Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 199 | 200 | (Page 201) | 202 | 203 | .... | 1897 | newer

  0 0

   Hii ndio gari aina ya Noah ambayo imepata ajali ikiwa imeharibika vibaya kwa mbele.
   Mmoja wa majeruhi wa ajali hiyo akiwa Amelazwa Pembeni baaada ya kupewa msaada
   Watu wakiendelea kutoa msaada kwa majeruhi wa ajali hiyo

  Ajali mbaya imetokea mda si mrefu eneo kati ya wami na segera,ajali hiyo imesababishwa na gari aina ya Noah ambayo ilikuwa inatokea Moshi mjini kuelekea Dar,Chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa gari hiyo na pia dereva alikuwa anasinzia, hali liyopelekea gari hiyo kuacha njia na kwenda kuparamia gari ya mizigo kwa mbele.

  Gari hilo aina ya Noah pia ilikuwa imebeba watu kupita uwezo wake ambapo abiria zaidi ya kumi na mbili walikuwa ndani ya gari hiyo.Mpaka chanzo chetu kinaondoka eneo la tukio hakuna aliyepoteza maisha bali watu ni majeruhi waliojeruhiwa vibaya sana.

  0 0

     Mwenyekiti wa Bodi wa benki ya Covenant Balozi.Salome Sijaona(katikati)akibonyeza kitufe cha kopyuta kuashiaria uzinduzi rasmi wa huduma ya” benki mtaani kwako” ambayo inawawezesha wananchi na wateja wa benki hiyo kutumia simu zao za kiganjani kupata huduma za kibenki ikiwemo kuweka na kutoa fedha katika akaunti zao.Anaeshuhudia kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Bi.Sabetha Mwambenja pamoja na wajumbe  wa bodi wa benki hiyo.
    Mwenyekiti wa Bodi wa benki ya Covenant Balozi.Salome Sijaona(kulia)akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma ya” Benki Mtaani Kwako” ambayo inawawezesha wananchi na wateja wa benki hiyo kutumia simu zao za kiganjani kupata huduma za kibenki ikiwemo kuweka na kutoa fedha katika akaunti zao.kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Bi.Sabetha Mwambenja.
    Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Covenant Bi.Sabetha Mwambenja(katikati)akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma ya” Benki Mtaani Kwako” ambayo inawawezesha wananchi na wateja wa benki hiyo kutumia simu zao za kiganjani kupata huduma za kibenki ikiwemo kuweka na kutoa fedha katika akaunti zao,pamoja nae katika picha ni  Mwenyekiti wa Bodi wa benki hiyo Balozi.Salome Sijaona(watatu kutoka kushoto) pamoja na wajumbe  wa bodi wa benki hiyo.
  =========  ========  ========
  BENKI YA COVENANT YAZINDUA HUDUMA YA BENKI MTAANI KWAKO
  Dar es Salaam 9, Januari 2014. Katika kuhakikisha inaendelea kupanua wigo na kusogeza huduma zake za kibenki karibu na wateja  wake benki ya Covernant imezindua huduma za kibenki kwa njia ya simu inayojulikana kama”Benki Mtaani kwako” huduma hii ambayo itawawezesha wateja wa benki hiyo kuweka na kutoa fedha katika akaunti zao kupitia simu za Mkononi.
  Akizungumza  wakati wa kuzindua huduma hiyo Mwenyekiti wa Bodi wa benki hiyo Balozi.Salome Sijaona,amesema kuwa benki yake inawalenga watu wa kawaida kabisa ambao wengi wao wanaishi maeneo ya nje ya mji wengi wao wakiwa wajasiriamali na wafanyabiashara wadogo hivyo kuanzisha huduma hii ni faraja kubwa kwa wateja wetu ambao hawatapata tabu tena ya kutoka sehemu waliko kuja katika tawi la benki hiyo kupata huduma.
  “Uzinduzi huu umekuja wakati muafaka ikiwa ni sehemu muhimu ya kuendelea kuboresha na kusogeza huduma zetu kwa wateja wetu, tuna wateja maeneo mengi ya mjini na vijijini, tumeona ni jambo jema kuwaanzishia huduma hii ambayo haita walazimu wao kuja katika tawi letu kupata huduma, aliongeza  Balozi Sijaona.
  “Tunawajali na kuwathamini wateja wetu na sasa tumewaletea huduma hii ya  kuweka na kutoa pesa kwenye akaunti zao kupitia simu za kiganjani wakiwa mahala popote pale, wote tunatambua kuwa dunia ya sasa teknolojia ndio kila kitu, mtu anapoweza kupata kila kitu kupitia simu yake ya mkononi ni jambo jema kwetu, natoa wito kwa wateja wetu kutumia huduma hii ambayo naamini ni suluhisho kwao watakapo kuwa na uhitaji wa kuweka au kutoa fedha katika benki yetu.”
  Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Bi. Sabetha Mwambenja amesema amefurahi kwa benki yake kuendelea kuboresha huduma kwa wateja wake na kuhakikisha wanafikia malengo ya huduma bora kwa wateja wake,Pia alizitaja sifa muhimu za huduma hiyo kuwa ni kulipia Ankara mbalimbali,kuhamisha fedha kwenda akaunti yoyote uliyokuwa nayo na covenant benki,kuhamisha fedha kupitia mtandao wowote wa simu za viganjani nchini,kutuma na kuchukua fedha ATM bila kadi ya benki hata kama aliyekutumia hana akaunti na Covenant benki,kupata miamala uliyofanyika kwenye akaunti yako na kusajili huduma hii mwenyewe kupitia simu yako na usajili unakamilika papo hapo.
  “Tunamipango mingi ya kuendelea kupanua na kuboresha huduma zetu, hadi kufikia sasa tunashukuru namna ambavyo wateja wetu wameendelea kutuunga mkono siku hadi siku, tunawaahidi kuendelea kuwaunga mkono na kuhakikisha tunatimiza ndoto zao za kuwa na maisha bora.”
  Tunaendelea kuwahamasisha Watanzania kuendelea kujiunga na huduma zetu ambazo zinafaida nyingi kwani wateja wanaweza kutumia akaunti zao wakati wowote,kuondoa adha ya kusafiri/kutembealea tawi la benki,kuhamisha fedha kwa uwapendao kwa urahisi zaidi,wanaweza kuwalipa washiriki wa biashara na wagavi bila wasiwasi,Pia hadi sasa tunazo akaunti za aina mbalimbali ambazo ni akaunti za akiba inayojumuisha akaunti ya Ahadi, Jerusalem, Tausi Women Entrepreneurs Account, Winner Junior account, Vikundi, Akaunti ya Akiba ya Bajaj, Akaunti ya Muda Maalum na nyinginezo na akaunti za biashara ni pamoja na akaunti binafsi na nyinginezo.

  Ili kujiunga na huduma hiyo Mteja wa benki hiyo atatakiwa kupiga namba *150*27#

  0 0

   IAA Rector Prof. Johannes Monyo signs the Memorandum of Understanding (MoU) in Arusha today to allow military personnel with the necessary skills and knowledge in Strategic Studies at IAA.

   The Command and Staff College (CSC) Commandant Maj General Kyunga signs the Memorandum of Understanding (MoU) in Arusha today to allow military personnel with the necessary skills and knowledge in Strategic Studies at IAA

   The Institute of Accountancy Arusha (IAA) Rector Prof. Prof. Johannes Monyo (2nd from R) exchange the MoU documents  with The Command and Staff College (CSC) Commandant Maj General Ezekiel-Elias Kyunga (1st from L). The MoU signed today in Arusha will equip military personnel with the necessary skills and knowledge in Strategic Studies at IAA.

  A group photo of members of military and IAA staff members after the signing ceremony early today.  The Institute of Accountancy Arusha (IAA) and the Tanzania People’s Defense Forces (TPDF) have today signed an  Memorandum of Understanding  to equip military personnel with necessary skills and knowledge in Strategic Studies.   The IAA Rector Prof. Johannes Monyo said in his speech that the move was beneficial for his institution and  TPDF's Command and Staff College (CSC ) which he added deserved a special mention for initiating it.

  “It is our understanding that many institutions in Tanzania are not used to working closely with Military personnel. TPDF and Command and Staff College realized that members of military forces are good partners in development. It is true that once good partnership is established the country tends to prosper faster”, Prof Monyo Said. 

   He also noted that the  CSC had enjoyed good working relationship with the IAA that has lasted for eight years and that in 2006 a special CSC tailored programme was developed and this was the beginning of a close working relationship between the two institutions. 

  The Rector said in this relationship the academic staff from IAA were invited to facilitate in a number of other related programmes conducted by CSC. But the target of CSC was to have long term programmes and academic partner with a capacity to run the new targeted programmes. CSC initially, consulted several institutions and universities in the country to establish long term courses in strategic studies but this effort was unsuccessful. 

  It is the flexibility of IAA management and the IAA Governing Council that authorized the commitment of resources in the year 2011 and allowed the development of Strategic Studies programmes at CSC- Monduli. 

   “Two curricula were developed in the area of Strategic Studies and these included the Ordinary Diploma and Postgraduate Diploma in Strategic Studies. These curricula were developed following NACTE standards. The Ordinary Diploma curricula comprising of NTA levels 5 and 6 were submitted to NACTE for validation and were approved. Furthermore, IAA developed Postgraduate Diploma in Strategic Studies Programme. 

  These programmes are currently in progress and have a total of 52 participants from EAC and SADC countries” he said He revealed that both programmes are aimed at equipping Military personnel with the necessary skills and knowledge in Strategic Studies that are needed at their workplace and elsewhere in the world. 

  The programmes, which commenced in May 2013, are expected to produce the first graduands by March this year (2014). Although this is the first collaborative arrangement with a partner from within the country IAA has two other collaborations with partners from foreign countries. IAA signed a MoU with Coventry University of UK way back in 2009 to run four masters degree programmes (MBA – ITM, MBA – LM, MBA – PSM and MSc. FI). 
  These programmes have been running for last four years. In 2013 IAA signed another MoU with Galgotias University of India to run three masters degree programmes namely; Master in Information Security, Master in Software Engineering and Master in Computer Application. These programmes started in November 2013. 

   In the same vein we are working with TMA to establish a Bachelor Degree in Military Science. This degree is expected to be run effective 2015 if the accreditation processes will be completed in time. Today we are here to officially sign the MoU between IAA and TPDF and inform Tanzanians in particular and the world at large that Military staff are good partners in development. 

   I would also like to take a moment of personal privilege to acknowledge some of those who helped to make this day and the event surrounding possible. 
  I wish to thank members of IAA Academic staff, members of CSC staff, TPDF headquarters, members of the Governing Council, NACTE, TMA and all others not mentioned above but helped in one way or the other to make this day possible.

  0 0

   Mwenyekiti wa kikundi cha TUAMKE akimwonesha Hassan Kibwana (katikati) akimwonesha Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel(kushoto) Moja ya mizinga ya nyuki waliyofadhiliwa na wakala wa huduma za Misitu(TFS) ikiwa ni moja ya njia ya vijana hao kujiajiri na kuweza kuchangia shughuli za maendeleo nchini, wakati wa ziara ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo leo katika Mkoa wa Pwani Kuangalia shughuli mbalimbali zinazofanywa na vijana.
   Baadhi ya Mizinga ya Nyuki inayosimamiwa na Kikundi cha TUAMKE kilichopo katika Mkoa wa Pwani.

  Mwnyekiti wa kikundi cha WAJASIRIAMALI GROUP kilichopo katika kata ya Ruvu Bw.Paul Jonathan (kulia)akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel(kushoto) zawadi ya batiki alipotembelea Kikundi hicho Leo Mkoani Pwani.


   Bweni la shule ya Sekondari ya Pangani lililojegwa na Vijana waliopata mafunzo kutoka Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi (NHBRA) Shughuli iliyoratibiwa na Mkoa wa Pwani ikiwa ni moja ya njia ya kuwawezesha vijana kujiimarisha kimaendeleo, wakati wa ziara ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo leo katika Mkoa wa Pwani Kuangalia shughuli mbalimbali zinazofanywa na vijana
   Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel(mwenye shati Jeusi) akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya Mtendaji wa kata ya Ruvu.Kulia ni Mtendaji wa Kata ya Ruvu Bw.Yusuph Mzumeni,wakati alipotembelea Miradi ya Vijana katika vijiji vilivyopo katika kata hiyo leo Mkoani Pwani.
   Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel(mwenye shati Jeusi) akiwaangalia vijana wajasiriamali wanaojishughulisha na utengenezaji wa Batiki alipotembelea Kikundi hicho Leo katika kata ya Ruvu Mkoani Pwani.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Kibaha Bi.Tatu Suleiman akimweleza Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel(mwenye shati Jeusi) makusudio yao ya kuendelea kuwasaidia vijana kuweza kukabiliana na changamoto za kimaendeleo na kumtaka Naibu Katibu Mkuu kusaidia kuratibu Mafunzo kwa vijana na viongozi mbalimbali wa Mkoa na Wilaya ya Ujasiriamali na umuhimu wa kuwanyajua vijana katika jamii,wakati wa ziara ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Leo katika Mkoa wa Pwani Kuangalia shughuli mbalimbali zinazofanywa na vijana
   Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Bi.Halima Kihemba akimweleza Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel(mwenye shati Jeusi) juu ya Mikakati mbalimbali inayotekelezwa na wilaya yake ya kuwawezesha vijana ili waweze kujiajiri na kupiga hatua kimaendeleo,ambapo mafunzo mbalimbali ikiwamo ufugaji nyuki,kilimo cha umwagiliaji na shughuli za ujenzi yamekuwa yakiratibiwa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali nchini, wakati wa ziara ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo leo katika Mkoa wa Pwani Kuangalia shughuli mbalimbali zinazofanywa na vijana
   Mkurugenzi wa Mji wa Kibaha Bi.Jenifa Omolo akimweleza Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel(hayupo pichani)kuendelea kusimamia utoaji asilimia tano (5%) ya mapato ya halmashauri kwa ajili ya kutumika katika shughuli mbalimbali za za maendeleo ya vijana,wakati wa ziara ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo leo katika Mkoa wa Pwani Kuangalia shughuli mbalimbali zinazofanywa na vijana
   Wajumbe Mbalimbali walioongoza na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel wakimsikiliza Mkurugenzi wa Mji wa Kibaha Bi.Jenifa Omolo, wakati wa ziara ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo leo katika Mkoa wa Pwani Kuangalia shughuli mbalimbali zinazofanywa na vijana
  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akikagua shamba la bamia linalolimwa na vijana katika kata ya ruvu Mkoani Pwani.PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO

  0 0

  Msimamizi mkuu wa mradi wa Ujenzi wa soko la Kisasa la Mwanza Commercial Complex, Injinia Zuma (katikati) akiwa na Bonge wa Clouds fm (kulia) na Afisa Habari wa Jiji la Mwanza Joseph Mlinzi (kushoto) kwenye eneo la mradi Ghana jijini Mwanza.
  Msimamizi mkuu wa mradi wa Ujenzi wa soko la Kisasa la Mwanza Commercial Complex, Injinia Zuma akiwa kazini kwa shughuli zake na majukumu ya asubuhi kila kunapo kucha.


  Mradi wa Ujenzi wa soko la Kisasa la Mwanza Commercial Complex, pindi utakapo kamilika utakuwa na mwonekano huu.

  Muonekano kwa ndani.
  Huu ni ujenzi wa mradi wa ujenzi Soko la Kisasa la Mwanza (Mwanza Commercial Complex), ambao tayari umekwishaanza takribani miaka miwili sasa na umefikia katika hatua hii nzuri.

  Mradi huu wa ujenzi wa kitenga uchumi hiki, unaendeshwa kwa ubia kati ya Halmashauri ya Jiji la Mwanza wakati Jiji hilo halijagwanywa kuwa pande mbili, na Mfuko wa Akiba kwa Watumishi wa Serikali za Mitaa (LAPF). Mradi huo unajengwa eneo la Ghana, katika Kata ya Nyamanoro iliyoko ndani ya mipaka ya Manispaa ya Ilemela.


  Watanzania wazalendo wa nchi hii ndiyo watakao pewa kipaumbele kuwekeza biashara katika mradi huu wa mwanza Commercial Complex.  Na mradi huu, hadi utakapokamilika, unakadiriwa kugharimu Sh bilioni 60.45.
  Moja kwa moja na muonekano engo nyingine ya katika ujenzi.
  Wadau wakiwa katika la juu la mjengo huo wa mradi.
  Hakuna haja ya kubeba vifusi vya zege na kupoteza muda, hii ni mashine ya kuchanganya zege iliyo na bomba maalim linalo safirisha zege hiyo hadi eneo la ujenzi kwa vitengo husika. 
  Mjengo kwa mbele.
  "Huu ni mradi wa Ujenzi wa soko la Kisasa la Mwanza Commercial Complex uliopo katika eneo la Ghana wilayani Ilemela jijini hapa, ambao pindi ukikamilika, hakika utatengeneza muonekano mwingine wa mvuto kwa jiji la Mwanza pengine hata eneo hili kugeuka kivutio cha utalii" Says Bonge wa Power Breakfast akihitimisha ziara yake kutembelea miji mbalimbali kanda ya ziwa iliyopewa jina la Clouds 14, kama sehemu ya kuazimisha miaka 14 ya Clouds Fm.
  PIX NA G. SENGO.

  0 0

  Abiria wa treni iliyokwama Dodoma wakiwa na watoto wao wakipata chochote wakati wakisubili hatima yao huku katika stesheni hiyo kukiwa hakutamaniki kwa uchafu unaotishia afya zao kutokana na abiria zaidi ya 1500 kutakiwa kutumia matundu manne ya vyoo.(Picha na John Banda)

   Wasafiri wa treni toka Kigoma na Mwanza kuelekea Morogoro na Dar es laam wakiwa wamelala kwenye mabehewa hawajui cha kufanya baada ya treni hiyo kushindwa kuondoka Dodoma kutokana na Maji kujaa relini Gulwe na Mzaganza.
   Abiria waliokuwa wakisafiri na treni kuanzia kigoma kwenda Dar es laam wakielekea kwenye ofisi ya mkuu wa stesheni ya Dodoma mara baada ya treni hiyo kukwama kuondoka kwa sababu ya mafuriko yaliyosababishwa na mvua maeneo ya Gulwe na Mzaganza.
   Abiria wakisongamana dirishani kupokea fedha za kujikimu 3500 zilizotolewa na shirika la reli baada treni hiyo kukwama kuondoka Dodoma.

   Abiria hao wakiwa kwenye foleni kuelekea kwa mkuu wa stesheni ya Dodoma, Zacharia Kilombele ambako walikuwa wanapewa pesa ya kujikimu tsh. 3500 kwa abiria zaidi ya 1500 walikwama kutokana na mafuriko.

  CHANZO: PAMOJA BLOG

  0 0

  JUMUIYA YA WATANZANIA ITALIA INASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA MTANZANIA MAREHEMU MAULIDI HAMID ABDALLA MAARUFU KWA JINA LA KIDISHI.

  Kidishi amefariki siku ya jumanne ya tarehe 7/01/2014 usiku . Marehemu amefariki katika hospitali ya COTUGNO mjini Napoli, baada ya kulazwa kwa muda wa wiki tatu.

  Marehemu katika uhai wake amewahi kucheza mpitra timu ya Black Fighters na hata Timu ya taifa zote za Zanzibar katika miaka ya themanini.

  Mipango ya mazishi inafanywa na tayari yameshafanyika mawasiliano na familia ya marehemu.

  TUNAPENDA KUWATANGAZI WATANZANIA WOTE KUWA KUTAKUWA NA MKUTANO WA HARAMBEE YA KUCHANGIA MIPANGO YA KUSAFIRISHA MWILI WA MAREHEMU NYUMBANI KWA MAZISHI , MKUTANO UTAFANYIKA PALEPALE ULIPOFANYIKA MKUTANO WA KWANZA WA MAREHEMU JUMA KIJUU.

  MUNGU AMLAZE MAHALA PEMA.. AMIN!

  0 0

  KAULI YA AWALI KUHUSU ONGEZEKO LA BEI ZA UMEME.


  Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), katika kikao chake cha tarehe 10 Desemba 2013 pamoja na mambo mengine, ilitoa maamuzi ya ongezeko la bei za umeme kwa viwango mbalimbali kwa makundi mbalimbali ya wateja hatua ambayo itaongeza mzigo wa gharama za maisha kwa wananchi na itaathiri uchumi wa nchi.


  Maamuzi hayo yamefikiwa kufuatia tarehe 11 Oktoba 2013, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuwasilisha maombi ya kurekebisha bei ya umeme kwa EWURA. TANESCO ilipendekeza kuongeza bei kwa asilimia 67.87 kuanzia tarehe 1 Oktoba 2013, asilimia 12.74 kuanzia tarehe 1 Januari 2014 na asilimia 9.17 kuanzia tarehe 1 Januari 2015.


  Vilevile TANESCO waliomba kuidhinishwa kwa kanuni ya kurekebisha bei ya umeme kulingana na mabadiliko ya bei za mafuta, mfumuko wa bei na mabadiliko ya thamani ya shilingi ya kitanzania.


  Maamuzi hayo ya Bodi ya EWURA ambacho ni chombo cha Serikali yamethibitisha kwamba Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo alisema uongo kwa nyakati mbalimbali mwaka 2012 na 2013 alipowahakikishia  wananchi kwamba bei ya umeme haitapanda hata baada ya TANESCO kuwasilisha mapendekezo ya kupandisha bei ya umeme.


  Aidha, kwa kuwa leo tarehe 9 Januari 2014 Waziri Muhongo amenukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari akisema kwamba sekta ya nishati sio porojo; natoa mwito kwake kuanza kwanza kujirekebisha yeye mwenyewe kwa kuacha porojo na uongo na kumshauri Rais Jakaya Kikwete kuzuia utekelezaji wa maamuzi ya kupandisha bei ya umeme ambayo yataongeza ugumu wa maisha kwa wananchi kinyume na ahadi ya maisha bora kwa kila mtanzania iliyotolewa na CCM.


  Pia, kwa nafasi ya Waziri Kivuli wa Nishati na Madini natoa mwito kwa wote wenye kuathirika na maamuzi hayo ndani ya wiki moja kuanzia sasa watume maoni na mapendekezo yao kwa barua pepe kupitia anuani mbungeubungo@gmail.com.

  Maoni na mapendekezo hayo yanaweza pia kutumwa kwa njia nyingine za kuwasiliana na Ofisi ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inayoongozwa na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).


  Maoni na mapendekezo hayo yahusu athari ambazo wamezipata na/au wanatarajia kuzipata kutokana na maamuzi hayo na mapendekezo ya hatua ambazo wanataka zichukuliwe. Narajia kupokea maoni na mapendekezo kutoka kwa wananchi mbalimbali hususan kutoka pia kwa wateja wa TANESCO ambao wamepandishiwa bei katika makundi yafuatayo:

  Kundi D1: Hili ni kundi la wateja wadogo wa majumbani, hasa vijijini, ambao hutumia wastani usiozidi wa Uniti 75 kwa mwezi. EWURA imeongeza wigo wa mahitaji ya umeme na kufikia uniti 75 kwa mwezi, kwa kile kilichoelezwa kuwa lengo likiwa ni kuongeza idadi ya wateja wa TANESCO wanaoweza kulipa kidogo kwa matumizi ya umeme kwa kiwango hicho, na pia kuwahamasisha kutumia zaidi umeme. Awali kundi hili lilikuwa linatunia wastani wa matumizi ya uniti 50 kwa mwezi. Bei mpya ni shilingi 100 kwa uniti moja, kutoka shilingi 60 za sasa, sawa na ongezeko la shilingi 40.

  Kundi T1: Hili ni kundi la watumiaji wakubwa wa umeme majumbani, biashara ndogondogo, mashine za kukoboa na kusaga nafaka, taa za barabarani, mabango n.k. Bei iliyoidhinishwa ni shilingi 306 kwa uniti moja, ikiwa ni ongezeko la Shilingi 85 ya bei ya sasa. TANESCO ilipendekeza ongezeko la shilingi 131.

  Kundi T2: Hili ni kundi la watumiaji umeme wa kawaida ambao hupimwa katika msongo wa volti 400, na ambao matumizi yao ya wastani kwa mwezi ni zaidi ya uniti 7,500 wateja wafanyabiashara kubwa, viwanda vya kati. Bei ya nishati iliyoridhiwa ni shilingi 205 kwa uniti moja, sawa na ongezeko la shilingi 73 ya bei ya sasa. TANESCO walipendekeza ongezeko la shilingi 145 ya bei ya sasa.

  Kundi T3-MV: Hili ni kundi la wateja wakubwa kama viwanda vikubwa waliounganishwa katika msongo wa kati (Medium Voltage). EWURA imeidhinisha bei ya nishati kwa kiwango cha shilingi 166 kwa uniti moja, sawa na ongezeko la shilingi 45 ya bei ya sasa. TANESCO walipendekeza ongezeko la shilingi 148 kwa uniti moja.

  Kundi T3-HV: Hili ni kundi la wateja wakubwa waliounganishwa katika msongo wa juu (High Voltage – Voti 66,000 na zaidi) ikiwa ni pamoja na ZECO, Bulyanhulu, na Twiga Cement. Bei iliyoidhinishwa ni shilingi 159 kwa uniti moja, sawa na ongezeko la shilingi 53 la bei ya sasa. TANESCO waliomba ongezeko la shilingi 80 kwa uniti moja.


  Mara baada ya kupokea maoni na mapendekezo hayo, pamoja na hatua ambazo nitachukua kupitia nafasi ya  Waziri Kivuli wa Nishati na Madini nitawasilisha pia mapendekezo kwa Kambi Rasmi ya Upinzani kuchukua hatua za kibunge na CHADEMA kuchukua hatua za nje ya Bunge ili kunusuru uchumi wa nchi na kutetea maslahi ya wananchi.


  Wenu katika uwakilishi wa wananchi,

  John Mnyika (Mb)

  Waziri Kivuli wa Nishati na Madini


  09/01/2014


  0 0
 • 01/09/14--20:28: PARTY YA MWAKA MPYA VOA
 • VOA HOLIDAY PARTY A.DIV. 051Mkuu wa idhaa ya Kiswahili ya VOA Mwamoyo Hamza akijichukulia maakuli wakati wa sherehe za mwaka mpya siku ya Jumatano huko VOA Washington Dc.VOA HOLIDAY PARTY A.DIV. 005Heather akijipakulia msosi. VOA HOLIDAY PARTY A.DIV. 024Intern wa VOA na mmiliki wa Bongovibez Bi.Mariam akiwa kwenye mkao wa kung'aa. VOA HOLIDAY PARTY A.DIV. 034Fatou Kalala prodyuza akifurahia kilaji chake. Kwa picha zaidi ungana na Sundayshomari.com

  0 0

  HESHIMA ZA MWISHO ZA KIJESHI BAADA YA MAZIKO.PICHA ZAIDI BOFYA MBEYA YETU BLOG.
  IBADA YA MAZIKO IKAFUNGWA KWA KUWASHA MISHUMAA KATIKA KABURI LA MAREHEMU BENADETHA OLOMI ALIYEZALIWA MWAKA 1962 NA ALIANZA KAZI KATIKA JESHI LA POLISI MWAKA 1982 NA AMEFARIKI AKIWA NA CHEO CHA S/SGT AKIWA ASKALI WA USALAMA BARABARANI. MAREHEMU AMEACHA MUME MMOJA NA WATOTO WATANO NA WAJUKUU WAWILI.

  MKUU WA WILAYA YA RUNGWE CHRISPIN MEELA AKITOA SALAM ZA RAMBIRAMBI KWA FAMILIA YA MAREHEMU NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA HASA WILAYA YA RUNGWE PIA KWA WANANCHI WOTE KWA KUSHITUSHWA NA KIFO CHA ALIYEKUWA ASKALI KATIKA KITENGO CHA USALAMA WA BARABARANI BENADETHA OLOMI (MAMA) BAADA YA MAUTI KUMKUTA AKIWA KAZIN MCHANGANI - ISONGOLE AMBAPO ALIGONGWA NA GALI ALIPOKUWA KASIMAMISHA GARI LINGINE LILILOKUWA LINATOKEA MBEYA KWENDA TUKUYU,NDIPO GARI LILILOKUWA LINAENDESHWA NA ERNEST NDOA KUTOKA WILAYA YA KYELA LIKAMGONGA NA KUSABABISHA KIFO PAPO HAPO. HIVYO CHRISPIN MEELA AMEWATAKA MADELEVA KUACHA KUENDESHA KWA KASI MAGARI SEHEMU ZA MAKAZI YA WATU NA SEHEMU ZA VITUO WANAPO SIMAMA ASKALI WA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZISIZO ZA LAZIMA

  0 0

  1(1)Mratibu wa matembezi ya Dar mpaka Moro Bw, Matukio Chumaa akiwa kwenye muonekano wa picha.
  ========  ========   ========  =====
  Kuanzia tarehe 11.01.2014 Matembezi ya hiyari kwa miguu kutoka Dar es Salaam mpaka Morogoro yataanza rasmi yakikadiriwa kuchukua siku zisizozidi kumi, lengo kuu likiwa ni kuhamasisha, kukumbushana na kuenzi Umoja, Amani na Utulivu kama Taifa moja likaitwa Tanzania ilhali juhudi yakinifu kuanzia ngazi ya mwananchi mmoja mmoja, familia, kaya, wilaya mpaka Taifa kujivika jukumu la kufahamu, kupambanua, kudadavua na mwisho wa siku kushirikiana kupitia njia za makusudi kuhakikisha maliasili na utajiri wa Taifa hili jadidu unamnufaisha kila Mtanzania, huku masuala ya Elimu, Afya, Ustawi wa Jamii, Ujasiriamali na Taaluma yakitiliwa mkazo pasi kuachwa kando.
  Matembezi haya yanatarajiwa kuwa na vituo kadhaa vikiwemo ; Kibaha, Mlandizi, Vigwaza, Chalinze, Mikese na kumalizia Morogoro, tunatarajia ndugu zetu Watanzania tujikimu kwa mahitaji kadha wa kadha tuwapo safarini, Nchi ikiwa Yetu, Wajibu ukiwa Wetu na UTAIFA tukiuweka na kuutanguliza mbele.
  Mpaka sasa matembezi haya ya hiyari yenye kauli mbiu Nchi Yangu, Wajibu Wangu : UTAIFA KWANZA hayajapata mdhamini yeyote na maandalizi yote mpaka sasa ni kufikia lengo la matembezi kama Tanzania iliyo moja bila kujali itikadi, imani, dini, asili ama hata tofauti za kiuchumi miongoni mwetu na kuangaza katika Tanzania yenye kutoa nafasi kwa kila Mtanzania.
  Kwa hakika maandalizi ya msingi yamekamilika na tarehe 11.01.2014 ndoto yetu ya kufanya matembezi ya hiyari yatafikisha ujumbe ulio wa Amani na Ustawi wa Taifa letu itachukua nafasi na kuwa halisia.
  Nchi Yangu, Wajibu Wangu : UTAIFA KWANZA

  0 0

  Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (katikati) akiongozana na wadau mbali mbali wa maendeleo wakati ziara yake ya kukagua maendeleo ya Mradi wa ujenzi wa bwawa la maji katika kata ya Meserani kijiji cha Nalarami,jimbo la Monduli.Wa tatu kushoto ni Diwani wa kata hiyo,Edward Lenanuu.
  Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akisikiliza maelezo kutoka kwa kaimu mhandisi wa maji wa wilaya ya Monduli,Bw. Wasiwasi Mgala (kushoto) wakati alipotembelea Mradi wa ujenzi wa bwawa la maji katika kata ya Meserani kijiji cha Nalarami,jimbo la Monduli.Katikati mwenye shati jekundu ni mwenyekiti wa CCM Monduli,Ruben Kunayi.

  0 0


  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

  MFUKO WA PENSHENI WA PSPF
  Bodi ya Wadhamini na Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) unatoa salamu za rambirambi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Wizara ya Fedha na Familia ya aliyekuwa Waziri wa Fedha Marehemu Dkt. William A. Mgimwa
  Mfuko utamkumbuka kwa ushauri wake na ushirikiano aliouonyesha akiwa Waziri wa Fedha katika kufanikisha maendeleo na ustawi wa Mfuko.

  Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.

  AMIN

  0 0  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua shule ya Sekondari ya Kiembe Samaki, wakati wa hafla fupi iliyofanyika shuleni hapo mjini Zanzibar leo Jan 10, 2014. Kulia ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Ali Juma Shamhuna. 
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua shule ya Sekondari ya Kiembe Samaki, wakati wa hafla fupi iliyofanyika shuleni hapo mjini Zanzibar leo Jan 10, 2014. Kulia ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Ali Juma Shamhuna. 
   -Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifunua kitambaa kuashiria kuweka jiwe la Msingi la shule ya Sekondari ya Kiembe Samaki, wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa shule hiyo iliyofanyika shuleni hapo mjini Zanzibar leo Jan 10, 2014.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza jambo na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kiembe Samaki, Amina Salum Khalfan, wakati alipokuwa akitembelea chumba cha Maabara baada ya kuzindua rasmi Shule hiyo wakati wa hafla fupi iliyofanyika shuleni hapo mjini Zanzibar leo Jan 10, 2014. Picha na OMR
     Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na mmoja wa wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Kiembe Samaki, 
  baada ya uzinduzi rasmi wa shule hiyo uliofanyika leo Jan 10, 2014, mjini Zanzibar
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikagua moja ya vitabu vya kumbukumbu za Maktaba ya Shule mpya ya Sekondari ya Kiembe Samaki wakati alipotembelea chumba hicho cha Maktaba baada ya kuzindua rasmi Shule hiyo wakati wa hafla fupi iliyofanyika shuleni hapo mjini Zanzibar leo Jan 10, 2014. Kulia ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Amina Salum Khalfan.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kiembe Samaki, Amina Salum Khalfan, wakati alipotembelea katika chumba cha Mawasiliano na mafunzo ya Kompyuta cha shule hiyo, baada ya uzinduzi rasmi wa shule hiyo uliofanyika leo Jan 10, 2014, mjini Zanzibar. Picha na OMR
   
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea chumba cha Maabala kati ya vyumba vinne vilivyopo shuleni hapo.
  Wanafunzi wa shule ya Msingi Kiembe Samaki, wakitoa burudani wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi.

  0 0


  Jengo la ARK lililokaribu na eneo la Jet katika Barabara ya Nyerere karibu na sheli ya Victoria linaendelea kuwaka moto mkubwa jioni hii katika eneo la ghala la kuhifadhia madawa. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam wapo eneo la tukio ambako hali bado si shwari. Sehemu iliyoathirika zaidi  ni ghala la kutunzia dawa za binadamu la kampuni ya Philips.  PICHA KWA HISANI YA SHUMBUSHO/LUKAZA BLOG.

  0 0

   
   Abiria waliokwama na treni Dodoma wakusubili mabasi kwa ajili ya usafiri wa kuelekea mikoa ya Morogolo na Dar es saalam ambapo shirika la Reli limewakodia mabasi kutokana na kushindwa kuendelea na safari kutokana na Mafiriko Gulwe na Godegode wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma.
   Abiria hao wakiwa hawajui la kufanya kutokana na kukosa chakula katika stesheni ya reli mkoani Dodoma walipotangaziwa kuanza kusafirishwa kwa mabasi lakini mpaka kufikia leo jioni zaidi ya abiria 900 kati ya 1600 walikuwa bado hawapatiwa usafiri huo.
    Mfanyakazi wa shirika Reli kituo cha Dodoma akiandika tangazo katika ubao wa matangazo lililowataka abiria waliokuwa wanaelekea mikoa ya kanda ya ziwa kurudishiwa nauli zao kutokana na usafiri wa treni kusitishwa kwa muda usiojulikana.
   Askari wa kuzuia Ghasia (FFU) wakiangalia usalama kwa abiria wa treni waliokwama kutokana na treni kushindwa kuendelea na safari tangu juzi mara baada ya kufika kituo cha reli mkoani Dodoma kutokana na mvua iliofunika kufunika reli wilayani Mpwapwa.

   
   Na John Banda, Dodoma
  SHIRIKA la Reli Tanzania (TRC) limelazimika kuwapakia kwenye mabasi abiria wake waliokwama kwa siku mbili katika Stesheni mkoani Dodoma waliokuwa wanasafiri kwa Treni kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa, kutokana na kushindikana kwa ukarabati  unaoendelea kufanyika mpaka sasa ambao umeonekana kushindikana kutokana na wingi wa maji yaliyopo kwenye eneo hilo la Gulwe na Godegode lililopo Wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma.


  Akizungumza na waandishi wa habari katika Stesheni hii Masta wa Kituo cha Reli Dodoma, Zakaria Kilombele alisema kuwa kutokana na hali hiyo ya ukarabati huo unaoendela kwa hivi sasa kwenye njia hiyo ya relishirika limeamua kuwasafisha abiria hao waliokwama kwa kutumia mabasi.


  Kilombele alisema abiria hao waliokwama kwa siku mbili toka wafike kutoka mikoa ya Kigoma,Tabora  na Singida na Mwanza mkoani hapa,jumla yao wamefikia 1800  na Shirika limewakodishia mabasi yapatayo 24, mpaka kufikia leo abiria wote watakuwa wamesafirishwa na mabasi hayo yaliyokondishwa na shirika. “Mpaka sasa tayari abiria wapatao 935 wameshaondoka na ninategemea hawa wengine waliobaki mpaka kufikia leo jioni ni matarajio yangu watakuwa wamesafirishwa, kwa kuwa ninategemea kuletewa mabasi yapatayo tisa “alisema Kilombele.


  Akizungumza kuhusu ukarabati unaoendelea kwenye eneo hilo korofi la
  Gulwe na Godegode alisema mpaka jana alasili hali ilikuwa nzuri na tuliruhusu gari la abiria kuendelea na safari, lakini ilipofika majira ya saa 12 jioni maji yalianza kujaa kwenye eneo hilo na ikalazimika abiria hao kurudishwa stesheni ya  Dodoma mjini.


  Hata hivyo wakizungumza  baadhi ya abiria hao walidai kuwa shirika hilo kitendo cha kuendelea kuwachelewesha juu ya safari kuna hatari ya kuwepo milipuko wa magonjwa matumbo kutokana na abiria walio wengi kujisaidia hovyo na kusababisha kila sehemu kuwa na vinyesi.


  Mawazo Elisha ambaye ni abiria alisema kwa siku mbili tulizokaa hapo stesheni karibu abiria wengi wamekuwa wanajisaidia kwenye mabehewa ya abiria ambayo yamekwama hapo stesheni na yale mabovu hali hiyo inatokana vyoo vilivyopo neo hili kujaa.


  “Vyoo vilivyopo vyote vimejaa na tunalazimika abiria kujisaidia kwenye mabehewa ambapo uchafu huu umetapakaa kwenye mataruma ya reli,hali ambayo imekuwa ikileta harufu kali katika eneo hilo”alisema Mawazo.


  Naye Joshua Lazaro alisema shirika kuendelea kuwaweka katika eneo hilo limesababisha biashara zao kama vile samaki wameanza kuharibika na kuanza kutoa harufu na wadudu wa aina ya vuza. Alisema miongoni mwa abiria wamesafirisha biashara zao kama hao samaki na dangaa kwa maana hiyo hivi sasa wameanza kuharibika na kutuletea hasara kubwa ambayo hatufahamu nani watahusika.
   
  Hata hivyo abiria walikuwa wameishakata tiketi kuelekea mkoa ya kanda ya ziwa walitangaziwa kurudishiwa nauli zao kutokana na mkanganyiko huo wa usafiri kwa njia hiyo ya reli uliojitokeza na mkuu huyo wa stesheni mkoa alisema hakutakuwepo na usafiri kwa muda usiojuilikana.

  Mapema wiki hii jumla ya abiria wapatao 1600 waliokuwa wametoka mikoa ya Kigoma,Tabora Mwanza na Singina waliokuwa wamesafiri kwa usafiri wa
  reli walikwama stesheni ya Dodoma mjini na kuwalazimu kufanya maandamano hadi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Rehema Nchimbi kwa lengo la kutaka kuwapatia usafiri mwingine.  0 0

  Ndg. Phares Magesa (MNEC -Temeke) akiwa na viongozi wa kituo cha watoto yatima New Hope Family cha Kigamboni mara baada ya kuwakabidhi msaada, Watanzania tuendelee kuchangia wenzetu wanaoishi katika mazingira magumu.

  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia Mabalozi na wawakilishi wa taasisi za kimataifa wakati wa Sherehe ya Kuukaribisha Mwaka Mpya (Sherry Party) aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es salaam leo January 10, 2014.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wengine wakisikiliza hotuba toka kwa Balozi wa DRC nchini Mhe Asumani Mpango ambaye pia ndiye Kiongozi wa Mabalozi nchini akihutubia wakati wa Sherehe ya Kuukaribisha Mwaka Mpya(Sherry Party) Ikulu jijini Dar es salaam leo January 10, 2014.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja Mabalozi na wawakilishi wa taasisi za kimataifa wanawake wakati wa Sherehe ya Kuukaribisha Mwaka Mpya (Sherry Party) aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es salaam leo January 10, 2014.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja Mabalozi na wawakilishi wa taasisi za kimataifa wakati wa Sherehe ya Kuukaribisha Mwaka Mpya (Sherry Party) aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es salaam leo January 10, 2014. PICHA NA IKULU

  0 0

  Zanzibar based photographer JAVED JAFFERJI presents  a copy of the book Zanzibar Photographic Journey- 50 Years of the Revolution prior to the official launch o the book at the residence of H.E Malim Seif Sharif Hamad, First Vice President of Zanzibar. Hon Malim Seif Sharif did the introduction for the book along with Dr Abeid Amani Karume, former President of Zanzibar,  who graced Forword for the same book.

  The Historical book will be launched with the exhibition at Peace Memorial Museum in Zanzibar before 12th JAN 2014 to celebrate the 50 years of revolution.

older | 1 | .... | 199 | 200 | (Page 201) | 202 | 203 | .... | 1897 | newer