokana na aina ya washiriki wake, pamoja na kupewa tafu kubwa na waandaaji wa mashindano ya Berlin Marathon, ambao wanataka kuiona Tanzania inatangazwa zaidi.
   
  Hivyo, shindano la Uhuru Marathon, lina nafasi kubwa ya kuwabeba Watanzania kwa kutangazika zaidi, hasa ukichukulia uzoefu mkubwa walionao waandaaji wa Berlin Marathon ikiwa pamoja na kuchangia kudumisha amani na upendo nchini.
   
  Mratibu wa mbio hizo, Innocent melleck anasema, ana imani mbio hizo zitajizolea umaarufu mkubwa, kutokana na jinsi zitakavyoteka hisia za watu mbalimbali, wakiwemo wanamichezo.
   
  Katika mbio hizo, zitakazowashirikisha watu wa kada mbalimbali, zitakuwepo pia mbio za kilomita 3, kilomita 5, Half Marathon kilomita 21 pamoja na Full Marathon yenyewe kilomita 42.
   
  Mratibu huyo anasema mbio za kilomita 3 zitakuwa maalumu kwa ajili ya viongozi wa kada mbalimbali, wakiwemo pia wale wa dini na zile za kilomita 5 pia zitakuwa za kuchangia kwa ajili ya watu wa mahitaji ya aina mbalimbali.
   
  “Hapa tunachotaka kufanya katika mbio za kilomita 3 ni kuwaomba kama vile viongozi maarufu wa dini mbalimbali pamoja na viongozi wetu ili kushiriki, kwa kudumisha amani na upendo.
   
  “Pia tutahakikisha kama mbio za kilomita 5, zinakuwa kwa ajili ya kuchangia watu wenye mahitaji mbalimbali na tayari tuna uhakika mkubwa wa wanariadha maarufu zaidi duniani kushiriki,” anasema.
   
  Mratibu huyo anafafanua kuwa wamejipanga mno katika hilo ili kuhakikisha wanafanya mambo makubwa zaidi na ambayo yataleta tija kwa taifa.
   
  Wakati Uhuru Marathon ikitambulishwa bungeni, kiongozi aliyeonekana kufurahishwa zaidi na hilo ni Spika Anne Makinda, ambaye hakuishia kulimwagia sifa tu, bali alitaka hata viongozi wahakikishe wanalifanikisha.
   
  “Ni wazo zuri hasa katika kipindi hiki ambacho tunapigania amani na mshikamano miongoni mwetu, tunatakiwa kuenzi mashindano kama haya ili kutufanya tuwe wamoja zaidi,” alisema Spika Makinda.
   
  Msaada wa Berlin Marathon
   
  Melleck anasema, wamefanya mazungumzo na waandaaji wa mashindano ya Berlin Marathon, kwani hilo ni moja kati ya mashindano makubwa zaidi duniani, likiwa linashirikisha washiriki mbalimbali walio maarufu zaidi.
   
  Shindano la Berlin Marathon au maarufu zaidi kwa jina la BMW Berlin Marathon kutokana na kudhaminiwa na kampuni ya BMW ni maarufu zaidi ndani ya Ujerumani na duniani kwa ujumla.
   
  Shindano hilo la Full Marathon la kiilomita 42.195 ambalo linawashirikisha wanariadha wa kulipwa na wale wa ridhaa, lilianza kwa mara ya kwanza mwaka 1974 na linafanyika kila wiki ya mwisho wa Septemba kila mwaka.
   
  Shindano hili kwa umaarufu wake, mwaka 2008 lilishirikisha wanariadha takriban 40,827 kutoka mataifa 107, huku waliomaliza mbio wakiwa 35,913 na lina zawadi mbalimbali za kuvutia.
   
  Uhuru Marathon je?
   
  Melleck anasema, ushirikiano wa Berlin Marathon una maana kubwa, kwani itasaidia kuitangaza zaidi Tanzania na kuifanya dunia itambue umuhimu wa amani, upendo, umoja na mshikamano miongoni mwetu.
   
  “Wanariadha wengi watashiriki katika mbio hizi, wengi wakiwa maarufu zaidi duniani, pamoja na viongozi wa kada mbalimbali na hivyo kutimiza lengo tulilojiwekea.”
   
  Mratibu huyo anasema, kuna kila haja kwa Watanzania, kuyathamini mashindano hayo, kwani yana lengo la kuwafanya wawe wamoja zaidi, hasa katika kipindi hiki kigumu ambacho kuna majaribu ya kila aina.
   
  “Waasisi wetu wa taifa na wale waliopigania uhuru, walikuwa na malengo mengi na tunatakiwa kuyadumisha hayo, hilo ndilo Uhuru Marathon inalotakapigania,” anasema.
   
  Kwa Watanzania itakuwa faraja zaidi, hasa ukichukulia jinsi taifa linavyoweza kufaidika kwa kuzalisha pia wanariadha wa aina mbalimbali.
   
  Hivyo Uhuru Marathon ni zaidi yambio, kwani inatukumbusha tulipotoka, tulipo na tunapokwenda!

  0 0


  HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA
  TANZANIA, MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE, KWA WANANCHI, TAREHE 31 JANUARY, 2013

  Utangulizi
  Ndugu Wananchi;
  Kama ilivyo ada naomba tuanze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, Mwenye Rehema, kwa kutujaalia uzima na kutuwezesha kuzungumza kwa mara nyingine kwa kutumia utaratibu wetu huu mzuri wa mawasiliano baina ya Rais na wananchi wa Tanzania kila mwisho wa mwezi.  Siku ya leo nitazungumzia safari yangu ya Ufaransa, Uswizi na Ethiopia.  Pia nitazungumzia ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi asili kutoka Mtwara kuja Dar es Salaam.

  Safari za Kikazi Nje ya Nchi
  Ndugu Wananchi;
           Safari yangu ya Ufaransa, Uswizi na Ethiopia ilikuwa na manufaa makubwa kwa nchi yetu.  Nchini Ufaransa licha ya kuimarisha uhusiano wa kirafiki baina ya nchi zetu, tumepata wawekezaji wengi wakubwa wenye nia thabiti ya kuja kuwekeza hapa nchini.  Pia tumekubaliana kuanza mazungumzo ya kuwa na mpango mwingine wa ushirikiano.  Mpango wetu wa sasa ulioanza mwaka 2006 uliisha mwaka 2010.  Mpango ule ulitusaidia sana kuboresha huduma za maji katika miji ya Utete mkoani Pwani na Mpwapwa mkoani Dodoma.

           Katika mkutano wa Kongamano la Uchumi wa Dunia uliofanyika Davos, Uswizi, tumehakikishiwa ushirikiano katika kuendeleza juhudi zetu za kuleta mapinduzi ya kijani ili tujihakikishie usalama wa chakula na kupunguza umaskini vijijini na kukuza uchumi wa nchi yetu.  Aidha, tulipata bahati ya kushirikishwa katika mjadala wa kuanzishwa kwa programu kubwa ya kuzisaidia nchi za Afrika kutatua matatizo ya upatikanaji wa umeme.  Naamini programu hiyo ikitekelezwa na wakubwa kuheshimu kauli na ahadi zao itakuwa msaada mkubwa kwa maendeleo ya nchi za Afrika zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara.


  Ndugu Wananchi;
           Nchini Ethiopia tulishiriki katika mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika na katika kikao cha African Peer Review Mechanism (APRM) ambapo taarifa ya tathmini ya utawala bora ya Tanzania na Zambia iliyofanywa na APRM ilijadiliwa.  Kwa jumla hatuna mahali tuliponyooshewa kidole kuwa tunafanya vibaya. 

   Tumepongezwa katika mambo mengi na tumepewa ushauri kwa baadhi ya maeneo waliyoona hatuna budi kuyaboresha.  Nilipata nafasi ya kusema ambayo niliitumia kufafanua baadhi ya mambo yaliyokuwamo kwenye taarifa.  Niliwashukuru na kuahidi kuufanyia kazi ushauri uliotolewa.  Tathmini ya nchi yetu ilipitishwa kwa kauli moja.

  Vurugu za Kupinga Gesi Kusafirishwa Kutoka Mtwara
  Ndugu wananchi;
  Kama mtakavyokumbuka tarehe 8 Novemba, 2012 kule Kinyerezi, Wilaya ya Ilala hapa Dar es Salaam, niliweka jiwe la msingi la ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi asili kutoka Mtwara na Songosongo kuja Dar es Salaam.  Karibu na mwishoni mwa Desemba, 2012 kukafanyika maandamano mjini Mtwara kupinga ujenzi wa bomba hilo.  

  Katika maandamano yale na baadaye kwenye kauli za wanasiasa na wanaharakati yakatolewa madai kuwa gesi hiyo itumike kwa maendeleo ya Mtwara na kwamba yale yanayotakiwa kufanyika Dar es Salaam yafanyike Mtwara.  Pia, zilitolewa shutuma nyingine dhidi ya Serikali eti kuwa kwa miaka mingi imewasahau na haiwajali wananchi wa Mikoa ya Kusini na ujenzi wa bomba hilo ni muendelezo wa hayo. Kauli mbalimbali za wanasiasa na wanaharakati ni kama vile ziliongeza mafuta kwenye kaa la moto na kuuchochea mpaka kukatokea matukio yaliyotusikitisha na kutshtua sote.  Baadhi ya ndugu zetu wamepoteza maisha na mali za watu na Serikali kuharibiwa. 

  Ndugu Wananchi;
  Katika hotuba yangu ya kuaga mwaka 2012 na kuukaribisha mwaka 2013, tarehe 31 Desemba, 2012, nililisemea jambo hili.  Leo mwezi mmoja baadae, napenda kusisitiza mambo mawili.  Kwanza kwamba, si kweli kuwa Serikali inapuuza Mikoa ya Kusini.  Na pili, kwamba kujenga bomba la kuipeleka gesi Dar es Salaam hakuinyimi Mikoa ya Mtwara na Lindi fursa ya kunufaika na gesi iliyopo Mtwara.
  Ndugu Wananchi;
           Serikali imefanya, inafanya na ina mipango ya kufanya mambo mengi mazuri kwa ajili ya kuleta maendeleo katika Mikoa ya Mtwara na Lindi.  Ipo mipango ya kuboresha miundombinu, huduma za kiuchumi na kijamii pamoja na kukuza uchumi ikiwa ni pamoja na ujenzi wa viwanda vikubwa na vidogo.  Serikali ya Awamu ya Tatu chini ya uongozi wa Rais Mstaafu, Mheshimiwa Benjamin Mkapa, ilijenga daraja katika Mto Rufiji maarufu kama Daraja la Mkapa.  Hii ilikuwa ni hatua kubwa ya awali katika safari ya kutatua matatizo ya usafiri ya Mikoa ya Kusini.  Serikali ninayoiongoza mie iliachiwa kazi ya kukamilisha ujenzi wa barabara za lami kufikia darajani na kuunanisha Mkoa wa Mtwara na Mkoa wa Ruvuma.  Kazi hiyo, tumeitekeleza vizuri na sasa tunakaribia kuimaliza.  Tulikamilisha ujenzi wa barabara ya kutoka Mnazi-Mmoja hadi Nangurukuru.  Mwaka 2009 tukaanza ujenzi wa barabara ya kilomita 56 kutoka Somanga hadi Ndundu (darajani).  Ujenzi wakilometa 36 za mwanzo ulienda vizuri.  Bahati mbaya ujenzi wa kilomieta 20 za mwisho umechelewa sana kwa sababu ya mmiliki wa kampuni iliyokabidhiwa kufanya kazi hiyo kufariki.  Kwa sababu hiyo, kampuni ilipata mtikisiko kiasi na kusababisha kazi kutotekelezwa kwa kasi tuliyoitarajia.  Sasa mambo yametengemaa na kazi inaendelea kwa kasi nzuri.  Matumaini yetu ni kuwa ifikapo mwezi Desemba, 2013 kazi hiyo itakuwa imekamilika. 
  Hali kadhalika, Rais Mstaafu, Mzee Benjamin Mkapa alituachia jukumu la kumaliza ujenzi wa Daraja la Umoja katika mto Ruvuma na ujenzi wa barabara ya lami kuanzia Mikoa ya Mtwara na Ruvuma.  Tumelikamilisha Daraja hilo na ujenzi wa barabara ya lami kutoka Masasi hadi Mangaka umekamilika.  Mchakato wa kujenga barabara ya kwenda Songea na kwenda Darajani umefikia  mahala pazuri.  Tenda ya ujenzi wa barabara kutoka Tunduru hadi Mangaka mpaka Darajani imeshatangazwa.  Kama mambo yataenda sawa miezi mitatu ijayo mjenzi atapatikana.  Wakati huo huo ujenzi wa barabara kutoka Namtumbo hadi Songea – Mbinga na Namtumbo – Tunduru unaendelea.  Hivyo basi, kwa barabara ya “MtwaraCorridor”  kazi iliyobaki ni kutoka Mbinga kwenda Mbambabay ambayo tutaifanya wenyewe kama tulivyofanya kwa Mnazi Mmoja – Nangurukuru na Somanga – Ndudu na Daraja la Umoja.
  Ndugu Wananchi;
  Ipo pia mipango ya kuipanua na kuijenga upya bandari ya Mtwara ili iweze kuhudumia mahitaji ya utafutaji na uchimbaji wa gesi baharini, kuhudumia na kuvifanyia matengenezo vyombo vinavyotumika katika utafiti, uchimbaji na uendelezaji wa gesi.  Pia iweze kuhudumia shughuli za kiuchumi zitakazotokana na uchumi wa gesi pamoja na zilizopo sasa.  Nilipozungumza na makampuni ya utafutaji gesi pale Mtwara tarehe 25 Julai, 2011 waliomba nikubali bandari ya Mtwara iwe mahali pa kuhudumia vyombo vyote vinavyofanya shughuli ya utafutaji na uchimbaji wa gesi na mafuta katika pwani ya Afrika ya Bahari Kuu ya Hindi.  Pia waliomba kuwa sehemu hiyo ya bandari iwe bandari huru.  Niliwakubalia bila ya kusita na tayari eneo la hekta 110 zimeshatengwa na kutangazwa rasmi kuwa bandari huru.  Vile vile waliomba wapewe sehemu ya bandari ya sasa kuendeshea shughuli na eneo la kujenga kituo cha mitambo ya kuchakata gesi na kusafirisha nje.
  Ndugu Wananchi;
  Baada ya kuzungumza na makampuni ya utafutaji gesi na mafuta na kuelezwa mahitaji yao nilibaini kuwa bandari ya Mtwara inahitaji kupanuliwa na kujengwa upya.  Bahati nzuri viongozi wa Mamlaka ya Bandari walikuwepo na walinihakikishia kuwa watafanya hivyo. 
  Tayari eneo la bandari limeongezwa kutoka hekta 70.68 hadi 2,693.68.  Eneo la bandari huru limeshatengwa hivyo hivyo na eneo la kampuni ya Dangote na makampuni ya gesi yaliyopo.  Aidha, mchakato wa kupanua bandari iliyopo, kujenga gati mpya na kuendelea na ujenzi hadi maeneo ya Msanga Mkuu ipo katika hatua mbalimbali za matayarisho na utekelezaji. 

  Ndugu Wananchi; 
           Kwa upande wa Mkoa wa Lindi mipango ya kupanua na kuijenga upya bandari ya Lindi imefikia hatua nzuri.  Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Dkt. Charles Tizeba alithibitisha hayo tarehe 1 Desemba, 2012 nilipotembelea bandari hiyo wakati wa ziara yangu ya Mkoa wa Lindi ya tarehe 1 mpaka 5 Desemba, 2012.  Hali kadhalika mipango ya kujenga bandari ya Kilwa iko mbioni.  Tena kwa upande wa Mkoa wa Lindi moja ya makampuni yaliyogundua gesi baharini wameamua kujenga bandari na kituo cha kuchakata na kusarifisha gesi nje ya mkoa huo kama ilivyo kwa Mtwara.  Naambiwa wametambua maeneo matatu, kilichobakia ni kuamua mojawapo ili ujenzi uanze.
  Ndugu Wananchi;
           Nilipotoka bandari ya Mtwara, siku ile nilitembelea Chuo cha VETA na kuzungumza na viongozi wa VETA taifa na wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuhusu kuwa na mitaala ya kutoa mafunzo mahsusi yanayohitajika na sekta ya gesi na mafuta.  Nilisisitiza kwamba tuwapatie vijana wetu mafunzo yatakayowawezsha kuajiriwa na makampuni ya gesi na yale yatakayokuwa yanatoa huduma kwa makampuni hayo.  Nilisema tusipofanya hivyo, makampuni hayo yataajiri watu kutoka nje na hatutakuwa na sababu ya kuwalaumu wala kulalamika. 
  Nafurahi kwamba agizo langu hilo limefanyiwa kazi ipasavyo.  Hivi sasa katika chuo cha VETA Mtwara mafunzo hayo yanatolewa.  Kampuni ya PetroBrass ya Brazil inaendesha mafunzo ya sekta ya gesi kwa vijana 25 kutoka mkoani Mtwara.  Aidha, chuo cha VETA kwa kushirikiana na Kampuni ya Gesi ya Uingereza (British Gas) na Volunteers Service Overseas ya Uingereza, kinatekeleza programu ya miaka mitatu iitwayo Enhancing Employerbility Through Vocational Training.  Programu hii inalenga  kutoa kozi zitakazowafanya wahitimu kuweza kuajiriwa katika sekta ya gesi.  Programu hii ilifunguliwa na Makamu wa Rais, Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal, tarehe 26 Novemba, 2012. 


  Ndugu Wananchi;
  Chini ya programu hii, walimu wa masomo yanayohusiana na gesi wanaongezewa ujuzi ili waweze kufikia viwango vya kimataifa.  Vile vile, Wizara ya Nishati na Madini imetoa upendeleo maalum wa kudhamini wanafunzi 50 kutoka mkoa wa Mtwara kusoma chuoni hapo ambao tayari wameshahitimu mafunzo ya msingi ya uunganishaji vyuma viwandani.  Mchakato wa kuwapata wanafunzi 50kwa ajili ya mafunzo kama hayo kutoka mkoa wa Lindi unaendelea.  Nimeambiwa mpaka wameshawapata vijana 25 bado 25. 
           Hali kadhalika, Wizara ya Nishati na Madini inadhamini wanafunzi 10 kupata mafunzo katika Chuo Kikuu cha Dodoma ambako kozi za mafuta na gesi zinatolewa.  Kipaumbele kwa udhamini huu unatolewa kwa wanafunzi wa mikoa ya Mtwara na Lindi wenye sifa za kudahiliwa katika mafunzo haya.  Wamepatikana watatu.  Wataalamu hawa na wengine wa fani mbalimbali za gesi na mafuta watafundishwa kwa kiwango cha shahada ya kwanza na baadae uzamili na uzamivu ili nchi yetu ijitosheleze kwa wataalamu wa sekta hii. 
  Kupanga Mji wa Mtwara
  Ndugu Wananchi;
           Baada ya kutembelea bandari ya Mtwara na Chuo cha VETA, nilikaa na kuzungumza na viongozi wa Serikali na Manispaa ya Mtwara.  Katika mazungumzo yangu nao niliwasisitizia umuhimu wa kuwa na mpango kabambe wa kuendeleza mji wa Mtwara – (Mtwara Masterplan) Mpango ambao utawezesha kujengwa mji mkubwa wa kisasa unaokidhi mahitaji ya mji wa uchumi wa gesi.  Niliwataka wahakikishe kuwa kuna maeneo ya viwanda, biashara, makazi, mahoteli, huduma za afya, elimu, mapumziko na burudani, viwanja vya michezo na kadhalika.  Kazi ya kutayarisha Masterplan hiyo imeanza na Manispaa ya Mtwara inashirikiana na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Makazi. 
  Kwa upande wa uwekezaji nafahamu kuwa mpaka sasa makampuni 51yameonyesha nia ya kuwekeza Mtwara katika viwanda, hoteli, shughuli za uchukuzi na huduma hasa kwa sekta ya gesi.  Wanachosubiri ni kutengewa maeneo ya kujenga, waanze.  Hivyo kukamilika mapema kwa Masterplan ya mji wa Mtwara kutasaidia kuongeza kasi ya uwekezaji huu kufanyika.  Viwanda hivi vyote vitasaidia kuongeza ajira kwa vijana wa Mtwara na Watanzania kwa jumla.  Nimeambiwa kwa mfano, wakati wa ujenzi wa kiwanda cha saruji watu zaidi ya 7,000 wataajiriwa.  
  Ndugu Wananchi;
           Kabla hata ya ugunduzi wa gesi iliyoko baharini, tulikuwa na mipango ya kutumia gesi ya Msimbati (Mnazi Bay) kwa ajili ya kuzalisha umeme, kuzalisha mbolea na kutumika katika kiwanda cha saruji.  Kwa upande wa umeme kulikuwa na mpango wa kujenga mtambo wa kuzalisha Megawati 300 kwa kushirikiana na mwekezaji binafsi.  Bahati mbaya wakati wa matatizo ya kifedha ya dunia mwaka 2009 mwekezaji huyo akashindwa kupata mkopo, hivyo mradi ukasimama kutekelezwa.  Haukufa wala haukuhamishiwa Dar es Salaam au Bagamoyo kama ambavyo imekuwa inapotoshwa kwa makusudi.  Mradi huo bado upo, tena mpango wa sasa ni kujenga Megawati 600 zitumike Mtwara na zingine kuziingiza kwenye gridi ya taifa kupitia Songea.
  NduguWananchi;
  Kwa upande wa kiwanda cha mbolea, wawekezaji wengi wameshajitokeza tangu mwaka 2008 mpaka sasa.  Mchakato umefanyika wa kuchambua wawekezaji wenye sifa na kutambuliwa.  Mambo mawili yamechelewesha utekelezaji kuanza.  Jambo la kwanza ni wawekezaji na kampuni ya Artumas iliyokuwa mbia na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (T.P.D.C) wakati ule, kushindwa kukubaliana nao juu ya bei ya kuwauzia gesi.  Wawekezaji walitaka bei ya gesi ipunguzwe, lakini kampuni ya Artumas na T.P.D.C. hawakuwa tayari kupunguza zaidi ya kiasi walichopunguza, ambacho wawekezaji bado waliona hailipi kwa kuzalisha mbolea.
   Sababu ya pili ni matatizo ya kifedha yaliyoikumba kampuni ya Artumas katika kipindi hicho.  Kufuatia machafuko ya masoko ya fedha na mdororo wa uchumi wa dunia mwaka 2008/2009 kampuni ya Artumas iliathirika na kulazimika kuuza hisa zake kwa wawekezaji wengine.  Katika kipindi hicho ilichopitia kampuni, mazungumzo na uwekezaji wa kiwanda cha mbolea hayakuweza kupewa kipaumbele.  Mtazamo wa sasa wa wabia wapya na T.P.D.C. ni kuwa wao wenyewe sasa wawekeze katika ujenzi wa kiwanda cha mbolea. Serikali imekubali rai yao hiyo na wanaendelea na matayarisho.
  Ndugu Wananchi;
           Kwa upande wa kiwanda cha Saruji kitakachojengwa na kampuni ya Dangote ucheleweshaji ulikuwa kwa sababu mbili.  Kwanza, kampuni ya Dangote iliomba eneo zaidi ya ililokuwa imeomba na kupewa.  Hoja yao ilikuwa kwamba eneo la ziada walilokuwa wanaliomba ndilo lenye malighafi nyingi na bora kwa utengenezaji wa saruji.  Hivyo, waliamua kusubiri mpaka watakapopewa eneo hilo. 
  Bahati mbaya eneo hilo lilikuwa linamilikiwa na mtu mwingine na alikuwa na hati miliki nalo.  Halmashauri ya Mtwara iliomba Serikali eneo hilo litwaliwe na baadaye ipewe kampuni ya Dangote. Serikali ilikubali.  Hata hivyo, mchakato ulichukua muda na hata pale ulipokamilika mwenye eneo aliupinga uamuzi wa Serikali Mahakamani.  Kesi ilichukua muda kusikilizwa na kumalizika.  Bahati nzuri Serikali ikashinda na mara baada ya uamuzi wa Mahakama ndipo kampuni ya Dangote ikamilikishwa eneo hilo. 
  Kampuni nayo ilichukua muda kuanza.  Hivi sasa, timu yake ipo kwenye eneo na mradi uko tayari kuanza kutekelezwa.  Niliambiwa kuwa katika magari yaliyopigwa mawe katika fujo za Mtwara ni pamoja na lile la mradi huu.  Huo ndiyo ukweli kuhusu ujenzi wa kiwanda cha saruji cha Dangote.  Madai kuwa kiwanda hicho kimehamishiwa Bagamoyo si ya kweli.   Ni uzushi wa makusudi wa watu wenye nia mbaya na Serikali.  Huwezi kudai kuwa mtetezi wa wananchi wa Mtwara kwa hoja za uongo na kufanya upotoshaji wa makusudi kabisa.
  Ndugu Wananchi;
           Ujenzi wa bomba la gesi ndiyo uliozua mzozo wote huu.  Zilijengwa hisia kuwa gesi yote inapelekwa Dar es Salaam na kwamba Mtwara itakosa gesi na maendeleo yatayotokana na gesi hiyo.  Na, wengine wakasema gesi inapalekwa Bagamoyo ili kuzidisha chumvi na kupandikiza chuki kwa wananchi dhidi ya Serikali kwamba Rais anapeleka gesi kwao. Kwanza, Kinyerezi iko Ilala na siyo Bagamoyo.  Pili, ukweli ni kwamba pale Mtwara kuna gesi nyingi ya kutosheleza mahitaji ya Mtwara, Lindi na Dar es Salaam na kubaki.  Gesi itakayoletwa Dar es Salaam ni asilimia 16 tu ya gesi yote iliyoko Mtwara kwa miaka ishirini ijayo.  Hivyo asilimia 84 ya gesi itabaki Mtwara kwa ajili ya kuuzwa nje ya nchi na kupelekwa kwingineko nchini.
           Kwa sababu hiyo, ndugu zetu wa Mtwara hawana sababu ya kuwa na wasiwasi. Ipo gesi ya kutosha kwa mahitaji ya sasa na ya miaka mingi ijayo.  Viwanda vinavyotumia gesi kama mali ghafi na vile vinavyohitaji gesi kama nishati vyote vitapata gesi ya kutosha.  Kwa upande wa uzalishaji umeme hali kadhalika ipo gesi ya kutosha kuzalisha umeme mwingi zaidi.  Hivi sasa tunacho kituo kinachozalisha umeme wa megawati 15 unaotumika Mtwara, Lindi, Tandahimba, Newala, Masasi, Nachingwea, Ruangwa, na Mtama. Bado umeme huo hautumiki wote hivi sasa. 


  Ndugu Wananchi;  
           Nayaeleza yote haya kuwathibitishia wananchi wa Mtwara kuwa tunawathamini sana na kuwajali.  Mimi nitakuwa mtu wa mwisho kuwapuuza na kuwatupa mkono wananchi wa Mikoa ya Kusini.  Aidha, sitakuwa tayari kuwaruhusu watu au mtu ye yote Serikalini kuwapuuza wananchi wa Mikoa ya Kusini au mkoa wo wote hapa nchini.  Hiyo haitakuwa sawa.  Nilishasema siku za nyuma na napenda kurudia tena leo kuwa kwangu mimi hakuna mkoa ulio bora kuliko mwingine.  Ni kutokana na msimamo wangu huo ndiyo maana tumeelekeza nguvu na rasilimali nyingi za Serikali  katika mikoa iliyokuwa inadaiwa kuwa imesahauliwa.  Kazi ya ujenzi wa barabara za lami iliyofanyika na inayoendelea kufanyika katika mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma, Rukwa, Kigoma na Kagera inajieleza yenyewe. Mipango ya kuboresha Kiwanja cha Ndege cha Mtwara kufikia hadhi ya kimataifa na uboreshaji wa viwanja vya ndege vya Lindi na Kilwa ni ushahidi mwingine kati ya mambo mengi tunayoweza kuyataja.   


  Ndugu Wananchi;
           Haya niliyoyasema ni sehemu ndogo tu ya yale yaliyofafanuliwa na kuelezwa kwa kina na Mawaziri na Wakuu wa Idara husika  za Serikali na Mashirika  ya Umma pale Mtwara katika mkutano wa Waziri Mkuu na viongozi wa Serikali, dini, vyama vya siasa na wazee wa Mkoa wa Mtwara tarehe 29 Januari, 2013. 
  Ndugu Wananchi;
  Napenda kutumia nafasi hii kutoa pongezi nyingi kwa Waziri Mkuu, Mheshimiwa Mizengo Pinda, kwa kazi kubwa na nzuri aliyoifanya kule Mtwara.  Uvumilivu wake, usikivu wake na utulivu wake vimesaidia sana kulivusha taifa katika moja ya mitihani mikubwa ambayo ingeikuta nchi yetu tangu Uhuru.  Nawapongeza Mawaziri na Wakuu wa Mashirika ya Umma na Idara za Serikali kwa mchango wao muhimu walioutoa, uliosaidia kufafanua masuala ambayo yalikuwa hayaeleweki vizuri.  Kwa wao nawasisitiza na kuwakumbusha wajibu wao wa kuelimisha jamii kuhusu shughuli wazifanyazo.  Wakifanya hivyo mara kwa mara migongano haitakuwepo na wapotoshaji hawatapata nafasi.
  Ndugu Wananchi;
           Nitakuwa mwizi wa fadhila kama sitawashukuru viongozi wa Serikali, vyama vya siasa, madhehebu ya dini, viongozi wa jamii, wazee, wana-Mtwara na makundi mbalimbali ya jamii, kwa muda waliotumia kuzungumza na Waziri Mkuu na kuwasikiliza wasaidizi wake wakifafanua masuala mbalimbali.  Uvumilivu wao na uelewa wao ndivyo vilivyosaidia kurejesha hali kuwa ya kawaida.  Nawaomba nao sasa, wote kwa pamoja washirikiane na Serikali kuelimisha umma kuhusu ukweli wa mambo.  Pia watumie nafasi hiyo kutahadharisha jamii na kuwataka watu kuwa waangalifu na kupima maneno wanayoambiwa na watu.  Wajiepushe na maneno au vitendo vinavyofarakanisha, kuchonganisha na kupandikiza chuki dhidi ya watu au Serikali. Waambieni kuwa ghasia hukimbiza wawekezaji kwani wakipata hofu kuwa hali ya amani na usalama ni ya mashaka, watatoka kwenda kuwekeza kwingine.  Vyema iwe hapa hapa nchini, lakini wanaweza kwenda nchi nyingine na sisi kupoteza kabisa.
  Ndugu Wananchi;
           Nawapa pole wananchi wa Mtwara na Masasi kwa usumbufu walioupata kutokana na ghasia zilizofanywa.  Nawapa pole waliofiwa na kujeruhiwa.  Nawapa pole waliopoteza au kuharibiwa mali zao.  Kwa kweli inasikitisha na kufadhaisha kuona watu wanafanya vitendo vya kuua, kuchoma moto nyumba za watu na majengo ya Serikali pamoja na , kuharibu na kuiba mali za watu.  Huu ni uhalifu ambao hauna maelezo na haukubaliki.  Tunaviachia vyombo husika vya dola na sheria kutimiza wajibu wao.  Kwa waliohusika iwe fundisho kwao na kwa wengineo kutokubali kutumika kwa maslahi ya watu wengine siku zijazo.  Sasa wameachwa pekee yao wakati wenzao wako huru na kufaidi maisha
  Ndugu Wananchi;  
  Hili sakata la bomba la gesi limefika mahali pazuri.  Yaliyopita si ndwele tugange yajayo.

  Mungu Ibariki Afrika!
  Mungu Ibariki Tanzania!
  Asanteni Sana kwa Kunisikiliza!

  0 0

  Katibu Mkuu wa CCM-Taifa,Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelekezo mafupi kuhusiana na bwawa la umwagiliaji kutoka kwa Injinia wa maji mkoa wa Kigoma,Elinatha Elisha (haonekani pichani).Kinana amefanya ziara ya kuutembelea mradi huo wa umwagiliaji katika kijiji cha Nyendara,Wilayani Kibondo mkoani Kigoma akiwa ameambatana na wajumbe wake wa chama cha CCM. 
  Katibu Mkuu wa CCM-Taifa,Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelekezo mafupi ya mitambo ya umwagiliaji kutoka kwa Injinia wa maji mkoa wa Kigoma,Elinatha Elisha.Kinana amefanya ziara ya kuutembelea mradi huo wa umwagiliaji katika kijiji cha Nyendara,Wilayani Kibondo mkoani Kigoma. 

  Sehemu ya mradi wa Bwawa la umwagiliaji,ambalo Katibu Mkuu wa CCM-Taifa,Ndugu Abdulrahman Kinana alitembelea na kujionea maendeleo yake,kwa mujibu wa Injinia kutoka Ofisi ya Umwagiliaji kanda ya Magharibi mkoani Tabora,Bwa.Bahati Balekele alieleza manufaa ya  Bwawa hilo kwa wakazi wa eneo hilo.alisema kuwa litasaidia katika matumizi ya Kilimo cha Umwagiliaji,Matumizi ya mifugo pamoja na matumizi ya majumbani.
  Katibu Mkuu wa CCM-Taifa,Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na baadhi ya wanakijiji Nyendara,alipokwenda kukagua mradi wa bwawa la Umwagiliaji la Nyendara
  Meneja wa kituo cha uzalishaji Umeme Wilaya ya Kibondo,Damson Lupenza akifafanua jambo mbele ya Katibu Mkuu wa CCM-Taifa,Ndugu Abdulrahman Kinana na wajumbe wake waliofika eneo hilo kwa ajili kukagua maendeleo ya mradi huo wa Umeme.
  Katibu Mkuu wa CCM-Taifa,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa kituo kinachozalisha umeme Wilaya ya Kibondo.
  Mmoja wa mafundi wa kituo cha kuzalisha umeme,Omary Mwinyimkuu akitoa maelezo mafupi kwa Katibu Mkuu wa CCM-Taifa,Ndugu Abdulrahman Kinana (pichani kati),alipokwenda kutembelea mradi wa Umeme,kijiji cha Twabangondozi,Wilayani Kibondo akiwa ameambatana na baadhi ya viongozi wa ngazi ya juu kichama wilayani humo akiwemo mkuu wa Wilaya,Mh Venance Mwamoto.


  Katibu Mkuu wa CCM-Taifa,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa sambamba na ameambatana na baadhi ya viongozi wa ngazi ya juu kichama wilayani humo akiwemo mkuu wa Wilaya,Mh Venance Mwamoto,alipokwenda kutembelea mradi wa ujenzi wa Machinjio katika cha Twabangondozi,Wilayani Kibondo.
  Sehemu ya mradi wa machinjia ya kisasa kabisa,ambao unatarajiwa kukamilika ndani ya mwezi huu na kuanza kutumika.ana alizindua matawi mawili ya CCM wilayani humo.
  Katibu Mkuu wa CCM-Taifa,Ndugu Abdulrahman Kinana akizindua tawi la umoja wa vijana wa CCM Wilayani Kibondo.Ndugu Kinana alizindua matawi mawili ya CCM wilayani humo.

  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akimkabidhi kijana wa kundi la muziki wa Bongo Fleva, mbuzi ambaye alimnunua kwa sh. milioni tatu, kwenye mnada aliofanya kwa ajili kupata fedha za kupeleka shule watoto wa wazazi kumi wasio na uwezo katika Wilaya ya Kibondo ambao wameshajitokeza. Mbuzi huyo ametolewa na Mkuu wa wilaya hiyo, Venance Mwamoto.Pichana na JIACHIE BLOG.

older | 1 | .... | 20 | 21 | (Page 22) | 23 | 24 | .... | 1904 | newer