Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 196 | 197 | (Page 198) | 199 | 200 | .... | 1898 | newer

  0 0

  KUNDI bingwa la miondoko ya mwambao, Jahazi Modern Taarab litaanza kutambulisha nyimbo zake mpya mwishoni mwa mwezi huu ambapo mji wa Morogoro utakuwa wa kwanza kupata uhondo huo.  Jahazi watafanya onyesho maalum mjini humo Ijumaa ya Januari 31 ndani ya ukumbi wa Tanzanite Complex.  Hii inakuwa ni mara ya kwanza kwa Jahazi kupiga ndani ya ukumbi huo uliofunguliwa kiasi cha mwaka mmoja uliopita.  Kwa mujibu wa mratibu wa onyesho hilo Warda Makongwa wa Planet FM ya mjini humo, wameamua kuandaa onyesho hilo kufuatia maombi ya mashabiki wengi waliotaka Jahazi nayo ibishe hodi ndani ya Tanzanite Complex.  Warda amesema Jahazi halitaenda hivi hivi bali litaandamana na nyimbo mpya kabisa ambazo hazijawahi kusikika hapo kabla.


  Amefafanua kuwa nyimbo hizo ni sehemu ya maandalizi ya albam mpya ijayo ya Jahazi Modern Taarab inayoongozwa na Mfalme Mzee Yussuf.


  0 0


  Ndege iliyoubeba mwili wa aliyekuwa Waziri wa Fedha Marehemu Dkt. Willium Mgimwa Ilipowasili katika uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere Leo Kutokea Nchini Afrika Kusini alipokutwa na Mauti siku chache zilizopita.
  Mjane Mama Jane Mgimwa(katikati) akiwa na Balozi wa Tanzania nchini Afrika kusini Radhia Msuya(kulia) mara baada ya kuwasili kutoka nchini Afrika kusini
  Naibu Waziri Wizara ya Fedha Saada Mkuya(kulia) akimsindikiza Mke wa Marehemu Mama Jane Mgimwa(katikati)katika chumba cha mapumziko mara baada ya kuwasili katika katika uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere Leo.Kushoto ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Mh. Sophia Simba.
  Baadhi ya Viongozi wa Serikali na Wabunge waliojitokeza kuupokea mwili wa aliyekuwa Waziri wa Fedha Dkt. Willium Mgimwa.
  Katibu Mkuu Kiongozi Ombeni Sefue akitoa heshima kwa kugusa Jeneza Lililobeba mwili wa aliyekuwa Waziri wa Fedha Marehemu  Dkt. Willium Mgimwa Katikati ni Waziri wa Ujenzi Mh. John Magufuli na wa Mwisho ni Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Mh.Fenella Mukangara.
  Mwili wa aliyekuwa Waziri wa Fedha Marehemu Dkt. Willium Mgimwa Ukiingizwa kwenye gari Maalum Tayari kwa ajili ya kuelekea nyumbani kwa marehemu kwa taratibu nyingine za mazishi.
  Mkurugenzi wa Idara ya Habari(MAELEZO) Bw. Assah Mwambene (wa kwanza Kushoto)akisalimiana na baadhi wa Watu waliofika kuupokea Mwili wa wa aliyekuwa Waziri wa Fedha Marehemu Dkt. Willium Mgimwa Leo Jijini Dar es Salaam.

                                                              Picha na Hassan Silayo-MAELEZO

  0 0

    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisani Kitabu cha maombolezo ya kifo cha aliyekuwa Waziri wa Fedha, Dkt. William Mgimwa, aliyefariki dunia Januari 01, 2014 huko nchini Afrika ya Kusini alikokuwa amelazwa kwa matibabu. Dkt. Bilal alifika kuhani msiba huo nyumbani kwa marehemu Mikocheni B, jijini Dar es Salaam, leo jioni.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji mke wa marehemu Dkt. Mgimwa, Jane Mgimwa, wakati alipofika kuhani msiba huo nyumbani kwa marehemu Mikocheni B, jijini Dar es Salaam, leo jioni
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwafariji wanafamilia wa marehemu Dkt. Mgimwa, wakati alipofika kuhani msiba huo nyumbani kwa marehemu Mikocheni B, jijini Dar es Salaam, leo jioni.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwafariji wanafamilia wa marehemu Dkt. Mgimwa, wakati alipofika kuhani msiba huo nyumbani kwa marehemu Mikocheni B, jijini Dar es Salaam, leo jioni.
  Baadhi ya Mawaziri na wabunge waliofika kuhani msiba huo nyumbani kwa marehemu Mikocheni B, leo.Picha na OMR

  0 0

   Magari makubwa yakiwa yamepaki kwenye barabara ya Mandela kuanzia TOT  mpaka Mwananchi ambapo imekuwa kero kwa watumiaji wa barabara hii.
  Hii imekuwa kero kwa watu wengi wanaoitumia barabara ya Mandela kwani magari haya yachukua nafasi kubwa ya barabara
  Pia kuna magari mengine yamepaki kwenye service roads 

  CHANZO: PAMOJA BLOG


  0 0

  Mkurugenzi wa Global Publishers, Eric Shigongo.

  Hiki ndicho ninachokifahamu mimi ndugu yenu.

  Maisha ni vita, maisha ni mapambano na mtindo pekee wa kukusogeza mbele ni kupigana! Hata uwe mwema kiasi gani utakuwa na maadui, Yesu alikuwa nao, Mtume Muhammad alikuwa nao, Mandela alikuwa nao na hata Mahatma Gandhi alikuwa nao.

  Hata ufanyeje maadui watakuwepo tu, utapingwa, utapuuzwa, hivyo basi kamwe usijaribu kuwafurahisha watu, eti unafanya vitu ili watu wakupende, utapoteza muda wako bure.

  Kumbuka kuwafurahisha watu ndio barabara kuelekea kwenye umasikini, siku zote fanya kitu ambacho moyo wako unaridhishwa nacho. Watu watakucheka, watakutukana matusi yote lakini mwisho wa siku kama ukiendelea mbele hao ndio watakuja kukupa mkono wa hongera pale utakapoibuka mshindi.

  USHUHUDA WANGU; Kwa miaka yote kumi na tano ambayo nimeishi na kufanya kazi Dar es Salaam, nimetukanwa sana, nimeitwa majina yote mabaya, nimehukumiwa sana. Badala ya kuwachukia walionitukana na wanaonitukana (hivi sasa wakisoma ) ambacho mimi hufanya ni kuziba masikio na kuyachukua matusi yao kama hamasa kisha kusonga mbele.

  Najua wapo watakaolia pindi nitakapokufa, lakini pia wapo watakaofurahi na kufanya sherehe kwamba nimekufa, cha muhimu kwangu ni urithi nitakaouacha hapa duniani baada ya mimi kuondoka, si urithi wa mali bali idadi ya watu ambao Mungu atasikia sauti zao wakisema "Mtu yule alikuwa mwenye dhambi lakini alisaidia kutupa tumaini na maisha yetu yakabadilika." 

  Hao wakiwa wengi itanitosha, yawezekana sauti zao zitamfanya Mungu aniangalie kwa jicho la huruma na kusema “KARIBU MWANANGU.”
  Nawatakia mwaka mpya wenye mafanikio, kumbukeni katika nchi hii ukifanya kazi kwa nguvu na ukiwa na malengo nafasi ya kufanikiwa ipo bila kujali historia ya maisha yako. 

  NAMUOMBA MUNGU MWAKA HUU 
  UWE WA MPENYO KWA KILA MMOJA WETU.

  Asanteni Mungu awabariki
  Eric Shigongo James
  Mkurungenzi Global Publishers Ltd

  0 0

   : Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifunua pazia kama ishara ya ufunguzi rasmi wa Hospitali ya KMKM Kibweni mjini Zanzibar leo Desemba 4, 2014

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kama ishara ya ufunguzi rasmi wa Hospitali ya KMKM Kibweni mjini Zanzibar leo Desemba 4, 2014 
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitembezwa sehemu mbalimbali baada ya kufungua rasmi Hospitali ya KMKIM Kibweni mjini Zanzibar leo  

  Askari wakakamavu wa kike wa KMKM wakiwa wamesimama kumlaki Rais Jakaya Kikwete alipowasili kufungua rasmi Hospitali ya KMKM Kibweni leo

  0 0

  Pichani ni Uongozi wa juu wa  Chama cha Wasanii wa Filamu hapa nchini.a.k.a Bongo Muvi,kulia ni Katibu Mkuu,William Mtitu,Mwenyekiti,Steven Mengere a.k.a Steve Nyerere,Katibu Msaidizi Bi.Devotha Mbaga,Mweka hazina Mkuu, Issa Mussa Cloud pamoja na Makamu Mwenyekiti ,Mahsein Awadh maarufu kama Dk Cheni wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuchaguliwa hapo jana na wadau mbalimbali wa tasnia hiyo waliokutana kwenye viwanja vya Lidaz club,jijini Dar.
  Pichani ni Mwenyekiti wa chama cha Wasanii wa Filamu nchini a.k.a Bongo Muvi, Steve Mengele ‘Nyerere’ akizungumza mara baada ya kuchagulia kushika wadhifa huo wa uenyekiti,Steve alisema kuwa atahakikisha haki inatendeka kwa kila msanii wa filamu,kuhakikisha kipato kinaongezeka katika tasnia yao,kama vile haitoshi alieleza kuwa atakutana wasambazaji wote wa filamu kuzungumza mikakati mbalimali ya kuhakikisha tasnia hiyo wasanii wake wananufaika na  kazi zao na kujiletea maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.Steve anashika nafasi hiyo ya Uenyekiti iliokuwa imeachwa wazi na Msanii Vincent Kigosi a.k.a Ray.
  “Tatizo kubwa kwa wasanii wa Bongo Movie hawajitambui kama wao ni watu wakubwa. Wanajiuza kirahisi kwa wasambazaji wakati karibu kila nyumba ya Mtanzania haukosi filamu moja ya Bongo Movie,” Aliongeza Nyerere ambaye pia anafahamika kwa jina la ‘Kata simu’.
  “Wasanii wa Bongo Movie tunadhulumiwa kwa sababu hatutambui haki zetu. Leo wasanii watatu wanakwenda Mwanza wanapewa shilingi milioni mbili, Diamond peke yake anapewa shilingi milioni 15,”alisema Nyerere
  .
  Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wasanii wa Filamu,Dk Cheni akiwashukuru wadau mbalimbali waliotoa ushirikiano mkubwa kwa namna moja ama nyingine kuhakikisha uchaguzi wa viongozi katika tasnia hiyo wanapatikana,ikiwa ni shemu ya kuhakikisha maendeleo yanazidi kupatikana ndani ya chama hicho
  Katibu Mkuu wa Chama cha Wasanii wa Filamu a.k.a Bongo Muvi,William Mtitu akizungumza machache na kuwashukuru Wanachama na wadau mbalimbali katika suala zima la kufanikisha kuwachagua viongozi wawatakao,ambao watahakikisha chama chao kinasimama imara.
  Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wasanii wa Filamu nchini a.k.a Bongo Muvi,Vincent Kigosi a.k.a Ray akitoa shukurani kwa wanachama na wadau wa tasnia yao waliofika kwenye uchaguzi huo,Ray amewataka viongozi hao wapya kuendelea kuijenga tasnia hiyo katika suala zima la kuhakikisha inaendelea kukua siku hadi siku.
  Ray akifafanua jambo kwa ufasaha mara baada ya kukabidhi nafasi yake ya uenyekiti kwa mwenyekiti mpya Steve Nyerere.
  Picha ya pamoja
  Mwenyeki wa Bongo Muvi Steve Nyerere na Mdau wa filamu hapa nchini wakiwa katika picha ya pozi.
  Baadhi ya Wasanii wa Bongo Muvi wakifuatilia mchakato wa uchaguzi wa viongozi wao.
  Waratibu wa Uchaguzi huo wa viongozi wa chama cha wasanii wa filamu nchini wakiongozwa na Mama Asha Baraka wakihesabu kura za washiriki waliongombea nafasi mbalimbali katika chama hicho.
  Mratibu wa uchaguzi wa viongozi mbalimbali wa chama cha Wasanii wa Filamu,Mama Asha Baraka akitoa muongozo na kuzungumza machcahe kuhusiana na uchaguzi huo.
  Sehemu ya Wagombea wakisikiliza matokeo yao,William Mtitu,Steve Nyerere,Dada Wastara pamoja na Dk Cheni.
  Baadhi ya Wasanii wa Bongo Muvi wakifuatilia mchakato wa uchaguzi wa viongozi wao.

  0 0
 • 01/05/14--03:02: MSIBA DMV NA TANZANIA
 • Jumuiya ya watanzania Washington Dc inasikitika kutangaza kifo mpendwa wao Zainab Buzohera Dullah au maarufu kwa jina la Zay B aliyefariki dunia saa mbili za usiku wa Jumamosi Januari 4 ,2014. Kwa mujibu wa mume wa marehemu  Zainab alikutwa na umauti huko Doctors Community hospital Lanham Maryland baada ya kuugua kwa muda mfupi. 

  Msiba upo  nyumbani kwa marehemu  5030 57th Ave Apt 303 Bladensburg Md 20710. Mipango ya kusafirisha mwili wa marehemu kwenda Tanzania inaendelea. Harambee itafanyika Jumapili January 5, 2014 saa 10 jioni katika anuani ifuatayo:5401 Annapolis Rd Bladensburg Md 20710.
  Gharama ni $15, 000.

  Tunakuomba tuma mchango wako kwenda CITI BANK. ATT: Ms. Ngalu Buzohera AC no.50070000.
  Routing 9106834936
  Shukran.

  0 0

   Meneja wa kituo cha  Redio Nuru Fm, Victor Chakudika cha mkoani Iringa akimkabidhi Muuguzi Mfawidhi wa Hospitali ya mkoa wa Iringa Rustica Tung'ombe moja ya viti vinavyotumiwa na walemavu , makabidhiano hayo yalifanyika katika hospitali hiyo mwishoni mwa wiki.'
   baadhi ya viti vya walemavu na fimbo za kutembelea vilivyotolewa na redio  Nuru Fm ya mkoani Iringa kwa hospitali ya rufaa mkoa wa Iringa(picha na Denis Mlowe).
    Baadhi ya Wafanyakazi wa Nuru FM wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wafanyakazi wa hospitali ya rufaa mkoa wa Iringa
  =========  =======  ==========
  HOSPITALI YA RUFAA IRINGA YAPATIWA VIFAA 
  Na Denis Mlowe,Iringa

  SHIRIKA lisilo la Kiserikali la Iringa Development of Youth Disabled and Children care (IDYDC) kwa kushirikiana na Redio Nuru Fm ya mjini Iringa wametoa misaada ya viti 5 vya kubebea wagonjwa na fimbo 20 za kutembelea kwenye hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 3.5

  Sambamba na kuisadia hospitali hiyo radio hiyo ilivisaidia vituo vya watoto ya yatima vilivyoko mkoani hapa vya Huruma Center,Sabasaba Center na kituo cha wazee Iringa vitu mbalimbali vikiwemo vyakula, vifaa vya usafi, sabuni na mipira kwa watoto hao.

  Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo wakati wakitimiza miaka mitatu tangu kuanzishwa kwa kituo hicho, meneja wa radio Victor Chakudika,aliitaka jamii kuwa na moyo wa kujitolea kwa jamii inayoishi katika mazingira magumu  kwa lengo la kuisaidia serikali majukumu ambayo wadau wenye uwezo wanaweza kuyatatua.

  Alisema lengo la redio kuwa jirani na jamii inayowahudumia katika kuwapatia matangazo yao ya kila siku hivyo misaada iliyotolewa ni kurudisha faida kwa jamii hiyo na itakuwa inafanyika kila mwaka kwa kutoa misaada kwa wanaohitaji hasa kwa wanaoishi katika  mazingira magumu na vituo mbalimbli vya afya vilivyoko mkoani hapa.

  Chakudika alisema radio hiyo inatambua umuhimu wa kuchangia huduma za afya, kwani bila wananchi husika kutokuwa na afya njema ina maana hata maendeleo hayatakuwepo hivyo ni wajibu wao kwa kusaidiana na serikali ya Tanzania kuhakikisha sekta ya afya inafanya kazi ipasavyo na kuwahudumia watu wote kwa usawa.

  Kwa upande wake Muuguzi Mfawidhi wa Hospitali hiyo Rustica Tung’ombe kwa niaba ya Mganga mkuu aliishukuru radio hiyo kwa kujali na kuthamini maisha ya Watanzania, kwa kuamini kuwa mchango huo si tu ni kusaidia shughuli za hospitali bali pia utasaidia kuongeza viti katika hospitali hiyo na kuwasaidia wagonjwa walemavu  katika kufanya mazoezi pindi wanapohitaji huduma ya vifaa hivyo.

  Alisema kushirikiana kujenga jamii ya Iringa ni jukumu la kila mwananchi hivyo vifaa vilivyoyolewa vitakuwa faida kwa kila mwanajamii na kuwataka kuendelea kutoa misaada katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa.

  0 0

    
   Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na  Bibi Jane Katingo, Mama Mzazi wa Aliekuwa Waziri wa Fedha, Dr. William Mgimwa wakati  alipokwenda  nyumbani kwa marehemu huyo katika kijiji cha Magunga, Iringa  kutoa pole na kuangalia maandalizi a mazishi  Januari 5, 20134.
   Waziri mkuu, Mizengo  Pinda  akizungumza na   jamaa wa karibu wa aliyekuwa waziri wa Fedha, Dr. WilliamMgimwa baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu katika kijiiji cha Magunga, Iringa kuwapa pole  wafiwa  na kukagua maadalizi ya  mazishi Desemba 5, 2014

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwafariji  wanafamilia wa aliyekuwa Waziri wa Fedha, Dr. William Mgimwa baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu katika kijiji cha  Magungua, Iringa kuwapa pole na kukagua maandalizi ya mazishi Desemba 5, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
   Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akisalimiana na  baadhi  ya waombolezaji baada a kuwasili nyumbani kwa  aliyekuwa  Wazri wa Fedha, Dr. William Mgimwa  katia kijiji cha Magunga ambako alikwenda kutoa pole na kukagua maandalizi ya  mazishi Januari 5, 2013. (Picha na  Ofisi ya Waziri Mkuu) 


  0 0


  0 0

   Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete akihutubia baada ya  kupokea maandamano ya watembeaji  kusherehekea miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar katika viwanja vya Maisara mjini Zanzibar leo January 5, 2014.
   Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete akikagua gwaride la Chipukizi kabla ya kupokea maandamano ya watembeaji  kusherehekea miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar katika viwanja vya Maisara mjini Zanzibar leo January 5, 2014.
   Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete akikagua Brass Band ya  Chipukizi kabla ya kupokea maandamano ya watembeaji  kusherehekea miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar katika viwanja vya Maisara mjini Zanzibar leo January 5, 2014. 
   Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na wana UVCCM baada ya  kupokea maandamano ya watembeaji  kusherehekea miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar katika viwanja vya Maisara mjini Zanzibar leo January 5, 2014.PICHA NA IKULU
   Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Mwenyekiwa CCM (Visiwani) na Rais wa Zanzibar  Dkt Ali Mohamed Shein na Viongozi wengine waki imba wimbo wa mashujaa wakati wa  ya kupokea maandamano ya watembeaji  kusherehekea miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar katika viwanja vya Maisara mjini Zanzibar leo January 5, 2014

    Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete akipokea maandamano ya watembeaji  kusherehekea miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar katika viwanja vya Maisara mjini Zanzibar leo January 5, 2014.

  0 0

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini kitabu cha maombolezo wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Dkt William Mgimwa viwanja vya Karimjee hall jijini Dar es salaam leo january 5, 2014
   Rais Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wakitoa heshima zao mwisho kwa mwili wa marehemu Dkt William Mgimwa viwanja vya Karimjee hall jijini Dar es salaam leo january 5, 2014
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji mjane wa marehemu na familia yake wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Dkt William Mgimwa viwanja vya Karimjee hall jijini Dar es salaam leo january 5, 2014. 
  Viongozi mbali mbali wa Serikali wakiwa wamebeba sanduku lenye mwili wa marehemu Dkt William Mgimwa  kwenye  viwanja vya Karimjee hall jijini Dar es salaam leo january 5, 2014 tayari kwa kusafirishwa kuelekea mkoani Iringa ambako ndiko mazishi yake yatafanyika.PICHA NA IKULU

  0 0

  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akisalimiana na Afisa Mawasiliano wa TASAF Zablon Bugingo 

  Makamu wa kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akitia saini kitabu cha wageni alipotembelea banda la TASAF

  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akisikilkiza  maelezo kuhusu  faida na matumizi ya asali ya masega kutoka kwa  Khamis Suleiman Masoud wa kikundi cha JUKUNUM Cooperative cha Vitongoji Kibokoni Pemba 

  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akipewa maelezo ya namna ya kutengeneza lulu toka kwenye gamba la Chaza Bahari na Mwajuma Haji Sharif (wa kwanza kulia mwenye kofia) toka kikundi cha Tujikomboe Co-operative Makombeni Pemba . Wa pili kulia ni Nasra Yusuf Yakuob wa kikundi cha Mwendapole Co-operative Mangapwani Unguja  

  Lulu ikionekana (vidoti) ikiwa imeganda katika gamba la Chaza Bahari kama vilivyokuwa vikioneshwa na washiriki toka Tujikomboe Co-Operative Makombeni Pemba katika Banda la TASAF 

  Chaza Bahari za ukubwa mbalimbali zikiwa na Lulu iliyotengenezwa kwa mtindo wa aina yake zikiwa katika banda la TASAF, bidhaa hizi zinawavutia watu wengi ambao walitembelea banda la TASAF 

  Baadhi ya bidhaa zitokanazo na gamba la Chaza Bahari na vile vitokanazo na Lulu iliyooteshwa kwa taaluma maalum kwenye gamba la Chaza Bahari vikiwa kwenye meza ya maonesho katika banda la TASAF (viwili vya Kushoto ni heleni na kulia ni Pete)

  Pete iliyotengenezwa kutokana na Chaza Bahari ikiwa imevaliwa katika kidole cha mkono wa mtazamaji aliyetembelea banda la TASAF

  Mratibu Msaidizi wa TASAF Unguja  Ali Kassim akikabidhi mfuko wenye makabrasha mbali mbali ya TASAF kwa Makamu wa Kwanza wa Rais Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad alipotembelea banda la TASAF

  SEhemu ya wananchi mbali mbali waliofika kwenye banda la TASAF kupata habari na makabrasha mbali mbali kuhusu TASAF wakati wa maonesho miaka 50  ya Mapinduzi ya  Zanzibar 

  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akipokelewa na Mratibu msaidizi wa TASAF Ali Kassim katika banda la TASAF 


  0 0


  MAAZIMIO YA KIKAO CHA DHARURA CHA KAMATI KUU YA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) KUHUSU HATUA ZA KINIDHAMU DHIDI YA WANACHAMA ZITTO ZUBERI KABWE, DR. KITILA MKUMBO NA SAMSON MWIGAMBA

  UTANGULIZI


  Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ilikaa kikao cha dharura ili kupokea, kujadili na kuamua juu ya utetezi wa mashtaka ya ukiukaji wa Katiba, Kanuni na Mwongozo wa Chama yaliyokuwa yanawakabili aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Zitto Zuberi Kabwe, aliyekuwa mjumbe wa Kamati Kuu Dr. Kitila Mkumbo na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Mkoa wa Arusha Samson Mwigamba. Kikao hicho cha dharura kilifanyika Dar es Salaam kati ya tarehe 3-4 Januari, 2014. Kabla ya kuanza kwa kikao, Kamati Kuu ilipokea taarifa kwamba Zitto Zuberi Kabwe amefungua mashtaka dhidi ya CHADEMA katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam. Aidha, Kamati Kuu ilijulishwa kwamba Mahakama Kuu imetoa amri ya zuio la muda ya kuizuia Kamati Kuu au chombo kingine cha Chama kutokukaa, kujadili na kuamua suala la uanachama wa Zitto Zuberi Kabwe. Kutokana na amri hiyo ya Mahakama Kuu, Kamati Kuu haikujadili na kuamua juu ya mashtaka dhidi yake.

  MASHTAKA

  Watuhumiwa wote watatu walishtakiwa jumla ya mashtaka 11 yanayohusu ukiukaji wa vifungu mbali mbali vya Katiba ya Chama, Kanuni za Uendeshaji Kazi za Chama, Kanuni za Kusimamia Shughuli, Mwenendo na Maadili ya Wabunge wa Chama na Mwongozo wa Kutangaza Kusudio la Kuwania Nafasi za Uongozi Kwenye Chama, Mabaraza na Serikali. Mashtaka yote yalitokana na watuhumiwa kuandaa kile kinachoitwa Mkakati wa Mabadiliko, 2013 kama ifuatavyo:


  1.   Kukashifu Viongozi Wakuu wa Chama, yaani Mwenyekiti wa Chama Taifa Mh. Freeman A. Mbowe, na Katibu Mkuu Dr. Wilbrod P. Slaa;

  2.   Kutokuwa wakweli na wawazi kwa kushirikiana na vikundi vya majungu kwa kuanzisha na kuratibu mtandao wa siri ulioitwa ‘Mtandao wa Ushindi’ nje ya utaratibu wa Chama ili kumwezesha Zitto Zuberi Kabwe kutwaa nafasi ya Mwenyekiti wa Chama Taifa;


  3.   Kutoa tuhuma za uongo dhidi ya viongozi wa Chama na bila kupitia vikao halali vya Chama;


  4.   Kujihusisha na vikundi vyenye misingi ya ukabila, udini na ukanda vyenye makusudi ya kubaguana ndani ya Chama na miongoni mwa jamii;


  5.   Kujihusisha na vikundi na vitendo vya kuchonganisha au kuzua migogoro ndani ya uongozi wa Chama na wanachama wake;


  6.   Kuandaa na kutekeleza mpango wa kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Chama Taifa bila kutangaza kusudio la kufanya hivyo kwa mujibu wa Mwongozo wa Chama;


  7.   Kutengeneza makundi na mitandao haramu ya kuwania uongozi ndani ya Chama kinyume cha Mwongozo wa Chama;


  8.   Kuwachafua viongozi na wanachama wenye nia au kusudio la kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Chama kinyume cha Mwongozo wa Chama;


  9.   Kujihusisha na upinzani dhidi ya Chama na makundi ya majungu ya kugonganisha viongozi na wanachama wakati wa uchaguzi wa Chama;


  10.             Kukashifu Chama na viongozi wa Chama nje ya Bunge kinyume cha Kanuni za Maadili ya Wabunge; na


  11.             Kuchochea mgawanyiko ndani ya Chama kinyume cha Kanuni za Maadili ya Wabunge.


  UTETEZI WA WATUHUMIWA.


  Watuhumiwa wote walijitetea kwa maandishi. Zaidi ya utetezi huo wa maandishi, Dr. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba waliitikia wito wa Kamati Kuu wa kujitetea kwa mdomo mbele yake. Hata hivyo, siku ya utetezi wao, ni Dr. Kitila Mkumbo peke yake aliyejitokeza kwenye Kamati Kuu na kujitetea kwa mdomo. Katika utetezi wake wa maandishi, licha ya kukiri kushiriki katika maandalizi ya kile kinachoitwa Mkakati wa Mabadiliko 2013, Dr. Kitila Mkumbo – kama ilivyokuwa kwa Samson Mwigamba – alikanusha na kukataa tuhuma zote za kukiuka Katiba ya Chama, Kanuni zake na Mwongozo wa Chama. Kwa maneno yake mwenyewe, Dr. Mkumbo alikanusha “kila tuhuma mojamoja na kwa ujumla wake dhidi ya[ke]”, na kwamba mashtaka hayo sio ya kweli na hakuvunja Katiba, Kanuni wala Mwongozo wa Chama.


  Aidha, licha ya kukiri kwake katika kikao cha Kamati Kuu ya Novemba mwaka jana kwamba walioshiriki kuandaa Mkakati huo ni pamoja na mtu anayejulikana kama M2, mara hii Dr. Kitila Mkumbo aliiambia Kamati Kuu kwamba “waraka husika ulikuwa ni wa siri na haukuwahi kusambazwa wala kushirikisha … wanachama au viongozi wa CHADEMA isipokuwa mimi binafsi na Samson Mwigamba….” Vile vile, ijapokuwa katika Kamati Kuu ya Novemba mwaka jana Dr. Mkumbo alidai kutokumfahamu kabisa M2, mara hii aliiambia Kamati Kuu kwamba anamfahamu fika M2 lakini hayuko tayari kumtaja mbele ya Kamati Kuu hadi atakapowasiliana naye!


  USHIRIKI WA ZITTO ZUBERI KABWE KATIKA MKAKATI WA MABADILIKO.


  Itakumbukwa kwamba katika kikao cha Novemba 2013, Dr. Kitila Mkumbo na Zitto Zuberi Kabwe walikataa kata kata kuhusika kwa Zitto Zuberi Kabwe katika maandalizi ya Mkakati wa Mabadiliko. Aidha, Zitto Zuberi Kabwe alidai mbele ya Kamati Kuu kwamba alikuwa ameusikia Mkakati huo kwa mara ya kwanza kwenye Kamati Kuu, na amerudia kauli hiyo mara nyingi na hadharani tangu avuliwe nafasi zake za uongozi. Hata hivyo, wakati wa mahojiano na wajumbe wa Kamati Kuu, Dr. Kitila Mkumbo alikiri kwamba yeye na waandishi wenzake wa Mkakati walimpa Zitto Zuberi Kabwe briefing juu ya Mkakati na kwamba alikuwa anaufahamu. Ukweli huu pia umethibitishwa na mawasiliano ya baruapepe iliyotumwa na Zitto Zuberi Kabwe mwenyewe kwa mtu anayeitwa ‘CHADEMA Mpya 2014’ tarehe 27 Oktoba, 2013, karibu mwezi mmoja kabla ya kikao cha Kamati Kuu ya Novemba iliyowavua madaraka.


  Zaidi ya hayo, baada ya kuonyeshwa waraka wa Chama juu ya mabadiliko ya Katiba ya Chama uliotumwa na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama wakati huo Shaibu Akwilombe Julai 2006 unaothibitisha kwamba mabadiliko ya Katiba yaliyoondoa ukomo wa uongozi yalifanywa kwa uwazi na kwa kushirikisha ngazi zote za Chama, Dr. Kitila Mkumbo alikataa kata kata kujadili suala hilo kwa madai kwamba tayari walishapeleka malalamiko yao kwa Msajili wa Vyama vya Siasa.


  Kuhusu tuhuma zao kwamba kuna ufisadi na ubadhirifu wa fedha za Chama unaofanywa na Mwenyekiti wa Chama, Katibu Mkuu na Mkurugenzi wa Fedha Anthony Komu na kwamba taarifa za matumizi ya fedha ni siri ya viongozi hao watatu, Dr. Mkumbo alionyeshwa taarifa mbali mbali za fedha zilizowasilishwa mbele ya vikao vya Kamati Kuu a Chama ambavyo yeye mwenyewe na Zitto Zuberi Kabwe walishiriki kama wajumbe wa Kamati Kuu. Aidha, Dr. Mkumbo alionyeshwa taarifa za kibenki zinazoonyesha jinsi michango ya Mzee Jaffer Sabodo na michango mingine ya watu binafsi zilivyopokelewa na kutumiwa na taarifa zake kuwasilishwa kwenye vikao vya Kamati Kuu walivyohudhuria yeye na Zitto Zuberi Kabwe.


  Zaidi ya hayo, Dr. Mkumbo alionyeshwa nyaraka za manunuzi ya vifaa vya Chama kama vile vile pikipiki, kadi, bendera, n.k, na jinsi ambavyo uamuzi wa manunuzi hayo yalifanywa na Kamati Kuu ambayo wao wenyewe ni wajumbe na walihudhuria vikao husika. Vile vile, Dr. Mkumbo alionyeshwa ushahidi wa maandishi kwamba Mwenyekiti wa Chama hakuhusika kwa namna yoyote ile katika manunuzi hayo na hakuna karatasi yoyote inayoonyesha saini ya Mwenyekiti katika manunuzi ya vifaa hivyo. Aidha, Dr. Mkumbo hakuweza kuthibitisha kwa namna yoyote kwamba CHADEMA ina mkataba wowote na watu binafsi wanaouza vifaa vya uenezi vya Chama kwa vile Kamati Kuu ya Chama katika vikao ambavyo vilihudhuriwa na Dr. Mkumbo na Zitto Zuberi Kabwe ilikwisharuhusu wafanya biashara binafsi kuagiza vifaa hivyo na kuviuza kwa wanachama wanaotaka kuvinunua. Kwenye yote haya, Dr. Kitila Mkumbo hakuwa na lolote la maana la kuiambia Kamati Kuu.


  MAAMUZI YA KAMATI KUU.


  Baada ya kusikiliza utetezi wa Dr. Kitila Mkumbo na baada ya kumhoji kwa kirefu, Kamati Kuu imeridhika bila mashaka yoyote kwamba Mkakati wa Mabadiliko 2013 haukuwa na lengo la kumwezesha Zitto Zuberi Kabwe kutwaa nafasi ya Mwenyekiti wa Taifa wa Chama peke yake. Mkakati huo ulikuwa na malengo makubwa zaidi ya kukibomoa Chama kwa kukichafua kwa wananchi na kuwachafua viongozi wake wa juu kwa kutumia tuhuma za uongo za ufisadi. Hii ni kwa sababu, kwa maoni ya Kamati Kuu, Chama cha siasa ambacho viongozi wake wa juu wanatuhumiwa kwa ufisadi hakiwezi kuaminiwa na wananchi kama tumaini lao la ukombozi.


  Kamati Kuu imeridhika kwa ushahidi wa nyaraka mbali mbali zilizoandaliwa na Zitto Zuberi Kabwe mwenyewe ama na mawakala wake wakitumia vitambulisho bandia katika mitandao ya mawasiliano ya kijamii kwamba mkakati wa kukibomoa Chama umeandaliwa na kutekelezwa kwa muda mrefu. Mkakati huo ulihusisha pia hujuma dhidi ya Chama kwa kuwaengua wagombea wake katika chaguzi mbali mbali kama ilivyotokea katika majimbo ya Mpanda Mashariki, Musoma Vijijini na Singida Mjini ambapo Zitto Zuberi Kabwe alishiriki moja kwa moja.


  Kwa sababu zote hizo, Kamati Kuu imeazimia ifuatavyo:

  1.    Kwamba kuanzia tarehe ya uamuzi wake, Dr. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba wafukuzwe uanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA); na


  2.    Kwamba, kwa vile Zitto Zuberi Kabwe amekishtaki Chama kinyume na matakwa ya Katiba ya Chama na Kanuni zake, na kwa vile Mahakama Kuu imeamuru vikao vyote vya Chama visijadili wala kuamua suala lolote linalohusu uanachama wa Zitto Zuberi Kabwe, viongozi wa ngazi zote za Chama, wanachama, washabiki na wapenzi wa CHADEMA popote walipo katika nchi yetu na nje ya Tanzania wasishiriki wala kusaidia kwa namna yoyote mikutano yoyote ya nje au ya ndani au shughuli nyingine yoyote ya kisiasa itakayofanywa na Zitto Zuberi Kabwe na mawakala wake kwa jina la CHADEMA.


  --------------------------------

  Dr. Wilbrod P. Slaa


  KATIBU MKUU


  0 0

   Rafiki wa mpendwa wetu Catherine Nyongole akishindwa kujizuia  mara tu alipomuaona mdogo wa marehemu Ngalu Buzohera alipofika nyumbani kwa marehemu kutoa pole na kujumuika nao katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao Zainab Buzohera aliyefariki jana jioni Jan 4, 2014 katika hospitali ya Doctor's Community iliyopo Goodluck Rd, Lanham, Maryland. Msiba upo nyumbani kwa wafiwa 5030 57th Ave, Bladensburg, Maryland na leo baadae kutafanyika harambee ya kuchangisha fedha ilikusaidia kuusafirisha mwili wa marehemu harambee itafanyika 5401 Anapolis Rd, Bladensburg, Marland kuanzia saa 10 jioni(4pm) Lengo ni kujitahidi kumsafirisha mpendwa wetu siku ya Jumatano Jan 8, 2014.Watanzania wakiamua hawashindwi na jambo.
   Watanzania wa DMV wakijumuika na wafiwa nyumbani kwa marehemu.
   Catherine Nyangole mwenye kilemba cheusi pamoja na WanDMV wakimpa pole mdogo wa marehemu Ngalu Buzohera nyumbani kwa marehemu.
   Watanzania wa DMV wakiendelea kutayarisha makulaji kwa ajili ya wageni watakaofika nyumbani kuwapa pole wafiwa.
   Watanzania DMV wakijumuika pamoja na wafiwa nyumbani kwao


  Watanzania wa DMV wakiwafariji wafiwa.

  0 0

  Joe Kahama (mwenye miwani na shati la draft) akiwa na waumini katika ibada na baadaye harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisda la Kimkunda,Kyaka,mkoani Kagera. Katika shughuli hiyo, Joe aliwatia homa wabunge wa majimbo ya eneo hilo pale alipoeleza kuwa hatoongea sana lakini watarajie kumsikia sana siku za mbele. Katika hafla hiyo, Joe alichangia shilingi milioni 3 na kushiriki mnada kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa hilo. Picha zifuatazo ni za tukio hilo.


  0 0

  Mume wa marehemu Dullah na mdogo wa marehemu Ngalu Buzohera wakiwa kwenye harambee ya kuchangisha fedha za kusaidia kusafirisha mwili wa mpendwa wetu marehemu Zainab Buzohera aliyefariki Jumamosi Jan 4, 2014 saa 2 usiku (8pm ET) WanaDMV walijumuika katika harambee iliyofanyika Bladensburg, Maryland na kuchangisha $22,938 kiasi kilichokuwa kinatakiwa ni $15,000 hii inamaanisha wanaDMV wanapoamua hufanya kweli shukurani kwa wote walioshiriki harambee hii kwa njia moja au nyingine lengo ni kufanikisha na Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema tunashukuru kwa kutuwezesha kufanikiwa harambee hii ya mpendwa wetu Zainab Buzohera. WanaDMV tunawashukuru wenzetu wa New York waliofika kwenye harambee hii kuja kusaidia kutimiza malengo.
  Shangazi wa marehemu Jasmine Bernett akiongea kwa niaba ya familia ya Buzohera huku akiwa amejawa na uso wa huzuni aliwashukuru  wote waliofika kwani lengo ni kusaidia kuchangia ili mwili wa marehemu Zainab uweze kusafirishwa nyumbani Tanzania kwa mazishi na matarajio ni kusafirisha siku ya Jumatano na kisomo kinatarajiwa kufanyika siku ya Jumanne jioni mahali patatangazwa baadae.
  Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV Bwn Idd Sandaly akielezea utaratibu wa harambee.
  Umati wa Watanzania waliokuja kwenye harambee.

  Dada Tuma akielezea utaratibu wa mnada utakavyokuwa.
  washika mahesabu wakijiweka sawa kabla ya harambee kuanza.
  Watanzania waliofiika kwenye harambee wakitoa michango yao kabla ya harambee haijaanza/
  Michango ikiendelea kabla ya harambee.
  Timu ya New York ikitoa mchango wake.
  Dada Tuma akiendesha mnada.
  Watanzania kutoka New York katika picha ya pamoja.
  Kutoka kushoto ni Yunus, Bob Miano, Mmiliki wa Vizion One Abdallah Kitwara na Albert Mateso wakiwa kwenye harambee.

  0 0

  Mahakama Kuu Kanda ya Dar Es Salaam,imeahirisha kutoa au kutotoa zuio la muda kwa kamati Kuu ya CHADEMA kutojadili uanachama wa Zitto Kabwe mpaka kesho mnamo  majira ya saa nane mchana.

  0 0

   Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),  Ilala, Jesca Njau (kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi wa Kampuni ya Mbindo, Phillemon Haule (kulia), mfano wa hundi yenye thamani ya sh. mil. 68 ikiwa ni msaada wa kugharamia ukarabati wa miundombinu ya maji katika wodi ya wazazi ya Hospitali ya Rufaa ya Amana, Ilala Dar es Salaam juzi. Wanaoshuhudia ni Mhandisi wa TBL, John Malisa (wa pili kushoto) na Mganga Mkuu wa hospitali hiyo, Dk. Meshack Shimwela.
   Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda ya Ilala, Jesca Njau (kushoto) akimkabidhi  Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Amana, Dk. Meshack Shimwela (wa pili kulia), mfano wa hundi yenye thamani ya sh. mil. 68 ikiwa ni msaada wa kugharamia ukarabati wa miundombinu ya maji katika Wodi ya Wazazi ya katika hospitali hiyo.Wanaoshuhudia makabidhiano hayo yaliyofanyika hospitalini hapo Dar es Salaam juzi, ni Mhandisi wa TBL, John Malisa (wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa Kampuni ya Mbindo, Phillemon Haule.
        Akina mama wakiwa katika wodo hiyo ya wazazi
   Malulu na Bertha Mturi wakiangalia watoto wachanga katika wodi hiyo
   Maulu na Jesca Njau wakitembelea Wodi ya Wazazi.
   Malulu akiwa na Dk. Shimwela alipokuwa akitembelea Wodi ya Wazazi kukagua miundombinu ya maji.

older | 1 | .... | 196 | 197 | (Page 198) | 199 | 200 | .... | 1898 | newer