Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 207 | 208 | (Page 209) | 210 | 211 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza kwenye kikao na watumishi wa idara ya afya wa hospitali kuu ya Mkoa iliyopo katika Manispaa ya Sumbawanga. Alisema kuwa lengo la kikao hicho ni kusikiliza kero, malalamiko pamoja na ushauri kwa ajili ya kuboresha huduma na utendaji katika hospitali hiyo. Kero mbalimbali zilitolewa ikiwepo upandishwaji wa vyeo kuchukua mda mrefu, kubadilishiwa muundo wa vyeo na kusababisha kupungua kwa mishara kimakosa, uhaba wa vitendea kazi pamoja na madaktari bingwa wa upasuaji ambapo kwa sasa hamna hata mmoja.
  Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Samson Mashalla akifafanua baadhi ya mambo ya kiutawala katika kikao hicho. 
  Wajumbe katika kikao hicho.
  Mmoja ya wahudumu wa afya akitoa kero yake.(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)

  0 0

  Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Bw. Jackson Mmbando (kulia) akisisitiza jambo wakati akiwatangaza washindi wa droo ya wiki ya tisa ya promosheni ya Airtel Mimi ni Bingwa iliyochezeshwa jana na kuwapata washindi wa pesa taslimu ya zaidi ya Shilingi milioni 22 na kumpata Edwin Edmund Kajimbo kutoka Iringa aliyejishindia tiketi mbili ya safari iliyogharamiwa kila kitu ya kwenda kuangalia mechi ya ligi kuu ya Uingereza moja kwa moja ‘live’ kwenye uwanja wa Old Trafford. Kushoto ni Msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha Tanzania Mrisho Millao.
  Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Bw. Jackson Mmbando (kulia) akimpigia simu Bw. Edwin Edmund Kajimbo mkazi wa Iringa aliejishindia tiketi mbili ya safari iliyogharamiwa kila kitu ya kwenda kuangalia mechi ya ligi kuu ya Uingereza moja kwa moja ‘live’ kwenye uwanja wa Old Trafford, katika droo ya tisa ya promosheni ya Airtel Mimi ni Bingwa. Wakati wa droo hiyo iliyochezeshwa jana, washindi 14 wa pesa taslimu ya zaidi ya Shilingi milioni 22 walipatikana. Kushoto ni Msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha Tanzania Mrisho Millao.


  0 0

  Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Professa Ibrahim Haruna Lipumba akimnadi mgombea wa Chama hicho katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki, Abdulmalik Haji Jecha, katika uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki zilizofanyika Bustani ya Kiembesamaki, Wilaya ya Magharibi Unguja.
  Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Professa Ibrahim Haruna Lipumba na viongozi wengine wa chama hicho wakirusha mabofu kama ishara ya uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki uliofanyika Bustani ya Kiembesamaki, Wilaya ya Magharibi Unguja.
  Baadhi ya wanachama wa Chama cha Wananchi (CUF) wakimsikiliza Mwenyekiti wa Chama hicho Professa Ibrahim Haruna Lipumba katika uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki katika kiwanja cha Bustani ya Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi Unguja.
  ========  ========    =========
  Na Miza Kona – Maelezo

  Mwenyekiti wa chama cha Wananchi CUF Taifa Profesa Ibrahim Haruna Lipumba amewataka wananchi wa Jimbo la Kiembesamaki kumchagua kiongozi atakayeweza kuingia katika bunge la katiba na kuyatetea na kuleta maslahi ya Zanzibar.

  Kauli hiyo ameitoa jana huko Kiembesamaki wakati alipokuwa akizindua kampeni na kumtambulisha mgombea uwakilishi kupitia chama hicho.  Amesema kiongozi bora ni yule atakaeweza kuitetea Zanzibar na kuipatia maendeleo na kupata mamlaka yake kamili pamoja na  kuleta mabadiliko.

  Aidha ameeleza kuwa CUF inataka kuleta mabadiliko katika mambo ya muungano na kuona kuwa haki inafanyika katika nchi zote.  Aidha amesema kupita chama cha CUF wananchi watapata kiongozi mzuri atakaeweza kuingia kwenye bunge la katiba na kuitetea nchi bila ya woga wala kupoteza mwelekeo.

  “Mpeleke mtu atakaeweza kuingia kwenye bunge la katiba na kutetea maslahi ya Zanzibar”, alifahamisha. Hata hivyo amesisitiza kuwa uchaguzi ufuate utaratibu uwe huru na haki bila ya kushirikisha vyombo vyengine.

  Nae mgombea uwakilishi AbdulMalik Haji Jecha amesema pindipo wananchi watamchagua ataitetea Zanzibar kwa moyo wa uzalendo na kuleta maendeleo kwa maslahi ya nchi.

  Uchaguzi huo mdogo wa jimbo la Kiembesamaki unafanyika kutokana na aliyekuwa mwakilishi wa Jimbo hilo Mansour Yussuf Himid kuvuliwa uwanachama kupitia CCM.

  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

  WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO

                                    
                                  


  TANGAZO


  Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, inawaalika Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini kote nchini kushiriki katika kikao kazi kitakachofanyika katika Hotel ya Tanga Beach Resort kuanzia Februari 3 hadi 8, 2014 Mkoani Tanga.


  Washiriki wote wanakumbushwa kulipa ada ya ushiriki kabla ya tarehe 30 Januari, 2014.


  Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Matumizi ya Tehama na Mitandao ya Kijamii katika kuimarisha Mawasiliano ya Serikali kwa Umma”


  “WOTE MNAKARIBISHWA”
  0 0


  0 0

  Na Frank Mvungi- MAELEZO.


   WIZARA ya Mambo ya Ndani ya Nchi imefanikiwa kukusanya sh. bilioni 83.4 kufikia mwaka 2013/2014 ambazo zinatokana na shughuli mbalimbali zilizofanywa na Idara ya Uhamiaji. Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mh Pereira Ame Silima wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam akieleza mafanikio ya Wizara.

  Mh Pereira alibainisha kuwa kwa kipindi cha mwaka 2006/2007 zilikusanywa shilingi bilioni 14.2 ambapo  kumekuwa na ongezeko la bilioni 69.2 kufikia mwaka 2013/2014 ambayo ni moja ya mafanikio ya Serikali ya awamu ya nne.


  Mh Pereira alibainisha kuwa Ongezeko hilo ni matokeo ya juhudi zilizofanywa na Serikali katika kuboresha mifumo ya makusanyo ya maduhuli kwenye vyanzo mbalimbali vya Wizara. Aliongeza kuwa jumla ya magari 192 yalitolewa kwa idara hiyo, 93 yakiwa ni msaada ya wafadhili.

  Alitaja vifaa vingine vilivyonunuliwa kwa ajili ya Idara hiyo ni pikipiki 206 na boti mbili (02) ambazo hutumika kufanya misako na doria katika maeneo mbalimbali nchini ikiwa ni hatua za maksudi katika kupambamna na uhalifu.


  Kwa upande wa jeshi la Polisi, Mh. Pereira alisema kuwa wamefanikiwa kupunguza uhalifu kutoka makosa 53,268 mwaka 2005 hadi  kufikia 45470 mwaka 2013. Alitaja sababu kubwa ya kupungua kwa vitendo vya uhalifu nchini kuwa ni ushirikiano mzuri toka kwa wananchi kwa kutumia mfumo wa ulinzi shirikishi,utii wa sheria bila shuruti,vifaa vya kisasa kwa askari yakiwemo magari, pikipiki na boti kwa ajili ya doria.

  Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi inaundwa na Jeshi la Polisi,Jeshi la Magereza,Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,Idara ya Uhamiaji,Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa,Idara ya Huduma kwa Jamii.


  Mwisho.


  0 0


  Askari akiwa amemnasa mahabusu aliye kimbia mara baada ya kujipaka kinyesi katika mahabusu ya mahakama ya wilaya ya Nyamagana na Mahakama ya Mwanza.

   HUWA YANASIKIKA KUTOKEA LAKINI LEO NI LAIVU BILA CHENGA...... Mahabusu mmoja aliyekuwa mahabusu ya mahakama ya wilaya ya Nyamagana na Mahakama ya Mwanzo iliyopo eneo la jirani na Mamlaka ya maji safi na Hifadhi ya Mazingira (MWAUWASA) jijini Mwanza alitoa vioja vya mwaka kwa kujaribu kutoroka kwa kujipaka kinyesi ili asiguswe wala kukamatwa.

  Mtuhumiwa huyo ambaye jina lake halikufahamika alijimwagia kinyesi kilichokuwa kwenye ndoo iliyokuwa ndani ya sero ya Mahakamani hapo na askari alipokwenda kufungua ili kuwapeleka watuhumiwa kwenye chumba cha Mahakama kusomewa kesi yake baada ya kutajwa na karani wa Mahakama ya mwanzo, baada ya kutajwa ndipo mahabusu huyo alipopata mwanya wa kukimbia na kutoa tahadhari kwa atakaye mgusa au kumshika atakumbana na kadhia ya kuchafuliwa kwa kupakwa kinyesi.

  Askari mwingine mwenye cheo cha sajenti, ambaye alikuwa akihushughulika na huduma nyingine mahakamani hapo, kwa kuwa alikuwa na uzoefu wa kupambana na mikasa na vioja kama hivyo vya mahabusu wanao kula njama za kutaka kutoroka aliamua kula naye sahani moja kwa kumkimbiza na kufanikiwa kumkamata.

   Baada ya kumkamata na kumrejesha katika chumba cha mahabusu mahakamani hapo, kwanza mtuhumiwa huyo aliamriwa kuzoa mtondoro wa kinyesi cha binadamu alichokuwa amejimwagia na kutapakaa chini na mara baada ya kumaliza kuzoa uchafu huo, alipelekwa kwa hakimu ambapo alisomewa kosa la kula njama za kutoroka na kukumbana na adhabu nyingine ya kuhukumiwa kifungo cha miezi sita (6) jela, huku kesi yake iliyokuwa ikimkabili awali ikiahirishwa.
  "Kama alivyojipaka ndivyo alivyo yazoa..."
  Moja baada ya jingine.
  Hatua kwa hatua chini ya ulinzi mkali wa askari shupavu.
  Huku akiweka kinyesi hicho kwenye ndoo mahabusu huyo alilazimika kukizoa kwa mikono kama muuza mkaa apimavyo mkaa kwenye kopo kuwauzia wateja wake. 
  Mchafuzi wa mazingira akiadabishwa kabla ya kwenda kusomewa kesi nyingine ya kula njama za kutaka kutoroka.
  Hatari....PICHA KWA HISANI YA GSENGO BLOG

  0 0

  Tarehe 27 January mimi Anna Peter ambaye ni mtangazaji wa East Africa Radio, mwanzilishi wa kampeni ya kusaidia kinamama na watoto wenye matatizo mbalimbali katika jamii 'SaidiaMaMa na mwimbaji pia nitakuwa nasherehekea siku yangu ya kuzaliwa.

  Mwaka huu nimeamua nitumie sauti yangu ambyo Mungu amenibariki kushare na Wasichana na wanawake wenzangu kokote pale duniani ujumbe huu 'Tunaweza' ambao wimbo wake utatoka rasmi siku hiyo tarehe 27.


  TUNAWEZA.

  Chorus;

  Wanawake Tunaweza, Wasichana Tunaweza

  Tunaweza, Tunaweza X2

  Kwa pamoja Tunaweza.


  VERSE I.

  Fanya kazi yako ya mikono,Kwa moyo

  Wala hutakosa kupata mapato.

  Amka kabla haujaisha usiku

  Amka kabla haujaisha usiku

  Upendeleo usikundanye

  Pia uzuri usikuhadae

  Angalia Shamba ukalime

  Biashara pia ukafanye


  VERSE II.

  Kwa mapato yako yote jipatie ufahamu kokote

  Mkamate sana elimu usimwache aende zake

  Hiyo ni silaha yakooo

  Ona madaktari wanawake

  Nasema Ona marubani wanawake

  Ona viongozi,maraisi wanawake.

  Chorus.


  Jipambe kwa mavazi ya kujisitiri

  Pamoja na adabu nzuri

  Na moyo wa kiasi

  Utaweza kuwa yeyote

  Utaweza kufanya chochote

  Unaweza,Utaweza

  --------end----------


  Mtunzi:Anna Peter

  Msanii:Anna Peter ft Hellen

  Mtayarishaji:Mr T Touch


  Studio:Seductive Rec


  0 0


  A section of Members stand for the EAC anthem during the Special Sitting.
  The Speaker of EALA with President Yoweri Museveni to the Parliament of Uganda.
  The President is led into the Chambers by the EALA Serjeant-at-Arms with the Speaker in tow.
  The Speaker of EALA receives President Yoweri Museveni to the Parliament of Uganda. 

  =======  ========  =========

  Kampala, Uganda: President Yoweri Museveni has today addressed the 4th Meeting of the 2nd Session of the 3rd East African Legislative Assembly in Kampala, Uganda.

  The President maintained that the EAC was on course and its progress irreversible.  The President noted that the Community was on the verge of prosperous economic development and better quality of life for its citizens following the significant progress in a number of socio-economic and political spheres.

  The Head of State remarked that what the region now needed was to strengthen competitiveness, address costs doing business and reduce risks.

  He noted that free movement was a key aspect of strengthening integration and remarked that the Republic of Uganda was committed to ensuring the Identity Cards’ project would soon be computerized to spur free movement.

  “Once this is done, many more people who cannot access passports which are expensive to acquire”, President Museveni remarked.

  On matters business, the Head of State remarked that the on-going digitization of customs’ systems had made business to be more efficient.

  The Head of State called for the opening up and the enhancement of the central corridor to fast track business opportunities and the clearance of cargo. He remarked that the President of the United Republic of Tanzania, H.E. Jakaya Mrisho Kikwete would review and revert back to the Summit over the matter.   The President said Uganda would commence the construction of the standard gauge railway from Malaba to Nimule and from Malaba to Kasese to Rwanda border.  

  The President urged the region to reduce the costs of transportation.   A forty foot container From Shanghai to Beijing costs on average 1600 USD, while it costs USD 3700 from Kampala to Mombasa. But the distance between the two cities in China is 1,238 Miles while that of Mombasa to Kampala is 1212, President Museveni added.  “ Ideally, the costs are high and the days are many due to inefficiencies”, he remarked.  This affects competition and catching up is a challenge”, he added.

  The business community, President Museveni said need to reap profits and create employment to enhance their economies, adding that real competition was not between neighbours in EAC but between the region and other nations.

  On the Single Tourism Visa, President Museveni maintained that the new date of implementation is February 2014.  He said that the countries had put in place systems of revenue sharing.  The share arrangement is such that the single entry visa costs USD 100 and that any. country that issues the visa is entitled to a 10 USD, then in addition, equitably sharing the balance accordingly while the rest of the Partner States.

  The President however cited violence and instability as hindering factors to prosperity in the continent.  The conflicts, President Museveni added are fueled by ideological mistakes.   The Head of State noted that instability in Congo, Central African Republic, South Sudan and Somalia among others had an impact on the region. He challenged countries to strive to see maintain nationalism. Prosperity arises out of nationalism and it is in the best interests of citizens of the region to attain this fact while putting to an end sectarianism.

  The President said Uganda’s economy was expected to grow by USD 28 Billion (Uganda Shillings 70 trillion) at the end of the financial year and remarked that the economy had expanded nineteen-fold than it was in 1986 when the NRM took power.

  He hailed the region for realizing the Monetary Union and cited infrastructure as a stimuli for development.  Such include roads, telecommunications, ICTs, piped water and electricity among others.

  The Head of State said the government had revamped East African Civil Aviation Academy (Soroti Flying School) and was looking at enhanced remuneration for the piloting staff to enable them deliver. The statement came in response to EALA Speaker’s plea for the transfer of the Soroti Flying School to be an institution of the EAC.
  The President noted that the future and destiny of the region was in their own destiny.

  In attendance were key government officials led by the Vice President of the Republic of Uganda, Hon Edward Ssekandi, EALA Members and representatives of the diplomatic corp among others.

  In her welcome remarks, the Speaker of the EALA, Rt. Hon Margaret Nantongo Zziwa noted that the Sitting was taking place at an irreversible time in the regional integration process.  She noted the envisaged entry of the Monetary Union as key in the integration process.

  “The signing of the integration pillar was a milestone and I thank the Summit and the Partner States for the historic achievement, Dr Zziwa maintained.

  The Speaker urged the region to draw upon the important lessons from other regions in order to manage the roadmap to the single currency carefully.

  “It is in our best interest to consult widely as a region to avoid what befell the Euro Zone – which today continues to reel from economic depression, huge public debts and unemployment” she added. The Speaker noted that the region had made significant accomplishments in 2013.  She cited infrastructural advancements in rail, energy ports and habors sub-sector as some of the achievements.

  “I note the positive construction of the Standard Gauge railway which commenced last year while concerted efforts were made to decongest the ports of Mombasa and Dar es Salaam”, the Speaker said.

  Rt. Hon Zziwa urged the stakeholders including the Private Sector to sustain efforts to rid Non Tariff Barriers.  “It is time for the Private sector for example to oversee an industry developed, implemented and monitored code that checks out on NTBs or their re-emergence”, Rt. Hon Zziwa said.

  On peace and security, the Speaker called for all cessation of hostilities in South Sudan noting that the recent deployment of the UPDF in Juba was sanctioned by the IGAD to stop the conflict from degenerating any further.

  Rt. Hon Zziwa shared the scorecard of 3rd EALA so far, over the last one year to an attentive audience.  She cited, inter-alia, the passage of 7 key Bills (One Stop Border Post Bill, 2012, EAC Vehicle Load Control Bill, 2012, EAC Appropriation Bill, 2012, EAC Supplementary Appropriation Bill, 2013, the East African Community Customs Management (Amendment) (No. 2) Bill, 2012 and the EAC Public Holidays Bill, 2013), several Reports and 25 Resolutions – all key to integration dispensation.

  Over the next two weeks, the Plenary shall debate on the EAC Co-operatives Societies Bill, 2013, debate on the Disaster Risk Reduction and Management Bill, 2014, the EAC Integration (Education) Bill 2014 and the EAC Supplementary Appropriation Bill, 2014. The Assembly is also set to debate and adopt various Committee Reports that shall be brought to the floor of the House.

  Moving the vote of thanks, Hon Joseph Kiangoi noted that Uganda had progressed following the leadership of President Museveni.

  “Your passion for education for all is helping to develop the country.  The initiatives on science and technology in higher institutions of learning cannot go unnoticed.   This has resulted in the building of an electrical car (The Kiira EV) in Uganda a few years ago, the only kind in East Africa.  Today, Mzee’s government is spearheading innovations in agriculture, health and in ICTs.  This is laudable” Hon Kiangoi remarked.

  Hon Kiangoi said that EALA was committed to actively playing its mandate to strengthen integration.

  0 0  0 0

  Marehemu Said Bwanamdogo

  0 0


  0 0


   
  Naibu Waziri wa Fedha Mh:Mwigulu Nchemba akipokea Zawadi ya Ua wakati akipokewa na Wafanyakazi wa Wizara hiyo jijini Dar leo,Tukio hilo limefanyika Nje ya Wizara ya Fedha ambapo mamia ya Wafanyakazi asubuhi ya leo walijitokeza Kuwalaki Mawaziri wapya walioteuliwa na Rais Kikwete wiki iliyopita ili kujaza nafasi za Mawaziri wanne zilizokuwa Wazi kutokana na Kujiuzulu pamoja na Kifo cha Waziri wa Fedha Marehemu Mgimwa. 
  Mh:Malima ambaye ni Naibu waziri wa Fedha akipokea Zawadi ya Ua wakati wa alipofika Rasmi Ofisini hii leo kwaajili ya Kuanza Majukumu yake baada ya Kuapishwa na Rais Jakaya Kikwete kuwa Naibu Waziri wa Fedha.
   
  Mapokezi yakiendelea asubuhi ya  leo Nje ya Wizara ya Fedha.
  Mapokezi Yanaendelea,Watumishi wa Wizara ya Fedha walijitokeza Kwa wingi  kuwapokea Manaibu Waziri wapya wa Wizara hiyo.(Mh:Mwigulu Nchemba na Mh:Adam Malima) Pembeni (Kushoto) ni Mkurugenzi wizarani hapo aliyeongoza mapokezi hayo
   
  Naibu Waziri wa Fedha Mh:Mwigulu Nchemba akilakiwa na Maofisa wa Wizara ya Fedha mapema hii leo asubuhi wakati alipofika Ofisini hapo rasmi kuanza kazi.
   Naibu Waziri wa Fedha Mh:Mwigulu Nchemba akibadilishana Mawazo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha wakati wa hafla ya Kuwapokea Mawaziri hao Wapya hii leo zoezi lililofanyika Wizara ya Fedha na Kukamilika Jioni ya Leo.  Picha Zote na HABARI KWANZA BLOG

  0 0

  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimtambulisha mgombea wa Uwakilishi Jimbo la Kiembesamaki CCM Mahamoud Thabit Kombo kwenye uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Uwakilishi wa Jimbo hilo uliofanyika leo 22 Januari 2014 katika uwanja wa Tawi la CCM Kiembe samaki.
  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Ilani Katiba na Sera ya CCM mgombea wa Uwakilishi Jimbo la Kiembesamaki CCM Mahamoud Thabit Kombo kwenye uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Uwakilishi wa Jimbo hilo uliofanyika leo 22 Januari 2014 katika uwanja wa Tawi la CCM Kiembe samaki. (Picha na OMR)

  0 0
 • 01/22/14--13:02: MAMBO YA MZALENDO PUB HAYO


 • 0 0
    M4C- Operesheni Pamoja Daima ilivyotikisa leo mkoani Ruvuma- Timu ya Katibu Mkuu, Dkt. Slaa akiwa na Mbunge Peter Msigwa. 
   Wananchi wakisikiliza mkutano huo
   Dr Slaa akisalimia Wananchi. 
   Dr Slaa akihutubia wakazi wa Ruvuma jana kwenye mkutano wa hadhara.
    Mbunge wa Chadema,John Mnyika akihutubia wananchi wa Uyui  Tabora mjini kwenye mkutano wao wa hadhara.M4C- Operesheni Pamoja Daima, mkutano wa Tabora mjini, Uyuwi, Timu ya Makamu Mkiti Zanzibar Said Issa Mohamed na John Mnyika


  0 0

   Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimtambulisha mgombea wa Uwakilishi Jimbo la Kiembesamaki CCM Mahamoud Thabit Kombo kwenye uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Uwakilishi wa Jimbo hilo uliofanyika leo 22 Januari 2014 katika uwanja wa Tawi la CCM Kiembe samaki.
  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Ilani Katiba na Sera ya CCM mgombea wa Uwakilishi Jimbo la Kiembesamaki CCM Mahamoud Thabit Kombo kwenye uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Uwakilishi wa Jimbo hilo uliofanyika leo 22 Januari 2014 katika uwanja wa Tawi la CCM Kiembe samaki.

    Wananchi na Wanachama wa CCM Zanzibar wakimsikiliza Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, alipokua  akihutubia kwenye uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Uwakilishi wa Jimbo hilo uliofanyika jana jioni 22 Januari 2014 katika uwanja wa Tawi la CCM Kiembe samaki.

   Mfalme wa Taarab Mzee Yusssuf na Mgombea Uwakilishi jimbo la KiembeSamaki CCM Mahamoud Thabit kombo wakitoa burudani kwenye uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Uwakilishi Jimbo hilo uliofanyika jana jioni 22 Januari 2014 katika uwanja wa Tawi la CCM Kiembe samaki. 
   Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai  akihutubia wananchi na wanachama wa CCM kwenye uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Uwakilishi wa Jimbo hilo uliofanyika jana jioni 22 Januari 2014 katika uwanja wa Tawi la CCM Kiembe samaki.
   Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wananchi na wanachama wa CCM kwenye uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Uwakilishi wa Jimbo hilo uliofanyika jana jioni 22 Januari 2014 katika uwanja wa Tawi la CCM Kiembe samaki.(Picha na OMR)

  0 0

  Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (kushoto) akimsikiliza Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM,Mzee Yusuph Makamba (wa pili kushoto) wakati alipokuwa akimtambulisha dada zake,wakati Mh Lowassa alipokwenda kumpa pole Mzee Makamba aliepatwa na msiba wa kufiwa na mama yake mzazi huko kijijini kwake Maezangula wilaya ya Korogwe,Mkoani Tanga jana.
  Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (katikati) na Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM,Mzee Yusuph Makamba wakimsikiliza Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia,Mh. January Makamba wakati wa mazungumzo yao.Mh Lowassa aliitembelea Familia ya Mzee Makamba kwa  kumpa pole kwa kupatwa na msiba wa kufiwa na mama yake mzazi huko kijijini kwake Maezangula wilaya ya Korogwe,Mkoani Tanga jana.

  0 0

   Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akimkaribisha Waziri Mkuu Mstaafu,Mh.Frederick Sumaye alipowasili mapema leo kwenye makao makuu ya ofisi hizo zilizopo Mikocheni jijini Dar,pichani kati anaeshuhudia ni Ofisa Mahusiano wa Clouds Media Group,Simon Simalenga.
    Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akitoa maelezo mafupi kwa Waziri Mkuu Mstaafu,Mh.Frederick Sumaye kwenye moja ya Ofisi za kampuni hiyo,alipofanya ziara fupi mjengoni humo na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na kampuni hiyo zikiwemo  na urushaji wa matangazo ya redio na Televisheni kwa ujumla. pichani kati anaeshuhudia ni Ofisa Mahusiano wa Clouds Media Group,Simon Simalenga.
   Mkuu wa Kitengo cha Habari Clouds FM,Joyce Shebe akitoa ufafanuzi mfupi  kwa Waziri Mkuu Mstaafu,Mh.Frederick Sumaye alipotembelea kitengo hicho cha habari na kujionea uandaaji wa habari ya televisheni na redio unavyofanyika.
   Mmoja wa Watangazaji kipindii cha Michezo Clouds FM,kiitwacho Sports Extra, Ibrahim Masoud a.k.a Maestro akifanya mahojiano mafupi na Waziri Mkuu Mstaafu,Mh.Frederick Sumaye kuhusiana ushabiki wake mkubwa kwa timu ya Simba sambamba na migogoro iliyoikumba club hiyo ya Msimbazi
   Ruge Mutahaba akitoa ufafanu mfupi kwa Waziri Mkuu Mstaafu,Mh.Frederick Sumaye,kuhusiana na Kifaa maalum na cha kisasa cha kurushia matangazo ya biashara,pichani nyuma ni Mkuu wa Kitengo cha Habari Clouds FM,Joyce Shebe akisikiliza.
   Waziri Mkuu Mstaafu,Mh.Frederick Sumaye akiwa kwenye chumba cha kurekodia mahojiano mbalimbali,akiwa amekutana na wadau wa Mfuko wa Dhamana ya Uwekezaji Tanzania (UTT),pichani kulia ni Afisa Masoko Mwandamizi wa UTT,Mfaume Kimario na Afisa Masoko na Uhusiano,Bwa.Rahim Mwanga
  Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akitoa maelezo mafupi kwa Waziri Mkuu Mstaafu,Mh.Frederick Sumaye kuhusiana na urushaji wa matangazo kwa njia ya kisasa ndani ya studio kuu ya redio Clouds FM,Sumaye amefanya ziara fupi mjengoni humo na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na kampuni hiyo zikiwemo  na urushaji wa matangazo ya redio na Televisheni kwa ujumla. 
  Ruge Mutahaba akimtambulisha Mkurugenzi mwanzake wa Maendeleo ya Biashara,Sheba Kussaga kwa Waziri Mkuu Mstaafu,Mh.Frederick Sumaye
  Mkuu wa Kitengo cha uzalishaji vipindi wa Clouds TV,Bwa Kanyopa akitoa ufafanuzi mfupi kwa Waziri Mkuu Mstaafu,Mh.Frederick Sumaye namna ya kuandaa na kuhariri vipindi vya televisheni.
  Ruhe Mutahaba akitoa maelezo mafupi kwa Waziri Mkuu Mstaafu,Mh.Frederick Sumaye kuhusiana na mitambo ya kisasa ya kurushia matangazo ya televisheni na ubora wa picha za televisheni unaotoka kwenye mitambo hiyo ya kisasa. 

  0 0

  Mara baada ya kuundwa kwa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa inayoongozwa na Katibu Mkuu Ndg. Abdulrahman Kinana mwanzoni mwaka mwaka jana, Sekretarieti hiyo imejiwekea utaratibu wa kufanya ziara mikoani kukutana na wananchi kusikiliza kero zao,kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na kuimarisha Chama mikoani. Utaratibu huu ni agizo la mkutano mkuu wa Taifa wa nane wa CCM uliofanyika Novemba 2012 mjini Dodoma. Nanukuu azimio hilo;
   
  “ Chama Cha Mapinduzi lazima kiwe karibu na wananchi, kisikilize changamoto zao na kiwasemee wananchi na hasa wanyonge” Moja ya maazimio ya Mkutano Mkuu wa nane wa CCM 2012.
   
  Kwa hiyo msingi wa kwanza wa ziara hizo ni maagizo ya Mkutano Mkuu wa CCM Taifa ambacho ndicho kikao cha juu kabisa cha Chama. Msingi wa pili ni ukweli kuwa CCM ndio iliyopewa dhamana na kuingia mkataba na wananchi kupitia ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010/2015, hivyo inayowajibu wa kukagua utekelezaji wa ilani hiyo.
   
  Na bila shaka wote tumeshuhudia jinsi ziara hizo zilivyoinua uhai wa Chama nchi nzima na kuongeza kasi ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi na kutatua kero mbalimbali za wananchi kwenye maeneo yao, kiasi cha kuongeza imani ya wananchi kwa CCM.
   
  Tumeshuhudia makundi mbalimbali ndani ya jamii yakija kueleza changamoto zao ndani ya Chama. Makundi hayo ni pamoja na makundi ya wakulima, wafugaji, wafanyabiashara, wanafunzi na wafanyakazi hasa walimu. Huu ni uthibitisho wa kuongezeka kwa imani yao kwa CCM.
   
  Katika mwendelezo wa ziara hizo mwishoni mwa mwaka jana Katibu Mkuu wa CCM na baadhi ya wajumbe wa Sekretarieti walifanya ziara ya siku 26 katika mikoa ya Ruvuma, Mbeya na Njombe. Pamoja na mambo mengine wananchi walilalamikia baadhi ya watendaji wa serikali hasa baadhi ya mawaziri wakiamini kuwa yapo mapungufu kadhaa yanayotokea kwenye wizara zao.
   
  CCM kama lilivyo agizo la Mkutano mkuu la kuwasemea wananchi tulisikiliza kilio chao na kwa kufuata utaratibu, baadhi ya mawaziri hao waliitwa na kuhojiwa kwenye Kamati Kuu ya CCM mwezi Disemba 2013.

   Utaratibu wa watendaji wa serikali kutoa taarifa za utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwenye vikao vya Chama sio mgeni na wala haujaanza jana. Wakuu wa wilaya hutoa kwenye wilaya, wakuu wa mikoa hutoa mikoani kwao,hivyo sio utaratibu mpya.
   
  Baada ya mahojiano hayo Kamati Kuu ya CCM ilitoa ushauri kwa serikali wa namna ya kurekebisha mapungufu yaliyoelezwa na wananchi. Kwakuwa kwa mujibu wa Katiba ya Nchi mwenye mamlaka na mawaziri ni Rais mwenyewe, CCM ililiacha suala hili kwake aangalie njia ipi bora ya kuondoa mapungufu tuliyoyaeleza.
   
  Na kwenye taarifa yetu kwa vyombo vya habari baada ya kikao hicho tulisisitiza kuwa sio lazima awafukuze mawaziri husika isipokuwa wanaweza kufanya mabadiliko katika mfumo,sheria nk ili mradi kuwepo na mabadiliko katika kushughulikia mambo yaliyolalamikiwa na wananchi.
   
  Hivi karibuni Rais amefanya mabadiliko kidogo kwenye baraza lake la mawaziri na kuwarudisha baadhi ya mawaziri waliolalamikiwa na wananchi na wabunge, ambao malalamiko hayo yaliungwa mkono na CCM. Ni kupitia malalamiko hayo ndipo lilipozaliwa jina la mawaziri mizigo. Baada ya uteuzi huo kukaibuka mjadala mkubwa nchini wakihoji kulikoni Rais kaamua kutowatimua mawaziri hao.
   
  Kwanza haikua hoja ya CCM kuwafukuza mawaziri hao bali kuchukua hatua za kurekebisha mapungufu husika. Kufukuza inaweza kuwa ni njia ya kutatua tatizo lakini sio njia pekee. Hivyo basi CCM tunaamini kuwa kurudishwa kwao wamepewa fursa ya kurekebisha mapungufu tuliyoyasema kwa niaba ya wananchi. Tunaamini mawaziri wote hawatabweteka bali watatimiza wajibu wao na kuhakikisha wanawatumikia wananchi ambao ndio waajiri wa serikali.
   
  Ifahamike kuwa Chama Cha Mapinduzi hakitasita kuchukua hatua kali dhidi ya mawaziri na watendaji wengine watakaoshindwa kurekebisha mapungufu na watakaoshindwa kutimiza wajibu wao vizuri. Wakumbuke kushindwa kwao kutimiza majukumu yao ni hujuma kwa Ilani ya uchaguzi ya CCM, CCM haitavumilia usaliti huo. Kukaa kimya kwa CCM itakua ni kujinyonga yenyewe jambo ambalo hatutaruhusu kabisa.
   
  Tunajua wapo baadhi ya watendaji wa serikali wasiopenda kuhojiwa utendaji wao, tunawasihi kwa moyo safi wasiotaka kuulizwa juu ya utendaji wao waondoke serikalini wenyewe kwani CCM tutakuwa wakali sana kwenye mapungufu,kwani tukikaa kimya tutakua tunajihujumu wenyewe.
   
  Tutatumia vizuri wingi wa wabunge wetu bungeni na wingi wa madiwani wetu kwenye halmashauri kuisimamia vizuri serikali. Hivyo kuanzia sasa kasi ya CCM kuisimamia serikali, kuisifu itakapofanya vizuri na kukosoa itakapofanya vibaya itaongezeka mara dufu kwa kila ngazi.
   
  Tunawaomba watanzania kwa ujumla tuwape muda wateule hawa wa Rais watimize wajibu wao, lakini tusisite kusema pale tutakapoona mambo hayaendi kama tunavyotarajia.Uwajibikaji wa kweli ndio msingi wa mafanikio na maendeleo yetu.
   
  CCM inawatakia kila lakheri kwenye kutimiza wajibu wao. Tuna matumaini makubwa kuwa wote kwa pamoja hawataisaliti ilani ya Uchaguzi ya CCM na kwamba hawatayaangusha matumaini ya wananchi kwa serikali yao.
   
  KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI!
   
   
  Imetolewa na;
  Nape Moses Nnauye
  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi
  23/01/2014


older | 1 | .... | 207 | 208 | (Page 209) | 210 | 211 | .... | 1898 | newer