Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1891 | 1892 | (Page 1893) | 1894 | 1895 | .... | 1898 | newer

  0 0

   Mkurugenzi wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna (wa pili kushoto), akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa wabunifu wa mitindo aliyeshiriki semina ubunifu na ufundi iliyoandaliwa na Benki ya NMB kwa wajasiriamali.
   Mkurugenzi wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna, akiangalia kazi za wabunifu wa mitindo wakati wa semina ya Ubunifu na Ufundi iliyofanyika Makao Makuu ya Benki ya NMB jijini Dar es Salaam.
   Mbunifu wa mavazi, Doris Mbwilo (kushoto), akitoa maelezo kwa Mkurugenzi wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna, wakati wa maonesho ya kazi za ubunifu na ufundi za wajasiriamali.
   Mkurugenzi wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna (kulia), akizungumza na mbunifu wa mavazi, Doris Mbwilo, wakati wa maonesho ya bidhaa za ubunifu na ufundi.
   Baadhi ya wabunifu wa mitindo walioshiriki semina ya Ubunifu na Ufundi.
  Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benki ya NMB, Donatus Richard, akizungumza na wajasiriamali wa kazi za ubunifu na ufundi.  MKURUGENZI wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna, amewaasa wajasiriamali na wafanya biashara wadogo kada ya ubunifu na ufundi kutumia benki katika kukuza biashara zao, ameyasema hayo katika uzinduzi wa semina ya Ubunifu na Ufundi ni Nguzo ya Uchumi, iliyofanyika leo Makao Makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam.


  Ametoa wito kwa wajasiriamali hao kuyashika na kuyatendea kazi mafunzo waliyoyapata ili kuweza kufanikiwa katika malengo yao ya kukuza biashara zao kwa kuzifanya zenye kuaminika.

  Amewataka kufungua akaunti za benki kama vile FANIKIWA zitawawezesha kulinda biashara zao na kuwafanya kuaminika na benki ili kuingia kwenye mfumo wa kibenki kupata mikopoa ambayo itawawezesha kukuza biashara zao.

  “Kuna mambo matatu mnayokwenda kufundishwa, moja ni umuhimu kuwa na akaunti, pili umuhimu wa mauzo ya bishara zako kupitia kwenye akaunti zenu na tatu ni faida ya kuweka akiba katika kukuza biashara zenu.

  “Mkiwa na mahesabu yanayoeleweka kwenye akaunti zenu ni rahisi kupata mikopo ya kibenki kuinua biashara zenu ili muweze kujiimarisha zaidi. Ubunifu mlionao kama mnaweka malengo na kuyasimamia na kuwa na mtiririko wa matumizi ya fedha yanayoeleweka mtaweza kuzilinda biashara zenu na kukuza ubunifu mlionao.”amesema Zaipuna na kuongeza kuwa.

  “NMB imeamua kuwafikia wajasiriamali wadogo kada ya ubunifu kwani ni kada iliyosahaulika katika jamii katika uwezeshwaji, sisi tunaamini kuwa Ubunifu na Ufundi ni nguzo ya Uchumi hivyo tunadhamira ya dhati ya kuimaraisha Uchumi wa wajasiriamali wabunifu kupitia mafunzo na mikopo ya kibenki ambayo itatolewa.”amesema.

  Kwa upande wa mtoa mada, Meneja wa wafanyabiashara wadogo wa NMB, Beatrice Mwambije ametoa wito kwa wajasiriamali hao kutambua kuwa kuna gharama ya kulipia ili kuweza kupata mafanikio wanayoyahitaji katika kazi zao.

  “Katika biashara yoyote ni muhimu sana kuwa na akaunti ili kuweza kutunza kumbukumbu zako za manunuzi, mauzo na matumizi ili kukujengea uwazi na uwaminifu kwa benki kukupa mkopo utakao kuwezesha kukua katika biashara yako.

  “Lakini katika mafanikio yoyote yale lazima kuna gharama ya kulipia ili uweze kuyafikia, unahitaji kuwa na watu sahihi ambao watakutoa sehemu moja hadi nyingine nao ni watu sahihi ambao fikra zao ni chanya na wakomavu zaidi.”amesema Mwambije.

  Nae Mkurugenzi wa Kampuni ya Ubunifu wa mavazi ‘Speshoz Tanzania’ Jeffrey Jessey amewataka washiriki wa semina hiyo kuwa mstari wa mbele kujifunza vitu vipya, kuchangamana na watu na kuwekeza zaidi kwa kile wanachokipa ili waweze kufika mbali katika tasnia ya Ubunifu na Ufundi.

  Kwa Upande wa washiriki wa semina hiyo wametoa kongole kwa NMB kwa kuwajali na kuwapa elimu ambayo itawatoa walipo na kupiga hatua zaidi katika kazi zao,

  “Nimefurahi sana kuwepo hapa leo, mafunzo haya ni kitu kikubwa sana kwetu sisi wabunifu wachanga katika kupiga hatua zaidi, tumejifunza mambo mengi na mazuri ambayo tukiyatendea kazi basi naamini tutafika mbali zaidi,”amesema Addam Mtaullah Mwenyekiti wa Umoja wa Mafundi Nguo Mbezi Luis (UMANGUMBE.

  “Kwanza niwapongeza NMB wametuletea jambo sahihi kwa wakati sahihi, lakini pia mafunzo tuliyopata hapa yametufungua akili kujua jinsi gani tunaweza kutumia njia za kibenki kukuza biashara zetu kwa kuwa na akaunti unaiweka pesa yako salama.”amesema Doris Mbwilo mshiriki wa semina hiyo.

  0 0

  KAMPUNI ya Mawasiliano ya Abel & Fernandes imeungana na Kampuni ya Afya ya AAR na wadau wengine kwa lengo la kushirikiana na Serikali katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa kisukari ambao kwa kiasi kikubwa umeelezwa kusababishwa na mtindo wa maisha.

  Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni hiyo jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Abel & Fernandes, Fatma Fernandes alisema kampeni hiyo dhidi ya kisukari imelenga kuboresha huduma za afya na maisha ya watu wanaoishi na ugonjwa huo.

  Alisema kampeni hiyo iliyopewa kaulimbiu ya ‘Tenda Leo, Mabadiliko ya Kesho ...tuungane kutokomeza kisukari’ imelenga kuwaunganisha wadau mbalimbali kuboresha huduma za kinga, tiba ili kudhibiti ugonjwa wa kisukari.

  Alisema watatoa huduma kwa mamia ya jamii iliyokumbwa na kisukari, kutoa taarifa muhimu kuhusu kisukari na kupaza sauti kwa wale waliokosa haki zao dhidi ya ugonjwa wa sukari.

  “Ugonjwa wa kisukari nchini unakua, kwa sababu hadi sasa watu zaidi ya milioni 4.2 wamebainika kuwa na ugonjwa huo. Abel & Fernandes tunaelewa tatizo hili, ndio maana tumeamua kuungana kuelimisha watu juu ya ugonjwa huo ili waweze kupata matibabu sahihi na kujua namna ya kujitunza,” alisema.

  Alisema ili kufikia malengo hayo ya uhamasishaji, Abel & Fernandes inakusudia kufanya kazi na madaktari na wataalam ili kuhakikisha kuwa huduma sahihi zinatolewa katika hospitali mbalimbali kwa walioathirika na ugonjwa huo.

  "Tunapaswa kuanza kwa vitendo sasa, ambapo hatua ya kwanza ni kuunga juhudi ya serikali kuboresha huduma zinazotolewa dhidi ya waathirika wa ugonjwa huo kwa kuanzisha mikakati ya kitaifa ya kuudhibiti na kuwa na ufuatiliaji wa mara kwa mara. Hii itaruhusu matumizi bora ya rasilimali, ambayo ni muhimu ikiwa mkoa utaandaa mikakati dhabhiti ya kudhibiti janga hilo,”alisema.

  Aidha, naye Dk. Akil Msei kutoka AAR alisema kwa mujibu wa ripoti za Shirika la Afya Duniani (WHO) takwimu zinaonyesha kila sekunde 10 mtu mmoja mwenye kisukari hufariki duniani na zaidi ya watu 40,000 wenye kisukari Tanzania hukatwa miguu.

  Alisema pia zaidi ya watu milioni 422 wana kisukari duniani hivyo kupelekea ugonjwa huu kushika nafasi ya 5 kama kisababishi cha vifo duniani.

  "Ugonjwa wa kisukari ni ugonjwa sugu na unaathiri watu wengi. Kuna aina mbili za ugonjwa wa kisukari; Aina ya 1 na Aina ya 2. Aina ya 2 inazuilika na hii ndio tunajaribu kushughulikia ili tuweze kuzuia kuongezeka kwa visa kama hivyo. "

  Alisema kampeni hii iliyoandaliwa kwa nia ya kuboresha maisha ya watu wenye ugonjwa wa kisukari itaanza kwa muda wa mwezi mmoja kwa kushirikisha watu wa kada mbalimbali katika utoaji wa elimu dhidi ya ugonjwa huo.

  “Tutakuwa na kampeni za barabara ambazo zitatembelea maeneo ya Tegeta na Kariakoo kwa kutoa huduma katika magariu maalumu ya kidijitali.

  “Kampeni inaenda sambamba na Siku ya wagonjwa wakisukari Novemba 14, 2019 ambapo tutakuwa na zahanati zinazotembea pamoja na kifungua kinywa kwa wagonjwa na wadau wote.

  Ungana nasi tunapopambana na Ugonjwa huu wa Kisukari. Kwa habari zaidi tembelea tovuti ya kisukari www.diabetesestanzania.com.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Abel & Fernandes, Fatma Fernandes akizungumza katika uzinduzi wa kampeni dhidi ya ugonjwa wa kisukari ambayo imelenga kuboresha na kutoa huduma bure kwa watu wanaoishi na kisukari huo nchini.
  Mmoja wa wahuduma wa afya walioandaliwa na kampuni ya Abel&Fernandes pamoja na AAR akitoa huduma kwa wananchi waliojitokeza kupata huduma na elimu ya kisukari kwa kutumia vituo vinavyotembea katika barabara maeneo ya Tegeta na Kariakoo jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli ameungana na wake wa viongozi
  mbalimbali katika kusherehekea miaka 10 ya umoja wao uitwao  New
  Millenium Women’s Group kwa kutoa misaada katika kituo cha kulea wazee
  cha Nunge Kigamboni jijini Dar es salaam leo.

  Mama magufuli, ambaye aliambatana na Mlezi wa umoja huo Mke wa Waziri
  Mkuu Mama Mary Magufuli, Mwenyekiti wake Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu
  Mama Tunu Pinda na Mama Asina Kawawa aliungana na wajumbe hao kutoa
  misaada mbali mbali ya ujenzi, chakula na nguo.

  Mama Magufuli alichangia jumla ya gypsum 178 huku Makamu wa Rais Mhe
  Samia Suluhu Hassan akituma mchango wa shilingi milioni 5 kwa ajili ya
  ukarabati wa Bwalo la kituo hicho kikongwe ambacho hadi leo Novemba
  15, 2019 kilikuwa na wazee 26.

  Umoja huo wa New Millenium Women’s Group ulichangia ujenzi wa mnara wa
  kisima cha maji kwa gharama ya shilingi milioni 1.9, vyakula na nguo
  vyenye thamani ya shilingi milioni 3.


  Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akitoa misaada ya nguo navyakula kwa kituo cha kulea wazee cha Nunge Kigamboni jijini Dar essalaam leo.
  Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa akitoa misaada ya nguo na vyakula kwa kituo cha kulea wazee cha Nunge Kigamboni jijini Dar essalaam leo.
  Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akitoa misaada wa gypsum 178 kaajili ya ujenzi wa bwalo la kituo cha kulea wazee cha Nunge Kigamboni jijini Dar es salaam leo.
  Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli katika picha ya pamoja na wajumbe wenzie wa umoja wa wake wa viongozi mbalimbali uitwao New Millenium Women’s Group na baadhi ya wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kigamboni katika kituo cha kulea wazee cha Nunge Kigamboni jijini Dar es salaam leo.
  Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli katika picha ya pamoja nawajumbe wenzie wa umoja wa wake wa viongozi mbalimbali uitwao New Millenium Women’s baada ya kukabidhi misaada katika katika kituo cha kulea wazee cha Nunge Kigamboni jijini Dar es salaam leo.
  Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli katika picha ya pamoja nawajumbe wenzie wa umoja wa wake wa viongozi mbalimbali uitwao New Millenium Women’s na wakaaazi wa kituo cha kulea wazee cha Nunge Kigamboni jijini Dar es salaam leo.
  Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiagana na wajumbe wenzie wa umoja wa wake wa viongozi mbalimbali uitwao New Millenium Women’s baada ya kukabidhi misaada katika katika kituo cha kulea wazee cha Nunge Kigamboni jijini Dar es salaam leo.
  Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwa na wajumbe wa umoja wa wake wa viongozi mbalimbali uitwao New Millenium Women’s Group akiwasili katika kituo cha kulea wazee cha Nunge Kigamboni jijini Dar es salaam leo. Wengine toka kushoto ni Mama Tunu Pinda, Mama Mary Majaliwa, Mama Janeth Magufuli, Waziri wa Elimu, sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako na Mama Asina Kawawa.
  Wajumbe wa umoja wa wake wa viongozi mbalimbali uitwao NewMillenium Women’s Group wakiwa katika kituo cha kulea wazee cha Nunge Kigamboni jijini Dar es salaam leo walikofika kutoa misaada mbalimbali katika kuadhimisha umoja huo.PICHA NA IKULU

  0 0
 • 11/15/19--11:04: GANGWE MPYA KWENYE GAME??

 • Ukiona mtu anaweza kufanya jambo lake bila uoga wa kuona wale wabishi na wakubwa zaidi yake kwenye hilo jambo nao wanafanya kwa wakati huo ni lazima ikupe maswali kidogo juu yake..Ndivyo ambavyo msanii anayekuja kwa kasi anavyowapa watu mshtuko na maswali baada ya kuachia ngoma yake inayokwenda kwa jina la BWEKA inapatikana hapa

  https://youtu.be/ZI8XdkybUEA

  jumatano ya wiki hii huku vyuma kama Diamond Platnumz,Harmonize na Ali Kiba nao wakiwa wametoa ngoma zao zinazozidi kushika chati kila siku.SALHA ambaye mbali na kuwa bado mchanga kwenye sanaa ya muziki ameonyesha kutokuogopeshwa na uwepo wa kazi za wasanii wakubwa sokoni kwa kuachilia nyundo yake kali ambayo kwa jinsi inavyozidi kupokelewa vizuri na wasikilizaji pamoja na vituo mbalimbali inatufanya tujiulize, 
   
  je huyu ni gangwe mpya wa muziki wa Tanzania??Haikuishia hapo ambapo wasanii wakubwa pia kama Benpol wameonyesha wazi kuikubali BWEKA kwa kuitupia katika mtandao wake wa kijamii wa Instagram muda mchache tu baada ya kuiachilia..Kwa haraka picha anayotupa ni ya ujasiri mkubwa katika sanaa yake licha ya kuwa binti mdogo wa miaka 19 tu..
   
  BWEKA ambayo imepikwa kwa mtayarishaji Aloneym ni kati ya mishale ambayo mwanadada huyu mwenye sauti ya kipekee ameanza kuirusha akiwa chini ya menejimenti yake ya The Collective Live.
   
  Salha ambaye pia yupo kwenye maandalizi ya kuachia video ya ngoma hii hivi karibuni,anaweka wazi kuwa BWEKA ni moja tu kati ya ngoma zake kali ambao unapatikana sasa YouTube na anaamini watanzania wataupokea kwa mikono miwili na utawakonga nyoyo sana huku maandalizi ya video na mambo mengine ya kimuziki akiyatupia katika page yake ya instagram inayokwenda kwa jina la Salhaofficialtz

  0 0

    Kaimu Kabidhi Wasii Mkuu au Ofisa Mtendaji Mkuu wa RITA Emmy Hudson (kushoto) akiwa  na Posta Master Mkuu Hassan Mwang'onde wakisaini hati ya makubaliano leo jijini Dar es Salaam baada ya RITA kuamua kuanza kutumia Shirika hilo kusafirisha nyaraka na vitendea kazi katika maeneo mbalimbali nchini. Wanaoshuudia na maofisa wa RITA na Shirika la Posta
    Kaimu Kabidhi Wasii Mkuu au Ofisa Mtendaji Mkuu wa RITA Emmy Hudson akiwa  na Posta Master Mkuu Hassan Mwang'onde wakiwa amesimama na kushika hati za makubaloano baada ya kutia saini leo jijini Dar es Salaam.Makubaliano hayo yanahusu RITA kuanza kutumia Shirika hilo kusafirisha nyaraka na vitendea kazi katika maeneo mbalimbali . Wanaoshuudia  kulia ni ofisa wa RITA na Shirika la Posta
   Kaimu Kabidhi Wasii Mkuu au Ofisa Mtendaji Mkuu wa RITA Emmy Hudson akiwa  ameshikana mkono na  Posta Master Mkuu Hassan Mwang'onde baada ya kusaini hati ya makubaliano  leo jijini Dar es Salaam ambapo RITA wataanza kutumia Shirika hilo kusafirisha nyaraka na vitendea kazi katika maeneo mbalimbali nchini.
   

  0 0  0 0

  Na Chalila Kibuda,Morogoro

  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare ameahidi kuwa Balozi wakusaidia wahitimu wa Chuo cha VETA Mikumi kwa wale wataokafanya vizuri kwenye masomo yao baaada yakumaliza mitihani yao kwa mwaka huu

  Kauli hiyo Ameitoa wakati wa mahafali ya 22 ya chuo cha ufundi stadi mikumi mkoani morogoro nakueleza kuwa mkoa wa morogoro unayo miradi mikubwa inayotekelezwa kama ule mradi wa kufua umeme wa bwawa la mwl nyerere ambao unahitaji watalaamu wanaozalishwa kutoka vyuo vya ndani na hivyo yeye akiwa kiongozi atahakikisha watakaofaulu vizuri wanapata ajira kwenye miradi hiyo

  Mkuu huyo wa mkoa ameeleza kuwa serikali ya awamu ya tano imedhamiria kwa dhati kuwaendeleza vijana kwakutoa wataalumu ambao wanatoka kwenye vyuo mbalimbali ikiwemo Veta na hivyo kila mwanafunzi anayesoma veta anatakiwa kufahamu kuwa ipo miradi inayowahitaji wao kuitumikia ikiwemo kujiajiri mwenyewe pamoja na kupenda kazi,kutafyta fursa,kuwa wajasiliamali, na kujiendeleza kitaaluma ili kumudu mabadiliko ya sayansi na teknolojia

  Nae kaimu mkuu wa chuo Veta Mikumu Emmanuel Munuo ameziomba asasi zisizo za serikali na wadau kuifaga mfano wa shirika la plan international kwa kutafyta vijana walioko vijijini kutambua mahitaji yao na kasha kuwapatia mafunzo ya ufundi stadi na elimy ya ujasiliamali ili kuwatengenezea fursa za kujiajiri au kuajiriwa katika sekta rasmi na isiyo rasmi.

  Nao baadhi ya wazazi na walezi wamewataka vijana wanaohitimu masomo kuwa waadilifu nakuutumia ujuzi waliupata kwa manufaa kwa jamii na taifa pamoja nakusoma kwa bidiii ili kuitumia fursa yakauli ya mkuu wa mkoa yakutumia miradi iliyopo Morogoro kwakupata ajira

  Jumla ya wahitimu 240,Wavulana 176 na Wasichana 64 wanahitimu kwa fani mbalimbali chuoni hapo.
   Mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare akipata maelezo kutoka mwanafunzi wa ngazi ya tatu katika ya uunganishaji Stanford Ngozo namna walivyotengeneza kabati wakati mkuu wa mkuu huyo alipotembelea karakana hiyo, mahafali ya 22 ya Chuo cha VETA Mikumi Mkoani Morogoro.
   Mkuu wa Mkoa wa Morogoro  Loata Ole Sanare akizungumza katika mahafali ya 22 ya Chuo cha VETA Mikumi Wilaya Kilosa Mkoani Morogoro.
   Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Adam Mgoi akizungumza kuhusiana na faida ya Chuo hicho kwa wakazi wa Kilosa kupata stadi za ufundi wakati wa Mahafali ya Chuo cha VETA  Mikumi wilayani Kilosa mkoani Morogoro
   Kaimu Mkuu wa Chuo cha VETA Mikumi Emmanuel Munuo akizungumza kuhusiana na historia ya chuo  hicho na mafanikio waliyoyapata katika kuandaa vijana wenye ujuzi .
   Sehemu ya wahitimu wa chuo cha VETA Mikumi wakifurahi wakati wakiingia katika viwanja vya Mahafali katika Chuo hicho
   icha ya pamoja na wahitimu waliopata tuzo mbalimbali


  0 0

  Mdau wetu Dk Bariki Zacharia Kingu akifurahia mara baada ya kutunukiwa shahada ya udaktari katika Chuo kikuyu cha udaktari KCMC mjini Moshi mapema leo .Mtandao huy tunampa hongera na kumtakia kila la Kheri katika maisha yake mapya ya kuhudumia watanzania katika kituo chake cha kazi
  Matina Nkurlu ambaye ni kaka yake Dk Bariki Zacharia Kingu akimpongeza mdogo wake mara baada ya kutunukiwa leo Shahada ya udaktari katika Chuo kikuyu cha Udaktari KCMC Mjini Moshi mapema leo
  Matina Nkurlu na dada yake Blandina Zacharia Kingu wakifurahia Pamoja na mdogo wao Dk Bariki Zacharia Kingu mara baada ya kutunukiwa shahada ya udaktari katika Chuo kikuu cha udaktari KCMC mjini Moshi mapema Leo.

  0 0

  Katika kutambua umuhimu wa vijana ambao ni Taifa la kesho, Wanafunzi wa kidato cha sita wa Shule ya Wasichana ya Barbro Johansson Model iliyopo jijini Dar es Salaam, wamepata elimu ya fedha na umuhimu wa matumizi makini ya fedha ikiwemo kuweka akiba benki, walipotembelea Makao Makuu ya benki hiyo kujionea shughuli mbalimbali za kibenki kwa vitendo.
  Mmoja wa Wanaafunzi akimlisha kipande cha keki Kaimu Mkurugenzi wa NMB – Ruth Zaipuna akikata keki pamoja na wanafunzi.Pamoja na hayo, Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna amewaasa wanafunzi hao kuwekeza nguvu zaidi katika elimu, kusoma kwa bidii na kuhakikisha wanatimiza malengo yao. 

  Kaimu Mkurugenzi wa NMB – Ruth Zaipuna akikata keki pamoja na wanafunzi.


  Wanafunzi wakifurahi pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa NMB- Ruth Zaipuna na Mwalimu wao- Jennifer Dominick.
  Wanafunzi wakipata elimu kutoka kwa Ofisa wa benki ya NMB- Monica Job. Wanafunzi hao walipata nafasi ya kujifunza na kutembelea idara na vitengo tofauti ili kufahamu shughuli zao lakini pia walitembelea Tawi la NMB Ohio. 
  Baada ya mafunzo hayo, wanafunzi wote walipata nafasi ya kufungua akaunti zitakazowawezesha kutunza fedha na kujijengea tabia ya kuweka akiba na kunufaika na huduma na bidhaa za benki ya NMB hususan Chipukizi na Mwanachuo Akaunti.


  0 0

  Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa, Uthmaan Madati akizungumza mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga wakati wa uzinduzi wa Duka la Tigo ‘Tigo Shop’ mkoani Kigoma.
  Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga akikata utepe wakati wa uzinduzi wa duka jipya la Tigo ‘Tigo Shop’ mkoani Kigoma. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa, Uthmaan Madati. 
  Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga akihakiki utendaji kazi wa mfumo wa kusajili namba za simu kwa alama za vidole katika duka jipya la Tigo lililopo eneo la Lubengela Mkoani Kigoma jana mara baada ya kuzindua duka hilo.Kulia ni Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa, Uthmaan Madati.
   
  Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga akizungumza na wakazi wa Kigoma pamoja na wafanyakazi wa Kampuni ya Tigo wakati wa uzinduzi wa duka la Tigo Mkoani Kigoma, Kulia ni Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa, Uthmaan Madati.   Wateja wa Tigo Mkoani Kigoma wataweza kupata huduma zilizoboreshwa zaidi katika duka jipya ‘Tigo Shop’ lililozinduliwa leo mkoani humo.

  Duka hilo jipya litakuwa sehemu maalumu kwaajili ya wateja kujionea na kufanya majaribio ya bidhaa na huduma mbalimbali mpya na za kidigitali kama Tigo Pesa zitolewazo na kampuni hiyo.

  Wateja pia wataweza kupata huduma ya kusajili upya namba za simu kwa mfumo wa alama za vidole.

  Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi, Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa, Uthmaan Madati alisema “Ufunguzi wa duka hili ni utekelezaji wa mkakati wa Tigo wa kufikisha huduma karibu na wateja na tunaamini kuwa duka hili litatoa fursa za biashara kwa wateja na kuchochea ukuaji wa uchumi mkoani hapa,” alisema Karembo.

  Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali mstaafu Emmanuel Maganga aliipongeza Tigo kwa Kwa jitihada zake za kuhakikisha wateja wanapata huduma zenye viwango vya kimataifa maeneo yote ya nchi.

  “Duka hili jipya litakuwa chachu katika uboreshaji wa huduma za mawasiliano hapa mkoani Kigoma.Mkoa huu una wakazi wachapa kazi na wafanyabiashara ambao wanatamani kujikwamua kiuchumi hivyo hii ni fursa muhimu kwao,” alisema.

  Aliongeza “Hii ni faraja kuona kwamba sasa huduma za Tigo zitapatikana kwa urahisi zaidi na hii itasaidia kufungua fursa nyingi za kiuchumi.”
  Duka hilo linalopatikana katika mtaa wa Lubengela Kigoma Mjini, ni la kwanza mkoani humo na litakuwa likitoa huduma sambamba na dawati la wateja lililopo Wilayani Kasulu.

  “Duka hili limewekwa katika eneo hili kimkakati ili kufikika kwa urahisi kwa wakazi wa Kigoma na maeneo jirani na mipakani,” alisema Madati.
  Duka hilo linaifanya Tigo kuongeza kasi ya usambazaji wa huduma zake maeneo mbalimbali ya nchi ili kufikia wateja wake zaidi ya 11.6 milioni jambo linalofungua milango kwa wateja kufurahia huduma za kidigitali zinazotolewa na kampuni hiyo.

  0 0

  Afisa Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Chama Siriwa (kulia) akimuelimisha mfanyabiashara wa Wilaya ya Gairo mkoani Morogoro kuhusu umuhimu wa kutunza kumbukumbu za mauzo wakati wa Wiki ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi Wilayani hapo.
  Afisa Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Morgan Njama (kulia) akiwaelimisha Wafanyabiashara wa Wilaya ya Kilosa katika Mji wa Mikumi mkoani Morogoro wakati wa Wiki ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi Wilayani hapo.

  Afisa Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bi. Dinah Lwaga (kulia) akichukua maoni ya Mfanyabiashara wa Wilaya ya Kilosa katika Mji wa Mikumi mkoani Morogoro wakati wa Wiki ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi Wilayani hapo.


  ********************************************


  Na Veronica Kazimoto

  Morogoro

  Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imewafikia na kuwaelimisha wafanyabiashara zaidi ya 700 kupitia kampeni ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi iliyofanyika mkoani Morogoro.

  Lengo la kampeni hiyo ilikuwa ni kutoa elimu kuhusu masuala mbalimbali ya kodi pamoja na kusikiliza malalamiko, changamoto na maoni kutoka kwa wafanyabiashara hao.

  Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa kampeni hiyo mwishoni mwa wiki, Afisa Msimamizi wa Kodi Mkuu wa TRA, Julius Mjenga amesema kuwa, mamlaka hiyo ililenga kuwafikia wafanyabiasha 500 lakini kutokana na mwitikio mkubwa, TRA imefanikiwa kuvuka lengo hilo na kuwafikia zaidi ya 700.

  “Wiki hii moja ya elimu kwa mlipakodi, tuliwalenga wafanyabiashara wa wilayani ambapo kumekuwa na changamoto ya kutokupata elimu ya kodi kwa wakati. Nashukuru tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa sababu tumeweza kuwaelimisha wafanyabiashara 774 katika kampeni hii”, alisema Mjenga.

  Mjenga ameongeza kuwa “Tumefika karibu wilaya zote za mkoa huu wa Morogoro ambazo ni Malinyi, Ulanga, Kilosa, Mvomero, Kilombero na Gairo na kila mahali tulipopita tumepata mwitikio mkubwa kutoka kwa wafanyabiashara na wananchi mbalimbali.”

  Kwa upande wa wafanyabiashara waliotembelewa na TRA, wameishukuru mamlaka hiyo kwa kuwaelimisha masuala mbalimbali yanayohusu kodi na kuomba elimu hiyo iwe endelevu.

  Wakizungumza kwa nyakati tofauti, baadhi ya wafanyabiashara hao wamesema kuwa, TRA ya sasa sio ile ya zamani kwa sababu sasa hivi maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania wamekuwa karibu na walipakodi na siku hizi hawana tabia ya kufunga biashara zao.

  “Zamani mtu alikuwa akisikia watu wa TRA wanakuja, anafunga duka anaondoka lakini siku hizi, TRA wamekuwa marafiki, wanatuelimisha na wala hawafungi biashara zetu, kwakweli tunashukuru sana,” alisema Eleonora Kisimba, mfanyabiashara wa duka la nguo wa wilayani Mvomero.

  Naye Stanphord Mjumbe ambaye ni mfanyabiashara wa duka la vifaa vya ujenzi wilayani Gairo mkoani hapa alisema kuwa, kampeni ya elimu kwa mlipakodi ifanyike mara kwa mara kwa sababu wafanyabiashara walio wengi hususani wadogo hawajasoma hivyo wanahitaji kuelimishwa zaidi juu ya haki na wajibu wao katika ulipaji kodi.

  “Sisi wafanyabiashara wadogo, tulio wengi hatujasoma hivyo tunahitaji elimu hii angalau kwa mwaka mara tatu ili tuweze kuelewa kwa kina haya mambo ya ulipaji kodi maana wakati mwingine tunakuwa hatujui haki zetu,” alisisitiza Mjumbe.

  Aidha, wafanyabiashara hao wameiomba Mamlaka ya Mapato Tanzania kurejesha Kodi ya Zuio kwa wamiliki wa majengo kwa kuwa baadhi yao hawataki wapangaji kuzuia asimilia kumi na kuiwasilisha TRA.

  Vilevile, wameomba kuelimishwa jinsi ya kulipa kodi ya mapato kwa awamu mara tu wanapokadiriwa kodi hususani kwa wafanyabiashara wapya kwani wengi wao wanapitiliza tarehe za kulipa kodi hiyo kwa kukosa uelewa. 

  Kampeni ya huduma na elimu kwa mlipakodi imemalizika tarehe 17 Novemba, 2019 na ilifanyika katika Mikoa ya Morogoro na Pwani ambapo wafanyabiashara wamepata fursa ya kutembelewa katika maduka yao na wengine walihudhuria semina kwa ajili ya kuelimishwa masuala mbalimbali yanayohusu kodi.

  0 0

  NA RIPOTA WETU, KISARAWE

  KATIKA hali isiyo ya kawaida, idadi kubwa ya wanawake wilayani Kisarawe mkoa wa Pwani wamejitokeza kujisajili Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili kupata Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) hatimaye watambulike kama walipakodi na waweze kufanya biashara zao kwa uhuru na halali.

  Hali hiyo ilijitokeza wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma, elimu ya kodi na usajili wa walipakodi inayoendelea katika mkoa wa Pwani ambapo katika wilaya za Mkuranga, Kibiti na Rufiji idadi kubwa ya wanaume ndiyo iliyokuwa inajitokeza kupata TIN lakini hali imekuwa tofauti katika Wilaya ya Kisarawe ambapo idadi kubwa ya wanawake ndiyo iliyojitokeza.

  Meneja wa Huduma kwa Mlipakodi kutoka TRA, Honesta Ndunguru amesema ni kweli kwamba idadi kubwa ya wanawake wamejitokeza kupata Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi katika Wilaya ya Kisarawe ukilinganisa na wilaya zingine za mkoa wa Pwani walikopita.

  Ndunguru amesema, TRA imevutiwa na mwamko wa wananchi wa wilaya zote katika mkoa wa Pwani na kuwapongeza wale wote waliojitokeza kupata huduma, elimu pamoja na kujisajili kuwa walipakodi.

  “Kwa mwitikio huu, inadhihirisha kwamba elimu ya kodi tunayoitoa inawafikia walengwa na wanafuata sheria ya kodi inayomtaka kila mfanyabiashara kujisajili na kupata Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi inayotolewa bure na TRA”, amesema Ndunguru.

  Kwa mujibu wa Ndunguru kati ya wananchi 10 waliojitokeza kupata TIN 8 kati yao walikuwa wanawake, tofauti na wilaya nyingine ambapo idadi kubwa walikuwa wanaume.

  Baadhi ya wanawake waliojitokeza katika viwanja vya stendi ya zamani ili kusajiliwa na kupata TIN hawakusita kueleza hisia zao ya kwamba wanawake wa wilaya ya Kisarawe wamepata mwamko wa kufuata sheria za nchi zikiwemo za kulipa kodi ili waweze kutumia fursa mbalimbali ambazo zionatokana na kutambulika na serikali kama vile kupata mikopo ya wajasiliamali na huduma zingine muhimu.

  “Binafsi nimehamasika na kuja kupata Tin kwa sababu nimeelimishwa na maofisa wa TRA na nimeelewa umuhimu wa kujisajili kama mlipakodi na kulipa kodi kwa nchi yangu”, amesema Fatma Omari

  Naye Sophia Ndume mkazi wa Kisarawe ameongeza kuwa wanawake wa Kisarawe ni wahangaikaji katika biashara ndiyo maana wamehamasika kwa wingi kuja kuchukua TIN ili wakafanya biashara zao kwa uhuru bila kubughudhiwa.Zainess Madeng’ha ambaye ni mmiliki wa saluni ya kike, amesema amehamasika kuchukua TIN baada ya kupata elimu kutoka kwa maofisa wa TRA na kwamba huduma hiyo imesogezwa karibu na inapatikana bure.

  “Kwa kweli nimeona nitumie fursa hii kwa kuwa huduma imenifuata dukani kwangu na vile vile Napata huduma hii bure bila kulipia chochote”, alisema.
  TRA inafanya wiki ya elimu kwa mlipakodi katika mikoa ya Pwani na Morogoro kwa lengo la kusogeza huduma za ulipaji kodi karibu na wananchi lakini pia kusajili walipakodi ili kuongeza idada ya walipakodi nchini.
  Zainess Madeng'ha (kulia), mkazi wa Kisarawe mkoani Pwani akifurahia kupokea Cheti cha Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) kutoka kwa maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika wiki ya mlipakodi inayoendelea mkoa wa Pwani.
  Afisa wa TRA akiwahudumia akina mama hawa kupata Vyeti vya Utambulisho wa Mlipa kodi yaani TIN, huko Kisarawe mkoani Pwani.
  Wanawake wa wilaya ya Kisarawe wakichangamkia fursa ya kupata Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN)

  0 0


   Mkurugenzi mtendaji wa benki ya NIC Tanzania Limited Margaret Karume, amewaasa wanafunzi wa shule ya sekondari Loyola kujifunza kwa kuzingatia mtizamo mpana wa kidunia ili kuendana na mfumo wa sasa wa kielimu wa kidunia unaohitaji wahitimu wenye uwezo mkubwa wa kuelewa mambo na matatizo mbali mbali na kisha kuyatafutia suluhisho.

  Karume aliyekuwa mgeni rasmi katika mahafali ya 21 ya shule hiyo alitoa wito huo, sambamba na kukabidhi mchango wa magodoro 100 kwa ajili ya kuboresha mazingira wanayoishi wanafunzi wa shule hiyo.

  Mkurugenzi huyo pia aliwaambia wanafuzi wa Loyola kuwa ili kuendana na dunia ya sasa, wanatakiwa kufanya jitihada binafsi za kutafuta maarifa na ujuzi na siyo tu kutegemea kile wanachofundishwa na waalimu wao darasani  na kusisitiza kuwa bado wana safari ndefu.

  “Elimu mliyoipata bado ni ya hatua za mwanzo tu, hasa ukizingatia kukua kwa utandawazi. Kutokana na mabadiliko makubwa yanayoenda sambamba na ukuaji wa haraka wa Sayansi na Teknalojia yanayomgusa kila mtu na katika kila nyanja ya maisha, sote tutalazimika kuendelea form 6 kujifunza mambo mapya hadi mwisho wa maisha yetu,” alisema

  Karume aliwaambia wahitimu hao watarajiwa kwamba ni wajibu wao kuendelea kujifunza mbinu mpya za kuyakabiliana na maisha na pia kujijengea uwezo wa kujiajiri pindi watakapomaliza elimu ya juu

  Elimu mliyopata na ambayo mtaendelea kuipata itafungua maisha yenu na ya jamii nzima ikiwa ni pamoja na familia zenu na watoto wenu. Elimu hii pia itawapa uwezo wa kiuchumi, itawapa uwezo wa kuwa na sauti, mtaongea, mtasikika na kusikilizwa, pia itawajengea heshima katika jamii na kuwapa uwezo wa kuchangia mambo mbali mbali katika maisha. 

  Aliwataka kuiga mifano ya wanafunzi waliosoma shuleni hapo na ambao wamefanikiwa kimaisha baadhi yao wakiwa ndani na wengine nje ya nchi

  Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule hiyo Padri Obwanda Meyo, SJ alimuhakikishia mgeni rasmi kuwa wanafunzi wake wamejiandaa vizuri kwa ajiili ya mitihani ya mwisho na hivyo watafanya vizuri 
  Mkurugenzi mtendaji wa benki ya NIC Tanzania Limited, Margaret Karume (kushoto) akiwa ni mgeni rasmi wa sherehe ya wahitimu wa kidato cha nne wa shule ya sekondari Loyola akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi  milioni 4.7/- kwa mkuu wa shule hiyo Father Ubwanda Meyo jana, ikiwa ni sehemu ya mchango wa benki ya NIC kwa ajili ya kununulia magodoro 100 yatakayotumika kwenye mabweni ya wasichana wa  shule hiyo.
  Mkurugenzi mtendaji wa benki ya NIC Tanzania Limited Margaret Karume akizungumza na wageni waalikwa , wanafunzi na walimu wa shule ya sekondari Loyola waliohudhuria kwenye mahafali ya wanafunzi wa kidato cha nne shule hiyo jana jijini Dar es salaam
  Mkurugenzi mtendaji wa benki ya NIC Tanzania Limited, Margaret Karume (wa pili kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa shule ya sekondari Loyola, Padri Obwanda Meyo (wa tatu kulia), mwakilishi wa wazazi watoto wa kidato cha nne, Joseph Tadayo (kulia), Brigitte Asenga na Annah Lupembe (kushoto) ambaye ni meneja wa tawi la NIC Kariakoo.
  Mkurugenzi mtendaji wa benki ya NIC Tanzania Limited Margaret Karume akifurahi na wanafunzi wahitimu wa kidato cha nne shule ya sekondari Loyola.
  Mkurugenzi mtendaji wa benki ya NIC Tanzania Limited, Margaret Karume (wa pili kulia mbele) akiwa kwenye picha ya pamoja na wahitimu wa kidato cha nne wa shule ya sekondari Loyola, Mkuu wa Shule Padri Obwanda (aliyebeba mtoto), Mwakilishi wa wazazi, Joseph Tadayo , Mwenyekiti wa PTA Luyola, Brigitte Asenge na Meneja wa Tawi la NIC Kariakoo, Annah Lupembe (mwisho kushoto)
  Mkurugenzi mtendaji wa benki ya NIC Tanzania Limited, Margaret Karume akiwa na kikombe alichopewa zawadi na uongozi wa shule ya sekondari Loyola.
  0 0

  Na Said Said Mwishehe,Michuzi Globu ya jamii

  KAMPUNI ya Teknolojia ya malipo ulimwenguni(VISA) imezindua kampeni katika msimu huu wa sikukuu Watanzania wenye kadi ya  VISA wataweza kufanya malipo yao ya manunuzi bila kutumia fedha taslimu ambapo pia watakaofanya manunuzi watapata zawadi mbalimbali .

  Kampeni hiyo imezinduliwa jijini Dar es Salaam na Kampuni ya VISA imewahimiza wanunuaji bidhaa katika Jiji hilo kwenda katika maduka makubwa kwa ajili ya kufanya manunuzi katika msimu huu wa sikukuu.

  Akizungumza kuhusu kampeni hiyo, Meneja wa VISA nchini Tanzania Olever Njoroge amesema itaendelea hadi Desemba 22 mwaka huu ambapo wateja ambao watafanya malipo kwa kutumia kadi ya VISA na VISA kwenye simu ya mkononi  watapata nafasi ya kushinda zawadi mbalimbali.

  Amesema kampeni hiyo ambayo wameizundua kwa ajili ya wateja wenye Kadi za VISA ina malengo  ya kuhamasisha utumiaji wa kadi ya VISA au VISA kwenye simu wakati wa manunuzi katika maduka ya Mliman City Mall, Shoppers Masaki na Shopers Mikochoni.

  "Kampeni hii ina malengo ya kukuza utumiaji wa kadi ya VISA na VISA kwenye simu ya mkononi, Tunawahamiza wateja wetu wa Tanzania kufanya malipo kwa njia ya Visa ambapo itawapa urahisi na usalama kipindi cha manunuzi wakati huu wa Krismasi,"amesema Njoroge.

  Ameongeza kuwa wanaileta VISA kwa Watanzania wakizingatia faida katika kufanya manunuzi yao kwa kutumia kadi ya VISA au VISA kwenye simu ya mkononi ma kwamba wanajivua kwamba sasa Watanzania wapo huru kutumia njia mpya za malipo bila kuwa na fedha mkononi.

  Amefafanua kuwa kampeni hiyo ya Krismasi na VISA itawapa wanunuzi  fursa ya kuchagua Zawadi za aina gani kumpatia mteja wao kwa njia rahisi na salama wanaponunua bidhaa kwenye Mall.

  Amesema mapema mwaka huu VISA kwa kushirikiana na benki 15 za Tanzania wazilizindua VISA kwa njia ya simu ya mkononi ."VISA kwa kushirikiana kwa njia ya simu ya mkononi ni suluhisho la malipo ya dijiti ambayo inaruhusu watumiaji kutumia fedha kwa kila mmoja bila kulipa ada ya ununuzi. 

  "Kutumia huduma hiyo ,mtu anapaswa kupakua app ya benki yake, atafute VISA kwenye app na alipe  bidhaa na huduma kwa kuiscan code ya QR au kwa kutumia nambari ya USSD,"amesema huku akielezea wazi Watanzania wengi wamekuwa na muamko mkubwa wa kutumia VISA kufanya malipo katika manunuzi mbalimbali.
   Mfanyakazi wa Kampuni ya VISA Mary Njau (kushoto) akiwa na moja ya wateja wanatumia VISA kufanya malipo wakati wa uzinduzi wa kampeni inayoitwa  'Sherekea na Visa' ambayo imezinduliwa jijini Dar es Salaam
   Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya VISA wakiwa wameshika bango wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kufanya malipo kwa kutumia kadi ya VISA katika kipindi hiki cha kuelekea msimu wa Sikuu ya Krismasi .Uzinduzi huo umefanyika Mliman City jijini Dar es Salaam
  Sehemu ya wafanyakazi wa kampuni ya VISA wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kufanya.malipo ya fedha kwa kutumia kadi ya VISA ambayo ni maalum katika kipindi hiki cha kuelekea Sikukuu ya Krismasi

  0 0

  MKUU wa Wilaya ya Ubungo – Kisare Makori (kushoto) na Mkuu wa Idara ya Wateja Binafsi wa Benki ya NMB – Omari Mtiga (wa pili kulia) wakifunua kitambaa kuashiria uzinduzi rasmi wa tawi jipya la NMB Mbezi Louis. Kulia ni Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam – Badru Idd.
  MKUU wa Wilaya ya Ubungo – Kisare Makori, akikata Utepe kuzindua rasmi Tawi jipya la Benki ya NMB Mbezi Louis wakati wa hafla ya uzinduzi huo iliyofanyika juzi Mbezi Mwisho jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam – Badru Idd, Mkuu wa Idara ya Wateja Binafsi wa NMB – Omari Mtiga, Katibu Tawala Wilaya ya Ilala – James Mkumbo na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo, Fortunata Shija.
   


  Benki ya NMB imefungua tawi lake jipya jijini Dar es Salaam ikiwa ni utekelezaji wa mpango wake wa kufikisha huduma za kibenki kwa Watanzania wengi ili kuchochea ukuaji wa uchumi.

  Ufunguzi wa tawi hilo la NMB Mbezi Louis unaifanya benki hiyo kuwa na jumla ya matawi matano ndani ya wilaya ya Ubungo pekee. 

  Akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa tawi hilo mwishoni mwa wiki, mkuu wa kitengo cha wateja binafsi wa NMB, Omari Mtiga, alisema uamuzi wa kufungua tawi hilo umetokana na tafiti mbalimbali zilizoonyesha kuwa Mbezi Louis ni eneo linalokuwa kwa kasi katika biashara.

  “Tumeona eneo hili linakuwa kwa kasi sana kibiashara lakini wateja wetu bado wamekuwa wakilazimika kusafiri kilometa 15 wakifuata huduma zetu katika matawi ya Ubungo, Sinza, Mlimani City na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Sambamba na kauli mbiyo yetu ya: Karibu Yako, tumeona tufungue tawi hapa hapa,” alisema.

  Akifungua tawi hilo, Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Makori, alisema upatikanaji wa huduma za kibenki ni muhimu katika kuchochea ukuaji wa uchumi wa nchi.

  “Ufunguzi wa tawi hili la NMB utasaidia kukuza idadi ya Watanzania wanaotumia huduma za kibenki ambao kwa hivi sasa wapo chini ya asilimia 20,” alisema.

  Aliipongeza NMB kwa kuja na njia za kidijiti za kufikisha huduma zake kwa Watanzania, akitolea mfano wa huduma inayowezesha watu kufungua akaunti ya benki hiyo moja kwa moja kwa kutumia simu za mkononi bila kulazimika kwenda katika tawi lolote la benki.

  “Hivi karibuni, NMB imekuja na huduma inayolenga kuwahudumia waendesha bodaboda. Hii ni hatua inayostahili pongezi,” alisema Makori.

  Tawi la Mbezi Louis linaifanya NMB kuwa na jumla ya matawi 224 nchi nzima

  0 0
  RC wa Songwe Brigedia Jenerali Mstaafu Nicodemas Mwangela aliye mbele na DC wa Ileje Ndg.Joseph Mkude wakiwa kwenye Maporomoko ya Lusalala yaliyopo kwenye Mto Sange Wilayani Ileje
  Mkuu wa Mkoa wa Songwe akiongozana na DC wa Ileje kutembelea kitalu cha miti cha Shamba la Iyondo Mswima.
  Barabara ya Isoko hadi Katengele na Sange ikikatisha katikati ya msitu wa asili wa Iyondo Mswima wanamoishi nyani jamii ya mbega wenye rangi nyeupe na nyeusi moja ya vivutio vya utalii.
  Mzee Yangison Mtawa aliye kushoto akitoa maelezo kwa RC Mwangela wa Songwe ambapo alielezea ugumu wa soko kwa bidhaa za mianzi anazozalisha.
  Viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Songwe na Wilaya ya Ileje wakigongeana glasi kusherekea Siku ya Kuzaliwa ya Mkuu wa Mkoa wao Nicodemas Mwangela aliyetimiza miaka 62.  Na Daniel Mwambene Ileje Utalii

  RC wa Songwe atembelea vivutio vya utalii wilayani Ileje afurahishwa na Mradi wa Shamba la Iyondo-Mswima akihimiza kulindwa kwa misitu ya asili iliyopo wilayani humo asherehekea siku yake ya kuzaliwa katika vilele vya milima ya shamba hilo.

  Ukiwa ni mwisho wa juma siku ya Jumamosi Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Jenerali Mstaafu Nicodemas Mwangela alitembelea vivutio vya utalii vilivyopo wilayani Ileje ikiwa ni sehemu ya utalii wa ndani kwa timu nzima aliyokuwa amefuatana nayo.

  Ziara hiyo ya siku moja ilimwezesha kufika hadi Kijiji cha Ndembo mahali panapozalishwa nyungo zitokanazo na mianzi ambapo aliweza kukutana na wasukaji akiwahimiza kuungana kkatika vikundi ili kuweza kutambuliwa na serikali na kuongeza uzalishaji wenye tija.

  Kiongozi huyo,aliweza kufika nyumbani kwa Mzee Mtawa akiagiza uongozi wa wilaya hiyo kuhakikisha wanamsaidia kutafuta soko la bidhaa anazozalisha mzee huyo baada ya kuambiwa kuwa amekuwa akisubiri tu matukio kama vile nane nane na kimondo baada ya hapo bidhaa alizozalisha kwa gharama zikihifadhiwa.

  Safari hiyo ikiendelea kwa kuupanda mlima Kashima ambao kwa madereva wengine huwa ni kipimo tosha cha fani hiyo kutokana na kona kali zilizofunikwa na misitu ya asili inayoongeza radhaa a utalii.

  Alipofika katika Mradi wa Shamba la Miti wa Iyondo Mswima aliweza kupokea taarifa ya mradi huo toka kwa Meneja wa hamaba Ndg.Deograsian Kavishe akiridhishwa na taarifa hiyo jinsi inavyoakisi uhalisia wa mazingira ya eneo hilo na kuwa kiutio tosha cha kitalii.

  Msafara ulielekea shamani ilikopandwa miti,huku macho yakiendelea kufaidi mandhari nzuri ya vilele vya milima vilivyofunikwa nyasi fupi ambazo baadeya zaweza potea kutokana na kufunikwa na miti inayoendelea kupandwa.

  Mara baada ya kufika sehemu maalum iliyokuwa imeandaliwa likafanyika tukio la kukumbuka tarehe ya kuzaliwa kiongozi huyo yaani ikifurahiwa na kila mmoja kutokana na mahali ilipoandaliwa huku ikinyunyiziwa na manyunyu yaliyoshuka polepole yakiashiria neema na utukufu wa Mwenyezi Mungu.

  Mwisho wa safari yake ilikuwa ni katika Maporomoko ya Lusalala yaliyopo kwenye Mto Sange ambapo kuliweza kuwatoa jasho watalii hao wa ndani kutokana na mteremko mkali ambao haukuonesha kumteteresha Brigedia Jenerali huyo mstaafu.

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Sebastian Waryuba (mwenye suti) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa duka jipya la Vodacom wilayani humo juzi. Kushoto kwake ni Mkuu wa mauzo kanda ya Pwani wa kampuni ya Vodacom Liston Clay Chale.
  Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Sebastian Waryuba (mwenye suti) akizungumza na wageni waalikwa na wafanyakazi wa Vodacom wilayani Tandahimba mwishoni mwa wiki. Kulia kwake ni Mkuu wa mauzo kanda ya Pwani kampuni ya Vodacom Liston Clay Chale.
  Mkuu wa mauzo kanda ya Pwani kampuni ya Vodacom Liston Clay Chale akimuelezea Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Sebastian Waryuba namna Vodacom Tanzania ilivyowekeza kufikisha huduma kwa wateja kote nchini.
  Wafanyakazi wa duka la Vodacom Korogwe mjini wakiwa kwenye picha ya pamoja kabla ya uzinduzi wa duka jipya la kisasa wilayani humo juzi
  Mkuu wa wilaya ya Korogwe, Kissa Kasongwa (katikati) akikata utepe kuzindua rasmi duka jipya la Vodacom mjini Korogwe juzi. Kulia ni Brigita Stephen mkuu wa kanda ya kaskazini Vodacom
  Wafanyakazi wa Vodacom wakiendelea na zoezi la usajili wa laini za simu kwenye uzinduzi wa duka jipya mjini Korogwe

  0 0


  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Mark Ocitti (kushoto), akipokea tuzo ya udhamini wa mashindano ya gofu ya Waitara trophy 2019 kutoka kwa mwenyekiti wa klabu ya gofu Lugalo, Brigedia Generali mstaafu, Michael Luwongo (kulia) katika hafla ya chakula cha jioni iliyofanyika jijini Dar es Salaam jumamosi.

  Mgeni rasmi Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamin Sitta  akimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza mashindano ya Gofu ya Waitara trophy 2019, Samuel Kileo aliyeshinda kwa NET 64

  Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamin Sitta  akimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Mark Ocitti kwa kampuni ya hiyo kudhamini mashindano ya Gofu ya Waitara trophy 2019
   Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Mark Ocitti akizungumza na wageni waalikwa kwenye hafla ya chakula jioni iliyoambatana na  kutoa zawadi kwa washindi wa mashindano ya Gofu ya Waitara trophy 2019.
   Wageni waalikwa waliohudhuria kwenye hafla ya chakula cha jioni


  0 0


  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Mtwara ambako alifungua Kongamano la Biashara na Wakandarasi kwa Kanda ya Kusini lililofanyika kwenye ukmbi wa Tawi la Benk Kuu - Mtwara, Novemba 18, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua Kongamano la Biashara na Wakandarasi kwa Kanda ya Kusini lililofanyika kwenye ukumbi wa Tawi la Benki Kuu- Mtwara, Novemba 18, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Baadhi ya washiriki wa Kongamano la Biashara na Wakandarasi kwa Kanda ya Kusini wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati alipofungua Kongamano hilo kwenye ukumbi wa Tawi la Benki Kuu- Mtwara, Novemba 18, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

  0 0

   Wakati kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa zikiendelea nchini, aliyekuwa Meya wa Jiji la Arusha Kalisti Lazaro amejiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kupokelewa na Ndg. Humphrey Polepole Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM.

  Ndugu Kalisti Lazaro aliyefika katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es Salaam ameeleza amefikia uamuzi huo baada ya kupitia wakati mgumu akiwa katika Wadhifa wake wa Meya wa Jiji la Arusha.

  Ndugu Kalisti amesema amepokea barua za maonyo mara kadhaa kutoka Uongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambazo zilimtaka kutokutoa ushirikiano na Viongozi wa Serikali ambao anatakiwa kufanya nao kazi ngazi ya Mkoa na Wilaya na kutompongeza hadharani Ndg. John Pombe Joseph Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi nzuri ambayo ameifanya Nchini ikiwamo katika Mkoa wa Arusha.

  Vitisho vya mara kwa mara ikiwamo dhidi ya uhai wake ndio vimepelekea kujivua nafasi zake zote katika Chadema na kujiunga na CCM, Chama ambacho kinashughulika na utatuzi wa kero za wananchi. Ndg. Lazaro pia amechukizwa na Chama chake kujitoa katika uchaguzi huku akiita kitendo hicho uvunjaji wa demokrasia ambacho ndani ya masaa mawili uamuzi wa Kamati Kuu ya Chadema iliwanyima mamilioni ya wapenda demokrasia haki ya kushiriki katika Uchaguzi huu wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji.

  Ndg. Kalisti Lazaro amesema sasa yuko tayari kuchapa kazi ya wananchi akiwa ndani ya Chama ya Mapinduzi na kwamba yuko tayari kwa maelekezo ya kazi kutoka Uongozi wa CCM.

  Ndg. Kalisti kwa kujiunga na CCM amejiuzuru nafasi ya Udiwani, Umeya wa Jiji la Arusha, Uenyekiti wa Mameya na Madiwani wote wa Chadema Nchini na Ujumbe wa Kamati Kuu ya Chadema.

  Ndugu Kalisti Lazaro atapokelewa rasmi na wanachama wa CCM Mkoa wa Arusha katika tarehe itakayopangwa hivi karibuni.

  Imetolewa na,

  IDARA YA ITIKADI NA UENEZI
  CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)

older | 1 | .... | 1891 | 1892 | (Page 1893) | 1894 | 1895 | .... | 1898 | newer