Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46201 articles
Browse latest View live

Waziri Nyalandu na Naibu wake wapokewa kwa shangwe Wizara ya Maliasili na Utalii leo jijini dar

0
0

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Bi. M.Tarishi (kushoto), Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mahmood Mgimwa (Katikati) na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu (Kulia) wakibadilishana mawazo baada ya mkutano wao na watumishi wa wizara ya maliasili na utalii.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mahmood Mgimwa akiongea na watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii.
 Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akisalimiana na baadhi ya watumishi wa Wizara ya Maliasili.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mahmood Mgimwa akisalimiana na Mkurugenzi Msaidizi katika Idara ya Wanyamapori, Profesa Kidegesho.

========  =======  =========
WAZIRI mpya katika Wizara ya Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu na Naibu Waziri mpya mh. Mahmood Mgimwa wamepokelewa kwa shangwe mapema leo makao makuu ya wizara ya Maliasili na Utalii jijini Dar es Salaam.

Wizara ya Maliasili na Utalii imefanya mapokezi ya Mawaziri wake wapya leo Jumanne 21 Januari 2014, ambapo watumishi waliopo Makao Makuu ya wizara wamepata fursa ya kukutana na kufanya maongezi na mawaziri hao. 

Mapokezi hayo yanafuatia mabadiliko ya Baraza la Mawaziri yaliyofanywa na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzanaia Mhe. Jakaya Kikwete.

Naibu Waziri Mhe. Mahmood Mgimwa amewaahidi wafanyakazi wa Maliasili na Utalii kufanya kazi kwa ushirikiano wa hali ya juu ili kuweza kuleta maendeleo ambayo wananchi wanayategemea kutoka katika Wizara hii.

Kwa upande wake, Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu amewakikishia wafanyakazi wa Wizara ya Maliasili na Utalii kufanya kazi kwa ushirikiano na weledi ili kuweza kuifanya Wizara kuongeza pato la Taifa kupitia Utalii. 

Aidha, Mhe Nyalandu amewaasa watumishi wote kudumisha amani na upendo katika maeneo yao ya kazi ili kujenga mazingira mazuri ya kazi na kuongeza ufanisi..

IDDI BONGE AJIANDAA KUMKABILI MWAKASANGA MARCH 23

0
0

Kocha wa mchezo wa ngumi Kwame Mkuluma kulia akimwelekeza jinsi ya kupiga ngumi bondia Iddi Kipandu 'Iddy Bonge' wakati wa mazoezi yanayoendelea kwa ajili ya mpambano wake wa march 23 na David Mwakasanga utakaofanyika ukumbi wa frends corner Manzese, mazoezi hayo   katika klabu ya biafra iliyopo kigogo Mbulahati Dar es salaam .

wabunge wanawake Tanzania watembelea ofisi za ubalozi mjini London

0
0

Mhe. Balozi wa Uingereza Peter Kalaghe (katikati mwenye suti) akiwa na wah. Wabunge Wanawake wakiongozwa na Mwenyekiti wa TWPG mama Anna Abdallah (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu wa TWPG Dk. Mary MWANJELWA-walipotembelea ofisi ya Ubalozi huo Mjini London tar. 19/1/2014. Ujumbe huo upo nchini Uingereza kwa mwaliko wa Bunge la nchi hiyo-CPA kwa mafunzo.

CCM NA CHADEMA WAZINDUA KAMPENI YA UCHAGUZI MDOGO WA UDIWANI KIBORILONI.

0
0

 Katibu Mwenezi wa CCM mkoa wa Kilimanjaro, Michael Mwita (Kushoto)
akiteta jambo na Mgombea wa kiti cha Udiwani kata ya Kiboriloni wa
tiketi ya chama cha Mapinduzi, Willy Adriano, wakati wa Uzinduzi wa
Kampeni kuelekea uchaguzi mdogo kuziba pengo lililoachwa wazi na
aliyekuwa Naibu Meya na Diwani wa Kata hiyo,, Marehemu Vincent Rimoy
aliyefariki dunia Novemba 6, mwaka jana.
 Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kilimanajro, Iddi Juma,
(aliyeshika kipaza sauti), akimnadi mgombea wa CCm katika Uchaguzi
mdogo wa Udiwani, Wlly Adriano katika uchaguzi uzinduzi wa kampeni za
uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Februari 9 mwaka huu kuziba pengo
lililoachwa wazi kufuatia kifo cha aliyekuwa Diwanbi wa Kata ya
Kiborloni, Vincent Rimoy, alyefariki dunia ghafla Novemba 6 mwaka
jana.
Katibu wa CCM mkoa wa Kilimanjaro, Steven Kazidi (kushoto), akiwa
akimtambulisha Mgombea wa Udiwani katika kata ya Kiboriloni, Willy
Adriano aliyesimama katikati, kulia kwake ni Mke wake.(Picha zote na
Taifa Letu.com Blog)

=========  =======  =========
Na Mwandishi Wetu, Moshi

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), mwishoni mwa wiki walifanya uzinduzi wa Kampeni za uchaguzi      mdogo wa udiwani katika kata ya Kiboriloni liliachwa wazi kufuatia kifo cha aliyekuwa diwani wa kata hiyo, Vincent Rimoy (CHADEMA), aliyefariki ghafla Novemba 6 mwaka jana.



Wa kwanza kufanya uzinduzi ni Chadema, waliozindua kampeni yao kwa
mbwembwe wakimtambulisha mgombea wao, Frank Kagoma ambaye ni
mwenyekiti wa mtaa wa Mnazi, uzinduzi ulioongozwa na viongozi
mbalimbali wa ngazi za juu wa chama hicho mkoani hapa akiwemo
mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Kilimanjaro na Mbunge wa Jimbo la Moshi  mjini, Filemon Ndesamburo.



Wakizungumza katika Nyakati tofauti katika uzinduzi huo uliofanyika,
Jumamosi ya Januari 18, mwaka huu, katika stendi ya kidia, viongozi wa
Chadema walianza kumnadi mgombea wao ambap[o walimtaja kama mtu sahihi  ambaye anaweza kuendeleza mapambano ya chama hicho ndani ya baraza la madiwani kupinga ufisadi na uonevu katika manispaa ya Moshi.



Meya wa Manispaa ya Moshi, Jafari Michael, aliwataka wananchi wa kata
hiyo kumchagua mgombea wa Chadema kwani ndiye mwenye uwezo wa
kutekeleza yale yote aliyoyaanzisha Marehemu Rimoy ndani ya kata hiyo
na baraza la madiwani.

“Wananchi wa kiboriloni msidanganyike, chaguo la kweli katika
maendeleo ya kata hii ni Kagoma, katika kipindi chake kama mwenyekiti
Kagoma alifanikiwa kuvunja magenge yote ya ujambazi na sasa mnatembea

vifua mbele bia wasiwasi, tupeni kagoma tuendeleze moto wa Chadema
ndani ya Baraza la Madiwani, tupeni kagoma tukamalizie kazi
aliyoianzisha Rimoy,” alisema Rimoy.

Naye Mbunge wa Jimbo la Moshi mjini, Filemona Ndesamburo alisema kazi
ya kuleta maendeleo katika kata hiyo na mkoa kwa ujumla  unaweza
kufanywa na watu makini wenye uthubutu kama alivyo na uthubutu Mgombe  wa kiti hicho, Frank Kagoma.



Kwa upande wao, Chama cha Mapinduzi CCM, waliofanya uzinduzi wao juzi,
kwa kumtambulisha mgombea wa kiti hicho kwa tiketi ya CCM, Wlly
Adriano walisema Maendeleo ya kata ya Kiborloni ni zaidi ya itikadi za
siasa na kuwataka wananchi wa kata hiyo kufanya uamuzi sahihi.

Akizungumza na maelefu ya wananchi waliojitokeza katika viwanja vya
stendi ya Kidia, Katibu wa CCM mkoa wa Kilimanjaro, Steven Kazidi
alisema wapo baadhi ya wanasiasa ambao wamekuwa wakitafuta madaraka  kwa njia mbalimbali, ikiwemo  kufanya vurugu na maandamano.



 “Unajua ukisikia nchi fulani ina maendeleo kiuchumi, kisiasa na mambo
mengine ni kwa sababu kuna amani, kwa hiyo hili jambo ndugu zangu ni
muhimu sana kulizingatia ili kutuwezesha kuendelea na kazi zetu za
kijamii vizuri” alisema Kazidi.

Kwa upande wake Mchumi wa CCM mkoa wa Kilimanjaro, Paul Matemu,
aliwataka  vijana kutokuuza shada zao za kupigia kura kwani kufanya
hivyo ni kuuuza maendeleo yake.

Aidha Matemu aliongeza kwa kusema  kuwa siasa bila maendeleo hakuna
kujenga msingi wa kuleta maendeleo, na kuwataka wananchi wa kata ya
kiboriloni kuchagua Willy Adriano ili aweze kuwawakilisha katika
baraza la madiwa la Manispaa ya Moshi.

Naye Mgombea udiwani kwa tiketi ya chama hicho, Willy Adriano, alisema
Siasa za Tanzania haziwezi kupiga hatua endapo wananchi hawatabadilika
na kuacha tabia ya kuchaguana kwa kuangalia kigezo cha itikadi za
kisiasa.

Uchaguzi mdogo wa udiiwani  katika kata ya Kiboriloni uunarajiwa
kufanyika Februari 9 mwaka huu kuziba pengo lililoachwa wazi kufuatia
kifocha aliyekuwa diwani wa kata hiyo kwa tikiketi ya chama cha
demokrasia na maendeleo (CHADEMA), Vincent Rimoy.

Rimoy ambaye alikuwa Naibu Meya wa Manispaa ya Moshi, alifariki dunia
ghafla, Novemba 6 mwaka jana, baada ya kudondoka akiwa shambani kwake   eneo la mandaka wilaya ya Moshi.

MWENYEKITI WA CCM MKOA WA MOROGORO AZINDUA KAMPENI ZA UDIWANI KATA YA LUDEWA KILOSA

0
0
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Morogoro Mh Innocent Kalogeris akisalimiana na baadhi ya viongozi wa CCM wilaya ya Kilosa alipowasili kwa ajili ya ufunguzi wa kampeni za udiwani kata ya Ludewa.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Morogoro Mh Innocent Kalogeris Akiwa ameongozana na viongozi wa CCM mkoa wa morogoro wakati wa maandamano ya ufunguzi wa Kampeni za udiwani kata ya ludewa Wilaya ya kilosa
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Morogoro Mh Innocent Kalogeris Pamoja na Mgombea wa Udiwani kata ya ludewa Ndugu Subiri Mwamalili Kulia wakati wakizindua shina la Umoja wa vijana wa Bodaboda kata ya ludewa kabla ya uzinduzi wa kampeni za udiwani katika kata hiyo
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Morogoro Mh Innocent Kalogeris akihutubia wakazi wa kata ya Ludewa wilaya ya Kilosa kwenye viwanja vya CCM Kata ya Ludewa na kuwataka wananchi wa kata hiyo kufanya maamuzi sahihi kwa wakati huu kwa kumchagua Ndugu Subiri Mwamalili Kutoka  CCM kwani ndio chama pekee Kinachowajali wananchi
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Morogoro Mh Innocent Kalogeris Akimnadi Mgombea wa Udiwani Kupitia CCM Ndugu Subiri Mwamalili .
 Mgombea wa Kiticha Udiwani kata ya Ya Ludewa Wilaya ya Kilosa  kwa tiketi ya CCM Subiri Mwamalili  akihutubia wakazi wa kata ya Ludewa wakati wa uzinduzi wa kmapeni za udiwani wa kata hiyo.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Morogoro Mh Innocent Kalogeris  Akimkabidi Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya kilosa jukumu la Kumnadi na kumtembeza kata yote ya Ludewa Mgombea wa Udiwani kata ya Ludewa Ndfugu Subiri Mwamalili.
Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kilosa Akimdani Mgombea wa Udiwani Kata ya Ludewa  Wilaya Kilosa Ndugu Subiri Mwamalili.ANGALIA PICHA ZAIDI

Kampuni ya Issere Sports yazawadiwa

0
0

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo, Amos Makala ambaye kwa sasa amehamishiwa Wizara ya Maji kama Naibu Waziri akimkabidhi vyeti vya utendaji bora wa huduma za michezo Mkurugenzi wa Masoko  Kampuni ya Issere Sports, Abbas Ally Issere katika kongamano la Wasanii lililoandaliwa na Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA),Makala kwa sasa amehamishiwa Wizara ya Maji kama Naibu Waziri.
========  ======  =======

KAMPUNI ya Issere Sports inayojishughulisha na uuzaji wa vifaa vya michezo nchini ni miongoni mwa wanamichezo, wasanii na awaandishi wa habari 1,000 waliotunukiwa vyeti vya utendaji bora katika fani za michezo kwa mwaka 2013 hadi 2014 katika kongamano lililofanyika ukumbi wa Lamada, Ilala Dar es Salaam.

Katika kongamano hilo ambalo kulitolewa mada mbili za kusaidia jamii ya wanamichezo kujiepuka na matumkizi ya dawa za kulevya, ya pili ikiwa ya maadili bora katika jamii, Kampuni ya Issere ni pekee iliyopata nafasi ya kuwakilisha nyingine zinazojihusisha na uuzaji wa vifaaq vya michezo.

Mkurugenzi wa Masoko wa Issere Sports, Abbas Issere aliyepokea vyeti hivyo kwa niaba ya wanamichezo wengine wa Kampuni hiyo alisema zawadi hiyo ni changamoto kwa wanamichezo kushirikiana pamoja badala ya kubaguana ili kurejesha heshima katika michezo kama ilivyokuwa miaka ya zamani na kutoa mfano kuwa katika riadha ilitawaliwa na Selemani Nyambui, Juma Ikangaa na Filbert bayi.

Kampuni ya Issere Sports ambayo imeingia mkataba wa kuuza jezi za Klabu ya Simba, imekuwa ikiuza na kusambaza jezi hizo nchini na Mashirika ya Umma, Wizara, Halmashauri za Wilaya na mashuleni katika ngazi ya shule za msingi, Sekondari na vyuoni.

Flaviana Matata Foundation kuendelea kushirikiana na PSPF kukuza elimu ya Tanzania

0
0
Muanzilishi wa Flaviana Matata Foundation (FMF),ambaye ni Mwanamitindo wa Kimataifa,Flaviana Matata akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika mkutano uliofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam leo,wakati akizungumzia mradi wake unaotambulika kama “FMF Stationeries Project”; mradi unaojihusisha na uhamasishaji wa mashirika mbalimbali, taasisi za serikali na watu binafsi kuchangia na kusambaza vifaa mbali mbali vya shule kama vile madaftari ya mazoezi, kalamu za wino, kalamu za risasi, rula, mikebe, vifutio na mabegi ya wanafunzi, kwa wanafunzi wanaosoma katika mazingira magumu hapa nchini Tanzania.

Afisa Mawasiliano,Masoko na Uenezi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF,Hawa Kikeke (kushoto) akizungumza na akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na jinsi Mfuko huo ulivyoweza kushirikiana na Flaviana Matata Foundation katika kusaidia kuinua elimu hapa nchini,ambapo kwa ushirikiano huo wamefanikiwa kusambaza vifaa vya shule (stationery kits) vinavyojumuisha mabegi ya shule, madaftari ya mazoezi na vitu vingine,Katika awamu ya kwanza ya mradi (Januari 2014) PSPF wamechangia “FMF Stationery kits” 1000 kwa wanafunzi wasiojiweza mkoani Pwani.
Mratibu wa Flaviana Matata Foundation (FMF),Lusajo Mwaisaka akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na Mpango Mkakati wa Flaviana Matata Foundation kuendelea kusaidia wanafunzi wasiojiweza katika maeneo mbali mbali hapa nchini.Kushoto ni  Muanzilishi wa Flaviana Matata Foundation (FMF),ambaye ni Mwanamitindo wa Kimataifa,Flaviana Matata.
 Muanzilishi wa Flaviana Matata Foundation (FMF),ambaye ni Mwanamitindo wa Kimataifa,Flaviana Matata pamoja na Afisa Mawasiliano,Masoko na Uenezi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF,Hawa Kikeke  wakifurahia jambo wakati wa kupata picha ya pamoja.

JOHNNIE WALKER YAFANIKISHA IRELAND SOCIETY OF TANZANIA GOLF CHAMPIONSHIP :

0
0
 Katka picha ya pamoja Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Bia
ya Serengeti Steve Gannon(kushoto)pamoja na mwandaaji wa mashindano ya 
Ireland Society of Tanzania Golf Championship(kulia)
  Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Steve
Gannon(kulia) akikabidhi Kombe kwa wachezaji wa timu ya Zimbabwe ambao 
waliibuka washindi katika mashindano hayo mwishoni mwa wiki.
Stuart Read akifanya yake ndani ya kiwanja namba moja
katika mashindano ya Ireland Society of Tanzania Golf Championship

  Mchezaji William Creighton mwenye asili ya Uingereza
akipiga mpira wa golf katika mashindano Ireland Society of
Tanzania Golf Championship ambayo yalidhaminiwa na Kampuni ya Bia ya
Serengeti kupitia kinywaji cha Johnnie Walker katika viwanja vya golf
Lugalo jijini Dar es Salaam.

 Mara baada ya kazi nzito ya kucheza golf wachezaji walipata
muda wakupongezana.

ALIYEKUA KATIBU TAWALA MKOA WA RUKWA SASA MKOA WA TANGA NDUGU SALUM MOHAMMED CHIMA AAGA UONGOZI WA MKOA WA RUKWA TAYARI KWENDA KURIPOTI TANGA

0
0
Katibu Tawala mpya wa Mkoa wa Tanga aliyehamishwa kutoka Mkoa wa Rukwa Ndugu Salum Mohammed Chima akizungumza katika hafla fupi ya kuagana na uongozi wa Serikali ya Mkoa wa Rukwa inayoongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Injinia Stella Manyanya (kulia) leo baada ya mabadiliko ya hivi karibuni ya Mhe. Rais Jakaya Kikwete ambapo ameteua Makatibu Tawala wapya watano na kuhamisha wengine akiwepo Ndugu Salum Chima. Katika salamu zake za kuaga ameomba viongozi wote wa Mkoa kushirikiana kwa pamoja kuhakikisha wanasimamia kikamilifu na kukamilisha miradi yote iliyoanzishwa ya Serikali na wahisani mbalimbali.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akitoa salam zake za maagano ambapo alisikitika kwa uhamisho wa kiongozi huyo ambaye kwake alikua kiungo muhimu na msaada mkubwa katika mambo ya kiutendaji. Aidha alisisitiza juu ya kuchapa kazi na ushirikiano baina ya viongozi wa Mkoa na wananchi katika kusukuma gurudumu la maendeleo ya Mkoa wa Rukwa. 
Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Ndugu Methew Sedoyyeka akitoa neno kwa niaba ya Wakuu wa Wilaya wa Mkoa wa Rukwa, alisema kuwa kwa Ndugu Chima kuhamishiwa Mkoa wa Tanga ambao ni Jiji akitokea Mkoa mdogo wa Rukwa ni "promotion" na anastahiki pongezi kwani uwezo wake wa kuchapa kazi ndo umemfikisha hapo alipo. Mkuu huyo wa Wilaya alisema kuwa sifa kubwa ya Ndugu Chima ni uwezo wake mkubwa wa kutoa maamuzi sahihi na ya haraka kwa wakati sifa ambayo ni muhimu kwa viongozi wa sasa katika maendeleo ya taifa letu.
Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali watu Ndugu Samson Mashalla (kulia) akiongea kwa niaba ya watumishi wote wa Sekretarieti ya Mkoa wa Rukwa. Alieleza kushtushwa na uhamisho huo uliokuwa wa ghafla ambapo kwa watumishi umekuwa ni kusikitisha kutokana na ukaribu, upole na upendo aliokuwa nao Ndugu Chima. Ndugu Chima aliwapenda watumishi wote wa ngazi za juu hadi za chini bila ubaguzi wa aina yeyote.
Baadhi ya viongozi na watumishi walihudhuria katika hafla hiyo fupi ya maagano. WATUMISHI WOTE NA VIONGOZI WA SERIKALI YA MKOA WA RUKWA WANAMTAKIA NDUGU CHIMA KILA LA HERI KATIKA KITUO CHAKE KIPYA CHA KAZI AMBACHO NI MKOA WA TANGA. Tunaamini kuwa Tanga imepata kiongozi thabiti mwenye uwezo mkubwa wa kuongoza katika kutoa maamuzi sahihi na ya haraka kwa muda muafaka, "tunaomba apewe ushirikiano atafanya". Kwa upande wake Katibu Tawala Mteule wa Mkoa wa Rukwa kwa sasa ndugu Symthies E.Pangisa aliyekuwa kaimu katibu tawala wa mkoa wa Mtwara anakaribishwa kwa dhati Mkoani Rukwa na ameahidiwa ushirikiano katika kusukuma gurudumu la maendeleo ya Mkoa wa Rukwa.  (Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @Rukwareview.blogspot.com)

ISIKILIZE SINGO MPYA YA KIRARU RARU YA MSANII KILI THE CITY

0
0

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mh.Jenista Mhagama atinga ofisini kwake leo.

0
0
Pichani kati ni Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Mh Jenista Mhagama akiwasili kwenye eneo lake la kazi huku akilakiwa na Wafanyakazi mbalimbali wa Wizara hiyo mara baada ya kuapishwa jana viwanja vya Ikulu jijini Dar
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Mh Jenista Mhagama akikaribishwa Ofisini kwake na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Sifuni Mchome.

NEWS NOW KUTOKA IRINGA:AMBAO HAWAJAFANYIWA TOHARA,WATAKIWA KUACHA KUWA NA AIBU,BADALA YAKE WAJITOKEZE KWENYE VITUO VYA AFYA

0
0
Baadhi ya Wananchi ambao hawajafanyiwa tohara, wametakiwa kuacha aibu na kujitokeza  kwenye vituo vya afya ili kuweza kupata huduma hiyo na kuacha  kukwepa kupata huduma katika vituo vyao ambavyo wamevizoea.


Hayo yamesemwa na meneja wa Mradi wa tohara mkoa wa iringa Dr.Abdalah Maganga, na kusema kuwa watu kuanzia umri wa miaka 25 kwenda juu wamekuwa hawajitokezi kupatiwa huduma hiyo kutokana na kuwa na aibu.


Dr.Abdalah  amesema kuwa asilimia kubwa ya watu wanaojitokeza kupata huduma hiyo ni wale wenye umri wa miaka 18 kushuka chini ,huku sababu kubwa akitaja kuwa ni kuhofia kukaa muda mrefu bila kufanya mapenzi kwa kipindi cha wiki sita wakati akisubiri kidonda kupona.


Hata hivyo ametaja sababu kubwa kuwa wengi wao hawapendi kufanyiwa tohara na wanawake kutokana na kuwa idadi kubwa ya wahudumu ni wanawake.


Amesema kuwa katika kampeni iliyofanyika katika kipindi cha wiki nne iliyolenga wilaya tatu imekuwa na mafanikio ambapo mpango wao ilikuwa ni kuwafikia WATU 15 elfu lakini wamefikia watu 16 elfu na 200 .


Aidha ameongeza kuwa  kuanzia tarehe 10 februali had 8 mach wataanza kampeni katika wilaya za mkoa wa Njombe na lengo ni kuwafikia watu 15 elfu huku akiahidi kurudia maeneo ambayo hawakuyafikia katika wilaya, ambazo tayari wamefanya kampeni ambazo ni kilolo,iringa vijijini,na mufindi kwa wiki mbili.

 =========   ========  ========== 

WAZAZI  WAASWA KUWAPELEKA WATOTO WAO SHULE KUTIMIZA HAKI YA MTOTO

Afisa elimu wa shule za sekondari Manispaa ya iringa DEVOTA LONGO amewaasa  wazazi kuwapeleka watoto wao waliofanikiwa kujiunga na elimu ya shule za sekondari ili kutimiza haki ya mtoto.


Afisa elimu huyo pia amesema  atawachukulia hatua wazazi ambao hawatafanya agizo hilo. amesema kuwa kumewekwa mipango madhubuti ya kukabiliana na wazazi wote ambao hawatawapeleka watoto wao mashuleni ikiwemo kuongea na maafisa watendaji ili kuwapa idadi ya wazazi ambao hawajawapeleka watoto mashuleni pamoja na kuwafikisha polisi.

Hata hivyo amewaomba watendaji wa kata kupitia shule zilizopo katika kata zao ili kuhakikisha wanafunzi waliofanikiwa kujiunga na kidato cha pili wamewasili mashuleni.


Mwenyekiti wa CCM kata ya Jangwani Moody Bawazir apiga jeki vifaa vya michezo timu ya uhuru na mzalendo

0
0

Kiongozi mzuri ni yule anayejitoa kwa watu wake. Mwenyekiti wa CCM kata ya Jangwani,Moody Bawazir  leo amekabidhi vifaa vya Michezo kwa Uongozi wa Timu ya Uhuru na Mzalendo ambayo inajiandaa na mashindano ya NSSF CUP,Vile vile wiki anatarajia kutekeleza Ilani ya chama chake cha CCM.

MH.MWIGULU NCHEMBA ASHIRIKI MAZISHI YA MJUMBE WA NEC WILAYA YA MKURANGA

0
0

Naibu Katibu Mkuu CCM Bara na Naibu Waziri wa Fedha,Hii leo ameungana na Wananchi wa Kigamboni kwenye Mazishi ya aliyekuwa Mjumbe wa NEC wa CCM Taifa Marehemu Rukia Ally Msumi aliyefariki Hospitali ya Taifa Muhimbili Tar.20.01.2014.



Akiwakilisha Chama Cha Mapinduzi Mh.Mwigulu Nchemba ametoa rambirambi kutoka CCM Mkoa wa Pwani,CCM Mkoa wa Dsm na CCM Makao Mkuu,Pia ameelezea kuwa Marehemu enzi za Uhai amekuwa Mwanachama mtiifu wa CCM na ameshika nyadhifa mblimbali za Uongozi ndani ya Chama ukiwao Udiwani miaka 10.


Mungu aipumzishe Roho ya Marehemu Mahali Pema Peponi
AMINA.

SEMINA YA WAFANYA BIASHARA NA KAMPUNI YA CHINA WORLD BUZ YAMALIZIKA LEO TRIPLE “A” JIJINI ARUSHA

0
0

MH. JUMA NKAMIA ALIVYOLAKIWA KATIKA KITUO CHAKE KIPYA CHA KAZI JIJINI DAR LEO

0
0

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Dkt. Fennela Mukangara akimkaribisha Naibu Waziri Mheshimiwa Juma Nkamia katika Ofisi za Wizara zilizopo katika jengo la Mfuko wa Pensheni wa PSPF jijini Dar es Salaam leo.

Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Juma Nkamia akiongea na Wanahabari Ofisini kwake katika tukio la kumkaribisha lililofanyika jijini Dar es Salaam leo kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara Prof Elisante Olegabriel.Picha na Benjamin Sawe.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Olegabriel akimkaribisha Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Juma Nkamia katika tukio la kumkaribisha lililofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania Bwana Clement Mshana (kushoto) akimpongeza Mheshimiwa Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Juma Nkamia wakati wa mapokezi yake katika Ofisi za Wizara zilizopo jijini Dar es Salaam leo katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara Prof. Elisante Olegabriel.
Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Juma Nkamia akisalimiana na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA Bwana Kulwa Magingila wakati wa mapokezi yake yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara Prof Elisante Olegabriel.

RAIS KIKWETE AFUNGUA KONGAMANO LA VIONGOZI WA DINI KUHUSU RASILISIMALI.

0
0
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa  na baadhi ya viongozi wa madhehebu mbalimbali ya Dini waliohudhuria Kongamano la siku mbili linalohusu Rasilimali za Gesi Asilia, Mafuta na Madini kwa Amani na Maendeleo ya Tanzania linalofanyika katika hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam.

DC RUANGWA AGNES HOKORORO (MB) AWATAKA WANANCHI WAKE KUJIUNGA NA CHF HILI KUCHANGIA MABORESHO YA HUDUMA ZA MATIBABU

0
0
 Meneja wa NHIF mkoa wa Lindi Fortunata Raymond  akiwaeleza wanahabari (hawapo pichani) namna ya utekelezaji wa zoezi la uhamasishaji wa wananchi kujiunga na CHF utakavyoendeshwa,sambamba na  mafanikio yanayotarajiwa kutokana na mkakati wa pamoja wa Mfuko na Mkuu wa wilaya ya Ruangwa ulivyokusudiwa.
 Nawaambieni CHF ndiyo mkombozi wa huduma za matibabu sasa…Mkuu wa wilaya ya Ruangwa Agnes Hokororo (MB) akitoa rai kwa wananchi wake Wilayani humo wakati wa uzinduzi wa kampeni za uhamasishaji wananchi kujiunga na CHF ulioenda sambamba na upimaji wa afya bure chini ya uratibu wa NHIF Lindi uliofanyika  leo hii kwenye viwanja vya CWT Ruangwa.
 Upimaji wa afya bure ukiendelea,madaktari wa mfuko na hospitali ya wilaya wameendelea kutoa huduma za uwiano wa uzito wa mwili (BMI),shinikizo la damu (BP) na sukari ambapo suala la lishe na shinikizo la damu (BP)ni changamoto  iliyoweza kubainika hivyo ushauri ulitolewa,kushoto ni Dr. Rashida Omari  wa hospitali ya wilaya akimpima kiwango cha sukari mzee Abdalah Ngawenje.



Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Agnes Hokoro (MB) akipima BMI kwenye viwanja vya CWT,anayempima ni afisa wa mfuko ofisi ya mkoa wa Lindi Laurent Hoja.
 Wananchi wakimsikiliza mkuu wa wilaya Agness Hokoro hayupo pichani wakati wa uzinduzi huo .

MAMIA WASHIRIKI MAZISHI YA MAMA WA MZEE MAKAMBA

0
0
 Mzee Yusufu Makamba akishauriana jambo na mwanae January Makamba wkati wa shughuli za mazishi zikiendelea. Mzee Yusufu Makamba amefiwa na mama yake mzazi aliyefahamika kama Mariam Masau Kivugo  kilichotokea tarehe 21 January 2014.
 Mzee Yusufu Makamba akiwa na mwanae January Makamba wakitafakari jambo baada ya kupata msiba mkubwa  wa kufiwa na Mama mzazi wa Mzee Yusufu Makamba, Mariam Kivugo.
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa Ndugu Abdallah Majura Bulembo akitoa salaam za pole kwa wafiwa wakati wa mazishi ya Bibi Mariam Masau Kivugo.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akitoa salaam za pole kwa niaba ya Chama  kwa Mzee Yusufu Makamba na Familia yake wakati wa mazishi ya Mama wa Mzee Yusufu Makamba.
 Mamia ya watu wakimsikiliza Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia Ndugu January Makamba wakati akitoa salaama za shukrani kwa niaba ya familia kwa wananchi wote waliojitokeza kwenye mazishi ya Bibi yake Marehemu Mariam Masau Kivugo yaliofnyika Mehazangulu,Tanga.
 Mwili wa Marehemu Mariam Kivugo ukipelekwa msikitini kwa ajili ya kuombewa kabla ya kuelekea makaburini.
 Watu wakiwa kwenye nyuso za huzuni wakati wa mazishi ya Bibi Mariam Kivugo ambaye pia ni mama wa Mzee Yusufu Makamba.
 :
Katibu wa NEC itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishiriki kuweka udongo kwenye kaburi la mama wa Mzee Yusuf Makamba aliyefariki tarehe 20 Januari 2014.

MAKAMU WA RAIS AWASILI ZANZIBAR KUZINDUA KAMPENI KIEMBESAMAKI LEO

0
0
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mgombea Uwakilishi Jimbo la KiembeSamaki CCM Mahmoud Thabit Kombo, alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar leo tarehe 22-2014 kwa ajili ya ufunguzi wa kampeni za uchaguzi mdogo utakaofanyika leo.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Unguja, Borafya Silima alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar leo tarehe 22-2014 kwa ajili ya ufunguzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Uwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki Zanzibar utakaofanyika leo.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Katibu wa CCM Mkoa wa Mjini Unguja, Alhajj Rajab Kundiya alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar leo tarehe 22-2014 kwa ajili ya ufunguzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Uwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki Zanzibar utakaofanyika leo. (Picha na OMR)
Viewing all 46201 articles
Browse latest View live




Latest Images