Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 204 | 205 | (Page 206) | 207 | 208 | .... | 1898 | newer

  0 0


  THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

  DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS


  Telephone:255-22-2114512, 2116898

                press@ikulu.go.tz             

  Fax: 255-22-2113425  PRESIDENT’S OFFICE,

        THE STATE HOUSE,

                P.O. BOX 9120,  

  DAR ES SALAAM.

  Tanzania.

   
  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Mhandisi Paul Mhangilwa Masanja kuwa Kamishna wa Madini nchini.

  Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Obeni Y. Sefue mjini Dar Es salaam leo, Ijumaa, Januari 17, 2014, imesema kuwa uteuzi huo wa Bwana Masanja ulianza jana, Januari 16, 2014.

  Taarifa hiyo imesema kuwa kabla ya uteuzi wake, Mhandisi Masanja alikuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA).


  Imetolewa na:

  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

  Ikulu,

  DAR ES SALAAM.


  17 Januari, 2014

  0 0


  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua athari za mafuriko yaliyokikumba kijiji cha Chipogoro wilayani Mpwapwa Januari 17, 2014. Kulia kwake ni Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara na Mbunge wa Mpwapwa, Gregory Tewu na kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Dr. Rehema Nchimbi.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitazama sehemu ya jengo la Kituo cha Polisi cha kijiji cha Chipogoro wilayani Mpwapwa ambayo imeporomoka kufuatia mafuriko yaliyokikumba kijiji hicho kufuatia mvua kubwa zianazoendelea kunyesha mkoani Dodoma januari 17, 2014. Kulia kwake ni Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Dr. Rehema Nchimbi.
  Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akikagua daraja ambalo lilizibwa na maporomoko ya maji yaliyoambatana na magogo , mawe na udongo na kusababisha mafuriko katika kijiji cha Chipogoro wilayani Mpwapwa januari 17,20134.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua athari za mafuriko katika kijiji cha Fufu wilayani Chamwino, Dodoma, Januari 17, 2014.Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rehema nchimbi na kulia kwake ni Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  =======  ======  ========
  *Amtaka Meneja TANROADS apitie upya maeneo korofi
  *Aahidi mabati 780, mifuko 2,600 ya saruji kwa walioathirika
  WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ametembelea vijiji vya Chipogoro na Fufu katika wilaya za Mpwapwa na Chamwino, mkoani Dodoma na kukagua maeneo mbalimbali ambayo yaliathiriwa na mafuriko kutokana na mvua kubwa zilizonyesha kati ya Januari 2 hadi Januari 11, mwaka huu.
  Akiwa katika kijiji cha Chipogoro tarafa ya Rubi, Waziri Mkuu alikagua kituo cha polisi na nyumba zilizobomolewa, choo cha zahanati na kukagua eneo la barabara inayojengwa ya kutoka Dodoma hadi Iringa katika eneo lenye matatizo ya makaravati kuziba.
  Kwenye kijiji cha Fufu katika tarafa ya Makangwa ambacho kiko umbali wa kilometa 30 kutoka Chipogoro, Waziri Mkuu alikagua maeneo ya makazi yaliyoathiriwa kwa mafuriko na kukagua baadhi ya nyumba zilizobomoka kabla ya kuzungumza na wananchi na kuwapa pole.
  Akizungumza na wakazi wa vijiji hivyo leo (Ijumaa, Januari 17, 2014), mara baada ya kupokea taarifa za maafa ya mafuriko hayo, Waziri Mkuu alimtaka Meneja wa TANROADS mkoa wa Dodoma, Eng. Leonard Chimagu kuhakikisha anasimamia wakandarasi wa barabara hiyo ambayo ujenzi wake bado haujakamilika na kuainisha maeneo korofi ili yafanyiwe marekebisho haraka.
  “Nimekagua matundu katika daraja moja pale Chipogoro na kuona ni madogo, mtaalamu anasema uchafu ulioziba ndiyo umesababisha maji yasipite. Mimi si mhandisi na hizi ni mvua za kwanza tu, sasa yakija maji mengi zaidi ya haya hali itakuwaje?, alihoji Waziri Mkuu.
  “Hata hapa Fufu, kuna mahali nimeona maji yanaonyesha yalikuja kwa kasi kubwa lakini upenyo wa kuingia kwenye makaravati na kutokea upande wa pili ni mdogo sana... barabara hii ni mkombozi lakini kama haitazingatia uhalisia wa maeneo itakuwa ni balaa,” alionya.
  Alimtaka pia awasimamie wakandarasi hao ili wanapoweka matoleo ya maji wahakikishe upande wa pili barabara maji hayo yanakwenda kwenye mikondo ya mto na siyo kuyaacha tu yasambae kiholela na kuishia kwenye makazi ya watu au mashamba yao.
  Waziri Mkuu aliahidi kutoa mifuko ya saruji 2,600 na mabati 1,560 ambapo kila kijiji kitapata mifuko 1,300 na mabati 780 ili kuwasaidia wakazi waliobomolewa nyumba zao waweze kujenga nyumba za kisasa.
  Alimwagiza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi kuwashirikisha wadau wengine katika mkoa huo ili waone wanawezaje kuchangia upatikanaji wa mabati mengi zaidi kwa ajili ya nyumba zilizoezuliwa.
  Kuhusu chakula cha msaada, Waziri Mkuu alimtaka Dk. Nchimbi aandae makisio ya mahitaji ya chakula yaliyopo na kuyafikisha Ofisi ya Waziri Mkuu ambako kuna Idara inayosimamia maafa ili waletewe chakula hicho haraka kwa sababu kipo.
  Alisema anakubaliana na ushauri uliotolewa kuhusu suala la ujenzi wa mabwawa ya kukinga maji ya mvua ili kupunguza kasi ya maji yanayoporomoka kutoka milimani lakini akasema Serikali imeanza na ujenzi wa Bwawa la Kidete lililoko wilayani Kilosa tangu yaliyopotokea mafuriko wilayani humo.
  Mapema, akitoa taarifa kwa Waziri Mkuu, Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Bw. Alfred Msovella, alisema nyumba 129 zilibomoka, vyoo 78 vimebomoka kikiwemo cha zahanati ambapo wakazi 1,390 wamepoteza vifaa mbalimbali ikiwemo vyakula, magodoro, vyombo vya ndani na mifugo.
  Bw. Msovella ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kongwa alisema hivi sasa, wakazi hao wanahitaji mahema 400, magodoro 381, madaftari ya wanafunzi na dawa za matibabu.
  Naye Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Bi. Fatma Salum Ally akitoa taarifa mbele ya Waziri Mkuu kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa shule ya msingi Fufu, alisema jumla ya nyumba 26 zilibomolewa na mali kama vyakula, samani, vyombo vya nyumbani na bidhaa za biashara kuharibika.
  Alisema eneo la kijiji cha Fufu ni tambarare na liko chini ya safu za milima na maji ya mvua yanayoporoka kutoka milimani, huondoka polepole. “Hata hivyo, hali hii ya mafuriko imechochewa na ujenzi wa barabara kuu kwa kiwango cha lami ambapo tuta la barabara mpya na vidaraja vidogo vilivyowekwa vimekuwa kizuizi cha maji mengi yanayotoka milimani na hivyo kuongeza tatizo la mafuriko,” alisema.
  Mikutano hiyo ilihudhuriwa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Bw. Gregory Teu ambaye pia ni mbunge wa Mpwapwa pamoja na mbunge wa Mtera, Bw. Livingstone Lusinde.
  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  DODOMA.
  IJUMAA, JANUARI 17, 2014

  0 0

  Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kutoka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bw. Ludovick Utouh akitoa taarifa ya ukaguzi maalum leo Bukoba.
  Naibu Waziri wa TAMISEMI Mhe. Agrey Mwanri akiendelea kutoa Maelezo ya Serikali. Kuhusu Suruhisho hilo ambapo yamebainika Makosa ya Meya Anatory kufanya makubaliano bila idhini ya Madiwani na Taratibu za serikali, Basi ajipime Mwenyewe na Kujiuzulu mara moja kwa Maslahi ya Manispaa ya Bukoba.
  Mkuu wa mkoa wa Kagera Mh.Fabian Massawe akimkaribisha mgeni Rasmi leo kwenye kikao hicho cha kukamilisha Ukaguzi Maalum" Exit Meeting"  Cha mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali leo Januari 17.2014 Mjini Bukoba ambapo kikao hicho kilianza mapema saa 5 Asubuhi.
  Wadau mbalimbali wakiwa kwenye kikao hicho kizito kilichofanyika leo mjini Bukoba na kupelekea Meya Anatory Amani kujiuzulu kufuatia ubadhirifu wa fedha uliobainika.
  ==
  SOMA TAARIFA YA CAG HAPA CHINI.
  ===== =====  =======

  TAARIFA YA CAG
  Waziri mkuu alituomba tufanye ukaguzi maalum,

  Mwaka 2013 tulifika bukoba na kufanya kikao cha kwanza na wadau.
  Katika kikao hicho nilitoa maombi ambayo mliyafuata nawashukuru,madiwani na wananchi walitusaidia saan  Natoa taadhari kwamba tulikuwa na adidu za rejea ambazo ndizo tulizofuata,tulipokea mombi ya wananchi wengi lakini hayakuwepo katika adidu za rejea,hatukuyafanyia kazi

  Kilichobainika
  Tunapohitaji maendeleo,tunafanya vitu kwa nia njema bila kufuata taratibu  Kuhusu uwekezaji wenye mashaka kwenye kituo cha kuosha magari,zabuni haikuwa shindanishi  ni kiyume na taratibu cha taribu anataja kifungu kilichokiukwa  Waliosaini ni Khamis kaputa na anatory amani huku wakijua ilikuwa ni makosa kufanya hivyo bila idhjini ya kikao cha madiwani,pia kamupuni husika ya ASEC ilikuwa haijasajiliwa na BRELA. hailipi kodi TRA  2.Issue ya Viwanja
  kati ya wananchi 800 waliotakiwa kugawiwa viwanja ni 300 waliogawawia kutokana na migogo ya viwanja kimila.  Manispaa ilingia makubaliano na UTT kupima viwanja elfu 5 kwa kuggawana faida ya asilimia 50 kwa 50 baina ya UTT manispaa ilisainiwa na kaimu meya ngalinda bila kupata idhini ya baraza la madiwani  Pia walikopa fedha kutoka UTT bila kupata ridhaa ya waziri mwenye thamana.
  3.Issue ya matengenzo ya barabara mpya  Manispaa ya bukoba iliingia mkataba na mkandarsai aitwaye KAJUNA INVESTMENT mkataba ulikuwa wa sh 138 milioni alilipwa fedha za dharula amabzo hazikuwa na nyaraka hivyo malipo ya mkandarasi huyu yaliongezwea hadi kufikia sh sh 227 kwa kutumia barua iliyosainwa na tofauti na hali ya awali.haikuwapa idhini ya mkandarsi wa serikali na kinyume na kanuni za manunuzi ya umma.anasoma kifungu kilichokiukwa  4.issue ya Ujenzi wa soku kuu
  Utaratibu wa kutaka kujenga soko kuu la bukoba haikupata idhini ya madiwani ya kumlipa mkandarasi mshauri OGM milioni 789 huku pia akawaita madiwani na kuwaeleza kuwa mkandarasi anahitaji jumla la miliini 590 mlioni. Mmojawapo wa madiwani mhg lunagisa alikataa pale pale kwenye kikao.  5.Issue ya kuhamisha wafanyabisha wa bukoba
  Mh Meya anatory aman aliomba mkopo kwa kazi hiyo bila kibali cha madiwani na mawaziri.mkpo huo hata hivyo haukupoatika
  6.Mkandaasi wa OGM hakuwa kwenye orodha ya walioomba zabuni ya kufanya kazi ya ukandarasi ushauri wa kufanya kazi katika ujenzi wa soko kuu lakini alionekana kwenye rodha baadye ya waliolipwa .Wakandarasi wote waliolipwa fedha hizo walikuwa hawalipi kodi TRA-hivyo TRA ina haki ya kuwadaiu hizo kodi.  7.Ujenzi wa stendi kuu ya bukoba
  Mradi huu hakutengezwa kwenye gazeti la sertikali lakini walipata mkandarasi na kumlipa fedha za kazi hiyo kinyume na taratibu za serikali.gazeti lilotangaza tenda hiyo halikupatikana.pia timu ya ukaguzi ilitembelea eneo al kazi na kubaini kuwa mkandarasi alilipwa fedha nyhingi tofauti na kazi aliyoifanya  9.Mradi wa maji
  Kila kata iliyopangwa kuwekwa mradi wa maji ilitakiwa kuchangia asilimia 2 hivyo kata anakotoka meya ilitiumiza kigezo na kupata huduma hiyo.fedha za kata zilitolewa na meya kwa kata yake.hivyo kitendo cha kata ya meya kupata huduma hakuwa na tatizo.Tuhuma hizi kuwa meya alitoa huduma kwa kata yakle ni uongo.
  10.Issue ya uuzwaji viwanja vya wazi.
  Mkataba wa kununua kiwanja kinacholalamikiwa hakufuata taratibu za ununuzi
  Ni katika bweni la sekondari ya PEACE inayomilikiwa na Meya.Tunapendekeza kuundwa kwa trimu maalum kuchunguza tuhuma hizi kwani katika eneo hili hatukufikia mwisho
  11.Ujenzi wa barabara kwa lami kwenye kata ya meya toafuti na fedha zilizoombwa
  Manispaa iliomba milioni 30 kukaqrabati barabarab hiyo akini TAMISEMI ilitao milioni 300 na walihoji TAMISEMI walisema hilo ni la kawaida hivyo tuhuma hizo ni UONGO  12.Mradi wa Ujenzi wa Bwawa 
  Hakuwahi kujadiliwa na baraza la madiwani,ulikuwa ni mradi wa wajanja tu  13.Issue ya wafganyabishara soko kuu kutolipa kodi
  Manispaa Imekosa mapato sh milioni 256 zimpotea kutokana na chanzo hizo cha wafanyabishara wa soko kuu kutolipa kodi kutokana na mgogoro unaondelea  14.Issue ya matumizi ya gari Sm 4663
  Gari hili limekuwa likiegeshwa kwa ofisi ya redio kasibante ya kagasheki.kumbukumbu za TRA zinaonesha kuwa ni mali ya halmashauri lakini alipohojiwa kagasheki alidai kuwa alinunua kwa fedha zake. Lakini halmshauri haina kumbukubu zozote juu ya gari hilo  Tunapendekeza alilrejeshwe kwenye halmshauri kama ataona ni manufaa kwa wananchi lakini kama haitawezekana basi gari hilo libadilishiwe usajhili ili lionekbnane ni la kiraia  15.Uteuzi wa wakala wenye upendeleo kwenye ushuru wa basi
  Zabubi ya aliyepata rufaa ilitenguliwa kwani haikuwa imesajiliwa na mamlaka husika
  Alibadilisha jina na kuomba tena kasha kupata,muombaji aliyeomba kwa tozo ya juu alinyimwa.  Manispaa ilifanya upendeleo na kukosa sh million 46 kwa mwaka
  16:Issue ya posho kwa madiwani katika safari ya mafunzo nje ya wilaya.
  Madiwani wawili walitakiwa kulipwa sh laki 4 kila mmoja kwa safari hawakusafiri lakini fedha hizo hazikurudishwa kwa manispaa na kukatiwa risiti,.hazionekjani zilipo
  17.Issue ya vibanda vya maduka
  Ukaguzi hakudhibitisha kuwepo tatizo la katika dai hili kwani nyaraka zinaonesha kutokuwepo tatizo.bali inashauri kuwepo kwa mkanganyiko na wapangaji wake  18.Issue ya deni katika uwanja wa mpira kaitaba.
  Uwanja ulikarabatiwa na kiwanda cha sukari kagera kwa madai ya kurejeshewa fedha zake.sehemu ya fedha hazijarudishwa.Tume inapendekeza kufanya muafaka na kiwana au itafute fedha za kulipa deni  19.Kutowajibika ipasavyo kwa ukaguzi wa ndani.
  Kipo kwa ajili ya kushauri na kuziba mianya ya matumizi mabaya ya fedha.
  Aliyekuwepo amehojiwa juu ya miradi hiyo na kwamba halikuwa hajui lolote na hakuweza kumshauri mkurugenzi ipasavyo  20.Mteuzi katika bodi ya maji.upendeleo kwa mmoja wa madiwani
  Waziri mwenye thamana aliteuwa


  Hitimisho.
  Hatukuweka chumvi,tuliyosema ndiyo ukweli tupu
  Namshukuru waziri mkuu kwa kunipa kazi hii ya kukaguzi katika manispaa  Utaratibu wa uwasilisahji wa ripoti maalum tutaipeleka kwa aliyeomba ukaguzi huu.
  ASANTENI AMEMALIZA  Mwanry anaongea sasa
  Kwa niaba ya waziri mkuu naomba nitoa taarifa hii kama ifuatavyo  Maelekezo ya waziri mkuu.
  Makosa ya meya anatory kufanya makubaliano bila idhini ya madiwani na taratibu za serikali basi ajipimemwenyewe na kujiuzuru kwa maslahi ya manispaa ya bukoba.  Akikataa basi madiwani wamuondoe
  Watumishi wa manispaa wachukuliwe hatua
  Bw Khamis kaputa avuliwe madaraka
  Mhandisi,mweka hazina nk wapoteze vyeoi vyao  Wakandarasi wote waliopata fedha bila taratibu wazirejeshwe

  0 0

   Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samuel Sitta (katikati) akifafanua kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es salaam kuhusu Serikali ya Tanzania ilivyodhamiria kuimarisha ushirikiano baina yake na nchi wanachama wa Jumuiya hiyo. Wa kwanza kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara hiyo Amantius Msole na wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Msaidizi  Idara ya Habari Maelezo Bi Zamaradi Kawawa.

  Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samuel Sitta akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es salaam juu ya  Shirikika la ndege la Tanzania (ATCL) kupanua huduma zake na kufika Bujumbura nchini Burundi, ATCL ilianza kufanya safari zake kati ya Tanzania na Burundi Desemba16, 2013 mara tatu kwa wiki kama moja ya hatua za kuimarisha usafiri wa anga kati ya nchi wanachama. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara hiyo Amantius Msole.

  1 Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samuel Sitta akisisitiza kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es salaam kuhusu Tanzania itakavyonufaika na mfumo wa himaya moja ya forodha katika kuimarisha biashara kati ya nchi wanachama wa Jumuiya hiyo.(Picha zote na Frank Mvungi-Maelezo).


  ======  =======  =======
  Na Frank Mvungi

  Serikali ya Tanzania imedhamiria kuimarisha ushirikiano baina yake na nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika Nyanja za miundombinu. Hayo yamesemwa na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Samuel Sitta wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.

  Mh.Sitta alibainisha kuwa mwishoni mwa mwaka 2013 Mawaziri wa Tanzania, Burundi, na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) walikutana kujadili namna ya kuimarisha miundo mbinu ya barabara, reli, anga, anga na maji.


  Mh.Sitta aliongeza kuwa katika kikao hicho ilikubaliwa kuwa Shirikika la ndege la Tanzania (ATCL) lipanue huduma zake na kufika Bujumbura nchini Burundi ambapo ATCL ilianza kufanya safari zake kati ya Tanzania na Burundi Desemba16, 2013 mara tatu kwa wiki kama hatua za awali za utekelezaji.


  Mh. Sitta alisisitiza kuwa katika mkutano wa 8 wa Baraza la la Mawaziri la Jumuiya hiyo umeridhia mfumo wa himaya moja ya Forodha na mpangokazi unaoainisha masuala ya utekelezaji katika kipindi cha miezi sita ili kuwezesha kuanzishwa kwa himaya hiyo ifikapo Juni 2014. Mh. Sitta akifafanua zaidi alisema mfumo wa himaya moja ya forodha unaainisha utaratibu wa mzunguko wa biashara, usimamizi wa mapato na mfumo wa kisheria.

  Katika mfumo huo Sitta alisema kuwa ilikubalika kuwa nchi wanachama zitakusanya mapato yake ya kodi. Aidha, kwa bidhaa zinazopitia nchi moja kuelekea nchi nyingine wanachama za Jumuiya hiyo zimekubaliana kuwa nchi husika itakusanya mapato yake na kuifahamisha mamlaka ya forodha mizigo ilipoingilia katika Jumuiya kwa kwa ajili ya kuruhusu bidhaa kuondoshwa.

  Mkutano wa 15 wa Kawida wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya Afrika Mashariki Uliofanyika Jijini Kampala, Uganda Novemba 30, 2013 na kuamua masula muhimu ya maendeleo ya Mkutano wa Jumuiya Afrika Mashariki.


  Baadhi ya masuala yaliyojadiliwa na kutolewa uamuzi ni pamoja na kutiwa saini kwa Itifaki ya Umoja wa Fedha, kuidhinishwa uundwaji wa Himaya ya Umoja wa Forodha (Single Cstoms Territory). 

  0 0

   Madiwani wakipiga makofi ikiwa ni ishara ya kumpongeza Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu (wa pili kushoto)  kukata utepe  wakati wa hafla ya kukabidhi madawati 500 yenye thamani ya sh. mil. 67.5 yatakayogawiwa katika Shule za msingi katika Kata 13 za jimbo hilo. Hafla hiyo imefanyika leo Chuo cha Ufundi Chang'ombe, Dar es Salaam. 
   Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu akizungumza baada ya kukabidhi madawati 500 yenye thamani ya sh. mil. 67.5 yatakayogawiwa katika shule zilizopo katika Kata 13 za Jimbo hilo. Madawati hayo yaliyonunuliwa kwa fedha za Mfuko wa Jimbo yalikabidhiwa kwa madiwani wa Kata hizo katika hafla iliyofanyika Chuo cha Ufundi Chang'ombe, Dar es Salaam
   Naibu Meya wa wa Manispaa ya Temeke, Juma Mkenga akitoa shukurani kwa Mbunge Mtemvu kutoa madawati hayo.
   Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Zena Mgaya akimpongeza Mtemvu kwa juhudi za kuinua kiwango cha elimu wilayani Temeke.
   Ofisa Elimu wa  Shule za Msingi Manispaa ya Temeke, Honorina Mumba akieleze furaha ya kupata madawati hao 500 yatakayopunguza tatizo la madawati wilayani Temeke.
   mwanafunzi Azizi Ally wa Shule ya Msingi Keko Magurumbasi, akitoa shukurani kwa Mtemvu kwa  niaba ya wanafunzi kwa kuwapatia madawati hayo  
  Fundi akiendelea kupiga msasa baadhi ya madawati hayo yaliotengenezwa VETA Chang'ombe.(PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG)   Mtemvu akiangalia wakati mwanafunzi Azizi Ally wa Shule ya Msingi Keko Magurumbasi akiandika jina lake.
   mwanafunzi Azizi Ally wa Shule ya Msingi Keko Magurumbasi, akitoa shukurani kwa Mtemvu kwa  niaba ya wanafunzi kwa kuwapatia madawati hayo  
  Fundi akiendelea kupiga msasa baadhi ya madawati hayo yalitotengenezwa VETA Chang'ombe

  0 0

  stage_name_hd
  Photo Credit: singsnap.com

  Kama mwandishi na mmiliki wa blog kama hii ya BC [mahali ambapo vipaji huibuliwa na majina kutambulishwa] mojawapo ya majukumu yangu ya kawaida kila siku au kila wiki ni pamoja na kupokea kazi mbalimbali za wasanii. Mara nyingi,kazi hizo zinakuwa bado hazijasikika katika masikio ya wapenzi na mashabiki wa muziki. Hivyo basi,ni jukumu langu pia kuzisikiliza nyimbo hizo, kuzifafanua na kuzielewa ili kupata maudhui yanayofaa katika kuitambulisha nyimbo na msanii mwenyewe.

  Kuna wanaochipukia na kuna wanaoanza safari ndefu ya kuelekea kwenye umaarufu au kujikimu na maisha. Kuna wanaokuwa wanarejea baada ya mapumziko na tafakuri na kuna ambao wanakuwa wameogopa kwamba wanaanza kusahauliwa na hivyo wanajifaragua kurejea kilingeni.

  Hivi sasa, kila jua linapozama,maelfu ya vijana wanajisogeza vitandani mwao kupumzisha mwili na akili huku ndoto zao zikilenga kwenye “kutoka” kwa maana ya kuwa msanii superstar ajaye. Kazi ya kuwaza ni kazi.Kazi ya kufanya kinachotakiwa kufanyika ili kutimiza lengo au malengo ni kazi zaidi.

  Sanaa inalipa. Sanaa ni kazi. Sina takwimu halisi lakini bila shaka tunakubaliana kwamba sanaa inatoa ajira kwa maelfu [kama sio mamilioni] ya vijana nchini mwetu.Na ni kweli kwamba ingelipa zaidi endapo taratibu na sheria mbalimbali [ambazo zipo] zingetumika vyema. Kuna wanaofaidi Jasho la hawa vijana na ndio maana kuna “mgando” katika utekelezaji wa sheria hizo. Hii ni mada ambayo natumaini kuifanyia kazi zaidi katika siku za usoni.

  Leo ninachotaka kuzungumzia ni jinsi ya kuchagua jina la kutumia kama msanii[ stage name]. Kwa mzaha unaweza usione umuhimu wa kupasua kichwa kwamba utoke na jina gani au jinsi gani jina unalotumia hivi sasa linaathiri soko au masoko ya kazi zako na maendeleo yako kwa ujumla kama msanii. Lakini endapo utatumia muda kidogo na kutizama majina japo 10 tu ya wasanii unaowajua au unaovutiwa na kazi zao ndani na nje ya Tanzania,utagundua kwamba, umakini unaohitajika katika kazi nzima ya sanaa[ ubunifu,umaridadi,hadhira, ujumbe nk] inahitajika pia katika zoezi la kuchagua jina.

  Kabla hata ya watu kusikia kazi yako,watasikia jina kwanza. Mtangazaji wa redio, televisheni au hata mwandishi wa makala ya burudani gazetini au kwenye blog nk atasema leo tunamtambulisha fulani bin fulani ambaye ni msanii mpya. Jina la wimbo wake ni … Tayari utaona kwamba jina linaanza na hivyo kuna umuhimu mkubwa wa kuzingatia unatumia jina gani.

  Bila shaka wewe msomaji,shabiki wa muziki,mtangazaji wa radio au televisheni utakubaliana nami kwamba jina la msanii linahusika [the name matters]. Yapo majina ambayo ukiyasikia unashikwa na tamaa ya kuisikia kazi yake. Kama kazi yake itakuwa sio nzuri kwa kiwango ulichotarajia, hilo ni suala jingine ila amini usiamini,jina unalojipa lina nafasi kubwa sana katika aina ya kazi za sanaa utakazokuwa unazitoa. Wanasaikolojia wanakubaliana katika hili pia.

  Ninapopokea kazi za wasanii[ hususani wale wapya kabisa ambao ndio kwanza wanataka “kutoka”] huwa natizama kwa makini kazi yake nikianza na jina analotumia yeye kama msanii na hata jina la wimbo. Ninapoona msanii amechagua kujiita “Bullet Hunter au Idiot Sucker au Mtambo wa Gongo” nk huwa naanza kushikwa na simanzi. Kwa bahati mbaya mara nyingi imekuwa ikitokea kwamba Bullet Hunter na kazi yake huwa imekaa kama bullet[risasi] zina mlio lakini zinaweza kuelekezwa kokote na kuua yeyote aliyepo mbele. Mifano ya majina ya kisanii yenye kuleta au kujenga taswira “fulani” kabla hata ya kusikia kazi ya msanii ni mingi. Sitaki kupoteza muda wako msomaji wangu kwa kukupa mifano laki zaidi.

  Jina unalolichagua ndilo litakalotumika kukutambulisha wewe kama msanii na kazi zako. Wenzetu wanasema ndio “brand” yako. Mtu akitaka kuelewa kazi zako kwa kutizama na kutafsiri jina lako tu atapata majibu gani?

  Hizi hapa chini ni mbinu zinazoweza kumsaidia msanii kuchagua jina la kisanii [stage name]
   
  • Unaweza kutumia jina lako…Lakini: Bahati nzuri kabisa ni kwamba baadhi ya wasanii hawahitaji kuongeza wala kupunguza kitu kutoka kwenye majina yao. Wanaweza au unaweza kutumia jina lako kamili na likakubalika. Mifano ya wasanii wa namna hiyo wapo wengi. Lakini kama utakavyoona katika dondoo zinazofuatia hapa chini, ni muhimu kuhahakisha kwamba vigezo hivi umevizingatia au kuviangalia kwa makini zaidi. 
  • Chagua Jina Unalolipenda: Mifano ya watu ambao walipozaliwa wazazi wao waliwapa majina fulani na baadae kidogo tu walipojielewa wakagundua kwamba hawayapendi  kabisa majina yao na kuamua kuyabadili ipo mingi sana.Katika karne hii hutaki kupitia hayo. Chagua jina ambalo unalipenda na hutolionea soni kuliitikia. Hii ni pamoja na jina lako kama msanii [stage name]. Hutaki kujipa jina ambalo baada ya muda mfupi ukisikia MC analitaja unataka kujificha badala ya kuwa na shauku ya kulivamia jukwaa. 
  • Liwe Rahisi Kutamkika: Unapochagua jina hakikisha  kwamba linakuwa rahisi kutamkika. Hapa ni muhimu kuzingatia kwamba ndoto yako [ na ya kila msanii] ni kuuza kazi zake kwa mataifa mbalimbali na watu wa asili mbalimbali. Je,mchina ataweza kutamka jina lako kirahisi? Mzungu wa Amerika je? Vipi Mhindi kutoka Mumbai? Kwa bahati mbaya, watu wengi wanaposhindwa kulitamka jina lako wanakata tamaa pia kuwaambia marafiki zao kuhusu “yule msanii ambaye jina lake siwezi kulitamka”. Unakosa masoko.Unapoteza fursa ya kuongeza mashabiki. 
  • Liwe Rahisi Kukariri au Kukumbukwa: Unapochagua jina hakikisha kwamba ni rahisi kukumbukwa. Mara nyingi hili huenda sambamba na kuchagua jina fupi[mara nyingi moja]. Japokuwa wapo wasanii au wanamuziki mbalimbali maarufu ambao walitumia majina yote mawili na yakakamata [mfano Michael Jackson] lakini kumbuka kwamba majina yote [Michael na Jackson] ni mepesi kukumbuka na pia marahisi kutamkika. Unapokuwa na jina rahisi kukumbukwa na mashabiki na wapenzi wa muziki inavutia zaidi na inapanua kirahisi zaidi wigo wako wa biashara. 
  • Linauzika?: Ushawahi kusikia jina la msanii fulani ambalo hapo kwenu linamaanisha tusi baya kabisa? Eeenh, nadhani umenielewa. Siku hizi ni rahisi kutizama maana ya jina lako katika lugha mbalimbali ulimwenguni. Google inatoa msaada huo kupitia ukurasa wake wa masuala ya ukalimani. 
  • Tumia jina moja tu badala ya mawili: Hii inaendana na hiyo hapo juu. Badala ya kutumia majina yako yote mawili jaribu kutumia au kuchukua jina moja. Jina hilo moja linaweza kuwa jina lako la mwanzo, kati au mwisho[mara nyingi la baba]. Mfano wa wasanii maarufu ambao waliamua kutumia majina yao ya mwanzo tu na kuachana na mengine ni Rihanna[ alipozaliwa alipewa jina  Robyn Rihanna Fenty], Beyonce [jina lake ni Beyoncé Giselle Knowles] au Madonna [ aliitwa Madonna Louise Ciccone] 
  • Unaweza kutumia Namba au Alama: Ingawa unahitaji kuwa makini zaidi unapoamua kutumia namba kwenye jina lako la kisanii, unapoamua kutumia jina lenye namba hakikisha kwamba linakuwa na maana au linaendana kwa karibu na kitu au vitu vinavyohusiana na maisha yako. Hivyo vinaweza kuwa jina la mtaa[maarufu ulipokulia] au hata nchi kwa mfano [#255 ambayo ni code ya miito ya simu ya kimataifa kwa Tanzania]. Baadhi ya wasanii maarufu ambao waliongeza au kuweka namba kwenye majina yao ni kama vile marehemu 2Pac[ jina lake ni Tupac Amaru Shakur] E-40 [ jina lake Earl Stevens) au Ke$ha ( alipozaliwa wazazi walimpa jina Kesha Rose Sebert). 
  • Unaweza kutumia jina la utani: Wengi wetu tulipokuwa watoto au mashuleni tulipachikwa majina ya utani. Nakumbuka mimi wenzangu shuleni waliniita CheGu. Nilikuja kuelewa baadae kwamba jina hilo lilitokana na misimamo yangu.Wakaona wanifananishe na Che Guevara[ mpigania haki za binadamu na uhuru aliyezaliwa Argentina na baada kupigana bega kwa bega na Fidel Castro kusaka utawala wa watu nchini Cuba na baadae Congo nk]. Nilichukia kuitwa CheGu. Leo hii nikiangalia nyuma na baada ya kuelewa maisha ya Che Guevara, nisingechukia na si ajabu ningekuwa msanii ningejiita jina hilo.Kwa upande wako unaweza pia kutumia jina ambalo ulikuwa unaitwa mtaani au shuleni kama utani. Lakini hakikisha masuala hayo hapo juu yanahusika.
   Lipo Au Lishachukuliwa Kwenye Mitandao Ya Kijamii?: Mwisho dunia ya leo imebadilika. Hata kusema imekuwa kama kijiji nahisi kuna mapungufu. Unapojiandaa kujipa jina ni vizuri kuhakikisha pia kwamba jina unalojipa unaweza pia kulitumia katika mitandao ya kijamii kwani mitandao hii [upende au usipende] ipo nasi sasa na muda mrefu ujao.

  Kumbuka kwamba jina [ambayo itabeba brand yako nzima] ndio itatumika katika masuala yote ya kujitangaza au kutafuta masoko ya kazi zako. Ni vigumu kufanya branding awareness bila kushirikisha mitandao ya kijamii. Kwa hiyo basi, ni vyema kuchunguza kwanza kama jina unalotaka kutumia bado linapatikana au limeshachukuliwa. Kama limeshachukuliwa achana nalo.Pia labda niongeze kwamba wakati huu huu wa kutafuta jina ni muhimu pia kuangalia upatikanaji wa vitu kama anuani ya tovuti yako nk.

  Jeff Msangi ni mwandishi,mwendeshaji mkuu wa mtandao wa BongoCelebrity.com na mdau wa karibu wa masuala ya burudani na muziki. Unaweza kuwasiliana naye kupitia jeffmsangi at gmail dot com.


  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  BUNGE LA TANZANIA
  images
  WITO KWA WAHESHIMIWA WABUNGE WOTE.

  Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anawatangazia Waheshimiwa Wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa wafike Jijini Dar es Salaam Jumapili tarehe 26 Januari 2014 kwa ajili ya shughuli za Kamati za Bunge zitakazoanza tarehe 27 Januari 2014 hadi tarehe 8 Februari 2014. Moja ya shughuli hizo ni pamoja na ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

  Imetolewa na
  Ofisi ya Bunge,
  Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na
  Uhusiano wa Kimataifa
  Dar es Salaam

  17 Januari 2014.

  0 0
 • 01/18/14--03:28: KIWANJA KINAUZWA BAGAMOYO


 • Kiwanja kinauzwa, kiko Bagamoyo Ukuni jirani na standi kuu ya mabasi yaendayo mikoani, kina square meter 2,400, kinafaa kwa ujenzi wa shule, hoteli na aina nyingine ya uwekezaji. Kina hati, bei ni maelewano.
  Kwa maelezo zaidi piga simu: +255 657 803139

  0 0

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua kazi ya uwekaji viti vipya katika ukumbi wa Bunge mjini Dodoma Januari 18,2014 ikiwa ni maandalizi ya Bunge la Katiba linalotarajiwa kuanza mwezi ujao.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa ameketi kitini wakati akikagua marekebisho yanayofanyika katika ukumbi wa Bunge mjini Dodoma Januari 18, 2013 ikiwa ni maandalizi ya Bunge la Katiba linalotarajiwa kuanza mwezi ujao. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
  =======  ======  ========
  WAZIRI MKUU ARIDHISHWA NA UKARABATI JENGO LA BUNGE
  *Ni maandalizi ya Bunge la Katiba
  WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema ameridhishwa na kazi ya ukarabati inayoendelea kwenye maeneo mbalimbali ya jengo la Bunge ikiwa ni maandalizi kwa ajili ya Bunge la Katiba.
  “Maendeleo ni mazuri na kazi inayofanywa ni nzuri, kikubwa ni kuhakikisha mnaikamilisha hii kazi katika muda uliopangwa,” alisisitiza.
  Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo asubuhi (Jumamosi, Januari 18, 2014), wakati akipokea maelezo ya ukarabati kutoka kwa Mhandisi Mkuu wa Ofisi Bunge, Eng. Dk. Philemon Mzee ambaye alikuwa akimtembeza kwenye maeneo mbalimbali yanayofanyiwa ukarabati. Kwa mujibu wa Dk. Mzee, kazi hiyo inatarajiwa kukamilika Januari 30, mwaka huu.
  Ndani ya ukumbi wa Bunge, Waziri Mkuu alikuta viti vyote vya zamani vimekwishaondolewa na akaonyeshwa sehemu moja ya mfano iliyopangwa viti vinane kuashiria muonekano utakavyokuwa mara baada ya kazi hiyo kukamilika.
  Dk. Mzee alimweleza Waziri Mkuu kwamba wanatarajia kuweka viti 670 vya wajumbe wa kawaida pamoja na viti 24 kwa ajili ya wajumbe wenye mahitaji maalum. “Kule nyuma tutaweka viti vya kuzunguka ili hata kama mjumbe mmoja ana ulemavu wa miguu na amekuja na baiskeli yake aweze kutoka na kukaa kwenye kiti chake kwa urahisi,” alisema.
  Alimweleza Waziri Mkuu kwamba viti vya Spika na Makatibu wa Bunge vipo tayari, mfumo wa vipaza sauti uko sawa na kwamba kila kipaza sauti kimoja kitakuwa kinatumiwa na watu wawili kulingana na mpangilio wa ukaaji ulivyo.
  Alipoulizwa na Waziri Mkuu kuhusu sehemu ya kukaa waandishi wa habari, Eng. Mzee alisema sehemu zao zitaendelea kubaki zilivyo. Alipohoji endapo kutakuwa na kazi za Kamati, zitafanyikia wapi, Waziri Mkuu alijibiwa kwamba kuna kumbi tisa za kutosha watu 25-30 zinaandaliwa katika jengo la utawala Annex.
  Waziri Mkuu pia alikagua sehemu ya mgawaha kwa ajili ya wajumbe wa bunge hilo na kuonyeshwa sehemu ya basement ambayo alikuta inafanyiwa matengenezo ili iweze kuchukua watu 500 kwa wakati mmoja. Pia alikagua mgahawa wa zamani wa bungeni na kuelezwa kwamba utatumiwa na watumishi tu na hivi sasa unafanyiwa ukarabati ili uweze kutosha watu 120 kwa wakati mmoja.
  Waziri Mkuu alikagua pia chumba cha Hansard ambako alielezwa kuwa kimeongezwa ili kiweze kutosha watumishi 80 ikilinganishwa na watumishi 25 waliokuwepo zamani. Pia alikagua server room ambayo imehamishiwa eneo yalipokuwa matawi ya benki na zahanati.
  Alipouliza kuhusu eneo la kuegeshea magari, Waziri Mkuu alielezwa kwamba limetengwa eneo la kutosha magari 400 ambalo hivi sasa linafanyiwa maandalizi.
  Katika jengo la Utawala Annex, Waziri Mkuu alielezwa jengo hilo litakuwa na ofisi, vyumba vya mazoezi (gym), zahanati na ofisi za kutolea huduma za kibenki.
  Akitoa maelezo kuhusu kazi ya ukarabati inayoendelea, Kamishna Msaidizi wa Magereza ambaye ni msimamizi wa ujenzi wa jengo la Utawala Annex, Eng. Salum Omari alisema walianza kazi hiyo Januari 2, mwaka huu na wanatarajia kuikamilisha ifikapo Februari 2, mwaka huu.
  Alipoulizwa kama watamudu kuikamilisha kazi hiyo katika tarehe iliyopangwa, Eng. Omari alimhakikishia Waziri Mkuu kwamba wataikamilisha katika muda huo.
  Waziri Mkuu amerejea jijini Dar es Salaam mchana huu.
  (mwisho)
  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  DODOMA.
  JUMAMOSI, JANUARI 18, 2014

  0 0

  THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

  DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS  Telephone:255-22-2114512, 2116898

                press@ikulu.go.tz             

  Fax: 255-22-2113425


  PRESIDENT’S OFFICE,

        THE STATE HOUSE,

                P.O. BOX 9120,  

  DAR ES SALAAM.

  Tanzania.

   
  TAARIFA KWA UMMA
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumamosi, Januari 18, 2014,  amefanya uteuzi wa Makatibu Tawala wapya wa mikoa mitano na kuhamisha makatibu tawala wengine na Wakurugenzi wa Majiji nchini.


  Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi (KMK), Balozi Ombeni Sefue iliyotolewa jioni ya leo, Ikulu, Dar Es Salaam inasema kuwa uteuzi na uhamisho huo unaanza leo hii.


  Kwa mujibu wa taarifa hiyo,  Makatibu Tawala wapya ni Ndugu Wamoja A. Dickolangwa ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa ambako alikuwa Kaimu Katibu Tawala; Ndugu Abdallah D. Chikota ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi. Kabla ya hapo, alikuwa Mkurugenzi wa Halmashauri wa Wilaya ya Newala na Ndugu Symthies E. Pangisa ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa. Kabla ya uteuzi wake, Ndugu Pangisa alikuwa Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara.


  Wengine ni Ndugu Alfred C. Luanda ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara. Kabla ya uteuzi wake,  alikuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora na Ndugu Jackson L. Saitabau ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe. Kabla ya hapo, alikuwa Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Arusha.


  Taarifa hiyo iliwataja waliohamishwa kuwa ni Ndugu Beatha Swai aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani na sasa anahamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI; Ndugu Sipora J. Liana ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Jiji la Arusha anahamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI; Ndugu Benedict Ole Kuyan ambaye alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga anahamishiwa Mkoa wa Mara na Ndugu Salum M.Chima ambaye alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa anahamishiwa Mkoa wa Tanga.


  Wengine waliohamishwa ni Ndugu Mgeni Baruani ambaye alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe anahamishiwa Mkoa wa Pwani; Ndugu Juma R. Iddi ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya anahamishiwa Jiji la Arusha kama Mkurugenzi; Eng. Omari Chambo ambaye alikuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Uchukuzi anahamishiwa Mkoa wa Manyara kama Katibu Tawala wa Mkoa huo na Dkt. John Ndunguru aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi anahamishiwa Mkoa wa Kigoma kama Katibu Tawala wa Mkoa huo.


  Imetolewa na:

  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

  Ikulu,

  DAR ES SALAAM.


  18 Januari, 2014


  0 0

  Naitwa Cyril August Chami (PhD) Mbunge wa Jimbo la Moshi Vijijini na Mjumbe wa NEC-CCM kupitia Wilaya ya Moshi Vijijini.

  Nimesikitishwa na kufadhaishwa sana na mtu au watu waliotengeneza akaunti kwa jina langu kwenye  Mtandao wa Kijamii wa Facebook na kujifanya yeye au wao ndio mimi.

  Wamepachika hata picha zangu zinazopatikana kirahisi kwa sababu ya majukumu ambayo nimeshawahi kuwa nayo kama Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, na Waziri wa Viwanda na Biashara.

  Hilo lenyewe, yaani kutengeneza akaunti kwenye Facebook kwa jina la mtu na kuweka picha zake bila ridhaa yake, ni kosa la jinai.

  Lakini ubaya zaidi ni kwamba mtu huyo au watu hao wanawasiliana na wapiga kura wangu kule Moshi Vijijini na walio nje ya jimbo na kuwauliza kero zinazowakabili. Wanawajibu hao wananchi kana kwamba wao ndio mimi. Kwa vile wao sio mimi, majibu yao siyo sahihi. Lakini kwao hilo halina tatizo maana nia yao ni kunichafua.

  Wanaenda mbali zaidi na kukitukana Chama changu cha Mapinduzi wakionyesha kuwa mimi ni shabiki na/au sympathiser wa CHADEMA.  Wanatukana wanachama wenzangu wa CCM na kwa maana hiyo, viongozi wangu wa CCM.

  Naamini wanajua kuwa nia yao hii ni ovu lakini nawaomba watambue kuwa hawatafanikiwa katika malengo yao kwa sababu mtetezi wangu ni mkubwa kuliko nia hiyo yao.

  Siyo siri kuwa asilimia kubwa ya mawasiliano kwenye mitandao yanafanyika kwa anwani feki, hivyo wajue kuwa hata wasomaji wangenishangaa sana kama ningejiundia akaunti ya Facebook,  niweke picha zangu, halafu NIANZE KUWATUKANA VIONGOZI, WANACHAMA NA CHAMA CHANGU CHA MAPINDUZI.

  Ifahamike kuwa wakati wao wanawauliza wananchi wangu kero zao kwa Facebook wakiwa kwenye viyoyozi mimi nilikuwa naongea na wananchi hao ANA KWA ANA, siyo tu kuzijua kero zao bali kuzitatua.

  Kwa mfano, kuanzia December 20 hadi Januari 17 nimetembelea Kata za Uru Kusini, Uru Kaskazini, Mbokomu, Old Moshi Mashariki, Old Moshi Magharibi, Kimochi, Kibosho Kati, Okaoni, Kibosho Magharibi, Kibosho Mashariki,  Mwika Kaskazini na Mwika Kusini. Nimefika pia TPC kumuonyesha DED wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi sehemu ya kujenga daraja la Samanga litakalounganisha vijiji vya Mikocheni na Chemichemi kwa shs 250 millioni na pia tumetembelea Kata ya Uru Mashariki kukagua barabara inayoanzia Kishumundu Parish hadi Materuni, na ambayo tuko mbioni kui-grade kwa shs 700 milioni na harakati za kuipata hiyo fedha zinakwenda vizuri.

  Nimeshiriki fundraising ya kujenga ukumbi wa kisasa Mawella Parish Kata ya Uru Kusini, fundraising ya kujenga bwalo Mangi Meli Sekondari Kata ya Old Moshi Mashariki na fundraising ya kuvijengea uwezo vikundi 16 vya WEKEZA kata za Okaoni na Kibosho Kati. Kabla ya hapo nilishiriki fundraising ya kujenga jengo la utawala Uru Seminari katikati ya Novemba 2013.

  Ningekuwa mtumiaji wa Facebook  ningepost events hizi zote na hata kutaja kiasi tulichopata na kiasi cha michango yangu na rafiki zangu.

  Hilo sikufanya.

  Kwa nini?
  Ni kwa sababu asilimia 98 ya wananchi hawa niliowatembelea hawatumii Facebook, nalijua hilo, ndiyo maana nawatembelea kituo kwa kituo nikitambua nikiwasiliana nao kwa Facebook nitapata majibu kutoka kwa asilimia 2 ya wapiga kura, tena walio nje ya jimbo. Na katika kipindi chote hicho sikuweza kwenda kwenye mitandao kwa sababu nilikuwa vijijini kwenye ziara kama Katibu Mwenezi wa CCM Moshi Vijijini, Ndugu Hussein Jamal alivyopost siku chache zilizopita.

  Watambue kuwa rekodi yangu ndani ya Bunge, CCM na Serikali inafahamika kuwa mimi si mpayukaji, sina ushabiki na upinzani, na ni kati ya makada wanaoipenda CCM kwa vitendo zaidi kuliko maneno. Kwa maana hiyo wengi wa wasomaji waliosoma hayo wanayonipandikizia wameshaanza kutia shaka kama huyo ndiye Chami wanayemfahamu, na katika hili wako sahihi.

  Watambue pia kuwa kama nia yao ni kuniharibia ndani ya CCM na jamii wameshashindwa kwa sababu maneno ya kupandikiziwa kwa wiki moja hayawezi kuaminika zaidi ya rekodi yangu inayofahamika tangu Uru Seminari nilikokuwa Mwenyekiti wa UVCCM kwa miaka 3, Chuo Kikuu cha Dar nilikokuwa Rais wa Wanafunzi Kampasi ya Mlimani, Ikulu nilikokuwa msaidizi wa Rais masuala ya Uchumi, Mbunge, Naibu Waziri na Waziri.

  Bila shaka wote nilioishi nao katika maeneo haya na kwingineko watakiri kuwa mimi si mwepesi wa kujisifu, kupayuka na wala si mtu wa matusi kwa mtu binafsi, viongozi wa dini, wa Chama au wale wa Serikali.

  Wakati nawaonya waache siasa hizi chafu, nawatahadharisha pia kuwa za mwizi ni arobaini! Ipo siku mtu huyu au watu hawa wataumbuliwa na jamii.

  Dr Cyril August Chami.
  Mbunge wa Moshi Vijijini.


  0 0

   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na wanachama wa shina la wakereketwa la stendi ya Kangowe mara baada ya kulifungua shina hilo.
   
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akipiga ngoma ya asili ya watu wa Bagamoyo kabla ya kuanza kuhutubia wakazi wa kata ya Magomeni.

   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kata ya Magomeni wilaya ya Bagamoyo kwenye viwanja vya shule ya msingi Majengo na kuwataka wananchi wa kata hiyo kufanya maamuzi sahihi kwa wakati huu kwa kumchagua mgombea kutoka CCM kwani ndio chama pekee chenye ukomavu wa kisiasa.

   
   Wapenzi na Wanachama wa  Chama Cha Mapinduzi wakijumuika kucheza ngoma ya asili ya Bagamoyo.


   
   Mgombea wa Kiti cha Udiwani Kupitia CCM Mwanaharusi Hamis Jarufu akipiga magoti kwa wapiga kura wake kama ishara ya kuomba kura.
   Mgombea wa Kiti cha Udiwani kata ya Magomeni wilaya ya Bagamoyo kwa tiketi ya CCM Mwanaharusi Hamisi Jarufu akihutubia wakazi wa kata ya Magomeni wakati wa uzinduzi wa kmapeni za udiwani wa kata hiyo.

   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana na baadhi ya viongozi wa CCM wilaya ya Bagamoyo alipowasili kwa ajili ya ufunguzi wa kampeni za udiwani kata ya Magomeni.

  0 0


  Viongozi wakuu wa jumuiya za Watanzania Italy  katika picha ya pamoja baada ya kusimamia kuaga mwili wa Mtanzania marehemu MAULIDI HAMIDI ABDALLAH tayari kusafirishwa kupelekwa nyumbani Tanzania kwa mazishi. Kutoka kushoto ni Mh. Kagutta N.M (katibu mkuu wa Jumuiya ya Watanzania Italy) anaefuata ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Rome Mh. ERASMUS PINDU LUHOYA na anemfuata ni Mh ABDULRAHAMAN A.ALLI (mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Italy) na wa mwisho kulia ni Katibu  wa Jumuiya ya Watanzania Rome Mh. ENDREW  C.MHELA


   

  0 0

  Mabondia Robinson Msimbe kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Ayubu Ula wakati wa mpambano wao uliofanyika Kiluvya madukani katika ukumbi wa Shimbikati Ula alishinda kwa point mpambano.
  Msanii wa mziki wa radha Selemani Jabir 'Msagasumu' akitoa burudani katika ukumbi wa shimbikati kiluvya maduka mawili kabla ya mpambano wa masumbwi uliofanyika katika ukumbi huo jana
   MABONDIA WAKIONESHABA UBABE WAKATI WA MPAMBANO ULIOFANYIKA KLUVYA MADUKANI KATIKA UKUMBI WA SHIMBIKATI PICHA NA www.superdboxingcoach.blogspot.com
  Msanii wa mziki wa radha Selemani Jabir 'Msagasumu' akitoa burudani katika ukumbi wa shimbikati kiluvya maduka mawili kabla ya mpambano wa masumbwi uliofanyika katika ukumbi huo jana kulia ni mmoja ya nmashabiki wake
  MASHABIKI WAKIMSHANGILIA BONDIA WAO ALIYESHINDA.

  MPAMBANO WA MASUMBWI UKIENDELEA

  0 0   Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya sherehe za Maulid kwa

  wanawake wa mkoa wa Dar es salaam, kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume
  Muhammad (S.W.A), Aisha Sururu (wa pili kushoto), akifuatilia jambo
  katika sherehe hizo, zilizoshirikisha na wanawake kutoka mkoa wa Pwani.  Kikundi cha kaswida kutoka madrasa ya Al Itiswam, Sokota  
  Temeke Dar es Salaam, ikisherehesha katika sherehe hizo.
   Mtoa mada ihusuyo elimu ya kiislam na mwanamke, Atwiya Adam Ahmad,  akieleza ujumbe muhimu kuhusu kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W), na  umuhimu wa kuadhimisha siku hiyo.
  Kikundi cha kaswida kutoka madrasa ya Al Itiswam, Sokota  
  Temeke Dar es Salaam, ikisherehesha katika sherehe hizo.
  ========   =======  =======
  WANAWAKE nchini wametakiwa kujiamini sambamba na kuwalea watoto katika  maadili mema ili kuzuia mmomonyoko wa maadili ambao ni chanzo cha  uhalifu nchini.  Mwanaharakati wa Kiislam na diwani wa viti maalum kwa tiketi ya Chama
  cha Mapinduzi Ilala,Aisha Sururu aliyasema hayo jijini Dar es salaam
  wakati wa maadhimisho ya Maulid ya kuzalima Mtume, Muhammad(S.A.W),  yaliyoandaliwa na wanawake wa mkoa huo.  "Kinamama na jamii nzima ya Kiislam sote tunapaswa tuwe wakuzi wazuri
  wa watoto wetu ilu kuzuia mmomonyoko wa maadili" alisema.

  Alisema wao kama wanawake wameamua kusherehekea mazazi ya Mtume kwa  kuwa kabla ya kuzaliwa mtume wanawake walidhalilishwa sana, lakini kwa  kipindi chake wanawake walipewa nafasi kubwa.  "Zamani wanawake tulinyanyaswa na kudhalilishwa sana ila enzi ya Mtume
  Mohamad ndo tukapewa nafasi. Hivyo wanawanke tuko mbele toka enzi ya
  mtume" alisema.

  Aliwataka wanawake kujiamini kwamba wanaweza katika mikakati yoyote ya  maendeleo kwa kuwa wanatambulika tangu enzi za mtume.  Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa baraza hilo, Mayasa Sadala
  aliitaka jamii kufuata taratibu za mtume alizoziacha ikiwemo stara ili
  kuendelea kuidumisha amani na utulivu.

  0 0


   MTANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) umetoa vyeti kwa wasanii 1,000 waliofanya kazi zao vizuri katika kipindi cha mwaka 2013-2014 katika kongamano lililofanyika ukumbi wa Lamada, Ilala Dar es Salaam.

  Katika kongamano hilo lililohudhuriwa na wasanii,wanamichezo,wanahabari na vijana zaidi ya 1,500 mgeni rasmi Rais Jakaya Kikwete aliyewakilishwa na Naibu Waziri wa Habari, Vijana utamaduni na Michezo, Amos Makala aliwaasa wasanii watumie kipato chao kujiandaa kwa maisha ya baadaye baadaye.

  Makala aliwataka wasanii kujiunga na Shiwata na kujenga nyumba zao za pamoja kwa gharama nafuu katika kijiji cha Mwanzega, Mkuranga ambako mpaka sasa zimejenga nyumba 55 kati ya hizo 38 zimekabidhiwa wenyewe na nyingine zinaendelea kujengwa ambazo zitakabidhiwa wenyewe Machi mwaka huu.

  Katika risala ya Shiwata kwa mgeni rasmi iliyosomwa na Kanali Mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Juma Ikangaa ambaye pia aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Riadha Tanzania (TAA),SHIWATA imetoa ekari 5 kwa ajili ya Rais Kikwete ajenge  nyumba katika kijiji cha Mwanzega Mkuranga na ekari 5 nyinguine kwaq ajili ya kilimo katika kijiji cha Ngarambe, Mkuranga.

  Pia risala hiyo imemuomba Rais Kikwete asaidie kurudisha vituo vya burudani, viwanja vya michezo, na wapewe sehemu ya bustani ya mnazi Mmoja kwa ajili ya maonesho ya wazi, ujenzi wa makao makuu ya Mtandao na ununuzi wa vifaa vya kisasa kwa ajili ya kazi zao.

  Pia SHIWATA iliomba kuwepo mwakilishi wa wasanii katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na taasisi zote za Umma kama Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na Sheria yHaki Miliki iangaliwe upya kwani ina upungufu.

  Katika kongamano hilo SHIWATA imezindua Mpango wake wa umoja ambao utawasaidia wasanii kujitegemea wenyewe katika kazi mbalimbali badala ya kusubiri misaada kutoka kwa wafadhili kwa kutoa misaada kwa wasanii wachanga kurekoodi miziki yao,kurekodi filamu, na kupata michezo.

  Taarifa ya SHIWATA iliyotolewa na Mwenyekiti wake, Cassim Taalib alisema mpango huo utawafaidisha wasanii  kupata fedha za matibabu, mazishi pamoja na kununua na kusambaza kazi za wasanii.

  Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga mstaafu, Henry Clemence aliyetoa mada kuhusu maadili mema na juzalendo, aliwataka wasanii kuwa na tabia nzuri wanapokuwa ndani na nje ya nchi kwa mavazi ya heshima na mwenendo bora.

  Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa alisema athari za matumizi ya dawa za kulevya zinaiaibisha Tanzania inayofahamika kuwa kisima cha wananchi waadilifu kwa wanavyotumiwa wasanii na wanamichezo kusaifirisha na kutumia dawa za kulevya.

  Mgeni rasmi Naibu Waziri Makala aliyemwakilisha Rais Kikwete aliwaasa wanamichezo kutumia fedha wanazozipata katika kazi zao vizuri ili ziwasaidie wanapostaafu na wanapozeeka na kuwataka wajiunge  na SHIWATA ili wapate nyumba za gharama nafuu katika kijiji chao cha Mwanzega, Mkuranga.

  0 0

  Mzee Yusuf akiwadatisha mashabiki waliofurika Dar Live.
  Mzee Yusuf na wanenguaji wake kazini.
  Umati wa mashabiki ukiserebuka.
  Leila Mohamed akiwa kazini.
  Shabiki akiserebuka.
  Chidi Boy akikunguta kinanda.
  Pozi la kinadada ndani ya Dar Live.
  Mashabiki na raha zao.
  WAPENZI wa muziki usiku wa kuamkia leo waliburudika kwa mapigo ya bendi ya taarab ya Jahazi katika onyesho la nguvu la kwanza kwa mwaka 2014 ndani ya uwanja wa Taifa wa Burudani Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar. (PICHA ZOTE NA ISSA MNALLY/GPL)

  0 0

   Makamu Mkurugenzi Uzalishaji, Songas , Mhandisi Elias Mnunduma, akiwaeleza baadhi ya viongozi wa dini pichani, namna uzalishaji wa gesi katika mitambo ya kuzalisha gesi ya Songas katika kisiwa cha Songosongo unavyofanyika
   Baadhi ya viongozi wa dini katika picha ya pamoja na mtaalamu wa uzalishaji Songas Mhandisi Elias Mnunduma baada ya kupata maelezo namna shughuli nzima ya uzalishaji inavyofanyika katika mtambo huo ikiwemo pia masuala ya usalama wa wafanyakazi na wageni wanaotembelea mahali hapo.

   Mtaalamu wa Masuala ya Gesi  na Msimamizi Mkuu wa Mitambo ya Kusafisha Gesi kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Mhandisi Sulatan Pwaga, akiwaeleza viongozi wa dini kuhusu mradi wa eneo linapojengwa mitambo ya kusafisha gesi.

   Viongozi wa dini wakiwasili katika ofisi za kijiji cha Songosongo. Wakiwa ofisini hapo, viongozi hao walipata taarifa kuhusu namna kijiji kinavyofaidika kwa kuwepo wa uwekezaji wa gesi kijijini hapo, ambapo kijiji hicho kimefaidika kwa  umeme na maji bure.

  Pichani ni moto unaotoka wakati wote uzalishaji  wa gesi unapoondelea katika mitambo. Kwa mujibu wa wataalam wa mtambo huo, moto huo unaonesha kwamba gesi ipo inazalishwa na vilevile uwepo wake unaashiria usalama wa mitambo na watu wanaofanya shughuli katika mtambo huo.


  ========  ======= =======
  VIONGOZI WA DINI WAMALIZIA ZIARA YAO SONGOSONGO

  Na Asteria Muhozya, Songosongo, Kilwa.


  Viongozi wa dini wamemaliza ziara yao ya kutembelea shughuli mbalimbali katika sekta ya gesi na mafuta kwa kutembelea kisiwa cha Songosongo eneo la kwanza kuzalisha gesi asilia.


  Wakiwa kisiwani humo walifanikiwa kukutana na uongozi wa kijiji cha Songosongo ambapo walipata taarifa mbalimbali za namna mradi wa gesi ulivyokinufaisha kisiwa hicho ikiwemo pia mipango ya baadae ya kuendeleza eneo hilo.


  Akieleza kuhusu manufaa yaliyoyopatikana kisiwani humo kutakana na kuwepo uwekezaji wa gesi, mjumbe wa Kamati ya Ustawi wa Jamii Kijijini hapo Bibi Chiku Abdalah alieleza kuwa, mbali ya kupata umeme na maji bure, kijiji kimefaidika na huduma nyingine za jamii ikiwemo wanafunzi kupata msaada wa elimu pamoja na afya.


  “ Tunawashukuru Pan Afrika na Songas, wanatujali wanatusaidia elimu za watoto wanatupatia maji, tunashirikiana nao vizuri’,Alisema.

  Naye Mjumbe  kamati ya Mipango, Uchumi na fedha kijijini hapo Bw. Yussufu Faraki alieleza kuwa, tayari shule ya chekechekea imejengwa kijijini hapo na fursa za ajira kwa vijana zimepatikana.


  “Tunakwenda vizuri na Songas na Pan Afrika, wamekarabati shule, wametuwekea watu wa mahusiano, walituletea mkunga, wanalipa ada. Tunakubali changamoto zipo lakini kila mmoja anamhitaji mwenzake alisema Faraki.


  Akielezea kuhusu ziara hiyo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava alisema kuwa, wamefika kijijini hapo kuona shughuli za maendeleo zinazotokana na uwekezaji katika sekta ya gesi asilia na kujenga uelewa mpana kuhusu uwekezaji wa gesi na faida zake kwa maendeleo ya eneo la uwekezaji ikiwemo pia maendeleo ya Taifa kwa ujumla.


  Kwa upande wake Katibu wa Jumuiya ya Kikirsto Tanzania (CCT) na Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Kongamano la viongozi wa dini Bw. John Mapesa alisema kuwa, Elimu ya Songosongo imejulikana kwa viongozi wa dini na namna wananchi wa eneo hilo wanavyoizungumzia sekta  ya gesi na namna walivyonufaika nayo.


  “Tumepata elimu ya kufaa, tunapoelekea katika kongamano letu, tutajua namna  nzuri ya kuishauri Serikali na Wizara katika sekta hizi  kwa Maendeleo ya Taifa”. Alisema.


  Kwa upande wake Afisa Uhusiano wa Jamii wa  Kampuni ya Songas Bw. Nicodemus Chipakapaka alieleza kuwa, Songas mbali na uchimbaji imejikita katika kutoa huduma za jamii kupitia elimu, afya ambapo shirika hilo limekuwa likigharamia wanafunzi wanafaulu kuendelea na masomo ya sekondari kijijini hapo. Mbali na hayo alieleza kuwa, Songas wamefanikiwa kuboresha zahanati ya kijiji,  ikiwemo pia kuwezesha uwepo wa wahudumu wa afya wanaohudumia wananchi kijijini hapo.


  Akieleza namna shirika la Pan Africa linavyosaidia katika shughuli za maendeleo kijijini hapo , Afisa Maendeleo ya Jamii wa Shirika hilo Bibi. Tura David alieleza kuwa, pamoja na mambo mengine, kwa kuzingatia umuhimu wa elimu na namna utakavyowanufaisha wana Songosongo, Shirika hilo limeanzisha mpango wa kuwasaidia wanafunzi 10 kila mwaka wanafaulu vizuri zaidi na kuwaendeleza katika shule zilizopo nje ya Songosongo na nje ya Wilaya hiyo.


  “Tunaamini mpango huu utasaidia na kuwa mfano mzuri wa uwepo wa gesi mahala hapa. Tunataka kujenga kizazi kilichoelimika.” Wenzetu wa Songas wameanzia chini zaidi kwa kuwaangalia wote wanaofaulu, sisi tunataka kupata walio wanafunzi bora zaidi.” Alisema.


  Aidha, aliongeza kuwa, tayari Shirika hilo limejenga Bweni la wasichana kijijini hapo lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 55.


  Akielezea zaidi kuhusu mradi wa gesi na mahali panapojengwa mitambo ya gesi, Mtaalamu wa Masuala ya gesi na Msimamizi Mkuu wa Mitambo ya Kusafisha Gesi kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC)  Mhandisi Sultan Pwaga alieleza kuwa, mitambo mipya inayojengwa ya kuzalisha gesi kisiwani humo inatarajiwa kuzalisha futi za ujazo milioni 140 kwa siku,  uzalishaji wa umeme wa zaidi ya megawati 10 , ambapo pia kutakuwa na mtambo wa kukandamiza gesi,  na mtambo wa kusafisha maji ya wastani wa lita 60,000 kwa siku ambapo wananchi wa Songosongo wanatarajiwa kufaidika na huduma za maji hayo.


  Aidha, Makamu Mkurugenzi uzalishaji  Songas, Mhandisi Elias Mnunduma alieleza kuwa, kwa sasa eneo hilo la Songosongo linazalisha kiasi cha gesi cha futi za ujazo milioni 105 kwa siku ambapo asilimia 80 ya gesi inauzwa Tanesco kwa ajili ya kuzalisha umeme na asilimia 20 inapelekwa viwandani.

  0 0

  Mchezaji wa Timu za Dacico Pooltable, Yohana Mathius, akijaribu kulenga shimo wakati wa mchezo wa kirafiki dhidi ya Mlimani Profesional Pooltable katika hafla ya Sherehe za kuwakaribisha wanafunzi wapya wa Dar es Salaam City College na Mlimani Profesional(School Bush) iliyofanyika kwenye ukumbi wa Chuo cha Dar es Salaam City College Kibamba jijini Dar es Salaam Jana.
  Wanafunzi wa Chuo cha Uandishi wa Habari na Utawala Dar es Salaam City College, wakati wa wakati wa kutafuta washindi wa Urembo Miss & Mr. Dacico kwenye Hafla ya kuwakaribisha wanafunzi wapya wa Vyuo vya DACICO na Mlimani Profesional, iliyofanyika Makao makuu ya Chuo cha DACICO kibamba Chama jana na kushirikisha michezo mbali mbali ikiwamo Soka, Pooltable, kuimba, kucheza muziki, kuogelea, Urembo Mr. & Miss New Intake DACICO na mashindano ya kujibu Mada(Debate).
  Wachezaji wa Timu za Dacico Fc, kiungo Machejo Dula (nyekundu) na mlinzi wa timu ya Mlimani Profesional Fc. Masanga Mkama wakiwania mpira wakati wa mchezo wa kirafiki katika hafla ya Sherehe za kuwakaribisha wanafunzi wapya wa Dar es Salaam City College na Mlimani Profesional(School Bush) iliyofanyika kwenye Viwanja vya Kibamba Chama, jijini Dar es Salaam Jana. hadi mwisho wa mchezo Dacico iliibuka na ushindi wa bao 1-0. BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0older | 1 | .... | 204 | 205 | (Page 206) | 207 | 208 | .... | 1898 | newer