Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live

RAIS KABILA ATUA DAR MCHANA HUU KWA ZIARA YA SIKU MOJA

$
0
0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha maafisa mbalimbali Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) alipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam mchana wa leo Januari 30, 2013.
 Matarumbeta ya Mzee Hozza ndani
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wakiingia hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency jijini Dar es salaam mchana wa leo Januari 30, 2013

 Ndege iliyomchukua Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ikiwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam  mchana wa leo Januari 30, 2013. Kiongozi huyo amewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku moja.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimjpokea Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) alipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam mchana wa leo Januari 30, 
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mgteni wake  Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wakmiangalia ngoma za utamaduni alipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijijni Dar es salaam  mchana wa leo Januari 30, 2013.Picha na IKULU

Kifo ni Haki Yangu kutoka kwa eric shigongo .!

$
0
0
BAADA YA KUSUBIRIWA KWA HAMU, HATIMAYE KILE KITABU 'Kifo ni Haki Yangu' CHA MTUNZI MAHIRI WA RIWAYA NCHINI TANZANIA, Eric James Shigongo, sasa kiko tayari kuanza kuuzwa karibu yako. Mtunzi huyo ameandaa zawadi ya VALENTINE kwako wewe msomaji wa mtandao huu, hivyo utajipatia kitabu hiki BURE, unachotakiwa kufanya ni kuhakikisha wewe ni mwanachama au umeshajisajili katika mtandao wa www.globalpublishers.info, kama bado fanya hivyo kuanzia leo kisha usubiri utaratibu wa kujipatia kitabu hiki na vingine BUREEE...Stay Tuned!

Airtel Yachezesha Droo ya Mwezi ya milioni 30

$
0
0

 

 Afisa huduma za Ziada, Fatma Ngororo akitoa ufafanuzi juu ya droo ya AMKA MILIONEA iliyochezeshwa leo makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto kwake ni Meneja huduma za Ziada Francis Ndikumwami, Meneja Mahusianao wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando akiwa na Afisa Michezo ya Bahati Nasibu, Bakari Maggid. 
 Meneja Mahusianao wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando akionyesha hundi itakayotolewa kwa mshindi aliyejishindia droo ya AMKA MILIONEA iliyochezeshwa leo makao makuu ya Kampuni hiyo jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Meneja Huduma za Ziada, Francis Ndikumwami pamoja na Michezo ya Bahati Nasibu, Bakari Maggid.
Meneja Mahusianao wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando akiongea katika mkutano na waandishi wa Habari katika droo ya AMKA MILIONEA iliyochezeshwa leo makao makuu ya Kampuni hiyo jijini Dar es Salaam. Pembeni yake ni Meneja huduma za Ziada Francis Ndikumwami akiwa na Afisa Michezo ya Bahati Nasibu, Bakari Maggid.

Glamour as Exim Bank opens second branch in Kilimanjaro region

$
0
0
 The Exim Bank Tanzania Managing Director Anthony Grant gives a speech during the launch of the Exim Bank Tanzania branch in Moshi Town on Monday.
 The Kilimanjaro Regional Commissioner (RC) Leonidas Gama (left) cuts a ribbon to open Exim Bank Tanzania’s new branch in Moshi Town, Kilimanjaro region on Monday. The branch is the bank’s second in the region. Looking on at the right is the Exim Bank Tanzania Managing Director Anthony Grant
 The Kilimanjaro Regional Commissioner (RC) Leonidas Gama (centre) displays cash drawn from the Exim Bank Tanzania ATM facility at the bank’s newly opened Moshi Branch. Right is the The Kilimanjaro Regional Commissioner (RC) Leonidas Gama. 
 The Exim Bank Tanzania Assistant Marketing Manager Anita Goshashy (left) hands over a banquet of flowers to the  Kilimanjaro Regional Commissioner (RC) Leonidas Gama (right) shortly after inaugurating the bank’s Moshi branch on Monday. Centre is the Bank Tanzania Managing Director Anthony Grant.
 The newly launched Exim Bank Tanzania (Moshi) Branch building in Moshi Town. The branch is the bank’s second in Kilimanjaro region.
Exim Bank Tanzania (Moshi) Branch staff pose for a photo during the event

kinana akagua miradi ya maendeleo ikiwemo soko la kimataifa la pamoja na ujenzi wa daraja la pamoja mpakani mwa tanzania na burundi, kibondo mkoani kigoma.

$
0
0


Jengo la Soko la Pamoja lililokaguliwa na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana mapema leo jioni,ikiwa na lengo la kurahisisha biashara ya mazao ya kilimo na bidhaa nyingine kati ya wananchi wa Nyabibuye na vijijini vya Mishiha nchini Burundi.
Mwenyekiti wa halmashauri ya Kibondo/Kokonko Bwa.Juma Magango akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana alipokwenda kukagua Soko la Pamoja  leo jioni.  


Katibu Mkuu,Ndugu.Abdulrahman Kinana akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya Mpya ya Kokonko Bwa.Peter Toima (kulia) pamoja na Mwenyekiti wa halmashauri ya Kibondo/Kokonko Bwa.Juma  Magango (shoto) na baadhi ya Wanachi wakielekea kukagua  Mradi wa daraja la Umoja ulioibuliwa na Wananchi wa Kijiji cha Nyabibuye mwaka 2011,ikiwa na lengo la kurahisisha biashara ya mazao ya kilimo na bidhaa nyingine kati ya wananchi wa Nyabibuye na vijijini vya Mishiha nchini Burundi,Mradi wa daraja hilo ni sehemu ya mpaka kati ya Tanzania na Burundi liofadhiliwa na serikali ya Japan kwa ushirikiano  na Serikali ya Tanzania kupitia Tanzania/Japan Food Aid Counterpart Fund.Mradi huo unajengwa na Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika kupitia ofisi ya Umwagiliaji na huduma za ufundi kanda ya Magharibi kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo na Wananchi wa kata ya Nyabibuye.




Wakielekea kukagua ujenzi wa mradi wa darja la pamoja.
Pichani ni  Mradi wa daraja la Umoja ulioibuliwa na Wananchi wa Kijiji cha Nyabibuye mwaka 2011,ikiwa na lengo la kurahisisha biashara ya mazao ya kilimo na bidhaa nyingine kati ya wananchi wa Nyabibuye na vijijini vya Mishiha nchini Burundi,Mradi wa daraja hilo ni sehemu ya mpaka kati ya Tanzania na Burundi liofadhiliwa na serikali ya Japan kwa ushirikiano  na Serikali ya Tanzania kupitia Tanzania/Japan Food Aid Counterpart Fund.

Mradi huo unajengwa na Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika kupitia ofisi ya Umwagiliaji na huduma za ufundi kanda ya Magharibi kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo na Wananchi wa kata ya Nyabibuye.

Mradi huo unaotarajiwa kukamilika februari 20,2013 utagharimu kiasi cha shilingi 260,000,000/=,aidha imeelezwa kuwa mradi huo utatekelezwa kwa awamu nne,awamu ya kwanza imeshaanza ambayo unahusisha ujenzi wa daraja,barabara KM1 inayotoka kwenye soko hadi darajani na hifadhi ya Mazingira,utekelezaji wa awamu ya kwanza umefikia 70% mpaka sasa.


Katibu Mkuu,Ndugu.Abdulrahman Kinana akisalimiana na  Msimamizi wa Mradi kanda ya Umwagiliaji kutoka Mkoani Tabora,Alfred Swai alipokwenda kukagua mradi  wa ujenzi wa  daraja la Umoja ulioibuliwa na Wananchi wa Kijiji cha Nyabibuye mwaka 2011,ikiwa na lengo la kurahisisha biashara ya mazao ya kilimo na bidhaa nyingine kati ya wananchi wa Nyabibuye na vijijini vya Mishiha nchini Burundi.
Msimamizi wa Mradi kanda ya Umwagiliaji kutoka Mkoani Tabora,Alfred Swai akitoa ufafanuzi mbele ya Katibu Mkuu,Ndugu.Abdulrahman Kinana kuhusiana na ujenzi wa Mradi wa daraja la Umoja ulioibuliwa na Wananchi wa Kijiji cha Nyabibuye mwaka 2011,ikiwa na lengo la kurahisisha biashara ya mazao ya kilimo na bidhaa nyingine kati ya wananchi wa Nyabibuye na vijijini vya Mishiha nchini Burundi,Mradi wa daraja hilo ni sehemu ya mpaka kati ya Tanzania na Burundi liofadhiliwa na serikali ya Japan kwa ushirikiano  na Serikali ya Tanzania kupitia Tanzania/Japan Food Aid Counterpart Fund.Mradi huo unajengwa na Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika kupitia ofisi ya Umwagiliaji na huduma za ufundi kanda ya Magharibi kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo na Wananchi wa kata ya Nyabibuye.
Katibu Mkuu,Ndugu.Abdulrahman Kinana akipanda mti kwenye shule ya sekondari ya Nyamtukuza iliopo kwenye Wilaya ya Kibondo,mkoani Kigoma,pichani shoto ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Bwa.Amani Ntibakazi. 
Katibu Mkuu,Ndugu.Abdulrahman Kinana akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Mpya ya Kokonko Bwa.Peter Toima pamoja na Mwenyekiti wa halmashauri ya Kibondo/Kokonko Bwa.Juma Magango wakikagua ujenzi wa shule hiyo ya  Nyamtukuza 
Katibu Mkuu,Ndugu.Abdulrahman Kinana wa tatu kutoka kushoto akishiriki kwenye ujenzi wa shule ya sekondari ya  Nyamtukuza 
Katibu Mkuu,Ndugu.Abdulrahman Kinana akisalimiana na wanafunzi wa shule ya sekondari ya  Nyamtukuza mara baada ya kuwahutubia mapema leo mchana,kulia kwake ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Bwa.Amani Ntibakazi. 
Katibu Mkuu,Ndugu.Abdulrahman Kinana akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya  Nyamtukuza mapema jioni ya leo,Kinana aliuahidi uongozi wa shule hiyo kuwapa umeme (Solar Pannel )mbili kwa ajili ya kuzalisha umeme shuleni hapo,Kampyuta moja pamoja na Televishen
Katibu Mkuu,Ndugu.Abdulrahman Kinana akipokelewa na wananchi wa kijiji cha Rumashi kata ya Nyabibuye,jimbo la Buyunga wilaya ya Kokonko.
Katibu Mkuu,Ndugu.Abdulrahman Kinana akizungumza kwenye mkutanno wa hadhara mapema leo jioni na Wananchi wa kijiji cha Rumashi kata ya Nyabibuye,jimbo la Buyunga wilaya ya Kokonko.
Sehemu ya shamba la Mahindi safi kabisa,ambalo pia Ndugu Kinana aliwahimiza wanakijiji cha Rumashi,kutumia Pembejeo za mbolea kuhakikisha wanapata mazao bora. 
Katibu Mkuu,Ndugu.Abdulrahman Kinana akisalimiana na Wananchi wa kijiji cha Rumashi kata ya Nyabibuye,jimbo la Buyunga wilaya ya Kokonko mapema leo jioni.

RAIS KIKWETE AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS KABILA IKULU, AMSINDIKIZA MGENI WAKE LEO

$
0
0
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mgeni wake Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kabla ya kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii ya Januari 30. 2013
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsidikiza  Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere baada ya kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii ya Januari 30. 2013.PICHA NA IKULU

mazungumzo ya Kikao cha Gesi Asilia

AYOUB NEFZI'S MOMEMT OF GLORY IN HIS HOME COUNTRY TUNISIA!

$
0
0

                                                  Nefzi's left pummeling Pascqua in his previous tournament.

Belgium based Tunisian Ayoub Nefzi will be in action in Tunis, Tunisia facing Belgium based Tunisian Ayoub Nefzi will be in action in Tunis, Tunisia facing Ghanaian Ishmael Tetteh on February 15 to compete for the IBF vacant Africa, Middle East & Persian Gulf (IBF AMEPG) Jr. Middleweight crown.
The tournament is a warm up event for Nefzi's bigger moment for then IBF vacant Intercontinental (IBF I/C title at the end of March in Belgium

Wafanyakazi wa TCAA-JNIA wapatiwa mafunzo ya kuzima Moto

$
0
0


Na Ally Changwila


Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Kituo cha Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA) wamepata  mafunzo ya jinsi ya  kuzima moto.


Mafunzo hayo ambayo yamehusisha watumishi1 52   kutoka TCAA- JNIA yaliongozwa na Sajenti Thomas Lichenjela kutoka Idara ya zimamoto viwanja vya ndege JNIA na kusimamiwa na Afisa Utumishi mwandamizi kutoka TCAA- JNIA  Bi Valerie Chilipweli.

Lengo la Mafunzo hayo ni kuwaandaa watumishi hao kuwa tayari kupambana na majanga  ya namna hiyo endapo yatatokea katika mazingira yanayowazunguka  na hasa ukichukulia kwa upande wa Usafiri wa Anga,  Usalama ni suala linalopewa kipaumbele.

wilaya mpya ya kakonko inayotamba kwa kilimo mkoani kigoma.

$
0
0

Pichani ni Wakazi wa kijiji cha Rumashi kata ya Nyabibuye ndani ya jimbo la Buyunga,wilaya ya mpya ya Kakonko,mkoani Kigoma wakichota maji ya bomba,kama walivyokutwa na Camera ya Jiachie.Wilaya mpya ya Kakonko ni matokeo ya mgawanyo wa Wilaya ya Kibondo.

Wakazi wa kijiji cha Rumashi  wamejikita zaidi kwenye kilimo cha Mahindi,Karanga Ndizi na matunda mbalimbali yakiwemo mapapai sambamba na ufugaji kwa ukiasi.Kwa mujibu wa mkazi mmoja wa kijiji hicho alieleza kuwa wamekuwa wakijitahidi sana kwenye kilimo,lakini kumekuwepo na changamoto ya upendeleo ya ugawaji wa pembejeo kwa baadhi ya watu ikiwemo pia na kucheleweshewa,hali inayowapelekea kuwa na wakati mgumu msimu wa kilimo unapowadia.

MARTIN SHIGELA AKAGUA UJENZI WA SOKO NA MAABARA YA KISASA KATIKA SHULE YA BITALE

$
0
0
10
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM UVCCM Bw. Martin Shigela akijenga msingi wa ngazi katika soko la Bitale wakati alipotembelea na kukagua ujenzi wa soko hilo lililopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Vijijini, Wajumbe wa Sekretarieti ya CCM wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Chama hicho Ndugu Abdurahman Kinana wapo wako katika mkoa wa Kigoma ili kuamgalia utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi na sherehe za miaka 36 ya chama cha Mapinduzi, zitakazofanyika Februari 3 katika uwanja wa Lake Tanganyika mkoani humo.

8
Soko jipya linalojengwa katika Kijiji cha Bitale nje kidogo ya mji wa Kigoma likiwa katika hatua za mwisho kukamilika.


4
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM UVCCM Bw. Martin Shigela akiongea na baadhi ya wana Bitale kabla ya kuanza kutembelea miradi na kuona shughuli za maendeleo.

3 Wananchi wakiwa katika mkutano mara baada ya kuwasili kijijini hapo.



1 Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM UVCCM Bw. Martin Shigela akipokelewa kwa maandamano mara baada ya kuwasili katika kata ya Bitale mkoani Kigoma
2
Kikundi cha ngoma cha kijiji cha Bitaeli kikitumbuzia na kutoa burudani, huku Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM UVCCM Bw. Martin Shigela

13Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM UVCCM Bw. Martin Shigela akizungumza na wanafunzi wa kidato cha nne wakati alipotembelea maabara ya kisasa iliyojengwa katika shule ya Sekondari ya Bitale
14 Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM UVCCM Bw. Martin Shigela akikagua ofisi ya Tawi la Simbo Wilaya ya Kigoma Vijijini .
15Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM UVCCM Bw. Martin Shigela akielekea katika ofisi ya Kata ya Simbo na ujumbe wa CCM kutoka mkoani Kigoma pamoja na wenyeji wao ili kukagua utekelezaji wa ujenzi huo.

kigoma ya sasaaa...sio ile ya zamaaani,yaa leo inasongaa mbeele.

Neno La Leo: Mwaka Ni Kama Noti Ya Elfu Kumi Ya Bongo, Ukiichenji, Inapukutika!

$
0
0

Ndugu zangu,

Leo ni mwisho wa mwezi wa mwaka mpya. Na mwaka ulivyo ni kama noti ya shilingi elfu kumi ya Bongo. Ukiichenji tu, utashangaa inavyopukutika!


Ukae sasa ukijua, kuwa kesho ndio Februari Mosi. Hivyo, mwaka mpya wa 2013, kama ilivyo kwa noti elfu kumi, ndio tutakuwa tumeuchenji. Subiri sasa uone siku, wiki na miezi inavyopukitika. Fumba na kufumbua utasikia tumeshaingia Juni tunaelekea Bajeti ya Serikali ya Julai, na ukitoka hapo utafikiri mwaka unateremsha milima ya Kitonga.

Inatukumbusha nini?

Umuhimu wa kupanga mambo yetu. Inahusu muda na matumizi ya muda. Na mwanadamu usipokuwa makini na muda, itakuwa sawa na kisa kile cha mzazi aliyeulizwa na wanawe; " Mbona nguo za Krismasi hatujanunuliwa?"


Mzazi akawajibu wanawe; " Jamani, Krismasi ya mwaka huu imekuja ghafla sana!"
Kana kwamba hakujua, kuwa kwenye kalenda ya mwaka tarehe ya Krismasi imeshawekwa, Desemba 25!

Ndio, Afrika mvua hainyeshi ghafla, huwa kuna dalili zake. Na katika maisha, mambo mengi hayaji ghafla, bali hutukuta tukiwa hatujajiandaa. Jiandae na mwaka unaoanza kupukutika kuanzia kesho, kama noti ya shilingi elfu kumi. Kila la kheri.

Maggid Mjengwa,
Iringa.
0788 111 765

Dkt. Migiro afanya ziara wilaya mpya ya Buhigwe Mkoani Kigoma

$
0
0
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akiwasalimia wananchi wa Kijiji cha Mnanila kilichopo kwenye Wilaya Mpya ya Buhigwe,Mkoani Kigoma wakati akiendelea na Ziara yake ya kutembelea Kata zote zilizopo wilayani humo.
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Buhigwe ambapo ndipo yalipo makao makuu ya Wilaya Mpya ya Buhigwe,Mkoani Kigoma wakati wa Ziara yake ya kutembelea wilaya hiyo jana.
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Kilelema kilichopo kwenye Wilaya Mpya ya Buhigwe,Mkoani Kigoma wakati wa Ziara yake ya kutembelea maeneo hayo na kuweza kujionea changamoto mbali mbali wanazokabiliana nazo wananchi hao ikiwa ni pamoja na kutembelea eneo lililotengwa kwa ajili ya Ujenzi wa Soko la Kimataifa litakalowanufaisha wakazi wengi wa wilaya hiyo ambao wako kando kando ya Mto Maragarasi unaopakana na nchi jirani ya Burundi.Dkt. Migiro pia amewaasa wananchi wa maeneo hayo kuwa na umoja,mshikamano na upendo ili kuweza kuhimarisha mambo mbali mbali ya Wilaya.
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akihutubia Mkutano wa hadhara kwenye Kijiji cha Buhigwe ambapo ndipo yalipo makao makuu ya Wilaya Mpya ya Buhigwe,Mkoani Kigoma wakati wa Ziara yake ya kutembelea wilaya hiyo jana.
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akicheza ngoma ya asili ya kabila la Waha waliokuja kumpokea.


Wananchi wa Kijiji cha Buhigwe wakimuaga Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro.
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akisalimiana na Viongozi mbali mbali wa CCM katika Kijiji cha Mnanila,Wilayani Buhigwe.
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akiwapungia watoto wa Kijiji cha Kilelema kilichopo kwenye Wilaya Mpya ya Buhigwe,Mkoani Kigoma mara baada ya kumaliza kuwahutubia wananchi wa Kijiji hicho jana.
Mmoja wa wananchi wa Kijiji cha Buhigwe ambapo ndipo yalipo makao makuu ya Wilaya Mpya ya Buhigwe,Mkoani Kigoma wakati wakimsikiliza Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro aliekuwa kwenye Ziara ya kutembelea wilaya hiyo jana.
Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe,Ndg. Gishuli Mbegesi (kulia) akikabidhi Taarifa ya Utekelezani wa Ilani ya Uchaguzi kwa Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro.
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akipokea ripoti ya Chama Wilaya ya Buhigwe,kutoka kwa Katibu wa CCM Wilaya ya Buhigwe,Bi. Bennosa Mjema.Katikati ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya hiyo,Ndg. Elisha Bagwanya
Baadhi ya Wakazi wa Kijiji cha Buhigwe wakimsikiliza Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro aliekuwa kwenye Ziara ya kutembelea wilaya hiyo jana.
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akicheza ngoma ya asili ya kabila la Waha sambamba na Bibi Buchiro Edmas Kapina wakati wa Ziara ya kutembelea wilaya ya Buhigwe,Mkoani Kigoma jana.
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akilakiwa kwa shangwe na kinamama wa Kijiji cha Kilelema.
Mjumbe wa Halmashauri ya Kijiji cha Kilelema,Everist Samson akisoma taarifa ya kijiji kuhusiana na changamoto mbali mbali zinazowakabili wananchi wa kijiji hizo zikiwemo zile za kuvamiwa na majambazi wanaotoka nchi jirani ya Burundi.Kijiji hiki kipo mpakani kabisa mwa Tanzania na Burundi kwa kijiji cha Buhema Mkoani Lutana,nchini Burundi.

Wananchi wa Kijiji cha Kilelema kilichopo kwenye Wilaya Mpya ya Buhigwe,Mkoani Kigoma wakimsikiliza kwa makini Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro (hayupo pichani).
Mwenyekiti wa Kijiji cha Kilelema,Benedict Samson Mahuta (kulia) akitoa ufafanuzi juu ya eneo la Soko kwa Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro (katikati),alietembelea eneo litakalojengwa soko la Kimataifa katika Kijiji hicho cha Kilelema.
Picha ya Pamoja na Watendaji wa Kijiji cha Kilelema.
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro (pili kulia) akiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe,Ndg. Gishuli Mbegesi Charles (kushoto) kuelekea kwenye eneo la mpaka wa Tanzania na Burundi unaotenganishwa na sehemu ya Mto Maragarasi.

TIMU YA ASHANTI BOXING YAANZA VEMA KLAB BINGWA YA MASUMBWI

$
0
0

Bondia Hamisi Matunda wa Klabu ya Mashine ya Maji kushoto akipambana na Abdallah Shamte wa Klabu Ya Ashanti ya ilala Shamte aliibuka na ushindi wa TKO raundi ya pili .

Bondia Hamisi Matunda wa Klabu ya Mashine ya Maji kushoto akipambana na Abdallah Shamte wa Klabu Ya Ashanti ya ilala Shamte aliibuka na ushindi wa TKO raundi ya pili .

Bondia wa Klabu Ya Ashanti ya Ilala Abdallah Shamte akipambana na Hamisi Matunda wa Mashine ya maji wakati wa mashindano ya klabu bingwaShamte aliibuka na ushindi wa TKO raundi ya pili Picha na www.Superdboxingcoach.blogspot.com.

TAASISI YA THE JOHN MASHAKA YAWAKUTANISHA WAANDISHI NA WATU WENYE ULEMAVU KUJADILI CHANGAMOTO MBALIMBALI

$
0
0

Katibu wa Taasisi ya The john mashaka Bi, Rabia Bakari akiungumza kwa ajili ya kufungua mkutano wa waandishi wa habari na wawakilishi wa vyama vya watu wenye ulemavu ili kujadili kwa pamoja kwa ajili ya ustawi wa wenye ulemavu na wengine wasiojiweza.
Mwenyekiti wa TUSPO Bw. E LLEZER Mdakima kushoto akizungumza wakati wa mkutano huo wengine kulia ni Mjumbe wa Taasisi ya The John Mashaka Bi, Latifa Masasi na Katibu wa taasisi hiyo Bi, Rabia Bakari picha na www.burudan.blogspot.com
Baadhi ya watu wanaotafsili lugha za alama wakiendelea na kazi hiyo wakati wa mkutano


Baadhi ya wawakilishi wakisikiliza kwa makini

VIONGOZI WA CHAMA CHA WAIGIZAJI TANZANIA NA BODI YA FILAMU WAONGEA LUGHA MOJA.

$
0
0
 Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini Bi. Joyce Fissoo akisisitiza jambo wakati wa kikao cha pamoja kati ya Wizara ya Habari ,Vijana, Utamaduni na Michezo. 
Mwenyekiti wa Chama cha Waigizaji Tanzania (TDFAA) Bw. Michael Sangu akichangia maoni cha kati ya viongozi wa Chama hicho na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo jijini Dar es Salaam wakati wa kikao cha pamoja kuzungumzia Kanuni na Sheria ya Filamu pamoja na changamoto  mbalimbali zinazoikabili tasnia hiyo kuelekea zoezi la urasimishaji wa kazi za wasanii nchini.Kutoka kushoto ni Bw.Christian Kauzen Katibu wa Chama cha waigizaji Tanzania,Bw. Sakuta Chilwa (wa tatu) Kutoka Kinondoni na Bw. Siasa Digaga kutoka wilaya ya Ilala.
======  ======  ======  ===
VIONGOZI WA CHAMA CHA WAIGIZAJI TANZANIA NA BODI YA FILAMU WAONGEA LUGHA MOJA.
Na. Aron Msigwa - MAELEZO
31/1/2013 –Dar Es Salaam.
Wasanii wa Filamu na Michezo ya kuigiza nchini wametakiwa kuzijua kanuni na taratibu zinazoongoza tasnia ya filamu na kuvitumia vyama vyao kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili ili kuepuka migogoro inayoweza kuzuilika.
Hayo yamebainishwa  katika kikao cha pamoja  kati ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na viongozi wa vyama vya waigizaji nchini (TDFAA) kilichofanyika leo jijini Dar  Es salaam kuzungumzia Kanuni na Sheria ya Filamu pamoja na changamoto  mbalimbali zinazoikabili tasnia hiyo kuelekea zoezi la urasimishaji wa kazi za wasanii  lenye lengo la kuongeza vipato vya wasanii na kukuza tasnia ya filamu nchini.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti viongozi wa vyama hivyo wamesema kuwa kuna haja ya wasanii wote nchini kuwa makini na kazi wanazozifanya na kutumia muda wao kuzijua sheria, kanuni na taratibu zinazoongoza tasnia ya filamu na Michezo ya kuigiza nchini hasa sheria ya Filamu na Michezo ya kuigiza ya mwaka 1976.
Wamesema kwa  kipindi kirefu  wahusika wa tasnia ya Filamu na Michezo ya kuigiza nchini ambao ni wasanii wamekuwa wakiingia kwenye fani hiyo pasipo kujua miiko na taratibu zinazoongoza tasnia hiyo na kujikuta wakiibua migogoro, kukiuka maadili na wakati mwingine kutonufaika na kazi zao kutokana na kukiuka vipengele vya katiba.
Viongozi hao wamefafanua kuwa ipo haja kwa wasanii kote nchini kujiunga na vyama na mashirikisho yanayoongoza tasnia hiyo ili waweze kusaidiwa wanapopata matatizo kuanzia ngazi ya wilaya mpaka taifa ili kuepusha hali ya sintofahamu waliyonayo wasanii wengi ambao wamejikuta wakikwama wanapotekeleza majukumu yao na kuishia kuilaumu serikali.
Akizungumza kwa msisitizo katika kikao hicho kwa niaba ya viongozi wenzake mwenyekiti wa Chama cha Waigizaji nchini Tanzania (TDFAA) Bw. Michael Sangu amesema kuwa ipo haja ya wasanii nchini kuvitumia vyama vyao wanapokuwa na changamoto mbalimbali zinazowakabili ili kuepusha migogoro inayoweza kutokea katika masuala ambayo yanaweza kutatuliwa kwa njia ya mazungumzo.


Kufuatia  hatua hiyo ya kukutana na viongozi wa Wizara hiyo Bw. Michael Sangu amesema kuwa   yapo mambo mengi ambayo wao wenyewe walikua hawayajui lakini kupitia vikao mbalimbali vya Wizara husika kupitia Bodi ya Filamu wameyaelewa na kuondoa hali waliyokua nayo ya kuilaumu serikali.
“Ni kweli yapo mambo mengi tulikua hatuyajui  hasa sheria yenyewe ya Filamu na Michezo ya kuigiza ya 1976 na kanuni mbalimbali zinazoongoza tasnia hii, ipo haja kwa sisi kama viongozi wa vyama vya wasanii nchini kuwa vikao vya mara kwa mara na wizara ili tuweze kujadili mambo yetu pale inapobidi ili kuboresha fani hii”
Amesema ipo haja ya vyama vya wasanii kuungana pamoja na kufanya kazi pamoja na serikali ili kuhakikisha kuwa tasnia ya filamu nchini inapendwa, kulindwa na kuheshimiwa na kuiomba Bodi ya Filamu nchini kuendelea kulinda maadili ya kazi za wasanii ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua wasanii husika na  kuzuia filamu zote zinazokiuka maadili ya mtanzania kuingia sokoni.
“ Nawaomba wasanii tuungane kwa pamoja na wasanii ambao bado hawajajiunga na vyama vyetu wajiunge ili tuwatambue na kuwasaidia kwani Chama cha Waigizaji Tanzania mpaka sasa tuna uongozi katika mikoa 12 na bado tunaendelea na mpango wa kuongeza maeneo ya utendaji  nchi nzima ili tuweze kuwafikia wasanii wote ”  Alisema  Sangu.
Kuhusu Urasimishaji wa kazi za wasanii  Bw. Sangu ameishukuru serikali  kufuatia zoezi hilo kwani litazuia wizi wa kazi za wasanii kwa kiasi kikubwa na kuiomba serikali kuijengea uwezo bodi ya Filamu kuwa mamlaka kamili ili iweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo na kuweka  utaratibu wa kudhibiti uingiaji wa filamu kutoka nje ya nchi ili kulinda soko  la filamu za ndani na  kuangalia namna ya kuwasaidia kupunguza tozo mbalimbali wanazotozwa wasanii kutokana na kazi zao ili waweze  kunufaika  kutokana na ugumu wa soko la filamu nchini  Tanzania.
Naye Katibu wa Bodi ya Filamu nchini Bi. Joyce Fissoo amesema kuwa Bodi ya Filamu itaendelea kushirikiana na vyama vya wasanii katika kulinda maadili ya kazi za wasanii nchini na kuwaomba wasanii na viongozi wa vyama vyao kuzitumia ofisi za Bodi ya Filamu kupata ufafanuzi wa masuala mbalimbali yahusuyo taratibu za upataji wa vibali vya filamu kwa mujibu wa sheria, ufafanuzi wa tozo mbalimbali, taratibu za ukaguzi wa Filamu na kumbi za maonyesho pamoja na mambo ya kuzingatia msanii anapotaka kutengeneza filamu.
Amesema Bodi ya Filamu imekuwa ikishirikiana na wasanii kwa kukutana nao, kuendesha mafunzo mbalimbali kwa waongoza filamu nchini na kutoa miongozo mbalimbali kwa wasanii kuhusu mambo ambayo hawatakiwi kuyafanya kwa mujibu wa sheria.
Amesema kuwa  zoezi la urasimishaji wa kazi za wasanii litawajengea wasanii uwezo wa kumiliki kazi zao wenyewe na kuwafanya wanufaike na kuwawezesha kupata mikopo kupitia Benki mbalimbali nchini kwa kuwa watakua wameingia kwenye mfumo rasmi unaotambuliwa wa kuwa na hati miliki ya kazi zao.

BREAKING NEWS: Ajali ya Jahazi la 'SUNRISE'.

$
0
0

BREAKING NEWS: Ajali ya Jahazi la 'SUNRISE'.
Jahazi la SUNRISE ambalo ilikuwa likitokea Mkoani Tanga kuelekea visiwani Zanzibar likiwa na abiria 32 limezama eneo la Nungwi.

Jitihada za kuwaokoa abiria hao zinaendelea kufanywa na maafisa wa uokoaji na hadi sasa wameokolewa watu 20 na wengine 12 hawajulikani walipo.
... 
Endelea kusikiliza East Africa Radio kwa taarifa zaidi.

SOURCE: ITV

Grand Malt Premier League kuanza leo

$
0
0


Na Mwandishi Wetu, Zanzibar.

MZUNGUKO wa pili wa Ligi Kuu ya Zanzibar maarufu zaidi kwa jina la Grand Malt Premier League, unatarajiwa kuanza leo pale kutakapokuwa na michezo miwili kati ya Mafunzo na KMKM zitakazokwaana katika Uwanja wa Amaan, huku Chipukizi na Falcon wakionyeshana kazi ndani ya Gombani, Pemba
 
KMKM wanaingia uwanjani wakitaka kuendeleza ubabe wao, kwani mpaka sasa ndio wanaoongoza ligi hiyo wakiwa wamejikusanyia pointi 23, wakati Mafunzo ikiwa nafasi ya pili ikiwa na pointi 22.
 
Ugumu wa mchezo huo ni kuwa kila timu itataka kujiimarisha zaidi kwani kuteleza ni kujiweka katika mazingira magumu ya kutwaa taji na iwapo KMKM itakubali kichapo, itaichia Mafunzo kushika usukani wa ligi hiyo yenye timu 12.
 
Chipukizi wao watataka kuutumia vema uwanja wa nyumbani, kwani ikiwa nafasi ya tano kwa pointi 17 ilizonazo itataka kuhakikisha inashinda, ili kuzidi kupaa katika msimamo wa ligi hiyo ambayo kwa sasa imeongezeka mvuto kutokana na udhamini wa Grand Malt.
 
Lakini wasitegemee mteremko kutokana na Falcon nayo kutaka kujinasua kutoka nafasi za chini. Kwa sasa timu hiyo inashikilia nafasi ya tisa ikiwa na pointi 13.
 
Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea kesho, pale kutakapokuwa na michezo miwili wakati Bandari na Malindi zitakapokwaana Uwanja wa Mao, huku Jamhuri na Duma zikionyeshana ubabe Uwanja wa Gombani, Pemba na Jumapili kutakuwa na mchezo mmoja tu kati ya Zimamoto na Mtende zitakazocheza ndani ya Mao.
 
Timu inayoshika mkia mpaka sasa ni Mundu ikifuatiwa na Malindi. Timu zote hizi zina pointi saba kila moja. Mchezaji anayeongoza kwa kupachika mabao ni Ali Manzi wa Mtende mwenye mabao saba, akifuatiwa na Faki Mwalimu (Chipukizi) na Juma Mohamed (Chuoni) walio na magoli sita.
 
Ligi Kuu ya Zanzibar kwa sasa inadhaminiwa na kinywaji kisicho na kilevi cha Grand Malt.

dkt shein azindua sherehe za miaka 36 ya kuzaliwa ccm

$
0
0
STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
                                                                                        

MAKAMO Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar na Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amezindua sherehe za miaka 36 ya kuzaliwa kwa CCM  na kueleza kuwa chama hicho kitaendelea kuwa imara huku akiwashangaa wanaoubeza Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Uzinduzi huo ulifanyika leo huko katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui ambapo pana historia kubwa ya ASP ambayo iliungana kuzaliwa kwa CCM, uzinduzi ambao ulienda sambamba na ukabidhishaji wa vifaa vya michezo kwa ajili ya mashindano ya mpira wa miguu katika kusherehekea kuzaliwa kwa chama hicho.

Katika maelezo yake, Dk. Shein alisema kuwa ipo haja kwa wanaCCM kujipanga zaidi ndani ya miaka 36 kwa lengo la kukivusha chama hicho ili kiendeleze wimbi la ushindi katika uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2015.

Dk. Shein alisema kuwa kuna ulazima wa kudumisha Muungano uliopo na kusema kuwa anawashangaa wanaotoa visingizio vya kudai hati za Muungano wakati kitendo cha kuziunganisha Zanzibar na Tanganyika hakikuwa siri.

Alieleza kuwa kwa wale wanaohoji masuala hayo majibu yake yapo na ushahidi upo hadi chumba kilichosainiwa hati hiyo kipo huko katika jengo la Ikulu mjini Zanzibar na kueleza kua kama wanataka uthibitisho zaidi waende UN, huku akieleza haja ya kuulinda na kuuenzi Muungano huo pamoja na viongozi wake waasisi hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na hayati mzee Abeid Amani Karume..

Pamoja na hayo, Dk. Shein aliwataka Wazanzibar watambue kuwa umoja na mshikamano walionao ndio ngao yao huku akisisitiza amani na utulivu nchini na kuwataka wale wote wanaokusudia kuvunja amani na utulivu uliopo sheria zitachukua mkondo wake. ‘Zanzibar si sehemu ya kuonesha misuli”,alisisitiza Dk. Shein.

Dk. Shein aliahidi kupita katika Matawi yote ya CCM pamoja na Maskani zake kwa lengo la kukiimarisha chama hicho na kuendelea kupata ushindi kwani chama hicho pamoja na viongozi wao wako imara na wako makini.
 

Katika hotuba yake hiyo, Dk. Shein aliwahakikishia wanaCCM kuwa CCM itashinda katika uchaguzi ujao wa mwaka 2015 kwani ndani ya chama hicho ushindi ni lazima.

Alisema kuwandani ya chama hicho kuna timu nzuri ya uongozi katika kuhakikisha inapata ushindi katika uchaguzo huo huku akieleza kuwa chama hicho kimejipanga kuanzia Mashina hadi Taifa lakini la msingi ni kuimarisha amani na utulivu.

Dk. Shein alieleza maendeleo yaliopatikana ndani ya Serikali za CCM, kwa upande wa Zanzibar na Tanzania Bara katika sekta zote huku akieleza kuwa chama hicho hakina ubaguzi wa rangi, dini, ukabila wala jinsia na kuwataka wanaCCM wasikubali kugawanywa.

Akieleza juu ya mashindano hayo ya mpira wa miguu ambayo yanadhaminiwa na familia ya  Mhe. Mohammed Raza pamoja na  familia ya Ibrahim Makungu, Dk. Shein alitoa pongezi kwa Wanafamilia hao kwa mchango wao huo mkubwa na kusisitiza kuwa michezo ina historia kubwa katika uanzishwaji wa chama cha ASP na TANU.

Alitoa nasaha zake kwa washiriki wote wa mashindano hayo kutambua kuwa azma ya mashindano hayo ni kushindana ili kupata ushindi katika mpira huo wa miguu ambao utazishirikisha timu sita kutoka katika mikoa sita Unguja mine na Pemba miwili.

Mapema Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai nae alisisitiza hja ya muuenzi na kuutunza Muungano uliopo  na kueleza kuwa Muungano wa Unguja na Pemba nao umetokana na Muungano uliopo na iwapo ukisambaratika Zanzibar itakuwa mashakani na ndio maana CCM iko imara katika kuhakikisha Muungano unadumishwa.

Alisema kuwa Wazanzibari wamekuwa wakihushishwa katika harakati kadhaa za Muungano ikiwa ni pamoja na kushiriki katika vita vya Kagera kwa kuikomboa nchi yao.

Nae,Mohammed Raza ambaye pia, ni Mwakilishi wa Jimbo la Uzini, liliopo Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja alisema kuwa vifaa hivyo ilivyotoa familia yake pamoja na familia ya marehemu Ibrahim Makungu ni miongoni mwa ufadhili wa mashindano hayo makubwa ya kusherehekea miaka 36 ya kuzaliwa kwa CCM  yatakayoaanza kesho.

Alisema kuwa timu zote za Unguja na Pemba zitapatiwa usafiri pamoja na malazi na vyakula hadi kumalizika kwa mashindano hayo ambayo kiingilio kitakuwa bure na mgeni rasmi katika fainali zake atakuwa Dk. Shein.

Viongozi mbali mbali walihudhuria katika hafla hiyo akiwemo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na viongozi wengine wa CCM. Ambapo pia sherehe hizo zilipambwa na taarabu, nyimbo maalum ya CCM, pamoja na vijana wa Kimasai ambao nao walionesha umahiri wao wa kucheza katika nyimbo zao za asili. Kilele cha Sherehe hizo zitafanyika Mkoani Kigoma Febuari 5 mwaka huu.  
Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar.
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live




Latest Images