Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

RAIS KIKWETE AONGOZA MAELFU YA WATU MAZISHI YA DKT WILLIAM MGIMWA MKOANI IRINGA LEO.

$
0
0
Rais  Kikwete na mkewe  wakiweka  shada la maua 
Mjane  wa Dr Mgimwa akiaga  mwili  huo kabla ya mazishi kijiji   cha Magunga  Iringa  leo 
Mwili  wa Dr Mgimwa ukishushwa kaburini  leo 
Wabunge  Deo  Sanga  wa jimbo la Njombe Kaskazin  kushoto na Deo Filikunjombe wa Ludewa  

MAELFU   ya  wakazi  wa mkoa  wa Iringa na  baadhi  ya  viongozi  wa  vyama  vya  siasa na  Serikali  wakiongozwa na  Rais Dr  Jakaya  Kikwete  wameshiriki  katika mazishi ya  aliyekuwa  mbunge wa   jimbo la Kalenga na  waziri wa fedha  Dr  Wiliam Mgimwa.


Huku   waziri  mkuu Mizengo  pinda katika  salam  zake za serikali akielezea  jinsi ambavyo  Taifa  lilivyopata  pigo kubwa  kufuatia  kifo  cha Dr Mgimwa kutokana na mchango  wake  katika baraza la mawaziri.


Katika  mazishi  hayo   yaliyofanyika  leo kijiji  kwake Magunga  jimbo la Kalenga   wananchi   mbali  mbali   walionyesha  kujipanga  barabarani  kutoka Manispaa ya  Iringa  hadi  kijijini kwake  huku  wakiupungia mkono msafara  wa    rais Kikwete na baadhi yao  wakilazimika  kutumia  usafiri wa baiskeli na pikipiki  kwenda katika mazishi  hayo.


Akitoa   shukrani za  familia kwa niaba ya  familia  mtoto wa marehemu Dr Mgimwa Godfrey  Mgimwa  aliishukuru   serikali kwa  jinsi ambavyo ilivyohangaika  kumuuguza baba  yake  na  kutoa wosia  mzito wa marehemu  Dr Mgimwa ambao  alimtaka kuufikisha kwa Rais  Kikwete..


Alisema  katika  uhai  wake kabla  ya kifo  chake  ikiwa ni siku tano kabla  Dr  Mgimwa alimwita na  kumtaka  kufikisha  shukrani zake kwa Rais  Kikwete kwa  kumtembelea mara mbili Hospital  alipokuwa amelazwa  pamoja na  spika wa bunge Anne makinda .


Pia  alisema  kuwa alieleza dhamira  yake ya  kuwatumikia  wana Kalenga na  kusema  zawadi kubwa ni msaada wa bati  zaidi ya  2000 kwa wananchi hao  ili kuendeleza ujenzi wa shule na  vituo  vya afya  jimboni.


"Baba  kabla ya  kufa  aliniachia  wosia  huo juu ya wana Kalenga kwa kuwashukuru kwa  ushirikiano  wao na  kutoa  bati ila alipenda  kuona  Kalenga  inakuwa na maendeleo zaidi"


Kwa  upande  wake  waziri Mkuu Pinda  alisema  kuwa  serikali imepata pigo kubwa  juu ya kifo hicho na kuwa  bado serikali  itaendelea  kuwa karibu na familia ya Dr Mgimwa  na pale  penye tatizo  isisite  kuwasiliana .


Hata  hivyo  Rais  Kikwete  hakupata  kuzungumza  chochote  katika msiba  huo  zaidi ya  kuweka mchanga na shada la maua pamoja na kuwapa mkono  ndugu wa Dr Mgimwa .

  
Spika  wa bunge Anne Makinda  alisema kuwa  bunge  limempoteza kiongozi na mbunge aliyependa kutumia  nafasi yake kwa ajili ya Taifa  na kuwa kamwe mchango  wake  hawataacha kuukumbuka.

habari picha kwa hisani ya Francis Godwin-Iringa

binti wa miaka 15 atekwa kwa siku tatu na kubakwa Makete Njombe

$
0
0
Na Edwin Moshi,Makete
Jeshi la polisi wilayani Makete  mkoani Njombe linamshikilia  Fransis Pilla (36) mkazi wa kijiji cha Iwawa na kata ya Iwawa  wilayani hapa kwa makosa  mawili ya  utekaji nyara na  ubakaji  kwa binti mwenye umri wa miaka 15 ambaye jina lake limehifadhiwa.

Akiongea na vyombo vya habari wilayani hapa afisa upelelezi wa jeshi la polisi wilaya ya Makete Bw Gozbert Komba  amesema kuwa siku ya tarehe 15 mwezi huu walipokea taarifa  kutoka kwa msamaria mwema ambaye pia ni mwajiri wake bw. Erick Mbilinyi (34) ya      mtendewa kutekwa na kufungiwa ndani ya nyumba ambayo haijakamilika ujenzi wake maarufu kwa jina la pagale ambapo walifika katika jumba hilo  na kumkuta akiwa amefungwa kamba mikononi na miguuni.

Amesema kuwa  mara baada ya kumkuta mtendewa huyo akiwa ametekwa walimhoji na yeye kukiri  kuwa amebakwa na  hajaoga tangu afanyiwe ukatili huo na hivyo kurahisishia  kupatikana kwa vipimo kutoka kwa madaktari kuwa ni kweli binti huyo amebakwa na kuongeza kuwa walikuwa wana mahusiano ya kimapenzi.

Katika hatua nyingine mrakibu huyo amebainisha kuwa  mtendewa huyo alisema kuwa alitekwa nyara kwa siku tatu,   na hajala chakula kwa siku zote hizo ambapo alitekwa nyara tangu tarehe 3  mwezi Januari mwaka huu  majira ya saa saba mchana  mpaka tarehe 5 mwezi huu majira ya saa saba na nusu mchana
 
Amesema polisi wanatarajia kumfikisha mahakamani siku chache zijazo

KONYAGI YAWAZAWADIA WAFANYAKAZI WAO WA MUDA MREFU

$
0
0
 Mkurugenzi wa Masoko wa Kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distilleries (TDL), Joseph Chibehe (kushoto) akimkabidhi cheti cha kwa kuwa mmoja wa wafanyakazi wa muda mrefu wa kampuni hiyo, Ashura Omari  wakati wa hafla ya wafanyakzi kufurahi pamoja na familia zao kwenye Hoteli ya Kunduchi Beach, Dar es Salaam. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa  TDL, David Mgwassa.
 Mkurugenzi Mtendajj wa Kiwanda cha Konyagi, David Mgwassa aimpatia Munisi cheti cha shukurani kwa kuwa mmoja wa wafanyakazi wa muda mrefu waliotumikia kiwanda hicho.

 Mgwassa akimtunuku Michael Mrema cheti kwa kuwa mmoja wa wafanyakazi wa muda mrefu wa TDL
 Wafanyakazi wa Kiwanda cha Konyagi na familia zao wakishindana kufukuza kuku
 Sssa ni wakati wa mapumziko
Watoto wa wafanyakazi wa TDL wakishindana mbio za magunia

RAIS KIKWETE AONGOZA MAMIA YA WAOMBOLEZAJI KATIKA MAZISHI YA DKT WILLIAM MGIMWA LEO

$
0
0
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mkewe Mama Salma Kikwete wakiweka shada la maua  wakati wa mazishi ya aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kalenga Marehemu William Mgimwa kijijini kwake Magunga jimbo la Kalenga, Iringa, leo Desemba 6, 2014
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete  na mkewe Mama Salma Kikwete wakitoa heshima baada ya kuweka shada la maua   wakati wa mazishi ya aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kalenga Marehemu William Mgimwa kijijini kwake Magunga jimbo la Kalenga, Iringa, leo Desemba 6, 2014.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa ameongozana na mkewe Mama Salma Kikwete akiweka udongo kaburini wakati wa mazishi ya aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kalenga Marehemu William Mgimwa kijijini kwake Magunga jimbo la Kalenga, Iringa, leo Desemba 6, 2014
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akimfariji Godfrey Mgimwa, mmoja wa watoto wa Marehemu wakati wa mazishi ya aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kalenga William Mgimwa kijijini kwake Magunga jimbo la Kalenga, Iringa, leo Desemba 6, 2014
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akimfariji  Mama mzazi wa  Marehemu wakati wa mazishi ya aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kalenga William Mgimwa kijijini kwake Magunga jimbo la Kalenga, Iringa, leo Desemba 6, 2014
 Mama Salma Kikwete   akimfariji Godfrey Mgimwa, mmoja wa watoto wa Marehemu wakati wa mazishi ya aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kalenga William Mgimwa kijijini kwake Magunga jimbo la Kalenga, Iringa, leo Desemba 6, 2014
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akimfariji  Mjane wa  Marehemu wakati wa mazishi ya aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kalenga William Mgimwa kijijini kwake Magunga jimbo la Kalenga, Iringa, leo Desemba 6, 2014
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akiwapa mkono wa pole wananchi wa Kalenga  wakati wa mazishi ya aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kalenga William Mgimwa kijijini kwake Magunga jimbo la Kalenga, Iringa, leo Desemba 6, 2014
Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akiwapa mkono wa pole machifu    wakati wa mazishi ya aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kalenga William Mgimwa kijijini kwake Magunga jimbo la Kalenga, Iringa, leo Desemba 6, 2014.PICHA NA IKULU

Diamond Feat Davido - Number One Remix (Official Video)

MAZISHI YA DKT WILLIAM MGIMWA

PICHA MBALIMBALI ZA KUMTAFUTA MR MBEYA

$
0
0




Na Mbeya yetu






SERIKALI MBILI NDIO NGUZO YA MUUNGANO – NDEJEMBI

$
0
0
DSC_0330
Sehemu ya vijana wakimsikiliza Mjumbe wa Halmashauri ya Taifa (NEC), Deo Ndejembi, wakati akitoa hotuba fupi baada ya kupokea matembezi hayo ya vijana.
DSC_0332
Mjumbe Baraza Kuu UVCCM Taifa, Chief Sylvester Yaredi, akisoma risala ya vijana kwa Mjumbe wa NEC Taifa kupitia vijana Deo Ndejembi kuhusu msimamo wa vijana wa serikali mbili katika kulinda muungano wa Bara na Visiwani.
DSC_0337
Mjumbe wa NEC Taifa kupitia vijana Deo Ndejembi, akimpongeza Mjumbe Baraza Kuu UVCCM Taifa, Chief Sylvester Yaredi kwa risala nzuri.
DSC_0401
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC) kupitia UVCCM, Deo Ndejembi, akizungumza na wanamatembezi kutoka UVCCM bara na visiwani kuhusu umuhimu wa Vijana kutoa Elimu na kuhamasisha umuhimu wa Serikali mbili kama njia bora ya kulinda Muungano wa Tanzania.
DSC_0407
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC) kupitia UVCCM, Deo Ndejembi akisalimiana na baadhi ya vijana walishiriki matembezi ya kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar waliowasili leo kutoka visiwani Zanzibar.
DSC_0355
Bi. Hilda Oddy, Katibu kata ya Ubungo, Uhamasishaji (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wengine wa UVCCM.
DSC_0212
Sehemu ya vijana wa UVCCM toka bara na visiwani wakitembea kutoka bandari ya Dar es Salaam hadi makao makuu ya UVCCM katika kuadhimisha miaka 50 ya mapinduzi ya Zanzibar huku na mabango yenye ujumbe mbalimbali wa kuhamasisha Serikali mbili.(Picha zote na Zainul Mzige). .awataka vijana kwenda kwa wananchi kuwaelimisha umuhimu wa Serikali mbili .asema kero za Muungano zinaweza kupatiwa ufumbuzi

Na Damas Makangale, MOblog
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC) kupitia UVCCM, Deo Ndejembi amewataka vijana wa CCM kwenda kwa wananchi na kuwaelimisha umuhimu wa kuwa na serikali mbili katika kulinda muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Akizungumza na wanamatembezi wa UVCCM kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya mapinduzi ya Zanzibar leo mchana katika makao makuu UVCCM jijini Dar es Salaam , Ndugu Ndejembi amesema serikali ndio nguzo kuu ya kudumisha muungano kati ya bara na visiwani.

“tunataka vijana waelewe kwamba serikali mbili ndio njia kuu ya kudumisha muungano wetu kwa kuwa waasisi wa muungano Mzee Karume na Baba wa taifa Nyerere walio mbali katika kuchanganya mchanga wan chi hizi mbili na ndio njia bora katika kudumisha upendo, undugu na amani katika nchi yetu,” amesema Ndugu Ndejembi.

Mjumbe huyo wa NEC taifa alilisitiza kwamba mapendekezo ya tume ya mabadiliko ya katiba ya serikali tatu itawagawa watanzania kati ya bara na visiwani na ni serikali mbili ndio itawaleta karibu watanzania.
Ndejembi aliongeza kuwa serikali tatu siyo suluhisho la kero mbalimbali za muungano bali matatizo ya sasa ndani ya muungano yanaweza kushughulikiwa na kupatiwa ufumbuzi wa kudumu kwa maslahi mapana ya taifa.

Mjumbe huyo wa NEC alisisitiza kwamba rasimu ya katiba ya pili iliyowasilishwa hivi karibuni na Jaji na Waziri Mkuu Mstaafu Joseph Warioba katika kipengele cha maadili na miiko ya uongozi, CCM haina matatizo kwa maadili ya viongozi kuwekwa katika katiba kwa maslahi ya taifa.


DSC_0223DSC_0228DSC_0232DSC_0234DSC_0245
Baadhi ya Wenyeviti wa UVCCM mkoa bara na visiwani mara baada ya kuwasili Makao Makuu ya UVCCM jijini Dar.
Kwa upande wake, Mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM Taifa, Chief Sylvester Yaredi aliyesoma risala ya wanamatembezi amesema takribani vijana 600 walishiriki matembezi hayo ambayo kati yao 35 walitoka katika maeneo mbalimbali ya Tanzania Bara.
“tunaunga mkono, kupongeza na kuenzi mapinduzi ya mwaka 1964, kwani mapinduzi hayo ni alama ya ukombozi wa wanyonge waliokandamizwa, kuonewa na kudhulumiwa haki na utu wao,” amesema Yaredi
Amesema kuwa vijana wanatambua kuwa mapinduzi ya mwaka 1964 ndio chachu ya muungano na kwamba vijana ndio tunu ya taifa na watalinda muungano kwa nguvu zao zote.
DSC_0252
Wanamatembezi wakiwa wamebeba picha za Waasisi wa Muungano na Viongozi wa sasa wa bara na visiwani.
DSC_0258
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC) kupitia UVCCM, Deo Ndejembi, akipokea maandamano hayo.
DSC_0272
Pichani juu na chini ni MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC) kupitia UVCCM, Deo Ndejembi, akipokea picha za waasisi wa Taifa.
DSC_0278DSC_0283
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC) kupitia UVCCM, Deo Ndejembi, akipokea picha ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
DSC_0286DSC_0289
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC) kupitia UVCCM, Deo Ndejembi, akipokea picha ya Dkt. Ali Mohamed Shein Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ).
DSC_0291DSC_0302
Baadhi ya Wenyeviti wa UVCCM mikoani bara na visiwani wakiwa na bendera za Chama na Taifa.

WAZIRI WA NISHATI NA MIGODI WA ALGERIA MHE. YOUCEF YOUSFI AWASILI NCHINI TANZANIA

$
0
0
Waziri wa Nishati na Migodi wa Algeria Mhe. Youcef Yousfi (kulia) akinyanyua kwa furaha zawadi ya kinyago ambayo ni moja  ya zawadi alizokabidhiwa na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kushoto).

Waziri wa Nishati na Migodi wa Algeria  Mhe  Youcef Yousfi ikiwa ni pamoja na ujumbe wake wamewasili nchini Tanzania. Nia na madhumuni ya ziara hiyo ni kudumisha ushirikiano katika sekta za nishati na gesi.
 Waziri wa Nishati na Migodi wa Algeria Mhe. Youcef Yousfi (kushoto) akibadilishana mawazo na Waziri wa Nishati na Madini (kulia) Profesa Sospeter Muhongo mara baada  ya kuwasili kwenye uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini  Dar es Salaam.

 Waziri wa Nishati na Migodi wa Algeria Mhe. Youcef Yousfi  akichangia mada kwenye kikao hicho

 Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia ) akizungumza na  waandishi wa habari (hawapo pichani). Aliyekaa upande wa kushoto ni Waziri wa Nishati na Migodi wa Algeria Mhe. Youcef Yousfi

 Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akizungumza na wakuu wa mashirika na idara wa Wizara ya Nishati na Madini ikiwa ni pamoja na ujumbe wa Waziri wa Nishati na Migodi wa Algeria uliowakilishwa na wakuu wa taasisi na mashirika

 Baadhi ya wajumbe kutoka Wizara ya Nishati na Migodi ya Algeria wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa na wakuu wa Idara kutoka Wizara ya Nishati na Madini.

MAMBO YA NATHAN MPANGALA HAYA.

HAAA HAAAA CHEKA NA WEWE KIDOGO KUHUSU VIBWEKA VYA HUYU YAHAYA

$
0
0

Yahaya kapata trip ya kikazi dodoma,
kufika akaamua kumtafuta mpenzi wake wa UDOM ili apate
pa kujificha,
kesho yake mrembo akamuomba amwazime laki 3,
Yahaya akampa A.T.M Kadi na Pin na kumwambia atumie
vyovyote anavyotaka,
kumbe A.T.M ina elfu 5 tu,
kabla hajashitukiwa akakwea gari ili arudi dar,
njiani simu ikakata chaji,
kafika home kaweka kwenye chaji akalala,
kuamka asubuhi anakuta sms kutoka kwa bosi wake ikisema
"Yahaya nimeweka milioni 10 kwenye akaunti namba yako,
usirudi kwanza dar mpaka uwalipe mafundi".

Mshauri Yahaya ameshika sumu muda huu anataka kujiua.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA WAZIRI WA NISHATI NA MIGODI WA ALGERIA NA UJUMBE WAKE IKULU DAR ES SALAAM LEO.

$
0
0
 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Nishati na Migodi wa Algeria, Youcef  Yousfi (wa kwanza kushoto kwake) aliyeongozana na Ujumbe wake kutoka Kampuni ya Sonatrach na Sonalegaz za nchini Algeria, wakati walipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, kwa mazungumo leo Jan 7, 2014.
 Makamu  wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Waziri wa Nishati na Migodi wa Algeria, Youcef  Yousfi, aliyeongozana na Ujumbe wake kutoka Kampuni ya Sonatrach na Sonalegaz za nchini Algeria, wakati walipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, kwa mazungumo leo Jan 7, 2014.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe kutoka Kampuni ya Sonatrach na Sonalegaz za nchini Algeria, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam leo Jan 7, 2014.
Makamu  wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na  Waziri wa Nishati na Migodi wa Algeria, Youcef  Yousfi,  baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam leo Jan 7, 2014. Kulia ni Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Mhongo. Picha na OMR

NBS YATOA CHANGAMOTO KWA WATANZANIA KUANZISHA NA KUMILIKI VIWANDA ILI KUONGEZA UZALISHAJI WA BIDHAA MBALIMBALI, AJIRA NA KUKUZA PATO LA TAIFA.

$
0
0
Mkurugenzi wa Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Morrice Oyuke ametoa wito huo wakati akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es salaam kutoa taarifa ya fahirisi za uzalishaji wa bidhaa za viwandani hadi kufikia mwaka 2012 zilizowekwa katika makundi mbalimbali kwa kufuata mwongozo wa Umoja wa Mataifa.
Mtafiti na mtaalam wa Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam Prof. Haji Semboje akizungumza wakati wa mkutano huo leo jijini Dar es salaam. Pamoja na mambo mengine amesema juhudi zinahitajika katika kuwahamasisha Watanzania kumiliki viwanda vidogo, vya kati na vile vikubwa.
Sehemu ya waandishi wa habari kutoka vyombo vya habari wakati wa mkutano huo leo jijini Dar es salaam.
=========== ==========  ========

NBS YATOA CHANGAMOTO KWA WATANZANIA KUANZISHA NA KUMILIKI VIWANDA ILI KUONGEZA UZALISHAJI WA BIDHAA MBALIMBALI, AJIRA NA KUKUZA PATO LA TAIFA.

Na.Aron Msigwa.
7/1/2014, Dar es salaam.

Wito umetolewa kwa watanzania kujitokeza kwa wingi katika kuanzisha na kumiliki viwanda vitakavyozalisha bidhaa mbalimbali hapa nchini kwa lengo la kuongeza ajira, kukuza pato la taifa na kupunguza hali iliyopo ya uagizaji wa bidhaa mbalimbali toka nje ya nchi.

Mkurugenzi wa Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Morrice Oyuke ametoa wito huo wakati akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es salaam kutoa taarifa ya fahirisi za uzalishaji wa bidhaa za viwandani hadi kufikia mwaka 2012 zilizowekwa katika makundi mbalimbali kwa kufuata mwongozo wa Umoja wa Mataifa.

Amesema kuwa ongezeko la viwanda nchini licha ya kuongeza ajira kitakwimu lina mchango mkubwa katika kusaidia kupima fahirisi za uzalishaji wa bidhaa za viwandani na kuongeza  kuwa uzalishaji wa bidhaa za viwandani hupima mabadiliko ya kiasi cha bidhaa zilizozalishwa na wazalishaji mbalimbali ambao kwa wastani wamejiajiri kuanzia wafanyakazi 50 na kuendelea.

Amefafanua kuwa Tanzania katika kipindi cha mwaka 2006 hadi 2012 imekua na kiwango cha juu cha mabadiliko ya fahirisi ya bei ya uzalishaji wa bidhaa za viwandani kwa jumla ya asilimia 10.8 ikilinganishwa  na asilimia 2.1 za mwaka 2011.

Ameongeza kuwa fahirisi za uzalishaji wa bidhaa za viwandani kwa mwaka 2012 zimeongezeka na kufikia 328 ikilinganishwa na 296 za mwaka 2011 na kuongeza kuwa ongezeko hilo limechangiwa na uzalishaji wa vinywaji na tumbaku kwa asilimia 16.8%, Viwanda vya chuma 14.6% na ongezeko na bidhaa za nguo na ngozi kwa asilimia -17.7%.

Bw. Oyuke ameyataja makundi mengine yatokanayo na bidhaa za viwandani kuwa ni pamoja na Mbao na bidhaa za mbao 0.3%, Karatasi na bidhaa za karatasi 5.0%, Kemikali, Petroli na bidhaa za Plastiki -7.9%, Bidhaa za udongo, vioo na bidhaa zisizo za metaliki 7.5% na bidhaa zitokanazo na chuma 11.0% .

Naye mtafiti na mtaalam wa Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam Prof. Haji Semboje akizungumza wakati wa mkutano huo amesema kuwa mfumo wa uzalishaji na biashara nchini unatokana na uwepo wa bidhaa za Kilimo na zile zisizo kuwa za kilimo na kuongeza kuwa juhudi kubwa zinahitajika katika kuwahamasisha Watanzania kumiliki viwanda vidogo, vya kati na vile vikubwa.

“Bado tunakabiliwa na changamoto ya umiliki wa viwanda hapa nchini kwa sababu viwanda vingi vikubwa vinamilikiwa na wageni, watanzania walio wengi wanamiliki viwanda vidogo vidogo” amesema Prof. Semboje.

Ameongeza kuwa hivi sasa kuna ongezeko kubwa la bidhaa mbalimbali zikiwemo nguo kutoka nje ya nchi jambo ambalo linaathiri uchumi wa ndani na kusisitiza kuwa kuwa juhudi zinahitajika katika udhibiti wa bidhaa zisizokidhi viwango na ambazo hazina chapa ya eneo zilikotengenezwa ambazo zinapatikana katika masoko ya Tanzania.

Prof. Semboje ameeleza kuwa kutokana na kuongezeka kwa uwezo wa watanzania kununua, kuagiza na kufanya biashara nje ya nchi ipo haja ya watanzania hao  na serikali kwa ujumla kupitia mamlaka husika za uwezeshaji wananchi kiuchumi kuangalia uwezekano wa kuwajenga uwezo wa kununua mitambo inayozalisha bidhaa hizo  na kuileta ndani ya nchini kwa lengo la kuongeza pato la taifa na kuwawezesha wananchi kiuchumi.

“ Ninapenda kutoa wito kwa Taasisi za Uwekezaji nchini kutoa kipaumbele kwa Watanzania katika suala la uwekezaji wa ndani pia kutoa elimu zaidi kwa watanzania katika uzalishaji wa kisasa kwa sababu tayari serikali imeshaweka mipango mizuri ya kuwaendeleza watanzania, changamoto tuliyonayo ni kuitafsiri mipango na sera zilizopo kwa manufaa ya nchi”

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL APOKEA SARAFU YA KUMBUKUMBU YA MIAKA 50 YA MAPINDUZI IKULU DAR LEO

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Meneja wa Sarafu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Jovent Rushaka (katikati) na Mshauri wa masuala ya Sarafu, Hassan Jarufu, wakati walipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam leo Jan 7, 2014 kwa ajili ya kumkabidhi Sarafu ya Kumbukumbu ya miaka 50 ya Mapinduzi. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea Sarafu ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Mapinduzi yenye uzito ya g 16, kutoka kwa Meneja wa Sarafu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Jovent Rushaka (katikati) na Mshauri wa masuala ya Sarafu, Hassan Jarufu, wakati walipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam leo Jan 7, 2014 kwa ajili ya kumkabidhi Sarafu hiyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiitazama  Sarafu ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Mapinduzi yenye uzito ya g 16, baada ya kuipokea kutoka kwa Meneja wa Sarafu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Jovent Rushaka wakati walipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam leo Jan 7, 2014 kwa ajili ya kumkabidhi Sarafu hiyo
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na kwa Meneja wa Sarafu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Jovent Rushaka (kushoto) na Mshauri wa masuala ya Sarafu, Hassan Jarufu baada ya kukabidhiwa Sarafu maalum ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Mapinduzi yenye uzito wa g 16, baada ya kukabidhiwa Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam leo Jan 7, 2014. Picha na OMR

NJE YA MAHAKAMA KUU KANDA YA DAR ES SALAAM LEO ILIKUWA HIVI KABLA YA KESI YA ZITTO KABWE KUTOLEWA UAMUZI.

$
0
0









Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini,Mh. Zitto Z. Kabwe pamoja na Mwanasheria wake,Albert Msando (kulia) wakiwasili katika Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam leo huku wakiongozana na wafuasi wanaopinga kuvuliwa uongozi wake,tayari kwa kwenda kusikiliza kesi yake aliyoifungua dhidi ya Chama Chake cha CHADEMA inayosikilizwa leo Mahakama Kuu.
Wafuasi wa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini,Mh. Zitto Kabwe wakimshangilia kiongozi wao alipokuwa akiwasili Mahakamani hapo leo.

Sehemu ya Wafuasi wa CHADEMA wasiomkubali Zitto Kabwe wakiwa na Mabango yao nje ya Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam

RAIS KIKWETE AKUTANA NA WAZIRI WA NISHATI NA MIGODI WA ALGERIA

$
0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Waziri wa Nishati na Migodi wa Algeria Mhe. Youcef Yousif aliyemtembelea Ikulu Dar es salaam Jana Desemba 7, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya Pamoja na Waziri wa Nishati na Migodi wa Algeria Youcef Yousif pamoja na ujumbe wake, pamoja na Waziri wa Nishati na Madini wa Tanzania Profesa Sospter Muhongo Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe Steven Masele na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhe E. maswi ugemi huo ulipomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 7, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Nishati na Migodi wa Algeria Mhe. Youcef Yousif aliyemtembelea Ikulu Dar es salaam Jana Desemba 7, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsindikiza Waziri wa Nishati na Migodi wa Algeria Mhe. Youcef Yousif aliyemtembelea Ikulu Dar es salaam Jana Desemba 7, 2014
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya Pamoja na Waziri wa Nishati na Migodi wa Algeria Youcef Yousif pamoja na ujumbe wake, pamoja na Waziri wa Nishati na Madini wa Tanzania Profesa Sospter Muhongo Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe Steven Masele na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhe E. maswi ugemi huo ulipomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 7, 2014.

BBALL KITAA CHINI YA MATAA

WAZIRI MUKANGARA AZINDUA BODI MPYA YA BAKITA JIJINI DAR LEO

$
0
0
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dr. Fennela Mukangara akiongea na Wajumbe wa Bodi ya Baraza la Kiswahili la Taifa mara alipozindua Bodi hiyo jana jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) Bi. Martha Qorro akimkaribisha Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dr. Fennela Mukangara (wa kwanza aliyekaa kulia) kuzindua Bodi hiyo jijini Dar es Salaam leo.wapili kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Prof. Hermas Mwansoko.
Mwenyekiti aliyemaliza muda wake wa Bodi ya Baraza la Kiswahili la Taifa Bw. Selemani Hegga akitoa shukrani zake kwa wajumbe wa Bodi hiyo hawapo( pichani) katika shughuli ya uzinduzi wa Bodi hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi Sihaba Nkinga akipata maelezo mafupi kutoka kwa Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) Bw. Godfrey Mngereza kuhusu Ukumbi wa ndani wa Maonyesho wa Sanaa alipotembelea BASATA leo jijini Dar es Salaam (jana), watatu kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleao ya Utamaduni Prof. Hermas Mwansoko.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi Sihaba Nkinga akitoa maelekezo kwa Wadau wa Sanaa alipotembelea Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kujionea shughuli zinazofanywa na Baraza hilo,nyuma ni Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) Bw. Godfrey Mngereza.

MWAKA MPYA MAMBO MAPYA...NEW ARRIVALS @AKCLASSIC

$
0
0
 WALE MABINGWA WA COSMETICS ZA UKWELI KUTOKA MBELE MBELE, AK CLASSIC COSMETICS MWAKA MPYA HUU WAMEWASHUSHIA MZIGO WA VITU VYA TOFAUTI KABISA!!  KUANZIA PRODUCTs ZA KUPUNGUA,TIBA ZA CHUNUSI,PRODUCTs ZA KUNG'ARISHA NGOZI YAKO,DAWA ZA KUONDOA STRETCH MARKS, BODY SHAPERs...NA BIDHAAA ZINGINE LUKUKI MUPYAAAAAA!!EM TUONGOZANE HAPA..

 KWA MAELEZO YA KINA NA PICHA ZAIDI WATEMBELEE www.akclassic.blogspot.com
 KUWEKA ODA NA KUFIKISHIWA BIDHAA MPAKA ULIPO PIGA  0753-482909/0713-468393.




ZITTO KABWE AIBWAGA CHADEMA MAHAKAMA KUU KANDA YA DAR ES SALAAM JIONI YA LEO.

$
0
0
Zitto Kabwe akipeana mikono na Wakili wa CHADEMA,Tundu Lisu baada ya kukibwaga chake chake.
 Wakili wa chama cha CHADEMA,Mh Tundu Lisu akizungumza na vyombo vya habari nje ya Mahakama kuu Kanda ya Dar Es Salam juu ya maamuzi yaliyotolewa na mahakama hiyo kuhusiana na kesi ya Zito Kabwe dhidi ya chama chake.

Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Zitto Kabwe amekibwaga chama chake,kufuatia  Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, John Mkamwa, kuridhia zuio la Zitto asijadiliwe na ngazi yoyote ya maamuzi ya Chadema, hadi kesi ya msingi aliyofungua dhidi ya chama hicho itakapomalizika. Jaji huyo amekubali kesi ya msingi iungurume na itaanza kusikilizwa Februari 13, mwaka huu.

Aidha Wakili wa chama cha CHADEMA,Tundu Lisu ameeleza kutoridhika na maamuziki ya Mahakama,hivyo akabanisha kuwa  Zitto Kabwe atabaki kuwa Mbunge wa Mahakama,na kama tujuavyo Mbunge wa Mahakama una  muda wake basi tujipe muda tuu..alibainisha Tundu Lisu.

 Tundu Lisu akiwatuliza na  kuwasihi wafuasi wa chama chake CHADEMA kutokufanya fujo na badala yake waondoke eneo hilo kwa utulivu na amani.Nje Mahakama makundi ya wafuasi wa CHADEMA na Zitto Kabwe walikuwa wakirushiana mawe kiasi hata mmoja wa wafuasi wa CHADEMA kujeruhiwa kichwani kwa jiwe.
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images