Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo amaliza ziara yake katika Mkoa wa Pwani.

$
0
0

Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Bi.Mwanamvua Mrindoko akimweleza Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof.Elisante Ole Gabriel(mwenyeshati Jeusi) Mpango wa kuendelea kuwawezesha vijana katika halmashauri yake kwa Kutekeleza mipango mbalimbali iliyowekwa ikiwamo kutoa mafunzo kwa vijana na kuongeza bajeti hadi kufikia shilingi milioni 40 kutoka milioni 10 iliyokuwa inatolewa hapo awali kwa mwaka wa fedha 2014-2015,wakati wa Ziara ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo kuangalia shuguhuli mbalimbali za vijana zinazoratibiwa na Wilaya hiyo.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof.Elisante Ole Gabriel(mwenyeshati Jeusi) akiongea na vijana wa kikundi cha bodaboda wakati wakati wa Ziara ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo kuangalia shuguhli mbalimbali za vijana leo katika wilaya ya Kisarawe.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof.Elisante Ole Gabriel(mwenye suti  Jeusi) akiwa katika picha ya pamoja na vijana wa kikundi cha bodaboda kutoka katika wilaya ya Kisarawe, wakati wa ziara yake ya kuangalia shuguhuli mbalimbali za vijana zinazoratibiwa na Wilaya hiyo
Afisa Maendeleo ya Jamii ya Vijana Toka Wilaya ya Mkuranga Bi.Safina Msemo akimweleza Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof.Elisante Ole Gabriel(kushoto) Mafanikio yaliyotokana na Utoaji wa asilimia tano(5%) katika pato la halmashauri kwa ajili ya shughuli za vijana,pia uandaaji  wa kambi ya vijana ya siku 40 watakayoshirikiana na Shirika la Nyumba la Taifa(NHC) kwa ajili ya kutoa mafunzo mbalimbali hasa katika sekta ya ujenzi, wakati wa Ziara ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Mkoani Pwani.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof.Elisante Ole Gabriel akimsisitiza Afisa Maendeleo ya Jamii ya Vijana Toka Wilaya ya Mkuranga Bi.Safina Msemo(kulia) kuendelea kusimamia na kuratibu shughuli zinazotekelezwa na vijana katika Wilaya hiyo ili kuweza kuwasaidia kuleta maendeleo kwa Vijana
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof.Elisante Ole Gabriel akisaini kitabu cha wageni alipotembelea kikundi cha MWAMKO FARM GROUP katika wilaya ya Mkuranga.kulia kwake ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Mkuranga Bi. Joyce Nampesya na Mbele yake ni Mwenyekiti wa Kikundi hicho Bw.Hemed Kassim.
Wanakikundi cha MWAMKO FARM GROUP toka Wilaya ya Mkuranga eneo la Kimanzichana wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof.Elisante Ole Gabriel wakati wa ziara yake Mkoani Pwani.
Sehemu ya Miradi wa Kikundi cha MWAMKO FARM GROUP toka Wilaya ya Mkuranga,mbali na Ufyatuaji wa Matofali pia wanajishughulisha na ulimaji wa Miti ya miembe na uuzaji wa maji kwa wanakijiji wa eneo hilo kutokana na Visima viwili wanavyovimiliki.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof.Elisante Ole Gabriel akiwa katika picha ya pamoja na wanakikundi cha MWAMKO FARM GROUP na baadhi ya Maafisa toka Wilaya ya Mkuraga.
Mwanakikundi cha NAMPULA CARVINGS Bw.Steven Mwidumbi akimuonesha Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof.Elisante Ole Gabriel(mwenye suti NYEUSI) kinyago mfano wa nyani wanaodandia Miti,wakati alipowatembelea leo katika wilaya ya Mkuranga. (Picha zote na Hassan Silayo-MAELEZO)

ASKARI POLISI NA ASKARI MAGEREZA WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA UJAMBAZI WA KUTUMIA SILAHA MBEYA.

$
0
0
Ulinzi ukiimarishwa Baada ya watuhumiwa wa ujambazi kufikishwa mahakamani
Mbele ni mshitakiwa wa nne Mbaruku Hamis akiingia mahakamani
Kutoka kushoto ni mshitakiwa wa pili Elinanzi Eliabu Mshana, Mshtakiwa wa nne Mbaruku Hamis, Mshitakiwa wa tatu Juma Mussa ambaye aliyekuwa Askari Magereza kwa Cheo cha Sajini , Anaefuatia ni Mshtakiwa wa kwanza PC James aliyekuwa Askari Polisi Wilaya ya Mbeya, na wa mwisho ni Mshitakiwa wa Tano Amri Kihenya .
Wa kwanza kushoto aliye vaa shati la Draft ni Dereva Ezekia Matatila (34) pamoja na wasikilizaji
Moja ya Gari lililotumika kufanya uharifu wa unyang'anyi wa kutumia silaha 
Washitakiwa wanne kati ya watano kutoka kushoto juu hadi wa nne wakiwa wanatoka mahakamani chini ya ulinzi mkali.
Mwenye Jaketi la Njano ndiye Mshitakiwa namba moja PC James 
Katikati ni Mke wa mshitakiwa wa tatu ambaye ni Askari Magereza Sajini Juma Mussa, Hata hivyo mwanamke huyo alizirai mahakamani wakati mumewe akiwa kizimbani.


**********************************

ASKARI wawili wa jeshi la Polisi na Magereza pamoja na watu watatu ambao ni raia wa kawaida wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Mbeya wakituhumiwa kwa ujambazi wa kutumia silaha.


Watuhumiwa hao watano kwa pamoja walifikishwa jana mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mbeya, Michael Mteite wakituhumiwa kwa kosa moja la unyang’anyi wa kutumia Silaha kinyume cha Sheria kifungu cha 287 sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.


Mwendesha mashtaka wa Serikali, Archiles Mulisa aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Mshitakiwa namba moja ambaye ni Askari Polisi PC James mwenye namba F8302 wa Wilaya ya Mbeya ambaye kabla ya kufikishwa mahakamani alivuliwa Uaskari baada ya kuhukumiwa kijeshi.


Aliwataja wengine kuwa ni mshtakiwa namba mbili kuwa ni Elinanzi Mshana(22)Mkazi wa Iyela Jijini Mbeya, Askari Magereza mwenye namba B 500 Sajenti Juma Mussa(37) wa Gereza la Ruanda Mbeya,Mbaruku Hamis(29) Mkazi wa Iyela na Amri Kihenya(38) Mkazi wa Iyela.


Akisoma mashtaka yao Mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Michael Mteite, Mulisa alisema watuhumiwa hao walitenda kosa hilo Januari 3, Mwaka huu majira ya saa 11 jioni katika eneo la Mlima Kawetere barabara ya Mbeya Chunya.


Alisema watuhumiwa hao kwa pamoja walitenda kosa hilo kwa kulizuia gari aina ya Pick Up lililokuwa likiendeshwa na Ezekia Matatira (34) Mkazi wa Iyunga Jijini Mbeya ambaye alikuwa na mtu aliyekuwa akifahamika kwa jina la Sreedhar Pasupelet(38) mwenye asili ya Kiasia wakitumia magari madogo mawili ambayo ni GX 100 Toyota Cresta T 782 BEU na Gari linguine ambalo lilikuwa na namba za Chesesi GX 6011832 AINA YA Grand Mark II.


Aliongeza kuwa mbinu iliyotumika ni watuhumiwa ni watuhumiwa hao kutega magogo barabarani huku wakiomba msaada kwa madai kuwa magari yao yameharibika na ndipo baada ya wahanga kusimama waliwapora vitu vyao wakiwa na mapanga ambavyo ni pesa shilingi Milioni 3.5, Mabegi matatu yenye nguo mbali mbali yenye nguo, Kompyuta mpakato, simu aina ya Sumsung yenye thamani ya Shilingi Laki mbili pamoja na simu ya Dereva aina ya Tekno ambayo aliitambua Mahakani na kutumika kama kielelezo.


Hata hivyo watuhumiwa wote kwa pamoja walikana kuhusika na matukio hayo ambapo upande wa Mashtaka ulileta Shahidi mmoja ambaye ni Dereva wa Pick up Ezekia Matatira ambaye aliwatambua washtakiwa wote watano na kuiambia mahakama kuwa siku hiyo ya Tukio aliagizwa na Bosi wake kwamba awapeleke wageni Chunya na ndipo alipotekwa katika eneo hilo huku watekaji wakiagizwa na Maaskari na yeye kufungwa  pingu na kutishiwa na panga.


Aidha kutokana na kesi hiyo Hakimu Mteite aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 15, mwaka huu ambapo upande wa Mashtaka utaleta mashahidi wengine huku watuhumiwa wakirudishwa Rumande baada ya dhamana yao kufungwa.


Ezekiel Kamanga

Mbeya yetu Blog

MDAU BUSHIRI KAUBANIKA NA MWATABU TAMARAWE WAMEREMETA

$
0
0

Bwana Bushiri Kaubanika akiwa na nyuso ya furaha baada ya kufunga pingu za maisha na Mwatabu Tamarawe 
Bwana Bushiri Kaubanika akiwa na nyuso ya furaha baada ya kufunga pingu za maisha na Mwatabu Tamarawe 
Bwana Bushiri Kaubanika akiwa na nyuso ya furaha baada ya kufunga pingu za maisha na Mwatabu Tamarawe 


Bwana Bushiri Kaubanika akiwa na nyuso ya furaha baada ya kufunga pingu za maisha na Mwatabu Tamarawe arusi iliyofungwa Gongolamboto mwisho wa lami na kufuatiwa na tafrilija iliyofanyika Kigogo Dampo Dar es salaam. Maharusi  wote ni walimu wa shule.

BONGO MOVIES YA JOYCE KIRIA YARUDI UPYA KATIKA LUNINGA YAKO!

$
0
0
 Msanii Pastor Myamba akiwa na crew ya Bongo Movies wakionesha alama ya 5 kama ishara ya kutua EATV hivi karibuni.

Ilikuwa inaongozwa na Super woman Joyce Kiria, safari hii inarudi ikiwa na watangazaji wapya kabisa. Je, unawafahamu? Usikose kuiona studio mpya full red carpert. Kauli mbiu ya msimu mpya ni WASANII TUWE MIFANO BORA KATIKA JAMII.

 Unachotakiwa kufanya ni kuendelea kutazama luninga yako kupitia kituo bora cha vijana Ting'a namba moja EATV hivi karibuni Bongo Movies inatua tena. 
Yes, ni very SOON! Tuwe pamoja katika kuhakikisha tunanyanyua na kuendeleza tasnia ya sanaa na wasanii hapa nchini. Bongo Movies, inachonga barabara, wengine wanafuata!
 Msanii anayefanana na marehemu Kanumba Lutazwa akiwa na crew ya Bongo Movies
Lutazwa, Selina na Hagai

SAFARI YA MWISHO YA MAHEREMU SULTAN SEKILO

$
0
0
 Jeneza lenye mwili wa Marehemu Sultan Sikilo,aliekuwa Mweka Hazina wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) na mchezaji wa timu ya Waandishi wa Habari za Michezo TASWA Fc ambaye pia alikuwa Mtangazaji wa Radio Aboud ya Mjini Morogoro,ukitolewa ndani ya Nyumba yao,eneo la Mbagala Maji Matitu kwa ajili ya kusaliwa na kuanza kwa safari ya kwenda mashikoni.
Waumini wa Kiislam wakiswalia Mwili wa Marehemu Sultan Sikilo.
Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Sultan Sikilo likiwa limebebwa tayari kwa safari ya kwenda kwenye nyumba ya Milele.
Wadau mbali mbali wakishirikiana kubeba Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Sultan Sikilo
Taratibu za Mazishi.
Wadau mbali mbali wakishiriki kwenye mazishi la Marehemu Sultan Sikilo leo kwenye Makaburi ya Kibada,Kigamboni Jijini Dar es Salaam.
Waombolezaji.

KAMPUNI YA VIJANA WA KITANZANIA YA (CHINA WORD BUZ) KUWAKOMBOA WAFANYABIASHARA WADOGO NA WA KATI

$
0
0
1
Meneja Mkuu wa kampuni hiyo nchini China Justin Luvanda akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari.

WAFANYABIASHARA WA STENDI YA DALADALA YA JAMATINI WANAFANYA KAZI KWENYE MAZINGIRA MAGUMU KUTOKANA NA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA MKOANI DODOMA

$
0
0
 Muuza Chipsi akiendelea kuwaaandalia wateja wake huku maji machafu yakiwa yametuama kibandani hapo hali inayotishia Afya za wateja wao, huku kilio cha wafanyabiashara hao kikielekezwa ofisi ya mhandisi wa manispaa kwa wanaotoza kodi.
 Wateja wakiendelea kupata huduma ya chakula kwa mama lishe bila kujali maji machafu yaliyotuama katika eneo hilo lililopo katika kituo cha Daladala Jamatini Dodoma iliyisababisha na kukosekana kwa miundombinu.
 Maji yakiwa yamezagaa katika vibanda vya wafanya biashara wa chakula (mama na baba lishe) kutokana na kukosekana na miundombinu ya kupitishi maji pindi mvua zinaponyesha.

Na John Banda, Dodoma
WAFANYABIASHARA wa chakula (mama lishe) wamo hatarini kupata magonjwa ya kuambukiza yakiwemo kipindupindu kutokana na maji ya mvua kutuama kwenye vibanda vyao ikiwemo kutengeneza harufu mbaya kutokana na kukaa kwa muda mrefu.
Mvua hizo zilizoanza kunyesha tangu mwishoni mwa mwezi uliopita zimekuwa zikisababisha kutuama kwa maji katika vibanda vya mama lishe wanaotoa huduma ya chakula katika kituo cha Daladala Jamatini Dodoma.


Wakiongea kwa niaba ya wenzao Martha Mboma, Zuhura Salumu na Doris Rebman walisema maji hayo yamewasababishia kuishi kwa hofu ya Afya zao kudhurika kutokana na uchafu unaosukumwa kutoka maeneo tofauti na kisha kuishia kwenye vibanda vyao.
Walisema hali hiyo imewasababishia kupoteza wateja ambao wanashindwa kwenda kupata huduma hiyo kutokana na kuhofia afya zao na wakati wao wamekuwa wakilipa manispaa kodi kila mwisho wa mwezi.


‘’Ona mwenyewe ndugu mwandishi kuna vinyesi vinaletwa na maji lakini pia watu wasio wastaarabu wamekuwa wakijisaidia haja ndogo kwenye chupa na kuzitupia kwenye maji hayo unadhani afya zetu zitakuwaje na hata hao wateja watakujaje au hawajipendi’’, alisema Mboma.


Aidha alisema mvua hizo zilizoanza kunyesha tarehe Des 23, 2013 usiku zilijaza maji hayo na yakaa kwa muda mrefu kiasi cha kutengeza harufu kali iliyosababisha usumbufu kwa wafanyabiashara japo wengine wameonekana hawaijali hali hiyo na kuendelea kutoa huduma bila kutafuta ufumbuzi.


Alisema tatizo hilo linatokana na ujenzi wa stendi hiyo mpya ambao haukuzingatia maji pindi mvua zitakapo nyesha ndiyo sababu ya walitengeneza bonde ambalo linaonekana kupokea maji toka pande zote wakati hakuna njia ya kuyatolea na wao kuruhusu mama lishe wapewe
maeneo katika eneo hilo.


Kwa upande wake mwenyekiti wa wafanyabiashara hao Haji Kulaya alisema tatizo hilo ni kubwa na tayali wameshawaona ofisi ya mhandisi wa manispaa zaidi ya mara nne kwa siku tofauti lakini wameshindwa kuchukua hatua yoyote zaidi ya kuishia kufika na kuangalia na kisha kutokomea.

Kwa upande wake Mhandisi wa Manispaa John Kitilla akiongea kwa njia ya simu alisema bado hajapata taarifa hiyo lakini atatuma watu kwenda kuona hali iliyopo na kisha watajua chakufanya baada ya kuona hali halisi iliyopo.

CHANZO: PAMOJA BLOG

BENKI YA NMB YAKABIDHI TISHETI ZA MIAKA 50 YA MAPINDUZI KWA VIJANA WA MKOA WA KUSINI PEMBA

$
0
0
Naibu Katibu wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mohamed Hamis , akipokea sehemu ya Tisheti maalum kwa niaba ya Makamu, kutoka kwa Meneja wa NMB Tawi la Zanzibar Town, Bakari Hamis Mohamed, kwa ajili ya Vijana wa Mkoa wa Kusini Pemba zitakazotumika katika sherehe za maadhimisho ya Miaka 50 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar, zinazofanyika kesho kwenye Uwanja wa Amani mjini Zanzibar. Katikati ni Meneja wa Huduma kwa Wateja wa benki hiyo, Abuu Msagula. Picha na OMR

RAIS KIKWETE APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO TOKA KWA BALOZI MPYA WA COMORO NCHINI TANZANIA LEO

$
0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea hati za utambulisho kutoka kwa balozi wa Comoro Mhe Ahamed El Badaoui Mohamed Fakih ikulu jijini Dar es salaam leo January 11, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe kwa balozi wa Comoro Mhe Ahamed El Badaoui Mohamed Fakih ikulu jijini Dar es salaam leo January 11, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia ngao aliyopewa zawadi baada ya ku[okea hati za utambulisho kutoka kwa balozi wa Comoro Mhe Ahamed El Badaoui Mohamed Fakih ikulu jijini Dar es salaam leo January 11, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na balozi wa Comoro Mhe Ahamed El Badaoui Mohamed Fakih baada ya kupokea hati zake za utambulisho ikulu jijini Dar es salaam leo January 11, 2014. Aliyeketi kushoto ni mkalimani. PICHA NA IKULU.

MATEMBEZI YA HIYARI KWAMIGUU DAR MPKA MORO YAANZA RASMI LEO

$
0
0
 Mratibu wa matembezi ya hiyari kwamiguu yajulikanayo kwa jina la , Matembezi ya Nchi Yangu Wajibu Wangu Utaifa Kwnza”Bw, Matukio Chuma (katikati), akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa matembezi hayo kabla yakuanza matembezi kueleke Mkoa wa Morogoro yalionzia Mbezi jijini Dar es Salaam leo Januariy 11- 2014 ya kilometa 200 yatakayochua siku kumi(kushoto), Mwanakikundi kutoka Umoja wa vijana,Bw Athumani Ali ambae anawakilisha wanachama wenzie wapatao 80 (kulia), Mwanafunzi kutoka Shule ya St Joseph Univerty Bw Joseph Serengeta akiwakilisha wanafunzi wa shule hiyo. Kwa  mujibu wa muandaaji Bw, Matukio Chuma lengo la matembezi hayo yamelenga kuenzi mchango mkubwa na kuthamini kujitoa mhanga kwa waanzilishi wa utaifa wetu, (Hayati) Mwl Julius Kambarage Nyerere, Abeid Amani Karume, Edward Moringe Sokoine na wengineo ambao walisimama kidete na leo tukawa na taifa likaitwa Tanzania.
 Hapa safari imepambamba moto Dar mpaka Moro eneo la Kibaha.
 Hapa safari imepambamba moto Dar mpaka Moro eneo la  Kibaha.
 Mratibu wa matembezi ya hiyari Matukio Chuma.

Zanzibar Photogarphic Journey presented to Former Prime Minister Edward Lowassa

$
0
0
Javed Jafferji , Tanzania top photogarpher and film maker had a pleasure to present a copy of his new book, Zanzibar Photographic Journey - 50 years of the Revolution to former Prime Minister of United Republic of Tanzania,  Edward Lowassa in Zanzibar prior to Revolution day in Zanzibar today.

The book consistd of 328 pages and it took almost one year to publish .

MKUU WA MKOA WA RUKWA INJINIA STELLA MANYANYA ASHIRIKI MKUTANO WA KUCHAGUA VIONGOZI WAPYA WA KANISA LA KKKT SUMBAWANGA.

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza kwenye mkutano Mkuu wa 8 wa kanisa la kiinjili na kilutheri Tanzania KKKT la mjini Sumbawanga ambapo utafanyika uchaguzi Mkuu wa Kanisa hilo na kuzaa Dayosisi mpya ya Ukanda wa Ziwa Tanganyika. Katika hotuba yake hiyo aliwaasaviongozi na waumini wa kanisa hilo kuepukana na vitendo vya rushwa katika kuweka uongozi kanisani hapo pamoja na kuepukana na mambo maovu na machafu ikiwemo kudumisha amani ya nchi.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akiimba moja ya wimbo wa maubiri na Baba Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Sumbawanga Askofu Damian Kiaruzi wakiwa miongoni mwa wageni waalikwa katika Mkutano huo.
Kwaya ya Kanisa hilo.
Sehemu ya waumini na waalikwa katika Mkutano huo.
Picha ya pamoja.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa akiagana na viongozi wa kanisa hilo na baadhi ya wageni waalikwa. (Picha Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)

“TUMEJIFUNZA MENGI KUTOKA TANZANIA”, ALGERIA

$
0
0

Na Asteria Muhozya, Arusha.


Mkurugenzi Mkuu wa Nishati katika Wizara ya Nishati na Migodi wa Algeria Bw. Bourraondj Mohamed Tawar amesema, Serikali ya Algeria imejifunza mambo mengi katika sekta ya madini, kufuatia ziara yao nchini Tanzania.


Aliyasema hayo jana wakati wakihitimisha ziara yao nchini kwa kutembelea maeneo mbalimbali ikiwemo ya uchimbaji na uzalishaji wa madini ya Tanzanite katika migodi ya TanzaniteOne Mererani na katika kiwanda cha kuzalisha mbolea ya kupanda ya Minjingu, Mkoani Arusha.


Aliongeza kuwa, ziara hiyo imekuwa ya manufaa kwa Serikali yao kutokana na kwamba pamoja na kufanikiwa katika sekta ya gesi lakini wamejifunza mengi katika sekta ya madini na katika mbolea ya kupandia ya Minjingu, hatua ambayo imewawezesha  kujifunza na kuona namna serikali ya Tanzania inavyoshughulikia sekta hizo kuanzia uchimbaji, teknolojia zinazotumika, uuzaji, na mambo yote yanayohusu sekta hizo.


Aidha, alieleza kuwa, wamekutana na mambo mengi mapya likiwemo la uchimbaji wa mbolea ya kupandia ya minjingu inayochimbwa kutokana na masalia ya ndege aina ya flamingo ambayo masalia yake yamekuwepo kwa miaka mingi.


“Nilikuwa nikisoma tu katika vitabu lakini sasa nimeona mwenyewe kwa macho, ni furaha sana na funzo kwetu, kwasababu tunatumia njia nyingine kuzalisha mbolea ya kupandia na si kama hii ya masalia ya ndege aina ya flamingo inayotumiwa na Tanzania”, Alisema.


Aidha, aliongeza kuwa, anaamini kuwa ushirikiano ulioanzishwa na nchi hizi mbili utakuwa wa manufaa kwa nchi zote na kuongeza kuwa,  anaamini kuwa, ushirikiano huo utaharakishwa ili  utekelezaji wake uanze haraka.


Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha kuzalisha mbolea ya Minjingu Bw. Tosky Hans alisema kuwa, ziara  hiyo ya wataalamu hao kutoka Algeria ni mafanikio kwao kwasababu ushirikiano huo utasaidia kujifunza mambo mengi kutoka Algeria ambao wamepiga hatua kubwa kiteknolojia na kitaaluma.


“Tutaangalia upande wa teknolojia wanatumia nini na kuzalisha nini, kwasabababu nia yetu ni kuongeza uzalishaji, kuwafikia wananchi wengi zaidi na kukidhi mahitaji ya mbolea kwa nchi za Afrika Mashariki”. Alisema Hans.


Akielezea kuhusu kupata fursa ya kutembelea katika mbuga za wanyama katika bonde la Ngorongoro Bw. Bourraondj Mohamed Tawar alisema, imekuwa ni furaha kwao kuona makundi makubwa ya wanyama mbalimbali na ndege katika mbuga hizo wakiwemo simba ambao walipata nafasi ya kuwaona vizuri.


Vilevile, alieleza kufurahishwa kwao kufika katika eneo la boma wanapoishi Watanzania jamii ya Maasai ambapo walishangazwa kuona namna Maasai hao wanavyoishi jirani na wanyama wa porini.


Wakati huo huo, Kamishna Msaidizi kanda ya Kaskazini Mhandisi Bw. Benjamini Mchwampaka anayesimamia shughuli za utafutaji na uchimbaji wa madini amewataka wachimbaji na wamiliki wa migodi kufuata sheria na taratibu za leseni ikiwemo kulipa kodi. Aliongeza kuwa, serikali haina ubaguzi kwa wachimbaji wakubwa au wadogo wote wanapewa fursa sawa.


“Tunawaangalia wachimbaji wote kwa usawa, wafuate sheria, wachimbe kwenye maeneo yao bila kuingiliana”. Alisema Mchwampaka.


Vilevile, aliwataka wachimbaji kuwa wazalendo kwa kulipa kodi Kama inavyowapasa bila kufuatiliwa na maafisa madini na kuwataka wakumbuke kuwa, Tanzania itajengwa na watanzania wenyewe pale wanapotimiza wajibu wao kikamilifu.

WANAWAKE viongozi wa kitaifa na mkoa wa Dar es salaam, waombwa kujitokeza kuungana na wanawake wengine sherehe ya Maulid

$
0
0

MWENYEKITI Kamati ya Maandalizi ya Sherehe za Maulid kwa wanawake wa    mkoa wa Dar es Salaam, kuadhimishwa kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W),  Aisha Sururu (wa kwanza kulia), akiwaongoza wanawake wengine kuomba    dua, baada ya kumaliza kikao cha maandalizi ya sherehe hizo

zitakazofanyika kesho, katika Ukumbi wa Diamond Jubilee.

=======  =====  =======
WANAWAKE viongozi wa kitaifa na mkoa wa Dar es salaam, wameombwa
kujitokeza ili kuungana na wanawake wengine wa kiislam, katika
sherehe ya Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W).

Wito huo ulitolewa na Kamati ya Maandalizi ya sherehe hizo kwa upande
wa wanawake, na kubainisha kuwa hawataalika mgeni rasmi, badala yake ,
viongozi na wanawake wengine wawe kitu kimoja kuadhimisha siku hiyo.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Aisha Sururu, alisema, sherehe itafanyika
Januari 14, katika ukumbi wa Diamond Jubilee, na kwamba
itawakutanisha wanawake waislam wa mkoa wa Dar es Salaam na mkoa
jirani wa Pwani.

"Wanawake wa hali ya chini, wamefikiria kwanini sherehe za kidini
ambazo hazina harambee, michango wala kitu chochote, tualike mgeni
rasmi? Wakaona ni vyema kutangaza ili nao kama wananchi wajumuike na
wanawake wa hali ya chini, ambao watafarijika zaidi, kuona wamekaa
mkekani pamoja na viongozi wakubwa,"alisema
Aisha.

Mwenyekiti huyo, ambaye pia ni diwani viti maalum Ilala, alisema, kwa
wale ambao hawatafikiwa kwa mualiko wa mmoja mmoja, wanaruhusiwa
kujumuika na wenzao siku hiyo ya maadhimisho.

Maulid ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W), huadhimishwa duniani  kote kila ifikapo mfungo wa sita kwa kalenda ya kiislam. ikiwa ni


kumbukumbu tangu kuzaliwa kwa kiongozi huyo wa wafuasi wa dini ya
kiislam.

Maandalizi ya sherehe hiyo kitaifa, mwaka huu yatafanyika mkoani
Kigoma, ambapo Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA), limesema
mgeni rasmi atakuwa Rais Jakaya Kikwete.

Wema Sepetu "IN MY SHOES" Episode 11 THE FINEST SHOW


SHEREHE ZA MIAKA 50 YA MAPINDUZI ZANZIBAR YAFANA.

$
0
0
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Ali Mohamed Shein akikagua gwaride la heshima wakati wa kilele cha sherehe za miaka 50 ya Mapoinduzi ya Zanzibar katika uwanja wa Amani Abeid Karume leo January 12, 2014. 
 Vijana wakiachia njiwa kama alama ya amani wakati wa kilele cha sherehe za miaka 50 ya Mapoinduzi ya Zanzibar katika uwanja wa Amani Abeid Karume leo January 12, 2014
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Ali Mohamed Shein wakimpongeza Rais Yoweri Kaguta Museveni aliyeongea machache wakati wa kilele cha sherehe za miaka 50 ya Mapoinduzi ya Zanzibar katika uwanja wa Amani Abeid Karume leo January 12, 2014
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Ali Mohamed Shein kwa hotuba nzuri aliyotoa  wakati wa kilele cha sherehe za miaka 50 ya Mapoinduzi ya Zanzibar katika uwanja wa Amani Abeid Karume leo January 12, 2014
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Yoweri Kaguta Museveni wakiongea  wakati wa kilele cha sherehe za miaka 50 ya Mapoinduzi ya Zanzibar katika uwanja wa Amani Abeid Karume leo January 12, 2014.PICHA NA IKULU

MIAKA 50 YA MAPINDUZI ILIVYOFANA ZANZIBAR LEO.

$
0
0
 Rais wa Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akiwapungia wananchi wa Zanzibar wakati akiingia kwenye uwanja wa Amani  na gari la wazi kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia mamia ya wakazi wa Zanzibar wakati akiwasili kwenye Uwanja wa Amani kwenye kilele cha sikukuu ya miaka ya 50 ya Mapinduzi.
 Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni akisalimiana na baadhi ya viongozi waandamizi wa Jeshi kwenye uwanja wa Amani wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

 Sehemu ya Umati uliofurika wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akikagua vikosi vya gwaride kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar kwenye uwanja wa Amani.



 Maandamano mbali mbali kutoka kwenye Mikoa na Taasisi za serikali na zisizo za Serikali yalipita mbele ya jukwaa kuu na kutoa heshima kwa Rais wa Zanzibar na viongozi wengine.
 Wakina mama hawakuwa nyuma kwenye maandamano ya mika 50 ya Mapinduzi kwenye uwanja wa Amani Zanzibar.



 Kikosi cha Mbwa kikiingia uwanjani tayari kuonyesha umati wa watu jinsi Mbwa wenye mafunzo wanavyoweza kufanya kazi zao vizuri.
 Askari wakionyesha jinsi askari waliokuwa chini ya mkoloni walivyokuwa wanafanya mambo yao ikiwa kila amri kutoka kwa lugha ya kiingereza.
 Kikosi cha Makomandoo wakionyesha namna ya kupambana na maadui bila kutumia silaha za moto kwenye uwanja wa Amani wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar. 
 Kikosi cha Kifaru kinaonyesha kifaru cha kivita.
 Vijana wa Halaiki wakionyesha ushiriki wao kwenye miaka 50 ya Mapinduzi "Mapinduzi Daima".
 Kikosi cha Mapinduzi kilichopambana na kuleta Mapinduzi ya Zanzibar kikipita mbele ya jukwaa kuu na kutoa heshima kwa Rais wa Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein,kwenye kikosi hicho amebaki mwana mama mmoja anayefahamika kwa jina la Fatma Abdalla Mussa watatu kutoka kulia.
 Sehemu ya Jukwaa kuu la uwanja wa Amani likiwa limefurika wakati wa sherehe za miaka 50 ya Mapinduzi. Picha na Adam Mzee


RAIS KIKWETE ATANGAZA JUMATATU JANUARI 13, 2014 SIKU YA MAPUMZIKO

$
0
0
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS


Telephone: 255-22-2114512, 2116898

E-mail:  ikulumawasiliano@yahoo.compress@ikulu.go.tz              

Fax: 255-22-2113425


PRESIDENT’S OFFICE,

      THE STATE HOUSE,

       P.O. BOX 9120,  

DAR ES SALAAM.

Tanzania.

 
                                         

TAARIFA KWA  UMMA.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametangaza kuwa kesho, Jumatatu, Januari 13, 2014, itakuwa ni Siku ya Mapumziko (Public Holiday) kwa Watanzania wote kusheherekea miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.


Rais Kikwete ameutangaza uamuzi huo mjini Zanzibar ambako leo ameungana na Watanzania na Wazanzibari wote kusheherekea miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Januari 12, mwaka 1964.


Mapinduzi hayo yaliyoongozwa na mwasisi wa Zanzibar na Taifa la Tanzania, Hayati Abeid Amaan Karume yalifanikiwa kuung’oa madarakani utawala dhalimu wa Sultan na kuwawezesha kwa mara ya kwanza katika historia Waafrika walio wengine kujitawala ndani ya nchi yao wenyewe.


Yalikuwa ni Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofungua njia ya kuzaliwa kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar– miezi mitatu baada ya Mapinduzi hayo – Aprili 26, 1964.               

Naye Rais wa Zanzibarna Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Ali Mohamed Shein ametangaza kuwa kesho itakuwa Siku ya Mapumziko Tanzania Visiwani kusheherekea miaka 50 ya Mapinduzi ya ZanzibarRais Shein alitangaza mapumziko hayo wakati alipohutubia wananchi kwenye Uwanja wa Michezo wa Amaan mjini Zanzibar katika kusherehekea miaka 50 ya Mapinduzi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametangaza kuwa kesho, Jumatatu, Januari 13, 2014, itakuwa ni Siku ya Mapumziko (Public Holiday) kwa Watanzania wote kusheherekea miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.


Rais Kikwete ameutangaza uamuzi huo mjini Zanzibar ambako leo ameungana na Watanzania na Wazanzibari wote kusheherekea miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Januari 12, mwaka 1964.


Mapinduzi hayo yaliyoongozwa na mwasisi wa Zanzibar na Taifa la Tanzania, Hayati Abeid Amaan Karume yalifanikiwa kuung’oa madarakani utawala dhalimu wa Sultan na kuwawezesha kwa mara ya kwanza katika historia Waafrika walio wengine kujitawala ndani ya nchi yao wenyewe.


Yalikuwa ni Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofungua njia ya kuzaliwa kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar– miezi mitatu baada ya Mapinduzi hayo – Aprili 26, 1964.               

Naye Rais wa Zanzibarna Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Ali Mohamed Shein ametangaza kuwa kesho itakuwa Siku ya Mapumziko Tanzania Visiwani kusheherekea miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.


Rais Shein alitangaza mapumziko hayo wakati alipohutubia wananchi kwenye Uwanja wa Michezo wa Amaan mjini Zanzibar katika kusherehekea miaka 50 ya Mapinduzi.


Mwisho.


Imetolewa na;

KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS

Ikulu,

es Salaam.

12 January, 2014



TANZANIA JOINS FORCES WITH BRITAIN'S NO. 1 SCHOOL TO UNEARTH FOOTBALL TALENT

$
0
0
By Jestina George,
“Tanzania has taken the first step towards producing their first Premier League player – thanks to Eton College, England’s premier public school.
Eton Coach, Glen Pierce speaking at the press conference on Friday 10 Jan 2014 at Tanzania House London. 
Together with Safarihub and charity organisation ACE Africa, Eton are sending Glen Pierce, head of sports, plus Ali Lyon, 19, Nicholas Zafirios, 18,  and Tom Pearson,18, who are on a gap year before starting university, to Tanzania to teach local children the finer arts of football.
Ali has already passed his  Level 1 Football Association coaching badge and the quartet cannot wait for the challenge ahead of them.
Coach Glen Pierce with Eton students who will be travelling to Tanzania, Nicolas Zafiriou, Ali Lyon and Tom Pearson
Pierce said: “We are about to embark on a wonderful trip. I have taught at Eton for 27 years and was offered the opportunity to take a sabbatical. This is an chance to see a new country with boys I tutored. We shall be going into schools to coach and to encourage kids to attend school through football. If they do not go to school they will not have this opportunity. We want to attract them to go to school and football is the icing on the cake. I hope the boys will be an encouragement to local kids.”

Eton was founded in 1440 and among the college’s more recent famous old boys are Prime Minister David Cameron, Mayor of London Boris Johnson, the Archbishop of Canterbury plus Prince Harry and Prince William, who Pierce taught.
Minister Counsellor  Amos Msanjila speaking Freddy Macha & Urban Pulse
Amos Msanjila, Minister Counselor of the High Commission, did not hide his pride about the venture. He said: “We are honoured to have the boys going because Eton is not a normal school. In Tanzania we do not have a culture of different schools, but I have been in England long enough to know which school you attend matters. Eton has produced 19 Prime Ministers so, as I said, it is not a normal school. The boys could have gone to any country in Africa, indeed in the world, and we have so much pleasure that they chose Tanzania.” 
Director of  Safari Hub, Dilip Navapurkar  speaking at the press conference on Friday 10 Jan 2014 at Tanzania House London.
Dilip Navapurkar from Safarihub said: “I recently formed the company and one aim is to set up a pilot scheme to play football. We hope to see Tanzania qualify for the World Cup for the first time and produce some top-class Premier League footballers, but it will not happen overnight.
"Tanzania has the raw talent, it is our belief that we will one day produce players who will perform on the world's biggest stage."

John Collenette, chairman of ACE Africa and Future Stars Academy, said: “I have been in Tanzania for five years and I am particularly excited about this venture. Children have different problems to confront in their daily lives and we are committed to help them.”
High Commissioner Peter Kallaghe speaking at the press conference on Friday 10 Jan 2014 at Tanzania House London.
Peter Kallaghe, the High Commissioner, hosted a reception in London on Friday to announce the collaboration with Eton College and sent the football party away with his best wishes. He said:“We are greatly honoured by this initiative. We are fully behind a wonderful plan. Eton has produced 19 British Prime Ministers, maybe we have the 20th travelling to Tanzania this weekend."
High Commissioner Pete Kallaghe poses with guests after the press conference.Images by Urban Pulse

CHADEMA YATOA TAARIFA KUHUSU TUHUMA DHIDI YA MWENYEKITI WAKE WA TAIFA, FREEMAN MBOWE

$
0
0

TAARIFA KWA UMMA

KUHUSU TUHUMA DHIDI YA MWENYEKITI WA TAIFA, FREEMAN MBOWE


Kama mojawapo ya mikakati ya baadhi ya watu wanaotaka kuhamisha mjadala wa makosa yanayowaandama ya utovu wa maadili na usaliti dhidi ya chama, hivi karibuni, Mwenyekiti wa Chama Taifa, Freeman Mbowe amezushiwa tuhuma zisizokuwa na ukweli wowote zikilenga kumchafua kwa nafasi yake ya uongozi na kuipaka matope taasisi anayoiongoza;


Tuhuma hizo ni pamoja na;

1.     Kwamba Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa mwaka 2005 eti alichukua fedha kutoka kwa Mbunge wa Musoma Vijijini (CCM), Nimrod Mkono kiasi cha sh.Milioni 40 ili Mwenyekiti Mbowe asifanye kampeni katika jimbo hilo.


2.     Mwaka 2008, eti Mbunge Mkono alimpatia Mwenyekiti wa Chama Taifa, sh. Milioni 20 kwa ajili ya uchaguzi mdogo wa Tarime, kisha akazitoa kwenye chama kama mkopo na akalipwa.


3.     Mwaka 2010, wakati wa uchaguzi mkuu Mbunge Mkono eti alimpatia Mwenyekiti wa Chama Taifa sh. Milioni 200 kwa ajili ya kampeni za mgombea urais.


4.     Mwaka huo huo wakati wa uchaguzi mkuu, eti Mwenyekiti wa Chama Taifa, alipokea sh. Milioni 100 kutoka kwa Rostam Aziz kwa ajili ya kampeni.


Idara ya Habari ya CHADEMA, inapenda kusema yafuatayo;

1.     Hakuna ukweli hata mmoja katika tuhuma hizo. Ni uongo na uzushi uliopangiliwa kama moja ya mikakati ya watu wenye malengo ya kutaka kuilaghai jamii kwamba viongozi wa CHADEMA hawana tofauti na wale wa CCM na kwamba chama hiki kikuu cha upinzani kinachobeba matumaini ya Watanzania katika kupigania haki zao na kupinga kila aina ya ufisadi, kionekane hakina tofauti na chama kilichoko madarakani, ambacho kimepoteza ushawishi kwa wananchi.


2.     Matokeo ya uongo huo ni kutaka kuisaidia CCM na kugeuza mjadala.

3.     Idara ya Habari ya CHADEMA inapenda kuuambia umma wa Watanzania wote, hususan wanachama, wapenzi, mashabiki wa CHADEMA na wapenda mabadiliko nchini kwamba,Mwenyekiti wa Chama Taifa, ameshawasiliana na mawakili walifanyie kazi suala hili kwa ajili ya kuchukua hatua za kisheria.


4.     Kwa uhakika tunapenda kuiambia jamii ya Watanzania wote, hususan wanachama, wapenzi, mashabiki wa CHADEMA na wapenda mabadiliko wote nchini, kwamba; Chama wala Mwenyekiti wa Chama Taifa, mahali popote na wakati wowote, hajawahi kupokea msaada wa fedha hizo kutoka kwa waliotajwa kwa malengo yaliyosemwa.


5.     Tungependa kuwaambia waliozusha tuhuma hizo, ni vyema kama wanapenda kutunza heshima kidogo waliyobakiza katika jamii kutokana na kuelemewa na mzigo wa tuhuma za utovu wa maadili na usaliti dhidi ya CHADEMA, badala ya kugeuka kuwa mabingwa wa kupika uongo, wajibu masuala ya msingi yanayowaandamana kuhusu mikakati yao ya kuhujumu CHADEMA na viongozi wake, ambayo iwapo chama kisingeibaini na kuchukua hatua za kinidhamu, ingesababisha kuua ndoto na matumaini ya Watanzania kufanya mabadiliko ya kimfumo na kiutawala, kwa kuiondoa CCM madarakani.


6.     Taarifa kuhusu baadhi ya tuhuma katika mkakati huo ambazo zimemlenga Mwenyekiti wa Chama Taifa, kwa kuhusisha shughuli zake binafsi za uwekezaji, zitajibiwa kupitia taasisi husika.

Imetolewa leo Dar es Salaam na;

Tumaini Makene

Ofisa Mwandamizi wa Habari- CHADEMA



Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images