Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

Article 2

$
0
0
 Mbunge wa Jimbo la Temeke Dar es Salaam, Abbas Mtemvu akihutubia katika mkutano wa Halmashauri Kuu ya Kata ya YOmbo Kilakala, leo, ambapo aliwaambia kuwa hatolifumbia mamcho  kulitokomeza kundi la  vijana la Mbwa Mwitu linalotishia usalama wa wananchi katika kata hiyo.Kutoka kulia mstari wa mbele ni Diwani wa Viti Maalumu, Wilaya ya Temeke, Mariam Mtemvu. Katibu wa Siasa na Uenezi Wilaya ya Temeke, Rutami  Mabunu,  Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kilakala  na Shomari Lyoto ambaye ni Katibu wa Kata hiyo. PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Kada wa CCM, Mwishehe Kilakala akijitambulisha katika mkutano huo.
 Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Kata ya Yombo Kilakala wakiwa katika mkutano huo


 Ofisa Mtendaji wa Kata ya Yombo Kilakala, Peter Makoye akitoa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama hicho. Kiasi kikubwa cha taarifa hiyo ilikataliwa na wajumbe kwamba haikuwa ya kweli.
 Camillius Haule  ambaye ni Katibu wa Uenezi wa Mtaa wa Kiembe Samaki, akielezea jinsi vijana wahalifu wanaoojiita Mbwa Mwiti wanavyotishia usalama wa wananchi katika kata hiyo.
 Mjumbe wa Kamati ya Mipango Kata ya Yombo Kilakala, Nasir Kinyogoli, akielezea ubadhilifu wa fedha za Ukimwi na Vicoba katika Kata hiyo.
 Asmah Zitiakielezea tatizo la walimu katika Shule ya Msingi Kigunga kuwachapa viboko wanafunzi kwa kukosa fedha za kulipia Tuisheni.
Katibu wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT), Kata ya Yombo Kilakala,FatumaMgendo akielezea masikitiko  kuhusu kitendo cha walimu wa Shule ya Msingi kwachapa viboko wanafunzi kwa kukosa hela ya kulipia tuisheni.

ziara ya ujumbe wa Algeria walipotembelea machimbo ya Tanzanite Mererani na kiwanda cha Mbolea cha Minjingu.

$
0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa Migodi katika Wizara ya Nishati na Migodi ya Algeria Bw. Bourroudj Mohamed Tawar (aliyenyoosha mkono) akiangalia mwamba uliotokana na masalia ya ndege aina ya flamingo, yanayozalisha Mbolea ya kupanda ya Minjingu. Mwenye koti jeupe ni  Mkuu wa uzalishaji wa kiwanda cha Minjingu Bw. Inyana Mwambete, katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda hicho  Bw. Tosky Hans na wa kwanza kulia ni Kamishna wa Madini Wizara ya Nishati na Madini Bw. Ally Samaje.

 Mkurugenzi Mkuu wa Migodi katika Wizara ya Nishati na Migodi ya Algeria Bw. Bourroudj Mohamed Tawar (aliyenyoosha mkono) akiangalia mwamba uliotokana na masalia ya ndege aina ya flamingo, yanayozalisha Mbolea ya kupanda ya Minjingu. Mwenye koti jeupe ni  Mkuu wa uzalishaji wa kiwanda cha Minjingu Bw. Inyana Mwambete, katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda hicho  Bw. Tosky Hans na wa kwanza kulia ni Kamishna wa Madini Wizara ya Nishati na Madini Bw. Ally Samaje.

 Mkurugenzi Mkuu wa Migodi katika Wizara ya Nishati na Migodi ya Algeria Bw. Bourroudj Mohamed Tawar (aliyenyoosha mkono) akiangalia mwamba uliotokana na masalia ya ndege aina ya flamingo, yanayozalisha Mbolea ya kupanda ya Minjingu. Mwenye koti jeupe ni  Mkuu wa uzalishaji wa kiwanda cha Minjingu Bw. Inyana Mwambete, katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda hicho  Bw. Tosky Hans na wa kwanza kulia ni Kamishna wa Madini Wizara ya Nishati na Madini Bw. Ally Samaje.

Mkurugenzi Mkuu wa Migodi katika Wizara ya Nishati na Migodi ya Algeria Bw. Bourroudj Mohamed Tawar (aliyenyoosha mkono) akiangalia mwamba uliotokana na masalia ya ndege aina ya flamingo, yanayozalisha Mbolea ya kupanda ya Minjingu. Mwenye koti jeupe ni  Mkuu wa uzalishaji wa kiwanda cha Minjingu Bw. Inyana Mwambete, katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda hicho  Bw. Tosky Hans na wa kwanza kulia ni Kamishna wa Madini Wizara ya Nishati na Madini Bw. Ally Samaje.


Ujumbe wa Algeria umepata nafasi ya kutembelea machimbo ya Tanzanite Mererani katika Kampuni ya TanzaniteOne ambapo walitembelea sehemu mbalimbali ikiwemo za uzalishaji, usafishaji, na uchongaji madini ya Tanzanite. 

Vilevile, wakiwa Mkoani Kilimanjaro walipata fursa ya kutembelea Kiwanda cha kuzalisha mbolea ya kupandia cha Minjingu ambapo walijionea namna mbolea hiyo inavyozalishwa kwa kutumia masalia ya ndege aina ya Flamingo waliokuwepo eneo hilo miaka mingi iliyopita. 

Aidha, ujumbe huo ulipata fursa ya kutembelea mbuga za wanyama katika bonde la ngorongoro ambapo wamehitimisha ziara yao nchini ya kujifunza na kubadilishana uzoefu na nchi ya Tanzania katika sekta za gesi, mafuta,umeme na madini.

TAARIFA YA MSIBA:MDAU TAJI LIUNDI ANATANGAZA KIFO CHA BABA YAKE MZAZI JAJI GEORGE BAKARI LIUNDI.

$
0
0
TAARIFA YA MSIBA: Nasikitika kutangaza kifo cha Baba Mzazi Jaji George Bakari Liundi kilichotokea ghafla leo Jumapili saa 7 mchana. 
Msiba upo KEKO JUU KJ 60(Nyuma ya Mgulani Shule ya Msingi). 
Taratibu za mazishi zinaendelea. 
Mawasiliano ya Taji Liundi: 0787 888 799

RADIO MBAO PRESENTS DJ KVELLI

$
0
0

This is my new Mix..I did the mix live on air on Radio Mbao ( www.radiombao.com), The Mix is dedicated to all listeners of Radio Mbao in 103 countries.The mix has bongo flava bangers from year 2013 and some few Kenyans bangers too. You can find my mix on hulkshare ,soundcloud, & Mixcrate.. Justsearch #RadioMbaoEndOfTheYearMix#EndOfTheYearMix #RadioMbao #DjKvelli



NAFASI ZA KAZI

$
0
0
Neema  Herbalist  ni  wauzaji  na  wasambazaji  wa  dawa mbalimbali  zitokanazo na  mimea.
 Tunatangaza  nafasi  za  kazi  ya  UWAKALA WA USAMBAZAJI   WA  DAWA  ZETU  kwa  vijana  wa  kitanzania wenye  sifa  zifuatazo :
i.                    Elimu  ya  kuanzia  kidato cha  nne  na  kuendelea.
ii.                 Awe  mkaazi  wa  Dar  Es  salaam.
iii.              Awe  maridadi , mwaminifu na  anaye  jituma .

MAJUKUMU  YA  KAZI :  Kuchukua  bidhaa  kutoka  kwetu  na kuzisambaza   kwa  wakala  wetu  mkuu  na  kwenye  maduka ya  madawa  yaliyopo  katika  kata  mbalimbali  za  jiji  la Dar  Es salaam.
Mwisho  wa  kupokea  maombi  ni  tarehe   31 JANUARY  2014.

Kazi  kuanza  rasmi  tarehe  03  FEBRUARI  2014.

Tuma  maombi  yako  kupitia  barua  pepe  yetu ambayo  ni : neemaherbalist@gmail.com

Kwa  maelezo  zaidi, tembelea : www.neemaherbalist.blogspot.com

Tahadhari ya Mvua Kubwa na upepo mkali

MWENYEKITI WA CCM TAIFA,DKT.JAKAYA KIKWETE AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU CCM MJINI ZANZIBAR

$
0
0
 Mwenyekiti wa CCM Taifa Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akifungua kikao cha siku moja cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kilichofanyika leo mjini Zanzibar ,pamoja na mambo mengine Kamati Kuu imeipongeza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, na wananchi wake kwa kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari wa mjini Zanzibar kuhusu yale yaliojiri kwenye kikao cha Kamati Kuu ya Halmashuri Kuu ya CCM Taifa na pia kutangaza uteuzi wa Ndugu Mahmoud Thabit Kombo kuwa mgombea wa uwakilishi wa jimbo la Kiembesamaki.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimtambulisha mgombea wa nafasi ya uwakilishi wa jimbo la Kiembesamaki Ndugu Mahmoud Thabit Kombo mara baada ya Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kumteua kuwa mgombea wa nafasi uwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki kwa tiketi ya CCM.Picha na Adam H. Mzee.
======  ======  ======

Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imekuwa na kikao cha siku moja leo tarehe 13/01/2014 mjini Zanzibar chini ya uongozi wa Mwenyekiti wa Taifa wa CCM Dr. Jakaya Kikwete.

Pamoja na mambo mengine Kamati Kuu imeipongeza sana Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, wazanzibari na watanzania kwa ujumla kwa kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Aidha Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imepongezwa kwa maandalizi mazuri na ya kufana ya sherehe hizo.

Kamati Kuu imetambua na kupongeza hatua kubwa ya maendeleo iliyofikiwa tangu mapinduzi mwaka 1964 mpaka leo. Wito umetolewa kuyalinda na kuyaendeleza mema yote yatokanayo na mapinduzi hayo na mafanikio yaliyoletwa na serikali inayoongozwa na CCM.

Aidha Kamati Kuu imemteua Ndg. Mahmoud Thabit Kombo kuwa mgombea wa uwakilishi jimbo la Kiembesamaki kupitia CCM.

Kesho mgombea huyu wa CCM atachukua fomu za tume za kugombea. Uzinduzi wa kampeni za CCM utafanyika tarehe 22/01/2014 kwenye viwanja vya Kiembesamaki ambapo mgeni rasmi atakuwa Mjumbe wa Kamati Kuu na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndg. Mohamed Gharib Bilal.

Kampeni za CCM zitafungwa tarehe 01/02/2014 huko Chukwani na mgeni Rasmi atakuwa Mjumbe wa Kamati Kuu na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Ndg. Balozi Seif Ali Idi.

Kampeni itaendeshwa na Kamati ya Siasa ya wilaya ya Dimani viongozi na wanachama wa wilaya husika, na ngazi zingine za Chama zitashirikiana na ngazi ya wilaya kuhakikisha CCM inashinda tena jimbo hili.

Kamati Kuu inawatakia kila lakheri kwenye kampeni na hatimaye uchaguzi huo. Kampeni na hata upigaji kura uendeshwe kwa amani na utulivu kama ulivyo utamaduni wetu.

Imetolewa na;
Nape Moses Nnauye
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi.

NEWS ALERT.AJALI MBAYA YA BASI LA SHABIBY NA PRINCES MUNAA

$
0
0

Abiria 28 wakiwemo watoto wanne wamejeruhiwa baada ya basi walilokuwa wamesafiria la Kampuni ya Shabiby kugongana na Lori tupu la mafuta na kupinduka katika kijiji cha Kisaki umbali wa kilometa 10 kwenye Barabara Kuu ya kutoka Mjini Singida kwenda Dodoma.


Taarifa zilizopatikana kwenye eneo la tukio zimeelezwa kuwa Basi hilo lenye namba T930BUW aina ya Yutong  lililokuwa likiendeshwa na Dereva wake ambaye


amekimbia mara baada ya ajali hiyo linakadiriwa kuwa na abiria wapatao 48 lilipata ajali hiyo jana saa 6:50 mchana wakati lilipojaribu kulipita lori hilo upande wa kulia .


Taarifa hizo ambazo pia zimethibitishwa na Mkuu wa Wilaya ya Singida zinasema kuwa kitendo hicho kilisababisha kuligonga Lori hilo RAA 496N aina ya MECEDES BENZ lililokuwa likitokea Mjini Kigali nchini Rwanda kwenda Dar es Salaam likiwa na dereva wake Barimana Benjamini (37) na kuanguka upande wa kulia wa Barabara na kujeruhi abiria wake .Habari picha kwa hisani ya superfeoblog.com







Kampuni ya City Ridez Travels & Tours inakuletea suluhisho la tatizo la usafiri mijini kwa gharama nafuu.

$
0
0
Tungependa kukukaribisha kwenye huduma yetu ya Usafiri jijini kwa kutumia mabasi maalumu kwa sababu kuu tatu au zaidi.

1. Tunaamini wafanyakazi wanaotumia muda mrefu njiani kwa kutafuta usafiri, au kwa kukwama kwenye foleni wakati wakielekea makazini, huwa wanafika wamechoka tayari na hivyo kupelekea kuwa na umakini wa kiwango cha chini pamoja na kupunguza uzalishaji.

2. Kukaa kwenye foleni kwa muda mrefu wakati ukiendesha gari, inaaminika kuwa ni mazingira yanayosababisha kiwango cha juu sana cha msongo, na ni sababu ya watu wengi kutokuwa na furaha kwa muda mwingi wawapo makazini.

3.Gharama za kuendesha gari kwa siku moja kwenye jiji la Dar es Salaam, kwenda kazini na kurudi zinakisiwa kuwa zaidi ya Tsh. 30,000/= kwa gari ya kawaida yenye viti vitano. Hii inamaana kuwa kwa kila kiti kimoja cha gari lako, kinakugharimu Tsh. 6000/=. Endapo unatumia kiti kimoja tu cha gari lako, inamaanisha unapoteza Tsh. 24,000/= kwa kila siku unapotumia gari lako kwenda kazini, kwa siku 20 za kazi ni sawa na Tsh. 480,000/= na ni zaidi ya Tsh. 5,760,000/= kwa mwaka zinazopotea kwa wewe kuendelea kutumia gari lako binafsi kwenda kazini na kurudi.

Kampuni ya City Ridez Travels & Tours ingependa kukuletea suluhisho la matatizo haya kwa ujumla wake. Lengo letu ni kupunguza idadi ya magari binafsi yanayotembea muda wa kwenda na kurudi kazini kwa kukuletea usafiri maalumu, wenye starehe, wakutegemewa na kwa gharama nafuu.

Hapa City Ridez Travels & Tours tunahusika na usafiri maalumu wa mabasi, kwa minajili ya kutoa njia mbadala ya kusafiri ukiwa ndani jiji. Kimsingi tukizingatia zaidi kwenye Ubora, Uaminifu na Usalama.

Njia tunazotoa Huduma kwa sasa.

TEGETA - POSTA - TEGETA (kupitia MWENGE)
GONGO LA MBOTO - POSTA - GONGO LA MBOTO
MBEZI KIMARA - POSTA - MBEZI KIMARA
MBEZI AFRICANA - POSTA - MBEZI AFRICANA  (kupitia Mbezi chini)
MBAGALA - POSTA - MBAGALA
TABATA SEGEREA - POSTA - TABATA SEGEREA
MWENGE - POSTA - MWENGE (kupitia Sinza)
Usafiri wa raha mustarehe.

Njia zinazotazamiwa baadae
MBAGALA KIJICHI - POSTA - MBAGALA KIJICHI
KUNDUCHI - POSTA - KUNDUCHI

Njia nyingine zitaongezwa kwa kuzingatia upatikanaji wa wateja na mahitaji

Gharama / Bei
Bei zetu zinatazamiwa kuwa ni bei nafuu kwa kua kila mtu analipa kwa kile anachotumia peke yake. Tiketi zetu zinapatikana kwa Tsh. 5500/= kwenda na kurudi kwa siku kwa njia fupi, na Tsh. 11000/= kwenda na kurudi kwa njia ndefu. Pia unaweza kujipatia tiketi za kwenda peke yake au kurudi kwa Tsh. 3300/=. Na kwa wale ambao wangependa kujipatia tiketi za wiki nzima (yaani siku 5) au mwezi mzima (yaani siku 20) tiketi hizi zina unafuu wa aslimia 10%. Tiketi zinapatikana kwa mawakala wetu au kwa kutumia simu yako ya mkononi. Au piga simu +255 715 400 666.

Tiketi hizi zinamaanisha kuwa tutakuchukua kutoka karibu na nyumbani kwako kukuleta mjini asubuhi na kukurudisha jioni, na kama unakaa mbali na barabara kuu, tutakupatia sehemu salama ya kuegesha gari lako bila wasiwasi.

Muda.
Tunahakikisha unakua mjini kila siku asubuhi kabla ya mida ya saa 1:00 asubuhi, hivyo basi tutakua tukiondoka maeneo tofauti jijini kwa muda tofauti kulingana na umbali na miundo mbinu ya eneo husika, (kuanzia mida ya 11:00 asubuhi na 12:30 asubuhi) vilevile tunatoa safari ya 7:30 asubuhi kwa wale wanaopenda kuchelewa kuingia mjini. 

Kwa jioni magari yanaondoka kuanzia saa 11:00 jioni na 11:30, vile vile kuna magari ya 1:30 usiku kwa wale wanaochelewa au wafanyakazi wa mabenki. (Unaweza kuwasiliana na mtoa huduma wetu ili kuangalia upatikanaji wa safari kuendana na mahitaji yako. +255 715 400 666)

Tiketi
Tunatoa aina mpya ya tiketi zinazowekwa QR codes kwa ajili ya usalama, na unaweza kuzipata kwa mawakala wetu, au kwa kununua mwenyewe kupitia namba yetu ya simu +255 687 644452 na utatumiwa tiketi yako kwenye simu yako ya mkononi, au barua pepe au hata kupitia mitandao ya kijamii baada ya kukamilisha malipo, na utatakiwa kuonyesha tu QR codes uliyotumiwa kwa ajili ya uthibitisho. Ni rahisi kiasi hicho. 

Kumbuka hautaweza kulipia ukiwa ndani ya gari, na kuna idadi maalumu ya wateja watakaohudumiwa kwa siku, hivyo ni muhimu kama utaweka siti yako mapema kuepuka usumbufu.

Kwa maelezo zaidi unaweza kutembelea ofisi zetu zilizoko kwenye jengo la NSSF Hifadhi house gorofa ya Saba, karibu na mnara wa askari, au ukapiga simu namba. +255 222 114 308 Mobile: +255 712 823 505 au barua pepe: cityridezsales@gmail.com, au tembelea kuras wetu wa facebook:www.facebook.com/cityridez.

KUNA TAARIFA YA UZUSHI INASAMBAZWA KUPITIA SMS KUHUSIANA NA TMA KUTOA TAHADHARI YA TSUNAMI

$
0
0
Dear wadau, 

Kuna taarifa inayosambazwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu za mkononi (SMS) kuhusiana na TMA kutoa tahadhari ya Tsunami

Taarifa hizo sio za kweli, uionapo ujumbe huu upuuzie kwa kuwa sio taarifa sahii, ni taarifa ya upotishaji

Taarifa rasmi ni kama ilivyotumwa awali kuhusiana na upepo mkali kwa Ukanda wa Bahari ya Hindi na Mvua kubwa.

Ujumbe huo unasomeka kama hivi:

TAHADHARI ya Tsunami: Kuanzia saa moja usiku
Tsunami itafika Tanzania na mawimbi yatakuwa makubwa
kuanzia muda huo. Taarifa zaidi itatolewa na Mamlaka ya
Hali ya Hewa Tanzania wakati wowote kuanzia sasa, kwa
mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk. Agness Kijazi.

Tunapenda kuwataarifu wadau wetu kuwa ili kutoa taarifa sahihi ni vizuri kuwasiliana na Ofisi zetu kwa maelezo ya kina zaidi kuepusha mkangamanyo kwa wananchi

Asante tena kwa ushirikiano wako,

Nakutakia Sikukuu njema ya Maulid,

Monica Mutoni
Ofisi ya Uhusiano
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.

KAMATI KUU YA CCM YATEUA MGOMBEA UBUNGE WA CCM JIMBO LA KIEMBESAMAKI ZANZIBAR

$
0
0


NAPE NNAUYE
ZANZIBAR, Tanzania.
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya taifa ya CCM,  imefanya kikao cha siku, Januari 13, 2014 mjini Zanzibar chini ya Mwenyekiti wa CCM Dk. Jakaya Kikwete na kujadili mambo kadhaa ikiwemo kumteua Mahmoud Thabit Kombo kuwa mgombea wa kiti cha Uwakilishi wa jimbo la Kiembesamaki.

Taarifa iliyotolewa leo mjini Zanzibar na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema, mgombea huyu wa CCM kesho, Jumanne, Januari 14, 2013, atachukua fomu za tume za kugombea.

Nape amesema uzinduzi wa kampeni za CCM utafanyika tarehe 22/01/2014 kwenye viwanja vya Kiembesamaki ambapo mgeni rasmi atakuwa Mjumbe wa Kamati Kuu na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mohamed Gharib Bilal.

"Kampeni za CCM zitafungwa tarehe 01/02/2014 huko Chukwani na mgeni Rasmi atakuwa Mjumbe wa Kamati Kuu na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Ndg. Balozi Seif Ali Idi", alisema Nape na kuongeza;

"Kampeni itaendeshwa na Kamati ya Siasa ya wilaya ya Dimani viongozi na wanachama wa wilaya husika, na ngazi zingine za Chama zitashirikiana na ngazi ya wilaya kuhakikisha CCM inashinda tena jimbo hili na Kamati Kuu inawatakia kila lakheri kwenye kampeni na hatimaye uchaguzi huo. Kampeni na hata upigaji kura uendeshwe kwa amani na utulivu kama ulivyo utamaduni wetu".

Nape alisema, pamoja na uteuzi huo, Kamati Kuu pia imeipongeza sana Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla kwa kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar na kufanikisha sherehe zake kwa ufanisi kutokana na maandalizi mazuri.

Kamati Kuu imetambua na kupongeza hatua kubwa ya maendeleo iliyofikiwa tangu mapinduzi mwaka 1964 mpaka leo. Wito umetolewa kuyalinda na kuyaendeleza mema yote yatokanayo na mapinduzi hayo na mafanikio yaliyoletwa na serikali inayoongozwa na CCM.
Mwenyekiti wa CCM, Dk. Rais Jakaya Kikwete, akifungua kikao cha Kamati Kuu ya CCM, leo katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM, Kisiwandui mjini Zanzibar. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar), Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein na Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana. (Picha na Adam Mzee)

MKUU WA MKOA WA RUKWA INJINIA STELLA MANYANYA AVAMIA KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI WIILAYA YA NKASI, AWATAKA KUBORESHA MAKUSANYO YA MAPATO YA HALMASHAURI YAO

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akihutubia baraza kuu la madiwani wa Wilaya ya Nkasi (Full Council) lililokua kwenye kikao cha kujadili na kupitisha bajeti ya fedha ya mwaka 2014/2015 na kupitisha sheria ndogondogo za halmashauri. Katika hotuba yake aliwataka madiwani na viongozi wa halmashauri na wilaya ya Nkasi kushirikiana kwa pamoja na kuweka pembeni itikadi zao katika kuunda vyanzo vipya vya mapato na kuvisimamia kwa kuwekeana mikakati maalum ya makusanyo kwa kila kijiji, kata, tarafa, halmashauri na Wilaya kwa ujumla. Alisema halmshauri hiyo haitaweza kuendelea kwa kuendelea kuwa tegemezi kutoka Serikali kuu na badala yake waongeze makusanyo ya ushuru na mapato yasaididie katika mipango ya kujiendeleza. Kikao hicho kilipitisha bajeti ya Tsh Bilioni 25.4.Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Kimanta akizungumza katika kikao hicho ambapo alisisitiza juu ya kuboresha na kusimamia upatikanaji wa mapato ya halmashauri ambayo pamoja na mambo mengine yatasaidia katika kuboresha miundombinu ya barabara katika Wilaya hiyo ambayo imekua ndio kilio kikubwa kwa wananchi wa Wilaya hiyo. Kulia ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Albinus Mugonya.Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Ndugu Kimulika Galikunga akitoa ufafanuzi wa baadhi ya mambo katika kikao hicho. Katikati ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Ndugu Peter Mizinga.
Wakuu wa Idara wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi waliohudhuria kikao hicho.Picha ya pamoja kati ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa na madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Nkasi. (Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @Rukwareview.blogspot.com)

WANANCHI UKONGA WAGOMEA FIDIA KIDUCHU BOMBA LA GESI

$
0
0

Mwenyekiti wa Kamati ya kufatilia malalamiko ya wananchi wa mji mpya relini Bw. Omari Msusa kushoto akihojiwa na vyombo vya habari kuhusu fidia wanayotakiwa kulipwa huku Mbunge wa Jimbo la Ukonga Dar es Salaam, Bi,Eugen Mwaiposa akimsikiliza kwa makini .

mbunge wa jimbo la Ukonga Dar es salaam, Bi,Eugen Mwaiposa (kulia) akisikiliza malalamiko ya wananchi wea eneo la Mji Mpya Relini jimboni kwake jana wakilalamika kutaka kulipwa fidia ndogo ambazo hazilingani na thamani ya nyumba zao.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mjipya Relini,Ilala Dar es Salaam Bw. Geofrey Chacha (aliyesimama) akitoa malalamiko ya wananchi mbele ya mbunge wa Jimbo la Ukonga, Bi. Eugen Mwaiposa wa pili kushoto wanaolalamikia kuhusu tahmini ya fidia ndogo inayopitishwa ili kupisha upanuzi wa bomba la gesi linalotoka Mtwara. 

Na Ripota wetu.

WANANCHI wa Mji mpya Relini wilaya ya Ilala waliopitiwa na mradi ya bomba la gesi ya Mtwara wamemuomba Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Bi. Eugen Mwaiposa awasilishe bungeni hoja ya kukataa mradi huo kutokana na kupunjwa fidia ya nyumba na mali zao wanayotakiwa kulipwa.

Wakizungumza na kutoa maazimio hayo katika mkutano wa dharura walioitisha na kuhudhuriwa na mbunge wao, wananchi hao walisema awali walikubali mradi huo kwa manufaa ya taifa lakini baada ya kuletewa dodoso la kutathmini mali na nyumba zao wamegundua kuna ujanja unatumika kuwanyima haki na kuwafanya kuwa masikini maisha yao yote.

Waliendelea kudai kuwa mpaka sasa hawajui serikali imemkabidhi nani jukumu la kuthamini nyumba zao kwani kampuni nyingi za ujanja ujanja zimejitokeza kutaka kuwathamini lakini kwa kiwango cha chini ambacho hakiwezi kumpatia makazi mengine.

Bw. Josephat Haule alisema waathirika wenzao katika Kata za Kivule, Pugu Kwalala na Mbande wao wamethaminiwa vizuri na wanatarajia kupata fedha za kujenga nyumba nyingine kutokana na gharama kuwa juu lakini wao nyumba iliyojengwa kwa sh. mil 57 anathaminiwa alipwe sh. mil. 11 na nyumba zenye thamani ya sh. mil. 10 wanataka alipwe sh, mil 3.

Bw. Robert Pius alisema kutoka taarifa ya Serikali itolewe ya  kutangaza kupitisha bomba la gesi eneo hilo waathirika wote walisimamisha uendelezaji wa makazi hayo na kusubiri kupewa haki zao lakini ni mwaka wa pili sasa hakuna taarifa zenye ukweli zinazowafikia hivyo kuwafanya waishi kama wanya aina ya digidigi porini,
Mbunge Mwaiposa akizungumza na wananchi hao aliahidi kushirikiana nao kujua ukweli wa kampuni gani iliyopewa jukumu la kuthamini nyumba na mali zao kwani anachofahamu ni kuwa Kampuni ya Kilwa Energy iliyopewa jukumu hilo awali hakiwa na uwezo wa kifedha kuwalipa wananchi kwa wakati.

Aliahidi kushirikiana na Kamati ya wananchi hao kushughulikia madai yao kwenda Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwenda kumuona Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, kwenda kumuona Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na ikishindikana wanakwenda kumlalamikia Rais Jakaya Kikwete.

Alisema wananchi wanateseka kwa vile kuhamisha makazi kutoka sehemu moja kwenda nyingine kunarudisha maendeleo nyuma na kama anavyofahamu Serikali ya Rais Kikwete ni sikivu na yenye kufanya kazi kwa ufasaha hajui sababu za wananchi wake kushindwa kutimiziwa ahadi zao katika kiwango kinachostahili.


"Wananchi wangu wanadhiki, wanashida ya fedha lakini si kwa malipo kidogo kiasi hicho, tunapiga picha tuoneshe umma thamani ya nyumba na kiasi wanachotakiwa kulipwa ili wakaendelee na maisha yao sehemu nyingine" alisema Bi. Mwaiposa.


Bi. Mwaiposa alikiri kuona nyumba zilizothaminiwa kwa fedha kidogo ambazo haziwezi kununua kiwanja kingine ambavyo kwa sasa katika maeneo hayo vinauzwa kati ya sh. mil. 10 mpaka sh. mil. 15 kwa kiwanja cha nusu hekari.

RAIS KIKWETE MGENI RASMI KONGAMANO LA WASANII IJUMAA

$
0
0

 Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Twalib 'Teacher' 
(kushoto)
 
MTANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) umeandaa kongamano la umoja na mshikamano linalofanyika Januari 17 (Ijumaa) kwenye viwanja vya hoteli ya Lamada ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais Jakaya Kikwete. 

Mwenyekiti wa SHIWATA,Caasim Taalib alisema madhumuni ya kongamano hilo ni kuhamasisha umoja kati ya wasanii ili kujenga uwezo na nguvu ya kumaliza matatizo yao ya kiuchumi.

Alisema wasanii, waandishi, wa habari na Vijana wanashindwa kumaliza matatizo yao ya kiuchumi bila kuombaomba au kusubiri misaada kutoka kwa wafadhili mbalimbali.  "Wasanii inatubidi tujifunze kujitegemea na tuache kusubiri wafadhili au serikali ituchangie hata kwa matibabu na katika mazishi yetu" alisema Taalib.

Katika kongamano hilo Shiwata itazingua mpango maalum ambao utawezesha wasanii kupata misaada ya fedha za kutengeneza filamu,kurekodi muziki,kuwezesha timu na vikundi mbalimbali kununua vifaa vya ichezona kuwapatia nauli ya usafiri ndani na nje ya nchi kwa shughuli za michezo na sanaa. 

Katika Mpango huo Shiwata pia itatoa fedha kwa mrithi wa msaniii kamaatakufa, akiugua au kulazwa kwa siku tatu katika hospitali zinazotambuliwa na Serikali.

Alisema Shiwata pia itatoia misada kwa wasanii wanaotaka kuoa au kuolewa ambako kila mwanachama atachangia sh. 1,000 kwa ajili ya kugharamikia mazishi ya msanii kununua sanduku n usafiri. 

Alisema Shiwata itakusanya zaidi ya sh. Mil.7 kutoka kwa wanachama 7,000 na wasanii watajiunga kwa sh. 20,000 ambazo zinaweza kulipwa kwa awamu tatu kutokana na uwezo wa msanii.

Sjiwata ina ekari 300 za makazi katika kijiji cha Mwanzega Mkuranga ambapo hivi sasa kuna nyumba 40 zilizojengwa kwa nguvu ya wasanii wenyewe na ekari 500 za kilimo.

IKOTA SUPER D ATIMIZA MIAKA 11 YA KUZALIWA LEO

$
0
0

 LEO NI SIKU YA KUZALIWA KWA MTOTO ZAINABU MHAMILA 'IKOTA' SUPER D AMBAPO ANATIMIZA MIAKA  11 TANGIA AZALIWE PICHANI AKIWA NA BABA YAKE MZAZI RAJABU MHAMILA 'SUPER D' AMBAYE NI KOCHA WA KIMATAIFA WA MCHEZO WA MASUMBWI NCHINI

HILI NDILO DAMPO JIPYA NA LA KISASA LA KUTUPIA TAKATAKA LINALO JENGWA JIJINI MBEYA

$
0
0
Huu ndio mwonekano wa Dampo hilo la kisasa kwa upande wa juu ambapo ujenzi upo katika hatua za mwishoni 
 Hili ni eneo ambapo magari yaliyobeba takataka yatakua yanaingia na kumwanga taka taka hizo .
 Mwonekano wa Karibu wa ndani wa Dampo hilo la kisasa Jijini Mbeya 
 Hii ni Chemba pekee ambayo ni maalum kwa ajili ya kupitishia takataka zenye kimiminika, pia kupitishia takataka ambazo zitakuwa zimesagwa na kupelekwa katika Bwawa maalum litakalo tumika kutengenezea umeme pamoja na mabaki mengine ya takataka yatatumika kutengenezea mbolea 
 Hapa Ndipo Takataka hizo zitakuwa zikitelemkia 
 Mwonekano zaidi wa Dampo hilo la kisasa kwa ndani ambapo kwa sasa wameweka kokoto ndogondogo chini  huku ujenzi ukiendelea .


 Kingo pembezoni mwa Dampo hilo la kisasa .
 Hii ni sehemu maalum ambayo itajengwa kisasa kwa ajili ya kuoshea magari baada ya kumwaga takataka 
Hii ni sehemu ya kupaki magari ambayo yatakuwa yakitupa takataka katika dampo hilo la kisasa 

HIVI NDIVYO TAKATAKA ZILIVYOKUWA ZIKITUPWA KABLA YA DAMPO HILO KUJENGWA KATIKA ENEO HILO.


Pichani ni jinsi takataka kutoka pande mbalimbali za jiji la Mbeya zilivyokuwa zikitupwa kabla ya Dampo hilo la kisasa kujengwa katika eneo hilo jirani na Mlima Nyoka Jijini Mbeya.

Dampo hilo la kisasa linategemea kuanza kufanya kazi hivi karibuni

PICHA ZOTE NA MBEYA YETU BLOG.

RAIS KIKWETE AMTEMBELEA RAIS MSTAAFU WA ZANZIBAR DKT SALMIN AMOUR

$
0
0
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt Salmin Amouralipomtembelea kumjulia hali nyumbani kwake Zanzibar Jumatatu Januari 13, 2014 baada ya kuhudhuria sherehe za miaka 50 ya Mapinduzi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana  na Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt Salmin Amouralipomtembelea kumjulia hali nyumbani kwake Zanzibar Jumatatu Januari 13, 2014 baada ya kuhudhuria sherehe za miaka 50 ya Mapinduzi. PICHA NA IKULU

Rais Kikwete aagana na Mwakilishi mkazi wa Umoja wa Mataifa ikulu jijini Dar

$
0
0
Mwakilishi mkazi na Mratibu wa Shughuli za Umoja wa Mataifa nchini(Resident Coordinator of the UN System) Bwana Alberic Kacou akimkabidhi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete nakala ya Ripoti ya mwaka Utendaji ya (UNDP) 2012-2013 wakati mwakilishi huyo alipokwenda kumuaga Rais Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo. Bwana Kacou anaondoka baada ya muda wake wa utumishi kumalizika hapa nchini(picha na Freddy Maro).

MPIGIE KURA MUIGIZAJI JUMA RAJAB AWEZE SHINDA TUZO YA AFRIKA MAGIC

$
0
0
Kumbuka kumpigia kura Muigizaji Juma Rajab Rashid a.k.a Cheche ili aweze kushinda tuzo ya Muigizaji Bora wa Kiume kwenye Tamthilia kwa kutuma ujumbe mfupi kwenda namba +2783142100415 au kwenye mtandao- huu  http://goo.gl/o72lu5 !  Kumbuka kuwa unaweza kupiga kura mara nyingi zaidi kila baada ya saa moja. Umoja wetu ni Ushindi kwa Mtanzania mwenzetu

Maisha Plus / Mama Shujaa wa Chakula imerudi tena

$
0
0
Maisha Plus / Mama Shujaa wa Chakula imerudi tena.. 

Zimebaki siku 9 tu za kujaza fomu ya ushiriki.

1. Kijana wa Tanzania, Burundi, Rwanda, Kenya, Uganda mwenye umri wa kati ya miaka 21 - 26, jaza fomu ya kushiriki shindano la Maisha Plus moja kwa moja mtandaoni kwa kubofya hapa

2. Kama wewe ni mkulima mwanamke mwenye umri wa miaka 18 mkazi wa Tanzania ama unamfahamu yeyote, jaza fomu moja kwa moja kwa kubofya hapa --> 
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images