Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46201 articles
Browse latest View live

SOLLY MAHLANGU AWAKUNA MASHABIKI WA INJILI UWANJA WA TAIFA.

0
0

MBONI AJUMUIKA NA WATOTO YATIMA MKOANI IRINGA

0
0
 
 Mtangazaji wa kipindi cha mboni show Mboni Masimba akimkabidhi zawadi mtoto yatima Ally Mustapha baada ya kuimba vizuri katika mlo uliandaliwa na Mboni katika ukumbi wa Highland hall
 baadhi ya watoto yatima wakiwa katika ukumbi wa highland hall  na mc wa shughuli hiyo Mc Zipompampa akiwa na mtoto Ally Mustapha. (Picha Zote na Denis Mlowe).

 Wageni rasmi katika hafla maalum ya mlo wa pamoja uliondaliwa na kipindi cha Mboni Show, Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Iringa ACP Ramadhani Mungi (kulia), Mboni Masimba katikati akiwa na mkurugenzi wa makampuni ya Asas, Salim Asas Abri, mgeni kutoka Nigeria.

=======  ======  =======
MBONI AJUMUIKA NA WATOTO YATIMA MKOANI IRINGA


Na Denis Mlowe,Iringa.


MTANGAZAJI wa kipindi cha ‘Mboni Show’ kinachorushwa na luninga ya EATV,Mboni Masimba leo amejumuika pamoja katika hafla na watoto yatima zaidi ya 200 walioko katika mkoa wa Iringa.


Katika hafla hiyo umejumuisha vituo vitatu vya watoto yatima vilivyoko mkoani Iringa vya Upendo center na Tosamaganga na kingine kilichoko katika wilaya ya Mufindi cha Moyo kwa Moyo.


Hafla  hiyo  ya  kula  chakula cha mchana na yatima  imefanyika katika ukumbi wa Highland hall na kuhudhuriwa na baadhi ya wafanyabiashara maarufu mkoani hapa akiwemo mkurugenzi wa makampuni ya Asas, Salim Abri Asas na mgeni rasmi alikuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa ACP Ramadhani Mungi..


Mbali ya kuwalisha watoto hao mboni ametumia muda huwa kuendesha  kipindi chake cha Mboni Show  kwaa kujumuika na watoto hao.

.

MOHAMED MATUMLA AMGALAGAZA NASSIBU RAMADHANI KWA POINT NA KUIBUKA NA PIKIPIKI

0
0

Bondia Mohamed Matumla kushoto akimwadhibu Nassibu Ramadhani wakati wa mpambano wao wa raundi kumi uliofanyika siku ya sikukuu ya krismas na kugombania pikipiki yenye thamani ya shilingi milioni 1.9 Matumla alishinda kwa pointi mpambano huo na kuibuka na bodaboda.
Bondia Mohamed Matumla kushoto akipambana na Nassibu Ramadhani wakati wa mpambano wao  uliofanyika siku ya sikukuu ya krismas na kugombania pikipiki yenye thamani ya shilingi milioni 1.9 Matumla alishinda kwa pointi mpambano huo na kuibuka na bodaboda picha nawww.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Lulu Kayage kushoto akipambana na Mariam Abdallah wakati wa mpambano wao wa kusherehekea sikukuu ya krismas kayage alishinda kwa k,o picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

lulu akinyooshwa mkono juu baada ya kushinda

l
Bondia Lulu Kayage kushoto akipambana na Mariam Abdallah wakati wa mpambano wao wa kusherehekea sikukuu ya krismas kayage alishinda kwa k,o picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Hamis Ajari kushoto akipambana na Cosmas Cheka wakati wa mpambano wao uriofanyika wakati wa sikukuu ya krismas cheka alishinda kwa point picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Sadiq Abdulazizi kushoto akipambana na Juma Fundi wakati wa mpambano wao uliofanyika wakati wa sikukuu ya krismas juma fundi alishinda kwa point mpambano uho picha nawww.superdboxingcoach.blogspot.com
Baadhi ya mashabiki waliouhulia mpambano huo uliokuwa mkali na kutoa burudani ya aina yake kwa mashabiki nchini

WENGI WAJITOKEZA KUUAGA MWILI WA ALIYEKUWA KOCHA WA MAKIPA SIMBA MAREHEMU JAMES KISAKA

0
0
 Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Kocha wa makipa wa Simba, marehemu James Kisaka likiingizwa kwenye basi la klabu hiyo, baada ya kutolewa heshima za mwisho katika misa iliyofanyika katika Kanisa la Muhimbili, Dar es Salaam. Marehemu Kisaka atasafirishwa kwenda kwao wilayani Muheza, Tanga kwa mazishi yatakayofanyika kesho. PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG

 Benny Kisaka ambaye ni mdogo wa marehemu James Kisaka akisoma wasifu wa marehemu kakake.


Aliyekuwa Kocha Msaidizi wa Simba, Jamhuri Kihwelo 'Julio', (kushoto) akijadiliana jambo na baadhi ya wachezaji wa soka waliokwenda kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu James Kisaka.

 Mjane wa marehemu James Kisaka, Teddy Kisaka akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa mumewe
Mjane wa marehemu James Kisaka, Teddy Kisaka akifarijiana na mtoto wa pili wa marehemu Kisaka, Boniface baada ya kutoa heshima za mwisho.
 Ndugu wa karibu wa marehemu Kisaka akilia alipokuwa akitoa heshima za mwisho
 Mtoto wa mwisho wa marehemu Kisaka, Christopher akitoa heshima za mwisho
 Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Jambo Concepts Tanzania Limited, Juma Pinto (kushoto), akisalimiana na Mwenyekiti wa zamani wa Klabu ya Simba, Hassan Dalali.
 Wachezaji soka wa zamani wakijadiliana jambo nje ya Kanisa la Muhimbili walipokwenda kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu James Kisaka. Kutoka kushoto ni Madaraka Selemani, Peter Tino, Khamis Kinye, Bakari Malima na Thomas Kipese.
 Aliyekuwa Kocha Msaidizi wa Simba, Jamhuri Kihwelo 'Julio', (kushoto) akijadiliana jambo na baadhi ya wachezaji wa soka waliokwenda kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu James Kisaka.
 Msanii wa filamu Jacob Steven JB akitoa heshima za mwisho
 Mchezaji wa zamani wa Simba Malota Soma akitoa heshima za mwisho kwa mchezaji mwenzie marehemu Kisaka.
 Mwandishi wa habari za michezo wa gazeti la Jambo Leo, Asha Kigundula akitoa heshima za mwisho
Benny Kisaka ambaye ni mdogo wa marehemu, akitoa taarisha ya usafiri wa kwenda kwenye msiba baada ya kutoa heshima za mwisho.

MUENDELESHO WA TAMASHA LA KRISIMASI LAFANYIKA MKOANI MOROGORO LEO

0
0
 Mmoja ya Waimbaji machachari katika anga ya muziki kiroho a.k.a Injili,Bone Mwaitege akionesha umahiri wake wa kucheza,na madansa wake kwenye uwanja wa Jamuhuri,mkoani Morogoro mapema leo ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa tamasha la Krismasi,ambapo hapo jana limezinduliwa rasmi jijini Dar katika uwanja wa Taifa na kuhudhuriwa na watu kibao.
 Mwimbaji wa nyimbo za kusifu na kuabudu,Upendo Kilahiro akiwaimbisha sehemu ya wakazi wa mji wa Morogoro waliojitokeza kwenye muendelezo wa tamasha la krisimasi lililofanyika jioni ya leo ndani ya uwanja
wa jamuhuri mkoani Morogoro.

 Madansa wa mwimbaji nyota wa muziki wa Injili hapa nchini,Rose Muhando wakiwajibika vilivyo.

 Malikia wa nyimbo za Injili,Rose Muhando akiimba kwa hisia wimbo wake mpya uitwao FACEBOOK,ndani ya uwanja wa jamuhuri,mkoani Morogoro mapema leo jioni.
 Sehemu ya mashabiki wakishangilia.
 Mwimbaji wa injili kutoka nchini Zambia,Eprahim Sekereti akiimba sambamba na kundi la Victoria singers,ndani ya uwanja wa Jamuhuri mkoani Morogoro jioni ya leo ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa tamasha la Krisimasi.
 Mwimbaji wa nyimbo za injili,Upendo Nkone akiwaimbisha mashabiki wake (hawapo pichani) waliofika kulishuhudia tamasha hilo la mwendelezo wa krisimasi mpaka mwaka mpya.
 Mmoja wa waimbaji wa nyimbo za kiroho kutoka mkoani Morogoro,Tumaini Njole akiimba huku akiwa katika staili ya kipekee kabisa,huku mayowe na shangwe zikisikika kutoka kwa mashabiki
 Sehemu ya mashabiki
 Vijana wa kundi la The Voice wakiwaimbisha mashabiki na watazamaji waliofika kwenye tamasha hilo ndani ya uwanja Jamuhuri mkoani Morogoro.

MAKAMBA AKUTANA NA MAASKOFU NA WACHUNGAJI MWANZA:AZITAJA SIFA ZA KIONGOZI WA TAIFA.

0
0
Naibu Waziri wa wizara ya Sayansi na Teknolojia Januari Makamba akizungumza na baadhi ya Maaskofu na Wachungaji wa mkoa wa Mwanza katika hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Kampuni ya The Great Zone Entertainment, inayojishughulisha na matamasha ya muziki wa Injili na sanaa.
Bishop Alex Lwakisumbwa ambaye ni mwenyekiti wa P.C.T mkoa wa Mwanza akizungumza  katika hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Kampuni ya The Great Zone Entertainment, inayojishughulisha na matamasha ya muziki wa Injili na sanaa, ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri wa wizara ya Sayansi na Teknolojia Januari Makamba.  
Mwenyekiti wa Umoja wa Makanisa jiji la Mwanza Bishop Charles Sekelwa akizungumza  katika hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Kampuni ya The Great Zone Entertainment, inayojishughulisha na matamasha ya muziki wa Injili na sanaa, ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri wa wizara ya Sayansi na Teknolojia Januari Makamba. 
Sehemu ya baadhi ya baadhi ya watumishi wa Mungu waliohudhuria hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Kampuni ya The Great Zone Entertainment, inayojishughulisha na matamasha ya muziki wa Injili na sanaa, ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri wa wizara ya Sayansi na Teknolojia Januari Makamba. 
Hafla ikiendelea katika ukumbi wa Victoria Palace Hotel jijini Mwanza.

Mkurugenzi wa The Great Zone Entertainment Fabian Fanuel (kulia) akitoa utambulisho wa baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo katika hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na kampuni yake, inayojishughulisha na matamasha ya muziki wa Injili na sanaa, ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri wa wizara ya Sayansi na Teknolojia Januari Makamba.
Meneja wa The Great Zone Entertainment Albert G. Sengo (kushoto) akitoa matarajio ya Kampuni.
Katika hafla hiyo Naibu Waziri wa wizara ya Sayansi na Teknolojia Januari Makamba akiwa mbele ya Maaskofu na wachungaji wa makanisa mbalimbali ya jijini Mwanza wakiwemo wafanyabiashara, aliridhia ombi la kuwa mlezi wa Kampuni ya The Great Zone Entertainment.
Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa makanisa ya Kikristo mkoa wa Mwanza Askofu Zenobius Isaya (Pentecoste) akizungumza  namna umoja wake ulivyolipokea wazo la ukuzaji wa majukwaa ya waimbaji wa muziki wa injili na sanaa ya jiji la Mwanza toka kwa Kampuni ya The Great Zone Entertainment
Baadhi ya Maaskofu.
Bahati Bukuku naye alikuwa sehemu ya waalikwa kwenye hafla hiyo.
Sala ya kuhitimisha hafla.
Naibu Waziri wa wizara ya Sayansi na Teknolojia Januari Makamba katika picha ya pamoja na wadau ambao huvutiwa na utendaji wake kutoka kushoto ni Ahmed Ibrahim kutoka Musoma, Bi Helen Kaji ambaye ni Meneja Kampuni ya Kinengena Agro and Minerals Logistics ya jijini Dar es salaam na Pilly Mgori wa Clouds Fm Mwanza.
Naibu Waziri wa wizara ya Sayansi na Teknolojia Januari Makamba akizungumza na wanahabari mara baada ya kumalizika hafla hiyo.
MWANZA:Naibu Waziri wa wizara ya Sayansi na Teknolojia Januari Makamba amesema taifa lipo katika kipindi Kigumu hivyo kuwataka maaskofu na wachungaji wa makanisa mbalimbali nchini kuiombea nchi yetu ili ipate kiongozi mwenye sifa zinazotajwa katika Biblia.
Akizungumza kwenye Hotel ya Victoria Palace katika Hafla ya chakula cha usiku kwa maaskofu na wachungaji wa makanisa mbalimbali ya iliyoandaliwa na Kampuni ya The Great Zone Entertainment, inayoshughulika na matamasha ya muziki wa Injili na sanaa, alisema ameamua kusema hayo mbele ya Maaskofu na Wachungaji ambao aliwaita watu wazito wenye kuaminiwa na kuheshimiwa katika jamii.
Hafla hiyo iliudhuriwa na Askofu Zenobius Isaya ambaye ni makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Makanisa ya Kikristo mkoa wa Mwanza,  Askofu Alex Mwakisumbwa mwenyekiti wa Makanisa ya Kipentokosti (P.C.T) pamoja na Askofu Charles Sekelwa ambaye ni mwenyekiti wa Umoja wa makanisa ya Kikristu mkoani Mwanza.
“Taifa linapita katika kipindi kigumu, linajaribiwa linapita kwenye wakati mgumu, ….Ndugu zangu yakusema yapo mengi, lakini nadhani tuzungumze machache yanayohusu nchi yetu na Taifa letu, kwa sababu wote ni watanzania hapa na wote tuna hamu ya kujua na kutafakari mustakabali wa nchi yetu, umoja wetu, amani yetu na utulivu wetu,” alieeleza.
Alisema nchi yetu inahitaji kuponywa, ili ianze upya (Reset) na kubainisha kuwa katika kuanza upya kama Taifa linahitaji aina ya viongozi wenye sifa za kama za viongozi wa dini ambazo zimebainishwa ndani ya Biblia na jukumu hilo kuhakikisha akiongozi wa sifa hizi anapatikana wqanalo wachugaji.
“Taifa lipo katika changamito kama rushwa, wizi, ubakaji, kumomonyoka kwa maadili  na ninyi viongozi wa dini mnaziona na kukabiliana nazo  kila siku, jamii yetu hii kwa sasa uongo umzidi, ubakaji umezidi, wizi umezidi mauaji yamezidi sasa nini kinaendelea na kutokea na kwa nini maovu yanaongezeka juu yetu?” alihoji Makamba.
Alisema katika hali kama hii kuna kipindi Mungu hukasirika na kutoa adhabu, hivyo kutaka Gharika pamoja na Sodoma na Gomola zilikuwa ni adhabu za Mungu kutokana na watu kupitiliza katika maovu hivyo adhabu ya kwanza ilikuwa ya Maji na ya pili ilikuwa Moto, hatujui inayofuata kwa nchi yetu itakuwa ya nini, japo kama Taifa hatutegemei kufuka huko.
Alieleza kwamba moja kati ya ujumbe wake kwa viongozi hao ni kama kizazi cha sasa ama taifa tunahitaji uponyaji wa hali ya juu na kwamba katika uponyaji huo viongozi wa dini wanayo nafasi kubwa sana ya kuiponya nchi hii ili iepuke adhabu kama za nyakati hizo zilizotolewa na Mungu.
“Shughuli za siasa zimeingiliwa na Matapeli, lakini hata shughuli yenu pia imeingilia na matapeli vilevile sasa tunapotafuta uponywaji wan chi yetu ninyi mnanafasi kubwa sana kwani uponyaji tunaoongea ni wa maovu ya kiroho, uongo ubakaji na vitu kama hivyo, ninyi mnanafasi kubwa sana. Viongozi wa siasa pia tunayo nafasi wote tunanafasi lakini ili tufanikiwe na nchi ipone lazima viongozi wa siasa wawe wasafi,” alieleza.
Alisema Askofu ama mchungaji akihubiri anapaswa kuwa msafi, na hata katika uongozi wa siasa anaposimama mtu na kusema yeye ni jawabu la matatizo ya wananchi ama yeye ni nyezo ya matatizo ni vizuri kumtazama sura yake kama ameacha (maovu).
Tunapoomba uongozi wa kisiasa zipo sifa kwani tunaomba kuongoza watu wa mungu ambao ni wale wale wanaokuja Makanisani ndiyo wanaokuja katika siasa, kuongoza watu wa mungu siyo kitu kidogo maana hata mamlaka ya serikali yametambuliwa hivyo lazima vigezo vya kuongoza watu hawa view vikubwa sana.
“Katika Biblia zinataja sifa za mtu atendae kazi ya Askofu ngoja nizisome (1 Timotheo 3.1)  zinasema … mtu akitamani kazi ya Askofu, atamani kazi nzuri. Basi, imempasa askofu awe mtu asiye na lawama, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi, anayejitawala, anayeheshimika, mkarimu, ajuaye kufundisha. Asiwe mlevi, wala mkali bali awe mpole, asiwe mgomvi wala mpenda fedha,” alisema na kuongeza katika siasa hatutafuti askofu lakini ni lazima sifa zifanane na hizi za askofu na kuwataka viongozi hao wa makanisa kuzisoma sifa hizo kila watu wanapopita kwao kutafuta uongozi wa nchi na kila mtu anayetafuta uongozi lazima ajipime kwa sifa hizi.
Alisema hata hivyo kumekuwa na mjadala mkubwa wa sifa za uongozi kuhusu kijana, uzoefu na kubainisha kwamba amekuwa akitoa mwito kwa vijana ambao hawana makandokando washiriki na kujitokeza katika kusaidia nchi ipone.
Makamba aleleza vijana wengi wamekuwa waoga waoga, wengi wamekuwa wakidai kutokuwa na fedha, uzoefu lakini maaskofu na wachungaji wanapaswa kuwa mashahidi kupitia vitabu kwani katika Yeremia imeelezwa jinsi Mungu alivyompatia unabii Yeremia ambaye alidai yeye bado mdogo na siwezi.
“Yeremia alipopewa unabii alilalamika mimimi mdogo mimi siwezi, lakini mungu alimwambiaje, ngoja nisome, (Yeremia 1: 4-10) ….Kabla sijakuumba ndani ya tumbo la mama yako nilikujua, kabla hujazaliwa nilikutenga kwa kazi maalumu, nilikuweka uwe nabii kwa mataifa,” alifafanua na kuongeza kuwa bwana alimwambia “Usiseme, ‘mimi ni mtoto mdogo. Utakwenda popote nitakapokutuma na kunena lo lote nitakalokuagiza, usiwaogope, kwa maana niko pamoja nawe nikuokoe.”
Kutokana na kauli hiyo ya Januari Makamba Askofu Jacoub Lutabija alisema amepokea ujumbe mzito ambao atakwenda kuutangaza kwa waumini wake Musima na kubainisha kwamba kwa ujumbe huo watu wenye hekina zao wametambua nini wanapaswa kufanya.
“Haya ni maneno mazito, mimi nimefurahi sana na nimueleze mgeni wetu nitakwenda Musoma kuwaeleza watu wangu juu ya ujumbe huu wenye maana sana kwa mustakabali wan chi yetu,” alisema.
Kwa upande wake Bahati Bukuku msanii wa Nyimbo za Injili, yeye aliwaasa wachungaji kuacha kuomba na kufunga mambo yanapokuwa mabaya kwani tatizo linaanzia pale maono yanapopuuzwa hivyo kuwataka kuangalia namna ya kuunga mkono kauli zenye maono kama hayo ambayo yanasaidia kuokoa nchi.

Tanzania Tai Shaolin Kung fu wakabidhi zawadi kwa Ndg. Magesa (MNEC)

0
0



Ndg. Phares Magesa(MNEC -Temeke ) kulia akipokea zawadi ya t-shirt toka kwa Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Tai Shaolin Kung Fu Ndg. Muarami ikiwa ni sehemu ya Shukrani zao baada ya kukubali ombi lao kuwa Mlezi wa Chama hicho, Magesa pia ni mchezaji wa Martial Arts.

WAKABIDHIWA VYETI VYA UKOCHA WA AWALI

0
0
 
Baadhi ya wahitimu wa mafunzo ya awali ya ukocha waliokabidhiwa vyeti vya kozi hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na vyeti vyao. (picha zote na Denis Mlowe).
 Baadhi ya wahitimu wa mafunzo ya awali ya ukocha waliokabidhiwa vyeti vya kozi hiyo kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa shule ya kimataifa ya Southern Highland Kitova Mungai.

 Mwenyekiti wa Chama cha Soka Wilaya ya Mufindi Gervas Choga akimkabidhi cheti ya kozi ya awali ya ukocha Lupyana Massawe, kulia ni mkurugenzi wa Hazina Foundation William Mungai makabidhiano yaliyofanyika katika ukumbi wa John's Corner mjini Mafinga. 

==========  =========  ===========

WAKABIDHIWA VYETI VYA UKOCHA WA AWALI


Na Denis Mlowe, Mufindi


ASASI isiyo ya Kiserikali ya Hazina Foundation iliyoko Mafinga imekabidhi vyeti 26 kwa wahitimu wa kozi ya awali ya ukocha kwa walimu wa Shule za Msingi na Sekondari wa Wilaya ya Mufindi.


Akikabidhi vyeti hivyo Mwenyekiti wa Chama cha Soka Wilaya ya Mufindi Gervas Choga aliwataka wahitimu hao kwenda kuvumbua vipaji vilivyojificha mashuleni na kuwaendeleza soka katika wilaya ya Mufindi.


Alisema mafunzo waliyopata ni muhimu sana kwa maendeleo ya soka la wilaya ya hiyo na taifa kwa ujumla na serikali inatakiwa kuwekeza  katika michezo na kuondokana na siasa iliyotawala sasa kwa watu wengi kujiingiza katika mpira kwa lengo la kupata umaarufu na mwisho kujiunga katika siasa.


Choga alisema vipaji vya soka vinaanzia shule za msingi hivyo ni jukumu la kila mmoja wenu kuweza kuandaa michezo ya kila mara katika shule mnazofundisha na maeneo yanayowazunguka.


“Nitahakikisha kila mmoja wenu anayafanyia kazi mafunzo haya na hakuna hata mmoja nisiyemjua hivyi katibu nakuagiza wafatilie wahitimu hawa na kuona wanafanya jambi kuhusu soka la wilaya yetu linakuwa, naomba vijana mtusaidie katika kuendeleza soka kwa kupitia mafunzo mliyopata” alisema Choga


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Hazina Foundation,William Mungai aliwataka wahitimu kuyatendea haki mafunzo hayo kwa kuwafundisha watoto mpira wa kisasa kuweza kufikia malengo ya kukuza soka la Mufindi na Taifa kwa ujumla.


Wiliam Mungai alisema mafunzo ya ukocha yatakuwa endelevu kwa walimu na wadau mbalimbali watakohitaji kujifunza ukocha ngazi ya awali na asasi ya Hazina itagharamia mafunzo hayo kwa vijana wa wilaya hiyo.


Alisema mafunzo hayo yanatakiwa kuanzia ngazi ya chini na bila kubagua jinsia kwa  kufundisha vijana wenye uwezo n kuthamini mpira wa miguu kunakuwa na faida kubwa na manufaa kwa vizazi vijavyo


Wiliam Mungai iliitaka serikali kuwekeza katika vyuo vyingi vya ufundishaji michezo kwa faida ya miaka ijayo katika kukuza michezo na kuongeza pato  la Taifa.


“Naomba sana  vijana wangu mwende mkafundishe soka la kisasa kwa vijana wetu nategemea sana kila mwaka kuongezeka kwa vipaji katika wilaya yetu na msiishie hapa na kozi hii ya awali mjiendeleze katika fani  yenu na kama mnavyojua soka la Tanzania kwa sasa lipo nyuma sana so tuanzie huku chini kwa kuibua vipaji vya kutosha” alisema Willam Mungai.


Mafunzo hayo yalioendeshwa na Kocha Bonifas Mkwasa mwezi Juni 25 hadi Julai 6  mwaka huu kwa udhamini mkubwa wa asasi ya hazina Foundation inayomilikiwa na Wiliam Mungai na makao makuu yako mjini Mafinga.




JACKIE CLIFF ATUHUMIWA KUKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA HUKO MACAO CHINA.

0
0

Jackie akiwa kwenye picha na rafiki yake Cheif Rocka aliye thibithisha habari za kukamtwa kwake huko China. 
Amesema huyu ni Jackie na hakuna ubishi ubalozi pia umethibithisha habari hizo. Sikiliza kwa makini Sauti hiyo hapo chini. HABARI ZAIDI BOFYA www.chinadaily.com. Sauti kwa hisani ya Bongo5.com

KALAMA NYILAWILA KUMVAA IBRAHIMU MAOKOLA DESEMBA 31 MSASANI KLABU

0
0

Msimamizi wa Mchezo wa ngumi katika kambi iliyopo sinza
makaburini, Bernald Lumbila (kushoto) akimwelekeza bondia Kalama Nyilawila jinsi ya kupiga ngumi katika mbavu Dar es saam. Nyilawila anajiandaa na mpambano wake dhidi ya Ibrahimu Maokola utakaofanyika Desemba 31 katika ukumbi wa Msasani Klabu Picha nawww.superdboxing coach.blogspot.com
Kalama Nyilawila akijifua

Na Mwandishi Wetu
BONDIA Kalama Nyilawila yupo katika mazoezi makali ya mwisho mwisho kabla ajamkabili mpinzani wake Ibrahimu Maokola siku ya Desemba 31  mpambano wa kufunga mwaka utakaoshirikisha mabondia mbalimbali akizungumza na mwandishi wa habari hizi Kalama ameseme yeye yupo fiti wakati wowote kwa ajili ya mpambano huo kwa ana usongo wa kuonesha ngumi zinachezwaje kwa mabondia chipkizi nchini

Mpambano huo utaanza kabla ya bondia Fransic Miyeyusho kupanda jukwaani kuvaana na David Chalanga kutoka Kenya mpambano wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi

na mapambano mengine ni Ibrahimu Class 'King Class Mawe' atavaana na Mohamed Kashinde uku Cosmas Cheka akioneshana ubabe na Iddy Mnyeke mpambano mwingine ni Antoni Mathias atakae menyana na Fadhili Majiha mapambano yote ya utangulizi ni ya raundi sita sita 

siku hiyo itasindikizwa na burudani za kila aina akiwemo mwana hi pop mashuhulu Kala Pina, Kimbunga Noma na wengine wengi ambao wata uanga mwaka na kukaribisha mwaka mpya kwa njia ya burudani


Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile

DAKTARI WA KUTIBU UMASKINI HUYU HAPA!

0
0

ZANZIBAR PAYS TRIBUTE TO MANDELA

0
0


Stone Town, Zanzibar– The Jahazi Literary & Jazz Festival in collaboration with Destination Zanzibar under Grassroots Traveller will host a memorial tribute to Nelson Mandela, former president of the Republic of South Africa who sadly passed away early December.


The evening of 28thDecember 2013, themed “Power of Education” is dedicated to celebrate the life of the legendary Nelson Mandela; a man who had inspired and touched countless number of people especially the youth, through his positive character and personal experiences.


His devotion and aspiration to nurture the youth of South Africa has sparked throughout Africa and beyond. He was a man who believed in change, not just change but positive transformation.


The Jahazi Literary & Jazz Festival believes in inspiring learning through literature and music by creating a platform in Zanzibar and East Africa in general for creative arts”, said Mr Ibrahim Dabo, a co-founder of the Jahazi Festival. Dabo also added that the aim is to bring talents and communities together in a friendly environment whereby ideas can be shared, authors and artists from all walks of life can learn from one another and produce eccentric collaborative works. “One of our core objectives is to encourage and educate the youth in nurturing their natural talents whilst surrounded by a culture that values education and peace building “ said Dabo.


The Jahazi Literary & Jazz Festival is thrilled to have the former president of Zanzibar, Hon.Dr. Amani Karume as the guest speaker for this event. Hon Dr. Amani Karume will contribute to our event in honouring the foundation and the various lessons Mandela gifted us with explained Ibrahim Dabo. As a co-founder, I am deeply grateful to have an African Presidential Lecturer, Hon. Dr Amani Karume’s contribution to the event in terms of his personal success in peace making and reconciliation in Zanzibar during his presidency.


Hafsa Mbamba founder of Destination Zanzibar said:  “The collaboration between the Jahazi Literary & Jazz Festival and Destination Zanzibar is an actual validation of how innovative business synergies are possible in showcasing Zanzibar as more than just a beach destination”. 

As an event management company we care for first hand, authentic and untamed experiences of Zanzibar added Mbamba. The memorial tribute to Mandela is our way of showing the world how we appreciate what Mandela stood for in the power of education” explained Mbamba: “Education is the most powerful weapon which you can use to change the world”, as Mandela once said. 


Rais Kikwete arejea nchini

0
0
 Makamu wa Rais Dk.Mohamed Gharib Bilal akimlaki Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya Kuwasili nchini akitokea jijini New York Marekani ambapo alikwenda kwa ukaguzi wa kawaida wa afya yake.Akiwa nachini Marekani Rais Kikwete alialikwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Ban ki Moon nakufanya naye mazungumzo kuhusu ushiriki wa majeshi ya Tanzania katika ulinzi wa Amani katika nchi mbalimbali.(picha na Freddy Maro).
Makamu wa Rais Dk.Mohamed Gharib Bilal akizungumza na Rais Dkt.Jakaya Kikwete Mrisho mara baada ya kumlaki muda mfupi baada ya Kuwasili nchini akitokea jijini New York Marekani ambapo alikwenda kwa ukaguzi wa kawaida wa afya yake nchini Marekani. Rais Kikwete alialikwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Ban ki Moon na kufanya naye mazungumzo kuhusu ushiriki wa majeshi ya Tanzania katika ulinzi wa Amani katika nchi mbalimbali

HELP FOR UNDERSERVED COMMUNITIES INC YAFADHILI WANAFUNZI 11 MASOMO YA UFUNDI VETA NCHINI

0
0
Na Nathan Mpangala

Help for Underserved Communities Inc. (HUC), imefadhili wanafunzi 11 kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Mbeya na Morogoro kozi mbalimbali za ufundi zinazotolewa VETA, ambapo baadhi yao wameshaanza mafunzo na wengine wanatarajiwa kuanza Januari mwakani.

Akizungumzia ufadhili huo, Rais wa asasi hiyo, Bi. Zawadi Sakapalla – Ukondwa, alisema, “ufadhili umelenga vijana wenye nia ya kujiendeleza lakini wamekuwa wakishindwa kufanya hivyo kutokana na uyatima na wazazi au walezi kutokuwa na uwezo wa kuwasomesha”.

Majina, kozi na mikoa wanayotoka vijana hao ni;  Joseph Mboya, Saidi Makope,  Yasini Musa (ufundi magari, Dar es Salaam), Neema Bungara (umeme wa magari, Dar es salaam), Francis Mustafa (ufundi magari, Morogoro), Hassan Bakari, Fadhili Munda (udereva, Dar es Salaam), David Mwasyeba (udereva wa pikipiki, Mbeya), Jamila Mwenda (usekretari/kompyuta, Dar es Salaam), Monica Mhelela (saluni na utengenezaji nywele, Dar es Salaam) na Rose Mawawa (ufundi cherehani, Dar es Salaam).

HUC ni asasi isiyo ya kiserikali yenye makao yake Marekani, inayosaidia upatikanaji wa maji safi na salama ya kunywa, maktaba za kijamii na vifaa vya elimu kwa maeneo yenye upungufu wa huduma za kujamii. Habari zaidi: https://www.facebook.com/pages/Help-for-Underserved-Communities-HUC-USA/412893725452394
Baadhi ya vijana waliopata ufadhili wa kozi mbalimbali za ufundi toka Help for Underserved Communities Inc. (HUC), wakisubiri taratibu za ujazaji fomu za kujiunga katika Chuo cha Mafunzo ya Ufundi(VETA) jijini Dar es salaam, hivi karibuni.
Ujazaji fomu za kujiunga na masomo ya ufundi VETA ukiendelea. Vijana hawa ni miongoni mwa vijana 11 wanaofadhiliwa na Help for Underserved Communities Inc. (HUC).
Baadhi ya vijana walipata ufadhili wa masomo ya ufundi toka Help for Underserved Communities Inc. (HUC), wakijaza fomu za kozi mbalimbali walizoomba VETA, jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Kutoka kulia ni Monica Mhelela, Joseph Mboya na Hassan Bakari.
Jamila Mwenda na Joseph Mboya wa Dar es Salaam, wakionesha nyuso za furaha baada ya ndoto zao za kusomea usekretari kwa Jamila na ufundi magari kwa Joseph kutimia. Jamila na Joseph ni miongoni mwa vijana 11 wanaofadhiliwa na Help for Underserved Communities Inc. (HUC) 

SHOW MATATA SANA YA MAPACHA WATATU YAJA.

0
0


Rais Kikwete atembelea na kuwafariji wagonjwa Muhimbili

0
0
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali mtoto Andrew Simba(15) aliyelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili wakati Rais alipowatembelea na kuwafariji  baadhi ya wagonjwa katika wodi ya Mwaisela leo.(picha na Freddy Maro).

SHEHENA ZA VIPODOZI FEKI ZAKAMATWA MKOANI IRINGA

0
0
 Baadhi ya shehena za vipodozi  zilizokamatwa na jeshi la polisi mkoa wa Iringa baada ya kushushwa katika roli katika makao makuu makuu ya jeshi mkoa wa Iringa.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Iringa ACP Ramadhani Mungi akionyesha shehena ya vipodozi vilivyokamatwa na jeshi hilo mkoani  Iringa katika makao makuu ya jeshi hilo jana.(picha na Denis Mlowe)
=========   ========   =========
SHEHENA ZA VIPODOZI FEKI ZAKAMATWA MKOANI IRINGA


Na Denis Mlowe,Iringa


JESHI la polisi mkoa wa Iringa limefanikiwa kukamata shehena ya vipodozi vyenye thamani ya mamilioni ya shilingi iliyokuwa inasafirishwa kutoka nchini Zambia kwenda jijini Dar es Salaam vilivyopigwa marufuku kwa matumizi ya binadamu.


Shehena hizo zilikuwa zimebebwa na gari aina ya lori la mafuta lenye namba za usajili T 247 BHP na tela lenye namba usajili T 598 BMK mali ya World Oil Ltd ya jijini Dar es Salaam.


Waliokamatwa na shehena hiyo ya vipodozi ni  Dereva wa lori Mohamed Sadru(23) na Kassimu Kaifa anayesadikika ndio mwenye mali.


Kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Iringa ACP Ramadhani Mungi  amethibitisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao na kusema kuwa walipata taarifa za kiitelejensia kutoka Tunduma kuwa kuna lori linasafirisha shehena hiyo kutoka nchini Zambia.


Mungi alisema walijiweka tayari kulikamata gari hilo kwa kukaa barabara kuu kuanzia saa moja jioni hadi ilipofika saa kumi alfajiri ndipo gari lilipofika na kukamatwa.


Anaongeza kuwa maafisa wa polisi mkoa wa Iringa walijipanga vizuri kuweza kulikagua gari hilo na waligundua kuna shehena kubwa ya vipodozi vilivyopigwa marufuku na TFDA na kuwaweka chini ya ulinzi dereva na roli hilo.


“Cha kushangaza gari la mafuta kuweza kubeba  vipodozi hivi vilivyopigwa marufuku hivyo tukaamua kuwashirikisha wadau wengine ambao ni TRA, TFDA na Tanroad kuweza kubaini makosa ambayo watuhumiwa hao wamefanya katika usafirishaji wa shehena hiyo.” Alisema Mungi


Mungi alisema uchunguzi wa awali unaonyesha shehena hiyo ina thamani kubwa na ndio maana watuhumiwa walikuwa wanasafirisha kwa njia ya magendo na wanaendelea kuchunguza kubaini thamani halisi ya mzigo huo.


Kwa upande wake Mratibu wa Mamlaka wa Chakula na Dawa (TFDA) mkoa wa Iringa, Deodata Rukupwa alisema shehena iliyokamatwa asilimia 100 ina kemikali iliyopigwa marufuku ya Hydroqunone na mamlaka hiyo.


Alisema vipodozi hivyo vitateketezwa kwa pamoja na jeshi la polisi na gari hilo kutaifishwa na serikali kutokana na kubeba mzigo wa magendo.


Rukupwa aliwataka wananchi kuwa makini katika kutumia vipodozi vilivyopigwa marufuku na serikali na kutoa taarifa wanapobaini kuna vipodozi vilivyopigwa marufuku vinauzwa.



majumba ya Mpapa yahitajika kulindwa na kutunzwa-Karune

0
0

Rais mstaafu wa awamu ya sita wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Amani Abeid Karume amesema majumba ya Mpapa ya yaliokabidhiwa wananchi 24 kutoka shehia 6 ya jimbo la bambi yanahitaji kulindwa na kutuzwa ili yaweze kudumu zaidi uhai wake.
Hayo ameyasema leo huko bambi wakati alipokua akiyakabidhi njumba hizo kwa familia hizo katika sherehe za kuzifungua nyumba hizo kwa wakadhi waliopewa katika kuazimisha miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanbar. 

Amesma azma ya awali ya mapinduzi ya Zanzibar ni kumpatia makazi bora mwana nchi wa ya Zanzibar ndio Rais wa awamu ya kwaza Abeid Aman Karume ni kuwajengea wananchi wake makazi hayo,hivyo azma hiyo ipopalepale na serikali haitorudi nyuma. 

Alisema nyumba hizo ni sehemu Ya nyumba zilizo jengwa sehemu mbali mbli za Zanzibar ijapo kluwazilisita kutokana na matukio yalio tokea miaka iliopita. Amesema majumba hayo yamemaliza na kuazia leo nihuru wananchi kuyatumia kwa kuweka familia zao.

GAZETI LA MTANZANIA LALEJEA MTAANI KWA KISHINDO BAADA YA KUMALIZA KIFUNGO CHA SERIKALI.

0
0
 Mhariri Mtendaji wa gazeti la Tanzania Daima, Ansbert Ngurumo (kushoto), akisoma nakala ya kwanza ya gazeti la Mtanzania baada ya kumaliza adhabu ya kufungiwa miezi mitatu na Serikali. Kulia ni Mhariri Mtendaji wa New Habari, Absalom Kibanda. (Picha na John Dande)
Mhariri Mtendaji wa New Habari, Absalom Kibanda (kushoto) na  Mhariri Mtendaji wa gazeti la Tanzania Daima, Ansbert Ngurumo wakisoma nakala ya kwanza ya gazeti la Mtanzania baada ya kumaliza adhabu ya kufungiwa na Serikali. 
 Askari wa Usalama Barabarani akisoma nakala ya gazeti la Mtanzania.

USIKU WA ZAWADI DAR LIVE DEC 3I, 2013

0
0
Viewing all 46201 articles
Browse latest View live




Latest Images