Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live

RAIS DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA UJENZI WA BARABARA YA TABORA-KOGA MPANDA KM 342.9, AFUNGUA BARABARA YA STALIKE MPANDA KM 36.9 PAMOJA NA STAND YA MABASI YA MIZENGO PINDA MPANDA MKOANI KATAVI

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe pamoja na Meneja Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) nchini Tanzania Dkt. Alex Mubiru kuashiria uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Tabora- Koga-Mpanda 342.9 inayojengwa kwa kiwango cha lami. Wengine katika picha ni Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli watatu kutoka kulia, Mtendaji Mkuu wa TANROADS Eng. Patrick Mfugale wa kwanza kulia,Waziri wa Madini Doto Biteko, Mkuu wa Mkoa wa Tabora Agrey Mwanri, Mkuu wa Mkoa wa Katavi Juma Homera, Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Isaack Kamwelwe pamoja na viongozi
wengine.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akielekea nje ya lango kuu ya Stendi hio ya mabasi kuzungumza na wananchi mara baada ya kuifungua.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kufungua stendi hio ya mabasi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Meneja Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) nchini Tanzania Dkt. Alex Mubiru mara baada ya kuweka jiwe la msingi la uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Tabora-Koga-Mpanda 342.9 inayojengwa kwa kiwango cha lami
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Wakandarasi, Wahandisi Washauri wa miradi ya barabara ya Tabora- Koga-Mpanda 342.9 katika sherehe fupi zilizofanyika katika manispaa ya Mpanda mjini mkoani Katavi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Isaack Kamwelwe mara baada ya kuzindua na kufungua miradi ya barabara mkoani Katavi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe pamoja na Meneja Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) nchini Tanzania Dkt. Alex Mubiru, Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa Tabora Agrey Mwanri kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa mradi wa barabara ya Tabora-Koga-Mpanda 342.9 katika sherehe fupi zilizofanyika katika manispaa ya Mpanda mjini mkoani Katavi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na viongozi wengine, akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Stendi Kuu ya Mabasi Mizengo Pinda nje kidogo ya Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi.
Sehemu ya Barabara ya Mpanda –Stalike iliyokamilika
kujengwa kwa kiwango cha lami.

PICHA NA IKULU

NMB YAKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO TIMU ZA JWTZ

$
0
0
Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi, Biashara ndogo na za Kati wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi (wa pili kushoto) akimkabidhi sehemu ya vifaa vya michezo Kanali wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Erasmus Bwegoge ikiwa ni udhamini wa NMB kwa timu ya JWTZ inayotarajia kushiriki michezo ya majeshi ulimwenguni. Kulia ni Meja wa JWTZ, Wilfred Abedinego akishuhudia.
Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi, Biashara ndogo na za Kati wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi (kushoto) akizungumza kabla ya kukabidhi vifaa vya michezo kwa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), ikiwa ni sehemu ya udhamini wa NMB kwa timu ya jeshi inayotarajia kushiriki michezo ya majeshi ulimwenguni, vifaa hivyo vinathamani ya shilingi milioni 18. Kulia ni Kanali wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Erasmus Bwegoge.
Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi, Biashara ndogo na za Kati wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi (wa pili kushoto) akimkabidhi jezi Kanali wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Erasmus Bwegoge ikiwa ni sehemu ya udhamini wa NMB kwa timu ya JWTZ inayotarajia kushiriki michezo ya majeshi ulimwenguni. Kushoto ni Meneja Mwandamizi Idara ya Wateja Binafsi, Ally Ngingite pamoja na Meja wa JWTZ, Wilfred Abedinego (kulia) wakishuhudia.

********************************

Na Mwandishi Wetu

BENKI ya NMB imekabidhi vifaa vya michezo kwa timu ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) ikiwa ni udhamini wao katika michezo mitatu, yaani mchezo wa ngumi, mieleka pamoja na mchezo wa riadha.

Udhamini huo wa vifaa vya michezo vyenye thamani ya shilingi milioni 18, umekabidhiwa leo jijini Dar es Salaam na Ofisa Mkuu wa Wateja Binafsi, Biashara ndogo na za Kati, Filbert Mponzi kwa viongozi wa JWTZ.

Aidha akizungumza kabla ya kukabidhi vifaa hivyo, Bw. Mponzi alisema Vifaa hivyo vya Michezo vilivyotolewa na NMB ni sehemu ya udhamini wa Benki ya NMB kwa Michezo ya ngumi, mieleka pamoja na riadha.

Aliongeza kuwa, Benki ya NMB inaushirikiano mkubwa na wa muda mrefu ambao umekuwa na faida kwa pande zote huku ukiendelea kuimarika siku hadi siku.

“…Kwa niaba ya NMB tunaomba mtuwakilishe vema na tutafurahi zaidi mkirudi hapa na medali za dhahabu, tutakuwa na furaha zaidi kwani si tu mmeshinda bali benki yetu itakuwa imeshiriki kufanikisha ushindi huo,” alisema Bw. Mponzi akikabidhi msaada huo.

Alibainisha kuwa NMB imekuwa ikishirikiana na JWTZ kudhamini michezo mbalimbali, jambo ambalo linaendelea kuboresha mahusiano mazuri kati ya pande zote.

Michezo ya Majeshi Duniani, World Military Games inayoshirikisha majeshi mbalimbali ulimwenguni, inatarajia kufanyika nchini China katika Jiji la Wuhan hivi karibuni

NMB Yawahakikishia Wateja Wake Wakubwa Huduma Bora

$
0
0
BENKI ya NMB imewahakikishia wateja wakubwa nchini huduma bora na timilifu kulingana na mahitaji yao ya kifedha, uhakika unaotokana na ukubwa wa mtaji wa benki hiyo unaofikia zaidi ya Sh. Bilioni 700.

Hayo yalisemwa jana na Kaimu Afisa Mkuu wa Idara ya Wateja Wakubwa wa NMB- Aziz Chacha, wakati akifungua Jukwaa la Wateja Wakubwa (NMB Executive Network), lililofanyika jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma.

Chacha alibainisha ya kwamba, uwezo wa kipesa unaotokana na ukubwa wa mtaji katika benki ya NMB ni mkubwa, unaowawezesha kuhudumia wateja wa kada zote, wakiwemo wateja wakubwa na kumudu kwa asilimia zote mahitaji yao ya kifedha.

Aliongeza ya kwamba wateja wakubwa wana mahitaji makubwa ya kihuduma, lakini wao wana nguvu ya kutosha kuyatimiza na ndio maana wakawaalika katika jukwaa hilo, ili kujadiliana kwa pamoja kujua namna ya kushughulika na changamoto zao na kuzitatua.

Kwa upande wake, Meneja Uhusiano wa Kitengo cha Wateja Wakubwa wa NMB, Amour Muro, alisema ‘NMB Executive Network’ ni jukwaa linalotumika kukutana na wateja wakubwa, ikiwa ni sehemu ya Wiki ya Huduma kwa Wateja.

“Hili ni moja ya majukumu yetu katika wiki hii na hii inatusaidia kuzungumza nao kujua namna ya kuongeza thamani ya huduma tunazowapatia. Kupitia Jukwaa kama hili, tunatanua uelewa na kuongeza thamani ya kupitia majadiliano tutakayofanya,” alisema Muro.

Alisema NMB kama taasisi inaamini katika huduma walizonazo, lakini njia bora na sahihi ya kuzifanyia maboresho mbalimbali ni kukutana na makundi tofauti ya wateja, kusikiliza changamoto zao na kuzifanyia kazi, ili kuwezesha upigaji hatua za maendeleo yao.

Magdalena Magali, ambaye ni mwakilishi wa Kampuni ya Saruji ya Tanzania Potland, kwa upande wake aliishukuru NMB kwa kuwaandalia jukwaa maluum wateja wakubwa na kupokea mawazo yao chanya kwa maendeleo ya mtu mmoja mmoja, wateja na taasisi hiyo kwa ujumla.

Aliipongeza NMB kwa mabadiliko chanya ya kimfumo kutoka analogi kwenda dijitali, uliojikita katika kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa haraka, wepesi na usalama na kuwataka Watanzania kuchangamkia huduma hizo ili kuokoa muda na kwenda na wakati.

Naye Steven Gideon, ambaye ni Ofisa Mipango na Bajeti wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), alisema kampuni yake inapongeza uamuzi wa NMB kukutana na kujadiliana nao, kwani njia rahisi ya kufikia malengo ni kufanyia kazi changamoto zilizopo ilikusonga mbele. 

Gideon aliwataka Watanzania kujali muda na kuendana na kasi za maendeleo kwa kuchagua kuifanya NMB kuwa mshirika sahihi wa ukuaji kiuchumi na kwamba siri ya mafanikio iko katika mapinduzi ya kiteknolojia yaliyofanywa na benki hiyo, yanayoongeza ufanisi kwa wateja.

 Kaimu Afisa Mkuu wa Idara ya Wateja Wakubwa wa NMB- Aziz Chacha,alipokuwa akizungumza  wakati akifungua Jukwaa la Wateja Wakubwa (NMB Executive Network), lililofanyika jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma.
 Wateja wakiwa katika picha ya pamoja

Benki UBA yatoa ushauri kwa taasisi za fedha nchini

$
0
0

Na MWANDISHI WETU -DAR ES SALAAM

TAASISI za fedha nchini, zimeshauriwa kubadilika katika kuwahudumia wateaja wao na kuacha kutoa huduma kwa mazoea wakati wanapotoa huduma kwa wateja wao, ili kuendana na kasi pamoja na ushindani uliopo kipindi hiki cha mabadiliko ya teknolojia ili kuweza kufanya vizuri kwenye soko la ushindani.

Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya UBA-Tanzania, wakati benki hiyo ilipoungana pamoja na wateja wake katika kusherehekea wiki ya wateja duniani iliyofanyika tawi la Nyerere.

“Nashauri taasisi zinazotoa huduma za kifedha lazima zibadilike na kuacha kutoa huduma kwa mazoea badala yake ziwe na ubunifu unaoendana na kipindi hiki cha ushindani wa soko la teknolojia kwani usipofanya hivyo ushindani ni mkubwa sana,” alisema Isiaka

Alisema UBA wanayo furaha kuungana na wateja wao kusherekea siku ya huduma kwa mteja duniani kwa kuwa wao ndio wanafanya benki hiyo kuwepo na kuendelea kutoa huduma stahiki na zenye ubora kwa wateja wao kwenye matawi yao yote nchini . 
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Ledgewood Investiment, Raymond Mubayiwa, alisema kuwa katika kipindi hiki cha kusherekea wiki ya huduma kwa wateja wamejifunza mengi ikiwamo kupata fursa ya kukutana na watoa huduma wao na kuzungumza nao kwa kina kuhusu masuala mbalimbali jambo ambalo kwao limewapa faraja kubwa.


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya UBA, Usman Isiaka akizungumza na wateja wa benki tawi la Nyerere jijini Dar es Salaam, ikiwani ni maadhimisho ya wiki ya wateja duniani
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya UBA, Usman Isiaka akiwagawia wateja wa benki hiyo keki wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja Dar es Salaam

TANZIA:MKUFUNZI WA SHOTOKAN-RYU KARATE AFARIKI DUNIA

$
0
0
Mkufunzi na Mkuu wa Idara ya Ufundi ya JKA/WF-­‐Tanzania kitaifa, pia Mwenyekiti wa Tanzania Shotokan-­‐Ryu Karate-­‐Do Association (TASHOKA) Abdallah Kambi Sensei  amefariki dunia.

Kambi Sensei aliyeingia madarakani tarehe 27 Julai 2019, amefikwa na umautio leo alfajiri katika hospital kuu ya Taifa Muhimbili, alipokua amelazwa kufuatia kusumbuliwa na kifua na tumbo, tangu mwezi August.

Mwenyekiti, JKA/WF-­‐Tanzania Jerome G. Mhagama, amethibitisha kutokea kwa msiba huo, na ameeleza taratibu za maziko ya Kambi Sensei aambaye alijiunga na JKA/WF-­‐Tanzania mwaka 2009 na kuwa mwanafamilia hai wa JKA mpaka umauti unamkuta.
 
Katika hatua nyingine Mhagama ameeleza taarifa nyingine za msiba wa mdau huyo wa mchezo wa Karate, huku wakitarajia majibu wa kikao cha familia ya marehemu.

Ndani ya JKA Kambi Sensei alikuwa mmoja wa Wakufunzi tegemezi mwenye Black Belt 4th Dan-­‐JKA, pia alikuwa na JKA International Licence yenye viwango vya Instructor class C, Judge class D & Examiner class D.
Bwana ametoa, Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe.
Alale mahali pema peponi.

SBL yawekeza Paundi Mil 10 kupanua uzalishaji wake Dar, Moshi

$
0
0
Kampuni inayoongoza kwa uzalishaji wa bia nchini, Serengeti Breweries Limited (SBL) imetangaza mpango wake wa upanuzi wenye thamani ya paundi milioni 10 kwa viwanda vyake vya Dar es salaam na Moshi. 

Uwekezaji huo unapelekea kampuni hiyo kuongeza uwezo wake wa uzalishaji wa bia na hivyo kukidhi mahitaji ya wateja wa bidhaa zake yanayoongeza kila siku. 

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa SBL, Mark Ocitti, kazi ya upanuzi tayari imeshaanza Dar es salaam, ambalo ni tawi la kwanza la uzalishaji kati ya matatu lililoanzishwa mwaka 1996. Matawi mengine ya uzalishaji ni Moshi na Mwanza 

"Upanuzi huu haumaanishi tu kupata uwezo wa ziada wa uzalishaji wa bia kwa sisi (SBL), lakini pia unaongeza fursa zaidi za ajira kwa watanzania na kuongeza uhitaji zaidi wa shayiri, mahindi na mtama ambavyo kampuni hununua kutoka kwa wakulima wa ndani," Mkurugenzi Mkuu huyo anasema. 

SBL kwa sasa imeajiri wafanyikazi wa moja kwa moja zaidi ya 800 na wengine katika viwanda vyake. Kuna maelfu ya wanufaika wengine wakiwamo wasambazaji, wasafirishaji, wakulima, wamiliki wa baa na wafanyikazi ambao hutegemea bidhaa za kampuni hiyon kama chanzo cha mapato. 

Kampuni hiyo hutegemea vyanzo vya ndani vya shayiri, mahindi na mtama kwa uzalishaji wake wa bia. Mkurugenzi huyo anafafanua kuwa, hadi kufikia mwishoni wa mwaka jana, kampuni yake ilichukua nafaka za ndani hadi kufikia tani 15,000, ambayo ni sawa na asilimia 60 ya mahitaji kamili ya malighafi ya SBL kwa uzalishaji wa bia kwa mwaka. 

SBL ina bidhaa nyingi zinazouzika na zina ubora wa hali juu kwa jina lake. Chapa yake kuu ya Serengeti Premium Lager imekuwa bia ya kwanza nchini Tanzania kufanywa kuwa malt kwa asilimia 100. Hivi karibuni SBL ilizindua bidhaa yake nyingine ya Serengeti Premium Lite, ambayo ni ya kwanza nchini Tanzania iliyoingizwa sokoni mwaka wa 2017. 

"Wateja wetu walionesha uhitaji wa bia halisi ya kitanzania na ndio maana tulizindua Serengeti Premium Lite miaka miwili iliyopita. Watanzania wameipokea vyema bidhaa hii mpya ambayo imekuwa ikifanya vizuri katika soko, "Ocitti anasema na kuwashukuru wateja kwa kuunga mkono chapa hiyo. 

Utafiti uliofanywa na Kampuni ya Deloitte mwaka 2018 juu ya uchangiaji wa SBL kwenye uchumi wa Tanzania ulionyesha kuwa, SBL ilichangia thamani ya shilingi bilioni 567 katika uchumi wa Tanzania kwa mwaka jana. Hii ni sawa na asilimia moja ya uchangia kwenye pato la taifa kwa bidhaa za ndani (GDP) ) ambalo kwa sasa linakadiriwa kufikia dola bilioni 55, karibia sawa na shilingi trilioni 127. 

SBL ilianzishwa na wajasiriamali wachache wa Kitanzania mwaka 1996 na kiwanda kimoja ambacho kilijengwa jijini Dar es salaam. Kati ya mwaka 2010 na 2013 muundo wa umiliki wa kampuni ulibadilika na kuja na bodi ya kampuni kubwa ya bia ya East Africa Breweries Limited (EABL), mtayarishaji wa vinywaji duniani, Diageo, ambao wamechangia ongezeko la uwekezaji zaidi kwa kufungua viunga vikuu viwili vya nyongeza vya uzalishaji katika Jiji la Mwanza na Moshi. 

Hadi sasa, kampuni imepanua wigo kwa kuzalisha bidhaa za bia zinazoongoza kama vile Pilsner Lager, Tusker Lager, Guinness na Senator Of Late - Serengeti Premium Lite. 

Halikadhalika, SBL pia inasambaza katika soko la Tanzania bidhaa zingine za kwanza za Diageo za Kimataifa kama vile Johnnie Walker, Gordons, Smirnoff Black ICE na zingininezo.

MSIMU WA FAMILIA MARATHON WAZINDULIWA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Mbio za Marathon zimekuwa ni sehemu ya Maisha ya watu wengi hasa mijini na kwa kiwango kikubwa imechochea sana kuboresha maisha ya Watanzania wengi. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Familia Marathon Balozi wa Familia Marathon Veronica Kundya alisema “ mazoezi yana mchango mkubwa wa kuboresha afya ya Familia hivyo kujenga taifa bora la lenye nguvu la kesho”.Mbio hizo za Familia Marathon zinatarajiwa kufanyika Disemba 8 2019 jijini Dar Es Salaam

Bank ya Letshego yazindua akaunti ya LetsGo Flexi

$
0
0

 Wateja kupata hadi riba ya asilimia 10 kwa mwaka

Watanzania watakiwa kujenga utaratibu wa kujiwekea akiba ili kuimarisha uchumi wa familia na nchi kwa ujumla ili kufikia malengo ya kujenga uchumi wa viwanda,hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Biashara wa Letshego Bank Solomon Haule alipokutana na wateja wa Bank hiyo kwenye hafla ya uzinduzi wa huduma ya LetsGo Flexi save akaunti, akaunt ya akiba inayotoa faida ya riba hadi asilimia kumi kwa mwaka kulingana na akiba ya mteja.

"LetsGo Flexi save ni akaunti jumuishi kwasababu imezingatia na kuweka mbele maslahi ya wateja wote bila kuangalia uwezo au kipato cha mtu kupitia akaunti hii hata wateja wadogo wenye akiba chini ya shiling 20,000 watapata riba ya hadi asilimia 5% kwa mwaka."

Hafla hyo pia iliambatana na uadhimishaji wa wiki ya huduma kwa mteja ambapo Letshego Bank ilipata nafasi ya kuwashukuru baadhi ya wateja wao wanaoendelea kuwaunga mkono.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Letshego Tanzania Andrew Tarimo (aliyekaa) akimhudumia mteja katika maadhimisho ya wiki ya Wateja. Benki hiyo imezindua akaunti maalum ya LetsGo Flexi ambapo wateja watapata riba ya asilimia kumi kwa mwaka kwa kuweka kiasi cha fedha cha kuanzia Tzs50, 000.

K.T.O YATOA VITABU NA VIFAA MBALIMBALI VYA THAMANI YA SH.MILIONI 165

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

SHIRIKA la Karibu Tanzania Organization (K.T.O) limetoa vitabu na vifaa mbalimbali vyenye thamani ya sh. milioni 165 kwa ajili ya kufundishia vyuo vya Maendeleo ya wananchi 31 ili kuweza kuongeza utoaji wa elimu katika vyuo hivyo.

Akizungumza katika mafunzo ya wa wakuu wa vyuo vya maendeleo ya wananchi Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Eusebius Mbonde amesema kuwa vitabu na vifaa ya kufundishia vitumike katika malengo yaliyokusudiwa wanafunzi.

Mbonde amesema kuwa wamekuwa wakishirikiana na shirika la K.T.O kwa muda mrefu ikiwemo katika utoaji wa mafunzo kwa walimu kila baada ya muda kutokana na mahitaji yaliyopo.

Amesema kuwa serikali imekuwa katika uendelezaji wa elimu nchini ikiwemo kwa vyuo vya maendeleo ya wanannchi katika kuhakikisha jamii yote inapata elimu katika mazingira yeyote.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la K.T.O Maggid Mjengwa amesema kuwa vyuo vya maendeleo ya wananchi vilianzishwa mwaka 1975 baada ya Rais wa Kwanza Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwenda Sweeden ambako alikuta mfumo huo na ndipo aliuleta nchini.

Amesema kuwa shirika limekuwa likifanya kazi na vyuo 31 kati ya vyuo 54 vilivyopo nchini katika program ya elimu haina mwisho kwa utoaji wa mafunzo pamoja na vifaa vya kufundishia. 

Mjengwa amesema K.T.O iko mbele katika kupigania elimu nchini kwa vyuo vya maendeleo ya wananchi ili kuhakikisha jamii haichwi nyuma katika kupata elimu hiyo.

Kwa upande wa Mwalimu Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Mtawanya -Mtwara Sophia Mkopi amesema kuwa wanashukuru kwa kupata vitabu pamoja na vifaa mbalimbali ambavyo ni komputa ,Projector .

Amesema kuwa vifaa hivyo watatumia katika vyuo na matokeo yataonekana kwa kwa wananchi kunufaika na elimu na kuweza kusaidia jamii kwa namna moja au nyingine.
 Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Eusebius Mbonde akizungumza na waandishi mara baada ya kukabidhi msaada wa vitabu na vifaa mbalimbali kwa wakuu wa vyuo vya maendeleo ya wananchi vilivyotolewa na Shirika la Karibu Tanzania Organization (K.T.O) katika mafunzo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam. 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Karibu Tanzania Organization (K.T.O) Maggid Mjengwa akizungumza na waandishi  habari kuhusiana na Shirika hilo katika utoaji wa mafunzo na vifaa mbalimbali kwa wakuu wa vyuo vya maendeleo ya wananchi katika mafunzo na ukabidhi wa vifaa mbalimbali jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Mtawanya mkoani Mtwara Sophia Mkopi akitoa maelezo kuhusiana na mafunzo yanayotolewa na  Shirika la K.T.O pamoja na misaada mbalimbali inayotolewa katika vyuo vya maendeleo ya wanannchi.
 Baadhi ya wakuu wa vyuo vya maendeleo ya wananchi  katika mafunzo yanayotolewa  na Shirika la K.T.O yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Eusebius Mbonde Akimkabidhi Komputa mpakato na Projector  Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi wa Chuo cha Kasulu FDC Mhandisi Ramadhan Simba  ,jijini Dar es Salaam.

DC KATAMBI KULA SAHANI MOJA NA WANAOWAKATISHA MASOMO WATOTO WA KIKE

$
0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi akizungumza na walimu na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mnadani ikiwa leo ni maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike
 Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mnadani wakati alipofika kuzungumza nao ikiwa ni maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike
Sehemu ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mnadani wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Dodoma (hayupo pichani) alipofika kuzungumza nao leo


Charles James, Michuzi TV

MKUU wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi amewaonya wanaume wanaooa watoto wa kike ambao bado ni wanafunzi huku akisema sheria kali itachukuliwa pia kwa wazazi ambao wanalazimisha watoto wao kuolewa.

Akizungumza katika Shule ya Sekondari ya Mnadani wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike, DC Katambi amesema hatokubali kuona binti yeyote anashindwa kuendelea na masomo kwa sababu ya kuolewa ndani ya Wilaya yake.

Amesema Serikali ya awamu ya tano imehakikisha inakuza elimu chini kwa kusimamia sera ya elimu bure nchini hivyo wao kama wasaidizi wa Rais Magufuli wana wajibu wa kuhakikisha kila mtoto anapata elimu bila kujali Jinsia yake.

" Serikali ya Rais Magufuli inapiga vita sana vitendo vya kinyanyasaji vinavyofanywa dhidi ya mtoto wa kike, ni rai yangu kwa jamii zetu kwa ujumla kuilinda haki ya mtoto wa kike isipotee.

Kama Mkuu wetu wa Nchi ametoa nafasi nyingi za kiuongozi kwa wanawake basi ni jukumu letu kuhakikisha watoto wetu wa kike wanapata elimu bora ili kuja kuitumikia Nchi yao katika nafasi mbalimbali, " Amesema DC Katambi.

Amewaonya wazazi wanaoendekeza mila potofu kwa watoto wa kike hasa kwa kukubali kuwaoza wakiwa bado wanafunzi pamoja na kuwafanyia vitendo vingine vya kikatili ikiwemo ukeketaji.

Amesema ili kuwa na Taifa imara lenye uchumi wa kati kupitia viwanda ni lazima pia kukubali kuwanyanyua wanawake na kutupilia mbali mila na tamaduni ambazo hazina tija kwa watoto wa kike.

" Hatuwezi kukubali kuona mabinti zetu wanakosa elimu ambayo Mhe Rais Magufuli ametupatia bure kwa sababu ya tamaa za wanaume ambao wanaoa wanafunzi au kwa mzazi atakayepokea mahari kumuoza binti yake.

Sheria ipo wazi kabisa ole wenu ukutwe na mwanafunzi wa kike, uwe ni Mwalimu, Mfanyabiashara, Mtumishi wa Serikali au Bodaboda tutahakikisha tunakuchukulia. Na yeyote tutakayemkamata atakua mfano kwa wengine, " Amesema DC Katambi.

Amewataka walimu na wanafunzi kushirikiana kutoa taarifa kwenye vyombo vya sheria pale wanapobaini kwamba kuna vitendo vya unyanyasaji na ukandamizaji wanavyofanyiwa watoto wa kike hasa wanafunzi.

RAIS DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI MKUBWA WA UMEME WA KUUNGANISHA MKOA WA KATAVI KWENYE GRIDI YA TAIFA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli, Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, Viongozi wa Mkoa wa Katavi, Mawaziri pamoja na Wabunge akivuta  utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi  mradi wa umeme wa kuunganisha mkoa wa Katavi kwenye Gridi ya Taifa kwa njia ya msongo wa Kilovolti 132 kutoka mkoani Tabora katika sherehe fupi zilizofanyika nje kidogo ya manispaa ya Mpanda.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani mara baada ya kuweka la msingi  mradi wa umeme wa kuunganisha mkoa wa Katavi kwenye Gridi ya Taifa kwa njia ya msongo wa Kilovolti 132 kutoka mkoani Tabora katika sherehe fupi zilizofanyika nje kidogo ya manispaa ya Mpanda.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kuweka la msingi  mradi wa umeme wa kuunganisha mkoa wa Katavi kwenye Gridi ya Taifa kwa njia ya msongo wa Kilovolti 132 kutoka mkoani Tabora katika sherehe fupi zilizofanyika nje kidogo ya manispaa ya Mpanda.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi na wafanyakazi wa Tanesco mara baada ya kuweka la msingi  mradi wa umeme wa kuunganisha mkoa wa Katavi kwenye Gridi ya Taifa kwa njia ya msongo wa Kilovolti 132 kutoka mkoani Tabora katika sherehe fupi zilizofanyika nje kidogo ya manispaa ya Mpanda.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wanafunzi wa Isukumilo na Mpanda Sekondari wakati akielekea Wilaya Mpya ya Tanganyika.

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Isukumilo na Mpanda Girls wakimsangilia wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliposimama katika barabara ya kuelekea katika Wilaya mpya ya Tanganyika.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia ramani ya majengo ya hospitali ya Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi wakati akipewa maelezo na Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo katika eneo la mradi huo wa ujenzi.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na viongozi wengine wa mkoa wa Katavi, Wabunge pamoja na Mawaziri, akivuta utepe kuashiria uzinduzi wa Ujenzi wa Hospitali za Wilaya ya Tanganyika, Mlele na Mpimbwe mkoani Katavi mara baada ya kuwasili katika Wilaya hiyo mpya ya Tanganyika.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli akiwapongeza Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo pamoja na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu mara baada ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Tanganyika..
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Salehe Mhando mara baada ya kukagua ujenzi wa Hospitali ya Tanganyika
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Isaack Kamwelwe wakivuta utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa barabara ya Mpanda-Ifukutwa-Vikonge km 35 katika eneo la majalila Wilayani Tanganyika mkoani Katavi. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mke wake Mama Janeth Magufuli, Mawaziri, viongozi wa mkoa wa Katavi pamoja na Wabunge, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Mpanda-Ifukutwa-Vikonge km 35 katika sherehe zilizofanyika katika eneo la majalila Wilayani Tanganyika mkoani Katavi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Katavi Juma Homera mara baada ya kuzindua ujenzi wa barabara ya Mpanda-Ifukutwa-Vikonge km 35 katika sherehe zilizofanyika katika eneo la majalila Wilayani Tanganyika mkoani Katavi. PICHA NA IKULU

MASHIRIKA YAPIMA AFYA MAONESHO YA CHAKULA DUNIANI KITAIFA SINGIDA

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt.Rehema Nchimbi akipima uzito katika banda la Mashirika ya Save the Children Tanzania, Shirika la chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) katika Maonesho ya Maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani yanayofanyika Kitaifa mkoani Singida leo. Kutoka kushoto ni Msaidizi wa Ofisi ya FAO, Mihambo Gabriel na Afisa Mradi Mkuu wa WFP, Florian Ngali.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.Rehema Nchimbi akipima uzito.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.Rehema Nchimbi akizungumza na waandishi wa habari.


Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akisalimiana na Meneja Mipango Mwandamizi wa Shirika la Save The Children Tanzania (SCT) Florian Fanuel na Afisa Mradi Mkuu wa WFP, Florian Ngali katika Maonesho ya Maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani yanayofanyika Kitaifa mkoani Singida.


Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Kilimo, Revocatus Kassimba, akizungumzia kukamilika kwa maandalizi ya maadhimisho hayo.
Mwalimu Elias Bubimbi kutoka Chuo cha Kilimo Mati- Mubondo (kulia) akimuelekeza mwananchi aliyetembelea banda la chuo hicho jinsi ya kutengeneza biskuti za mbaazi.
Afisa Mifugo Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Deograsias Ruzangi akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.Rehema Nchimbi alipotembelea banda la wizara hiyo.
Majasiriamali Rosemary Luhasile kutoka Nantakunganirwa Group akimpa zawadi ya dagaa Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.Rehema Nchimbi.


Afisa Mfawidhi Kituo cha Wizara cha Ukuzaji Viumbe Maji (Mwamapuli) akimuelekeza jinsi ya ufugaji wa samaki Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.Rehema Nchimbi alipotembelea banda la kituo hicho. Wa tatu kutoka kulia ni Mzee Juma Ibrahim Mkhofoi mfugaji maarufu wa samaki mkoani Singida.
Afisa Ubora Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB), Idd Mkolamasa, akimuelekeza jambo Mkuu wa Wilaya ya Singida, Paskas Muragili alipotembelea banda la CPB.




Dotto Mwaibale na Boniphace Jilili, Singida

SHIRIKA la Save the Children Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limeendesha zoezi la upimaji wa uzito na urefu kwa wananchi katika maonesho ya maadhimisho ya siku ya chakula duniani ambayo kitaifa yanafanyika mkoani Singida.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Meneja Mipango Mwandamizi wa shirika hilo, Florian Fanuel alisema wanafanya zoezi hilo katika maonesho hayo kupitia mradi wa boresha lishe ambao unaiwezesha jamii kujenga lishe bora na kuondokana na utapiamlo na lishe duni.

"Hapa tunaonesha jinsi ambavyo jamii inaweza kujizalishia chakula chenye lishe bora lakini pia tunatumia fursa ya maadhimisho haya kutoa elimu na huduma za lishe"alisema Fanuel.

Wakati huo huo mkuu wa mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akizungumza baada ya kupima uzito na urefu aliwahimiza wananchi wa mkoa huo na wa mikoa ya jirani kufika kwenye maonesho hayo ili kupata elimu hiyo.

Alisema kupitia maonesho hayo ni vyema kila mwananchi kujitathimini juu ya lishe aliyonayo kuwa yuko sawa kilishe ama laa baada ya kupata elimu kutoka kwa wataalamu hao.

"Watanzania wengi hawathamini afya zao, mtu yuko tayari kumiliki gari zuri, nguo nzuri lakini anasahau lishe " alisema Dkt Nchimbi.

Nchimbi alisema pamoja na kupata elimu ya lishe pia maonesho hayo yanatoa fursa ya wananchi kupata elimu ya utunzaji wa ardhi,matumizi ya mbegu sahihi ili kuongeza kiwango cha uzalishaji.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Kilimo, Revocatus Kassimba alisema maandalizi ya maonesho hayo yamekamili na lengo hasa ni kuwapa elimu ya lishe wananchi ili kuondokana na lishe duni.

Alisema takwimu zinaonyesha uzalishaji wa chakula unatosheleza, hivyo watanzania hawana haja ya kuwa na lishe duni, ni elimu tu ambayo inahitajika ya namna ya kutumia vyakula wanavyovizalisha ili wawe na lishe bora.

Waziri Kigwangalla Mgeni Rasmi mbio za Rock City Marathon

$
0
0
 WAZIRI wa Maliasili na Utalii Dk Hamisi Kigwangalla anatarajiwa kuongoza maelfu ya washiriki wa mbio za Rock City Marathon zinazoratarajiwa kufanyika Oktoba 20, mwaka huu kwenye viunga vya Jengo la Biashara la Rock City Mall, jijini Mwanza.
 
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa mapema hii leo jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mbio hizo, Bw Clement Mshana, ushiriki wa Waziri Kigwangalla unaenda sambamba na ushiriki wa viongozi wengine waandamizi wa serikali kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bw John Mongella ambaye tayari amethibitisha kushiriki katika mbio za KM 42.
“Uwepo wa Waziri mwenye dhamana na masuala ya utalii kwenye mbio hizi unatokana na yeye kuunga mkono agenda iliyobebwa na mbio hizi ambayo mbali na kukuza vipaji vya mchezo huo ni kutangaza utalii hususani katika  ukanda wa Ziwa kupitia mchezo wa riadha,’’Alisema
Mbio hizo zilizoanzishwa miaka kumi iliyopita zinatarajiwa kupambwa na burudani mbalimbali zikiwemo ngoma za asili na maonesho ya waadau  mbalimbali wa utalii ikiwemo Wizara ya Maliasili na Utalii, Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) sambamba  na wadhamini wa mbio hizo ambao ni pamoja na  kampuni za TIPER na  Pepsi.
Wadhamini wengine ni pamoja na, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), CF Hospital, Metro FM,  Mwanza Water, Pigeon Hotel, The Cask and Grill, SDN na Kampuni ya Ulinzi ya Garda World. 
 “Ukanda wa Ziwa una vivutio vingi ambavyo lazima vitangazwe kimataifa kwa nguvu kubwa zaidi na mbio hizi zimekuwa kama chachu ya kufanikisha agenda hiyo hususani kwa mwaka huu ambapo zinatarajiwa kuhusisha wadau wengi zaidi wa masuala ya utalii ambao pamoja na mambo mengine watapata fursa ya kuonesha bidhaa na huduma zao kwenye viunga vya mbio hizo’’ alibainisha. 
Aidha, zikiwa zimesalia siku chache tu kabla ya kufanyika kwa mbio hizo tayari wadau mbalimbali wanaotarajia kushiriki wameonesha kufurahishwa na zawadi zitakazotolewa kwa washindi na washiriki zikiwemo medali na fedha taslimu zaidi ya Sh Mil 30.
“Pamoja na medali washindi wa kwanza wa mbio za kilomita 42 kwa wanaume na wanawake watajinyakulia sh. Mil 4 kila mmoja, sh.mil 2/-  kwa washindi wa pili na sh. Mil 1/- kwa washindi wa tatu, huku washindi wanne hadi kumi na tano nao pia wakiibuka na zawadi  za medali na pesa taslimu.’’
“Kwa upande wa mbio za  Kilomita 21, pamoja na medali washindi wa kwanza kwa wanaume na wanawake watajinyakulia sh.  Mil 2/- kila mmoja, sh. Mil 1/-kwa washindi wa pili na sh. Laki 7/- kwa washindi wa tatu huku pia washindi wanne hadi wa kumi na tano wakiibuka na  zawadi za pesa taslimu na medali kila mmoja.’’ alitaja
Kuhusu mbio za kilomita tano ambazo zitahusisha washiriki kutoka mashirika na taasisi mbalimbali (corporates), Bw Mshana alisema inatarajiwa kuwa zitaongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Dk Philis Nyimbi sambamba na washiriki wenye ualbino ambapo zawadi za fedha taslimu zitatolewa kwa washindi watatu wenye ualbino pekee.
“Kwa washindi wa mbio za kilomita 2.5 zitakazohusisha watoto wenye umri kati ya miaka 7 hadi 10 washindi watapatiwa  fedha taslimu.’’ Alibainisha.
Akizungumzia usajili wa mbio hizo Bw. Mshana alitoa wito kwa washiriki kuendelea kujisajili kupitia vituo na mawakala wa mbio hizo katika mikoa ya Mwanza, Dar es Salaam, Dodoma, Pwani na Arusha
‘’Kwa sasa usajili wa mbio hizo unaendelea kupitia vituo mbalimbali katika mikoa ya Mwanza (Rock City Mall, Pasiansi Afro Twist Gym), Dodoma (Shabiby Bus Terminal), Dar es Salaam (Shamo Tower, Imalaseko Super Market (Posta), Heleana Fashion – Dar Free Market), Arusha pamoja na Bagamoyo mkoani Pwani.’’
 “Pia usajili unaweza kufanyika kwa njia ya  mtandao kupitia website yetu ya Rock City Marathon ambayo ni www.rockcitymarathon.co.tz. ’’ alitaja
Mwisho.

RAIS DKT. MAGUFULI AJIANDIKISHA DAFTARI LA WAPIGA KURA KWA AJILI YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KATIKA KITONGOJI CHA SOKOINE CHAMWINO MJINI DODOMA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akijiandikisha katika daftari la Wapiga Kura kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mtaa katika Kitongoji cha Sokoine Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 12/10/2019. Kulia aliyekaa ni Afisa wa NEC Mary Joseph Mwambongo 


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuangalia Afisa kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC Mary Joseph Mwambongo akimalizia taratibu za uandikishaji katika katika Kitongoji cha Sokoine Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 12/10/2019.
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akijiandikisha katika daftari la Wapiga Kura kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mtaa katika Kitongoji cha Sokoine Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 12/10/2019. Kulia aliyekaa ni Afisa wa NEC Mary Joseph Mwambongo 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama kwenye msari na mke wake Mama Janeth Magufuli pamoja na wananchi wengine wakati wakielekea kujiandikisha katika daftari la Wapiga Kura kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mtaa katika Kitongoji cha Sokoine Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 12/10/2019.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Kitongoji  cha Sokoine Chamwino mkoani Dodoma leo mara baada ya kujiandikisha katika katika Kitongoji cha Sokoine Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 12/10/2019. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika foleni ya kuchukua chakula pamoja na Waandishi wa Habari mkoani Dodoma leo tarehe 12/10/2019. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ana kula chakula pamoja na Waandishi wa habari wa Vyombo mbalimbali vya habari wa mkoani Dodoma leo. PICHA NA IKULU


Vodacom Tanzania PLC yawazawadia Watoa Huduma wa Kituo cha Huduma kwa Wateja

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Plc, Hisham Hendi akimkabidhi cheti cha kutambua mchango wake kwa kutoa huduma bora kwa wateja, Stella Mboyelwa kwenye maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja. Wengine mwisho kulia ni Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Vodacom Tanzania Plc, Harriet Lwakatare na Wendyline Malawa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Plc, Hisham Hendi akimkabidhi cheti cha kutambua mchango wake kwa kutoa huduma bora kwa wateja, Restituta Masondore kwenye maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja. Wengine mwisho kulia ni Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa kampuni hiyo, Harriet Lwakatare na Wendyline Malawa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Plc, Hisham Hendi akimkabidhi cheti cha kutambua mchango wake kwa kutoa huduma bora kwa wateja, Kelvin Mrema kwenye maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja. Wengine mwisho kulia ni Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa kampuni hiyo, Harriet Lwakatare na Wendyline Malawa.
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Vodacom Tanzania Plc, Hisham Hendi akimkabidhi cheti cha kutambua mchango wake kwa kutoa huduma bora kwa wateja, Godfrey Shayo kwenye maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja. Wengine mwisho kulia ni Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa kampuni hiyo, Harriet Lwakatare na Wendyline Malawa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Plc, Hisham Hendi (kushoto) akiwapongeza wafanyakazi wa kituo cha huduma kwa Wateja (Call Centre) kwa namna wanavyotoa huduma bora kwa wateja wao, wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa Wateja . Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Vodacom Tanzania Plc, Harriet Lwakatare.

Wafanyakazi wa Kituo cha Huduma kwa wateja Vodacom (call centre) wakimsikiliza mkurugenzi wao , Hisham Hendi.

KIKOSI CHA SIMBA SC CHATUA KIGOMA,KUTIFUATANA KESHO NA MASHUJAA FC

$
0
0
Na Editha Karlo wa Michuzi Tv,Kigoma

TIMU ya mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara klabu ya simba sc imewasili kigoma kwa ajili ya mechi ya kirafiki   dhidi ya Mashujaa FC na  Aigle Noir ya nchini Burundi. 

kocha wa simba SC,Patrick Aussems amesema kuwa amefurahi kwa timu yake kuwasili mkoani humo na kwamba wamejipanga kupata ushindi katika michezo hiyo.

Amesema mechi hizo za kirafiki ni maandalizi ya kujiweka tayari na mchezo unaofuata  dhidi ya Azam fc katika ligi kuu.

Katibu wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Kigoma KFA mkoani, Omary  Gindi amesema mikakati ya chama hicho ni kuhakikisha timu ya mashujaa  inapanda ligi kuu msimu ujao.

Amesema katika mchezo huo viingilio vitakuwa sh.5,000 kwa viti vya kawaida na vip itakuwa sh.10,000 .

Kwa mara ya simba Kikosi hicho kimewasili mkoani hapa  baada ya miaka 18 ya kucheza na timu ya reli.

Simba watua kigoma tayari kwa mechi ya kirafiki kesho na timu ya mashujaa

TEKNOLOJIA MPYA YA KUZUIA WIZI WA PIKIPIKI NA VYOMBO VYA MOTO YAJA NCHINI

$
0
0
Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Benson Security Systems na AfriTrack wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuzindua mfumo wa kimtandao wa kudhibiti vyombo vya usafiri jijini Arusha.


Na.Vero Ignatus,Arusha

Teknolojia ambayo itakayotumia mtandao wa mawasiliano wa internet imezinduliwa na Kampuni ya Benson ya jijini Arusha ikishirikiana AfriTrack ya jijini Dar es Salaam yenye uwezo wa kuthibiti wizi wa pikipiki na vyombo vya moto


Miqdaad Kassam ni Mkuu wa Uendeshaji wa Kampuni ya Benson, amesema wakati wa uzinduzi huo kuwa,kwa kutumia teknolojia hiyo,pikipiki ikiibiwa, itapatikana kwa kuwa itaonekana eneo iliyopo

“Ni teknolojia rahisi itakayodhibiti wizi wa pikipiki ambao sasa ni moja ya matatizo sugu yanayolalamikiwa na wateja wengi.Ukifunga kifaa cha kudhibiti wizi katika pikipiki yako,hata kama ikiibiwa usiwe na wasiwasi,itapatikana tu,”alisisitiza Kassam katika uzinduzi huo.

Salma Rothbletz ni Mkuu wa Huduma kwa Wateja katika Kampuni hiyo,alisema kifaa hicho maalum hufungwa katika pikipiki na kuunganishwa na simu ya mkononi ambapo mteja hupata taarifa zote za uendeshaji wa pikipiki katika siku yake.

Alifafanua kuwa mfumo huo hudhibiti udanganyifu wa madereva katika matumizi ya mafuta na umbali aliotumia kwa siku katika uendeshaji wa pikipiki,jambo litakalowawezesha wamiliki wa pikipiki kuwa na uhakika wa mapato, kwa zile zinazofanya usafiri wa abiria.

“Mfumo huu utawasaidia wamiliki wa pikipiki za kusafirisha abiria kufuatilia biashara yao kwa ukaribu na uhakika kwa kuwa wanaweza kujua kiasi cha mafuta kilichotumika kwa siku na hata umbali ambao pikipiki imetembea,” alifafanua.

Suhail Sheriff ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya AfriTrack, amesema katika uzinduzi huo kuwa mtandao huo wa udhibiti wa vyombo vya usafiri unatumika pia katika malori na magari ya abiria na utasaidia kupunguza ama kuondoa kabisa ajali za barabarani.

Amesema kuwa mfumo huo hudhibiti hali ya dereva kama yuko timamu kuendesha chombo husika na iwapo kuna dosari hutoa ishara ya tahadhari kwa dereva mwenyewe na mwenye gari kabla ya madhara yoyote, ikiwa ni pamoja na ajali, kutokea.

“Kama gari lina hitilafu za kiufundi au dereva ana tatizo lolote, mathalan la kiafya, mfumo hugundua na baada ya muda hutoa ishara ya tahadhari unaosaidia hatua za kuzuia madhara yatokanayo na hitilafu hiyo kuchukuliwa haraka,”alisema Mkurugenzi Mtendaji huyo.

Sheriff amesema kuwa vyombo vya usafiri vinapokuwa katika maeneo yasiyo na mtandao wa mawasiliano, ikiwa ni pamoja na porini na bahari kuu ambapo mawasiliano ni magumu,wanatumia mfumo wa mawasiliano wa setelaiti kufuatilia mwenendo wa vyombo hivyo katika maeneo hayo yasiyo na mtandao.

Aidha amesema kuwa mfumo huo tayari umeshaanza kwa mafanikio makubwa katika nchi za Ivory Coast, Malawi,Zambia na sasa umeingia nchini katika miji ya Dar es Salaam, Arusha, Mwanza na Mbeya

Kiure, Omar Kiure ni Mwakilishi wa Kampuni ya Uhandisi ya amesema katika uzinduzi huo kuwa mfumo huo wa udhibiri magari na madereva katika sekta ya usafirishaji ni ukombozi kutokana na kukithiri kwa wizi hasa wa mafuta unaosababisha hasara kubwa.

“Wizi wa mafuta katika katika sekta ya usafirishaji na ujenzi ni sehemu ya tatizo sugu na linalokera mno katika sekta ya ujenzi na kwa kweli mfumo huu utatusaidia kudhibiti wizi huu unaotutia hasara mno na kusababisha gharama kuwa juu,” alisema Kiure.

Athilyo Choga ni Mwakilishi wa Jeshi la Polisi Mkoani Arusha amesema katika uzunduzi huo kuwa mfumo huo wa udhibiti utasaidia jeshi hilo kudhibiti na kupunguza au kumaliza kabisa tatizo la ajali za barabarani

WAZIRI LUGOLA AAGIZA POLISI KUWAKAMATA WANAOWAPOTOSHA WANANCHI UANDIKISHAJI UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia), ajiandikisha katika daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali ya Mitaa, katika Kituo cha Senta, Kijiji cha Nyamitwebili, Jimbo la Mwibara, Wilayani Bunda, Mkoa wa Mara, leo. Lugola ameliagiza Jeshi la Polisi Nchini, kuwakamata na kuwafunguliwa mashataka watu ambao wanawapotosha wananchi kutokujitokeza kujiandikisha kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Kushoto ni Mwandikishaji wa Kituo Kituo hicho, Nicolaus Zakaria. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia), akimpongeza Mwandikishaji wa Kituo Kituo cha Senta, Kijiji cha Nyamitwebili, Wilayani Bunda, Mkoa wa Mara, Nicolaus Zakaria, baada ya kujiandikisha katika daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali ya Mitaa. Lugola ameliagiza Jeshi la Polisi Nchini, kuwakamata na kuwafunguliwa mashataka watu ambao wanawapotosha wananchi kutokujitokeza kujiandikisha kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akizungumza na wananchi wa Kibara, JImbo la Mwibara, Wilayani BUnda, Mkoa wa Mara, leo, mara baada ya kujiandikisha katika daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali ya Mitaa, Jimbo la Mwibara, Wilayani Bunda, Mkoa wa Mara, leo. Lugola ameliagiza Jeshi la Polisi Nchini, kuwakamata na kuwafunguliwa mashataka watu ambao wanawapotosha wananchi kutokujitokeza kujiandikisha kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Kushoto ni Mwandikishaji wa Kituo Kituo hicho, Nicolaus Zakaria. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (wapili kulia), akiwa katika foleni ya kwenda kujiandikisha katika daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali ya Mitaa, Jimbo la Mwibara, Wilayani Bunda, Mkoa wa Mara, leo. Lugola ameliagiza Jeshi la Polisi Nchini, kuwakamata na kuwafunguliwa mashataka watu ambao wanawapotosha wananchi kutokujitokeza kujiandikisha kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Kushoto ni Mwandikishaji wa Kituo Kituo hicho, Nicolaus Zakaria. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

******************************************

Na Felix Mwagara, MOHA, Mwibara

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola ameliagiza Jeshi la Polisi Nchini, kuwakamata na kuwafunguliwa mashataka watu ambao wanawapotosha wananchi kutokujitokeza kujiandikisha kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Lugola amesema watu hao wanawarubuni wananchi kwa njia za mitandao ya kijamii, kuwafuata majumbani kwao, wakiwapotosha kususia uchaguzi huo, pamoja na kuwadanganya kuwa walishajiandikisha kipindi cha uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, hivyo watatumia vitambulisho hivyo hivyo katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 24, 2019.

Akizungumza na wananchi Jimboni kwake Mwibara, Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara, mara baada ya kujiandikisha katika kituo cha Sokoni, Kata ya Kibara, alisema taarifa hizo amepewa na viongozi wa Serikali ya Kijiji pamoja na vyanzo mbalimbali, kuwa kuna kundi la wananchi wanapita mitaani kuwapotosha wananchi na pia kuwatisha wasifike vituoni kujiandikisha wakiwa na lengo la kuvuruga uchaguzi.

“Wananchi Kibara, wacha niwaambie, Serikali ya awamu ya tano si ya kuchezewa, watu hao ni wapotoshaji na lengo lao wanataka kuvuruga uchaguzi ambao ni muhimu kwa maendeleo ya wananchi, sasa naagiza polisi kuwasaka na kuwakamata watu hao, ili wawe mfano,” alisema Lugola.

Lugola aliongeza kuwa, Wizara yake inalinda amani katika uchaguzi huo, hivyo haiwezi kukaa kimya kuwaacha wapotoshaji hao wakiendelea kuharibu na kutamba mitaa jambo ambalo Serikali haiwezi ikawaacha.

Pia aliwataka wananchi wajitokeze kwa wingi katika vituo mbalimbali nchini kujiandikisha ili waweze kuwachagua viongozi wao na kuiletea maendeleo nchi.

“Leo mmejitokeza wengi, nawapongeza, nafikiri wengi wenu mmekuja labda baada ya kuniona mimi mbunge wenu nimefika, lakini bado siku hazijaasha, waambieni wananchi wajitokeze kuja kujiandikisha leo, pamoja na Kesho, viongozi msichoke, fanyeni kazi kwa nguvu zote, kwa maendeleo ya jimbo let una nchi kwa ujumla,” alisema Lugola.

Alisema kupitia uchaguzi huo, viongozi wa vijiji na mitaa watasaidia Wizara yake baada ya kuwapata viongozi hao ambao pia wataunda Kamati ya ulinzi na usalama ya Kijiji na usalama wa eneo husika unaimarishwa zaidi kutokana na uwepo wa viongozi hao.

Aidha, Mwenyekiti wa Kijiji cha Kibara B, Laurent Mafwili Mnyaga, alikiri kuwepo kwa tatizo hilo kijijini kwake, lakini agizo alilolitoa Waziri Lugola litasaidia wananchi kujitokeza kwa wingi na pia litawasaidia viongozi wa Kijiji chake kuwahamasisha wananchi waende kujiandikisha kwa wingi zaidi, kwasababu wapotoshaji hao wanawajua na Serikali ya Kijiji hicho watahakikisha wanawapeleka polisi.

“Nimefurahi sana kumuona Mbunge wetu kufika Mwibara na kutuhamasisha zaidi, lakini alilolisema ni sahihi kabisa, baadhi ya wananchi wamepotoshwa wasije kujiandikisha, wakidanganywa kuwa kadi za zamani zitatumika kapigia kura uchaguzi wa Serikali za Mitaa jambo ambalo si sahihi,” alisema Mafwili.

Aliongeza kuwa, licha ya kukabiliwa na changamoto ya wananchi kupotoshwa, kutishwa na watu mitaani wenye nia ovu na serikali, lakini Mwenyekiti huyo alisema utoaji wa elimu kuhusu uandikishaji haukua na nguvu kiasi kilichosababisha wananchi kutokujitokeza kwa wingi.

Waziri Lugola tayari amejiandikisha katika Kijiji hicho na kupongezwa na wananchi hao, ambao wengi wao walijitokeza baada ya kumuona Mbunge wao kujitokeza katika kituo hicho.

Vodacom Yadhamini Mkutano Mkuu wa Mwaka wa ZATI, Zanzibar

$
0
0
Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano wa Kikanda Vodacom Tanzania, Aileen Meena akimkabidhi laini ya Vodacom kwa Waziri wa Habari na mambo ya kale wa Zanzibar, Mahmoud Thabit Kombo kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa ZATI.
Mfanyakazi wa Vodacom Zanzibar, Fahad (mwenye kofia) akimuelezea jambo Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, Mahmoud Thabit Kombo.
Wadau wa Utalii

RAIS DKT. MAGUFULI AWASILI MKOANI LINDI KUHUDHURIA SHEREHE ZA KILELE CHA MBIO ZA MWENGE WA UHURU NA KUMBUKUMBU YA MIAKA 20 YA KIFO CHA BABA WA TAIFA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitelemka kutoka katika ndege aina ya Bombadier ya ATCL alipowasili Uwanja wa Ndege wa Mtwara tayari kuelekea mkoani Lindi kuhudhuria sherehe za kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru na kumbukumbu ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wananchi wa Mji wa Mikindani waliokuwa wakisherehekea Siku ya Mikindani katika tamasha kubwa la utamnaduni la Urithi wakati akiwa njiani kuelekea mkoani Lindi kuhudhuria sherehe za kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru na kumbukumbu ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mmoja wa wafanyakazi wa Uwanja wa hedge wa Mtwara Bw. Jackson Elia baada ya kushuka kutoka katika ndege aina ya Bombadier ya ATCL mara tu alipowasili tayari kuelekea mkoani Lindi kuhudhuria sherehe za kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru na kumbukumbu ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakwanwa mara baada ya kushuka kutoka katika ndege aina ya Bombadier ya ATCL alipowasili tayari kuelekea mkoani Lindi kuhudhuria sherehe za kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru na kumbukumbu ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wananchi wa kijiji cha Mnazi Mmoja akiwa njiani kuelekea mkoani Lindi kuhudhuria kwenye sherehe za kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru na kumbukumbu ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere .PICHA NA IKULU


Viewing all 46334 articles
Browse latest View live




Latest Images