Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live

SERIKALI YASITISHA UTARATIBU WA KUKODISHA WAFANYAKAZI UNAOFANYWA NA BAADHI YA WAKALA BINAFSI WA HUDUMA ZA AJIRA

0
0

TAMKO LA SERIKALI KUHUSU KUSITISHA UTARATIBU WA KUKODISHA WAFANYAKAZI UNAOFANYWA NA BAADHI YA WAKALA BINAFSI WA HUDUMA ZA AJIRA

1. Wizara ya Kazi na Ajira imekua ikipokea malalamiko  toka kwa wadau mbalimbali kuhusu utaratibu wa udalali wa kukodisha wafanyakazi katika makampuni unaofanywa na baadhi ya Wakala Binafsi wa Huduma za Ajira nchini.

2. Wizara imefanya uchunguzi wa kina kuhusu suala hili na kubaini kuwa utaratibu wa kukodisha wafanyakazi unaofanywa na baadhi ya Wakala Binafsi wa Huduma za Ajira ni kinyume cha Sheria ya Huduma za Ajira Na. 9 ya Mwaka 1999 [Sura 243 kama ilivyorejewa Mwaka 2002]. Kwa mujibu wa Kifungu 4 cha Sheria hii, majukumu ya msingi ya Wakala wa Huduma za Ajira ni kuwaandaa na kuwaunganisha Watafuta Kazi na Waajiri kwa kutoa mafunzo na  ushauri elekezi kwa watafuta kazi,  kutafuta fursa za ajira na kutoa taarifa za soko la ajira.  Hivyo, Mawakala hawapaswi kuwa waajiri wa wafanyakazi waliowatafutia kazi kwa niaba ya Waajiri wengine.

3. Aidha, uchunguzi umebaini kwamba  utaratibu huu ni ujanja unaotumiwa na baadhi ya Waajiri na Mawakala kwa lengo la kukwepa kodi na kujipatia faida kwa kukwepa kutoa haki za msingi za wafanyakazi kwa mujibu wa Sheria za Kazi. Baadhi ya makampuni yanayokodisha wafanyakazi yamefanyiwa uhakiki na TRA na kubainika kukwepa kodi ya mapato ya ajira (PAYE) na  na kodi ya mapato ya kampuni kinyume na Kifungu cha 7 cha Sheria ya Kodi ya Mapato ya Mwaka 2004 [Sura 332 kama ilivyorejewa Mwaka 2008].

4.Uchunguzi huu umebaini  athari mbalimbali kwa wafanyakazi wanaoajiriwa kwa utaratibu huu. Athari hizo ni pamoja na:
·        Wafanyakazi kukosa haki ya hifadhi ya jamii kama vile likizo ya uzazi na matibabu kinyume na Sheria mbalimbali za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii;
·        Uwepo wa ubaguzi katika malipo ya mishahara kwa kazi ya aina moja kinyume na  kifungu cha 7(10) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Na.6 ya mwaka 2004 ambacho kinamtaka mwajiri kuchukua hatua stahiki kwa kuhakikisha kuwa wafanyakazi bila kujali jinsia zao wanalipwa mishahara linganifu na ya haki kwa kazi yenye uzito na thamani sawa;
·        Kukosa fursa za kujiendeleza kielimu na mafunzo;
·        Kukosekana kwa usalama na uhakika wa ajira ;
·        Wafanyakazi kulipwa mishahara ya kima cha chini kinyume na sekta wanayofanyia kazi.

5. Kwa taarifa hii, Wizara ya Kazi na Ajira imeamua kusitisha mara moja utaratibu wa Mawakalakuwaajiri  wafanyakazi wanaowatafutia kazi.  Aidha, Mawakala na Kampuni husika waliopo katika utaratibu huu kwa sasa wanapaswa kuwahamisha  wafanyakazi waliokodishwa kutoka kwa Wakala kwenda  kwa Kampuni husika. Waajiri na Wakala wanatakiwa kukamilisha zoezi hili ndani ya kipindi cha mwezi mmoja na kuwasilisha taarifa za utekelezaji kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Kazi na Ajira kabla au ifikapo tarehe 28/02/2014.

6. Uchunguzi zaidi unaendelea kubaini kama kuna wafanyakazi wa Kigeni wanaohusishwa katika utaratibu wa kukodishwa ili hatua zinazotahili ziweze kuchukuliwa ikiwa ni pamoja na kuwataka waombe vibali vya ajira kwa mujibu wa Sheria ya Uhamiaji Na.7 ya mwaka 1995na Sheria ya Huduma za Ajira Na.9 ya mwaka 1999. Wageni watakao kidhi vigezo wataajiriwa na kampuni walipokodishwa; ambazo kwa wakati huo zitakua ndiyo mwajiri wao.

7. Wizara ya Kazi na Ajira inawaelekeza Wakala wa Huduma za Ajira nchini kwamba, kwa utaratibu wa sasa watapaswa kuwasilisha barua za maombi ya  usajili wa Uwakala kwaKAMISHNA WA KAZI  kwa mujibu wa Sheria ya Huduma za Ajira Na. 9 ya mwaka 1999 [Sura 243 kama ilivyorejewa Mwaka 2002] ili waweze kufanya shughuli za Uwakala wa Huduma za Ajira kisheria. Maombi haya yawasilishwe ndani ya kipindi cha mwezi mmoja tangu kutolewa kwa tangazo hili. Baada ya muda huo Wakala asiye na kibali cha Kamishna wa Kazi hatoruhusiwa kuendesha shuguli za huduma za ajira nchini. Aidha, Mawakala watakaopata leseni ya Kamishna wa Kazi yatakua yakitangazwa ili yatambuliwe na Umma.

8. Nasisitiza, maelekezo haya yatatolewa kwa Makampuni na Wakala  waliohusishwa katika uchunguzi kwa ajili ya utekelezaji.


IMETOLEWA NA
GAUDENTIA MUGOSI KABAKA (MB)
WAZIRI WA KAZI NA AJIRA

27/01/2014

MAFUNZO YA SIKU TATU YA UELIMISHAJI WA SHERIA YA UVUVI YAFUNGWA ZANZIBAR LEO.

0
0
 Meneja Hifadhi ya Ghuba ya Menai Anas Masoud Othman akifunga mafunzo ya  siku tatu juu ya uelimishaji wa sheria ya uvuvi Nambari 7 ya mwaka 2010 yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Maendeleo ya wavuvi wa Kojani (KOFDO) kwa ufadhili wa The Foundation For Civil Society katika skuli ya Kitogani Mkoa wa kusini Unguja. (wa kwanza kushoto) ni Mratibu wa KOFDO Omar Mohd Ali na (wakati) ni  Mchumi Omar Katibu wa SACCOS ya Uwemacho ya Mkoa wa Kusini Unguja.
 Baadhi ya ashiriki wa mafunzo juu ya uelimishaji wa sheria ya uvuvi Nambari 7 ya mwaka 2010 yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Maendeleo ya wavuvi wa Kojani (KOFDO) kwa ufadhili wa The Foundation For Civil Society katika skuli ya Kitogani Mkoa wa Kusini Unguja.
 Mratibu wa Jumuiya ya Maendeleo ya wavuvi wa Kojani (KOFDO) Omar Mohd Ali akitoa maelezo namna Jumuiya ilivyojipanga kutoa uelewa wa sheria nambari 7 ya mwaka 2010 kwa wavuvi, wakuu wa madigo na wadau wengine wa uvuvi katika mafunzo yaliyofanyika skuli ya Kitogani chini ya ufadhili wa The Foundation For Civil Society.
icha ya pamoja ya washiriki wa mafunzo juu ya uelimishaji wa sheria nambari 7 ya mwaka 2010 yaliyandaliwa na KOFDO kwa ufadhili wa The Foundation For Civil Society katika skuli ya Kitogani Mkoa kusini Unguja. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).

GERMANY PRO HOLOCAUST EDUCATION

0
0
DSC_0083
United Nations Information Centre (UNIC), National Information Officer, Usia Nkhoma-Ledama delivering a message from the UN Secretary General’s to commemorate the victims of the Holocaust of 1933.

By Damas Makangale, MOblog Tanzania.
THE Federal Republic of Germany is strongly supports the international cooperation in Holocaust education through the European Union, the United Nations and other International bodies in today’s globalized world.

Speaking to invited guests during the International day of commemoration in memory of the victims of the Holocaust today in Dar es Salaam, Embassy of the Federal Republic of Germany, First Secretary, Holger Pfingsten said that teaching about the Holocaust is not limited in educating students about historical facts but to make them understand the consequences of Hitler’s dictatorship.

“The uniqueness of the Holocaust and to make them appreciate the values and institutions that ensure and protect our freedom and democracy today and to encourage them to take an active role in safeguarding these achievements,’ he said.

He said that education in Germany as a consequence of the Nazi period is federalized and therefore the responsibility of the German States and education policy is however coordinated on a national level by a council of the cultural ministers of every State.
DSC_0047
First Secretary, Head Administration, Federal German Embassy, Holger Pfingsten with some students following attentively the commemoration in memory of the Victims of the Holocaust.

Pfingsten added that they approve the common guidelines for teaching and Education about the Nazi Period is part of the compulsory curriculum of all German schools at all levels of education and the Holocaust is treated as the most important aspect.

“A crime against Humanity and all its values on an unimaginable scale committed by Germans that fills us with grieve, shock and above all deep shame,” he underscored.

He further noted that the media play a key role while Germany to this day has a strong public broadcasting sector which is obliged to put a particular emphasis on information about the Nazi period and the Holocaust in particular.

On her part United Nations Information Centre (UNIC) National Information Officer, Usia Nkhoma Ledama who delivered a speech on behalf of the UN Secretary General, Ban ki- Moon said that the UN was founded to prevent any such horror from happening again. “Yet tragedies from Cambodia to Rwanda to Srebrenica show that the poison of genocide still flows,”

“We must be ever vigilant against bigotry, extremist ideologies, communal tensions and discrimination against minorities,” she explained.
DSC_0051
First Secretary, Head Administration, Federal German Embassy, Holger Pfingsten gives a key note message to invited dignitaries during the International day of commemoration in memory of the victims of the Holocaust.
DSC_0063
Students from Secondary schools and Universities listening attentively during the ongoing session of the international day of commemoration in memory of the victims of the Holocaust.


DSC_0123DSC_0096
Section of Secondary school and University students viewing a live video of “Blinky and me”.
DSC_0127
UNIC, National Information Officer, Usia Nkhoma-Ledama overseeing Questions and answers session after viewing the video “Blinky and me” to Secondary and University students in Dar es Salaam to commemorate the victims of the Holocaust.
DSC_0134
Above and below: Students from Secondary schools and Universities airing their views about Holocaust Education around the Globe and role of youth in promoting and protecting Peace and tranquility across the world.
DSC_0164DSC_0169DSC_0173
First Secretary, Head Administration, Federal German Embassy, Holger Pfingsten, elaborate a point to students during the International day of Holocaust Victims.
DSC_0181
UNIC Librarian Officer, Harriet Macha handover different publications of the UN to some invitees and students.
DSC_0176
Usia Nkhoma –Ledama in tete a tete with first Secretary of Germany Embassy in Dar, Holger Pfingsten.

RAIS KIKWETE NA MKEWE WAPOKEA VIFAA KUTOKA KWA MWENYEKITI WA KUSAIDIA ELIMU YA OPPORTUNITY EDUCATION FOUNDATION WA MAREKANI

0
0
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea jezi ya timu ya baseball ya Chicago Cubs  toka kwa mmiliki wa  timu hiyo na Mwenyekiti wa taasisi ya kusaidia elimu ya Opportunity Education Foundation wa Marekani Bw. Joe Ricketts wakati alipomtembelea Ikulu Jumapili Januari 27, 2014 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea  akipokea moja ya Tabuleti 61  kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Wama Nakayama iliyoko kijijini Nyamisati, Rufiji, Mkoa wa Pwani    toka kwa Mwenyekiti wa taasisi ya kusaidia elimu ya Opportunity Education Foundation wa Marekani Bw. Joe Ricketts wakati alipomtembelea Ikulu Jumapili Januari 27, 2014 .PICHA NA IKULU.
 Mwenyekiti wa taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi Dkt Shukuru Kawambwa, Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya WAMA Nakayama Dkt Ramadhani Dau na Mkuu wa Shule hiyo wakipokea moja ya Tabuleti 61 alizozitoa kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Wama Nakayama iliyoko kijijini Nyamisati, Rufiji, Mkoa wa Pwani leo Januari 27, 2014 toka kwa  Mwenyekiti wa taasisi ya kusaidia elimu ya Opportunity Education Foundation wa Marekani Bw. Joe Ricketts akikabidhi moja ya Tabuleti 61 alizozitoa kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha pili katika Shule hiyo.
 Mwenyekiti wa taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi Dkt Shukuru Kawambwa, Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya WAMA Nakayama Dkt Ramadhani Dau na Mkuu wa Shule hiyo wakiangalaia matumizi ya ya Tabuleti 61 katika darasa la  kidato cha pili katika Shule ya Wama Nakayama iliyoko kijijini Nyamisati, Rufiji, Mkoa wa Pwani leo Januari 27, 2014 toka kwa  Mwenyekiti wa taasisi ya kusaidia elimu ya Opportunity Education Foundation wa Marekani Bw. Joe Ricketts akikabidhi moja ya Tabuleti 61 alizozitoa kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha pili katika Shule hiyo.

==========  =======  =======
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS



Telephone: 255-22-2114512, 2116898 

E-mail:  ikulumawasiliano@yahoo.com

              press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425


PRESIDENT’S OFFICE,

      THE STATE HOUSE,

              P.O. BOX 9120,  

DAR ES SALAAM.

Tanzania.

 

TAARIFA KWA UMMA 

Serikali kusambaza tabuleti za kufundishia sekondari


Yaanza kazi hiyo kwa kushirikiana na taasisi ya Marekani ya Opportunity Education Trust

Serikali inakusudia kutoa maelfu kwa maelfu ya tabuleti za kufundishia masomo mbali mbali  kwa wanafunzi na walimu wa shule za sekondari nchini kama njia ya ubunifu zaidi, ya kisayansi na ya uhakika ya kukabiliana na changamoto zinazoikabili sekta ya elimu kwa kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT).



Ili kufanikisha mpango huo, Serikali inakusudia kuingia ushirikiano (partnership) na taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya Opportunity Education Trust ya Marekani ambayo leo, Jumatatu, Januari 27, 2014, inazindua mpango wa majaribio wa utoaji wa tabuleti hizo kwa wanafunzi na walimu wao wa shule za sekondari nchini.


Mpango wa Serikali wa kusambaza tabuleti kwa wanafunzi na walimu wa shule za sekondari ulitangazwa usiku wa jana, Jumapili, Januari 26, 2013 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete wakati alipokutana na kuzungumza na Bwana Joe Ricketts, mwenye taasisi ya Opportunity Education Trust na mmoja wa matajiri wa Marekani.


Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam, Rais Kikwete amemweleza kwa undani Bwana Ricketts hatua ambazo zimechukuliwa na Serikali yake kupania na kuboresha elimu tokea mwaka 2006, hatua ambazo zimechangia kupanua kwa kasi na kwa kiwango kikubwa wigo wa utoaji elimu nchini na changamoto ambazo zimezuka kutokana na upanuzi huo mkubwa.


Rais Kikwete amesema baadhi ya changamoto hizi ni ukosefu wa walimu, na hasa walimu wa masomo ya sayansi, na ukosefu wa vitabu vya kufundishia changamoto mbili kubwa ambazo zinatatuliwa na matumizi ya tabuleti.


“Mbali na upanuzi mkubwa wa nafasi za wanafunzi kupata elimu ya ngazi mbali mbali, pia tumepanua sana ufundishaji wa walimu. Mwaka 2005, vyuo vyetu vyote vilikuwa vinatoa walimu 500 sasa tunatoa walimu 12,000 kwa mwaka. Hivyo, tunaamini kuwa katika mwaka mmoja ama miwili ijayo, tutakuwa tumemaliza tatizo la walimu wa masomo ya sanaa,” Rais Kikwete alimwambia Ricketts na kuongeza:


“Lakini bado tunakabiliwa na upungufu mkubwa wa walimu wa sayansi, kama zilivyo nchi nyingine. Tuna upungufu wa walimu 26,000 na kwa mwaka vyuo vyetu vyote vinahitimisha walimu 2,100 tu. Hii ina maana kuwa itabidi kusubiri miaka 13 kuweza kumaliza tatizo hili kwa mahitaji ya sasa. Hili haliwezekani na hii ndiyo maana halisi ya kutumia sayansi na teknolojia ya namna hii kufundishia wanafunzi wetu.”


Rais Kikwete alisema kuwa matumizi ya teknolojia kufundishia nchini ni jambo linalowezekana kwa urahisi kwa sababu mtandao wa mawasiliano wa National Fibre Network ambao karibu umefikia kila wilaya sasa.


Rais Kikwete alimshukuru Bwana Ricketts na  taasisi yake kwa kukubali kuchangia maendeleo ya sekta ya elimu nchini kwa kusambaza teknolojia ya kisasa kama moja ya njia za ubunifu zaidi za kufundishia hasa masomo ya sayansi.


Chini ya mpango huo wa majaribio wa kusambaza teknolojia hiyo ya kisasa, taasisi ya Opportunity Education Trust inatoa tabuleti 1100 kwa ajili ya walimu na wanafunzi wa sekondari katika shule 33.


Bwana Ricketts ambaye ni mwenyeji wa Omaha, Nebraska alimwambia Rais Kikwete: “Hapa tunafanya majaribio na Tanzania ni nchi ya kwanza duniani miongoni mwa nchi ambazo tunaunga mkono mipango ya maendeleo kunufaika na mpango huo wa majaribio. Ni azma yetu kuwa baada ya kuwa tumefanya tathmini ya mafanikio na changamoto za hatua hii ya majaribio, tutaupanua mpango huu kushirikisha shule nyingi zaidi kwa kushirikiana na Serikali kwenye mpango wake mkubwa wa kusambaza teknolojia hii katika shule zote za sekondari hapa Tanzania.”


Bwana Ricketts na wataalam wake pamoja na maofisa wa Serikali wameanza kutekeleza mpango huo leo, Jumatatu, Januari 27, 2014, kwa kutoa tabuleti kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wama Nakayama iliyoko Mkoa wa Pwani.


Baada ya leo, shughuli hiyo itahamia Zanzibar na Pemba, kabla ya Bwana Ricketts na wataalam wake kutoa tabuleti kwa shule zilizoko mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza, Kagera na Morogoro.


Shule zinazonufaika katika mpango huo ni za Serikali na binafsi na kwa kuanzia masomo ambayo yanapatikana katika tabuleti hizo ni hesabu, jiografia, historia na kiingereza.


Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu,

DAR ES SALAAM.


27 January, 2014




RAIS KIKWETE ATUA MAGOLE, AKAGUA DARAJA LA DUMILA, AONGEA NA WANANCHI

0
0
Rais JK akielekea kukagua daraja la Dumila lililokatika kutokana na mvua kubwa iliyonyesha eneo hilo.
Rais Kikwete akikagua daraja hilo.
Rais Kikwete akisalimiana na wananchi wa kijiji cha Magole mkoani Morogoro waliokumbwa na mafuriko ambao kwa sasa wanaishi katika mahema yaliyopo Shule ya Sekondari Magole.
Rais Kikwete akisalimiana na bibi mmoja wa kijiji cha Magole.
Rais Kikwete akiingia katika mojawapo ya hema.
...Akitafakari jambo.
Wananchi wa Magole waliokumbwa na mafuriko.
Rais Kikwete (kushoto) akijadiliana jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge William Lukuvi.
Rais Kikwete akiongea na wakazi wa Magole leo.
Wananchi wa Magole wakiwa nje ya mahema yao.
Helkopta iliyokuja na Rais Kikwete ikitua eneo la daraja la Dumila mkoani Morogoro leo.
Rais Kikwete akishuka katika helkopta aliyokuja nayo.…
Helkopta iliyokuja na Rais Kikwete ikitua eneo la daraja la Dumila mkoani Morogoro leo.
RAIS Dk. Jakaya Kikwete leo ametua kwa helikopta kijijini Magole, Dumila ili kukagua daraja lililoharibiwa na mvua pamoja na kuongea na wananchi wa eneo hilo waliokumbwa na mafuriko yaliyotokea Januari 22, mwaka huu wilayani Mvomero, Morogoro.
PICHA ZOTE KWA HISANI YA GPL

The day WAMA Nakayama girl's Secondary school in Rufiji went digital with Opportunity tablets...

0
0


 Chairman of the Opportunity Education Foundation Joe Ricketts from Omaha, Nebraska, in the US signs the visitor's book upon arrival at the WAMA Nakayama Girl's Secondary School at Nyamisati village in Rufiji District, Coast Region, January 27, 2014 as hostess Tanzania First Lady and school founder Salma Kikwete with the school's Chairman of Board of Directors Dr Ramadhani Dau look on prior to the launch of the a programme that aims at providing Tanzania secondary school students with tablets pre-loaded with educational materials.
 Wanawake na Maendeleo (WAMA) Chairperson Tanzania First Lady Salma Kikwete welcomes Chairman of the Opportunity Education Foundation Joe Ricketts  on prior to the launch of the a programme that aims at providing Tanzania secondary school students with tablets pre-loaded with educational materials.
 Chairman of the Opportunity Education Foundation Joe Ricketts from Omaha, Nebraska, in the US presents a Chicago Cubs jersey to his hostess Tanzania First Lady and school Salma Kikwete 
  Chairman of the Opportunity Education Foundation Joe Ricketts from Omaha, Nebraska, in the US heads for the hall of  the WAMA Nakayama Girl's Secondary School at Nyamisati village in Rufiji District, Coast Region January 27, 2014 with hostess Tanzania First Lady and school founder Salma Kikwete and  the school's Chairman of Board of Directors Dr Ramadhani Dau and headmistress
 Standing ovation as the VIP's enter the hall
  Chairman of the Opportunity Education Foundation Joe Ricketts from Omaha, Nebraska, in the US stand at attention   as the National Anthem and school song raise the curtains upon arrival at the WAMA Nakayama Girl's Secondary School at Nyamisati village in Rufiji District, Coast Region January 27, 2014 with  hostess Tanzania First Lady and school founder Salma Kikwete, Minister for Education and Vocational Education Dr Shukuru Kawambwa (right) with the school's Chairman of Board of Directors Dr Ramadhani Dau (left)


 WAMA Nakayama students sing the National Anthem
 Chairman of the Opportunity Education Foundation Joe Ricketts from Omaha, Nebraska, in the US stand at attention   as the National Anthem and school song raise the curtains upon arrival at the WAMA Nakayama Girl's Secondary School at Nyamisati village in Rufiji District, Coast Region January 27, 2014 with  hostess Tanzania First Lady and school founder Salma Kikwete, Minister for Education and Vocational Education Dr Shukuru Kawambwa (right) with the school's Chairman of Board of Directors Dr Ramadhani Dau (left)
  WAMA Nakayama school's Chairman of Board of Directors Dr Ramadhani Dau makes his welcome note
 WAMA Nakayama ..school Headmistress Ms Tuma Mensa delivers her speech
 One of WAMA beneficiaries gives his testimony 
 Representative of the Opportunity Education Foundation in Tanzania Mbakileki Mutahaba speaks out about the Opportunity Tablet programme
 Chairman of the Opportunity Education Foundation Joe Ricketts from Omaha, Nebraska, in the US makes a brief speech
 Traditional entertainment by WAMA Nakayama students
 Friends of WAMA Nakayama
 PPF Director General Mr William Erio (left) whose instution is one of the major donors was also in attendance
 A short play the students
 Minister for Education and Vocational Education Dr Shukuru Kawambwa gives his statement
 Coast Regional Commissioner Hon. Hajat Mwantumu Mahiza speaks
 Chairman of the Opportunity Education Foundation Joe Ricketts gets ready to hand over the tablets with  a word or two to Tablet Manager from the foundation's office in Tanzania, Ms Sandra Tetty.

 Tablet Manager from the foundation's office in Tanzania, Ms Sandra Tetty hand over one of the tablets to First Lady and school founder Salma Kikwete, Minister for Education and Vocational Education Dr Shukuru Kawambwa (right) with the school's Chairman of Board of Directors Dr Ramadhani Dau and school's headmistress Ms Tuma Mensa

 irst Lady and school founder Salma Kikwete in return hands over the tablets to students
 A visibly excited student holds shows off her tablet to the rolling cameras
 Mr Joe Ricketts joins in to bask in the warmth of the historical moment
 First Lady and school founder Salma Kikwete gives her statement of gratitude
 Some of the WAMA Nakayama students
 Tablet tutor sits with the students
 Another standing ovasion for First Lady as she and her guests leave the hall
 A group photo with members of the Opportunity Education Foundation team
 With WAMA Nakayama teachers and administrators
 With student representatives
 With Nyamisati Village leaders
 With WAMA Nyamisati friends
 Form two students with the tablets
 Now, this is awesome....
 PPF Director General Mr William Erio offers some tips on how to operate the Kindle-like Opportunity tablets

 Now, where is the log in icon?
 Hey, you have to log in first...
 Open sesame!
 Simply can't believe this is happening to us...
 Okay, show us how its done...
 Girls, I have decided to offer a tablet to each students of the entire school...
 Sir, thank you...
 Okay, Sir, I start by logging in my personal details...Easy like ABC
 Well, Sir, it took me just under ten minutes to grasp how to use this. We are very, very thankful for your generosity, Sir. We really are....
 Minister for Education and Vocational Education Dr Shukuru Kawambwa is happy and thankful for this pilot programme
 Multi-tablet charging decks. One full charge lasts for over eight hours.
 And this is our humble library...
 At the computer lab
Hey, i told you no Facebook, Instagram of Whatsapp in here.... Just lessons and important references like wikipoedia and encyclopedia etc. Good for us, ain't it?

A NEW era dawned in Tanzania's digital education landscape today when a programme that aims at providing secondary school students with tablets pre-loaded with educational materials was launched.

The programme’s ultimate goal is to provide each secondary school student in the country with a tablet to enable them access educational materials electronically.

It will be implemented by the government and an American NGO -- Opportunity Education Foundation (OEF).

Implementation will begin with a pilot phase in 10 secondary schools on Tanzania Mainland and Zanzibar, which will involve provision of about 1,100 tablets pre-loaded with Science, Mathematics, Geography and History materials for Form Two students. 

Each Form Two student in those schools will get one tablet, according to Tablet Manager from the foundation's office in Tanzania, Ms Sandra Tetty.

The donation makes Tanzania the first country in the world to receive the tablets under the OEF educational support programme, which earmarks 34 countries around the globe.

Launching of the programme involved handing over of 61 tablets to WAMA Nakayama Girls Secondary School at Nyamisati in Rufiji District by OEF Founder, Mr Joe Ricketts.

They were received by the Minister for Education and Vocational Training, Dr Shukuru Kawambwa and WAMA Chairperson, Mama Salma Kikwete. Mr Ricketts pledged a further donation of tablets for the entire school.

Dr Kawambwa hailed the donation, saying it was a valuable support to the government in its effort to improve the quality of education in the country through technology.

He noted that when rolled out throughout the country, the programme would go a long way toward addressing the shortage of teachers and text books in secondary schools.

The minister said his ministry had prepared science and mathematics content for secondary schools, which would be loaded into the tablets ready to be used by the students, while efforts to digitalise materials for other subjects go on.

This would entail replacement of the content in the donated tablets, which according to Ms Tetty, is about 60 per cent relevant to the country's O level and A level syllabuses.

"We are committed in this. We have started and there will be no going back," said the minister, adding that the government was also planning to use Tele-Presence technology in which one teacher can teach students in different schools connected to the system at the same time.

He said tomorrow he would launch a small model of the technology, which would be used to smoothen operations at his ministry. 

Dr Kawambwa commended Mama Salma and WAMA for being a ‘’shoulder on which to lean’’ in the effort to promote education, especially targeting disadvantaged children.

President Jakaya Kikwete met with Mr Ricketts at the State House in Dar es Salaam on Sunday, where he thanked the OEF Founder for supporting development of the country's education sector.

The president underscored the importance of science and technology for development, saying he strongly believed that the use of tablets in secondary schools would help address various challenges facing the sector

The customised Opportunity Education Tablets are fitted with simplified features that allow easy access of the content and uploading of any other educational materials. They also have long battery life.

Beneficiaries of the pilot phase will be Form Two students at Ilboru, Mzumbe, Msalato, Fidel Castro (Pemba), WAMA Nakayama (Coast), Bwiru Boys, J Ossian (Bukoba), Laureatte (Zanzibar), Notredame (Arusha) and Tusiime (Dar es Salaam).The 10 schools are part of 33 secondary schools which have been receiving support from the foundation.

MPIGA TUMBA MAHIRI WA TWANGA PEPETA,MCD AFARIKI DUNIA USIKU HUU MJINI MOSHI.

0
0
Aliyekuwa mpiga Tumba mahiri katika muziki wa dansi hapa nchini,Soud Mohamed,ambaye pia alifahamika sana kwa jina la MCD,aliyekuwa bendi ya African Stars a.k.a Twanga Pepeta na baadae akahamia bendi ya Mashujaa Band,amefariki Dunia usiku huu katika hospitali ya KCM-Moshi.

Taarifa hizo za kufariki kwa mwanamuziki huyo aliyekuwa nyota katika upigaji tumba,zimethibitishwa rasmi na Msemaji wa Bendi ya Twanga Pepeta,Hassani Rehani,kuwa MCD amefarika usiku huu.Taarifa zinaeleza kuwa MCD amefariki akisumbuliwa na maradhi ya mda Mrefu.Tutazidi kupeana taarifa kadiri ya zitakavyokuwa zikiingia.

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI-AMEN.

MKUTANO WA HADHARA WA CHADEMA HAPO JANA ULIOFANYIKA MKOANI IRINGA

0
0
Dr Slaa akihutubia katika mkutano wa hadhara katika uwanja wa Mwembetogwa mjini Iringa mapema jana (picha na Francis Godwin Blog).
Hii ndio  Helbopta  iliyowakusanya  wana Iringa  leo uwanja wa Mwembetogwa 
Dr Slaa akiwasili katika  kiwanja cha Mwembetogwa leo 
Mbunge wa  jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa akiwahutubia wana Iringa leo 
Mbunge Halima Mdee akiwahutubia  wananchi wa jimbo la Iringa mjini mapema jana. 
Katibu  mkuu wa Chama cha demokrasia na maendeleo (Chadema) Dr Slaa akimpokea kada wa CCM ambae amehamia  Chadema leo (jana) ,kulia ni kada wa TLP Bw  Samson .
Dr Slaa akimpokea kada wa  TLP Bw Samson Mrisho ambae amejiunga na Chadema leo (jana) uwanja wa Mwembetogwa 

MAHAFALI YA 7 YA DIT, TAASISI YA TEKNOLOJIA YA DAR ES SALAAM, YAFANYIKA JIJINI DSM

0
0

NA: HIDAN .O. RICCO.
 
Mahafali ya saba ya Taasisi ya Teknolojia ya Dar Es Salaam imefanyika wiki iliyopita jijini DSM ikihudhurisha wahitimu zaidi ya 500 katika ngazi ya  Astashahada, Stashahada na Shahada ya juu. 

Taasisi ya Teknologia ya Dar Es Salaam, DIT ambayo zamani ilikuwa ikijulikana kama Chuo cha Ufundi cha Dar Es Salaam, maarufu kama Dar Tech, inayo Idara 8 kama ifuatavyo, Idara ya Uhandisi Kompyuta, Idara ya Uhandisi Ujenzi, Idara ya Uhandisi Migodi, Idara ya Uhandisi Umeme, Idara ya Uhandisi Elektroniki na Mawasiliano ya Anga, Idara ya Uhandishi Mitambo, Idara ya Sayansi na Teknologia ya Maabara, Idara ya Teknologia ya Habari. 

Wahitimu kutoka Idara mbalimbali walitunukiwa Vyeti, Diploma, na Shahada ya juu kulingana na masomo waliyochukua. 

Mgeni Rasmi katika Hafla hiyo alikuwa Mheshimiwa Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbaraw, Mbunge akimuwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Gharib Bilal,  ambaye alikuwa na udhuru. 

Maandamano ya mahafali yalianza saa 7.30 mchana kwa Wahitimu kuingia viwanja vya michezo katika Taasisi hiyo, na Mgeni Rasmi aliwasili muda wa saa 8.00 akiongozana na jopo na Wahadhiri pamoja na Mkuu wa Taasisi Profesa John Kondoro. 

Baada ya Mlau [Chief of Protocol] kutoa salamu za makaribisho, na kusimika Rungu rasmi katika meza iliyoandaliwa kama inavyofanya katika ukumbi wa Bunge, Wimbo wa Taifa uliimbwa na baadae Mkuu wa Taasisi alisoma hotuba yake, ikifuatiwa na hotuba ya Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Teknolojia ya Dar Es Salaam ambaye ndie aliyemkaribisha Mgeni Rasmi kusoma hotuba yake na baadaye zoezi la kutunuku Vyeti kuanza.
 
Wahitimu wa ngazi ya cheti [Astashahada] katika fani ya Ufundi wa Teknolojia ya Habari yaani Basic Technician Certificate in Information Technology, ndio waliokuwa wa kwanza kutunukiwa wakifuatiwa na Idara zingine, na hatimaye kumalizia na Wahitimu wa Shahada ya Juu.

Wahitimu 49 wa fani ya Uhandisi Ujenzi, yaani Bachelor of Engineering in Civil Engineering ndio waliokuwa wa kwanza kutunukiwa Shahada ya juu wakifuatiwa na 24  wa fani ya Uhandisi Kompyuta yaani Bachelor of Engineering in Computer Engineering. 

Wahitimu wote wa Shahada ya Juu mara baada ya kutunukiwa Shahada zao walivaa rasmi kofia zao kuashiria kwamba sasa ni wahitimu kamili, huku brass band ya Jeshi la Magereza wakipiga wimbo maalum wa fan fair wakati wahitimu kutoka Idara mbalimbali wakitajwa majina yao na kuinuka katika viti vyao na kujipanga mbele ya Jukwaa la Mgeni Rasmi kupokea tuzo hizo.
 
Zoezi la mwisho lilikuwa ni kutangazwa rasmi kwa Wahitimu bora wa kila Program na Idara wanazotoka. Upande wa Stashahada walikuwa wahitimu 8 wote wa jinsia ya kiume, na upande wa Shahada waliotunukiwa walikuwa wahitimu 5 wanne wakiwa ni wanaume na mmoja ni msichana aliyetambulika kwa jina la Cecylia Kuguru, ambaye alishangiliwa na ukumbi mzima uliokuwa umefurika na wazazi, walezi, wanafunzi pamoja na wageni waalikwa.
 
Mgeni Rasmi Profesa Makame Mbarawa kwa Mamlaka aliyopewa alitangaza hapo hapo kumpa scholarship  ya kusoma Masters Degree mhitimu huyo katika Chuo chochote atakachopenda. 

Tamko hilo liliongeza vifijo na nderembo uwanjani hapo huku Mgeni Rasmi akiwahimiza wanafunzi wengine kusoma kwa bidii, kuwa wanafunzi bora na hatimaye kujipatia nafasi kama hizo za kusomeshwa bure na Serikali.
Mhitimu Cecylia Kuguru anatokea Idara ya Uhandishi Elektroniki na Mawasiliano Anga, mafunzo ambayo yanamuwezesha kupata ajira na nafasi ya Juu katika Idara ya Mawasiliano ya angani kama Control Tower ya Mawasiliano ya ndege, meli na kadhalika. 

Mwanafunzi Mhitimu bora ndugu Elias Eliud kwa niaba ya wahitimu wenzake alitoa neno la shukrani, na baadaye sherehe zilifungwa kwa kupigwa picha za pamoja Wahitimu bora na Mgeni Rasmi, Wakuu wa Idara pamoja na Wageni Waalikwa.




BODI YA USHAURI YA TFDA KWA WIZARA YA AFYA YAKUTANA NA MKUU WA MKOA WA MWANZA

0
0

Bodi ya  Ushauri ya Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii (MAB) yakutana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Injinia Evalist Ndikilo kwa lengo la kutambua mchango wa mkoa na ushirikiano unaotolewa kwa TFDA katika masuala ya Udhibiti wa Bidhaa za Chakula, Dawa, Vipodozi  na Vifaa tiba.

Akizungumza katika ziara hiyo Mwenyekiti wa MAB, Balozi Dkt. Ben Moses, amepongeza ushirikiano uliopo baina ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na TFDA kanda ya Ziwa na kutoa wito wa kudumisha ushirikiano uliopo kwa  kuwa lengo la udhibiti litafanikiwa ikiwa ushirikiano uliopo utadumishwa. 

'

Naye Mkuu wa Mkoa amesifu kazi kubwa inayofanywa na TFDA katika kulinda afya ya wananchi kwani afya za wananchi zikiimarika basi uchumi wa unchi nao utaimarika. Vilevile,  katika kueleza changamoto ambazo mkoa unakabiliana nazo katika masuala ya udhibiti wa chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba,  Injinia Ndikilo alieleza kuwa  usafi katika machinjio ni changamoto kubwa na kwamba anatarajia kulipatia ufumbuzi hivi karibuni baada ya kuitisha kikao cha wadau.

Aidha, Injinia Ndikilo ametoa wito kwa  TFDA  kuona fursa iliyopo ya kuhamasisha wafanya biashara kujenga kiwanda cha dawa jijini Mwanza kutokana na idadi kubwa ya wananchi pamoja na kuimarisha udhibiti wa bidhaa za chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba kufuatia kujengwa kwa kituo cha Biashara cha Jiji la mwanza ambapo milango ya biashara nyingi itakuwa wazi hususan bidhaa zinazodhibitiwa na TFDA.
Wajumbe wakiendelea na mazungumzo Yao na Mkuu wa mkoa wa Mwanza.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Injinia Ndikilo, akifafanua jambo kwa wajumbe wa Bodi ya TFDA ofisini kwake.

MUIGIZAJI WA KUNDI LA VICHEKESHO LA FUTUHI LA JIJINI MWANZA ALIEJULIKANA KWA JINA LA MZEE DUDE AMEFARIKI DUNIA

0
0
MUIGIZAJI WA KUNDI LA VICHEKESHO LA FUTUHI LA JIJINI MWANZA, LINALORUSHA MCHEZO WAKE KUPITIA LUNINGA YA STAR, MZEE DUDE, AMEFARIKI DUNIA, JANA SAA 12 JIONI KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO, BAADA YA KUUGUA KWA MUDA MFUPI. 
TAARIFA ZAIDI JUU YA KIFO CHAKE NA MAZISHI TUTAENDELEA KUKUJUZANA HAPA HAPA JAMVINI

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI-AMIN

Exim Bank beats Community Police 2-1 in friendly

0
0
Exim Bank’s play-maker Lusajo Adam (right) overturns Mashaka Jongo (left) of Community Police FC during a friendly match played at Karume Stadium over the weekend whereby Exim Bank won 2-1
Exim Bank’s play-maker Lusajo Adam (right) scrambles for a ball with Mashaka Jongo (left) of Community Police FC during a friendly match played at Karume Stadium over the weekend whereby Exim Bank won 2-1. 
Exim Bank’s defender Phinias Enock (left) dribbles the ball to pass Meu Emmanuel (right) of Community Police FC during a friendly match played at Karume Stadium over the weekend whereby Exim Bank won 2-1. 
Exim Bank’s midfielder Daniel Kapingu (right) scrambles for a ball with Meu Emmanuel (left) of Community Police FC during a friendly match played at Karume Stadium over the weekend whereby Exim Bank won 2-1. 

======  =======  ========
Exim Bank beats Community Police 2-1 in friendly

EXIM Bank Tanzania’s football team ‘Innovation Team’ has continued the winning trend thanks to Roger Timoth who scored twice and beat Community Police FC 2-1 during a friendly match played at Karume Stadium in Dar es Salaam over the weekend.

Exim Bank played an impressive performance in the first half scoring one goal during the first half as result of wonderful display of Roger Timoth in the 40th assisted by Lusajo Adam.

Community Police FC tried to get a consolation goal before the end of the first half but this was not possible because of Exim Bank’s solid defense and by the end of the first half, Community Police FC was one goal behind.

Exim Bank managed to double the score through Roger Timoth again in the 57th minute of the game after receiving a through pass from midfielder Norbert Misana thanks to team work that was exhibited by the team.Community Police FC however made a comeback into the game scoring a consolation goal in the 74th minute through Salum Mashaka after getting a good assist from Hassan Abdul following a blunder made by the Exim Bank defense.

Community Police FC wonderful display in the second half was not enough to get the equalize and by the end of the final whistle, Exim Bank emerged winners. Speaking after the final whistle, the Exim Bank Innovation Team captain Fadhil Seleman attributed his team’s win to team spirit and vigorous training undertaken by his team.

“We always take routine trainings to ensure that we are always physically fit. We played as a team so we deserved to win. “Our good performance is backed by the support accorded by the bank’s management because it understands the importance of sports in people’s daily lives,” said Fadhil.

WAZIRI MUHONGO AWEKA SAINI LESENI ZA UCHIMBAJI MADINI

0
0
 Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Profesa Sospeter Muhongo akisaini moja ya Leseni alizozitoa za uchimbaji Madini. Wanaoshuhudia, aliyesimama ni Kaimu Kamshina wa Madini anayeshughulikia Leseni Bw.  John Mayopa na anayeangalia ni Kamshina wa Madini Paul Masanja.

 Mmmoja wa Wamiliki Kampuni ya J.S Contractors Bw. Sisti Siyvester Mganga akieleza jambo kuhusu Kampuni ya J.S na namna itakavyofanya kazi. Kampuni hii inatarajia kuzalisha madini  aina ya ‘dimension stone’ na kokoto za ujenzi katika eneo la  Kihangaiko Bagamoyo.

 Mwakilishi wa Kampuni Ya Osiris Gold T) Ltd. Bw.Shehzada Walli akimweleza Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Prof esa.Sospeter Muhongo kuhusu Kampuni hiyo. Leseni  iliyosainiwa ya kampuni hiyo itaiwezesha kuchimba madini ya Dhahabu katika eneo la Rwamgaza Geita.

Mwakilishi wa Kampuni ya Kamal Steel akieleza jambo wakati wa kikao cha kusaini Leseni za Uchimbaji Madini. Kampuni hiyo imepewa Leseni ya kuchimba madini aina ya ‘Marble’ katika eneo la Kidayi Kilosa.


======= ========  =======
WAZIRI MUHONGO AWEKA SAINI LESENI ZA UCHIMBAJI MADINI

Na Asteria Muhozya


Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Sospeter Muhongo   ameweka saini Leseni tatu za Uchimbaji wa Madini kwa Kampuni zinazotarajia kuzalisha madini aina mbalimbali kulingana na maeneo waliyoomba kufanya shughuli hizo.


Kampuni zilizosainiwa Leseni ni Kampuni ya J.S Construction, inayomilikiwa na Bw. Sisti Slyvester Mganga ambaye ameingia ubia Bw. Nakui Chen Kampuni hiyo yenye Leseni ML 501/2014 ina eneo la ukubwa wa km 0.29. Aidha, shughuli za uchimbaji zitafanyika katika eneo la Kihangaiko Bagamoyo na   Madini yatakayozalishwa ni ‘dimension stone’ na kokoto za ujenzi za granite.


Vilevile, kampuni nyingine iliyowekewa saini ya Leseni ni Osiris Gold (T) Ltd. inayomilikiwa na Watanzania Ezekieli Kihali na Shehdaza Walli leseni namba ML 513/2014. Madini yatakayozalishwa na Kampuni hii ni dhahabu katika eneo la ukubwa wa km 9.94, Rwamgaza Geita.


Aidha, Mhe. Muhongo ameweka saini leseni ya uchimbaji wa madini aina ya Marble kwa Gagan S.Gupta, Sameer S.Gupta na Shailesh B.Bhandari ambao wanamiliki Kampuni ya Kamal Steel katika eneo la Kidayi Kilosa. Kampuni hii yenye Leseni ML 514/2014 ina eneo la Km 9.52.


Wakati akitoa Leseni hizo za uchimbaji, amewakumbusha wamiliki wa leseni kuhusu kodi na wajibu wa mwenye leseni katika jamii inayohusika ili wananchi na Taifa waweze kufaidika na rasilimali hizo. Uwekaji saini huo umefanyika katika ofisi za Wizara ya Nishati na Madini, Dare s Salaam.


MAFUNZO YA BIASHARA YA HEWA UKAA YAENDELEA LEO MJINI BAGAMOYO.

0
0
Pichani kulia ni Injinia Ladslaus Kyaruzi  na Afisa Mazingira Mwandamizi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais akiwasilisha mada kuhusu mfumo wa biashara ya hewa ukaa katika siku ya pili ya warsha ya mafunzo hayo Mjini Bagamoyo leo, kushoto Mchambuzi wa Mifumo wa Komputa kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Mayala Mwendesha.
Sehemu ya washiriki wa warsha ya Mafunzo ya mfumo wa Biashara ya hewa Ukaa mjini Bagamoyo....(Picha na Evelyn Mkokoi).

MAGHOROFA YANAYOJENGWA SIKU HIZI KAMA UYONGA MAJANGA MATUPU..!


MIAKA 10 YA ONYESHO LA MITINDO 'LADY IN RED

0
0
WABUNIFU mbali mbali kupamba  miaka 10 ya onyesho la mavazi lijulikanalo kama ‘Lady in Red Super  brand, 10th Anniversary’ linalotarajiwa kufanyika Februari  14,  ambapo pia litatumbuizwa na burudani kutoka kwa  Babloom Trio bendi na Wanne Star, kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Fabak Fashions inayoandaa onyesho hilo, Asia Idarous Khamsin, alisema tayari maandalizi ya onyesho hilo yameshakamilika na tayari wabunifu mbalimbali wameanza mchakato wa kuandaa  mavazi yao watakayoonyesha siku hiyo.

Asia Idarous alipongeza wadau mbali mbali  kwa kuliunga mkono onyesho hilo la ‘Lady in red’ hadi kufikisha miaka 10, tokea kuanzishwa kwake, na kutamba kuwa la kipekee kwa mwaka huu. “Februari  14, mwaka huu ndiyo siku pekee kwa wadau wa mitindo na urembo ambapo watashuhudia wabunifu mbalimbali siku hiyo wakipamba jukwaa, wakiwemo wakongwe na wale wanaochipukia” alisema Asia Idarous.

Na kuongeza kuwa, kwa mwaka huu wametoa fursa kwa wabunifu wanaochipukia kuonyesha mitindo yao sambamba na wakongwe ili kuleta changamoto kwen ye tasnia hiyo ya ubunifu na mitindo hapa nchini.

Aidha, katika onyesho hilo ambalo litafanyika siku hiyo ya Februari 14, ambayo pia itakuwa ni siku ya Wapendanao ‘Valentine’s  Day’ , kiingilio kitakuwa sh 30,000 kwa viti vya kawaida huku viti maalum ikiwa sh 50,000, ambapo pia kutakuwa na burudani kutoka bendi ya Babloom Trio  na Mwanamuziki  mahiri wa nyimbo na ngoma za asili, Wanne Star.

 Asia Idarous aliyashukuru makampuni mbalimbali ambayo yamejitokeza kudhamini onyesho hilo wakiwemo kampuni ya nywele ya Darling-‘Quality hair additions’,  na  Zanzi ‘Cream liqueur’ ambao ni wadhamini wakuu mwaka huu. Wengine ni  CXC, Times fm, Clouds media, Vijimambo blog, michuzi media group, channel ten, Elite Computer, Eventlites, One touch-solution, Raysa Style,Paka Wear, Dj Bula, Magic fm, DTV, Jambo Leo, I View Vayle Spring, Voice of American na mengine mengi.

MTEMVU AZINDUA BONANZA LA MAVETERANI YOMBO MAKANGARAWE,TEMEKE

0
0
 Mtemvu akihutubia wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo, ambapo aliahidi kuyadhamini kwa timu zote kuzinunulia jezi za TMK. Kushoto ni Mwakasendile na Mungia Mbwana mratibu wa michuano hiyo.
 Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Matemvu akikagua timu ya Veterani ya Yombo Kilakala wakati wa uzinduzi wa michuano ya maveterani ya Ujirani Mwema, katika Kata ya Yombo Kilakala, Temeke, Dar es Salaam juzi. Timu 12 kutoka sehemu mbalimbali za jiji zilishiriki kwenye michuano hiyo. Timu hiyo ilicheza na Kigamboni Veterani.
 Mtemvu akikagua timu ya Kigamboni Veterani. Kushoto ni Diwani wa Kata ya Makangarawe, Victor Mwakasendile.PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Timu za New Kivule Veterani (waliovaa Bluu) na Kitunda (waliovaa bluu nyeusi) wakipepetana


 Ni mtanange kwa kwenda mbele
 Hapiti mtu hapa
 Sasa nawatoka
 Wanachi wakishuhudia mpambano huo
 Timu za Yombo Makangarawe Veterani (BLUU)  wakicheza na Kigamboni Veterani huku wananchi wakishuhudia
 Mlinda mlango wa Kigamboni akiwania mpira na mchezaji wa Yombo Makangarawe

wananchi waaswa kuwa makini kuchagua viongozi bora watakaowaletea maendeleo na sio bora kiongozi

0
0
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa,Bi Jesca Msambatavangu akizungumza na wakazi wa wilaya ya Mufindi wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi wa kugombea nafasi ya Udiwani 
 Baadhi ya Wanachama wa CCM na wananchi kwa ujumla wakiwa wamejumuika katika kijiji cha cha Kilala Ibumu wakisikiliza yaliyokuwa yakijiri kwenye kampeni za kugombea udiwani 
Pichani ni Bwa.Hemed Mbena ambaye ndiye mgombea Udiwani katika kijiji cha Kilala Ibumu kupitia chama cha CCM akiwahutubia wakazi wa kijiji hicho,wilayani Mufindi wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi wa kugombea nafasi ya Udiwani 

======  ======  ======= 
Wananchi wametakiwa kuwa makini katika kuchagua viongozi wanaoweza kuwaletea maendeleo na sio bora kiongozi kwa kufuata ushabiki wa vyama.


Hayo yamesemwa na katibu wa CCM wilaya ya Mufindi, MIRAJI MTATURU wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi wa Madiwani katika kijiji cha kilala ibumu kata ya image wilaya ya kilolo.


Mtaturu amesema kuwa wananchi wanapaswa kutumia busara katika kuchagua viongozi na kuangalia chama ambacho kinaweza kuwaletea maendele na sio kuchagua chama ambacho hawajui kimetoka wapi wala hawajui kina malengo gani.


Kwa upande wake mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa ,JESCA MSAMBATAVANGU amesema kuwa wananchi wanapaswa kuchagua kiongozi anayetoka katika chama cha ccm kwani ndiyo chama pekee kinachoweza kuwaletea maendeleo katika nchi na kutokimbilia chama cha chadema kwa sababu kinachagia kuwapotosha vijana kwa kuleta fujo.



Aidha amewataka wananchi kuiamini CCM na kuipa uongozi huku akiwataka wananchi wa kijiji cha Kilala Ibumu kumchagua HEMEDI MBENA ambaye ndiye mgombea udiwani katika kijiji hicho kupitia chama cha CCM.

Waziri Mkuu atembelea maeneo vinapojengwa viwanda vya MEIS na Dangote.

0
0
Na Eleuteri Mangi- MAELEZO, Mtwara.

Mradi wa uzalishaji gesi asilia umeonesha kuwa ni kichocheo kikuu na muhimu katika kuleta na kuinua sekta ya viwanda  nchini kwa manufaa ya taifa na wananchi wake.

Kauli hiyo ilitolewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda wakati wa ziara ya kikazi ya siku mbili katika mikoa ya Lindi na Mtwara hivi karibuni alipokuwa akitembelea mikoa hiyo kwa lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa bomba la kuisafirisha gesi asilia kutoka Mtwara kwenda Dar es salaam. 

“Ujenzi wa viwanda vya vya saruji vya MEIS kilichopo kijiji cha machole mkoani Lindi na Dangote kilichopo kijiji cha Msijute mkoani Mtwara unaoendelea ni dalili nzuri na njema kwa nchi na maendeleo ya na watu wake” alisema Waziri Mkuu Pinda.

Ujenzi wa viwanda hivi unaoendelea umefikia hatua mbalimbali ni matokeo ya kugunduliwa gesi asilia katika mikoa hiyo ambapo itakuwa ndio chanzo kikuu cha nishati ya umeme katika viwanda hivyo.  

Waziri Mkuu Pinda alisema kuwa viwanda hivi vitanufaika na umeme wa kuendeshea uzalishaji wa saruji katika viwanda hivyo ambao chanzo chake kikuu ni gesi inayopatikana katika mikoa hiyo.

Ili kuhakikisha viwanda hivyo vinapata umeme wa uhakika Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo alisema kuwa gharama ya kuunganisha umeme kwa wananchi nchini imepungua katika maeneo mbalimbali nchini.

Prof. muhongo alisema kuwa kwa sasa maeneo ya vijiji vyote vya mikoa ya Mtwara na Lindi wamepewa ofa maaluum ya kuunganishiwa umeme kwa gharama ya sh. 99,000/= za kitanzania ofa ambayo itaisha mwezi Juni mwa huu ikilinganishwa na gharama ya mwanzoni ambapo nchi nzima wananchi waishio vjijini bado wanaendelea kuunganishiwa umeme kwa sh. 177,000/=.

Wananchi wa maeneo hayo wamehimizwa kuchangamkia fursa hii iliyotolewa na serikali ili kuboreha maisha yao hasa katika karne hii ya sayansi na teknolojia.

Waziri Pro. Muhongo ameenda mbali zaidi na kusema kuwa wananchi wa mikoa ya Mtwara na Lindi wanaoishi karibu na bomba la kusafirishia gesi kutoka Mtwara kwenda Dar es salaam wamepunguziwa zaidi gharama ya kuunganisha umeme kwa sh.27, 000/= za kitanzania.

Muhongo amesisitiza kuwa hakuna serilkali yeyote duniani inayotoa huduma ya kuunganishiwa umeme kwa bei ndogo kama hii. 

Waziri Muhongo amaeendelea kusema kuwa wananchi waishio mijini nao wamepewa fursa hiyo ya kujihakikishia kuunganishiwa nishati hiyo kwa gharama ya sh. 330,000/= za kitanzania.  

Kutokana na uhakika wa nishati hiyo katika viwanda vya saruji vya MEIS na Dangote, wakazi wa maeneo yanayozunguka viwanda hivyo na watanzania kuwa ujumla watanufaika na kujengwa viwanda hivyo ambapo zaidi ya wananchi 70000 wataajiriwa.

Naye Mkurugenzi Mendaji wa Kiwanda cha saruji cha MEIS Merea Barabuu alisema kuwa kiwanda hicho kinatarajiwa kukamilika mwaka huu ifikapo Desemba kwa kuwa vifaa vyote vimekamilika na vipo tayari.

Barabuu alisema kuwa kiwanda hicho kinatarajiwa kuzalisha takribani tani 500 hadi 700 kwa siku ambapo kwa mwaka ni sawa na tani 200,000 hadi 250,000 ambapo malighafi zote za kuzalisha saruji zinapatikana ndani ya mkoa wa Lindi.

Katika ziara hiyo Waziri Mkuu katika msafara huo aliambatana Mke wake Mama Tunu Pinda,Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa) Hawa Ghasia, watumishi wa wizara ya Nishati na Madini, watendaji wa shirika la TPDC, viongozi wa shirika la umeme TANESCO na wabuge wa maeneo ya mikoa hiyo.

MOHAMMED ENTERPRISES TANZANIA'S EXPANSION PLAN IN AFRICA

0
0
BeqsooUCAAIEJjg
The World Economic Forum brought together political, business and civil society leaders to discuss economic development issues. It also attracted a host of entrepreneurs, among them Forbes' youngest member of the rich list, Mohammed Dewji, Group Chief Executive Officer of Mohammed Enterprises Tanzania. CNBC Africa's Bronwyn Neilson spoke with him about the company's expansion on the continent.
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live




Latest Images