Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live

KAMPENI YA MNADA KWA MNADA YA TCRA YAWAFIKIA WAKAZI WA TABORA

$
0
0

Wananchi katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada Mkoani Tabora.WAKATI wa Mkoa wa Tabora na viunga vyake wamejitokeza kwa wingi katika kampeni ya Mnada kwa Mnada ambapo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikishirikiana na Kampuni ya simu, Jeshi la Polisi Kitengo cha Uhalifu Mitandaoni na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Idara ya Uhamiaji kwa ajili ya utoaji wa huduma za usajili wa laini za simu kwa kutumia vitambulisho vya kitaifa na kuhakikiwa na kampuni za simu kwa kuweka alama za vidole kwa laini za simu.


Kampeni tangu imeanzishwa imekwenda katika Mikoa 15 lengo kuu ni nchi nzima kufiwa na Kampeni hiyo.

Mwakilishi wa Mkuu wa Kanda ya Kati wa TCRA Joseph Kavishe amesema ni fursa kwa wananchi wa Mkoa wa Tabora katika Uwanja wa Chipukizi na viunga vyake kupata huduma kutokana na kuwa na mnyororo wadau wa mawasiliano. 

Kavishe amesema kuwa Mnada kwa Mnada TCRA ilianzisha ili kutoa fursa ya Wananchi kuhudumiwa hasa wakati huu usajili wa laini za simu kwa alama za vidole.

Aidha amesema Kampeni hiyo ni kuimarisha ulinzi katika mawasiliano ya simu pamoja kufanya mawasiliano kuwa salama katika nchi.

Amesema kuwa kampeni ya Mnada kwa Mnada ni kwa ajili ya kutoa elimu ya mawasiliano kwa kushirikiana na wadau katika kujibu changamoto wanazokutanazo katika utumiaji wa mawasiliano nchini.

Kavishe amesema kuwa wananchi wasio kuwa na Vitambulisho vya NIDA wahakikishe wanapata katika usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole na huduma nyinginezo za Mawasiliano hayo.

Amesema kuna watu wengine wanatumia mawasiliano ya simu bila kujua ambapo Jeshi Polisi lipo katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada ili kuwaelewesha makosa ya jinai ya matumizi ya simu.

Aidha amesema Kampeni hiyo ni endelevu katika kuwafikia ikiwa kuhakikisha kila mwananchi anajisajili laini yake kwa alama za vidole kwa kutumia kitambulisho cha taifa cha NIDA.

Kavishe amesema kuwa TCRA iko kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi ili mtumie Mawasiliano kwa usalama kutokana na elimu tunayotoa.

Hata hivyo amesema kuwa wananchi wajitokeze katika kujisajili kwa alama za vidole kabla ya Desemba 31.

"TCRA tumejidhatiti katika kuwafikia wananchi katika utoaji wa elimu za utumiaji wa bidhaa za mawasiliano kwa kutatua changamoto katika huduma hiyo" amesema Kavishe.

 Wananchi wakiwa katika foleni ya kusajili ili kupata vitambulisho vya Taifa na kuweza kusajil laini kwa alama za vidole.


Wananchi katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada Mkoani Tabora.

DC Katambi ampongeza Rais Magufuli kwa kutekeleza ilani ya CCM ndani ya muda mfupi

$
0
0

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe Patrobas Katambi akiwa na viongozi wa Kamati ya Siasa ya Wilaya hiyo sambamba na watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo.

Charles James, Michuzi TV

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe Patrobas Katambi amemshukuru Rais Dk John Magufuli kwa namna alivyotekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi ndani ya kipindi kifupi.

DC Katambi amesema Rais Magufuli amefanya mambo makubwa kwenye afya, elimu, miundombinu na miraidi ya maendeleo na kuwataka Watanzania kuzidi kumuombea.

Amesema zawadi pekee ambayo imekua Watanzania wanaweza kumpatia Rais Magufuli kutokana na utendaji kazi wake basi ni kufanya kazi kwa bidii, kuwa wazalendo na kuweka maslahi ya Taifa mbele.

" Hakuna Taifa lolote duniani ambalo limefanikiwa bila kufanya kazi siri yao kubwa kuwa na umoja wa kitaifa, mshikamano na upendo hivyo ni vema Watanzania tukawa na upendo na Serikali yetu hii ambayo inafanya kazi usiku na mchana kutuletea maendeleo.

" Lakini jambo lingine na kubwa la kumpatia Rais Magufuli ni kumwaga kura nyingi sana mwakani kwenye uchaguzi Mkuu kwa sababu kwa haya mambo makubwa anayofanya Reli ya Kisasa, Bwawa ka Umeme, Ndege, Ubanaji wa matumizi na kuzuia ufisadi vyote hivyo vinatosha kumfanya asiangaike kuomba kura," Amesema DC Katambi.

Akizungumza mbele ya kamati ya siasa ya Wilaya hiyo, DC Katambi amewaahidi kuendelea kusimamia kwa upana maslahi ya umma na mtumishi yeyote atakwenda kinyume na maagizo na kasi ya Rais Magufuli hatosita kumchukulia hatua.

Amesema kwenye maeneo ya kuchukua hatua ataendelea kuchukua hatua bila kumuonea mtu.

" Lazima tugombane tunavyoona mtu hafati misingi ya utumishi ya umma na niwaambie watendaji na watumishi wote waliopo ndani ya Wilaya hii sitomchekea mtu hakuna udugu wala urafiki kwenye mali za umma. Kwa viongozi wenye kasoro mimi sina unafiki. Kabla sijatumbuliwa mimi mwingine atakua amesagwa kabisa," Amesema DC Katambi.

Mamia ya watu wajitokeza kupata mafunzo ya uwekezaji soko la Hisa yanayotolewa kupitia Vodacom

$
0
0



Afisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar Es Salaam (DSE), Moremi Marwa akizungumza na wanahisa waliojitokeza kupata mafunzo ya uwekezaji kwenye soko la Hisa yaliyotolewa kupitia Vodacom. Mafunzo yalifanyika jijini Dar Es Salaam leo.
Sehemu ya wanahisa waliojitokeza kwenye mafunzo ya uwekezaji kwenye soko la Hisa yaliyolewa na Vodacom, mafunzo yalifanyika jijini Dar Es Salaam leo.

KAMPUNI YA VODACOM TANZANIA YAFANYA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA WANAHISA WAKE JIJINI DAR

$
0
0

 Sehemu ya wanahisa waliojitokeza kwenye mkutano wa mwaka wa Vodacom Tanzania Plc uliofanyika jijini Dar Es Salaam leo.
Mkuu wa Mipango na Uwekezaji wa Vodacom Tanzania Plc, Hilda Bujiku akizungumza na wanahisa waliohudhuria mkutano mkuu wa mwaka wa wanahisa wa Vodacom Tanzania jijini Dar Es Salaam leo.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Vodacom Tanzania Plc, Bw. Ali Mufuruki (katikati) akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa mwaka wa wanahisa wa Vodacom uliofanyika jijini Dar Es Salaam leo. Wengine pichani ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Hisham Hendi (kushoto) na Mkurugenzi wa Fedha Jacques Marais.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Vodacom Tanzania Plc, Hisham Hendi akibadilishana mawazo na Mkurugenzi, Bi. Margaret Ikongo kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa wanahisa wa Vodacom Tanzania Plc uliofanyika leo jijini Dar Es Salaam

Kampuni ya Vodacom yalipa Zaidi ya TZS bilioni 54.5 kama gawio kwa Wanahisa

$
0
0




· Vodacom yatoa taarifa ya ongezeko la faida kwa mwaka kufikia TZS billioni 90.2


 Kampuni ya mawasiliano ya simu za mikononi inayoongoza Tanzania, Vodacom Tanzania PLC imetangaza faida ya mwisho wa mwaka ya kiasi cha TZS bilioni 90.2 kwa mwaka wa fedha 2018/2019 ulioishia mwezi Machi mwaka huu.

Wakati huo huo Kampuni ya Vodacom ambayo ina mtandao wenye kasi zaidi nchini inajivunia thamani iliyojitengenezea katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni ikiwemo TZS bilioni 54.5 ambazo zimelipwa kama gawio kwa wanahisa.

Ongezeko hili limechangiwa na kuongezeka kwa mapato yatokanayo na huduma ambayo yanafikia TZS bilioni 1018.9, ambayo yamesababishwa na kukua na kuimarika kwa mapato yatokanayo na huduma za M-pesa, ununuzi wa Intaneti (Bando) na mapato yatokanayo na ujumbe wa simu. Kampuni ya Vodacom imepata wateja wapya wapatao milioni 1.2 katika mwaka huu wa fedha jambo ambalo linaongeza idadi yake ya wateja kufikia milioni 14.1.

Katika mwaka huu wa fedha kampuni ya Vodacom ilifanya uwekezaji mkubwa wa zaidi ya TZS bilioni 171.4 sawa na (asilimia 16.7% ya Mapato) katika kupanua mtandao wake, kuongeza maeneo yanayopata mtandao wa 4G katika miji mikubwa nchini, kuongeza uwezo na kuboresha mtandao kuweza kutoa huduma ya data ya kiwango cha juu kwa wateja.

Wakati huo Shilingi bilioni 59 zimewekezwa katika mishahara, mafunzo na maendeleo ya wafanyakazi wake wa kudumu wapatao 548 pamoja na kutoa ajira isiyo ya moja kwa moja kwa zaidi ya Watanzania 127,000.

Akiongea katika mkutano mkuu wa mwaka wa kampuni ya Vodacom leo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa kampuni ya Vodacom bwana Ali A. Mufuruki amesema, “Kampuni ya Vodacom vile vile inajivunia uwekezaji wake katika jamii ambao una thamani ya jumla ya shilingi trilioni 1.1, ambazo ni fedha zilizochangiwa katika uwezeshaji wa jamii kupitia kodi, ada za udhibiti katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita ambapo malipo ya zaidi ya Shilingi trilioni 0.4 yalifanyika katika mwaka 2019 peke yake.”

“Ukuaji katika sekta ya mawasiliano imekuwa wa pole pole katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni. Tukiwa kama watendaji muhimu katika sekta hii, tunajivunia kuwa chanya katika ukuaji wa sekta hii,” alihitimisha bwana Mfuruki.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, afungua Kongamano la Kitaifa la Ushiriki wa Watanzania katikaMiradi ya Kimkakati. Septemba 20.2019

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akihutubia kwenye Kongamano la Kitaifa la Ushiriki wa Watanzania katika Miradi ya Kimkakati, lililofanyika katika ukumbi wa LAPF jijini Dodoma. Septemba 20.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizindua mwongozo wa Taifa wa ushiriki wa wananchi katika uwekezaji na tovuti ya miradi ya mikakati, kwenye Kongamano la Kitaifa la Ushiriki wa Watanzania katika Miradi ya Kimkakati, lililofanyika katika ukumbi wa LAPF jijini Dodoma. Septemba 20.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Mwenyekiti wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Dkt. Festus Limbu, wakati akiwasili kwenye ukumbi wa LAPF jijini Dodoma, kufunga Kongamano la Kitaifa la Ushiriki wa Watanzania katika Miradi ya Kimkakati. Septemba 20.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).


Mwenyekiti wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Dkt. Festus Limbu, akizungumza na washiriki, kwenye Kongamano la Kitaifa la Ushiriki wa Watanzania katika Miradi ya Kimkakati, lililofanyika katika ukumbi wa LAPF jijini Dodoma. Septemba 20.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).




Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Binilith Mahenge, akizungumza na washiriki, kwenye Kongamano la Kitaifa la Ushiriki wa Watanzania katika Miradi ya Kimkakati, lililofanyika katika ukumbi wa LAPF jijini Dodoma. Septemba 20.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu,Jenista Mhagama, akizungumza na washiriki, kwenye Kongamano la Kitaifa la Ushiriki wa Watanzania katika Miradi ya Kimkakati, lililofanyika katika ukumbi wa LAPF jijini Dodoma. Septemba 20.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).



MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR BALOZI SEIF ALI IDDI AFUNGA MKUTANO WA MAWAZIRI WA SADC JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akihutubia wakati wa kufunga Mkutano wa Mawaziri wa SADC wa Sekta ya TEHAMA, Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewa waliokutana kwa siku kuanzia Septemba 19-20, 2019 jijini Dar es Salaam. Picha zote na Matokeo Chanya+. Meza kuu.
Mawaziri wa SADC wa Sekta ya TEHAMA, Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewa waliokutana kwa siku kuanzia Septemba 19-20, 2019 jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhandisi Isack Kamwelwe akizungumza wakati wa kufunga Mkutano wa Mawaziri wa SADC wa Sekta ya TEHAMA, Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewa waliokutana kwa siku kuanzia Septemba 19-20, 2019 jijini Dar es Salaam. Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Mchezo Dkt. Harrison Mwakyembe akimkaribisha mgeni rasmi kufunga Mkutano wa Mawaziri wa SADC wa Sekta ya TEHAMA, Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewa waliokutana kwa siku kuanzia Septemba 19-20, 2019 jijini Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Sekta ya Uchukuzi Bw. Leonard Chamriho akizungumza wakati wa kufunga Mkutano wa Mawaziri wa SADC wa Sekta ya TEHAMA, Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewa waliokutana kwa siku kuanzia Septemba 19-20, 2019 jijini Dar es Salaam. 
Mawaziri wa SADC wa Sekta ya TEHAMA, Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewa waliokutana kwa siku kuanzia Septemba 19-20, 2019 jijini Dar es Salaam. Brass Bendi wakiongoza shughuli.
Mawaziri wakiwa katika picha ya pamoja.
Kamati ya maandizi.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi Na Mawasiliano Dkt Jim Yonazi (wa pili toka kulia, mstari wa mbele) pamoja na viongozi wengine wakiwa na watoa huduma walioshughulika na mkutano huo.

KAMISHNA JENERALI PHAUSTINE KASIKE ARIDHISHWA NA KASI, UJENZI WA NYUMBA ZA GHARAMA NAFUU, GEREZA KUU ISANGA

$
0
0
Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike(mwenye miwani) akiangalia mbao zinazotumika katika hatua mbalimbali za ujenzi wa mradi wa nyumba za makazi ya Maafisa na askari katika Gereza Kuu Isanga, alipotembelea eneo hilo la ujenzi, leo Septemba 21, 2019. (Picha zote na Jeshi la Magereza).
Muonekano wa nyumba takribani 20 ambazo tayari zimejengwa katika mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi ya Maafisa na askari katika Gereza Kuu Isanga zikiwa katika hatua mbalimbali ya ujenzi.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akisalimiana na Maafisa wa Jeshi la Magereza mkoani Dodoma alipowasili kwenye ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi ya Maafisa na askari katika Gereza Kuu Isanga, leo Septemba 21, 2019.


Na ASP. Lucas Mboje, Dodoma;

KAMISHNA Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike amekagua ujenzi unaoendelea wa nyumba za makazi ya Maafisa na askari katika Gereza Kuu Isanga ambao unatumia nguvu kazi ya wafungwa wa gereza hilo, jijini Dodoma na ameridhika na kasi ya ujenzi huo.

Akiwa eneo hilo la ujenzi leo(Jumamosi), Kamishna Jenerali Phaustine Kasike ameelezea kufurahishwa, kuridhika na kasi ya hatua mbalimbali za ujenzi ulipofikia na ameupongeza Uongozi wa Magereza mkoani Dodoma kwa usimamizi mzuri wa mradi huo.

“Mmeonesha namna gani mmejipanga vizuri katika kutekeleza Mkakati wa Jeshi katika kutatua uhaba wa makazi ya Maafisa na Askari, hivyo niwapongeze sana kwa kazi nzuri mnayoendelea kuifanya, chapeni kazi,” alisema Kamishna Jenerali Kasike.

Kwa upande wake Mkuu wa Magereza Mkoani Dodoma, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Keneth Mwambije amemshukru Kamishna Jenerali kwa kutembelea mradi huo na kujionea hatua mbalimbali za ujenzi ikiwemo kuwatia moyo Maofisa, askari na Wafungwa wanaoshiriki kikamilifu katika ujenzi huo.

Aidha, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Keneth Mwambije, amemhakikisha Mkuu huyo wa Jeshi la Magereza kuwa wataendelea kutekeleza mkakati huo wa ujenzi wa nyumba za tofali za kuchoma ili kuhakikisha kuwa wanatekeleza maelekezo ya Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama aliyoyatoa kwa Jeshi hilo kuhusu ujenzi wa makazi ya Maafisa na askari kwa kutumia nguvu kazi ya wafungwa waliopo magerezani.

Ujenzi wa nyumba hizo za tofali za kuchoma ulianza rasmi Aprili, 2019 ambapo hadi sasa jumla ya nyumba 20 zimejengwa na zipo katika hatua mbalimbali za ujenzi, moja kati ya nyumba hizo tayari imekwishapauliwa, nyumba tano(05) zimekwisha fungwa lenta na nyingine 14 zinasubilia kufungwa lenta hivi karibuni.

SIMBACHAWENE: MABADILIKO YA TABIANCHI HUATHIRI SHUGHULI ZA KIUCHUMI

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. GeorgeSimbachawene akizungumza katika Maadhimisho ya Siku ya Amani Duniani.
Sehemu ya washiriki wa Maadhimosho ya Siku ya Amani Duniani wakifuatiliamatukio.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene akiwa na viongozi wengine kuanzia kushoto ni Mkurugenzi wa Jukwaa la Mabadiliko ya Tabianchi Rebeca Muna, Mkurugenzi wa MashtakaBiswalo Mganga, Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa (UN)-Tanzania AmonManyama na Clara Makanya kutoka Shirika la Mazingira.
Mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Amani Duniani Waziri wa Nchi Ofisiya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachaweneakivishwa skafu na skauti alipowasili katika tukio hilo.
Picha ya pamoja ikiwahusisha mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu waRais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene (walioka katikati)mara baada ya kuhutubia Maadhimisho hayo.

**********************


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. GeorgeSimbachawene amesema mabadiliko ya tabianchi nchi huathiri moja kwa mojashughuli za kiuchumi na ustawi wa jamii hivyo huatarisha amani.

Akizungumza kwenye kwenye Maadhimisho ya Siku ya Amani Duniani
yaliyofanyika Jijini Dodoma Septemba 21 Mhe. Simbachawene ambaye alikuwamgeni rasmi alisema kwa kiasi kikubwa mabadiliko ya tabianchi huchangiwa nashughuli za kibinadamu.

Alisema kuwa shughuli hizo husababisha kuongezeka kwa halijoto, kupunguakwa kiwango cha mvua, kukauka kwa vyanzo vya maji na kuongezeka kwamagonjwa ya binadamu, wanyama na mimea.

"Kwa kiasi kiasi kikubwa mabadiliko ya tabianchi huchangiwa na shughuli zakibinadamu zikiwemo uchafuzi wa hali ya hewa, uchomaji misitu, ukataji miti bilakuotesha na shughuli za kilimo na ufugaji zisizozingatia uhifadhi wa mazingiraambazo huchangia kuongezeka kwa hali ya joto," alisema Waziri huyo.

Aliongeza kuwa pamoja na athari za mabadiliko haya kuzikumba nchi zote
duniani pia huzikumbwa nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania na hi ni kutokanana ukeli kuwa ukuaji wa uchumi wetu hutegemea zaidi shughuli za kiuchumi.

Kutokana na hali hiyo Waziri huyo alibainisha kuwa ili kukabiliana changamotohizo kama nchi tunahitaji kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ili kuhimili nakujiepusha na majanga yanayosababishwa nayo.

Alitahdharisha kuwa majanga yanayotokana na hali hiyo husababisha hasara zakiuchumi na kijamii zinazochangia kuongezeka kwa umaskini na hata migogoroya kijamii.

“Chanzo cha kupotea kwa amani kwa baadhi ya maeneo ni chanzo chake ni
mabadiliko ya tabianchi na hali ikibadili watu wakakosa mahitaji kama maji
hawawezi kukubali kufa lazima watatumia nguvu yoyote kuyapata kwa
kugombana.

“Hali ya hewa ikibadilika kusababisha kukosekana kwa maji watu watapambanana kutafuta yake kidogo yaliyopo na katika kuyatafuta lazima watagombana hivyo kusababisha vurugu hivyo amani ina uhusiano mkubwa na mabadiliko yatabianchi”alisema.

Mhe. Simbachawene alidokeza kuwa Serikali inatambua umuhimu wa mazingirahivyo imeendelea kufanya jitihada kubwa za kutunza na kusimamia mazingirakwa kuanzisha miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa ukuta wa kingo za bahari.

Kwa upande mwingine Waziri Simbachawene alihimiza jumuiya za kimataifakuweka mkazo katika kukabiliana na janga la mabadiliko ya tabia nchi kwakuzingatia kuwa uchumi wetu hutegemea shughuli zitokanazo na mazingira.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa (UN)-Tanzania Amon
Manyama alipongeza Serikali kwa jiihada zake za kulinda amani hususana katikakukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Alisema kuwa ni jambo jema kuchukua hatua madhubuti za kukabiliana na
changamoto hiyo na kuwa amani ni msingi wa kuanzishwa kwa UN hivyo
tuhakikishe jitihada hizi zinadumu.

RC MAKONDA ATOA TUZO NA ZAWADI KWA WANAFUNZI NA WALIMU WA SHULE ZILIZOFANYA VIZURI MITIHANI YA TAIFA ELIMU YA MSINGI NA SEKONDARI DARE S SALAAM

$
0
0
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda ametoa tuzo na zawadi mbalimbali kwa wanafunzi, na walimu ambao shule zao zilifanya vizuri kwenye mitihani ya taifa ya elimu ya msingi na sekondari mwaka 2018 katika hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya maonesho ya biashara Sabasaba jijini Dar es Salaam Septemba 21, 2019.

Sambamba na zawadi hizo, Mhe. Makonda pia ameahidi kutoa ofa kwa walimu 30 wa jiji la Dar es Salaam wakiwa na wenza wao kwenda kwenye mbuga ya wanyama ikiwa ni furaha yake baada ya shule za jiji la Dar es Salaam kufanya vizuri kwenye mitihani hiyo lakini pia kwenye michezo ya Umiseta.

Kandoni na hafla hiyo, Maafisa wa Mwalimu Bank, benki ambayo ilikuwa miongoni mwa wadau wakubwa wa walimu kusapoti shughuli hiyo, walikabidhi kadi za ATM kwa walimu ambao ni wateja wa benki hiyo sambamba na kuandikisha wateja wapya ambao walijitokeza kufungua akaunti.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Mhe. Makonda pamoja na mambo mengine aliipongeza Benki ya Mwalimu na wadau wengine kwa kuunga mkono elimu na walimu.

Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa Mwalimu Bank, Bw. Richard Makungwa alisema asilimia kubwa ya wanahisa wa benki hiyo ni walimu na kuwahimiza walimu kutumia huduma za benki hiyo ili kufikia lengo la kuanzishwa kwake la kuwainua walimu kiuchumi.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda (kulia), akimkabidhi tuzo Afisa Mtendaji Mkuu wa Mwalimu Commercial Bank, Bw. Richard Makungwa kutokana na benki hiyo kuwa miongoni mwa taasisi zilizofanikisha hafla ya utoaji tuzo na zawadi kwa wanafunzi na walimu wa mkoa wa Dar es Salaam waliofanya vizuri kwenye mitihani ya taifa ya elimu ya Msingi na Sekondari mwaka 2018. Hafla hiyo imefanyika kwenye ukumbi wa Karume ulio katika viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaa (Sabasaba) jijini Dar es Salaam leo Septemba 21, 2019. Benki ya Mwalimu inamilikiwa kwa kiasi kikubwa na walimu kote nchini.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda akitoa cheti kwa mmoja wa walimu wa shule ya sekondari iliyofanya vizuri kwenye mitihani hiyo
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda akitoa hotuba yake.
Sehemu ya walimu waliohudhuria hafla hiyo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mwalimu Commercial Bank Plc, Bw. Richard Makungwa, akitoa hotuba yake.
Afisa Uhusiano wa Mwalimu Commercial Bank, Bw. Michael Kachala, (kulia), akimuelimisha Mwalimu huyu ambaye ni mteja wa Mwalimu Commercial Bank, namna ya kutumia ATM card. Benki ya Mwalimu iko katika mtandao wa ATM za Umoja Switch kote nchini.
Walimu wakijaza fomu za kufungulia akaunti, kandoni mwa hafla ya utoaji tuzo na zawadi kwa walimu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambao shule zao zilifanya vizurio kwenye matokeo ya mitihani ya taifa ya eli mu ya Msingi na Sekondari mwaka 2018. Hafla hiyo ilifanyika viwanja vya Maonesho Sabasaba jijini Dar es Salaam Septemba 21, 2019.
Mkurugenzi wa Fedha wa Mwalimu Commercial Bank, Bw.Selemani Kijori (mwenye miwani), akizungumza na mmoja wa walimu ambaye alifika kwenye meza ya benki hiyo kuhudumiwa.
Mkurugenzi wa Fedha wa Mwalimu Commercial Bank, (MCB)Bw.Selemani Kijori (mwenye miwani) pamoja na timu yake Afisa wa Huduma kwa wateja wa MCB, Bi.Martha Gambosi(wapili kulia) na Afisa Uhusiano wa benki hiyo, Bw.Bw. Michael Kachala, wakichambua ATM cards za wateja wa benki hiyo tayari kuwakabidhi.
Afisa mahusiano wa tawi la Mlimani Mwalimu Commercial Bank, Barabara ya Sam Nujoma jijini Dar es Salaam wa Benki ya Mwalimu Bw. Abdulhakim Salimu (kushoto), akimwelekeza mteja namna ya kujaza fomu ya kufungulia akaunti.
Elimu ya ATM card ikiendelea kutoklewa hapa ni Afisa Uhusiano wa benki hiyo, Bw.Michael Kachala (kulia), akifafanua jambo kwa mteja
Afisa wa Huduma kwa wateja wa Malimu Commercial Bank (MCB), Bi.Martha Gambosi (kulia) akimweleza jambo Mwalimu huyu (aliyeipa mgongo camera) kuhusu huduma zitolewazo na benki hiyo.

DKT. ASHATU KIJAJI KUTATUA CHANGAMOTO YA MAJI KIJIJI CHA MWONGOLO KONDOA VIJIJINI

$
0
0
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango ambae pia ni Mbunge wa Kondoa Vijijini Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akizungumza na wananchi wa wa Kijiji cha Mwongolo wilayani Kondoa, ambapo wananchi hao walimuomba awatatulie kero ya maji ambayo imekua changamoto kubwa kijijini hapo.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Kondoa, Dodoma Alhaji Othman Gora(kushoto) akiteta jambo na Katibu wa CCM Wilaya hiyo Bw. Nicholaus Kasendamila wakati wa mkutano wa hadhara kati ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango ambae pia ni Mbunge wa Kondoa Vijijini Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji na Wananchi wa Kijiji cha Mwolongo alipotembea Kijiji hicho.
Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Mwolongo wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Fedha na Mipango ambae pia ni Mbunge wa Kondoa Vijijini Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (hayupo pichani), alipokuwa anatolea majibu ya baadhi ya changamoto zilizotolewa na wanakijiji hao.
Bi. Khadija Irorya akimuelezea Naibu Waziri wa Fedha na Mipango ambae pia ni Mbunge wa Kondoa Vijijini Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (hayupo pichani), changamoto ya ukosefu wa maji katika Kijiji hicho na kumuomba awasaidie kuitatua kero hiyo iliyodumu kwa muda mrefu.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango ambae pia ni Mbunge wa Kondoa Vijijini Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akiteta jambo na Diwani wa Kata ya Ilolo Bw. Ramadhani Bakari alipotembea Kijiji hicho.

……………………

Na Mwandishi wetu, Kondoa

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kondoa Vijijini mkoani Dodoma Dkt. Ashatu Kijaji ameahidi kumaliza kero ya maji inayo wakabili wakazi wa Kijiji cha Mwongolo mkoani humo.

Ametoa ahadi hiyo alipokutana na wananchi wa kijiji hicho ambao walimweleza kuhusu changamoto yao ya muda mrefu ya kukosa huduma ya maji safi na salama pamoja na changamoto nyingine za ukosefu wa miundombinu mingine inayoweza kuchochea kasi yao ya maendeleo.

Wananchi hao walisema kero kubwa inayo waumiza ni upatikanaji wa maji katika kijiji hicho ambapo wanawake wamekuwa wakilazimika kwenda umbali mrefu kuchota maji jambo ambalo limewafanya kuchoka na kuhatarisha usalama wa maisha yao.

Dkt. Kijaji alisema kuwa amekuwa akichimba visima katika vijiji mbalimbali wilayani humo ambapo hadi sasa jumla ya visima 65 vimeshakamilika na kutoa huduma ya maji kwa wananchi.

“Leo nimekamilisha kisima cha 65 Shule ya Msingi Kalamba niliposoma ndani ya miaka minne ya uongozi wangu, hapa Mwongolo ni nyumbani na kwa mapenzi niliyonayo kwa ndugu zangu wa Mwongolo, mhandisi akimaliza kuchimba kisima cha kijiji cha Mwaisanga atakuja Mwolongo katika kipindi cha mwezi huu au wa kumi kisima kitakuwa kimechimbwa” alisisitiza Dkt. Kijaji.”

Aidha ameahidi kufuatilia visima 14 vilichoahidiwa kuchimbwa kwenye sehemu ya machinjio ya kijiji hicho na Wizara ya Maji kupitia Wakala wa Uchimbaji Visima na Mabwawa, (DDCA), ili nao waweze kupata maji kwa ajili ya shughuli zao za kila siku.

Aliongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano ni sikivu hivyo itaendelea kuboresha huduma mbalimbali za jamii kama vile Sekta ya elimu, huduma za afya, nishati, maji, miundombinu ili ziweze kuwafikia wananchi wote nchini kwa urahisi zaidi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Mwolongo Bw. Miraji Ramadhani, amemshukuru Dkt. Ashatu Kijaji kwa kutenga muda wa kwenda kutembelea kijiji hicho na kutatua baadhi ya kero zilizokuwa vinawasumbua muda mrefu.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji ameahidi hadi kufikia 2020 vijiji vyote 84 vya Jimbo lake la Kondoa Vijijini vitakua vimepata huduma ya maji kwa njia ya visima vya maji ili kumaliza kabisa kero ya maji Jimboni humo.

BENKI YA NMB YAADHIMISHA SIKU YA USAFI DUNIANI KWA KUFANYA USAFI MAENEO MBALIMBALI

$
0
0
Wafanyakazi wa benki ya NMB tawi la Sengerema mkoani Mwanza nao walishiriki katika kufanya usafi kwenye mji huo.

Wafanayakazi wa benki ya NMB tawi la Kalius mkoa wa Tabora nao walishiriki katika kufanya usafi kwenye mji huo


Katika kuadhimisha siku ya usafi duniani wafanyakazi wa benki ya NMB wameshiriki kufanya usafi katika maeneo mbalimbali nchini kote, tazama matukio ya picha katika mikoa na maeneo mbalimbali zikionesha wafanyakazi hao wakifanya usafi.
Wafanyakazi wa benki ya NMB Kanda ya Mashariki wakiendelea na usafi.


Wafanyakazi wa benki ya NMB Kanda ya Mashariki wakiendelea na usafi.
Wafayakazi wa benki ya NMB Tarime Mkoani Mara wakiendelea wakifanya usafi jana katika mji wa huo.

Wafanyakazi wa NMB Kanda ya Dar es salaam nao walifanya usafi jijini Dar es salaam.

TAMASHA LA JAMAFEST LAANZA KWA MATEMBEZI YA BURUDANI JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Maandamano ya burudani yakiingia Uwanja wa Uhuru katika Tamasha la Jamafest linalofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 21-28 September 2019 
 Matembezi ya Burudani yakielekea uwanja wa Uhuru katika Tamasha la Jamafest linalofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 21-28 September 2019  Jukwaa la burudani litakalotumiwa na wasanii mbalimbali katika Tamasha la Jamafest linalofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 21-28 September 2019  Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe wa pili toka kulia akiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la JAMAFEST Bi Joyce Fissoo wa kwanza toka kulia wakiingia katika Uwanja wa Uhuru kwa ajili ya kupokea matembezi ya burudani toka kwa washiriki wa nchi za Afrika Mashariki katika Tamasha la Jamafest linalofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 21-28  September 2019.  Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe wa pili toka kulia akiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la JAMAFEST Bi Joyce Fissoo wa kwanza toka kulia wakiingia katika Uwanja wa Uhuru kwa ajili ya kupokea matembezi ya burudani toka kwa washiriki wa nchi za Afrika Mashariki katika Tamasha la Jamafest linalofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 21-28 September 2019  Washiriki wa Tanzania katika Tamasha la Jamafest linalofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 21-28 September 2019  Mama Singi kutoka Arusha ambaye anauza nguo za Vitenge na Batiki lakini pia ni msanii wa muziki ambaye atapata nafasi ya kuimba katika Tamasha la Jamafest linalofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 21-28 September 2019  Mama Singi kutoka Arusha ambaye anauza nguo za Vitenge na Batiki katika Tamasha la Jamafest linalofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 21-28 September 2019  Mama Singi kutoka Arusha ambaye anauza nguo za Vitenge na Batiki katika Tamasha la Jamafest linalofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 21-28 September 2019  Mama Singi kutoka Arusha ambaye anauza nguo za Vitenge na Batiki katika Tamasha la Jamafest linalofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 21-28 September 2019  Bidhaa mbalimbali katika Tamasha la Jamafest linalofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 21-28 September 2019  Tamasha la Jamafest linalofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 21-28 September 2019  Mshiriki kutoka Burundi katika Tamasha la Jamafest linalofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 21-28 September 2019  Washiriki wa Tanzania katika Tamasha la Jamafest linalofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 21-28 September 2019  Washiriki wa Uganda katika Tamasha la Jamafest linalofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 21-28 September 2019  Bidhaa mbalimbali za asili katika Tamasha la Jamafest linalofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 21-28 September 2019  Bidhaa mbalimbali za asili katika Tamasha la Jamafest linalofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 21-28 September 2019  Bidhaa mbalimbali katika Tamasha la Jamafest linalofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 21-28 September 2019  Bidhaa mbalimbali katika Tamasha la Jamafest linalofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 21-28 September 2019  
Bidhaa kutoka Zanzibar katika mabanda ya biashara katika Tamasha la Jamafest linalofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 21-28 September 2019  
Mshiriki wa Tanzania katika Tamasha la Jamafest linalofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 21-28 September 2019  
Mshiriki wa Tanzania katika Tamasha la Jamafest linalofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 21-28 September 2019  Mshiriki wa Tanzania katika Tamasha la Jamafest linalofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 21-28 September 2019  Mshiriki wa Tanzania katika Tamasha la Jamafest linalofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 21-28 September 2019  Mshiriki wa Tanzania katika Tamasha la Jamafest linalofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 21-28 September 2019  Washiriki wa Burundi wakicheza ngoma katika Tamasha la Jamafest linalofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 21-28 September 2019  Washiriki wa Burundi wakicheza ngoma katika Tamasha la Jamafest linalofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 21-28 September 2019  Washiriki wa Burundi wakicheza ngoma katika Tamasha la Jamafest linalofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 21-28 September 2019  Washiriki wa Burundi wakicheza ngoma katika Tamasha la Jamafest linalofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 21-28 September 2019  Washiriki wa Burundi wakicheza ngoma katika Tamasha la Jamafest linalofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 21-28 September 2019  Washiriki wa Burundi wakicheza ngoma katika Tamasha la Jamafest linalofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 21-28 September 2019  Washiriki wa Kenya wakicheza ngoma katika Tamasha la Jamafest linalofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 21-28 September 2019  Washiriki wa Rwanda wakicheza ngoma katika Tamasha la Jamafest linalofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 21-28 September 2019  Mabanda yenye bidhaa mbalimbali katika Tamasha la Jamafest linalofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 21-28 September 2019

Uzinduzi Wa Rock City Marathon 2019 Jijini Mwanza

$
0
0

DC Nyamagana Akoshwa Na Maandalizi, Ubora Wa Zawadi Za Rock City Marathon

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mkoa wa Mwanza Dkt. Phillis Nyimbi mwishoni mwa wiki alizindua msimu wa kumi wa mbio ndefu za Rock City Marathon 2019 kwa jiji la Mwanza huku akionyeshwa kuridhishwa na maandalizi ikiwemo zawadi na ubora wa medali zitakazotolewa kwa washindi na washiriki wa mbio hizo.

Mbio za Rock City Marathon zinatarajiwa kufanyika Octoba 20, mwaka huu kwenye viunga vya jengo la kibiashara la Rock City Mall lililopo jijini Mwanza ambapo zaidi sh Mil 30 zitatolewa kwa washindi sambamba na fulana pamoja na medali.

Uzinduzi huo ulishirikisha wadau mbalimbali wa mbio hizo, wakiwemo viongozi kutoka Serikalini, Viongozi kutoka Taasisi mbalimbali, Wadhamini wa mbio pamoja na baadhi ya wanariadha kutoka vilabu vya mchezo huo jijini Mwanza.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela, Dkt. Nyimbi mbali na kuwapongeza wadau hao kwa maandalizi mazuri ya mbio hizo pia alithibitisha ushiriki wake pamoja na ushiriki wa Mkuu wa Mkoa huo Bw John Mongella sambamba na viongozi waandamizi wa mkoa huo kwenye mbio hizo zenye umaarufu mkubwa katika ukanda wa Ziwa.

"Kwa kuzingatia ubora wa maandalizi pamoja na uzito wa malengo ya mbio hizi nitamke bayana kuwa Serikali ya Mkoa wa Mwanza tupo tayari kushirikiana na waandaaji wa mbio hizi si tu kwa kushiriki bali pia kuhakikisha kwamba mwaka huu mbio hizi zinafana na zinavutia washiriki wengi zaidi hususani wa kimataifa,'' alisema Dk Nyimbi.

Mbio za Rock City Marathon zilizoanzishwa miaka kumi iliyopita zimezidi kujiongezea umaarufu kila mwaka na tayari zimefanikiwa kuwavutia baadhi ya wadhamini ikiwa ni pamoja na kampuni za TIPER, Pepsi, Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA).

Wadhamini wengine ni pamoja na kampuni ya uwakili ya Lis Law Chambers & Consultants, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), CF Hospital, Metro FM, Mwanza Water, Pigeon Hotel, Kampuni ya Usafi ya SDN na Kampuni ya Ulinzi ya Garda World.

Kwa upande wake Mratibu wa mbio hizo kutoka kampuni ya Capital Plus International (CPI) Bi Magdalena Laizer mbali na kuwashukuru wadau wa mbio hizo wakiwemo wadhamini alitoa wito kwa washiriki wa ndani hususani wa mikoa ya Kanda ya Ziwa pamoja na wadhamini kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mbio hizo ambazo kwa mwaka jana zilifanikiwa kuhusisha washiriki zaidi ya 1200.

Akizungumza kwenye hafla hiyo Mshauri wa masuala ya Ufundi wa mbio hizo Bw John Bayo alisema maandalizo ya mbio hizo kwasasa yamekamilika kwa asilimia 70 huku akitumia fursa hiyo kutangaza njia zinakazotumika wakati wa mbio hizo zinazohusisha mbio za 42 km, 21 km, 5 km na 2.5 km.

Alisema kwasasa usajili wa mbio hizo unaendelea kupitia vituo mbalimbali katika mikoa ya Mwanza (Rock City Mall, Pasiansi Afro Twist Gym), Dodoma (Shabiby Bus Terminal), Dar es Salaam (Shamo Tower na Imalaseko Super Market), Arusha pamoja na Bagamoyo mkoani Pwani.

“ Pia usajili unaweza kufanyika kwa njia ya mtandao kupitia website yetu ya Rock City Marathon,’’ alitaja. 



Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mkoa wa Mwanza Dkt. Phillis Nyimbi (alievaa suti nyeusi) akifungua pazia kuashiria uzinduzi rasmi msimu wa kumi wa mbio ndefu za Rock City Marathon 2019 kwa jiji la Mwanza wakati wa hafla fupi ya uzinduzi huo iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini humo. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mratibu wa mbio hizo kutoka kampuni ya Capital Plus International (CPI) Bi Magdalena Laizer (wa kwanza kushoto) na wadau mbalimbali wa mchezo huo jijini humo. Mbio hizo zinatarajiwa kufanyika Octoba 20, mwaka huu kwenye viunga vya jengo la kibiashara la Rock City Mall lililopo jijini Mwanza.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mkoa wa Mwanza Dkt. Phillis Nyimbi (alievaa suti nyeusi) akifurahia muonekano wa medali pamoja na ramani ya njia zitakazotumika kwenye mbio za Rock City Marathon 2019 wakati wa hafla fupi ya uzinduzi rasmi msimu wa kumi wa mbio hizo kwa jiji la Mwanza iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini humo. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mshauri wa masuala ya Ufundi wa mbio hizo Bw John Bayo (kushoto kwake) na wadau mbalimbali wa mchezo huo jijini humo. Mbio hizo zinatarajiwa kufanyika Octoba 20, mwaka huu kwenye viunga vya jengo la kibiashara la Rock City Mall lililopo jijini Mwanza.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mkoa wa Mwanza Dkt. Phillis Nyimbi (katikati) akionyesha moja ya medali itakayotolewa kwa washindi na washiriki wa mbio za Rock City Marathon 2019 wakati wa hafla fupi ya uzinduzi rasmi msimu wa kumi wa mbio hizo kwa jiji la Mwanza iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini humo. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mshauri wa masuala ya Ufundi wa mbio hizo Bw John Bayo (kulia) na Mratibu wa mbio hizo kutoka kampuni ya Capital Plus International (CPI) Bi Magdalena Laizer (kushoto).Mbio hizo zinatarajiwa kufanyika Octoba 20, mwaka huu kwenye viunga vya jengo la kibiashara la Rock City Mall lililopo jijini Mwanza.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mkoa wa Mwanza Dkt. Phillis Nyimbi (kulia) akionyesha fomu ya usajili wa mbio za Rock City Marathon 2019 kuthibitisha ushiriki wake kwenye mbio hizo wakati wa hafla fupi ya uzinduzi rasmi msimu wa kumi wa mbio hizo kwa jiji la Mwanza iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini humo. Kushoto ni Mratibu wa mbio hizo kutoka kampuni ya Capital Plus International (CPI) Bi Magdalena Laizer. Mbio hizo zinatarajiwa kufanyika Octoba 20, mwaka huu kwenye viunga vya jengo la kibiashara la Rock City Mall lililopo jijini Mwanza.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mkoa wa Mwanza Dkt. Phillis Nyimbi (kulia) akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla fupi ya uzinduzi rasmi msimu wa kumi wa mbio za Rock City Marathon kwa jiji la Mwanza iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini humo.
Mshauri wa masuala ya Ufundi wa mbio hizo Bw John Bayo akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla fupi ya uzinduzi rasmi msimu wa kumi wa mbio za Rock City Marathon kwa jiji la Mwanza iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini humo.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mkoa wa Mwanza Dkt. Phillis Nyimbi (mwenye suti nyeusi) akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa mbio za Rock City Marathon wakiwemo viongozi kutoka Serikalini, wadhamini wa mbio hizo pamoja na wawakilishi wa washiriki wa mbio za watoto (waliovaa nguo nyekundu) wakati wa hafla fupi ya uzinduzi rasmi msimu wa kumi wa mbio za Rock City Marathon kwa jiji la Mwanza iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini humo.
 

DC KOROGWE AZINDUA WIKI YA USIKILIZWAJI, UTOAJI HUDUMA NA UTATUZI WA KERO ZA WANANCHI WILAYA YA KOROGWE

$
0
0
Wakati wa uzinduzi wa wiki ya usikilizwaji,utoaji huduma na utatuzi wa kero za wananchi wilayani Korogwe, Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mhe. Kissa G. Kasongwa amekemea watumishi wote wa Serikali ambao wanatabia ya kutowasikiliza na kuwahudumia wananchi vizuri pale wanapokwenda katiaka ofisi zao na kuongeza kuwa wananchi ndio mabosi wa wahusika wote serikalini. 

Alisema kama yeye Mkuu wa Wilaya wa Korogwe anatoa kiti chake ofisini na kukaa nje katika eneo la kuegeshea magari ili kuwasikiliza wananchi kwa unyenyekevu wote.

Mhe. Kasongwa alitoa rai kwa watumishi wote wa idara na taasisi, kuwa waende wawasikilize wananchi na kuto watolea maneno mabaya na kuwahimiza kufanya kazi kwa bidii na weredi ili kufikisha azma ya Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kutaka kuwafikia wananchi wanyonge.

Taasisi mbalimbali zitatoa huduma katika wiki hii, ikiwa ni pamoja na Mfuko wa Fidia kwa wafanyakazi (WCF) , PSSSF, NHIF, NSSF, NIDA, RITA, PCCB, TRA, Damu Salama, Jeshi la zima moto, Benki mbalimbali ikiwa ni pamoja na NMB na CRDB, Kampuni za Simu ikiwa ni pamoja na Halotel, TTCL, Mawakili wanaotoa msaada wa kisheria pamoja na taasisi mbalimbali
Mhe. Kissa G. Kasongwa Mkuu wa Wilaya ya Korogwe akizindua rasmi wiki ya usikilizwaji,utoaji huduma na utatuzi wa kero za wananchi wilayani hapo kuanzia tarehe 21 - 24 Septemba 2019, katika viwanja vya ofisi ya Mkuu wa Wilaya Korogwe tarehe 21.09.2019
Viongozi wa Dini wakifungua kwa maombi wiki ya usikilizwaji,utoaji huduma na utatuzi wa kero za wananchi 
Katibu Tawala wa Wilaya ya Korogwe Bi. Rehema Bwasi akitoa maelezo ya chimbuko la wiki ya usikilizwaji,utoaji huduma na utatuzi wa kero za wananchi katika Wilaya hiyo.
Mbunge wa Korogwe mjini Mhe. Mary Chatanda akitoa sakamu zake kwa wananchi wakati wa uzinduzi wa wiki ya usikilizwaji,utoaji huduma na utatuzi wa kero za wananchi wilayani Korogwe.
Mbunge wa Korogwe Vijijini Mhe. Timotheo Mzava akitoa salamu zake kwa wananchi wakati wa uzinduzi wa wiki ya usikilizwaji,utoaji huduma na utatuzi wa kero za wananchi wilayani Korogwe.
Mwenyekiti wa CCM Korogwe vijijini Bw. Nassoro Malingumu akitoa salamu zake wakati wa wiki ya usikilizwaji,utoaji huduma na utatuzi wa kero za wananchi wilayani Korogwe
Mwenyekiti wa CCM Korogwe mjini Bw. Immanuel Chale akitoa salamu zake wakati wa wiki ya usikilizwaji,utoaji huduma na utatuzi wa kero za wananchi wilayani Korogwe
Wananchi mbalimbali wakiwa katika uzinduzi wa wiki ya usikilizwaji,utoaji huduma na utatuzi wa kero za wananchi 
Waananchi mbalimbali kutoka Wilayani Korogwe wakipata huduma wakati wa wiki ya usikilizwaji,utoaji huduma na utatuzi wa kero za wananchi.

MAKAMU WA RAIS SAMIA SUHULU AFUNGUA TAMASHA LA JAMAFEST 2019 JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akipiga ngoma kuashiria ufunguzi wa Tamasha la JAMAFEST lililoanza Septemba 21-28, 2019 katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Tamasha la Sanaa na Utamaduni kwa nchi za Afrika Mashariki likiwa tayari limefanyika katika nchi tatu, Kigali (Rwanda), Nairobi (Kenya), Kampala (Uganda) na sasa linafanyika Dar es Salaam, Tanzania. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akifungua Tamasha la JAMAFEST lililoanza Septemba 21-28, 2019 katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Tamasha la Sanaa na Utamaduni kwa nchi za Afrika Mashariki likiwa tayari limefanyika katika nchi tatu, Kigali (Rwanda), Nairobi (Kenya), Kampala (Uganda) na sasa linafanyika Dar es Salaam, Tanzania. Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Mchezo Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza wakati ufunguzi wa Tamasha la JAMAFEST lililoanza Septemba 21-28, 2019 katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Tamasha la Sanaa na Utamaduni kwa nchi za Afrika Mashariki likiwa tayari limefanyika katika nchi tatu, Kigali (Rwanda), Nairobi (Kenya), Kampala (Uganda) na sasa linafanyika Dar es Salaam, Tanzania.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Michezo na Utamaduni wa Rwanda Mhe. John Ntigengwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa Tamasha la JAMAFEST lililoanza Septemba 21-28, 2019 katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Tamasha la Sanaa na Utamaduni kwa nchi za Afrika Mashariki likiwa tayari limefanyika katika nchi tatu, Kigali (Rwanda), Nairobi (Kenya), Kampala (Uganda) na sasa linafanyika Dar es Salaam, Tanzania.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan (kushoto) akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Michezo na Utamaduni wa Rwanda Mhe. John Ntigengwa (kulia) mara baada ya kufika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, Tanzania. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Msanii wa muziki wa Bongofleva Diamond Platnumz wakati wa ufunguzi wa Tamasha la #JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania kuanzia Septemba 21-28, 2019.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan (kushoto) akisalimia wananchi mara baada ya kufika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, Tanzania katika ufunguzi wa JAMAFEST. Meza kuu... Brass Bendi ikiongoza nyimbo za Taifa za mataifa ya #Tanzania #Kenya #Uganda #Burundi #Rwanda wakati wa uzinduzi wa Tamasha la #JAMAFEST2019 #JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Bendera za mataifa yanayoshiriki Tamasha la #JAMAFEST 2019
Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya Diamond Platnumz akitoa burudani wakati wa Ufunguzi wa Tamasha la #JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Burudani ya ngoma kutoka #Tanzania #Kenya #Uganda #Burundi #Rwanda ikipamba moto katika uwanja wa Uhuru wakati wa ufunguzi wa Tamasha la JAMAFEST.
Ngoma ya #Burundi ikipamba moto wakati wa ufunguzi wa Tamasha la JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Ngoma ya #Kenya ikipamba moto wakati wa ufunguzi wa Tamasha la JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Ngoma ya #Uganda ikipamba moto wakati wa ufunguzi wa Tamasha la JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Burudani ya ngoma kutoka #Tanzania #Kenya #Uganda #Burundi #Rwanda ikipamba moto katika uwanja wa Uhuru wakati wa ufunguzi wa Tamasha la JAMAFEST.

RAIS DKT MAGUFULI ATOA SHILINGI MILIONi 10 KUISAIDIA TIMU YA TAIFA YA SOKA YA WALEMAVU (TEMBO WARRIORS) KUSHIRIKI MASHINDANO YA AFRIKA NCHINI ANGOLA MWEZI UJAO

$
0
0

Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike akiongea machache mbele ya wachezaji na viongozi wa Timu ya Soka ya Taifa ya Soka ya Walemavu TEMBO WARRIORS kabla ya kukaikabidhi timu hiyo msaada wa shilingi milioni 10 uliotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuisaidia timu hiyo kushiriki kwenye mashindano ya mpira wa miguu kwa watu wenye ulemavu Afrika (CANAF) yaliyopangwa kuanza Oktoba 1, mwaka huu huko nchini Angola kwenye hafla fupi iliyofanyika katika Studio zaShirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Mikocheni jijini Dar es salaam leo Septemba 22, 2019.





Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike akimkabidhi Rais wa Shirikisho la Soka la Watu Wenye Ulemavu Tanzania (TAFF) Shilingi Milioni 10 taslimu mbele ya wachezaji na viongozi wa Timu ya Soka ya Taifa ya Soka ya Walemavu TEMBO WARRIORS ukiwa ni msaada uliotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuisaidia timu hiyo kushiriki kwenye mashindano ya mpira wa miguu kwa watu wenye ulemavu Afrika (CANAF) yaliyopangwa kuanza Oktoba 1, mwaka huu huko nchini Angola kwenye hafla fupi iliyofanyika katika Studio za Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Mikocheni jijini Dar es salaam leo Septemba 22, 2019



Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike akiongea baada ya kumkabidhi rais wa Shirikisho la Soka la Watu Wenye Ulemavu Tanzania (TAFF) Bw. Peter Sarungi Shilingi Milioni 10 taslimu mbele ya wachezaji na viongozi wa Timu ya Soka ya Taifa ya Soka ya Walemavu TEMBO WARRIORS ukiwa ni msaada uliotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuisaidia timu hiyo kushiriki kwenye mashindano ya mpira wa miguu kwa watu wenye ulemavu Afrika (CANAF) yaliyopangwa kuanza Oktoba 1, mwaka huu huko nchini Angola kwenye hafla fupi iliyofanyika katika Studio za Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Mikocheni jijini Dar es salaam leo Septemba 22, 2019



Katibu Mkuu wa Tanzania Paralympic Committee Tuma Dandi ambaye pia ni mwanahabari wa TBC baada ya Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike kumkabidhi Rais wa Shirikisho la Soka la Watu Wenye Ulemavu Tanzania (TAFF) Shilingi Milioni 10 taslimu mbele ya wachezaji na viongozi wa Timu ya Soka ya Taifa ya Soka ya Walemavu TEMBO WARRIORS ukiwa ni msaada uliotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuisaidia timu hiyo kushiriki kwenye michezo ya dunia nchini Angola baadaye mwaka huu kwenye hafla fupi iliyofanyika katika studio za Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Mikocheni jijini Dar es salaam leo Septemba 22, 2019



Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Bw. Gerson Msigwa akiongea machache baada ya Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike kumkabidhi Rais wa Shirikisho la Soka la Watu Wenye Ulemavu Tanzania (TAFF) Shilingi Milioni 10 taslimu mbele ya wachezaji na viongozi wa Timu ya Soka ya Taifa ya Soka ya Walemavu TEMBO WARRIORS ukiwa ni msaada uliotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuisaidia timu hiyo kushiriki kwenye mashindano ya mpira wa miguu kwa watu wenye ulemavu Afrika (CANAF) yaliyopangwa kuanza Oktoba 1, mwaka huu huko nchini Angola kwenye hafla fupi iliyofanyika katika Studio za Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Mikocheni jijini Dar es salaam leo Septemba 22, 2019



Wachezaji wa wachezaji na viongozi wa Timu ya Soka ya Taifa ya Soka ya Walemavu TEMBO WARRIORS akifurahia baada ya Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike kumkabidhi Rais wa Shirikisho la Soka la Watu Wenye Ulemavu Tanzania (TAFF) Shilingi Milioni 10 taslimu mbele yao ukiwa ni msaada uliotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuisaidia timu hiyo kushiriki kwenye mashindano ya mpira wa miguu kwa watu wenye ulemavu Afrika (CANAF) yaliyopangwa kuanza Oktoba 1, mwaka huu huko nchini Angola kwenye hafla fupi iliyofanyika katika studio za Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Mikocheni jijini Dar es salaam leo Septemba 22, 2019



Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Bw. Gerson Msigwa katika picha ya pamoja na Rais wa Shirikisho la Soka la Watu Wenye Ulemavu Tanzania (TAFF) Bw. Peter Sarungi, wachezaji na viongozi wa Timu ya Soka ya Taifa ya Soka ya Walemavu TEMBO WARRIORS na wafanyakazi wa TBC Kitengo cha Michezo na viongozi wa Shirika baada ya kukabidhi msaada wa shilingi milioni 10 uliotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuisaidia timu hiyo kushiriki kwenye mashindano ya mpira wa miguu kwa watu wenye ulemavu Afrika (CANAF) yaliyopangwa kuanza Oktoba 1, mwaka huu huko nchini Angola kwenye hafla fupi iliyofanyika katika studio za Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Mikocheni jijini Dar es salaam leo Septemba 22, 2019 PICHA NA IKULU

TIGO TANZANIA YACHANGAMKIA fursa za Mkutano wa Mawaziri wa SADC

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji kutoka Tigo, Simon Karikari, akiwasilisha mada kuhusu Upatakanaji wa huduma za Mawasiliano vijijini, wakati wa Mkutano  wa Mawaziri wa SADC wa Sekta ya Tehama, Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewa, uliofanyika katika Ukumbi wa JNICC DSM, jana. Tigo ni kampuni pekee yenye internet ya kasi ya 4G+ na ndio mtoa huduma rasmi ya Wi-Fi katika wa mkutano huo.

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AWAAPISHA VIONGOZI MBALIMBALI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Mussa Lulandala kuwa Balozi katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
 
Viongozi mbalimbali walioapishwa wakila Kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi wa Umma Ikulu jijini Dar es Salaam.





Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kuwaapisha Viongozi mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Bw. Loata Sanare kuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Bw. Alphayo Kidata kuwa Katibu Tawala mkoa wa Mtwara katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Ally Possi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Bi. Mary Maganga kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango anayeshughulikia Utawala katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Viongozi wengine wa Serikali Kuu katika picha ya pamoja na viongozi waliopishwa Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Sanare kushoto pamoja na Mkuu wa Mkoa wa zamani wa Morogoro Dkt Stephen Kebwe mara baada ya hafla fupi ya Uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

UONGOZI TANGA CEMENT WAJIVUNIA MAFANIKIO,WAZUNGUMZIA UMUHIMU WA KUONGEZEWA MABAHEWA KUSAFIRISHA SARUJI

$
0
0
Na Said Mwishehe,Michuzi TV -Tanga

UONGOZI wa kiwanda cha kutengeneza Saruji cha Tanga Cement mkoani Tanga kimesema kinajivunia mafanikio waliyonayo yakiwemo ya kuendelea kutengeneza saruji ya kiwango cha ubora wa kimataifa na kuwa na soko la uhakika.

Hata hivyo pamoja na mafanikio hayo, uongozi huo umesema pamoja na kuingia makubaliano na Shirika la Reli Tanzania(TRC), kuna changamoto ya  uchache wa mabehewa kwa ajili ya kusafirisha saruji jambo ,hivyo wametoa rai ya kuongeza mabehewa japo 300.

Hayo yameelezwa wakati ziara ya waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari nchini ambao wamepata fursa ya kutembelea kiwanda hicho kuona shughuli mbalimbali za uzalishaji, kupata taarifa za mafanikio na changamoto.

Akizungumza jana mkoani hapa, Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Tanga Cement Reinhardt Swart amewaambia waandishi wa habari kiwanda kinajivunia kuendelea kuzalisha saruji iliyo bora ukilinganisha na washindani wao kwa kuwa na viwango vya ubora wa Kimataifa na hivyo kuwa na soko la uhakika.

"Mkakati wetu siku zote ni kuendelea kuzalisha saruji inayokidhi viwango vya ubora wa kimataifa.Gharama tunazotumia ni kubwa katika uzalishaji ambazo zinatokana na umeme, mafuta na klinka ambayo inatumika wakati wa kutengeneza saruji kiwandani,"amesema Swart.

Alipoulizwa kuhusu usafiri wa kutumia reli kusafirisha saruji, Mkurugenzi Mtendaji huyo amesema mara nyingi wamekuwa wakipata changamoto ya kutokuwepo kwa mabehewa ya kutosha ambapo hali hiyo inasababisha kiwanda kushindwa kufikisha sokoni zaidi ya tani 10,000 - 15,000 kwa mwezi.

Amefafanua kwamba changamoto hiyo inasababisha kuongezeka kwa bei ya saruji kutokana na kukosekana kwa bidhaa sokoni.Hata hivyo amesema ni nafuu na rahisi sana kusafirisha saruji kwa kutumia reli na kuongeza kuwa inakuwa nafuu zaidi endapo unasafirisha mzigo maeneo ya mbali zaidi. 

"Ni rahisi kwa upande wa kampuni na kwa upande wa serikali pia kwani matumizi ya reli yanapunguza kwa kiasi kikubwa uharibifu wa barabara hivyo kufanya miundombinu ya umma kubaki salama. Ukweli uliopo kama kampuni tunapendelea zaidi matumizi ya reli,"amesema.

Ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa kwa mwezi kiwanda kinahitaji zaidi ya mabehewa 455, hivyo kama watapata mabehewa 300 yatakayojikita kwao itakuwa heri zaidi na kilio cha kutokuwepo kwa mabehewa kitapungua.

"Tunaweza kupeleka mabehewa 40 kutoka Tanga mpaka Arusha ndani ya wiki moja. Kila behewa linaweza kubeba tan 40 za saruji,"amesema wakati anafafanua kwa waandishi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Tanga Cement Mkoani Tanga,Reinhardt Swart akiwaeleza Wahariri wa Vyombo vya habari mbalimbali pamoja na waandishi waliotembelea Kiwanda chicho mwishoni mwa wiki,namna wanavyojivunia mafanikio waliyonayo yakiwemo ya kuendelea kutengeneza saruji ya kiwango cha ubora wa kimataifa na kuwa na soko la uhakika.Pichana na Michuzi JR.

Wahariri wa Vyombo vya habari mbalimbali pamoja na waandishi waliotembelea Kiwanda cha Tanga Cement wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Tanga Cement Mkoani Tanga,Reinhardt Swart alipokuwa akiwaeleza shughuli mbalimbali zifanywazo na Kiwanda hicho,mwishoni mwa wiki. 


Baadhi ya Wakuu wa vitengo na maofisa wa Kiwanda cha Tanga Cement wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri katika kikao hicho kilichowakutanisha Wahariri wa Vyombo vya Habari mbalimbali, Waandishi wa habari na Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda hicho,Reinhardt Swart ambaye alieleza mambo mbalimbali yahusuyo kiwanda hicho.


Baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari na waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Tanga Cement Mkoani Tanga,Reinhardt Swart wakati alipokuwa akizungumza. 
Mmoja wa Wahariri akiuliza swali kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Tanga Cement Mkoani Tanga,Reinhardt Swart. 

Baadhi ya Wakuu wa vitengo na maofisa wa Kiwanda cha Tanga Cement wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri katika kikao hicho kilichowakutanisha Wahariri wa Vyombo vya Habari mbalimbali, Waandishi wa habari na Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda hicho,Reinhardt Swart ambaye alieleza mambo mbalimbali yahusuyo kiwanda hicho.Picha na Michuzi JR.
Meneja Rasilimali Watu wa Kiwanda cha Tanga Cement,Diana Malambugi akifafanua ni namna gani Kampuni hiyo imekuwa ikitoa ajira katika ngazi mbalimbali za Idara za Kiwanda hicho,ikiwemo na namna ya kuhakikisha mambo ya jinsia yanazingatiwa huku akibainisha kuwa Katika kiwanda hicho suala hilo limezingatiwa vilivyo.
Mhandisi Gadiel Benjamin wa Kiwanda cha Tanga Cement akionesha sampuli za udongo na madini ya aina ya Limestone yanayotumika kutengenezea Saruji. katika kiwanda hicho wakati alipotoa mada kuhusu uzalishaji wa Saruji,mbele ya Wahariri wa Vyombo vya habari mbalimbali pamoja na waandishi waliotembelea Kiwanda hicho mwishoni mwa wiki.
Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Kiwanda cha Tanga Cement ,Nuru Mtanga akifafanua jambo na kuwashukuru wahariri wa vyombo vya habari na waandishi wa habari kutokana na namna wanavyotoa ushirikiano kwa kiwanda hicho.

Msimamizi wa Uzalishaji wa kiwanda cha Tanga Cement ,Logolieki Mollel akitoa maelezo kwa wahariri wa vyombo vya habari na waandishi wa habari  nama saruji inavyochanganywa kitaalamu na hatimae kuipata Saruji iliyo bora na yeye kiwango cha Kimataifa
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live




Latest Images