Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 195 | 196 | (Page 197) | 198 | 199 | .... | 1898 | newer

  0 0
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu  Sera, Uratibu na  Bunge Mhe.William Lukuvi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Mazishi ya aliyekuwa waziri wa  Fedha Marehemu Dk. William Mgimwa akiongea na waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu mwili wa marehemu  kuwasili tarehe nne saa saba mchana uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere  na Shirika la Ndege la Afrika ya Kusini na kuzikwa tarehe  sita katika kijiji cha Magunga mkoani Iringa. Kulia ni Naibu waziri wa Fedha Saada Salum Mkuya.

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu  Sera, Uratibu na  Bunge Mhe.William Lukuvi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Mazishi ya aliyekuwa waziri wa  Fedha Marehemu Dk. William Mgimwa akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) ratiba ya mazishi ya Marehemu Mgimwa aliyefariki jana  nchini Afrika ya Kusini alikokuwa anapata matibabu. Kulia ni Naibu waziri wa Fedha Saada Salum Mkuya. 

  Katibu Mkuu ofisi ya Waziri Mkuu  Dk. Florens  Turuka (kulia) na Katibu Mkuu wizara ya Afya na Stawi wa Jamii Charles Pallangyo (kushoto) wakimsikiliza  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na  Bunge Mhe.William Lukuvi (hayupo pichani) wakati akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu ratiba ya mazishi ya  aliyekuwa waziri wa  Fedha Marehemu Dk. William Mgimwa.

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu  Sera, Uratibu na  Bunge Mhe.William Lukuvi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Mazishi ya aliyekuwa waziri wa  Fedha Marehemu Dk. William Mgimwa akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam  kuhusu ratiba ya mazishi ya Marehemu Mgimwa ambapo  mwili wa marehemu  utawasili tarehe nne saa saba, ibada na heshima za mwisho zitatolewa tarehe tano katika ukumbi wa Karimjee na mazishi yatafanyika  tarehe  sita katika kijiji cha Magunga mkoani Iringa.
  Wapigapicha kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakimpiga picha  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu  Sera, Uratibu na  Bunge Mhe.William Lukuvi (hayupo pichani) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Mazishi ya aliyekuwa waziri wa  Fedha Marehemu Dk. William Mgimwa wakati akiongea nao leo jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano uliopo Ofisi ya Waziri Mkuu kuhusu ratiba ya mazishi.
  Picha na Anna Nkinda - Maelezo.


  Na Kiza Sungura- MAELEZO Dar es Salaam

  KAMATI ya Taifa inayohusika na mazishi ya aliyekuwa waziri wa Fedha Dk. William Mgimwa  imetoa ratiba ya mazishi ambapo mwili wa marehemu utawasili siku ya jumamosi tarehe nne saa saba mchana  katika uwanja wa Mwalimu Nyerere  Terminal  II na kupelekwa nyumbani kwake Mikocheni B jijini Dar es salaam.

  Akizungumza na waandishi wa habari jana Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Uratibu na Bunge) Dk. William Lukuvi alisema kamati itakayohusika na mapokezi ya mwili wa marehemu ni ofisi ya Waziri Mkuu  itakayohusika na ndugu, viongozi na wananchi na Kamati ndogo ya mkoa wa Iringa inayoongozwa na mkuu wa mkoa huyo Dk. Christine Ishengoma.

  Dk. Lukuvi alisema siku hiyo ya jumamosi saa kumi na moja jioni mwili marehemu utapelekwa katika hospitali ya Lugalo na tarehe tano siku ya jumapili saa tano na nusu asubuhi mwili wa marehemu utapelekwa katika  ukumbi wa Karimjee kwa ajili ya ibada na kutoa heshima za mwisho.

  Alisema ifikapo saa nane mchana mwili wa marehemu Dk. Mgimwa utapelekwa uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere Terminal I kwa ajili ya kuelekea Mkoa wa Iringa.

  Ifikapo saa kumi kamili alasiri mwili wa marehemu utakuwa umewasili Mkoa wa Iringa katika uwanja wa ndege Nduli  na kuagwa na viongozi na wananchi wa mkoa huo katika ukumbi wa Siasa kilimo na baada ya hapo utapelekwa kijijini kwake Magunga.

  Waziri Lukkuvi alimalizia kwa kusema kuwa shughuli za mazishi ya Marehemu Dk. Mgimwa zitafanyika 6.1.2014 kuanzia majira ya saa sita mchana  katika kijiji cha Magunga mkoani Iringa na atazikwa kwa heshima zote za Kiserikali.


  0 0


   John Mnyika-Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mbunge wa Jimbo la Ubungo-Chadema
  --
     CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO.

  Kutokana na maswali kutoka kwa wanahabari wa vyumba mbalimbali vya habari juu ya agenda za kikao cha Kamati Kuu kesho,Chama kimetoa kauli ifuatayo;

  Ni kweli kutakuwa na mkutano maalum wa Kamati Kuu ya chama kesho tarehe 3 Januari 2014 Jijini Dar Es Salaam. Ajenda kuu katika mkutano huo ni tatu;

  Mosi: Kupokea taarifa kuhusu mchakato na maudhui ya mabadiliko ya katiba Kamati Kuu itapokea taarifa juu ya
  kupitishwa kwa marekebisho ya sheria ya mabadiliko ya katiba 2013, kupitishwa kwa muswada wa kura ya maoni wa 2013, uteuzi wa wajumbe wa Bunge Maalum na kutolewa kwa Rasimu ya Katiba Mpya.


  Pili: Kupokea utetezi (wa mdomo) wa wanachama watatu kuhusu tuhuma mbalimbali zilizoelekezwa kwao.

  Wanachama hao walishajulishwa makosa yao kwa maandishi na wamewasilisha utetezi wao wa maandishi. Wataitwa kwenye kikao kwa kuzingatia matakwa ya kanuni 6.5.2 (b) na 6.5.2 (d) kupewa nafasi ya kujitetea mbele ya kikao kinachohusika.

  Tatu: Mpango Kazi wa Chama kwa mwaka 2014

  Mpango Kazi wa chama ni sehemu ya hatua za utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Chama wenye dhima ya kuleta uongozi bora, sera sahihi, mikakati makini na oganizesheni thabiti kwa maendeleo endelevu ya chama na taifa.

  John Mnyika
  Mkurugenzi wa Mawasiliano

  0 0


   Vikosi Maalum Vya Ulinzi na Usalama Wakiangalia kwa makini na kuondoa kitu kilichodhaniwa kuwa ni bomu kwenye kituo cha mabasi Shekilango jijini Dar es Salaam,  kwenye makutano ya Barabara za Morogoro na Shekilango Leo Mchana.Hata hivyo vyombo vya ulinzi na usalama vilifanikiwa kuondoa kitu hicho bila madhara yoyote kwa wananchi.Habari zaidi baaadae.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akiwakabidhi funguo ya boti na "Life Jacket 8" kwa Uongozi wa kijiji cha Ilanga/Muze ikiwa ni sehemu ya msaada wa boti na Injini moja kusaidia huduma za afya ya mama wajawazito na wagonjwa mwambao wa Ziwa Rukwa. Msaada huo wenye thamani ya Shilingi Milioni 20 umetolewa na Mfadhili Bi. Adrianne Strong kwa kushirikiana na waumini wenzake wa Kanisa la University United Methodist Church la Washington DC Marekani, Mfadhili huyo alishawishika kutafuta msaada huo baada ya kufika Mkoani Rukwa katika kufanya utafiti na kubaini mambo mengi ikiwemo umbali kati ya wananchi na vituo vya kutolea huduma za afya.
  Hapo awali yalifanyika majaribio ya Boti kabla ya makabidhiano rasmi.
  Kabla ya makabidhiano ya Boti hiyo Mkuu wa Mkoa wa Rukwa aliamuru Boti hiyo kupelekwa ziwani kwa ajili ya majaribio.
  Haikuwa kazi rahisi kwani Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya aliwaongoza viongozi wengine wa Chama na Serikali ya Mkoa na Halmashauri kuvua viatu na kukanyaga maji ili kuweza kufikia Boti hiyo iliyobebwa na wananchi wa kijiji cha Ilanga hadi ziwani.
  Wananchi wa kijiji cha Ilanga wakishirikiana kubeba Boti hiyo hadi ziwani.
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akiongea na wananchi wa Kijiji cha Ilanga muda mfupi kabla ya kukabidhi msaada huo kwa uongozi wa kijiji. Katika hotuba yake hiyo aliwashukuru wote waliosaidia upatikanaji wa msaada huo ambao ni Bi. Adrianne Strong na waumini wenzake wa Kanisa la University United Methodist Church la Washington DC Marekani, Dkt. Francis Mashigala wa Hospitali  Kuu ya Mkoa wa Rukwa aliyekuwa anaratibu msaada huo na Bwana Hussein Kandoro (Mwanasheria Ofisi ya Waziri Mkuu) aliyesaidia kusafirisha Boti hiyo kufika Mkoani Rukwa. Kwa upande mwingine aliuita mwaka huu mpya 2014 kuwa ni mwaka wa afya ambapo alihamasisha juu ya upimaji wa virusi ya Ukimwi, kupiga vita unyanyapaa na Ukimwi, mama wajawazito kujifungulia kwenye vituo vya afya na kupeleka shule watoto wenye umri wa kwenda shule.  
   Mkurugenzi Mtendaji wa Halamashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Ndugu Adam Misana akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Ilanga na kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kuzungumza na wananchi wake. Katika kauli yake alisistizia agizo la Mkuu wa Mkoa wa Rukwa la kuhakikisha kuwa shughuli za uvuvi katika ziwa Rukwa zinafungwa kwa muda wa miezi mitatu kuanzia Januari hadi Machi kupisha mazalio mapya ya Samaki. Alisema kuwa doria zitaendeshwa katika Ziwa hilo na yeyote atakaekamatwa akivua katika kipindi hicho hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake. 
  Dkt. Francis Mashigala wa Hospitali Kuu ya Mkoa wa Rukwa aliyekuwa mratibu wa msaada huo wa Boti akitoa maelezo mafupi juu ya msaada huo  kwa wananchi wa kijiji cha Ilanga.
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa na Msafara wake walipata fursa ya kutembelea Shamba darasa la moja ya shule zilizopo katika kata ya Mtowisa kwenye kijiji cha Ilanga ambalo limepandiwa kwa mbolea aina ya Minjingu Mazao. Serikali ya Mkoa ikiongozwa na Injinia Manyanya ilitoa agizo kwa kila shule kuwa na shamba angalao ekari tano zitakazotumika kama shamba darasa na kusimamiwa na Afsa Ugani wa eneo husika na kupatiwa ruzuku ya pembejeo inayotolewa Serikali. 

  Mpango huo una faida mbili ambapo licha kuwa shamba darasa pia utatibu tatizo la ukosefu wa chakula mashuleni na hivyo kuongeza mahudhurio na kuongeza ufaulu kwa wanafunzi.  (Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @Rukwareview.blogspot.com)

  0 0

  IMG_0647

  Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akikagua shamba la mahindi katika  kijiji cha Mamba wilayani Mlele akiwa katika mapumziko, jimboni kwake Katavi Januari 2, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

   Mbunge wa Mufindi Kusini Menrad Kigola akizungumza  na mmoja wa watoto waishio katika mazingira hatarishi katika kituo cha itulituli.(picha zote na Denis Mlowe)

  Mbunge wa Mufindi Kusini Menrad Kigola akiwa katika sherehe za mwaka mpya 2014 na watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi jijini 
  =========  ========  =========
  NG’O WATAKIWA KUTIMIZA WAJIBU WAO KWA WATOTO YATIMA


  Na Denis Mlowe,Mufindi.


  WAKURUGENZI wa mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) yanayoanzishwa kwa lengo la kuhudumia jamii na hasa watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu nchini wametakiwa kutimiza malengo ya uanzishwaji wa mashirika hayo kwa kuwanufaisha walengwa badala ya kuangalia maslahi yao binafsi.


  Hayo yamesemwa na Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kusini (CCM) Menrad Kigola wakati wa hafla fupi ya kukabidhi msaada wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya shilingi laki 7 kwa kituo cha watoto yatima na wale wanaoishi ktk mazingira magumu wa kituo cha Ifulifuli kilichopo wilaya Mufindi mkoani Iringa na kuongeza kuwa kumekuwa na utitiri wa NGOs ambazo zimekuwa zikipata mamilioni ya pesa kutoka kwa wahisani lakini badala ya kuwasaidia walengwa waliokusudia pesa hizo huishia kuwanufaisha watu wachache kwa manufaa yao binafsi.


  Kigola ambaye pia alipata wasaa wa kula chakula cha mchana na watoto hao kwa lengo la kuukalibisha mwaka mpya amewataka watoto yatima kote nchini kutojiona wa thamani ya chini kufutia maswaibu wanayoyapitia na badala yake kuwekeza muda wao mwingi kusoma hali itakayosaidia Taifa  kuwa na hazina kubwa ya wasomi ktk siku za usoni.


  Alisema imekuwa ni kawaida ya baadhi ya asasi zinazolea watoto yatima kutumia misaada wanayopatiwa kwa manufaa ya waanzilishi kuliko malengo halisi ya asasi hizo.


  “Kuna baadhi yenu mmekuwa mnaanzisha asasi kwa lengo la kuwanyonya watoto yatima hakika haimpendezi mwenyezi MUNGU kuwatumia watoto yatima kwa manufaa yenu” alisema Kigola


  Kwa upande wake Mkurugenzi wa kituo hicho kinachomilikiwa na kikundi cha MPENDE JIRANI,Wilson Ngogi ameitaka serikali kupitia vyombo vyake kuweka mikakati madhubuti itakayosaidia kubaini mashirika yanayokwenda kinyume na sheria na taratibu za uanzishwaji wake.
  0 0


  0 0

  The family of the Late Tony Barretto, his wife Pearl and children Catherinerose (CR) and Johnpaul (JP), regret to announce his untimely demise on 31st December, 2013, in Dar es Salaam.

  We gather to celebrate his life on Saturday 4th January, 2014, at the Diamond Jubilee Hall, Upanga (Malik Road) as follows:
  9:00am -10:30am Spiritual Service 10:30 am-12:30pm Last respects 2:00 pm Crematorium (Makumbusho Bagamoyo Road) Tony's request was that there be no mourning colours or floral tributes.

  Friends wishing to send condolence messages or donate to the charities that Tony supported please contact Johnpaul Barretto, by email: madevu.tb@gmail.com or send to Bank M Limited, Kisutu Branch, Tshs A/C: 0210025551 or US$ A/C: 0210025552 May his soul rest in eternal peace

  0 0

  Makamu mwenyekiti taifa wa chama cha mapinduzi (CCM) Phillip Mangula amewataka viongozi wa matawi kusimamia ipasavyo kanuni za uchaguzi na uongozi na maadili wa chama hicho kwa kupiga vita rushwa hasa kuelekea katika chaguzi za serikali za mitaa zinatarajiwa kufanyika mwaka huu.


  Kauli hiyo ameitoa leo jijini Dar es salaam katika salama za mwaka wakati akizungumza na wajumbe wa halmashauri kuu ya tawi la ofisi ndogo za chama hicho lilipo Mtaa wa Lumumba.


  Amewataka viongozi hao kuweka misingi mizuri ambayo itawezesha kupatikana viongozi wazuri ambao hawatokani na mianya ya rushwa ili kuwa na dira nzuri kuelekea katika uchaguzi Mkuu utakaofanyika 2015.


  “Nataka kanuni za uchaguzi na uongozi na maadili ziheshimiwe ili kupata viongozi ambao hawatatokana na rushwa, na hakikisheni katika vikao vyenu vya chama mnasimamia agenda mbili ambayo ni uchaguzi na kujadili mwenendo wa katiba mpya”.


  “Mkifuatilia hatua moja hadi nyingine katika mchakato wa kuipata katiba kuanzia ushiriki wa wajumbe wa bunge maalum hadi katika mjadala wa wajumbe wakipitia kifungu kimoja hadi kingine mtakuwa na nafasi kubwa ya kutoa maoni yenu pale itakaporudi kwa wananchi,”alisema Mangulla.


  Akizungumzia uwepo wa serikali tatu katika rasimu ya katiba mpya, Mangula amesema bado ni mapema mno kuzungumzia hatia ya suala hilo kwani mchakato wa kuipata katiba bado mrefu ambao mbali na wawakilishi wa bunge maalumu la katiba utashirikisha tena wananchi ambao watapiga kura yao ya mwisho.


  Mbali na kuwapongeza tume ya katiba mpya kwa kufanya kazi kwa uwazi, amewapongeza wanachama wa ccm kwa jinsi walivyoshirikia ama mmoja mmoja au katika kundi katika kuhakikisha wanatoa maoni yao katika rasimu ya katiba ambayo imewasilishwa kwa Rais Jakaya Kikwete mwishoni mwa mwaka jana. 

  0 0

  Mbunge Amina Mwidau, akimkabidhi kikombe cha ushindi Nahodha wa timu ya APL Mwera Shabani Athuman, baada ya timu hiyo kutawazwa kuwa mabingwa wa ligi ya Mwidau CUP, mjini Pangani leo.
   Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga, Amina Mwidau (CUF), akihutubia kabla ya kuchezwa kwa fainali kati ya timu ya APL Mwera na Torino (kulia) ni Katibu wa Chama cha Soka Wilaya ya Pangani, Salehe Swazi.
   Mgeni rasmi katika Mashindano ya Mwidau CUP, Amina Mwidau akijadiliana na viongozi wenzake wakati wa mchezo wa fainali ya Mwidau CUP kati ya APL Mwera dhidi ya Torino leo mjini hapa.
  =========     ========  =========
  APL Mwera yaibuka kidedea Mwidau CUP


  Na Mwandishi Wetu, Pangani.


  TIMU ya Soka la APL kutoka Kata ya Mwera, imetoka kifua mbele huku wakitangazwa mabingwa wapya wa kombe la Mwidau CUP. Timu hiyo iliibuka na ushindi dhidi ya timu ya Torino ya mjini Pangani, ambayo ilishindwa kufua dafu kwa kufungwa kupitia penati.

  Hadi dakika tisini za mchezo huo wa fainali hiyo ya Mwidau CUP zinamalizika timu zote zilishindwa kutambiana na kulazimika kutoka suluhu ya bao 1-1.


  Kutokana na hali hiyo timu hizo ilizilazimu kuingia katika hatua ya matuta ambap kati ya penati nne zilipingwa kwa kila timu, Torino ilipoteza penati mbili huku APL Mwera ilipoteza moja hali hiyowafanya kuibuka na ushindi na kutawazwa mabigwa wa ligi hiyo.


  Timu hizo hadi zinakwenda mapumziko katika kipindi cha kwanza kila timu ilitoka huku ikishindwa kuona nyau ya mwenzake lakini ilipofika dakika ya 57, mchezaji Christopher Gunda wa APL alifanikiwa kuziona nyavu za Torino. Hata hivyo katika dakika ya 62 Torini ilijibu mapigo na kusawazina bao hilo ambapo hadi dakika 90 timu zote zilishindwa kutambiana na kuamua kupigwa matuta.

  Awali akihutubia kabla ya kuanza kwa mchezo huo mgeni rasmi katika mashinda hayo ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga, Amina Mwidau (CUF), aliwataka vijana kuthamini michezo kwani ajira ambayo imekuwa na manufaa kwa Taifa.


  “Kwa imani yangu ninaamini hata hapa Pangani tunao wachezaji wazuri kupitia timu zetu hizi zilizoshiriki ligi hii ya Mwidau CUP ambao wana uwezo wa kufanya vizuri katika timu kubwa za ndani na nje ya nchi yetu,” alisema Mwidau. 

  0 0

  Mmoja wa wafanyakazi katika ofisi ya Mhandisi wa manispaa ya Dodoma akitoa amri ya kuondoa kimoja ya vibanda vilivyojengwa kiholela katika stendi ya daladala Jamatini wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa vibanda vya wafanyabishara.
   Mhandisi masaidizi manisaa ya Dodoma Luanda akitoa maelekezo kwa mama lishe waliopo katika stendi ya Daladala ya Jamatini kujenga vibanda sawa na vipimo vilivyowekwa sawasawa na utaratibu na sheria ndogo ndogo za manispaa hiyo.
   Mwajuma Salum maarufu Bibi Ndonga (64) akimlalamikia kwa kumuonyesha Mhandisi msaidizi wa manispaa ya Dodoma Luanda stakbadhi ambazo amekuwa akilipia katika kipindi cha miezi miwili bila kukabidhiwa eneo la kuweka kibanda chake cha biashara na viongozi wa eneo hilo mhandisi
  huyo alifika kuona utaratibu uliotumika kujenga vibanda vya biashara.
   Asikari wa kutuliza Ghasia wakiwa na mtutu wa Bunduki kusimamia uhakiki wa vibanda vya wafanyabiashara katika stendi ya Daladala Jamatini Dodoma kama utaratibu uliyowekwa ulifuatwa wakati wa ugawaji na ujenzi.

  PICHA NA JOHN BANDA, DODOMA
  PAMOJA BLOG

  0 0


  Join Us Tomorrow at Hill Park Parking Lot, from 12.00 Noon for a Rotaract Kwanza Car Wash Fundraiser!All at the University of Dar es Salaam. Not to miss! Music, Volunteering and much more. Bring a friend and the car! Each car wash is 5,000 and we are trying to raise 250,000/= to support an orphanage center here in Dar es Salaam.

  0 0

  DC KANGOYE KAZINI

  MKUU wa Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, Christopher Kangoye, amesema vijana wakiwezeshwa kikalimifu kushiriki shughuli za uzalishaji, umasikini Tanzania utakuwa historia.  Pia, amewaasa vijana kutumia elimu walizonazo katika kujiajiri ili kuharakisha maendeleo badala ya kukaa vijiweni na kubaki kuwa walalamishi na wakati mwingine kutumiwa na wanasiasa kama ngazi ya kutimiza malengo yao.

  Kangoye, ambaye amekuwa mhamasisha mkubwa wa vijana nchini, amesema Tanzania inaweza kuwa taifa linalotoa misaada kwa nchi zingine na kuachana na utegemezi iwapo vijana wataitambua na kutumika kikamilifu kwa shughuli za maendeleo.

  Aliyasema hayo juzi wakati alipokuwa akizungumza na vijana katika sherehe za kusimikwa Kamanda wa UVCCM wilaya na makamanda wa Kata wilayani Kongwa, ambapo Naibu Spika wa Bunge Job Ndugai, alisimikwa kuwa Kamanda wa Vijana wilaya.

  Kangoye, ambaye alikuwa mgeni rasmi, aliema Hayati Baba wa Taifa, Julius Nyerere na Nelson Mandela ni alama ya harakati za vijana katika maendeleo na ukombozi wa Bara la Afrika na kwamba, walianzisha mageuzi hayo wakiwa vijana.

  ‘Vijana wanatakiwa kuwa mstari wa mbele kukataa umasikini kuanzia ngazi ya familia hadi taifa kwwa kufanya kazi kwa bidii ili kuleta mageuzi ya kiuchumi katikka taifa letu. Tanzania inaweza kuwa taifa linalotoa misaada badala ya kuwa tegemezi iwapo vijana watajitambua na kuitoa kuleta maendeleo.‘Muda wa kukaa vijiweni na kuilalamikia serikali haupo , tuna fursa na rasilimali nyingi zinazoweza kuleta mageuzi ya kiuchumi na kutufanya kuwa taifa tajiri,’ alisema Kangoye.  Alisema harakati zozote ziwe na kisiasa, kiuchumi na kijamii huanzia kwwa vijana na kwamba, ni wakati sasa wa kuamka na kuleta mageuzi kwa maslahi na ustawi wa Tanzania ya sasa na inayokuja.Naye Ndugai akizungumza baada ya kusimikwwa kuwa Kamanda wa Vijana wilayani humo, aliungana na Kangoye kwa kuwataka vijana kujituma katika shughuli za uzalishaji ili kuacha kuwa tegemezi.  Alisema kuna vijana wengi wenye elimu na ujuzi wa kutosha, lakini hawataki kufanya kazi na badala yake wanasubiri serikali iwafanyie kila kitu, jambo ambalo amesema haliwezekani.‘Tufanye kazi ndugu zangu ili tuachane na umasikini na kuwa tegemezi, fursa zipo za kutosha kinachotakiwa ni kuamua kama alivyosema DC Kangoye ili tulete mageuzi kwenye taifa letu’ alisema.  Katibu wa UVCCM Wilaya ya Kongwa, Asia Alamga, alisema kabla ya kuwasimika makamanda hao walifanya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwa ni pamoja na kutembelea wafungwa, wagonjwa kwenye hospitali za wilaya na kata na kutoa misaada ya kijamii.

  0 0  Aida Nakawala 25 mkazi wa kijiji cha Chiwanda Wilaya ya Momba Mkoa wa Mbeya, hivi karibuni alijifungua watoto wanne  mapacha kwa mkupuo(Quadliplets) katika usiku wa kuamkia Mwaka mpya anaendelea vizuri.  Mwanamke huyo ambaye kwa hivi sasa anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Wazazi ya Meta akiwa na watoto wake wote wanne alijifungua majira ya saa 10 alfajiri usiku wa kuamkia Januari Mosi Mwaka huu katika Hospitali ya Wilaya ya Mbozi na watoto wakiwa na uzito wa kawaida tofauti na matarajio ya Wengi.

  Muuguzi na msimamizi wa Watoto katika chumba cha Joto Sista Frolence Maisa amesema hali za watoto ni nzuri ambapo mama mzazi anahitaji kupatiwa vyakula vinavyoweza kumuongezea maziwa mengi kutokana na idadi ya watoto aliyonayo.


  kikosi cha blog ya Mbeya yetu  Kikiongozwa na Joseph Mwaisango ambacho kilifika kumjulia hali kiliguswa na hali hiyo na kujitolea kamsaada kidogo wa nguo za watoto sabuni  chupa na dishi  hivyo kuwaomba wadau wengine kumsaidia mama huyo ili aweze kuwalea vizuri watoto wake.

  Katibu msaidizi wa hospitali ya  Rufaa Mbeya Mwansasu akipokea msaada huo kwa niaba ya mzazi
  KATIKA hali isiyokuwa ya Kawaida Mwanamke mmoja, Aida Nakawala 25 mkazi wa kijiji cha Chiwanda Wilaya ya Momba Mkoa wa Mbeya, hivi karibuni alijifungua watoto wanne  mapacha kwa mkupuo(Quadliplets) katika usiku wa kuamkia Mwaka mpya anaendelea vizuri.'

  Mwanamke huyo ambaye kwa hivi sasa anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Wazazi ya Meta akiwa na watoto wake wote wanne alijifungua majira ya saa 10 alfajiri usiku wa kuamkia Januari Mosi Mwaka huu katika Hospitali ya Wilaya ya Mbozi na watoto wakiwa na uzito wa kawaida tofauti na matarajio ya Wengi. 

  Kwa mujibu wa Muguuzi wa Hospitali ya Wilaya ya Mbozi aliyemfanyia huduma mwanamke huyo, Grace Konga alisema mzazi huyo ni miongoni mwa wazazi 9 waliojifungua katika Mkesha wa Mwaka mpya huku yeye akivunja rekodi kwa kujifungua watoto wanne kwa njia ya kawaida. 

  Muuguzi huyo alisema watoto hao walizaliwa wakiwa na uzito uliotofautiana kwa mtoto  wa kwanza hadi wa mwisho kuanzia kilogramu 1.6,1.5,1.5  na  2.0 ambapo baada ya kuona hali hiyo ilibidi kumpa rufaa kwa ajili ya msaada zaidi katika Hospitali ya wazazi ya Meta ambapo wapo katika Chumba cha Joto hadi sasa. 

  Aidha kwa mujibu wa Muuguzi na msimamizi wa Watoto katika chumba cha Joto Sista Frolence Maisa amesema hali za watoto ni nzuri ambapo mama mzazi anahitaji kupatiwa vyakula vinavyoweza kumuongezea maziwa mengi kutokana na idadi ya watoto aliyonayo. 
  Alisema kwa hivi sasa watoto wananyonya vizuri amb  po maziwa yakipungua kwa mama itahitajika msaada wa maziwa ya Kopo aina ya Laktojeni ili watoto waendelee kupatiwa maziwa kama kawaida na afya zao kuimarika.

  Kwa upande wake Mzazi wa watoto hao Aida Nakawala alisema hali yake kiuchumi siyo nzuri kuweza kumudu kuwalea watoto hao na kuongeza kuwa mume wake ni mkulima aliyemtaja kwa jina la Web Simkanda hivyo anaomba msaada wa hali na mali kutoka kwa wasamaria wema.

  Alisema huo ni uzao wake wanne ambapo mtoto wake wa kwanza anaumri wa miaka saba, anayefuata ana miaka miwili na miezi tisa huku mwingine akiwa amefariki dunia mara baada ya kujifungua kabla ya uzao huu unaofanya kuwa na watoto Sita.

  Alipoulizwa kuhusu kuwepo kwa hali kama hiyo ya kujifungua watoto zaidi ya mmoja katika familia yao alisema Mama yake mzazi amewahi kujifungua mapacha wawili tu na hakuna mtu mwingine aliyewahi kuzidisha idadi hiyo ya watoto kama yeye .

  Hata hivyo kutokana na kuguswa kwa  mahitaji ya binti huyo na wanawe kikosi cha blog ya Mbeya yetu ambacho kilifika kumju ulia hali kiliguswa na hali hiyo na kujitolea kamsaada kadogo hivyo kuwaomba wadau wengine kumsaidia mama huyo ili aweze kuwalea vizuri watoto wake.

  0 0

  DAR ES SALAAM, Tanzania.

  MAKAMU Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula amecharuka na kusema kwamba Wana-CCM ambao wameanza sasa kutangaza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwakani, ni wasaliti wakubwa ndani ya Chama.

  Mangula, ametoa karipio hilo, leo (jana) wakati akitoa Salamu za Mwaka Mpya wa 2014 katika mkutano wa dharura wa Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi Tawi la Ofisi Ndogo ya Makao Makuu jijini Dar es salaam.

  Huku akinukuu kanuni zinalzolinda Maadili ya Uchaguzi na uteuzi wa wagombea ndani ya Chama, Mangula, alisema hadi sasa hakuna kikao chochote cha ngazi ya juu cha Chama, kilichoruhusu wanachama kuanza kutangaza nia za kugombea uchaguzi hadi pale itakapofika mwaka 2015.

  Makamu huyo wa CCM (Bara), alisema, wanachama wanaojipitisha sasa kwa wananchi kwa namna moja au nyingine kwa lengo la kutangaza nia ya kuwania nafasi katika uchaguzi mkuu ujao, ilihali muda wa kufanya hivyo haujafika ni wasaliti au waasi ndani ya Chama.

  Mangula alisema, wanaofanya hivyo ni waansi na wasaliti wakubwa kwa sababu wanaibua na kuendeleza makundi mapemba huku wakijua kwamba hali hiyo hukifanya chama kuwa na wakati mgumu wakati wa uchaguzi.

  Kutokana na hali hiyo, amesisitiza kuwa Chama, hakipo tayari kuona au kuwavumilia watu wachache ndani ya Chama wanaoendelea kuvuruga umoja, mshikamano na misingi ya Chama kwa sababu tu ya umangimeza na uroho wa madaraka uliokiuka kiwango.

  Mangula aliwataka wana-CCM na kwa jumla wakiwemo hao wa Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, kuzingatia wakati wote misingi mizuri ambayo itawezesha kupatikana viongozi wazuri ambao hawatokani na mianya ya rushwa ili kuwa na dira nzuri kuelekea katika uchaguzi Mkuu utakaofanyika 2015.

  CHANGAMOTO
  Wakati Mzee Mangula akiendelea kutoa karipio hilo kwa wanaojitangaza kabla ya wakati kuwania uongozi katika nafasi mbali mbali kabla ya wakati katika uchaguzi mkuu ujao, wapo viongozi kadhaa, akiwemo Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli Edward Lowassa wamekuwa wakifanya matukio na kuzungumza kauli ambazo huonyesha wazi wanajipigia chapuo la kwania Urais 2015.

  Akizungumza katika Ibada mwaka mpya kwenye kanisa la KKKT Monduli, Mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu wa zamani, Edward  Lowassa alikaririwa akisema kuwa  mwaka 2014 ni mwanzo wa safari ya kutimiza ndoto zake za kuona Watanzania watapata elimu bora na bure, na pia kuondokana na umasikini na kwamba ana imani kwa nguvu na msaada wa mungu atafika.

  "Safari hii ina miba, milima na mabonde, lakini kwa msaada wa Yesu nitafika", alikaririwa Lowassa huku mwandishi akisema kiongozi huyo alisema bila kufafanua ni safari ya Kuelekea wapi.

  "Hata hivyo Lowassa amekuwa miongoni mwa wana CCM wanaotajwa kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa mwakani, ingawaje hajatangaza rasmi", alifafanua mwandishi huyo.

  Lowassa alikaririwa zaidi akisema, "Safari hii tumeianza yenye matumaini, yenye ndoto za mtanzania za kuwa na elimu bora na bure,ndoto ya mtanzania kuwa na elimu makini,ndoto ya mtanzania kuwa na maji safi, ndoto ya mtanzania kuwa na matumaini ya maisha".

  Kwa mujibu wa mwandishi huyo, kwa upande mwingine, Lowassa aliwataka wale wanaomuunga mkono kutokuogopa kufanya hivyo hadharani, na kuongeza kuwa wakati ndiyo huu wa kufanya hivyo.

  Wakati Viongozi wa CCM, kama Mzee Mangula wakipaza sauti kupinga wana-CCM kujinadi kabla ya wakati kuwania au kugombea nafasi mbali mbali katika uchaguzi mkuu ujao, baadhi ya viongozi wa CCM wakiwemo Wenyeviti wanaonekana kushabikia kinachokatazwa.

  Katika karamu ya cha kila ambayo Lowassa anadaiwa kuwa huifanya kila mwaka, ambayo aliifanya mwaka mpya, Monduli,  viongozi kadhaa wa CCM waliudhuria na kuzungumza, ambapo Mwenyekiti wa Wenyeviti wa CCM nchini, Mgaya Msindai ambaye ni Mwenyekiti wa CCM, mkoa wa Singida, alikaririwa akitangaza rasmi kuwa Wenyeviti wa Chama hicho wako nyuma ya Lowassa katika safari yake hiyo.

  "Napenda kuwaumbua ndugu zangu kuwa sisi wenyeviti wa CCM tuko pamoja na Mh Lowassa katika safari yake hiyo, kwa sababu tunajua nguvu na uwezo wake katika kuwatumikia wananchi ", alikaririwa Msindai akisema.

  Naye Mwenyekiti wa Wenyeviti wa Umoja wa Vijana wa CCM Nchini, Manko Hiru ambaye ni Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Mara alikaririwa pia akitangaza kwenye chakula hicho kuwa Vijana wanamuunga mkono Lowassa.

  "Sisi Vijana ni wapiganaji wako (Mh Lowassa ) wewe ni jemedari kwa hiyo jemedari hua wa mwisho kufa, sasa Kama kufa sisi Vijana ndiyo tutakuwa wa kwanza kufa kabla yako, tutakukinga, sisi UVCCM ni ngao yako" alikaririwa akisema.

  Mbali na viongozi hao, mbunge wa kuteuliwa UWT  mkoa wa singida, Diana Chilolo ambaye ni Mwenyekiti wa Wenyeviti wa Jumuiya ya Wanawake wa CCM, Tanzania, naye alikaririwa akisema wanawake wana matumaini makubwa na Lowassa.

  "Tuna matumaini makubwa sana na wewe Mh Lowassa kwani uwezo wako unajua Ilani na kila mtanzania, wanawake wanakuunga mkono kwa dhati katika safari yako"alikaririwa Diana akisema katika hafla hiyo inayoelezwa kuhudhuriwa na wageni zaidi elfu nne kutoka kila pembe ya Tanzania.

  RASIMU YA PILI KATIBA MPYA
  Akizungumzia kuhusu msimamo wa Chama Cha Mapinduzi katika muundo wa serikali tatu uliomo katika rasimu ya Pili ya Rasimu ya Katiba mpya, iliyowasilishwa kwa Rais Jakaya Kikwete hivi majuzi, Mangula alisema msimamo wa CCM kuhusu hili unajulikana lakini hakuna sababu ya kuzungumzia kwa kina kwa sasa kwa kuwa mchakato bado mrefu.

  Alisema, alisema, licha ya kwamba msimamo wa CCM unajulikana hadi sasa kuhusu hilo la serikali tatu, bado uamuzi wa mwisho ambao upataswa kuheshimiwa na kila mtu ni wa mwananchi wenyewe baada ya kufanyika kura ya maoni ya katiba.

  "Nataka kanuni za uchaguzi na uongozi na maadili ziheshimiwe ili kupata viongozi ambao hawatatokana na rushwa, na hakikisheni katika vikao vyenu vya chama mnasimamia agenda mbili ambayo ni uchaguzi na kujadili mwenendo wa katiba mpya” Mangula aliiasa Kamati ya Siasa ya Ofisi Ndogo na kuongeza.

  “Mkifualia hatua moja hadi nyingine katika mchakato wa kuipata katiba kuanzia ushiriki wa wajumbe wa bunge maalum hadi katika mjadala wa wajumbe wakipitia kifungu kimoja hadi kingine mtakuwa na nafasi kubwa ya kutoa maoni yenu pale itakaporudi kwa wananchi".

  Mbali na kuwapongeza tume ya katiba mpya kwa kufanya kazi kwa uwazi, amewapongeza wanachama wa CCM kwa jinsi walivyoshirikia mmoja mmoja au katika makundi katika kuhakikisha wanatoa maoni yao katika rasimu ya katiba ambayo tayari imewasilishwa kwa Rais Kikwete.


  0 0


  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na uongozi wa Wilaya ya Nkasi alipotembelea shamba la shule ya Msingi Matala ambalo pia linatumika kama shamba darasa ukiwa ni mpango ulioanzishwa na uongozi wa Mkoa wa Rukwa kusaidia elimu ya kilimo mashuleni na kusaidia upatikani wa chakula kwa wanafunzi. Katika mpango huo kila shule Mkoani Rukwa imetakiwa kuwa shamba ekari zisizopungua tano ambazo zitapatiwa ruzuku ya pembejeo inayotolewa na Serikali na kusimamiwa na afisa ugani wa eneo husika na kuwa shamba la mfano kwa wananchi katika Kilimo bora.
  Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Hassan Kimanta akimuongoza Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi katika ujenzi unaondelea wa mradi wa maji katika kijiji cha Matala Wilayani humo jana.
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akiweka jiwe la msingi katika ujenzi wa mradi wa maji katika kijiji cha Matala Wilayani Nkasi jana. Mradi huo unaofadhiliwa na Serikali, mpaka kukamilika kwake utatumia zaidi ya Tshilingi milioni 300. Jumla ya vijiji kumi (10) katika wilaya ya Nkasi vinategemewa kupata maji ya uhakika kutokana na miradi inayoendelea ambapo zaidi ya Tsh. Bilioni tisa zimeshatengwa kukamilisha ujenzi wake. Changamoto zinazoikabili miradi hii ni kuchelewa kwa fedha kutoka Wizara ya maji pamoja na uhaba wa mabomba na viungio vyake kutoka viwandani.
  Picha ya pamoja.
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akimkabidhi jezi Kapteni wa Timu ya Matala FC Filbert Ndiela kama moja ya kampeni zake Mkoani Rukwa kuhamasisha michezo kwa vijana, ujasiriamali na kujituma katika shughuli za maendeleo. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Kimanta. Katika hotuba yake Injinia Manyanya alitoa onyo kali kwa wananchi wenye tabia ya kulima kwenye vyanzo vya maji na kuwaomba wananchi kujali afya zao kwa kujitolea kupima VVU na kinamama wajawazito kujifungulia kwenye vituo vya afya au zahanati.
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya baada ya hotuba yake na kabla ya kuondoka kwenye mkutano wa hadhara wananchi walimuomba awachezee ngoma yao ya kabila la kifipa ambayo aliitendea haki vilivyo kama anavyoonekana pichani kulia. (Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @Rukwareview.blogspot.com)

  0 0


  Dar es Salaam,Tanzania

  MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imeahirisha kutoa hukumu ya kesi iliyofunguliwa jana na Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Zuberi Kabwe (Chadema), kuhusu ombi la kuitaka Mahakama hiyo kuizuia Kamati Kuu ya Chama hicho, kutomjadili katika kikao ambacho kilipangwa kufanyika leo jijini Dar es Salaam.


  Wanachama wa Chadema, wakitwangana nje ya Mahakama Kuu, jijini Dar es Salaam. 


  Jaji John Utumwa alisitisha kutoa hukumu hiyo mpaka siku ya Jumatatu saa 4:00 asubuhi.Hata hiyo baada ya Jaji huyo kuahirisha kesi hiyo, nje ya Mahakama hiyo kulikuwa na vurugu kubwa baada ya kundi linalo unga mkono maamuzi ya Chadema kutwangana na kundi linalo muunga Zitto Kabwe. 


  Mwanachama wa Chadema, anayepinga hoja za Zitto Kabwe, akimtwanga mfuasi wa Zitto Kabwe. 


  Hatua hiyo ilisababisha Askari wa Jeshi la Polisi kuingilia kati, huku wakiungana na upande wa Chadema na kuwatwanga marundi wafuasi wa Zitto waliokuwa na mambango kama ilivyokuwa kwa wenzao wa Chadema.

  Kesi hiyo ilifunguliwa jana na wakili wa Mbunge huyo Albert Msando huku wakili wa Chadema Tundu Lissu akiweka pingamizi,hata hivyo Jaji John Utumwa wa Mahakama hiyo alitupilia mbali mapingamizi yote yaliyowekwa na Tundu Lissu.

  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akikata utepe kufungua Kituo cha Afya Bumbwini Kiongwe,Jimbo la Bumbwini Wilaya ya Kaskazini B,Mkoa wa Kaskazini Unguja jana,katika shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akifungua pazia  kukifungua Kituo cha Afya Bumbwini Kiongwe,Jimbo la Bumbwini Wilaya ya Kaskazini B,Mkoa wa Kaskazini Unguja jana,katika shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar,(kulia) Waziri wa Afya Juma Duni Haji.
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipata maelezo kutoka kwa Daktari dhamana Abdulwahab  Mohamed,baada ya kukifungua Kituo cha Afya  Bumbwini Kiongwe,Jimbo la Bumbwini Wilaya ya Kaskazini B,Mkoa wa Kaskazini Unguja jana,katika shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar,
    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimuuliza suala Daktari wa huduma za Mama na  Mtoto,Halima Abdalla Saidi,wakati alipotembelea sehemu mbali mbali zinazotoa huduma katika kituo cha Afya Bumbwini Kiongwe,Jimbo la  Bumbwini Wilaya ya Kaskazini B,Mkoa wa Kaskazini Unguja,baada ya  kukifungua jana,katika shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.

  Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa akizungumza na wananchi wa Bumbwini Kiongwe jana,alipofungua kituo cha Afya kijiji hapo,katika katika shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar,(kushoto) Katibu Mkuu Wizara ya Afya  Dk.Saleh Mohamed Jidawi,na Waziri wa Afya Juma Duni Haji,[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
   Wasoma Utenzi kutoka Kiwengwa kaskazini B,Ashura Abdalla na Pili Pandu,wakitoa burudani yao wakati wa ufunguzi wa Kituo cha Afya Bumbwini Kiongwe jana, na mgeni  Rais wa  Zanzibar na
  Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,katika katika shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar, [Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
    Wananchi wa Kijiji cha Bumwini Kiongwe,wakimsikiliza Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa akizungumza baada ya kukifungua Kituo cha Afya kijijini hapo jana,  katika katika shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar,
   Wafanyakazi wa Wizara ya Afya katika vituo mbali mbali waliofika kujumuika na wafanyakazi wa kituo cha Afya Bumbwini Kiongwe,Jimbo la Bumbwini Wilaya ya Kaskazini B,Mkoa wa Kaskazini
  Unguja,wakimsikiliza Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa akizungumza baada ya kukifungua Kituo hicho jana,  katika katika shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar,
   Katibu wa Halmashauri Jimbo la Bumbwini Hassan Ali Kombo,akisoma risala wakati wa sherehe za ufunguzi wa Kituo cha Afya Bumbwini Kiongwe jana, na mgeni  Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,katika katika shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.

  0 0

  Haya sasa… Mchakato wa Kupata Washiriki 30 wa Maisha Plus

  Na washiriki 10 wa Mama Shujaa wa Chakula , 2014 Umeanza!


  Fomu zinapatikana: 


  IRINGA - EBONY FM 87.8

  SONGEA- JOGOO FM 93.0

  SHINYANGA- FARAJA FM 21.3

  ZANZIBAR - ZENJI FM 96.8

  MOROGORO- ABOOD RADIO 89.7

  MWANZA- PASSION FM 99.9

  MTWARA- PRIDE FM 87.8

  BUKOBA- RADIO VISION 98.0FM

  MBEYA- BOMBA FM 104.0

  TABORA- CG FM 89.5

  DODOMA – IMPACT FM 94.4

  ARUSHA- RADIO 5 104.5


  Pamoja na ofisi  za zifuatazo: ..... ACTIONAID,ADGL KIVULINI, CONCERN, COWEA, CVM/APA, KICKSTAR-Money Maker, LBTIC, INADES FORMATION, NORWEGIAN CHURCH AID, OXFAM, SHDEPHA+, RISE TANZANIA,TREE OF HOPE, SASA Foundation, PWC, UZIKWASA, ADP Mbozi, VSO Tanzania, WOPATA, WOWAP, WOMEN PARALEGALS, KAWOCONET, MZALENDO PUB kwa Dar es Salaam.


  Nani Anapaswa kuchukuwa Fomu:

  Mama Shujaa:  Wakina Mama na wasichana Wakulima na Wafugaji, kuanzia miaka 18 na kuendelea


  Maisha Plus:  Vijana, wasichana na wavulana kuanzia umri wa miaka 21 mpaka 26


  fomu hizi zinaweza kujazwa moja kwa moja kupitia tovuti yetu ya www.maishaplus.tv na kupitia Facebook.com/MaishaPlus


  Mwisho wa kurudisha Fomu ni: Tarehe 24 Mwezi wa Kwanza 2014


  Mwaka huu kutakuwa na washiriki Maisha Plus kutoka Burundi, Rwanda, Uganda, Kenya pamoja na Tanzania.  Wahi kuchukua fomu yako sasa ujishindie Mamilioni ya Pesa.   

  MAISHA PLUS/MAMA SHUJAA WA CHAKULA 2014
older | 1 | .... | 195 | 196 | (Page 197) | 198 | 199 | .... | 1898 | newer