Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

Grooveback Yasherehekea Miaka 5 Jumamosi Hii pale East 24- Arcade Mikocheni


TRANSEVENTS LTD KUZINDUA MABASI YENYE UWEZO WA KUTEMBEA NCHI KAVU NA MAJINI NCHINI TANZANIA

$
0
0
Kampuni ya Transevents Marketing Ltd kutoka Nchini Tanzania kwa kushirikiana na kampuni la Dutch Amfibious Transport(DAT) linalotengeneza mabasi ambayo kutoka Uholanzi  yanauwezo wa kutembea nchi kavu na majini na ambayo itakuwa ni Teknolojia ya kwanza kwa Afrika itakayo anzia Tanzania kuwa na aina hiyo ya mabasi.

Mabasi hayo ya aina yake ambayo yatakuwa na uwezo wa kubeba abiria wa kutosha yanatarajiwa kuzinduliwa mwakani nchini Tanzania , pamoja na hayo mabasi hayo yataweza kupunguza foleni kwa kiasi kikubwa na kurahisisha swala zima la usafiri ambapo mabasi hayo na baadhi ya magari mengine madogo yatakuwa na uwezo wa kupita majini na Nchi kavu.

Baadhi ya Mabasi hayo yatakuwa yanatokea Mombasa hadi Mtwara kupitia Baharini kisha nchi kavu.

Mchakato huo umekwisha anza kufanyiwa kazi pia kwa ushirikiano wa SUMATRA.Mchakato huu umekwisha anza kufanyiwa upembuzi yakinifu na kazi pia kwa ushirikiano na taasisi pamoja na Mamlaka mbalimbali za hapa nchini zikiwemo, SUMATRA, Jeshi la Polisi na kitengo cha Usalama barabarani.

Video hizi Mbili zinaelezea kwa kina na kuonesha jinsi Mabasi haya yatakavyokuwa yakifanya kazi hapa nchini Tanzania

Tazama Video la Basi hilo tangia Linatengenezwa hadi Linafanyiwa majaribio  

Tazama video ya Basi hilo Likiwa linafanya safari zake Nchi kavu na Baharini pamoja na abiria ndani. 

MKALI KUJULIKANA KRISIMASS.

$
0
0
Na Mwandishi Wetu.

Mabingwa wa muziki wa dansi nchini Msondo Ngoma na  Mlimani Park Orchestra “Sikinde” kesho  mchana zitachuana vikali katika viwanja vya TCC Club  Chang’ombe, Temeke.

Mpambano huo wa kusherekea sikukuu ya Krismasi litakuwa la kufunga mwaka 2013 na pia litaamua ni bendi gani bora kati ya magwiji hao wa muziki wa dansi nchini mwaka huu.

Mratibu wa mchuano huo Joseph Kapinga amesema pambano huo litanzaza saa nane alasiri hadi majogoo.

Kapinga alisema Sikinde wataingia TCC wakitokea Bagamoyo walipokuwa wakipiga kambi wakati kambi ya Msondo Ngoma imebaki kuwa siri kwa muda wote.

Mratibu huyo alisema kila bendi litapiga kwenye jukwaa lake ili kuondoa hujuma.Kapinga alisema kila bendi itatapewa muda wa saa moja kupiga jukwaani kabla ya kumpisha nyingine.

Kiongozi wa Msondo Ngoma Saidi Mabera  alisema jana kuwa watapiga nyimbo zao zote kali ili kuhakikisha wanaibuka kidedea.

Alitaja baadhi ya nyimbo ambazo watazipiga kuwa ni  'Nimuokoe Nani', 'Zarina', 'Mwanaidi', 'Kanjelenjele', 'Bahati', 'Sesilia', 'Usiue Usiibe', 'Asha Mwana Seif', 'Kauka Nikuvae', Chuma Chikoli Moto', 'Kilio cha Mzima', 'Ajali' na  'Suluhu'.

Baadhi ya wanamuziki wanaounda Msondo Ngoma ni Shaaban Dede, Mabera, Abdul Ridhiwani Pangamawe, Athumani Kambi, Saad Ally 'Mashine', Eddo Sanga, Huruka Uvuruge, Zahoro Bangwe, Ibrahim Kandaya,  James Mawilla,  Juma Katundu, Hamisi Mnyupe, Roman Mng’ande `Romario’  na Hassan Moshi.

Naye kiongozi wa Sikinde Hamisi Mirambo alijigamba kuwa wataibuka na ushindi mnono.“Tuna waimbaji wazuri na hakuna itakachotuzuia kushinda,” alisema Mirambo.

Alitaja baadhi ya nyimbo ambazo watazipiga kuwa ni 'Selina', Wiki endi', 'Penzi la Fukara', 'Hiba', 'MV Mapenzi’,  'Supu Umelitia Nazi' na 'Jinamizi la Talaka'.

Sikinde inaundwa na wanamuziki kama Hassan Rehani Bitchuka, Hassan Kunyata, Kaingilila Maufi, Tonny Karama, Shaaban Mabuyu, Habib Abassi, Juma Choka, Ally Jamwaka,  Mbaraka Othman, Hamisi Milambo, Shaaban Lendi, Joseph Benard, Ramadhani Mapesa na Habibu Jeff.

Pambano umeandaliwa na Bob Entertainment na Keen Arts chini ya udhamini wa Konyagi, Nipashe, CXC Africa na Saluti5.

MH. KIZIGHA AWASHUKURU WAPIGA KURA

$
0
0
Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam, ambaye pia ni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Angela Kizigha, akizungumza na viongozi wa Jumuia hiyo katika Kata za wilaya ya Temeke, leo Mbagala, kuwashukuru viongozi wa Jumuia ya Wazazi Kata zote za wilaya hiyo kwa kumchagua kuwa Mwenyekiti katika uchaguzi uliopita. . Kushoto ni Katibu wa Jumuia hiyo mkoa wa Dar es Salaam, Mohamed Cholage.
Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam, ambaye pia ni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Angela Kizigha, akimvalisha kitenge cha sare maalum ya Jumuia hiyo, Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kilakala, Henedi Fereji, alipogawa sare hizo kwa wajumbe 60 waliohudhuria kikao maalum kilichofanyika leo, Mbagala Kuu, kuwashukuru viongozi wa Jumuia ya Wazazi Kata zote za Temeke, kwa kumchagua kuwa Mwenyekiti wa mkoa huo katika uchaguzi uliopita. Kushoto ni Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Wilaya ya Temeke, Sophia Kinega na Watatu ni Katibu wa Jumuia hiyo mkoa wa Dar es Salaam, Mohamed Cholage. (Picha na Bashir Nkoromo).

Rais Kikwete atoa zawadi ya XMASS kwa A WATOTO YATIMA NA WAZEE WASIOJIWEZA

$
0
0
 Kaimu Kamishna wa Ustawi wa Jamii Beatrice Fungamo (katikati) akimkabidhi  Mwakilishi wa Makao ya Watoto Kurasini wilayani Temeke Bibi  Beatrice Mgumiro mbuzi watatu, kilo 150 za mchele na lita ishirini za mafuta ya kupikia  ikiwa ni zawadi ya Krismas zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete. Zawadi hizo ambazo ni mbuzi, mchele na mafuta zilitolewa jana na Rais Kikwete ili kuwakumbuka watoto walio katika makundi maalum ili nao washerehekee sikukuu kwa furaha.

 Kaimu Kamishna wa Ustawi wa Jamii Beatrice Fungamo (kushoto) akimkabidhi  Mkuu wa Kituo cha Mahabusu ya Watoto Ramadhani Yahaya (kulia)  mbuzi wawili (2), kilo 100 za mchele na lita ishirini za mafuta ya kupikia  ikiwa zawadi ya Krismas zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete. Zawadi hizo ambazo ni mbuzi, mchele na mafuta zilitolewa jana na Rais Kikwete ili kuwakumbuka watoto walio katika makundi maalum ili nao washerehekee sikukuu kwa furaha.
 Kaimu Kamishna wa Ustawi wa Jamii Beatrice Fungamo (kushoto) akimkabidhi  Msaidizi wa Mkuu wa Kituo cha Watoto Yatima Msimbazi  Sister Maria Silvana  (kulia)  mbuzi watatu, kilo 100 za mchele na lita ishirini za mafuta ya kupikia  ikiwa zawadi ya Krismas zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete. Zawadi hizo ambazo ni mbuzi, mchele na mafuta zilitolewa jana na Rais Kikwete ili kuwakumbuka watoto walio katika makundi maalum ili nao washerehekee sikukuu.
Kaimu Kamishna wa Ustawi wa Jamii Beatrice Fungamo (kushoto) akimkabidhi  Mkurugenzi WA  Kituo cha Vosa  Mission Hochimin Mugarura (kulia)  mbuzi wawili, kilo 100 za mchele na lita ishirini za mafuta ya kupikia ikiwa zawadi ya Krismas zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete. Zawadi hizo ambazo ni mbuzi, mchele na mafuta zilitolewa jana na Rais Kikwete ili kuwakumbuka watoto walio katika makundi maalum ili nao washerehekee sikukuu.  Picha na MAELEZO, Dar es salaam

OOOOOOOOOO  OOOOOO  OOOOOOO

Na Kiza Sungura-MAELEZO,Dar es salaam .

 Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Dkt Jakaya Mrisho kikwete ametoa jumla ya kilo za mchele 1,200 , lita 220 za mafuta na mbuzi 25 kwa ajili ya zawadi ya sikukuu ya Krismas kwa makundi maalum. Zawadi hizo zilikabidhiwa jana (leo) na Kaimu Kamishna wa Ustawi wa Jamii Bibi Beatrice Fungamo kwa niaba ya Rais Kikwete kwenye sherehe fupi iliyofanyika katika Uwanja wa Mahabusu ya Watoto jijini Dar es salaam. 

 Alisema kuwa Rais Kikwete ametoa zawadi ili kuwakumbuka watoto walio katika makundi maalum kama vile yatima, wazee wasiojiweza na watato walioko katika mkinzano na Sheria ili nao waweze kuungana na Watanzania wengine katika kusherekea sikukuu ya Krismas. Bibi Fungamo alisema kuwa nje ya kutoka zawadi kwa vituo mbalimbali vya Mkoa wa Dar es salaam pia ametoa katika makunndi mengine ya mikoa mingine hapa nchini. 

 Alisema kuwa kwa upande wa Dar es salaam ametao kwa vituo 11 vinavyosaidia kutoa huduma kwa watoto na wazee wasiojiweza ambazo ni Kituo cha Watoto Ibn Kathir, Tabata, Ilala, Makao ya Watoto Kurasini, Temeke, Makao ya Watoto Yatima Msimbazi, Kituo cha Kwetu Mbagala Girls Home, Kituo cha Yatima Group, na Kituo cha CHAKUWAMA. Vingine vya mkoani Dar es salaam ni Mahabusu ya Watoto, Makao ya Watoto Yatima Mburahati, Kituo cha Tuwapende Watoto Bunju, Makao ya Wazee wasiojiweza Msimbazi na Vosa Mission Kongowe. 

 Alisema kuwa kwa vituo vya mikoani na maeneo mengine nje ya Dar es salaam zawadi zao watapatiwa katika maeneo yao . Bibi Fatuma alivitaja vituo vya nje ya Dar es salaam vilipatiwa zawadi na Rais Kikwete ni Kituo cha Mabaoni Chakeckale Pemba, Kituo cha Werezo cha Unguja, Mahabusu ya Wototo Moshi mkoani Kilimanjaro na Makao ya Wazee wasiojiweza Sukamaela mkoani Singida. Vingine ni Makao ya wasiojiweza Bukumbi, Misungwi mkoani Mwanza na Makazi ya Wazee wasiojiweza Msufini , Muheza mkoani Tanga. 

 Alisema kuwa Rais Kikwete ametoa zawadi hizo kwa kutambua kuwa watoto na wazee hao wanapaswa kujumuika na wanajamii wengine katika kusherehekea sikukuu hiyo vema.   Hatua hii ya Rais Kikwete ni sehemu ya utamaduni wake aliojijengea wa kuwakumbuka watu wenye mahitaji mbalimbali .

Makamu wa Rais Dkt. Bilal, amjulia hali mzee Ali Machano Muasisi wa ASP

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mzee Ali Machano (122) mmoja kati ya Waasisi wa ASP wakati alipomtembelea kumjulia hali kijijini kwake Moga Mkoa wa Kaskazini Unguja leo Disemba 24-2013. (Picha na OMR).

DR. JOSE CHAMELEONE ATUA MWANZA KUPIGA BONGE LA SHOW USIKU WA LEO TAREHE 24 CCM KIRUMBA MWANZA.

$
0
0
Mwanamuziki mahiri toka nchini Uganda Dr. Jose Chameleone akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza kuhusiana na Tamasha lililopewa jina la 'Badilisha Concert' litakalofayika leo 24 dec 2013 katika uwanja wa CCM Kirumba kuanzia saa 12 jioni hadi majogoo kama sehemu ya kuikaribisha sikukuu ya Christmass. Pembeni yake anaonekana meneja wake na mwisho kabisa kulia ni mmoja wa wadhamini wa Tamasha hilo Mr. James Njuu wa K Vant Gin.
Mwanamuziki mahiri toka nchini Uganda Dr. Jose Chameleone akisalimiana na mmoja kati ya wasanii wa Jambo Squard mbele kidogo ni Dogo Dee na mwisho kabisa (kushoto) katika mstari ni mwanamuziki Bob Haisa ambao wamefika kumpa sapoti katika show ya Badilisha Concert itakayofanyika leo CCM Kirumba Mwanza. 
Mwanamuziki mahiri toka nchini Uganda Dr. Jose Chameleone akisalimiana na ndugu zake wasanii wa Tanzania waliofika leo kuzungumza na waandishi wa habari katika Hotel Gold Crest Mwanza.
Kwa mujibu wa mratibu wa tamasha hilo Denis (kushoto) kutoka Silver Intertainment amesema kuwa kampuni yake imeamua kuweka kiwango kidogo cha kiingilio ili watu wote wa Kanda ya Ziwa waipate zawadi ya mwaka kushuhudia burudani kali.
"Zawadi nyingi huwekwa kwenye boxi lakini hii yaani mimi ni zawadi iliyo nje ya boxi maalum kwa wakazi wa Mwanza" pia Jose Chameleone anasema kuwa najivunia kuwa Mwanza mji ambao kwangu ni sawa na nyumbani.
Jose Chameleone amekwepa kulizungumzia suala lake la hivi majuzi kukumbatiana na mdogo wake Weasal na binamu yake Radio ile hali walikuwa kwenye bifu kali akisema yote yatafanyika lakini undugu utabaki pale pale akisita kuendelea kulizungumzia suala hilo kwa undani akisema hawezi kuzungumzia masuala ya familia nje ya familia anaheshimu utamaduni wa kiafrika.



Jose Chameleone akiwa na wasanii wa Tanzania kutoka kushoto ni Bob Haisa, King Houston, Chemeleone (mwenyewe) Dogo Dee, Chuse, na Jambo Squard team.
Jose Chameleone akiwa na wadhamini waliosimamia mzigo ukasimama.
Take two na wadhamini.
Jose akiwa na wanahabari wa Mwanza.
Uskose usiku wa leo ndani ya uwanja wa CCM Kirumba.

HABARI SAWIA KWA JAMII

$
0
0
Wakulima 1000 katika wilaya ya Arumeru Arusha walazimika kubuni aina mbadala ya kilimo cha mazao ya mboga mboga na wafanya biashara wa wakubwa na wadogo nchini kunufaika na mfumo mpya wa kielektro.niki. karibu jina langu ni sophia kessy.

========  =======  =======


Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji EWURA waridhia ombi la Tanesco kuongeza bei ya umeme na wafanya biashara waitaka serikali kuongeza wigo wa ukaguzi wa bidhaa feki madukani. Mimi ni sophia kessy karibu

Mwimbaji nyota wa nyimbo za injili solly Mahlangu awasili jijini dar leo,kutumbuiza kesho tamasha la krisimasi uwanja wa taifa

$
0
0
 Mwanamzuki mwimbaji  wa Kimataifa wa nyimbo za Kiroho a.k.a Injili kutoka nchini Afrika Kusini,Solly Mahlangu pichani kati akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwal J.K.Nyere jijini Dar jioni ya leo.Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa tamasha la krisimasi,Bwa.Alex Msama na wadau wengine waliofika kumlaki mwanamuziki huyo mahiri anaetarajiwa kutumbuiza hapo kesho kwenye uwanja wa Taifa wakati wa tamasha la krisimasi.
 Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotions Ltd,inayoandaa tamasha la Krisimasi,Bwa.Alex Msama akizungumza na baadhi ya Wanahabari kuhusiana na ujio wa mwanamuziki wa Afrika Kusini,Solly Mahlangu aliyewasili jioni ya leo jijini Dar tayari kuungana na wanamuziki wengine wa nyimbo ya Injili kwa ajili ya kutumbuiza hapo kesho kwenye tamasha la Krisimasi,ambalo linasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wake.
Mwanamuziki wa nyimbo za Injili,Solly Mahlangu akiwapungia mikono mashabiki wake waliofika kumlaki mara baada ya kuwasili jioni ya leo kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwal J.K.Nyere jijini Dar jioni .Kulia kwake ni Mwenyekiti wa tamasha la krisimasi,Bwa.Alex Msama na wadau wengine waliofika kumlaki mwanamuziki huyo mahiri anaetarajiwa kutumbuiza hapo kesho kwenye uwanja wa Taifa wakati wa tamasha la krisimasi.

SALAAM ZA XMASS

Mdau anahoji TRA na UPS hawafanyi kazi Zanzibar?

$
0
0
 Habari Kaka Michuzi swali langu ni fupi tu

Hivi unapotuma kajimzigo chako kutoka ulaya kisichokuwa na thamani yoyote Main destination ni Zanzibar lakini unaambiwa uende ukagomboe mwenyewe JNU Airport ni maana yake nini?

Mara ya tatu natuma kwa njia ya UPS courier mzigo unafikia Dar es Salaam agent wa UPS anakwambia ukitaka mzigo ukomboe mwenyewe safiri uje Dar es Salaam ulipe Document hand-over fees Tsh.55,000/ uende mwenyewe Airport au 

Lipa Tsh.90,000/- ya agent wa UPS na hatujui Malipo ya TRA na vile vile hatujui muda gani inaweza kuchukua mwezi au miwili 

Mzigo wangu tokea tarehe 12 December umewasili Dar es Salaam hadi hii leo haujapatiwa ufumbuzi na kumbuka hii ni DOOR TO DOOR service SIO DOOR TO AIRPOT  Ndani ya mzigo kuna   Audio Mixer ambayo haina thamani yoyote clearance ya kazini tu nimeona niitume Tennis table bat 1 na mipira ya mazoezi (£10.00 nimenunua ebay)  

jumla mzigo hata thamani ya £100 haufiki lakini imeshakuwa big deal 
sasa je kama huu mzigo unaenda ZANZIBAR kwani ni usifanyiwe Clearance ZNZ wakati pia ipo TRA kule? hadi mtu aende Dar es Salaam hivi hii ni haki?

Na hizi fee za hawa UPS hii ni haki mbona unapo book mzigo huambiwi kama utahitaji kulipa fee ya agent au ya kupewa document?

Wenye data naomba ufafanuzi au opinion zaidi nimeshalalamika UPS UK na wao wanasema wanasubiri info kutoka TZ kila nikiwapigia hapa Ila hadi hii leo ni 12 days sasa hakuna info yoyote....

Rais Kikwete akutana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa

$
0
0
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Ban Ki Moon akimkaribisha Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwenye ofisi yake iliyopo Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani 24/12/2013.

Bwana Ban Ki Moon alimwalika Rais Kikwete ambapo viongozi hao wawili walijadili masuala mbalimbali ya kimataifa hususan masuala ya amani na ushiriki wa majeshi ya Tanzania katika kudumisha amani sehemu mbalimbali Afrika na katika nchi nyingine duniani. Tanzania ina majeshi ya kulinda amani katika nchi kadhaa ikiwemo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Darfur nchini Sudan na Lebanon.

Rais Kikwete yupo jijini New York nchini Marekani ambapo anaendelea vyema na ukaguzi wa kawaida wa afya yake.(picha na Freddy Maro)
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Ban Ki Moon akimkaribisha Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa ajili ya kufanya mazungumzo nae.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika Mazungumzo na Mwenyeji wake,Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Ban Ki Moon alipomtembelea ofisi kwake jijini New York, Marekani 24/12/2013
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Mwenyeji wake,Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Ban Ki Moon mara baada ya kumaliza mazungumzo yao jijini New York, Marekani 24/12/2013.

TAMASHA LA KRISIMASI KUFANYIKA LEO UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR

TAMASHA LA CHRITMAS MKOANI DODOMA KUFANYIKA LEO UWANJA WA JAMHURI

$
0
0
 Mratibu wa Tamasha hilo John Banda akizungumza na Waandishi wa habari juu ya kukamilika kwa maandalizi ya tamasha hilo, Kushoto ni Mmoja wa waimbaji kwenye tamasha hilo Beatrice Wiliam (BSS 2011) Maandalizi ya Tamasha la Chrismas ndani ya Dodoma Tayari yamekamilika wasanii Kibao toka ndani na nje ya Tanzania Tayali wapo Dodoma na Asubuhi ya leo wameshiriki ibada ya pamoja katika kanisa la Mlima wa moto Sabasaba Dodoma.
 Josephine Sudai akionyesha uwezo wake wa kuimba ndani ya kanisa la mlima wa moto Dodoma kabla ya saa 7 mchana kuelekea uwanja wa Jamhuri kwenye tamasha la Chrismas
 Jubilee Lugobo toka jiji Dar es salaam nae yupo Dodoma kwa ajili ya tamasha hilo
  Lusekelo Mwandiga akiimba kwa mbwembwe ndani ya kanisa la mlima wa moto sabasaba Dodoma kabla ya kushiriki tamasha hilo
Mwanadada Rose Kimaryo ndani ya tamasha hilo na hapa ni mlima wa moto sabasaba
 Mwimbaji Beatrice Wiliamu akihojiwa katika moja ya Radio station IMPACT FM kuhusiana na Tamasha hilo.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AIFARIJI FAMILIA YA MAREHEMU SHEIKH SULEIMAN AMOUR JENDELE ZANZIBAR

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akishiriki kwenye Dua ya pamoja na Familia ya marehemu Sheikh Suleiman Amour (82) kwenye Makaburi alipozikwa kijijini kwake Jendele Wilaya ya Kati Unguja kwa ajili ya kufariji familia hiyo leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiifariji familia ya marehemu Sheikh Suleiman Amour (82) aliyefariki Dunia hivi karibuni wakati alipofika nyumbani kwa marehemu katika kijiji cha Jendele Wilaya ya Kati Unguja leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akishiriki kwenye Dua ya pamoja na Familia ya marehemu Sheikh Suleiman Amour (82) wakati alipofika nyumbani kwa Marehemu katika kijiji cha Jendele Wilaya ya Kati Unguja kwa ajili ya kufariji familia hiyo leo.Picha na OMR 

Usaili wa Shindano la Vipaji kwa watoto la "MO Kids Got Talent 2013" wakamata watoto zaidi ya 100

$
0
0
DSC_1678 (2)
Chief Judge wa Shindano la "MO Kids Got Talent", Salma Mziray, akitoa maoni yake kwa baadhi ya washiriki wa usaili wa shindano hilo uliofanyika kwenye hotel ya Ledger Plaza Bahari Beach jijini Dar es Salaam. Kulia ni Jaji Neema Theobald na kushoto ni msanii wa filamu nchini Hidaya Njaidi wakiwa meza kuu.
DSC_1672
Pichani juu na chini ni baadhi ya washiriki wakionyesha vipaji vyao mbele ya majaji.
DSC_1705
Binti huyu kipaji chake ilikuwa ni kuimba taarab.
DSC_1785
Mambo ya Alingo nayo yalihusika.


DSC_1797
DSC_1745
DSC_1768
Hapo sasa twende kazi.....!!!
A04A7088
Majaji wa shindano la "MO Kids Got Talent" wakishuhudia kipaji cha mmoja wa watoto wanaojua kuogelea akijitosa kwenye bwawa la kuogelea lililopo Ledger Plaza Bahari Beach jijini Dar.
A04A7095
Chief Judge, Salma Mziray, akizungumza na mmoja wa washiriki kabla ya kuonyesha kipaji chake.
DSC_1773
Pichani juu na chini ni baadhi ya watoto walioshiriki usaili huo hawakuondoka mikono mitupu walipewa zawadi ya madaftari pamoja na sabuni ya Unga ya kufulia MO Detergent.
DSC_1692 (2)
DSC_1756
DSC_1788
DSC_1802
DSC_1726
A04A7120
Meneja Mkuu Ledger Plaza Bahari Beach, Wissem Souifi (kulia) pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Fros Africa, Bw. Peter Sekasiko (katikati) wakijumuika na wazazi pamoja na familia zao kwenye fukwe za hoteli ya Ledger Plaza, Bahari Beach jijini Dar leo.

TAMASHA LA KRISIMASI LAFANA UWANJA WA TAIFA,SOLLY MAHLANGU WA AFRIKA KUSINI AWAKUNA VILIVYO WATAZAMAJI

$
0
0
 Mgeni rasmi wa tamasha la Krisismasi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu na Bunge,Mh.William Lukuvi akizungumza mbele ya watazamaji waliofika kwenye tamasha hilo jioni ya leo,lililofanyika ndani ya uwanja wa Taifa jijini Dar.Lukuvi amewataka watazamaji na washabiki wa tamasha hilo  na Watanzania kwa ujumla kusherehekea sikukuu ya krismasi na mwaka mpya kwa amani,upendo na utulivu,ameongeza kuwa pia Serikali itahakikisha usalama upo na wa kutosha kwa watu wake,pichani kati ni Mbunge wa Msalala,Mh.Ezekiel Maige pamoja na Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotions Ltd,ambao ndio waandaji wa tamasha hilo Bwa.Alex Msama.
 Mmoja wa wageni waalikwa katika tamasha la Krisimasi,Mbunge wa Msalala,Mh.Ezekiel Maige pichani kati akiwatakia heri na fanaka Watazamaji na Watazania kwa ujumla katika kusherehekea sikukuu ya Krisimasi na mwaka mpya. 
 Mwimbaji wa nyimbo za injili kutoka nchini Zambia,Epraim Sekereti akiimba jukwaani kwenye tamasha la krismasi jioni ya leo ndani ya uwanja wa Taifa,ambapo mgeni rasmi alikuwa Mh.Lukuvi.
  Baadhi ya Waimbaji wa nyimbo za Injili kutoka kikundi cha Living Waters wakitumbuiza jioni ya leo kwenye tamasha la Krisimasi lililofanyika jioni ya leo ndani ya uwanja wa Taifa,jijini dar.
 Baadhi ya waimbaji waliombatana na mwanamuziki nyota kutoka nchini Afrika Kusini Solly Mahlangu,wakimpa back up mkali huyo wa injili. 
 Baadhi ya Wapiga vyombo wa mwanamuziki Solly Mahlangu wakiwajibika jukwaani.
 Baadhi ya mashabiki wa Mwanamuziki Solly Mahlangu kutoka nchini Afrika kusini wakifurahia
 Pichani juu na chini ni Mwanamuziki mahiri kutoka nchini Afrika Kusini,Solly Mahlangu akiwaimbisha mashabiki wake jioni ya leo kwenye tamasha la krisimasi,lililofanyika ndani ya uwanja wa Taifa jijini dar. 
Sehemu ya umati wa watu waliofika kwenye tamasha hilo jioni ya leo.
 Mwimbaji wa nyimbo za Kiroho a.k.a Injili Upendo Nkone akiimba kwa hisia jukwaani jioni ya leo mbele ya mashabiki kibao (hawapo pichani) wakati wa tamasha la krisimasi likiendelea jioni ya leo ndani ya uwanja wa Taifa,jijini Dar.
 Pichani shoto ni Mwimbaji nyota wa muziki wa injili,Rose Muhando akiwa sambamba na skwadi lake zima,wakishambulia kwa namna ya pekee kabisa,huku miluzi na shangwe za watazamaji zikivuma kila kona ya uwanja,jioni ya leo kwenye tamasha la krisimasi.
 Rose Muhando akiimba wimbo wake wa Utamu kwa Yesu mbele ya mashabiki wake (hawapo pichani) jioni ya leo ndani ya uwanja wa Taifa,ambako tamasha la Krisimasi likiendelea jioni ya leo. 
 Muimbaji wa nyimbo za kuabudu,Upendo Kilahiro akiimba kwa hisia jukwaani jioni ya leo kwenye tamasha la krisimasi,linaloendelea hivi sasa ndani ya uwanja wa Taifa jijini Dar.

 Baadi ya Waimbaji wa kundi la Glorious wakiimba jukwaani 
Mwimbaji wa nyimbo za injili,Boni Mwaitege pichani kati na madansa wake wakiwaimbisha mashabiki wao jioni ya leo .
 Sehemu ya umati wa Watu wakifuatilia tamasha la Krisimasi,linalofanyika jioni ya leo ndani ya Uwanja wa Taifa,ambalo limejumuisha wanamuziki mbalimbali ndani na nje ya Tanzania.
 Kundi la waimbaji mahiri wa muziki wa injili The Voice wakiimba Acapera zao jukwaani jioni ya leo kwenye tamasha la Krisimasi linalofanyika hivi sasa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar.Tamasha hilo huandaliwa kila mwaka na kampuni ya Msama Promotions Ltd
 Mgeni rasmi wa tamasha la Krisismasi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu na Bunge,Mh.William Lukuvi akiwasalimia mashabiki watazamaji mbalimbali waliofika kwenye tamasha hilo,linalofanyika hivi sasa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar .

WANAFUNZI WA CBE WATOA MKONO WA KHERI YA X MASS KATIKA KITUO CHA WATOTO YATIMA- MIYUJI

$
0
0
 Hii ni nembo ya kituo hiki iyonacho sadifu mazingira harisi ya watoto wanolelewa mahari hapa.
Remidius M. Emmanuel (Rais wa Serikali ya wanafunzi CBE ya Dodoma) akikabidhi zawadi hizi kwa mlezi wa kituo hiki zilizopokelewa na mtoto katika kituo cha Watoto Yatimu cha Miyuji jana tarehe 24/12/2013 mnamo saa tano asubuhi, akitoa pongezi kwa Mlezi wa kituo hicho Sister Glory Shayo kwa kulea watoto hawa. Rais aliwasilisha baadhi ya vitu kwaajili ya watoto hao.Vitu vilivyotolewa ni Mchele kilo 50,Ngano kilo 50,Mafuta kula lita 20,Mafuta ya kujipata  dazan 1 naMaji carton 2.
Mlezi wa kituo hicho Sister Glory Shayo akipoke ndoo mbili za mafuta ya kula
Mtoto anayelelewa kwenye kituo icho akipokea mafuta kwa niaba ya watoto wenzake wanaolelewa katika kituo hicho
Huu ndio msaada uliotolewa na uongozi wa Serikali ya wanafunzi CBE ya Dodoma hapo jana.



 Rais akiwa na watoto hawa akionyesha upendo kwa watoto Yatima
 Mhe, Remidius M. Emmanuel (Rais wa Serikali ya wanafunzi CBE ya Dodoma) akiwa na baadhi ya viongozi katika kituo cha Watoto Yatimu cha Miyuji jana tarehe 24/12/2013 mnamo saa tano asubuhi, akitoa pongezi kwa Mlezi wa kituo hicho Sister Glory Shayo kwa kulea watoto hawa. Rais aliwasilisha baadhi ya vitu kwaajili ya watoto hao
 "Napenda tuwe mfano mzuri ndani na nje ya chuo, hata Mkoa kuwatembele watoto hawa kujiona nao ni sehemu ya jamii kiujumla" Maneno ya Rais.
Mhe, Yohana akimsikiliza Mhe, Remidius M. Emanuel anavyo toa zawadi hizo
 Watoto hawa wakiongea na ndugu Dominicky Stephano na nyuso zao zikionekana ni za furaha 


 Waziri wa Fulsa na Mipango Mhe, Riziki Shaweji akiwa na Naibu Waziri wa Fedha Mhe, Simba


 Zawadi zilizo tolewa





 Mhe Ignas alipata bahati ya kutembelea shamba la mboga mboga hili ni shamba ambalo kituo kimeweza kuliwekeza kwa ajili ya kilimo hiki cha mboga mboga:


 Hakuna mahari popote duniani panapoweza kuondokana na janga la njaa pasipo kuwekeza katika kilimo vivyo hivyo hivyo katika kituo hiki wameamua kupigana na adui njaa kwa kujiandalia mazao yao: Tazama mashamba haya:

Airtel yawatakia Watanzania heri ya sikukuu

$
0
0
Kampuni ya mitandao ya simu za mkononi ya Airtel imewaasa Watanzania wote kote nchini kulinda amani na utulivu wa nchi katika kipindi hiki cha sikukuu ikiwa ni baada ya kuwatakia heri ya Christmas na mwaka mpya.

Akizungumza kwenye ofisi za makao makuu ya Airtel, Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando alisema sikukuu za Christmas na mwaka mpya ni sikukuu muhimu sana kwa wananchi wa taifa hili hivyo zinapaswa kusherehekewa kwa amani na utulivu.

“Ninawaomba wateja wa Airtel na watanzania wote kwa ujumla kutambua umuhimu wa sikukuu hizi na kuepuka kufanya matukio ambayo yanaweza kuhatarisha amani na utulivu wa taifa,” alisema Mmbando.

Aidha alisema katika msimu huu wa sikukuu bado Airtel inazidi kudhihirisha kuwa ni baba lao  kwa wateja wake kwa kutoa  huduma zilizo za gharama nafuu zinazowawezesha kutuma na kupokea pesa bure pia kutumia huduma mbalimbali za inataneti na kupiga kwenda mitandao yote.

“Airtel  bado ni baba lao kupitia huduma zetu mbalimbali, Wateja wetu bado wanaweza kunufaika na huduma zetu ambapo kwa sasa wateja wanaweza kupata vifurushi vya inataneti kwa gharama nafuu, kupiga simu kwenda mitandao yote na pia kutuma na kupokea pesa bure,” alisema Mmbando.

Ikumbukwe kuwa vifurishi vyote vya siku vya Yatosha vinadumu kwa masaa 25 tangu mteja anapojiunga ikiwa na lengo maalumu la kumfanya mteja aweze kufurahia huduma hiyo na kuwafaidisha watanzania waendelee kuokoa pesa nyingti walizokuwa wakizitumia kwenye mawasiliano na kuanza kuzitumia katika shughuli nyingine za uchumi wa taifa na jamii kwa ujumla.

Salamu za Chrismas na Mwaka Mpya Toka Thehabari.com

$
0
0
x-mas-tmgGAZETI la Mtandao la Thehabari.com (www.thehabari.com) linawatakia wasomaji wake na Watanzania wote kwa ujumla Heri ya Krismas na Mwaka Mpya 2014. Gazeti hili lina watakia wasomaji wake wote mwaka mpya wenye heri na mafanikio tele. Thehabari.com team imewaandalia mipango imara na ya uhakika itakayoboresha hali ya upatikanaji habari mpya kwa haraka zaidi na zenye uhakika ili kuzindi kutii kiu ya wasomaji wetu. Chagua Thehabari.com kwa habari zilizofanyiwa uchunguzi wa makini.
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images