Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 203 | 204 | (Page 205) | 206 | 207 | .... | 1898 | newer

  0 0

   Rais Jakaya Kikwete, akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu, George Liundi wakati wa shughuli za kuagwa mwili huo zilizofanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif, wakitoa heshima za miwsho mbele ya Jeneza lenye mwili wa marehemu George Liundi, wakati wa shughuli za kuagwa mwili huo zilizofanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, leo. Kulia ni Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa, akielekea kutoa heshim za mwisho
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif, wakitoa heshima za miwsho mbele ya Jeneza lenye mwili wa marehemu George Liundi, wakati wa shughuli za kuagwa mwili huo zilizofanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, leo. Kulia ni Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa, akielekea kutoa heshim za mwisho
   Rais Jakaya Kikwete (wa pili kushoto) Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif, Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba mpya, Jaji Joseph Warioba, Makamu mwenyekiti wa CCM Bara, Philp Mangula na Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu na Bunge) William Lukuvi, wakishiriki Misa maalum ya kumuombea marehemu George Liundi, wakati wa shughuli za kuagwa mwili zilizofanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo
   Rais Jakaya Kikwete (wa pili kushoto) Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif, na Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu na Bunge) William Lukuvi (kushoto) wakijumuika na waombolezaji  katika misa maalum ya kumuombea marehemu George Liundi, wakati wa shughuli za kuagwa mwili zilizofanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
   Rais Jakaya Kikwete (wa pili kushoto) Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif, na Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu na Bunge) William Lukuvi (kushoto) wakitafakari msiba huo wakati wa shughuli za kuagwa mwili zilizofanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
   Sehemu ya wanafamilia wakishiriki shughuli hiyo. 

   Mjukuu wa marehemu, ambaye ni motto wa mtangazaji, Taji Liundi, akisoma wasifu wa marehemu. 
   Baadhi ya viongozi wakielekea kutoa heshima za mwisho.
  Rais Jakaya Kikwete, akiagana na Makamuwa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif, baada ya shughuli za kuagwa mwili wa marehemu Lindi, zilizofanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, leo
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Mmwenyekiti wa Chama cha CUF, Prof Ibrahim Lipumba, baada ya shughuli za kuagwa mwili wa marehemu Lindi, zilizofanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, leo. Picha na OMR

  0 0

  Rais wa Chama cha Wafanyabiashara,Wenyeviwanda na Kilimo (TCCIA) Injinia Peter Chisawillo akizindua rasmi utafiti utakaohusisha ukusanyaji wa maoni kupitia ujumbe mfupi wa simu (SMS Mobile System) kuhusu madhara yatokanayo na urejeshwaji wa ada za biashara kila mwaka kwa lengo la kuishawishi serikali kuweka sera, sheria na taratibu rafiki kwa mazingira ya ufanyaji biashara nchini leo jijini Dar es salaam.
  =======  ======  =========
  TCCIA YAZINDUA UTAFITI KUKUSANYA MAONI YA WAFANYABIASHARA KUHUSU ATHARI ZA UREJESHWAJI WA ADA YA LESENI ZA BIASHARA.

  Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
  16/5/2014, Dar es salaam.

  Chama cha Wafanyabiashara,Wenyeviwanda na Kilimo (TCCIA) kimezindua rasmi utafiti utakaohusisha ukusanyaji wa maoni kupitia ujumbe mfupi wa simu (SMS Mobile System) kuhusu madhara yatokanayo na urejeshwaji wa ada za biashara kila mwaka kwa lengo la kuishawishi serikali kuweka sera, sheria na taratibu rafiki kwa mazingira ya ufanyaji biashara nchini.

  Akizungumzia utafiti huo leo jijini Dar es salaam Rais wa cha hicho Injinia Peter Chisawillo amesema kuwa mwanzoni mwa mwaka wa fedha wa 2013/2014 serikali ilitangaza urejeshwaji wa ada ya leseni za biashara nchi nzima na kuongeza kuwa utaratibu huo unaomlazimu mfanyabiashara kukata leseni na kuilipia kila mwaka unakwenda kinyume na sheria ya leseni ya mwaka 1972.

  Amesema kuwa sheria hiyo na hasa marekebisho yake ya mwaka 2004  yaliwezesha leseni za biashara kutolewa bure na mara moja tu kwa kipindi cha maisha yote ya biashara jambo ambalo linakiukwa.

  “Tayari kuna malalamiko mengi kwa jumuiya ya wafanyabiashara yanayotufikia kutoka kuanzia ngazi za wilaya na mikoa juu ya urejeshwaji wa ada hiyo, sekta binafsi inailalamikia serikali kwa kutoishirikisha katika urejeshaji wa utaratibu huu ambao unaiathiri sekta hii moja kwa moja” amesema Injinia Chisawillo.

  Ameeleza kuwa sekta binafsi inaamini kuwa serikali imeamua kuongeza mapato bila kuzingatia nia ya urasimishaji wa sekta isiyo rasmi kwa lengo la kuharakisha uchumi kwa ujumla na kuongeza kuwa hakuna mwongozo maalum uliotolewa na serikali kuelekeza namna maombi ya leseni yatakavyoshughulikiwa.

  Amesema sekta binafsi inaamini kuwa ili kuondoa urasimu na usumbufu kwa wafanyabiashara pindi wanapoomba leseni kila mwaka , serikali itumie kumbukumbu zilezile kila mwaka bila kulazimu mfanyabiashara  kufuata mlolongo wa taratibu za kuomba leseni kila mwaka kwa lengo la kuokoa muda na kupunguza kupanda kwa gharama za uendeshaji wa biashara.

  Aidha Injinia Chisawillo amesema kuwa utafiti huo unaofanywa na TCCIA) utafanyika kwa muda wa wiki 4 ukiwahusisha wanachama wote  takribani 22,000 (Elfu Ishirini na mbili) na wale wasio wanachama na unafadhiriwa na Shirika lisilokuwa la kiserikali la BEST –AC ili kuwawezesha wafanyabiashara hao kutuma ujumbe mfupi wa maneno kupitia simu zao kwenda namba 15539  na kutoa maoni kuhusu urejeshwaji wa ada hiyo

  0 0

  Tungependa kukukaribisha kwenye huduma yetu ya Usafiri jijini kwa kutumia mabasi maalumu kwa sababu kuu tatu au zaidi.

  1. Tunaamini wafanyakazi wanaotumia muda mrefu njiani kwa kutafuta usafiri, au kwa kukwama kwenye foleni wakati wakielekea makazini, huwa wanafika wamechoka tayari na hivyo kupelekea kuwa na umakini wa kiwango cha chini pamoja na kupunguza uzalishaji.

  2. Kukaa kwenye foleni kwa muda mrefu wakati ukiendesha gari, inaaminika kuwa ni mazingira yanayosababisha kiwango cha juu sana cha msongo, na ni sababu ya watu wengi kutokuwa na furaha kwa muda mwingi wawapo makazini.

  3.Gharama za kuendesha gari kwa siku moja kwenye jiji la Dar es Salaam, kwenda kazini na kurudi zinakisiwa kuwa zaidi ya Tsh. 30,000/= kwa gari ya kawaida yenye viti vitano. Hii inamaana kuwa kwa kila kiti kimoja cha gari lako, kinakugharimu Tsh. 6000/=. Endapo unatumia kiti kimoja tu cha gari lako, inamaanisha unapoteza Tsh. 24,000/= kwa kila siku unapotumia gari lako kwenda kazini, kwa siku 20 za kazi ni sawa na Tsh. 480,000/= na ni zaidi ya Tsh. 5,760,000/= kwa mwaka zinazopotea kwa wewe kuendelea kutumia gari lako binafsi kwenda kazini na kurudi.

  Kampuni ya City Ridez Travels & Tours ingependa kukuletea suluhisho la matatizo haya kwa ujumla wake. Lengo letu ni kupunguza idadi ya magari binafsi yanayotembea muda wa kwenda na kurudi kazini kwa kukuletea usafiri maalumu, wenye starehe, wakutegemewa na kwa gharama nafuu.

  Hapa City Ridez Travels & Tours tunahusika na usafiri maalumu wa mabasi, kwa minajili ya kutoa njia mbadala ya kusafiri ukiwa ndani jiji. Kimsingi tukizingatia zaidi kwenye Ubora, Uaminifu na Usalama.

  Njia tunazotoa Huduma kwa sasa.

  TEGETA - POSTA - TEGETA (kupitia MWENGE)
  GONGO LA MBOTO - POSTA - GONGO LA MBOTO
  MBEZI KIMARA - POSTA - MBEZI KIMARA
  MBEZI AFRICANA - POSTA - MBEZI AFRICANA  (kupitia Mbezi chini)
  MBAGALA - POSTA - MBAGALA
  TABATA SEGEREA - POSTA - TABATA SEGEREA
  MWENGE - POSTA - MWENGE (kupitia Sinza)
  Usafiri wa raha mustarehe.

  Njia zinazotazamiwa baadae
  MBAGALA KIJICHI - POSTA - MBAGALA KIJICHI
  KUNDUCHI - POSTA - KUNDUCHI

  Njia nyingine zitaongezwa kwa kuzingatia upatikanaji wa wateja na mahitaji

  Gharama / Bei
  Bei zetu zinatazamiwa kuwa ni bei nafuu kwa kua kila mtu analipa kwa kile anachotumia peke yake. Tiketi zetu zinapatikana kwa Tsh. 5500/= kwenda na kurudi kwa siku kwa njia fupi, na Tsh. 11000/= kwenda na kurudi kwa njia ndefu. Pia unaweza kujipatia tiketi za kwenda peke yake au kurudi kwa Tsh. 3300/=. Na kwa wale ambao wangependa kujipatia tiketi za wiki nzima (yaani siku 5) au mwezi mzima (yaani siku 20) tiketi hizi zina unafuu wa aslimia 10%. Tiketi zinapatikana kwa mawakala wetu au kwa kutumia simu yako ya mkononi. Au piga simu +255 715 400 666.

  Tiketi hizi zinamaanisha kuwa tutakuchukua kutoka karibu na nyumbani kwako kukuleta mjini asubuhi na kukurudisha jioni, na kama unakaa mbali na barabara kuu, tutakupatia sehemu salama ya kuegesha gari lako bila wasiwasi.

  Muda.
  Tunahakikisha unakua mjini kila siku asubuhi kabla ya mida ya saa 1:00 asubuhi, hivyo basi tutakua tukiondoka maeneo tofauti jijini kwa muda tofauti kulingana na umbali na miundo mbinu ya eneo husika, (kuanzia mida ya 11:00 asubuhi na 12:30 asubuhi) vilevile tunatoa safari ya 7:30 asubuhi kwa wale wanaopenda kuchelewa kuingia mjini. 

  Kwa jioni magari yanaondoka kuanzia saa 11:00 jioni na 11:30, vile vile kuna magari ya 1:30 usiku kwa wale wanaochelewa au wafanyakazi wa mabenki. (Unaweza kuwasiliana na mtoa huduma wetu ili kuangalia upatikanaji wa safari kuendana na mahitaji yako. +255 715 400 666)

  Tiketi
  Tunatoa aina mpya ya tiketi zinazowekwa QR codes kwa ajili ya usalama, na unaweza kuzipata kwa mawakala wetu, au kwa kununua mwenyewe kupitia namba yetu ya simu +255 687 644452 na utatumiwa tiketi yako kwenye simu yako ya mkononi, au barua pepe au hata kupitia mitandao ya kijamii baada ya kukamilisha malipo, na utatakiwa kuonyesha tu QR codes uliyotumiwa kwa ajili ya uthibitisho. Ni rahisi kiasi hicho. 

  Kumbuka hautaweza kulipia ukiwa ndani ya gari, na kuna idadi maalumu ya wateja watakaohudumiwa kwa siku, hivyo ni muhimu kama utaweka siti yako mapema kuepuka usumbufu.

  Kwa maelezo zaidi unaweza kutembelea ofisi zetu zilizoko kwenye jengo la NSSF Hifadhi house gorofa ya Saba, karibu na mnara wa askari, au ukapiga simu namba. +255 222 114 308 Mobile: +255 712 823 505 au barua pepe: cityridezsales@gmail.com, au tembelea kuras wetu wa facebook:www.facebook.com/cityridez

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Winch Energy Tanzania akiwasilisha mada mbele ya Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo (aliyekaa upande wa kulia) kwenye ukumbi ulioko kwenye ofisi  za Wizara ya Nishati na Madini. Lengo la kikao hicho lilikuwa ni kampuni ya Winch Energy Tanzania kutambulisha majukumu yake ikiwa ni pamoja na kusambaza umeme wa nishati ya jua.
  Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter  Muhongo akisisitiza jambo katika kikao hicho.


  0 0

  ZIFF INAKARIBISHA FILAMU ZA WATANZANIA
  Tamasha la filamu la Nchi za Jahazi - ZIFF linatangaza kuwa tarehe za kufunga kupokea filamu zitazoshindana katika kinyanganyiro cha ZIFF2014 ni tarehe 31 January, 2014, hii ikiwemo pia filamu za Kiswahili (Bongo Movies)
  Mashindano yamo katika nyanja tofauti pamoja na:
  1. Filamu Bora ya Tamasha (Golden Dhow)
  2. Filamu ya pili kwa ubora (Silver Dhow)
  3. Documentary Bora (Golden Dhow)
  4. Documentary ya Pili kwa ubora (Silver Dhow)
  5. Filamu Fupi Bora (East Africa Talent Award)
  6. SIGNIS Award (Best documentary)
  7. Verona Award (Best African Feature film)
  8. Sembene Ousmane Award (Best Development film $5000)
  ZUKU Awards
  1. Best Swahili Film (Tsh 1 mil)
  2. Best Swahili Film Actor (Tsh 500,000)
  3. Best Swahili Film Actress(Tsh 500,000)
  4. Best Camera
  5. Best Sound
  Haya shime tujitowe kimasomaso mwaka huu watanzania turudishe heshima yetu afrika mashariki.
  Tanzania ilikuwa nchi ya kwanza kuwa na filamu iliyoshinda kimataifa:
  FESPACO  - Arusi ya Mariamu, 1985- (Tuzo 12 kimataifa)

  Ikashinda tena FESPACO - Mama Tumaini (1987) Tuzo ya Unicef)
  Kenya na Uganda wakati huo bado wamelala!!
  ZIFF 2014 -Tarehe 14-22 June- ZANZIBAR.

  Tembelea www.ziff.or.tz kwa maelezo zaidi.

  0 0

  Former President of Zanzibar Dr Abeid Amani Karume with First Vice President of Zanzibar His Exellency Maalim Seif Sharif Hamad, jointly launched the book celebrating  50 years of Revolution in Peace Memorial Museum in Zanzibar.

  The launch was followed by exhibition in the Peace Memorial Museum with over  over 100 pictures and the historic exhibition will be  open for school children of  Zanzibar, free of charge.

  Javed  Jafferji who is mastermind  and creator of this book and  exhibition said  "I am very happy to have this historic launch in Peace Memorial  Museuem , I am so happy to get support from Honourable Abeid Amani Karume and Maalim Seif Sharif Hamad to participate in this book by contributing for forword and introduction. The book took almost one year to design, publish and print, this is the best book which I have published in last 20 years."

  Javed is acclaimed photographer and has published almost 60 books on Tanzania. He was awarded as one of Africa’s Top 100 people as well by www.africaalmanac.com some time ago. This was for his efforts to promote Africa and his contribution by promoting Tanzania over the span of his career.

  He is also a film maker and has produced a number of films promoting the islands of Zanzibar along with other acclaimed documentaries and feature film Glamour: The Reality Behind Dreams which was shown in last year’s film festival alongside a documentary on First Vice President on Zanzibar, Journey to the State House: The Life of Seif Shariff Hamad. He is also the producer for a number of other feature films from the island including: Black Magic, Lovers Island , Room No 13 and Zamora. Many of his films has won international and national awards.  0 0

  Mbunge wa Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa  (kushoto) akimnadi mgombea udiwani wa kata ya Nduli Ayub Mwemba  leo wakati wa uzinduzi wa kampeni kwa Chadema

  Mgombea udiwani wa kata ya Nduli Ayub Mwemba  akihutubia leo (jana) wakati wa uzinduzi wa kampeni kwa Chadema
  Mbunge wa Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa  (kushoto) akiendelea kumnadi mgombea udiwani wa kata ya Nduli Ayub Mwemba  leo wakati wa uzinduzi wa kampeni kwa Chadema.  Kwa picha na habari kamili BOFYA HAPA

  0 0

  Wananchi katika manispaa ya Iringa wametakiwa kuweka mazingira katika hali ya usafi kwa kipindi hiki cha msimu wa mvua, ili kuweza kuepuka magonjwa mbalimbali ya mlipuko.


  Hayo yamesemwa na Afisa afya wa manispaa ya Iringa, MERCY KINENEKEJU ,na kusema kuwa wananchi wanatakiwa kufanya usafi nje ya makazi yao na kutupa taka sehemu husika.


  KINENEKEJU ameongeza kuwa kutokana na changamoto waliyonayo ya magari ya kubebea taka, wanafanya jitihada za kupata magari kupitia mradi wa Word  Bank ifikapo FebruarI mwaka huu watapata msaada wa gari moja ili kupunguza mlundikano wa taka katika baadhi ya maeneo.


  Wakati huohuo ameviomba vyombo vya habari kuzidi kutoa elimu kwa wananchi juu ya usafi wa mazingira ili kuweka manispaa katika hali ya usafi.


  WAKAZI WA IRINGA WAOMBWA KUWACHUKIA VIBAKA NA KUWAFICHUA KUSHIRIKIANA NA JESHI LA POLISI MKOANI HUMO.

    
  Wananchi mkoani Iringa wameombwa kuwachukia vibaka na kuwafichua kwa kushirikiana na jeshi la polisi kulinda usalama wa mkoa kwa kuwadhibiti na kuwamaliza .


  Hayo yamesemwa na kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Iringa, RAMADHAN MUNGI  na kusema kuwa vibaka hao wanafahamika na endapo wananchi watawafichua watasaidia kuwadhibiti na kuwafanya wafanyabiashara na wananchi kuishi kwa usalama.


  Kamanda amesema kuwa jeshi la polisi linaupungufu wa polisi na maeneo mengi yanavibaka, hivyo linahitaji msaada wa wananchi katika kutenda kazi kwani bila ushirikiano wao hawataweza kuwadhibiti.


  Hata hivyo amesema kuwa kwa ushirikiano huo kutasaidia kuweka mikakati ya kuzuia uhalifu katika mkoa ,kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia kutunza amani ya nchi yetu.


  Aidha ameongeza kwa kusema kuwa hali ya usalama katika mkoa wa iringa ni nzuri kwa sasa na uhalifu unazidi kupungua huku akisisitiza ushirikiano ili kulinda usalama.


  KATIBU WA CCM ALIPONGEZA JESHI LA POLISI.

  Katibu wa CCM mkoa, Menga Hassani amelipongeza jeshi la polis mkoa wa iringa kwa kufanya kazi yake kwa ufasaha.


  Hayo yameyasema na mwenyekiti huyo baada ya jeshi la polisi kuwakamata baadhi ya viongozi wa chama hicho kwa kuzidisha muda wakati wa mikutano .


  Wakati huohuo amevitaka vyama vya kisiasa vinavyofanya mikutano kutii sheria zilizowekwa na serikali ikiwa na kufuata muda ambao umepangwa.


  Hata hivyo kuhusiana na tukio hilo kutokea amesema ni tatizo la kupishana kwa muda baina ya viongozi wa chama na jeshi la polisi.
  0 0

    Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mohamedraza Hassan Dharamsi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu maendeleo ya Jimbo lake tokea alipochaguliwa kuwa mwakilishi Mwezi Februari mwaka 2012 katika Hoteli ya Grand Palace Malindi Mjini Zanzibar, kushoto  Afisa mwandamizi wa Idara ya Habari maelezo Zanzibar Ramadhan Ali. 
    Waandishi wa habari kutoka vyombo mbali mbali wakimsikiliza Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mohamedraza Hassan Dharamsi (hayupo pichani) katika Hoteli ya Grand Palace Malindi alipokuwa akieleza  mafanikio aliyopata tokea aliposhinda uchaguzi wa Jimbo lake mwaka 2012.
    Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Muhamedraza Hassan Dharamsi akiwaonyesha waandishi wa habari masuala aliyoyapa kipaumbele katika uongozi wake ndani ya  Jimbo hilo ikiwemo elimu katika mkutano uliofanyika Hoteli ya Grand Palace Malindi Mjini Zanzibar.

  Mwandishi wa Habari wa Idara ya Habari Maelezo Salum Vuai akimuuliza swali mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mohamedraza Hassan Dharamsi katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika Hoteli ya Grand Palace Malindi Mjini Zanzibar.

   
  ========  ========   =========
  NA RAMADHANI ALI/MAELEZO ZANZIBAR 
                                  
  Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mohamedraza Hassan Dharamsi amemuomba Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK. Ali Muhammed Shein kuanzisha utaratibu wa kuwafanyia tathmini viongozi wa majimbo juu ya utekelezaji wa majukumu yao kama anavyofanya kwa viongozi wa Taasisi za Serikali ili kufahamu utekelezaji wa majukumu yao kwa wananchi.

  Mohamedraza amesema uamuzi wa Dk. Shein kuwaita watendaji wa Taasisi za Serikali na Mashirika ya Umma  kila robo ya mwaka (bango kitita) umesaidia sana kuamsha ari ya viongozi kutekelezaji  wajibu wao kwa taifa.

   Ushauri huo ameutoa  leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari katika Hoteli ya Grand Palace Malindi kuelezezea mafanikio yaliyofikiwa na jimbo la Uzini  tokea aliposhinda uchanguzi mdogo wa Jimbo hilo mwaka 2012.

  Amesema wakati wagombea katika nafasi mbali mbali wanapoomba kura kutoka kwa wananchi hutoa ahadi nyingi ambazo watazitekeleza iwapo watashinda lakini baada ya kuopata ushindi viongozi hao huwadharau wapiga kura zao.

  “Mh. Rais naomba suala la Bango kitita lisiishie kwa viongozi wa Serikali pekee na sasa lipelekwe kwa viongozi wa majimbo kuwapima utekelezaji  wa ahadi walizozitoa kwa wananchi,” alisisitiza Mwakilishi huyo. Amesema iwapo viongozi wataweza kutekeleza ahadi wanazotoa kwa wananchi wao hakuna sababu ya kutoleta maendeleo katika majimbo jambo ambalo litawafanya wananchi kuwa na ari, upendo na kuwa karibu na viongozi wao.

  Ameahidi kuwa ataendelea kuwatumikia wananchi wa Uzini kwa hali na mali katika kufanikisha  ilani ya CCM na tayari ametekeleza ahadi zake  kwa asilimia mia moja licha ya changamoto nyingi anazokabiliana nazo.
  Ameongeza kuwa matatizo mengi yaliyokuwa yakilikabili Jimbo hilo ikiwemo miundo mbinu ya barabara, maji safi na salama na mitaji kwa wafanyabiashara ndogo ndogo limepungua.

  “Kazi kubwa iliyopo mbele yangu kwa sasa nikishirikiana na viongozi wengine wa Jimbo ni kupunguza  wimbi kubwa la vijana wanaoshindwa kuendelea na masomo  kutokana na umaskini wa wazazi wao kwa kuwapeleka katika vituo vya mafunzo ya amali kwa gharama zangu” aliahidi Mohamedraza.

   Hata hivyo  ameomba mashirikiano zaidi katika kupunguza tatizo la umaskini na kuwaletea wananchi maendeleo bila ya kujali itikadi za kisiasa na kuwashauri viongozi kuacha malumbano ambayo hayasaidii kuwakwamua wananchi.

   Akizungumzia rasimu ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyowasilishwa hivi karibuni, Muhamedraza amesema ataendelea kuunga mkono msimamo wa Chama cha Mapinduzi  wa Serikali mbili lakini zenye hadhi sawa kwani zilizoungana ni nchi mbili zilizokuwa na mamlaka kamili kabla ya kuungana.

  Muhamedraza Hassan Dharamsi lishinda uchaguzi mdogo wa Jimbo la Uzini baada ya kufariki aliekuwa Mwakilishi  wa Jimbo hilo Maalim Mussa Khamis Silima kutokana na ajali ya gari Mkoani Dododma mwishoni mwa mwaka 2011.

  Wakati wa kampeni zake kwa wananchi mwakilishi huyo aliahdi kutumia mshahara wake  na maposho mengine atakayopata  katika kupeleka maendeleo ndani ya  Jimbo la Uzini. 

                                                             IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.

  0 0

  ZIARA ya Rais wa TFF Jamal malinzi hatimaye imemelizika leo hapa jijini Mwanza kwa matukio mawili makubwa kufanyika.

  Tukio la Kwanza limefanyika majira ya saa 2:30 katika ofisi za Halmashauri ya jiji la Mwanza ambapo Shirikisho hilo limesaini mkataba kati yake na Halmashauri hiyo kwaajili ya kuboresha uwanja wa Nyamagana.

  Ili ipate kumwaga fedha zake za msaada kiasi cha dola laki 5 ambapo nyingine dola laki 1 zitatoka Halmashauri ya jiji la Mwanza, FIFA  ilikuwa ikitaka uthibitisho toka TFF kuwa uwanja huo kwa miaka yote utatumika kwa matumizi ya michezo yaani soka na si vinginevyo  kwaajili ya kuanza uboreshaji wa uwanja huo uliokuwa na utata wa kutaka kubadilishwa matumizi.

  Tukio la pili Malinzi na timu yake ya wataalamu toka TFF, majira ya saa 4 asubuhi imetembelea na kukikagua kituo cha elimu na soka cha Alliance Academy ikiwa ni mwanzo wa mpango wa kitaifa wa kuwekeza katika soka la vijana. BOFYA PLAY KUSIKILIZA TAARIFA KAMILI.

  Rais wa TFF Jamal Malinzi (katikati mwenye miwani) akiwa ameongozana na Mkurugenzi wa kituo cha Elimu na Ukuzaji vipaji vya michezo cha Alliance Academy James Bwire (kulia) akikagua mabweni ya wavulana ya kituo.
  Rais wa TFF Jamal Malinzi (wa pili kutoka kushoto) akiwa na Mwenyekiti wa Chama Cha soka mkoa wa Mwanza (MZFA) Jackson Songora (wa kwanza kushoto), mkurugenzi wa kituo hicho James Bwire (wa tatu kutoka kushoto) pamoja na mwakilishi wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa kitengo cha michezo (kushoto) wakifurahia jambo ndani ya moja kati ya mabweni ya wavulana Alliance Academy.
  Msafara wa rais huyo pia uliambatana na wawakilishi wa vyombo mbalimbali vya habari.
  Vijana wetu hulala hapa.
  Bweni vyumba baada ya vyumba.
  Tofauti na eneo la kukaa watazamaji kwa kila kiwanja, katika eneo hili vimeunganika viwanja viwili vyenye ukubwa wa mita 100 kila kimoja (nazungumzia maeneo ya kuchezea) na kingine kilichopo eneo la mabweni ya wasichana, ambapo TFF kupitia rais wake Jamal Malinzi imeahidi kuvikarabati viwanja hivi kwa kuvisawazisha kwa greda, kuviwekea magoli ya kisasa, kuweka udongo wenye rutuba na kuviwekea nyasi za kupanda zenye kiwango.


  Shule ya Alliance Academy imeongeza eneo hili lenye ukubwa wa hekta takribani 600 ambapo kunajengwa vyumba vya madarasa, ukumbi wa mikutano na ofisi kwa walimu.
  Ujenzi ukiendelea ukumbi wa mikutano.
  Majadiliano.
  Hili ni eneo jingine na majengo haya ni mabweni ya wasichana Shule ya Secondary Alliance Academy Mwanza.
  Msafara umefika hapa katika kiwanja cha soka wasichana ambapo ni moja kati ya viwanja vitakavyo kutana na mpango wa maboresho wa TFF utakao anza haraka wiki chache zijazo.
  Rais wa TFF Jamal Malinzi (kulia) hapa alikutana na Mwakilishi wa vilabu mkoa wa Mwanza ambaye pia ni mwenyekiti wa Halmashauri ya Kariuwa ya mkoani Tabora, John Kadutu (kushoto) ambapo walikumbushana mambo mawili matatu na kufurahi kwa pamoja.
  Jamal Malinzi alipata fursa ya kuzungumza na wachezaji na wanafunzi vijana wanaochukua masomo ya usimamizi na uamuzi wa michezo (marefa), kikubwa sanjari na kuzingatia michezo pia alisisitiza kuiweka elimu mbele. 
  Jiografia kuelekea ofisi kuu za kituo.
  Katibu mkuu wa Alliance School Sports Academy (ASSA) Bi. Mariam D. Lima akisoma risala mbele ya rais wa TFF Jamal Malinzi na wajumbe wake walio hudhuria ziara ya rais huyo shuleni hapo.
  Moja kati ya Madhumuni ya kuanzishwa kwa kituo hiki ni pamoja na:-
  1. Kujenga, kuimarisha, kuelimisha na kukuza vipaji vya vijana wa kike na wakiume katika michezo mbalimbali na kukuza michezo hiyo kwa manufaa yao na watanzania kwa ujumla.

  2. Kuanzisha, kuendesha na kuendeleza vituo vya michezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na semina na makongamano kwa vijana hapa nchini Tanzania.

  3. Kuandaa mashindano mbalimbali ya ndani na nje ya nchi kwa kufuata taratibu zilizowekwa.

  4. Kuwajengea vijana uwezo wa kujiamini kwa kuwapa maandalizi bora kimichezo na kitaaluma katika kufikia lengo lililokusudiwa.

  LENGO KUU / MAHUSUSI
  Kuhakikisha kuwa kituo kinakuwa bora na mfano wa kuigwa Afrika.
  Katibu mkuu wa Alliance School Sports Academy (ASSA) Bi. Mariam D. Lima akimkabidhi risala rais wa TFF Jamal Malinzi mbele ya wadau waliohudhuria ziara ya rais huyo shuleni hapo.
  Rais wa TFF Jamal Malinzi akimkabidhi mpira Captain wa Mwanza Starehe Club ambaye pia ni mwenyekiti wa uwanja wa CCM Kirumba John Tegete.
  Pia Rais wa TFF Jamal Malinzi alikabidhi mipira 10 kwa Katibu mkuu wa Alliance School Sports Academy (ASSA) Bi. Mariam D. Lima kwaajili ya matumizi ya kituo.
  Picha ya pamoja.

  0 0


  IMG_0030Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na wanakijiji wa  Mtanzania Januari 16, 2013 wakati alipokwenda kuwapa pole  kufuatia uvamizi waliofanyiwa  na watu wanaosadikiwa kuwa wafugaji ambao waliua watu watatu  na kuchoma nyumba . Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Erasto Mbwilo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)IMG_0042Baadhi ya wananchi wa Kiteto  wakimsikiliza  Waziri Mkuu , Mizengo Pinda wakati alipowahutubia  Januari 16, 2014 katika mji wa Kibaya alipokwenda kuwapa pole wakulima wa wilaya hiyo  ambao walishambuliwa, kuuwawa na nyumba zao kuchomwa moto na  watu wanaosadikiwa kuwa  ni wafugaji. IMG_0050Baadhi ya wananchi wa Kiteto  wakimsikiliza  Waziri Mkuu , Mizengo Pinda wakati alipowahutubia  Januari 16, 2014 katika mji wa Kibaya alipokwenda kuwapa pole wakulima wa wilaya hiyo  ambao walishambuliwa, kuuwawa na nyumba zao kuchomwa moto na  watu wanaosadikiwa kuwa  ni wafugaji. 

  IMG_0017Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na viongozi wa wilaya ya Kiteto baada ya kuwasili wilayani humo  Januari 16, 2014  kufuatilia suala la mauaji ya wakulima. IMG_0021Eneo la Mtanzania  wilayani Kiteto  ambalo ni moja kati ya maeneo ya  makazi  yaliyovamiwa na watu wanaodaiwa kuwa wafugaji  ambapo watu watatu waliuawa na nyumba kuchomwa moto. Mlheshimiwa Waziri Mkuu, Mizengo  Pinda alitembelea eneo hilo Januari  16, 2014. 
  IMG_0059Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiagana na wazee  wa Kiteto wakati alipoteta nao baada ya kuhutubia  mkutano wa hadhara katika mji mdogo wa Kibaya Janauari 16, 2014. Alikwenda Kiteto kuwapa pole wakulima  ambao walishambuliwa na watu wanaosadikiwa kuwa ni wafugaji ambao waliua na  kuchoma moto nyumba. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara amemteua Mheshimiwa Pindi Chana kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Filamu na Michezo ya kuigiza katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.
  Uteuzi huu unatokana na Mamlaka aliyopewa Waziri huyo chini ya kifungu cha 13(i) cha Sheria ya Filamu na Michezo ya kuigiza Na.4. ya mwaka 1976.
  Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara hiyo kwa Vyombo vya habari uteuzi wa Mwenyekiti na Wajumbe wengine wa Bodi umeanza tarehe 3 Desemba 2013.
  Aidha Waziri huyo amewateua Wakili wa Kujitegemea Silvester Sengerema ,Dr. Vicensia Shule kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam  na Bishop Hiluka kutoka Shirikisho la Filamu Tanzania kuwa wajumbe wa Bodi hiyo katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.
  Wajumbe wengine ni Jacob Sarungi kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali , Ntobi Fredrick kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, na Joyce Fissoo ambaye ni Katibu wa Bodi ya Filamu.
  IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI (MAELEZO)

  0 0

  The Glasgow 2014 Commonwealth Games, British High Commission, Tanzania Olympic Committee and UNICEF Team up to Stop Violence Against Children in Tanzania


  Dar es Salaam, United Republic of Tanzania, 17 January 2014 - The Glasgow 2014 Commonwealth Games Queen’s Baton will arrive in Dar es Salaam on Saturday, 18 January. The actual run is planned for Sunday, 19 January, and will kick off from the National Stadium at 2.00 pmto State House where it will be presented to H.E. President Jakaya Kikwete. It is expected that over 300 people will be involved in the 12.4 km race.


  Tanzania Olympic Committee’s Secretary General, Filbert Bayi, the British High Commissioner to Tanzania, Dianna Patricia Melrose, and the UNICEF Tanzania Representative, Dr. Jama Gulaid, will kick off the Relay, and be amongst the guests at State House.

  This year, the Glasgow 2014 Commonwealth Games, the Commonwealth Games Federation and UNICEF have launched a ground-breaking partnership globally. In Tanzania, the event represents a unique opportunity for the Tanzania Olympic Committee, the British High Commission, UNICEF and other partners to harness the power of sport to help children grow up healthy, happy and safe.

  The Queen’s Baton relay in Tanzania will be themed around the slogan: “Stop Violence Against Children, Let Them Play!”.

  Speaking ahead of the Queen’s Baton Relay, British High Commissioner Dianna Melrose said: “The Glasgow 2014 Commonwealth Games is teaming up with UNICEF to transform children’s lives across the Commonwealth. It's the first time a charity affiliation to the Games has taken place. I am delighted the UK is supporting this excellent cause. Violence against children is a worrying issue and we must do all we can to stop it.”

  “The aim is to use the event as a catalyst to create awareness and better understanding of the issue of violence against children amongst a more general audience in Tanzania”, says the Tanzania Olympic Committee’s Secretary General, Filbert Bayi.

  The Tanzania Violence Against Children Study, released by the Government and UNICEF in 2011 revealed that in Tanzania, violence affects a majority of children, everywhere. Some of the key findings are:

   · one in three girls and one in seven boys in Tanzania experiences sexual violence before the age of eighteen;
   · most sexual assaults occur at home or in school - and children often know their sexual attacker;
   · rates of physical violence are alarmingly high, nearly three out of four boys and girls experience being punched, whipped or kicked during their childhood, while one quarter of all children are emotionally abused;
   · the majority of children do not report their experience, few seek services, and even fewer

  actually receive any care, treatment or support.

  “Violence Against Children is an important public health problem in the country. Each of us has an important role to play in improving the safety of the home, school, and other spaces where children spend most of their time”, says the UNICEF Representative in Tanzania, Dr. Jama Gulaid.

  The public has been invited to participate in and support the relay runners as they pass through the streets of Dar es Salaam. Ahead of the run on Sunday, the Queen’s Baton will visit the Children’s Cancer Ward at Muhimbili National Hospital.


  Tanzania is the twenty-ninth stop for the Queen’s Baton run on its route through 70 Commonwealth countries and territories, covering over 190,000 km. The Queen’s Baton Relay was launched on October 9th 2013 from Buckingham Palace in London, with the international route starting in India the following day. Prior to arriving in Tanzania, the Baton has visited Ghana, Nigeria, Cameroon, Kenya, Uganda and Rwanda. Its next stop will be the Seychelles.

  The Baton will be taken to Zanzibar on 20th January, the first time the Queen’s Baton Relay has visited the island. It will be relayed through the streets of Stone Town, before being presented to H.E. President Shein.
  The Commonwealth Baton will reach England on May 31 2014 for its final lap to Glasgow and the opening ceremony of the Glasgow Commonwealth Games on 23 July 2014.

  0 0

   FAMILIA YA MZEE JUMANNE ALI SHOMARI WA CHANG'OMBE DAR ES SALAAM, INASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA BABA YAO MPENDWA JUMANNE ALI SHOMARI KILICHOTOKEA LEO ALFAJIR NYUMBANI KWAKE, MAZIKO YATAFANYIKA LEO AL ASRI KATIKA MAKABURI YA KISUTU, HABARI ZIWAFIKIE KAKA YAKE MASUNGA SHOMARI WA NZEGA, SHIJA SHOMARI WA SHINYANGA, JIBUTE SHOMARI WA MWANZA,SEIF ABDALLAH WA IGURUBI, FAMILIA YA SAID NASORO MSHANA ILBORU ARUSHA, BIBI KHADIJA HASSAN KACHENJE WA USANGI KIRICHE, NDUNGU NA JAMAA WOTE POPORE WALIPO. 

  0 0   Tanzania: World Bank Supports Land Ownership Reform and Better Access to Financial Services


  DAR ES SALAAM, January 17, 2014 – Today the Government of United Republic of Tanzania and the World Bank signed the Financial Agreement for additional financing to the Private Sector Competitiveness Project (PSCP) for a total amount of US$60.2 million.


  The Private Sector Competitiveness Project (PSCP) supports the implementation of Tanzania’s program to develop the private sector by lowering the cost of doing business. Today’s funds support the scaling up of two components: strengthening the country’s business environment and improving access to financial services. The US$60.2 million PSCP is financed by a credit from the World Bank’s International Development Association (IDA)*.

  “During the past decade, Tanzania has experienced high rates of economic growth, due to economic reforms, sound macroeconomic policies, and an expanding public sector,” said Philippe Dongier, World Bank Country Director for Tanzania. “The PSCP’s focus on securing land ownership and improving access to finance will facilitate increased flows of private investment into the country’s industries, light manufacturing firms and farms, while boosting shared growth and jobs and improving the quality of life for Tanzanians.”

  The PSCP supports activities designed to improve land registration, land use planning and regularization of tenure rights. The project has already piloted a faster land demarcation and registration approach to replace the traditional high cost registration, (which is about 10 times more expensive.) 

  Today’s project will help to further advance land administration reform, complete business registration reform, and help implement the Government’s Big Results Now initiative to speed up delivery of priority programs such as agriculture, education, energy, transport and water.

  Already PSCP activities have helped 166,000 households participate in microfinance, benefiting more than one million people. Another 35,000 people have benefitted by participating in Village Savings and Loan Associations and Village Community Banks. The additional financing aims to build on this success by strengthening the legal and regulatory framework for the financial sector, improving the capacity of financial regulators, and supporting the development of products such as finance leasing and savings bonds

  0 0

    
  Mwenge wa Jumuiya ya Madola (Queens Baton Relay) utatembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili jumapili ya tarehe 19, Januari, 2014 kuanzia saa tatu kamili hadi saa nne asubuhi. Mwenge huo unatarajia kufika Hospitali ya Taifa Muhimbili ukiongozwa na Mheshimiwa Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi. Dianna Melrose.
   
  Dhumuni la Mwenge huo kimataifa ni kutembelea nchi zote ambazo ni wanachama wa Jumuiya ya Madola katika kuhamasisha maandalizi ya Tamasha la Nne la Michezo na Utamaduni la Jumuiya ya Madola. Mwenge huu unakimbizwa kilomita 190,000 kupitia nchi 70 ambazo ni wanachama wa Jumuiya ya Madola. Safari ya mwisho ya Mwenge huu itakuwa Julai 23, 2014, Glasgow, Scotland kwa ajili ya ufunguzi wa sherehe za michezo ya 20 ya Jumuiya ya Madola.
   
  Hii ni mara ya tano Mwenge huu kufika nchini Tanzania na utakuwa nchini kwa siku tatu ukisaidia   kuhamasisha ushirikiano, kuimarisha umoja na, kuongeza ari ya wananchi hususani vijana waweze kuelewa nini maana ya michezo ya jumuiya ya madola.
   
  Nia ya mwenge huu kuja Hospitali ya Taifa Muhimbili ni kutembelea watoto wanaougua saratani mbalimbali ili kuwapa matumaini ya kuishi na kwamba jamii inawanathamini. Watoto hawa watapata fursa ya kuushika mwenge huu na kupiga picha kama kumbukumbu muhimu katika maisha yao.
   
  Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano
  Januari 17, 2014

  0 0

  CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO – CHADEMA  KANDA YA KASKAZINI.(Tanga, Kilimanjaro, Arusha & Manyara)
   TAARIFA KWA UMMA
  WAGOMBEA WA UDIWANI – KANDA YA KASKAZINI
  Tarehe 15 Januari 2014, wagombea wafuatao wa CHADEMA walipitishwa na TUME YA UCHAGUZI kuwania nafasi za uwakilishi (UDIWANI) katika maeneo ya kata mbalimbali za kanda ya Kaskazini.
  Wagombea hawa walipita katika mchujo wa uteuzi wa chama. Chama kina matarajio makubwa sana kuwa wananchi wa maeneo haya ya kata hizi watapata fursa nzuri ya kuwachagua wagombea wa CHADEMA ambao wana dhamira njema sana na ya kweli katika kuwatumikia.
  Wagombea waliopitishwa pamoja na mikoa yao ni:
  JINA LA MGOMBEA
  KATA
  JIMBO
  MKOA
  BI. MWANAISHA MOHAMED OMARI
  KIOMONI
  TANGA DC
  TANGA
  BW. KAGOMA FRANK HENRY
  KIBORLONI
  MOSHI MJINI
  KILIMANJARO
  BW. ALLY BANANGA
  SOMBETINI
  ARUSHA MJINI
  ARUSHA
  BW. CHARLES SAMWEL MGATA
  PARTIMBO
  KITETO
  MANYARA
  BW. SANING’O KONE
  LOLERA
  KITETO
  MANYARA
   Katika uchaguzi huu CHADEMA imejipanga kushiriki kikamilifu sana tukiwa na uhakika kuwa chama kimewapa wananchi wapiga kura chaguo lao kwa kuzingatia uwezo wa wagombea, utayari wa wagombea wetu kushirikiana na kuwatumikia wananchi na dhamira njema ya kutatua matatizo na kero za wananchi zilizoletwa na CCM kwa kushindwa kutimiza wajibu wao.
  Aidha chama kimesikitishwa sana na uhuni na ushenzi uliofanywa wa kumteka mgombea wa CHADEMA ndg. ALLY SAIDI JAHA saa nane mchana siku ya tarehe 15.01.2014 muda mfupi kabla ya muda kurudisha fomu kufungwa. Tukio hili limetokea huku tukiwa na taarifa zilizopatikana baadae kuwa mida ya saa nne asubuhi mgombea wetu alifuatwa na kiongozi mmoja wa CCM wa wilaya.
  Uongozi wa kanda tumesharipoti tukio hili polisi na kupewa RB namba LUS/RB/75/2014 TAARIFA.16.01.2014 ya kutekwa/kupotea kwa ndg ALLY SAIDI JAHA. Hali kadhalika uongozi chama wa Jimbo la Mlalo umeshwandikia barua msimamizi wa uchaguzi kuhusu tukio hili la kutekwa nyara na kupotea kwa mgombea wetu na kuwa baada ya kupata taarifa ya tukio hili kwa kina chake, chama kitakuwa na mahali pa kuanzia.
  Hivi sasa tumetuma timu ya intellijensia ya chama kuchunguza kwa kushirikiana na Red Brigade ya wilaya ili kupata undani wa tukio hili ambalo limetufedhehesha sana na ambalo litakuwa limewanyima demokrasia ya kuchagua kwa watu wa Mtae ya kiongozi na chama wanachokitaka. 
  Niwahakikishie wakazi wa Mtae na Watanzania wote wapenda mabadiliko ambao jambo hili limetukera wote kuwa ndg Ally Saidi Jaha atatafutwa mpaka apatikane akiwa mzima au vinginevyo ili ifahamike nini kimemtokea na pia awaeleze watu wa Mtae na Watanzania wote hili jambo kuna nini nyuma yake. Hapa kuna mtu au watu watawajibika kwa gharama yoyote, hili jambo halitaisha kirahisi hivi hivi.
  Niwaombe wakazi wa Kanda ya Kaskazini, kwenye uchaguzi huu tuunganishe nguvu zetu kwa sisi wenyewe kujitolea na muda wetu na rasilimali zetu, ili tuwashughulikie CCM ambao wamekuwa wakiendelea kuwatesa Watanzania kwa sera zao mbovu na uongozi wa kihuni ambao haujali kabisa maisha ya Watanzania.
   Imetolewa na Amani Golugwa
  Katibu wa Kanda ya Kaskazini
  +255 754 912 914 au 0784 343 275
  golugwa@gmail.com

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na timu maalum inayohakiki maeneo mapya ya utawala kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Pichani kulia na timu yake ya Mkoa iliyokuwa ikiratibu maeneo hayo ofisini kwake leo tarehe 17 Januari 2014. Timu hiyo kutoka TAMISEMI inaongozwa na Mwanasheria wa TAMISEMI Ndugu Eustard Ngatale (watatu kulia).

   Katika kikao hicho kifupi Mkuu huyo wa Mkoa ameiomba mamlaka husika kupitia timu hiyo kuangalia upya vigezo vinavyotumika katika kugawa maeneo mapya ya utawala na upandishaji wa madaraja kutoka kijiji, kata, Tarafa, Halmashauri, Miji na Manispaa. 

  Alisema kuwa kuna maeneo mengine ambayo yakiangaliwa kwa kigezo kimoja cha wingi wa watu bila kuangalia umbali wa huduma na giografia ya eneo husika unakuta wananchi wanakosa huduma zao za msingi na kupata tabu kubwa katika kuzipata.

   Alitolea mfano vijiji vikubwa vya mwambao ambavyo kupata huduma katika kata zao ni lazma wavuke upande mmoja wa Ziwa kwenda upande mwingine jambo ambalo ni hatarishi kama ilivyotokea kwa wananchi wa Kijiji cha Kipwa Mwambao mwa Ziwa Tanganyika ambao hivi karibuni walipoteza watu 15 katika ajali ya boti walipokwenda kupata huduma ya afya. Wengi ya waliofariki katika ajali hiyo mbaya walikuwa ni watoto chini ya umri wa miaka 5.  
  Kikao kikiwa kinaendelea ambapo kwa upande wake Mwanasheria wa TAMISEMI Ndugu Eustard Ngatale alisema kuwa kubariki na kuhalalisha uanzishwaji wa maeneo mapya ya Utawala vipo vitu mbalimbali vya kuzingatia ambavyo ni pamoja na kuwepo kwa makubaliano ya wananchi na viongozi wa maeneo husika kupitia mihutasari ya vikao maalumu vya kisheria vya WDC, Halmashauri, DCC na RCC katika ngazi ya Mkoa. (Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @Rukwareview.blogspot.com)

  0 0

  1

  Mkurugenzi huyo amesema Shirika la nyumba badala ya kwenda kutoa msaada wa sabuni na vyakula katika vituo vya watoto yatima au kusaidia biskuti limeamua kubadilisha maisha ya vijana wa Tanzania kwa kuwapa mafunzo na kuwapatia mashine za kutengeneza matofali ya udongo ambayo wao NHC watakuwa ndiyo wateja wakuu wa kununa matofali hayo, lakini pia shirika hilo linatoa mashine za kufyatulia matofali zipatazo 640 katika wilaya 160 mikoa yote ya Tanzania bara na kiasi cha shilingi 500,000 kila mkoa kama mtaji wa kununulia saruji kwa vikundi hivyo, Katikati ni Injinia Kwanama Elias Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo kutoka Nation Housing&Building Research Agency (NHBRA) na kushoto ni Bw.Julius Njelwa kutoka VETA, mafunzo hayo yameratibiwa kwa pamoja na (NHC), (VETA) na (NHBRA) kwa pamoja.(PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)3 
  Baadhi ya maofisa wa Shirika la Nyumba NHC wakiwa katika maadalizi hayo kushoto ni Suzan Omary Meneja Mawasiliano NHC, Muungano Saguya Meneja huduma kwa jamii NHC na Ephraim Kibonde mtangazaji wa Clouds Radio.

  0 0


  JE UNGEPENDA KUFAHAMU MAJINA YA WATU/KAMPUNI ZILIZOPATA MGAO WA UVUNAJI KATIKA MASHAMBA YA MITI YA SERIKALI 2014 KAMA NDIVYO BASI USISITE KUTEMBELEA UKURASA WA FACEBOOK WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII:Ministry of Natural Resources and Tourism - Tanzania UKITEMBELEA USISAHAU KULIKE PAGE HIIhttps://www.facebook.com/pages/Ministry-of-Natural-Resources-and-Tourism-Tanzania/214617361925291

older | 1 | .... | 203 | 204 | (Page 205) | 206 | 207 | .... | 1898 | newer