Mkurugenzi wa Nchi wa shirika la Compassion Internation Tanzania Mch.Joseph Mayalaakizindua jengo jipya la jiko la kisasa lenye majiko matatu pamoja na stoo ya kuhifadhia chakula katika kituo cha P.A.G kilichopo njiro mkoani Arusha jana kilicho gharimu shilingi mil.17(picha na pamela Mollel)
Mkurugenzi wa Nchi wa shirika la Compassion Internation Tanzania Mch.Joseph Mayala akiimba na watoto wanaoishi katika mazingira magumu muda mchache baada ya kuzindua jiko jipya la kisasa lenye majiko matatu pamoja na stoo ya kuhifadhia chakula katika kituo cha P.A.G kilichopo njiro mkoani Arusha jana kilicho gharimu shilingi mil.17(picha na pamela Mollel)
===== ======= ===== =====
Na Pamela Mollel,Arusha
Shirika la Compassion Internation Tanzania pamoja na washirika wenza wanampango wa kuwahudumia watoto zaidi ya laki mbili na nusu kwa mawaka wa fedha 2012-2013 ifikapo 2020 hapa Nchini.
Mkurugenzi wa Nchi wa shirika la Compassion Internation Tanzania Mch.Joseph Mayala alitoa kauli hiyo jana wakati akizindua jiko jipya la kisasa lenye stoo ya kuhifadhia chakula cha watoto katika kituo cha P.A.G kilichopo njiro Mkoani Arusha
Mch.Mayala alisema kuwa lengo hasa la kuwahudumia watoto ni kuwajengea maarifa zaidi na uwezo wa kufanya mambo mbalimbali hasa katika maeno ya uongozi sanjari na kukuza teknolojia ya habari na mawasiliano kwa watoto wanaohudumiwa katika vituo kwa kuhakikisha vinakuwa na mtandao
Pia alitaja lengo jinge kwa mwaka huu wa fedha kuwa ni pamoja na vituo kuwa na kompyuta pamoja na madarasa ili kuwajengea uwezo wa kuhimili teknolojia sambamba na kuimarisha ushirika wenza na makanisa kwa kuhakikisha kwamba wanawaandaa ili leo na kesho waweze kuwahudumia watoto wanaoishi katika mazingira magumu katika eneo lao husika kutokana na kujengewa uwezo wa awali.
Hata hivyo aliweka wazi juu ya elimu ya sekondari kwa vijana na watoto kuwa mwaka jana waligundua matokeo hayakuwa mazuri hivyo wameamua kuwa na mikakati ya kuwa na madarasa ya ziada kwaajili ya vijana waliopo sekondari ili waweze kupata msaada katika maeneo ambayo wanakutana na changamoto kielimu.
“Tumegundu kuwa tunamfadhili mtoto ndiyo lakini kuna umuhimu wa kuijengea pia uwezo familia ili leo na kesho kutwa au compassion hawapo inakuwa rahisi familia kumudu kumsomesha motto”alisema
Hata hivyo alisema kuwa tayari wameshafungua vituo vipya 8 mkoa wa Dar es salama huku akidai kuwa wanampango wakuanzisha vituo vingine vipya mkoa wa Kigoma na katika baadhi ya maeno ya wilaya ya Tabora vijinini
Kwa uapnde wake Mkurugenzi wa kituo cha P.A.G Amani Simon Msemo alisema kiasai cha million 17 zimetumika katika ujenzi wa jengo pamoja na majiko matatu ya kutumia kuni na stoo ya kuhifadhia chakula.
Msemo alisema kuwa wataondokana na changamoto kubwa waliyokuwa nayo ya awali ya kupika nje jambo ambalo lilikuwa likiwapelekea kushindwa kwenda na ratiba hasa nyakati za mvua
“Matumizi ya kuni yalikuwa makubwa hivyo kuchangia katika uharibifu wa mazingira unaotokana na ukataji mkubwa wa kuni katika maeno mbalimbali ya Nchi yetu”alisema Msemo
Pia alitoa shkurani kwa uongozi mzima wa kanisa,Shirika la Compassion pamoja na muwezeshaji wa kituo Esther Mgimba na wenzake kwa kitendo cha kukamilisha huduma hiyo.