Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46194 articles
Browse latest View live

MAKAMBA AWASIHI BODABODA WA MWANZA: URAHISI NA UHARAKA WA UPATIKANAJI LESENI USIWE TIKETI YA VIFO VYA WANANCHI.

0
0
NAIBU wa Waziri wa Wizara ya Sayansi na Teknolojia January Makamba ametaka ujio wake Jiji la Mwanza usihusishwe na Kampeni za chini kwa chini za Urais bali ni kutekeleza ombi la Umoja wa waendesha pikipiki Mkoa wa Mwanza kuwasaidia kupata Bima ya Afya baada ya kuwawezesha kupata pikipiki 1745 za FEKON na si vinginevyo.

Kauli hiyo ya Makamba ameitoa leo wakati wa kufungua kongamano kubwa la siku moja la Umoja wa Madereva wa pikipiki Mwanza lililofanyika katika uwanja wa michezo wa Nyamagana Jijini hapa, alisema kwamba kuna baadhi ya watu wameanza kuhoji ujio wangu Mwanza “Niko hapa kwa ajili ya shughuli hii mliyonialika bali kuja kushiriki Kampeni muhimu ya Bima ya Afya kwa ajili ya Usalama wa badae” na si vinginevyo.

Makamba amesema kwamba upatikanaji wa Leseni kwa urahisi na uharaka usiwe tiketi ya Kifo  kwa wananchi (ZAIDI MSIKILIZE KWA KUBOFYA PLAY)


Awali kabla ya kongamano hilo madereva hao wa bodaboda walifanya maandamano toka makao makuu ya ofisi zao yaliyopo mtaa wa malango mmoja wilayani Nyamagana jijini Mwanza hadi katika uwanja wa historia wa Nyamagana.
Wadau wa Bodaboda wakiingia uwanja wa Nyamagana.
Ndani ya uwanja wa Nyamagana madereva wa Bodaboda wamejitokeza kiasi cha kutosha.


Huku wengine wakizidi kumiminika viwanjani hapa kuhudhuria kongamano lao.
Naibu wa Sayansi na Teknolijia ambaye pia ni mbunge wa Bumbuli mhe. January Makamba akiingia katika uwanja wa Nyamagana kushiriki kongamano la Bima ya Afya kwa waendesha pikipiki maarufu kama Bodaboda wa mkoa wa Mwanza.
Kila mmoja viwanjani hapa alikuwa na kiu ya kusalimiana ana kwa ana na Naibu waziri huyo.
Licha ya kutoa elimu ya uelimishaji kujitambua kwa Bodaboda wa jiji la Mwanza ili kuepukana na maisha magumu uzeeni kwa wadau hao wa usafiri, Mkuu wa mkoa waMwanza Evarist Ndikilo ndiye aliye mkaribisha Mhe. Naibu waziri wa Sayansi na Teknolojia kuhutubia maelfu ya wadau hao. 
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Injinia Evaris Ndikilo kabla ya kumkalibisha mgeni rasmi aliwaasa bodaboda kufuata sheria na kanuni ikiwa ni pamoja na kuhakikisha shughuli zao zinafanyika kwa umakini na kwa amani na utulivu huku wakihakikisha usalama kwanza katika kazi zao kwa kuwa wanatumia vyombo vya moto.


Injinia Ndikilo aliwataka pia kufuata sheria za barabarani kutokana na kuwepo watumiaji wengine, kuwa waangalifu na abiria wengine wanaowachukua kutokana na baadhi yao kuwateka na kuwafanyia ukatili, kuwauwa na kuwanyanganya pikipiki zao nyakati za usiku na kuwataka kukataa kushiriki katika shughuli za uhalifu na badala yake wawabaini na kuwatolea taarifa kwa viongozi na jeshi la polisi.


Makamba alisema kuwa kupatikana kwa Bima za Afya kutatawezesha wanaopata ajali kupatiwa matibabu na kupata fidia pindi wanapopata ajali na kupata ulemavu na kifo jambo ambalo ni hakika lazima wakubali kukata bima kutoka Kampuni ya Ndege Insurance na Shirika la Bima la Taifa (NIC) yaliyokubali kuingia mkataba na wa waendesha pikipiki Mkoa wa Mwanza. 
Ametoa wito kwa Jeshi la Polisi kuachana na tabia ya manyanyaso kwa waendesha pikipiki ya kuwabambikia kesi na makosa bali washirikiane nao kuwabaini walio wachache wanaojipenyeza kujifanya ni bodaboda kumbe ni wanaofanya vitendo vya kihuni, uhalifu na wizi kwa kivuli cha bodaboda jambo ambalo litasaidia pia kuwabaini wanaovunja sheria taritibu zilizopo.
“Mimi leo nimekubali kuwa Mlezi wenu lakini kila kijana lazima amiliki pikipiki yake mwenyewe badala ya kuwa mtu wa kuajiliwa tunahitaji kila mmoja ajiajili kwa kuwa na chombo chake, kazi ya pikipiki iwe ya usalama isiwe leseni ya kifo na ulemavu, msije mkadanganywa na baadhi ya watu kuwa watawatetea bali sisi wa viongozi wa Serikali Taifa, Mkoa, Wilaya na Jiji na kuweni makini kwa kufuata sheria za usalama” alisisitiza
Tangu kuingia mkataba na Kampuni ya Tanzania China Dev Ltd wamefanikiwa kuwakopesha 1745 na awamu ya kwanza umoja umlikopesha pikipiki 265, awamu ya pili 450 na awamu ya tatu pikipiki 1000 na wanachama wapatao 1745 wamenufaika na kupata ajira .
Mstahiki meya wa Jiji la Mwanza Stanslaus Mabula alikuwa ni mmoja kati ya viongozi walioshiriki zoezi la kuendesha bahati nasibu ya waendesha bodaboda 100 waliobahatika kuandikishwa Bima ya Afya bure katika kongamano hilo.
Zoezi la bahati nasibu ya Bima ya Afya linaendelea na waliobahatika ndiyo hawa waliokuwa wakifika mbele katika mstari.
Mwakilishi toka jeshi la polisi na bahati nasibu ya Bima ya Afya.
Kongamano hilo limelenga kutoa elimu kwa waendesha pikipiki juu ya kufuata sheria za usalama barabarani, kusoma na kupata cheti na hatimaye leseni, kuhimiza kuvaa kofia ngumu, kuhimiza kuacha kujichukulia sheria mkononi na kuhimiza waendesha pikipiki kufuata taratibu zote zilizowekwa na serikali kwa wanachama wa wilaya za Sengerema, Nyamagana, Ilemela , Kwimba, Ukerewe, Magu na Misungwi.

Ndikilo kusanyikoni.

Burudani ndani ya Kongamano hazikukosekana.
Wadau walikuja na vyombo vyao.
No Parking.

UTENDAJI KAZI WA MBUNGE FILIKUNJOMBE WAWAVUTIA WAPIGA KURA WAAMUA KUMBEBA MGONGONI

0
0

Wananchi  wa kata  ya Manda  Ludewa wakimfuta  jasho  mbunge  wao  Deo Filikunjombe kama  kumpongeza kwa utekelezaji  mzuri wa ahadi  na uwakilishi  uliotukuka bungeni 
Mbunge wa  jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe akiwa amebebwa na mpiga kura  wake kama  kumpongeza kwa utendaji wake mzuri 
Mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe akifurahia  baada ya  kupongezwa kwa  kubebwa mgongoni na mpiga kura wake.
Mbunge Filikunjombe kati  akipokea  zawadi ya  mbuzi  kutoka kwa  mkazi wa manda huku mkewe Habiba  akishukuru (picha na Blogu ya Francis Godwin)

LORI LA MAFUTA LAKAMATWA LIKISAFIRISHA VIPODOZI HATARI

0
0

Baadhi  ya  vipodozi vilivyokamatwa 
Mifuniko ya  tenki la mafuta  ikiwa imefunguliwa baada ya kutolewa vipodozi 
Ndani ya  lori  hilo  baada  ya  kutolewa  vipodozi  hivyo 
Kamanda wa  polisi  mkoa  wa Iringa Ramadhan Mungi  akionyesha shehena ya  vipodozi  ambavyo  vimekamatwa vikisafirishwa  ndani ya  lori la mafuta  leo 
Kamanda  wa  polisi  mkoa  wa Iringa ,Ramadhan Mungi akionyesha lori la mafuta  lililokuwa na shehena ya vipodozi .
Jina  la kampuni  linalomiliki  lori  hilo 
Maofisa  wa mamlaka ya chakula  na dawa  Manispaa ya  Iringa  wakikagua  vipodozi  hivyo 
Na Francis Godwin Blog

JESHI la  polisi  mkoa  wa  Iringa  limewakamata  watu  wawili  akiwemo  dereva  wa tenki  la  mafuta  lenye namba za usajili  T 247 BHP  wakisafirisha shehena  ya   vipodozi maboksi 779 vikiwa vimewekwa ndani ya tenki  hilo la mafuta  kutoka nchi  za  kusini  mwa Tanzania  kuelekea  jijini  Dar es Salaam .

Kamanda  wa  polisi wa mkoa  wa  Iringa Ramadhan  Mungi  alisema  kuwa  lori hilo lenye namba za usajili  T 247 BHP  likiwa na tela  lenye namba T 598 BMK   ni mali ya kampuni ya  World OIL Ltd  ya  Jijini Dar es Salaam lilikuwa  likiendeshwa na  Mohamed  Sadru (23) mkazi  wa  Mbezi Temboni jijini  Dar es Salaam .

 Mbali  ya  dereva   huyo  pia  jeshi  hilo  linamshikilia mfanyabiashara  aliyekuwa akisafilisha  mzigo  huo  Bw Kassim Kaifa (23) mkazi  wa jijini Dar es Salaam  kwa tuhuma  za  kuhusika na mzigo  huo.

Kamanda Mungi  aliwaeleza  wanahabari  leo    kuwa  mtego wa jeshi  la  polisi  uliweka  baada ya  kupokea  taarifa  kutoka kwa rai  wema kuhusiana na lori  hilo kutumika isivyo  kwa kusafirisha vipodozi  hivyo.

Alisema  kuwa  taarifa  kuhusiana na lori  hilo kusafirisha vipodozi  badala ya  mafuta   waliitapata  kutoka  jana  na mtego  wa  kulikamata  lori hilo  umefanikiwa majira ya saa 9 alfajiri  ya leo 

Hata   hivyo  alisema  kuwa  sehemu  kubwa ya  vipodozi  hizo   ni  vile  ambavyo vilipigwa marufuku na  serikali kutokana na kuwa na madhara  makubwa kwa afya  ya  watumiaji  wa vipodozi  hivyo.

Alisema  kuwa  jeshi la  polisi  limefanikiwa  kumata  vipodozi hivyo kwa  kushirikiana na mamlaka ya  chakula na  dawa ,wakala  wa  barabara  mkoa  wa Iringa  na mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) 

Kamanda huyo  alisema kuwa  watuhumiwa hao   watafikishwa mahakamani  mara  baada ya  uchunguzi  kukamilika na  kuwa ni mapema  kwa  sasa  kuitaja thamani  ya vipodozi  hivyo na  nchi  ambayo lori  hilo  lilikuwa  likitoka kutokana na sababu  za kiusalama.

HAFLA YA UZINDUZI WA KITABU CHA SIMULIZI ZA MZEE MANDELA.

0
0




Ndugu zangu, 

Nami nitapata fursa ya kutoa hotuba. Nitazungumzia umuhimu wa kuhifadhi historia kwenye maandishi ili iwe ni kumbukumbu ya miaka mingi kwa wengine kujifunza. Maana, historia haibadiliki, lakini inapotea.

Na taifa linalodai kuwa watu wake wameelimika tunalipimaje?
Jibu; Ni kwa kuangalia idadi ya machapisho yanayozalishwa kila mwaka. Kuangalia pia ubora wa machapisho hayo.

Na machapisho ni jambo moja, na kuyasoma machapisho hayo ni jambo jingine kabisa.
Tuna lazima ya kuwajengea watu wetu kiu ya kupenda kusoma. Ni moja ya malengo yangu ya kuandika kitabu cha ' Simulizi Za Mzee Madiba'. Kwamba watu watafute vitabu zaidi vya kusoma. 

Leo Jumamosi pale Makumbusho ya Taifa nitasimulia utoto wangu na jinsi nilivyoanza kuelewa maana ya vita vya ukombozi kutoka Ubaguzi wa rangi Afrika Kusini kutokana na kucheza mpira na watoto wa wakimbizi wanachama wa ANC waliokuwa wakikaa jirani na sisi pale Biafra Kinondoni. 

Leo Jumamosi kutakuwa na nafasi pia ya kuulizana maswali, kujadiliana na kupeana ufafanuzi, kama Watanzania.

 Mgeni Rasmi Kwenye Uzinduzi Ni Ndugu Mobhare Matinyi.
Siku Njema.
Maggid Mjengwa 0754678252

TAN COMMUNICATION MEDIA YATOA MSAADA WA VYAKULA KWA WATOTO WAISHIO KATIKA MAZINGIRA MAGUMU

0
0
DSCF1967Vicky Mwakoyo ambaye ni Creative Meneja wa kampuni ya  Tan Communication Media inayomiliki kituo cha Radio 5 Arusha akimkabidhi Mlezi mkuu wa kituo cha Moshono Fundation msaada katika kampeni ya Ushindi  kwa ajili ya kuwafariji watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi katika vituo jijini Arusha juzi tarehe 26/1213 katika viwanja vya Matongee  Carnivo.
DSCF1941
KAMPUNI ya Tan Communication media imetoa misaada ya chakula yenye thamani ya shilingi milioni moja na laki mbili kupitia kampeni ya Ushindi  kwa ajili ya kuwafariji watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi katika vituo kumi jijini Arusha.
Akizungumza wakati wa chakula cha pamoja  cha mchana jana Meneja mbunifu wa kampuni hiyo Vicky Mwakoyo alisema kuwa lengo ni kuwafariji watoto hao ambao jamii ya watanzania imewasahau.
Mwakoyo alisema kuwa  watanzania wanatakiwa kubadilika na kuwajali watoto yatima ikiwa ni pamoja na kutenga muda wao kukaa  na kucheza nao ikiwa ni pamoja na kuwapatia zawadi mbalimbali ili wasijione kama ni wapweke na wameachwa peke yao.
“Watoto wote ni sawa na watoto hawa hawajapenda ni mapenzi ya Mungu hivyo tunawajibu wa kutenga muda wetu na kukaa na watoto hawa kama hivi leo unaona wamefurahi kama watoto wengine wenye wazazi”alisema Mwakoyo
Aidha aliongeza kuwa ni vyema jamii ikajenga utamaduni wa kuwasaidia watoto hawa na isiishie misimu ya kipindi cha sikukuu tu kwa kuwa wanamahitaji ya chakula kila siku.
“Naomba niiombe serikali kupitia Wizara ya maendeleo ya jamii jinsia na watoto kuangalia namna ambavyo inaweza kushirikiana na vituo vya kulelea watoto yatima kwa kuwapatia fungu ili kupunguza ukali wa maisha katika vituo hivyo kwa kuwa vina mchango mkubwa kwa taifa”alisema meneja huyo
Tukio hilo liliofanyika katika viwanja  vya  Matongee  Carnivo  limewakutanisha watoto Yatima zaidi ya Mia moja na hamsini ambapo walipata nafasi ya kushiriki michezo mbalimbali kama kuvuta kamba,kukimbia kwenye magunia,mashindano ya kula na kuimba muziki.
Vituo hivyo vilivyopatiwa misaada ni pamoja na Bethlehemu,Moshono Foundation,Tumain,Mama na Watoto,St.Joseph,Camp Mosses,Kambarage Lemara na Karama.

SIKU ZA MWANZO ZA NAPE NNAUYE

0
0
Maisha ni safari ndefu..Siku za mwanzo za mwanasiasa Nape Nnauye

JOYCE KIRIA HILI NALO NENOOOO UJUE OHOOOO.....!

0
0
https://fbcdn-sphotos-f-a.akamaihd.net/hphotos-ak-prn1/1486740_239965026179198_703462224_n.jpg
"MAELEZO YANGU HAYA YATAONDOA UTATA WOTE NA HOPE MTANIELEWA"

Kiruuuuuuuuuuuuuuuu wananchi wenye hasira kali angalieni msinitoe roho!

Kwa yeyote niliyemkwaza anisamehe bureeee..

Wacha niwape uzoefu-
1. Ndoa ya kwanza nilichangisha kama UTAMADUNI wa wengi kwenye jamii yetu...
Lakini Pamoja na michango tena mingi, tuliingia gharama zetu kubwa sana, na kama haitoshi tulikopa. Baada ya shughuli tulianza KUPIGA MIAYO YA NJAA hatuna ela na madeni juu..binafsi nilijuta sana lakini siku zote MAJUTO ni Mjukuu...(siku isiyokuwa na jina Ndoaikasambaratikia****)
2. Ndoa ya pili.(BOMANI/SERIKALINI)Mungu akanikutanisha na Henry Kilewo anaejua nini maana ya Mke, anaeniheshimu na kunitunza, anaenipenda na kunijali.

Henry akaandaa sherehe NDOGO SANA ndugu jamaa na marafiki WACHACHE sana, kwa GHARAMA ZAKE. Mume wangu Henry Hakusumbua mtu yeyote. Baada ya lile tukio wala hatukupata ile adha ya madeni na kuishiwa pesa kabisa ndani. Tukaendelea na maisha matamu kwa Upendo na Uaminifu mpaka sasa.
3.KUMUHUSISHA MUNGU KWENYE TENDO/ KUBARIKI NDOA..
Kwa Mkristo hili ni tukio kubwa sanaaaaaa. Mungu wetu husamehe makosa yoooote tunayotenda hapa duniani haijalishi! Ukirudi kundini unasamehewa kila kitu. Ndivyo tulivyofanya jana tulirudishwa kundini kisha TUKABARIKIWA. OOOH MY LORD JESUS THANK U SO MUCH KWA REHEMA NA NEEMA. HAKUNA WA KUFANANA NA WEWE YEHOVA. kama Mungu amenisamehe wewe ni nani hata unihukumu??. lets go back to the story
Ningekuwa na mawazo mgando ningefanya sherehe ya kukata na shoka.. kwanza kutetea jina langu(umaarufu mavi) na kuwazodoa waliochonga sana kwamba kanisa nitalisikia kwenye tv na redio na magazeti)

Mazoea- kwa hiyo watu wengi huwa wanafanya sherehe kubwa sana haijalishi anaanza au anaendelea ili KUWAFURAHISHA WATU WENGINE.....na hasa akiwa na jina mjini Atajitutumua hata kama uwezo hana atafanya kila awezalo aweke heshima uchwara mjini.
Mimi Joyce Kiria namshukuru Mungu amenipa Akili za Maisha siyo za darasani za kukopi na kupesti. Nilizotumia wakati ule ikala kwangu!
Ningekuwa na Akili za kukopi na kupesti NINGEFANYA PATI KUBWA SANA BILA KUCHANGISHA MTU kwa sasa namshukuru Mungu si haba uwezo wa sherehe ninao, NA HATA NINGEAMUA KUCHANGISHA NDUGU JAMAA NA MARAFIKI NINGEPATA PESA NYINGI SANA KWA TAARIFA YAKO.
HITIMISHO.
TZ ndo nchi iliyobaki tunachangisha sherehe. Jirani zetu wanachangia ugonjwa na Elimu. Tukubali kubadili mitazamo yetu.

Kama unauwezo wa kufanya Sherehe fanya kwa sababu ni jambo jema sana. Usiwasumbue watu kwa michango. Haina maana hata kidogo.
Kwa sisi ambao hata uhakika wa maisha bora hatuna, tunaishi tu bora kumekucha tunamshukuru Mungu, siyo lazima tuchangishe watu, tujikite ktk kuboresha maisha yetu ili baadae tufanye sherehe bila kutegemea michango, michango ni shida kubwa sana. Kama kuna watu waliomaliza salama bila kubaki na umasikini ni wachache sana...

Au tuendelee kuchanga lakini hizo fedha zikatusaidie kwenye maisha. Wahusika wakaanzishie miradi ya kuwasaidia. Siyo kula kunywa na kucheza kwaito hapana aiseeeee...

Pia jana tulibatiza Watoto wetu ambao Tunawapenda sana. Tungeweza pia kufanya sherehe kubwa... 
Kwa kuwa hatukufanya Sherehe na uwezo tunao, mwakani tutawapeleka Shule watoto kadhaa wenye uhitaji kwenye jamii yetu. Yule binti aliyeshindwa kufanya mtihani wa 4m4 kule rombo, tutampeleka private kwa sababu walisema hawana uwezo huo ndo maana alikuwa tayari kuendelea kusoma wakati mtoto akiwa na wiki kadhaa toka azaliwe, wale watoto 3 wa Stela aliyekatwa mkono huko dodoma kama unawakumbuka, watoto 2 wa Gati Chacha aliyekatwa mguu huko Tarime Mara n.k

Tuchangie maendeleo tuachane na sherehe....Kenya wameweza kwa nini TZ tushindwe?!

Wanangu nitawasihi sana wasifanye SHEREHE bali wasaidie wengine au waanzishe miradi na kama wana uwezo basi wafanye bila kuathiri uchumi wao na wasisumbue watu.

Joyce kiria
Mwanamabadiliko

Nawapenda wote...

ROSE MUHANDO AWAKUNA WAKAZI WA TANGA UWANJA WA MKWAKWANI LEO.

0
0


Mwimbaji mahiri wa nyimbo za kiroho a.k.a Injili,na anaetamba na wimbo mpya wa Facebook,Rose Muhando akiwa sambamba na skwadi lake zima wakilishambulia jukwaa vilivyo jioni ya leo ndani ya uwanja wa Mkwakwani wakati wa muendelezo wa tamasha la Krisimasi lililofanyika leo Mkoani Tanga.Tamasha hilo ndio kwa mara ya kwanza linafanyika mkoani humo,limezindundiliwa jijini Dar siku ya Krisimasi ndani ya uwanja wa Taifa na kuhudhuriwa na watazamaji lukuki.Tamasha hilo baada ya kufanyika mkoani Tanga,kesho litafanyika jijini Arusha na baadae mkoani Dodoma likiwajumuisha waimbaji mbalimbali wa nyimbo za Injili.

 Pichani kulia ni Mwimbaji wa kimataifa wa nyimbo za kusifu na kuabudu kutoka nchini Zambia,Epfrahim Sekeleti akiimba pamoja na mwimbaji mwingine mahiri wa nyimbo injili hapa nchini,Bon Mwaitege pichani shoto.

Mwimbaji mahiri wa nyimbo za kiroho a.k.a Injili,Rose Muhando akiwa sambamba na skwadi lake zima wakilishambulia jukwaa vilivyo jioni ya leo ndani ya uwanja wa Mkwakwani wakati wa muendelezo wa tamasha la Krisimasi lililofanyika leo Mkoani Tanga.Tamasha hilo ndio kwa mara ya kwanza linafanyika mkoani humo,limezindundiliwa jijini Dar siku ya Krisimasi ndani ya uwanja wa Taifa na kuhudhuriwa na watazamaji lukuki.Tamasha hilo baada ya kufanyika mkoani Tanga,kesho litafanyika jijini Arusha na baadae mkoani Dodoma likiwajumuisha waimbaji mbalimbali wa nyimbo za Injili.
 Baadhi ya Waimbaji  wa nyimbo za injili wakilishambulia jukwaa jioni ya leo kwenye tamasha la muendelezo wa Krisimasi,ndani ya uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga.
 Mwimbaji mahiri anaetamba sana na wimbo wake wa Mama ni Mama,Bone Mwaitege akitumbuiza mbele ya watazamaji (hawapo pichani) mapema leo kwenye tamasha la muendelezo Krisimasi lililofanyika ndani ya uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga.

THABIT ABDUL AACHANA NA MASHAUZI CLASIC AIBUKA NA BENDI YAKE YA WAKALI WAO, KUZINDULIWA PASAKA

0
0
Mwanamuziki mkali wa kuandaa na kupangilia muziki mwenye uwezo wa kupiga ala zote za muziki, kama, Kinanda, Gitaa zote yaani Solo, Bass na Rhythim, na zaidi katika kukaanga 'Chips', kuzicharaza drams, Thabiti, Abdul, ameamua kuachana na kazi za kutumwa na badala yake ameamua kuunda kundi lake jipya la Taarab, linalokwenda kwa jina la Wakali wao.

Akizungumza na mtandao huu wa www.sufianimafoto.com, Thabit, alisema kuwa kundi lake hadi sasa lina jumla ya wasanii 13, na linaendelea na mazoezi yake maeneo ya Kinondoni katika ukumbi wa Way Bar ili kujiweka sawa kwa ajili ya kuandaa albam yao ya kwanza itakayokuwa na jumla ya nyimbo nne.

Aidha alisema kuwa katika bendi hiyo iliyo chini ya Meneja wake, Godfrey Ngowi, hadi sasa imekwishaanza kufanya shoo katika baadhi ya maeneo huku ikiwa na waimbaji wengi wapya yaani Ma Under Ground, na wapiga vyombo aliowataja kwa majina kuwa ni Jumanne Ulaya, anayepiga solo, Shomari Zizu, anayepiga Gitaa la Bass, Omary Alli na Ndage Ndage, wanaopiga Kinanda.

Bendi hiyo inatarajia kutambulishwa rasmi mwezi Februari na kuzinduliwa ramsi mwezi wa nne katika Sikuku ya Pasaka, ambapo itazinduliwa rasmi bendi hiyo ikiwa ni pamoja na uzinduzi wa Video zake, Albam na Vyombo vipya, ambapo kila shabiki atakayeingia getini atapatiwa Cd moja ya Audio yenye nyimbo za bendi hiyo.

Thabiti, alizitaja baadhi ya nyimbo hizo kuwa ni pamoja na Kalieni Viti Sio Umbea, Lipo Linalo Kusumbua, Mtu Mzima Hovyo na Subira Haina Kikomo.
ZAIDI BOFYA www.sufianimafoto.com

TASWA FC YAANZA MWAKA MPYA KWA KUICHAPA TWANGA PEPETA 1-0

0
0
 Beki wa timu ya Taswa Fc Sufianimafoto (kulia) akiwania mpira na mshambuliaji wa Twanga Fc, wakati wa mchezo wa kirafiki wa Bonanza la kufunga mwaka na kuukaribisha mwaka mpya wa 2014, lililofanyika kwenye Viwanja vya Leaders Club Kinondoni, leo jioni. Katika mchezo huo Taswa ilianza mwaka mpya kwa ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Juma Pinto katika kipindi cha pili.
 Mshambuliaji wa Taswa Fc, Juma Pinto (katikati) akiwatoka mabeki wa Twanga Pepeta Fc, wakati wa mchezo huo.
 Beki wa Taswa Fc, Athuman (kulia) akiwatoka wachezaji wa Twanga Pepeta.
 Winga wa Taswa Fc, Zahro Milanzi (kulia) akimiliki mpira......
 Kocha wa Twanga Pepeta Fc, ambaye pia ni Mkurugenzi wa bendi hiyo Asha Baraka, akitoa mawaidha kwa wachezaji wake wakati wa muda wa mapumziko.
 Wachezaji wa Taswa Fc, wakimsikiliza Kocha mchezaji Ally Mkongwe, wakati wa mapumziko.


 Benchi la Twanga likiwa haliamini kilichotokea uwanjani...
 Hapa utaenda wewe mpira utabaki.........tulia kama ulivyooooo.....
 Hapiti mtu hapa........
 Mwamuzi wa mchezo huo akichezesha huku akiwa na chupa ya soda ya Novida iliyo na kinywaji cha Konyagi ndani yake......

SIKILIZA WIMBO MPYA WA SNURA - UKO NYUMA SANA

0
0
Baada ya mashabiki kuomba sana Snura kuimba wimbo wa taarabu sasa ameamua kusikiliza vilio vya  mashabiki wake na nakutoa wimbo mmoja wa taarabu na kusema asante kwa mashabiki wake wimbo huo unaitwa "Uko nyuma Sana" - kinanda kimepigwa na Thabit Abdul na aliyepiga gitaa ni Jumanne Ulaya au j4.Usikilize hapa

VIDEO YA SALAMU ZA MWAKA MPYA ZA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHESHIMIWA DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE KWA WATANZANIA,TAREHE 31 DESEMBA,2013

0
0

RAIS KIKWETE AOMBOLEZA KIFO CHA DKT WILLIAM MGIMWA

0
0
Marehemu Dkt. William Mgimwa

TAMASHA LA KRISMASI NA MWAKA MPYA LAFIKIA TAMATI MKOANI DODOMA

0
0
 
 Mwimbaji wa Injili,Upendo Nkone akiimba kwa hisia jukwaani jana jioni kwenye kilele cha tamasha la Krismasi na Mwaka mpya mkoani Dodoma
Pichani shoto ni Mwimbaji mahiri wa muziki wa Injili,Rose Muhando akiwa na skwadi lake zima wakilishambulia jukwaa kwa namna ya pekee kabisa,mbele ya umati mkubwa wa watu (hawapo pichani),waliojitokeza kwa wingi  kwenye kilele cha tamasha la Krismasi na Mwaka mpya mkoani Dodoma.
 Baadhi ya Wapenzi na washabiki wa Injili wakiimba kwa hisia. 
 Pichani kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions Ltd,wanaondaa matamasha ya Krismasi na Pasaka,Bwana.Alex Msama akimkaribisha mgeni rasmi, Mbunge wa Jimbo la Tarime (CCM),Mh.Nyambari Nyangwine kwenye kilele cha tamasha la Krismasi na Mwaka mpya lililofanyika jana jioni kwenye uwanja Jamhuri mkoani Dodoma.


 Vijana wakali wa Vocal,The Voice wakiimba jukwaani jana jioni kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma wakati wa kilele cha tamasha la krismasi na Mwaka Mpya.
Waimbaji mahiri wa nyimbo za Injili pichani kulia ni  Edson Mwasabwite,Tumaini Njole na Faraja Ntaboba kutoka nchni Congo-DRC wakilishambulia jukwaa kwa pamoja kwenye kilele cha tamasha la Krismasi na Mwaka mpya mkoani Dodoma
 Upendo Nkone pichani kulia akiwa sambamba na waimbaji wa nyimbo za Injili, pichani pili kulia Edson Mwasabwite,Faraja Ntaboba pamoja na Mwanadada Tumaini Njole wakilishambulia jukwaa kwa pamoja kwenye kilele cha tamasha la Krismasi na Mwaka mpya mkoani Dodoma.

Mbunge wa Jimbo la Tarime (CCM),Mh.Nyambari Nyangwine ambaye pia alikuwa ndiye mgeni rasmi akizungumza machache kwenye kilele cha tamasha la Krismasi na Mwaka mpya lililofanyika jana jioni kwenye uwanja Jamhuri mkoani Dodoma,Mh Nyangwine alitumia fursa yake ya kuwataka Watanzania kuwa watulivu,wenye kuendelea kujenga mshikamano ili kuendelea kuidumisha amani ya nchi walionayo,pia amewataka vijana popote pale walipo kuacha kulalamika kuhusu suala la ajira,kwani serikali haiwezi kuwapa ajira wote nchini,Badala yake wajitume na kujiajiri wenyewe katika suala mazima ya kujikwamua na lindi la umaskini.Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions Ltd,Bwana.Alex Msama.
 Sehemu ya umati wa watu waliofika kwenye tamasha jana jioni  ndani ya uwanja wa Jamhuri
 Kundi la The Glorious wakiimba jukwaani
 Sehemu ya wapenzi na washabiki waliojitokeza kwenye tamasha hilo 
 Mwimbaji mahiri wa nyimbo za Injili,Bone Mwaitege akiwaimbisha washabiki na wapenzi wa muziki wa injili waliofika kwenye kilele cha tamasha la Krismasi na Mwaka mpya mkoani Dodoma
 Sehemu ya umati wa watu wakifuatilia yaliyokuwa yanajiri kwe jukwaa la tamasha hilo.

CLOUDS FM YAADHIMISHA MIAKA YAKE 14,YATOA MSAADA WA VIFAA MBALIMBALI HOSPITALI YA TEMEKE JIJINI DAR

0
0
 Mtangazaji wa kipindi cha Clouds FM, Dr Isaac Maro akikabidhi msaada wa vifaa kwa Dr Muzdalifat Abeid, bingwa wa magonjwa ya wanawake na uzazi hospitali ya Temeke, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 14 ya Clouds FM.

 Mtangazaji wa kipindi cha Clouds FM, Dr Isaac Maro akikabidhi msaada wa vifaa kwa Dr Muzdalifat Abeid, bingwa wa magonjwa ya wanawake na uzazi hospitali ya Temeke, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 14 ya Clouds FM.
 Mtangazaji wa Kipindi cha Power Breakfast, Paul James (PJ), akikabidhi msaada wa pedi kwa mmoja wa wakina mama walio katika wodi ya wazazi wa hospitali ya Temeke.

 Msanii wa mashairi na kughani, Mrisho Mpoto akikabidhi msaada wa pedi za watoto kwa Mama Leah Othman katika hospitali ya Temeke ikiwa ni katika kuadhimisha miaka 14 ya Clouds FM.

 Mtangazaji wa Jahazi, Ephraim Kibonde akimfariji mmoja wa akina mama katika wodi ya wazazi katika hospitali ya Temeke.

 Mtangazaji wa kipindi cha Ampilifaya, Millard Ayo akimhoji mmoja wa vijana ambao wameacha kutumia madawa kwa msaada wa kituo cha Keko Youth. Clouds FM ilitembelea kituo hicho ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 14 na kutoa msaada wa mashine ya kupaka rangi kwa vijana hao

 Baadhi ya wafanyakazi wa Clouds FM wakiwa katika picha ya pamoja na wanawake waliokuwa katika wodi ya watoto katika hospitali ya Temeke, baada ya kukabidhi misaada yao ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 14 ya Clouds FM.


 Mtangazaji wa kipindi cha Ampilifaya, Millard Ayo akiwa amempakata mtoto, baada ya kutembelea hospitali ya Temeke na kukabidhi misaada ikiwa ni sehemu ya miaka 14 ya Clouds FM.

 Mtangazaji wa kipindi cha Club 10, Perfect Chrispin akikabidhi michango ya papo kwa papo iliyotolewa na wafanyakazi wa Clouds FM kwa kituo cha mwanzilishi wa kituo cha Keko Youth, Yohana Victor Haule. Mbele yao ni mashine ya kupaka rangi iliyotolewa na Clouds FM kama msaada kwa kituo hicho.

  Mwanzilishi wa kituo cha Keko Youth, Yohana Haule akimkabidhi zawadi ya kuku Meneja wa Vipindi wa Clouds, Seba Maganga, ikiwa ni kama shukrani kwa kutembelea kituo chao.
=========  ======= ========

Miaka 14 ya Clouds FM yaadhimishwa kwa shwangwe kubwa

  • Shughuli za kijamii na burudani zatawala


Kituo cha Redio namba moja hapa nchini, Clouds FM kimefikia kilele cha mwezi wa maadhimisho ya miaka 14 toka kimeanzishwa. Maadhimisho hayo ambayo yamefanyika kwa mwezi mzima sasa, yalianza na watangazaji wa vipindi tofauti kwenda mikoa mbalimbali ili kuweza kusherekea miaka hii 14 pamoja na wasikilizaji wao sehemu walipo.

Ikiwa ndio siku ya kilele cha maadhimisho hayo, Clouds FM imetembelea hospitali ya Temeke na kituo cha kuhudumia vijana wanaotumia madawa ya kulevya cha Keko Youth, ambapo misaada mbalimbali imetolewa. Wakiwa katika hospital ya Temeke, Clouds FM imetoa vifaa mbalimbali vya hospitali katika wodi ya wanawake na watoto, huku Keko Youth wakipewa vitendea kazi ambavyo vitawezesha vijana kujiajiri baada ya kumaliza matibabu.

Akizungumzia maadhimisho hayo ya Clouds FM, Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga alisema sherehe hizi kwa mwaka huu ni za kipekee kwa Clouds FM hasa kwa kuwa wameweza kufanikisha  mambo mengi makubwa toka walipoanza. ‘Maadhimisho haya ya miaka 14 kwa mwaka huu yana lengo moja kubwa, kuwashukuru wasikilizaji wetu kwa kutufikisha hapa tulipo, na ndio maana tumeanza kwa kuwapa misaada wanaohitaji, halafu tunamalizia kwa burudani’’ alisema Kusaga.

Akielezea zaidi mafanikio ya Clouds FM kwa kipindi cha miaka 14, Kusaga alisema redio imefanikiwa kuwafikia watu wengi zaidi, imeongeza ubunifu lakini pia kumekuwa na uboreshaji wa hali ya juu wa mitambo ya kutangazia pamoja na maudhui.

‘Kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo tumefanikiwa kushinda tuzo ya Super Brand, na kwa mwaka huu pekee radio imefanikiwa kuanza kusikika mikoa ya Njombe, Songea, Njombe, Sumbawanga, Katavi na Geita, kupitia mitandao kwa wasikilizaji wetu nje ya nchi lakini pia tumefanikiwa kufanya tamasha la Fiesta kwa mafanikio zaidi’ alisema Kusaga.

Kusaga pia aligusia mchango wa Clouds FM katika kuhamasisha maendeleo na uzalendo hapa nchini akitoa mfano wa semina za Fursa ambazo zilifanikiwa kwenda nchi nzima zikizungumza na vijana kuamka na kuchangamkia fursa katika sehemu wanazoishi. ‘Semina za Fursa zimekuwa mfano mkubwa namna Clouds FM ilivoweza kutumia nguvu yake kama radio inayosikilizwa zaidi katika kuchagiza maendeleo, na kwa hakika mafanikio ya semina yamekuwa ni makubwa sana’ alisisitiza Kusaga.
  
Kusaga pia alitoa shukrani za pekee kwa watanzania kwa kuinga mkono Clouds FM sio kwa kusikiliza tu bali hata katika kuhudhuria matamasha na shughuli nyingize za Clouds. Kilele cha maadhimisho ya miaka 14 ya Clouds FM kitamalizika kwa burudani kubwa ambayo itafanyika katika viwanja vya Mwembeyanga ambayo itajumuisha wasanii na watu wengine maarufu.
‘Kumekuwa na mafanikio makubwa katika redio yetu kwa kipindi cha miaka 14, na naomba niseme, bila ninyi wasikilizaji wetu tusingeweza kufika hapa’ alimaliza Kusaga

TIMU YA MADEREVA TAXI IRINGA ''YAIGAGADUA'' 2-1 TIMU YA MADEREVA DALADALA KOMBE LA IRINGA SERVICE STATION

0
0

Mgeni  rasmi  katika mashindano hayo kamanda wa  polisi  mkoa wa Iringa,Ramadhan Mungi akikabidhi  zawadi kwa mshindi wa  pili timu  ya daladala  Iringa
kamanda  wa  polisi  mkoa  wa Iringa Ramadhan Mungi  akikabidhi zawadi  kwa mabingwa  wa mashindano  hayo zawadi  ambazo ni jezi, mpira  na  fedha kiasi 

Hiki ndicho  kituo  kilichofadhili mchezo  huo 

Na  Francis Godwin,Blogu.
MASHINDANO  ya soka  kwa  ajili ya  kuhamasisha  utii wa  sheria  za usalama  barabarani kwa madereva mjini  Iringa  yamemalizika   kwa  timu ya madereva   Taxi  mjini Iringa  kuibika na ubingwa katika mashindano  hayo.

Mashindano  hayo  yaliyodhaminiwa na kituo cha mafuta  cha Iringa Service Station yalishirikisha  timu  4   za madereva wa  daladala,gari  pick-up,madereva  daladala ,madereva  Taxi na madereva boda boda .

Katika  mchezo  huo   ulioambatana na   hafla ya kuuaga  mwaka  2013 na kuukaribisha   mwaka 2014  na  kupigwa katika  uwanja  wa Samora Iringa ,kamanda  wa  polisi  mkoa  wa Iringa Ramadhan Mungi ndie alipata  kuwa mgeni wa  rasmi katika mchezo  huo ambao ulionyesha  kuwa na mvuto mkubwa  kutokana na timu zote  kuonyesha uwezo wake.

Mbali  ya  timu ya daladala  kufanikiwa  kuonyesha uwezo  wao mkubwa kwa  kuifunga  ngoli la  kufutia machozi kwao  goli  lililofungwa  dakika ya  10  ya mchezo  ila bado  timu ya Taxi  haikukubali  kushindwa katika  mchezo huo.

Hadi  timu  zote  mbili  zinakwenda mapumziko kipindi  cha kwanza  timu ya Taxi ilikuwa haijapata  kuliona  lango la timu ya daladala .

Hata   hivyo  kipindi  cha  pili  kilikuwa na neema  kubwa kwa  timu ya daladala ila bado walishindwa  kutumia vema neema  hiyo  ya magoli  zaidi ya mawili  ya wazi .

Kasoro  kubwa  zilizojionyesha kwa  timu ya daladala ndizo  zilipelekea  timu ya Taxi kujipatia  goli la kwanza  ikiwa ni dakika 65 ya mchezo na  kuongeza goli la pili dakika ya 85 na  kuibuka na ushindi mnono wa goli 2-1

kwa ushindi  huo  timu ya Taxi iliibuka na zawadi  ya jezi  seti  mmoja ,mpira mmoja na Tsh 200,000  wakati  timu ya daladala  ikiambulia jezi  seti moja, mpira  mmoja na Tsh 100,000 huku mshindi wa tatu timu ya boda boda ikipata  seti  ya  jezi ,mpira mmoja na Tsh 100,000 na timu  iliyoshika nafasi ya  nne  timu  ya Pick up  aikipata  seti  ya  jezi ,mpira mmoja na Tsh 50,000

Mratibu  wa  mashindano  hayo Feisal Asas  alisema  kuwa  lengo la kituo  chake  cha Iringa ServiceStation  kuanzisha mashindano  hayo ni  kuamusha hamasa ya michezo kwa   vijana  hasa kwa madereva hao pamoja na  kuwapa  elimu ya usalama  wa barabarani.

Awali mwenyekiti  wa kamati ya usalama barabarani mkoa  wa Iringa  Salim Asas  alisema  kuwa jitihada mbali mbali zimekuwa  zikifanyika na kamati  hiyo  katika  kutoa  elimu na mafunzo zaidi kwa madereva ili  kupunguza  idadi ya ajali  za  barabarani .

Akizungumza kabla ya kukabidhi  zawadi mgeni rasmi ,kamanda wa  polisi  mkoa  wa Iringa Ramadhan Mungi  alisema  kuwa mashindano  hayo  ni chanchu kwa madereva  kujikumbusha sheria za usalama  barabarani.

Kwani  alisema ajali  za barabarani sehemu  kubwa  zinachangiwa na madereva  wasiozingatia  sheria hivyo  iwapo madereva  hawatakuwa makini vifo vya  watanzania  vitokanavyo na ajali  vitaendelea  kuongezeka  zaidi.

Alisema  kuwa takwimu  zinaonyesha  kuwa kati ya mwaka  2012  watu 13  walikufa kwa ajili ya  boda  boda na mwaka 2013 ni  watu 27 wakati  waliojeruiwa  pia  wamezidi  kuongezeka na kuwa sehemu kubwa  ajali  za boda boda zimekuwa nyingi zaidi.

Kamanda Mungi  alipongeza  jitihada za  kamati ya  usalama barabarani  chini ya mwenyekiti  wake Asas kwa kujitolea  kusomesha madereva bodaboda zaidi ya 10000 kwa  kipindi cha miaka miwili  iliyopita. 
===========  ======= =======

Wachezaji wa  timu  daladala  Iringa  wakipita  kuwapa mkono madereva Taxi

Timu  ya Taxi
timu ya  Daladala  Iringa
Shabiki  wa  Taxi
Kamanda  wa polisi Iringa Ramadhan Mungi  akitoa  neno  kwa  madereva hao 
Mratibu  wa mashindano  hayo  kushoto Bw Feisal Abri Asas akifuatilia mashindano hayo  katika  uwanja wa  Samora 
Furaha ya  ushindi  baada ya  kuinyuka  timu ya daladala  Iringa
Ushindi  ulivyowapagaisha mashabiki na wachezaji wa  timu ya Taxi Iringa
Viongozi  mbali mbali wakiwa  katika meza kuu kabla  ya kukabidhi  zawadi kwa bingwa wa mashindano hayo  kutoka kushoto ni katibu  wa chama cha soka Iringa Ramadhan Mahano , mwenyekiti wa kamati ya  usalama  barabarani  mkoa wa Iringa Salim Abri Asas ,mgeni rasmi kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi,  mjumbe wa  soka  Iringa mzee Mwakasala na Ambwene
Zawadi  kwa mshindi  wa  nne  timu ya  magari  madodo  jezi ,Tsh 50,000

Mh. Lowassa alivyoukaribisha mwaka mpya 2014 kijijini kwake Ngarashi,Monduli

0
0

Waziri Mkuu mstaafu na mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akizungumza katika tafrija aliyoiandaa kwa wananchi wake na wageni mbalimbali ya kuukaribisha mwaka mpya 2014,iliyofanyika jana nyumbani kwake Ngarashi Monduli.Pembeni yake ni mkewe mama Regina Lowassa.

Waziri Mkuu mstaafu na mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwasalimia wageni waalikwa waliofika kwenye tafrija hiyo aliyoiandaa kwa wananchi wake na wageni mbalimbali ya kuukaribisha mwaka mpya 2014,iliyofanyika jana nyumbani kwake Ngarashi Monduli.
Waziri Mkuu mstaafu na mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (katikati) akizungumza na Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Mh. Goodluck Ole-Medeye wakati wa tafrija hiyo iliyofanyika jana nyumbani kwake Ngarashi Monduli. 

Wageni waalikwa mbalimbali

PATA GAZETI LAKO LA PATA HABARI KWA TSH 500 TU

0
0


MTEMVU AZIDI KUWAAIA KAZI WATANZANIA UGHAIBUNI

0
0
 Mwenyekiti wa Wakala wa Kituo cha Kazi cha Bravo, ambaye pia ni Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu (wa pili kulia) akimkabidhi Mkazi wa Chamazi, Dar es Salaam, Warda Ibrahim tieketi na nyaraka zingine kwa ajili ya safari ya kwenda Dubai, Falme za Kiarabu kufanyaka zai aliyotafutiwa na kituo hicho. Anayeshuhudia makabidhino hayo yaliyofanyika Dar es Salaam hivi karibuni ni Mkurugenzi Mtendaji wa Bravo, Mohamed Omar na Ofisa Uhusiano wa kituo hicho,
 Mwenyekiti wa Wakala wa Kituo cha Kazi cha Bravo, ambaye pia ni Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu (kulia) akimkabidhi Mkazi wa Temeke, Dar es Salaam, Ummy Mushi tiketi na nyaraka zingine kwa ajili ya safari ya kwenda Dubai, Falme za Kiarabu kufanyaka zai aliyotafutiwa na kituo hicho. Anayeshuhudia makabidhino hayo yaliyofanyika Dar es Salaam hivi karibuni ni Mkurugenzi Mtendaji wa Bravo, Mohamed. Omar. Hadi sasa kituo hicho kimewapatia kazi Watanzania 16 Ughaibuni.
Mtemvu akiwa katika picha ya pamoja na akina mama hao wanaokwenda kufanya kazi Dubai pamoja na wadhamini wao. (PICHA NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG

KIVUMBE KUANZA MASHINDANO YA MBUNGE MGIMWA CUP 2014 JIMBO LA MUFINDI KASKAZIN

0
0
 Mbunge  wa  jimbo la Mufindi kaskazin Bw Mahmoud Mgimwa akikabidhi  vifaa vya  michezo kwa  timu  shiriki .



 Mbunge  wa  jimbo la Mufindi kaskazin Bw Mahmoud Mgimwa akionyesha  uwezo  wake  katika soka kabla ya  kuzindua mashindano hayo 


 Na Francis Godwin Blog 

JUMLA  ya   timu  5  za  jimbo la  Mufindi Kaskazin  zajitosa  kuwania  kombe la  Mbunge Mahmoud Mgimwa ( Mgimwa  Cup) katika  tarafa  ya Sadani .
 Timu   hizo  ni  kutoka  kijiji  cha  Ikweha,Ugenza,Ilangamoto, Sinai na Ukeremi ambazo   zote  zimepata  kutambaana  kuondoka na  ubingwa  katika  mashindano  hayo.
 Akifungua  pazia  la mashindano  haya  wakati  wa  hafla ya  kuukaribisha  mwaka mpya  2014  jana  katika  uwanja  wa kijiji cha Ugenza kata ya  Ikweha, Mgimwa  alisema  kuwa  lengo la mashindano hayo ni kuhamasisha  kasi  ya maendeleo kwa  vijana  kupitia  michezo .
Alisema  kuwa mashindano hayo yameanzishwa na kusimamiwa na shirika la Mgimwa foundation pamoja na umoja wawanafunzi walio maliza vyuo vikuu wilayani katika  wilaya ya Mufindi  (MUYOWIRUDE)
Mgimwa alisema nidhamira yake na viongozi anaoshirikiana nao kuhakikisha vijana katika jimbo lake wananufaika kwa kupitia michezo kasi  ya  maendeleo kwa  jimbo hilo kupitia  vijana  inazidi  kukua  zaidi
Mbunge   huyo  alisema zawadi mshindi wa kwanza atapata jumla ya Track suti 16 zenye thamani ya shiringi 480,000/=pamoja na mipira miwili yenye thamani ya shilingi 150,000 na  kufanya  zawadi  zote  kuwa na  jumla  ya Tshs. 630,000
 Huku mshindi  wa  pili atazawadiwa seti ya Jezi yenye thamani ya shilingi 250,000/=pamoja na mipira miwili ya Shilingi 150,000 na  kufanya zawadi zote kufikisha  kiasi cha  Shilingi 400,000 wakati mshindi wa tatu atapata mipira miwili yenye thamani ya shilingi 150,000
 Kabla ya  mashindano  hayo mbunge  huyo alikabidhi  seti ya Jezi  kwa  kila timu pamo na mpira mmoja wa mazoezi. Pia alikabidhi mipira miwili kwa waamuzi wa mashindanohayo kwa ajili ya kushindania sambamba na hilo pia Mgimwa alisema atatoa zawadi mbali mbali kama .
  Kwa mfungaji wa goli la kwanza katika mashindano hayo atapata shilingi 20,000 mchezaji mwenye nidhamu atapata shilingi 30,000 na  timu yenye nidhamu itapata shilingi 50,000 huku mchezaji bora atapata shilingi 50,000
Hivyo  aliwataka  vijana kwa kupitia mashindano hayo kuhakikisha wana  wasikiliza vema  watakapo kuwa wakipatiwa mafunzo ya stadi za maisha kwakupitia wawezeshaji toka shirika la (MUYOWIRUDE).
Ambao wataenda sambamba na michezo hiyo kwani watapa kujifunza bure elimu  mbali  mbali .Kiongozi wa  wanafunzi hao Marko Shayo alisema wao watatoa elimu yanamna yakujikinga na maambukizi ya Ukimwi,Elimu ya Ujasiriamali kwa kutumia zilizopo  katika jimbo  lao
Viewing all 46194 articles
Browse latest View live




Latest Images