Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1894 | 1895 | (Page 1896) | 1897 | 1898 | .... | 1904 | newer

  0 0

  Benki ya Exim Tanzania imetoa msaada wa taulo za kike kwa wanafunzi wa kike zaidi ya 2,400 wa Shule za Sekondari na Msingi zilizopo Mkoani Shinyanga.

  Shule hizo ni pamoja na Shule ya Sekondari ya Kiislamu Istiqaama, Shule ya Msingi Mwenge, Shule ya Msingi Mapinduzi, Shule ya Msingi Jomu, Shule ya Msingi Ibadhi pamoja na Kituo cha Agape aids control Programme zilizopo mkoani humo.

  Akizungumza wakati wa akikabidhi msaada huo mwishoni mwa wiki, Meneja wa Benki hiyo tawi la Shinyanga, Bi Sarah Paul alisema hatua hiyo ni muendelezo wa mpango wa uwajibikaji wa kwa jamii (CSR) wa benki hiyo unafahamika kama Exim Cares.

  Alisema benki hiyo imekuja na mpango huo ili kusaidia wanafunzi wa kike kwa kuwapatia hitaji hilo muhimu kiafya sambamba na kutoa elimu kuhusu hedhi salama kwa wanafunzi wa kike pindi wakiwa shuleni.

  Kwa mujibu wa Bi Sarah, kupitia mpango huo, benki hiyo inatarajia kutoa misaada mingine kama hiyo kwa shule kadhaa katika mikoa mingine ikiwemo Tabora na Iringa.

  "Benki ya Exim inafarijika sana kuwa sehemu ya agenda muhimu za kijamii na hiyo ni moja ya imani yetu, kwa hiyo tumeamua kuja na mpango wa kusaidia mtoto wa kike na ili kuhakikisha kwamba msaada huu unakuwa na tija zaidi taulo hizi tulizotoa zinaweza kutumika zaidi ya mara moja na itawasaaidia zaidi wahusika,’’ alisema.

  Kwa mujibu wa ripoti ya UNESCO inakadiriwa kuwa msichana mmoja kati ya kumi katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara anakosa kwenda shule wakati wa mzunguko wa hedhi.

  Aidha katika baadhi ya tamaduni suala la hedhi linapewa tafsiri potofu zaidi na hivyo kuongeza changamoto kwa watoto wa kike na hivyo kuathiri maudhulio yao mashuleni na hatimaye kuathiri taaluma zao.

  "Benki ya Exim imejitolea kikamilifu kuhakikisha kuwa vijana wa Kitanzania wanapata elimu, licha ya changamoto zinazowakabili na hili tutalifanikisha kwa kuhakikisha tunakuwa sehemu ya kuwasaidia kuzitatua changamoto hizo na utoaji wa taulo hizi ni sehemu ya mkakati wa kukamilisha adhima hiyo,’’ alisema.

  Akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo, Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Istiqaama Bw Mbaraka Songoro alisema msaada huo kutoka benki ya Exim si tu unaonyesha utu bali pia ni unaonyesha heshima kwa watoto wa kike.

  "Sisi kama shule tunaona hii kama heshima kubwa kwa wapokeaji wa msaada huu na kwa jamii kwa ujumla. Misaada ya namna hii inaonesha namna watu na taasisi makini kama Benki ya Exim zinavyowachukulia watoto wa kike…tunashukuru sana '' Alisema

  Akitoa neno la shukrani kwa benki hiyo kwa niaba ya wanafunzi wenzie, Mwananfunzi Fathihiya Faiz, kidato cha tatu .kutoka Shule ya Sekondari Istiqaama.alisema mbali na uhitaji walio nao kwa bidhaa hiyo muhimu pia wameupokea msaada huo kama ishara ya upendo na heshima kutoka kwa benki hiyo hatua ambayo itawafanya wasome wakitambua kuwa zipo taasisi na watanzania wanaowajali na kutambua changamoto za kijinsia wanazopitia.

  "Kwa msaada huu tunaamini hatutakabiliwa tena na magonjwa ambayo yanaweza kutokea kwa ukosefu wa taulo za hedhi. Pia msaada huu utaziba pengo ambalo wazazi wetu hawawezi kuliziba kwa sababu ya changamoto kadhaa zinazowakabili zikiwezo za kiuchumi,’’ alisema.
   Wafanyakazi wa Benki ya Exim tawi la Shinyanga, wakiongozwa na Meneja wa Tawi hilo Bi Sarah Paul (wa pili kushoto) wakiwa kwenye picha ya pamopa na walimu pamoja na wanafunzi wa Kituo cha Agape aids control Programme kilichopo Mkoani Shinyanga baada ya kukabidhi msaadawa taulo za kike kwa wanafunzi hao kituo hicho mwishoni mwa wiki.
   Wafanyakazi wa Benki ya Exim tawi la Shinyanga, wakiongozwa na Meneja wa Tawi hilo Bi Sarah Paul wakiwa kwenye picha ya pamopa na walimu pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kiislamu Istiqaama iliyopo Mkoani Shinyanga baada ya kukabidhi msaadawa taulo za kike kwa wanafunzi hao mwishoni mwa wiki.

   Wafanyakazi wa Benki ya Exim tawi la Shinyanga, wakiongozwa na Meneja wa Tawi hilo Bi Sarah Paul (katikati) wakiwa kwenye picha ya pamoja na walimu pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mapinduzi iliyopo Mkoani Shinyanga baada ya kukabidhi msaadawa taulo za kike kwa wanafunzi hao.Kupitia mpango wake wa uwajibikaji wa kwa jamii (CSR) unaofahamika kama Exim Cares,  benki hiyo iliweza kutoa msaada taulo hizo kwenye shule sita zikiwemo za Msingi na Sekondari mkoani humo,mwishoni mwa wiki
   Ofisa Mauzo wa Benki ya Exim tawi la Shinyanga, Bi Stella Malebetoh (Kulia) akifurahi pamoja na baadhi ya wanafunzi wa kike wa Shule ya Sekondari ya Kiislamu Istiqaama iliyopo Mkoani Shinyanga baada ya kukabidhi msaada wa taulo za kike kwa wanafunzi hao. Kupitia mpango wake wa uwajibikaji wa kwa jamii (CSR) wa benki hiyo unafahamika kama Exim Cares, iliweza kutoa msaada taulo hizo kwenye shule sita zikiwemo za Msingi na Sekondari mkoani humo mwishoni mwa wiki.
  Meneja wa Benki ya Exim tawi la Shinyanga, Bi Sarah Paul (Kushoto) akikabidhi msaada wa taulo za kike kwa walimu wa Shule ya Sekondari ya Kiislamu Istiqaama iliyopo Mkoani Shinyanga ikiwa ni msaada wa benki hiyo kwa wanafunzi wa kike wanaosoma shule hiyo. Kupitia mpango wake wa uwajibikaji wa kwa jamii (CSR) unaofahamika kama Exim Cares,  benki hiyo iliweza kutoa msaada taulo hizo kwenye shule sita zikiwemo za Msingi na Sekondari mkoani humo,mwishoni mwa wiki.

  0 0


  Meneja Chapa na Mawasiliano wa NBC, David Raymond (kulia), akizungumza na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika hafla ya kuchangisha fedha kwa njia ya vichekesho na burudani iitwayo ‘Cheka Nisome’ iliyodhaminiwa na NBC yenye lengo la kuwasaidia wanafunzi wanaoshindwa kuendelea na masomo kutokana na kushindwa kumudu gharama za ada. Hafla hiyo ilifanyika chuoni hapo jijini Dar es Salaam juzi. Hafla hii iliratibiwa na Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ( DARUSO ).
  Baadhi ya wahudhuriaji wakishangilia moja ya onesho lililokuwa likifanywa na mmoja wa wachekeshaji mahiri kutoka Kenya, Erick Omondi katika hafla iliyoandaliwa mwishoni mwa juma lililopita na Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ( DARUSO ) na kudhaminiwa na Benki ya NBC yenye lengo la kuwasaidia wanafunzi wanaoshindwa kuendelea na masomo kutokana na kushindwa kumudu gharama za ada chuoni hapo. 


  Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Bw. Emmanuel Mapunda (katikati) akisalimiana na Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ( DARUSO ) Bw. Hamis Mussa katika hafla ya kuchangisha fedha kwa njia ya vichekesho na burudani iitwayo ‘Cheka Nisome’ iliyodhaminiwa na NBC yenye lengo la kuwasaidia wanafunzi wanaoshindwa kuendelea na masomo kutokana na kushindwa kumudu gharama za ada. . Hafla hiyo ilifanyika chuoni hapo jijini Dar es Salaam juzi. Kulia ni Meneja Chapa na Mawasiliano wa NBC Bw. David Raymond.
  Meneja Chapa na Mawasiliano wa Benki ya NBC Bw. David Raymond (kulia), akisalimiana na Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ( DARUSO ) Bw. Hamis Mussa katika hafla ya kuchangisha fedha kwa njia ya vichekesho na burudani iitwayo ‘Cheka Nisome’ iliyodhaminiwa na NBC yenye lengo la kuwasaidia wanafunzi wanaoshindwa kuendelea na masomo kutokana na kushindwa kumudu gharama za ada. Hafla hiyo ilifanyika chuoni hapo jijini Dar es Salaam juzi. Katikati ni Meneja wa NBC Tawi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Bw. Emmanuel Mapunda.  0 0

  Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa MNH-Mloganzila, Dkt. Julieth Magandi
  akikabidhiwa hati ya msaada wenye thamani ya milioni 10 uliotolewa na Benki ya NMB PLC, kulia ni Meneja wa Benki hiyo Tawi la Kibaha Bw. Hosea Lyatuu.
  Mkuu wa Idara ya Huduma za Ukunga, Afya ya Uzazi Mama na Mtoto MNH-
  Mloganzila Bi. Christina Mwandalima (kushoto) akiishukuru NMB kwa msaada huo, katikati ni Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Dkt. Mohamed Mohamed.
  Bw. Hosea Lyatuu (wa pili kulia) akizungumza na uongozi wa Hospitali ya
  Mloganzila wakati akikabidhi msaada kwa niaba ya Benki ya NMB.
  Baadhi ya viongozi wa MNH-Mloganzila wakiwa katika picha ya pamoja na
  wafanyakazi wa NMB mara baada ya kukabidhiwa msaada.
  Vitanda 10, magodoro 10 na strecha mbili zilizokabidhiwa hospitalini hapa naBenki ya NMB.

  *********************************

  Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imepokea msaada kutoka Benki ya NMBwenye thamani ya Tsh. Milioni 10 ambao unalenga kuunga mkono juhudi zaserikali za kuboresha huduma za afya nchini.

  Akikabidhi msaada kwa niaba ya Benki ya NMB PLC, Meneja wa Benki hiyo tawila Kibaha, Bw. Hosea Lyatuu ametaja msaada huo ni vitanda 10, magodoro 10pamoja na strecha mbili ambapo ameeleza kuwa NMB imekuwa ikitoa misaadakatika sekta tatu ikiwemo elimu na afya kwa lengo la kuisaidia jamii.

  “Tumeamua kutoa msaada huu katika hospitali ya Mloganzila ili kuhakikisha kuwa kuna vitanda vya kutosha kwa ajili ya kutoa huduma za afya na benki yetu hufanya hivi ikiwa ni sehemu ya kurudisha fadhila kwa jamii,” amesema Bw. Lyatuu.

  Bw. Lyatuu amefafanua kuwa wanatambua mchango unaotolewa na watoa
  huduma za afya hivyo wameamua kutoa msaada katika sekta hii ili kuhakikishajamii inapata huduma pasipo shida yoyote.

  Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa MNH-Mloganzila, Dkt. Julieth Magandi ameishukuru Benki ya NMB kwa msaada huo ambao utaongeza idadi ya vitanda vitakavyotumika kwa ajili ya kutolea huduma hospitalini hapa.

  “Tunawashukuru kwa msaada huu kwani umekuja wakati muafaka wakati hospitali hii inajikia katika kuanzisha huduma mpya hivyo tunatumaini NMB mtaendelea na juhudi hizi kwani hospitali yetu bado inahitaji msaada wenu kwa lengo la kuhudumia jamii,” amesema Dkt. Magandi.

  0 0

  Mkurugenzi wa T-Pesa, Lulu Mkudde (kulia), akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo katika hafla ya uzinduzi wa ushirikiano wa huduma za kifedha kati ya NBC na T-Pesa ambapo wateja wa NBC wataweza kutoa na kutuma pesa kutoka katika akaunti zao kupitia huduma ya simu za mkononi ya T-Pesa. Kushoto ni Mkuu wa Huduma za Kibenki Kidigitali wa Benki ya NBC, Deogratius Mosha.

  Mkurugenzi wa Huduma ya T-Pesa, Lulu Mkudde (kulia), akionyesha jinsi ya kufanya muamala wa kifedha kutoka katika akaunti ya Benki ya NBC kupitia huduma ya kifedha kupitia T-Pesa ya Kampuni ya TTCL, katika hafla ya uzinduzi wa ushirikiano wa huduma za kifedha kati ya T-Pesa na NBCambapo wateja wa NBC wataweza kutoa na kutuma pesa kutoka katika akaunti zao kupitia huduma ya simu za mkononi ya T-Pesa. Kushoto ni Mkuu wa Huduma za Kibenki Kidigitali wa NBC, Deogratius Mosha. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam leo.
  Mkuu wa Huduma za Kibenki Kidigitali wa Benki ya NBC, Deogratius Mosha (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo katika hafla ya uzinduzi wa ushirikiano wa huduma za kifedha kati ya NBC na T-Pesa ambapo wateja wa NBC wataweza kutoa na kutuma pesa kutoka katika akaunti zao kupitia huduma ya simu za mkononi ya T-Pesa. Kulia ni Mkurugenzi wa T-Pesa, Lulu Mkudde.
  Mkurugenzi wa T-Pesa, Lulu Mkudde (kulia), akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo katika hafla ya uzinduzi wa ushirikiano wa huduma za kifedha kati ya NBC na T-Pesa ambapo wateja wa NBC wataweza kutoa na kutuma pesa kutoka katika akaunti zao kupitia huduma ya simu za mkononi ya T-Pesa. Kushoto ni Mkuu wa Huduma za Kibenki Kidigitali wa Benki ya NBC, Deogratius Mosha.


  0 0


  Bw. Paul Koyi, Rais wa Shirikisho la Wenye Viwanda nchini Tanzania TCCIA akizindua tovuti maalum ya LAKE VICTORIA BASIN TOURISM EXPO 2019. ambayo itatumika kwa ajili ya washiriki wa maonesho hayo kujisajili kulia kwa ke ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TA L-VIC INVESTMENTS LIMITED Bw. Anic Kashasha na Bw. Gabriel Nderumaki Mkuu wa Chaneli ya Safari inayoonesha masuala ya utalii.
  Bw. Paul Koyi, Rais wa Shirikisho la Wenye Viwanda nchini Tanzania TCCIA akizungumza wakati wa uzinduzi wa tovuti maalum ya LAKE VICTORIA BASIN TOURISM EXPO 2019. ambayo itatumika kwa ajili ya washiriki wa maonesho hayo kujisajili katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TA L-VIC INVESTMENTS LIMITED Bw. Anic Kashasha na kushoto ni Franklin Mziray Mshauri wa masuala ya habari.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TA L-VIC INVESTMENTS LIMITED Bw. Anic Kashasha akizungumza katika uzinduzi hio katikati ni Bw. Paul Koyi, Rais wa Shirikisho la Wenye Viwanda nchini Tanzania TCCIA na kulia ni Bw. Gabriel Nderumaki Mkuu wa Chaneli ya Safari inayoonesha masuala ya utalii.
  Bw. Paul Koyi, Rais wa Shirikisho la Wenye Viwanda nchini Tanzania TCCIA akimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TA L-VIC INVESTMENTS LIMITED Bw. Anic Kashashamara baada ya kufanya uzinduzi huo.
  Bw. Paul Koyi, Rais wa Shirikisho la Wenye Viwanda nchini Tanzania TCCIA na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TA L-VIC INVESTMENTS LIMITED Bw. Anic Kashasha wakipata maelezo kutoka kwa Bw. Ali Nchahaga mratibu wa maonesho.
  ...................................................................
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TA L-VIC INVESTMENTS LIMITED Bw. Anic Kashasha amempongeza na kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Joseph Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kufungua uchumi wa utalii katika mikoa ya Kanda ya Ziwa, kufuatia kuyapandisha hadhi mapori kadhaa ya akiba na kuyafanya hifadhi za Taifa (National Parks) ambazo sasa zitaruhusu shughuli za uchumi wa utalii kushamiri katika mikoa hiyo
  Bw Kashasha amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Protea Cortyad Oysterbay jijini Dar es salaam wakati akizungumzia Uzinduzi wa tovuti ya LAKE VICTORIA BASIN TOURISM EXPO 2019 ambayo itatumika kwa ajili ya washiriki wa maonesho hayo kujisajili.

  amesema ili kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika kukuza utalii kanda ya ziwa tumeanzisha tovuti rasmi ambayo itatumika kwa wadau kujiorodhesha kwa njia ya mtandao ili kushiriki kwenye maonyesho ya utalii yatakayofanyika Kabuhara Beach, Maruku, Bukoba Vijijini mkoani Kagera kuanzia tarehe 28 Disemba hadi 30 2019, ambapo pia watahudhuria kwenye Kongamano la Utalii litakalofanyika tarehe 28 na 29 Disemba 2019 kwenye Ukumbi wa ELCT Hotel Bukoba mjini.
  Kashasha amemshukuru pia Bw. Paul Koyi, Rais wa TCCIA kwa kutenga muda wake pamoja na majukumu yake mengi na kujumuika kwake katika uzinduzi wa tovuti hiyo.

  Huu ni uthibitisho wa utayari wa uongozi mpya wa TCCIA chini ya uongozi wake, kuhakikisha taasisi hiyo inakuwa karibu zaidi na wafanyabiashara ili kuongeza ufanisi katika shughli za biashara.

  Ni muhimu sana kuliweka wazi hili kwamba Bw. Paul Koyi, Rais wa TCCIA mwenyewe akiwa ni mfanyabiashara mzoefu ni mwenye maono ya kibiashara kweli. Ninalisema hili kwa sababu tulipokutana naye na kumuelezea ni nini tunachokifanya, alituelewa haraka sana na kuahidi kutupatia ushirikiano ili kuhakikisha malengo ya mradi wa Lake Victoria Basin Tourism Expo yanafanikiwa.

  Aidha, alikubali mara moja kupokea ombi letu la kushirikiana pamoja na TCCIA kwenye mradi wa muda wa kati ambapo tutajikita katika kufanya shughuli za kusisimua utalii wa ndani na utalii wa kikanda (Intra-EAC Tourism).
  Ameongeza kuwa jambo hili linatarajiwa kufanyika kwa kuitumia rasilimali kubwa ya maji ya Ziwa Viktoria ambapo Bonde lake ni mali ya asili inayomilikiwa na nchi 5 kati ya 6 zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki.
  Mkakati huu utatekelezwa kwa kuishirikisha kampuni ya Marine Services Company Limited (MSCL), inayomiliki meli na kuendesha shughuli za usafirishaji wa abiria na mizigo ikiwa na meli 15 ambapo meli 9 kati ya hizo zimo na zinafanya kazi ndani ya Ziwa Viktoria.
  Hivyo tunatarajia kuwekeana saini makubaliano ya kushirikiana (MOU) na Tanzania Chamber of Commerce Industry and Agriculture (TCCIA) ambayo itatuongoza kuingia kwenye ushirikiano wa kufanya kazi pamoja na East African Business Council (EABC) kwenye mradi wa kusisimua na kukuza utalii wa kikanda (Intra-EAC Tourism).
  Amesema kuwa wameshaanzisha mchakato wa kuzishirikisha Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Wizara ya Maliasili na Utalii, Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na taasisi yake ya Lake Victoria Basin Commission, Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na TradeMark East Africa.
  Amemaliza na kusema mradi huu utakuwa na manufaa makubwa kwa kukuza utalii lakini pia kuongeza kasi ya mashirikiano baina ya wananchi wa nchi wana chama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

  0 0

   Wenyeji wa Mkoa wa Kilimanjaro watakaoenda likizo mwaka huu kwa msimu wa sikukukuu wameandaliwa burudani mbalimbali kwenye Tamasha  kubwa linalotarajiwa kufanyika  tarehe 22 Disemba 2019 kwenye Viwanja vya Chuo cha Ushirika Moshi.
  Tamasha hilo linalojulikana kama ‘Twenzetu Kilimanjaro Fest’ 2019 limendaliwa na Kampuni ya Real PR Solutions ya jijini Dar es Salaam.
  Akizungumzia Tamasha hilo ambalo linatarajiwa kuzinduliwa rasmi hivi karibuni, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo Bw Clement Mshana amesema ni sehemu ya mkakati wa kufanikisha Mpango wa Kuendeleza Utalii wa Ndani (Domestic Tourism Promotion Initiative (DTPI) unaotarajiwa kufanyika mikoa mbalimbali nchi nzima kwa kuanza  na Mkoa wa Kilimanjaro.
  “Tamasha hili la Twenzetu Kilimanjaro Fest  linatarajiwa kupambwa na matukio kadhaa ya burudani zikiwemo, Mbio za kujifurahisha za Capital Mountain Run zitakazohusisha Km 5, Km 10 pamoja na mbio za watoto za Km 3 na Mbio za Baiskeli za KM 60, Maonesho ya Utalii na Biashara, Burudani na viburudisho mbalimbali ikiwemo michezo ya watoto, vyakula vya asili na muziki.’’ Alitaja.
  Alisema katika Mkoa wa Kilimanjaro Tamasha hilo hasa litahusisha agenda kuu tatu ambazo ni pamoja na kutangaza Utalii wa ndani, upandaji wa miti  pamoja na kuhamasisha uwekezaji wa viwanda katika mkoa huo.
  Aidha katika mkakati wake wa kufanikisha agenda hizo, kampuni hiyo ya Real Pr Solutions imeandaa matukio kadhaa ya kijamii ili kuunganisha wadau mbalimbali wa mkoa huo kama utembeleaji wa vivutio mbalimbali vya Utalii vilivyopo mkoani Kilimanjaro ikiwemo, Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi na maporomoko mbalimbali ya maji yaliyopo mkoani humo.
  “Tutukio hili la  utembeleaji wa vivutio na upandaji miti linatarajiwa kufanyika Disemba 21, 2019 yaani siku moja kabla ya Tamasha,’’ alisema huku akitaja tukio jingine kuwa ni upandaji wa miti zoezi ambalo litatekelezwa kwa uratibu wa pamoja na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) likihusisha wadau mbalimbali ikiwemo mashirika na taasisi za umma ikiwemo shule na vyuo mbalimbali mkoani Kilimanjaro.
  Mbali na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS)aliwataja baadhi ya wadau muhimu katika ufanikisha tamasha hilo kuwa ni pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na  Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).
  “ Wengine ni pamoja na Kampuni ya Ujenzi ya CRJE (East Africa) Limited, HAL, Kilimanjaro Wonders Hotel, Nyumbani Hotels na Afrimax Strategic Partnerships.”
   “Kwa niaba ya kamati ya maandalizi ya Tamasha hili ninawaomba sana wadau mbalimbali wajitokeze kutuunga mkono ili tuweze kufanikisha maandalizi ya Utekelezaji wa Mpango huo.’’ Alisema.

  0 0

  Wakazi wa wilayani Babati mkoani Manyara na viunga vyake wamejitokeza katika kupata namba za vitambulisho vya Taifa ili kukidhi matakwa ya usajili wa laini za simu kwa alama za vidole.

  Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA ipo katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada ya Uhamasishaji wa usajili wa laini za simu kwa alama za vidole na kuongeza kuwa ambaye hatatimiza matakwa ya kisheria ya kusajili laini ya simu kwa alama za vidole laini hiyo itafungwa

  Kampeni ya Mnada kwa Mnada ambapo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikishirikiana na Kampuni ya simu, Jeshi la Polisi Kitengo cha Uhalifu Mitandaoni na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Idara ya Uhamiaji kwa ajili ya utoaji wa huduma za usajili wa laini za simu kwa kutumia vitambulisho vya kitaifa na kuhakikiwa na kampuni za simu kwa kuweka alama za vidole kwa laini za simu.

  Kampeni tangu imeanzishwa imekwenda katika maeneo ya miji na Mkoa lengo Wananchi kutumia fursa ya kusajili laini za simu kwa alama za vidole ambayo unakwenda nchi nzima 

  Akizungumza na Wananchi wa Wilaya ya Babati katika Stendi ya mabasi ya Zamani ya Magugu Mkuu wa Kanda ya Kasikazini wa TCRA Mhandisi Emelda Salum amesema ni fursa kwa wananchi wa Babati na maeneo Mbalimbali wamefika katika Viwanja vya Stendi ya Zamani ya Magugu kupata namba ya kitambulisho cha Taifa katika mfumo wa NIDA na kuweza kusajili laini ya simu kwa alama za vidole.

  Mhandisi Salum Amesema katika Kampeni hiyo imekuwa inafanywa na kanda hiyo ikiwa kila mwananchi aweze kuwa na namba ya Kitambulisho au Kitambulisho cha Taifa kutokana Ushirikiano na NIDA kuwa katika Kampeni hiyo.Amesema kuwa Mnada kwa Mnada TCRA ilianzisha ili kutoa fursa ya Wananchi kuhudumiwa kwa pamoja kwa huduma za mawasiliano na usajili wa laini za simu kwa alama za vidole.

  Amesema Kampeni hiyo ni kuimarisha ulinzi katika huduma za simu pamoja kufanya mawasiliano kuwa salama katika nchi na kuongeza kuwa muda ulioabakia ni 27 mdogo hivyo kila mtu atumie kutafuta taarifa zinazokidhi usajili wa laini kwa alama za vidole.

  Hata hivyo amesema kuwa kampeni ya Mnada kwa Mnada ni kwa ajili ya kutoa elimu ya mawasiliano kwa kushirikiana na wadau katika kujibu changamoto wanazokutanazo katika utumiaji wa mawasiliano nchini.

  Hata hivyo amesema kuwa kuna watu wengine wanatumia mawasiliano ya simu bila kujua ambapo Jeshi Polisi lipo katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada ili kutoa elimu kuhusiana makosa ya jinai ya matumizi ya simu yasiofuata sheria.

  Kampeni hiyo ni endelevu katika kuwafikia wananchi kuhakikisha kila mwananchi anasajili laini ya simu kwa alama za vidole kwa kutumia kitambulisho cha taifa au namba ya kitambulisho hicho.Salum amesema kuwa TCRA iko kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi ili watumie Mawasiliano kwa usalama kutokana na elimu tunayotoa kupitia Kampeni ya Mnada kwa mnada.

  Hata hivyo amesema kuwa wananchi wajitokeze kujisajili kwa alama za vidole kabla ya Desemba 31 kwa kufika katika maduka ya watoa huduma wa Kampuni za Simu za Mkononi."TCRA tutahakikisha tunawafikia wananchi wote kupata elimu ya utumiaji wa bidhaa za mawasiliano kwa kutatua changamoto katika huduma hiyo" amesema Mhandisi Salum.

  Ameongeza kuwa Kampeni iko katika mikoa yote iliopo katika kanda ya Kaskazini.Nae Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa TCRA Makao Makuu Mabel Masasi amesema kuwa wananchi wameitikia kwa kujitokeza kwa wingi kuangalia namba vitambulisho kwa ajili ya kusajili laini za simu kwa alama za vidole na wengi wamepata namba hizo na kufanya usajili kwa watoa huduma wa Kampuni za Simu za Mkononi.

  Masasi amesema kuwa Wananchi wa watumie Kampeni ya Mnada kwa Mnada ya TCRA kupata elimu na baada ya kuisha Mnada sehemu husika waende katika mamlaka husika kupata utaratibu wa vitambulisho vya Taifa.
   Mwananchi akisajili laini ya simu kwa alama za vidole moja ya Kampuni ya huduma za Simu za Mkononi wakati wa Kampeni ya Mnada kwa Mnada uliofanyika Viwanja vya Magugu wilayani Babati mkoani Manyara.
  Mkuu wa Kanda ya Kaskazini wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Emelda Salum akizungumza na Wananchi wa Wilaya ya Babati mkoani Manyara wa Katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada iliyofanyika katika Viwanja vya Stendi ya Zamani ya mabasi ya Magugu ya usajili wa Laini za Simu kwa Alama za vidole.

   Afisa Habari Mwandamizi wa  Mamlaka ya a Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mabel Masasi akitoa maelezo kwa Wananchi namna ya kufuata utaratibu wa kuangalia namba ya kitambulisho cha Taifa kwa maafisa wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) wakati wa Kampeni ya Mnada kwa Mnada iliyofanyika Viwanja vya Magugu wilayani Babati mkoani Manyara.
   Wananchi wakipata huduma ya usajili wa Laini za simu wakati Kampeni ya Mnada kwa Mnada iliyofanyika Viwanja vya Magugu wilayani Babati mkoani Manyara.
   Afisa Habari Mwandamizi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mabel Masasi akitoa maelezo kwa Wananchi wa Babati.
   Wananchi wakihudumiwa usajili wa Laini za simu wakati Kampeni ya Mnada kwa Mnada wa TCRA uliofanyika Viwanja vya Magugu wilayani Babati mkoani Manyara. 
   Bibi zetu ambao wamezaliwa mapacha  wamejitokeza  kupata namba zao za vitambulisho vya Taifa  (NIDA) na kisha kujisajili kwa njia ya alama za vidole.

  0 0

   Meneja wa Benki ya Exim tawi la Tabora, Bw Emmanuel Nkelebe (Kulia) akikabidhi msaada wa taulo za kike kwa mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya wasichana ya Tabora (Tabora Girls Secondary School) Emmaculata Olola ikiwa ni sehemu ya mpango wake wa uwajibikaji wa kwa jamii (CSR) unaofahamika kama Exim Cares. Wanaoshuhudia ni pamoja na Afisa Mauzo wa benki hiyo Bi Hawa Dachi (wa pili kulia) na walimu wa shule hiyo.
   Meneja wa Benki ya Exim tawi la Tabora, Bw Emmanuel Nkelebe (Kulia) akikabidhi msaada wa taulo za kike kwa mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya wasichana ya Tabora (Tabora Girls Secondary School) Naroka Mbaga ikiwa ni sehemu ya mpango wake wa uwajibikaji wa kwa jamii (CSR) unaofahamika kama Exim Cares. Wanaoshuhudia ni pamoja na Afisa Mauzo wa benki hiyo Bi Hawa Dachi (wa pili kulia) na walimu wa shule hiyo.
  Meneja wa Benki ya Exim tawi la Tabora, Bw Emmanuel Nkelebe (wa pili kulia) akikabidhi msaada wa taulo za kike kwa Mlezi wa wanafunzi wa kike wa Shule ya Sekondari ya wasichana ya Tabora (Tabora Girls Secondary School) Bi. Agnes Mlelwa ikiwa ni sehemu ya mpango wa benki hiyo wa uwajibikaji wa kwa jamii (CSR) unaofahamika kama Exim Cares.


  0 0

  ASASI ya Tanzania Election Alliance(TanEA) imesema kuwa ili wananchi 
  wadhihirishe utashi wao katika chaguzi ni dhahiri chaguzi lazima ziwe huru, haki,  wazi, sawa na za kuaminika huku ikisisitiza wapiga   kura wanapaswa kupiga kura bila woga, hofu au kuingiliwa  kusiko stahili. 

  Hayo yamesemwa leo Desemba 2,2019 jijini Dar es Salaam na Wallance 
  Mayunga wakati akizungumza na waandhsi wa habari walipokuwa wakitoa 
  tathimini yao ya uchaguz ii wa Serikali za Mitaa uliofanyika Novemba 24,2019.

  Amefafanua chaguzi ni michakato, ambayo idadi kubwa ya watu inachagua watu wachache miongoni mwao ili wawakilishe na kufanya maamuzi kwa niaba yao katika nafasi za kuchaguliwa au nafasi za kisiasa kupitia uchaguzi. Kupitia uchaguzi mtu anapewa nafasi ya kutenda kwa niaba ya wengine. 

  "Hili hufanyika kwa kupiga kura, katika chaguzi za kisiasa, raia huamua nani awawakilishe katika nafasi ya Urais, Udiwani na kadhalika.Chaguzi za 
  kidemokrasia zinamanisha wananchi sio tu wanapata fursa za kuchagua, bali pia mazingira yanayo faa kuchagua kwa uhuru, haki, uwazi na usawa,"amesema Mayunga.

  Amefafanua ili kampeni ziwe huru na zenye utulivu wagombea na vyama vya siasa vinavyo shiriki kwenye uchaguzi havitawaliwi na vitisho au rushwa na mwamba wagombea wanafuata taratibu na mwenendo  katika kuendesha kampeni zao na kufuata kanuni za maadili zinazo ongoza mchakato wa uchaguzi.

  "Vyama na wagombea wanaoshindana wanapatiwa fursa sawa za kusikilizwa.Pia vyama na wagombea wanao shindana wanapatiwa fursa sawa za kusambaza ujumbe wao kupitia vyombo vya habari na njia nyinginezo, zinazo kubalika katika kuwafikia Watanzania,"amesema.

  Akifafanua zaidi kuhusu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2019, amesema kuwa TanEA ilifanya uangalizi katika mikoa 13 ya Tanzania Bara na wilaya zipatazo 40 na jumla ya Watazamaji 150 walisambazwa katika Wilaya na Mikoa hiyo." TanEA inatumia fursa hii kuwapongeza Watanzania wote kwa kuwa na utaratibu wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Siyo nchi zote duniani wanayo nafasi hii.

  "TanEA inavipongeza vyombo vya habari kwa kufanya kazi kwa ushirikiano na asasi za kiraia katika  kuelimisha na kuhamasisha umma kujitokeza na kushiriki katika uchaguzi huu,"amesema Mayunga.


  Hata hivyo TanEA wanatoa mapendetunatoa mapendekezo kadhaa kwa Serikali yakiwamo ya kushauri Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ufanyike sanjari na uchaguzi mkuu, kwa vile imedhihirisha hamasa katika uchaguzi wa Serikali za mitaani ndogo ukilinganisha na uchaguzi Mkuu unaochagua Rais, Wabunge na Madiwani.

  " Ikiwezekana hili lifanyiwe kazi katika uchaguzi ujao wa 2025 mara baada ya uchaguzi mkuu wa 2020. Wananchi wengi wanadhani uchaguzi wa Serikali Mitaa hauna umuhimu. Ikifanyika hivi pia itapunguza gharama za uchaguzi kwa Watanzania, ambao ndio walipa kodi,"amesema Mayunga.

  Pia wamependekeza vibali vya kutoa elimu ya mpiga kura, uraia na 
  utazamaji/uangalizi wa uchaguzi vitolewe mapema. "Kwa mfano, mwezi Januari ili kutoa fursa kwa AZAKI na Taasisi mbalimbali kujiandaa kupata rasilimali na kupanga programu husika,".

  Ameongeza mapendekezo mengine ni kwamba Asasi za Kiraia zishiriki 
  kikamilifu katika kutoa elimu ya Mpiga kura na vile vile kushiriki kikamilifu 
  katika uangalizi ili kuishauri Serikali kuboresha mazingira ya uchaguzi ikiwemo kasoro na dosari zinazojitokeza. 

  Pia wanatoa mwito kwa AZAKI kushirikiana katika masuala haya muhimu ya Elimu ya Mpiga kura na uangalizi wa uchaguzi.Vyombo vya habari vinapaswa viendelee kushiriki kikamilifu pia kuelimisha wananchi, kusambaza taarifa sahihi kuhusu masuala ya uchaguzi na mchakato wa uchaguzi, tunavishauri vyombo vya habari vitimize wajibu wake ipasavyo.

  "Tunaiomba Serikali ikae pamoja na makundi mbalimbali ya wadau wa uchaguzi kama vile AZAKI, vyama vya siasa, taasisi mbalimbali kufanya tathmini ya kungalia dosari zilizo jitokeza katika uchaguzi huu wa serikali za Mitaa uliopita na kuzifanyia kazi ili kuufanya uchaguzi ujao uwe huru, haki na usawa. 

  "Pia vyama vya Siasa vishirikiane na serikali katika kuboresha mazingira ya uchaguzi. Serikali iendelee kutunza Demokrasia hapa nchini ili wananchi waweze kushiriki kikamilifu katika michakato ya uchaguzi na chaguzi,"amesema Mayunga.

  Pamoja na mambo mengine amesema uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019 nchini Tanzania si wa kawaida ukilinganisha na chaguzi nane zilizopita.Pia ni bora viongozi na wanachama na vyama hivyo na zaidi kujiepusha na hotuba zenye chembe chembe za kwenda kinyume cha sheria na utawala bora.

  0 0

  Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

  IMEELEZWA kuwa haki ya wakimbizi kurejea nchini mwao au kubaki kwa wakimbizi waishio nchini wakitokea Burundi itaendelea kuwepo na kuwa la hiari na hiyo ni pamoja na kupata  huduma za msingi ikiwepo ulinzi kwa wakimbizi watakaobakia nchini na kwa wale watakaorejea nchini mwao watahakikishiwa usalama wa kurejea nchini mwao.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kamishna Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), George Okoth Obbo amesema, kupitia kikao cha siku tano cha mkutano wa 21 wa Tripartite commission kilichowakutanisha na Waziri wa mambo ya ndani wa Tanzania Kangi Lugola na wawakilishi kutoka Burundi na Shirika linalohusika na masuala ya wakimbizi duniani (UNHCR) walipata wakati mzuri wa kujadili masuala yahusuyo wakimbizi ikiwemo kuheshimu uhuru wa wakimbizi hao kubaki au kurejea makwao.

  "Wakimbizi kurejea Burundi ni hiari na watakaoamua  kurejea katika nchi zao tutashirikiana nao kwa Kuhakikisha wanarejea nchini mwao salama kabisa,  tutawafikisha kwenye mipaka ya nchi zao na wale watakao endelea kubaki nchini UNHCR kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania na Burundi tutaendelea kushirikiana nao kwa kuhakikisha wanapata mahitaji yote ya msingi" ameeleza Okoth -Obbo.

  Pia amesema kuwa kupitia mkutano huo wamekubalina kuwa Tanzania iendele kutoa taarifa za wakimbizi hasa vyeti vya kuzaliwa, vifo na vyeti vya wakimbizi katika shirika la UNHCR.

  "Taarifa zinazowahusu wakimbizi ni muhimu sana katika kuisaidia kutoa mahitaji ya msingi ni vyema Tanzania ikaendelea kutoa taarifa kupitia nyaraka mbalimbali zinazoonesha  ndoa, uzazi na vifo"

  Amesema kuwa UNHCR Tanzania inahitaji dola za kimarekani 126 na kueleza kuwa wadau mbalimbali wamekuwa wakishiriki kwa namna moja au nyingine kwa Kuhakikisha wakimbizi hao wanapata huduma muhimu hasa zile za kijamii.

  Okoth amesema kuwa  baada ya mkutano huo alitembelea kambi za Nduta na Mtendeli zilizopo Mkoani Kigoma ambapo alipata wasaa wa kuzungumza na wakimbizi pamoja na viongozi na washiriki wanaohudumia wakimbizi katika nchi hizo.

  " Niipongeze Serikali ya Tanzania na wananchi wake kwa kubeba jukumu la kubeba wakimbizi wapatao 246,000 katika nchi yao na katika kambi nilizopita Kigoma nilipata kushuhudia wakimbizi wakijiandikisha kwa hiari ili wapate kurejea makwao." Ameeleza.

  Ikumbukwe kuwa idadi kubwa ya wakimbizi wanatoka katika nchi za Burundi na Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo huku 87 ya wakimbizi hao wakiishi katika kambi tatu zilizopo Mkoani Kigoma.
   Kamishna Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), George Okoth Obbo akizungumza mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani),jijini Dar  kuhusu mambo mbalimbali yaliyojadiliwa kwenye kikao chao cha siku tano kilichowakutanisha Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tanzania Mhe.Kangi Lugola,Wawakilishi kutoka Burundi na Shirika linalohusika na masuala ya wakimbizi Duniani (UNHCR),namna walivyojadili  masuala yahusuyo wakimbizi ikiwemo kuheshimu uhuru wa wakimbizi hao kubaki au kurejea makwao.
  Baadhi ya Waandishi wa habari wakifuatilia yaliyokuwa yakizungumza na  Kamishna Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), George Okoth Obbo,jana jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Mkuu wa Kitengo cha Wafanyabiashara wa Kati na Wadogo wa Benki ya NBC, Evance Luhimbo (kushoto) akizungumza na wafanyabiashara wadogo na wa kati wa maeneo ya Kariakoo  katika semina ya siku moja iliyoandaliwa na benki hiyo kwa lengo la kuwawezesha kimafunzo kuhusu ukuaji wa biashara, masuala ya mitaji, kodi na jinsi nyingine ya kuendesha biashara jijini Dar es Salaam jana.
   Mkuu wa Kitengo cha Wafanyabiashara wa Kati na Wadogo wa Benki ya NBC, Evance Luhimbo akizungumza na wafanyabiashara  wadogo na wa kati wa maeneo ya Kariakoo, katika semina ya siku moja iliyoandaliwa na benki hiyo kwa lengo la kuwawezesha kimafunzo yatakayosaidia katika ukuaji wa biashara zao jijini Dar es Salaam jana.

   Meneja Maendeleo ya Viwanda wa Chama cha Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA), Patrick Magai akitoa elimu kuhusu fursa za viwanda katika semina ya siku moja iliyoandaliwa na benki ya NBC kwa wateja wake wafanyabiashara wadogo na wa kati wa maeneo ya Kariakoo jana. 
   Msaidizi wa Msajili Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), George Chuwa akizungumza katika semina ya siku moja iliyoandaliwa na benki ya NBC kwa wateja wake wafanyabiashara wadogo na wa kati wa maeneo ya Kariakoo jiijini Dar es Salaam jana. 
    Ofisa Msimamizi wa Walipa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Joyce Ng`oja akitoa elimu kuhusu kodi katika semina ya siku moja iliyoandaliwa na benki ya NBC kwa wateja wake wafanyabiashara wadogo na wa kati wa maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam jana.

   Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Guru Planet, Nickson Martin akitoa elimu kuhusu uhifdhi wa bidhaa katika semina ya siku moja iliyoandaliwa na benki ya NBC kwa wateja wake wafanyabiashara wadogo na wa kati wa maeneo ya Kariakoojiji jijini Dar es Salaam jana.

    Mkurugenzi wa Biashara wa NBC, Elvis Ndunguru (wa pili kushoto) akizungumza jambo na wafanyabiashara wadogo na wa kati wa maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam wakati wa semina iliyoandaliwa na benki hiyo yenye lengo la kuwawezesha kimafunzo kuhusu ukuaji wa biashara zao jijini humo jana.

   Mkurugenzi wa Biashara wa NBC, Elvis Ndunguru (kushoto) akizungumza na wafanyabiashara wadogo na wa kati wa maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam katika semina ya siku moja yenye lengo la kuwawezesha kimafunzo kuhusu ukuaji wa biashara zao, masuala ya kodi, mitaji na taratibu nyingine za uendeshaji wa biashara jijini  Dar es Salaam jana.

  0 0

  Barclays bank Tanzania has started to rebrand its properties in the country following a take-over by ABSA Group Limited last year.

  Yesterday the banks unveiled its first Absa branded branch at Palm Village along Mwai Kibaki Road in Dar es Salaam and with the bank’s Managing Director, Abdi Mohamed, assuring customers that the changes would not affect the quality of service attached with the bank.

  “We are getting ready to change our name from Barclays Bank Tanzania to Absa Bank Tanzania. This is in line with our parent company Absa Group Limited’s decision to rebrand all its operations to Absa, as announced in July 2018,” said the MD during the ceremony to unveil the new Absa branded branch.

  he noted that over the coming weeks, people in the country will witness more of Absa branded branches, ATMs and some other branded assets take on the warm, vibrant red colour palette of the Absa brand, symbolic of the many shades under our hot African sun.“This is the look-and-feel we will be rolling out across our Tanzania branch network,” he declared.

  According to Mr Mohamed the change was part of one of the largest rebranding projects in Africa scheduled to be completed by mid-2020 and part of a broader, multi-country rebrand programme happening at Group-level.

  Appreciating the size of the task ahead and in preparation to change their name, the bank started to introducing Absa’s warm, vibrant red colour palette on some of its assets, including bank branches and ATMs, to ensure that they make their clients and the general public aware of the changes ahead of before new legal name changes.He noted that the bank will continue to be known as Barclays Bank Tanzania until the process was officially concluded.

  “We will continue to listen to our customers and use their feedback to create a business that is relevant and meets their needs. There will always be a demand for physical branches in Tanzania, and branch-based banking remains a key part of our offering,” he said.

  Unveiling the branded branch on behalf of the Minister for Finance and Planning, Dr Phillip Mpango, the Assistant Commissioner for External Finance, Ms. Mamelta Mutagwaba, noted that the move was a clear testimony of how the bank is committed to continue doing business in the country.

  “It is important to note that customers are usually sensitive, and jittery when it comes to re-branding because of the fear that they will lose the services, value for money, reliability that made them loyal.

  We call upon banking consumers in Tanzania to have confidence in Absa, and that they will get the same standard of services they have been getting from Barclays. On your part, we expect Absa to reciprocate this trust by making sure that the transition over rebranding is smooth and as flawless as can be”, she said.

  She noted; “The government has embarked on a drive to make Tanzania a middle income industrial economy. Such endevour requires concerted efforts involving both the private sector and the public sector. Within this context, private public partnership is needed especially by engaging the banking sector. To achieve this ambition, the country needs to invest heavily in infrastructure, business support, manpower training, and in social amenities.

  “The ascendancy of Tanzania onto this industrialization route has seen the launching of infrastructural mega projects, as manifested by the on-going construction of the Standard Gauge Railway, Stigler’s Gorge Hydroelectric power. Construction of Chato airports and Terminal 3 at Mwalimu Nyerere International Airport. Such projects require massive investments. It is our expectation that the banking sector will take the initiative and expand its credit portfolio to accommodate financing of such projects. 

  “This is one aspect of public finance demand, the other is on productive sectors that are crucial to creating the needed linkages in the industrialization mix, especially agriculture. Traditionally, commercial banks has not been able to adequately finance agriculture, either because of the risk involved in crop failure or the long production cycle which delays the commencement of loan repayment.

  “We call upon banks to come up with innovative financing packages that can cater for the agricultural sector. In addition, banks should try to deal with the various obstacles that have tended to make the agricultural sector not bankable. On our part, the government, and the ministry of finance in particular, will work with other ministries to make sure that impediments to advancing loans to the agricultural sector are removed”, added Ms. Mamelta.
  Ministry of Finance and Planning Assistant Commissioner for External Finance who was representing Finance’s Minister, Mrs. Mamelta Mutagwaba (second left), cuts a ribbon to official launch the first Absa branded branch in Tanzania at Palm Village, Mwai Kibaki Road in Dar es Salaam on Tuesday. Looking on from left are; Barclays Tanzania Board Chairman, Simon Mponji, BBT Managing Director, Abdi Mohamed, Chinese Business Chamber Chairman, Janson Huang, BBT Head of Retail Banking, Oscar Mwamfwagasi and BBT Head of Communications and Corporate Relations, Aron Luhanga.  0 0

   Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Plc, Rosalynn Mworia (kulia) akizungumza wakati wa kongamano la Data Tamasha linalokusanya wadau mbalimbali wa takwimu kwa maendeleo endelevu linalofanyika jijini Dar Es Salaam. Wengine ni Meneja Mkazi wa CRS Tanzania, Kelli Hynes na Mkurugenzi Uendeshaji wa FSDT, Irene Mlola.
   Mkuu wa Kitengo kinachoangalia ufanisi wa Kampuni ya Vodacom Tanzania Plc, Zaituni Ally akizungumza wakati wa kongamano la Data Tamasha linalokusanya wadau mbalimbali wa takwimu kwa maendeleo endelevu linalofanyika jijini Dar Es Salaam. 


  0 0

   Mmoja wa washindi wa droo ya kwanza ya kampeni ya Ibuka Kidedea na NBC  Malengo, Scholastika Peter (kulia), akibonyeza kitufe cha kompyuta ili kumpata mmoja wa washindi wa droo ya pili jijini Dar es Salaam leo. Wanaoangalia kulia kwake ni Meneja Amana za Uwekezaji, Dorothea Mabonye, Meneja Uhusiano Wateja Binafsi, Deogratius Kibodya, Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Innocent Shayo na Mkuu wa Bidhaa wa NBC, Japhet Fungo. Katika droo ya pili, washindi watano wamejishindia tiketi za kwenda Ushelisheli, huku watatu wakishinda safari za kwenda Serengeti, kila moja akitunukiwa bakshishi ya kuandamana na mwenza atakayemchagua.
   Meneja Masoko wa benki ya NBC, Alina Maria Kimaryo ( kulia), akikabidhi zawadi ya  pikipiki kwa mmoja wa washindi wa droo ya kwanza ya kampeni ya Ibuka Kidedea na NBC Malengo, Daudi Majani, katika hafla iliyofanyika pamoja na droo ya pili ya kampeni hiyo jijini Dar es Salaam leo. Katika droo ya pili, washindi watano wamejishindia tiketi za kwenda Ushelisheli, huku watatu wakishinda safari za kwenda Serengeti, kila moja akitunukiwa bakshishi ya kuandamana na mwenza atakayemchagua. 
   Mmoja wa washindi wa droo ya kwanza ya Ibuka Kidedea na NBC Malengo, Scholastika Peter, akifurahia zawadi yake ya pikipiki mara baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa Bidhaa wa benki hiyo, Japhet Fungo (kulia). 
   Ofisa wa Benki ya NBC, Hussein Issa ( kulia), akikabidhi zawadi ya  pikipiki kwa mmoja wa washindi wa droo ya kwanza ya kampeni ya Ibuka Kidedea na NCB Malengo, Honest Kimaro, katika hafla iliyofanyika pamoja na droo ya pili ya kampeni hiyo jijini Dar es Salaam leo. Katika droo ya pili, washindi watano wamejishindia tiketi za kwenda Ushelisheli, huku watatu wakishinda safari za kwenda Serengeti, kila moja akitunukiwa bakshishi ya kuandamana na mwenza atakayemchagua. 
  Baadhi ya washindi wa zawadi ya bodaboda wakipozi kwa picha ya kumbukumbu na maofisa wa NBC mara baada ya kukabidhiwa zawadi zao jijini Dar es Salaam leo. Pikipiki hizo tano zilizokabidhiwa leo zina thamani ya shs milioni 12.3.

  0 0

  Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Pwani, Joseph Mutalemwa,akizumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kumkabidhi zawadi Mshindi wa promosheni ya Tigo Chemsha Bongo 2019 
  “Kuna vitu vikitokea kwenye maisha yako inakuwa ngumu kuficha hisia zako. Nashukuru TIGO kwa kuleta mchezo huu wa #TigoChemshaBongo nilicheza nikiamini nitashinda pesa lakini nimeambulia zawadi kubwa kabisa ya gari” Mzee Shaban Khamis 
  BAHATI IMEMUANGUKIA Mzee Shaban Khamis toka Zanzibar kushinda Gari aina ya Renault Kwid Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Pwani, Joseph Mutalemwa, amempongeza Mzee Shaban kwa kutumia fursa ya #TigoFiesta2019 Chemsha Bongo vizuri 

  Mkazi wa Zanzibar, Shaban Khamis Ali(49) akifurahia mara baada ya kukabidhiwa gari yake aina Renault Kwid yenye thamani ya 23m/- baada ya kuibuka mshindi wa promosheni ya Tigo Chemsha Bongo 2019.   Dar es Salaam Desemba 5 2019.Mkazi wa Zanzibar, Shaban Khamis Ali(49) amekabidhiwa rasmi gari yake aina ya Renault Kwid yenye thamani ya 23m/- baada ya kuibuka mshindi wa promosheni ya Tigo Chemsha Bongo 2019.

  Promosheni hiyo iliyodumu kwa siku 90 kuanzia tarehe 4 Agosti hadi 14 Novemba 2019 na wateja wa Tigo walipata nafasi ya kujishindia zawadi za pesa taslim kila siku na droo ya mwisho mshindi alikuwa anajinyakulia zawadi ya gari. Promosheni hii ilishuhudia washindi 90 kila siku waliojishindia Tshs 100,000 na washindi wengine 90 waliojishinda Tshs 50,000. Pia tuliwapa washindi 12 kili wiki kwa mda wa wiki 12, Tshs 1,000,000.


  Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Shabaan alisema “Wakati napigiwa simu,nilikuwa nyumbani najipanga kutoka kuenda katika mihangaiko yangu ya kibiashara, basi nilipopata ile taarifa kwamba nimeibuka mshindi nilifurahi sana kwani sikutegemea kabisa kuwa ningeibuka mshindi katika promosheni hii, habari hizi naziona kama ndoto kwangu, nashukuru Tigo kwa kunifungia mwaka vizuri na kutimiza ndoto yangu ya kumiliki gari, kwani itanisaidia katika mizunguko yangu ya kibiashara “alisema kwa furaha. 
  Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Pwani, Joseph Mutalemwa, alimpongeza mshindi huyo na kutumia fursa hiyo kuwashukuru wateja wote wa kampuni ambao walishiriki na baadhi yao kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo zawadi za fedha taslimu ambayo yalitolewa na kampuni hiyo. “Tunayo furaha kubwa katika kipindi hiki tunachoelekea katika msimu wa sikukuu kumkabidhi mshindi wetu wa gari ya aina Renault Kwid,yenye thamani ya 23m/-, gari hili ni jipya kabisa,. Tunawashukuru wateja wetu nchi nzima walioshiriki kwenye promosheni hii ya miezi mitatu ambayo imemalizika mwishoni mwa mwezi wa Novemba 2019”. alisema Mutalemwa. 

  Aliongeza kuwa, promosheni hii ambayo ilianza jijini Mwanza katika msimu wa Tigo Fiesta 2019-Saizi Yako imepata mafanikio makubwa kutokana na wateja wengi kujitokeza kushiriki na baadhi yao kufanikiwa kujishindia zawadi(fedha taslim) mbalimbali na hivyo Tigo kufanikisha lengo lake ambalo lilikuwa ni kuwashukuru wateja kwa kuiunga mkono kampuni kupitia kununua bidhaa zake mbalimbali. Kwa kumalizia Mutalemwa aliwashukuru wateja wote wa Tigo kwa kuendelea kuunga mkono kampuni na kuahidi kuwa promosheni mbalimbali za kunufaisha wateja wa kampuni hiyo zinatendelea kubuniwa katika siku za usoni.

  0 0

  UTAFITI uliyofanywa na Shirika linalohusika na usalama  na Ustawi wa wanyama Duniani (World Animal Protection) umebaini kuwa kuku wengi wanaouzwa katika maeneo mbalimbali nchini wakidaiwa kuwa ni wa kienyeji si wa kienyeji kama inavyosemwa.

  Utafiti huo umebaini kuku hao si wa kienyeji bali ni kuku wa kisasa maarufu kama kuku wa kizungu wanaofungwa majumbani kwa kupewa majani pamoja  na dawa mbalimbali za kuwakuza na kuwafanya kuwa wagumu.

  Akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati akiwasilisha ripoti ya utafiti huo uliyofanywa katika nchi nne Tanzania ikiwamo, Msemaji Mkuu wa Shirika hilo, Victor Yamo alisema utafiti huo ambao ulifanywa Juni hadi Julai mwaka huu katika mikoa ya Arusha na Dar es Salaam umebaini jambo hilo hivyo watumiaji wanapaswa kuwa makini.

  Yamo amesema kuku wengi wanauzwa katika mikoa hiyo wamekuwa wakupewa dawa za kuwakuza  ambazo zina madhara kwa binadamu pindi wanapotafuna mifupo yao

  "Wakati watu wetu wakitembelea kwenye masoko mbalimbali kuulizia bei ya kuku na wakabaini uwepo wa kuku wa kisasa wengi na mwananchi uuziwa kwa kuambia kuwa ni wa kienyeji jambo ambalo ni uongo," alisema.

  Amesema utafiti huo ulifanyika kwa lengo la kujua walaji wananunua nyama za aina gani, kutoka wapi pamoja na  kuangalia kama wanafahamu ubora wa chakula na matumizi ya dawa za wanyama.

  "Tunaamini kuwa mteja ataelewa nyama anayotaka kununua au kula inaubora au tatizo kiasi gani itakuwa rahisi kujiepusha nayo na kutafuta kitu kingine mbadala cha kula," alisema

  Aidha Yamo amesema kwa sasa Shirika lao linafanya jitihada kubwa kuhakikisha linaimarisha ustawi na haki za wanyama na sheria za kuwalinda wanyama hao zinapitishwa na serikali husika katika kila nchi.

  Amesema pamoja na kuyafanya hao wanatoa wito kwa watanzania waanze kuelewa kuwa kama watashindwa kuangalia ustawi wa wanyama hasa wanaoliwa kuna hatari kubwa ya kupotea.

  "Ni ukweli uliyowazi kuwa ustawi wa wanyama ni muhimu sana na kwa kutambua hilo tumekuwa tukienda mashuleni kufundisha jambo hilo na masuala ya usalama wa chakula na ubora wa dawa," alisema.
  Mtaalamu wa masuala ya kutetea Haki na Ustawi wa Wanyama kutoka shirika la World Anima Protection ,Dkt Victor Yamo akizungumza na Waandishi wa habari leo jijini Dar,alipokuwa akiwasilisha ripoti ya utafiti uliyofanywa katika nchi nne Tanzania ikiwamo, kuhusu kubainika kwa kuku wengi wanaouzwa katika maeneo mbalimbali nchini wakidaiwa kuwa ni wa kienyeji kumbe si wa kienyeji kama inavyosemwa.

   Baadhi ya Waandishi wa Habari wakimsikiliza mtaalamu huyo wa Haki na Ustawi wa Wanyama kutoka shirika la World Anima Protection ,Dkt Victor Yamo alipokuwa akiendelea kufafanua mambo mbalimbali yahusuy haki na ustawi wa Wanyama nchini Tanzania 
   Mtaalamu wa masuala ya kutetea Haki na Ustawi wa Wanyama kutoka shirika la World Anima Protection ,Dkt Victor Yamo akifafanua jambo kwa msisitizo mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar,alipokuwa akiwasilisha ripoti ya utafiti uliyofanywa katika nchi nne Tanzania ikiwamo, kuhusu kubainika kwa kuku wengi wanaouzwa katika maeneo mbalimbali nchini wakidaiwa kuwa ni wa kienyeji kumbe si wa kienyeji kama inavyosemwa.


  0 0

  BENKI ya NMB imekabidhi zawadi kwa washindi tisa wa MastaBoda kama washindi wa wiki baada ya kufikisha miamala hamsini kupitia mfumo wa malipo wa Mastercard QR katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam. Zoezi hilo liliendeshwa na Meneja Mahusiano Kitengo cha Kadi- Yusuph Achayo na kushuhudiwa na Mwenyekiti wa Waendesha Bodaboda- Michael Massawe. 

  MastaBoda ni kampeni inayoendeshwa na NMB kwa ajili ya kuwawezesha waendesha Bodaboda kuunganishwa katika mfumo wa kibenki ili waweze kupokea malipo kupitia mfumo wa Mastercard QR pamoja na mitandao ya simu iliyo unganishwa na mfumo wa malipo wa Mastercard QR. 

  Akikabidhi zawadi hizo Achayo ametoa wito kwa waendesha Bodaboda ambao hawajajiunga na mfumo wa MastaBoda kujiunga ili kuendesha biashara zao kisasa kwa usalama wa fedha zao. 

  Nao washindi walioibuka na kitita cha Sh, 50,000. Wameimwagia sifa NMB kwa kutimiza ahadi, kwani zinawaongezea nguvu ya kupambana ili kufika mbali zaidi katika kuendesha biashara zao. 

  “Tangia nijiunge na mfumo huu, hii ni mara yangu ya pili kushinda, najisikia furaha sana. Tangu nianze kufanya miamala na QR nina amani, badala ya kutembea na pesa sasa fedha yangu inaingia moja kwa moja benki, mfumo huu pia unaookoa muda hasa katika kutafuta chenchi. .”alisema Ebenezer Elisha (Mwenge) ambaye pia ni mmoja wa washindi. 

  Washindi wengine waliojizolea kitita hicho ni Goodluck Ntaya (Kawe Ukwamani), Mohamed Abdallah (Buguruni Rozana) Twaliha Mfinanga(Rozani Mafleti) na Frorian Byabato (Roziani Mafleti).

   Dereva wa Bodaboda wa kituo cha Ubungo Plaza- Abubakar Mohamed, akipokea pesa taslimu 50,000 Kwa kuibuka mshindi kwa kufanya miamala mingi - kulipwa na wateja wake kupitia mfumo wa Mastercard QR. 
  Dereva wa Bodaboda wa Kituo Sayansi Adam nae alikabidhiwa zawadi ya fedha taslimu 50,000 kwa kufanya miamala mingi ya kulipwa na wateja wake kupitia mfumo wa Mastacard QR

   Meneja Mahusiano wa Kitengo cha Kadi Benki ya NMB - Yusuph Achayo (kushoto) akimkabidhi zawadi ya fedha taslimu 50,000 dereva Bodaboda wa Kituo cha Kibamba Hospitali-Jonas Ruben. Akishuhudia ni Mwenyekiti wa Chama cha Waendesha Bodaboda Mkoa wa Dar es Salaam, Michael Massawe.
   Bodaboda wa Kituo cha Kimara kwa Msuguri - Gasper Ngoh akipokea zawadi ya fedha taslimu 50,000 kwa kufanya miamala mingi ya kulipwa na wateja wake kupitia mfumo wa Mastercard QR. 

  0 0
  Mwenyekiti wa bodi ya TASAF, Dr. Moses Kusiluka (aliyevaa shati nyeupe) akikagua baadhi ya bidhaa zinazouzwa na baadhi ya walengwa wa TASAF katika kijiji cha Khusumay wilayani Karatu kama njia mojawapo ya kujiongezea kipato.

  Mwenyekiti wa Bodi ya TASAF Dr.Moses Kusiluka ambaye pia ndiye Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Ikulu ( aliyevaa koti ) akikagua moja ya majengo  ya Shule ya Sekondari yaliyojengwa na TASAF katika kijiji cha Khusumay wilaya ya Karatu.
  Nyumba za Walimu na hosteli ya wanafunzi ( picha ya juu na chini ) yaliyojengwa na TASAF katika Shule ya Sekondari ya Khusumay yanaelezwa kuhamasisha wanafunzi kuhudhuria masomo na kupunguza tatizo la mimba kwa watoto  wa kike.

  Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Bw. Ladisilaus Mwamanga akifungua bomba la maji kwenye moja ya nyumba zilizojengwa na TASAF katika Shule ya Sekondari Khusumay wilaya ya Karatu Mkoani Arusha.
  Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya TASAF,Wadau wa Maendeleo na Menejimenti ya TASAF akiangalia ujenzi wa daraja linalojengwa na walengwa wa TASAF katika kijiji cha Nala wilaya ya Karatu mkoani Arusha kwa utaratibu wa Ajira ya Muda.
   Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Uongozi ya TASAF, Maafisa wa Serikali na Wadau wa Maendeleo wakiangalia ng’ombe wa mmoja ya Walengwa ambao amewapata baada ya kujumuishwa kwenye Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika kijiji cha Nala wilaya ya Karatu mkoani Arusha.  Na Estom Sanga- Karatu

  Katibu Mkuu ofisi ya Rais-Ikulu -Dr. Moses Kusiluka ametoa wito kwa Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF kufanya kazi kwa bidii ili waweze kuondokana na umaskini uliokithiri.

  Dr. Kusiluka ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa Bodi ya taifa ya Uongozi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF ameyasema hayo kwa nyakati tofauti alipotembelea na kukutana na baadhi ya walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini na kukagua miradi inayotekelezwa na TASAF katika wilaya ya Karatu mkoani Arusha ambako aliambatana pia na baadhi ya Wajumbe wa bodi .

  Amesema Serikali inatambua changamoto ya Umaskini unaowakabili wananchi ,lakini akasisitiza kuwa ili kuitokomeza changamoto hiyo wananchi wanapaswa kujituma kwa kufanyakazi kwa bidii na maarifa na kutumia vizuri mazingira wezeshi yaliyowekwa na Serikali kuinua mapato yao.

  Aidha Dr. Kusiluka amehimiza wazazi kutilia mkazo suala la elimu kwa watoto wao ambao amesema Hiyo ndiyo njia ya uhakika ya kujenga jamii bora ya baadaye itakayoleta ukombozi wa kweli wa ujenzi wa uchumi thabiti wa kaya husika na taifa kwa ujumla huku ikikemea vikali vitendo vyovyote vinavyoathiri maendeleo ya wanafunzi hususani watoto wa kike.

  ‘’tumieni vizuri fursa mliyoipata ya kuwa shuleni ili mtimize ndoto zenu za kuwa wataalamu wa fani mnazozitaka katika utumishi wa taifa hapo baadaye’’ alisisitiza Dr. Kusiluka baada ya kukagua nyumba na hosteli ya wanafunzi wa kike katika shule ya sekondari ya Khusumay ambayo yamejengwa na TASAF.

  Katika hatua nyingine Mwenyekiti huyo wa Bodi ya taifa ya Uongozi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii- TASAF amesema licha ya mafanikio makubwa yaliyopatikana katika utekelezaji wa Shughuli za Mfuko huo , Serikali imeanza kuchukua hatua madhubuti za kuhakikisha kuwa Mfuko huo unaendelea kuwa nyenzo muhimu katika kusaidia jitihada za kupunguza umaskini nchini.

  Wakiwa katika kijiji cha Khusumay,Wajumbe hao wa bodi ya taifa ya Uongozi ya TASAF ,walitembelea kaya za baadhi ya walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini na kujionea namna walengwa hao walivyofanikiwa kuboresha makazi yao, kununua mifugo hususani mbuzi, ng’ombe ,kuku na nguruwe kwa kutumia ruzuku waliyoipata kutoka TASAF kama njia mojawapo ya kukuza uchumi wa kaya za Walengwa hao.

  Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF- Bw. Ladislaus Mwamanga ameishukuru serikali kwa kuendelea kuuthamini Mfuko huo na kuridhia utekelezaji wake kuendelea katika sehemu ya pili ambayo amesema imeagizwa kutekelezwa katika maeneo yote nchini.

  0 0

  Meat consumers in Tanzania ranked poorly on animal welfare and food safety issues compared to its neighbours according to a report launched today by World Animal Protection in Dar el Salaam, Tanzania. The report entitled “Consumers perceptions on animal welfare and food safety” shows that meat consumers in Tanzania are less concerned about how an animal is treated before it lands on their table as food.   
   
  The survey indicates that 37.2% of the Tanzanians who participated in the study do not consider meat being free from chemical contamination as important. Similarly, 54.37% of the participants did not consider how the animal is raised as being important while 60.7% and 56.8% did not consider the welfare of the animal during transportation and slaughter to be important.  

  However, 89.9% of the respondents would purchase more meat and meat products with a food safety assurance marker from supermarkets and fast food restaurants while 38.2% of the respondents will purchase more if the production was environmentally friendly and 36.7% would increase their meat consumption if the production system was animal welfare friendly. 60.1% of the people interviewed would purchase more if assured the meat is free of chemicals.
  The report further shows that 53.3% were able to link the use of antibiotics in farming systems to poor welfare within the production system and 79.4% of the participants knew that antibiotics in the meat had a negative impact on the health of the consumers. 87.8% of the consumers were able to connect poor animal welfare to poor quality of meat that ends on their plates while 61.8% were willing to pay more for meat that is produced in high welfare. In addition, 71.4% percent of people interviewed would stop sourcing and tell their family and friends to stop sourcing meat if they knew supermarkets sourced meat products from poor animal welfare producers.

  Dr. Victor Yamo – Campaigns Manager: Animals in Farming for World Animal Protection while launching the report in a media breakfast in Dar el Salam, noted that “Of significant importance is that consumers are willing to pay more if they are assured that the meat products are free from antibiotics and chemicals and the animals are raised and transported in high welfare conditions and ultimately slaughtered humanely
  Dr Yamo further observed that “This survey points to a significant need for enhanced education and sensitization of Tanzanian consumers on animal welfare and the correlation between how animals are raised and the quality of the meat that ends up on their tables” He noted that it was important that producers and key players along the meat value chain adopted high welfare production systems.  

  He reminded the Veterinary professionals in Tanzania of their critical role in not only educating producers and consumers on the importance of animal welfare in ensuring wholesome products but also the important role in ensuring that appropriate policies, regulations and/or legislations around animal welfare and food safety are in place to not only protect the consumers but also to ensure that the Tanzanian production system met international standards.

  The study further highlighted the influx of international brands such as Game and KFC into the Tanzanian market. Dr. Yamo noted that “These international and regional brands have incredible market power which they should use to help address the animal welfare and food safety concerns being raised by the Tanzanian consumers such as addition of chemicals to prolong the shelf life of meats and the rampant misuse of antibiotics to mask poor animal welfare conditions.”
  He reminded the consumers that the indiscriminate use of antibiotics in farm animals has led to proliferation of antimicrobial resistance and development of superbugs which has had serious impact on human health. He concluded by saying that“Consumers should demand for antibiotic-free, higher welfare produced meat and meat products from the outlets where they obtain their meat and meat products.” 

  0 0


  Na Chalila Kibuda, Michuzi TV ,Lindi

  Wananchi wa Mkoa wa Lindi wamejitokeza katika usajili wa laini za simu kwa alama za vidole huku Wananchi hao wakipata fursa ya kupata namba za vitambulisho kutoka Mamlaka ya Vitambulisho vya vya Taifa (NIDA) kwa ambao walikamilisha taratibu zote za mamlaka hiyo.

  Akizungumza na Wananchi wa Mkoa wa Lindi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo Katibu Tawala Msaidizi Dkt.Bora Haule amesema kuwa mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) ihakikishe inaongeza nguvu ya usajili kwa muda uluobaki kwani wasipofanya hivyo Wananchi watashindwa kupata mawasiliano.

  Dkt.Haule amesema usajili wa laini za simu kwa alama za vidole kufanya mawasiliano yanakuwa salama kwani huduma nyingi zinafanyika kwenye simu hivyo usalama huo ni kila mwananchi asajili laini ya simu.

  Amesema kuwa Wananchi wa Mkoa wa Lindi ambao hawajafanya utaratibu wa kupinga picha mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) wafanye hima kuweza kupata namba au Kitambulisho kukidhi matakwa ya usajili laini ya simu kwa alama za vidole.

  Aidha amesema kuwa Kampeni ya sasa mtu haachwi nyuma katika usajili kwani usajili huo serikali imewekeza kuwa bure kuondoa changamoto ya kizingizio cha fedha kuchangia Wananchi.

  Nae Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Semu Mwakyanjala amesema kuwa takwimu zinaonyesha waliosajiliwa kwa alama za vidole ni zaidi ya milioni 18 na zoezi linaendelea.

  Amesema kuwa serikali imewekeza fedha kwa ajili ya Wananchi wajisajili kwa mfumo wa alama za vidole.Mwakyanjala amesema TCRA iko karibu katika kuratibu ili asiweze kuachwa nyuma mtu asisajiliwe labda itokee kwa mtu mwenyewe kuwa na matatizo mbalimbali ikiwemo ya kiafya.

  Mwakyanjala amesema wanafanya Kampeni katika vyombo vya habari katika kila Mkoa ili kila mtu kuweza kupata taarifa za usajili wa alama za vidole.

  Nae Mratibu wa Shughuli za Usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Wales Maisha amesema wanakumbana na Wananchi kujisajili mara mbili kwa majina tofauti.

  Amesema kuwa wanaongeza nguvu katika usajili ili kuhakikisha kila mtu anapata kitambulisho cha taifa kwa kufuata taratibu zilizowekwa.

  Wananchi wakiwa katika foleni ya kuhudumiwa namba za vitambulisho vya Taifa katika mfumo wa Mamlaka hiyo
  KatibuTawala Msaidizi wa Mkoa wa Lindi Dkt.Bora Haule akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi wakati wa Uhamasishaji wa Usajili laini simu kwa alama za vidole uliofanyika katika uwanja wa Ofisi Manispaa ya Lindi.
  Mratibu wa Shughuli za Usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Mkoa wa Lindi Wales Maisha akizungumza kuhusiana namna wanavyowafikia Wananchi katika usajili huo pamoja na kukutana na changamoto Wananchi kujisajili zaidi ya mara mbili uwanja Fisi Manispaa ya Lindi.
  Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Semu Mwakyanjala akizungumza na Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Karibu Tawala Msaidizi Dkt.Bora Haule mara baada kufungua usajili wa laini za simu kwa alama za vidole katika uwanja Fisi Manispaa ya Lindi.
  Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Semu Mwakyanjala akizungumza na waandishi habari kuhusiana na mamlaka hiyo ilivyojipanga katika kutoa elimu ya usajili wa laini simu kwa alama za vidole tangu walivyotangaza usajili huo
  Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Semu Mwakyanjala akizungumza na Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Karibu Tawala Msaidizi Dkt.Bora Haule mara baada kufungua usajili wa laini za simu kwa alama za vidole katika uwanja Fisi Manispaa ya Lindi.

  Wananchi wakiwa katika foleni ya kupata namba au vitambulisho vya Taifa kwa ajili ya kusajili laini za simu kwa alama za vidole. 

older | 1 | .... | 1894 | 1895 | (Page 1896) | 1897 | 1898 | .... | 1904 | newer