Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

UJERUMANI YAIPATIA TANZANIA MSAADA WA SH. BIL. 32.7 KUSAIDIA AFYA YA MAMA NA MTOTO

$
0
0
Na Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam

Ujerumani kupitia Benki yake ya Maendeleo (KFW) imeipatia Tanzania msaada wa Euro milioni 13, sawa na sh. bilioni 32.74 kwa ajili ya kuboresha afya ya uzazi na watoto wachanga na pia kukinga maambukizi ya Virusi vya UKIMWI (VVU) kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto kupitia mradi ujulikanao kama Tumaini la Mama.

Hafla ya utiaji saini mkataba wa msaada huo imefanyika Jijini Dar es Salaam kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James kwa niaba ya Tanzania na Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Ujerumani Dkt. Annika Calov.

Msaada huo ni kwa ajili ya kutekeleza awamu ya tatu ya mradi huo unaotekelezwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ambapo umelenga kuwapatia huduma akima mama na watoto wanaotoka katika kaya masikini

Alisema kupitia mradi huo pia vifaa tiba vinavyohusiana na afya ya uzazi vyenye thamani ya zaidi ya shilingi za Tanzania milioni 900 katika vituo vya Afya vilivyoko katika mikoa iliyochaguliwa kwa ajili ya kuimarisha utoaji wa huduma za afya vimetolewa.

Mradi huu ulianza mwaka 2012 ambapo Serikali ya Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani kupitia Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KfW) ilitoa Euro milioni 13 sawa na shilingi za Tanzania bilioni 25.5 kupitia mkataba uliosainiwa tarehe 2 Desemba 2009. 

“Awamu ya pili ya mradi ilianza mwaka 2016 ambapo Ujerumani ilitoa msaada wa Euro milioni 20 sawa na shilingi za Tanzania bilioni 48.2 kupitia mkataba uliosainiwa tarehe 15 Machi 2015. Siku ya leo Serikali yenu imeahidi kupitia mkataba huu, kutoa msaada mwingine wa Euro milioni 13 sawa na shilingi za Tanzania bilioni 32.4 kutekeleza awamu ya tatu ya mradi, tunaishukuru sana,” alisema Bw. James. 

James alisema mradi huo ni muhimu kwa kuzingatia kwamba unaongeza nguvu katika juhudi za Serikali za kupunguza vifo vya mama na mtoto lakini pia kuongeza tabia ya kutumia bima ya afya kwa watanzania na hii inaenda sambamba na awamu ya Pili ya Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano na awamu ya Tatu ya MKUZA. 

“Kwa mfano, katika awamu ya Pili ya Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano, Serikali imelenga kwamba, hadi mwaka 2020: Vifo vitokanavyo na uzazi vipungue kutoka 454 mwaka 2015 hadi 250 katika kila vizazi hai 100,000; muda wa kuishi uongezeke hadi miaka 66 kutoka miaka 56; na maambukizi ya VVU na UKIMWI yapungue kutoka asilimia 9 hadi 3,” alisema .

Naye Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Ujerumani Dkt. Annika Calov alisema nchi yake inajivunia uhusiano mzuri na Tanzania na kwamba mradi huo wa Tumaini la Mama umelenga kuboresha afya akina mama wanaotoka katika familia maskini.

“Lengo kubwa ni kuboresha afya za mama na mtoto na kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto na kwa kuanzia mradi huu umekijita katika mikoa mitano ya Mbeya, Songwe, Tanga, Lindi na Mtwara,” alisema Calov.

Akizungumza katika hafla hiyo Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bernard Konga alisema tangu mwaka 2012 mradi ulipoanza, jumla ya akinamama 1,157,191 wamenufaika na bima ya afya kupitia NHIF na kaya maskini 627,000 zimenufaika na huduma za CHF kwa kulipiwa ada za kujiunga. 

“Akina mama na watoto wao wanapatiwa huduma kwa njia ya bima ya afya kupitia vituo vya afya 1097 vilivyoko katika mikoa hiyo iliyolengwa pamoja na mfuko kutoa vifaa tiba kwenye vituo,” alisema Konga. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (katikati), Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KFW) hapa nchini Dkt. Anna Calov (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NIHF) Bw. Bernard Konga wakionesha Mikataba ya msaada kati ya Serikali ya Tanzania na Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani wa Euro milioni 13, sawa na shilingi za Tanzania bilioni 32.74 kwa ajili ya kuboresha afya ya uzazi na watoto wachanga na pia kukinga maambukizi ya Virusi vya UKIMWI (VVU) kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto kupitia mradi ujulikanao kama “Tumaini la Mama. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (katikati) akitia saini Mkataba wa msaada kati ya Serikali ya Tanzania na Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani kupitia Benki yake ya Maendeleo (KFW) wa Euro milioni 13, sawa na shilingi za Tanzania bilioni 32.74 kwa ajili ya kuboresha afya ya uzazi na watoto wachanga na pia kukinga maambukizi ya Virusi vya UKIMWI (VVU) kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto kupitia mradi ujulikanao kama “Tumaini la Mama. Kushoto ni Mkurugenzi wa KFW nchini, Dkt. Anna Calov na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NIHF) Bw. Bernard Konga. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (katikati), akitia saini Mkataba wa msaada kati ya Serikali ya Tanzania na Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani kupitia Benki yake ya Maendeleo (KFW) wa Euro milioni 13, sawa na shilingi za Tanzania bilioni 32.74 kwa ajili ya kuboresha afya ya uzazi na watoto wachanga na pia kukinga maambukizi ya Virusi vya UKIMWI (VVU) kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto kupitia mradi ujulikanao kama “Tumaini la Mama. Kushoto ni Mkurugenzi wa KFW nchini, Dkt. Anna Calov na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NIHF) Bw. Bernard Konga. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano-Wizara ya Fedha na Mipango)

KADA CCM AVAMIWA DAR, AKATWAKATWA MAPANGA KICHWANI, ATUPWA BARABARANI

$
0
0

 
*Ni yule aliyegombea ubunge jimbo la Vunja..

*Akutwa roud about ya Kawe akiwa hajitambui


Na Said Mwishehe,Michuzi TV

KADA wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)ambaye pia amewahi kugombea ubunge katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 katika Jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro Inocent Shirima amenusurika kufa baada ya kuvamiwa na kukatwa mapanga kichwani akiwa karibu na nyumbani kwake eneo la Goga Kinzugi jijini Dar es Salaam.

Kwa sasa Shirima anaendelea kupata matibabu katika moja ya Hospitali iliyopo jijini Dar es Salaam ili kuokoa maisha yake kutokana na hal yake kutokuwa nzuri kiafya.

Akizungumza na Michuzi Blogu leo Septemba 9,2019 kwa njia ya simu Shirima ameelezea hatua kwa hatua tukio la kuvamiwa kwake a kisha kujeruhiwa kwa kukatawa mapanga kichwani ambapo amesema tukio hilo lilitokea Jumatano ya wiki iliyopita saa tano usiku.

Amesema kuwa akiwa anarejea nyumbani , umbali wa mita 300 kutoka katika nyumba yake kulikuwa na watu wenye bodaboda na mmoja alikuwa amesimama barabarani kama vile anatengeneza bodaboda na alipofika eneo hilo alisimamishwa kama anaombwa msaada.

"Kwa ilikuwa ni maeneo ya karibu na nyumbani sikuwa na wasiwasi, hivyo nikasimamisha gari yangu , baada ya kufungua kioo cha gari nikashtukia nimepigwa na kitambaa usoni.Hiyo ilitokea hata kabla ya kuuliza kuna kitu gani.

"Baada ya hapo inaonekana walichukua gari na kuanza kuzunguka na mimi hadi saa saba usiku.Walinipiga kwa mapanga na nadhani waliamini wameshaniua, hivyo wakaenda kunitelekeza katika eneo la round about ya barabara ya Kawe.Lengo lao ilikuwa ni kuniweka hapo ili nigogwe na gari itakayopita,"amesema Shirima.

Ameongeza kuwa wakati wanafanya hayo yote hakuwa anajitambua kwani alishapoteza fahamu na ndio maana waliokuwa wanafanya unyama huo waliamini ameshakufa."Wamenikata mapanga, wakaniburuza kwenye lami na kisha kunitelekeza nije nigongwe na gari."

Amefafanua kuwa baada ya kumjeruhi na kumuacha eneo hilo, watu hao wamechukua fedha zake Sh.milioni 11 ambazo alichelewa kuzipeleka katika duka la saruji kwani anajihusisha na biashara ya kuuza tofali.Pia wamechukua flashi mbili,simu ya mkononi la laptop.

Hata hivyo amesema kuwa baada ya kutupwa eneo hilo, kuna vijana wengine wa bodaboda wa maeneo ya nyumbani kwake baada ya kumuona akiwa hapo walisimamisha bodaboda zao kwa ajili ya kumpa msaada na hata wao walikuwa wanajua ameshakufa.

"Walidhani ni maiti na baada ya kuniona napumua ndipo waliponchukua na kunipeleka Hospitali ya Kairuki ambapo pale nilifanyiwa opereshani kwa saaa nane,"amesema Shirima.

Alipoulizwa kwa sasa hali yake ikoje ?Amejibu hali yake bado mbaya na kuna eneo ambalo amehifadhiwa akiendelea kupata matibabu.Hata hivyo amesema kwa kuwa yeye ni mwanasiasa kuna maswali mengi anajiuliza katika tukio hilo.

"Kama ni majambazi walishanidhibiti na nikawa sijitambui kwanini watake kuniua kwa kunikata mapanga kichwani?Ndani ya gari kulikuwa na vitu muhimu zaidi wameacha, kulikuwa na nyaraka muhimu hawakuchukua, kwanini? Hili tukio linaleta wakati mgumu kwangu na familia yangu ambayo kwa sasa haina amani kabisa,"amesema Shirima.

Amesema kama lengo lao ni kumuua maana yake wataendelea kumtafuta tena kwani walichotarajia sicho ambacho kimetokea."Waliamini wameniua , lakini niko hai unadhani nini ambacho kitaendelea?"

Alipoulizwa kama tayari Polisi wanafahamu tukio hilo, Shirima amejibu Polisi wanazo taarifa na amesikia wanaendelea na uchunguzi lakini yeye kama yeye bado hajahojiwa na polisi kuhusu tukio hilo ikiwa pamona na kuchukua maelezo yake.

Alipoulizwa anahisi nini kutokana na tukio hilo, amejibu hana jibu la moja kwa moja lakini kwa kuwa yeye ni mwanasiasa huenda ndani yake imeingia siasa 

"Tukio hili lina mambo mengi, katika uchaguzi uliopita niligombea ubunge na kushika nafasi ya pili.Nakumbuka wakati wa uchaguzi kule nyumbani Moshi watu walivamia nyumba yangu, walimkuta baba yangu mdogo ambaye walimuua kwa kumchinja,"amesema Shirima.

Amesema anakumbuka siku hiyo alipanga kusafiri lakini alibadili safari , hivyo waliovamia nyumba yake waliamini yupo lakini baada ya kufika wakamkuta baba yake mdogo na ndipo walipoamua kumuua.

"Mawazo yangu nahisi hili tukio lina siasa na sasa tunakwenda kwenye uchaguzi sijui nini kitatokea tena.Siamini katika ujambazi maana kama ni majambazi walishanidhibiti iweje wanipige mapanga,"amesisitiza Shirima.

Rais Magufuli amjulia hali Baba Askofu Yuda Ruwaichi aliyelazwa MOI Jijini Dar es Salaam

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Madaktari wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili pamoja na Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) wakimuombea Sala Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Dar es Salaam Mhashamu Yuda Thadeus Ruwa’ichi ambaye anapatiwa matibabu katika Taasisi hiyo ya MOI mara baada ya kufanyiwa upasuaji wa Kichwa jana usiku.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Madaktari wa Muhimbili pamoja na MOI mara baada ya kumjulia hali Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Dar es Salaam Mhashamu Yuda Thadeus Ruwa’ichi ambaye amelazwa katika Taasisi hiyo ya MOI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwajulia hali wagonjwa wengine waliolazwa MOI.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisaini Kitabu mara baada ya kuwasili katika Kituo cha Polisi cha Selander Bridge wakati akitokea katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli ametembelea Kituo cha Polisi cha Selander Bridge wakati akitokea katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiondoka mara baada ya kutembelea kituo hicho. PICHA NA IKULU


NMB YAENDELEA KUWA MKOMBOZI KWA JAMII, YAKABIDHI MSAADA WA VIFAA TIBA KITUO CHA AFYA JKT MPWAPWA.

$
0
0
Benki ya NMB imeendelea kuwa mkombozi kwenye Jamii maeneo mbalimbali hapa Nchini kutokana na kutoa misaada sehemu zenye changamoto kubwa.

Hayo yalielezwa na Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mkoani hapa alipozungumza wakati wa kupokea msaada wa vifaa tiba vilivyotolewa na Benki ya Nmb jana kwa ajili ya Kituo cha afya cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Kikosi cha 826 Mpwapwa .

Shekimweri alisema benki ya NMB imeendelea kuwa mkombozi katika Jamii kutokana na kutoa misaada kwenye maneo yenye changamoto kubwa ya mahitaji.

“Mfano ni hivi vifaa tiba mlivyokabidhi leo ,tunajua wote jinsi eneo la kutolea huduma za afya lilivyo na changamoto ,watu ni wengi katika Jamii wanaofika hapa kwa jili ya matibabu,ni kweli benki mnaigusa jamaii moja kwa moja”alisema.

Hata hivyo aliwashukuru NMB kwa kuendelea kutoa misaada katika Wilaya hiyo kwa sababu kwa mwaka huu hiyo ni mara ya tatu kwa kupata msaada wa mabati kwa baadhi ya shule za Msingi pamoja na madawati .

Naye Mwakilishi wa Mkuu wa JKT Nchini Kanali Festus Mang’wela aliwashukuru benki ya Nmb kwa msaada waliotoa kwa ajili ya kituo hicho cha afya cha 826 Mpwapwa Mkoani Dodoma .

Kanali Mang’wela alisema kituo hicho kinahudumia watu wengi wakiwemo familia za askari,Askari wenyewe na Jamii inayokizunguka Kikosi hicho . Alibainisha kuwa vifaa hivyo walivyopokea vitawasaidia kutokana na kikosi hicho kuanza kupokea wanafunzi wa kidato cha sita wanaofika kwa ajili ya kozi maalumu ya kijeshi ya miezi mitatu tangu mwaka jana.

Kwa upande wake Meneja wa Benki ya Nmb Kanda ya Kati Nsolo Mlozi alisema wamekabidhi msada huo wa vifaa tiba wenye thamni yash milioni tano. Alivitaja vifaa hivyo kuwa ni vitanda vitano vya kawaida ,mashuka 25,magodoro tano na vitanda vya kujifungulia akinamama viwili vyote vikiwa na thamani hiyo.

Mlozi alisema benki hiyo inasaidia jamii katika sekta kuu nne ambazo ni elimu kwa kuchangia madawati na mabati ya kuezekea ,afya kwa kutoa vifaa tiba ,majanga na kutoa elimu kwa wananchi namna ya utunzaji wa fedha .

Hata hivyo alisema mpaka sasa benki hiyo imeshatoa misaada wenye thamni ya kiasi cha zaidi ya sh milioni 110 kwa jamii Mkoa wa Dodoma.
  Mkuu wa Wilaya Mpwapwa, Jabiri Shekimweri (wa kwanza kushoto)  akipokea msaada wa mashuka pamoja na vifaa tiba kutoka kwa  Meneja wa Benki ya Nmb Kanda ya Kati Nsolo Mlozi (wapili kulia) akiwa Meneja Mwandamizi Mahusino ya Kibenki na Seriaklia NMB ,Josephine Kulwa(kulia) wakimkabidhi ,msaada huo uliotolewa kwa ajili ya Kituo cha Afya cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Kikosi cha 826 Mpwapwa Mkoani Dodoma, NMB jana  ilikabidhi msaada huo wenye thamani ya zaidi ya sh milioni tano,katikakati ni  mwakilishi wa Mkuu wa JKT Kanali Festus Mng'wela .
 Meneja wa Benki ya Nmb Kanda ya Kati Nsolo Mlozi (kulia) akikabidhi msaada wa kitanda, mashuka na vifaa tiba kwa ajili ya Kituo cha afya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kikosi 826 Mpwapwa Mkoani Dodoma. Jana NMB ilikabidhi msadaa wa sh milioni tano wa vifaa hivyo ,wengine ni Mkuu wa Wilaya Mpwapwa Jabiri Shekimweri (wa kwanza kushoto) na Mkuu wa Kikosi Hicho Luten Kanal Mohamed Karuma na mwakilishi wa Mkuu wa JKT Kanali Festus Mng'wela waliobaki ni staafu wa benki ya NMB

tukio la Uzinduzi Wa Programu ya Vodacom Digital Accelerator jijini Dar

$
0
0



Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC Hisham Hendi (katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa programu ya “Vodacom Digital Accelerator,” yenye lengo la kusaidia wajasiriamali wapya na wanaoendelea kuanzisha biashara yenye faida na yenye kuzalisha kipato kupitia sekta ya teknolojia Vodacom imeshirikiana na kampuni ya Smart Codes. Kushoto ni Mkurugenzi wa Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia na kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Smart Codes, Edwin Bruno

Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC Hisham Hendi (katikati) na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Smart Codes, Edwin Bruno (Kulia) wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Uhusiano na Mawasiliano Rosalynn Mworia, wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu uzinduzi wa programu ya “Vodacom Digital Accelerator,” yenye lengo la kusaidia wajasiriamali wapya na wanaoendelea kuanzisha biashara yenye faida na yenye kuzalisha kipato kupitia sekta ya teknolojia ( Smart lab) Vodacom imeshirikiana na kampuni ya Smart Codes.

Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC Hisham Hendi (katikati) na Mkurugenzi wa Uhusiano na Mawasiliano wa kampuni hiyo Rosalynn Mworia (Kushoto), wakimsikiliza Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Smart Codes, Edwin Bruno wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu uzinduzi wa programu ya “Vodacom Digital Accelerator,” yenye lengo la kusaidia wajasiriamali wapya na wanaoendelea kuanzisha biashara yenye faida na yenye kuzalisha kipato kupitia sekta ya teknolojia. Codes.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa programu ya “Vodacom Digital Accelerator,” yenye lengo la kusaidia wajasiriamali wapya na wanaoendelea kuanzisha biashara yenye faida na yenye kuzalisha kipato kupitia sekta ya teknolojia ( Smart lab) hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam ambapo kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania Plc imeshirikiana na kampuni ya Smart Codes.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC Hisham Hendi akipiga picha "selfie" na wadau pamoja na wageni waalikwa kwenye tafrija mchapalo ya uzinduzi wa programu ya Vodacom Digital Accelerator
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC Hisham Hendi akizungumza kwenye hadhara ya tafrija mchapalo ya uzinduzi wa programu ya “Vodacom Digital Accelerator,” yenye lengo la kusaidia wajasiriamali wapya na wanaoendelea kuanzisha biashara yenye faida na yenye kuzalisha kipato kupitia sekta ya teknolojia, Vodacom imeshirikiana na kampuni ya Smart Codes.

Wafanyakazi wa Vodacom wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa programu ya Vodacom Digital Accelerator jijini Dar Es Salaam jana.
Kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi inayoongoza Vodacom Tanzania Plc na Smart Lab leo wamezindua kampeni ya “Vodacom Digital Accelerator,” programu yenye lengo la kusaidia wajasiriamali wapya na wanaoendelea kuanzisha biashara yenye faida na yenye kuzalisha kipato.


Programu hii ambayo itakuwa inafanyika kila mwaka ina lengo la kubainisha na kusaidia wajasiriamali wanaochipukia katika sekta ya simu, mawasiliano, teknolojia katika taasisi za kifedha, habari, afya, elimu na biashara ya mtandao (E-commerce) watakuwa na hatua tatu ambazo zinajumuisha kutuma maombi, kuchaguliwa na hatua ya kuongeza kasi ya biashara (Mchapuo).

Akiongea katika hafla ya uzinduzi, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC Bwana Hisham Hendi amesema kwamba ushirikiano kati ya Vodacom Tanzania na SmartCodes ni hatua muhimu kuelekea katika kutoa fursa kwa wajasiriamali wanaoanza kwa kupitia sekta ya teknolojia ambayo itapelekea kuwepo kwa mifumo inayofanya kazi ambayo itanufaisha jamii, hususani kwa vijana nchini. Amewahamasisha vijana wengi zaidi kuwa wabunifu na kutumia fursa hii kama njia ya kujiwezesha kiuchumi kupitia katika kutatua matatizo ya maendeleo ya jamii katika jamii zao.

“Kampuni ya Vodacom mara zote inakusudia kuleta mabadiliko endelevu yenye manufaa kwa jamii ambako tunaendesha shughuli zetu sambamba na mtazamo wa mkakati wetu wa kibiashara na programu ya Vodacom Accelerator inakusudia kuthibitisha suala hilo.” Aliongeza bwana Hisham.

Alifafanua zaidi kwamba kama kampuni ambayo inakusudia kufikisha Tanzania katika ulimwengu wa kidigitali, kampuni ya Vodacom Tanzania inahamasisha fikra za biashara katika sekta ya teknolojia ambazo zitaleta mabadiliko endelevu.

“Teknolojia ya Digitali haibadilishi namna tunavyofanya biashara Afrika tu bali pia inabadilisha tunavyotazama na kutatua masuala yanayohusu maendeleo. Kwa hiyo ni kwa heshima kubwa kwamba tutatengeneza fursa ya kutambua fikra kama hizo, kuziunga mkono na kuziboresha kwa lengo la kukuza manufaa yake katika jamii, Alisema.

Aliongeza pia, Vodacom imeshirikiana na Smart Lab, kituo maarufu cha ubunifu ambacho kinakusudia kuleta matokeo halisi ambayo yatabadilisha mwelekeo wa ubunifu wa mifumo ya kiuchumi. Kwa hiyo, hii itakuwa ni fursa kwa wafanyabiashara wanaoanza na wavumbuzi katika vigezo vya kiteknolojia vilivyochaguliwa kuonyesha bidhaa zao na kunufaika kutokana na programu hii ikiwemo kupata mpango wa ushirikiano na kampuni ya Vodacom, ushauri, msaada wa kitaalamu, masoko na fursa ya kupata nafasi ya kuwa karibu na mtandao mkubwa wa washirika wa kampuni za Vodacom na Smart Lab na hatimaye wateja kuweza kufanya majaribio na kupata uzoefu wa masuluhisho yao.



Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Smart Codes bwana Edwin Bruno ameonyesha furaha yake kuhusu programu hii mpya kwa kusema kwamba, “Tunafuraha kuwa sehemu ya programu ya “Vodacom Accelerator” na kwa kushirikiana na Vodacom, kwa pamoja tunatumaini kutengeneza jukwaa la chapa ya kipekee kwaajili ya vijana wenye ari katika teknolojia. Progamu hii inaenda sambamba na mkakati wetu wa shirika wa kupeleka ujumbe kuhusu kusaidia vijana walioko katika zama za digitali na tunashukuru kwa Vodacom Tanzania ambao wameona haja ya kutengeneza mzunguko mpya wa hadithi za mafanikio ya wajasiriwamali wa kiafrika wanaojenga kampuni za teknolojia zinazokuwa kwa kasi ambao wanatoka ndani ya nchi.”

Alieleza kwa kina kwamba “jamii ya wavumbuzi na wabunifu imeibuka nchini Tanzania kutoka katika vituo vichache mwaka 2011 mpaka kufikia zaidi ya 45 mwaka 2019. Lakini kumekuwa na ushirikishwaji mdogo kutoka katika upande wa mashirika ambapo kampuni ya Vodacom katika ushirikiano huu na kampuni ya Smart Lap itaongoza katika kuziba pengo hilo. Tunatazamia katika zama zijazo za ushirikishwaji wa teknolojia kwa Tanzania ambayo ina mifumo yenye kuleta mabadiliko ambayo italeta manufaa kwa kizazi kijacho.”

Katika kipindi cha programu ambapo pia kina lengo la kuongeza rasilimali za shirika, mtandao, washauri, na washirika, washiriki watawasilisha maendeleo ya mifumo yao kwa jopo la wawekezaji na washiriki wengine katika mwisho wa kipindi cha miezi mitatau ya kuongeza kasi, ambapo mshindi atapata msaada zaidi kutoka Vodacom Tanzania Plc, Smart Lab na washirika wake kwa muda wa nyongeza wa miezi 6.

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Vodacom Rosalynn Mworia alisema kwamba kampuni ya Vodacom imewekeza zaidi ya dola za kimarekani 150,000 katika mpango huu ili kusaidia vijana kielimu na utaalamu kusudi waweze kufikia malengo yao ya kibiashara.

Kampuni ya Vodacom Tanzania inaongoza katika mageuzi ya sekta ya teknolojia Tanzania (fintech) ambayo ni moja ya sekta zinazokuwa kwa kasi zaidi barani Afrika. Na wakati huo huo teknolojia ikiwa inaendelea kusaidia uendeshaji wa kila siku wa biashara na huduma.

Uzinduzi pia ulihudhuriwa na wadau wengine kutoka serikalini, jamii ya wawekezaji, vituo vya uvumbuzi, taasisi za kifedha, mashirika, wafanyabiashara chipukizi, maprofesa wa vyuo vikuu, washirika wa maendeleo, Mabalozi na watendaji wengine katika teknolojia na jamii ya wavumbuzi.

African Refugee Convention turns 50 to warm welcome

$
0
0
The High Commissioner for Refugees, Sadruddin Aga Khan (right) and OAU Secretary General Mr. Diallo Telli at the signing of the OAU Convention in 1969 in Geneva, Switzerland ©UNHCR


This week, 50 years ago, Organization of African Unity (OAU) member states gathered in Addis Ababa, Ethiopia, to adopt the OAU Convention Governing the Specific Aspects of Refugee Problems in Africa (1969 OAU Refugee Convention).

UNHCR, the UN Refugee Agency, warmly welcomes this milestone for the Convention, which was adopted on September 10, 1969 as the world’s first regional refugee protection treaty and the regional complement to the 1951 UN Refugee Convention. “It was a progressive treaty that expanded on the definition of refugee among other advances, and it remains relevant half-a-century later,” said Cosmas Chanda, UNHCR’s representative to the African Union (AU).

In 1969, many African states had recently gained their independence, while others were still under colonial or minority rule. The Convention reflects this context. In addition to the international refugee definition from the 1951 Convention, the 1969 OAU Refugee Convention affords refugee protection to individuals who fled because of “external aggression, occupation, foreign domination or events seriously disturbing public order.” This broader regional definition, as well as the Convention’s provisions on voluntary repatriation and solidarity, ensure its influence and value till this day.

The 1969 OAU Refugee Convention also addresses responsibility sharing, an issue that has now gained global prominence with the affirmation of the Global Compact on Refugees (GCR) in the UN General Assembly in December 2018. The Convention provides that where a state “finds difficulty in continuing to grant asylum to refugees”, it may appeal to other parties to the treaty and they “shall in the spirit of African solidarity and international co-operation take appropriate measures to lighten the burden”.

It is in this spirit that also on Tuesday, Rwanda formally agreed to evacuate refugees and asylum-seekers living in dire and life-threatening circumstances in Libya. The memorandum of understanding was signed in Addis Ababa by the Rwandan government, UNHCR and the African Union. 

UNHCR welcomes Rwanda’s commitment to help refugees and asylum-seekers from Libya as a fitting tribute to the 1969 OAU Refugee Convention’s anniversary. The deal embodies the spirit of the regional instrument and, now, of the GCR.

Several African states have, since 1969, adopted progressive refugee laws and policies in line with the 1969 OAU Refugee Convention. Others are revising their refugee laws and policies to reflect both the Convention and the GCR, as well as the changing nature of displacement in Africa.

The AU declared 2019 as the “Year of Refugees, Returnees and Internally Displaced Persons: Towards Durable Solutions to Forced Displacement in Africa”, in part to commemorate the 1969 OAU Convention’s 50th anniversary. The Convention has been ratified by 47 of the AU’s 55 member states; UNHCR calls on African states that are not yet party to the Convention to ratify it, and on others to fully implement it.

Standard Chartered bank yazindua programu ya 'future Makers' kusaidia vijana wa kizazi kijacho kupata elimu ya kifedha

$
0
0

Mkurugenzi wa fedha wa benki ya Standard Chartered duniani Bw, Andy Halford akizungumza jambo kwenye mkutano wa mafunzo ya elimu ya uchumi. kushoto ni bw. Bernard Dadi Mkurugenzi wa mifumo wa malipo ya taifa wa benki kuu ya Tanzania (BoT) na kulia ni Bi. Irene Madeje Mkurugenzi wa shughuli mbalimbali katika sekta ya kifedha ya Deepening Trust.

Wakifuatilia kwa ukaribu mafunzo yanayofanyika kutoka kushoto ni Rayson Foya Mkuu wa kitengo cha fedha wa Standard Chartered bank tanzania, Kariuki Ngari Mkurugenzi mtendaji wa benki Standard Chartered Afrika Mashariki, Sanjay Rughani Mkurugenzi mtendaji wa benki ya Standard Chartered Tanzania, Bernard Dadi Mkurugenzi wa mifumo wa malipo ya taifa wa benki kuu ya Tanzania (BoT), Mkurugenzi wa fedha wa benki Standard Chartered duniani Bw, Andy Halford na bi. Irene Madeje Mkurugenzi wa shughuli mbalimbali katika sekta ya kifedha ya Deepening Trust. 


Sarah Zacharia (19yrs) akizungumza jinsi alivyonufaika na mradi wa Goal initiativa ulioanzishwa na benki ya Standard Chartered kwa ajili ya kuwasaidia wasichana/mabinti. Sarah yupo katika klabu ya Ali Mbowa iliyopo Temeke akijifunza kutengeneza mazulia kwa kutumia uzi na kwa sasa anafanya biashara hiyo inayomsaidia kupata kipato.

Vijana na wanafunzi kutoka vyuo, shule na taasisi mbalimbali wakifuatilia mafunzo kuhusu elimu ya uchumi yanatolewa na watu na wadau mbalimbali kutoka benki ya Standard Chartered. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Mwalimu Julius nyerere jijini Dar es salaam.

  Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya Standard Chartered Tanzania,Sanjay Rughani, akizungumza na vijana pamoja na watu mbalimbali waliofika katika mkutano/ mafunzo kuhusu elimu ya uchumi (financial education) uliofanyika katika ukumbi wa julius nyerere Dar es salaam.

Mkutano ukiendelea.

Wakizindua rasmi program ya " Future Makers" ambayo inalenga kusaidia vijana na kizazi kijacho kuweza kupata elimu ya kifedha, kutoka kushoto Mkurugenzi mtendaji wa benki ya Standard Chartered Tanzania Sanjay Rughani, Mkurugenzi wa mifumo wa malipo ya Taifa wa Benki kuu ya Tanzania (BoT) Bernard Dadi, Mkurugenzi wa fedha wa Standard Chartered bank duniani Mr. Andy Halford, Mkurugenzi mtendaji wa Standard Chartered Afrika mashariki Mr. Kariuki Ngari, Mkurugenzi wa shughuli mbalimbali katika sekta ya kifedha ya Deepening Trust Irene Madeje na kulia ni Rayson Foya ambaye ni Mkuu wa kitengo cha fedha wa benki Standard Chartered Tanzania

 
Standard Chartered Bank today launched its new community investment approach called Futuremakers by Standard Chartered. The initiative focuses on helping the next generation learn, earn and grow. The launch of Futuremakers by Standard Chartered was with a focus on Financial Education.

The launch of Futuremakers by Standard Chartered is a result of the Bank’s development of its community strategy to be more responsive to the changing social and economic needs across its markets around social and economic inequality and the limited opportunities for young people.

For the past 17 years in Tanzania, the Bank has been investing on areas of Youth, Health and Education. The Bank has been championing tackling avoidable blindness and visual impairment – through its programme, Seeing is Believing. Last year, the Bank achieved its global target of raising USD 100 Million towards Seeing is Believing, two years ahead of target.

“Seeing is Believing has reached more than 176 million people through 193 projects across 37 countries. The initiative has changed the lives of millions of individuals and families, making it easier for many to return to education and work. As a result, this has boosted local economies and strengthened communities” said, Mr. Andy Halford, the Bank’s Group Chief Executive Officer.

Mr. Andy said that, “according to the International Labour Organization, globally, more than 200 million young people are either unemployed, or they have jobs, but continue to live in poverty due to low income. At Standard Chartered Bank we believe everyone should have access to opportunities to realize his or her full potential and believe that we can make a difference in promoting greater economic inclusion in our markets”.

Speaking at the launch event, the Bank’s newly appointed East Africa CEO, Kariuki Ngari. said, that, “the launched Financial Education program plays a big role in enabling us achieve the goal of promoting equality and enabling youths achieve their full potential. In this regard, the Futuremakers builds on the success of our existing community programmes. We will, therefore, continue to incorporate financial education into all programmes. We will also expand GOAL, our existing girls’ education programme, and we will develop new global community programmes in employability and entrepreneurship.”

The Chief Executive Officer, Sanjay Rughani said that, “we want to use the unique skills of the Bank, and of our employees, to share skills and build the capacity of young people to access jobs and economic opportunities that will help close the inequality gap.”

The launch event was also attended by Irene Madeje, Director of Operations from the Financial Sector Deepening Trust (FSDT). Irene elaborated on the role of FSDT in supporting underserved individuals, households and enterprises, by offering them capacities and opportunities to improve their lives.

The event was officiated by the Director of the National Payment System from the Bank of Tanzania, Mr. Bernard Dadi who commended Standard Chartered Bank for developing and launching the Financial Education program as it will help close the inequality gap in our communities.

The launch of Futuremakers by Standard Chartered Bank fully aligns with the Bank’s purpose to drive commerce and prosperity through its unique diversity and reinforces its promise to be Here for Good.

Multichoice Talent Facotry Academy wapongezwa kwa kuiwakilisha vyema Nchi.

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bibi Susan Mlawiakiwa katika picha ya pamoja na Vijana waliorejea kutoka nchini Kenyawalikokuwa katika mafunzo ya uandaaji wa filamu kwa mwaka mmojayaliyoandaliwa na Kampuni ya Multichoice chini ya dawati lijulikanalo kama“Multichioce Talent Factory Academy” baada ya kupokea taarifa ya mafunzowaliyopata walipomtembelea ofisini kwake Jijini Dodoma.
Meneja Biashara kutoka Kampuni ya Multichoice Bw.Jonson Mshana (kulia)
akitoa maelezo mafupi kuhusu “Multichioce Talent Factory Academy” iliyodhaminivijana wanne katika mafunzo ya uandaaji wa filamu kwa mwaka mmojayaliyoandaliwa na Kampuni hiyo Nchini Kenya walipofika ofisi ya Katibu MkuuWizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bibi. Susan Mlawi (kulia) kuelezeanamna walivyonufaika na mafunzo hayo.
Jamal Mohamed Kishuli ambaye ni miongoni mwa Vijana wanne
waliorejea kutoka nchini Kenya walikokuwa katika mafunzo ya uandaaji wa filamukwa mwaka mmoja yaliyoandaliwa na Kampuni ya Multichoice chini ya dawatilijulikanalo kama “Multichioce Talent Factory Academy” akizumngumza wakatiwalipomtembelea Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo BibiSusan Mlawi ofisini kwake Jijini Dodoma.
Bw.Wilson Nkya miongoni mwa Vijana wanne waliorejea kutoka nchini Kenyawalikokuwa katika mafunzo ya uandaaji wa filamu kwa mwaka mmojayaliyoandaliwa na Kampuni ya Multichoice chini ya dawati lijulikanalo kama“Multichioce Talent Factory Academy” akizumngumza wakati walipomtembeleaKatibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bibi Susan Mlawi(hayupo katika picha) ofisini kwake Jijini Dodoma.
******************

Na Shamimu Nyaki – WHUSM

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi.Susan Mlawiamewapongeza vijana wanne waliofanya vizuri katika mafunzo ya uaandaaji waFilamu yalioandaliwa na Kampuni ya Multichoice yaliyofanyika nchini Kenyaambapo amewataka kutumia taaluma waliyopata kutengeneza filamu bora zenyemaudhui ya kuitangaza nchi yetu na kuleta ushindani katika soko.

Katibu Mkuu Bibi. Susan ameyasema hayo leo ofisini kwake Jijini Dodoma baada yakutembelewa na vijana hao ambao amewataka kufika katika Bodi ya FilamuTanzania kuwasilisha uelewa waliopata na kushauri namna ambavyo Bodi hiyoinaweza kuwatumia katika tasnia hiyo.

“Nawapongeza sana kwa kufanya vizuri katika mafunzo mliopewa,naamini
mtayatumia vizuri katika kukuza vipaji vyenu na kusaidia mawazo kwa wengineambao hawajapata nafasi hii,Lakini pia mtatumia ujuzi na taaluma mliyopatakatika kuleta mapinduzi ya utengenezaji wa filamu hapa nchini”alisema Bibi Susan.

Naye Meneja wa masuala ya Biashara wa Kampuni ya Multichoice Bw.JonsonMshana amesema kuwa Kampuni hiyo imeanzisha dawati la kusaka vipaji vyauandaaji wa kazi za filamu (Multichoice talent Factory Academy) kwa Bara laAfrika ili vijana wenye uwezo na vipaji kupata fursa ya kuongezewa maarifapamoja na kutafuta ajira kwa njia rahisi.

Bw.Jonson ameongeza kuwa Kampuni hiyo kila mwaka inatafuta vijana wanneambao wanapatikana kwa kuomba nafasi hiyo na hatimaye kufanyiwa usaili nakujiunga na wenzao kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika ikiwemo Kenya,Ethiopia,Uganda na Nigeria.

Naye Kijana Jamal Mohamed Kishuli ambaye amejifunza “Art Designer” amesemakuwa vijana wanapaswa kujiamini katika kila wanachokifanya na kutokata tamaalakini pia zinapotokea fursa za kuonyesha uwezo wao basi wasisite kujitokeza ilikupata nafasi ya kujitangaza kupitia vipaji walivyonayo.

Vijana hao walikua katika mafunzo ya Uandishi wa Mswada (Script Writer),
Uandaaji (producer) Uongozaji (Directing) na Art Desgner ambayo wamejifunzakwa mwaka mmoja katika Chuo Kikuu cha Kenyata nchini Kenya.

Majeruhi watatu ajali ya moto Morogoro waruhusiwa

$
0
0
Daktari Bingwa wa Upasuaji, Dkt.Edwin Mrema akiongea na waandishi wa habari kuhusu hali za majeruhi wa ajali ya moto wanaoendelea kupatiwa matibabu. 
Kutoka kulia ni Shabani Abdalla Omary na Mikidaki Issa ambao ni majeruhi wa ajali ya moto walioruhusiwa leo wakiwa kwenye picha ya pamoja na madaktari na wauguzi waliowahudimia.Majeruhi watatu kati ya 11 wa ajali ya moto wanaoendelea kupatiwa matibabu Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wameruhusiwa kutoka hospitalini leo baada ya afya zao kuanza kuimarika.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo. 


Na Sophia Mtakasimba



Majeruhi watatu kati ya 11 wa ajali ya moto wanaoendelea kupatiwa matibabu Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wameruhusiwa kutoka hospitalini leo baada ya afya zao kuanza kuimarika.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Daktari Bingwa wa Upasuaji ambaye pia ni mtaalamu wa kutibu majeraha ya moto Dkt. Edwin Mrema, amesema kuwa majeruhi hao wameruhusiwa kwa kuwa afya zao zimeanza kuimarika na kuelekeza kuwa watahitajika kuhudhuria kliniki ya wagonjwa wa nje ili kufuatilia maendeleo ya afya zao.

“Hadi kufikia leo tuna wagonjwa kumi na moja miongoni mwao ni hawa wawili na mmoja ataruhusiwa kesho, hawa wagonjwa tuliwapokea wakiwa katika hali ya hatari zaidi lakini leo tumefikia hatua ya kuwaruhusu kwenda nyumbani maana yake hali ya hatari waliyokuwa nayo imetoka, na sehemu kubwa ya vidonda walivyokuwa navyo vimepona, upumuaji wao ni nzuri na afya zao kwa ujumla zinaruhusu, lakini wataendelea kuja Hospitali kuhudhuria kliniki ya nje” alifafanua Dkt. Mrema.

Pamoja na kufuatilia mwenendo wa matibabu yao, amesema wataendelea kuhudhuria kliniki ya saikolojia ili kuwahimairisha zaidi kifikira.

Dkt. Mrema amesema wagonjwa wameanza kupatiwa huduma za mazoezi ya viungo (physiotherapy) kwani majeraha ya moto walioyapata yanaweza kusababisha baadhi ya viungo visikae sawa.

Aidha, Dkt. Mrema amesema kuna wagonjwa wawili ambao kutokana na kuugua sana ilibidi kuwafanyia upasuaji kuondoa baadhi ya viungo ili kuokoa maisha yao,lakini kwa sasa hali zao zinaendelea vizuri.

Katika hatua nyingine, mmoja wa majeruhi aliyeruhusiwa Bw. Shabani Abdalla Omary amemshukuru kwa dhati Mh. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuwatembelea hospitali hapo pamoja na kuwagharamia gharama zote za matibabu na pia ameshukuru madakrati na wauguzi wa MNH kwa huduma nzuri waliyowapa kipindi chote cha matibabu.

“Namshukuru Rais, alifika kutuona na akatupatia kiasi cha fedha Mungu ambariki sana sina cha kumlipa, lakini pia nawashukuru sana wauguzi na madaktari wa MNH kwa sababu nilivyofika hapa nilikuwa na hali ngumu mno ila kwa sasa naendelea vizuri” amesema Bw. Omary.

RAIS DKT MAGUFULI AMTEUA KAMISHNA DIWANI ATHUMANI KUWA MKURUGENZI MKUU WA IDARA YA USALAMA WA TAIFA, AMWAPISHA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Uzinduzi Klabu Ya Wafanyabiashara NBC Dodoma,serikali yawaomba kuchangamkia fursa za Kibiashara.

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Bilinith Mahenge ametoa wito kwa wafanyabishara jijini humo kuhakikisha wanachangamkia fursa za mikopo inayotolewa na taasisi za kifedha ili waweze kunufaika na ongezeko kubwa la fursa za kibiashara zinazoibuka katika jiji hilo ambalo ni makao makuu ya nchi.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa mkoa huyo wakati wa hafla ya jioni ya Uzinduzi wa Klabu ya wafanyabiashara ya Benki ya NBC ya mkoa wa Dodoma, Mkurugenzi wa jiji hilo Bw Godwin Kunambi mbali na kuipongeza benki hiyo kwa mabadiliko makubwa ya kihuduma alisema ipo haja ya makusudi kwa wafanyabiashara wa jiji hilo kuitumia vema benki hiyo ili kupata nguvu ya kiuchumi itakayowawesha kufaidi vema fursa ya mabadiliko ya ukuaji wa uchumi katika jiji hilo.

“Dodoma kwasasa kuna utekelezaji wa miradi mikubwa mingi ikiwemo barabara, Stendi ya mabasi ambayo ni kubwa zaidi Afrika Mashariki, upanuzi wa uwanja wa ndege, ujenzi wa viwanja vya mapumziko ambayo vitachochea mzunguko mkubwa wa pesa na ongezeko la watu. Hivyo ni fursa kwa wafanyabiashara kushirikiana vema na benki kama NBC ili kukuza mitaji itayowawezesha kufanya uwekezaji utakaowanufaisha na mabadiliko hayo,’’ alibainisha.

Alitolea mfano umuhimu wa wafanyabiashara hao kuwekeza kwenye sekta ya usafiri ambapo kwasasa serikali jijini humo ipo kwenye mpango wa kuondoa gari ndogo za abiria maarufu kama vipanya kwenye mizunguko ya mjini ili kutoa fursa kwa gari kubwa ‘coaster’ kufanya kazi hiyo.

Akizungumza kuhusu uanzishwaji wa Klabu hiyo, Mkuu wa Kitengo cha wateja wa Kati na Wadogo wa benki ya NBC, Bw Evance Luhimbo alisema pamoja na mambo mengine klabu hizo zinalenga kutoa mafunzo kwa wateja wa benki hiyo kuelewa mabadiliko ya uboreshwaji wa huduma za za benki hiyo, kuwakutanisha pamoja wajadili fursa za kibiashara sambamba na kuwajengea uelewa kuhusu masuala mbalimbali ya kibiashara ikiwemo masuala ya kodi na taratibu za kijiunga na taasisi wadau biashara ili ziwasaidie.

“Benki ya NBC kwasasa ipo kwenye mabadiliko makubwa ya kihuduma kwa wateja wateja wetu na ili mabadiliko haya yaweze kuwafikia wateja wetu ni vema kuwa nao karibu zaidi. Mbali na benki kuwajengea uelewa kama hudua zetu na taasisi wadau ikiwemo Chemba ya biashara, viwanda na kilimo (TCCIA)na Baraza la. Uwezeshaji (NEEC)na nyingine nyingi pia tumekuwa tukipokea maoni kutoka kwa wateja wetu yanayotuwezesha kubuni huduma zinazoendana na uhalisia wa mahitaji yao ya kifedha,’’ alisema.

Awali wakiwasilisha mada kwenye kongamano la uzinduzi wa Klabu hiyo muwakilishi wa TCCIA, Bw Patrick Magai na muwakilishi wa NEEC Bi Nyakao Mturi walitoa wito kwa wafanyabiashara wadogo kuunganisha nguvu ya kimitaji ili wapate nguvu ya pamoja itakayowawezesha kushiriki fursa kubwa za kibiashara ndani na nje ya nchi.

Akizungumza kwa niaba ya wafanyabiashara hao Bw Ponsian Rweyemela ambaye ni mfanyabiashara jijiji humo pamoja na kuipongeza benki hiyo kwa mabadiliko makubwa ya kiutendaji pia aliiomba benki hiyo pamoja na taaisisi nyingine za kifedha kuongeza idadi ya mashine za kuweka na kutolea fedha (ATM) ilikuendana na ukuaji wa jiji hilo pamoja na ongezeko la watumiaji wa mashine hizo.
Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Bw Godwin Kunambi(kulia-mbele) akifurahia uzinduzi wa rasmi wa Klabu ya wafanyabiashara ya Benki ya NBC ya mkoa wa Dodoma uliofanyika katikati ya wiki jijini humo. Wengine ni baadhi ya wateja na maofisa wa benki hiyo akiwemo Mkurugenzi wa Idara ya wateja wa kati na wadogo Bw Elibariki Masuke.

Sanlam Tanzania ya wapeleka washindi wa mbio Capetown marathon

$
0
0
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Sanlam kitengo cha bima ya maisha, Khamis Suleiman (Kushoto), akizungumza na waandishi wa habari katika hafla fupi ya kuwazawadia washindi wa mashindano yalioisha hivi karibuni yaitwayo “Life is a Marathon competition” na
kuwapa fursa ya kwenda kushiriki na kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya fainali ya “Sanlam Cape Town Marathon”, katika ofisi za makao makuu ya kampuni hiyo, jiji Dar es Salaam, jana. Kulia ni Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Sanlam kitengo cha bima Gift Noko.


=========   ========  ======

Kampuni ya Sanlam Tanzania imetoa zawadi kwa washindi wa mashindano yalioisha hivi karibuni yaitwayo “Life is a Marathon competition” na kuwapa fursa ya kwenda kushiriki na kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya fainali ya “Sanlam Cape Town Marathon” yatakayo fanyika tarehe 15 septemba mwaka huu. 

Washindi hao ni Jamia Abdallah na lister Lusulo Pakua. Vile Vile balozi wa Sanalam Maulid Kitenge na wateja wa Sanlam Stephen Mndeme na Innocent Shaku wamepata nafasi ya kushiriki katika mashindano hayo. 

Hatua ya kwanza ya mashindano ya “Life is a Marathon competition” yalihusisha washindani kuwasilisha picha na video zao zikionyesha jinsi watakavyo jiandaa kushiriki katika mashindano hayo, baada ya hapo washindi walichaguliwa na kupitia mazoezi mbali mbali ya kujiandaa. 

Akizungumza katika hafla ilyofanyika ofisi za Sanlam Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Mr Khamis Suleiman, aliwapongeza wachezaji kwa kujituma kwao na kuwasihi kuonyesha juhudi zaidi katika mashindano yanayokuja. 

“Tunafuraha sana kuona jinsi wachezaji hawa walivyofanya vizuri na mkiwa mnajianda kusafiri napenda kuwatia moyo mkafanye vizuri zaidi. Iwe unafanya mazoezi kwa ajili ya mashindano ya mbio au unajifunza kuendesha baiskeIi inabidi uwe na mshirika ambaye atakusaidia kufanikisha malengo yako, na hii ndio ngao yetu hapa Sanlam Tanzania, tumejikita katika kutuoa huduma na bidhaa za kidigitali ambazo zitakusaidia wewe katika hatua zote za maisha.” 

Sanlam ilizindua mashindano ya “Life marathon” tarehe 8 Agosti kwa lengo la kuonyesha umuhimu wa ushirikiano katika kuwezesha watu kufanikisha malengo yao na kuwa na maisha bora, pia ni moja ya njia ya kampuni ya Sanlam kutambua na kuwapongeza wanamichezo mbali mbali nchini Tanzania 

Ikiwa ni mashindano pekee ya marathon yenye daraja la dhahabu barani Africa, Sanlam Cape town marathon huleta pamoja zaidi ya vilabu 23 vya kimataifa na wakimbiaji takribani 15,000 kila mwaka.

Tigo yazindua Huduma ya ‘Office Internet’ kwa wafanyabiashara wadogo na wakati Tanzania

$
0
0

Afisa Mkuu wa Tigo Business, Pavan Ramdhani akimkabidhi Router Mkuu wa Idara ya masoko wa Dstv Baraka Shelukindo. mara baada ya uzinduzi wa huduma mpya ya ‘Office Internet’ ikiwalenga wafanyabiashara wadogo na wa kati nchini, ambapo huduma hiyo ina mfumo wa kisasa uliounganishwa na Microsoft.Hafla hiyo ilifanyika katika Makao makuu ya ofisi za Tigo Jijini Dar es salaam. 

Afisa Mkuu wa Tigo Business, Pavan Ramdhani akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya ‘Office Internet’ ikiwalenga wafanyabiashara wadogo na wa kati nchini, ambapo huduma hiyo ina mfumo wa kisasa uliounganishwa na Microsoft
Kaimu mkuu wa mauzo-Nick kazuka akifanua jambo kwa waandishi wa habari mara baada ya. uzinduzi wa huduma mpya ya ‘Office Internet’ ikiwalenga wafanyabiashara wadogo na wa kati nchini, ambapo huduma hiyo ina mfumo wa kisasa uliounganishwa na Microsoft 

waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini uzinduzi wa uzinduzi wa huduma mpya ya ‘Office Internet’ ikiwalenga wafanyabiashara wadogo na wa kati nchini, ambapo huduma hiyo ina mfumo wa kisasa uliounganishwa na Microsoft.Hafla hiyo ilifanyika katika Makao makuu ya ofisi za Tigo Jijini Dar es salaam.
Mtaalam bidhaa Tigo Business Brian Swai akifafanua jambo kwa wageni waalikwa uzinduzi wa huduma mpya ya ‘Office Internet’ ikiwalenga wafanyabiashara wadogo na wa kati nchini, ambapo huduma hiyo ina mfumo wa kisasa uliounganishwa na Microsoft.Hafla hiyo ilifanyika katika Makao makuu ya ofisi za Tigo Jijini Dar es salaam.


Ni huduma ya intaneti yenye kasi inayokwenda sambamba na mfumo wa kisasa wa kibiashara kutoka Microsoft


Dar es Salaam: Septemba 12, 2019, Kampuni ya simu ya Tigo, kupitia kitengo chake cha Tigo Business leo imetangaza rasmi uzinduzi wa huduma mpya ya ‘Office Internet’ ikiwalenga wafanyabiashara wadogo na wa kati nchini, ambapo huduma hiyo ina mfumo wa kisasa uliounganishwa na Microsoft . Hatua hii inazidi kuifanya Tigo kuendelea kuwa kinara wa ubunifu kuiwezesha kampuni katika kujitolea kufanya biashara zake kwa malengo.


Sambamba na uzinduzi wa huduma ya ‘Home Internet’ uliyofanywa na Tigo hivi karibuni, huduma ya ‘Office Internet’ inakuja na faida endelevu kwa wateja wenye biashara ndogo na za kati ambao hupendelea huduma za intaneti kwa mkataba. Hii inadhihirisha matumzi bora ya mtandao wa wenye kasi nchini Tanzania wa 4G+.


Afisa Mkuu wa Tigo Business, Pavan Ramdhani, aliwaambia wateja wa Tigo kuwa, kwa sasa wana uwezo wa kutoa huduma bora zinazoendana na wakati kwa kushirikiana na wataalamu wa Microsoft. “Tulifanya kazi kwa ushirikiano wa karibu sana na wateja wetu, ambapo walituonyesha maeneo matatu muhimu yenye changamoto; Muda unaotumika kuunganisha huduma ya intaneti, Kasi ya huduma hiyo na ukosefu wa maana halisi, Matumizi ya intaneti na zana zenye uhusiano na biashara. Tuna furaha kutangaza kuwa, ‘Office Internet ina huduma ya daraja la kwanza iliyounganishwa na mtandao wa Tigo 4G+, wenye watumiaji wengi duniani kote chini ya ushirikiano wa Microsoft.

Huduma hii kwa ujumla wake inatumika bila muunganisho wa waya, kwa maana ya kwamba mteja wetu anatakiwa kuwasha kifaa chake cha Modem au Router. Ofisi ya mteja inaweza kuunganisha vifaa 10 hadi 32 kwenye inteneti kwa mara moja. Microsoft 365 inaruhusu kufanya mambo mbalimbali ikiwamo utumaji wa barua pepe za kibiashara, Kutuma na kuhifadhi ujumbe katika mtandao, Matumizi ya Microsoft katika masuala yote ya kibiashara ikiwamo mikutano ya moja kwa moja mtandaoni


Kujiunga na huduma ya ‘Office Internet’ tembelea duka lolote la Tigo nchini ili kujisajili. Wateja wanaotumia huduma hii watapewa kipaumbele katika huduma kwa wateja. Kwa nyongeza, mteja anaweza pia kupiga 0711100101 au barua pepe Tigobusiness@tigo.co.tz.

UZINDUZI WA MAFUNZO STADI ZA KAZI KWA VIJANA NA MAADHIMISHO YA MIAKA MIA YA ILO

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia vipuri vilivyo chongwa na wanafunzi wa Chuo cha Don Bosco Dodoma, kwenye uzinduzi wa mafunzo ya ufundi stadi kwa vijana na uwekaji wa kumbukumbu ya miaka 100 wa ILO, uliyofanyika katika viwanja vya Don Bosco, jijini Dodoma, Septemba 14.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia dawati lililotengenezwa katika Chuo cha Don Bosco Dodoma, kwenye uzinduzi wa mafunzo ya ufundi stadi kwa vijana na uwekaji wa kumbukumbu ya miaka 100 wa ILO, uliyofanyika katika viwanja vya Don Bosco, jijini Dodoma, Septemba 14.2019. 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia mfano wa nyumba uliyojengwa na matofali ya kisasa ya kupachika , kwenye uzinduzi wa mafunzo ya ufundi stadi kwa vijana na uwekaji wa kumbukumbu ya miaka 100 wa ILO, uliyofanyika katika viwanja vya Don Bosco, jijini Dodoma, Septemba 14.2019. 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia ramani za nyumba zinazojengwa na matofali ya kisasa ya kupachika , kwenye uzinduzi wa mafunzo ya ufundi stadi kwa vijana na uwekaji wa kumbukumbu ya miaka 100 wa ILO, uliyofanyika katika viwanja vya Don Bosco, jijini Dodoma, Septemba 14.2019.
Makamu Mkuu wa Shirika la Don Bosco Kanda ya Afrika, Augustine Sellam akizungumza, kwenye uzinduzi wa mafunzo ya ufundi stadi kwa vijana na uwekaji wa kumbukumbu ya miaka 100 wa ILO, uliyofanyika katika viwanja vya Don Bosco, jijini Dodoma, Septemba 14.2019. 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Makamu Mkuu wa Shirika la Don Bosco Kanda ya Afrika, Augustine Sellam akizungumza, kwenye uzinduzi wa mafunzo ya ufundi stadi kwa vijana na uwekaji wa kumbukumbu ya miaka 100 wa ILO, uliyofanyika katika viwanja vya Don Bosco, jijini Dodoma, Septemba 14.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama akizungumza, kwenye uzinduzi wa mafunzo ya ufundi stadi kwa vijana na uwekaji wa kumbukumbu ya miaka 100 wa ILO, uliyofanyika katika viwanja vya Don Bosco, jijini Dodoma, Septemba 14.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, wakati akiwasili katika viwanja vya Don Bosco, kwenye uzinduzi wa mafunzo ya ufundi stadi kwa vijana na uwekaji wa kumbukumbu ya miaka 100 ya ILO, jijini Dodoma, Septemba 14.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Msimu Mpya wa Tigo Fiesta 2019 ulivyozinduliwa rasmi jijini Dar

$
0
0

Mwenyekiti wa kamati ya Fiesta Sebastian Maganga akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa. Uzinduzi msimu mpya tamasha la Muziki la Tigo Fiesta 2019 mkutano huo ulifanyika katika ofisi za Clouds Media Group. 

Meneja Mawasiliano wa wa Tigo Woinde shisael akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu Uzinduzi msimu mpya tamasha la Muziki la Tigo Fiesta 2019 kushoto kwake ni Mwenyekiti wa kamati ya Fiesta Sebastian Maganga katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika mapema jana katika ofisi za Clouds Media Group.

Uzinduzi msimu mpya tamasha la Muziki la Tigo Fiesta 2019 likiwa na maandalizi lukuki ikiwemo burudani na promosheni kabambe
Wafanyakazi wa Tigo na Clouds media Group wakifurahia mara baada ya uzinduzi wa Chapa ya Uzinduzi msimu mpya tamasha la Muziki la Tigo Fiesta 2019 likiwa na maandalizi lukuki ikiwemo burudani na promosheni kabambe

TATIZO LA BARABARA IFAKARA MLIMBA KUWA HISTORIA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema changamoto ya barabara ya kutoka Ifakara hadi Mlimba iliyokuwa inawakabili wananchi wa maeneo hayo kwa muda mrefu imepatiwa ufumbuzi baada ya Serikali kupanga kuijenga kwa kiwango cha lami.

Amesema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imedhamiria kuboresha miundombinu ya barabara nchini ikiwemo barabara ya kutoka Ifakara hadi Mlimba yenye urefu wa km. 126.5.

Waziri Mkuu aliyasema hayo jana jioni (Jumapili, Septemba 15, 2019) wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Matangini, Mlimba wilayani Kilombero.

“Serikali imedhamiria kuimarisha barabara katika maeneo mbalimbali nchini ikiwa ni pamoja na ujenzi wa barabara ya Ifakara-Mlimba kwa kiwango cha lami lengo likiwa ni kurahisisha usafiri pamoja na kukuza uchumi wa wananchi na Taifa kwa ujumla.”

Alisema Serikali inatambua umuhimu wa barabara hiyo kwa ajili ya kuboresha maendeleo ya wananchi na kwamba itajengwa kwa kiwango cha lami, hivyo aliwataka wananchi hao waendelee kuiamini Serikali yao.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alimuagiza Kaimu Ofisa Elimu Mkoa wa Morogoro, Jackson Mpankuli ahakikishe amepeleka walimu katika shule ya msingi Matangini na Mwangazaambazo zinakabiliwa na upungufu wa walimu.

Waziri Mkuu alisema hadi Sepetemba 30 mwaka huu kiongozi huyo awe ameshawahashimia walimu katika shule husika. Waziri Mkuu alitoa agizo hilo baada ya Mbunge wa Jimbo la Mlimba, Suzan Kiwanga kulalamikia upungufu wa walimu hao.

Mbunge huyo alisema katika jimbo kuna tatizo kubwa la upungufu wa walimu hali inayosababisha baadhi ya wazazi kukodi walimu kwa ajili ya kuwafundisha watoto wao, hivyo Waziri Mkuu aliagiza walimu wahamishiwe katika shule ndani ya wiki mbili.

Akizungumza na wananchi katika eneo la Mchombe alipokuwa njiani kuelekea Mlimba, Waziri Mkuu aliwataka wazazi, walezi na viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro kuhakikisha wanadhibiti ongezeko la mimba kwa watoto wa shule.

“Lazima kuwalinda watoto wa kike ili wasipate mimba kwani watashindwa kuendelee na masomo, hivyo watashindwa kutimiza ndoto zao. Viongozi simamieni utekelezaji wa sheria kwa kuwachukulia hatua wote waliowapa mimba wanafunzi.”

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, Mbunge wa jimbo la Kilombero, Lijualikali na Mbunge wa Mlimba, Suzan Kiwanga waliiomba Serikali iwasaidie ujenzi wa barabara za kutoka Ifakara hadi Mlimba na barabara ya Ifakara hadi Kidatu ambayo ujenzi wake unasuasua.

Pia Suzan alitumia fursa hiyo kuishukuru Serikali kwa kutenga fedha kwa ajili ya upembuzi yakinifu kwa barabara ya Ifakara-Mlimba na baadae kuwekwa lami kwa awamu na kusema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano ikiahidi kitu inatekeleza

Waziri Mkuu anaendelea na ziara yake ya kikazi mkoani Morogoro ambapo anatarajiwa kutembelea Halmashauri za wilaya ya Ulanga na Malinyi kukagua miradi ya maendeleo ukiwemo mradi wa ujenzi wa hospitali ya wilaya na kuzungumza na wananchi pamoja na watumishi.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiongea na wananchi wa Mbingu, Kata ya Igima, wilayani Kilombero, mkoani Morogoro Septemba 15.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwasalimia wananchi wa Kata ya Mchombe, wilayani Kilombero, kwenye mkutano wa hadhara, Septemba 15.2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwahutubia wananchi wa Kata ya Mrimba, wilayani Kilombero, kwenye mkutano wa hadhara, Septemba 15.2019

WAFANYABIASHARA CHALINZE WANUFAIKA NA MAFUNZO KUTOKA BRELA

$
0
0


Baadhi ya wafanyaiashara wa  Halmashauri ya Chalinze wakisikiliza mafunzo yanayotolewa na BRELA kwaajili ya kuwarahisishia wafanyabiashara hao kujipatia Leseni kwa njia ya Mtandao.Na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.
WAKALA wa usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) watoa mafunzo kwa wafanyabiashara wa Halmashauri ya Chalinze wapewa mafunzo kwaajili ya kujipatia leseni kwa njia ya mtandao.

Akizungumza na waaandishi wa habari Afisa Biashara mwandamizi kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara, Boniface Mrema amesema kuwa wafanyabiashara wa halmashauri ya Chalinze wamepewa mafunzo wezeshi kwaajili ya kupata leseni mpya au kurudia kusajili leseni zao za biashara.

"Wafanyabiashara wa halmashauri ya Chalinze wamepewa mafunzo na maafisa wa kutoka Wakala ya Usajili biashara na Leseni (BRELA) ili waweze kupata leseni za biashara zao kwa njia ya mtandao na kuachana na namna ya zamani ambayo ilikuwa ikiwapotezea muda wa kufanya biashara zao". Amesema Mrema.

Nae Afisa Leseni Mwandamizi wa BRELA, Abas Kothema amesema kuwa Tanzania ya Viwanda lazima iwe na mfumo sahihi wa kusajili biashara kwa njia ya mtandao kwani mataifa mengi duniani husajili biashara kwa njia ya mtandao.

Pia amewaasa wafanyabiasha wa Manispaa zilizochaguliwa kwaajili ya kupewa mafunzo wachukue fursa hiyo kwaajili ya kujipatia leseni zao kwa njia ya mtandao na kutokupoteza muda.

Hata hivyo Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa halmashauri ya Chalinze, Lawrence Tsingay ameishukuru Serikali ya awamu ya tano kwa kuwachagua wafanyabiashara wa Chalinze kuwa wamojawapo kati ya halmashauri zilizochaguliwa kupewa mafunzo ya kujisajili na kujipatia leseni kwa njia ya Mtandao.

Nae Mfanyabiashara Farida Khamis amewashukuru maafisa BRELA kwa kazi wanayoifanya na kuwaelimisha wafanyabiashara wa Chalinze kwani wamewapunguzia muda wa kupanga foleni walipokuwa wakitafuta leseni za biashara zao.
Afisa Leseni Mwandamizi wa BRELA, Abas Kothema akizungumza na wafanyabiashara wa  Manispaa ya Chalinze kwaajili ya kuwajengea uwezo waweze kujipatia Leseni za Biashara kwa njia ya mtandao.

Afisa biashara Mwandamizi kutoka Wizara ya Biashara na Viwanda, Boniface Mrema akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutoa mafunzo kwa wafanyabiashara wa Halmashauri ya Chalinze ambayo yanahusu wafanyabiashara kujipatia Leseni kwa njia ya Mtandao baada ya kuzinduliwa Mwanzoni mwa Oktoba,2019.
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara  Halmashauri ya Chalinze, Lawrence Tsingay akizungumza mara baada ya kupewa mafunzo kwaajili ya kuijipatia Leseni kwa njia ya Mtandao katika mafunzo yaliyofanyika Chalinze leo.
Mfanyabiashara  wa Halmashauri ya Chalinze, Farida Khamis akizungumza mara baada ya kupewa mafunzo ya kujisajiri na kujipatia Leseni kwa njia ya mtandao. Amesema kuwa Mafunzo hayo yamekuja kwa muda muafaka kwani itawarahisishia kujipatia leseni bila kupanga foleni.

WANANCHI WA KIBADA KUJENGA MTARO KUNUSURU MAKAZI YAO

$
0
0

Sehemu ya mtaro huo unaoendelea kuchimbwa kwa nguvu za wananchi wa Kata ya Kibada wilayani Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu, Globu ya jamii
KAYA 970 zilizopo katika mtaa wa Kiziza na Nyakale Kata ya kibada wilayani kigamboni jijini Dar es Salaam zimeungana kutafuta ufumbuzi wa changamoto ya maji kujaa katika makazi yao kwa kutengeneza mtaro wa kupitisha maji pindi mvua zinaponyesha ili kunusuru makazi yao.

Ili kukamilisha mradi wa uchimbaji wa mtaro uliowashirikisha wananchi kujenga hadi kukamilika kwake zinatarajia kutumika kwa shilingi  ya Bilioni moja au Bilioni 1.2.

Akizungumza wakati wa ziara ya kutembelea baadhi ya mitaro katika eneo la kiziza na nyakale kuangalia maendeleo ya ujenzi wa mtaro ulipofikia,Mwenyekiti wa mradi wa mitaro kata ya Kibada, Nazzar Nicholaus alisema ulianza kutengenezwa januari 2018 na kasi ya ujenzi unaenda vizuri.

Nicholas ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo ya wananchi kwa Rais Magufuli,alisema ilikukamilisha mradi wote wa ujenzi wa mtaro wananchi wamekubaliana kushirikiana kwa kujitolea fedha,vifaa na Nguvu kazi.

"Ili kufanikisha mradi huu tunahitaji mkono mrefu na mkono mrefu tunazungumzia serikali.Hata hivyo wananchi tumeamua kuunga mkono juhudi za serikali za kutatua kero za wananchi chini ya Rais mpendwa Dk.John Magufuli kwa kuanza kuitatua kero hii," aliongeza

"Wakati wa kipindi cha mvua ndipo wananchi wa maeneo haya wanakuwa katika wakati mgumu Kutokana na maji kutuama katika makazi yetu hali inayofikia wanafunzi kushindwa kwenda shule na wafanyakazi kushindwa kwenda kwenye majukumu yao hivyo kwa umoja wetu tumeamua kutatua kero hii," alisema Nicholas

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Kibada,Amin Sambo alisema mradi huo ulianza mwaka 2005 chini ya wizara ya Ardhi ambapo wananchi wa eneo hilo walipoona mradi huo umesimama ndipo walipoamua kushirikiana kwa pamoja na kuamua kutengeneza moja ya Mtaro mkubwa ambao utapitisha maji kiurahisi n miitado midogo kuunganishwa kwa mtaro huo mkubwa.

"Tunautengeneza mtaro huo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, tumeamua kuchangishana na kutengeneza mtaro huo nia yetu ni kumsaidia Rais Magufuli kwa kutumia rasiliamari zetu wenyewe tulizonazo," alisema na kuongeza

"Tayari kazi imeanza na hadi sasa kuna kampuni moja ijulikanayo kwa jina la Plasisco imejitolea kutupatia Makaravati mawili ambayo yatatandikwa katika mtaro huo," amesema.

Wakati huo huo Mwenyekiti wa Mtaa WA Kiziza kata ya Kibada ,Adinani Simba amesema tatizo la maji katika eneo hilo lilianza siku nyingi mvua zinaponyesha na kuathiri nyumba nyingi na watu kushodwa kutoka kwenda kufanya shughuli zao.

Ame1sema katika eneo hilo 1kuna mitaro kama minne ambayo inahitajika kutengenezwa lakini 1wananchi wa eneo hilo wameamua kushirikiana na kutengeza mtaro mmoja mkubwa utakaopitisha maji kutoka katika mtaro mingine.
Kazi ya kuchimba mtaro ikiendelea katika Kata ya Kibada wilayani Kigamboni jijini Dar es Salaam ili kunusuru kaya 970 ambazo zimekuwa na changamoto ya maji kujaa wakati wa mvua za masika.
Mwenyekiti wa Mradi wa kuchimba Mtaro Kibada wilayani Kigamboni jijini Dar es Salaam, Nizzar Nicholaus akizungumzia kasi ya ujenzi wa mtaro huo unaojengwa kea lengo la kunusuru makazi ya wananchi wa eneo hilo.

Ofisa Mtendaji Kata ya Kibada, Salome Ngonyani akizungumza baada ya ziara ya kukagua mtaro unaochimbwa na wananchi wa Kata hiyo kwa ajili ya kunusuru makazi yao.

Benki Ya NBC Yaandaa Kongamano La Kibiashara Kwa Ajili Ya Wateja Wake Dodoma

$
0
0
Benki ya NBC imeratibu kongamano maalum la kibiashara kwa ajili ya wateja wake wadogo na wakati jijini Dodoma ambalo pamoja na mambo mengine lililenga kuwaongezea wateja hao hao uelewa kuhusiana na mabadiliko ya kihuduma na fursa za kiuwezeshaji kutoka benki hiyo.

Akizungumza wakati wa kongamano hilo lililofanyika hivi karibuni jijini humo, Meneja Ukuzaji wa Biashara Kitengo cha biashara ndogondogo na za kati wa Benki hiyo, Bw Jonathan Bitababaje alisema kufuatia uboreshwaji mkubwa wa huduma za benki hiyo ambazo zinaendana na kasi ya kiteknolojia na fursa za kiuchumi kumekuwa na hitaji kubwa kwa wateja hao kujengewa uelewa ili waweze kwenda sambamba na mabadiliko hayo.

“NBC kwasasa tumefanya mabadiliko makubwa ya kihuduma yanayoendana na kasi ya kiteknolojia na ukuaji wa uchumi na tumeona kuwa mabadiliko haya yatakuwa na tija zaidi kwa wateja wetu hasa wadogo na wakati ikiwa tu tutawajengea uelewa wa kutosha ili waweze kwenda sambamba mabadiliko haya badala ya kuwa changamoto,’’ alibainisha.

Alisema mbali na kuwajengea uelewa kuhusu huduma za benki hiyo,kupitia kongamano hilo washiriki waliweza kutoa maoni yao ikiwa ni mrejesho wa huduma wanazopata kutoka benki hiyo, hatua aliyosema itasaidia taasisi hiyo kuboresha zaidi huduma hizo sambamba na kubuni huduma mpya zinazoendana na mahitaji ya wateja hao.

Aidha katika kongamano hilo la siku moja, mbali na masuala ya kibenki washiriki walipata fursa ya kusikiliza na kuchangia mada kutoka kwa wawakilishi wa taasisi nyingine ikiwemo Chemba ya biashara, viwanda na kilimo (TCCIA)na Baraza la Uwezeshaji (NEEC) ambao walielezea fursa mbalimbali za kibiashara ndani na nje ya nchi ikiwemo nafasi ya taasisi hizo katika kuwaunganisha wafanyabiashara na wenzao kutoka nje ya nchi.

“ Kwa kushirikiana na benki ya NBC tumekuwa tukishirikiana mambo mengi yanayolenga kuwasaidia wafanyabiashara wetu na hivi karibuni tunatarajia kuwasafirisha wafanyabiashara kwenda nchini China kwa ajili ya safari ya kibiashara ya siku kumi ambapo wahusika watalipa gharama ya kiasi cha Dola za Kimarekani 2500 tu ambayo itagharamia mahitaji yao yote ya msingi ikiwemo nauli ya kwenda na kurudi, gharama za chakula na huduma nyingine ikiwemo ya wakalimani,’’ alisema Bw Patrick Magai, Meneja Maendeleo Viwanda kutoka TCCIA.

Wakizungumza wakati wa kongamano hilo lililofutiwa na Uzinduzi wa Klabu wa Wafanyabiashara ya Benki hiyo mkoani humo, baadhi ya washiriki walisema pamoja na huduma za kifedha ipo haja ya taasisi za kifedha hapa nchini kuongeza ushirikiano zaidi na wafanyabiashara hao pindi wanapotafuta zabuni kubwa zenye kuhitaji dhamana kutoka taasisi hizo.

“Pia ipo haja kwa taasisi za fedha nchini kutambua baadhi ya changamoto zinazotukabili wateja wao kwenye biashara zetu kwa kubuni huduma zinazotambua changamoto zetu ikiwemo kuangalia namna ya kushirikiana nasi pindi tunapokabiliwa na changamoto ya ucheleweshwaji wa malipo yetu kutoka kwa wateja wetu,’’ alisema mmoja wa wafanyabiashara hao ambae ni Mkandarasi, Dr Steven Masangia.


Meneja Ukuzaji wa Biashara Kitengo cha biashara ndogondogo na za kati wa Benki hiyo, Bw Jonathan Bitababaje akiwasilisha mada kuhusiana na huduma za benki hiyo wakati wa Kongamano la kibiashara lililoandaliwa na Benki hiyo kwa ajili ya wateja wake wadogo na wa kati mkoani Dodoma lilillofanyika hivi karibuni jijini humo.


Maofisa waandamizi wa Benki ya NBC wakichangia mada kwenye kongamano hilo.
Maofisa waandamizi wa Benki ya NBC wakichangia mada kwenye kongamano hilo.
Maofisa waandamizi wa Benki ya NBC wakichangia mada kwenye kongamano hilo.
Baadhi ya wateja wa benki ya NBC wakichangia mada wakati wa kongamano hilo.
Baadhi ya wateja wa benki ya NBC wakichangia mada wakati wa kongamano hilo.
Baadhi ya wateja wa benki ya NBC wakichangia mada wakati wa kongamano hilo.
Baadhi ya wateja wa benki ya NBC wakichangia mada wakati wa kongamano hilo.
Muwakilishi kutoka Baraza la Uwezeshaji (NEEC) Bi Nyakao Mturi akiwasilisha mada wakati wa Kongamano hilo.

Benki ya Exim Yazindua Kampeni Kuhamasisha Matumizi ya Huduma Salama za Kifedha

$
0
0
Benki ya Exim Tanzania leo imezindua kampeni maalum inayolenga kuhamasisha wateja wake kuhusiana na matumizi ya mtiririko wa huduma maalumu za kiusalama kwenye masuala ya fedha zinazotolewa na benki hiyo.

Kupitia mtoririko huo imebainishwa kuwa wateja wa benki hiyo wanapata huduma mbalimbali ikiwemo huduma ya usafirishaji wa fedha kwa usalama (Cash-In-Transit service), huduma ya kiusalama ya malipo (Host to host services), huduma za kisasa za hundi (Corporate Cheque Capture service) pamoja na huduma ya kuweka (deposit) pesa kwenye akaunti ya benki hiyo wakati wowote kwa kutumia mashine ya kuwekea fedha (Cash Deposit Machines services). 

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam leo Mkuu wa Idara ta Masoko na Mahusiano wa benki hiyo Bw Stanley Kafu alisema kupitia huduma hizo wateja wa benki hiyo hawahitaji tena kupanga foleni kwenye matawi ya benki hiyo ili kupata huduma za kifedha au hata kuhofia muda wa kufungwa kwa huduma za benki hiyo kwa kuwa wanaweza kupata huduma wakiwa kwenye maeneo ya kazi. 

“Huduma hizi ni sehemu ya mkakati wa benki ya Exim Tanzania kutoa huduma kwa wateja bila kubanwa na muda wa kazi au umbali wa kijiografia.,’’ alisema Kafu 

Akifafanua kuhusu huduma ya usafirishaji wa fedha kwa usalama (Cash-In-Transit service), Kafu alisema inamuondolea mteja hatari (risk) ya kuibiwa, kuvamiwa, kunyang’anywa pesa wakati anazitoa ofisini kwake kupeleka benki kwa kuwa atapatiwa huduma ya kusafirisha fedha hizo kuelekea na kutoka benki kwa kutumia usafiri maalumu ukiwa na walinzi wenye mafunzo maalum ya kulinda fedha. 

“ Kupitia huduma yetu ya Host- to- Host service, mteja wetu anaruhusiwa kutumia matawi yetu yote Tanzania nzima kupokea malipo yake ya invoices kutoka kwa wateja wake wote nchi nzima. Huduma hii ni kwa wateja ambao wanatoa na kupokea hundi nyingi kutoka kwa watu mbalimbali kama vile vyuo vikuu, mashule, viwanda, kampuni za usafirishaji, kumpuni za clearing and forwarding, biasahara za mitandaoni, shughuli kama hoteli na utalii.’’ alitaja 

Aidha akizungumzia huduma ya ‘corporate cheque capture’ Kafu alisema hudumahiyo inayotumia ‘scanner’ inamuwezesha mteja kuweka hundi zake (deposit cheque) wakati wowote bila kutembelea tawi lolote la benki. 

“Hakuna haja ya kupanga foleni tena, huduma ipo ofisini au nyumbani kwako. Huduma hii ni maalumu kwa wateja wote wenye biashara ambazo zinapokea hundi (cheque) kwa wingi kila siku bila kujali ni shilingi za kitanzania ama dola za kimarekani, au inatoka benki gani hapa Tanzania. Hapa tunahusisha biashara kama za usafirishaji, mashirika ya bima, wauza magari au pikipiki na vipuli, maduka ya jumla, mawakala wa gesi, pamoja na viwanda mbalimbali.’’ Alitaja. 

Kuhusu huduma ya mashine ya kuweka fedha (Cash Deposit Machine), Kafu alisema , inamsaidia mteja kuweka (deposit) pesa kwenye akaunti ya benki hiyo wakati wowote bila kutembelea tawi la benki ambapo mteja akishaweka pesa katika mashine hiyo anapata risiti ambayo inaonyesha kuwa pesa tayari imeshaingia kwenye akaunti, na kisha mteja anaweza kuendelea kufanya miamala kama vile kutoa (withdraw) au kutuma malipo mbalimbali. 

“ Mashine hii inafanya kazi masaa 24 siku saba za wiki hivyo hakuna haja ya kupanga foleni tena, huduma ipo ofisini au kiwandani kwako. Huduma hii inamuondolea mteja risk (hatari) na wasiwasi wa kuibiwa, kuvamiwa, kunyang’anywa pesa wakati anazitoa ofisini kwake kupeleka benki.’’ Alisema. 

Aliongeza kuwa benki hiyo itaendelea kubuni huduma za kisasa zaidi ambazo si tu zinaokoa muda kwa wateja hao bali pia kuwahikikia usalama wao na fedha zao ili kwenda sambamba na kauli mbui ya benki hiyo inatosema “ Exim Tupo Kazini Leo Kwa Ajili Ya Kesho.
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images