Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46327 articles
Browse latest View live

MAMIA YA WAMZIKA DEUSDEDIT MTAMBALIKE

$
0
0
Jaji Mstaafu Mark Bomani,Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye  na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) Mh.Stephen Wassira ni miongoni mwa viongozi mbali mbali walioshiriki mazishi ya kada maarufu ambaye pia alishawahi kuwa Mkuu wa Wilaya katika Wilaya mbalimbali nchini.
Mama Anna Mkapa,Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka na Mwenyekiti wa CCM Moshi Mjini Elizabeth Minde wakiwa miongoni mwa mamia ya Watanzania waliojitokeza kumzika kada wa siku nyingi Deusdedit Mtambalike.
Waombolezaji wakiwa kwenye nyuso za huzuni wakati wa mazishi ya mpendwa wao Deusdedit Mtambalike.
Sala ya kumuombea Marehemu Deusdedit Mtambalike aliyefariki tarehe 15 Januari 2014 nchini Afrika ya Kusini ilisomwa nyumbani kwake kabla ya Mazishi.
Wanandugu wa Marehemu Deusdedit Mtambalike wakiwa wamebeba mashada ya maua .
Mwanasiasa wa siku nyingi na ambaye alishawahi kushika nyazfa mbalimbali za serikali Balozi Paul Rupia akitoa salaam za pole kwa familia ya marehemu Deusdedit Mtambalike na kumuelezea marehemu kama mtu aliyemwema na asiyechoka kushauri kwenye jambo lolote alotakiwa kushauri.
Jaji Mstaafu Mark Bomani akimuelezea marehemu Deusdedit kama mtu ambaye hakusita wala kuwa na woga katika kuzungumzia jambo lenye manufaa kwa jamii.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akitoa salaam za rambirambi kwa niaba ya CCM Makao Makuu wakati wa mazishi wa aliyekuwa Kada wa Chama Cha Mapinduzi Marehemu Deusdedit Mtambalike.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais(Mahusiano na Uratibu) Mheshimiwa Stephen Wassira akitoa salaam za pole kwa niaba ya Serikali kwenye mazishi ya Ndugu Deusdedit Mtambalike yaliofanyika nyumbani kwa marehemu Kimara Bonyokwa.
Watoto wa Marehemu Deusdedit Mtambalike wakiwa wenye nyuso za simanzi na huzuni pamoja na Mama yao na Ndugu wa karibu wakati wa sala ya mwisho kabla ya mazishi ya Baba yao mpendwa.
Sehemu ya watu waliojitokeza kwenye mazishi ya Deusdedit  Mtambalike
Profesa Mahalu akiweka mchanga kama ishara ya kumzika rafiki yake Marehemu Deusdedit Mtambalike
Mke wa Marehemu Deusdedit Mtambalike akiweka shada la maua juu ya kaburi .
Watoto wa marehemu wakiweka shada la Maua kwenye kaburi la baba ya mpendwa Marehemu Deusdedit Mtambalike aliyefariki dunia tarehe 15 Januari 2014 nchini Afrika ya Kusini.

Mahojiano na Faria Zam kuhusu msaada wa watoto walemavu Zanzibar

$
0
0
Pichani: Faria Zam muazilishi wa Hilmy Disability Charity Organisation nchini Uingereza akihojiwa na Abou Shatry wa Jamii Production Washington DC.

Karibu katika ya mahojiano na Jamii Production na Faria Zam a.k.a Ferry Butcher ambae ni muazilishi wa kusaidia watoto walemavu Zanzibar kupitia (Hilmy Disability Charity Organisation) kutoka nchini Uingereza pale alipopata fursa ya kuhojiana na Abou Shatry kuhusu maswali mbalimbali ya kusaidia watoto wa walimavu Zanzibar siku ya Ijumaa Jan 17, 2014 Washington DC. Mahojiano haya yameandaliwa na mwanaharakati Anu Khelef kutoka Leicester nchini Uingereza
Ungana nasi kwa kusikiliza

SHIRIKA LA POSTA TANZANIA LASHIRIKI MAADHIMISHO YA MIAKA 34 YA SIKU YA POSTA BARANI AFRIKA.

$
0
0
Pichani kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Masuala ya Kimataifa wa Shirika la Posta Tanzania,Bwa. Elia Madules akizungumza mbele ya Wanahabari (hawapo pichani),mwishoni mwa wiki ndani ya Ofisi ya Makao Makuu wa ya shirika hilo jijini Dar,kuhusiana na maadhimisho ya  miaka 34 ya siku ya Posta Barani Afrika,Siku ambayo Posta zote katika Afrika hufanya maadhmisho yanayohusu shughuli za Kiposta,Pichani kati ni Kaimu Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara,Bi.Fadya Zam pamoja na Kaimu Meneja Mipango Bwa.Nehemiah Kyabalasi
Pichani kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Masuala ya Kimataifa wa Shirika la Posta Tanzania,Bwa. Elia Madules akifafanua jambo kwa ufasaha mbele ya Wanahabari (hawapo pichani),mwishoni mwa wiki ndani ya Ofisi ya Makao Makuu wa ya shirika hilo jijini Dar,kuhusiana na maadhimisho ya  miaka 34 ya siku ya Posta Barani Afrika,Siku ambayo Posta zote katika Afrika hufanya maadhmisho yanayohusu shughuli za Kiposta.Bwa.Elia alisema kuwa dhamira ya Shirika hilo ni kuhakikisha kuwa Watanzania wanafaidika  na matunda ya huduma bora na za kisasa za mawasiliano ya Posta ambayo ni pamoja na kuwarahisishia  upatikanaji wa huduma za kibiashara  na kupanua wigo wa huduma jumuishi za kifedha 
Pichani kati ni Kaimu Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara,Bi.Fadya Zam akifafanua zaidi kuhusiana na  maadhimisho hayo ya  miaka 34 ya siku ya Posta Barani Afrika Mbele ya Wanahabari (hawapo pichani),Siku ambayo Posta zote katika Afrika hufanya maadhmisho yanayohusu shughuli za Kiposta,Bi Fadya aliongeza  kuwa siku hiyo ni Kumbukumbu ya kuanzishwa kwa umoja wa Posta Barani Afrika (PAPU) mnamo tarehe 18 Januari 1980,akabainisha kuwa hivyo Umoja huo ambao ni Shirika tanzu la Umoja wa Afrika (AU) umetimiza miaka 34.Bi Fadya alisema kuwa hivi sasa PAPU ina nchi  Wanachama 43 na Tanzania ndio mwenyeji wa makao yake Makuu yaliyoko jijiini Arusha.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Shirika hilo la Posta Tanzania,wakifuatilia mkutano huo uliohusu  maadhimisho hayo ya  miaka 34 ya siku ya Posta Barani Afrika.
Pichani Kulia aliyesimama ni Mkuu wa Uhusiano Shirika la Posta Tanzania,Bwa.Wilfred Mlugo akitoa muongozo kwenye mkutano huo.
Pichani kulia ni Kaimu Meneja Mipango,Bwa.Nehemiah Kyabalasi akielezea mipango mbalimbali ya Shirika hilo kwa Wanahabari (hawapo pichani).Bwa.Nehemiah alieleza kuwa maadhimisho hayo yanafanyika wakati shirika la posta limetimiza miaka 20 tangu kuanzishwa kwake mnamo tarehe 1 januari,1994,ambapo tangu wakati huo yamekuwepo mafanikio ya kuridhisha lakini pia changamoto za hapa na pale hazikosi.

Video ya Sky's the limit- Wise Ft Absoulute iliyoangozwa na Mtanzania kutoka Kansas City U.S

$
0
0
Agalia Video ya nyimbo ya ''Sky's the limit- Wise Ft Absoulute'' video ambao amei-Direct mTanzania Eddy Mohamed Eddy kutoka Kansas City

Kampuni ya China Word Buz yaelezea njia mbadala zitakazopunguza gharama za wafanyabiashara wadogo kufuata bidhaa nchini China

$
0
0
1a
Ofisa mtendaji mkuu wa kampuni ya China Word Buz na mwakilishi wa wamiliki wa viwanda 45 nchini China vilivyoingia mkataba wa kibiashara na kampuni hiyo China Bwana Cheng Wang Wu akizungumza na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Palace jijini Arusha wakati wa semina na waandishi hao kuhusu mfumo wa kampuni hiyo utakaosaidia wafanyabiashara wadogo wa Tanzania kutafuta soko la bidhaa nchini China na kuwapa taarifa sahihi za masoko kwa msaada wa kampuni hiyo,Mfumo huo hautampa gharama kubwa mfanyabiashara kama vile Usafiri , Chakula, Hoteli.kwani hatalazimika kusafiri kwenda China ili kununua bidhaa badala yake kampuni hiyo itamuagizia na kumfikisha mahali alipo ama kumshauri ni njia gani anaweza kutumia kupata bidhaa kutoka China, kulia ni Shafii Mwaijande Ofisa Mtendaji Mkuu wa China Word Buz kwa upande wa Tanzania.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-ARUSHA)2
Meneja Mkuu wa kampuni hiyo nchini China Justin Luvanda akifafanua jambo wakati wa semina hiyo kwenye hoteli ya Palace jijini Arusha, kulia ni Ofisa mtendaji mkuu wa kampuni ya China Word Buz na mwakilishi wa wamiliki wa viwanda 45 nchini China vilivyoingia mkataba wa kibiashara na kampuni hiyo China Bwana Cheng Wang Wu na kushoto ni mmoja wa maofisa wa kampuni hiyo China.3Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo hapa nchini Bw. Shafii Mwaijande akionyesha kipeperushi kinachoelezea moja ya makampuni makubwa ya bishara ambayo yamesaini mikataba ya kibiashara na kampuni ya China World Buz, katikati ni Ofisa mtendaji mkuu wa kampuni ya China Word Buz na mwakilishi wa wamiliki wa viwanda 45 nchini China vilivyoingia mkataba wa kibiashara na kampuni hiyo China Bwana Cheng Wang Wu na wa pili kutoka kushoto ni Meneja Mkuu wa kampuni hiyo nchini China Justin Luvanda .



6 
1

TV Talk Show Ya "Changamoto za Mahusiano Na Ufumbuzi Wake" 22nd January 2014

$
0
0

Tunapenda kutoa mwaliko kwa wageni 30 tu watakaohudhuria katika kipindi kipya kitakachorushwa TBC1 siku ya Jumapili tarehe 26th January 2014 saa 3 hadi saa 4 usiku na kurudiwa siku ya Jumatano Tarehe 29th January 2014 saa 8 hadi saa 9 mchana. Wageni lazima wawe na uzoefu sana na mambo ya Mahusiano na wawe tayari kuleta changamoto katika kipindi au kusaidia kupata ufumbuzi wa tatizo. 

Kipindi kitarekodiwa siku ya Jumatano saa 12 jioni hadi saa 2 usiku. Tafadhali thibitisha kuhudhuria kwako kupitia namba:+255 755 285 023

Mada itakayoongelewa na “Changamoto Katika Mahusiano na Ufumbuzi Wake". Wataalikwa Wataalamu mbalimbali na wazoefu wa mambo ya mahusiano kama wageni wawezeshaji.

Wale wote wenye michango ya msingi au maoni au ufumbuzi au maswali mnayopenda wahusika waulizwe pia mnaweza kuniandikia mapema.

TV Talk Show itajulikana kama "Wake Up & Change" au "Amka na Badilika" na ni kipindi kitakachorushwa kila wiki siku ya jumapili usiku na kurudiwa Jumatano.

1. Madhumuni ya Kipindi

a) Kubadilisha mitazamo ya watazamaji ili iwe mitazamo chanya zaidi kwa mambo mbalimbali pamoja na kuwahamasisha kubadili tabia na kuchukua hatua katika kukabiliana na matatizo.
b) Kutafuta na kutoa majibu kwa masuala muhimu yanayohitaji kupatiwa ufumbuzi au utatuzi wa matatizo na pia kujibu maswali yanayohusiana na mada husika kutoka kwa watazamaji waalikwa.
c) Kukifanya kipindi kama jukwaa la majadiliano katika mambo muhimu ya kijamii na kitaifa na kuhamasisha mabadiliko chanya.

2. Ubunifu wa Kipindi

Kipindi kimebuniwa ili kuleta majadiliano yatakayoleta hisia kwa wote watakaohusika katika mjadala na pia watazamaji. Jambo hili ni muhimu zaidi ili kuleta matokeo chanya kwa wote wanaoangalia kipindi. Kwa ujumla kipindi kimebuniwa kutatua matatizo mbalimbali ya watu binafsi, familia, jumuiya, jamii na taifa kwa ujumla huku kikitoa mikakati na mipango ya kutatua matatizo na kuwahamasisha watazamaji kubadilika. Studio itakoyorekodi vipindi hivyo pia imetengenezwa katika hali ya ubunifu na kupendezesha kipindi.


3. Mada Zitakazoongelewa

Kutakuwa na mada mbalimbali na mpya ambazo zitaongelewa kila wiki. Mada hizi zitategemea utafiti utakaofanywa na mamombi ya watazamaji ili mradi tu liwe ni tatizo ambalo linaigusa jamii au watu wengi. Mfano wa mada hizi ni pamoja na biashara; mahusiano; kazi na ajira; kilimo; Wanawake, rushwa; madawa ya kulevya nk.

4. Mpangilio wa Kipindi:

a) Kuwakilisha mada husika na kuitambulisha huku takwimu zikitolewa toka chanzo cha kuaminika.
b) Kulielezea tatizo husika katika uhalisia wake na kuwafanya watazamaji waone ukubwa wa tatizo.
c) Kulijadili tatizo na kulichambua kwa kina huku maswali yakijibiwa
d) Kuwakilisha majibu na ufumbuzi wa tatizo
e) Kuhamasisha watazamaji wazinduke/waamke, kubadilika na kuchukua hatua ya kutatua tatizo kama lilivyo ainishwa.
f) Kipindi kitaendeshwa kwa mtindo wa majadiliano yenye hisia kali na hivyo kupeleka hisia kwa watazamaji pia.

5. Walengwa wa Kipindi:

a) Vijana 
b) Wanafunzi
c) Wafanyabiashra
d) Wanandoa
e) Na wananchi wote kwa ujumla.


6. Urushaji wa Kipindi na Upatikanaji katika DVD 

a) Kipindi kitakuwa kinarekodiwa na kurushwa katika Luninga siku ya Jumapili saa 3 hadi saa nne usiku kwa muda wa saa moja. TBC1 na kurudiwa Jumatano Mchana
b) Baadhi ya vipindi vitavyoonekano kama ni mafunzo muhimu na adimu kwa watu na jamii vitarekodiwa katika DVD na kusambazwa na kuuzwa kwa bei nafuu kwa walengwa. 


Karibuni sana.

Castle Lite kuwapeleka Watanzania nchini Afrika Kusini kushuhudia onesho la Timbaland

$
0
0
Meneja wa Bia ya Castle Lite,Victoria Kimaro akisisitiza jambo juu ya namna wateja wa bia hiyo watakavyoweza kushiri kwenye Promosheni hiyo,ambapo amesema mteja atatakiwa kununua bia hiyo ya chupa na atakapoifungua ataona namba zilizowekwa ndani ya kizibo na atatakiwa kutuma jina lake na namba hiyo kupitia ujumbe mfupi wa simu kwenda kwenye namba 15499.
Meneja wa Bia ya Castle Lite,Victoria Kimaro akionyesha namba itakayokuwa inatumika kwenye Promosheni hiyo.
Meneja Habari na Mawasiliano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Edith Mushi (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na Promosheni yao mpya kupitia Bia ya Castle Lite  ya kupata washindi 12 watakaokwenda nchini Afrika Kusini kushuhudia onyesho kubwa la msanii maarufu duniani,Timothy Zachery Mosley kwa jina Maarufu anafahamika kama TIMBERLAND,Promosheni hiyo itaendeshwa kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia leo Januari 20 mpaka Machi 30.Kulia ni Meneja wa Bia ya Castle Lite,Victoria Kimaro.

MTEMVU AWANDALIA MSOSI MARAFIKI ZAKE KUTOKA CHUO KIKUU CHA BUFFALO MAREKANI

$
0
0
 Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu (kushoto) na Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Buffalo cha Marekani, Tyler Choi wakati wa hafla ya chakula cha usiki alichowaandalia marafiki zake hao  jana kwenye Hoteli ya Sea Cliff, Masaki Dar es Salaam. 
Mtemvu (wa tatu kulia) akiwa na baadhi ya wageni kutoka Chuo Kikuu cha Buffalo Marekani wakipata mlo wa usiku. Ujumbe huo umepangiwa kuonana na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa na kutembelea baadhi ya shule na Hospitlai katika Jimbo la Temeke.
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Temeke, Ally kushoto) na wenzie wakipata mlo huo.


Mtemvu akidadiliana jambo na Mkurugenzi wa Kampuni ya African Maraika, Fiona Barrelto (katikati)  na mkewe Mariam wakati wa hafla hiyo.
Mfanyakazi wa Hoteli ya Sea Cliff (katikati) akichangamsha hafla hiyo.
Wafanyakazi wa Hoteli ya Sea Cliff wakiiimba wimbo huku wakipiga makofi ikiwa ni moja ya sham rashamra ya hafla hiyo.
Wageni ambao ni wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Buffalo Marekani wakiwa wamesiamama walipokuwa wakitambulishwa kwenye hafla hiyo.
Mtemvu akielezea umuhimu wa ziara ya marafiki zake hao nchini.
Mwanafunzi Tyler Choi wa Chuo Kikuu ccha Bufalo akitoa shukurani kwa kuandaliwa hafla hiyo pamoja na kuahidi kudumisha urafiki uliopo na Mtemvu na Jimbo la Temeke kwa ujumla.
Barrelto ambaye ni mfadhili mkubwa katika sekta ya elimu Jimbo la Temeke, akielezea umuhimu wa kudumisha urafiki uliopo kati ya chuo hicho na Mtemvu (kushoto). Kulia ni Mke wa Mtemvu, Mariam ambaye pia ni Diwani wa Viti Maalum Temeke.


GAZETI LA CHAMPIONI LAPONGEZWA

$
0
0
Mhariri Kiongozi wa Championi, Saleh Ally (kulia) akimpa zawadi ya shilingi elfu hamsini (50,000) Bi. Rose Majembe baada ya kumkuta kwenye biashara yake ya kukaanga mihogo, Mwenge jijini Dar es Salaam. Katikati ni wahariri wa Championi, John Joseph na Philip Nkini mwingine ni dada aliyekutwa akinunua mihogo.
Mhariri Kiongozi wa Championi, akizungumza na msomaji wa gazeti hilo aliyemkuta maeneo ya Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam.
Mhariri Kiongozi wa Championi, Saleh Ally na wahariri wake John Joseph na Philip Nkini wakimpa zawadi ya chupa ya chai mwanamama huyu waliyemkuta maeneo ya Magomeni Mikumi jijini Dar es Salaam akisoma gazeti la Championi.
Bodi ya Uhariri ya Championi ikimpongeza askari wa JWTZ baada ya kumkuta akisoma gazeti la Championi.
BODI ya Uhariri ya Gazeti la Championi, leo ilitembelea maeneo mbalimbali ya jijini Dar es Salaam na kuzungumza na wasomaji wake ambao walitoa maoni mbalimbali ambapo walilipongeza gazeti hilo kutokana na habari zake makini.
(PICHA : RICHARD BUKOS / GPL)

AJALI MBAYA YA GARI AINA YA NOAH NA LORI MKOANI SINGIDA,WATU 13 WAFARIKI PAPO HAPO LEO

$
0
0
Gari ya abiria aina ya Noah imepata ajali mbaya baada ya kugongana uso kwa uso na Lori,hali iliyopelekea gari hilo la abiria (Noah kuburuzwa na kutupwa kando kando ya barabara kama lionekanavyo pichani mapema leo asubuhi,ajali hiyo imetokea kijiji cha Issuna,kijiji cha kwanza kutokea Manyoni mkoani Singida likielekea Mkoani Dodoma.

Ajali hiyo ya kusikitisha ilitokea huku mvua kubwa ikinyesha eneo hilo,hali iliyopelekea kupata msaada haraka kuwa ya taabu,Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani Singida alibainisha kuwa marehemu wote na majeruhi walikimbizwa hospitali Mkoani Singida.


Aidha mpaka sasa imekuwa vigumu kujua idadi kamili ya abiria waliokuwa kwenye gari hiyo aina ya Noah,hali inayopelekea pia utata wa kutambua majina ya marehemu.Katika ajali hiyo Dereva wa Lori na Kondakta wake walikimbia eneo la tukio,Polisi bado inawatafuta kufahamu kwa kina cha chanzo cha ajali hiyo kutokea.


Jamii yatakiwa kujitolea kuwasaidia yatima

$
0
0
 Meneja wa Kampuni ya Vodacom mkoani Mbeya Emmanuel Sagenge (Kushoto) akikabidhi msaada kwa Mwenyekiti wa mtandao wa watoto mkoa wa Mbeya  Zahara Mansoor, wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika katika kituo cha kulea watoto yatima cha Nuru Orphans Centre kilichopo Uyole Jijini Mbeya. Msaada huo utagawanywa katika vituo vitatu ambavyo niNuru, Iwambi na Chipro vyote vipo jijini Mbeya.
Wafanyakazi wa Vodacom mkoani Mbeya mjini wakishusha vitu kwenye gari ikiwa ni moja ya msaada iliyotolewa na kampuni hiyo kwenye vituo vya kulea watoto yatima mkoani Mbeya vikiwemo Nuru Orphans Centre, Iwambi Orphans Centre na Chipro Orphans Centre vyote vipo jijini Mbeya. Msaada huo umegharimu zaidi ya shilingi milioni tatu.

========  ======  ========
Jamii yatakiwa kujitolea kuwasaidia yatima

Wito umetolewa kwa jamii ya Watanzania kujitolea kuwalea watoto yatima ili kupunguza wimbi la watoto wa mitaani na wale wanaoishi katika mazingira magumu ili kuweka jamii yenye usawa na kujenga nguvu kazi  imara ya taifa siku za usoni.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Mtandao wa  Yatima Mkoani Mbeya ambaye pia ni Meneja Mradi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Nuru Orphanage Centre kilichopo uyole Mkoani Mbeya Bi. Zahara Mansoor wakati akipokea msaada wa unga wa sembe, sabuni, mafuta ya kupikia, mchele, maharage, maziwa na chumvi pamoja na pamoja vifaa vya shule kama vile; penseli, kalamu, madaftari, miswaki,kutoka kwa wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wa Mkoani humo.

Mkurugenzi huyo amesema tatizo la watoto yatima limekuwa changamoto kubwa katika jamii hususani katika nchi zinazoendelea huku bado watoto hao wakikosa sehemu ya kuishi au mahali pazuri pa kulelewa kufuatia watu wengi wanaojitolea kuwalea watoto hao kukosa uwezo wa kukidhi mahitaji yao ya kila siku.

“Ninapenda jamii itambue kuwa jukumu la kulea watoto yatima sio la watu fulani wachache tu ni jukumu letu sote kuhakikisha tunaunganisha nguvu kazi na kuwa na nyoyo za upendo katika kuwalea watoto hawa, ili tujenge jamii yenye usawa na nguvu mali ya taifa letu siku za usoni, wengi tunasema Watoto ni taifa la kesho yatima pia wanahitaji kupata nafasi katika taifa hilo la kesho hivyo ni lazima tujitolee kuwasaidia”, alisema Bi. Mansoor

Bi. Zahara aliongezea kuwa ni vema kwa makampuni na taasisi mbali mbali kujenga utamaduni wa kujitolea kwa ajili ya watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu na sio kuwaachia jukumu hilo wenye vituo pekee.

“Ninawashukuru wafanyakazi wa Vodacom Tanzania kwa msaada wao, msaada huu utatusaidia katika vituo vyetu vitatu vya Chipro, Iwambi na Nuru,Pia napenda kutoa wito kwa Watanzania kujitolea katika kuwasaidia watoto hawa.

Kwa upande wake Meneja wa Vodacom Mbeya mjini, Emmanuel Sagenge alisema kampeni ya Pamoja na Vodacom ni matokeo ya kuguswa kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo na matatizo mbali mbali yanayoikumba jamii inayowazunguka na kuamua kutoa sehemu ya kipato chao katika kuwasaidia yatima.

 “Ni jambo la ujasiri kwa waanzilishi wa vituo vya kulea watoto yatima nchini kwani si kila mtu anaweza kufanya hilo, sisi kama wafanyakazi tunao wajibu wa kuwezesha vituo hivi kwa kile tunachokipata kutokana na kufanya kazi kwetu ili kuwatia nguvu na hata kuwahamasisha wengine wafanye hivyo.” Alisema Bw. Sagenge.

 Meneja huyo alimalizia kuwa wafanyakazi wa kampuni hiyo hawataishia hapo kwani zoezi hilo ni endelevu itahakikisha popote pale huduma zao zilipo basi na wao watawafikia wote wanaohitaji msaada. Na kisha kutoa wito kwa taasisi na watu binafsi pamoja na wafanyakazi wa sekta ya simu kuiga mfano wao na kuwa na utamaduni wa kujitolea kusaidia ama kulimaliza kabisa swala zima la kuwasaidia watoto waishio katika mazingira magumu kwani bado safari ya kuwa na jamii bora ni ndefu.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA BALOZI MTEULE WA TANZANIA NCHINI MALAYSIA.

$
0
0
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na kumkaribisha Balozi mteule wa Tanzania nchini Malaysia, Dkt. Aziz Ponary Mlima, wakati alipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo kwa ajili mazungumzo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika mazungumzo na Balozi mteule wa Tanzania nchini Malaysia, Dkt. Aziz Ponary Mlima, wakati alipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo kwa ajili mazungumzo. Picha na OMR


WAZIRI MKUU AAGIZA HALMASHAURI ZITUMIE VIJANA

$
0
0
 WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amezitaka Halmashauri zote 160 za Miji na Wilaya zilizoko nchini kuhakikisha zinaunda vikundi vya vijana vya ujenzi wa nyumba nafuu (building brigades) ili viwe sehemu ya miradi ya kila Halmashauri.

Ametoa agizo leo (Jumatatu, Januari 20, 2014) wakati akizungumza na wahitimu wa mafunzo ya wataalam wa mashine za kutengeneza matofali kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za gharama nafuu kwenye hafla fupi iliyofanyika Mwenge jijini Dar es Salaam.

Mafunzo hayo yaliyoanza Januari 6 - 17, mwaka huu yaliendeshwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) pamoja na Mamlaka ya Elimu ya Ufundi Stadi (VETA) kwa kushirikiana na Wakala wa Utafiti wa Vifaa Bora vya Ujenzi (NHBRA) iliyo chini ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.  

Mafunzo hayo ambayo yanahusu namna ya kutumia mashine za Hydraform ni pamoja na kutambua udongo unaofaa kutengenezea matofali na namna ya kujenga kwa kutumia matofali hayo.

Waziri Mkuu alisema alimshawishi Mkurugenzi Mtendaji wa NHC, Bw. Kyando Mchechu atafute mbinu za kutumia teknolojia rafiki wa mazingira ili kuepuka janga la uharibifu wa mazingira unaosababishwa na matumizi makubwa ya kuni mbichi ili kuchoma matofali.

“Licha ya kuwa utengenezaji wa matofali ya kuchoma unatekeleza azma ya Serikali ya kutaka wananchi wake wawe na nyumba bora, kwa kweli roho huwa inaniuma hasa ukizingatia kiasi kikubwa cha miti inayokatwa kuyachoma hayo matofali hadi yawe imara, tena ikiwa mibichi,” alisema.

Aliipongeza Wakala wa Utafiti wa Vifaa Bora vya Ujenzi (NHBRA) kwa kubuni mashine hizo ambazo alisema zinauzwa kwa bei ambayo Halmashauri inaweza kuzimudu. “Mkurugenzi Mkuu ameniambia kila mashine inauza kwa sh. 450,000/- na inaweza kutengeneza matofali 700 kwa siku moja… hayo matofali yanatumia mifuko saba tu ya saruji. Hili ni jambo linalowezekana!” alisisitiza.

“Wakurugenzi wapangeni vijana wenu katika building brigades  ili wanufaike na mapando huu. Na Wakurugenzi wa Dodoma itabidi tuwapigie kelele ili wawasimamie wananchi waweze kupata nyumba kupitia mpango huu,” aliongeza.

Alisema anataka wachangamkie haraka hizo mashine kwa sababu  zinasaidia uhifadhi wa mazingira, zinachochea ufanisi wa teknolojia, zinapunguza gharama za ujenzi na zinasaidia kutoa ajira kwa vijana.

“Kila Halmashauri itapewa mashine nne, na kila mashine inahudumiwa na vijana 10 kwa hiyo itachangia ajira ya moja kwa moja kwa vija 6,400. Hata hivyo aliwasihi watakaoendesha miradi hiyo wasitoze bei kubwa kwa matofali watakayotengeneza ili wananchi wengi waweze kumudu bei na wabadili hadhi za makazi yao,” alisema.

Alimtaka Bw. Mchechu aweke mpango wa kuendeleza kampeni hiyo kwa miaka mitano mfululizo ili uweze matokeo chanya kwa jamii badala kuanzisha mwaka na kuachia katikati.

Mapema, Mkurugenzi Mtendaji wa NHC, Bw. Kyando Mchechu alisema chini ya mpango wa kusaidia miradi ya maendeleo inayofanywa na jamii (CSR), Shirika lake limekuwa linachangia sekta za afya na elimu na hivi sasa wamelenga vijana hasa kutoa ajira katika sekta ya ujenzi.

“Shirika limegawa mashine 640 za kufyatulia matofali na kila Halmashauri itapatiwa mashine nne, …kwa kuanzia NHBRA wameahidi kutoa mashine 320 kwa mkupuo mara zitakapokamilika,” alisema.

Aliwasihi wakuu wa wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri watoe ushirikiano kwa shirika hilo ili mpango huo wa kutoa jaira kwa Vijana uweze kufanikiwa.

Mafunzo hayo yalihusisha wataalamu 50 waili kutoka kila mkoa ambapo kati yao 34 walikuwa ni walimu wa VETA na 16 ni wahitimu wa VETA.

NHC na Tumeelezwa na VETA zimekubaliana ya kuwatumia vijana waliohitimu VETA kutengeneza matofali katika Kanda Tano zenye miradi ya ujenzi wa nyumba za gharama nafuu wakitumia mashine za kisasa za Hydraform.
)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 3021,
DAR ES SALAAM.
JUMATATU, JANUARI 20, 2014.

Komando Hamza Kalala uso kwa Uso na Kamanda Ras Makunja

$
0
0
Juzi Kati ndani ya studio za Sibuka FM,Katika kipindi cha Pepeta Afrika,
mgeni rasmi nyota wa wiki alikuwa kamanda Ras Makunja kiongozi wa bendi maarufu barani ulaya Ngoma Africa band aka FFU Ughaibuni,aka
Anunnaki Alien au "Watoto wa Mbwa". Kamanda Ras Makunja alifanya
maohijiano ya TV na Redio Sibuka, na alizungumuzia zaidi nafasi ya
muziki wa dansi wa Tanzania katika masoko ya kimataifa,

Mwanamuziki huyo wa Tanzania mwenye makao yake nchini Ujerumani
alitoa wito kwa watanzania waishio ndani na nje ya Tanzania 
kuzipa nafasi bendi za muziki za Tanzania ili ziweze kuvusha muziki wake
nje ya mipaka ya Tanzania ,pia kufanya tour za kimataifa.

Ras Makunja aliutaja muziki wa dansi wa Tanzania "Bongo Dansi" kuwa una nafasi kubwa katika soko la kimataifa hiwapo Watanzania wenyewe watakuwa mstari wa mbele katika kuutanga na kuzipendekeza bendi za Tanzania kwa maporomota na waandaaji wa maonyesho ya kimataifa.
Katika studio za Sibuka FM,jijini Dar-es-salaam Ras Makunja aliongozwa na mwanamuziki mkongwe nchini Komandoo Hamza Kalala ambaye aliutaja muziki wa Ngoma Africa band aka FFU ughaibuni kuwa ni muziki ulipangiliwa kwa mtindo wa kushambulia na kuteka washabiki katika masoko.

Komando Hamza Kalala alimtaja Kamanda Ras Makunja kuwa ni mojawapo wa wanamuziki wachache wa kitanzania wanao ipeperusha
bendera ya Bongo kimataifa bila ya uwoga.
Usikose kuwasikiliza FFU wa Ngoma Africa band at www.ngoma-africa.com

Mzee Arnold Wifred Nkhoma apumzishwa kwenye nyumba yake ya milele makaburi ya Kinondoni jijini Dar

$
0
0
DSC_0198
Gari lilibeba mwili wa Marehemu Mzee Arnold Wifred Nkhoma likiwasili nyumbani kwa binti yake Changanyikeni, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
DSC_0201DSC_0231
Wajukuu wa marehemu wakiwa wamebeba Jeneza la Babu yao kuliingiza ndani tayari kwa heshima za mwisho kabla ya kuelekea Kanisani kwa Ibada.
DSC_0001

Baadhi ya waombolezaji waliofika kwenye msiba wa Mzee Arnold Nkhoma wakisaini kitabu cha maombelezo nyumbani kwa mmoja wa mabinti wa marehemu Prof. Alice Wamunza Nkhoma.
DSC_0007
Baadhi ya waombolezaji wakimfariji mmoja watoto wa marehemu Bi. Agnes Nkhoma Darch (katikati).
DSC_0074
Waombolezaji wakiwa nyumbani kwa mtoto wa marehemu Prof. Alice Wamunza Nkhoma, Changanyikeni - Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
DSC_0096
Roy Ledama (kushoto) akibadilishana mawazo na baadhi ya waombolezaji.
DSC_0330
Familia ya karibu ya marehemu.
DSC_0290
Kushoto ni mabinti wawili wa Marehemu wakiwa na ndugu zao wakaribu kwenye majonzi mazito.
DSC_0275
Vitukuu wa marehemu mzee Arnold Nkhoma.


DSC_0285DSC_0295
Waombolezaji wakitoa heshima za mwisho.
DSC_0345DSC_0360
Mtoto wa Marehemu Prof. Alice Wamunza Nkhoma akitoa heshima za mwisho kwa baba yake mpendwa Mzee Arnold Nkhoma.
DSC_0363
Mtoto wa marehemu Bi. Agnes Nkhoma Darch akitoa heshima kwa baba yake.
DSC_0366DSC_0368
Mjukuu mkubwa wa marehemu Bi. Usia Nkhoma Ledama akitoa heshima za mwisho kwa babu yake.
DSC_0372
Vilio na simanzi vilitawala.
DSC_0374
Ndugu wa karibu wa marehemu wakiendelea kutoa heshima za mwisho.
DSC_0379
Mama Usia na mjukuu wake Vanessa Roy Ledama wakitoa heshima za mwisho kwa marehemu.
DSC_0381
Mjukuu wa marehemu Bi. Sawiche Wamunza Nkhoma akitoa heshima za mwisho kwa babu yake.

DSC_0109
Familia ya Marehemu Mzee Arnold Nkhoma pamoja na waombolezaji wakipata chakula cha mchana kabla ya kutoa heshima za mwisho.
DSC_0114
DSC_0148
DSC_0167
DSC_0383

RAIS KIKWETE ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA MKUU WA MKOA WA SINGIDA KUFUATIA VIFO VYA WATU 13 KWENYE AJALI ILIYOTOKEA LEO

HIVI NDIVYO WATU 13 WALIVYOPOTEZA MAISHA PAPO HAPO KUFUATIA AJALI MBAYA YA NOAH NA LORI LEO MKOANI SINGIDA.

$
0
0
DSC05846
Kamanda wa polisi mkoa wa Singida, SACP Geofrey Kamwela, akitoa taarifa ya ajali ya Noah T.730 BUX kuongwa na Lori aina ya Scania T.687 AXB katika barabara kuu ya Singida- Dodoma eneo la kijiji cha Isuna tarafa ya Ikungi wilaya ya Ikungi.Abiria 13 waliokuwa kwenye Noah wamefariki dunia na watatu wamepata majeraha madogo madogo.Ajali hiyo imetokea leo.(Picha na Gasper Andrew).
IMG-20140120-WA0000
(KUMRADHI KWA PICHA WADAU).Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Isuna tarafa ya Ikungi wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida, wakitoa miili ya abiria wa Noah T.730 BUX waliofariki baada ya gari hilo kugongwa na lori aina ya Scania T.687 AXB kwenye barabara kuu ya Singida – Dodoma leo. Noah hiyo ilikuwa ikitoea Itigi wilayani Manyoni akienda Singida mjini.(Picha na Nathaniel Limu).
DSC05820
DSC05824
ABIRIA 13 wakiwemo watatu wa familia moja wamefariki dunia mkoani Singida leo, baada ya gari walilokuwa wakisafiria aina ya Noah T.730 BUK, kugongwa na Lori aina ya Scania.
Ajali hiyo ya kusikitisha imetokea leo saa  1.32 asubuhi katika barabara kuu ya Singida-Dodoma eneo la kijiji cha Isuna tarafa ya Ikungi wilaya ya Ikungi mkoani Singida.
Kamanda wa polisi mkoa wa Singida,SACP ,Geofrey Kamwela, amesema gari hilo aina ya Noah lilikuwa likitokea Itigi wilaya ya Manyoni na lilikuwa na safari ya kuja Singida mjini.
Amesema hadi sasa miili ya abiria 10 wamekwisha tambuliwa na ndugu zao na miili ya abiria watatu,bado haijatambuliwa na miili yote bado imehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhia  maiti cha hospitali ya mkoa mjini Singida
Alitaja waliotambuliwa na makazi yao kwenye mabano kuwa ni Omari Shaban (44) na mke wake Salma Omari  na mtoto wao Nyamumwi Omari (10) wote wakazi wa Itigi mjini.
Kamwela alitaja wengine kuwa ni Haji Mohammed (29) (Msisi),Mtunku Rashidi (68) (Sajaranda),Salehe Hamisi (28) (Sajanranda),Samir Shaban (20) (Puma),Mwaleki Nkuwi (35) (Ikungi),Athumani Kalemba (38) na Ramadhan Mkenga (Sajaranda).Katika ajali hiyo,abiria watatu walinusurika na kupata majeraha madogo madogo.
Amefafanua juu ya ajali hiyo,Kamanda huyo alisema kuwa lori aina ya scania T.687 AXB wakati likipishana na noah,lilihama upande wake na kuifuata noah ambayo ilikuwa upande wake wa kushoto,na kuligonga na kisha kuliburuza kati zaidi ya 15.
“Kwa sasa bado hatujajua chanzo cha ajali hiyo mbaya ingawa baadhi ya watu wanadai kuwa huenda dereva wa lori alisisia na kusababisha lori hilo kuhama upande wake na kufuata noah.Uchuguzi utakapokamilika,tutatoa taarifa hiyo”,amesema.
Wakati huo huo,mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa mjini Singida,Dk.Banuba Deogratius amekiri kupokea miili ya abiria hao 13 na kusema kati yao,watoto ni wawili.habari kwa hisani ya moblog.

KAMPUNI YA CHINA WORLD BUZ YAENDESHA SEMINA KWA WAFANYABIASHARA JIJINI ARUSHA LEO

$
0
0
Shafii Mwaijande Ofisa Mtendaji Mkuu wa China Word Buz kwa upande wa Tanzania akizungumza na wafanya biashara wadogo na wakati kwenye ukumbi wa Triple A jijini Arusha wakati wa Semina kwa wafanya biashara hao iliyofanyika leo, kuhusu mfumo utakaosaidia wafanyabiashara wadogo wa Tanzania kutafuta masoko ya bidhaa nchini China na kuwapa taarifa sahihi za masoko kwa msaada wa kampuni hiyo,Mfumo huo hautampa gharama kubwa mfanyabiashara kama vile Usafiri , Chakula, Hoteli.kwani hatalazimika kusafiri kwenda China ili kununua bidhaa badala yake kampuni hiyo itamuagizia na kumfikisha mahali alipo ama kumshauri ni njia gani anaweza kutumia kupata bidhaa kutoka China, kulia ni Ofisa mtendaji mkuu wa kampuni ya China Word Buz na mwakilishi wa wamiliki wa viwanda 45 nchini China vilivyoingia mkataba wa kibiashara na kampuni hiyo China Bwana Cheng Wang Wu2
Shafii Mwaijande Ofisa Mtendaji Mkuu wa China Word Buz kwa upande wa Tanzania akiwaelezea na wafanyabiashara wadogo malengo kampuni hiyo katika kuwakomboa wafanya biashara.



5Baadhi ya wafanya biashara wakiwa katika semina hiyo6Baadhi ya wafanyabiashara wakifuatilia majarida yanayoelezea mifumo ya ufanyaji kazi wa kampuni hiyo.7Uongozi wa kampuni ya China World Buz ukipiga picha ya pamoja na wafanyabiashara hao baada ya kumalizika kwa semina hiyo.8Shafii Mwaijande Ofisa Mtendaji Mkuu wa China Word Buz kwa upande wa Tanzania akizungumza na maofisa wa kampuni hiyo kutoka china.9Wakuu wa Kampuni hiyo wakipiga picha ya pamoja na maofisa wao

RAIS KIKWETE AWAAPISHA MAWAZIRI NA MANAIBU WAZIRI IKULU LEO

$
0
0
 Rais Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali, Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Katibu Mkuu Kiongozi wakipozi na mawaziri na manaibu waziri baada ya hafla ya kula viapo
 Rais Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali, Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Katibu Mkuu Kiongozi wakipozi na mawaziri baada ya kiapo.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi (Mb) Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Ikulu jijini Dar es salaam leo. Kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue
 Mhe. Mathias Meinrad CHIKAWE (Mb) Waziri wa Mambo ya Ndani akila kiapo
 Mhe. Dkt. Asha-Rose Mtengeti MIGIRO (Mb) Waziri wa Katiba na Sheria
 Mhe. Lazaro Samuel NYALANDU (Mb) Waziri wa Maliasili na Utalii akila kiapo
 Mhe. Dkt. Seif Seleman RASHIDI (Mb) Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii akila kiapo
Rais Kikwete akimuapisha  Mhe. Saada Mkuya SALUM (Mb) Waziri wa Fedha
 Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Dismas KAMANI (Mb) Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi akila kiapo
Mhe. Adam Kighoma Ali MALIMA (Mb) Naibu Waziri wa Fedha akila kiapo
 Mhe. Charles Muhangwa KITWANGA (Mb) Naibu Waziri (Nishati) akila kiapo


 Mhe. Amos Gabriel MAKALLA (Mb) Naibu Waziri wa Maji
 Mhe. Janet Zebedayo MBENE (Mb) Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara
 Mhe. Jenista Joakim MHAGAMA (Mb) Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi akila kiapo
 Mhe. Dkt. Pindi Hazara CHANA (Mb) Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto akila kiapo
 Mhe. Godfrey Weston ZAMBI (Mb) Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika akiapishwa
 Mhe. Mwigulu Lameck NCHEMBA (Mb)  Naibu Waziri wa Fedha akila kiapo
                        

 Mhe. Dkt. Kebwe Stephen KEBWE (Mb) Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii akila kiapo
  Mhe. Juma Selemani NKAMIA (Mb) Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Mhe. Mahmoud Hassan MGIMWA (Mb)  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na familia ya Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi (Mb) Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.
 Rais Kikwete na baadhi ya wanafamilia ya Mhe. Mathias Meinrad CHIKAWE (Mb) Waziri wa Mambo ya Ndani 
 Rais Kikwete na familia ya Mhe. Dkt. Asha-Rose Mtengeti MIGIRO (Mb) Waziri wa Katiba na Sheria
  Rais Kikwete na familia ya Mhe. Lazaro Samuel NYALANDU (Mb) Waziri wa Maliasili na Utalii 
 Rais Kikwete na familia ya Mhe. Dkt. Seif Seleman RASHIDI (Mb) Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii
 Rais Kikwete na baadhi ya wanafamilia wa  Mhe. Saada Mkuya SALUM (Mb) Waziri wa Fedha
 Rais Kikwete na familia ya Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Dismas KAMANI (Mb) Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi 
 Rais Kikwete na familia ya Mhe. Adam Kighoma Ali MALIMA (Mb) Naibu Waziri wa Fedha 
 Rais Kikwete na familia ya Mhe. Charles Muhangwa KITWANGA (Mb) Naibu Waziri (Nishati)
  Rais Kikwete akiwa na familia ya Mhe. Amos Gabriel MAKALLA (Mb) Naibu Waziri wa Maji
  Rais Kikwete akiwa na familia ya Mhe. Janet Zebedayo MBENE (Mb) Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara
  Rais Kikwete akiwa na familia ya Mhe. Jenista Joakim MHAGAMA (Mb) Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi 
 Rais Kikwete akiwa na familia ya Mhe. Dkt. Pindi Hazara CHANA (Mb) Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto 
 Rais Kikwete akiwa na familia ya Mhe. Godfrey Weston ZAMBI (Mb) Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika 
 Rais Kikwete akiwa na familia ya Mhe. Mwigulu Lameck NCHEMBA (Mb)  Naibu Waziri wa Fedha
  Rais Kikwete akiwa na familia ya Mhe. Juma Selemani NKAMIA (Mb) Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
 Rais Kikwete akiwa na familia ya Mhe. Mahmoud Hassan MGIMWA (Mb)  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii
  Rais Kikwete akiwa na familia ya Mhe. Dkt. Kebwe Stephen KEBWE (Mb) Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii 
 Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali akiwa na baadhi ya mawazir na naibu waziri waliokula kiapo leo
  Rais  Kikwete na Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi wakiwa na makamanda na viongozi katika Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
 Rais Kikwete na Mhe. Mathias Meinrad CHIKAWE (Mb) Waziri wa Mambo ya Ndani wakiwa na wakuu wa vyombo vilivyo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani
 Rais Kikwete akiongea na Mhe. Mathias Meinrad CHIKAWE (Mb) Waziri wa Mambo ya Ndani na wakuu wa vyombo mbalimbali vya dola vilivyo chini ya wizara ya mambo ya ndani
 Mhe. Mathias Meinrad CHIKAWE (Mb) Waziri wa Mambo ya Ndani akiwa na viongozi wa vikosi mbalimbali vilivyo chini ya wizara yake
Mhe. Mwigulu Lameck NCHEMBA Naibu Waziri wa Fedha na Mhe. Adam Kighoma Ali MALIMA (Mb) Naibu Waziri wa Fedha na baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya fedha. PICHA NA IKULU.

muigizaji maarufu katika Tamthilia ya Isidingo The Need ya Afrika Kusini, Lesego Motsepe a.k.a Lettie Matabane afariki dunia

$
0
0
Aliyekuwa muigizaji maarufu katika Tamthilia ya Isidingo The Need ya Afrika Kusini, Lesego Motsepe maarufu zaidi kwa jina la Lettie Matabane, amefariki dunia nchini mwake Afrika Kusini mapema leo.


Lettie, ambaye alijipatia umaarufu mkubwa katika tamthilia hiyo kuanzia mwaka 1998 hadi 2008 alipoamua kuondoka, alikuwa akiishi na virusi vya Ulimwi kwa zaidi ya miaka 15. Mwaka 2011, aliwashitua mashabiki wake baada ya kuwatangazia kuwa yeye ni muathirika wa ukimwi. 

Hata hivyo wengi walimpongeza kwa kuwa na ujasiri wa kujitangaza hadharani, kwani kwa miaka mingi alikuwa akifanya kazi ya ubalozi wa mambo ya ukimwi. Aliianza kazi hiyo ya ubalozi kabla hajaathirika na hata alipoathirika hakushituka sana ingawa hali hiyo ilibadili maisha yake kabisa.



Tamthilia ya Isidingo ni miongoni mwa tamthilia kongwe na maarufu nchini Tanzania ambayo imekuwa ikioneshwa na televisheni ya ITV kwa zaidi ya miaka kumi sasa bila kuchosha watazamaji wake.
Mungu ailaze roho yake mahala pema - AMEEN!
Viewing all 46327 articles
Browse latest View live




Latest Images