Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1888 | 1889 | (Page 1890) | 1891 | 1892 | .... | 1897 | newer

  0 0


  Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya Aggrey & Clifford, Ibrahim Kyaruzi, akipokea tuzo kwa niaba ya kampuni kutoka kwa Mkurugenzi wa kampuni ya Bankable Tanzania Limited Lawrence Mafuru (Kushoto)

  Kampuni ya matangazo na ukuzaji masoko ya Aggrey & Clifford, kwa mara nyingine imepata tuzo kutokana na kuwa miongoni mwa makampuni 100 ya kati yanayofanya vizuri kibiashara.

  Kampuni ya Aggrey & Clifford ambayo hivi karibuni ilisherehekea miaka kumi tangu kuanzishwa kwake, ilitunukiwa tuzo hiyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam kwenye hafla fupi iliyofanyika Serena Hotel.

  0 0

  KINA mama wameshauriwa kuwanyonyesha watoto wao kuanzia umri 0 hadi miezi sita ili waweze kupata afya bora ambayo itamsaidia kumjenga kimwili na kiakili katika ukuaji wake.

  Hayo yalisemwa na Mratibu Lishe Mkoa wa Dar es Salaam, Neema Kweba ambapo alisema kuwa kitendo cha kuacha kuwanyonyesha kabla ya muda kwa kisingizio cha maziwa hayatoki kunaweza kusababisha udumavu wa mwili na akili.

  Alisema mtoto anatakiwa kunyonyeshwa maziwa ya mama kuanzia anapozaliwa (umri 0) hadi umri wa hadi umri wa miaka miwili na zaidi huku akifikisha miezi sita anatakiwa kupewa vyakula mchanganyiko yakiwamo maziwa ya mama yake.

  Alisema maziwa ya mama yana virutubisho vingi ambavyo vinasaidia katika ukuaji wake jambo ambalo linawamfanya mtoto kuwa na afya bora Na kuendelea kukua bila ya matatizo yoyote.

  "Kuna baadhi ya kina mama wana tabia ya kuwaachisha watoto kunyonya kabla ya wakati kwa kisingizio cha maziwa hayatoki, jambo ambalo ni uongo na kwamba linaweza kusababisha udumavu kwa mtoto kwa kushindwa kukua ipasavyo," alisema Kweba.

  Aliongeza kuwa, hivyo basi wanapaswa kubadilika na kunyonyesha watoto wao kuanzia umri 0 hadi miaka miwili na kwamba wakifikisha umri wa miezi sita wanapaswa kuwaanzishia vyakula mchanganyiko vyenye virutubisho huku akiendelea kunyonya,hali ambayo itaimarisha afya yake.

  "Ninawasihi wanawake wenzangu acheni tabia ya kusingizia maziwa hayatoki ili muweze kuwaachisha watoto wenu kabla ya wakati, kufanya hivyo kunaweza kusababisha udumavu kwa mtoto au kukosa afya bora, kwa sababu maziwa ya mama ni muhimu kwa afya yake na kwamba yanamsaidia katika ukuaji wa afya ya mwili na akili," alisema Kweba.

  Aliongeza kuwa, mtoto anapokosa afya bora, madhara yake ni makubwa ikiwa ni pamoja na kupata udumavu au utapiamlo, ukosefu wa kinga za mwili ,jambo ambalo linaweza kusababisha ubongo wake kushindwa kukua ipasavyo.

  Alisema kuwa kila mzazi anayenyonyesha ana wajibu wa kuhakikisha anamnyonyesha mtoto hadi afikie umri wa miaka miwili au zaidi huku akiendelea kumpa chakula mchanganyiko, jambo ambalo litamsaidia mtoto kuwa na afya bora pamoja na kumkinga na maradhi.

  Alisema mkakati wa Mkoa ni kuhakikisha kuwa wanaendelea kutoa elimu ya lishe kwenye vituo vya afya, zahanati na hospitali pamoja na majumbani ili kuwaelimisha wazazi au ndugu wanaobaki na watoto ili waweze kuzingatia elimu ya lishe bora kwa mtoto.

  0 0

   Mkuu wa Kitengo cha Fedha Taslim na Miamala kwa Wateja Wakubwa na wa Kati  wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Jimmy Myalize akizungumza na baadhi ya wateja wao wa makampuni wa jijini Mwanza, walipokutana na kufanya mazungumzo nao wakiwafahamisha huduma mbalimbali zitolewazo na NBC na pia kupata mrejesho kutoka kwao juu ya huduma hizo na jinsi wanaweza kuwahudumia vizuri zaidi, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho  ya mwezi wa huduma kwa wateja  wa benki hiyo jijini humo hivi karibuni.
   Mkuu wa Kitengo cha Fedha Taslim na Miamala kwa Wateja Wakubwa na wa Kati  wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Jimmy Myalize (kushoto), akiwasikiliza wateja wa benki hiyo Malesh Mathade (kulia), pamoja na Mitesh Metha, walipokutana na wateja wao wa makampuni mkoani Mwanza ikiwa ni sehemu ya maadhimisho  ya mwezi wa huduma kwa wateja  wa NBC jijini humo hivi karibuni. NBC katika kipindi cha mwezi wa huduma kwa wateja imefanya mikutano kama hiyo kwa wateja wake sehemu mbalimbali nchini.

   Mkuu wa Kitengo cha Fedha Taslim na Miamala kwa Wateja Wakubwa na wa Kati wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Jimmy Myalize (katikati),akishikana mikono na Mteja wa NBC kutoka kampuni ya Marine Services,  Erick Hamissi, walipokutana na wateja wao wa makampuni mkoani Mwanza ikiwa ni sehemu ya maadhimisho  ya mwezi wa huduma kwa wateja  wa NBC jijini humo hivi karibuni.. Kulia ni Nelson Julius naye kutoka Marine Services.
   Meneja wa Huduma kwa Wateja Wakubwa wa Benki ya NBC, Mary Opiyo (wa tatu kushoto), akishikana mikono na mteja wa benki hiyo, Mkurugenzi wa Bugando Medical Centre, Padre Engelbert Nyandwi, katika hafla waliyoiandaa kwa wateja wao wa makampuni ikiwa ni sehemu  ya maadhimisho  ya mwezi wa huduma kwa wateja  jijini humo hivi karibuni. Wengine kutoka  kushoto ni maofisa uhusiano wateja wa benki hiyo, Abdallah Aruga na  Fainess Jeremiah.
  Mkuu wa Kitengo cha wafanya biashara wa kati wa Benki ya NBC Moses Minja (kushoto), akishikana mikono na mteja wa NBC kutoka kampuni ya Marine Services, Erick Hamissi, walipokutana na wateja wao wa makampuni  mkoani Mwanza ikiwa ni sehemu ya maadhimisho  ya mwezi wa huduma kwa wateja  wateja jijini humo  hivi karibuni. Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Fedha Taslimu na Miamala kwa Wateja Wakubwa na wa Kati wa  NBC, Jimmy Myalize.

  0 0


  Meneja Mkuu wa QNET, kanda ya Kusini mwa Jangwa la Sahara ya Afrika, Bwana Biram Fall.

  ***********************

  QNET, Kampuni ya biashara ya mtandao inayoongoza duniani imesisitizia jitihada zake za kuhakikisha kwamba wateja wake wote na wawakilishi wake wa kujitegemea (IRs) duniani kote hasa barani Afrika wanahudumiwa vizuri. QNET kupitia programu yake ya mafunzo ya mauzo ya mtandao ujulikanao kama QNETPRO inatoa mafunzo na kurudia kuwafundisha wawakilishi wake wa kujitegemea kwa lengo la kuwapatia weledi zaidi na kuwa na viwango bora vya maadili ya utendaji.

  Kwa mujibu wa Meneja Mkuu wa QNET, kanda ya Kusini mwa Jangwa la Sahara ya Afrika, Bwana Biram Fall amesema. “QNET imejidhatiti katika kutengeneza wauzaji wa moja kwa moja wenye weledi zaidi katika sekta hii ya biashara ya mauzo ya moja kwa moja kwa njia ya mtandao. Tuna viwango vya juu vya utaalamu na kupitia QNETPRO, tunatoa elimu inayohitajika katika huduma kwa wateja, masoko na mauzo ya moja kwa moja kwa wawakilishi wetu wa kujitegemea. Tunatumia mbinu kama mafunzo ya ana kwa ana, semina zinazotolewa kwa njia ya mtandao, video, maonyesho na ushauri.”

  QNETPRO inawezesha na kufundisha maadili ya msingi ya shauku, kujenga sifa au jina jema, maadili ya utendaji wa kibiashara, uwajibikaji, kufanya kazi kwa bidii, uaminifu, ukweli na kumiliki uwajibikaji.

  Bwana Fall amesema. “Tunajitahidi katika kudumisha sifa njema ambazo zinastawi kwa uwajibikaji. Kujenga mauhisano ya kudumu na kuhamasisha kila mmoja afanye mambo sahihi na kudumu katika utamaduni wa uendeshaji wa biashara wenye uwajibikaji.”

  Programu ya mafunzo na uthibitishaji ya QNETPRO ni jitihada za QNET za kukuza
  ufahamu kwa kiwango cha juu na kuwakumbusha wawakilishi wote wa kujitegemea kuhusu umuhimu wa kujenga tabia ya kufanya biashara ya mauzo ya moja kwa moja kitaalamu wakati wote. Programu hii ina lengo la kufundisha kanuni zilizoko katika sera na taratibu za QNET kuwezesha uelewa bora na kutimiza vigezo.

  Aliendelea bwana Fall. “QNET imeahidi kuipatia sekta ya mauzo ya moja kwa moja wawakilishi bora na wenye weledi zaidi katika kila kanda ambako inaendesha biashara zake. Sisi ni waanzilishi na sauti ya sekta ya mauzo ya moja kwa moja katika masoko mengi yanayochipukia na tunachukua jukumu hili kwa umakini mkubwa. Kusudio letu ni kuelimisha, kutaarifu na kufundisha wawakilishi wetu wa kujitegemea waweze kuwa na viwango vya juu katika kufanya biashara. Kama wajasiriamali wanaochipukia, sio tu kwamba wanajenga biashara inayowasaidia kuweza kuwa na uhuru wa kifedha, lakini
  kikubwa ni kwamba wanaongoza wimbi kubwa la mabadiliko.”

  Alihitimisha kuwa, “Katika QNET tunaamini katika utekelezaji wa yale yote
  tunayoyasema. Tunataka uzingatiaji kamili wa kanuni za maadili za utendaji za QNET kama utimizaji wa vigezo vya sera na taratibu zetu. Wakati huu ambapo sekta ya mauzo ya moja kwa moja imekuwa ni kazi ya kitaaluma ya kukimbiliwa katika masoko mengi yanayoibukia, ni muhimu sana kwetu kuweka viwango vya juu. Tunachukulia ukiukaji wa sera na taratibu zetu kwa umakini mkubwa. Tunatekeleza majukumu yetu kwa vitendo kupitia katika mchakato wetu wa ukaguzi na upitiaji wa uadilifu wa mitandao yetu imara. Kwa miaka mingi QNET imesitisha vibali vya wawakilishi (IRs) wengi sana katika zaidi ya nchi 30 kwa kuthibitisha kuwa hawakutimiza vigezo, ukiukaji
  wa sera, au utendaji usiozingatia maadili.”

  Mwisho, kwa kupitia programu hii, QNET inaelimisha watu kwamba biashara hii ni ya muda mrefu. Ili waweze kujenga biashara ya kudumu na ambayo itawalipa kwa muda mrefu wanapaswa kufanya mambo yao kwa usahihi. Biashara hii haikukusudiwa kuwa ni kampeni ya muda mfupi, ni kuhusu kusisitizia ujumbe wa ustahimilivu kwa kila mmoja anayetaka kufanya biashara hii ya QNET.

  QNET haitaki watu wafikirie kwamba biashara yake ni kama mpango wa kujipatia mafanikio haraka haraka au mfumo wa kujitajirisha haraka haraka. QNET inataka watu waone biashara hii kama fursa ya kweli ya kuwa mjasiriamali kwa kufuata utaratibu ule ule wa kufanya kazi kwa bidii na kujitolea na maadili ambayo yanatakiwa ili mtu aweze kujenga aina yeyote ile ya biashara ya kawaida.

  Katika mwaka 2019 pekee, timu yetu ya wakufunzi wa QNETPRO wametoa mafunzo kwa zaidi ya IRs 35,000 katika vituo 35 duniani kote. Hii inajumuisha: Hong Kong, Singapore, Dubai, Uturuki, Sudan na Tanzania. Nchi nyingi katika ukanda wa Afrika magharibi (Ghana, Senegali, Ivory Coast, Mali, Burkina Faso, Togo, Cameroun, Guinea na Niger, Sierra Leone) pia wamepatiwa mafunzo ya QNETPRO.
  0 0


  Kaimu Afisa Mkuu-Tigo Pesa, Angelica Pesha akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)katika hafla ya uzinduzi wa kampeni ya Tigo Pesa Mastercard QR, mapema leo Jijini Dar Es salaam.
  Kaimu Afisa Mkuu-Tigo Pesa, Angelica Pesha akionesha kwa waandishi wa habari jinsi ya kulipia kwa Tigo Pesa Mastercard QR,katika hafla ya uzinduzi wa kampeni ya Tigo Pesa Mastercard QR,Mapema leo Jijini Dar es salaam.
  Kaimu Afisa Mkuu-Tigo Pesa, Angelica Pesha(katikati), akijibu maswali ya waandishi wa habari (hawapo pichani)kulia kwake ni Mkurugenzi na Meneja wa Mastercard Afrika Mashariki, Frank Molla jinsi ya kulipia kwa Tigo Pesa Mastercard QR,katika hafla ya uzinduzi wa kampeni ya Tigo Pesa Mastercard QR, pembeni ni Mkuu wa Kitengo cha Malipo- Mshana Mshana.
  Kaimu Afisa Mkuu-Tigo Pesa, Angelica Pesha(katikati), akimuonyesha Mkurugenzi na Meneja wa Mastercard Afrika Mashariki, Frank Molla jinsi ya kulipia kwa Tigo Pesa Mastercard QR,katika hafla ya uzinduzi wa kampeni ya Tigo Pesa Mastercard QR, pembeni ni Mkuu wa Kitengo cha Malipo- Mshana Mshana.
  Mkurungezi Mtendaji wa Tigo Simon Karikari akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Tigo na Mastercard mara baada ya hafla ya uzinduzi wa kampeni ya Tigo Pesa Mastercard QR, mapema leo Jijini Dar Es salaam.
   
   
   Wateja wanaweza kujipatia fedha papo hapo baada ya kulipia kwa Tigo Pesa Matsercard QR.


  .Kampuni ya Mawasiliano ya Tigo kwa kushirikiana na Mastercard wamezindua kampeni kwaajili ya kuwazawadia wateja wanaofanya malipo kwa njia ya Tigo Pesa Mastercard QR katika maduka na maeneo yanayoruhusu kulipa kwa Mastercard QR.


  Kampeni hiyo imelenga katika kuhakikisha wateja wanapata huduma rahisi na ya uhakika nchi nzima.


  Akizungumza leo wakati wa hafla ya uzinduzi, Kaimu Mkuu wa huduma za fedha (MFS), Angelica Pesha alisema “Kama kampuni ya kidigitali siku zote tunalenga kuleta sulushisho na kufanya maisha ya wateja wetu kuwa rahisi zaidi.Kumekuwa na ongezeko la uhitaji wa njia mpya na salama ya malipo kwa wateja pale wanapotaka huduma na bidhaa kwenye maduka na maeneo mengine ya kibiashara yanayoruhusu mfumo wa Mastercard QR.”


  Aliongeza, “Tigo Pesa Mastercard QR ni fursa ya kuchochea agenda ya ujumuishwaji wa watu kiuchumi kwasababu Tigo Pesa ni huduma kamili ya kifedha.Kwa kupitia Tigo Pesa Mastercard QR si tu tunapanua wigo wa utoaji wa huduma zenye usalama kwa wateja bali tunasogeza huduma zenye uharaka karibu na wateja wetu,” alisema Pesha.


  Mkurugenzi na Meneja wa Mastercard Afrika Mashariki, Frank Molla alisema “Mastercard imejizatiti katika kutafuta njia mbadala ya kifedha kwa kuja na suluhisho linatoa nafasi kwa wateja kupata huduma za malipo zenye usalama na za uhakika.Shabaha hii ya kuleta mbadala wa fedha ni jambo la kujivunia hasa tunapoungana na Tigo.”


  Aliongeza “Kwa sasa biashara nyingi zinapokea malipo ya Mastercard QR ambapo wateja wanaweza kutumia njia hii ya kidigitali kujipatia zawadi ya fedha kwa malipo waliyofanya.”


  Mteja wa Tigo anaweza kufanya malipo kwa njia ya Mastecard QR kupitia App ya Tigo Pesa kwa kuscani QR code au kwa kufuata hatua zifuatazo:


  Piga *150*01#,


  Chagua namba 5,


  Chagua 2, (Lipa kwa Mastercard QR).


  Baada ya malipo,mteja atapokea zawadi ya hadi asilimia 3 ya fedha kulingana na kiwango cha malipo aliyofanya.


  Mastercard QR ni njia ya haraka na ya kidigitali yakufanya malipo ambayo kwa sasa inakubalika katika maeneo mbalimbali ya kibiashara kwa wateja wote wa Tigo Pesa.


  Mteja anaweza kufurahia huduma ya Tigo Pesa Mastercard QR katika maeneo maarufu kama vituo vya mafuta vya Puma, migahawa ya KFC, Pizza Hut na Samaki Samaki, Century Cinemax, Supermarket ya Shoppers, JD Phamacies pamoja na maduka ya GSM Mall.


  Mwisho//  0 0


  Mkuu wa Bidhaa na Huduma wa Tigo, David Umoh akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani ) wakati wa uzinduzi wa Simu simu yenye sifa za smartphone ‘Kitochi 4G Smart’ yenye uwezo wa 4G kwa bei nafuu ,Pembeni yeke ni Afisa Mkuu wa Biashara wa Tigo, Tarik Boudiaf .Uzinduzi huo umefanyika Katika makao makuu ya Tigo jijini Dar Es salaam
  Mkuu wa Bidhaa na Huduma wa Tigo, David Umoh akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani ) wakati wa uzinduzi wa Simu simu yenye sifa za smartphone ‘Kitochi 4G Smart’ yenye uwezo wa 4G kwa bei nafuu .Uzinduzi huo umefanyika Katika makao makuu ya Tigo jijini Dar Es salaam
  Afisa Mkuu wa Biashara wa Tigo, Tarik Boudiaf akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani ) wakati wa uzinduzi wa Simu simu yenye sifa za smartphone ‘Kitochi 4G Smart’ yenye uwezo wa 4G kwa bei nafuu .Uzinduzi huo umefanyika Katika makao makuu ya Tigo jijini Dar Es salaam
  Mkuu wa Bidhaa na Huduma wa Tigo, David Umoh akijibu maswali ya waandishi wa habari (hawapo pichani ) wakati wa uzinduzi wa Simu simu yenye sifa za smartphone ‘Kitochi 4G Smart’ yenye uwezo wa 4G kwa bei nafuu ,Pembeni yeke ni Afisa Mkuu wa Biashara wa Tigo, Tarik Boudiaf .Uzinduzi huo umefanyika Katika makao makuu ya Tigo jijini Dar Es salaam .
  Wateja wataweza kuipata kwa gharama ya Sh49, 000/-


  Dar es Salaam. Oktoba 30, 2019. Kampuni inayoongoza katika mageuzi ya kidigitali nchini, Tigo, leo imezindua simu yenye sifa za smartphone ‘‘Kitochi 4G Smart’ ya kwanza kwenye soko la simu Tanzania yenye uwezo wa intaneti ya 4G kwa watanzania wote ili kufungua fursa za kijamii na kiuchumi.

  Simu hiyo inayojulikana kama ‘Kitochi 4G Smart’ inapatikana sokoni kwa gharama nafuu ya Sh49, 000/- na inakuja na Applications kama WhatsApp, Facebook, Twitter na YouTube.

  Akizungumza wakati wa uzinduzi wa simu hiyo, Afisa Mkuu wa Biashara wa Tigo, Tarik Boudiaf alisema “Kama waanzilishi wa kwanza wa mtandao wa kasi wa 4G hapa nchini tangu mwaka 2014, tunavunja mipaka tena kwa kuhakikisha kila mmoja anapata simu ya 4G kwa gharama nafuu ili kuwa sehemu ya mabadiliko ya kidigitali na hatimaye kuchangia ujumuishwaji wa kidigitali hapa nchini,” alisema Boudiaf.

  Boudiaf aliongeza kuwa kwa muda mrefu gharama kubwa ya simu zenye uwezo wa 4G imekuwa kikwazo kwa watanzania wengi kumiliki simu zenye uwezo wa intaneti ya kasi hivyo ujio wa simu hiyo ni msaada kwa watanzania wengi.

  “Kwa ujio wa simu hii ya ‘Kitochi 4G Smart’ kwenye soko yenye uwezo wa Facebook ya bure kwa miezi mitatu itawapa wateja wetu uwezo wa kujumuika kwenye mitandao na hivyo kufanya kila mmoja kuwa sehemu ya mageuzi ya kidigitali,” alisema.

  Naye, Mkuu wa Bidhaa na Huduma wa Tigo, David Umoh alisema “Kitochi 4G Smart inadhihirisha dhamira ya Tigo ya kuwahudumia wateja wake katika kila hatua ya maisha.Kwa hatua hii ni imani yetu kuwa hakuna mtu ambaye atashindwa kupata manufaa yatokanayo na intaneti ya kasi ya 4G.”

  Aliongeza, “Kitochi 4G Smart itaongeza wigo wa upatikanaji wa intaneti ya 4G kwa watanzania wote na kusaidia katika ufikiwaji wa taarifa na maarifa yatakayosaidia katika kutumia vema fursa za kijamii na kiuchumi.”

  Tigo inapanua wigo wa uvumbuzi kwa kuendelea kutoa bidhaa na huduma zenye kukidhi mahitaji ya wateja sokoni na zaidi kuchangia mageuzi ya kidigitali nchini.Kitochi 4G Smart ni hatua nyingine kutoka Tigo baada ya Smartphone ya Kiswahili, Facebook ya bure, App ya Tigo Pesa Pesa na App ya Tigo.

  Wateja wa Tigo wanaweza kujipatia simu ya Kitochi 4G kwa kuweka oda kwa kupiga namba 100 na kufanya malipo ya awali.itochi 4G Smart inakuja na App kama Facebook, WhatsApp, YouTube,Twitter, Gmail, Google Map na zingine nyingi zinazopatikana kwenye kaiOS App store.

  0 0

  Mwenyekiti wa Bodi ya T-PESA, Brigedia Generali mstaafu, Ramadhan Kimweri (katikati) akizungumza kwenye uzinduzi wa huduma mpya ya Bando la TamTam ambalo linampa uhuru zaidi mteja wa TTCL kufurahiya mawasiliano nafuu ya huduma ya maongezi, inatenti pamoja na ujumbe mfupi(SMS) leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Corporation, Waziri Kindamba pamoja na Afisa Mkuu wa T-Pesa, Bi. Lulu Mkudde.
  Afisa Mkuu wa T-Pesa, Bi. Lulu Mkudde (kushoto) akizungumza kwenye uzinduzi wa huduma mpya ya Bando la TamTam ambalo linampa uhuru mteja wa TTCL kufurahiya mawasiliano nafuu ya muda wa maongezi, inatenti pamoja na ujumbe mfupi(SMS) leo jijini Dar es Salaam. 
  Mwenyekiti wa Bodi ya T-PESA, Brigedia Generali mstaafu, Ramadhan Kimweri (kulia) akipongeza moja ya kikundi cha burudani kwenye hafla ya uzinduzi huo. 
  Mmoja wa wateja wa TTCL akipata huduma kwenye uzinduzi wa huduma mpya ya Bando la TamTam.   KAMPUNI ya T-PESA imezinduwa huduma mpya ya Bando la TamTam ambalo linampa uhuru zaidi mteja wa TTCL kufurahiya mawasiliano nafuu ya huduma ya maongezi, inatenti pamoja na ujumbe mfupi (SMS).

  Huduma hiyo imezinguliwa leo jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Bodi ya T-PESA, Brigedia Generali mstaafu, Ramadhan Kimweri huku akisisitiza kuwa bidhaa hiyo imebuniwa kwa lengo la kuendelea kurahisisha huduma kwa wananchi kwa bei nafuu zaidi. Aidha aliwaomba Watanzania na wateja kwa ujumla kuendelea kutumia huduma za T-PESA ikiwa ni pamoja na kufurahiya mawasiliano ya huduma mpya ya Bando la TamTam.

  “...T-PESA inawaletea huduma bora ya kipekee kabisa ya BANDO ambalo ni NAFUU na lenye MVUTO wa aina yake kwa watumiaji. Wananchi watapata fursa ya kupata huduma kwa siku, wiki na mwezi ikiwa na muda wa maongezi, huduma ya Inatenti na ujumbe mfupi (SMS),” alisema Bw. Kimweri.

  Awali akifafanua juu ya huduma ya Bando Tam Tam la T-PESA, Afisa Mkuu wa T-Pesa, Bi. Lulu Mkudde alisema huduma hiyo itakuwa na virushi vya aina tatu, ambayo ni pamoja Kifurushi cha Siku, ambacho kinampa mteja MB 500 za kutumia intaneti, SMS 50 na dakika 5 za kupiga simu mitandao yote kwa masaa 24 kwa shilingi 500 tu.

  Alibainisha kuwa Kifurushi cha pili cha Wiki, ambacho kinampa mteja GB 1 ya kutumia intaneti, SMS 100 na dakika 5 za kupiga simu mitandao yote kwa siku 7 za wiki kwa shilingi 1000, huku akikitaja Kifurushi cha tatu cha Mwezi, ambacho kinampa mteja GB 2 za kutumia intaneti, SMS 300 na dakika 20 za kupiga simu mitandao yote kwa siku 30,kwa shilingi 5000 tu.

  Aidha alibainisha kuwa ili kuendelea kuboresha huduma za T-PESA, kampuni imeendelea kusajili mawakala nchi nzima hadi kufikia sasa T-PESA inamawakala wanaozidi zaidi ya 19,000 nchi nzima, uwepo wa mawakala hao wamechangia katika kufikisha huduma za kifedha katika maeneo mbalimbali nchini.

  “... T-PESA imekuwa miongoni mwa kampuni zenye gharama nafuu za miamala kulinganisha na watoa huduma wengine. Hivyo watanzania wanahaki ya kujivunia zaidi na kutuunga mkono zaidi kwa kutumuia huduma zetu za T-PESA.” Alisisitiza.

  “...Vifurushi hivi vinapatikana kwa mteja wa T-PESA. Jinsi ya kujiunga ni rahisi, mteja anatakiwa kupiga*150*71#. kuchagua namba 3 kununua Muda wa Maongezi au Vifurushi, halafu namba 2 kununua Vifurushi, kisha kuchagua namba 1 Bando Tam Tam.”

  0 0

   Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda akikabidhi cheti cha shukrani kwa Kaimu Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Benjamin Nkaka (kushoto), kwa kutambua mchango wa benki hiyo katika kufanikisha kongamano la wanawake lililopewa jina la ‘Madirisha’ lililoandaliwa na Kampuni ya GS1 kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), na Taasisi ya Kusaidia Sekta Binafsi ya Kilimo (PASS) ambalo benki hiyo ililidhamini na kufanyika jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni   Mwenyekiti wa Bodi ya GS1, Jumbe Menye.
   Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhandisi Stella Manyanya (kulia), akizungumza na Meneja Mahusiano Wateja wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Chiku Chambuso (kushoto), pamoja na mwenzake, Lena Mwakisale katika banda la benki hiyo wakati wa kongamano la wanawake lililopewa jina la ‘Madirisha’ lililoandaliwa na Kampuni ya GS1 kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), na Taasisi ya Kusaidia Sekta Binafsi ya Kilimo (PASS) ambalo benki hiyo ililidhamini na kufanyika jijini Dar es Salaam jana.
   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akisalimiana na Meneja Mahusiano Wateja wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Lena Mwakisale pamoja mwenzake Isdory Maumba (kushoto), alipokutana nao wakati wa kongamano la wanawake lililopewa jina la ‘Madirisha’ lililoandaliwa na Kampuni ya GS1 kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), na Taasisi ya Kusaidia Sekta Binafsi ya Kilimo (PASS) ambalo benki hiyo ililidhamini na kufanyika jijini Dar es Salaam jana.

   Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda akihutubia wakati wa kongamano la wanawake lililopewa jina la ‘Madirisha’ lililoandaliwa na Kampuni ya GS1 kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), na Taasisi ya Kusaidia Sekta Binafsi ya Kilimo (PASS) ambalo Benki ya NBC  ililidhamini na kufanyika jijini Dar es Salaam jana.

   Kaimu Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Benjamin Nkaka (kulia), akishikana mikono na Kaimu Mwenyekiti Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Angelina Ngalula wakati wa kongamano la wanawake lililopewa jina la ‘Madirisha’ lililoandaliwa na Kampuni ya GS1 kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi na Taasisi ya Kusaidia Sekta Binafsi ya Kilimo (PASS) ambalo benki hiyo ililidhamini na kufanyika jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya GS1, Jumbe Menye.
  Baadhi ya wanawake waliohudhuria wa kongamano la wanawake lililopewa jina la ‘Madirisha’ lililoandaliwa na Kampuni ya GS1 kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), na Taasisi ya Kusaidia Sekta Binafsi ya Kilimo (PASS) ambalo benki hiyo ililidhamini na kufanyika jijini Dar es Salaam jana.  BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imewataka wafanyabiashara na wajasiriamali wanawake nchini kuondoa hofu ya kutembelea na kuzungumza na wataalamu wa masuala ya fedha na biashara katika matawi ya benki hiyo ili kufahamu huduma zao na jinsi wanavyoweza kupata huduma za kifedha zitakazoweza kuinua biashara na maisha yao.

  Akizungumza wakati wa Kongamano la Kwanza la Wafanyabiashara Wanawake wakubwa na wa kati jijini Dar es Salaam jana ambao benki hiyo ililidhamini, Kaimu Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa NBC, Benjamin Nkaka, alisema ni vyema kwa wafanyabishara hao wanawake kuzoea kufanya kazi na benki kwani ni njia rahisi na pekee itakayoweza kustawisha biashara zao.

  “Kuna hofu imejengeka kwa wengi kuja benki. Hofu hiyo iondoke. Njooni benki muweze kufahamu ni nini tunakitoa katika kusapoti wajasiriamali hasa wanawake,” alisema Nkaka.

  Alisema miongoni mwa majukumu ya benki hiyo ni kusaidia katika kukuza uchumi hasa wa wanawake wajasiriamali, na kuongeza:

  “Kwa zaidi ya miaka 50 ya huduma za benki hii nchini, tunafahamu kuwa miongoni mwa changamoto zinazowakabili  wajasiriamali wanawake ni elimu ya mikopo. Sisi tunatoa elimu hiyo pamoja na ushauri kwa wateja wetu wafanyabiashara kadri biashara yao inavyoendelea na kuwaunganisha na mnyororo wa thamani.

  “NBC pia huwakutanisha wateja na wadau mbalimbali kama vile Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), Wakala wa Usajili wa Leseni za Biashara (BRELA) na taasisi nyingine. Katika harakati zetu za kuwasapoti wanawake, tumeanzisha Vikundi Akaunti ambazo hazina makato yoyote, huku pia tukishirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi ya Kilimo (PASS) kutoa mikopo yenye garantii ya hadi asilimia 80 kuwawezesha wanawake kuingia kwenye kilimo kwa nguvu.”

  Mkutano huo ulihudhuriwa na takriban wanawake wajasiriamali na wafanyabiashara 1,000 kutoka mikoa yote ya Tanzania huku mgeni rasmi akiwa Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda.

  Wanawake hao walikutanishwa kupitia mwavuli unaofahamika kama ‘Madirisha’ huku wadau mbalimbali wa maendeleo wakipata nafasi ya kuwaonyesha wanawake hao fursa mbalimbali zilizopo nchini katika kuboresha uchumi wao kama vikundi.

  Kampuni ya GS1 iliandaa kongamano hilo kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) pamoja na taasisi ya PASS.
   


  0 0

  Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya NMB – Ruth Zaipuna akiongea kwenye mdahalo ulioandaliwa na shirika la ‘International Finance Corporation’ (IFC) kuhusu Usawa wa Kijinsia Kazini. Mdahalo huo uliofanyika jana jijini Dar es Salaam, ulikutanisha Wakurugenzi kutoka taasisi za Fedha, Wajasiriamali na Jinsia nchini. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered – Sanjay Rughani na kushoto ni Bi. Hodan Addou kutoja Umoja wa Mataifa.

  0 0


  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mtwara-Mikindani  Bw. Emanuel Mwaigobeko akizungumza wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na benki ya Exim Tanzania kwa ajili ya wadau wa zao la korosho mkoani Mtwara iliyolenga kupata wasaa wa kujadili fursa mbalimbali za kibiashara hususani katika zao hilo pamoja na  uboreshaji wa huduma zitolewazo na benki hiyo kwa wadau hao mkoani humo.

   Mmoja wa wadau wakubwa wa Korosho mkoani Mtwara Bw Ramesh Kennedy akizungumza wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na benki ya Exim Tanzania kwa ajili ya wadau haoili kupata wasaa wa kujadili fursa mbalimbali za kibiashara hususani katika zao hilo pamoja na  uboreshaji wa huduma zitolewazo na benki hiyo kwa wadau hao mkoani humo.
  Mkuu wa huduma ya rejareja wa benki ya Exim, Bw. Andrew Lyimo (wa kwanza kushoto) pamoja na Mkuu wa Hazina na Masoko ya Fedha wa benki hiyo Bw Arafat Haji (wa kwanza kulia) wakiwaongoza wageni waalikwa akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mtwara-Mikindani  Bw. Emanuel Mwaigobeko (alievaa suti nyeusi) kupata chakula wakati wa hafla hiyo.

  Mtwara ; Octoba 31, 2019: Benki ya Exim Tanzania mapema wiki hii iliandaa hafla ya chakula maalum kwa ajili ya wadau mbalimbali wa zao la korosho mkoani Mtwara ili kupata wasaa wa kujadili fursa mbalimbali za kibiashara hususani katika zao hilo, mipango ya ukuaji na uboreshaji wa huduma zitolewazo na benki hiyo kwa wadau hao mkoani humo.
  Akizungumza kwenye hafla hiyo iliyohudhuliwa na wadau mbalimbali wa zao la korosho wakiwemo viongozi wa kiserikali, wafanyabiashara wakubwa na wadogo pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo, Mkuu wa huduma ya rejareja wa benki ya Exim, Bw. Andrew Lyimo alisema kupitia hafla hiyo  walilenga pia  kutoa fursa miongoni mwa wateja hao ili waweze kufahamiana na kufungua wigo wa kufanya biashara pamoja.
  “Pamoja na kushukuru kwa namna ambayo wateja wetu wamekuwa nasi hadi kufikia mafanikio ya kuikuaji na ubora wa huduma zetu, hafla hii inatoa fursa kwa wateja wetu pia kufahamiana wao kwa wao na hivyo kufungua milango ya fursa baina yao,’’ alisema Lyimo.
  Alisema ukuaji wa benki hiyo unaoshuhudiwa kwasasa ni matokeo ya ushirikiano baina yake na wateja wake ambao kwa kiasi kikubwa wameonyesha imani kubwa kwa benki hiyo hali ambayo imekuwa ikiiwezesha benki hiyo kubuni huduma bora na rafiki za kibenki ili kulinda na kurejesha imani hiyo kwa wateja wa benki hiyo.
  Pamoja na mambo mengine hafla hiyo ilipambwa na shuhuda mbalimbali kuhusu ubora wa huduma za benki hiyo kutoka kwa wadau hao.
  Akizungumza kwenye hafla hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Bw. Emanuel Mwaigobeko alisema  mkoa huo umejipanga kwa dhati kuhakikisha ununuzi wa mkorosho unaenda vyema kwa kuzuia watu wachache kuharibu taswira ya serikali pamoja na sekta nzima ya kilimo cha zao hilo.
  Pamoja na kuipongeza benki  ya Exim kwa namna inavyoshirikiana  na wadau wa zao hilo mkoani Mtwara, Bw Mwaigobeko alizitaka taasisi zinazohusika na masuala ya fedha mkoani humo kusaidia katika kuwajengea uelewa wa kutosha kuhusu masuala ya kifedha wakulima na wafanyabiashara wa zao hilo mkoani humo.
  Alisema ni matarajio yake kwamba wakulima watakuwa waaminifu kupeleka korosho safi ili wasiharibu ubora wa korosho za Tanzania katika soko la ndani na nje.


  0 0
 • 11/01/19--05:57: VIZIWI WANOLEWA NA TCRA
 • MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa imeendesha semina ya siku moja kwa watu wenye matatizo ya kutosikia (Viziwi) katika Mkoa wa Simiyu yenye lengo la kuwajengea uelewa juu ya matumizi sahihi na salama ya mawasiliano.

  Mafunzo hayo ambayo yamefanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, ambapo zaidi ya viziwi 50 wameshirikia mafunzo hayo.

  Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa Kanda ya Ziwa wa TCRA, Mhandisi Francis Mihayo amesema kuwa TCRA imeandaa mafunzo hayo kwa viziwi ili waweze kuepuka na madhara ambayo wanaweza kupata ikiwa watatumia vibaya mawasiliano.

  Mihayo ameongeza kuwa viziwi ni moja kati ya watu ambao wameendelea kukumbwa na tatizo la matumizi mabaya ya mitandao kama facebook, instagram, whatsap na twitter kwa kurusha vitu ambavyo siyo sahihi.

  “ Mara nyingi wamekuwa wakijikuta wakichukuliwa hatua kali za kisheria kwa kikuka sheria zilizopo za matumizi sahihi ya mawasiliano, kutokana na hali tumeona ni vyema tukawapa elimu jinsi gani ya wanaweza kuepuka kwa kuzitambua sheria,” amesema Mhandisi Mihayo.

  Aidha Mihayo amesema kuwa amekuwa wakipata malalamiko mengi kutoka kwa viziwi juu ya kutapeliwa kupitia simu, ambapo kupitia mafunzo hayo wataweza kuwafundisha namna bora ya kuepuka hali hiyo.

  “ Tunawaelimisha pia umuhimu wa kusajili laini zao kwa njia ya alama za vidole, tunatambua changamoto wanazozipata katika zoezi hili, ndiyo maana tumewaita hapa ili kuwapatia elimu na kutatua changamoto hiyo,” alisema Mihayo.

  Akizungumza kwa niaba ya viziwi hao Makamu mwenyekiti wa viziwi mkoa, Alex Benson viziwi wameeleza kukumbwa na tatizo la mawasiliano baina yao na watu wanaohusika katika zoezi la kusajili laini za simu kwa njia ya alama za vidole (Biometric Registration).

  Wamesema kuwa tatizo hilo limesababisha viziwi wengi katika mkoa huo kushindwa kujisajili, kutokana na kushindwa kuelewana na watoa huduma wa makampuni mbalimbali ya simu wakati wa kujisajili kwa mfumo huo.

  Bensoni amesema kuwa mbali na tatizo hilo, Bado Viziwi wameendelea kukumbwa na tatizo la kutapeliwa na watu wenye nia mbaya kupitia simu, ambapo alisema kupitia mafunzo hayo wataweza kutatuliwa changamoto hizo.

  Akifungua mafunzo hayo Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Festo Kiswaga ameipongeza TCRA kwa kuona umuhimu wa zoezi hilo, kwani viziwi wanayo haki ya kupata elimu ya mawasiliano kama watu wengine. 

  Baadhi watu wasiosikia (viziwi) wakiwa katika mafunzo ya utumiaji wa mawasiliano.
   Afisa anayeshughulikia Masuala ya Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dorice Mhimbila akizungumza na watu wasiosikia wa mkoa wa Simiyu wakati mamlaka hiyo ilipokwenda kutoa elimu ya utumiaji wa mawasiliano.

  0 0

  Mkuu wa Kitengo cha mauzo na usambazaji wa Vodacom Tanzania Plc,George Lugata (kushoto) akitambulisha simu mpya ya kitochi yenye 4G na zana za simu janja inayofahamika kwa jina la Smart Kitochi kwa waandishi wa habari jana, inayotumia KaiOS, mfumo ambao unaongoza duniani katika teknolojia ya simu janja, ni ya kwanza kupatikana katika soko nchini Tanzania kwa kiasi cha Tsh 48,000 ikiwa na kifurushi cha GB 4, dakika 100 za maongezi na SMS 500 kwa kila mwezi ndani ya miezi sita ya kwanza.Wengine ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na uhusiano cha kampuni hiyo Jacquiline Materu na balozi wa Smart Kitochi, Sylvester Mujuni maarufu kama Mpoki.
  Mteja wa kwanza kununua simu mpya ya kitochi yenye 4G na zana za simu janja Smart Kitochi, Lydia Mtei mkazi wa Mbezi Beach akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha mauzo na usambazaji wa Vodacom Tanzania Plc,George Lugata mara baada ya kuzindua simu hiyo kwenye duka la Vodashop mlimani city jana ambapo itapatikana katika maduka yote ya Vodacom nchini. Wengine ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na uhusiano cha kampuni hiyo Jacquiline Materu na balozi wa Smart Kitochi, Sylvester Mujuni maarufu kama Mpoki.
  Balozi wa Smart Kitochi, Sylvester Mujuni maarufu kama Mpoki akielezea zana zilizomo ndani ya Smart Kitochi mbele ya waandishi wa habari jana, Vodacom ni kampuni ya kwanza nchini kuleta simu ya kitochi yenye uwezo wa simu janja kwa kupata huduma za Apps muhimu kama vile WhatsApp, Google Assistant, Facebook, YouTube na nyingine nyingi.


  Baadhi ya wateja waliojitokeza kununua simu za Smart Kitochi jana kwenye duka la Vodacom Mlimani city jijini Dar Es Salaam.  Simu inapatikana katika maduka yote ya Vodacom nchini
  Wateja kupata data, muda wa maongezi na SMS bure kwa miezi 6 ya kwanza

  Kampuni inayoongoza kwa teknolojia ya Mawasiliano Tanzania, Vodacom, leo inatangaza uzinduzi wa simu mpya inayofahamika kwa jina la Smart Kitochi. Simu hii inatumia KaiOS, mfumo ambao unaoongoza duniani katika teknolojia ya simu janja.

  Uzinduzi huu unaongeza hatua kubwa si kwa kampuni hizi mbili tu, bali hata kwa nchi. Ni simu janja ya kwanza kupatikana katika soko nchini Tanzania kwa kiasi cha Tsh 48,000 (Dola 20 za Marekani) ikiwa na kifurushi cha GB 4, dakika 100 za maongezi na SMS 500 kwa miezi sita ya kwanza.

  Smart Kitochi inatumia apps muhimu kama vile WhatsApp, Google Assistant, Facebook, YouTube na nyingine nyingi zikiwapa fursa watanzania kujiunga na huduma ya inteneti. Ikiwa na sifa zote za simu janja kama vile kuwa na Wi-Fi, GPS, simu hii ina uwezo wa kutumia laini mbili zenye uwezo wa uhifadhi wa GB 4 + MB 512. Pia ina betri yenye nguvu ya mAh 1400 na kudumu saa sita. Ikiwa inazinduliwa leo hapa nchini, simu hii pia itaanza kupatikana katika nchi nyingine za Afrika hivi karibuni.

  “Tuna furaha kuwaleteeni simu hii mpya sokoni kwa ushirikiano na mshirika wetu KaiOS Technologies,” anasema George Lugata, Mkuu wa Kitengo cha Mauzo wa Vodacom. “Pamoja na uwepo wa matumizi makubwa katika mtandao wa mawasiliano nchini, bado tunakumbana na changamoto za kidigitali kwa sababu ya uwepo mdogo wa matumizi ya simu janja, kwa kufanya hivyo tunawaletea Smart Kitochi kwa bei nafuu kwa kila mtu.

  KaiOS inatumia mfumo mwepesi kabisa ambao una sifa zote za simu janja ambazo ni pamoja na kuwa na uwezo wa kutosha wa uhifadhi. Pamoja na sifa hizo simu hiyo inatumia mifumo ya 3G na 4G/LTE, Wi-Fi, GPS, pamoja na NFC.

  Simu ya KaiOS inakuja ikiwa na apps maarufu kama WhatsApp, Google Assistant, Facebook, YouTube, and Google Maps. Halikadhalika simu hii ina app ya KaiStore, ambayo ni kati ya apps zaidi ya 200 zinazotumiwa na watoa huduma mbalimbali wa mawasiliano duniani.

  KaiOS Technologies ni ya tatu kwa ukubwa duniani katika mfumo wa utoaji huduma za mawasiliano ya kidigitali, ikiwa na zaidi ya aina 100 za vifaa vinavyosambazwa katika Mabara ya Ulaya, Afrika, Asia na Marekani.

  “Mgawanyiko wa matumizi ya mfumo wa kidigitali Afrika bado ni mpana. Tumejikita zaidi katika kutoa fursa pamoja na kuleta teknolojia mpya yenye utatuzi wa mambo mbambali na ndiyo maana tumeamua kufanya kazi na Vodacom. Smart Kitochi ni hatua moja muhimu katika kuuwaunganisha wale ambao walikuwa nyuma katika matumizi ya inteneti na rasilimali zote muhimu za mawasiliano nchini na kwingineko’” anasema Afisa Mtendaji Mkuu wa KaiOS Technologies, Sebastien Codeville.

  “Simu ya Smart Kitochi inapatikana katika maduka yote ya Vodashop nchini na katika vituo vyote vya huduma na mauzo ya bidhaa zetu nchini kote kwa bei ya punguzo ya Tsh 48,000. Niwaombe Watanzania na hasa wateja wetu kujitokeza kununua simu hii ili waweze kufurahia huduma za Mtandao Supa na kufurahia apps kama vile Facebook, WhatsApp, YouTube, Instagram na nyingine nyingi zinazopatikana katika simu janja,” alihitimisha Lugata.

  0 0


  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Mtwara

  WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa amezindua Mwongozo wa Uwekezaji Mkoani Mtwara (MIG) katika Kongamano la Uwekezaji na Maonyesho ya Biashara lililofanyika kwenye viwanja vya Chuo Cha Ualimu Mtwara.

  Mwongozo huo umetayarishwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa kushirikiana na Mkoa chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).

  “Kuja kwenu Mtwara leo hii hamjapoteza nauli na muda wenu, mmekuja Mtwara mahali sahihi kwa uwekezaji na mtatumia nafasi ya leo kusikia nini kimeandaliwa kwa ajili ya kuwaambia fursa zipi zinapatikana mkoani Mtwara.” Amesema Waziri Mkuu Majaliwa

  Waziri Mkuu amesema Serikali ya awamu ya Tano imedhamiria kwa dhati kuiondoa Tanzania kwenye uchumi wa chini kwenda Uchumi wa Kati na hakuna njia nyingine isipokuwa ni kuvutia uwekezaji, Serikali inakaribisha wawekezaji kuwekeza hapa nchini iwe ni Mtanzania au mgeni kutoka nje ya nchi atapokelewa ili aweze kuwekeza hapa nchini. 

  “Wakati nikizungumza na wakuu wa mikoa Juni 18, 2018 jijini Dodoma nilitoa maelekezo na dira ya kila mkoa kupata wawekezaji, niliagiza kila mkoa lazima ujipange kuhakikisha unatangaza fursa zilizopo katika mkoa.” Alifafanua Waziri Mkuu. 

  Mheshimiwa Majaliwa alisisitiza Mikoa ambayo bado haijaandaa miongozo ya uwekezaji ifanye hivyo mara moja kabla mwaka huu haujaisha. Pia aliwaonya watumishi wanaokuwa vikwazo kwa wawekezaji waache mara moja na wanaobainika wachukuliwe hatua stahiki.

  “Niipongeze Taasisi ya ESRF chini ya Mkurugenzi wake Dkt. Tausi Kida imefanya kazi kubwa na nzuri, baada ya kufanya utafiti imetoa tathmini ya nini kifanyike, wapi tufanye nini ili tuweze kufanikisha uwekezaji hapa nchini” Amesema Waziri Mkuu Majaliwa na kuongeza….Kila ninapokwenda kuzindua Miongozo ya Uwekezaji nimekuwa nikukutana na ESRF ikiongozwa na Dkt. Tausi Kida, hongera sana kwa kazi nzuri mnayofanya.” Alipongeza Waziri Mkuu.

  Waziri Mkuu pia ameipongeza UNDP kwa kufanya kazi kwa pamoja na Serikali na kuahidi kuwa Serikali itaunga mkono shughuli za UNDP ambazo Serikali ya awamu ya Tano na zile zilizotangulia daima zimekuwa zikifanya kazi kwa pamoja na UNDP na zinatambua mchango mkubwa unaotolewa na Taasisi hii ya kimataifa.

  Uzinduzi huo pia ulihudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji, Mhe. Angela Kairuki. Wakati akimkaribisha Waziri Mkuu kuhutubia, Mhe. Kairuki alieleza hatua ambazo Serikali imechukua kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini na kupelekea Tanzania kupanda kutoka nafasi ya 144 hadi 141 kwenye urahisi wa kufanya biashara duniani. 

  Mawaziri wengine waliohudguria na kutoa neno ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Bashungwa, na Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga.

  Wakati akitoa salaamu, Mwenyeji wa Mkoa huo, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa aliwakaribisha wageni waalikwa na kuelezea jinsi Mkoa ulivyojipanga kuwapokea na kuwasaidia wawekezaji. Pia alitoa fursa kwa Wakuu wa Mikoa jirani walihudhuria halfla hiyo ya uzinduzi wa Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa wa Mtwara kutoa neno. Waliohudhuria ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Godfrey Zambi, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Chrintina Mdema na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo.

  Akizungumza kwenye hafla hiyo, Mwakilishi Mkazi wa UNDP hapa nchini, Bi.Christine Musisi alisema UNDP itaendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuboresha maisha ya wananchi. Alisema UNDP itaendelea kusaidiana na Mikoa katika utekelezaji wa miongozo hii kwa kutoa ushauri wa kitaalam na rasilimali fedha panapohitajika.

  Awali akiwasilisha Muhtasari wa Fursa za Uwekezaji katika Mkoa wa Mtwara katika Kongamano la Uwekezaji, Mtafiti Mkuu Mshiriki kutoka Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF) Dkt. Oswald Mashindano alisema ESRF ilifanya utafiti kwenye halmashauri zote za Mkoa wa Mtwara na utafiti huo ulibaini uwepo wa fursa nyingi za uwekezaji. Dkt. Mashindano alitaja timu ya wataalam kutoka ESRF walioshiriki kuandaa Mwongozo wa Uwekezaji ikijumuisha Prof. Haidari Amani, Bi. Margareth Nzuki, Bw. Mussa Mayala Martine, na Bw. James Kasindi.

  Dkt. Mashindano alitaja fursa mbalimbali za uwekezaji ambazo zimepewa kipaumbele na mkoa. Fursa hizi ziko katika makundi mbalimbali ikiwa ni pamoja na uwekezaaji katika kilimo hasa korosho, kilimo cha umwagiliaji wa mpunga na miwa, ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji wa mpunga na mazao ya bustani; uwekezaji katika mifugo hasa ranchi na unenepeshaji wa mifugo; uwekezaji katika uvuvi hasa uvuvi ndani ya bahari kwa kutumia nyenzo na teknolojia za kisasa pamoja na ufugaji wa samaki; uwekezaji katika viwanda hasa Kuchakata Korosho na mazao mengine kama mhogo, nazi, choroko, mbogamboga na matnda, kuchakata na kufungasha chimvi, Chakula cha Mifugo, Kuchakata Samaki, Kiwanda cha Kutengeneza Maji ya Chupa nk.

  Fursa za uwekezaji katika eneo la miundombinu zilijumuisha ujenzi wa jengo kwa ajili ya matengenezo na maegesho ya ndege, stendi za kisasa, ujenzi wa kituo cha michezo ikijumuisha uwanja wa mpira, masoko ya kisasa nk. Aidha Dkt. Mashindano alitaja makundi mengine ya fursa za uwekezaji kuwa ni pamoja na uwekezaji katika utalii akilenga uwekezaji kwenye fukwe, michezo ya baharini, ujenzi wa hoteli, majumba ya starehe, kambi za watalii, kuendeleza maeneo ya kihistoria nk. Pia zilibainishwa fursa za uwekezaji katika huduma za kijamii zikijumuisha afya na elimu. Kwa upande wa afya kuna fursa ya ujenzi wa hospitali na kiwanda cha kutengeneza maji ya wagonjwa na vifaa tiba. Kwa upande wa elimu alitaha fursa ya kuendesha chuo maalum cha ujuzi pamoja na shule binafsi za kisasa.

  Baada ya uzinduzi wa Mwongozo wa Uwekezaji washiriki walipata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali ya uwekezaji Mkoani Mtwara.
  Maonesho ya biashara na Uwekezaji yanafikia kilele leo Novemba 3, 2019.
  Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (katikati), akionyesha nakala za Mwongozo wa Uwekezaji Mkoani Mtwara (MIG), baada ya kuuzindua kwenye Chuo Cha Ualimu Mtwara Novemba 1, 2019. Wanaoshuhudia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angela Kairuki (wapili kulia), Mwakilishi Mkazi wa UNDP, Bi. Christine Msisi (wapili kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe.Gelasius Byakanwa (wakwanza kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dkt. Tausi Kida. 
  Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (watatu kushoto), akikata utepe, kuzindua Mwongozo wa Uwekezaji Mkoa wa Mtwara (MIG), kwenye Chuo Cha Ualimu Mtwara Novemba 1, 2019. Wanaoshuhudia ni kutoka kulia ni Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga, Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dkt. Tausi Kida, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angela Kairuki Mwakilishi Mkazi wa UNDP, Bi. Christine Msisi na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe.Gelasius Byakanwa. 
  Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida, huku Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angela Kairuki (katikati) akishuhudia, mara baada ya Waziri Mkuu kuzindua Mwongozo wa Uwekezaji Mkoa wa Mtwara Novemba 1, 2019.
  Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida, huku Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angela Kairuki (katikati) akishuhudia, mara baada ya Waziri Mkuu kuzindua Mwongozo wa Uwekezaji Mkoa wa Mtwara Novemba 1, 2019.
  Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akihutubia kongamano hilo na kisha kuzindua Mwongozo huo Novemba 1, 2019.
  Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akimpatia nakala ya Mwongozo wa Uwekezaji Mkoa wa Mtwara (MIG) Mwakilishi Mkazi wa UNDP hapa nchini, Bi. Christine Msisi akitoa hotuba yake.
  Viongozi waandamizi wa ESRF walioshiriki katika utafiti huo kutoka kushoto,Bw. Mussa Mayala Martine, Dkt. Oswald Mashindano na Bi. Margareth Nzuki.
  Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akimpatia nakala ya Mwongozo wa Uwekezaji Mkoa wa Mtwara (MIG), Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga huku Mhe. Kairuki (katikati) akishuhudia. 
  Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akimpatia nakala ya Mwongozo wa Uwekezaji Mkoa wa Mtwara (MIG), Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa huku Mhe. Kairuki (katikati) akishuhudia. 
  Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akimpatia nakala ya Mwongozo wa Uwekezaji Mkoa wa Mtwara (MIG) Mwakilishi Mkazi wa UNDP hapa nchini, Bi. Christine Msisi. Wanaoshuhudia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mhe. Angela Kairuki (wapili kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida. Mwongozo huo umetayarishwa na (ESRF) kwa kushirikiana na Mkoa wa Mtwara chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).

  0 0  0 0

  Benki ya NBC Yatangaza kupata ongezeko la faida kwa asilimia 300

  Dar es Salaam, 3 Novemba, 2019: BENKI ya NBC imeonyesha ufanisi mkubwa katika utendaji wake baada ya kutangaza kupata ongezeko la faida (baada ya kodi) la asilimia 367 katika kipindi cha robo ya tatu ya mwaka huu ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.

  Mafanikio hayo yanatajwa kusababishwa na ufanisi wa benki hiyo katika nyanja mbalimbali ikiwemo katika usimamizi wa mizania, kuongezeka kwa mapato yatokanayo na ada ya mihamala na kuboreshwa kwa huduma za mikopo, kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Bw Theobald Sabi.

  Kwa mujibu wa ripoti yake ya kifedha ya robo ya tatu ya mwaka 2019 iliyotolewa hivi karibuni, hadi kufikia mwezi Septemba mwaka huu, benki hiyo ilikuwa na jumla mikopo yenye thamani ya TSh 987 bilioni huku ikiwa na amana za wateja zenye thamani ya Tsh 1.717 Trilioni

  "Jumla kuu ya Mikopo yetu imeongezeka katika kipindi cha robo mwaka kwa asilimia 3.7, hasa ikichangiwa na ongezeko la uombaji wa mikopo kutoka kwa wateja wetu wakubwa, wa reja reja na wa kati huku amana zetu (customer deposits) kwa ujumla ziliongezeka kwa asilimia 19.3" Aliongeza Bw Sabi.

  "Umakini na ufanisi wetu katika suala zima la utoaji wa mikopo limeanza kutupa faida kwa kuwa hata kiwango cha mikopo chechefu kimeendelea kupungua hadi kufikia asilimia 6.9 kutoka asilimia 10.1 katika kipindi kama hiki mwaka uliopita,’’ alibainisha Bw Sabi.

  Aliongeza kuwa mkakati wa mabadiliko ya kidigitali unaotekelezwa na benki hiyo umeendelea kuzaa matunda ya ukuaji huo huku akibainisha kuwa mfumo wa miamala kwa njia ya simu umekua kwa asilimia 50 ikilinganishwa na kipindi kama hicho kwa mwaka jana.

  “Ongezeko hili ni ishara kwamba wateja wetu wanapokea vizuri mabadiliko ya uboreshaji wa huduma zetu hasa kidigitali na hivyo kutupunguzia kiasi cha muda ambao tungeutumia kuwahudumia kupitia matawi yetu na hivyo tunajikuta tunapata muda wa kutosha kubuni na kutekeleza huduma nyingine bora zaidi kwa ajili yao,’’ alisema.

  Alihamasisha zaidi wateja wa benki hiyo wakiwemo wa reja reja na wateja wakubwa yakiwemo mashirika na taasisisi (corporates)kuendelea kutumia huduma hizo za kidigitali kwa kuwa ni salama na zinatoa huduma ya malipo ya ya aina zote yakiwemo malipo makubwa kwa ndani na nje ya nchi.

  Aidha Bw Sabi aliitaja huduma nyingine ya kielectronic inayokua kwa kasi kuwa ni NBC Wakala ambayo kwasasa ina mtandao wa mawakala zaidi ya 2,000 waliotapakaa nchi nzima.

  “Wateja sasa wana uwezo wa kuzifikia akaunti zao na hufanya mihamala kwa urahisi zaidi kupitia maelfu haya ya mawakala nchi nzima.’’

  “Mawakala wa NBC kwasasa wamefuzu kufanya mihamala kupitia mfumo wa kielectronic wa malipo serikalini (GePG) na hivyo wateja wanaweza kuwatumia kufanya malipo yao kwenye taasisi na mashirika ya serikali na ndio sababu Benki ya NBC sasa ni moja wapo ya benki inayoongoza kwa Makusanyo ya Mapato ya Serikali kupitia GePG.’’Alisema. 
   
   Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya NBC Bw  Theobald Sabi.
   

  0 0

  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (wa tatu kushoto), akifurahi mara baada ya kufunua pazia kuzindua mashindano ya Kimataifa ya Kilimanjaro Marathon 2020, kwenye Hoteli ya Coral Beach, Dar es Salaam Mwishoni mwa wiki. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Michezo wa wizara hiyo, Yusufu Singo na Rais wa Riadha Tanzania (RT), Antony Mtaka na kutoka kulia ni Woinde Shisael Meneja Mawasiliano wa Kamouni ya Tigo Wadhamini wa Kili Half Marathon na Pamela Kikulu Meneja Bia ya Kilimanjaro Wadhamini wakuu wa mbio ndefu za Km 42. Mashindano hayo yatafanyika Machi Mosi mwakani. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA 
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (wa tatu kushoto), akifunua pazia ikiwa ni ishara ya kuzindua mashindano ya Kimataifa ya Kilimanjaro Marathon 2020, kwenye Hoteli ya Coral Beach, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Wanaoshudia kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Michezo wa wizara hiyo, Yusufu Singo na Rais wa Riadha Tanzania (RT), Antony Mtaka na kutoka kulia niWoinde Shisael Meneja Mawasiliano wa Kamouni ya Tigo Wadhamini wa Kili Half Marathon na Pamela Kikulu Meneja Bia ya Kilimanjaro Wadhamini wakuu wa mbio ndefu za Km 42.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (kushoto), akikabidhiwa zawadi na Pamela Kikulu Meneja Bia ya Kilimanjaro Wadhamini wakuu wa mbio ndefu za Km 42.
  Meneja wa Grand Malt, David Tarimo wadhamini wa mbio za Km 5, akielezea kuhusu udhamini huo pamoja na sifa za kinywaji hicho.
  Woinde Shisael Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Tigo Wadhamini wa Kili Half Marathon akielezea kuhusu udhamini wao na kuwaomba watanzania kuisapoti kampuni hiyo kwa kujisajili kwa wingi kujiunga na mtandao huo mkubwa nchini. 
  Pamela Kikuli Meneja Bia ya Kilimanjaro Wadhamini wakuu wa mbio ndefu za Km 42. zielezea kuhusu udhamini wa mbio ndefu na kuitangaza bia ya Kilimanjaro yenye jina linalotukuza Mlima Kilimanjaro ambao ni kivutio kikubwa cha utalii nchini.
  Mkurugenzi wa Kampuni ya Executive Solutions Waratibu wa mashindano hayo akiongoza hafla hiyo ya uzinduzi na kuelezea umuhimu wa watu kuanza kujisajili ili kushiriki mashindano hayo makubwa nchini na nje ya Nchi.
  RAIS WA TOC, FILBERT bAYI AKIELEZEA UMUHIMU WA WATANZANIA KUSHIRIKI NA KUSHINDA MASHINDANO HAYO, ILI WAPATE FURSA YA KUSHIRIKI MASHINDANO YA OLIMPIKI.
  Rais wa RT, Anthony Mtaka akitangaza nyongeza ya bonasi kwa wanariadha watanzania watakaoshinda mashindano hayo.
  Waziri Dk. Mwakyembe akihutubia katika hafla hiyo
  Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Leodger Tenga akitoa neno la shukrani wakati wa hafla hiyo.
  Waziri Dk. Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa RT, BMT na wadhamini wa mashindano hayo
  Waziri Dk. Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa RT, BMT na wadhamini wa pamoja na waandaji na waratibu wa Kilimanjaro Marathoni.
  Na Richard Mwaikenda 

  WANARIADHA wa Tanzania watakaoshinda mashindano ya Kimataifa ya Kilimanjaro Marathon 2020, kuibuka na kitita cha sh. mil. 7 ambapo sh. Mil 4 ni zawadi ya kawaida na sh. mil 3 ni motisha.

  Motisha hiyo ilitangazwa na Rais wa Chama cha Riadha Tanzania (RT), Antony Mtaka wakati wa hafla ya uzinduzi wa mashindano hayo, uliofanywa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe katika Hotel ya Coral Beach, Masaki, Dar es Salaam jana.

  Waziri Mwakyembe ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo, alisema kuwa motisha hiyo iwe ni kichocheo kikubwa kwa wanariadha wa Tanzania kushiriki kwa wingi na kushinda mbio hizo.Alisema kuwa huwa inashangaza kuona zawadi ya 1-39 zinakwenda kwa wakimbiaji wa kutoka nje, wakati Tanzania ina watu wenye misuli, mikono na vifua lakini hushindwa, wakati watu hao hao wakikimbizwa na polisi hukimbia sana.

  “Nitafurahi sana kuona bahasha nyingi za zawadi zikibaki nchini, naomba wenye uwezo mkubwa tushiriki kwenye mbio hizi zenye jina kubwa kimataifa,” alisema Dk.Mwakyembe.Aliwapongeza waandaji wa mashindano hayo ambayo sasa yamekuwa yanavutia watu wengi kutoka mataifa 56 Ulimwenguni, hali inayochangia ukuaji wa uchumi wa Tanzania.Alisema kitendo hicho kimesaidia sana kuutangaza Mlima Kilimanjaro na vivutio vingine vya utalii vilivyopo nchini. Pia imesaidia mashindano hayo kuwa na wadhamini wengi.

  Rais wa RT, Mtaka ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, aliwaasa wanariadha wa Tanzania kuachana na kasumba ya kukimbilia kushiriki mashindano ya nje ambako hata zawadi wanazopewa ni sawa na zinazotolewa na Kilimanjaro marathoni na mara nyingine kuzidi.

  Aliwataka wajenge tabia ya kupenda kushiriki mashindano ya nyumbani na hasa Kilimanjaro Marathon yenye hadhi kubwa sawa na mengine ya kimataifa. Alisema kuwa waandaji wameamua kutoa motisha ili wanariadha wa kitanzania washiriki kwa wingi na kushinda.

  Alisema kuwa wanariadha wakienda nje kushiriki baadhi hulipwa dola 1000 ambayo ni sawa na sh. 2,460,000 za Tanzania na wengine hulipwa dola 500, kiasi ambacho ni kidogo ukilinganisha na zawadi ya sh. mil. 4 na nyongeza ya motisha sh. mil. 3, jumla sh. mil 7 kwa mshindi wa mbio za Km 42.

  Mshindi wa Tigo Kili Half Marathon Km 21, hulipwa sh. mil. 2 kwa upande wa wanaume na wanawake pia.Mashindano hayo mwaka huu yametimiza miaka 18 tangu ilipoanzishwa 2001.Naye, Rais wa Kamati ya Olympic Tanzania TOC, Filbert Bayi, alisema kuwa wanariadha inabidi wayathamini mashindano ya Kilimanjaro Marathon, kwani ni kipimo tosha cha washindi kupata fursa ya kushiriki mashindano ya Olympic Tokyo, Japan 2020.

  Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Leodger Tenga, alisema hakuna njia ya mkato katika mafanikio, hivyo kuwataka wanariadha kutobweteka, bali wajitahidi sana kufanya mazoezi ambayo ni msingi wa mafanikio ya ushindi.

  Hafla hiyo iliwakilishwa pia na Pamela Kikuli Meneja wa Bia ya Kilimanjaro wadhamini wakuu wa mbio ndefu za Km 42, Woinde Chisael Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Simu ya Tigo inayodhamini mbio za Km. 21 na David Tarimo Meneja wa kinywaji aina ya Grand Malt wadhamini wa mbio za Km. 5.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt.Anna Mghwira akizawadiwa samaki aina ya Kambare na mwanakijiji wa Suwa Wilayani Handeni Mkoani Tanga. Dkt Mghwira yupo ziarani Handeni kujifunza na kujionea athari ya mafuriko ya mvua yaliyotokea hivi karibuni Mkoani Tanga. Bwawa la Suwa limeathirika kwa kiasi kikubwa sana ambalo ni chanzo cha maji Handeni vijijini.Picha na Jamal Zuberi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tanga (OMM-Tanga)


  0 0  Meneja wa NBC Tawi la Zanzibar, Ramadhani Lesso (kushoto) akipongezana na Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Damas Ndumbaro, huku mchezaji mwenzao Mbunge wa Kenya, Kassim Sawa akiwangalia wakati wa mashindano ya kwanza ya gofu ya Mabalozi yaliyofanyika katika viwanja vya gofu vya Sea Cliff kisiwani Zanzibar jana. Mashindano hayo yalidhaminiwa na Benki ya NBC kama moja ya shughuli za kusapoti sekta za michezo na utalii nchini. 


  Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Damas Ndumbaro (kushoto), Mbunge wa Kenya, Kassim Sawa (kulia), na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi Maalum wa Benki ya NBC, Ashura Waziri (wa pili kulia), wakimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza wa mashindano ya kwanza ya gofu ya mabalozi, Eliah John yaliyodhaminiwa na Benki ya NBC kama moja ya shughuli za kuisapoti sekta ya michezo na utalii nchini. Mashindano hayo yalifanyika katika viwanja vya gofu vya Sea Cliff kisiwani Zanzibar jana. 


  Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Damas Ndumbaro (kulia) akimkabidhi zawadi mshindi wa pili wa mashindano ya kwanza ya gofu ya mabalozi, Issa Mohamed Chaap yaliyodhaminiwa na Benki ya NBC ikiwa ni sehemu ya shughuli za kusapoti sekta za michezo na utalii nchini. Mashindano hayo yamefanyika katika viwanja vya gofu vya Sea Cliff kisiwani Zanzibar jana.
  Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Damas Ndumbaro (kushoto) akipokea zawadi ya kushiriki katika Mashindano ya kwanza ya gofu ya mabalozi kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Wateja Rejareja Maalum wa Benki ya NBC, Ashura Waziri yaliyofanyika katika viwanja vya gofu vya Sea Cliff Kisiwani Zanzibar jana. Mashindano hayo yalidhaminiwa na NBC ikiwa ni sehemu ya shughuli za kusapoti sekta za michezo na utalii nchini.
  Mbunge wa Kenya, Kassim Sawa (kushoto), akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Wateja Rejareja Maalum wa Benki ya NBC, Ashura Waziri baada ya kushiriki mashindano ya kwanza ya gofu mabalozi yaliyodhaminiwa na NBC katika viwanja vya gofu vya Sea Cliff Kisiwani Zanzibar jana ikiwa ni moja ya shughuli za kusapoti sekta za michezo na utalii nchini.

  Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Damas Ndumbaro akijiandaa kupiga mpira wakati wa Mashindano ya kwanza ya Golf ya Mabalozi yaliyodhaminiwa na Benki ya NBC ikiwa ni sehemu ya shughuli za kuisapoti sekta ya Michezo na Utalii zinazoendelea kufanyika sehemu mbalimbali nchini. Mashindano hayo yamefanyika katika viwanja vya Sea Cliff kisiwani Zanzibar jana.
  Wacheza gofu wakipozi kwa picha pamoja mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushikiano wa Afrika Mashariki pamoja na maofisa wa Benki ya NBC wakati wa mashindano hayo mjini Zanzibar jana.
  BENKI ya NBC imedhamini mashindano ya kwanza ya gofu ya mabalozi visiwani Zanzibar huku ikiahidi kuendelea kusapoti sekta ya michezo na utalii visiwani humo kutokana na mchango wake katika maendeleo ya taifa.

  Akizungumza wakati wa mashindano hayo katika Viwanja vya Gofu vya Sea Cliff visiwani humo jana, Mkuu wa Kitengo cha Wateja maalumu binafsi wa Benki ya NBC, Ashura Waziri alisema licha ya kuwa michezo husaidia afya kitu ambacho ni muhimu katika uzalishaji mali, lakini pia michezo yenyewe inaweza kuongeza ajira na kuinua uchumi wa wanamichezo na kwa taifa.

  “Naihakikishia Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar kwa kupitia Kamisheni ya Utalii kuwa NBC itaendelea kuisaidia kwenye michezo kama tulivyofanya kwa kudhamini gofu ya mabalozi, tunathamini michezo kwa wafanyakazi wetu pia, tunaihakikishia wizara ya michezo pia tutaendelea kusapoti michezo,” akaongeza.

  Naye Meneja wa Tawi la NBC mjini Zanzibar, Ramadhani Lesso alisema NBC imekuwa mdau mkubwa wa maendeleo visiewani humo na ndio sababu ya kuitikia wito wa Wizara ya Habari na Utalii kupitia Kamisheni ya Utalii kushiriki katika mashindano hayo kwani wamekuwa wakishirikia kwa muda mrefu aatika kusapoti utalii visiwani humo.

  “Kama mnavyofahamu benki yetu ina ATM zisizopungua 7 hapa Zanzibar na zote zinatoa huduma ya Visa ambayo ni maalumu kwa ajili ya wananchi wote lakini zaidi kwa watalii. Kwahiyo utakuta watalii wanafaidika sana wanapotumia mashine zetu za kutolea pesa na mashine nyingine zilizopo mahotelini.

  “Watalii ni muhimu sana kwetu ndio maaana tulipopata mualiko huu kutoka kwa Mkurugenzi wa Kamisheni ya Utalii tuliona ni sehemu muhimu sana kwetu kwa ajili ya kuunga mkono serikali kwa upande wa maendeleo na vilevile ikiwa ni sehemu ya michezo kama ilivyo sera ya michezo,” aliongeza.

  Pamoja na hayo meneja huyo akatoa wito kwa serikali na wadau wa michezo kuunga mkono juhudi za kusapoti mchezo wa gofu ufundishwe mashuleni na sehemu zote ili watanzania wote waweze kuucheza a kuupenda.

  Katika mashindano hayo, ambayo mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri wa Mambo na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Damas Ndumbaro, ambaye pia alikuwa mshiriki, Eliah John aliibuka kidedea kwa kushika nafasi ya kwanza huku Issa Mohamed Chaap wote wa visiwani humo kushika nafasi ya pili.

  0 0

  Shehena ya Vyavu haramu aina na Makokoro vilivyokamatwa katika Operesheni   inayoendelea  katika vijiji vinavyolizunguka bwawa la Nyumba ya Mungu vikiwa tayari kwa kuteketezwa kwa moto.

  Na.Vero Ignatus,Kilimanjaro.

  Mkuu wa Wilaya ya Mwanga  Thomas Apson,ameteketeza  kwa moto nyavu aina ya makokoro na vyandarua vya kujikinga na mbu, vinavyotumika kwa uvuvi haramu vilivyokamatwa katika oparesheni  inayoendelea  katika vijiji vinavyolizunguka bwawa la Nyumba ya Mungu  vyenye thamani vya shs.39.3mil.

  Apson  amesema kuwa  katika oparesheni hiyo  wavuvi haramu 14 katika bwawa hilo wametiwa mbaroni kwa kuwatishia polisi wenye silaha waliokuwa doria na kuwataka waweke silaha ili  wazichape ngumi kavu kavu.

  Afisa Tarafa ya Lembeni  Gikila Salisali  amesema, baadhi ya watumishi wa umma  wasiokuwa waaminifu wamekuwa kikwazo katika vita hivyo kwa  wanashirikiana na wavuvi haramu na kuiomba serikali iwape boti ili kuimarisha doria ndani ya  bwawa.

  Wananchi wa vijiji hivyo bi Eda Eliakimu na bakari kingazi wakazi wa nyumba ya Mungu wameipongeza serikali kwa kutangaza upya vita hivyo ambavyo wamesema vinaweza kusaidia kupunguza kasi ya uvuvi haramu ambao umekuwa tishio kwa samaki wachanga ambao  wangeweza  kubadili maisha yao.

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo (kushoto), akipokea sehemu ya msaada wa madawati 150 yaliyotolewa na Benki ya NMB kutoka kwa Meneja wa benki hiyo Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd.

  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo (wa tatu kulia), akikata utepe wakati wa hafla ya kukabidhi madawati 150 kwa Shule ya Msingi, Mkunguni, Hananasif pamoja na Sekondari ya Hananasif. Kulia kwake ni Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd.

  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Changolo (kulia), akipokea sehemu ya msaada wa mabati 180 kwa ajili ya Shule ya Msingi Turiani kutoka kwa Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. Benki ya NMB ilitoa madawati 150 kwa shule ya Msingi Hananasif, Mkunguni pamoja na Shule ya Sekondari Hananasif.
  Mwanafunzi wa Darasa la V Shule ya Msingi Mkunguni, Jane Shija, akimshukuru Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam baada ya kukabidhi msaada wa madawati 150.
  Baadhi ya wanafunzi wakiwa wamekaa katika madawati mapya waliyokabidhiwa na Uongozi wa Benki ya NMB.

  ***********************************


  Na Mwandishi Wetu

  MKUU wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo, ameimwagia sifa Benki ya NMB kwa jinsi inavyojitolea katika miradi ya maendeleo nchini wakati alipokuwa akipokewa msaada wa madawati na mabati kwa shule nne za Kinondoni, uliotolewa na Benki hiyo leo jijini Dar es Salaaam.

  NMB kupitia Meneja, Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd walikabidhi msaada wa mabati 180 kwa ajili ya Shule ya Msingi Turiani, Madawati 150 kwa shule za msingi, Hananasif, Mkunguni pamoja na shule ya sekondari Hananasif.

  Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika Hananasif Sekondari Chongolo alisema, Serikali inatambua na kuthamini mchango wa Benki hiyo kwani imekuwa ikigusa sekta mahsusi za Elimu, Afya na Miundombinu nchini kote.

  “Kwa dhati napenda kutoa shukrani zangu kwa Benki ya NMB kwa jinsi ambavyo imekuwa mstari wa mbele kutoa misaada na kuunga mkono juhudi za Serikari ya Awamu ya tano katika kutatua chanagamoto zinazowakabili watanzania.
  “Msaada huu wa mabati na madawati kwa shule hizi unaenda kuongeza chachu ya vijana wetu kupata Elimu katika mazingira rafiki kwa kipindi cha miaka mitano.” amesema Chongolo na kuongeza.

  “Binafsi napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa NMB kwa jinsi ambavyo wamekuwa wakiunga juhudi za Serekali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli kwa kutoa misaada katika maeneo mbali mbali ya nchi.

  Chongolo alisema shule hizo zinakabiliwa na upungufu mkubwa wa miundombinu ya kujifunzia kwa wanafunzi na kuahidi kuwa Serikali inayafanyia kazi mapungufu yaliyopo, kwa kushirikiana na sekta binafsi kuzitatua.

  Kwa upande wa Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam Badru Idd, amesema misaada hiyo ni sehemu ya misaada ambayo NMB imepanga kuitoa kwa mwaka ambapo kila mwaka hutenga Bilion 1, huku mwaka huu wameshatoa misaada zaidi ya Milioni 800 ikiwemo hiyo waliyoitoa kwenye shule hizo.

  “Kama NMB ni utaratibu wetu wa kurudisha kwa jamii katika kile tunachokipata kila mwaka, jamii ndio tunayoihudumia na ndio wateja wetu. Katika Bilioni 1 tunayoitenga kila mwaka hadi sasa tumeshatoa zaidi ya Milioni 800.

  “Leo tuko hapa kwa ajili ya kutoa msaada wa Mabati 180 kwa shule ya Tuliani, Madawati 50 kwa Shule ya Msingi ya Hananasif, Madawati 50 kwa Shule ya Sekondari ya Hananasifu na 50 mengine kwa Shule ya Msingi ya Mkunguni.” alisema Idd.

older | 1 | .... | 1888 | 1889 | (Page 1890) | 1891 | 1892 | .... | 1897 | newer