Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live

RAIS DK.MAGUFULI APOKEA GAWIO LA SH.BILIONI 11 KWA MWAKA 2018 KUTOKA PUMA ENERGY TANZANIA

$
0
0
KAMPUNI ya Mafuta ya Puma Tanzania imetangaza gawio la Sh.bilioni 22 kwa wanahisa wake kwa mwaka 2019 ambapo leo Novemba 24 imekabidhi gawio la Sh.bilioni 11 kwa Rais Dk.John Magufuli Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.

Taarifa ya Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari imefafanua kwa kina kuwa kampuni inamilikiwa kwa pamoja na serikali (Kupitia Msajili wa Hazina, Wizara ya Fedha) pamoja na Puma Investments Limited, kila moja ikiwa na umiliki wa hisa kwa asilimia 50. 

Kampuni ya Puma ni ya mkondo wa kati kimataifa katika masula ya mafuta na pia kampuni ya mafuta inayojihusisha na uhifadhi mkubwa na usambazaji.

Imeelezwa kuwa majukumu makuu ya kampuni ni masoko na usambazaji wa bidhaa za petroli ndani ya Tanzania. Kampuni inauwezo wa kuhifadhi jumla ya lita za mafuta 94 milion, vituo 52 vya mafuta maeneo mbalimbali nchini na inahudumia viwanja vinane vya ndege.

Taarifa hiyo imesema kufikia mwisho wa mwaka ulioishia Desemba 31 2018 kampuni ilitengeneza faida kabla ya kodi ya jumla ya Shilingi bilioni 25. Kampuni iliwekeza takribani shilingi bilioni 16 kwa mwaka 2018 kununua na kuendeleza miundombinu ikiwemo ukamilishwaji wa mfumo wa kujazia mafuta katika jengo namba Tatu (Termina 3) katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Dar e salaam.

Pia ununuzi wa vituo viwili vya mafuta kwenye jiji la Dodoma ikiwa ni kuiunga serekali mkono katika kuhamia Dodoma.

"Wakurugenzi wa kampuni wamependekeza gawio la Sh.bilioni 22 bolioni kwa mwaka ulioishia Disemba 2018. Hivyo Kila mwanahisa atapata shilingi 11 bilioni. (2017 gawio lilikuwa 18 bilioni, 2016 gawio lilikua 14 bilioni na 2015 gawio lilikua 9 bilioni.) 

"Kutokana na utendaji mzuri wa kampuni ya Puma Energy, gawio limekua kwa asilimia 57 ikilinganishwa na gawio la mwaka 2016 na kwa asilimia 22 ikilinganishwa na gawio na mwaka 2017. 

"Ukuaji huu unaendana sambamba na mikakati ya kampuni ya kuhakiksha kampuni inaendelea kukua, kutengeneza faida, kukuza ajira nchini, kuchangia pato la taifa kupitia kodi, na kuendelea kuiunga serekali mkono katika kuwaletea wananchi wa Tanzania maendeleo,"imesema taarifa hiyo

Dominic Dhanah, Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania Limited amesema kuwa ufanisi wa kibiashara wa Puma Energy Tanzania kwa mwaka 2018 ulikua mzuri kwa pande zote za mauzo pamoja na mapato. Ufanisi wetu mkubwa unatokana zaidi na biashara ya mafuta ya ndege ambako kwa sasa sisi ndio tunaongoza katika soko. 

Pia ameongeza kuwa taaarifa za masoko zilizochapishwa na Mamlaka ya udhibiti (EWURA) inaonesha kuwa uwepo wa Puma Energy kwenye soko la mafuta umeongezeka kutoka asilimia 12% mwaka 2015 hadi asilimia 14 kwa mwaka 2017

Dhanah pia amepongeza juhudi za serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na rais Dkt John Pombe Magufuli na Serikali yake katika mikakati yake ya kukusanya kodi, kutoa fursa kwa wawekezaji wa nje na ndani na kuanzisha miradi mikubwa ya kimkakati kama ilivyooneshwa kwenye bajeti ya 2019/20. 

Amesema kuwa mikakati hiyo imewezesha PumaEnergy Tanzania kupata kazi ya kuuza mafuta katika mradi wa reli ya kati “standa gauge”, mradi wa bwawa la umeme la Mwl. Nyerere kule Rufiji, Daraja jipya la Salender na miradi mingine mingi ya kimkakati.

" Miradi hii mikubwa inatoa fursa kwa wawekezaji mbali mbali kufanya biashara na kufanya makampuni mengi ikiwemo Puma kutengeneza faida zaidi. Puma itaendelea kufanya kazi kwa ukaribu zaidi na Serikali ya Awamu ya tano, na kuendelea kuchangia katika maendeleo ya taifa, hivyo uongozi wa Puma Energy utaendelea kutoa ushrikiano kama ambavyo wamekua wakishirikiana siku zote.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipokea mfano wa hundi ya gawio yenye thamani ya Bilioni 11 kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Mafuta ya PUMA Energy Tanzania Dkt Selemani Majige (wa pili kushoto) akiwa pamoja na Ofisa Mawasiliano na Mwanasheria wa Kampuni hiyo Goodluck Shirima (kulia). Gawio hilo limekabidhiwa leo Ikulu Chamwino, Jijini Dodoma. Katikati ni Spika wa Bunge, Job Ndugai na kushoto ni Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania Selemani Majige(wa kwanza kulia) akiwa na wageni wengine waalikwa wakati wa tukio la kampuni,mashirika na Taasisi zikabidhi gawio kwa Serikali ambapo Rais Magufuli amepokea gawio leo Novemba 24,2019 Ikulu Chamwino jijini Dodoma
Godluck Shirima kutoka Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania(wa kwanza kushoto) akifuatilia hotuba ya Rais Dk.John Magufuli wakati wa ghafla ya Taasisi, Mashirika na Kampuni kukabidhi gawio kwa Serikali,ambapo Kampuni ya Puma amekabidhi gawio la Sh.bilioni 11 kwa Rais Magufuli leo Novemba 24,Ikulu ya Chamwino Mjini Dodoma
 Rais Dk.John Magufuli akiwa na viongozi mbalimbali wa Taasisi,Mashirika na Kampuni baada ya tukio la kukabidhiwa kwa gawio iliyofanyika leo Novemba 24 Ikulu Mjini Dodoma

NMB YAANDAA KONGAMANO LA SOKO LA HISA NA DHAMANA ZA SERIKALI KWA WEWEKEZAJI

$
0
0
 Meneja wa Masoko ya Fedha kutoka Benki Kuu (BoT), Bw. Lameck Kakulu (wa kwanza kulia) akielezea kuhusu soko la hisa Tanzania kwa wawekezaji mbalimbali wakati wa kongamano lililoratibiwa na Benki ya NMB jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Mkurugenzi wa utafiti, Sera na Mipango wa Mamlaka ya Masoko na Mitaji (CMSA), Alfred Mkombo, Meneja Mwandamizi wa huduma za Dhamana kutoka NMB, Bw. Avith Massawe na Mkurugenzi Mtendaji wa FIMCO Bw Ivan Tarimo.  
 Mweka Hazina wa Benki ya NMB, Aziz Chacha akiongea na wawekezaji wa Soko la Hisa na Dhamana za Serikali kuhusu huduma mpya ya uhifadhi wa dhamana na usimamizi wa uwekezaji katika masoko ya mitaji wakati wa kongamano lililoratibiwa na Benki ya NMB jijini Dar es Salaam.
Meneja Mwandamizi wa Huduma za Dhamana kutoka NMB, Bw. Avith Massawe akiwafunda wawekezaji wa soko la hisa na dhamana za serikali wakati wa kongamano hilo.

Zawadi zenye thamani ya zaidi ya 500m/- kutolewa kwa washindi

$
0
0

Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa-Tigo Pesa, James Sumari akizindua kampeni iitwayo kishindo cha funga mwaka, kwaajili ya wateja wanao tumia Tigo Pesa. kushoto ni Meneja wa Wateja Maalum-Tigo Pesa, Mary Rutta.
Meneja wa Wateja Maalum-Tigo Pesa, Mary Rutta akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kampeni iitwayo kishindo cha funga mwaka, kwaajili ya wateja wanao tumia Tigo Pesa Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa-Tigo Pesa, James Sumari


Kampuni ya Tigo, kupitia kitengo cha Tigo Pesa imezindua kampeni ijulikanayo kama ‘Kishindo cha Funga Mwaka’ kwa ajili ya kutoa zawadi zenye thamani ya zaidi ya 500m/- kwa wateja wa Tigo wanaoweka na kupokea pesa kwenye akaunti zao za Tigo Pesa.

Wateja wa Tigo wanatakiwa kuweka pesa kwenye akaunti zao za Tigo Pesa ili kuweza kushiriki kwenye kampeni hiyo ambayo ni maalumu kwa ajili ya msimu huu wa kufunga mwaka ambapo washindi wa zawadi watafunga mwaka kwa kishindo

Kampeni hiyo itakayodumu kwa kipindi cha mwezi mmoja itashuhudia washindi watatu wakiibuka na fedha taslimu ikiwamo 20m/- kwa mshindi wa kwanza, 15m/- kwa mshindi wa pili na 10/- kwa mshindi wa tatu. Pia, kila wiki kutakua na washindi nane watakaopata 5m/- kila mmoja. Pamoja na washindi wa wiki na wa mwezi, kutakua na washindi nane kila siku ambao wataibuka na 1m/- kila mmoja.

“Wateja wanatakiwa kuweka pesa kwa Wakala au kupokea pesa kwenye akaunti zao za Tigo Pesa kutoka benki, mitandao mingine au vyanzo vingine mbalimbali na moja kwa moja watakuwa kwenye nafasi ya kushinda. Hakuna gharama yoyote ya kuweka au kupokea pesa kwa Tigo Pesa,” alisema Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa - Tigo Pesa, James Sumari, wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo.

Kwenye kampeni hii hakuna masharti ya kushiriki kwa mteja wa Tigo Pesa isipokuwa; kadiri unavyoweka pesa nyingi ndivyo unajiweka kwenye nafasi nzuri zaidi ya kushinda.

“Tunategemea kupata washindi wapatao 331 ndani ya kipindi cha mwezi mmoja na wiki moja wa kampeni yetu na lengo kubwa ni kuonesha na kurudisha shukrani kwa wateja wetu kwa kuwa pamoja na Tigo Pesa kwa kipindi cha mwaka mzima,” alisema Sumari.

Huduma ya Tigo Pesa imeendelea kuwa mstari wa mbele katika ubunifu, na kuongeza huduma na bidhaa bora zaidi ikiwamo kutoa mikopo, huduma za bima na huduma kwa makampuni na taasisi zinazowezesha kulipa na kukusanya pesa kwa ufanisi jambo linaloifanya Tigo Pesa kuwa huduma kamili ya kifedha ikiwa na mawakala zaidi ya 150,000 nchi nzima.

BENKI YA BIASHARA NA MAENDELEO tdb YAAHIDI KUSHIRIKIANA NA TANZANIA KATIKA KUKUZA MAENDELEO

$
0
0
Na Benny Mwaipaja, Dodoma

RAIS wa Benki ya Biashara na Maendeleo Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB) Dkt. Admassu Tadesse ameahidi kuwa Benki yake itaendelea kushirikiana na Tanzania kwa kuipatia mikopo yenye masharti nafuu kwa ajili ya kutekeleza miradi yake ya kimkakati ya maendeleo kwa sababu uchumi wake uko imara na inakopesheka

Dkt. Tadesse ametoa ahadi hiyo Jijini Dodoma alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango ambapo wawili hao wamezungumzia masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Serikali na Benki hiyo hususan Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) na ujenzi wa mradi wa kufua umeme kwa njia ya maporomoko ya maji ya mto Ruhudji mkoani Njombe

Amesema kuwa miezi michache iliyopita Benki yake imeipatia Tanzania mkopo wenye masharti nafuu wa dola bilioni 1 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kipaumbele inayotekelezwa na Serikali na kwamba wako mbioni kutoa kiasi kingine kikubwa cha fedha hivi karibuni.

Kwa upande wake Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango amesema kuwa Benki hiyo ya Biashara na Maendeleo Mashariki na Kusini mwa Afrika TDB imekuwa mdau muhimu katika maendeleo ya Taifa na kwamba pamoja na kiasi cha dola bilioni moja kilichopokelewa na Serikali mwezi Agosti Mwa huu 2019, Serikali inatarajia kupata kiasi kingine cha dola milioni 300.

Amesema kuwa kiasi hicho cha fedha kitaelekezwa katika ujenzi wa miundombinu ya Reli ya Kati ya Kiwango cha Kimataifa (SGR) pamoja na miradi ya kuzalisha nishati ya umeme ili nchi iweze kuimarisha sekta ya uzalishaji viwandani kwa kuwa na umeme wa uhakika.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Dkt. Hamis Mwinyimvua akizunguza wakati wa kikao na Rais huyo wa TDB amesema kuwa amefurahi kwamba Benki hiyo imeonesha nia ya kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa kufua umeme wa Ruhudji (MW 358) wenye thamani ya dola za Marekani milioni 460.2 ambapo kati ya hizo dola milioni 407 zitatumika kujenga mitambo ya kufua umeme na kiasi kingine cha dola milioni 53 kitatumika kujenga njia ya kusafirishia umeme urefu wa km 170.

Alisema kuwa lengo la Serikali ni kuzalisha megawati 10,000 za umeme ifikapo mwaka 2025 na kwamba kutekelezwa kwa mradi huo kutasaidia kufikia azma hiyo ili kuimarisha masuala ya uzalishaji viwandani na uendeshaji wa miundombinu mingine inayotumia nishati hiyo ya umeme.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Masanja Kadogosa amemweleza Rais huyo wa Benki ya Biashara na Maendeleo Mashariki na Kusini mwa Afrika Dkt. Admassu Tadesse kwamba ujenzi wa kipande cha Reli ya Kisasa kati ya Dar es Salaam na Morogoro umefikia asilimia 72 hivi sasa na kuishukuru Benki hiyo kwa utayari wake wa kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa Reli kipande cha Mwanza hadi Isaka.

Tanzania ni mongoni mwa wanahisa 31 wa Benki ya Biashara na Maendeleo Mashariki na Kusini Mwa Afrika (TDB) ambapo hadi kufikia Disemba 31 mwaka 2018, Tanzania ilikuwa imeshika nafasi ya 4 ya uwekezaji katika Benki hiyo ikiwa na asilimia 8.33 ya hisa.

 Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akisalimiana na Rais wa Benki ya Biashara na Maendeleo Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB) Dkt. Amassu Tadesse (kushoto), alipotua katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma akiwa katika ziara yake ya kikazi hapa nchini. Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali Bw. Doto James.
 Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Dkt.  Hamis Mwinyimvua (katikati) akizungumza wakati wa mkutano na Rais wa Benki ya Biashara na  Maendeleo  Mashariki na  Kusini mwa Afrika (TDB) Dkt. Admassu Tadesse (hayupo pichani) kushoto ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Prof.  Florens Luoga na kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James, jijini Dodoma. 
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James akiteta jambo na Rais wa Benki ya Biashara na  Maendeleo  Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB) Dkt. Admassu Tadesse, Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma baada ya kumalizika kwa mkutano kati ya Rais huyo na Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli. 
Rais wa Benki ya Biashara na  Maendeleo  Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB), Dkt. Admassu Tadesse (kulia) akimweleza jambo Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) walipokutana na kufanya mazungumzo, Jijini Dodoma
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James (kulia) na  Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Dkt.  Hamis Mwinyimvua wakisikiliza kwa makini mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea kati ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt Philip Isdor Mpango (Mb) na Rais wa Benki ya Biashara na Maendeleo Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB), Dkt. Admassu Tadesse (hawapo pichani), Jijini Dodoma

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) na Rais wa Benki ya Biashara na  Maendeleo  Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB), Dkt. Admassu Tadesse (kulia), wakifurahia jambo baada ya kumalizika kwa mazungumzo kati ya ujumbe wa Tanzania na Benki hiyo walipokutana Jijini Dodoma.
Ujumbe kutoka Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka Benki ya Biashara na Maendeleo Mashariki na Kusini mwa Afrika ulioongozwa na Rais wa Benki hiyo Dkt. Admassu Tadesse (wa nne kulia) jijini Dodoma.Picha na Josephine Majura WFM – DODOMA).

 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (wa pili kushoto) akiongoza ujumbe wa Tanzania kumpokea Rais wa Benki ya Biashara na  Maendeleo  ya Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB), Dkt. Admassu Tadesse alipowasili Uwanja wa Ndege Jijini Dodoma.

Shule ya Sekondari Orkeeswa ya jijini Arusha yang'ara michezo ya shule za Kimataifa

$
0
0

 Ndajiri Lonyori kutoka shule ya sekondari Orkeeswa akipokea kombe la ushindi wa mchezo wa mpira wa kikapu wa wasichana chini ya miaka 19 wakati wa wikiendi ya michezo kwa shule za kimataifa iliyofanyika mkoani Moshi wikiendi hii. Shule ya sekondary Orkeeswa kutoka mkoani Arusha iliibuka kidedea baada ya kuchota makombe 15 katika michezo mbalimbali iliyoshiriki.
 Ndajiri Lonyori kutoka shule ya sekondari Orkeeswa akionesha kombe lao la ushindi wa mchezo wa netball chini ya miaka 15 wakati wa wikiendi ya michezo kwa shule za kimataifa iliyofanyika mkoani Moshi wikiendi hii. Shule ya sekondary Orkeeswa kutoka Arusha iliibuka kidedea baada ya kuchota makombe 15 katika michezo mbalimbali iliyoshiriki.
 Amani Isaya kutoka shule ya sekondari Orkeeswa akionesha kombe lao la ushindi wa  mchezo wa volleyball chini ya miaka 19 wakati wa wikiendi ya michezo kwa shule za kimataifa iliyofanyika mkoani Moshi wikiendi hii. Shule ya sekondary Orkeeswa kutoka Arusha iliibuka kidedea baada ya kuchota makombe 15 katika michezo mbalimbali iliyoshiriki. 
Emmanuel Meibuko golikipa wa timu ya shule ya sekondari Orkeeswa akipokea kombe la ushindi wa mpira wa miguu wa wavulana chini ya miaka 19 baada ya kuibuka washindi kwa goli 3 - 2 katika mechi iliyokuwa ngumu sana kwa vijana hao wakati wa wikiendi ya michezo kwa shule za kimataifa iliyofanyika mkoani Moshi wikiendi hii. Shule ya sekondary Orkeeswa kutoka Arusha iliibuka kidedea baada ya kuchota makombe 15 katika michezo mbalimbali iliyoshiriki. 


Shule ya Sekondari Orkeeswa iliyopo mkoani Arusha iliibuka kidedea baada ya kuchota makombe 15 katika michezo mbalimbali ya Shule za Kimataifa. 
Shule hizo kutoka mikoa mbalimbali nchini zilikutana mkoani Kilimanjaro na kuchuana vikali katika michezo ikiwemo mpira wa kikapu, mpira wa miguu, tennis, swimmings, netball, volleyball, frisbie, rugby na michezo mingineyo. 
Timu za kikapu U19 wasichana na U19 wavulana pamoja na timu ya mpira wa miguu ya shule hiyo zilionekana kuwa imara zaidi baada ya kushinda kwa kishindo timu za shule mbalimbali zilizo pambana nao. 
Shule za kimataifa nchini zilikuwa na wikiendi ya michezo iliyoanza mwishoni mwa wiki,Ijumaa na kufikia tamati Jumapili.

TCRA YAKABIDHI VIFAA VYA TEHAMA SHULE YA SEKONDARI KIBAHA

$
0
0

Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka hiyo Mhandisi Lawi Odiero (mwenye miwani) akimkabidhi Mkuu wa Shule ya Sekondari Kibaha Chrisdome Ambilikile hati ya vifaa vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) viliyotolewa na TCRA katika hafla kiliyofanyika shuleni hapo Kibaha mkoani Pwani.
Mwakilishi ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani ,Katibu Tawala Msaidizi Abdulahman Mdimu akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya vifaa vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) vilivyotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa Shule ya Sekondari Kibaha iliyofanyika shuleni hapo Kibaha mkoani Pwani.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka hiyo Mhandisi Lawi Odiero akizungumza kuhusiana na vigezo vilivyotumika TCRA kutoa vifaa vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama)katika Shule ya Sekondari Kibaha.
Mkuu wa Shule ya Sekondari wa Kibaha Chrisdome Ambilikile akizungumza kuhusiana na msaada wa vifaa vya Tehama katika shule hiyo katika hafla ilyofanyika shuleni hapo.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Fredrick Ntobi akitoa maelezo kuhusiana na utaratibu wa utoaji wa vifaa vya Tehama kwa Mamlaka hiyo katika shule ya Sekondari.
Mwanafunzi wa Kidato cha Sita wa Shule ya Sekondari Kibaha Samuel Makoye akitoa maelezo kuhusiana na msaada wa vifaa vya Tehama waliopewa katika shule hiyo.
Picha kati ya TCRA,Wanafunzi ,Walimu pamoja na viongozi wa serikali Mkoa wa Pwani 

************************************

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)imesema kuwa itaendelea kusaidia vifaa mbalimbali vya Tekonolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) kwa shule za sekondari zinazofanya vizuri katika matokeo ya mitihani ya kitaifa ili kuweza kuwaanda vijana kuendana na mabadiliko ya sayanasi na teknolojia .

Akizungumza na mara baada ya kukabidhi vifaa mbalimbali vya Tehama Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka, Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka hiyo Mhandisi Lawi Odiero amesema kuwa vifaa vya Tehama wanavitoa kwa shule zinazofanya vizuri katika matokeo kidato cha Nne na Tano ambapo ni Kibaha sekondari ni miongoni mwa shule zilizofanya vizuri .

Amesema kuwa vifaa hivyo vitachochea shule hiyo kuendelea kufanya vizuri kwani vitabu mbalimbali vinapatikana katika mitandao ikiwemo na marejemeo mengineyo kwani dunia ndio inakwenda huko.

“Hatutarajii kuona vijana wetu mnatumia vifaa vya Tehama kinyume sheria kwani sheria mtandaoni imeanisha makosa hivyo wanafunzi mtakuwa watu wa kutumia Tehama katika maendeleo ya kufanya vizuri kwa kuendeleza rekodi ya shule ya sekondari Kibaha”amesema Odiero.

Nae Mgeni rasmi Mwakilishi wa Matibu Tawala wa Mkoa Abdulahman Mdimu amesema kuwa wanashukuru kwa msaada waliotoa TCRA na wanafunzi kutunza vifaa hivyo.

Amesema kuwa shule ya Sekondari Kibaha kutokana na kupata kigezo cha kupata vifaa vya Tehama kuongeza juhudi zaidi kwani kuna shule shindani nazo zinahitaji vifaa hivyo.

Mkuu wa Shule ya Sekondari Kibaha Chrisdome Ambilikile amesema kuwa kutokana na kukua kwa Tehama sasa tunatakiwa kuondokana mfumo wa ufundishaji wa vitabu na daftari ambapo nchi zingine zilishaanza ufundishaji huo.

Amesema kuwa shule inajenga jengo kubwa pamoja na kuweka vyumba vya Tehama ili kukidhi mahitaji ya wanafunzi waliopo katika shule hiyo na kuongeza kuwa TCRA kuendelea kuingalia shule hiyo kwa jicho linguine kwa kuwaongeza vifaa vvya Tehama.

Mwanafunzi wa Kidoto cha Sita Samuel Makoye amesema kuwa dunia ya sasa imekwenda na mabadiliko mbalimbali ya ya Tehama ambapo wanafunzi lazima tufuate tekonolojia hiyo.

kwani kutumia tofauti na matarajio ni hasara kwani na mtakuwa

WATANZANIA KUNUFAIKA NA OFA KABAMBE ZA BLACK FRIDAY KUPITIA VODACOM M-PESA

$
0
0
Meneja masoko wa Vodacom M-Pesa, Noel Mazoya (wa kwanza kushoto) akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar Es Salaam kuhusu ofa ya hadi asilimia 10 itakayotolewa na Kampuni ya Vodacom tarehe 29 wiki hii,siku maarufu duniani kwa manunuzi ya bidhaa kwenye maduka na mtandaoni ijulikanayo kama BLACK FRIDAY. Wateja wa Vodacom watalipa kupitia huduma za LIPA KWA SIMU na M-PESA MASTERCARD na watarudishiwa hadi asilimia 10 papo hapo wakilipa kupitia mtandao wowote kwenye maduka mbalimbali yaliyopo kwenye malls tofauti nchini. Wengine kwenye picha, wapili toka kushoto ni Meneja Uendeshaji wa Mr Price Tanzania, Paul Namuhisa, Meneja wa Easybuy Africa, Juliana Siyame na Meneja wa malipo kwa njia ya Mtandao Vodacom, Loius Maro.
Meneja masoko wa Vodacom M-Pesa, Noel Mazoya akiwa kwenye picha ya pamoja na Meneja Uendeshaji wa Mr Price Tanzania, Paul Namuhisa, Meneja wa Easybuy Africa, Juliana Siyame na Meneja wa malipo kwa njia ya Mtandao Vodacom, Loius Maro, mara baada ya kutangaza ofa maalum ya BLACK FRIDAY itakayotolewa siku ya ijumaa wiki hii 
Baadhi ya warembo watakaohudumia wateja kwenye maduka mbalimbali yaliyoorodheshwa kote nchini siku ya ijumaa kwenye ofa ya BLACK FRIDAY.

…………….
Wateja kurudishiwa hadi 10% ya gharama za malipo siku hiyo.

Kampuni ya Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na wafanyabiashara mbalimbali nchini imezindua kampeni kabambe inayowawezesha wateja wake kufurahia punguzo kubwa wanapofanya malipo kupitia huduma yake ya M-Pesa. Kampeni hiyo iliyoziduliwa jijini Dar es salaam inalenga kuongeza matumizi ya huduma za kidigitali kwenye kufanya malipo hasa kwenye kipindi hiki cha BLACK FRIDAY, siku maarufu duniani kwa manunuzi ya bidhaa kwenye maduka na mtandaoni. 

Kupitia huduma zake mbili za LIPA KWA SIMU na M-PESA MASTERCARD Vodacom M-Pesa wanawawezesha watanzania kufanya malipo kwa wafanyabiashara ndani ya nchi na mitandaoni kupitia simu zao na kurudishiwa hadi 10% ya gharama za malipo siku hiyo ya BLACK FRIDAY ambayo kwa mwaka 2019 itakuwa ijumaa tarehe 29 Novemba.

Meneja masoko wa Vodacom M-Pesa, Noel Mazoya alisema, ‘Black Friday hii tumeandaa ofa ya hadi asilimia 10 ya gharama ambayo wateja wetu watalipa kupitia huduma za LIPA KWA SIMU na M-PESA MASTERCARD. Kupitia huduma ya LIPA KWA SIMU, M-Pesa tutawarudishia hadi asilimia 10 papo hapo wakilipa kupitia mtandao wowote kwenye maduka mbalimbali yaliyopo kwenye malls tofauti nchini. Baadi ya maduka ni kama ifuatavyo kwa Dar es salaam: Mlimani city (Mr Price, Just Fit sports gear, Atsoko, Cassandra Julac, Joo Africa na Vodashop Mlimani, Dar Free Market (Home of events, Zurii house of beauty, Vodacom service desk) City Mall (Kanzu Point, Ley Jewerly, G Best Zone), Rock City Mall Mwanza (Street Soul, Chief Empire Classic, Café Mambo, Upendo Unique beauty shop na Vodashop Rock City) na Aim Mall Arusha (Street Soul, Supa Clean) na mengine mengi. Wauzaji pia watatoa punguzo kabambe la Black Friday. 

Meneja uendeshaji wa Mr Price Tanzania Paul Namuhisa alisema ‘Tunafurahi kushirikiana na Vodacom katika kampeni hii. Pamoja na punguzo la hadi asilima 10 ukinunua bidhaa kupitia M-Pesa, Tunatoa punguzo la asilimia 20 kwa manunizi ya bidhaa kwa siku hiyo, huu ni muendelezo wa utamaduni wetu wa kuleta kitu kipya kwa wateja wetu kila siku’


Kwa Upande mwingine, Vodacom kwa ushikiriano na Easybuy Africa itawarudishia wateja hadi asilimia 10 ya kiasi watakacholipa kwa M-PESA MASTERCARD kupitia tovuti ya www.easybuyAfrica.com. Wateja watarudishiwa hadi asilimia 10 wakifanya shopping kutoka mitandao kama Amazon.com, eBay, H&M, Walmart, GAP, Fashionova n.k kupitia EasyBuyAfrica.com na kulipa kwa M-PESA MASTERCARD. Pia watafurahia punguzo la hadi asilimia 10 ya oda zao kutoka EasyBuy pamoja na discount za hadi asilimia 85 kutoka tovuti husika siku ya BlackFriday.

Meneja wa Easybuy Africa, Juliana Siyame alisema, ‘Easybuyafrica inawezesha wateja kununua bidhaa yoyote wanayohitaji kutoka mitandao tofauti duniani na kuwaletea popote walipo Tanzania. Kipindi hiki cha Black Friday tunawawezesha kufurahia huduma zetu kukiwa na punguzo kubwa kwenye bidhaa tofauti pamoja na ofa maalum ya 10% discount wakiagiza nasi ijumaa hii tarehe 29. Ushikiriano wetu na M-Pesa Mastercard umeaongeza faida zaidi kwa wateja wetu kwa kuwapa njia salama ya kulipa mtandaoni’

Wateja ambao bado hawana M-Pesa Mastercard wanaweza kutengeneza kadi zao kwenye menyu ya M-Pesa kwa kupiga *150*00# >Chagua Lipa kwa M-Pesa > Chagua M-Pesa Mastercard kisha > Tengeneza Kadi. Baada ya hapo watapata namba ya kadi, code ya CVV na tarehe ya mwisho wa matumizi, taarifa zinazohitajika kwenye malipo mtandaoni.

MSAKO WA MISS UTALII KIKANDA KUANDA DESEMA,2019

$
0
0
 Rais wa shindano miss Utalii, Gideon Chipungahelo akizungumza wakati wa semina ya kuwajengea uwezo wahariri na waandishi wa habari, katika hoteli ya kitalii ya Jaromax iliyopo Manzese jijini Dar es Salaam. Amesema kuwa Shindano la Mlimbwende wa utalii tukitaka mabadiliko katika urembo ni lazima kufanya mambo mazuri zaidi ya urembo na kuwawezesha washiriki kuwa na maarifa mengi ya masuala ya Utalii.
 Baadhi ya Walimbwende wa 2013 na 2014 walioshiriki katika Shindano waliohudhulia semina ya waandano la Miss Utalii.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Costantine Kanyasu akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa Shindano la kutafuta mlimwende katika utalii (Miss Tourism), katika Hoteli ya Kitalii ya Jaromax iliyopo Manzese jijini Dar es Salaam.

 Afisa sanaa wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), Bona Masenge akizungumza wakati wa semina ya kuwajengea uwezo wahariri na waandishi wa vyomo vya haari jijini Dar es Salaam katika hoteli ya kitalii ya Jaromax iliyopo Mazese jijini Dar es Salaam.

 Rais wa Sanaa za Maonesho, Wilium Chitanda akizungumza wakati wa Semina ya kuwajengea uwezo wahariri na waandishi wa vyombo vya habari hapa nchini kwaajili ya kuandika habari za Miss Utalii kwa uelewa zaidi. Semina hiyo imefanyika katika Hoteli ya Kitalii ya Jaromax iliyopo Manzese jijini Dar es Salaam.
 Rais wa shirikisho la Sanaa za Ufundi Tanzania(TAFCA), Adrian Nyangamawe akizungumza katika semina ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari katika habari za mlimbwende wa Utalii (Miss Tourism) katika semina iliyofanyika hoteli ya Kitalii ya Jaromax iliyopo Mazese jijini Dar es Salaam.


 Baadhi ya Walimbwende wa 2013 na 2014 walioshiriki katika Shindano waliohudhulia semina ya waandano la Miss Utalii.
Moja ya watoa Mada katika Semina ya kuwajengea uwezo wahariri na waandishi wa habari.

MCHAKATO wa usaili wa kumtafuta mlimbwende wa urembo katika utalii (Miss Tourism) kuanza Desemba, 2019.

Akizungumza na wakati wa semina ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari katika hoteli ya kitalii ya Jaromax iliyopo Manzese jijini Dar es Salaam, Afisa sanaa wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), Bona Masenge, amesema kuwa shindano la Mlimbwende katika utalii litaambatana na kutembelea vivutio vilivyopo hapa nchini.

 Bona amesema kuwa BASATA imewaamini waandaaji wa Shindano la Miss utalii kwani kunavigezo mbalimbali ambavyo wamekidhi vya kikanuni, kisheria na kwaajili ya kuandaa shindano hilo.

"Baraza la sanaa Tanzania (BASATA) linahusika na mashindano haya kwa ukaribu ili kuhakikisha waandaaji wa mashindano haya wanakidhi vigezo na kufata taratibu na sheria zilizowekwa na Baraza".
 Amesema Bona

Bona amesema kuwa Shindano la Mlimbwende wa Utalii limeweza kuwapa ajira za kudumu vijana kwa kuinua vipaji vya  vijana wengi na kukuza utalii hapa nchini.

"Mashindano ya mlimbwende wa Utalii yameweza kuinua vipaji kwa washiriki na baadhi wameweza kupata ajira za kudumu na yameweza kukuza utalii kitaifa na kimataifa".

Kwa upande wake Rais wa shindano la miss Utalii, Gideon Chipungahelo amesema kuwa Shindano la Mlimbwende wa utalii tukitaka mabadiliko katika urembo ni lazima kufanya mambo mazuri zaidi ya urembo na kuwawezesha washiriki kuwa na maarifa mengi ya masuala ya Utalii.
Amesema watakaohitaji kushiriki Mahindano hayo wakae mkao wa kula kwani tunata yanayotakiwa ni Mapinduzi Makuwa katika tasnia nchini.

"Miss yourism Tanzania (Mlimbwende wa utalii Tanzania) historia yake kabla na baada ya uhuru shindano la kwanza la kupata mshindi wa dunia katika ulimbwende wa Utalii. 
Amesema Chipunagahelo.


Hata hivyo mchakato huo wa kutafuta Mlimbwende katika utalii utachukua zaidi ya Miezi sita ili kuwapa muda majaji kufanya kazi ya kutafuta Mrembo anayekidhi vigezo vyote na atakayetuwakilisha duniani na kutuletea taji la dunia hapa nchini.

NSSF, NHC, WHC KAMILISHENI MIRADI YA NYUMBA KIGAMBONI -MAJALIWA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifafanuliwa jambo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Vijana, Kazi na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, wakati akikagua mradi wa nyumba za NSSF, zilizopo Tuangoma katika Wilaya ya Kigamboni, jijini Dar es Salaam, Novemba 27, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akizungumza na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, wakati alipotembelea mradi wa nyumba za NHC, zilizopo Mtoni Kijichi katika Wilaya ya Kigamboni, jijini Dar es Salaam, Novemba 27, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)




Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi wa NSSF, Balozi Alli Siwa, wakati alipokagua Miradi ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Taifa na Shirika la Nyumba la Taifa ya Ujenzi wa nyumba Tuangoma, Mtoni Kijichi na Dungu, Novemba 27, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mradi wa nyumba za NSSF, zilizopo Tuangoma katika Wilaya ya Kigamboni, jijini Dar es Salaam, Novemba 27, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akioneshwa jambo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Vijana, Kazi na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, wakati akikagua mradi wa nyumba za NSSF, zilizopo Tuangoma katika Wilaya ya Kigamboni, jijini Dar es Salaam, Novemba 27, 2019. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiwasalimia Watoto wa Chekechea wa Shule ya Kids Paradise, iliyopo ndani ya Mradi wa Nyumba za NHC, Mtoni Kijichi wilayani Kigamboni, jijini Dar es Salaam, wakati alipokagua Miradi ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Taifa na Shirika la Nyumba la Taifa ya Ujenzi wa nyumba Tuangoma, Mtoni Kijichi na Dungu, Novemba 27, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mradi wa nyumba za Watumishi Housing, uliyopo Dege wilayani Kigamboni, jijini Dar es Salaam, Novemba 27, 2019. 
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mradi wa nyumba za Watumishi Housing, uliyopo Dege wilayani Kigamboni, jijini Dar es Salaam, Novemba 27, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

****************************************

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema nyumba zote zinazojengwa na Taasisi za Umma katika wilaya Kigamboni jijini Dar es salaam zinapaswa kukamilika haraka ili ziuzwe ua kupangishwa kama ilivyokusudiwa.

Ameyasema hayo leo (Jumatano, Novemba 27, 2019) baada ya kukagua miradi ya ujenzi wa nyumba za NSSF, NHC na Watumishi Housing iliyopo katika wilaya ya Kigamboni.

Waziri Mkuu amesema inasikitisha kuona kwamba watumishi wa umma na wananchi jijini Dar es Salaam hawana nyumba nzuri za kuishi wakati zipo nyumba nyingi nzuri zimejengwa na zinahitahi umaliziaji mdogo tu ili ziweze kukalika.

Hivyo, Waziri Mkuu ameitaka Menejimenti ya NSSF kakamilisha haraka ujenzi na uwekaji wa miundombinu ya umeme, maji safi na maji taka katika nyumba zake 161 zilizoko Tuangoma, 820 zilizoko Mtoni Kijichi na 439 zilizoko Dungu ili ziuzwe na kuepusha uwezekano wa uharibifu unaoweza kutokea kwa nyumba hizo kakaa muda mrefu bila kupata wanunuzi au wapangaji.

Ili kufanikisha jambo hilo Mheshimiwa Majaliwa amemtaka Mthamini Mkuu wa Serikali atathimini nyumba hizo na kutoa bei halisi ya soko kwa sasa ili kuwawezesha Watanzania wengi na hasa watumishi wa Umma kununua na kupanga katika nyumba hizo.

Pia, Waziri Mkuu amemtaka Mkuu wa wilaya na viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Kigamboni kuwasaidia watumishi wa wilaya na Halmashauri hiyo kuingia mikataba rafiki itakayowawezesha watumishi hao kupewa kipaumbele katika kununua au kupanga kwenye nyumba hizo.

Mheshimiwa Majaliwa pia ameitaka Menejimenti ya NSSF kufikiria namna ya kuzungumza na viongozi wa vyuo mabalimbali kama vile Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Chuo cha Mwalimu Nyerere ili wanafunzi wa vyuo hivyo wapatiwe fursa ya kupanga katika nyumba hizo kwa bei watakazomudu.

Pia Mheshimiwa Majaliwa ameuagiza uongozi wa Mkoa wa Dar es salaam ukishirikiana na SUMATRA kuanzisha njia za mabasi ya daladala zitakazoanzia au kupitia kwenye nyumba za NSSF Mtoni Kijichi na Dungu ili kuwezesha wapangaji na wananchi watakaonunua nyumba hizo kupata usafiri wa umma. 

Vilevile, Waziri Mkuu ameuagiaza uongozi huo kuhakikisha kwamba eneo la Mtoni Kijichi zilipojengwa nyumba za NSSF na NHC linapata huduma za Shule, Kituo cha Afya na Kituo cha Polisi kwani litakuwa na wakazi wengi .

Ili kuongeza thamani ya nyumba hizo na kuvutia wapangaji na wanunuzi, Mheshimiwa Majaliwa ameitaka Menejimenti ya NSSF kuboresha barabara kwenye mitaa yote zilipojengwa nyumba hizo kwa kushirikiana na TARURA.

“Nashauri ziwekwe taa za sola kwenye barabara za mitaa yote ya nyumba hizi ili kupendezesha eneo na kuwafanya wananchi wahamasike kununua na kuishi katika nyumba hizi” amesema Majaliwa.

Akiwa kwenye Mradi wa Nyumba za NHC Mtoni Kijichi, Mheshimiwa Majaliwa alitembelea Shule ya Awali ya Kids Paradise na kufurahishwa na utaratibu mzuri wa shirika hilo wa kukumbuka kujenga jengo zuri la Shule hiyo na kulipangisha ili kuhakikisha kwamba watoto wanaoishi katika nyumba hizo wanapata fursa ya kusoma elimu ya awali.

Akizungumza baada ya kukagua Mradi wa ujenzi wa nyumba za NHC Mwongozo, Mheshimiwa Majaliwa ameutaka uongozi wa NHC kuwa karibu na wateja wanaopanga au kununua nyumba zao. “ Shughulikieni malalamiko yote yanayotolewa na wateja wenu ili wajenge imani kwenu, Alisisitiza Majaliwa.

Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama alisema wizara yake imeyapokea maelekezo yote yaliyotolewa na Waziri Mkuu na kwamba watafanya kila njia ili kuhakikisha kwamba majengo yote yanakamilika haraka na kuuzwa au kupangishwa.

Naye Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi, william Lukuvi alimwambia Waziri Mkuu kuwa amekwishatoa maagizo kwa NHC ijenge uzio japo wa waya na wapande michongoma ili kuweka ulizi kwenye eneo la nyumba zao za Dungu.

Mheshimiwa Lukuvi alisema amewapa NHC miezi mitatu ili wafanye marekebisho katika nyumba ambazo zimelalamikiwa na wateja kuwa zina kasoro ili kujenga imani kwa wateja wao.

Mapemba Mkadiriaji Majengo wa NSSF, Abon Mhando ambaye pia ni Kaimu Meneja wa Miradi wa NSSF alimwambia Waziri Mkuu kuwa Mradi wa ujenzi wa nyumba wa Tuangoma una jumla ya nyumba 161 na kati ya hizo nyumba 76 zimekamilika. Aliwataja wakandarasi wanaojenga mradi huo kuwa ni Kampuni za CASCO, Advent na NANDRA.

Alisema Mradi wa Dungu una jumla ya nyumba 439 na kati ya hizo nyumba 95 zimekamilika na jumla ya makampuni 13 yameshiriki katika ujenzi wa mrdi huo.

Kuhsu mradi wa Mtooni Kijichi Mhando alisema mradi huo una jumla ya nyumba 820 na kati ya hizo nyumba 417 zimekamilika.

Wakazi wa mAKAMBAKO WANUFAIKA NA MAFUNZO YA USAJILI WA LAINI KWA NJIA YA VIDOLE

$
0
0

Afisa Habari Mwandamizi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mabel Masasi akizungumza na Wananchi wa Mji Mdogo wa Makambako wakati wa Kampeni ya Mnada kwa Mnada wa Uhamasishaji wa Wananchi kujisajili laini za simu kwa alama za vidole.
 Wananchi wakiwa katika mstari kupata namba ya kitambulisho cha Taifa ili aweze kusajili laini za simu kwa alama za vidole katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada katika Viwanja vya Idara ya Maji ya Mji Mdogo wa Makambako mkoani Njombe.


 Foleni ya Wananchi wa Mji Mdogo wa Makambako na viungo vyake wakiwa katika mistari ya kupata namba za vitambulisho vya Taifa.
 Mkuu wa Nyanda za Juu Kusini wa TCRA Asajile John akizungumza na Wananchi wa Mji Mdogo wa Makambako wakati wa Kampeni ya Mnada kwa Mnada uliofanyika Idara ya Maji ya Mji huo.
 Mkuu wa Nyanda za Juu Kusini wa TCRA Asajile John akizungumza na Wananchi wa Makambako wakati wa usajili wa laini za simu kwa alama.


WAKAZI wa Makambako mkoani Njombe na viunga vyake  wamejitokeza katika kupata namba za vitambulisho vya Taifa ili kukidhi matakwa ya usajili wa laini za simu kwa alama za vidole.

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA ipo katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada ya  Uhamasishaji wa usajili wa laini za simu kwa alama za vidole.

Kampeni  ya Mnada kwa Mnada ambapo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikishirikiana na Kampuni ya simu, Jeshi la Polisi Kitengo cha Uhalifu Mitandaoni  na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Idara ya Uhamiaji  kwa ajili  ya utoaji wa huduma za usajili wa laini za simu kwa kutumia vitambulisho vya kitaifa na kuhakikiwa na kampuni za simu kwa kuweka alama za vidole kwa laini za simu.

Kampeni tangu imeanzishwa imekwenda katika maeneo ya miji na Mkoa lengo Wananchi kutumia fursa ya kusajili laini za simu kwa alama za vidole ambayo unakwenda nchi nzima

 Mkuu wa Nyanda za Juu Kusini  wa TCRA  Asajile John   amesema ni fursa kwa wananchi wa Mkoa wa Njombe katika Mji Mdogo wa Makambako kufika katika Viwanja vya idara ya maji kupata namba ya kitambulisho cha Taifa katika mfumo wa NIDA.

 Amesema katika Kampeni hiyo imekuwa inafanywa na kanda hiyo ili kila mwananchi aweze kuwa na namba ya vya Taifa au kuwa na kitambulisho kutokana Ushirikiano na NIDA kuwa katika Kampeni hiyo.

John  amesema kuwa  Mnada kwa Mnada TCRA ilianzisha ili kutoa fursa ya Wananchi kuhudumiwa kwa pamoja huduma za mawasiliano pamoja na usajili wa laini za simu kwa alama za vidole.

Amesema Kampeni hiyo ni kuimarisha ulinzi katika  huduma  za simu pamoja kufanya mawasiliano kuwa salama katika nchi na kuongeza kuwa muda ulioabakia ni mdogo hivyo kila mtu atumie kutafuta taarifa zinazokidhi usajili wa laini kwa alama za vidole.

Hata hivyo amesema  kuwa kampeni ya Mnada kwa Mnada ni kwa ajili ya kutoa elimu ya mawasiliano kwa kushirikiana na wadau katika kujibu changamoto wanazokutanazo katika utumiaji wa mawasiliano nchini.

Hata hivyo amesema kuwa
 kuna watu wengine wanatumia mawasiliano ya simu bila kujua ambapo Jeshi Polisi lipo katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada ili kutoa elimu kuhusiana  makosa ya jinai ya matumizi ya simu yasiofuata sheria.

Amesema Kampeni hiyo ni endelevu katika kuwafikia ikiwa kuhakikisha kila mwananchi anajisajili laini yake kwa alama za vidole kwa kutumia kitambulisho cha taifa.

Amesema  TCRA iko kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi ili watumie Mawasiliano kwa usalama kutokana na elimu tunayotoa.

Hata hivyo amesema kuwa wananchi wajitokeze katika kujisajili kwa alama za vidole kabla ya Desemba 31 na muda uliobakia ni mdogo tangu tangazo lilipotolewa.

"TCRA tutahakikisha tunawafikia katika wananchi katika utoaji wa elimu za utumiaji wa bidhaa za mawasiliano kwa kutatua changamoto katika huduma hiyo" amesema.John

Ameongeza kuwa  Kampeni hiyo imeanza kwa Mikoa yote iliyopo katika Nyanda za Juu Kusini.

Kwa upande wa Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa TCRA Mabel Masasi amesema kuwa wananchi wameitikia kwa kujitokeza kwa wingi  kuangalia namba  vitambulisho kwa ajili ya kusajili laini za simu kwa alama za vidole.
Masasi amesema kuwa Wananchi wa watumie Kampeni ya Mnada kwa Mnada ya TCRA kupata elimu na baada ya kuisha Mnada sehemu husika waende katika mamlaka husika kupata vitambulisho.

Wafanyakazi wa Benki ya NBC wajitolea damu kusaidia wenye mahitaji

$
0
0
Watanzania wamehimizwa kushiriki zoezi la kuchangia damu kwa hiari ili kukidhi mahitaji makubwa ya damu na kuokoa maisha ya wenzao pamoja na kusaidia huduma za afya nchini.

Hayo yamesemwa jana jijini Dar es Salaam na Ofisa Fedha Mkuu wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Waziri Barnabas akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Bbenki hiyo, Theobald Sabi wakati wa tukio la kuchangia damu kwa hiari lililondaliwa na NBC akisema kwamba huo ni utamaduni wa benki hiyo wa kuchangia damu kwa kujitolea.

Alisisitiza kwamba ni muhimu kwa watanzania kuanza kujitokeza na kujitolea damu kwa hiari ili kuendelea kuokoa maisha ya wenye mahitaji. "Hii ni mara ya tatu kwa benki hii na wafanyakazi wake kushiriki kwenye kampeni ya uchangiaji damu ili kuokoa maisha ya wakinamama wanaojifungua, waliopata ajali na watu wengine wenye mahitaji ya damu nchini,” aliongeza.

Barnabas aliongeza kwamba kwamba mahitaji ya damu bado yapo juu kwenye mahospitali hasa kwenye upasuaji na bado mwamko upo chini kwa wananchi kama uchangiaji wa damu kwa hiari.

"Ni muhimu sana kwa watanzania wenzetu kuungana nasi katika shughuli ya kujitolea ya kuchangia damu ambayo inatarajiwa kumalizika kesho,” alisema.

Alisema kwamba kwenye shughuli hiyo wanatarajia kukusanya takriban chupa 100 kutoka kwa wafanyakazi wa benki hiyo na watu wengine kutoka maeneo mbalimbali ya jiji ili kupunguza mahitaji makubwa ya damu nchini na alisisitiza kuwa kampeni hiyo inapaswa kuwa endelevu kukidhi matarajio ya nchini.

Kwa upande wake, Kaimu Ofisa Rasilimali watu wa benki hiyo, Grace Mgondah alisema kwamba wanatarajia wafanyakazi 500 kutoka kwenye matawi mbalimbali watashiriki katika zoezi hilo la siku mbili ya kujitolea damu kwa hiari.

"Hii ni sehemu ya huduma kwa jamii ambayo benki yetu ya NBC inasikia fahari kuwahudumia na ninatoa wito kwa watanzania wenzetu kujitokeza kwa wingi kuja kutuunga mkono,” alisisitiza.

Fatuma Mjungu kutoka Kitengo cha Taifa cha Damu Salama (NBTS) alisema kwamba mwaka huu wanatarajia kukusanya chupa 450,000 za damu kutoka kwenye taasisi mbalimbali na watu wanaojitolea kwa hiari. "Mahitaji ya damu kwa sasa nchini ni chupa 520,000 lakini asilimia moja tu ya watanzania wote wakichangia damu tunaweza kukidhi mahitaji ya damu kwa taifa,” aliongeza

Mjungu pia ametoa wito kwa taasisi na makampuni nchini kuinga mkono benki hiyo ya NBC kwa kuhamasisha wafanyakazi wake na wananchi wengine kwa ujumla kujitolea damu kwa ajili ya watu wenye uhitaji.
 Ofisa Fedha Mkuu wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Waziri Barnabas (katikati), akihojiwa na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati yeye na mwenzake, Fanuel Jenga (kushoto), wakijitolea damu katika zoezi lililoandaliwa na benki hiyo kwa wafanyakazi wake kujitolea damu kusaidia wenye mahitaji kupitia Mpango wa Taifa wa Damu Salama.

 Ofisa Fedha Mkuu wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Waziri Barnabas (kulia), pamoja na Mhasibu wa benki hiyo, Fanuel Jenga (kulia kwake) wakichukuliwa vipimo vya damu kabla ya kujitolea damu jijini Dar es Salaam leo, katika zoezi liloandaliwa na benki hiyo kwa wafanyakazi wake pamoja na wakazi wengine wa jiji hilo kusaidia wenye mahitaji kupitia Mpango wa Taifa wa Damu Salama. Kushoto ni Evelyn Dielly kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama.

  Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) wakijitolea damu  katika zoezi liloandaliwa na benki hiyo kwa wafanyakazi wake pamoja na wakazi wengine wa Jiji la Dar es Salaam leo kujitolea damu kusaidia wenye mahitaji kupitia Mpango wa Taifa wa Damu Salama.
 Mkazi wa Chalinze, Joshua Mjuni akijitolea damu katika zoezi liloandaliwa na NBC kwa wafanyakazi wake pamoja na wananchi wengine leo, kujitolea damu kusaidia wenye mahitaji kupitia Mpango wa Taifa wa Damu Salama. Anayemhudumia ni muuguzi kutoka Damu Salama, Peter Chami.
 Ofisa Uhamasishaji wa Mpango  wa Taifa wa Damu Salama, Fatuma Mjungu, akihojiwa na waandishi wa habari katika zoezi la uchangiaji damu wa hiari lililkoandaliwa na Benki ya NBC jijini Dar es Salaam leo.

Mshindi wa promosheni ya Tigo Chemsha Bongo apatikana

$
0
0

Mtaalam wa Huduma za ziada-Tigo, Fabian Felician na Jehud Ngolo- Afisa Mwandamizi Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania. wakimpigia simu Shaban Khamis Ali,mkaazi wa Zanzibar, mshindi wa promosheni ya Tigo Chemsha bongo
Mtaalam wa Huduma za ziada-Tigo, Fabian Felician na Jehud Ngolo- Afisa Mwandamizi Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania. wakimpigia simu Shaban Khamis Ali,mkaazi wa Zanzibar, mshindi wa promosheni ya Tigo Chemsha bongo

Droo ya mwisho ya promosheni ya ‘Tigo Chemsha Bongo’ imefanyika jijini Dar es Salaam ambapo mkaazi wa Zanzibar, Shabani Khamis Ali (48) amejishindia gari mpya aina ya Renault KWID yenye thamani ya 23m/-. Khamis akiongea baada ya kupigiwa simu na Mtaalam wa Huduma za Ziada kutoka Tigo, Fabian Felician, kumfahamisha kuwa ameibuka mshindi, alisema anayo furaha kufanikiwa kuwa miongoni mwa washindi kupitia promosheni hiyo kwa kujishindia gari mpya.

“Sikutegemea kabisa kuwa ningeibuka mshindi katika promosheni hii, Habari hizi naziona kama ndoto kwangu, nashukuru Tigo kwa kunifungia mwaka vizuri na kutimiza ndoto yangu ya kumiliki gari, kwani itanisaidia katika mizunguko yangu ya kibiashara “alisema kwa furaha.

Mtaalam wa Huduma za Ziada kutoka Tigo, Fabian Felician, alimpongeza mshindi huyo na kutumia fursa hiyo kuwashukuru wateja wote wa kampuni ambao walishiriki na baadhi yao kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo zawadi za fedha taslimu ambayo yalitolewa na kampuni hiyo.

“Tunayo furaha kubwa katika kipindi hiki tunachoelekea katika msimu wa sikukuu kumpata mshindi wetu wa gari ya aina Renault Kwid,yenye thamani ya 23m/-, gari hili ni jipya kabisa, baada ya kumpata mshindi taratibu zengine zitafata ili tuweze kumkabidhi Shaban Khamis Ali gari lake jipya. Tunawashukuru wateja wetu kutoka nchini pote walioshiriki kwenye promosheni hii ya miezi mitatu ambayo imemalizika mwishoni mwa mwezi wa Novemba 2019”. alisema Felician.

Aliongeza kuwa, promosheni hii ambayo ilianza jijini Mwanza katika msimu wa Tigo Fiesta 2019-Saizi Yako imepata mafanikio makubwa kutokana na wateja wengi kujitokeza kushiriki na baadhi yao kufanikiwa kujishindia zawadi(fedha taslim) mbalimbali na hivyo Tigo kufanikisha lengo lake ambalo lilikuwa ni kuwashukuru wateja kwa kuiunga mkono kampuni kupitia kununua bidhaa zake mbalimbali.

Kwa kumalizia Felician aliwashukuru wateja wote wa Tigo kwa kuendelea kuunga mkono kampuni na kuahidi kuwa promosheni mbalimbali za kunufaisha wateja wa kampuni hiyo zinatendelea kubuniwa katika siku za usoni.

SBL yashauri mfumo wa pamoja wa kodi kwa nchi za Afrika Mashariki kuharakishwa

$
0
0

· Asema utofauti wa kodi za ndani unasababisha kuongezeka bidhaa bandia za pombe

 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Mark Ocitti, ameshauri kuharakishwa kwa utaratibu wa kuoanisha mfumo wa kodi kwa nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Ocitti amesema, pamoja na kwamba hatua nzuri na kubwa imefikiwa, vikwazo vya kibiashara vilivyopo havina budi kushughulikiwa ili kuongeza kasi ya uwekezaji pamoja na kurahisisha biashara ya bidhaa na huduma miongoni mwa nchi wanachama

Akizungumza katika mkutano wa Biashara na Uwekezaji wa Wakuu wa Nchi za EAC uliofanyika jijini Arusha, Ocitti alisema tafsiri tofauti za vipengele vya kisheria kama ‘bidhaa za nje’ imesabisha kuwepo kwa kodi kubwa kwa bidhaa zinazotoka ndani ya nchi wanachama jambo ambalo limepunguza kasi ya ukuaji wa biashara.

“Utekelezaji wa kuoanisha mfumo wa kodi miongoni mwa nchi wanachama umekuwa hauendi vizuri sana kwa sababu mbali mbali ikiwamo utofauti ya kiuchumi pamoja na kufikiria suala la mapato, viwanda vya ndani, ushindani na nyinginezo,’ alisema

Akizungumzia athari zake kwenye sekta ya uzalishaji wa bia, alisema utofauti wa kodi za ndani miongoni mwa nchi wanachama, umesababisha kuongezeka kwa pombe haramu na kuongeza kuwa bado kuna changamoto katika utekelezaji wa kanuni itayoweka mfumo wa kodi unaofanana kutokana na utofauti wa maendeleo ya kiuchumi na pia hakuna msukumo wa kisheria unatoa msisitizo kwa jambo hilo.

“Kasi ndogo ya upitiaji wa Itifaki ya Ushuru wa Forodha kwa nchi wanachama wa EAC unaathiri baadhi ya shughuli pamoja na kuzifanya bajeti za nchi hizi kutegemea kwa kiasi kikubwa ushuru wa forodha. Hata hivyo, kuanzia mwaka 218 kumekuwa na mfumo mzuri kati ya nchi wanachama kwa kukuliana muundo wa 0%, 10%, 25% na 35.

Akizungumzia namna kampuni ya Bia ya Afrika Mashariki (EABL) ambayo ni kampuni mama ya SBL ilivyoathirika alisema imekuwa ni bahati nzuri kuwa makampuni yaliyo chini ya EABL yamesajiliwa kama makapuni ya ndani kwa nchi wanachama na hivyo hayajaathirika sana kwa kuwa bidhaa zake zinazalishwa ndani ya nchi hizo.

“Hata hivyo, uwekaji wa viwango vya pamoja kwa bidhaa ambazo zipo tayari kwa ajili ya kutumika (RTD) imeleta shida kwa mfano kwenye biashara ya bidhaa hizo zinazotoka Kenya kuja Tanzania,” alisema
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni Bia ya Serengeti Mark Ocitti (wa pili kulia) akizungumza wakati wa mkutano wa Baraza la Biashara la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Arusha leo. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Ushuru na Biashara wa Sekretariati ya EAC Kenneth Bagamuhunda akifuatiwa na Meneja wa kanda wa Coca cola  na wa kwanza kulia ni David Tarimo kutoka kampuni PWC.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni Bia ya Serengeti Mark Ocitti (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watoa mada na wachangiaji muda mfupi baada ya kumalizika kwa mkutano wa Baraza la Biashara la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Arusha leo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni Bia ya Serengeti Mark Ocitti akizungumza wakati wa mkutano wa Baraza la Biashara la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Arusha leo.

4th INTERNATIONAL THERMAL & HEALTHCARE TRAVEL SUMMIT, BALIKESIR TURKEY.

$
0
0
The summit was officially opened by the Mayor of Balikesir Mr. Yücel Yilmaz and flagged by mayors of respective municipals among other government officials and high dignitaries. 

Balikesir is known as an important health destination with its resources and potential, important candidate to be “Thermal center of the Future”. 

Providing remedy for citizens and inhabitants of the region for centuries with healing waters in almost every district. Balikesir derives its power in health, tourism, not only from its healing waters but also from its unique nature. 

The guests were treated to a detailed tour of Edremit, Gonen and Sindirgi and enjoyed these facilities. Edremit, Sindirgi and Gonen are districts located at Balikesir region.THERMAL treatment is famous in Turkey with 5-star thermal hotels and facilities.
Various government leaders and stakeholders follow the 4th international thermal & healthcare travel summit held in Endremit, Turkey. The summit featured many countries including Tanzania.
Turkish Healthcare Travel Council President, Emim Cakmak invites various delegation during the 4th International Thermal Healthcare Travel Summit' held in Endremit, Balikesir in Turkey. 
Turkish Healthcare Travel Council President Emim Cakmak handovers appreciation certificate to the Mayor of Balıkesir Metropolitan Municipality,Yucel Yilmaz for successfully hosting the summit
Some of healthy stakeholders discuss various matters during the summit 
Delegations of 4th International Thermal Healthcare Travel Summit in a group picture after the event 
Turkish Healthcare Travel Council President Emim Cakmak (middle) handovers appreciation certificate to Balikesir regional leaders for successfully hosting the summit

Delegates being entertained by special entertainment group
Participants in a group picture after the summit.

Shabiki Yanga, Barcelona ashinda Milioni 76.2 za M-BET

$
0
0
Dar es Salaam.Shabiki wa timu ya kongwe ya soka nchini, Yanga, Barcelona na Manchester City, Samson Auzebio Mlembe (23) ameshinda Sh 76, 200, 750 kupitia mchezo wa Perfect 12 wa kampuni ya M-BET.

Msemaji wa kampuni ya M-Bet Tanzania David Malley amesema kuwa Mlembe ameshinda fedha hizo baada yakubashiri kwa usahihi mechi 12 za ligi mbalimbali duniani.

Malley alisema kuwa Mlembe ambaye ni mkazi wa Dodoma amekuwa mshindi wa tano kwa mwezi Novemba na 17 miezi 11 na kuweza kubadili maisha yao kupitia mchezo wa Perfect 1.

Alisema kuwa M-BET ni inaendelea kuwa nyumba ya mabingwa kwa kutoa washindi wengi zaidi ambapo mpaka sasa wametumia zaidi ya Sh milioni 700 kwa washindi na bonusi kwa mwezi Novemba peke yake.

“Tunazidi kuinua vipato kwa Watanzania, tumeweza kutoa zaidi ya mamilioni ya fedha kwa mwezi huu na kuwa kampuni pekee iliyoweza kutoa fedha nyingi kwa washindi,” alisema Malley.

Kwa upande wake, Mlembe alisema kuwa hakufikiria kabisa kuwa Allen Mushi kuwa ni tapeli wa mjini baada ya kupokea simu yake.Mlembe alisema kuwa anamfahamu Mushi kutokana na kumuona akiwakabidhi fedha washindi wengi Perfect 12 na kuamini kuwa ameshinda.

“Mpaka sasa sijapanga nitumie fedha hizi kwa mambo gani, ni fedha nyingi ambayo sikutegemea kuipata, nitakaa na wazazi wangu na kujua nini cha kufanya, kwa kweli siwezi kukurupuka,” alisema Mlembe.

Alisema kuwa kuna biashara mbalimbali za kufanya, lakini lazima uweke mikakati na mipango sahihi kabla ya kuanza.

Msemaji wa Kampuni ya M-BET Tanzania, David Malley (kulia) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya Sh milioni 76.2 Mkazi wa Dodoma, Samson Mlembe aliyeshinda mchezo wa kubashiri wa Perfect 12. Katikati ni Shabani Mwanga, Mkuu wa Kitengo cha Kodi za Michezo ya Kubahatisha (TRA), mkoa wa kodi wa Ilala.

4th INTERNATIONAL THERMAL & HEALTHCARE TRAVEL SUMMIT, BALIKESIR TURKEY.

$
0
0
The summit was officially opened by the Mayor of Balikesir Mr. Yücel Yilmaz and flagged by mayors of respective municipals among other government officials and high dignitaries. 

Balikesir is known as an important health destination with its resources and potential, important candidate to be “Thermal center of the Future”. 

Providing remedy for citizens and inhabitants of the region for centuries with healing waters in almost every district. Balikesir derives its power in health, tourism, not only from its healing waters but also from its unique nature. 

The guests were treated to a detailed tour of Edremit, Gonen and Sindirgi and enjoyed these facilities. Edremit, Sindirgi and Gonen are districts located at Balikesir region.THERMAL treatment is famous in Turkey with 5-star thermal hotels and facilities.
Turkish Healthcare Travel Council President Emim Cakmak handovers appreciation certificate to the Mayor of Balıkesir Metropolitan Municipality,Yucel Yilmaz for successfully hosting the summit
Some of healthy stakeholders discuss various matters during the summit
Delegations of 4th International Thermal Healthcare Travel Summit in a group picture after the event 


Turkish Healthcare Travel Council President Emim Cakmak (middle) handovers appreciation certificate to Balikesir regional leaders for successfully hosting the summit

Various government leaders and stakeholders follow the 4th international thermal & healthcare travel summit held in Endremit, Turkey. The summit featured many countries including Tanzania.
Turkish Healthcare Travel Council President, Emim Cakmak invites various delegation during the 4th International Thermal Healthcare Travel Summit' held in Endremit, Balikesir in Turkey. 



Delegates being entertained by special entertainment group
Participants in a group picture after the summit.

TUME YA USHINDANI TANZANIA YAJIPANGA KUADHIMISHA WIKI YA USHINDANI DESEMBA 3 HADI 5

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

TUME ya Ushindani Tanzania (FCC) kwa kushirikiana na Mamlaka za EWURA, LATRA, PURA, FCT, TCAA, TCRA na TASAC wataadhimisha maadhimisho ya siku ya ushindani Duniani ambayo huadhimishwa Novemba 5 kila mwaka na mwaka huu itaenda sambamba  na kongamano litakalowakutanisha wadau na wananchi kwa malengo ya kuwajengea uwezo na ufahamu zaidi kuhusiana na maadhimisho hayo pamoja na shughuli zinazofanywa na Mamlaka hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa bodi ya ushindani nchini (FCC), Profesa. Humphrey Moshi amesema Tanzania imekuwa ikiadhimisha siku ya ushindani tangu mwaka 2015 na kwa mwaka huu maadhimisho hayo yamekuja na kauli mbiu inayoendana na masuala ya kiushindani yanayojitokeza kote Duniani ya " Kuhakikisha Ushindani Madhubuti katika Ukuaji wa Dunia ya Kimtandao."

Amesema kuwa kilele cha maadhimisho hayo yatakayofanyika Desemba 5 na Waziri mwenye dhamana ya Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa atakuwa mgeni wa heshima.

Prof. Moshi amesema kuwa mitandao imekuwa ikikuza biashara kama ikitumiwa vizuri, "Biashara mtandao ni ile inayohusisha mabadilishano ya taarifa kupitia mtandao wa kompyuta, kimsingi ni jambo zuri kwa kuwa tafiti zinaonesha kuna masoko ya kutangaza bidhaa kwa urahisi hata kwa kuvuka mipaka ukilinganisha miaka iliyopita" ameeleza .

Vilevile amesema kuwa lazima jamii itambue fursa za masoko ya mtandao licha ya kuwepo na baadhi ya changamoto,lakini tume hiyo itaendelea kuhakikisha inawezesha masoko na kuwasiliana kwa urahisi, na hiyo ni pamoja na kuimarisha mifumo na uwezo wa biashara.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani nchini Godfrey Machimu amesema kuwa maadhimisho ya mwaka huu yatahusisha maonesho mbalimbali kutoka kwa wadau pamoja na kupata fursa ya kujua utendaji kazi wa Mamlaka hizo.

Machimu amesema kuwa Tume ya Ushindani kupitia maadhimisho hayo wanaamini italeta chachu katika kutatua changamoto za biashara mtandao zinazowakabili wananchi kote nchini.

Siku ya Ushindani Duniani imekuwa ikiadhimishwa na Mamlaka za ushindani Duniani kote kuanzia Mwaka 1980, wakati wa Umoja wa Mataifa uliporidhia na kukubaliana na kanuni za kuzuia mienendo potofu ya biashara.
Mwenyekiti wa Tume ya Ushindani Prof. Humphrey Moshi akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo jijini Dar, kuhusu namna Tanzania ilivyojiandaa kuadhimisha siku hiyo,amesema Tanzania imekuwa ikiadhimisha siku ya ushindani tangu mwaka 2015 ,lakini kwa mwaka huu maadhimisho hayo yamekuja na kauli mbiu inayoendana na masuala ya kiushindani yanayojitokeza kote Duniani ya " Kuhakikisha Ushindani Madhubuti katika Ukuaji wa Dunia ya Kimtandao." 
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani Godfrey Machimu akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani),leo jijini Dar akieleza kuhusu tume hiyo   ikishirikiana na Mamlaka za EWURA, LATRA, PURA, FCT, TCAA, TCRA na TASAC wataadhimisha maadhimisho ya siku ya ushindani Duniani ambayo huadhimishwa Desemba 5 kila mwaka,ambapo mwaka huu itaenda sambamba na kongamano litakalowakutanisha wadau na wananchi kwa malengo ya kuwajengea uwezo na ufahamu zaidi kuhusiana na maadhimisho hayo pamoja na shughuli zinazofanywa na Mamlaka hizo.

 Mkurugenzi wa Utafiti na Muungano wa Makampuni na Urabishi Dkt. Allan Syril Mlulla akifafanua zaidi mbele ya Waandishi wa habari  namna maadhimisho hayo adhimu kwa Wadau yatakavyofanyika sambamba na kutoa elimu na kueleza shughuli mbalimbali zinazofanywa na Tume hiyo.
Baadhi ya Waandishi wa habari wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo. Picha na Michuzi JR.

TCRA yaongeza muda wa usajili kwa Wananchi wa Makambako hadi Desemba Sita.

$
0
0
Afisa uhamiaji akihudumia Mwananchi katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada uliofanyika Mji mdogo wa Makambako.
Kampuni za simu wakisajili Wananchi wa Mji Mdogo wa Makambako laini za simu kwa alama za vidole.
Wananchi wakipata huduma ya usajili wa laini za simu kwa alama za vidole katika Mji Mdogo wa Makambako.

*************************************

Kufuatia na kujitokeza kwa wingi kwa wakazi wa Makambako na viunga vyake vya jirani katika zoezi la kupata namba za vitambulisho vya taifa na kusajili simu Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kushirikiana na Mamlaka ya vitambulisho vya taifa NIDA na watoa huduma wote wa makampuni ya simu wameongeza muda wa zoezi hilo ambapo sasa zoezi hilo utafanyika kwa wiki nzima kuanzia Desemba 2 hadi 6 2019.

Akizungumzia maendeleo ya zoezi hilo linaloratibiwa na TCRA mkuu wa kanda ya Nyanda za juu Kusini Mhandisi Asajile John amesema lengo la serikali ni kuhakikisha kuwa wananchi wote wanaopata huduma za msingi kwa urahisi hivyo kuongeza huko kwa siku kunalenga kutekeleza malengo hayo.

Amesema huo ni muendelezo wa kampeni ya “Mnada kwa Mnada, Karibu tukuhudumie” iliyoanzishwa na kuratibiwa na TCRA na kushirikisha wadau wengine inayolenga kutoa elimu ya utumiaji bora na salama wa huduma za mawasiliano na kuhamasisha usajili wa laini kwa kutumia namba za vitambulisho vya taifa.

Barclays Bank hosts its Zanzibar customers to a thanks-giving cocktail event

$
0
0
Barclays Bank Tanzania Limited (BBT) on Tuesday, 26th of November hosted its Zanzibar customers to a cocktail event. The event was not only a platform to appreciate the continued support of its customers but was also used to provide an opportunity for clients to join BBT in its transition journey and be informed of the expected milestones as the Bank prepares to rebrand into Absa.

Speaking during the event, the bank’s Managing Director, Mr. Abdi Mohamed said, “Our brand and name change to Absa is proceeding as planned. We have taken a sequenced approach and expect some branches to reflect several elements of the new brand in the first half of December, while some branches will retain the current look. The intention is to take our customers and the public with us through the transformation journey visually. We will however continue to operate and trade as Barclays Bank Tanzania Limited until our name officially changes, as approved by the Regulator.”

Speaking on the bank’s commitment to Tanzania, Mr. Mohamed said, “Barclays is committed to serving its customers and we are proud of the momentum we have built over the past 3 years. Our commitment to our clients has been demonstrated in the successful execution of key financing transactions amounting to TZS 529bn, across sectors such as Oil & Gas, Public Sector, Manufacturing and Agriculture. In addition, our non-funded strategy and focus has been reaffirmed by The Asian Banker 2019 recognition of BBT as the best ‘Cash Management Bank in Tanzania’.

Responding to a question on whether customers can have the same confidence in Absa as they had in Barclays, the bank’s Head of Retail Banking, Mr. Oscar Mwamfwagasi said ”Absa Group is committed to building on Barclays' heritage in Africa and the strengths that we already have on the continent. We have a deep history and local knowledge in Tanzania. Our main products and services haven’t changed. Our customers can bank with us as confidently as they always have.

You can bank with us as safely as you always have. Absa Group is one of the largest banking groups in Africa, with a balance sheet of more than USD 91 billion, as well as new systems with robust security provisions. ”

In conclusion, Mr. Mwamfwagasi; called for clients to remain vigilant, saying “We will not ask any customer for additional information during this time, and all customer account details will remain the same before and after the transition.”

Barclays Bank’s Managing Director, Abdi Mohamed (on the right) in conversation with a client during the cocktail event.
Barclays Bank’s Finance Director, Obedi Solomon Laiser (in the middle) engaging with clients during the cocktail event.

Barclays Bank’s Human Resource Director, Patrick Foya ( right) engaging with customers during the cocktail event


Barclays Bank’s Chairman, Simon Mponji (left) and Dr Suleiman Rashid Mohamed (extreme right) in conversation with clients during the cocktail event.

Barclays Bank’s Corporate Director, Brian Kalero (Right) in conversation with clients during the cocktail event.

Tigo wazindua kampeni ya wakala kinara

$
0
0
Tigo yazindua kampeni ya kufunga mwaka kwa ajili ya mawakala iitwayo Wakala Kinara. Kampeni hiyo itakayo anza rasmi tarehe 1 disemba hadi 31 disember itahusisha mshindi wa kwanza kupokea milioni 20 akifuatiwa na wa pili milioni 10. #TigoWakalaKinara

Kampuni ya Mawasiliano Tigo jana yakutana, yawapongeza mawakala wa Tigo pesa pamoja na kuzindua promosheni mpya ya mawakala iitwayo Wakala Kinara.

“Kama tunavyofahamu tulizindua kampeni ya ‘Kishindo Cha Kufunga Mwaka’ kwa ajili ya mteja wa Tigo pesa hivyo kampeni tunayozindua leo ni mahususi kwa ajili ya mawakala wa Tigo pesa.”‬‪Kaimu Mkuu wa kitengo cha Tigo Pesa, Angelica Pesha‬ 

Tigo yazindua kampeni ya kufunga mwaka kwa ajili ya mawakala iitwayo Wakala Kinara. Kampeni hiyo itakayo anza rasmi tarehe 1 disemba hadi 31 disember itahusisha mshindi wa kwanza kupokea milioni 20 akifuatiwa na wa pili milioni 10. #TigoWakalaKinara

Baadhi ya mawakala wa Tigo pesa wakiwa pamoja uongozi wa kampuni ya mawasiliano Tigo, baada ya kupokea tuzo za mawakala wa Tigo pesa waliofanya vizuri katika mwaka 2019.
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live


Latest Images