Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live

Vodacom Yawapongeza Wateja wake kote nchini

$
0
0
Mkurugenzi wa Huduma Kwa Wateja Vodacom Tanzania, Harriet Lwakatare (kulia) akimuhudumia Mteja, Peter Mbuya Mkazi wa Tabata Kimanga kwenye duka la Voda lililopo makao makuu ya kampuni hiyo leo, Katikati ni Mtaalam wa Mtandao kutoka Vodacom, Hendrick Rupia. Hii ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja.
Meneja wa Vodacom Kanda ya Kati, Andrew Temu (kushoto) akimkabidhi zawadi Emmanuel Machela (34) Mkazi wa Nzuguni Dodoma leo,Kampuni hiyo imekabidhi zawadi hizo katika wiki ya huduma kwa wateja inayoendelea. Anayeshuhudia katikati ni msimamizi wa maduka ya Vodacom Kanda ya Kati,Suzana Mwaipopo.
Meneja wa Vodacom Kanda ya Kati, Andrew Temu (kushoto) akimkabidhi zawadi Omari Lubasi mkazi wa Kikuyu Mjini Dodoma leo akiwa ni miongoni mwa wateja waliopata zawadi hiyo katika wiki ya huduma kwa wateja wa Kampuni ya simu ya Vodacom. Anayeshuhudia katikati ni msimamizi wa maduka ya Vodacom Kanda ya Kati, Suzana Mwaipopo na makabidhiano hayo yalifanyika Ofisi za Vodacom Kanda ya Kati Mjini Dodoma.
Mkurugenzi wa Biashara Vodacom Tanzania, Linda Riwa (kulia) akinyanyua juu Champagne kuzinduzi rasmi wiki ya huduma kwa wateja iliyofanyika kwenye duka la Voda makao makuu jijini Dar Es Salaam leo. Pembeni yake ni Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja Vodacom, Harriet Lwakatare.
Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja Vodacom Tanzania, Harriet Lwakatare akimlisha keki mmoja kati ya wateja waliokuwepo dukani siku ya leo.

Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja Vodacom Tanzania, Harriet Lwakatare akizungumza na waandishi na wateja waliohudhuria siku ya huduma kwa wateja wa Vodacom Tanzania, Pia alitoa shukurani kwa wateja na wafanyakazi wa Vodacom kwenye wiki hii na alitoa wito kwa wateja wasajili laini zao kwa alama ya vidole kote nchini.. Kulia ni George Lugata, Mkuu wa Idara ya Mauzo na Usambazaji wa kampuni hiyo.

SHIRIKA LA TTCL LAZINDUWA WIKI YA HUDUMA KWA MTEJA.

$
0
0

Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation), Mh. Balozi Mteule Mohamed Mtonga (kushoto) akikata keki kuashiria uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Mteja wa TTCL leo jijini Dar es Salaam. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Corporation, Waziri Kindamba akishuhudia.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation), Mh. Balozi Mteule Mohamed Mtonga (kushoto) akimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Corporation, Waziri Kindamba (kulia) kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Mteja wa TTCL leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation), Waziri Kindamba (wa pili kushoto) akimlisha keki Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation), Mh. Balozi Mteule Mohamed Mtonga mara baada ya kuzinduwa Wiki ya Huduma kwa Mteja wa TTCL iliyofanyika katika duka la huduma kwa wateja wa kampuni hiyo jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation), Mh. Balozi Mteule Mohamed Mtonga (kulia) akimlisha keki mmoja wa wateja wa TTCL kwenye hafla ya uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Mteja wa TTCL leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation), Mh. Balozi Mteule Mohamed Mtonga (kushoto) akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Mteja wa TTCL leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation), Waziri Kindamba.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation), Waziri Kindamba (kulia) akizungumza na wateja wa TTCL (hawapo pichani) kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Mteja wa TTCL leo jijini Dar es Salaam.
Kulia ni mmoja wa wafanyakazi wa TTCL akimuhudumia mmoja wa wateja kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Mteja wa TTCL leo jijini Dar es Salaam.
Kulia ni mmoja wa wafanyakazi wa TTCL akimuhudumia mmoja wa wateja kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Mteja wa TTCL leo jijini Dar es Salaam.


SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation) leo limezinduwa rasmi maadhimisho ya wiki ya huduma kwa mteja huku likisisitiza kuwa shirika hilo litaendelea kuleta mapinduzi makubwa katika eneo la utoaji huduma pamoja na ubunifu kwenye bidhaa zake.

Akizinduwa maadhimisho hayo, Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation), Mh. Balozi Mteule Mohamed Mtonga amesema shirika litaendelea kufanya mapinduzi makubwa eneo la utoaji huduma pamoja na ubunifu katika bidhaa zake ili kuhimili ushindani uliopo sokoni.

Alisema ripoti ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa mwaka unaoishia Desemba 2018, ilibaini kuwa TTCL ni Shirika la huduma za Mawasiliano linalokua kwa kasi, huku likiongoza kwa idadi ya ongezeko la wateja na hata huduma ya T PESA nayo ikitajwa miongoni mwa huduma zinazostawi kwa kasi kubwa.

"Hadi sasa, tumeweza kuwafikia asilimia 2 ya Wateja wa huduma za simu Nchini , yaani Wateja zaidi ya milioni mbili huku huduma ya T PESA ikifikisha Wateja zaidi ya laki nne, Mawakala elfu kumi na nne na miamala ya takribani Tsh bilioni tano za Kitanzania."

Aidha alisema katika kuwajali zaidi wateja wake kihuduma TTCL imezinduwa rasmi huduma ya TTCL App na namba maalum ya WhatApp ya Huduma kwa wateja kuboresha zaidi huduma zake.

Akifafanua zaidi juu ya huduma hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation), Waziri Kindamba aliongeza kuwa kila mwaka, wamekuwa wakiwapatia wateja wao huduma mpya na huduma ya mwaka huu itaenda sambamba na utoaji wa zawadi kemkem za kuonesha shukrani kwa wajeja wao.

"Mwaka huu 2019, tunawaletea huduma ya TTCL App ambayo ni Application itakayowawezesha Wateja wa TTCL Corporation kujiunga na vifurushi, kuongeza salio na kupata salio la akaunti yake kupitia simu za mkononi (i.e simu janja) na tablets."

Akifafanua zaida huduma hizo, alisema ndani ya TTCL App mteja ataweza kuongeza na kuangalia salio kupitia App hiyo itakayopatikana bure kwa wateja wa TTCL bila kujali kama ana kifurushi cha intaneti muda huo.Wateja watakaotumia TTCL App wataweza kupata huduma za ziada kama dondoo za afya, soko la hisa na kubadilisha fedha, kuona matangazo mbalimbali ya TTCL, kuunga kifurushi kwa namba nyingine, kumnunulia rafiki muda wa maongezi nk.

"TTCL App haitaji usajili maalumu ili kutumia. Sisi tumetimiza wajibu wetu, kazi kwenu Wateja wetu, kufurahia huduma hii nzuri na rahisi sana kuitumia. Pamoja na TTCL App, tumewaongezea Wateja wetu njia nyingine rahisi ya kuwasiliana nasi kupitia Huduma ya WhatsApp ambapo kwa namba 0738 151511, alisema.
Huduma zikiendelea kwenye duka la TTCL Samora jijini Dar es Salaam sambamba na maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Mteja.
Tupo tayari kuwahudumia wateja wetu kwa bashasha...! Ndivyo wanavyoonekana watoa huduma wa TTCL kwenye maadhimisho hayo.

KUFUATA MIONGOZO HUPUNGUZA USUGU WA WADUDU DHIDI YA DAWA

$
0
0
Mwakilishi kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) Bi. Comfort King-Giboie akisisitiza jambo mbele ya timu ya Afya ngazi ya Mkoa (RHMTs) juu ya namna ya kujikinga dhidi ya maambukizi kwa kufuata miongozo (IPC guideline) katika Mkoa wa Kigoma.
Wataalamu wa Afya ngazi ya Mkoa wakifuatilia kwa makini mafunzo ya namna ya kujikinga dhidi ya maambukizi kwa kufuata miongozo ya IPC, yaliyoandaliwa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Shirika lisilo Lakiserikali la MSH kupitia mradi wa MTaPS.
Afisa kutoka Kitengo cha Uhakika Ubora, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Erick Kinyenje akitoa mafunzo ya namna yakuchanganya dawa za kuua vijidudu mbalimbali katika maeneo yakutolea huduma za Afya.Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Dkt. Paul Chaote aakieleza jambo mbele ya Watoa huduma za Afya ngazi ya Mkoa, wakati wa mafunzo ya namna bora yakujikinga dhidi ya maambukizi mkoani Kigoma.


Na WAMJW – KIGOMA

Watumishi wa Sekta ya Afya nchini, wameaswa kufuata miongozo na taratibu za utoaji huduma za Afya wakati wa kutoa huduma kwa mgonjwa (IPC Standards) ili kupunguza tatizo la usugu wa wadudu dhidi ya dawa.

Hayo yamesemwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Dkt. Paul Chaote, wakati akifungua mafunzo ya namna ya kujikinga dhidi ya maambukizi kwa kufuata miongozo (IPC Guidline) wakati wa kumuudumia mgonjwa Mkoani Kigoma.

Dkt. Paul Chaote amesema kuwa usugu wa dawa ni moja kati ya tishio kubwa kwa Afya ya binadamu nchini, huku akidai kuwa Shirika la Afya Duniani (WHO) limeshauri nchi wanachama kuanzisha mikakati ya kukabili dhidi ya tatizo hili.

“Usugu wa dawa umekuwa moja ya tishio kubwa kwa Afya ya Wananchi katika jamii, hivyo Shirika la Afya Duniani (WHO) linashauri kuanzishwa kwa afua/mikakati mbali mbali ili kuweza kupambana na tatizo hili la usugu” Alisema Dkt. Paul Chaote.

Dkt. Paul Chaote aliendelea kusema, matumizi ya dawa yasiyo na ulazima yanaweza kupelekea tatizo la usugu wa wadudu dhidi ya dawa, huku akisisitiza kufuata miongozo ya njia za kukinga (IPC Standards) wakati wa kumuhudumia mgonjwa, kama njia kuu ya kupambana dhidi ya usugu wa wadudu dhidi ya dawa.

“Kufuata miongozo ya IPC (Infection, Prevention, Control) ni njia yenye gharama nafuu ambayo tunaweza kuifanya, ambayo itakuwa msaada mkubwa katika lengo letu la kupambana dhidi ya usugu wa wadudu dhidi ya dawa” Alisema Dkt. Chaote.

Naye, Afisa kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dkt. Boniface Marwa amesema kuwa takwimu zinaonesha kuwa watu 700,00/ hufariki Dunia kutokana na tatizo linalosababishwa na usugu wa wadudu dhidi ya dawa, huku akidai kuwa asilimia 89% ya vifo hivyo hutokea Barani Afrika na Asia.

Aliendelea kwa kusisitiza kuwa jitihada za makusudi ni lazima zichukuliwe na kila mtaalamu katika Sekta ya Afya ili kupambana na tatizo hili linalozidi kuwa tishio Duniani, huku akisisitiza juu ya kufanya tafiti mbali mbali ili kupata dawa mpya zitazoweza kupambana na wadudu sugu.

“Takribani watu 700,000 hufariki Duniani, kutokana na tatizo la usugu wa wadudu dhidi ya dawa, na asilimia 89% ya vifo hivyo hutokea Barani Afrika na Asia” Alisema Dkt. Boniface Marwa.

Kwa upande wake Afisa kutoka Kitengo cha Uhakiki Ubora, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Erick Kinyenje amewataka Wataalamu kutoka Sekta ya Afya mkoa wa Kigoma kuhakikisha wanapeleka Elimu juu ya muongozo wa kudhibiti na kukinga magonjwa (IPC Guidline) walioipata kwa watumishi wenzao katika maeneo yao ya kutolea huduma za Afya ili kukinga maambukizi katika maeneo hayo.

“Niwaombe mtusaidie kuifikisha Elimu hii mlioipata hapa kwa wWataalamu katika maeneo yenu yakutolea huduma za Afya, na kuisambaza miongozo hii ya njia bora za kukinga na kudhibiti maambukizi ya magonjwa katika maeneo hayo, hii itasaidia kupunguza maambukizi na jambo litalosaidia kupunguza usugu wa wadudu dhidi ya dawa”, alisema Bw. Erick Kinyenje.

Mafunzo hayo yaliyofadhiliwa na Shirika lisilo la Kiserikali la Management Science for Health (MSH) kupitia mradi wa Medicines, Technology and Pharmaceutical Services (MTaPS), yanatarajia kuendelea katika mikoa yote iliyo katika hatari ya kupata ugonjwa wa Ebola ili kuhakikisha ugonjwa huo hauingii nchini.

BENKI YA DUNIA YAIKOPESHA SERIKALI MKOPO WENYE MASHARTI NAFUU KUKABILIANA NA UMASKINI NCHINI.

$
0
0
Serikali ya Tanzania na Benki ya Dunia zimetiliana saini mkopo wenye masharti nafuu wa dola za Kimarekani milioni 450 kugharamia sehemu ya pili ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii -TASAF.Mkataba huo umetiwa saini na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Dotto James kwa niaba ya serikali na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bi. Bella Bird.

Akizungumza baada ya kutia saini mkataba huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango amesema kupatikana kwa fedha hizo ni kiashirio kingine cha Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dr. John Magufuli ilivyokusudia kuweka mazingira wezeshi ya kuondoa kero ya umaskini kwa wananchi wake.

Amesema Mkopo huo wenye masharti nafuu utaelekezwa zaidi katika kusaidia jitihada za Serikali za kutatua kero ya umaskini nchini kote kwa kuwashirikisha wananchi ambao ni walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wenye uwezo wa kufanyakazi kushiriki kwenye miradi ya maendeleo kwenye maeneo yao na kisha kulipwa ujira kama njia mojawapo ya kuwaongezea kipato.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bi. Bella Bird amesema Tanzania imekuwa mfano bora katika kuhudumia wananchi wanaokabiliwa na umaskini mkubwa kupitia mfuko wa hifadhi ya jamii jambo ambalo limeifanya Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo ya Dunia kuridhia kiasi hicho kikubwa cha fedha kutolewa kwa utaratibu wa Mkopo wenye masharti nafuu .

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Taifa ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF- Dr. Moses Kusiluka ameishukuru Serikali kwa kutambua mchango mkubwa unaotolewa na TASAF katika kusaidia jitihada za kupunguza umaskini nchini.

Amesema kupatikana kwa fedha hizo kutasaidia kuwafikia wananchi wenye uhitaji mkubwa nchini kote na kuwa kichocheo cha kuharakisha maendeleo na hatimaye kuliwezesha taifa kupunguza umaskini kwa kiwango kikubwa na kuboresha miundombinu katika sekta za elimu, afya maji huku mkazo mkubwa ukiwekwa katika kukuza uchumi wa kaya za walengwa.

Katika hatua nyingine Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Bw. Ladislaus Mwamanga ameishukuru serikali kwa uamuzi wa kuendelea kutekeleza Mpango wa kunusuru Kaya Maskini na kuahidi kusimamia kwa uaminifu raslimali fedha ili ziweze kunufaisha taifa kupitia Walengwa.

Amesema uzoefu uliopatikana katika sehemu ya kwanza ya Mpango umeonyesha kuwa Walengwa wengi wamebadili maisha yao kwa kutumia fursa zinazotolewa na Mpango huku akitaja sekta za elimu, afya na uzalishaji mali kuwa zimechangia kwa kiwango kikubwa kuboresha maisha ya Walengwa.

Hafla hiyo imehudhuriwa pia na wawakilishi wa mashirika yanayochangia fedha kwa ajili ya kutekeleza shughuli za serikli kupita Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF. Utekelezaji wa sehemu ya pili ya Mpango wa Kunusuru Kaya maskini unatarajiwa kuanza wakati wowote baada ya kuzinduliwa rasmi na utahudumia takribani Kaya milioni 1.3.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dotto James (kushoto) na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bi. Bella Bird (kulia) wakitia saini mkataba wa kuipatia Tanzania Mkopo wenye masharti nafuu kutoka Benki ya Dunia kutekeleza sehemu ya Pili ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kupitiaTASAF. 


Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Ikulu Dr. Moses Kusiluka (katikati) akizungumza mara baada ya kutiwa saini ya mkopo wenye masharti nafuu kati ya serikali ya Tanzania na Benki ya Dunia ,fedha zitakazotumika kutekeleza sehemu ya pili ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unatekelezwa na serikali kupitian TASAF.Kulia kwake ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bw. Dotto James na kushoto kwake ni Mkurugenzi Makazi wa Benki ya Dunia Bi. Bella Bird.
Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bi. Bella Bird (katikati) akizungumza baada ya kutia saini mkopo wenye masharti nafuu kwa ajili ya kutekeleza miradi ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa kamati ya taifa ya Uongozi ya TASAF ,Dr. Moses Kusiluka na kulia kwake ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bw. Dotto James.
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF ,Bw. Ladislaus Mwamanga (aliyevaa miwani) akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) baada ya serikali kutia saini mkataba wa mkopo wenye masharti nafukutoka Benki ya Dunia, fedha zitakazotumika kutekeleza mradi wa kupunguza umaskini nchini .  

WAJUMBE WA MABARAZA YA KISWAHILI BAKIZA NA BAKITA WAKUTANA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Viongozi wa BAKITA na BAKIZA wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kikao cha mashauriano.Kutoka kulia waliosimama mbele ni Bi Mwanahija(Katibu Mtendaji - BAKIZA), Dkt.Muhammed Seif Khatib( Mwenyekiti - BAKIZA),Dkt.Sewangi( Katibu Mtendaji- BAKITA) na Dkt.Samwel( Mwenyekiti - BAKITA) na wajumbe wengine.

..............................................

Viongozi wa Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) na Baraza la Kiswahili Zanzibar (BAKIZA) wamekutana jijini Dar es salaam ili kujadiliana mambo mbalimbali kuhusu maendeleo ya Lugha ya Kiswahili katika mkutano uliofanyika kwenye ofisi za Baraza la Kiswahili la Taifa, jijini Dar es Salaam huku mambo kadhaa ya mashirikiano yalijadiliwa.

Katika majadiliano hayo Ilisisitizwa mabaraza mawili yafanye kazi kwa karibu ili kusadia watanzania kutumia kiswahili kwa ufasaha na usahihi.

Kikao hicho pia kilikubaliana wajumbe kutoka pande zote za Muungano wawe wajumbe wa Mabaraza yote mawili pi kuwepo na kiungo thabiti ili kurahisisha shughuli za uendelezaji wa lugha ya kiswahili kwa pande zote mbili.

Jambo lingine lilijadiliwa ni pamoja na Maneno mapya ya fani na kitaaluma( Istilahi) zinapoandaliwa kwa ajili ya matumizi ni vyema Mabaraza yote yashirikishwe kwa karibu na kukubaliwa kwa maelewano kutimiza malengo ya kukuza kiswahili kwa mafanikio makubwa.

Wajumbe hao pia walikubaliana kuwa uandaliwe mkutano wa vyama vya Kiswahili vya Tanzania kwa ajili ya kukimarisha Kiswahili na kuleta utangamano wa wadau wa lugha hii adhimu ya Kiswahili

DC KINONDONI AFANYA ZIARA MBEZI JUU KUKAGUA UTEKELEZAJI WA UTATUZI WA CHANGAMOTO YA UPATIKANAJI MAJI

$
0
0
Na Ripota Wetu,Michuzi TV

MKUU wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam Daniel Chongolo amefanya ziara katika Kata ya  Mbezi Juu kwa lengo la kujionea utekelezaji wa utatuzi wa changamoto ya upatikanaji wa maji kwa wananchi wa eneo hilo.

Akizungumza akiwa katika Kata hiyo leo Oktoba 8 ,2019  Chongolo amesema amefanikiwa kuona kinachoendelea kwa sasa katika kutatua changamoto ya maji kwa wananchi wa Mbezi Mtoni na maeneo yanayozunguka eneo hilo.

" Tumekubaliana na DAWASA Kawe kushughulikia changamoto hizo kwa haraka, nami baada ya wiki mbili nitarudi tena kuangalia maendeleo ya kazi ya kuwafikishia maji wananchi. Lengo la Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Jemedari wetu Rais John Magufuli ni kuhakikisha kuwa wanaKinondoni wote wanapata maji safi na salama ifikapo 2020,"amesema

Ameongeza kuwa mpaka sasa tupo zaidi ya asilimia 80 na kuongeza matanki matano yamekamilika na kila moja lina uwezo wa kihifadhi lita milioni sita." Mungu ni mwema, kwani ni hakika mama wa Kinondoni ikifika 2020 atasahau kubeba ndoo ya maji kichwani,".
 MKUU wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam Daniel Chongolo akielezwa jambo kutoka kwa mmofa wa Wafanyakazi wa DAWASA Kawe,akiwa kwenye ziara yake katika Kata ya  Mbezi Juu kwa lengo la kujionea utekelezaji wa utatuzi wa changamoto ya upatikanaji wa maji kwa wananchi wa eneo hilo.
 MKUU wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam Daniel Chongolo akimsikiliza mmoja wa Wananchi wanaoishi katika eneo hilo la Mbezi Juu kuhusu changamoto ya upatikanaji wa maji kwa Wananchi.

WAZIRI MKUU AWASILI RUANGWA KUSHIRIKI MBIO ZA MWENGE

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Lindi, Oktoba 8, 2019. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewasili wilayani Ruangwa, mkoani Lindi ili kushiriki mbio za mwenge kitaifa hapo kesho. Mwenge huo umewasili mkoani humo leo.

Akizungumza na viongozi wa kitaifa na kimkoa mara baada ya kuwasili mkoani humo, Waziri Mkuu amesema kesho ataungana na wakazi wa Ruangwa kuupokea mwenge huo. "Kesho nitaungana na wana Ruangwa ili kesho kutwa uendelee wilaya ya Nachingwea," amesema.

Waziri Mkuu ambaye ni mbunge wa jimbo la Ruangwa, amesema: "Nimeiona hamasa kubwa waliyonayo wanaLindi huu ya mapokezi ya mwenge wa uhuru lakini kikubwa zaidi ni ugeni mkubwa wa wageni akiwemo Mheshimiwa Rais, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli."

Amesema mbali ya maadhimisho ya kumaliza mbio za mwenge nchi nzima, mwaka huu Tanzania inaadhimisha kumbukumbu ya miaka 20 ya kifo cha Baba wa Taifa. 

"Tuendelee kuwahamasisha wanaLindi na Watanzania wote washiriki kwenye makongamano yanayofanyika nchini kote. Kumbukumbu ya Baba wa Taifa isaidie kuelimisha vijana wetu ambao hawajui historia ya kazi za waasisi wa Taifa letu."

"Pia walioko madarakani, watumie fursa hii. Waige na kuenzi kazi za viongozi kama Mwalimu Nyerere na pia wajenge tabia ya kujua tabia ya ulipotoka, na mahali ulipo."

Mapema, akitoa taarifa ya maandalizi ya kilele cha mbio za mwenge kwa Waziri Mkuu, Waziri wa Nchi OWM - Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama alisema mbio hizo zilianza Aprili 2, mwaka huu na leo zimeingia Lindi ambao ni mkoa wa 31.

Alisema hadi kufikia tarehe 14, ambayo ni siku ya kilele utakuwa umepita katika Halmashauri 195 za nchi mzima. "Katika kipindi hicho chote, vijana wetu sita ambao ni wakimbiza mwenge, walizindua miradi ambayo wameridhika nayo na ile yenye dosari, hawakusita kuikemea," alisema. 

Alisema makongamano mbalimbali yameandaliwa ili kuenzi kifo cha Baba wa Taifa ambaye Oktoba 14, atatimiza miaka 20. Pia vijana 88 ambao walipanda mlima Kilimanjaro ikiwa ni sehemu ya kumbukumbu hizo watashiriki sherehe hizo mjini Lndi.

RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA BARABARA YA SUMBAWANGA –KANAZI KM 75 PIA AFUNGUA MIRADI YA MAENDELEO NKASI MKOANI RUKWA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe pamoja na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaack Kamwelwe kuashiria ufunguzi wa barabara ya Sumbawanga-Kanazi km 75 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami katika sherehe zilizofanyika Kanazi mkoani Rukwa.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Kanazi mara baada ya kufungua barabara ya Sumbawanga-Kanazi km 75 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami katika sherehe zilizofanyika Kanazi mkoani Rukwa. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli watano kutoka kulia walioshika utepe, Wabunge wa mkoa wa Rukwa, Kamati ya Miundombinu, Mawaziri, akakata utepe kufungua barabara ya Sumbawanga-Kanazi km 75 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami katika sherehe zilizofanyika Kanazi mkoani Rukwa. 
Sehemu ya Barabara ya Sumbawanga-Kanazi km 75 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami kama inavyoonekana.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua moja ya chumba cha hospitali ya Wilaya ya Nkasi mara baada ya kuweka jiwe la msingi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gril la dirisha la moja ya chumba  cha hospitali ya Wilaya ya Nkasi mara baada ya kuweka jiwe la msingi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifungua kituo cha Afya cha Nkomolo Nkasi mkoani Rukwa.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, Waziri wa Tamisemi Selemani Jafo, Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugora, Mbunge wa Nkasi Ally Keissy, akikata utepe kuashiria ufunguzi kituo cha Afya cha Nkomolo Nkasi mkoani Rukwa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mbunge wa Nkasi Ally Keissy mara baada ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli, wakiangalia zoezi la uandikishaji la wapiga kura wa Viongozi wa Serikali za mitaa Nkasi mkoani Rukwa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na mwanachi wa Nkasi Albina Kasanya (74) ambaye alikuwa amemaliza kujiandikisha katika kituo cha Hospitali ya Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari wa Nkasi waliokuwa pembezoni mwa majengo ya hospitali ya Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa. 
Sehemu ya Majengo ya Hospitali ya Wilaya ya Nkasi ambayo ipo katika hatua za mwisho kukamilika Nkasi mkoani Rukwa.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Bi Paskalia Mikael mara baada ya kusimama katika kijiji cha Chala mkoani Rukwa wakati akielekea Nkasi.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanachi wa Chala mara baada ya kuwasili kijijini hapo.
Wanafunzi wa Kasu Sekondary Wakishangilia mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwasili katika kijiji hicho.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanachi wa Kasu mkoani Rukwa. PICHA NA IKULU

VODACOM YATOA MSAADA WA KOMPYUTA ZILIZOUNGANISHWA KWENYE MTANDAO WA INTANETI KWA SHULE ZA MKOA WA SIMIYU

$
0
0

Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Foundation, Rosalynn Mworia akimwelekeza Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye jinsi mfumo wa Instant School unavyofanya kazi, tumetoa Kompyuta mpakato 20, Router 10 na uunganishaji Inteneti kwa mwaka mzima kwa shule kumi mkoani Simiyu.
Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Foundation, Rosalynn Mworia akizungumza na wageni waliohudhuria kwenye sherehe ya makabidhiano ya Kompyuta mpakato 20, Router 10 na uunganishaji Inteneti kwa mwaka mzima kwa shule kumi mkoani Simiyu. 

………………………….


Hii ni sehemu ya ajenda ya Vodacom ya kusaidia ukuwaji wa elimu kwa kupitia mfumo wa kidigitali nchini Tanzania.

8 Oktoba 2019, Simiyu. Kampuni inayoongoza ya Mawasiliano ya Vodacom PLC nchini Tanzania imetoa msaada wa kompyuta na kipanga njia (Router) zenye thamani ya zaidi ya TZS milioni 48 pamoja na kuunganisha kwenye mtandao wa intaneti kwa shule kumi katika mkoa wa Simiyu kama sehemu ya mpango wake kusaidia ukuwaji wa sekta ya elimu.

Programu hii ni ushirikiano wa pamoja na Mfuko wa Huduma ya Mawasiliano ya (UCSAF) yenye lengo la kushinikiza ujumuishaji wa kusoma kwa mfumo wa kidigitali katika shule Tanzania. Kupitia ushirika huu shule 300 haswa vijijini zitapokea kompyuta na kuunganishiwa mtandao intaneti.

Akiongea katika shule ya Sekondari ya Simiyu mkoani Simiyu, Naibu Waziri wa Kazi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi, Atashasta Nditiye alisema mchango wa kompyuta unaenda mbali katika kuunga mkono agizo la serikali la kukuza maendeleo ya kijamii vijijini na mijini Tanzania kupitia mfumo wa mawasiliano.

“Vodacom imekuwa mshirika wa serikali katika maendeleo. Nina furahi kuona ushirika huu katika utekelezaji wa mradi wa serikali wa kuunganishwa kwa shule za uma nchini katika mfumo wa kidigitali. Tunashukuru sana kwa mchango huu na tunataka kampuni zingine kuiga zoezi hili katika kusaidia sekta ya elimu.”

Mkurugenzi wa Taasisi ya Vodacom Foundation, Rosalynn Mworia alisema mpango huo ni sehemu ya ajenda ya kukuza mafunzo bora nchini Tanzania ambao unaelekea kufanikiwa kwa mipango ya maendeleo ya kimataifa. Kompyuta hizo pia zitawezesha shule hizo kuunganishwa mfumo wa upatikanaji wa elimu kwa njia ya kidigitali kupitia mtandao wa Vodacom.

“Tunafurahi kusaidia sekta ya elimu kama sehemu ya mpango wetu wa uwekezaji wa kijamii. Tumeshirikiana na serikali kuhakikisha kuwa hakuna mtu anayesalia katika utimiaji wa mfumo wa kidigitali. Mbali na uchangiaji wa kompyuta, pia tunasaidia kila shule na kuunganishwa kwenye mtandao wa intaneti bure”. Mworia alisema.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa UCSAF Justina Mashiba alisema, “Tunajivunia kufanya kazi na Vodacom kuhakikisha mpango wetu unafanikiwa kwa kuunganisha shule zote za uma na upatikanaji wa mtandao ili kutumia kikamilifu vifaa vya teknolojia ya habari na mawasiliano”.

“Mchango huu ni kusaidia kazi yetu ya kuhakikisha huduma za mawasiliano zinapatikana kila mahali haswa katika jamii za pembezoni”.Hafla hiyo ni sehemu ya awamu ya kwanza wa michango ya kompyuta inayotolewa na Vodacom Foundation na UCSAF kwa shule za uma nchini.

Vodacom imekuwa ikishiriki katika kusaidia maendeleo ya teknolojia ya mawasiliano ya habari shuleni kupitia mpango wake wa shule nzuri ambapo madawati 75 na kompyuta zilitolewa katika shule za sekondari ya Kambangwa, Makumbusho, Mtakuja pamoja na shule ya sekondari ya Kinyerezi.

DKT. KIJAJI AIPA TRA SIKU 75 KUANDAA ORODHA KAMILI YA WALIPAKODI, MAJENGO NA MABANGO

$
0
0
Na Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, ameipa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA miezi miwili na nusu hadi ifikapo Disemba 31 mwaka 2019, kuandaa na kuwasilisha wizarani orodha ya walipakodi, idadi ya majengo na mabango yote yaliyoko katika mkoa wa Dar es Salaam ili kupata takwimu sahihi za idadi ya walipakodi. 

Dkt. Kijaji ameyasema hayo Jijini Dar es Salaam alipofanya ziara ya kikazi katika Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, Mkoa wa Kikodi wa Temeke ili kukagua utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka hayo ili kubaini fursa na changamoto za masuala ya ukusanyaji kodi.

Amesema kuwa pamoja na Mamlaka hiyo kufanya vizuri katika makusanyo ya mapato Mwezi Septemba, 2019, ambapo kiasi cha shilingi trilioni 1.78 kimekusanywa, kiasi hicho bado ni kidogo ikilinganishwa na mwamko wa wananchi uliopo hivi sasa katika kulipa kodi.

Aidha Mhe. Kijaji amerejea kuitaka TRA kuwasilisha kwake takwimu ya ongezeko la walipa kodi lililotokana na zoezi la kugawa vitambulisho vya wajasiriamali nchini kwa kuwa lengo la Mhe. Rais Dkt. John Magufuli kugawa vitambulisho hivyo lilikuwa ni kuongeza wigo wa walipa kodi watakao kuwa wanafuzu kwa kuongeza mitaji yao, hivyo ni vyema kujua idadi yao kamili na mahali walipo.

Kwa upande wa kodi ya majengo, Dkt. Kijaji ameitaka Mamalaka ya Mapato Tanzania kuhakikisha inapata orodha ya nyumba zote nchini kwa kuorodhesha wamiliki wa nyumba hizo na mawasiliano yao na kisha kuandaa kanzidata itakayosaidia kurahisisha ukusanyaji wa kodi hiyo. 

“Ili kuongeza mapato yanayotokana na kodi ya majengo ni lazima TRA wafanye kazi usiku na mchana kuhakikisha kanzidata hiyo inakamilika ambayo itatumika kuwakumbusha walipa kodi kupitia ujumbe mfupi wa simu ambapo itasaidia katika ukusanyaji wa kodi hiyo kama ilivyo kwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi inapowakumbusha wananchi kulipa kodi a ardhi kupitia simu zao” Alisema Dkt. Kijaji

“Nataka pia mkague watumiaji wote wa mashine za utoaji risiti za kieletroniki (EFD) kwa wafanyabiashara wa Temeke ili kuhakikisha kila anayeuza anatoa risiti na anayenunua anadai risiti na kwa kufanya hivyo itasaidia kuongeza makusanyo ili Taifa liendelee kujitegemea kimapato” alisisitiza Dkt. Kijaji 

Awali akimkaribisha Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Mkoa wa Kikodi wa Temeke, Bw. Paul Walalaze, alisema mkoa wake una idadi ya walipakodi 437,539 na kwamba katika mwaka 2018/19, mkoa wake ulipanga kukusanya shilingi bilioni 395 na kufanikiwa kukusanya sh. bilioni 328.5 sawa na asilimia 85 ya lengo.

“Tumekusanya pia kodi ya majengo sh. bilioni 1.4 kati ya malengo ya kukusanya bilioni 1.6, kodi ya mabango sh. bilioni 2.2 kati ya lengo la kukusanya sh. bilioni 2.3 sawa na mafanikio ya asilimia kati ya 87 na asilimia 95" aliongeza Bw. Walalaze.

Kwa upande wake Afisa Mwandamizi Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Bw. Hamisi Lupenja, amemhakikishia Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Kijaji kwamba watatekeleza maelekezo yote yaliyotolewa ili kuboresha ukusanyaji wa mapato ya Serikali ikiwemo kutoa elimu kwa walipakodi.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), katikati, akikagua kanzidata ya walipakodi wa majengo na mabango, katika Ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, mkoa wa Kikodi wa Temeke Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Bi. Hellen Gibbe Msimamizi Msaidizi wa Kodi na kushoto ni Msimamizi wa Kitengo cha Mapato yasiyo ya Kodi, wote kutoka TRA-Temeke.
 Mkuu wa masuala ya usimamizi wa Data na Ukaguzi wa ritani Bw. Pius Kunjumu (aliyesimama nyuma) akitoa ufafanuzi wa jambo kwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango (Hayupo pichani) alipofanya ziara katika Ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, Mkoa wa Kikodi wa Temeke, Jijini Dar es Salaam, kusikiliza fursa na changamoto ya utendaji kazi wa Mamlaka hayo ili kuongeza ufanisi katika ukusanyaji kodi.
 Meneja Msaidizi wa Kitengo cha Madeni wa TRA-Temeke, Bw. Nicholaus Migera, (aliyesimama) akitoa ufafanuzi wa jambo kwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango (Hayupo pichani) alipofanya ziara katika Ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA Mkoa wa Kikodi wa Temeke, Jijini Dar es Salaam, kusikiliza fursa na changamoto ya utendaji kazi wa Mamlaka hayo ili kuongeza ufanisi katika ukusanyaji kodi.
 Afisa Mwandamizi Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Bw. Hamisi Lupenja akifafanua jambo mbele ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (hayupo pichani) alipofanya ziara ya kikazi katika Ofisi hizo za TRA Mkoa wa Kikodi wa Temeke Jijini Dar es Salaam.
 Afisa Mwandamizi Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Bw. Hamisi Lupenja (kulia) na Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, Mkoa wa Kikodi wa Temeke, Jijini Dar es Salaam. Bw. Paul Walalaze, wakisikiliza hoja za watumishi wa TRA-Temeke, Jijini Dar es Salaam wakati Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (hayupo pichani) alipofanya ziara ya kikazi katika Ofisi hizo.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akisikiliza kwa makini hoja mbalimbali za watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Ofisi ya Temeke (hawapo pichani), alipotembelea Ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, Mkoa wa Kikodi wa Temeke, Jijini Dar es Salaam
Katibu wa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), Bw. Moses Dulle, akitoa ufafanuzi wa baadhi ya mambo wakati Dkt. Kijaji aliofanya ziara ya kikazi kukagua utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA, Mkoa wa Kikodi wa Temeke, Jijini Dar es Salaam
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)

WAZIRI MKUU ASISITIZA MSHIKAMANO KWA WATANZANIA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea Mwenge kutoka kwa mmoja wa wakimbiaza Mwenge wa Uhuru,Nkwimba Madirisha Nyangogo wakati aliposhiriki katika mapokezi ya Mwenge wa Uhuru wilayani Ruangwa yaliyofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi ya Nangumbu, Oktoba 9, 2019.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea Mwenge kutoka kwa mmoja wa wakimbiaza Mwenge wa Uhuru, Nkwimba Madirisha Nyangogo wakati aliposhiriki katika mapokezi ya Mwenge wa Uhuru wilayani Ruangwa yaliyofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi ya Nangumbu, Oktoba 9, 2019. Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Ruangwa, Hashim Mgandilwa.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikimbiza Mwenge wa Uhuru wakati ulipopokelewa kijijini kwake Nandagala wilayani Ruangwa, Oktoba 9, 2019. Kushoto ni Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru, Mzee Ali Mkongea.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru wakati mwenge huo ulipopokelea wilayani Ruangwa katika uwanja wa Shule ya Msingi ya Nangumbu, Oktoba 9, 2019.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa ameubeba Mwenge wa Uhuru wakati aliposhiriki katika mapokezi ya Mwenge huo wilayani Ruangwa yaliyofanyika katika uwanja wa Shule ya Misngi ya Nangumbu, Oktoba 9, 2019. Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Ruangwa, Hashim Mgandilwa na kushoto ni Kiongozi wa Mbio za Mwenge, Mzee Ali Mkongea.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wakimbiza Mwenge wa Uhuru wakati aliposhiriki katika mapokezi ya Mwenge huo wilayani Ruangwa yaliyofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi ya Nangumbu wilayani humo, Oktoba 9, 2019. Wa tatu kushoto ni Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru, Mzee Ali Mkongea na wa nne kulia ni Mkuu wa wilaya ya Ruangwa, Hashim Mgandilwa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru, Mzee Ali Mkongea wakati alipozungumza katika mapokezi ya Mwenge wa Uhuru wilayani Ruangwa yaliyofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi ya Nangumbu wilayani humo, Oktoba 9, 2019. Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Ruangwa, Hashim, Mgandilwa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru, Mzee Ali Mkongea wakati mwenge huo ulipopokelewa wilayani Ruangwa katika uwanja wa Shule ya Msingi ya Nangumbu, Oktoba 9, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati aliposhiriki. Katika mapokezi ya Mwenge wa Uhuru wilayani Ruangwa yaliyofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi ya Nangumbu wilayani humo, Oktoba 9, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

*Ashiriki mbio za mwenge kijijini kwao

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Watanzania waendelee kushikamana na wazingatie ujumbe wa mbio za mwenge za mwaka huu unaohimiza umuhimu wa maji, uchaguzi wa Serikali za mitaa, vita dhidi ya rushwa, malaria, UKIMWI na dawa za kulevya.

Ametoa wito huo leo asubuhi (Jumatano, Oktoba 9, 2019) wakati akizungumza na viongozi wa Halmashauri za Lindi na Ruangwa na wananchi wa kijiji cha Nangumbu kwenye uwanja wa shule ya msingi Nangumbu ambako mwenge huo ulipokelewa saa 1:44 asubuhi ukitokea Nyangao wilayani Lindi.

Waziri Mkuu ambaye ni mbunge wa jimbo la Ruangwa, aliwasili wilayani Ruangwa jana jioni, ili kushiriki mbio za mwenge. Kesho (Alhamisi, Oktoba 10) mwenge huo utaelekea Nachingwea, ambapo Ijumaa (Oktoba 11) utaenda Liwale, Jumamosi (Oktoba 12) utaenda Kilwa na Jumapili (Oktoba 13) utakuwa Manispaa ya Lindi ambako utahitimisha mbio hizo na kuzimwa Oktoba 14, mwaka huu.

Waziri Mkuu amewataka wananchi wote wajiandikishe kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa ili Tanzania iweze kupata viongozi bora. “Tuitikie kaulimbiu ya mwaka huu kwa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Hapa Ruangwa, hadi jana jioni watu 28,000 walikuwa tayari wamejiandikisha. Tukachague viongozi wachapakazi na waadilifu watakaoleta maendeleo kwa nchi yetu,” amesisitiza.

Mapema, akizungumza baada ya kupokea mwenge huo saa 2:21 asubuhi, Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Bw. Hashim Mgandilwa alisema utakimbizwa kwenye kata saba na vijiji 17 ambapo miradi mitatu mikubwa yenye thamani ya sh. bilioni 2.9 itazinduliwa.

Katika kijiji cha Nangumbu, mwenge ulizindua mradi wa mabweni na klabu ya kupiga vita rushwa kwenye shule ye sekondari ya Hawa Mchopa. Ukiwa njiani, mwenge huo ulipitishwa kijiji cha Nandagala ambako Waziri Mkuu alizaliwa. Pia aliupokea na kuukimbiza kidogo akiwa na wanakijiji wenzake, kisha mwenge huo ukaendelea kukimbizwa kuelekea kata ya Likunja ambako watazindua mradi wa maji wa Kitandi. Pia mwenge huo utazindua mradi wa barabara ya lami kwenye kata ya Nachingwea, iliyoko Ruangwa mjini.

Akizungumza kabla ya kuanza kwa mbio za mwenge wilayani Ruangwa, kiongozi wa mbio za mwenge Kitaifa, Bw. Mzee Ali Mkongea alimshukuru Waziri Mkuu kwa kujumuika na wananchi kushiriki ratiba ya mapokezi ya mwenge wilayani humo.

Alisema Serikali ya awamu ya tano, ndani ya miaka mitatu (2015-2018) imekamilisha kwa wakati miradi 124 ya maji ambapo aliitaja baadhi yake kuwa ni miradi mikubwa ya Chalinze, Bagamoyo, Arusha, Tabora na Musoma. Pia alisema Serikali imeendelea na uchimbaji wa visima virefu na vifupi vya maji kwa gharama ya sh. bilioni 14.

“Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzana kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar zimeingia mkataba na Serikali ya India wa dola za Marekani milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maji kwenye miji 28 ya Tanzania. Lakini kuna changamoto nyingi kwenye miradi hii ikiwemo matumizi mabaya ya fedha za umma na wakandarasi kujenga baadhi ya miradi chini ya kiwango.”

“Pia kumekuwa na shughuli za kibinadamu karibu na vyanzo vya maji. Wananchi tusaidiane kuvilinda vyanzo hivi kwa sababu kazi ya kuvitunza si ya Serikali peke yake bali inaanza na mimi na wewe,” alisema.

Aliwasihi wananchi hao wajitokeze kwa wingi kujiandikisha kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa ili waweze kuchagua viongozi wazalendo ambao wana calibre ya Rais, Dkt. John Pombe Magufuli.

Akitoa takwimu za ugonjwa wa malaria nchini, Bw. Mkongea alisema mkoa wa Kigoma unaongoza kwa maambukizi ya ugonjwa huo kwa asilimia 24, ukifuatiwa na Geita (asilimia 17), Mtwara (asilimia 15) na Lindi wenye asilimia 12.  

“Niwasihi wananchi tumieni vyandarua vinavyotolewa bure na Serikali hasa akinamama wajawazito na watoto walio na umri chini ya miaka mitano. Kuna maeneo tumekuta baadhi ya watu wakivitumia kuvulia samaki na kufungia bustani ili kuku wasiingie. Haya si matumizi yake hata kidogo,” alisisitiza.

COCA-COLA KWANZA YADHAMINI MATEMBEZI YA HISANI

$
0
0


 Meneja Biashara na Masoko wa Cocacola Kwanza, Wahida Mbaraka, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuhusu matembezi ya hisani ya Dasani Charity Walk kwa ajili ya kuchangia akina mama wanaosumbuliwa na Saratani ya Matiti yatakayofanyika Dar es Salaam Oktoba 14.Kulia ni Mratibi Miradi wa Asasi ya Saratani ya Matiti,Kisa Mwakatobe.


Kampuni ya vinywaji baridi ya Coca-Cola Kwanza inadhamini kwa mara ya nne mfululizo matembezi ya kilomita 5 yenye lengo la kukusanya zaidi ya Tsh 100m kuwasaidia kina mama wenye saratani ya matiti nchini Tanzania. Matembezi hayo yatafanyika Jumatatu 14/10/2019 katika viwanja vya The Green (zamani uwanja wa Farasi).

Fedha nyingine itatumika kuelimisha vijana mashuleni na kusaidia ujenzi wa hosteli ambayo itakuwa inatumiwa na akina mama wanaokuja jijini Dar es Salaam kufuatilia matibabu. Matembezi hayo vile vile yatajumuisha mbio za kilomita 9.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam 9/10/2019 meneja masoko na biashara wa Coca-Cola Kwanza Wahida Mbaraka amesema kampuni yake inaona fahari kutumia sehemu ya faida yake kudhamini matembezi hayo ya hisani kusaidia kuboresha maisha ya akina mama nchini.

Mashindano hayo ambayo yanaandaliwa na asasi ya saratani Tanzania (TBCF) yanatarajia kuwaleta pamoja washiriki zaidi ya elfu mbili mia tano na mgeni rasmi atakuwa John Ulanga, Mkurugenzi Mkazi wa chapa ya Afrika Mashariki.

’Siku hizi saratani ya matiti siyo tishio kwa wanawake peke yake bali hata kwa wanaume vile vile. Napenda kuchukua nafasi hii kuwaomba wanaume kujitokeza kupima ili kuona kama wana dalili za saratani ya matiti au la”, alisema Mbaraka.

Akizungumza katika mkutano huo, mratibu wa programu wa TBCF Kisa Mwakatobe amesema watatumia matembezi hayo ya hisani mbali na mazoezi ya mwili pia yatatoa elimu jamii kuhusu saratani ya matiti na haki zinazohusiana na matibabu na maisha kwa ujumla.Amesisitiza umuhimu wa kupima afya mara kwa mara kwani ugonjwa huo ukigundulika katika hatua za awali unaweza kutibiwa kirahisi.

RC MAKONDA AZINDUA MFUMO WA KUWEZESHA WANANCHI KUTOA MALALAMIKO DHIDI YA WATENDAJI WASIOTEKELEZA MAJUKUMU YAO KWA KUTUMIA SIMU ZA MKONONI.

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo October 09 amezindua Mfumo wa kuwawezesha wananchi wa Mkoa huo kuwasilisha kero na changamoto walizonazo kwa kutumia simu ya mkononi au Computer na ujumbe wao kuwafikia watendaji kwa haraka na kupatiwa majibu ndani ya muda mfupi jambo litakalosaidia kuokoa Muda na gharama za usafiri.

RC Makonda amesema ameamua kuanzisha mfumo huo baada ya kubaini kuwa wananchi wengi wamekuwa wakifika kwenye ofisi za umma na kupewa majibu ya “Njoo Kesho” pasipokujua kuwa wamepoteza muda na nauli zao kufuata huduma.

Aidha RC Makonda amebainisha kuwa mfumo huo utakuwa ukipokea taarifa za malalamiko ya Watendaji wasiowajibika kuanzia ngazi ya Mtaa, Kata, Wilaya hadi Mkoa na taarifa zitawafikia Viongozi wote kuanzia RC Makonda mwenyewe, Mkuu wa Wilaya husika, Mkurugenzi, Katibu tawala na Mkuu wa idara.

Hata RC Makonda amewahimiza wananchi kutumia mfumo huo kueleza kero zote zinazowakabili ikiwemo Afya, Barabara, Elimu, Maji, Umeme, Miradi inayokwama pamoja na kutoa taarifa pindi wanapobaini uhalifu kwenye mtaa.

Jinsi kuwasilisha ujumbe andika neno DSM kisha eleza changamoto zako kisha tuma kwenye namba 11000 au ingia kwenye Website www.malalamiko.dsm.go.tz na ujumbe wako utapokelewa mara moja na kupewa mrejesho.

MAADHIMISHO YA MIAKA 145 YA SIKU YA POSTA DUNIANI, SHIRIKA LA POSTA LAKABIDHI ZAWADI KWA WASHINDI WA BARUA KIMATAIFA NCHINI

$
0
0
Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu (Mawasiliano), Dkt. Jim Yonazi (katikati mbele waliokaa), akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa shindano hilo, walimu, wazazi pamoja na wageni wengine waliohudhuria kwenye hafla hiyo.

Mgeni rasmi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano), Dkt. Jim Yonazi, akimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza wa shindano la uandishi wa barua Kimataifa nchini, Joan John Erasto (wapili kushoto), wa Shule ya Sekondari Binza, mkoani Simiyu. Hafla ya maadhimisho ya miaka 145 ya Siku ya Posta Duniani imefanyika jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni mwalimu wa shule hiyo, Japhet Kilela.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Elia Madulesi akitoa maelezo katika hafla hiyo. Kulia ni Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano), Dkt. Jim Yonazi. Wapili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika, Dkt. Haruni Kondo.

Baadhi ya Maofisa wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), wakifuatilia hotuba mbalimbali katika maadhimisho hayo. 

Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika, Mwanaisha Said, akizungumza katika hafla ya maadhimisho hayo. 

Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu-Mawasiliano, Dkt. Jim Yonazi akimkabidhi zawadi mshindi wa tatu wa uandishi wa barua, Hasnein Rizwan kutoka shule ya Sekondari ya Almuntazir Boys Seminary ya jijini Dar es Salaam.

Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu (Mawasiliano), Dkt. Jim Yonazi akimkabidhi cheti mshindi wa pili wa shindano hilo, Grace Kahimba wa Shule ya Msingi ya St. Ann’s ya Morogoro. Kulia ni Kaimu Postamasta Mkuu Mwanaisha Said na wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika, Dkt. Haruni Kondo. 

Mshindi wa kwanza nchini katika shindano la Kimataifa la uandishi wa barua, Joan John Erasto, akiisoma barua yake iliyompatia ushindi wakati wa hafla hiyo.

Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania, Dkt. Haruni Kondo akizungumza katika maadhimisho hayo, leo jijini.Kaimu Postamasta Mkuu Mwanaisha Said, akimkaribisha Mgeni rasmi, Naibu Katibu Mkuu (Mawasiliano), Dkt. Jim Yonazi (katikati), kuzungumza katika hafla hayo.





Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu (Mawasiliano), Dkt. Yonazi akizungumza katika maadhimisho hayo.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Uwakala wa Usafiri wa ndege nchini (MAUFU), Maua Katandula, ambao ni mmoja wa wadhamini wa shindano la kimataifa la Uandishi wa Barua nchini, akizungumza katika maadhimisho hayo.

SHINDANO LA MISS UNIVERSE TANZANIA LARUDI KWA KISHINDO

$
0
0

Baada ya kimya cha mwaka mmoja, kampuni ya Compass Communication imeandaa tena mwaka huu, shindano la Miss Universe Tanzania.

Baada ya kufanya usaili na warembo takriban 90 kutoka mikoa tofauti nchini, shindano hili la kitaifa la mwaka huu linahusisha warembo 10 kutoka mikoa ya Mwanza, Arusha, Dodoma na Dar es salaam linatarajiwa kufanyika tarehe 12 mwezi wa kumi katika Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam kuanzia saa 1 jioni.

Katika miaka ya nyuma shindano hili limeweza kuibua vipaji vya wengi na wameendelea kufanya vyema katika ulimwengu wa urembo na kuipeperusha vyema bendera ya taifa letu. Baadhi yao ni pamoja na Flaviana Matata, Nelly Kamwelu pamoja na Hellen Dausen.

“Urembo ni sanaa na urembo ni kazi, na ndio maana sisi kama Compass Communications tumeona fursa na kuamua kuendeleza vipaji vya wasichana wengi wenye ndoto na wenye kuamini kuzifikia kupitia tasnia hii ya urembo” ameeleza mkurugenzi wa kitaifa wa shindano hili, Maria Sarungi Tsehai

Pia kwa Mwaka 2019 mashindano haya yanaadhimisha miaka 12 tangu kuanza kufanyika hapa nchini mwaka 2007. Kama ilivyo adha mshindi wa Miss Universe hapa nchini ataenda kuiwakilisha nchi katika mashindano ya dunia hapo baadae mwaka huu.

Maria Sarungi Tsehai ameeleza kuwa mafanikio haya yametokana na ushirikiano mzuri na wadau wote wa tasnia,. “Tunaishukuru sana Serikali, Wizara husika pamoja na Baraza la Sanaa (BASATA) kwa kutupatia ushirikiano kwa miaka yote na ni matumaini yetu kuzidi kupata ushirikiano kutoka kwenu na kusongesha kwa pamoja hili gurudumu la sanaa”, ameongezea Bi Sarungi

Miss Universe kwa mwaka 2019, imedhaminiwa na Precision Air, Serena Hotel, Sea Cliff Luxury apartments , Kwanza TV, Pepsi , Samaki Samaki Fish and More pamoja na Timeless Saloon.
Imetolewa, Dar es Salaam 09/October/2019

Kwa maelezo zaidi wasiliana na Saddam Khalfan
+255 712 785 161
saddam@compass-tz.com

PIA TUNAPENDA KUUTARIFU UMA KUHUSU  MABADILIKO YA VENUE KUTOKA SEA CLIFF KWENDA SERENA SABABU YA HALI YA HEWA.

KLABU YA ROTARY YA MZIZIMA DAR ES SALAAM YATOA MSAADA WA TAULO ZA KIKE

$
0
0

Rais Mstaafu wa klabu ya Rotary ya Mzizima Dar es salaam, Dkt. Emeria Mugonzibwa akizungumza na wasichana wa Shule ya Sekondari Jangwani leo jijini Dar es salaam kabla ya kukabidhi msaada wa taulo za kike uliotolewa na klabu ya Rotary ya Mzizima Dar es salaam kwa wanafunzi wa kike wenye mahitaji maalum wa Shule hiyo.
Rais Mstaafu wa klabu ya Rotary ya Mzizima Dar es salaam, Dkt. Emeria Mugonzibwa akikabidhi msaada wa taulo za kike uliotolewa na klabu ya Rotary ya Mzizima Dar es salaam kwa wanafunzi wa kike wenye mahitaji maalum wa Shule Sekondari Jangwani leo jijini Dar es Salaam.

WALENGWA WA TASAF WILAYANI RUNGWE WAISHUKURU SERIKALI KWA KUWAKUMBUKA.

$
0
0
Na Estom Sanga- RUNGWE. 

Kamati ya Uongozi ya Taifa ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii –TASAF imefanya ziara katika Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya kukagua miradi inayotekelezwa na Mfuko huo na kuonyesha kuridhishwa kwake na mafanikio makubwa yaliyopatikana kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini . 

Kabla ya kutembelea halmashauri ya Wilaya ya Rungwe, Wajumbe wa Kamati hiyo ya Uongozi ya Taifa ya TASAF,walikutana na Mkuu wa mkoa wa Mbeya ,Bw. Albert Chalamila ambaye amewaeleza wajumbe hao kuwa utekelezaji wa miradi ya TASAF mkoani humo imeleta hamasa kubwa kwa wananchi kuuchukia umaskini kwa kufanyakazi kwa bidii. 

Mkuu huyo wa mkoa wa Mbeya amesema licha ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kutotekelezwa katika baadhi ya maeneo ya mkoa huo,mafanikio yake yamesababisha wananchi ambao hawajafikiwa na huduma za Mpango huo kuomba wajumuishwe ili nao waweze kunufaika na utaratibu huo wa serikali wa kuzifikia kaya maskini. 

Aidha Bw. Chalamila amesema sekta za elimu, afya,na shughuli za uzalishaji mali vimepata msukumo mkubwa kwa kaya za Walengwa wa TASAF ambao kabla ya kuanza kwa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini waliishi katika hali ya unyonge uliosababishwa na umaskini wa kipato jambo ambalo amesema limepungua kwa kiwango kikubwa baada ya Serikali kupitia TASAF kuanza kutekeleza Mpango huo. 

Wakiwa Katika halmashauri ya wilaya Rungwe,Wajumbe wa Kamati hiyo ya Uongozi ya taifa ya TASAF wamepata fursa ya kukutana na baadhi ya Wananchi wanaonufaika na huduma za Mfuko huo ambao wameonyesha baadhi ya mafanikio waliyopata hususani katika sekta ya uboreshaji wa makazi, elimu,afya na huduma ya maji ambayo wamesema umewasaidia kuboresha maisha yao na kuwapa hamasa kubwa ya kukabiliana na umaskini. 

Akizungumza kwa nyakati tofauti katika ziara hiyo,Kaimu Mwenyekiti wa kamati hiyo Dr. Naftal Ng’ondi amewahimiza walengwa wa TASAF kutumia vizuri fursa hiyo ili waweze kuunga mkono jitihada za serikali za kuondoa kero ya umaskini miongoni mwao,kwani amesema mkakati huo unapaswa kuwa wa muda ili waweze kupisha wananchi wengine waweze kunufaika nao. 

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Bw. Ladislaus Mwamanga akijibu hoja ambayo imekuwa ikiibuliwa na wananchi katika maeneo ambayo hayakujumuishwa kwenye huduma za Mpango, amesema serikali imeamua katika sehemu ya pili ya Mpango wa kunusuru Kaya Maskini maeneo yote nchini yajumuishwe kwenye huduma za Mpango huo. 

Bwana Mwamanga amesema uamuzi huo wa serikali ambao unaweka msisitizo kwa Wananchi watakaojumuishwa kwenye Mpango kufanyakazi za maendeleo watakazozibua kwenye maeneo yao na kisha kulipwa ujira kwa kazi hizo jambo ambalo amesema litachangia kuboresha maisha yao. Hata hivyo amefafanua kuwa Walengwa ambao ni wazee , wagongwa wa muda mrefu, watoto yatima na walemavu ambao hawana msaada wataendelea kupata huduma za uhawilishaji fedha ili waweze kujikimu .
 Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya Taifa ya TASAF wakipata maelezo ya namna chanzo cha maji kilichojengwa katika eneo la Bulyaga Juu ,nje kidogo ya mji wa Tukuyu kilivyojengwa kupitia utaratibu wa Ajira ya Muda unaotekelezwa na Serikali kupitia TASAF.Maji hayo hayakauki katika kipindi chote cha mwaka.
 Mmoja wa Wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya Taifa ya TASAF,Dkt. Naftal Ng’ondi (mwenye kote cheupe) akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa Walengwa wa TASAF katika chanzo cha maji kilichojengwa wa TASAF katika eneo la Bulyaga juu ,halmashauri ya Rungwe kwa utaratibu wa Ajira ya Muda.
 Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Ladislaus Mwamanga (aliyeinama) akigusa maji kwenye chanzo cha maji kilichojengwa na Walengwa wa TASAF katika eneo la Bulyaga juu, nje kidogo ya mji wa Tukuyu kupitia utaratibu wa Ajira ya Muda.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Bw. Albert Chalamila (aliyevaa suti ya bluu) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa kamati ya uongozi waTaifa ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii -TASAF na menejimenti ya Mfuko huo baada ya kukamilisha mazungumzo ofisini kwake. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF ,Bw. Ladislaus Mwamanga.

DODOMA YA KIJANI INAWEZEKANA - SAMIA SULUHU HASSAN

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akikagua miti iliyopandwa wakati wa kampeni ya kukijanisha Dodoma katika eneo la Mzakwe jijini Dodoma ikiwa sehemu ya ufuatiliaji wa ukuaji wa miti hiyo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Bw. Godwin Kunambi wakati wa ziara ya ukaguzi wa miti iliyopandwa wakati wa kampeni ya kukijanisha Dodoma.  Wengine katika picha ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Bw. Patrobas Katambi na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandishi Joseph Malongo
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Mwakilishi wa Wakala wa Misitu Tanzania Kanda ya Kati Bi. Teddy Yoramu  juu ukuaji wa miti iliyopandwa katika eneo la Mzakwe jijini Dodoma wakati wa kampeni ya Kuifanya Dodoma ya Kijani.

Lulu Mussa na Monica Sapanjo

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema azma ya kuifanya Dodoma kuwa ya Kijani iko pale pale.
Hayo yamesemwa leo mara baada ya kutembelea shamba la miti lililopo katika eneo la Mzakwe katika Kambi ya Jeshi la Makutupora Jijini Dodoma, ikiwa ni ufuatiliaji wa Kampeni aliyozindua mwaka 2017 ya kuifanya Dodoma kuwa ya kijani.

Makamu wa Rais ameupongeza uongozi wa Kambi ya Jeshi ya Makutupora, Wakala wa Misitu Tanzania na Watendaji wa Ofisi yake kwa kuhakikisha miti iliyopandwa mwezi Desemba 2017 inastawi.

“Vitabu vya dini vinasema Moja kati ya sadaka endelevu ni kupanda miti, miti hii imekuwa na kustawi kwasababu ya jitihada zenu za kuimwagilia na kuitunza, msikate tamaa, endeleeni na kazi hii njema ambayo matokeo yake yanaonekana ikiwa ni pamoja na kuimarika kwa mifumo ya hali ya hewa ambayo huimarisha shughuli za kilimo na maendeleo ya viwanda.” Alisisitiza Makamu wa Rais.

Nae Mkuu wa Kambi ya Jeshi ya Makutupora Luteni Kanali Festo Mbanga amesema kuwa miti 2300 ilipandwa  tarehe 21/12/2017 na kati ya hiyo miti 2076 imekuwa na kustawi ikiwa ni sawa na asilimia 90.3 ya miti yote iliyopandwa.“Katika miti iliyooteshwa awali baadhi haikuota, hivyo tumefanya jitihada za kuirudishia, tumepanda takriban miti 300 ya ziada” alisema Luteni Kanali Mbanga.

Katika hatua nyingine Makamu wa Rais ameagiza Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) kuhakikisha tafiti zinakamilika mapema kutoka katika sampuli ya udongo iliyochukuliwa ili kubaini aina ya miti inayostawi katika eneo hilo na Jiji la Dodoma kwa Ujumla.

Kampeni ya Kukijanisha Dodoma ilizinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 21/12/2017 katika eneo la Mzakwe Jijini Dodoma ambapo miti 2300 ilipandwa siku hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo, Simon Karikari asikiliza na kutatua kero za wateja wa Tigo katika wiki ya huduma kwa wateja.

$
0
0

Mkuu wa kitengo cha huduma kwa wateja (Tigo)Bi. Mwangaza Matotola -, akimkaribisha Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Mawasiliano Tigo Bw. Simon Karikari pamoja na viongozi wa idara mbalimbali katika kituo cha kisasa cha huduma kwa wateja. Tukio hilo liliambatana na ukataji wa keki.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mawasiliano TIGO Bw. Simon Karikari akimuongoza mteja katika duka la Tigo Mlimani City kukata keki ya kusherehekea wiki ya Huduma Kwa Wateja pamoja na kushiriki katika kutoa huduma kwa wateja.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo, Simon Karikari, akijibu na kutatua maswali ya wateja wa Tigo katika kituo cha cha kisasa cha huduma kwa wateja , zoezi hilo limefanyika katika wiki ya huduma kwa wateja.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo, Simon Karikari, akijibu na kutatua maswali ya wateja wa Tigo katika kituo cha cha kisasa cha huduma kwa wateja , zoezi hilo limefanyika katika wiki ya huduma kwa wateja.
Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya mawasiliano TIGO Bw. Simon Karikari ametembelea duka la Tigo Mlimani City na kupata nafasi ya kushiriki katika wiki ya huduma kwa wateja na wateja wa Tigo waliokuwa wakiendelea kupata huduma.

Benki ya NBC yatoa msaada wa madawa na vifaa tiba kwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro

$
0
0
 Meneja Uendeshaji wa Benki ya NBC  Tawi la Morogoro, Joceline Msuya (wa tatu kushoto) akizungumza wakati akikabidhi  msaada wa madawa na vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 9 kusaidia hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro pamoja na nyingine zenye uhitaji vilivyotolewa na NBC ikiwa ni sehemu ya shughuli za kuisaidia jamii za benki hiyo zinazoendelea kufanyika sehemu mbalimbali nchini. Makabidhiano hayo yalifanyika Hospitalini hapo Mkoani Morogoro jana. Kushoto kwake ni Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, Dk. Francis Semwene. Madawa hayo yamenunuliwa kutoka Bohari Kuu la Madawa Nchini (MSD)

 Meneja Uendeshaji wa Benki ya NBC Tawi la Morogoro, Joceline Msuya (wa tatu kulia), akishikana mikono na Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, Dk. Francis Semwene  wakati akimkabidhi msaada wa Madawa yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 9 kusaidia hospitali hiyo  na  nyingine zenye uhitaji vilivyotolewa na NBC ikiwa ni sehemu ya shughuli za kuisaidia jamii za benki hiyo zinazoendelea kufanyika sehemu mbalimbali nchini. Makabidhiano hayo yalifanyika Hospitalini hapo Mkoani Morogoro jana. Madawa hayo yamenunuliwa kutoka Bohari Kuu la Madawa Nchini (MSD)
 Meneja Uendeshaji wa Benki ya NBC Tawi Morogoro,  Joceline Msuya (wa nne kushoto), akimkabidhi  Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, Dk. Francis Semwene msaada wa madawa na vifaa tiba vyenye thamani zaidi ya shilingi Milioni 9 kusaidia  hospitali hiyo pamoja na nyingine zenye uhitaji vilivyotolewa na NBC ikiwa ni sehemu ya shughuli za kuisaidia jamii za benki hiyo zinazoendelea kufanyika sehemu mbalimbali nchini. Makabidhiano hayo yalifanyika hospitalini hapo, Morogoro jana. Madawa hayo yamenunuliwa kutoka Bohari Kuu la Madawa Nchini (MSD)
Meneja Mahusiano wa Benki ya NBC Tawi la Morogoro, Grace Kapesa (wa nne kushoto), akimkabidhi  Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, Dk. Francis Semwene msaada wa madawa na vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 9 kusaidia hospitali hiyo pamoja na nyingine zenye uhitaji vilivyotolewa na NBC ikiwa ni sehemu ya shughuli za kuisaidia jamii za benki hiyo zinazoendelea kufanyika sehemu mbalimbali nchini. . Madawa hayo yamenunuliwa kutoka Bohari Kuu la Madawa Nchini (MSD).

Viewing all 46343 articles
Browse latest View live




Latest Images