Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46194 articles
Browse latest View live

HIVI NDIVYO VODACOM ILIVYOZIKUTANISHA TIMU ZA WABUNGE WA ZANZIBAR,MUUNGANO NA UGANDA MIAKA 50 YA MAPINDUZI

0
0
 Ofisa Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Kampuni ya Vodacom Hassan Saleh akimkabidhi Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Pandu Ameir Kificho kombe lililotolewa na Vodacom kwa ajili ya mshindi wa mechi maalum kati ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Wabunge wa Bunge la Tanzania kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Mchezo huo ulichezwa kwenye Uwanja wa Amaan Mjini Zanzibar na kufadhiliwa na Vodacom Tanzania.
 .Spika wa Baraza La Wawakilishi Pandu Ameir Kificho akilikagua kombe lililotolewa na Kampuni ya Vodacom kwa ajili ya mshindi wa mechi maalum kati ya Timu ya Soka ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Wabunge wa Bunge la Tanzania kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Mchezo huo ulichezwa kwenye Uwanja wa Amaan Mjini Zanzibar na kudhaminiwa na Vodacom. Timu ya Bunge ilishinda bao moja kwa bila. 
 Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar Pandu Ameir Kificho akimkabidhi Nahodha wa Timu ya Soka ya Wabunge wa Bunge la Tanzania Amos Makala amabe pia ni Naibu Waziri wa Habari,Vijana Utamduni na Michezo kombe kufuatia kuichapa timu ya Baraza la Wawakilishi kwenye mechi maalum ya kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Katikati ni Ofisa Mkuu wa Mauzo na Usamabazaji wa Vodacom Hassan Saleh waliodhamini mechi hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Amaan Mjini Zanzibar.
 Kikosi cha Timu ya soka ya Wabunge wa Bunge la Tanzania kikiwa na kombe muda mfupi mara baada ya kukabidhiwa baada ya kuifunga timu ya Baraza la Wawakilishi bao moja kwa bila kwenye mechi maalum ya kusherehekea mika 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Mchezo huo ulidhaminiwa na kampuni ya Vodacom.
 Kikosi cha Timu ya Netiboli kinachoundwa na Wabunge wa Bunge la Uganda kikiwa katika picha ya pamoja muda mfupi kabla ya kushuka uwanjani kuvaana na kombaini ya Zanzibar ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Katikati  ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AWAJULIA HALI MAWAZIRI WALIOLAZWA MUHIMBILI, CLEOPA MSUYA NA HARUNA ALI SULEIMAN.

0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa Msuya, aliyelazwa katika jengo la Moyo Hospitali ya Taifa Muhimbili, wakati alipofika kumjulia hali leo, Jan 15, 2014. Kulia ni mke wa Makamu, Mama Zakia Bilal (kushoto) ni Meneja wa Jengo hilo la Moyo, Sr. Salome Kassanga.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na  Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa Msuya, aliyelazwa katika jengo la Moyo Hospitali ya Taifa Muhimbili, wakati alipofika kumjulia hali leo, Jan 15, 2014. Kushoto ni mke wa Makamu, Mama Zakia Bilal.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimjulia hali Waziri wa Kazi na Utumishi wa Umma wa Zanzibar, Haruna Ali Suleiman, aliyelazwa katika jengo la Moyo Hospitali ya Taifa Muhimbili, wakati alipofika kumjulia hali leo, Jan 15, 2014. Katikati ni mke wa Makamu, Mama Zakia Bilal (kushoto) ni Meneja wa Jengo hilo la Moyo, Sr. Salome Kassanga. Picha na OMR Meneja wa Jengo hilo la Moyo, Sr. Salome Kassanga. Picha na OMR

NGUMI KUPIGWA MKOA WA PWANI IJUMAA

0
0

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMIMchezo wa masumbwi unatarajia kufanyika siku ya ijumaa katika ukumbi wa Shimbikati  pub uliopo Kiluvya Mkoa wa pwani, mpambano  huo wa mchezo wa ngumi katika mkoa wa pwani umeandaliwa na kocha wa mchezo huo Jafar Ndame

Akizungumzia mpambano huo ambao unasubiriwa kwa hamu na wakazi wa kiluvya pamoja na vitongoji vyake, litawakutanisha mabondia Azizi Abdallah atakaepambana na Sadam Manjapa huku Julius Kisarawe akivaana na Haji Gamba, na Tasha Mjuaji akimkabiri Roja mjeshi na mapambano mengine mengi ya utanguliza pamoja na burudani nyingine nyingi

Mipambano hiyo ya masumbwi itakuwa chini ya chama cha ngumi za kulipwa PST na Rais wake Emanuel Mlundwa ambao ndio wasimamizi wakuu wa mchezo huo siku hiyo

mbali na kuwepo kwa mchezo huo wa masubwi pia kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi wakiwemo mabondia wakali kama vile Floyd Maywether,Manny Paquaio,Oscar Dela Hoya,Mohamed Ali,mike Tyson, pamoja na mabondia mbalimbali pia kutakuwa na vifaa vya mchezo wa masumbwi kama vile glove,gumshiti,clip bandeji na vifaa mbalimbali vitakavyokuwa vikiuzwa na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masum,bwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kwa ajili ya kuhamasisha mchezo huo 
ili wapenzi wajue sheria na taratibu za mchezo wa masumbwi

Mzee Arnold Nkhoma atoa shukrani kwa kutimiza miaka 100 iliyoambatana na mnuso wa nguvu alioandaliwa na wajukuu zake

0
0
DSC_0172
Jicake la Mzee Arnold Nkhoma la kusheherekea miaka 100 ya kuzaliwa kwake....Hongera sana Mzee Nkhoma Mungu akuzidishie 100 mingine uvunje rekodi ya dunia.
DSC_0188
Happy Birthday to you.....How old are you now...!!!...Watoto, wajukuu na vitukuu wakimwimbia Mzee Arnold Nkhoma.
DSC_0204
Pichani juu na chini ni watoto wa mzee Arnold Nkhoma wakimlisha cake baba yao kwa niaba ya watoto wengine.
DSC_0206
Kwa picha zaidi ingia hapa
DSC_0019
Birthday Boy...Mzee Arnold Nkhoma akiwasili kwenye Kanisa la Mtakatifu Andrew lililopo Magomeni jijini Dar kuhudhuria Ibada ya kutoa shukrani kwa kutimiza miaka 100 akiwa amesindikizwa na mmoja wa watoto wake wa kiume pamoja na mjukuu wake Sawiche Wamunza (kushoto).
DSC_0029
Birthday Boy Mzee Arnold Nkhoma akihudhuria Ibada pamoja na kutoa shukrani ya kutimiza miaka 100 kwenye kanisa la Mtakatifu Andrew lililopo Magomeni jijini Dar. Aliyeketi nae ni mmoja wa watoto wake wa kiume aliyemsindikiza baba yake.
DSC_0079
Baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki wa Mzee Arnold Nkhoma waliohudhuria ibada hiyo.


DSC_0117
Mchungaji wa Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Andrea akifanya maombi maalum kwa ajili ya Mzee Arnold Nkhoma na familia walipofika kanisani kwa ajili ya kutoa shukrani ya kutimiza miaka 100 babu yao.
DSC_0120
Mchungaji Mkuu wa kanisa la Mtakatifu Andrea akimwaga maji ya baraka kwa Mzee Arnold Nkhoma pamoja na familia yake.
DSC_0162
Baadhi ya wajukuu pamoja na kitukuu cha Mzee Arnold Nkhoma wakipata Ukodak.
DSC_0201
Ndugu, jamaa na marafiki wakipata Ukodak na Birthday Mzee Arnold Nkhoma mara baada ya kumalizika kwa ibada.
DSC_0215
Mjukuu mkubwa wa Mzee Arnold Nkhoma, Bi. Usia Nkhoma Ledama akipata Ukodak na Babu yake pamoja na Baba zake wakubwa.
DSC_0033
Baada ya hapo mnuso ulihamia nyumbani kwa mjukuu mkubwa wa Mzee Arnold Nkhoma, Bi. Usia Nkhoma Ledama.. Pichani wajukuu mapacha wakimsindikiza Birthday Boy sehemu maalum iliyoandaliwa kwa ajili yake.
DSC_0126
Mmoja wa watoto wa Mzee Arnold Nkhoma akitoa utambulisho wa kaka na dada zake waliozaliwa na Birthday Boy kwa wageni waalikwa.
DSC_0133
Mjukuu mkubwa wa Mzee Arnold Nkhoma, Bi. Usia Nkhoma Ledama akizungumza machache kwa wageni waalikwa.
DSC_0148
Wajukuu wa Birthday Boy Mzee Arnold Nkhoma wakisakata rhumba kwenye mnuso wa babu yao.

Rais Kikwete awajulia hali Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa David Msuya na Waziri Haroun Ali Suleiman wa Zanzibar

0
0
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali Waziri Mkuu Msaafu Mzee Cleopa David Msuya aliyelazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili jana jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakimjulia hali Waziri wa nchi Afisi ya Rais Kazi na Utumishi wa Umma wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar(SMZ) Bwana Haroun Ali Suleiman aliyelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam, Jana (Jumanne)(picha na Freddy Maro). 

NI KWELI IMETOKEA MKOANI MBEYA: WAENDESHA BODABODA UYOLE WAKIMBIA NA MAITI YA MWENZAO BAADA YA MCHUNGAJI KUWAAMBIA WAMEFWATA UBWABWA

0
0


 Mchungaji wa Bodaboda Bahati Mwasote akiendesha Ibada ya mazishi.
Baadhi ya Waendesha Boda Boda wakiwa wamekusanyika sehemu ya mazishi ya kijana huyo.
Mchungaji Edward Mtweve wa kanisa la Tanzania Assemblies of God[TAG]Uyole Njia Panda amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya Waendesha pikipiki[Bodaboda]kuvuruga ibada ya mazishi ya mwendesha pikipiki aitwaye Gabriel Osward Ngalele.

Vurugu hizo zilitokea katika Kanisa hilo baada ya Gabriel Ngalele kufariki kwa ajali ya gari Januari 13 majira ya saa 11 alfajiri eneo la SAE akiwa na abiria wake ambapo walifariki papo hapo baada ya kugongwa na Roli.


Taratibu za mazishi zilipokamilika mwili wa marehemu ulipelekwa katika Kanisa hilo wakati mchungaji akiendesha Ibada aliomba utulivu kwa wafiwa ambapo walitulia lakini vijana zaidi ya 300 waendesha bodaboda walilipuka kwa kelele hali ilyomfanya mchungaji kuomba utulivu katika Ibada.


Hata hivyo vijana hao waliendelea kujaa katika kanisa hilo na kukosekana utulivu hali iliyomlazimu mchungaji kuwaambia kama wamekosa utulivu basi watakuwa wamefuata ubwabwa katika msiba huo hali iliyofanya kutokea mtafaruku mkubwa.


Katika mtafaruku huo ilpelekea vijana kuuchukua mwili wa marehemu hadi kwenye makaburi huku wakimwacha mchungaji ambapo ililazimu jeshi la polisi kuingilia kati na kuzuia fujo kanisani na kuamua kumresha nyumbani kwake kwa ulinzi mkali.


Wakati mchungaji akisindikizwa nyumbani kwake vijana waliendelea na taratibu za mazishi kwa utaratibu uliosimamiwa na Mwenyekiti wa Bodaboda Jiji Vicent Mwashoma huku mchungaji wa Bodaboda Bahati Mwasote akiendesha Ibada ya mazishi.


Katika mazishi hayo baadhi ya Viongozi mbalimbali walishiriki akiwemo mlezi wao Nwaka Mwakisu,Mlezi wa Bodaboda Taifa Respisius Timanywa ambaye aliwaasa vijana kuhudhuria mafunzo ili kupunguza ajali za mara kwa mara.


Kwa upande wake mchungaji Edward Mtweve wa Kanisa la TAG amesema amesikitishwa sana na kitendo cha kuvurugwa kwa Ibada kwani amesema kuwa wengi wa waliokuwa wakifanya fujo walikuwa ni walevi na wavuta bangi na si waumini wa Kanisa lake.


Aidha Mtweve na Baraza la wazee wamesema kuwa hawakusudii kuchukua hatua zozote dhidi ya vijana ambao wamefanya fujo kwani yote wanamwachia Mungu na kwamba katika kanisa hilo hakuna tukio lilowahi kutukia. Pia amesema kitendo cha kuchukua mwili wa marehemu madhabahuni ni cha utovu wa nidhamu kwani vijana wanapaswa kuwa na hofu ya Mungu.

Wakikabidhi rambirambi kwa mjane ,Mwenyekiti wa Bodaboda Jiji Vicent Mwashoma amesema pesa za rambirambi zitumike kusaidia familia ya marehemu badala ya ndugu kutumia pesa hizo kuendeshea msiba huo.


Habari kwa hisani ya Ezekia Kamanga
wa Mbeya yetu

“TUMEPATA TAARIFA SAHIHI KUHUSU GESI NA MAFUTA’’, - VIONGOZI WA DINI

0
0
 Na Asteria Muhozya ( Mtwara, Lindi na Kilwa)

Kusudi la Wizara ya Nishati na Madini kufanya kazi kwa kushirikiana na viongozi wa dini katika sekta za gesi na mafuta kwa manufaa ya Watanzania limefikiwa.


Akizungumza baada ya ziara ya kutembelea Bomba Jipya la gesi asilia Mtwara- Dar es Salaam, Mtambo wa kusafisha umeme wa Mnazi Bay, na maeneo mbalimbali ya uendelezaji wa gesi asilia katika Mkoa wa Mtwara na Lindi, Katibu wa Jumuiya ya Kikrsito Tanzania (CCT) na Mwenyekiti wa Sekretariati  ya kongamano la viongozi wa dini Bw. John Mapesa, alieleza kuwa, viongozi wa dini wamepata elimu sahihi ambayo hawakuifahamu kabla kuhusu sekta hizo.


Aliongeza kuwa, viongozi hao wamekuwa wakipata habari ambazo si sahihi kuhusu rasilimali hizo lakini baada ya kutembelea, kujifunza, kuona na kusikia kutoka kwa watalaamu mbalimbali kuhusu namna miradi hiyo inavyofanyika, wanatarajia kuwa walimu kwa watanzania wengine ili kuwa na uelewa wa pamoja.


“Sisi tuna nafasi kubwa sana ya kukutana na wananchi kutoa elimu, kwani wanatuamini na wanatusikiliza kwa kwasababu tunawasaidia kiroho. Wizara imefanya sehemu yake na sisi tunayo sehemu yetu ya kuwafikia kupitia umoja wetu”.  Alisema.


Aliongeza kuwa, viongozi wa dini ni sehemu ya jamii na wanaposhirikishwa kwa kuelezwa mipango mbalimbali ya Serikali ni jambo la muhimu kwasababu wanayo nafasi ya moja kwa moja ya kuwasiliana na wananchi ikiwemo kushauri. Hivyo, elimu waliyoipata na taarifa walizozipata zitakuwa na mchango katika kuleta amani na ustawi wa jamii wakati huu ambapo nchi inaelekea katika kupokea uchumi mkubwa kupitia rasilimali hizo.


“Nawaambia Watanzania wenzangu tushiriki kikamilifu katika uchumi huu wa gesi na mafuta  kila mmoja kwa namna yake  kwani kuna mafanikio makubwa sana yanakuja. Kuna fursa nyingi na Mwenyezi Mungu hawezi kuleta baraka kwa ajili ya kutuangamiza, analeta kutuletea furaha ili tufaidike. Juhudi za Serikali kuhakikisha kila mmoja anafaidika tumeziona”. Alisema.


Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini aliyeongoza ujumbe huo, Mhandisi Ngosi Mwihava alisema kuwa, kufuatia ziara hiyo ya viongozi wa dini, inaonesha kuwa serikali ni sikivu na inasikiliza matarajio ya wananchi.


“Tuliona kuwa kuna uelewa tofauti tofauti katika rasilimali hizi, viongozi waliomba tuwaelimishe na sisi tumefanya hivyo kwasababu tunajua wanayo nafasi kubwa ya kuwafikia wananchi na wana mchango mkubwa katika kufikia maendeleo tunayoyatarajia”. Alisema   Naibu Katibu Mkuu.


Aliongeza kuwa, lengo kubwa la ziara hiyo ya viongozi wa dini ni kutaka kuweka uelewa wa pamoja kuhusu rasilimali hizo kwa makundi mbalimbali yenye uwakilishi Kitaifa hali ambayo itasaidia kufahamu fursa zilizopo, mipango ya serikali na kila mmoja kwa nafasi yake ajue namna fursa zilizopo katika sekta hiyo zitakavyotumiwa.



“Katika mchakato wa maendeleo, kuna wadau wengi, hivyo mwanya upo kwa wadau kuchangia katika uwekezaji inaweza kuwa kuwekeza kwa kushirikiana na serikali au kufanya binafsi”. Alisema Naibu Katibu Mkuu.


Aliongeza kuwa, anaamini ziara hiyo imetoa mwanga kwa viongozi wa dini katika kuelekea kwenye kongamano la kujadili rasilimali hizo na namna zitakavyowanufaisha watanzania.


Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Mstaafu Mhe. Joseph Simbakalia aliwataka viongozi hao kuwasaidia wananchi kuyaweka matarajio ya uchumi huo kwenye  kiwango halisi  kwa kuzingatia kwamba, uchumi wa gesi ni sekta mpya Tanzania na hivyo, maandalizi yakutosha yanahitajika ikiwemo kujifunza kwa usahihi kutokana na ukweli kwamba biashara hiyo ni ghali.


“Mmefanya vizuri sana kuja, kawaambieni vijana na wananchi wajiandae kujua watafanya nini katika uchumi huu kuanzia kwenye elimu na uwekezaji ili tufike tunakotaka kwenda. Msipofanya hivyo, hatutakwenda vizuri”. Alisema Simbakalia.


Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Ludovick Mwananzila aliwataka viongozi hao kuwaelimisha wananchi ukweli kuhusu gesi kusafirishwa kwenda Dar es Salaam, ugunduzi wake na manufaa yake kwa Taifa kwasababu wamepata nafasi ya kuona yale  yanayofanyika na kusikia mipango mbalimbali.


“ Waelimisheni ukweli, Dar es Salaam ndio kuna viwanda vingi vya uzalishaji tofauti na Lindi na Mtwara, lakini haimanishi kwamba Mikoa hii itabaki bila manufaa, tuna kiwanda cha sementi kinatarajiwa kujengwa hapa Lindi tunatarajia kitatoa fursa nyingi, si hilo tu, tuna mipango mingi ya kuhakikisha kuwa wananchi wote wananufaika”. Alisema.


Aidha, aliwataka viongozi hao  kuwaelimisha wananchi kuacha kuchukua mifano ya nchi ambazo hazikujiandaa katika uchumi wa gesi na kuongeza kuwa, ni elimu pekee ndio itasaidia kuleta mabadiliko kwa wananchi.


“Kilwa kwa mfano, katika kijiji cha Songosongo wanapata si chini ya milioni 20 kwa mwezi kutokana na faida za gesi, wanapata umeme bure, maji bure, sasa katika hayo vurugu za nini? Alisema Mkuu wa Mkoa.


Naye Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mhe. Abdalah Ulega aliutaka ujumbe huo kuwaeleza wananchi kuwa, mafanikio katika sekta ya gesi yapo na wananchi wameanza kufaidika nayo.


Aliongeza kuwa, kama isingekuwa mafanikio makubwa yaliyopatikana katika sekta hiyo kwa wilaya ya Kilwa, wananchi wangekuwa na maisha magumu, kutokana na ukweli kuwa, sekta hiyo imesaidia katika kuboresha huduma mbalimbali za jamii wilayani humo.


Vilevile, aliongeza kuwa, Wilaya tayari inayo mpango wa kupanua mji wa kilwa ili kusaidia kuongeza fursa mbalimbali za uzalishaji na uwekezaji zitakazosaidia kuleta maendeleo wilayani humo, hivyo amewataka wananchi kujiandaa kuwekeza katika maeneo mbalimbali.


Naye mwekezaji wa ndani wilayani humo Bw. Sultan Sultan akielezea uzoefu wake katika sekta ya gesi na mafuta, amewataka watanzania kufikiria kuwekeza katika nyanja mbalimbali zinazoendana na sekta hiyo.


“Kuna mtandao mkubwa sana wa uchumi katika sekta hii, tusifikirie gesi tu, kwa uzoefu wangu unahitaji kuwa na mtaji mkubwa lakini kuna zaidi ya gesi. Mimi nimewekeza katika hoteli ambazo zinawahudumia wawekezaji wa gesi hapa tuangalie yapo mengi, Alisema.


Aidha aliwataka viongozi wa dini kuwasaidia vijana kuzitambua fursa, kuwaelimisha kuhusu sekta hiyo na kujiandaa kikamilifu hasa katika katika elimu.


“Vijana wetu wa sasa wako kwenye hamu ya kupata maendeleo ya haraka, wasaidieni namna ya kuyafikia maendeleo kwa utaratibu na kwa ustaarabu,”. Aliongeza.


Ziara hiyo ya viongozi wa dini ni hatua ya awali ya kupata uelewa kuhusu sekta hiyo, ikiwa ni maandalizi ya kuelekea katika kongamano la viongozi wa dini na Serikali linalotarajiwa kufanyika tarehe 21 na 22 januari,2014 jijjini Dar es Salaam ambapo zaidi ya viongozi 100 wanatarajia kushiriki kutoka Mikoa yote nchini. Aidha pamoja na kutembelea miradi hiyo, baadhi ya viongozi pia walipata nafasi ya kutembelea bahari kuu kuangalia namna shughuli za utafutaji na uzalishaji wa gesi na mafuta zinavyofanyika.

TODAYNEWS KUTOKA MKOANI IRINGA:KAMPENI ZA UCHAGUZI MDOGO KUANZA KESHO,JESHI LA POLISI LATOA TAHADHARI SUALA LA VURUGU

0
0
Kufuatia kampeni za uchaguzi mdogo ambazo zitaanza kesho Chama cha mapinduzi  (CCM), kimesema kuwa kimejiandaa vizuri na kinauhakika wa kuchukua nafasi hiyo.  Akizungumza na katibu wa CCM mkoa,Bwa Mtenga Husein amesema kuwa kura za maoni kwa wagombea zimefanyika leo na  wagombea wanakabidhi fomu hii leo katika kata ya Nduli.

Katibu amewataka wanachi kumchagua kiongozi atakayewaletea maendeleo na si kufuata chama anachotoka,hii itapelekea kuwasaidia wananchi kumpata kiongozi  mwenye uadilifu, makini na mwenye kujituma katika suala zima la kuleta na kujenga maendeleo kwa Wananchi wake halikadhalika kwa maendeleo ya Taifa kiujumla.


Kwa upande wa jeshi la polisi,akizungumza kamanda wa Mkoa wa Iringa Ramadhani Mungi,amewaonya wanasiasa wote ambao watajinadi kuwania nafasi hizo kutumia lugha nzuri na zenye staha katika suala zima la kulinda amani na utulivu kwa kipindi chote cha kampeni.Aidha ameongeza kwa kusema kuwa kwa yoyote atakayetumia lungha itakayosababisha kuvunja amani hawataweza kumvumilia.


======  =====  ======  ======
WAFANYABIASHARA NA ABIRIA WALALAMIKIA KERO YA KITUO CHA IPOGORO -IRINGA. 

Baadhi ya Wananchi wanaoishi katika manispaa ya Iringa wameiomba Serikali kukarabati eneo la stendi ya Ipogoro kutokana na mazingira ya eneo hilo kutoridhisha, hususaN  kipindi hiki cha mvua.


Wananchi hao wameyasema hayo leo walipokuwa wakizungumza ana kwa ana na mshika kalamu wa hapa jamvini,aliyefika eneo la tukio,na kujionea hali halisi ya eneo hilo ambalo limeonekana kuwa kero kwa wakazi wake.

Baadhi ya Wananchi ambao ni Wafanyabiashara wa eneo hilo wamesema kuwa mara kadhaa wamekuwa  wakidaiwa ushuru  kwa ajiri ya kuboresha eneo hilo,lakini wanashangaa hakuna linalofanyika katika kuboresha stendi hiyo.

Aidha wameitaka serikali kuboresha miundombinu ya eneo hilo la stendi ya ipogoro ili kuraisisha utendaji kazi wa Wafanyabiashara hao na wakazi wengine wa eneo hilo kwa ujumla sambamba na watumiaji wa kituo hicho a.k.a abiria. 

Rais Kikwete awaapisha Balozi mpya wa Tanzania nchini Malaysia na Kamisha wa Tume ya Usuluhishi,ikulu jijini dar leo

0
0
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wateule aliowaapisha ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Kushoto ni Kamishna wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi Bwana Jafari Omari na kulia ni Balozi mpya wa Tanzania nchini Malaysia Dkt.Aziz Ponary Mlima 
Picha na Freddy Maro wa Ikulu.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo asubuhi amewaapisha Balozi mpya wa Tanzania nchini Malaysia na Kamishna wa Tume ya usuluhishi na Uamuzi.Walioapishwa leo katika hafla fupi iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam ni Dkt.Aziz Ponary Mlima anayekuwa Balozi mpya wa Tanzania nchini Malaysia na Bwana Jafari Omari anayekuwa Kamishna wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi.
Balozi mpya wa Tanzania nchini Malaysia Dkt.Aziz Ponary Mlima akila kiapo mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Kamishna wa Tume ya usuluhishi na uamuzi Bwana Jafari Omari akila kiapo mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.

Rais Mstaafu Benjamin Mkapa amkabidhi Rais Kikwete vitabu vya Hotuba zake

0
0
 Rais Mstaafu awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa leo amemkabidhi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete nakala ya vitabu vya hotuba zake alizozitoa kwa nyakati tofauti wakati wa uongozi wake wa miaka kumi.Pichani Rais Mstaafu Benjamin Mkapa akikabidhi Rais Kikwete vitabu hivyo katika hafla fupi iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.VitABU hivyo vimechapishwa na kampuni ya Mkuki na Nyota chini ya Mkurugenzi wake Bwana Walter Bgoya Picha na Freddy Maro.

Mh. Lowassa akutana na uongozi wa bodaboda mkoa wa Dar

0
0
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (katikati) akisikiliza maelezo kutoka kwa mmoja wa viongozi wa shirikisho la waendesha bodaboda jijini Dar es Salaam,waliomtembelea ofisini kwake leo.Mh. Lowassa alikutana na viongozi hao kupanga utaratibu wa kufanya harambee ya kuchangia saccos ya shirikisho hilo.Mwezi Disemba mwaka jana,Mh Lowassa alikuwa mgeni rasmi katika tamasha la bodaboda kwenye viwanja vya leaders jijini Dar es Salaam ambapo aliahidi kukutana na uongozi huo kwa ajili ya kuandaa harambee ya kuwasaidia kumiliki pikipiki waendesha bodaboda wa Dar es salaam.

WIZARA YA AFYA ZANZIBAR YATILIANA SAINI MKATABA WA KUTOA HUDUMA ZA MAGONJWA YA AKILI KATIKA HOSPITALI YA MAKUNDUCHI KUSINI UNGUJA.

0
0
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk. Mohammed Jiddawi  na Dk. Peter McGovern  wakitia saini makubaliano ya kuanzisha huduma za Aya ya magonjwa ya akili katika Hospitali ya Makunduchi. Katikati ni Naibu Waziri wa Afya Dk. Sira Ubwa Mamboya akishuhudia utiaji saini  katika sherehe  zilizofanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja Mjini Zanzibar.
 Dk. Ingvar  Bjelland kutoka Hospitali ya Chuo Kikuu cha Haukeland  nchini Norway na Daktari bingwa wa magonjwa ya akili wa Hospitali ya Kidongo chekundu wakitia saini makubaliano ya kuanzishwa huduma za magonjwa ya Afya ya akili katika Hospitali ya Makunduchi Kusini Unguja.
Dk. Ingvar  Bjelland kutoka Hospitali ya Chuo Kikuu cha Haukeland  nchini Norway  akitoa maelezo jinsi  Hospitali hiyo itakavyotoa huduma ya magonjwa ya Afya ya akili Zanzibar katika sherehe za kutiliana saini zilizofanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja Mjini Zanzibar. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

======  ======  ==========
RAMADHANI ALI/MAELEZO ZANZIBAR .
                                  
Wizara ya Afya ya Zanzibar imetiliana saini mkataba wa makubaliano  wa kuanzishwa kwa majaribio kutolewa huduma za maradhi ya afya ya akili katika Hospitali ya Makunduchi iliyoko Mkoa wa kusini Unguja. 
Uwamuzi wa kuifanya Hospitali ya Makunduchi  kuanzisha  huduma hiyo inatokana na mapendekezo ya Wizara ya Afya   ya mwaka 2008 na taarifa ya Afya ya akili  Zanzibar  ya Jumuia ya Ulaya.

Wadau watatu  wanashirikiana katika mpango huo ambao  ni Hospitali ya Chuo Kikuu cha Haukeland cha Norway,  Hospitali ya Afya ya akili ya Kidongochekundu na Mradi wa kuimarisha Afya Zanzibar.

Katika sherehe za utiaji saini zilizofanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja, Wizara iliwakilishwa na Katibu Mkuu Dk.  Mohammed Jiddawi, Chuo Kikuu cha Haukeland kiliwakilishwa na Dk. Ingavr Bjelland, Dk. Peter McGovern alitia saini kwa upande wa Mradi wa kuimarisha Afya kijiji cha Makunduchi na Dk. Khamis  Othman alitia saini kwa upande Hospitali ya Kidongo Chekundu.

Wadau hao watatu watashirikiana katika kuimarisha kujenga uwezo huduma za maradhi ya Afya ya akili kwa visiwa vya Unguja na Pemba, kuanzisha mtaala wa kufundisha masomo ya afya ya akili wafanyakazi wa Hospitali ya Makunduchi kwa mujibu wa  Shirika la Afya duniani (WHO)  na kuunga mkono maendeleo ya mafunzo yanayotolewa kwa wauguzi wa Hospitali ya Makunduchi na Hospitali ya Kidongo chekundu.

Katika hatua za awali zitakazoanzia mwaka huu, kliniki ya afya ya magonjwa ya akili  ya Hospitali ya Mkunduchi itasimamiwa kwa kiasi kikubwa na Hospitali ya Kidongo chekundu na mafunzo yatatolewa katika mwaka wa kwanza wa kuanzishwa huduma  katika Hospitali hiyo.

Hatua  ya pili ya mpango huo itakayoanza mwezi Januari mwakani  ambapo kliniki hiyo itakuwa imeimarika na Hospitali mama ya Kidongo chekundu kuridhika na hatua iliyofikia, Hospitali hiyo itaruhusiwa kujiendesha yenyewe katika masuala mbali mbali ya uongozi na tiba. Kwa mujibu wa makubaliano hayo Hospitali ya Chuo Kikuu cha Haukeland itasimamia na kuimarisha mitaala ya elimu ya magonjwa ya Afya ya akili kwa wafanyakazi wa Hospitali ya Makunduchi ikiwemo kusimamia mafunzo hayo.

Wadau wote kwa pamoja wamekubaliana kuendeleza na kuimarisha  huduma za  magonjwa ya afya ya akili katika kliniki ya Makunduchi kwa mujibu wa misingi ya Shirika la Afya Duniani.   Hospitali ya Makunduchi itakuwa ni  ya pili kutoa huduma za magonjwa ya  Afya ya akili kwa kisiwa cha Unguja na kwa Kisiwa cha Pemba huduma hiyo bado inaendelea kutolewa katika Hospitali ya Chake Chake tu.

SHIRIKA LA VIWANGO TANZANIA (TBS) KWA KUSHIRIKIANA NA JESHI LA POLISI KANDA MAALUMU YA DAR ES SALAAM WAFANYA OPERESHENI YA KUSAKA WAFANYABIASHARA WA NGUO ZA NDANI ZA MITUMBA LEO

0
0
 Askari Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar Es Salaam wakibeba maborota ya mitumba ya nguo za ndani kama sidiria na chupi leo katika soko la Karume katika operesheni ya kukataza kuuza nguo za ndani za mitumba ambapo operesheni hiyo ikiendeshwa na shirika la Viwango Tanzania (TBS)
 Marobota ya nguo za ndani yakipakizwa katika magari ya polisi leo wakati shirika la viwango Tanzania Kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Nchini wakati walipoendesha operesheni Kataza kuuza nguo za ndani ambazo zishatumika(mitumba)
 Askari Polisi wakiendelea na operesheni hiyo katika Soko la Karume huku wafanyabiashara wa Sokoni hapo wakishuhudia zoezi hilo
 Magari ya polisi yakiwa Yamebeba Marobota ya Mitumba ya Nguo za Ndani mapema leo katika Soko la Karume katika Operesheni kataza kuuza nguo za ndani za mitumba
 Msafara kuelekea katika Kituo cha Polisi cha Msimbazi kwaajili ya kupeleka Mzigo uliokamatwa wa nguo za ndani zilizotumika almaarufu kama mitumba kwaajili ya kuteketezwa na moto wakati wa operesheni kataza kuuza mitumba ya nguo za ndani
 Msafara wa polisi ukielekea Kituo Cha Msimbazi mapema leo mara baada ya Kukamata wafanyabiashara na bidhaa zao za nguo za ndani za mitumba
 Msafara ukiingia Katika kituo cha Msimbazi 
 Mzigo Ukiwasilishwa katika kituo cha Polisi Cha Msimbazi Kwaajili ya kwenda kuteketezwa na Moto
 Mmoja wa Wafanyakazi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) akishusha sidiria za mitumba ambazo zimekamatwa leo katika operesheni kata kuuza nguo za ndani za mitumba
 Mzigo Ukishushwa mara baada ya kufikishwa katika Kituo Cha Polisi Cha Msimbazi
Afisa Habari wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Bi Roida akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kukamata marobota ya nguo za ndani ambazo zimeshatumika wakati Nguo hizo zilishapigwa marufuku kuuzwa nchini.Picha zote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog

Ratiba ya Mazishi ya Marehemu Mzee George Bakari Liundi

0
0

MBUNGE LITA KABATI AELEZA ALIYOYAFANYA HADI SASA KATIKA UBUNGE

0
0
 Mbunge wa Viti maalum Jimbo la Iringa akizungumza na wananchi hawapo pichani kuelezea kazi alizofanya katika jimbo la Iringa katika mkutano uliofanyika katika kiwanja cha Mwembetogwa.
 baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano wa ccm katika kiwanja cha mwembetogwa
baadhi ya wanachama vijana wa chadema waliorudisha kadi wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa ccm wilaya katika mkutano uliofanyika katika viwanja vya mwembetogwa. (picha zote na Denis Mlowe)
=========  ========  ===========
MBUNGE LITA KABATI AELEZA ALIYOYAFANYA HADI SASA KATIKA UBUNGE

Na Denis Mlowe,Iringa

Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati ameeleza kazi mbali mbali alizozifanya katika jimbo la Iringa mjini ikiwa ni pamoja na kujenga kituo cha polisi kilichoko jirani na chuo Kikuu cha Iringa(Tumaini).

Kabati alisema hayo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Mwembetogwa kuwa ataendelea kutatua  kero za wananchi wa Iringa mjini kila anapopata nafasi za kuwahudumia wananchi hao.

Alisema kuwa kamwe hatarudi nyuma katika utendaji na kuwa siku zote atawapigania wananchi wa jimbo la Iringa mjini na kuwa kuwa siku zote kwake atahakikisha anatenda zaidi na amekuwa akijenga hoja za kusaidia Jimbo la Iringa mjini na sio kutoa kejeli kwa serikali akiwa mbungeni .
 
Akielezea mambo ambayo amepata kutekeleza alisema ni pamoja na kusaidia sekta ya elimu vitabu na kompyuta pamoja na kusaidia vikundi vya vikoba katika jimbo hilo la Iringa mjini kusaidia vijana katika harakati za kujikwamua kiuchumi kwa kuanzisha mashindano ya Kabati Star Search.

Kwa upande wake katibu wa CCM Iringa mjini Hassan Mtenga alisema yeye alikuwa jimbo la Freeman Mbowe ambae sasa anatangaza kutogombea jimbo la Hai.

Alisema zama za ubunge wa Mchungaji Peter Msigwa katika jimbo la Iringa mjini umekwisha na sasa atake ataondoka na asipotaka ataondoka.

"Mwambieni mbunge Msigwa wakati  wa kuwadanganya wananchi umekwisha  na lazima sasa awaeleze wananchi  wa jimbo la Iringa mjini  wapi  anapelekea fedha za mfuko wa  jimbo ambazo  zinatolewa kila mwezi na Rais Jakaya  Kikwete"

Hata  hivyo alimuagiza meya  kupambana ili  fedha  kiasi cha Tsh milioni 15  zinazotolewa na rais Kikwete kuona zinafanya kazi gani katika ofisi ya mbunge  pia kutembelea  Hospital  na vituo vya afya  ili  kuona changamoto mbali mbali ndani ya wiki tatu kupeleka majibu katika ofisi yake.

Aidha aliwataja  vijana  kuleta maendeleo  ya mji wa Iringa na sio vijana  wa kutumiwa kuvuruga maendeleo ya mji wa Iringa.

" Nawaombeni  wananchi  kuwa tayari  tumemshika pua mbunge Msigwa na naomba  wananchi tusaidiane kumnywesha panado na  ninamuomba  Msigwa fedha za kiinua mgogo  zake asije  tena katika jimbo la Iringa mjini atumie  kwa kazi nyingine  ....tumeanza mkakati  huu kwa ajili ya kumng’oa Msigwa

ODAMA BAND WANAPIGA AINA ZOTE ZA MUZIKI

0
0


ODAMA BAND from THT
TUNAPIGA HAINA YOTE YA MZIKI
TUNAWEZA KUPIGA SHUGHULI ZOTE kama HARUSI,DINNER,KUSINDIKIZA WASANI WOTE,GOSPEL NA KADHALIKA.
CONTACT: 0653022006
0713623121
0719277372

Viongozi wa Dini Watembelea Mabomba ya Gesi- Mtwara - Lindi

0
0
Ujumbe wa Viongozi wa dini wakiangalia mojawapo ya visima vya nchi kavu vya kusafisha gesi katika eneo la Mnazi Bay, Mtwara.

Viongozi wa dini wametembelea Bomba Jipya la Gesi asilia la Mtwara- Dar es Salaam, mtambo wa kusafisha umeme wa Mnazi Bay na maeneo mengine mbalimbali ya uendelezaji wa gesi asilia katika Mkoa wa Lindi na Mtwara. Viongozi hao wamefanya ziara hiyo ikiwa ni maandalizi kabla ya kufanyika Kongamano la Viongozi wa dini linalotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam tarehe 21 na 22 mwezi Januari, 2014.
Viongozi wa dini wakipata maelezo kutoka kwa Mtaalamu wa Masuala ya gesi na Msimamizi Mkuu wa Mitambo ya kusafisha gesi Mhandisi Sultan Pwaga katika eneo la Madimba kinapojengwa Kiwanda cha kutakasa Gesi.
Mafundi wa Kampuni ya China Petroleum Pipline (CPP) wakiendelea na kazi ya kuunganisha mambomba ya gesi katika kambi ya Madangwa.
Meneja Mradi wa Bomba la gesi kutoka Da r es Salaam hadi Mtwara Mhandisi Kapuulya Musomba akiwaeleza viongozi wa hatua mbalimbali zilizofikiwa katika utekelezaji wa Mradi huo. Katikati ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava. 

LIYUMBA ASHINDA KESI YAKE YA KUKUTWA NA SIMU GEREZANI

0
0
MKURUGENZI wa zamani wa Utawala na Utumishi (DPA) wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba ameshinda kesi ya kukutwa na simu gerezani iliyokuwa inamkabili hivi punde katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam. 

Liyumba ameshinda kesi hiyo baada ya upande wa Jamhuri na mchunguzi wa kesi hiyo kushindwa kuithibitishia mahakama kuhusu tuhuma hiyo. Hukumu hiyo imesomwa na Hakimu Mkazi, Augustina kuanzia saa 3:30 mpaka 4:20 

WAKULIMA WATESWA NA SAMBAZAJI DAWA FEKI ZA KILIMO *WAIOMBA SERIKALI KUWADHIBITI WACHAKACHUAJI

0
0

Baadhi ya dawa zinazodaiwa ni feki






TANGU kuanzishwa kwa kauli mbiu ya kilimo kwanza, kumekuwa na juhudi kubwa zinazofanywa na serikali kuhakikisha wakulima wanaingia kwenye kilimo cha kisasa.


Juhudi hizo zimetiliwa nguvu zaidi katika kuimarisha upatikanaji wa pembejeo za kilimo ili kuwafanya wakulima kuzitumia na kuimarisha kilimo chao.
Baadhi ya dawa zinazodaiwa kuwa feki



Pamoja na juhudiz hizo za serikali, bado kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wakulima juu ya pembejeo hizo za kilimo, ambapo zimekuwa zikilalamikiwa kwa kuharibu mazao.

Kwa mfano, mboleo ya Minjingu imekuwa ikilalamikiwa na  wakulima kwa kile kinachoelezwa kukausha mazao yao na kutokuwa na virutubisho vya msingi kwa ajili ya ukuaji wa mazao.

Katika kuonyesha kuwa kuna matatizo ya msingi katika kupatikana kwa dawa na mbolea kwa ajili ya mazao ya wakulima, kelele nyingi zimekuwa zikisikika pia bungeni kulalamikia mbolea na dawa feki.

Katika Bunge lililopita baadhi ya wabunge waliitaka serikali kushughulikia malalamiko ya wakulima kutokana na mbolea na dawa zinazosambazwa na mawakala kutokuwa na ubora.

Wabunge hao walieleza kuwa pamoja na serikali kuhamasisha wakulima kwa kauli mbiu ya kilimo kwanza lakini kumekuwa na tatizo la mbolea na dawa hizo kutokidhi viwango na matokeo yake kuua mazao.  Katika kujibu malalamiko ya wabunge, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, aliwahi kueleza kuwa serikali inafanyia kazi malalamiko ya dawa na mbolea ya Minjingu.

Wakati hali ikiwa hivyo bungeni, wakulima sehemu mbalimbali nchini wameendelea na kilio cha kupatikana kwa dawa feki za kilimo, kitu ambacho kimezidi kuwaathiri katika kilimo chao.

Kwa mfano, wakati wakulima wakitafuta mbinu za kuongeza tija kwenye kilimo, baadhi ya wafanyabiashara wameingiza na kusambaza dawa bandia.  Dawa hizo ambazo zinatengenezwa na baaadhi ya kampuni zilizoko mkoani Morogoro zimesambazwa kwa kutumia nembo ya kampuni zingine za dawa nchini.

Baadhi ya wakulima wanasema kuwa dawa hizo ambazo hazijapata vibali au kuthibitishwa na mamlaka husika, zinatishia kupunguza ufanisi wa kilimo.  Dawa hizo, zikiwemo aina ya Karate 50ec na Selecron720ec, zinasambazwa kwa wakulima zikiwa na nembo na vifungashio vya kampuni zingine za dawa za kilimo.

Inadawa dawa hizo zinatengenezwa mkoani Morogoro lakini maelezo yaliyopo kwenye kopo yanaonyesha zimetengenezwa nchini Zimbabwe na Malawi. Baadhi ya wakulima mkoani Mbeya wanaeleza kuwa, dawa hizo hazina ubora na zimekuwa kikwazo kwa maendeleo yao katika kuongeza tija ya uzalishaji.

Mkulima John Mwaipopo, mkazi wa wilaya Mbarali, anasema serikali inatakiwa kuwakamata wafanyabiashara wanaouza dawa zisizo na ubora. “Wakulima wananyanyasika kwa kuuziwa dawa na pembejeo zisizo na ubora kila kukicha.Tumewahi kuuziwa saruji iliyochanganywa na chumvi eti ni mbolea, sasa tumeanza kuletewa dawa feki,”anaeleza.

Pamoja na malalamiko hayo, Mkurugenzi Msaidizi wa Afya ya Mimea, kutoka Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Fabian Mkondo, anaeleza kuwa wamepokea malalamiko hayo na wanafanyia kazi.  Kwa jumla, malalamiko juu ya kuwepo kwa dawa na mbolea feki yamechangia kushusha ari ya wakulima na kuondoa dhana ya kilimo kwanza, kitu ambacho kinaweza kuleta athari zaidi katika uzalishaji.

Katika kuendelea kuonyesha namna ambavyo kumekuwa na usambazaji wa mbolea na dawa feki, wakulima wa mpunga, mahindi na mazao mengine katika Kata ya Dakawa na maeneo mbalimba, wilayani Mvomero, nao wamekumbwa na dhahama hiyo.  Wakulima hao wanalalamikia kitendo cha mawakala wa mbolea na pembejeo, kuwasambazia mbolea na dawa feki zinazoua mazao yao kupitia mfumo wa vocha.

Wakulima hao wanaeleza kuwa kumekuwa na ujazo mdogo wa mbolea na mbolea hiyo imekuwa ikiua mazao , kuyadumaza, kubadilisha rangi na hatimaye kukauka.  Katika kusikia kilio cha wakulima hao, Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, anakiri kupokea malalamiko ya wakulima na amekubaliana na malalamiko yao.

Vilevile, Bendera anawataka mawakala kusambaza mbolea na dawa zilizo na viwango tofauti na hivyo serikali itawachukulia hatua kali za kisheria. Mnyororo wa malalamiko ya wakulima juu ya pembejeo zisizo na ubora upo pia kwa wakulima wa  Kata ya Ikuwo wilayani Makete mkoani Njombe, ambao wanalalamikia wafanyabiashara wa pembejeo wanaowauzia mbegu za mazao, zisizokuwa na ubora unaotakiwa kulingana na mazingira yao.

Wananchi hao, walitoa malalamiko hayo , walipotembelewa na wataalamu wa mbegu kutoka kampuni ya Highland Seed Growers mkoani Mbeya. Wanasema baadhi ya wafanyabiashara wa pembejeo, wamekuwa na tabia ya kuwauzia mbegu za mazao ambazo hazina ubora unaotakiwa na kusababisha kukosa mavuno mazuri.

Wanaeleza kuwa kutokana na wengi wao kutokuwa na utaalam mzuri wa kutambua mbegu bora, wamejikuta wakiingia hasara ya kununua na kutumia mbegu zisizofaa zinazouzwa na baadhi ya kampuni.

Ofisa Kilimo wa Kata ya Ikuwo, Olimpa Ukwama, anaeleza kuwa hali hiyo,imetokana na wakulima hao kutotafuta ushauri wa kitaalam kutoka kwa wataalam wa kilimo kabla ya kutumia mbegu na dawa zinazosambazwa na kampuni mbalimbali wilayani humo.

Meneja Masoko wa Kampuni ya Highland Seed Growers, John Mbele, anasema utafiti uliofanywa na kampuni hiyo, umebaini chanzo cha hali hiyo ni ufahamu mdogo wa wakulima kuhusu namna ya kutambua mbegu na dawa bora na kuchelewa kufikishwa kwa pembejeo.

Kwa msingi huo, kuna umuhimu kwa serikali kuchukua hatua za haraka kupambana na mtandao wa kusambaza dawa na mbolea feki kwa wakulima, ili kutekeleza kauli mbiu ya kilimo kwanza kwa vitendo.

Kushindwa kuwabana watu hao wanaosambaza mbolea na dawa feki kwa wakulima kutachangia kushusha uzalishaji na kurudisha nyuma ari ya wakulima katika kujishughulisha na kilimo, kwa kuwa matumaini yao ya uzalishaji yanakuwa yanapotea. 

Kupotea kwa matumaini kwa wakulima kutachangia baadhi yao kuogopa kutumia mbolea na dawa zozote hivyo kurudi kwenye kilimo kwa kijadi ambacho hakitazalisha kulingana na matarajio ya serikali na wakulima.

TBL YATOA MSAADA WA SH. MIL 57 ZA UJENZI WA KISIMA ZAHANATI YA MVUTI DAR

0
0
 Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tganzania (TBL), Kanda ya Ilala, Jesca Njau (kushoto) akimkabidhi Meneja wa Kampuni ya NJ Hydro Drilling, Arnold Mwanga, mfano wa hundi yenye thamani ya sh. mil. 57, ikiwa ni msaada wa kuchimba kisima cha maji katika Zahanati ya Mvuti, wilayani Ilala, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Anayeshuhudia katikati ni Mganga Mfawidhi wa zahanati hiyo, Mary Kalonge.
  Mganga Mfawidhi wa zahanati hiyo, Mary Kalonge (katikati) akitoa shukurani kwa Meneja Mauzo wa TBL, Jesca Njau kwa msaada huo kutoka TBL.
 Mwanafunzi wa Masuala ya Uhusiano aliye katika mafunzo kwa vitendo TBL, Bertha Mturi akiwa amembeba mmoja wa watoto waliofika kupata matibabu katika Zahanati ya Mvuti.
 Wananchi wa Mvuti wakishuhudia Mkandarasi wa Kisima akikabidhiwa msaada wa fedha za kugharamia ujenzi wa kisima hicho.
 Wafanyakazi wa TBL wakiwa na baadhi ya wauguzi wa Zahanati hiyo ya Mvuti baada ya kukabidhi hundi.
 Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tganzania (TBL), Kanda ya Ilala, Jesca Njau (kushoto) akimkabidhi Meneja wa Kampuni ya NJ Hydro Drilling, Arnold Mwanga, mfano wa hundi yenye thamani ya sh. mil. 57, ikiwa ni msaada wa kuchimba kisima cha maji katika Zahanati ya Mvuti, wilayani Ilala, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Anayeshuhudia katikati ni Mganga Mfawidhi wa zahanati hiyo, Mary Kalonge.
 Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Mvuti, Mary Kalonge akitoa shukurani kwa TBL kupatiwa msaada huo muhimu.
 Mmoja wa wananchi wa Kijiji cha Mvuti, akitoa shukurani kwa TBL kwa zahanati hiyo kupatiwa msaada wa kisima cha maji. Kulia ni Bertha Mturi kutoka TBL
Majengo ya Zahanati ya Mvuti. (PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Viewing all 46194 articles
Browse latest View live




Latest Images