Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

Rais Magufuli ashuhudia utiaji saini mikataba kati ya Tanzania na Barrick Gold Corp

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia utiaji saini wa mikataba ya makubaliano ya kuendesha kwa pamoja kapuni ya Twiga ya uchimbaji wa Madini kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Barrick ambapo kwasasa kampuni mpya ya ubia ya Twiga, Serikali itakuwa na hisa ya asilimia 16 .Halfa iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam. Januari 24, 2020.
Waziri wa Madini Mhe. Dotto Biteko akikidhiana mikataba na Rais wa kampuni ya Barrick Dkt. Mark Bristow iliyosainiwa mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika hafla utiaji saini wa mikataba ya makubaliano ya kuendesha kwa pamoja kapuni ya Twiga ya uchimbaji wa Madini kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Barrick ambapo kwasasa kampuni mpya ya ubia ya Twiga, Serikali itakuwa na hisa ya asilimia 16 Ikulu jijini Dar es Salaam. Januari 24, 2020.

Waziri wa Madini Mhe. Dotto Biteko akiwa na Rais wa kampuni ya Barrick Dkt. Mark Bristow wakionyesha Mikataba iliyosainiwa mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika hafla ya utiaji saini wa mikataba ya makubaliano ya kuendesha kwa pamoja kapuni ya Twiga ya uchimbaji wa Madini kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Barrick ambapo kwasasa kampuni mpya ya ubia ya Twiga, Serikali itakuwa na hisa ya asilimia 16 Ikulu jijini Dar es Salaam. Januari 24, 2020. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza katika hafla ya utiaji saini wa mikataba ya makubaliano ya kuendesha kwa pamoja kapuni ya Twiga ya uchimbaji wa Madini kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Barrick ambapo kwasasa kampuni mpya ya ubia ya Twiga, Serikali itakuwa na hisa ya asilimia 16 .Halfa iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam. Januari 24, 2020.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mkono na Rais wa kampuni ya Barrick Dkt. Mark Bristow katika hafla ya utiaji saini wa mikataba ya makubaliano ya kuendesha kwa pamoja kapuni ya Twiga ya uchimbaji wa Madini kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Barrick ambapo kwasasa kampuni mpya ya ubia ya Twiga, Serikali itakuwa na hisa ya asilimia 16 .Halfa iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam. Januari 24, 2020.
Rais wa kampuni ya Barrick Dkt. Mark Bristow akizungumza mbele ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika hafla ya utiaji saini wa mikataba ya makubaliano ya kuendesha kwa pamoja kapuni ya Twiga ya uchimbaji wa Madini kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Barrick ambapo kwasasa kampuni mpya ya ubia ya Twiga, Serikali itakuwa na hisa ya asilimia 16 .Halfa iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam. Januari 24, 2020

Wageni waalikwa wakipiga makofi mara baada yay a hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika hafla ya utiaji saini wa mikataba ya makubaliano ya kuendesha kwa pamoja kapuni ya Twiga ya uchimbaji wa Madini kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Barrick ambapo kwasasa kampuni mpya ya ubia ya Twiga, Serikali itakuwa na hisa ya asilimia 16 .Halfa iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam. Januari 24, 2020. PICHA NA IKULU


BENKI YA NMB YAKABIDHI VIFAA VYA UJENZI ‘SINGIDA DC’ VYENYE THAMANI YA SHILINGI MIL.20

$
0
0
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kati, Nsolo Mlozi (wa tatu kulia) akimkabidhi mabati Mkuu wa Wilaya ya Singida, Mhandisi Paskas Muragili kwa ajili ya kumazia ujenzi wa vyumba vya madarasa katika wilaya hiyo. Wa pili kutoka kushoto ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe na kushoto ni Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Singida, William Mponzi.
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kati, Nsolo Mlozi, akizungumza na Wananchi wa Kata ya Msange wakati akikabidhi msaada huo wa vifaa vya ujenzi, nondo, mabati, mbao, misumari na makowa kwa ajili ya kusaidia kumalizia ujenzi wa madarasa ya Shule ya Msingi Msange.
 Wananchi wa Kata ya Msange wakiwa kwenye hafla ya kupokea msaada huo.
 Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe,  akizungumza na Wananchi wa Kata ya Msange wakati wa hafla ya kupokea msaada huo.
 Wazazi na wanafunzi wakiwa katika hafla hiyo.
 Muonekano wa jengo la Zahanati ya Kijiji cha Mwachambia kilichopo Kata ya Maghojoa. Kata hiyo haina kituo cha afya wala zahanati hivyo nguvu ya pamoja inahitajika ili kumalizia jengo hilo.
 Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe, akiwa na wakina mama wa Kata ya Maghojoa baada ya kupokea msaada huo. 
 Viongozi wakiwa meza kuu wakati wa kupokea msaada huo. Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe, akisisitiza jambo kwa wananchi wa Kata ya Ngimu Kijiji cha Misuna wakati wa kupokea msaada huo.
 Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Singida, William Mponzi akiwaeleza wananchi wa  Kata ya Msange ambao hawajafungua akaunti wakafungue katika benki hiyo.
Picha ya pamoja baada ya kupokea msaada wa vifaa vya ujenzi kwa ajili ya kumalizia Zahanati ya Kijiji cha Mwachambia. Wa pili kutoka kushoto ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe, wa nne kutoka kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Singida, Mhandisi Paskas Muragili, kulia kwa DC Muragili ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Elia Digha, Diwani wa Kata ya Maghojoa, Churi na Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Singida, William Mponzi na viongozi wa Chama na Serikali wa wilaya hiyo.
 
Na Dotto Mwaibale, Singida
BENKI ya NMB imekabidhi msaada wa vifaa vya ujenzi katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida vyenye jumla ya thamani ya shilingi milioni 20, kwa lengo la kukamilisha majengo ya zahanati na vyumba vya madarasa. 
Akikabidhi msaada huo kwa Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhandisi Paskas Muragili, Meneja wa Kanda ya Kati wa benki hiyo, Nsolo Mlozi, alisema wametoa vifaa hivyo kwa kuwa NMB ni benki inayomjali mteja na ina utaratibu wa kutenga asilimia moja ya faida inayopata na kurudisha kwa jamii
Nsolo alisema, azma ya benki hiyo mbali ya kuboresha huduma zake mbalimbali za kibenki, inajitahidi kuhakikisha ipo bega kwa bega na serikali ya Awamu ya Tano katika kuchochea na kuunga mkono juhudi za maendeleo ya kijamii na kiuchumi, hususan kwenye eneo la miundombinu ya afya na elimu.
Akipokea msaada huo, Muragili mbali ya kuishukuru NMB, aliwapongeza wananchi kwa kujitoa kama nguvu kazi kama sehemu ya kuchochea muktadha chanya wa maendeleo endelevu kwenye sekta ya elimu na afya.
“Sisi kama wilaya tupo pamoja na nyinyi, na ofisi yangu itachangia mifuko kumi ya saruji ili kusaidia kasi ya ujenzi wa matundu ya vyoo kwenye shule hii ya msingi Misuna ili kupunguza changamoto iliyopo” alisema Muragili, huku Benki hiyo ikichangia msaada wa mabati,mbao, misumari kwenye shule hiyo
Kwa upande wake, mdau mkubwa wa maendeleo, ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Singida kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Aysharose Mattembe, alisema 
"kwa niaba ya wananchi wa wilaya ya Singida ninawashukuru sana benki ya NMB, kiukweli benki hii haijachangia wilaya  ya Singida pekee, ikumbukwe imeshawahi pia kuchangia wilaya nyingine za mkoa wa Singida huko nyuma, ikiwemo Hospitali ya Rufaa ya mkoa wetu,” alisema na kuongeza:
“Mfano miaka minne iliyopita NMB walichangia vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi milioni ishirini na tano katika hospitali yetu,” alisema Mattembe huku akiwataka wadau  wengine wa maendeleo  kuiga mfano wa benki hiyo. 
nye shughuli mbalimbali  zenye tija mkoani hapa, aliwahimiza na kuwahamasisha wananchi ambao bado hawana akaunti NMB waende  kufungua akaunti ili kuipa nguvu ya kuendelea kuchangia kwenye jamii.
Naye Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Singida, Elia Digha pamoja na kuipongeza benki hiyo, aliwataka viongozi wa NMB kusogeza zaidi huduma za kibenki kwenye maeneo ya kata na vijiji, mathalani, eneo hilo la Kata ya Msange ambalo lina wakulima wazuri wa zao la vitunguu lakini wananchi wake wanapata shida sana kupata huduma za kibenki labda mpaka wasafiri kuelekea mjini
Katika hafla hiyo ya makabidhiano shule za msingi Misuna na Msange sambamba na zahanati za Mwachambia na Mwakichenche zilikabidhiwa msaada wa mabati, nondo, misumari na mbao vyenye thamani ya shilingi milioni tano kila moja kutoka kwenye benki hiyo.

HAKIKISHENI KILA MKULIMA ANAKUWA NA AKAUNTI BENKI-NAIBU WAZIRI BASHE

$
0
0


Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe akisisitiza jambo wakati wa kufunga Warsha ya kuwajengea uwezo Wenyeviti na Mameneja wa Vyama Vikuu vya Ushirika na Miradi ya Pamoja iliyofanyika Jijini Dodoma, kulia ni Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Dkt. Titus Kamani, (kushoto) Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume Dkt. Benson Ndiege akifuatiwa na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) Prof. Alfred Sife
Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania (TFC) Bi.Theresia Chitumbi akieleza masuala ya Vyama vya Ushirika wakati wa Warsha ya kuwajengea uwezo Wenyeviti na Mameneja wa Vyama Vikuu vya Ushirika na Miradi ya Pamoja iliyofanyika Jijini Dodoma hivi karibuni




Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Dkt. Benson Ndiege akiongea na wajumbe wa Warsha ya kuwajengea uwezo Wenyeviti na Mameneja wa Vyama Vikuu vya Ushirika na Miradi ya Pamoja iliyofanyika Jijini Dodoma, hivi karibuni
 Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Dkt. Titus Kamani akielezea Sekta ya Ushirika nchini wakati wa Warsha ya kuwajengea uwezo Wenyeviti na Mameneja wa Vyama Vikuu vya Ushirika na Miradi ya Pamoja iliyofanyika Jijini Dodoma hivi karibuni




Naibu Waziri wa Kilimo, Mheshimiwa Hussein Bashe amewataka viongozi wa Vyama Vikuu vya Ushirika na Miradi ya Pamoja kuhakikisha kuwa wakulima watakaouza mazao yao kupitia Vyama vya Ushirika wanakuwa na Akaunti za Benki kwa lengo la kuwawezesha kupata fedha zao kwa wakati na uhakika.

Mheshimiwa Bashe ametoa agizo hilo leo Ijumaa, Januari 24, 2020 Jijini Dodoma alipokuwa akifunga Warsha ya kuwajengea uwezo Wenyeviti na Mameneja wa Vyama Vikuu vya Ushirika na Miradi ya Pamoja iliyofanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 22 Januari 2020 ambayo iliandaliwa kwa pamoja kati ya Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC) na Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU).

“Hakikisheni kila mkulima anafungua Akaunti Benki ili iweze kumsaidia kupata fedha zake kwa wakati na uhakika, nafahamu wakulima wamekuwa wakicheleweshewa malipo yao bila sababu za msingi; tunataka tatizo hili litatuliwe mara moja,” alisema Mhe. Bashe

Naibu Waziri amesema kuwa Benki ziko tayari kuwahudumia wakulima bila gharama yoyote watakapofungua akaunti kwenye Benki hizo na kupitishia malipo ya mazao yao wakati wa kuyauza kupitia Vyama vya Ushirika na kuondoa udanganyifu na wizi unaofanywa na watendaji wa Vyama wasio waadilifu.

“Wakulima wamekuwa wakinyanyasika sana kwani kuna udanganyifu mwingi na wizi unaofanywa kwa wakulima wakati wa msimu wa mauzo. Katika maeneo mengine utakuta fedha inaletwa kwenye AMCOS lakini malipo hayafanyiki na badala yake mkulima anaambiwa kuendelea kusubiri kwa muda usiojulikana,” alisema Mhe. Bashe.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Bashe amevitaka Vyama vya Ushirika kuagiza Pembejeo kwaajili ya wakulima ili kurahisisha upatikanaji wake na kupunguza gharama za uzalishaji kwa mkulima.

“Katika kuagiza Pembejeo ikiwezekana tumieni fedha zenu wenyewe badala ya kukopa Benki ambazo zinawatoza riba kubwa na mlipaji wa mikopo hiyo ni mkulima na hivyo kuendelea kumdidimiza badala ya kumkomboa,” alisema Naibu Waziri.

Aidha, Mhe. Bashe amewataka watu wote wakiwemo baadhi ya viongozi waliochukua mali za wanaushirika popote nchini wazirejeshe mali hizo kwenye Vyama vya Ushirika na kushindwa kufanya hivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

“Lazima viongozi wa Ushirika tubadilike ili vyama vya Ushirika viweze kuchangia na kulifanya Taifa letu kufikia Uchumi wa Kati. Tunatakiwa kuwa na viongozi sahihi ambao ndio madereva, makondakta na wapiga debe sahihi kwenye Vyama vyetu,” alisema Mhe. Bashe

Watalii zaidi ya 60 Wawasili na Treni ya Kifahari ya Rovols (Pride of Africa), wakitokea Afrika Kusini, watatembele maeneo mbalimbali ya kitalii nchini

$
0
0
  Wafanyakazi wa Treni ya Kifahari ya Rovol Rail wakishusha mizigo mara baada ya treni hiyo kuwasili katika stesheni ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) Jijini Dar es Salaam ikitokea Afrika ya Kusini ikiwa na Watalii Zaidi ya 60 kutoka nchi mbalimbali duniani  ikwemo Marekani na Uingereza ambao wataende kutalii katika meneo mbalimbali hapa nchini ikiwemo Jiji la Dar es Salaam, Mji wa Zanzibar, Serengeti na Ngorongoro, hii ni safari ya kwanza kwa treni katika safari tano kwa mwaka 2020.
Mtaalam wa masuala ya Kihitoria na Utamaduni wa Afrika kutoka Afrika Kusini , Nicholas Schofield akifurahia jambo baada ya kuwasili katika Stesheni ya Treni TAZARA Jijini Dar es Salaam akiwa na treni ya Kifahari  Rovol Rail( Pride of Africa) iliyowasili leo Januari 25, 2020 ikiwa na watalii Zaidi ya 60 kutoka nchi mbalimbali duniani ikiwemo Marekani na Uingereza ambao wataende kutalii katika meneo mbalimbali hapa nchini ikiwemo Jiji la Dar es Salaam, Mji wa Zanzibar, Serengeti na Ngorongoro, hii ni safari ya kwanza kwa treni katika safari tano kwa mwaka 2020.
Watalii wakishuka kwenye treni ya Kifahari  Rovol Rail( Pride of Africa) iliyowasili leo Januari 25, 2020 katika Stesheni ya Treni TAZARA Jijini Dar es Salaam ikiwa na watalii Zaidi ya 60 kutoka nchi mbalimbali duniani ikiwemo Marekani na Uingereza  ambao wataende kutalii katika meneo mbalimbali hapa nchini ikiwemo Jiji la Dar es Salaam, Mji wa Zanzibar, Serengeti na Ngorongoro, hii ni safari ya kwanza kwa treni katika safari tano kwa mwaka 2020.
Watalii wakienda kupanda usafiri wa kuwapeleka hotelini mara baada ya kushuka  kwenye treni ya Kifahari Rovol Rail( Pride of Africa) iliyowasili leo Januari 25, 2020 katika Stesheni ya Treni TAZARA Jijini Dar es Salaam ikiwa na watalii Zaidi ya 60 kutoka nchi mbalimbali duniani ikiwemo Marekani na Uingereza  ambao wataende kutalii katika meneo mbalimbali hapa nchini ikiwemo Jiji la Dar es Salaam, Mji wa Zanzibar, Serengeti na Ngorongoro, hii ni safari ya kwanza kwa treni katika safari tano kwa mwaka 2020.
Mwimbaji wa Bendi ya Polisi akicheza na mmoja wa  wafanyakazi wa treni ya kifahari ya Rovols (Pride of Afrika), mara baada ya kuwasili kwa treni hiyo Jijini Dar es Salaam ikitokea Afrika ya Kusini ikiwa na  watalii Zaidi ya 60 kutoka nchi mbalimbali duniani ikwemo Marekani na Uingereza ambao wataende kutalii katika meneo mbalimbali hapa nchini ikiwemo Dar es Salaam, Mji wa Zanzibar, Serengeti na Ngorongoro, hii ni safari ya kwanza kwa treni katika safari tano kwa mwaka 2020.
Watalii wakicheza  na Bendi ya Polisi mara baada ya kuwasili kwa treni  ya kifahari ya Rovols (Pride of Africa), Jijini Dar es Salaam ikitokea Afrika ya Kusini ikiwa na  watalii Zaidi ya 60 kutoka nchi mbalimbali duniani ikiwemo Marekani na Uingereza ambao wataende kutalii katika meneo mbalimbali hapa nchini ikiwemo  Jiji la Dar es Salaam, Mji wa Zanzibar, Serengeti na Ngorongoro, hii ni safari ya kwanza kwa treni katika safari tano kwa mwaka 2020.
Bendi ya Polisi ikitoa Burudani kwa Watalii Zaidi ya 6O (hawapo pichani)  waliowasili na Treni ya kifahari ya Rovols (Pride of Afrika), watalii hao watatembelea maeneo mbalimbali ya kitalii hapa nchini ikiwemo Jiji la Dar es Salaam, Mji wa Zanzibar, Serengeti na Ngorongoro, hii ni safari ya kwanza kwa treni katika safari tano kwa mwaka 2020.
Watalii wakipiga picha waimbaji wa Bendi Polisi mara baada ya kuwasili kwa treni  ya kifahari ya Rovols (Pride of Africa), Jijini Dar es Salaam ikitokea Afrika ya Kusini ikiwa na  watalii Zaidi ya 60 kutoka nchi mbalimbali duniani ikiwemo Marekani na Uingereza ambao wataende kutalii katika meneo mbalimbali hapa nchini ikiwemo  Jiji la Dar es Salaam, Mji wa Zanzibar, Serengeti na Ngorongoro, hii ni safari ya kwanza kwa treni katika safari tano kwa mwaka 2020.
 Treni ya Kifahari ya Rovols Rail (Pride of Africa) ikiwa imepaki katika Stesheni ya TAZARA Jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwashusha watalii Zaidi ya 60  kutoka nchi mbalimbali duniani ikiwemo Marekani na Uingereza waliowasili na Treni hiyo ikitokea Afrika ya Kusini, watalii hao watatembelea katika meneo mbalimbali hapa nchini ikiwemo  Jiji la Dar es Salaam, Mji wa Zanzibar, Serengeti na Ngorongoro, hii ni safari ya kwanza kwa treni katika safari tano kwa mwaka 2020.

Treni ya Kifahari  ya Rovol Rail ikiwasili katika stesheni ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) Jijini Dar es Salaam ikitokea Afrika ya Kusini  ikiwa na Watalii Zaidi ya 60 kutoka nchi mbalimbali duniani ikwemo Marekani na Uingireza ambao wataende kutalii katika meneo mbalimbali hapa nchini ikiwemo Jiji la Dar es Salaam, Mji wa Zanzibar, Serengeti na Ngorongoro, hii ni safari ya kwanza kwa treni katika safari tano kwa mwaka 2020.

Mtalii akipiga picha Bendi Polisi waliokuwa wakitoa burudani kwa watalii waliowasili na Treni ya Kifahari ya Rovols Rail (Pride of Africa), katika Stesheni ya TAZARA Jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwashusha watalii Zaidi ya 60  kutoka nchi mbalimbali duniani ikiwemo Marekani na Uingereza waliowasili na Treni hiyo ikitokea Afrika ya Kusini, watalii hao watatembelea katika meneo mbalimbali hapa nchini ikiwemo Jiji la Dar es Salaam, Mji wa Zanzibar, Serengeti na Ngorongoro, hii ni safari ya kwanza kwa treni katika safari tano kwa mwaka 2020.
(Picha na Idara ya Habari-MAELEZO)

WAZIRI KAIRUKI APONGEZA JUHUDI ZA BRELA

$
0
0
Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji, Mhe. Angellah Kairuki amepongeza juhudi zinazofanywa na Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) katika kuhamasisha urasimishaji wa Biashara.

Hayo yamebainiswa leo alipohudhuria kama Mgeni rasmi kwa niaba ya Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan katika Warsha ya kwanza ya Wanawake wa Kiislamu katika ujasiriamali na Tanzania ya viwanda iliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika Warsha hiyo Mhe. Kairuki amesema ni muhimu sana kwa Wajasiriamali kurasimisha Biashara kwa kuwa itafungua fursa nyingi sana.

“Kurasimisha Biashara ni muhimu sana, na ninafurahi sana kuwaona BRELA hapa, kwa sababu, urasimishaji wa biashara unakuja na fursa mbalimbali ambazo zinazaidia ukuaji na kuongeza kipato”.Alisema Mhe. Kairuki.

Naye Msaidizi wa Usajili Mkuu kutoka BRELA, Bw. George Chuwa ametoa wito kwa wanawake wote wajasiriamali kusajili majina ya Biashara zao, Alama za Biashara au huduma, Usajili wa Kampuni na pia huduma zingine za BRELA.

“Natoa rai kwa wanawake wajasiriamali wote kutumia huduma za BRELA ambazo zote zinapatikana kwa njia ya mtandao. 

Huduma hizo ni pamoj na Usajili waa Majina ya Biashara, Usajili wa Alama za Biashara au Huduma, Usajili wa Kampuni, Kutoa Hataza, Kutoa Leseni za Biashara Kundi A pamoja na kutoa Leseni za Viwanda”.

Aidha Bw. Chuwa ameeleza kuwa ili kuweza kufungua huduma katika mfumo wa ORS hitaji la kwanza ni kuwa na namba ya utambulisho wa Taifa kisha kutembelea www.brela.go.tz ili kupata huduma zote. 

Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji, Mhe. Angellah Kairuki akisikiliza kwa makini jambo katika Warsha ya kwanza ya Wanawake wa Kiislamu katika ujasiriamali na Tanzania ya viwanda iliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.
 Msaidizi wa Usajili Mkuu kutoka BRELA, Bw. George Chuwa akiwasilisha mada kuhusu nafasi ya BRELA kufanikisha Tanzania ya Viwanda katika Warsha ya kwanza ya Wanawake wa Kiislamu katika ujasiriamali na Tanzania ya viwanda iliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam

Ally Rehmtullah Azindua Duka la Kisasa la Mavazi Yaliyobuniwa na Wabunifu wa Tanzania

$
0
0

Naibu Waziri Habari, Utamduni,Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza akiwa ameshika moja kati ya bidhaa zilizobuniwa na Mbinufu wa mitindo ya mavazi wa Tanzania, Ally Rehmtullah mara baada ya kuzindua duka la mavazi ya aina mbalimbali yaliyobuniwa na Rehmtullah. Hafla iliyofanyika leo Chole Road Masaki jijini Dar Es Salaam 
Naibu Waziri Habari, Utamduni,Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza akizungumza jambo na Mbinufu wa mitindo ya mavazi wa Tanzania, Ally Rehmtullah kwenye hafla ya uzinduzi wa duka la mavazi na mitindo yaliyobuniwa na wabunifu wa Tanzania
Naibu Waziri Habari, Utamduni,Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza akiwa kwenye picha ya pamoja na wabunifu mbalimbali.

Kamati ya Bunge ya Uwekezaji Yatembelea Kiwanda cha ALAF.

$
0
0

Mwenyekiti wa Chama cha wafanyakazi wa Kiwanda cha ALAF, Wilberforce Msokwa akiwaongoza wajumbe wa Kamati ya Bune ya Kudumu ya Mitaji ya Umma walipotembelea kiwanda hicho.
Meneja wa Usalama pakazi wa Kiwanda cha ALAF, Fredrick Nowi (katikati) akimuongoza Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kuduma, Dk Raphael Chegeni (kushoto) wakati wajumbne wa kamati hiyo walipotembelea kiwanda hicho

Wajumbne wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mitaji ya Umma, wakiangalia jinsi uzalishaji unavyofanyika katika Kiwanda cha ALAF jijini Dar es Salaam walipotembelea ijumaa



Fundi Mitambo na Uzalishaji wa Kiwanda cha ALAF, Paul Luambano (kulia) akiwaelezea wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mitaji ya Umma jinsi mitambo inavyofanya kazi wakati kamati wajumbe wa kamati hiyo walipotembelea kiwandani hapo kuangalia jinsi uzalishaji unavyofanyika

 
 
==========  ========  =========
Kamati ya Bunge ya Uwekezaji ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Mhe. Raphael Chegeni, leo imefanya ziara katika kiwanda cha ALAF jijini Dar es salaam. 

Madhumuni ya ziara hii ni kuipa Kamati hiyo uelewa zaidi kuhusu shughuli mbalimbali za uzalishaji wa bidhaa zinazofanywa na kiwanda hicho.

Tarehe 14 Januari mwaka huu, Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Bw. Dipti Mohanty alipata mwaliko wa kuhudhuria kikao cha Kamati hiyo ya Bunge ya Uwekezaji, ambapo alipata fursa ya kuelezea mafanikio ya kampuni hiyo na changamoto mbalimbali za kibiashara.

Kamati hiyo iliipongeza ALAF kwa mafanikio makubwa iliyopata hivi karibuni, na kuahidi kuitembelea kampuni hiyo, ahadi ambayo imetimizwa leo na Mwenyekiti wa Kamati pamoja na Wajumbe wote.

Katika ziara ya leo, Kamati imepata fursa ya kutembelea kiwanda cha ALAF na kujionea hatua za uzalishaji, bidhaa na huduma mbalimbali. Pamoja na kukutana na baadhi ya wafanyakazi wa ALAF, pia walitembelea kituo cha afya kinachotoa huduma za matibabu kwa wafanyakazi na familia zao,.

Mtendaji Mkuu, Dipti Mohanty ameishukuru Kamati ya Bunge ya Uwekezaji kwa kupata muda wa kutembelea ALAF. Mtendaji Mkuu huyo ameahidi kuendelea kushirikiana na Serikali katika juhudi zake za kujenga Tanzania ya viwanda, na kuikaribisha Kamati hiyo kutembelea ALAF tena.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji, Mhe. Raphael Chegeni, alisema wamekuja kuangalia jinsi gani wanaweza kusaidia ukuwaji wa sekta ya viwanda pamoja na kutatua changamoto mbalimbali zikiwemo upatikanaji wa nishati ya umeme wa hakika pamoja na malipo ya VAT zinazodaiwa kutoka kwa mamalaka ya mapato TRA. 

Vodacom Tanzania plc yaionesha PAPU namna inavyoweza kuhusika kwenye ujumuishwaji kifedha( financial inclusion)

$
0
0

Mkuu wa mauzo wa Vodacom kanda ya kaskazini, Brigita Stephen (kulia) akizungumza jinsi ambavyo kampuni ya Vodacom inaweza kuwa mshirika na PAPU katika ujumuishwaji wa kifedha (financial inclusion) kwenye mkutano wa Pan African Postal Union (PAPU) uliofanyika jijini Arusha. Pembeni ni Naibu katibu mkuu wizara ya ujenzi, uchukuzi na mawasiliano, Dkt. Jim Yonaz.
  
Mkuu wa mauzo wa Vodacom kanda ya kaskazini, Brigita Stephen (kulia) akizungumza jinsi ambavyo kampuni ya Vodacom inaweza kuwa mshirika na PAPU katika ujumuishwaji wa kifedha (financial inclusion) kwenye mkutano wa Pan African Postal Union (PAPU) uliofanyika jijini Arusha. Pembeni ni Naibu katibu mkuu wizara ya ujenzi, uchukuzi na mawasiliano, Dkt. Jim Yonaz.


WAFANYABIASHARA WA MADINI WANAOFUATA SHERIA WALINDWE-MAJALIWA

$
0
0

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofunga semina ya Viongozi wa  Dola katika Usimamizi na Udhibiti wa Rasilimali Madini kwenye ukumbi wa St. Gaspar jijini Dodoma, Januari 26, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Adelardus Kilangi baada ya kufunga semina ya Viongozi wa  Dola katika Usimamizi na Udhibiti wa Rasilimali Madini kwenye ukumbi wa St. Gaspar jijini Dodoma, Januari 26, 2019. Kulia ni Waziri wa Madini, Doto Biteko , Wa tatu kulia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Madini, Stanslaus Nyongo na wapili kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila
Baadhi ya washiriki wa  semina ya Viongozi wa  Dola katika Usimamizi na Udhibiti wa Rasilimali Madini wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipofunga semina hiyo kwenye ukumbi wa St. Gaspar jijini Dodoma, Januari 26, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa semina ya Viongozi wa  Dola katika Usimamizi na Udhibiti wa Rasilimali Madini baada ya kuifunga semina hiyo kwenye ukumbi wa St. Gaspar jijini Dodoma, Januari 26, 2019. Waliokaa kutoka kushoto ni Katibu  Mkuu, Wizara ya Madini, Profesa. Simon Msanjila, Waziri wa Madini, Doto Biteko, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt.  Adelardus Kilangi, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Bilinith Mahenge na kulia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Madini, Stanslaus Nyongo.
  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
………….
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameviagiza vyombo vya Ulinzi na Usalama vihakikishe vinawalinda wafanyabiashara wa madini wanaofanya kazi zao kwa kufuata sheria na kujiepuka kamata kamata zisizo na tija.
“Katika kipindi cha hivi karibuni kumejitokeza malalamiko mengi kutoka kwa wawekezaji na wadau wa madini kuhusu kukamatwa au kubughudhiwa bila sababu za msingi. Kutokana na hali hiyo, natumia nafasi hii kukemea suala la ukamataji holela wa wawekezaji au wadau wa madini pasipo kufuata taratibu.”

Ametoa agizo hilo leo (Jamapili, Januari 26, 2020) wakati akifunga semina ya ushiriki wa vyombo vya Ulinzi na Usalama katika usimamizi na udhibiti wa rasilimali madini katika ukumbi wa Mtakatifu Gaspar jijini Dodoma.
Waziri Mkuu amesema kwamba vyombo vya Ulinzi na Usalama vinatakiwa vitumie Sheria, Kanuni na Miongozo mbalimbali iliyowekwa mahsusi kwa ajili ya kuimarisha usimamizi wa sekta ya madini. 

Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuviagiza vyombo vya Dola kusimamia na kudhibiti utoroshwaji wa madini na kuhakikisha kuwa masoko yote ya madini  nchini yanalindwa.

“Nyote mtakubaliana nami kwamba kila taasisi ina utaalamu na wataalamu wake. Kwa hivyo, hatunabudi kufanya kazi kwa kuheshimu na kutambua utaalamu ama taaluma za wengine tunaoshirikiana nao.” 

“Sasa ni vema tukaondoa tofauti zetu na kuwa kitu kimoja kwa lengo la kuimarisha udhibiti na usimamizi wa rasilimali madini. Aidha, tutambue kuwa kuna nyakati hatuhitaji kutumia nguvu nyingi bali ushauri tuu ili kutatua changamoto husika.”  

 Waziri Mkuu ameelekeza kwamba kuanzia sasa  wadau wote wanaopatikana na madini wapewe utaratibu wa kuelekea sokoni kuuza madini hayo badala ya kuwakamata wakiwa wanaenda sokoni. 
Waziri Mkuu amesema Wizara ya Madini kupitia Tume ya Madini ina ofisi mikoa yote ya Tanzania Bara, hivyo hakuna sehemu ambayo wanaweza kusema walikosa msaada wa kitaalamu. “Ni wajibu wetu sote kama watumishi wa umma kujenga mazingira rafiki ya kazi, kuaminiana na kufanya kazi kwa ushirikiano.” 

Wakati huo huo,Waziri Mkuu amesema kuazia sasa suala la migodi kutegemea bidhaa mbalimbali kutoka nje ya nchi lifikie ukomo kwa kuhakikisha kuwa, kila huduma inayohitajika migodini, inapatikana nchini. 
Waziri Mkuu amesema nchi inawajibu wa kutoa huduma zinazokidhi mahitaji ya wadau wa madini kwa maana ya kutoa huduma kwa ubora stahiki na kwa wakati muafaka. 

Amesema sekta ya madini inazalisha ajira ila kuna changamoto ya ubora wa ajira, mishahara na stahiki katika kazi zinazofanana na suala la unyanyasaji wa wafanyakazi. Waziri Mkuu amesema masuala mengi hapo yanaweza kuonekana haraka kwenye maeneo yao ya kazi, hivyo ni vyema wakawa na taarifa hizo kwa wakati na kuwasilisha kwa wahusika ili mambo yawekwe sawa na kuipeleka sekta mbele.  

Akizungumzia kuhusu suala la unyanyasaji wa wafanyakazi wazalendo amesema si suala la kufumbiwa macho kama ilivyo suala la usalama wa watenda kazi katika migodi.  

Kadhalika, suala la udhibiti wa wageni kufanya kazi ambazo zinaweza kufanywa na Watanzania wenzetu pia ni jukumu letu na hivyo ni wajibu wetu kusimamia mikataba tuliyoingia na wawekezaji hususani eneo  la urithishaji wa madaraka na ujuzi kwa wazawa. Kwa upande wa Wizara ya Madini na Tume ya Madini, Waziri Mkuu amewaagiza watafute suluhu ya changamoto ya usalama wa wafanyakazi kipindi wakiwa kazini na baada ya kumaliza muda wa kazi kwa hiari au kwa kustaafu au kumaliza mkataba. “Tumepokea malalamiko mengi sana katika eneo hilo.” 

“Hivyo, ni wajibu wetu kushirikisha wadau wote wanaohusika na masuala ya ajira, bima za wafanyakazi, afya za wafanyakazi na usimamizi wa stahiki za wafanyakazi kukaa kwa pamoja na kutatua changamoto hii ili isiendelee kukomaa.”

Vilevile, Waziri Mkuu ameagiza suala la utunzaji wa mazingira liwekewe mkazo wa kipekee maana nje ya mazuri yote yaletwayo na Sekta ya Madini, uharibifu wa mazingira unaweza kugharimu maisha ya binadamu, wanyama na mimea. 

Waziri Mkuu amesema “mazingira yetu ndio uhai wetu sisi na vizazi vijavyo, hivyo ni wajibu wetu kama Wizara kuhakikisha wawekezaji wetu ni watu wema kwa mazingira yetu.” 

Pia, Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kumpongeza na kumshukuru Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa uthubutu mkubwa alioufanya ambao umeleta mageuzi makubwa katika Sekta ya madini.“Hili linadhihirishwa na kitendo cha utiaji saini makubaliano ya uanzishwaji wa Kampuni ya Twiga Minerals uliofanywa juzi Jijini Dar es Salaam tarehe 24 Januari 2020 ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Sheria Mpya ya Madini ya mwaka 2017.”

Awali, Waziri wa Madini Doto Biteko alisema lengo la semina hiyo ni kujenga uelewa wa pamoja kwenye masuala ya usimamizi wa sekta ya madini nchini.
Alisema suala la kudhibiti utoroshwaji wa madini linafanyika kwa kushirikiana kati Wizara ya Madini na vyombo vya Ulinzi na Usalama na kwamba wanaendelea kushirikiana katika kutatua changamoto zinazojitokeza.

Waziri Biteko ametumia fursa hiyo kutuma salamu kwa wafanyabiashara wanaojihusisha na utengenezaji na uuzaji wa madini bandia pamoja na wanaotaka kuuza madini nje ya mfumo kuwa zama zao zimekwisha.

Tamasha la KAN lamalizika kwa kishindo

$
0
0
Msanii Lawrence Okello kutoka Uganda kwenye siku ya kufunga tamasha la KAN

Mpenzi wa burudani Kazeneza akishangilia kwenye tamaasha la KAN
Umati wa mashabiki kwenye tamasha la KAN siku ya mwisho
Msanii Victor Kunonga na Mwenzake kutoka Zimbabwe wakitumbuiza
Wafanya kazi wa KAN wakimbeba Mkurugenzi waKAN Dave Ojay kushiria furaha siku ya kufunga tamasha.

Msanii Fareed Kubanda maarufu kama Fid Q akitumbuiza kwenye jukwaa la KAN

Msanii Tear Drops kutoka Kenya akitumbuiza kwenye jukwaa la KAN 
 

Msimu wa pili wa tamasha la Knowldge Art and Networking (KAN) umemalizika jana kwa kishindo na kuacha wapenzi wa burudani wakiwa na hamu ya kuendelea kupata burudani.

Tamasha hilo lenye kauli mbiu ya Maendeleo ni Watu Si Vitu imetokana na moja ya nukuu za Mwalimu Julius Nyerere lilifanyika kwenye viwanja Chuo cha Maendeleo na Ushirikiano wa Kimataifa (MS TCDC) kuanzia tarehe 22 mpaka 25 Januari mwaka huu.

Tamasha hili lilikua na fursa za kujifunza kutoka kwa wasanii wa sanaa za maonesho na utumbuizaji kutoka nchi saba za Afrika, kushirikishana maarifa na kuendeleza mahusiano yetu ya karibu katika jukumu letu la kuleta maendeleo, lakini pia kujenga mtandao.

Tamasha hili pia litahusisha wasanii wanaojikita katika sanaa ya kutoa uelewa wa maarifa mbalimbali (Conscious artists), ikiwa ni pamoja na wasanii wa sanaa za maonesho na utumbuizaji. Sanaa hii hujikita katika kuleta ufahamu na kuzunguzumzia masuala ya maendeleo na urithi wa tamaduni za Kiafrika. Pia wasaani hao watazungumzia masula yanayohusiana na jamii ya mkoa wa Arusha na Afrika kwa ujumla.

Kwa ujumla, malengo makuu ya tamasha hili ni pamoja na kutoa nafasi kwa wadau wa maendeleo kuakisi yaliyopita wakati wakitafakari yanayokuja, kutazama fursa zilizopo katika taaluma na kuhamasisha.

Pili, tamasha linalenga kutoa fursa kwa ajili ya kuchambua changamoto zilizopo katika jamii kama vile mimba za utotoni, wakimbizi, tatizo la ajira kwa vijana, rushwa, kisha kuchukua hatua za kukabiliana na changamoto hizi.

Na tatu ni kutengeneza na kuimarisha mtandao wa wadau wa maendeleo na uongozi ambao umeazimia kutoa mwamko kwa jamii ambao utaleta hamasa kwa jamii ya Waafrika.

Ezra vMbogori ni Mkurugenzi wa MSTCDC alisema,MSTCDC inatambua nguvu ya sanaa na kuamini kwa dhati kuwa kuiambatanisha sanaa pamoja na maisha katika jamii, inaweza kuwa ni njia thabiti ya kuiimarisha jamii.

"Jitihada za kuboresha hali ya maisha, kupunguza kutokuwepo kwa usawa, ni katika mambo yanahusishwa katika mila na desturi zilizorithiwa katika mfumo wa jamii. Utamaduni, ikiwa ni pamoja na sanaa, ni njia ya kuleta maendeleo ambayo tukijikita nayo inaweza kutuletea maisha mapya katika jamii,"alisema Mbogori.

Wasanii waliotumbuiza kwenye jukwaa la KAN ni pamoja na Vitali Maembe, Fid Q, Siti & The Band, Florence John from Tanzania, Sandra Nankoma kutoka Uganda, Juma Tutu, Bengatronics kutoka Kenya, Victor Kunonga kutoka Zimbabwe, na Isabella Novela kutoka Mozambique.

Tamasha hilo pia lilileta paamoja wasanii wa kazi za mikono 9 wakiwa na kazi mbalimbali kutoka Nchi tano za Afrika ikiwemo Kenya, Uganda, Tanzania, Congo na Zimbabwe.

artivists came up with different projects that they will be working between January 8 towards festival date and they will showcase their projects during the project.

Wasanii hao ni Mugabo Baretigire, Pamela Aobo, Arinitwe Peter, Sikhulile Sibanda from Zimbabwe Masoud Kibwana, Emmanuel Manoti Anderson, Naiteiemu Nyanjom na Reuben Kabamba.

WAZIRI BASHUNGWA AKUTANA NA MTENDAJI MKUU WA BRELA KUJADILI DIRA MPYA

$
0
0
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Bashungwa amekutana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni  (BRELA) Bw. Godfrey Nyaisa kwa Mara ya kwanza tangu alipomteua kuchukua nafasi hiyo.

Mhe. Bashungwa na Bw Nyaisa wamekutana leo Januari 27,2020 katika Ofisi ndogo ya Wizara iliyopo waterfront Jijini Dar es Salaam ili kujadili dira mpya ya BRELA.

Katika mazungumzo yake Waziri Bashungwa amemtaka Bw. Nyaisa kuhakikisha analipa uzito wa kipekee suala la uboreshaji wa Mfumo wa Usajili kwa njia ya mtandao (ORS) pamoja na huduma kwa mteja ili kupunguza usumbufu kwa wadau.

“Ninakutaka ufanyiekazi mapungufu yote yaliyopo BRELA hasa upande wa mifumo na huduma kwa wateja ili kwenda na kasi ya Mhe. Rais John Pombe Magufuli ya kuwa na Tanzania ya viwanda”.

Aidha Waziri Bashungwa amebainisha kwamba BRELA ni mlango wa wawekezaji na Wafanyabiashara hivyo huduma inapokuwa nzuri wateja wataongezeka pia mapato ya nchi yataongezeka.

Kwa Upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA Bw. Nyaisa ametoa shukrani zake kwa uteuzi aliopata na kuahidi kufanya maboresho makubwa.

“Nakuahidi kujenga BRELA mpya itakayojibu mahitaji ya wadau wake wote kwa haraka. Nitumie fursa hii pia kuwajulisha wadau wote kuwa tunaandaa mkutano nao kwa nia ya kufahamiana, kupata maoni  na ushauri wao katika kuijenga BRELA mpya”.

Bw. Nyaisa aliteuliwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa kuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA tarehe 19 Januari, 2020 akichukua nafasi ya Bi. Loy Muhando aliekuwa akikaimu nafasi hiyo.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa (kulia) akifanya mazungumzo na  Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA)  Bw. Godfrey Nyaisa alipomtembelea katika Ofisi ndogo ya Wizara iliyopo waterfront Jijini Dar es Salaam ili kujadili dira mpya ya BRELA. 

 Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa (kulia) akimkaribisha Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Bw. Godfrey Nyaisa (kushoto) mara baada kuwasili katika Ofisi ndogo ya Wizara iliyopo waterfront Jijini Dar es Salaam ili kujadili dira mpya ya BRELA.

KINONDONI YA SAINI MKATABA NA JWTZ UJENZI WA UWANJA W AKISASA, JENGO LA UTAWALA, MEYA SITTA ASEMA MKURUGENZI KAGURUMJULI NI MSIKIVU.

$
0
0

Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni leo imesaini mkataba na Jeshi la Wananchi (JWTZ) kwa ajili ya ujenzi wa Uwanja wa wa kisasa wa mpira wa miguu pamoja na Jengo la kisasa la Utawala la Halmashauri hiyo.

Mkataba huo umesainiwa leo na Mstahiki Meya wa Halmashauri hiyo Mhe. Benjamini Sitta pamoja na Luteni Kanali David Michael Luoga na kushuhudiwa na watendaji wa Halmashauri hiyo pamoja na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Kinondoni Harlod Maruma.

Akizungumza na wandishi wa habari wakati wa utiaji saini wa mkataba huo, Mhe. Meya Sitta amesema kuwa mradi wa ujenzi wa jengo la utawala utagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 1.6 huku ujenzi wa uwanja wa kisasa wa mpira wa miguu ukigarimu kiasi cha shilingi Bilioni 2.7.

Amefafanua kuwa uamuzi wa kutumia JWTZ umetokana na kufuata ushauri uliokuwa unatolewa na Mhe. Rais Dk. John Pombe Magufuli wakutumia Locol Fundi (Foce Account).

Mhe. Meya amesema kuwa miradi hiyo mikubwa miwili iliyosainiwa leo itajengwa na Jeshi la Wananchi kwakuwa wana amini watafanya kazi hoyo kwa umakini mkubwa na wa haraka kulingana na mkataba huo ulivyoeleza.

“ Tunamshukuru Mhe. Rais wetu mpendwa, Dk. Magufuli kwa kutuonyesha njia ya kufanya kazi kwa kutumia wanajeshi kwa kuwa itakamilika kwa wakati, hapa hakuna michakato, miradi hii mikubwa itafanywa na jeshi la JWTZ” amesema Meya Sitta.

Aidha Mhe. Meya Sitta amesema “ tunampongeza Mkurugenzi wetu Aron Kagurumjuli, kwakweli tuna mkurugenzi makini, msikivu ,ambaye anafuata maelekezo na ni mchapakazi ndio mana leo Kinondoni yetu ipo hapa” ameongeza.

Kwa upande wake Luteni Kanali Luoga ameipongeza Manispaa ya Kinondoni kwa kuwaamini kufanya kazi hiyo na kuahidi kukalimisha ujenzi huo kwa muda wa miezi sita.

Luteni Luoga amesema katika ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu, awamu ya kwanza itakamilika kwa kipindi cha miezi mitatu na nusu na awamu ya pili itatumia miezi miwili na nusu.

Ameongeza kuwa katika ujenzi huo ,licha ya kwamba Jeshi la Wananchi litafanyakazi hiyo,lakini pia litatoa nafasi kwa watu wengine ikiwemo Mama ntilie pamoja na vijana wengine lengo likiwa ni kila mwananchi apate kipato.

“ Tunampongeza Mhe. Meya Sitta, Mkurugenzi Kagurumjuli kwa kutuamini, nasisi tunawahakikishia kuwa Jengo la utawala pamoja na uwanja tutakamilisha kwa kipindi cha miezi sita kama ilivyo kwenye mkataba wetu”amesema Luteni Kanali Luoga.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni Mhe. Harlod Muruma amefafanua kuwa ujenzi huo wa miradi mikubwa miwili iliyotiwa saini leo ni utekelezaji wa ilani CCM.

Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Mhe. Benjamini Sitta katikati mwenyesuti, akiwa na Kaimu Mkurugenzi Mahudu Kazi wa kwanza kulia, Luteni Kanali wa JWTZ David Luoga wakipitia nyaraka za mkataba wa ujenzi wa Jengo la Utawala pamoja na Uwanja wa kisasa wa mpira wa miguu.
mradi wa ujenzi wa jengo la utawala utagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 1.6 huku ujenzi wa uwanja wa kisasa wa mpira wa miguu ukigarimu kiasi cha shilingi Bilioni 2.7.
Luteni Kanali wa JWTZ David Luoga, akiwaonyesha Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Benjamini Sitta, Kaimu Mkurugenzi Mahudu Kazi, mchoro wa uwanja wa mpira wa miguu utakavyokuwa. Mwenye shati la kijani kulia ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni Mhe. Harlod Muruma.

Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Mhe. Benjamini Sitta mwenyesuti akipeana mkono na Luteni Kanali David Luoga wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) mara baada ya kusaini mkataba na ujenzi wa miradi miwili mikubwa ya Jengo la Utawala pamoja na Uwanja wa mpira wa miguu.

DKT.MANONGI AWAPONGEZA WATUMISHI WA NCAA KWA KUCHAPA KAZI

$
0
0



Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya hifadhi wa Ngorogoro (NCAA) Dkt Freddy Manongi akiongea na watumishi wa Mamlaka hiyo wakati kikao cha kusikiliza maoni, kero na ushauri katika kuboresha utendaji kazi.
Naibu kamishna wa NCAA anayesimamia huduma za Shirika Bw. Asangye Bangu akijibu hoja mbalimbali za watumishi wakati wa kikao cha pamoja na watumishi hao.
Viongozi wa Kimila wa kabila la Kimasai (Laigwanan) wakimsikiliza kamishna wa Uhifadhi wa NCAA Dkt Freddy Manongi katika kikao cha pamoja kujadiliana mambo mbalimbali kuhusu uhifadhi.


Sehemu ya Watumishi wa NCAA wakimsikiliza Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka hiyo kuhusu masuala mbalimbali ya utendaji kazi.

…………………………………………………
Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Dkt Freddy Manongi amewapongeza watumishi wa Mamlaka hiyo kwa kufanya kazi kwa bidii, uzalendo na kujituma katika kutimiza malengo ya Mamlaka hiyo.

Dkt Manongi ametoa pongezi hizo wakati akizungumza na watumishi wa Mamlaka hiyo ikiwa ni utaratibu aliojiwekea wa kukutana na watumishi na kusikiliza kero, maoni, ushauri na malalamiko yanayohusu utendaji kazi wa watumishi na namna ya kuendelea kuboresha mazingira ya utendaji kazi.

Kamishna Manongi amebainisha kuwa jitihada za watumishi wa NCAA zimesaidia ongezeko la mapato ya shirika kutoka makusanyo ya shilingi bilioni 60 mwaka 2014/2015 hadi kufikia kiasi cha shilingi Bilioni 143 katika mwaka wa fedha 2018/2019.

“Ushirikiano, kujituma na jitihada katika kazi umetusaidia kutimiza malengo tuliyopewa na kupelekea ongezeko la mapato kutoka Bilioni 60 mwaka 2015 hadi Bilioni 143 mwaka 2018/2019 na tunaamini kama tutaendelea na moyo huu wa kufanya kazi kwa moyo tutaisaidia Serikali yetu kuongeza mapato zaidi kwa miaka ijayo” ameongeza Dkt Manongi.

Kwa upande wake Naibu Mhifadhi wa Mamlaka hiyo anayesimamia huduma za Shirika Bw. Asangye Bangu amewahakikishia watumishi hao kuwa NCAA itaendelea kuweka utaratibu wa kuhakikisha kuwa watumishi wanaendelea kupata mafunzo ya muda mfupi na mrefu ili kuwaongezea uwezo na tija katik utendaji kazi wao ili kutimiza malengo makuu matatu yay a mamlaka ambayo ni uhifadhi, utalii na maendeleo ya jamii.

Katika kuhakikisha NCAA inaboresha huduma kwa wadau wake Mamlaka hiyo inatarajia kuanzisha kituo cha huduma kwa wateja (Customer Call Centre) Jijini Arusha hivi karibuni ili kusaidia wadau mbalimbali katika upatikanaji wa huduma popote wanapokuwa bila kulazimika kufika ofisini.

Meneja Rasilimaliwatu wa Mamlaka hiyo Bw. Samson Ntunga amewaasa watumishi wa NCAA kuendelea kufanya kazi kwa uadilifu, uaminifu, uvumilivu, upendo, kuepuka migogoro na kuhakikisha kuwa wanazingatia maadili na misingi ya utendaji kazi katika utumishi wa Umma.

Katika hatua nyingine Uongozi na watumishi wa NCAA walitumia fursa ya kikao hicho kukutana na viongozi wa jamii ya Kimasai (Laigwanan) ambao ni wenyeji wanaoshi katika hifadhi ya Ngorongoro ikiwa ni sehemu ya mikutano endelevu ya kujadili mahusiano ya utendaji kazi na jamii hiyo, changamoto na mbinu mbalimbali katika kuendeleza kazi za uhifadhi kama sehemu ya wadau muhimu katika hifadhi hiyo.  

SERA YA USHIRIKA MSINGI WA MABADILIKO CHANYA YA SEKTA YA USHIRIKA

$
0
0


 Mkurugenzi mstaafu wa Rabo Foundation Netherlands Bw. Pierre Van Hedel akielezea namna Vyama vya Ushirika vinavyofanya kazi katika nchi ya Netherlands kwa lengo la kujifunza na kuongeza ujuzi katika maboresho ya Sera ya Ushirika ya Tanzania


 Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika wa Kifedha Bw. Josephat Kisamalala akieleza jambo wakati wa Warsha ya maboresho ya Sera ya Maendeleo ya Ushirika

 Mkurugenzi wa Mipango Ufuatiliaji na Tathmini wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Bw. Buji Bampebuye akifafanua jambo katika kikao cha Warsha ya kujadili maboresho ya Sera ya Ushirika (2002) kilichokuwa kikifanyika Mkoani Morogoro hivi karibuni
Mjumbe wa Bodi ya Chama Kikuu cha Ushirika wa Akiba na Mikopo Tanzania (SCCULT) Bi. Anna Lupiano akieleza matarajio ya Vyama katika maboresho ya Sera ya Maendeleo ya Ushirika
 Mshauri wa Kibiashara wa Shirika la Kimataifa lisilo la Kiserikali AGRITERRA Bw. Raymond Lyimo akitoa mada kwa wajumbe wa Warsha ya maboresho ya Sera ya Maendeleo ya Ushirika
 Mshauri wa Kibiashara wa Shirika la Kimataifa lisilo la Kiserikali AGRITERRA Bw. Mikidadi Waziri akitoa mada wakati wa Warsha ya maboresho ya Sera ya Ushirika






Mkurugenzi wa Mipango Ufuatiliaji na Tathmini wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC) Bw. Buji Bampembuye amesema wadau wote wa Ushirika wakitekeleza majukumu yao ya Kiushirika kupitia dira na mwelekeo wa Sera ya Ushirika, ni dhahiri kwamba Sekta ya Ushirika itakuwa na mabadiliko chanya na yenye tija kwa wananchi.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Warsha ya kujadili maboresho ya Sera ya Ushirika (2002) iliyoanza Jumanne 28 Januari, 2020 hadi 29 Januari 2020, Mkoani Morogoro.

“Ushirika ni moja ya nyenzo muhimu inayoweza kutumika nchini katika kuondoa umaskini na kuondokana na uchumi tegemezi. Hivyo, kwa kuimarisha Sera ya Ushirika tunajiwekea misingi imara ya kuendeleza Ushirika nchini,” alisema Bw. Bampebuye

Bw. Bambebuye amesema Tanzania tunaweza kujifunza mambo mengi mazuri kutoka kwenye nchi zilizofanikiwa katika Sekta ya Ushirika pia tunaweza kutumia tafiti zetu zilizowahi kufanyika na kuingiza yatakayoongeza chachu ya ukuaji wa Sekta ya Ushirika na kupata Sera itakayokuwa ikijibu Changamoto za wakulima na Wanaushirika kwa ujumla.

Mshauri wa Kibiashara wa Shirika la Kimataifa lisilo la Kiserikali linalojishughulisha na masuala ya Ushirika nchini liitwalo AGRITERRA Bw. Mikidadi Waziri akitoa mada katika Warsha hiyo ameeleza kuwa Shirika hilo kama mdau wa Ushirika limekuwa likifanya kazi katika kuongeza msukumo wa Maendeleo katika Sekta ya Ushirika kupitia mafunzo kwa Vyama vya Ushirika ya Utawala Bora, Usimamizi wa Fedha na uhamasishaji.

Bw. Mikidadi alisema kuwa baadhi ya Changamoto zilizopo katika Sekta ya Ushirika ni pamoja na ushiriki mdogo wa vijana na wanawake hususan katika ngazi za uongozi za Vyama vya Ushirika. Hivyo, akashauri haya ni mambo ya msingi ya kuzingatiwa katika maboresho ya Sera ili kuhakikisha kuwa Sekta inakuwa endelevu na inatoa fursa za kiuchumi kwa makundi yote ya jamii zetu.

Kwa upande wake Mjumbe wa Bodi ya Chama Kikuu cha Ushirika wa Akiba na Mikopo Tanzania (SCCULT) Bi. Anna Lupiano amesema uboreshaji wa Sera ya Ushirika unatoa matazamio ya kupata utendaji na utekelezaji wa majukumu utakaoenda kujibu changamoto mbalimbali za Sekta ya Ushirika.

Bi. Lupiano ametoa wito kwa Viongozi na Watendaji wa Vyama vya Ushirika kufuata na kutekeleza matakwa ya Sera mpya itakapokuwa tayari katika hatua za utekelezaji ili kuboresha na kuhakikisha uendelevu wa Vyama vya Ushirika.

WATEJA WA BENKI YA CRDB WAFURAHIA PUNGUZO LA ASILIMIA 10 TIPS BEACH KIDIMBWI

$
0
0
Januari 26, 2020 wateja wa Benki ya CRDB walifurahia kupata punguzo la asilimia kumi kwa malipo yao katika Mgahawa maarufu wa Tips Beach Kidimbwi iliyopo Mbezi Beach Dar es Salaam.

Akizungumza katka mgahawa huo, Mkuu wa Kitengo cha Biashara ya Kadi wa Benki ya CRDB, Farid Seif, alisema kuwa lengo la kampeni hiyo ni kuwahamasisha wateja wa Benki hiyo kufanya malipo kwa kutumia kadi na kuachana na mfumo wa kutembea na fedha taslimu. “Pamoja na punguzo la asilimia kumi kwa malipo yao, wateja wetu pia watapata nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo fulana, vikombe na nyingine vingi.

Meneja wa  Bar ya Tips Beach Kidimbwi, Bi Joan Pascal, alisema kuwa wateja wao wamefurahia sana kampeni hiyo kwani ni mwanzo mpya wa kuachana na utamaduni wa kutumia fedha taslimu kufanya malipo.
 
Afisa Mauzo wa Benki ya CRDB, Francis Mgani (kushoto), akimkabidhi zawadi ya fulana, Patrick Michael, baada ya kufanya malipo kwa kutumia TemboCardvisa wakati wa mwendelezo wa kampeni ya “Chanja, Lipa, Sepa” ya kuhamasisha wateja wa benki hiyo kufanya malipo kwa kutumia kadi na kuachana na mfumo wa kutembea na fedha taslimu. Kampeni hiyo hiyo ilifanyika katika Mgahawa wa Beach Kidimbwi uliopo Mbezi Beach, jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
 Wakala FahariHuduma, Nasra Abdallah (kulia), akitoa huduma kwa mmoja wa watu waliofika katika Bar ya Beach Kidimbwi.
 Mteja akifungua akaunti Mpya ya Benki ya CRDB.
 Afisa wa Benki ya CRDB, Bi. Rehema, akimpa zawadi mteja wa benki hiyo baada ya kufungua akaunti Mpya wakati wa mwendelezo wa Kampeni ya “Chanja, Lipa, Sepa” ya kuhamasisha wateja wa benki hiyo kufanya malipo kwa kutumia kadi na kuachana na mfumo wa kutembea na fedha taslimu.
Mteja wa Benki ya CRDB, akifanya malipo kwa kutumia TemboCardvisa wakati wa mwendelezo wa kampeni ya ‘Chanja, Lipa, Sepa’ ya kuhamasisha wateja wa benki hiyo kufanya malipo kwa kutumia kadi na kuachana na mfumo wa kutembea na fedha taslimu, iliyofanyika Mbezi Beach jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Meneja Mahusiano na Huduma za Uwakala CRDB, Fadhil Mollel.

WAZIRI JAFO AZINDUA JENGO LA OFISI ZA ALAT, AWAPONGEZA KUHAMIA MAKAO MAKUU

$
0
0
Charles James, Michuzi TV

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Selemani Jafo ameipongeza Jumuiya ya Tawala za Mitaa nchini (ALAT) kwa kufanikiwa kujenga jengo la Ofisi zao jijini Dodoma.

Mhe Jafo ametoa pongezi hizo leo jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa ofisi za Jumuiya hiyo na kusema wametii kwa vitendo agizo la Rais Dk John Magufuli la kuifanya Dodoma kuwa Makao Makuu ya Nchi.

Jengo hilo ambalo lilianza kujengwa Septemba 2018 limekamilika tayari kwa kuanza kutumika ambapo limegharimu kiasi cha Shilingi Milioni 121.3 ambazo ni fedha za ndani.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Waziri Jafo ameupongeza uongozi wa ALAT kwa ujenzi huo ambao umeacha historia kwani kabla ya hapo Jumuiya hiyo haikuwahi kumiliki ofisi zao wenyewe na badala yake walikua wamepanga.

" Nimeridhika na ujenzi wa jengo hili, hakika ni mzuri na thamani ya fedha imeonekana, Viongozi mliopo mtakumbukwa kwa hili ambalo mmelifanya. Mmefanya jambo la kihistoria na hii ndio maana ya uongozi ni alama.

Kwa muda mrefu ALAT ilikua ni kichaka cha watu kunufaisha matumbo yao lakini chini ya Mwenyekiti Gullamal Mukadam hata zile Halmashauri zilizokua haziipendi ALAT zitaanza kutoa michango bila kunung'unika," Amesema Mhe Jafo.

Ameipongeza Jumuiya hiyo kwa namna ambavyo imekua ikisimamia miradi ya serikali za mitaa na kuahidi kuwa serikali itaendelea kushirikiana nao katika miradi mbalimbali ambayo imekua ikitekelezwa.

" Serikali za mitaa ndio utu wa mgongo wa Nchi yetu, tutaendelea kupeleka miradi mbalimbali ya kimaendeleo haswa kwenye afya na elimu na tunaamini hatua kubwa za kimaendeleo ya kiuchumi itapigwa kwa ushirikiano uliopo baina ya serikali na ALAT," Amesema Mhe Jafo.

Pia Waziri Jafo amezitaka Halmashauri zote nchini zinazodaiwa na Mabenki mikopo iliyokopwa na madiwani ziyalipe madeni hayo mara moja ili kuepusha Mabenki hayo kuzuia viinua mgongo vya madiwani pindi watakapomaliza muda wao.

" Nafahamu kuna halmashauri hazijalipa madeni ya madiwani wanayodaiwa benki baada ya madiwani wetu kukopa wakitegemea watakuwa wanakatwa kwenye posho zao za kila mwezi.

Ninawaagiza wakurugenzi wa halmashauri zote zinazodaiwa zikiongozwa na halmashauri ya Gairo kulipa madeni hayo mara moja ili kuondoa usumbufu wa kuzuiliwa viinua mgongo vyao madiwani wetu hawa," Amesema Mhe Jafo.

Awali akisoma taarifa ya ujenzi wa jengo hilo, Katibu Mkuu wa ALAT, Elirehema Kaaya amesema kukamilika kwa ujenzi wa jengo lao hilo kutaokoa kiasi cha Sh Milioni Tano kila mwezi walichokua wakitumia kama pango kwenye ofisi zao zilizopo jijini Dar es Salaam.

" Mhe Waziri ujenzi umetumia takribani miaka miwili na tulijenga kwa fedha zetu wenyewe ambapo kiwanja pia kilikua ni chetu na mhandisi ni kutoka Jiji la Dodoma," Amesema Kaaya.

Nae Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Mhe Gulamal Mukadam amesema malengo yao ni kujenga jengo refu la kitega uchumi ambalo litaongezea kipato kikubwa kitakachowawezesha kuzidi kujiendesha wenyewe.

" Tunaipongeza serikali ya awamu ya tano kwa miradi makubwa ya kimaendeleo inayotekelezwa kwenye serikali za mitaa hasa kwenye sekta ya Elimu, afya na miundombinu.

Lengo letu baada ya kukamilika kwa ujenzi huu ni kujenga jengo kubwa la kitega uchumi ili kuendana na Sera ya Rais Magufuli ya kukuza uchumi ambapo tunaamini licha ya kutupatia fedha nyingi litakua msaada pia kwa halmashauri zetu," Amesema Mukadam.
Muonekano wa Jengo la Ofisi za Jumuiya ya Tawala za Mitaa lililozinduliwa leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Selemani Jafo jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Selemani Jafo (katikati) akizindua jengo la ofisi za Jumuiya ya Tawala za Mitaa (ALAT) leo jijini Dodoma. Kulia ni Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Gullam Mukadam.
Mwenyekiti wa ALAT, Gullam Mukadam akizungumza wakati wa uzinduzi wa jengo la ofisi ya Jumuiya hiyo jijini Dodoma.

Wadau mbalimbali wa ALAT wakifuatilia uzinduzi wa jengo la ofisi za Makao Makuu ya Jumuiya hiyo jijini Dodoma leo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Selemani Jafo akizungumza wakati wa uzinduzi wa jengo la Ofisi za ALAT jijini Dodoma Leo.
Katibu Mkuu wa ALAT, Elirehema Kaaya akisoma taarifa ya jengo hilo mbele ya mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Selemani Jafo (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa jengo la Ofisi za ALAT jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Selemani Jafo akiwa na viongozi wa serikali na ALAT wakati wa uzinduzi wa jengo la Ofisi za Jumuiya hiyo.

MRADI WA KUJENGEA UWEZO WATAALAM NA WAKULIMA KATIKA KILIMO CHA AUMWAGILIAJI WAFANIKIWA KWA KIASI KIKUBWA. DODOMA

$
0
0


Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Marco Ndonde akifungua mkutano wa majadiliano ya wadau kuhusu mradi wa mafunzo na matunzo wa skimu za kilimo cha Umwagiliaji. Uliyofanyika Jijini Dodoma.
Bw. Ukombeso Emmanuel Afisa Kilimo kutoka Manyara akiongea na waandishi wa Habari hawapo katika Picha kuhusu faida iliyopatikana kutokana na mradi wa mafunzo na matunzo wa skimu za kilimo cha Umwagiliaji, katika Mkutano wa wadau uliofanyika Jijini Dodoma leo.
Katika Picha ni sehemu ya Washiriki katika majadiliano ya kubadilishana mawazo kuhusu mradi wa mafunzo na matunzo wa skimu za kilimo cha Umwagiliaji. Iliyofanyika Jijini Dodoma.


Imeelezwa kuwa , Mradi wa kujengea uwezo kwa wakulima na wataalamu katika Kilimo cha Umwagiliaji nchini umefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupitia matumizi ya muongozo yakinifu wa umwagiliaji na Mafunzo ya uendeshaji na matunzo ya skimu za umwagiliaji katika maeneo ya mfano yaliyo chaguliwa na mradi huo.

Hayo yamelezwa Leo Jijini Dodoma na kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Marco Ndonde alipofungua warsha ya wadau na wataalam ya kubadilishana malengo na mbinu zitakazotumiwa kufanya mafanikio ya mradi kuwa endelevu ili kuwezesha ukuzaji wa sekta ya umwagiliaji kote nchini. .

Bw. Ndonde amesema kuwa, mradi huo umekuwa wa mafanikio kwa kiasi kikubwa kutokana na wadau wa kilimo hicho kutumia mwongozo wa umwagiliaji kwa umakini katika kutekeleza shughuli zote za kilimo cha Umwagiliaji.

Akiongea katika Warsha hiyo, Afisa Kilimo kutoka Ofisi za Kilimo cha umwagiliaji Manyara Bw. Lukombeso Emmanuel, amesema Serikali imefanya uwekezaji mkubwa katika eneo la umwagiliaji kupitia Mradi huo jambo ambalo limewawezesha wakulima wenyewe kuweza kupata uelewa hususan katika eneo la matunzo ya miundombinu ya umwagiliaji jambo ambalo awali muamko ulikuwa mdogo.

“Kwa upande wetu sisi kama wataalam katika ngazi zote tumejengewa uwezo juu ya uibuaji, , utekekelezaji, uendeshaji na mafunzo pamoja na ufuatiliaji na tathmin kwa kufuata mwongozoyakinifu wa Umwagiliaji na namna ya kuwawezesha wakulima kufanya shughuli zao kufuata Mwongozo huo.” Alisisitiza Bwana Lukumbeso

Pamoja na mafanikio hayo mradi umekuwa na changamoto mbalimbali kwa wakulima kama vile uelewa mdogo kuhusu Sheria, kanuni na Miongozo ya Kilimo cha Umwagiliaji jambo ambalo linatafutiwa ufumbuzi wa kudumu kupitia kuitambulisha rasmi Sheria ya Umwagiliaji kwa wadau mbalimbali na kutoa elimu kwa umma kupitia vyombo vya habari.

Awamu hiyo ya pili ya mradi wa kujengea uwezo wakulima katika Kilimo cha Umwagiliaji unafadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) kwa kushirikiana na Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji.

Pizza Hut na KFC Yafungua mgahawa wa 14 nchini

$
0
0
Pizza Hut Tanzania, imemaliza mwaka 2019 kwa kishindo,kwa kufungua mgahawa wa 8 nchini uliopo katika jengo la Mikocheni Plaza, ambao ulifunguliwa rasmi katika mkesha wa mwaka mpya ikiwa ni wa pili kufunguliwa katika mwezi huo ambapo pia imefungua mgawaha mpya wenye viwago vya kimataifa katika uwanja mpya wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere International Airport (JNIA), Desemba 16, 2019.

Mtandao wa migahawa mingine ya Pizza Hut ipo katika maeneo ya Mlimani City, Oysterbay Mall, Mkuki House, Shoppers Plaza, Peugot House na  mjini Arusha katika eneo la maduka ya TFA .

Kampuni ya Dough Works Ltd, ambayo  inamiliki mtandao wa migahawa hiyo inafurahi kufungua mgahawa wa 8 nchini Tanzania na pia inajivunia kupitia uwekezaji huo kuweza kuzalisha ajira zaidi ya 400 “Tunayo furaha kuona biashara yetu inazidi kukua na kuwafikia wananchi wengi na bidhaa zetu za Pizza, zenye viwango vya kimataifa kuzidi kufurahiwa na wateja wetu”. alisema Vikram Desai, Mkurugenzi Mkuu katika hafla ya uzinduzi wa mgahawa mpya wa Pizza Hut wa Mikocheni Plaza iliohudhuriwa na wadau mbalimbali ikiwemo wafanyakazi wa kampuni hiyo.

Mbali na kusherekea kufungua migahawa mipya ya Pizza Hut, Kampuni ya Dough Works Ltd, kwa sasa inaendesha  mtandao wa migahawa 4 ya KFC kuanzia Oktoba 3,mwaka jana.Katika kipindi cha miezi 3 mtandao wa migahawa ya KFC umezidi kukua na kuwa na migahawa 6 baada ya kufunguliwa migahawa mipya miwili mwezi Desemba mwaka jana.Kwa sasa migahawa ya KFC iko katika maeneo ya Kariakoo,Jengo la Diamond Plaza,Mlimani City,Uwanja wa ndege mpya wa JNIA na Mikocheni Plaza, Kampuni inao mpango wa kupanua huduma zake Zaidi kufikia maeneo mengine il ziwafikia wananchi wengi kwa karibu.

Mtandao wa migahawa ipatayo 14 ya KFC na Pizza Hut, inahudumia zaidi ya watu 1,000 ambao hufika kupata chakula pia inatoa huduma za kusambaza chakula chake maarufu cha Pizza na kuku maofisini mpaka majumbani na kampuni imejipanga kupanua huduma zake katika mikoa mbalimbali ikiwemo katika  mikoa ya Dodoma, Arusha na Mwanza. 

Kampuni pia inayo sera ya kusaidia huduma za kijamii kupitia sera yake ya kurudisha sehemu ya faida yake kwa jamii ambapo mwaka huu imepanga kutekeleza miradi mbalimbali ya kusaidia jamii nchini.

Mkurugenzi wa Dough Works Ltd,Vikram Desai alisema “Tunayo furaha kubwa kuona mtandao wetu  umefungua migahawa 4 katika kipindi kifupi na kuwawezesha wateja wetu kupata huduma zetu kwa urahisi,tutaendelea kupanua huduma zetu katika mikoa mingine na matarajio yetu hadi kufikia mwisho wa mwaka huu tuwe tumefungua mtandao wa migahawa yetu katika miji ya Dodoma na Mwanza ambayo itawezesha watanzania wapatao 250 kupata ajira”,alisema.

Kufunguliwa kwa migahawa ya kisasa ya Pizza Hut&KFC katika eneo moja katika jengo la Mikocheni Plaza, kunatoa fursa kwa wateja kupata huduma bora za chakula hususani Pizza na nyama ya kuku zinazotolewa na migahawa hiyo,inao ukubwa wa eneo la kutosha kuhudumia wateja 90 kwa wakati mmoja,menu za chakula za kidigitali,sehemu nzuri na salama za watoto kuchezea, na mazingira rafiki ya kukutana kwa chakula cha kifamilia na mijumuiko ya sherehe ndogondogo.

Pia migahawa hiyo inauza vyakula mbalimbali vya kuku waliotengenezwa kwa viwango vya kimataifa kwa gharama nafuu ambayo wananchi wengi wanaweza kumudu kuanzia  kati ya shilingi 7500/ -shilingi 10,000 kiwemo vinywaji vya soda.
 Meneja Mkuu wa Migahawa ya kuuza Pizza Hut Afrika ya KFC,  Ewan Davenport (katikati)  akikata utepe  wakati wa uzinduzi wa mgahawa wa kuuza Pizza  Hut ulioipo katika jengo la Mikocheni Plazza jijini Dar es Salaam, Kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Dough Works LimIted ,Vikram Desai ( kulia)  na Meneja  wa Mgahawa wa Pizza Hut  Mikocheni Emmanuel Sizya.
 Meneja Mkuu wa Migahawa ya kuuza Pizza Hut Afrika ya KFC,  Ewan Davenport (katikati)  akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo, Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Dough Works Limeted ,Vikram Desai ( Kushoto) na Meneja  wa Mgahawa wa Pizza Hut  Mikocheni Emmanuel Sizya.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Dough Works Limited ,Vikram Desai (kulia) akiongea  kwa wandishi wa Habari hawapo pichani wakati wa hafla ya uzinduzi wa  Mgahawa w Pizza Hut  na KFC uliopo katika jengo la Mikocheni  Plaza jijini Dar es Salaam. Wapili kutoka kulia ni   Meneja Mkuu wa Migahawa ya  Pizza Hut Afrika , Ewan Davenport 

SBL yazindua mpango wa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wa kilimo

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Mark Ocitti (kushoto) akifurahia jambo na Mkuu wa Chuo cha Kaole Wazazi College of Agriculture muda mfupi kabla ya kusaini utakayoiwezesha SBL kutoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wa klimo wa chuo hicho.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Mark Ocitti (kushoto) akibadishana mkataba na Mkuu wa Chuo cha Kaole Wazazi College of Agriculture muda mfupi baada ya kusaini mkataba huo utakaiwezesha SBL kutoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wa kilimo wa chuo hicho kila mwaka

Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha Kaole Wazazi College of Agriculture watakaonufaika na mpango wa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wa kilimo unaotolewa na Kampuni ya Bia ya Serengeri, wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Mark Ocitti (kushoto) na mkuu wa chuo hicho Sinani Simba muda mfupi baada ya kusaini mkataba wa ufadhili.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Mark Ocitti (kulia) akimpongeza mmoja wa wanafunzi wa Chuo cha Kaole Wazazi College of Agriculture ambaye ni mnufaika wa programu ya ufadhili wa elimu kwa wanafunzi wa kilimo Emmanuel Ntandu muda mfupi
baada ya SBL kusaini mkata wa ufadhili na chuo hicho mjini Bagamoyo jana. 

****************************** 

Bagamoyo, January 29, 2020: Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), leo imezindua mpango wa ufadhili wa masomo utakaowanufaisha wanafunzi 30 kutoka katika jamii za wakulima hapa nchini kupata elimu ya ngazi ya chuo katika vyuo vya ndani vinavyofundisha masomo ya kilimo. 

Ukijulikana kama Kilimo-Viwanda scholarship program, mpango huu unalenga kuongeza wataalamu wa kilimo watakaowasaidia wakulima nchini kuongeza uzalishaji, alisema Mkurugenzi Mtendaji wa SBL, Mark Ocitti wakati wa uzinduzi wa program hiyo katika chuo cha Kaole Wazazi College of Agriculture kilichopo Bagamoyo mkoani Pwani. 

“Ni muhimu kwetu sisi kama SBL kuiunga mkono Serikali katika kuwajengea uwezo wakulimawetu kupitia kuwaongezea wataalamu wa kilimo watakaosadia kuwashauri na hivyo kuongezatija katika kilimo,” alisema Ocitti. 

Chuo cha Kaole Wazazi College of Agriculture ni moja kati ya vyuo vitatu ambavyo kampuni ya SBL inashirikiana navyo katika kutoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wa kilimo hapa nchini. 

Mkurugenzi huyo alifafanua kuwa, programu hiyo inawalenga siyo tu wanafunzi wanaotokakatika familia zenye vipato duni lakini pia wanafunzi wanaotoka katika jamii za wakulima katikasehemu mbali mbali hapa nchini. Kila chuo kitapata nafasi ya kutoa wanafunzi 10 kila mwaka na
watakaolipiwa ada na SBL mpaka watakapomaliza masomo yao. 

Kwa mujibu wa Ocitti, programu hiyo ni sehemu ya mkakati wa SBL wa kuongeza kiasi cha nafaka ambacho kampuni hiyo inanunua kwa ajili ya uzalishaji wa bia ambazo ni pamoja na mahindi, shayiri na mtama. Alisema, mwaka jana SBL ilinunua zaidi ya tani za ujazo 17,000 zanafaka kutoka kwa wakulima wa ndani sawa na asilimia 70 ya mahitaji yake yote ya malighafi kwa mwaka. 

“Kampuni ya SBL inalengo la kuongeza kiasi cha malighafi inayonunua kutoka kwa wakulima wa ndani hadi asilimia 85 kufikia mwaka 2020 na ndiyo maana tumeona umuhimu wa kusaidia kusomesha wataalamu wa kilimo ili wakafanye kazi ya kuboresha kilimo chetu. Kwa sasa
kampuni inanunua malighafi kutoka kwenye mtandao wenye wakulima 400 hapa nchini,”.alisema. 

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Kaole Wazazi College of Agriculture Sinani Simba aliishukuru kampuni ya SBL kwa kuja na wazo la kutoa ufadhili wa masomo ya kilimo na kuongeza kuwa ili kilimo kiwe cha tija wataalamu wengi wanahitajika. 

“Tunayo Furaha kwa kuwa ufadhili huu unawalenga wanafunzi wanaotokea katika familia zenyevipato duni ambao kama siyo msaada wa SBL, wasingeweza kupata fursa ya kuendelea namasomo,” alisema

TMDA YAKAGUA SHEHENA 3160 ZA DAWA ,VIFAA TIBA NA VITENDANISHI

$
0
0


Kaimu Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Proches Patrick akizungumza na waandishi wa habari pamoja na Timu ya Maafisa Habari wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto walipotembelea Mamlaka hiyo kuangalia mafanikio ya miaka minne ya serikali ya awamu ya tano ikiwa Kampeni ya Tumeboresha sekta ya Afya iliyoratibiwa na Maafisa habari wa Taasisi 17 zilizo chini ya Wizara.


Mkuu wa Msafara na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Gerald Chami akitoa maelezo kuhusiana na kampeni ya Tumeboresha sekta ya Afya kwa kuangalia mafanikio ya miaka minne ya serikali ya awamu ya tano.
Meneja wa Mawasiliano na Elimu kwa Umma Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Gaudensia Simwanza akitoa akizungumza kuhusiana na mamlaka hiyo namna inavyofanya kazi za udhibiti wa dawa nchini
Mkaguzi wa Dawa wa Kanda ya Kaskazini wa (TMDA) Titus Malulu akitoa maelezo kuhusiana na wanavyofatilia dawa zikiwa sokoni kwa kutumia maabara hamishika.
Meneja wa Mawasiliano na Elimu kwa Umma Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Gaudensia Simwanza akionesha maabara hamishika ambayo wanaweza kukagua dawa sehemu yeyote.
Picha ya pamoja ya Kaimu Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Proches Patrick na waandishi wa habari pamoja na Timu ya Maafisa Habari wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto walipotembelea Mamlaka hiyo kuangalia mafanikio ya miaka minne ya serikali ya awamu ya tano ikiwa Kampeni ya Tumeboresha sekta ya Afya iliyoratibiwa na Maafisa habari wa Taasisi 17 zilizo chini ya Wizara.
 
Na Chalila Kibuda,Michuzi Blog, Arusha

Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Kanda ya Kaskazini imesema katika kipindi cha miaka minne ya Rais Dk.John Magufuli imefanikiwa kukagua shehena 3,160 za dawa, vifaa tiba, vitendanishi kupitia vituo vya forodha vya Namanga, ,Holili ,Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro pamoja na Tarakea.

Hayo yalielezwa jana na Kaimu Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa Mamlaka hiyo Proches Patrick amesema kuwa katika ukaguzi huo ni mafanikio kwao kwani kunafanya dawa,vifaa tiba na vitandanishi kuwa salama na bora kwa kulinda afya za watumiaji

Patrick amesema katika utendaji wao wa kazi wamechunguza ubora,Usalama na ufanisi wa sampuli 243 za dawa, vifaa tiba na vitendanishi huku maeneo 5,531 yanayojihusisha na biashara za dawa ,vifaa tiba na vitendanishi vimekaguliwa pamoja na watendaji wa vituo vya afya 152 wamepatiwa mafanzo ya utoaji wa taarifa za madhara yatokanayo na matumizi ya dawa na vifaa tiba.

Amesema kwa kazi zote zilizofanyika ni mafanikio kwa kanda ya Kaskazini TMDA imefanikiwa kufanya kazi kwa kwa kutumia mfumo wa Kieletroniki unaowezesha utoaji wa huduma huduma ndani ya siku moja.

Patrick kuwa wakati walipokuwa hawana mifumu huo walikuwa wanatumia siku tatu kwa wanaohitaji kibali kusafiri na kufika katika ofisi za TMDA.

Patrick amesema kuwa licha ya kutoa vibali vya waingizaji dawa lakini wanafatilia dawa hizo katika soko ili kujiridhisha dawa zinazotumika ni zile zilizopewa kibali na mamlaka hiyo.

“TMDA ipo kulinda afya za wananchi kuhakikisha dawa wanzotumia zina ubora na ikitokea kuleta madha kwa wananchi dawa hiyo inaondoka katika soko mara moja”amesema Patrick

Patrick amesema kuwa TMDA baada ya kutoa vibali vya uingizaji dawa huwa wanafanya utafiti wa dawa hizo katika kuhakikisha wananchi wanapata dawa zenye ubora.

Hata hivyo amesema katika mikakati hiyo kwa kanda ya kaslazini wameweza kusajili kiwanda cha dawa za mifugo ambacho kitaanza hivi karibuni.
 
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>