Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live

MJASIRIAMALI WA SABUNI ZA MAJI ATIMKA NA MILIONI 30 ZA VODACOM

0
0
 Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Bw.Matina Nkurlu(katikati)akishuhudiwa na Msimamizi wa bodi ya  Michezo ya kubahatisha nchini,Bw.Humudi Abdulhussein(kushoto)wakati akimpigia mshindi wa droo kubwa ya mwezi ya promosheni ya  Timka na Bodaboda Bi.Jovita Mosha(44)mkazi wa Ubungo external jijini Dar es Salaam aliyeibuka na kitita cha shilingi Milioni 30.kulia ni Mkuu wa kitengo cha Mtandao  na huduma za ziada wa kampuni hiyo Bw.Charles Matondane. 
 Msimamizi wa bodi ya  Michezo ya kubahatisha nchini,Bw.Humudi Abdulhussein(kushoto)pamoja na Mkuu wa kitengo cha mtandao na huduma za ziada wa Vodacom Tanzania Bw.Charles Matondane(kulia)wakifurahia jambo wakati Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Bw.Matina Nkurlu(katikati)alipokuwa akiongea na mshindi wa droo kubwa ya mwezi ya promosheni ya  Timka na Bodaboda Bi.Jovita Mosha(44)mkazi wa Ubungo external jijini Dar es Salaam aliyeibuka na kitita cha shilingi Milioni 30.Promosheni hiyo imebadilisha maisha ya watanzania zaidi ya 700.
 Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Bw.Matina Nkurlu,akisisitiza jambo kwa   waandishi wa Habari (hawapo pichani)kuhusiana napromosheni hiyo ilivyobadilisha maisha ya wateja wao na watanzania kwa ujumla,mara baada ya kumtangaza mshindi wa droo kubwa ya mwezi ya"promosheni ya  Timka na Bodaboda" Bi.Jovita Mosha(44)mkazi wa Ubungo external jijini Dar es Salaam aliyeibuka na kitita cha shilingi Milioni 30.

WAZIRI MKUU PINDA ATEMBELEWA NA UJUMBE WA MUUNGANO WA UTEPE MWEUPE

0
0
 David Lamuya kutoka Muungano wa  Utepe  Mweupe  (THE WHITE RIBBON ALLIANCE ) akimvisha utepe mweupe Waziri mkuu  Mizengo Pinda wakati ujumbe huo ulipomtembelea ofisini kwake leo. Kampeni yao inaitwa Wajibika  Mama Aishi.

Waziri mkuu Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka Muungano wa Utepe Mweupe walipo mtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es salaam  .Muungano wa Utepe Mweupe wanaedesha kampeni inayoitwa   Wajibika Mama Aishi.       (PICHA ZOTE  NA OFISI YA WAZIRI MKUU)


SMZ YASHAURIWA KUIMARISHA HALI YA USALAMA WA ENEO LA NYARAKA

0
0
Na Miza Kona   -Maelezo Zanzibar       

Serikali ya Mapinduzi imeshauriwa kuimarisha hali ya usalama wa eneo la Nyaraka kwa kuweka kamera za kuangaza usalama kwa ukaribu CCTV ili kuepusha wizi  usitokee katika Idara hiyo.

Akiwasilisha Muhtasari wa Ripoti ya Kudumu ya Katiba, Sheria na Utawala ya Baraza La Wawakilishi kwa mwaka wa Fedha 2013/2014 Mwenyekiti wa Kamati hiyo Ussi Jecha Simai amesema kuwekwa vyombo vya usalama katika idara hiyo kutasaidia kuepusha kuibiwa kwa nyaraka za Taifa na kuipatia hasara nchi.

Aidha amesema Kamati imesikitishwa na na taarifa za wizi wa nyaraka muhimu uliotokea katika Idara na kusisitiza kuwekwa kwa vyombo vya CCTV ili kuweza kubaini wizi huo unapofanyika.  Pia Kamati hiyo wameomba serikali kupitia vyombo vyake usalama kufanya uchuzi wa tukio hilo kwa kila aliyehusika na wizi wa nyaraka kuchukuliwa hatua za kisheria.

Hata hivyo Kamati hiyo imeitaka serkali kuandaa mpango wa kuzifanyia ukaguzi Nyaraka zote  zikiwemo Ofisi ya Vizazi na Vifo pamoja na Wakfu na baada ya muda na ripoti yake ipelekwe katika Baraza ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Wizara.

“Hivi sasa Idara ya Nyaraka imefanywa kama vile ni eneo la kuhifadhia vitu vya kale visivyohitajika tena, eneo lenyewe lipo katika hali hatarishi kiusalama, jengo finyu,halitoshelezi kuhifadhi kwa ufanisi nyaraka nyingi zilizomo”,alieleza. 

Aidha alifahamisha kuwa ustawi wa kiafya kwa wafanyakazi wa Taasisi hiyo upo katika hali ya hatari kutokana na mazingiramagumu  wanayofanyia kazi  kwa kukosa vifaa muhimu ikiwemo ukosefu wa vipoza hewa katika vyumba vya kuhifadhia Nyaraka.

Akichangia Ripoti ya Kamati hiyo Mwakilishi wa Jimbo la Kitope Makame mshimba Mbarouk amesema wizi wa nyaraka umesababishwa kudharauliwa na kutothaminiwa kwa nyaraka za asili pamoja na ukosefu wa vifaa muhimu wa kuchunguza na kubaini wizi unafanyika  hivyo serikali ichukuwe  hatua za kisheria kwa yoyote atakaehusika na wizi huo.

Aidha ameiomba serikali kuanzisha Mahakama za wawekezaji ambazo zitaweza kutekeleza kazi zake ili kuepusha unyang’anyi wa ardhi pale wanapokuja kuwekeza na kupata haki zinazostahiki.   
            
IMETOLEWA NA IDARA YA HABRI MAELEZO                                                                       

RAIS KIKWETE AZINDUA KONGAMANO LA KILIMO AFRICA MASHARIKI

0
0
  
 :Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea kitabu cha Mandela toka kwa Mkurugenzi wa Programu wa Spintelligent ya Afrika Kusini Bi. Amore Swart baada ya kufungua rasmi kongamano la Kilimo Afrika Mashariki katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo Januari 28, 2014.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo toka kwa Bi Meab Mdimi wa Kampuni ya Kilimo ya TECHNOSERVE  baada ya kufungua rasmi kongamano la Kilimo Afrika Mashariki katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo Januari 28, 2014.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo katika banda la Mpango wa Kuendeleza Sekta ya Kilimo Kusini mwa Ukanda wa Afrika (SAGCOT)    baada ya kufungua rasmi kongamano la Kilimo Afrika Mashariki katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo Januari 28, 2014.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati wa kufungua rasmi kongamano la Kilimo Afrika Mashariki katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo Januari 28, 2014. PICHA NA IKULU.

UVCCM YAUNGA MKONO KAZI ZA SEKRETARIETI YA CHAMA CHA MAPINDUZI

0
0
 Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi, Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
 Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo.
  Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi, Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, wakati akitoa tamko la Jumuiya ya Vijana wa CCM kuunga mkono kazi ya sekretarieti ya Chama cha Mapinduzi chini ya Katibu Mkuu, Mh. Abdulrahaman Kinana. 
DAR ES SALAAM, Tanzania


JUMUIYA ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) imeunga mkono kazi zinazofanywa na sekretarieti ya chama cha Mapinduzi chini ya Katibu Mkuu Abdulrahaman Kinana huku ikiwatupia lawama baadhi ya vigogo kutokana na kukwamisha juhudi hizo.


Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi, Paul Makonda amesema, vijana wa UVCCM wanatambua na kuthamini juhudi za Katibu Mkuu na Sekretarieti yake katika kukijenga chama kwa kusimamia barabara misingi na shabaha ya kuundwa kwake.

Makunda alisema, inapofika wakati wasimamizi wa chama wanapoanza kupigwa  vita juu ya kusimamia kanuni za chama hii siyo sahihi.


“Haiwezekani matajiri na watu wenye uchu wa madaraka watake kukihodhi na waratibu mikakati ya kukihujumu kwa pesa zao hali sisi vijana tukitazama, tunasema kutakilinda chama chetu na tutawalinda viongozi wetu waadilifu”Alisema.


Hata hivyo Makunda alisema, wanaobezwa leo  kuwa wanaharibu chama ndiyo wameweza kurudisha imani ya wananchi kwa chama , imani na matumaini ambayo tayari yalishaanza kupotea na chama kuonekana si tena cha wanyonge, wakulima na wafanyakazi wa nchi hii.


Aidha Makunda alisema, mtu anayebeza ziara zilizofanyika na kuwaita viongozi walizozifanya ziara hizo ni waropokaji na wahuni anapaswa kuchukuliwa hatua kali za kinidhamu ili iwe fundisho kwa wengine.


“Muhuni ni mtu mjinga, mtu wa hovyo, hana maadili, asiyependa chama, mhaini na mzandiki anayepaswa kuchukuliwa hatua kali za kinidhamu ili iwe fundisho kwa wengine” Alisema Makonda.

CCM CHAENDELEA KUMNADI MGOMBEA WAKE KATIKA KAMPENI ZA UCHAGUZI MDOGO WA JIMBO LA KIEMBESAMAKI ZANZIBAR

0
0
 Mwenyekiti wa Mkoa wa magharibi kichama Yussuf Muhammad Yussuf     akimnadi mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mahmoud Thabit Kombo katika kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki zilizofanyika Bustani ya Kiembesamaki, Wilaya ya Magharibi Unguja.
 Baadhi ya wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wakimsikiliza Mwenyekiti wa Mkoa wa magharibi kichama Yussuf Muh’d Yussuf (hayupo pichani) katika kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki katika kiwanja cha Bustani ya Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi Unguja.

 Mgombea Uwakilishi wa Jimbo la Kiembe Samaki Mahmoud Thabit Kombo akimpa maiki mwanawe Sukainnah Mahmoud Thabit awasalimie wanachama wa (CCM) katika kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki zilizofanyika Bustani ya Kiembesamaki, Wilaya ya Magharibi Unguja.

Mgombea Uwakilishi wa Jimbo la Kiembe Samaki Mahmoud Thabit Kombo akiwahutubia wananchi waliofika katika kampeni zake katika kiwanja cha Bustani ya Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi Unguja leo. 
Picha na Makame Mshenga wa Maelezo Zanzibar

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA WAZIRI WA FEDHA NA MANAIBU WAKE IKULU DAR.

0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Waziri wa Fedha, Saada Mkuya wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Jan 28, 2014 kwa mazungumzo, akiwa ameongozana na manaibu wake, Mwiguku Nchemba na Adam Malima
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mkurugenzi wa Kampuni ya Statoil Tanzania Oystein Michelsen, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Jan 28, 2014 kwa mazungumzo. Kushoto ni Meneja wa Biashara wa Kampuni ya Statoil Tanzania, Oivind Holm.
 -Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Waziri wa Fedha, Saada Mkuya na manaibu wake, Mwigulu Nchemba na Adam Malima, wakati walipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Jan 28, 2014 kwa mazungumzo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni ya Statoil Tanzania Oystein Michelsen (wa pili kushoto) Meneja wa Biashara wa Kampuni ya Statoil Tanzania, Oivind Holm (wa pili kulia) Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa kampuni hiyo, Genevieve Kisanga (kulia) na Msaidizi wa Mkurugenzi, Grace Usara baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na OMR 

BARAZA LA MADIWANI MAKETE LAPITISHA RASIMU YA BAJETI 2014/2015

0
0
 Baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya Makete likiendelea.
 Diwani wa kata ya Matamba mh. Asheli Mwalyoyo akichangia hoja
 Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Makete Mh. Daniel Okoka akiongoza kikao hicho
 Mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro akitoa ufafanuzi kuhusu suala la leseni katika baraza hilo.
 Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Makete ambaye pia ni katibu wa kikao hicho Bw. Iddi Nganya akisoma taarifa ya rasimu ya bajeti ya halmashauri yake kwa mwaka 2014/2015.
 Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Makete Francis Chaula akisikiliza kwa makini hoja za madiwani katika kikao hicho.
Baraza maalum la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Makete mkoani Njombe leo Januari 28 limejadili na kupitisha rasimu ya bajeti ya halmashauri hiyo kwa mwaka 2014/2015

Katika kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Makete madiwani hao wamejadili hoja mbalimbali zilizopo katika rasimu hiyo ikiwemo uboreshaji wa namna ya kuongeza mapato kutoka kwenye vyanzo vyote vilivyoainishwa na halmashauri hiyo

Baadhi ya hoja zilizochangiwa na madiwani hao ni pamoja na halmashauri kuwa na vyanzo vya kukusanya mapato lakini kumekuwa na tatizo la mapato hayo kutofika kama yalivyokusanywa wakimaanisha kumekuwepo na kukosekana kwa uaminifu kwa baadhi ya watendaji wanaokusanya mapato hayo

Diwani wa kata ya Matamba (CCM) Mh. Asheri Mwalyoyo ametolea mfano katika kata yake kuwa kumekuwepo na ukusanyaji wa mapato lakini taarifa zinazofika wilayani zinaonesha yamekusanywa mapato kidogo ilihali ana uhakika yamekusanywa mengi

"Tuchukulie kwenye kata yangu ya Matamba ushuru tu wa pombe kwa vilabu 10 tu ni shilingi 60,000/- kwa mwezi lakini kwenye taarifa huku wilayani inaonesha ushuru wa pombe za kienyeji ni 70,000/- sasa hii inashangaza maana tuna vilabu vingi, hapa ni kukosekana kwa uadilifu wa baadhi ya watendaji wanaokusanya mapato hayo" alisema Mwalyoyo

Naye diwani wa kata ya Tandala Mh. Egnatio Mtawa ameshangazwa na hatua ya rasimu hiyo kuonesha kutegemea kwa kiasi kikubwa mapato ya pombe na kudai kuwa wahusika wote wakiwemo watendaji na wao kama madiwani walikuwa wavivu wa kufikiri kubuni vyanzo vipya vya kukusanya mapato badala ya kutegemea ushuru wa pombe kwa kiasi kikubwa

Amesema hii inaashiria wananchi wazidi kunywa pombe kwa wingi ili mapato yapatikane lakini pia njia hiyo itachochea vilabu na baa kufunguliwa mapema tofauti na sheria inavyoruhusu hivyo kupata wingi wa wananchi watakao kuwa wamelewa muda wote hasa muda wa kufanya kazi

Aidha rasimu hiyo pia imeainisha vyanzo vipya vitakavyosaidia kuongeza mapato ya halmashauri ikiwemo ushuru wa majengo ambapo watu waliokwisha jenga nyumba tayari watakuwa wanalipia ushuru wa jengo kwa mwaka na wale ambao bado wana mpango wa kujenga watalipia kabla ya ujenzi kuanza

Halmashauri ya wilaya ya Makete ni miongoni mwa wilaya ambayo ina vyanzo vichache vya mapato hali inayosababisha upatikanaji wa mapato yake kuwa mdogo, hivyo inaendelea kubuni vyanzo vipya ili mapato yake yaweze kuongezeka zaidi ya sasa

Na Edwin Moshi, Makete

Mwanafunzi Chuo cha Ardhi atoa changamoto kwa vijana kupitia kitabu chake Dar es Salaam

0
0
 Nguku anaelezea kwamba kitabu hicho yenye kauli mbiu “Sio Serikali ni Mimi, Wewe na Sisi,”inatoa hamasa kwa watu hasa hasa kundi la vijana waweze kuwa na uthubutu wa kutimiza malengo yao katika maisha. Wanaoshuhudia ni mama yake mkubwa Bi. Anna Kikwa na baba yake mdogo Bw. Emmanuel Mallewo.
   Bi. Kikwa (kushoto) na Bw. Mallewo wakionyesha kitabu cha 'Safari Ya Ndoto' alichokiandika mwanao Aman (katikati) anayesoma shahada ya uchumi mwaka wa tatu katika chuo kikuu cha Ardhi.
Mtunzi wa kitabu cha 'Safari Ya Ndoto' Aman Nguku akihojiwa na waandishi wa habari katika uzinduzi wa kitabu hicho jana. Wanaoshuhudia ni walezi wake Bi. Kikwa na Bw. Mallewo.



=====  =======  ======
Vijana wakitanzania wameaswa kuacha kulalamika na kuishi katika maisha ya nadharia, badala yake wameshauriwa kubadilika kuwa watendaji na wenye uthubutu wa kutimiza malengo yao katika maisha. Maneno hayo yalisemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Amajat Investment Bw. Aman Nguku jijini Dar es Salaam jana katika uzinduzi wa kitabu chake kiitwacho ‘Safari Ya Ndoto’ inayobeba kauli mbiu “Sio Serikali ni Mimi, Wewe na Sisi.” 
 Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Bw. Nguku alisema imefika wakati sasa watanzania hasahasa kundi la vijana waamke kutoka usingizini na kutimiza malengo yao ya kimaisha ambayo wanapenda kufikia. 

 “Imetosha kusema kesho, kufikiri bila kutenda na kuongea bila vitendo. Kinachotakiwa ni kuanza utekelezaji,” alinukuu Bw. Nguku kutoka kwenye kitabu chake chenye kurasa 108. Akielezea madhumuni ya kuandika kitabu hicho, Bw. Nguku ambaye pia ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu anayesomea shahada ya Uchumi katika Chuo Kikuu cha Ardhi jijini Dar es Salaam alisema: 

 “Hiki kitabu ni mahususi kwa wale watu ambao wana ndoto mbali mbali katika maisha yao lakini hawajui pakuanzia, iwe ndoto ya kuwa mfanyabiashara maarufu, mwanasiasa au daktari bingwa. Hiki kitabu ni ramani maalum kwao.” 

 Aliendelea, “Kitabu hiki kinaweza pia kuwa changamoto kwa wale ambao wamekata tamaa katika maisha. Kwa kusoma maandishi ya kitabu hiki, wanaweza wakafufua ndoto zao na kufanikiwa katika yale waliyoyapanga.” 
 ‘Safari Ya Ndoto’ pia inabeba dondoo kutoka kwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, mfanyabiashara maarufu Bw. Reginald Mengi na Mkurugenzi Mtendaji wa Helvetic Solar Contractors Bw. Patrick Ngowi. 
 Kitabu hiki kinasambazwa katika maduka mbali mbali jijini Dar es Salaam na nchi nzima ili watanzania wengi wapate kukisoma. Kinauzwa kwa Tsh 5000 tu. Kwa sasa, mtunzi Nguku pia anaandika vitabu vingine viwili venye vichwa ‘Ndogo lakini muhimu, kesho’ na ‘What is life for!’ (Maisha ni ya nini!).

MAANDALIZI YA SHEREHE ZA MIAKA 37 YAPAMBA MOTO MKOANI MBEYA

0
0
 Katibu wa CCM Mkoa wa Mbeya Luteni Mstaafu Maganga Sengelema akifafanua jambo mbele ya Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kwenye uwanja wa Sokoine mjini Mbeya ikiwa sehemu ya maandalizi ya sherehe za miaka 37 ya CCM ambayo kitaifa mwaka huu inafanyika mkoani Mbeya.
 Katibu wa CCM Mkoa wa Mbeya Ndugu Maganga Sengelema akimuonyesha Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye sehemu ya kuweka jukwaa la waandishi wa habari kwenye uwanja wa Sokoine ambapo sherehe za miaka 37 ya CCM zitasheherekewa kitaifa.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akifafanua jambo wakati wa maandalizi ya awali katika uwanja wa Sokoine ambao unategemewa kufanyika kwa sherehe za mika 37 ya CCM tarehe 2 mwezi wa februari mwaka huu,mgeni wa heshima anategemewa kuwa Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishiriki kurekebisha uwanja wa Sokoine ili uweze kutumika vizuri wakati wa sherehe za miaka 37 ya CCM . Picha na Adam H. Mzee

NEW ARRIVALS @AK CLASSIC COSMETICs

0
0
 KILA SIKU WANAKUJA NA MAMBO TOFAUTI NA MAKUBWA ZAIDI.WALE MABINGWA WA COSMETICS ORIGINAL KABISA KUTOKA MBELE MBELE, @AK CLASSIC COSMETICS  WAMEWASHUSHIA TENA MADINI MAPYAA KABISA!!  KUANZIA PRODUCTs ZA KUPUNGUA,TIBA ZA CHUNUSI,PRODUCTs ZA KUNG'ARISHA NGOZI YAKO,DAWA ZA KUONDOA STRETCH MARKS, BODY SHAPERs,LACEWIGS...NA BIDHAAA ZINGINE LUKUKI MUPYAAAAAA!!EM TUONGOZANE HAPA..

 KWA MAELEZO YA KINA NA PICHA ZAIDI WATEMBELEE BLOGUNI www.akclassic.blogspot.com
 KUWEKA ODA NA KUFIKISHIWA BIDHAA MPAKA ULIPO PIGA  0753-482909/0713-468393.
WAPO KINONDONI KWA MANYANYA NA SINZA KUMEKUCHA.

KARIBUNI SANA.

NAPE AJICHANGANYA WA WANANCHI SOKO LA MWANJELWA MBEYA

0
0
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa  Nape Nnauye akicheza draft na vijana wafanyabiashara wa soko la Sido Mwanjelwa jijini Mbeya. Nape yupo mjini Mbeya kwa ajili ya maandalizi ya sherehe za miaka 37 ya CCM ambazo kitaifa zitasheherekewa mkoani hapo.Katibu wa NEC alikutana na vijana mbali mbali ambao walifurahi sana kumuona kiongozi wao akiwa pamoja nao kiasi soko zima lilipuka kwa nyimbo za hamasa za CCM zilizoimbwa na Kapteni John Komba,Nape pia alipata fursa ya kusalimiana na baadhi ya madereva wa Taxi wa kituo maarufu cha Mafiati.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akila chakula cha mchana kwenye kibanda cha Mama Lishe anayefahamika kama Bi. Tandiwa Tewete kwenye soko la Sido Mwanjelwa mjini Mbeya.
 
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akikatiza katikati ya soko la Sido Mwanjelwa kwenda kwenye viwanja vya mpira vya soko hilo kushuhudia mechi ya mpira ya wafanyabiashara wa sokoni hapo.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akiangalia mechi ya mpira kati ya timu ya soka ya sokoni Sido wauza Mitumba na wafungua Mabelo kwenye uwanja wa mpira wa sokoni Sido.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa timu za mpira sokoni Sido Mwanjelwa mjini Mbeya mara baada ya mpira kumalizika.

KAMPUNI YA REX ENERGY YATAMBULISHA TEKNOLOJIA MPYA YA KUHIFADHI NA KUSAMBAZA UMEME.

0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya kusambaza vifaa vya umeme wa jua (solar) ya Rex Energy Bw Francis Kibhisa akizungumza na Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali (hawapo pichani),kuhusiana na uzinduzi na utambulisho wa teknolojia  mpya yenye uwezo mkubwa wa kuhifadhi na kusambaza Umeme,mkutano huo umefanyika mapema leo asubuhi kwenye makao makuu ya ofisi hizo zilizopo mtaa wa Makamba,Gerezani jijini Dar.
Pichani mbele kushoto ni Ofisa Mauzo wa kampuni ya Rex Energy,Bwa.Medard Rweikiza pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo,Bwa.Francis Kibhisa wakiwaonesha na kuwaeleza baadhi ya Waandishi wa Habari namna moja ya kifaa cha kisasa kabisa chenye uwezo mkubwa wa kuzalisha umeme kwa kutumia Mwanga wa Jua (Solar).Kwa habari zaidi ingia www.rexsolarenergy.com
 Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Rex Energy,Bwa.Francis Kibhisa akitoa ufafanuzi wa namna moja ya kifaa (pichani),kinachotumia teknolojia ya kisasa katika suala zima la kuzalisha umeme kwa kutumia mwanga wa jua (Solar Power) mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani),Bwa.Francis alibainisha kuwa kifaa hicho kina uwezo wa kuwasha vifaa vya ndani kama vile taa,redio, friji, TV kwa wakati mmoja,na huuzwa kwa gharama nafuu.Pichani kulia ni Ofisa Mauzo wa kampuni ya Rex Enegy,Bwa.Medard Rweikiza akisikiliza
Baadhi ya  Wafanyakazi wa Kampuni ya Rex Energy wakiwa katika picha ya pamoja mara baada kumaliza mkutano wao na Waandishi wa habari mapema leo asubuhi.

Airtel yajipanga kwa droo kubwa ya milioni 50/- ya ‘Mimi ni Bingwa’

0
0
Afisa Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jane Matinde akisisitiza jambo wakati akichezesha droo ya kumi ya promosheni ya Mimi ni Bingwa liyofanyika jana katika ofisi za makao makuu ya Airtel jijini Dar es salaam. Kushoto ni Muwakilishi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha Bw. Emmanuel Ndaki.

WAKATI washindi wa tiketi wa awamu ya kwanza ya promosheni ya ‘Mimi ni Bingwa’ wakitarajiwa kuwasili nchini Alhamis, kampuni hiyo ya simu imechezesha droo nyingine na kumchagua mkazi wa jijini Dar es Salaam, Msemwa George Makuzi kuwa mshindi wa tiketi mbili za kwenda Old Trafford katika wiki ya kumi ya droo hiyo.

Akizungumza mara baada ya droo hiyo, Afisa Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jane Matinde alisema kilele cha promosheni hiyo kinakaribia, ambacho tutashuhudia mshiriki wa ‘Mimi ni Bingwa’akiondoka na kitita cha shilingi milioni 50 katika droo kubwa itakayohusisha kila aliyejisajili katika promosheni hiyo.

“Tukiwa tunafikia kilele cha promosheni ya ‘Mimi ni Bingwa’, nataka niwahakikishie wateja wote wa Airtel kuwa washiriki wapya bado wanakaribishwa kutokana na kuwa mshindi wa pesa taslim ya milioni 50 atapatikana kupitia droo ya bahati nasibu.

“Kupitia droo hii kubwa, ndiyo tutajua ni nani ataondoka na zawadi kubwa ya ‘Mimi ni Bingwa’. Kutokana na vigezo na masharti ya promotion hii, kila namba iliyosajiliwa kwa ajili ya promosheni, hata kama mshiriki alijibu swali moja tu, ataingia katika droo kubwa.

“Hii sasa ni nafasi kwa wateja wa Airtel ambao hajajisajili kwenye promosheni kujisajili kwa kutuma ujumbe mfupi (SMS) wenye neno “BINGWA” kwenda namba 15656, na kujibu maswali mengi iwezekanavyo, na unaweza kuwa mshindi wa zawadi kubwa ya shilingi milioni 50 au zawadi nyingine za milioni 1 kila siku na milioni 5 kila wiki kwa wiki zilizobaki,” alisema Jane.

Alisema kuwa ‘Mimi ni Bingwa’ imeonyesha mafanikio makubwa kwa kuwa imepokelewa vizuri na wateja waliojisajili kwa wingi na kujikusanyia pointi kwa kujibu maswali mengi yaliyorahisi yanayoulizwa.

Jane aliongeza kuwa Airtel itaendelea kuanzisha promosheni na kampeni mbali mbali zinazolenga kuwazawadia wateja wake pamoja na kuyabadilisha maisha yao na kuwa washiriki mahiri wa kuubadilisha uchumi wa Tanzania.

Alibainisha kuwa washindi wote wa tiketi za safari iliyogharamiwa kila kitu ya kwenda Old Trafford watasafiri kabla ya mwisho wa mwezi wa Februari, huku akiongeza kuwa mkakati ni kuwawezesha washindi kwenda Uingereza katika awamu tatu tofauti.

Katika droo hiyo ya wiki ya kumi, Bi Hawa Mohammed Hussein kutoka Tanga na Godlove William Kayonga kutoka Mara walijishindia shilingi milioni 5 kila mmoja na washindi wengine 12 kujinyakulia shilingi milioni 1 kila mmoja.

Washindi wengine wa tiketi za ‘Mimi ni Bingwa’ ni pamoja na Edwin Edmund Kajimbo kutoka Iringa, Michael Joseph Shirima kutoka Kinondoni jijini Dar es Salaam, Bw. Shaibu Rashid Dege, Mtendaji wa kijiji cha Nang’olo wilayani Kilwa – mkoani Lindi, Leonard Dickson Lyatuu kutoka Arusha, Joseph Steven Mambo kutoka Kawe jijini Dar es Salaam, Emmanuel Mahenge Jacob kutoka Njiro in Arusha, Rashid Jacob Kagombola kutoka Bukoba mkoani Kagera, Harrison Wilson Mwambogolo kutoka Kigogo jijini Dar es Salaam na Salma Farid Mughery kutoka Dar es Salaam.

KUELEKEA KILELE CHA MIAKA 37:CCM YAJIVUNIA MAFANIKIO YAKE

0
0
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mkutano wa CCM Mkoa wa Mbeya.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisisitiza jambo wakati akijibu baadhi ya maswali ya waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano katika ofisi za CCM Mkoa wa Mbeya.


 Wakati CCM inatimiza miaka 37 tangia kuanzishwa kwake februari 5 mwaka 1977,Chama hicho kinajivunia sana mafanikio makubwa kiliyopata hasa katika kudumisha Umoja na Mshikamano kwa  Watanzania ,kutunza na kuilinda Amani ya nchi hii na kujenga misingi imara ya uchumi wa nchi,akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano CCM Mkoa wa Mbeya Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye  alisema  sherehe za miaka 37 zimeanza nchi nzima na zilizinduliwa rasmi tarehe 26 na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) Dk.Ali Mohamed Shein Unguja Zanzibar.


  Kilele cha sherehe hizi  kitakua tarehe 2 februari ,Nape alisema “kwa nini tarehe mbili na sio tano ni kwa sababu tarehe tano ni siku ya kazi hivyo tumeona tufanye tarehe mbili ili tuwaruhusu watu wengi zaidi waweze kushiriki” Sherehe hizi zitahitimishwa hapa jijini Mbeya kwenye uwanja wa Sokoine na zitahitimishwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete.


Viongozi mbali mbali wa Kitaifa wa CCM wameanza kuwasili na kesho anategemewa kuwasili Makamu Mwenyekiti  wa CCM (Bara) Ndugu Philip Japhet  Mangula ambaye pia ni mlezi wa mkoa wa Mbeya  akitanguliwa na Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana.


  Nape alisema “Tarehe 2 asubuhi saa moja kutakuwa na matembezi ya mshikamano yatakayoongozwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama ,Rais Jakaya mrisho Kikwete matembezi hayo yatafanyika kwenye jiji la Mbeya yataanzia eneo la Soweto na yataishia kwenye ofisi za CCM mkoa wa Mbeya, baada ya matembezi hayo wananchi watakwenda kwenye viwanja vya Sokoine ambapo kutakuwa na burudani mbali mbali vikiongozwa na TOT, Vikundi vya muziki wa kizazi kipya, sherehe hizo zitaonyeshwa moja kwa moja na baadhi ya televisheni pamoja na kurushwa moja kwa moja na baadhi ya radio.


Wakazi wa Mbeya waombwa kujitokeza kwa wingi wakati wa mapokezi ya Mwenyekiti wa  Chama Cha Mapinduzi  tarehe moja na pia washiriki kwenye matembezi na sherehe zitakazofanyika tarehe2.


Maadhimisho ya sherehe hizi yataambatana na shughuli mbali mbali nchi kote ,ikiwa pamoja na shughuli  za utunzaji wa mazingira kama kupanda miti,kushiriki shughuli za maendeleo kujenga shule na zahanati,usafi  pamoja na kutembelea wagonjwa hospitalini.

Waziri Muhongo apata ugeni kutoka nchini Ufaransa

0
0
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akiwa pamoja na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Marcel Escure (kulia kwa Waziri) pamoja na Waziri Mstaafu wa Viwanda na Nishati wa Ufaransa Bw. Eric Besson (kulia kwa Balozi), pamoja na watendaji kutoka Ubalozi wa Ufaransa na Wizara ya Nishati na Madini, wakati walipomtembelea wizarani ili kufahamu fursa za uwekezaji katika sekta hizo.
Waziri wa Nishati na Madini , Profesa Sospeter Muhongo (wa kwanza kulia) , Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Marcel Escure (kulia kwa Waziri), Waziri mstaafu wa Viwanda na Nishati kutoka nchini Ufaransa Bw. Eric Besson (kulia kwa Balozi), pamoja na mtendaji kutoka Ubalozi wa Ufaransa nchini, wakifurahia jambo mara baada ya kumaliza mazungumzo yaliyolenga katika kuendeleza sekta za Nishati na Madini nchini.

Na Teresia Mhagama

Balozi wa Ufaransa nchini Bw. Marcel Escure akiongozana na Waziri mstaafu wa Viwanda na Nishati kutoka nchini Ufaransa, Bw. Erick Besson wamemtembelea wizarani Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ili kufahamu fursa za uwekezaji katika sekta za Nishati na Madini.

Waziri huyo mstaafu wa Ufaransa, Bw.Erick Besson alikuwa akiiwakilisha kampuni ya GDF Suez ya Ufaransa.

Katika suala la usimamizi wa bomba la gesi asilia, Profesa Muhongo alimweleza Bw. Besson kuwa Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) litahitaji kupata uzoefu na pengine mbia aliyebobea katika usimamizi wa bomba hilo atakayeshirikiana na TPDC katika usimamizi wa bomba la gesi nchini.

Kuhusu umeme, Waziri Muhongo alimweleza Waziri mstaafu huyo wa Ufaransa kwamba serikali inajikita katika miradi ya usambazaji umeme kwa utaratibu wa ubia au mikopo ya bei nafuu na ina mpango wa kujenga njia ya umeme ya msongo wa 400kv kuelekea ziwa Tanganyika hivyo aliikaribisha kampuni ya GDF Suez kuwekeza katika miradi hiyo ya usambazaji umeme.

Aidha Profesa Muhongo alimweleza Bw. Besson kuwa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) linatafuta mbia watakayeshirikiana naye katika kuendesha mtambo wa kuzalisha umeme kwa kutumia makaa ya mawe, Kiwira mkoani Mbeya hivyo kama wana nia ya kuwekeza katika eneo hilo pia wanakaribishwa kuingia katika ushindani wa kupata nafasi hiyo.

Naye Waziri mstaafu wa Viwanda na Nishati kutoka nchini Ufaransa, Bw. Besson alimshukuru Profesa Muhongo kwa taarifa nzuri kuhusu fursa za uwekezaji nchini na ameahidi kupata taarifa zaidi za uwekezaji katika mashirika ya TPDC, STAMICO na TANESCO ili kuona jinsi kampuni ya Suez itakavyoshirikiana na mashirika hayo katika kuendeleza sekta za Nishati na Madini.

Waziri Mkuu wa Finland apokewa Rasmi ikulu-Afanya mazungumzo na Rais Kikwete

0
0
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha waziri Mkuu wa Finland Jyrki Katainen katika viwanja vya ikulu jijini Dar es Salaam leo.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Waziri Mkuu wa
Finland Jyrki Katainen wakipokea heshima katika jukwaa wakati wa mapokezi rasmi yaliyofanyika viwanja vya ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
 Waziri Mkuu wa Finland Jyrki Katainen akiikwetkagua gwaride la heshima liliandaliwa na jeshi la wananchi wa Tanzania wakati wa mapokezi rasmi yaliyofanyika katika viwanja vya ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi. 
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimuongoza mgeni wake Waziri Mkuu wa Finland Jyrki Katainen kukagua ngoma za utamaduni katika viwanja vya ikulu.  
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Waziri Mkuu wa Finland Jyrki Katainen wakikutana kwa faragha ikulu jijini Dar es Salaam leo.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza ujumbe wa Tanzania katika mazungumzo rasmi na mgeni wake Waziri mkuu wa Finland Jyrki Katainen ikulu jijini Dar es Salaam leo.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na mgeni wake Waziri Mkuu wa Finland Jyrki Katainen mara baada ya kufanya mazungumzo rasmi ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Waziri Mkuu huyo yupo nchini Tanzania kwa ziara ya siku mbili(picha na Freddy Maro)

LG YAZINDUA TV AINA YA OLED AMBAYO NIYA KWANZA KWA UBORA DUNIANI

0
0
image.jpeg
Bw. Valerian Banda ambaye ni msemaji wa Kampuni ya Garnet Star ambao ni wasambazaji wa vifaa vya LG akiongea kuelezea TV ya kwanza ulimwenguni aina ya OLED ambayo ndiyo imeingia katika soko ya nchini Tanzania.
image.jpeg
 Mkurugeni wa Kampuni ya Garnet Star ambao ni wasambazaji wa bidhaa za LG, Tanzania, Rajesh Kumar (kulia) na Meneja Masoko wa LG, Shakti Vellu (kulia) wakisaidia kuzindua TV ya kwanza ulimwenguni aina ya OLED ambayo ndiyo imeingia katika soko ya nchini Tanzania. Uzinduzi huo ulifanyika katika duka lao lililoko Quality Center jijini Dar es Salaam.
image.jpeg
Bw. Valerian Banda ambaye ni msemaji wa Kampuni ya Garnet Star ambao ni wasambazaji wa vifaa vya LG akionyesha miwani ya 3D inayotumika kuangalia kwa TV ya kwanza ulimwenguni aina ya OLED ambayo ndiyo imeingia katika soko ya nchini Tanzania.

LG imezindua TV ya kwanza ulimwenguni aina ya OLED ambayo ndiyo imeingia katika soko ya nchini Tanzania, TV aina ya OLED inayojikunja ni mwanzo wa burudani ndani ya nyumba. Aina yake ya kujikunja ambayo inaitwa IMAX inatupa uzoefu wa hali ya juu pamoja na kuangalia kwa starehe kubwa.

TV hii mpya aina ya OLED kutoka LG ikiwa na teknolojia ya rangi nne, ambayo kwa mujibu wa kampuni inaongeza pikseli nyeupe kwa rangi nyekundu, kijani na blu kwa mtazamo bora. Itakuwa na screen nyembamba aina ya OLED ambayo ukubwa wake ni 4.3mm. Pamoja na stendi yake ambayo ina vipimo ifuatavyo 1227x799x192mm na uzito wa kilo 17.2.

TV aina ya OLED LG namba 55EA9800 inakuja na idadi ya chaguo ya kuunganisha ambayo ni HDMI port (x4), port ya kusikiliza muziki ( 3.5mm), RF, AV ( composite), port ya muziki, USB 2.0 (x2), USB 3.0 na LAN port.”

TV hii pia ina kitako ambacho ni wazi kama kioo ambacho TV huwa haionekani kama imeungana nacho na TV huonekana kama inaning’inia hewani. Pia TV hii imewezeshwa kuwa na muonekano wa spika tano kwenye kitako chenye LG 55EA9800 zenye uwezo waku toa sauti ya watti 40.

Bwana Rajesh Darji, wa Garnet Star Ltd Distributor wa LG Home Entertainment Products amesema“ Hii TV aina ya OLED inapatikana katika maduka makubwa ya LG na wakala wake.

KING CLASS MAWE ASAINI MKATABA WA KUPAMBANA NA CHEKA FEB 8 PTA SABASABA

0
0

BONDIA bora wa mwaka 2013,2014 katika uzito wa  KG 63  Ibrahimu Class 'King Class Mawe' ame saini mkataba wa kupambana na Cosmas Cheka Feb 8 mwaka huu katika ukumbi wa PTA Sabasaba Dar es salaam.

Mara baada ya kusaini mkataba huo wa kucheza raundi 10 za ubingwa wa Taifa kg,60 amesema atafanya mazoezi ya kutosha kuhakikisha ana msambaratisha mpinzani wake raundi za awali kwa kuwa alikuwa anachonga sana juu yake

mpambano huo uliodhaminiwa na Promota Maarufu nchini Jay Msangi utakuwa na msisimko wa aina yake kutokana na mabondia hao kuwa gumzo katika ulimwengu wa masumbwi ndani na nje ya nchi ya tanzania

King Class aliongeza kwa kusema kuwa nipo fiti nimejiandaa na ninasubili tu kuvishwa ubingwa huo wa taifa kwani Cheka ana ujanja kwangu mbinu zake zote nimesha zikamata

King Class Mawe anae nolewa na jopo la makocha wanao ongozwa na Habibu Kinyogoli 'Masta' Rajabu Mhamila 'Super D' Kondo Nasoro 

Bondio huyo amewashukulu wadau wa mchezo wa ngumi kwa kumuwezesha kuchaguliwa kuwa bondia bora wa mwaka katika uzito wake kwa kuwapita mabondia wengine wanne na yeye kuibuka kidedea katika kin'yan'gan'yiro hicho

CHADEMA NA MKUTANO WAO WA HADHARA WA OPERESHENI M4C PAMOJA DAIMA NDANI YA MTIBWA.

0
0
 Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya, Afande Sele akiwahutubia wananchi wa Kata ya Tungi mjini Morogoro jana, katika mkutano wa hadhaa wa Operesheni M4C Pamoj Daima, ambao pia ulihutubia na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe.
 Sehemu ya maedlfu ya wakazi wa mji wa Ifakara, wakitawanyika baada ya mkutano wa Operesheni M4C Pamoja Daima, ambao ulihutubiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe jana.
 Mbunge wa Kawe, Halima Mdee akiwahutubia maelfu ya wakazi wa mji wa Mtibwa, katika mkutano wa Operesheni M4C Pamoja Daima, uliofanyika jana, ambao pia ulihutubia na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.
 Baadhi ya wa mji wa Ifakara wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe mbalimbali, wakati wa mkutano wa Operesheni M4C Pamoja Daima, ambao ulihutubiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe jana.
 Mwenyekiti wa Chama cha Demokreasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee wakiondoka baada ya kuhutubia mkutano wa Operesheni M4C Pamoja Daima, uliofanyika mjini Ifakara jana.
 Mwenyekiti wa Chama ch Demokrasia na Mendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akiwahutubia maelfu ya wakzi wa mji wa Mtibwa katika mkutano wa Operesheni M4C pamoja Daima jana.
 Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akimtambulisha mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya, Afande Sele, wakati wa mkutano wa Operesheni M4C Pamoja Dama, uliofanyika katika Kata ya Tungi mjini Mororgoro jana.
Maelefu ya wakazi wa mkji wa Ifakara, wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa Operesheni M4C Pamoja Daima, ambao ulihutubiwa na Mweneyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) jana.
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live




Latest Images