Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel Catalog



Channel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | (Page 2) | 3 | 4 | .... | 1897 | newer

  0 0

   Exim bank Tanzania, Mororgoro branch Manager Anna Wesiwasi, (right) hands over a bundle of juice which is part of several food items donated to less privileged children living at Convent of Immaculate heart of Mary Sisters orphanage of Morogoro- Mgolole, when the bank staffs went to celebrated their Christmas with these children. Among the food items donated were; 50kgs, Rice, 25kgs sugar, 25kg wheat flour, a goat, cooking oil 10 ltrs, juice 2 cartons, biscuits 1 box. According to Wesiwasi, their visit to the orphanage was to enjoy with these children, whom most of them had lost their parents.
   Exim bank Tanzania, Mororgoro branch Manager Anna Wesiwasi, (right) addresses a section of less privileged children living at Convent of Immaculate heart of Mary Sisters orphanage of Morogoro- Mgolole, when the bank staffs went to celebrated their Christmas with these children. Among the food items donated were; 50kgs, Rice, 25kgs sugar, 25kg wheat flour, a goat, cooking oil 10 ltrs, juice 2 cartons, biscuits 1 box. According to Wesiwasi, their visit to the orphanage was to enjoy with these children, whom most of them had lost their parents
   One of the Exim bank Tanzania, Mororgoro branch staff member, takes a goat donated by his bank for slaughter during their visit to Convent of Immaculate heart of Mary Sisters orphanage of Morogoro- Mgolole to celebrated their Christmas with the less privileged children who most had lost their parents. Among the food items donated were; 50kgs, Rice, 25kgs sugar, 25kg wheat flour, a goat, cooking oil 10 ltrs, juice 2 cartons, biscuits 1 box.
  Exim bank Tanzania, Mororgoro branch Manager Anna Wesiwasi, (second right, hind row) in a group photo with Mother General of Convent of Immaculate heart of Mary Sisters orphanage of Morogoro- Mgolole (third right) and Head of the orphanage center Sister Felister Mwinuka (right), together with the bank staff members and a section of less privileged children living in that orphanage, shortly after handing over several food items donated to the children during their visit which aimed at celebrating together their Christmas with these children. Among the food items donated were; 50kgs, Rice, 25kgs sugar, 25kg wheat flour, a goat, cooking oil 10 ltrs, juice 2 cartons, biscuits 1 box.

  0 0


  0 0



  Gwiji la Muziki wa Taarabu nchini, na Mshindi wa Tuzo ya Mtumbuizaji bora wa Kike, Hadija Kopa akifanya makamuzi  katika tamasha maalum la Washindi wa Kili Music Award 2012 kwenye uwanja wa Ushirika Moshi Mkoani Kilimanjaro

  Na Peter Mwenda

  MALKIA wa Mipasho nchini, Khadija Kopa na kundi lake cha Tanzania One Theatre (TOT)leo kitatoa shoo kabambe kusherekea sikukuu ya Krismas kwa wakazi wa Kata ya Kivule, Ilala kusherekea sikukuu ya Krismas kwenye ukumbi wa Vegetable Garden Pub.

  Akizungumza jana, Kopa alisema kikundi hicho ambacho kitamba na nyimbo kemkem za taarab zinazotingisha katika miundoko ya Pwani ukiwemo Full Stop, Stop in Town na Mjini Chuo Kikuu ameahidi kukonga nyoyo za mashabiki wake katika eneo hilo kwenye sikukuu hiyo.

  Alisema TOT taarab imesheheni kila idara ikiwa na wanamuziki wenye uwezo mkubwa wa kupiga taarab yenye mahadhi yanayokubalika akiwepo mkongwe Abdul Misambano, Mwanamtama Amir, Ali Star, Rukia Juma na Kopa Junior anayeimba nyimbo za Omar Kopa.

  Mkurugenzi wa Vegetable Garden Pub, Anicety Mkwaya alisema maandalizi ya burudani hiyo imekamilika na zawadi zitatolewa kwa wale watakacheza taarab vizuri na watakaovaa vizuri.

  Alisema burudani katika ukumbi huo zinaendelea ambako Januari 29 bendi ya Msondo Ngoma itatoa burudami katika ukumbi huo.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akikabidhi zawadi za skukuu ya krismas na mwaka mpya 2013 kwa watoto yatima wa kituo cha Bethania mjini Sumbawanga. Katika msimu huu wa Skukuu Mkuu huyo wa Mkoa ameamua kusherehekea kwa kuwatembelea watoto yatima na wafungwa wa gereza mahabusu Sumbawanga na gereza la Mollo kwa kuwapa chakula cha skukuu pamoja na kuskiliza kero zao mbalimbali. Zawadi alizotoa ni Mbuzi, Mchele pamoja na sabuni za kufulia kwa watoto yatima wa kituo cha Bethania vikiwa na thamani ya Tsh. 380,000/= 
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akiwa kwenye picha ya pamoja na watoto yatima wa kituo cha Bethania Mjini Sumbawanga waliofaulu na kuchaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2013 katika shule mbalimbali Mkoani Rukwa. Mkuu huyo wa Mkoa ameahidi kugharamia masomo yao kwa kidato cha kwanza na sare za shule pamoja na vitendea kazi vingine. Kulia ni Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Sumbawanga Ndugu Festo Chonya akimuwakilishha Mkuu wa Wilaya hiyo Ndugu Methew Sedoyyeka.
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya watoto yatima wa kituo cha Bethania Mjini Sumbawanga alipowatembelea kuwafariji kwa chakula katika msimu huu wa sikukuu. 
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa akizungumza na watoto yatima wa kituo cha Bethania, kulia ni Mkuu wa kituo hicho Ndugu Emmanuel Mwampimbwe. Mkuu huyo wa Mkoa aliagiza watoto yatima katika kituo hicho pamoja na vituo vingine watambuliwe na watengenezewe vitambulisho vitakavyowawezesha kupatiwa huduma bure katika hospitali za Serikali Mkoani Rukwa.
  Ndugu ASP. A. Kimati akisoma taarifa ya gereza la Mollo kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya alipotembelea gereza hilo jana kutoa salamu na chakula cha sikukuu kwa wafugwa wa gereza hilo na kuskiliza kero zao mbalimbali. Mkuu huyo wa Mkoa alipokea kero mbalimbali kutoka kwa wafugwa 195 wa gereza hilo ikiwemo uhaba wa sare za wafungwa, wafugwa kutopewa nakala za hukumu zao, kesi zao kusikilizwa kwa kiswahili lakini hukumu kuandikwa kiingereza, kutokukubalika kwa dhamana zao, kutokuwepo kwa hakimu katika Wilaya ya Nkasi, na baadhi ya kesi kuchelewa kuskilizwa. 
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akijumuisha ziara yake gerezani Mollo kwa kuzungumza na viongozi wa Jeshi la Polisi na Jeshi la magereza Mkoani humo ambapo aliahidi kufuatilia kero zote zilizowasilishwa kwa kushirikiana na pande zinazohusika kuhakikisha zinapatiwa ufumbuzi. Alisema kuwa ataendelea kuweka msukumo wa ujenzi wa mahakama za Nkasi na Wilaya mpya ya Kalambo. Aidha aliutaka uongozi wa gereza hilo kufyatua matofali kwa ajili ya ujenzi wa mabweni ya wafungwa katika gereza hilo ambapo yeye atasaidia upatikanaji wa mabati na vifaa vingine vya madukani, kwa sasa mabweni yanayotumika katika gereza hilo ni ya mabati magumu ambayo kutokana na hali ya hewa ya maeneo hayo kunakuwa na baridi kali kwenye msimu wa baridi. (Picha na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)

  0 0

  Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli,Mh. Edward Lowassa na mkewe Mama Regina Lowassa wakiungana na Wakristo wengine kwenye ibada ya Sikukuu ya Krismas iliyofanyika leo kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),Mwanakwerekwe Zanzibar.
  Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli,Mh. Edward Lowassa akitoa salaam za Xmas kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),Mwanakwerekwe Zanzibar mara baada ya ibada ya Sikukuu hiyo leo.Mh. Lowassa yuko visiwani humo kwa mapumziko ya sikukuu hiyo,ambapo amewataka watanzania kusherehekea sikukuu hizi za krismas na mwaka mpya kwa amani na upendo huku tukilinda umoja na mshikamano uliojengwa na waasisi wetu Mwalimu Julius Nyerere na Sheikh Abeid Karume.

  0 0



  0 0


  Mafahali mawili wanaotegemea kuzichapa tarehe 25, 2012 kugombea mkanda wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati Mtanzania Francis Cheka na Mmalawi Chiotcha Chimwemwe nusura wazichape kavukavu wakati wa upimaji uzito na mkutano wa waandishi wa habari katika hoteli ya nyota 5 ya Naura Springs, jijini Arusha leo tarehe 25 Desemba 2012. Hii ni mara ya kwanza kwa ngumi za kulipwa kupewa hadhi kubwa kama hiyo ya kuwekwa kwenye hoteli ya nyota tano (5) hapa Tanzania.

  Wawili hao walikuwa katika hoteli hiyo ya kifahari ya Naura Springs inayomilikiwa na bwana Felix Mrema anayemiliki mahoteli lukuki katika jiji la Arusha na Moshi ambazo ni Naura Springs Hotel, Impala Hotel, Ngurudito Hotel, Impala Moshi na Livingstone Hotel za Moshi!

  Mpambano huo uliopewa jina la “Vurumaini chini ya Mlima Meru”umekuwa ni gumzo katika jiji la Arusha, Moshi, Tanga, Dodoma, Manyara pamoja na nchi jirani za Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda na unaandaliwa na kampuni ya kizalendo ya Green Hills (T) Limited inayomilikiwa na bondia wa zamani wa taifa katika ngumi za ridhaa na kuloipwa George Andrew na familia yake.


  Aidha, watalii wengi walioko katika jiji la Arusha wakati huu wa sikukuu ya Xmas wameonyesha nia zao za kuliangalia pambano hili na wengine wameshakata tiketi tayari kuingia katika ujwanja wa Sheik Amri Abeid kuwashughudia mafahali hao wawili wakitoana jasho. Chiotcha mwana wa Chimwemwe mwanajeshi wa ngazi ya Luteini Usu katika jeshi la Malawi amepania kulibeba juu taifa lake lililoko pembezoni mwa ziwa Nyasa kwa kumwonyesha Francis Cheka kuwa ngumi zinaendana na ushupavu.

  Chimwemwe anadai kuwa hakuja Tanzania kutalii kama walivyo watalii wengine bali alikuja kuwakilisha nchi yake aipendayo ya Malawi na kurudi kwao na mshipi wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati. Alisema kuwa kushinda kwake sio kitu cha kubahatisha ila ni uhakika. 

  Naye Francis mwana wa Cheka, Mtanzania aliyeipeperusha vyama bendera ya taifa hili katika mapambano mengi bila kuzivunja nyoyo za mashabiki wa ngumi nchini alisema kuwa “Mwache Mmalawi huyo ajifurahishe tu kwani hajui kinachongojea ulingoni”

  Cheka aliyejizolea sifa kemkem kati ya mabondia wa kitanzania aliendelea kusema kuwa yeye sio mzungumzaji sana ila ngumi zake ndizo zitakazozungumza siku ya tareeh 26 Desemba, 2012.
  “Asifikirie kuwa ngumi ni kupiga makelele tu na ukashinfa” alisema Chelka akimwangalia Chimwemwe wakati alipokuwa anajigamba kwa sifa kemkem!


  Mpambano huo wa kukata na shoka unakuja wakati ambako Arusha imekuwa ni jiji na linataka kutumia mapambano mengi ya ngumi ya kimataifa kukuza hadhi ya jiji hilo kama “Geneva ya Afrika” kutokana na mandari yake na mikutano mingi ya kimataifa inayofanyika katika jiji hili.

  Francis Cheka anakutana na Chimwemwe baada ya kuutema mkanda wake wa IBF wakati alipokutana na Karama Nyilawila kugombea mkanda mwingine mbali na IBF hivyo kuupoteza ubingwa wa IBF. Cheka amepania kuuchukua tena mshipi huo na kuudhihirishia ulimwengu kuwa yeye kweli ni moto wa kuotea mbali!

  Mpambano huo utahudhuriwa na viongozi wengi wakiongozwa na Meya wa jiji la Arusha Mstahiki Gaudence Lyimo pamoja na wageni wengi wanaofanya kazi kwenye mashirika kadhaa ya kimataifa ikiwa ni pamoja na mahakama ya kimataifa ya wahalifu wa kivita wa Rwanda, Jumuiya ya Afrika ya Mashariki na Kati, ILO, UNICEF, WFP na nyingine nyingi.

  Aidha watalii wengi wameacha kwenda mbugani siku ya pambano ili washughudie wenyewe ni nani zaidi kati ya Cheka na Chimwemwe., Pamabano hilo linaratibiwa na Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Nchini (TPBC) chini ya Rais wake Onesmo Ngowi na kupewa baraka zote na Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (IBF).
  Waamuzi wa pambano ni:
  Onesmo Ngowi - Kamishna Mkuu, Roman Chuwa ambaye ndiye Kamishna wa TPBC mkoa wa Arusha –(Kamishna Mkuu Msaidizi), Nemes Kavishe (Refarii), Boniface Wambura – (Jaji), Gallous Ligongo –(Jaji), Mark Hatia –(Jaji).


  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (wa pili kulia) akiwa mbele ya Kaburi la Rais wa zamani wa Zanzibar  Hayati Idris Abdulwakil, wakati alipozuru Kijiji cha Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja juzi. Rais  Wakil alifariki dunia mwaka 2001. Dk Bilal alifika  eneo hilo  juzi katika ziara yake ya kuwatembelea  wazee mbali mbali mkoani humo, jana.  (Desemba 24, 2012.
   Makamu akiondoka katika kijiji hicho cha Makunduchi baada ya kuzulu Kaburi la Hayati, Abdulwakil, jana.
    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mzee Ali Khamis Abdallah (98) ambaye ni mmoja kati waasisi  10,  waliokaa pamoja na  kuunganisha vyama vya African Association na Shiraz Association na kuwa Chama cha Afro Shiraz Party (ASP), wakati akiwa katika ziara yake ya kutembelea wazee, leo nyumbani kwake Mbweni, mjini Unguja. Kulia ni mke wa Mzee Ali, Asha Ali Ghulam Hussein. 

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mzee Ali Khamis Abdallah (98) ambaye ni mmoja kati waasisi  10,  waliokaa pamoja na  kuunganisha vyama vya African Association na Shiraz Association na kuwa Chama cha Afro Shiraz Party (ASP), wakati akiwa katika ziara yake ya kutembelea wazee, leo nyumbani kwake Mbweni, mjini Unguja. .Picha Zote na Ofisi ya Makamu wa Rais

  0 0

  Pichani juu ni taswira mbalimbali za watoto wakijiachia ndani ya Dar Live muda huu, kabla ya Ndonga za mwaka kuanza kati ya mabondiaMbwana Matumla na David Charanga kutoka Kenya, bondia Mada Maugo na Yiga Juma wa Uganda na Bahati Mwafyela atakayechapana na Chupaki Chipindi. Baada ya ndondi hizo wakali Diamond Platinumz na Ommy Dimpoz watashusha shoo bab kubwa ndani ya ukumbi huo. Wapenzi wote wa burudani mnakaribishwa Dar Live leo.

  0 0


  Warembo wenye asili ya Asia wakitoa burudani wakati wa mkesha wa X-MASS na SKYLIGHT BAND katika kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo. Mmoja wa warembo hao anatoa huduma ya kuuza vinywaji katika ukumbi huo nae akaona aonyesha kipaji chake kwa mashabiki wa Bendi hiyo na kweli anaweza.
  Shine Bright like Diamond...Beautiful like a Diamond in the Sky.........Mmoja wa Shabiki wa SKYLIGHT Band mwenye asili ya Asia akipiga Kolabo na Aneth Kushaba AK47 kwenye mkesha wa X-MASS usiku wa kuamkia leo katika kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar es Salaam.
  Aneth Kushaba AK47 akiongoza safu ya vijana wa SKYLIGHT BAND Joniko Flower na Sony Masamba (kulia) kushambilia jukwaa wakati wa mkesha wa X-MASS Thai village jijini Dar.
  Ghafla Jukwaa lilivamiwa na msanii wa Bongo Flava Beka aliyepanda Jukwaani kusindikiza usiku wa mkesha wa X-MASS sambamba na Sam Machozi a.k.a Sam Mapenzi (kulia).
  Baadhi ya Mashabiki wa SKYLIGHT BAND wakionekana kulipuka kwa burudani ya msanii Beka akisindikizwa na Sam Machozi. Kwa mbali anaonekana Super star Sinta a.k.a JLO wa Bongo (mwenye Sketi ya pundamilia) akisakata rhumba.


  SKYLIGHT BAND wakiwajibika jukwaani.
  Baadhi ya mashabiki wa SKYLIGHT BAND wakijinafasi kwa raha zao kwenye dancing floor.
  Twende kazi....hapo chacha.
  Carolina Mama njoo tucheze........ ni moja ya Hit Song ya SKYLIGHT Band ukiisikii hutotamani kukaa chini.
  Umeshawahi kuona Pedesheee wa Kike??? basi huyo hapo pichani ni Mrembo Eshe Mushi akitunza pesa Wasanii wa SKYLIGHT BAND mpaka wa piga vyombo...Chezea toto la kichaga weweeee.
  Aneth Kushaba AK 47 katika hisia kali.
  Surprise nyingine ya Msanii Amini sambamba na Beka walitoa sapoti ya kutosha kwa SKYLIGHT BAND kuongeza vionjo.
  Wadau wakipata Ukodak nao waliohudhuria.
  Baadhi ya Mabaunsa wanaohakikisha Amani na usalama unakuwepo katika ukumbi huo kwa mashabiki wa Band hiyo. Ukileta fujo lazima ukae chini mwenyewe.

  0 0

   Mabingwa wa Kombe la Ujirani Timu ya hoteli ya Seronera wakifurahia ushindi baada ya kuilaza kwa mabao 5-4 hoteli ya Four Seasons Safari Lodge  katika Uwanja wa Kifaru katika Hifadhi ya Serengeti mkoani Mara leo. Hadi mechi inaisha timu hizo zilitoka sare ya 1-1 kabla kupigwa mikwaju ya penati ambapo Serena walifunga mabao 4 na dhidi ya 3 ya wapinzani wao.
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiikagua  timu ya hoteli ya  Serena  kabla ya kucheza na hoteli ya Four Seasons Safari Lodge katika Uwanja wa Kifaru katika Hifadhi ya Serengeti mkoani Mara. leo hadi mechi inaisha timu hizo zilitoka sare ya 1-1 kabla kupigwa mikwaju ya penati ambapo Serena walifunga mabao 4 na dhidi ya 3 ya wapinzani wao.
    Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na timu ya hoteli ya  Serena  kabla ya kucheza na hoteli ya Four Seasons safari Lodge  katika Uwanja wa Kifaru katika Hifadhi ya Serengeti mkoani Mara. leo hadi mechi inaisha timu hizo zilitoka sare ya 1-1 kabla kupigwa mikwaju ya penati ambapo Serena walifunga mabao 4 na dhidi ya 3 ya wapinzani wao.
   Nahodha wa hoteli ya Seronera Jamali Kitonga akifurahia baada ya kukabidhiwa kombe la Ujirani mwema na Rais Jakaya Kikwete baada ya timu yake kuilaza kwa mabao 5-4 hoteli ya Four Seasons Safari Lodge katika Uwanja wa Kifaru katika Hifadhi ya Serengeti mkoani Mara leo Hasdi mechi inaisha timu hizo zilitoka sare ya 1-1 kabla kupigwa mikwaju ya penati ambapo Serena walifunga mabao 4 na dhidi ya 3 ya wapinzani wao.
    Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi nahodha wa timu ya hoteli ya Seronera Jamali Kitonga kombe la Ujirani mwema  baada ya timu hiyo  kuilaza kwa mabao 5-4 hoteli ya Four Seasons katika Uwanja wa Kifaru katika Hifadhi ya Serengeti mkoani Mara leo Hasdi mechi inaisha timu hizo zilitoka sare ya 1-1 kabla kupigwa mikwaju ya penati ambapo Serena walifunga mabao 4 na dhidi ya 3 ya wapinzani wao.PICHA NA IKULU



  0 0


  Kwa mujibu wa Breaking News  toka Radio One, zilieleza kuwa  Padre anayejulikana kwa jina la Ambrose Mkenda anadaiwa kupigwa Risasi na Watu wasiofahamika kwenye geti la nyumbani kwake wakati akifunguliwa aingie nyumbani kwake maeneo Kitomondo Mjini Zanzibar, ambako ndiko makazi yake yalipo akiwa ndani ya gari aliyokuwa akiendesha pekee yake.


  Hali yake sio nzuri kwani Risasi aliyopigwa imemdhuru maeneo ya mdomoni. 



  Waliompiga Risasi Padre huyo inasemekana ni watu waliokuwa kwenye pikipiki, ambao walimvamia akisubilia afunguliwe geti  kuingia nyumbani kwake.

  0 0

  ...Chezea Diamond wewe!
  Watu weweee: Kila mmoja akiwa na shauku ya kumpa mkono Diamond.
  ...Leka dutigite: Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe na Diamond wakiwapagawisha mashabiki kwa wimbo wa Leka dutigite.
  Ommy Dimpoz 'on da stage'!
  Dimpoz na wasanii wake wakiwasha moto kuwakumbuka wapendwa wao waliotangulia mbele ya haki.
  ...Dimpooo...zzz: Umati ukipiga yowe wakati Ommy Dimpoz akifanya kufuru stejini.
  ...Platnumz hewani: Diamond akiwa amebebwa juu na madansa wake.
  ...Nataka kulewa, zikinipanda nimwage radhi.
  ...Nataka kulewa, lewa...: Diamond akiimba wimbo wake wa Nataka Kulewa.
  ...Nature ua... Nature ua... Nature ua..: Ndivyo Juma Nature alivyokuwa akienda sambamba kwa staili hiyo na mashabiki.
  ...Wanaume Halisi wakiendeleza libeneke ndani ya Dar Live.
  Shakira akipelekeshana puta na Dimpoz stejini.
  KR Muller akigonga mvinyo ndani ya mask.
  ...Zitto kazini: Siyo siasa tu, hata mistari mi mkali.
  Kikosi cha Diamond Platnumz kazini.
  Dimpoz na Shakira wakimwaga nyuki stejini.
  Manjonjo ya madansa wa Dimpoz.
  Diamond akiwachizisha mashabiki.
  Madansa wa Dimpoz wakionyesha umahiri wao.
  ...Wakizidi kukonga nyoyo za mashabiki.
  Zitto Kabwe akicheza kwenye kiti baada ya kunogeshwa na swagga za Dar Live.
  Platnumz na dansa wake kama 'The Wacko Jacko'.
  Shughuli pevu ya Diamond na madansa wake.
  ...Waacheni watoto waje kwangu: Ndivyo allivyokuwa akichombeza Diamond wakati akitaka kumchukua mtoto huyu.
  Platnumz akiipagawisha meza ya wageni waalikwa.
  Waalikwa wakionyesha nyuso za tabasamu wakiongozwa na Mwasiti (wa pili kulia) na Prodyuza aliyetengeneza wimbo wa Leka dutigite, Tudi (wa tatu kushoto).
  Prodyuza na Mwanamuziki mkongwe, Ally Mohammed 'Baucha' akikamua stejini.
  ...Nimpende naniii... Nimpende...: Wapambe "Wemaaaaaaaaaaaaa!"
  Madansa wa Extra Bongo wakinogesha zaidi burudani za X-Mas ndani ya Dar Live.
  Mpiga gitaa la besi wa Extra Bongo, Hosea Mgoachi akijiachia na shabiki jukwaani.
  Pozi la Platnumz.
  ---
  Wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya nchini Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' na Omary Nyembo 'Ommy Dimpoz' usiku wa kuamkia leo wameweka historia kwa kufanya shoo ya aina yake ndani ya ukumbi wa kisasa wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam. Wasanii hao walisindikizwa na mkali Juma Nature na kundi lake la Wanaume Halisi, Msanii mkongwe Ally Baucha pamoja na Bendi ya Extra Bongo. Shoo hii imeletwa kwenu kwa hisani kubwa ya Serengeti Premium Lager na Vodacom - Wajanja wa Kujirusha.
  (PICHA ZOTE : RICHARD BUKOS NA ISSA MNALLY / GPL)

  0 0
 • 12/26/12--04:27: 147 Critics:John F Kitime (2
 • Bloggers Nawaletea muendelezo wa 147 Critics ambapo leo tunamsikiliza mdau muhimu na makini kwenye Muziki wa Dansi na kwa upande mwingine kwenye Filamu akielezea kuhusiana na marekebisho ya sheria ya ushuru wa bidhaa Sura 147 yanayogusa Muziki na Filamu. Tusikilize 147 Critics:John F Kitime (2) akiwa ni mtu wa pili kuelezea maoni yake kupitia link hii:- http://youtu.be/A2jRIqoqE_I Wasalaam. E.N.M.Manase Mdau -TFCA

  0 0

   Katibu Mkuu Wizara ya kazi uwezeshaji wananchi kiuchumi na ushirika Bi Asha Ali Abdallah wanne kutoka kushoto akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa SACCOS huko katika ukumbi wa baraza la wawakilishi la zamani.PICHA NA MAKAME MSHENGA - MAELEZO ZANZIBAR.
   Katibu Mkuu Wizara ya kazi uwezeshaji wananchi kiuchumi na ushirika Bi Asha Ali Abdallah ambae ni mgeni rasmini akiwahutubia wanachama wa SACCOS hiyo ya wadi ya nyerere Jimbo la magomeni Mjini Unguja wanapo kopa mikopo wahakikishe kurejesha ili na wana chama wengine wapate kukopa  mikopo hiyo. 
   Mwenyekiti wa SACCOS ya Tujipe Moyo Safia Maulid Haji akiwasalimia wana SACCOS pamoja na kumkaribisha mgeni rasmini hawapo pichani huko katika ukumbi wa baraza la wawakilishi la zamani.
   Mwenyekiti wa  SACCOS ya Tujipe Moyo Safia Maulid Haji (wapili kulia) akiwa na muakilishi wa jimbo la magomeni Salmin Awadhi Salmin wa kwanza kulia pamoja na mgeni rasmin wakisikiliza utenzi uliosomwa na Amina Mkombe hajupo pichani katika ufunguzi wa SACCOS  hiyo huko katika ukumbi wa Baraza la wawakilishi la zamani.
  Baadhi ya wana SACCOS ya Tujipe Moyo wakiwa wamekaa wakimsubiri mgeni rasmi hayupo pichani katika ufunguzi wa SACCOS yao huko katika ukumbi wa baraza la wawakilishi la zamani.

  0 0


  Staa wa Vichekesho na Filamu Bongo, Said Mohamed Ngamba ‘Mzee Small’ akiwa amelazwa hospitali kutokana na maradhi yanayomsumbua.

  KWENU mnaohusika na sanaa ya filamu Bongo. Mnajitambua sina haja ya kuwataja mmojammoja kwa majina, nitamaliza ukurasa bure. Mimi najua mpo poa, mnaendelea na majukumu yenu ya kila siku. Binafsi niko poa, naendelea na majukumu yangu ya kila siku ikiwamo hili la kuwaandikia barua.

  Barua yangu leo moja kwa moja nailekeza kwa nyinyi wote ambao watu sasa hivi wanawatambua kwa jina la mastaa wa filamu katika soko la Bongo, Bongo Movies. 
  Kikubwa ni kwamba, natambua mchango mlionao katika kusogeza gurudumu la maendeleo ya nchi. Natambua umuhimu wenu wa kuwatibu watu kisaikolojia kupitia filamu zenu mnazozifanya. 

  Hongereni kwa hilo.Katika taaluma yangu ya uandishi wa habari, mara kadhaa nimeshuhudia uwezo wenu katika kufanikisha mambo yanayowahusu, iwe ni sherehe au misiba. 
  Eeeh, kwenye sherehe basi mnalipuka na kushangweka kwelikweli. Kwenye misiba, mnahakikisha mnamsindikiza mtu anayewahusu kwa hadhi anayostahili.

  Hoja hapa ni kwamba, hadhi ile ambayo mnajitutumua hadi kwenye misiba, kwa nini tusioneshe kwa mkongwe wa sanaa nchini, Said Ngamba ‘Mzee Small’? Tunashindwa nini? Mbona pesa zipo?  
  Kwa nini tusimsaidie mzee wetu ambaye tunaimani alikuwa chachu ya vijana wengi kuingia kwenye sanaa?

  Mzee wetu anasumbulia na ugonjwa wa kupararazi. Anashindwa kufanya shughuli zake za sanaa ambazo ndiyo chanzo cha pato lake la kila siku.
  Binafsi nilisikitishwa na kupongeza kitendo cha Rais wa Shirikisho la Filamu nchini TAFF, Saimon Mwakifwamba kuingilia kati na kuanza kutembeza ‘bakuli’ la michango kwa ajili ya kumsaidia mzee huyo.

  Nilisikitika kwani sikuona haja ya yeye kuingilia kati suala hilo ambalo naamini lilikuwa chini ya uwezo wenu, mnaweza bwana! Kikubwa ni kipi haswa? Mbona mna ‘mauwezo’, msinifanyie hivyo bwana.

  Kwani kuna tatizo gani tukiweka nukta katika starehe hata kwa siku moja, tusipige kilevi siku hiyo halafu tujichangishe fedha za kumpa sapoti mwenzetu kwenye kipindi hiki ambacho anaumwa?

  Hakika hili ni dogo, tukiamua tunaweza tena haliwezi kuharibu bajeti zenu hata kidogo.

  Ni yule yule,
  Mkweli Daima.
  Joseph Shaluwa

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaliminana na maofisa wa Usalama wa Wilaya ya Kati, wakati alipowasili eneo hilo kwa ajili ya kufungua rasmi Kituo cha Polisi cha Kiboje, kilichpo Mkoa wa Kusini Unguja leo
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilala na Kamishina wa Polisi wa Zanzibar, Mussa Ali Mussa, wakifunua kwa pamoja kitambaa kuashiria ufunguzi rasmi wa Kituo cha Polisi cha Kiboje, baada ya kukamilika kwa ujenzi wa kituo hicho ulioanza Februari 14, 2012 na kuzinduliwa leo Desemba 26, wakati wa hafla ya uzinduzi huo iliyofanyika Kiboje Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe  kuashiria ufunguzi rasmi wa Kituo cha Polisi cha Kiboje, baada ya kukamilika kwa ujenzi wa kituo hicho ulioanza Februari 14, 2012 na kuzinduliwa leo Desemba 26, 2012, wakati wa hafla ya uzinduzi huo iliyofanyika Kiboje Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja. Kush
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti, Saleh Ahmed Said, kutoka Migoz Supermarket, ambaye ni mmoja kati ya watu waliochangia ujenzi  wa Kituo hicho cha Polisi cha Kiboje, wakati wa hafla za ufunguzi wa kituo hicho zilizofanyika leo Desemba 26, 2012 Wilaya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilala, akisikiliza maelezo kutoka kwa Kamishina wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa, wakati akitembelea kukagua jengo la Kituo cha Polisi cha Kiboje, baada ya kufungua rasmi jengo hilo lililoanza kujengwa Februari 14, 2012 na kuzinduliwa leo Desemba 26, 2012, wakati wa hafla ya ufunguzi huo iliyofanyika Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilala, akisikiliza maelezo kutoka kwa Kamishina wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa, wakati akitembelea kukagua jengo la Kituo cha Polisi cha Kiboje, katika Chumba cha Mawasiliano baada ya kufungua rasmi jengo hilo lililoanza kujengwa Februari 14, 2012 na kuzinduliwa leo Desemba 26, 2012, wakati wa hafla ya ufunguzi huo iliyofanyika Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilala, akisikiliza maelezo kutoka kwa Kamishina wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa (kulia) wakati akitembelea kukagua jengo la Kituo cha Polisi cha Kiboje katika Chumba cha Ofisi ya Polisi Jamii, baada ya kufungua rasmi jengo hilo lililoanza kujengwa Februari 14, 2012 na kuzinduliwa leo Desemba 26, 2012, wakati wa hafla ya ufunguzi huo iliyofanyika Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja.
   Kikundi cha Sanaa cha Polisi kikitoa burudani ya maigizo.

  Kikundi cha ngoma cha Tukulanga kikitoa burudani wakati wa hafla hiyo.
  Picha Zote na Ofisi ya Makamu wa Rais

  0 0


  Wadau!

  Tunatafuta wadau wawili au watatu wa uhakika wenye uwezo wa ku supply kwa pamoja jumla ya tani 500 kwa mwezi za PET flakes (makopo matupu yanayotumika kutunza maji ya kunywa, soda, n.k).

  Ikiwa upo Tanzania na una uhakika unaweza ku supply kiwango hicho kwa mwezi. Tafadhali tuwasiliane kupitia e-mail hii(info@g12.hk).

  Naomba kwa wale wenye uwezo huo ndio wanitafute, hii biashara ina process zake ambazo siyo rahisi kwa mtu ambaye hana investment ya kutosha.

  Pia inawezekana huna investment, lakini unajua namna ya kupata haya material, usisite kunitafuta then nitakuunganisha na wadau wakubwa ili uweze kuuza kwao, finally sisi tutanunua kwao, ili kurahisisha mchakato mzima na kuhakikisha kila mwenye interest anafaidi kulinagana na mchango wake.

  Nyongeza kuhusu makopo tunayotaka:
  The recycling source of PET flakes is usually from soft drink bottles. Such as Coca bottle, sprite bottle, mineral water bottle

  G12 International Company Ltd.

  0 0

  Mgombea nafasi ya Uenyekiti wa UVCCM kata ya Kawe Amani Nkurlu (kulia) akirudisha fomu ya kugombea nafasi hiyo kwa Katibu wa UVCCM kata ya Kawe Bi. Aisha Katundu.
  Katibu wa UVCCM kata ya Kawe Bi. Aisha Katundu (kushoto) akipokea fomu aliyoijaza Bw. Amani Nkurlu kwa nafasi ya kugombea Uenyekiti UVCCM kata ya Kawe alipofika ofisini hapo leo saa 7 mchana.
  Mgombea wa Uenyikiti wa UVCCM kata ya Kawe, Amani Nkurlu, akizungumza machache na Katibu wa CCM Kawe Bi. Aisha Katundu katika ofisi za CCM Kawe.


  Amani Nkurlu akijaza fomu ya kugombea nafasi ya Uenyekiti wa UVCCM kata ya Kawe.
  Baadhi ya wakereketwa wa CCM katika picha ya pamoja nje ya ofisi ya CCM Kawe. Kutoka kushoto ni Katibu Mwenezi wa tawi la Umbwelani Kawe- Ramadhani Malenge, Katibu wa Wazazi Kawe- mama Katenda, mgombea nafasi ya ukatibu UVCCM kata ya Kawe – Sambili Tegemeo na mgombea nafasi ya Uenyekiti UVCCM kata ya Kawe - Amani Nkurlu.Picha na Josephat Lukaza

  Baada ya uchaguzi wa UVCCM katika kata la Kawe kuvurugika mapema mwaka huu, uchaguzi huo unaorudiwa sasa umefika patamu ikibakia siku moja tu kuchukua fomu huku vijana wengi wakijitokeza kuwania nafasi mbali mbali katika jumuiya hiyo ya vijana illiyopo wilayani Kinondoni.
  Akizungumza na waandishi wa habari, mmoja wa wagombea wa Uenyekiti wa UVCCM katika kata hiyo, Amani Nkurlu (23) alisema “Siku zote nimekuwa nikitafakari ni kwa namna gani nitaweza kutoa mchango wangu katika chama na kuchangia mustakabali wa taifa letu Tanzania kwa ujumla.”

  “Ninaamini CCM bado inahitaji vijana makini na wengi zaidi wakukisemea, kuishauri na kuleta chachu ya maendeleo katika utendaji wake wa kazi wa kila siku kichama na kiserikali. Hii ndio dira yangu kwa CCM, nina imani na chama changu na nimejikita katika kuchangia mabadiliko hayo kupitia Umoja wa Vjiana,” Nkurlu alisema. 

  Nkurlu ambaye ana Shahada ya Mawasiliano kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT) ameshawahi kushika nyadhifa mbali mbali za uongozi ukiwemo; Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM – Tawi maalum la Kambarage SAUT, Waziri wa Mambo ya Nje, Mbunge katika serikali ya wanafunzi, na Rais wa AIESEC akiwa hapo hapo chuoni. Mwaka 2010 Nkurlu pia alipata kugombea nafasi ya Umakamu wa Rais katika serikali ya wanafunzi chuoni hapo lakini hakufanikiwa kwa kupata kura 1278 kati ya kura 2995 zilizopigwa na 54 kuharibika.
  Hivi sasa Nkurlu anamalizia Stashahada ya juu kutoka Chuo cha Diplomasia na pia ni mwajiriwa katika moja ya makampuni ya mawasiliano na matangazo jijini Dar es Salaam kama Mshauri wa Mawasiliano.

  0 0

  MzeeYusuf akiwapagawisha mashabiki waliofurika katika ukumbi wa Dar Live usiku wa 'Boxing Day'.
  Mke wa Mzee Yusuf, Leila Rashid, akizikonga nyoyo za wapenzi wa taarab usiku wa kuamkia leo.
  Khadja Yusuf akiwachizisha wapenzi wa taarab ndani ya Dar Live.
  Mwimbaji wa Jahazi Modern Taarab, Fatma Mahmoud 'Mcharuko' akiwapa raha mashabiki.
  Nyomi iliyohudhuria shoo hiyo kali kutoka Jahazi Modern Taarab.
  Mzee Yusuf akiongea na mashabiki wake.
  ...Khadja Yusuf kazini.
  Bi. Leila Rashid akiendeleza makamuzi.
  Mzee Yusuf akizidi kukoleza burudani ndani ya Dar Live.
  Wapenzi wa taarab wakijiachia kwa raha zao na Jahazi.
  Sehemu ya nyomi iliyotia timu mahali hapo.
  ---
  Kundi la Jahazi Modern Taarab chini ya kiongozi wake, Mzee Yusuf ' Mfalme' usiku wa 'Boxing Day' lilifanya makamuzi ya nguvu ndani ya ukumbi wa maraha wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam na kuzikonga nyoyo za wapenzi wa taarab waliofurika mahali hapo. Pichani juu ni baadhi ya matukio yaliyochukia nafasi wakati wa shoo hiyo.
  (PICHA: ISSA MNALLY NA RICHARD BUKOS / GPL)

older | 1 | (Page 2) | 3 | 4 | .... | 1897 | newer