Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1875 | 1876 | (Page 1877) | 1878 | 1879 | .... | 1903 | newer

  0 0

   Mkurugenzi wa Hazina wa Benki ya Biashara ya Mkombozi,  Nwaka Mwabulambo (katikati) akizungumza na waandishi wa habari wakati alipomtembelea Bw,Salim Rashid mkazi wa Tuangoma Jijini Dar es Salaam anayesumbuliwa na ungonjwa wa saratani ya ulimi na kutoa mchango wa sh. miloni moja kwaajili ya matibabu pia nakumfungulia akaunti ya pamoja (Joint Akauti) kulia ni Fatuma Rashid mke wa Salim Rashid,Meneja Mikopo wa Benki hiyo Bw. Andrew Chimazi. (PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON)
   Bi-Fatuma Rashid (katikati) akiushukuru uongozi wa benki
   hiyo kwa mchango wao walioutoa (kulia) Meneja wa Benki ya Biashara ya Mkombozi, Tawi la Kariakoo, Bonphace Mahenge, na Mkurugenzi wa Hazina wa benki hiyo ,  Nwaka Mwabulambo.
   Meneja wa Benki ya Biashara ya Mkombozi, Tawi la Kariakoo, Bonphace Mahenge (kushoto), akimshuhudia, Fatuma Rashid mke wa Salim Rashid (katikati) akijaza fomu kwa alama ya kidole kufungua akaunti ya pamoja (Joint Akaunt) kwa ajili ya michango ya kumsaidia.Uongozi wa benki hiyo ulimtembelea, Salim Rashid mkazi wa Tuangoma Jijini Dar es Salaam anayesumbuliwa na ungonjwa wa saratani ya ulimi baada ya kuona matangazo kwenye vyombo vya habari.
   Bi-Fatuma Rashid akiwa na mume wake Bw.Salim Rashid ayesumbuliwa na ungonjwa wa saratani ya ulimi.
   Uongozi wa benki hiyo ukishauriana jambo ulipomtembelea Bw.
  Salim Rashid mkazi wa Tuangoma Jijini Dar es Salaam anayesumbuliwa na ungonjwa wa saratani ya ulimi.
   ........................................................
  BENKI ya Biashara ya Mkombozi  imeahidi kuendelea kushiriki  shughuli mbalimbali za kijamii kwa kuchangia watui wenye mahitaji maalumu.
  Hatua hiyo imefikiwa  baada ya uongozi wa benki hiyo kutoa msaada kwa  familia ya Salim Rashid mkazi wa Tuangoma Jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam mara baada ya kutembelea familia hiyo Nwaka Mwabulambo Mkurugenzi wa Hazina wa Benki hiyo alisema kuwa  katika kuelekea miaka kumi ya benki hiyo bebki imeamua kushiriki na familia hiyo kwa kutoa maada wa kuwafungulia akaunti ili jamii iweze kuwasaidia.

  Alisema baada ya kupata taarifa kutoka katika vyombo mbalimbali kuhusu uhitaji wa Rashid ambaye anasumbuliwa na saratani  uongozi wa benki uliamua kushiriki kwa vitendo kwa  kuisadia familia hiyo kwa kutoa mchango wa sh. miloni moja sambamba na kufungua akaunti ya pamoja ili kuirahisishia familia hiyo kwenye zoezi la ukusanyaji wa fedha za msaada kutoka kwa jamii.

  “Kama tunavyofahamu simu za mkononi zina ukomo wa utoaji fedha hivyo benki kwa kuliona hilo  tumeamua kuirahisishia jamii kazi hii kwa kufungua akaunti ya pamoja (Joint Akauti) ambayo itawezesha jamii na taasisi mbalimbali kuchangia kiasi chochote cha fedha ili  kuirahisishia  familia hii  iweze kupata msaada wa fedha za matibabu,”alisema Mwabulambo

  Alisema kwa kutambua umuhimu wa kushiriki shughuli za kijamii benki itaendelea kushirikiana na wadau wengine kuchangia shughukli mbalimbali za kijamii kama njia ya kutoa shukrani kwa kile wanachokipata kutoka kwa wateja wao ambao ndiyo wadau

  Aidha aliongeza kuwa tayari uongozi wa benki umewashawishi watumishi wake kuona umuhimu wa kuchangia matibabu ya Rashidi huku ikiwataka  watanzania wengine kuona umuhimu wa kutoa michango kwa familia hii na zinmgine zenye mahitaji .

  Aliitaja akaunti namba ambayo watanzania wanaweza kutoa michango yao kwa familia hiyo kuwa ni  00420111912801 na kusema kuwa kufanya hivyo  kutarahisisha matibabu ya Rashid ambaye tayari alishaanza matibabu hapa  nchini na nje ya nchi.

  Kwa upande wake Fatuma Rashid mke wa Salim Rashid   aliushukuru uongozi wa benki hiyo kwa mchango wao na kuwaomba kuendelea kuwa nao bega kwa bega katika kufanikisha matibabu zaidi ya Rashid.

  “Nashukuru Benki ya Ukombozi kwa kuliona tatizo la mume wangu na kulichukulia uzito kwa kuchangia kiasdi hicho cha fedha sambamba na kufungua akaunti, hii imetupa moyo kuwa jamii ipo pamoja nasi,”alisema Fatuma.

   kufungua akauti kwa familia hiyo ili kuwezesha jamii kuweza kushiriki kucahngia gharama za matibabu.

  “Kama Benki tumeitembelea familia hii ya Rashid ili  kuifariji na tumeshaifungulia akaunti ya pamoja itakayowezesha jamii kutoa michango yao ya hali na mali ili kuwezesha matibabu ya Salim ambaye anasumbuliwa na saratani,”alisema na kuongeza kuwa hii pia itasaidia taasisi mbalimbali kuweza kuchangia zaidi matibanu hayo.

  Hata hivyo aliwaomba watanazia wote wenye mapenzi mema kuwa karibu na familia hiyo ili kuwezesha matibabu yaanyike na kuimarisha afya ya mume wake.

  0 0


   Wananchi wafurika katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada inayofanyika katika Soko la Mlowo mkoani Songwe.


   Wananchi wakipata huduma za usajili wa vitambulisho vya Taifa katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada katika Soko la Mlowo mkoani Songwe. 
   Wananchi wakisoma kitabu cha Muongozo wa Mawasiliano cha Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
   Wananchi wakipata huduma za usajili wa vitambulisho vya Taifa katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada katika Soko la Mlowo mkoani Songwe.
  Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mabel Masasi akitoa vipeperushi na vitabu  mbalimbali vya Elimu ya mawasiliano kwa Wananchi mkoani Songwe katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada inayofanyika katika Soko la Mlowo mkoani Songwe.

  WAKAZI wa Mkoa wa Songwe  na viunga vyake wamejitokeza kwa wingi katika kampeni  ya Mnada kwa Mnada ambapo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikishirikiana na Kampuni ya simu, Jeshi la Polisi Kitengo cha Uhalifu Mitandaoni  na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kwa ajili  ya utoaji wa huduma za usajili wa laini za simu kwa kutumia vitambulisho vya kitaifa na kuhakikiwa na kampuni za simu kwa kuweka alama za vidole kwa laini za simu.


  Mkuu wa nyanda za Juu Kusini wa TCRA na sio Kaskazini  Mhandisi  Asajile John amesema ni fursa kwa wananchi wa Mkoa wa Songwe katika Soko la Mlowo na viunga vyake  kupata huduma kutokana na kuwa na mnyororo wadau wa  mawasiliano. 

  John amesema kuwa  Mnada kwa Mnada TCRA ilianzisha ili kutoa fursa ya Wananchi kuhudumiwa hasa wakati huu usajili wa laini za simu kwa alama za vidole.

  John amesema  kuwa kampeni ya Mnada kwa Mnada ni kwa ajili ya kutoa elimu ya mawasiliano kwa kushirikiana na wadau katika kujibu changamoto wanazokutanazo katika utumiaji wa mawasiliano nchini.

  John amesema kuwa wananchi wasio kuwa na Vitambulisho vya NIDA wahakikishe  wanapata katika usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole na huduma nyinginezo za Mawasiliano hayo.

  Amesema kuna watu wengine wanatumia mawasiliano ya simu bila kujua ambapo Jeshi Polisi lipo katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada ili kuwaelewesha makosa ya jinai ya matumizi ya simu.
  Aidha amesema Kampeni hiyo ni endelevu katika kuwafikia ikiwa kuhakikisha kila mwananchi anajisajili laini yake kwa alama za vidole kwa kutumia kitambulisho cha taifa cha NIDA.

  Mhandisi John amesema kuwa TCRA iko kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi ili mtumie Mawasiliano kwa usalama kutokana na elimu tunayotoa.

  John amesema kuwa wananchi wajitokeze katika kujisajili kwa alama za vidole kabla ya Desemba 31.

  "TCRA tumejidhatiti katika kuwafikia  wananchi katika utoaji wa elimu za utumiaji wa bidhaa za mawasiliano kwa kutatua changamoto katika huduma hiyo"amesema John

  0 0

  Rais wa Uganda Mh. Yoweri Museveni na Mwenyeji wake Rais wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli wakisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Bw. Abdulmajid Nsekela wakati walipotembelea mabanda kwenye kongamano la biashara kati ya Tanzania na Uganda linalofanyika leo kwenye ukumbi wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tazania Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Bw. Abdulmajid Nsekela wakati walipotembelea mabanda kwenye kongamano la biashara kati ya Tanzania linalofanyika leo kwenye ukumbi wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tazania Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Bw. Masanja Kadogosa wakati walipotembelea mabanda kwenye kongamano la biashara kati ya Tanzania na Uganda linalofanyika leo kwenye ukumbi wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo.
  Rais wa Uganda Mh. Yoweri Museveni na Mwenyeji wake Rais wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Bandari (TPA) Deusdedit Kakoko wakati walipotembelea banda la mamlaka hiyo.
  Rais wa Uganda Mh. Yoweri Museveni na Mwenyeji wake Rais wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli wakitembelea mabanda mbalimbali katika Kongamano la Biashara kati ya Tanzania na Uganda kwenye ukumbi wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
  Mkurugenzi wa Benki ya CRDB Bw. Abdulmajid Nsekela akizungumza na Mkurugenzi wa Bohari ya Dawa MSD Bw.Laurean Rugambwa Bwanakunu wakizunguza katika kongamano hilo.
  Kutoka kulia Kutoka kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli TRC Bw Masanja Kadogosa, Mkurugenzi wa TTCL Bw Waziri Kindamba na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Malelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbas.
  Kutoka kulia ni Waziri Mh. Omary Mgumba Naibu Waziri wa Kilimo, Mh Dotto Biteko Waziri wa Madini, Mh. Luhaga Mpina Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Immocent Bashungwa Waziri wa Biashara na Viwanda wakiwa katika Kongamano hilo.
  Kutoka kushoto ni Mh. Hamad Masauni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Abdallah Ulega, Naibu Waziri wa Ardhi Dkt Angelina Mabula na Anthony Mavunde Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Anthony.
  Meneja Uhusiano wa Benki hiyo, Godwin Semunyu kulia akiwa pamoja na baadhi ya washiriki wa mkutano huo
  Mkurugenzi wa Benki ya CRDB Bw. Abdulmajid Nsekela akizungumza na Mkurugenzi wa Bohari ya Dawa MSD Bw.Laurean Rugambwa Bwanakunu wakizunguza katika kongamano hilo

  0 0

  Jengo lenye huduma za kibingwa ambalo linahudumia hadi wanachama 350 wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wanahudumiwa kwa siku. Limegharimu Shilingi Milioni 800 tulizowezeshwa na NHIF na tangu 2017 wameshamaliza kurejesha malipo.
  Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Prof. Abel Makubi akiongea na maofisa habari wa wizara ya afya na taasisi zake
  Maabara ya Vinasaba iliyopo kwenye hospitali ya rufaa ya kanda ya Bugando
  Wafamasia kitengo cha kuchanganya dawa kwa ajili ya matumizi ya binadamu ikiwemo magonjwa ya moyo,ngozi kwa akina mama na watoto

  Picha ya pamoja ya Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Prof. Abel Makubi akiwa na Maofisa Habari na Mahusiano kutoka Wizara ya Afya na Taasisi zake ambao wapo mkoani Mwanza kujionea hali ya maboresho ya hospitali hiyo.

  ………………………


  Na.Catherine Sungura, Mwanza


  Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imefanikiwa kukusanya zaidi ya shilingi bilioni tatu kwa mwezi baada ya kuimarisha mfumo wa makusanyo wa kieletroniki katika utoaji huduma.


  Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa hospitali hiyo Prof. Abel Makubi wakati akielezea mafanikio ya hospitali hiyo kwa maofisa habari wa Wizara ya Afya na Taasisi zake waliotembelea hospitali hiyo kujionea maboresho ya sekta ya afya katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano.


  Prof.Makubi alisema kuwa baada ya kuimarisha mfumo huo hospitali hiyo imeweza kukusanya kiasi hicho cha fedha tofauti na awali ambapo walikua wakikusanya shilingi milioni mia nane kwa mwezi.


  “Licha ya makusanyo haya mfumo huu pia umesaidia kurahisisha utoaji wa huduma kwa wepesi na kwa haraka kwani zamani kulikuwa na upotevu wa mafaili na hivyo kuleta malalamiko kwa wagonjwa”. Alisema Prof.Makubi.


  Kwa upande kwa huduma za kibingwa na bobezi mkurugenzi huyo alisema kuwa baada ya Serikali kushusha huduma za kibingwa kwenye hospitali za rufaa za kanda hospitali hiyo imefanikiwa kununua mashine kadhaa za uchunguzi wa magonjwa ikiwemo CT- SCAN ya kisasa, kwa mapato ya ndani yenye thamani ya shilingi bilioni 1.7 na hivyo kuweza kuwaondolea adha wakazi wa mwanza na majirani zake.


  “Pia tumeboresha huduma za maabara kwa kununua vifaa vya kisasa zaidi ya nane kwa ajili ya kupima magonjwa mbalimbali kwa muda wa masaa matatu kutoka masaa 12 yaliyokuwa yakitumika kutokana na vifaa vya zamani na hivyo imeleta faraja kwa wagonjwa kuongezeka kupata huduma hospitalini hapa tofauti na nyuma ambapo vipimo vingi walikua wanavipata nje ya hospitali yetu”. Alisema Mkurugenzi huyo.

  Hata hivyo Prof. Makubi alisema katika kuboresha miundombinu wameweza kujenga jengo zuri lenye huduma zote za madaktari bingwa ambapo wanapokea wagonjwa 350 kwa siku wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Taifa (NHIF) ambalo limegharimu shilingi milioni 800 walizowezeshwa na NHIF na tangu mwaka 2017 wamefanikiwa kumaliza kulipa mkopo huo.

  Prof.Makubi ameipongeza Wizara ya Afya pamoja na NHIF kuhamasisha wananchi kukata bima ya afya na hivyo kuongeza watumiaji wa bima hiyo kwa asilimia 70 tofauti na awali ambapo walikuwa wakipata wanachama hao kwa asilimia 30 hadi 40.

  0 0

   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba (kushoto) na Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe (katikati), Bungeni jijini Dodoma, Septemba 6.2019.
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, Bungeni jijini Dodoma, Septemba 6.2019. 
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, nje ya jengo la Bunge, jijini Dodoma, Septemba 6.2019.
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mwita Waitara, nje ya jengo la Bunge, jijini Dodoma, Septemba 6.2019.
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na wanafunzi wa shule ya Capital Dodoma, nje ya jengo la Bunge, jijini Dodoma, Septemba 6.2019.
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Septemba 6.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).


  0 0

  MRATIBU wa Malaria kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,(TAMISEMI), Stella Kajange, amesema ugonjwa wa Malaria umepungua kwa asilimia 50 akimaanisha kuwa kiwango cha maambukizi ya vimelea vya ugonjwa huo vimepungua kutoka asilimia 15 kwa mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 7.3 kwa mwaka 2018.

  Akizungumza na waandishi wa habari, wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani wakati wa mkutano wa wadau wa masuala ya malaria alisema kupungua kwa ugonjwa huo wa Malaria kumetokana na mafanikio waliyopata kati ya Serikali, wadau na wahisani wakiwemo. Alisema Tanzania inaendelea vizuri katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa malaria ambao ugonjwa huo umekuwa ni tishio kwa jamii.

  “Licha ya kupungua kwa ugonjwa huu nchini lakini ugonjwa huu bado ni tishio kwa jamii na hivyo serikali inaendelea na utekelezaji wa afua mbalimbali ili kuhakikisha tatizo hilo linapungua,”alisema Kajange

  Aidha aliongeza sera ya mwaka 2007 inaelezea muelekeo wa nchi katika kuhakikisha kuwa wananchi wanakuwa na afya njema ili waendelee na shughuli zao mbalimbali za uzalishaji na kujipatia kipato.

  “Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo tunatekeleza sera mbalimbali kwa faida ya wananchi wetu kuhakikisha wanakuwa na afya njema,”alisema na kuongeza kuwa 

  “Serikali ya Tanzania inafanya kazi na wadau mbalimbali wa Maendeleo……tunawashukuru sana PMI kwa pamoja na USAID na wadau wengine kwa kutuunga mkono kwa miradi inayotekelezwa sehemu mbalimbali nchini,”alisema Kajange

  Naye Msimamizi wa Kitengo cha Kupambana na Malaria Mradi wa Taifa wa kudhibiti Malaria (NMCP),Winfred Mwafongo alisema ugonjwa wa Malaria unaathiri zaidi kundi la wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano.

  Alisema katika mikakati yao waliyojiwekea ni kuhakikisha wanadhibiti Malaria nchini ambapo tayari wameweka utaratibu wa afua ambazo zinazohusika na udhibiti wa Malaria.

  Alisema miongoni mwa afua hizo ni kuhakikisha kuna kuwepo na matumizi ya vyandarua vyenye dawa ,kuangamiza vijidudu na upuliziwaji wa viuadilifu kudhibiti mbu.

  Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Mradi wa VectorWorks Waziri Nyoni alisema mradi huo umedumu nchini takribani miaka mitano ambao ulijikita katika usambazaji wa vyandarua vyenye dawa katika mikoa mbalimbali.

  “Mradi umedumu nchini ndani ya miaka mitano na mwaka huu mwezi September ndio mwisho wa mradi huu,tunaamini kwa ushirikiano tulioupata umeweza kuleta tija kwa jamii katika kuhakikisha wananchi wanatumia vyandarua vilivyowekwa dawa,”alisema. 

  Akizungumzia kuhusu uendelevu wa shughuli zilizokuwa zikitekelezwa na VectorWorks, Waziri Nyoni alisema kuwa “tumejenga mifumo thabiti ya kuhakikisha utaratibu wa ugawaji wa vyandarua kwa walengwa kupitia vituo vya kutolea huduma nchi nzima na kupitia shule za msingi katika mikoa 14, na uwajibikaji unaendelea bila changamoto yoyote, tumejenga uwezo wa bohari kuu ya dawa (MSD) kuendelea na utaratibu huu na pia watendaji ngazi za halmashauri wataendelea kusimamia utoaji wa huduma hizi hata bila uwepo wa VectorWorks ambayo ni mafanikio makubwa ya mradi” 

  Aidha alisema nchini Tanzania mradi huo ulijikita katika maeneo matatu ikiwemo kushauri serikali juu ya sera zinazohusu masuala ya malaria, ,Utekelezaji wa afua ya ugawaji wa yyandarua vyenye dawa, kufanya tafiti juu ya ugonjwa wa malaria na upimaji wa matokeo ya program za malaria.

  Mradi wa VectorWorks umekuwa ukifadhiliwa na USAID kupitia mfuko wa Rais wa Marekani wa kudhibiti Malaria (PMI).
  Mkurugenzi wa mradi wa VectorWorks Waziri Nyoni (kulia) akimkabidhi cheti maalum Msimamizi wa kitengo cha kudhibiti malaria nchini Winfred Mwafongo (kushoto) wakati wa halfa wa kumalizika mradi huo ambao umedumu kwa miaka mitano. VectorWorks imekuwa ikiendesha mradi wa kugawa vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu hapa nchini chini ya ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani – USAID kupitia Mfuko wa Raisi wa Marekani wa kudhibiti malaria.

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais Dkt John Pombe Magufuli akihutubia wakati wa ufunguzi wa kongamano la kwanza la kibiashara kati ya Tanzania na Uganda lililofanyika jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo limewashirikisha wafanyabiashara wa Tanzania na Uganda huku wakiongozwa na marais Dkt John Pombe Magufuli na Mhe. Yoweri Museveni. Picha zote na Matokeo Chanya+.
  Wafanyabiashara wa Tanzania na Uganda wakifuatilia hotuba za marais wa Tanzania na Uganda.
  Rais wa Uganda Rais Yoweri Museveni akihutubia wakati wa ufunguzi wa kongamano la kwanza la kibiashara kati ya Tanzania na Uganda lililofanyika jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo limewashirikisha wafanyabiashara wa Tanzania na Uganda.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais Dkt John Pombe Magufuli akifuatilia hotuba ya Rais wa Uganda Mheshimiwa Yoweri Museveni wakati wa ufunguzi wa kongamano la kwanza la kibiashara kati ya Tanzania na Uganda lililofanyika jijini Dar es Salaam.
  Wafanyabiashara wa Tanzania na Uganda wakifuatilia.
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Palamagamba Kabudi akiwakaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais Dkt John Pombe Magufuli na Rais wa Uganda Mheshimiwa Yoweri Museveni wakati wa ufunguzi wa kongamano la kwanza la kibiashara kati ya Tanzania na Uganda lililofanyika jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Palamagamba Kabudi,

  0 0


  Na Said Mwishehe,Michuzi Blogu 

  TAASISI tatu nchini Tanzania zisizo za kiserikali wamemuomba Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika(SADC)Rais John Magufuli kuingilia kati kutafuta ufumbuzi wa sintofahamu inayoendelea nchini Afrika Kusini.

  Wakizungumza leo Septemba 6,2019 , na waandishi wa vyombo vya habari viongozi wa taasisi hizo ambazo ni Action for Change(ACHA), The Right Way(TRW) na Mtandao wa Mashirika ya Kutetea Haki za Binadamu Kusini mwa Afrika(SAHRINGON) wamesema kuna kila sababu ya viongozi kuchukua hatua ya kukomesha machafuko yanayoendelea Afrika Kusini.

  Akizungumza kwa niaba ya taasisi hizo, Martina Kabisama kutoka SAHRINGON amesema kwa pamoja wanatoa mwito kwa Mwenyekiti wa SADC Dk.Magufuli kuchukua hatua za haraka kukomesha ukatili unaofanywa nchini humo dhidi ya watu wa mataifa mengine ya Afrika.

  "Wimbi la kushambuliwa kwa watu wanaoitwa wageni si peke linatokea Afrika Kusini, bali pia limetokea katika nchi mbalimbali katika ukanda wetu.Mfano siku za karibuni kuna mbunge mmoja nchini Kenya alitoa kauli inayoumiza kwa wale aliowaita wageni.

  "Uzalendo ambao uliasisiwa na waasisi wa mataifa ya Afrika na mababa wa Afrika umevamiwa na kuufanya uzalendo usinyae."Ni suala la kupiga kengele kwamba Waafrika kwa pamoja waungane na kuanisha zaidi chanzo cha ubaguzi huu mpya unaobagua watu wa mataifa mengine , miongoni mwa watu wa mataifa,"amesema.

  Kabisama ameongeza ACHA, TRW na SAHRINGON wanatambua kuwa Tanzania ndiye Mwenyekiti wa SADC , hivyo wanayo imani kuwa Rais wetu mpendwa Dk.Magufuli anaweza kuitumia nafasi aliyonayo kumaliza sintofahamu inayoendelea nchini Afrika Kusini.

  "Tunatoa mwito wa mikakati ya kuvunja minyonyoro ya utengano wa namna hii ya unyanyasaji wa aina hii ambavyo vyote ni dalili ya kutengana na siyo kuungana-Muungano wa Afrika.

  "Viongozi wa Afrika budi warejee uongozi uliotukuka(uongozi wa pamoja na wa mmoja mmoja) kujiamini na weledi, kutengeneza mitandao na viongozi wenzao wa Afrika...

  "Ili kupambanua vikwazo kwa pamoja na kupambana kwa pamoja dhidi ya ubaguzi wa watu wa mataifa unaoota mizizi katika ukanda huu wa dunia,"amesema.

  Kabisama amesema kile kilichotokea kwa kaka na dada zetu nchini Afrika Kusini ambapo raia wetu wa Afrika wa damu wanaumia kwa kiwango kikubwa kwa kunyanyapaliwa uto wao, haki zao za binadamu a fursa ya maendeleo yao ni fedheha kwa wanaotekeleza vitendo hivyo.

  "Kinachotokea nchini Afrika Kusini na sehemu zingine za bara letu ni cha kihistoria ambapo machafuko ya ukatilii yameachwa bila kushughulikiwa na wahusika."Kwa mshangao wetu Afrika Kusini ni miongoni mwa nchi zilizoridhia na kusaini mikataba na mapatano ya kimataifa.

  "Mathalani mkataba wa kimataifa wa kupinga aina zote za ubaguzi na mkataba wa kuondoa aina zote za unyanyasaji dhidi ya wanawake.Ziko wapi sheria za kimataifa huko Afrika Kusini?"

  Ameongeza wakati wanatoa mwito huo kwa ajili ya kuvunja minyororo hiyo ya ubaguzi na kutengwa , pia wanatoa mwito kwa raia wa Afrika kusimama kidete kupigania amani endelevu na utulivu milele.

  "Iwapo waafrika wanaota ndoto ya uzalendo wa Afrika , ndoto hiyo ni budi iwe kweli kupitia uhuru , usawa na mshikamano,"amesema Kabisama.
   Mratibu Taifa  wa Mashirika ya kutetea Haki za Binadamu kusini mwa Afrika (SAHRINGON),Martina Mnenegwa Kabisama akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar kuhusu kutoa mwito kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo  Kusini mwa Afrika (SADC) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli kuchukua hatua za haraka kukomesha ukatili unaofanywa nchini Afrika Kusini dhidi ya Watu wa Mataifa mengine.  Picha na Michuzi JR

  0 0

  Nairobi, September 6, 2019: Airtel Africa, a leading telecommunications services provider with operations in 14 countries across Africa, is pleased to announce the appointment of George Mathen as Managing Director for Airtel Tanzania PLC. The appointment will take effect on the 1st of October, 2019.

  Mr. Mathen has more than 20 years’ of experience in senior management roles, with experience in the telecommunications and FMCG sectors. Prior to joining Airtel Africa, he was CEO – Homes, at Bharti Airtel In India where he designed and implemented the Airtel Home strategy. Prior to taking up the role, he has also been the CEO of various circles within the India business. Before joining Bharti Airtel, George also spent ten years’ in Coca-Cola India in several capacities including Area General Manager and Sales Manager across various regions. He holds a Bachelor of Commerce degree and has done his Masters in Business Administration. 

  Commenting on this appointment, Raghunath Mandava, Airtel Africa’s Chief Executive Officer, said: “We are excited to welcome George as Managing Director for Airtel Tanzania PLC. He will be responsible for the profitable growth of the business and help Airtel be the preferred telecom brand to bridge the digital divide and preferred partner to grow financial inclusion. 

  I would also wish to take this opportunity to sincerely thank Sunil Colaso, the outgoing Managing Director, leaving after 13 years’ of dedicated service to Airtel, including the last 6 years’ as Managing Director for Airtel Tanzania PLC. We wish him the very best as he starts a new chapter in his life.”


  0 0


  Na Mwandishi wetu,Tabora

  Wafanyabiashara katika Mkoa wa Tabora,wengi hawajilipi mishahara kutokana na kazi zao wanazofanya na hivyo kukosa fursa ya kufahamu namna biashara zao zinavyokua au zinavyodorora.

  Haya yamebainishwa na Meneja wa NMB kanda ya Magharibi, Sospeter Magese,wakati akizungumza na wafanyabiahara wa Mkoa wa Tabora, alisema wengi huwa hawajilipi mishahara na kufanya mahesabu yao kutokuwa vizuri.

  “Inashangaza mfanyabiashara anawalipa wafanyakazi wake mshahara lakini yeye akiwa mkurugenzi hajilipi mshahara na pia huchanganya matumizi binafsi na ya biashara jambo amvalo huyumbisha mitaji yao.

  Akizungumza katika kikao cha kupokea maoni ya wafanyabiashara juu ya huduma inayotolewa na NMB, Magese aliwaeleza kuwa kupitia mishahara yao ndio matumizi ya binafsi yanaweza kutoka huko na sio katika biashara.

  Aliwaeleza kuwa benki ya NMB ni benki yao na waitume kwani imejipanga kushirikiana nao katika kukuza uchumi wa Taifa.Mwenyekiti wa wafanyabiashara wenye akaunti benki ya NMB,Ahadi Mviombo,aliwahimiza wafanyabiashara kutenga sehemu ya mauzo yao kwa ajili ya kulipa madeni wanayokopa.

  “Kama ukiweza kutenga angalau shilingi elfu tano kila siku kwa ajili ya marejesho mtihani utakuwa umeshinda”AlisemaMfanyabiashara Mwalimu Mambo,aliipongeza NMB kwa utaratibu wake wa kuwafundisha wafanyabiashara namna ya kuweka mahesabu sawana kutafuta faida.

  “Tunashukuru kwa elimu tunayopewa na benki hii ambayo kwa kweli inatusaidia sana katika biashara zetu”Alisema

  Kikao hicho chenye lengo la kupokea maoni kutoka kwa wafanyabiashara ziadi ya 300 wenye akaunti NMB pia kilihudhuriwa na wafanyakazi wa benki hiyo ambao walitoa elimu ya huduma mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo.
  Baadhi ya wafanyabiashara wakifurahia jambo wakati wa kongamano la wanachama wa klabu ya wafanyabiashara mkoa wa Tabora uliolenga kuwapa mafunzo na nidhamu ya biashara. Kongamano hilo liliandaliwa na Benki ya NMB kuwapa elimu na fursa zakukuza biashara zao kupitia benki hio.

  0 0


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wakeRais wa Uganda Mheshimiwa Yoweri Kaguta Museveniwakiangalia mabanda mbalimbali ya wafanyabiashara waTanzania na Uganda kabla ya kuzungumza na wafanyabiashara
  wa Mataifa hayo katika Ukumbi wa Julius Nyerere Convention
  Centre jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha yapamoja na Rais wa Uganda Mheshimiwa Yoweri KagutaMuseveni kabla ya kuelekea katika mkutano wa
  Wafanyabiashara wa Uganda na Tanzania uliofanyika katika
  ukumbi wa mkutano wa Mwalimu Nyerere
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katikamazungumzo na Rais wa Uganda Mheshimiwa Yoweri KagutaMuseveni mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wakeRais wa Uganda Mheshimiwa Yoweri Kaguta Museveniwakiangalia mabanda mbalimbali ya wafanyabiashara wa
  Tanzania na Uganda kabla ya kuzungumza na wafanyabiasharawa Mataifa hayo katika Ukumbi wa Julius Nyerere ConventionCentre jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Uganda Mheshimiwa Yoweri KagutaMuseveni akizungumza na wadau mbalimbali wa biasharakutoka Uganda na Tanzania katika mkutano wao wamajadiliano uliofanyika katika Ukumbi wa Julius NyerereConvention Centre jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza nawadau mbalimbali wa biashara kutoka Uganda na Tanzaniakatika mkutano wao wa majadiliano uliofanyika katika Ukumbi
  wa Julius Nyerere Convention Centre jijini Dar es Salaam.

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dkt. John Pombe Magufulivakipeana mikono na mgeni wake  Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni baada ya kufungua rasmi jengo la Taasisi ya Mwalimu Julius Nyerere Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Ijumaa Septemba 6, 2019
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dkt. John Pombe Magufuli na mgeni wake  Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni wakisaidiwa na viongozi  wengine wakikata utepe kuashiria ufunguzi  rasmi wa jengo la Taasisi ya Mwalimu Julius Nyerere Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Ijumaa Septemba 6, 2019
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dkt. John Pombe Magufuli na mgeni wake  Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni wakitembezwea na Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Julius Nyerere Julius Nyerere ndani ya jengo walilolifungua kwa pamoja  jijini Dar es salaam leo Ijumaa Septemba 6, 2019
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dkt. John Pombe Magufuli  na mgeni wake  Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na wanafamilia wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage nyerere wakati wa sherehe za ufunguzi  rasmi wa jengo la Taasisi ya Mwalimu Julius Nyerere Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Ijumaa Septemba 6, 2019.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dkt. John Pombe Magufuli akimwonesha  Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni baadhi ya picha na maelezo ya kumbukumbu ya Baba wa Taifa walipowasili katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini kwa
  ajili ya Kongamano la Wafanyabishara wa Tanzania na Uganda jijini Dar es salaam leo Ijumaa Septemba 6, 2019
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dkt. John Pombe Magufuli na mgeni wake Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni wakisikiliza maeleo  kutoka kwa  Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya CRDB Bw.Abdulmajid Nsekela walipotembelea vibanda vya maonesho  wakati wa Kongamano la Wafanyabishara wa Tanzania na Uganda vkatika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Ijumaa Septemba 6, 2019 .PICHA NA IKULU
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dkt. John Pombe Magufuli akiomba wahudhuriaji kusimama kwa dakika tatu za heshima ya kumkumbukaaliyekuwa Rais wa Zimbabwe Marehemu Robert Mugabe aliyefariki jana huko Singapore akiwa katika matibabu. Hii ilikuwa ni kabla ya kuanzakuhutubia Kongamano la Wafanyabishara wa Tanzania na Uganda lililohudhuriwa pia na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Ijumaa Septemba 6, 2019


  0 0

  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akitoa hutuba yake katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania-UTPC uliofanyika leo katika ukumbi wa Idris AbdulWakil,Vuga Mjini Zanzibar.
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akitoa hutuba yake katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania-UTPC uliofanyika leo katika ukumbi wa Idris AbdulWakil,Vuga Mjini Zanzibar. [Picha na Ikulu] 07/09/2019.
  Baadhi ya Washiriki wa Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania-UTPC wakiwa katika ufunguzi mkutano huo uliofunguliwa leo na RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) katika ukumbi Idrisa Abdul Wakili Vuga Mjini Zanzibar
  Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Muungano wa klabu za Waandishi wa Habari Tanzania-UTPC wakiwa katika ukumbi Idrisa Abdul Wakili Vuga Mjini Zanzibar katika ufunguzi wa mkuitano huo uliofanywa leo na RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani)
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) pamoja na Viongozi wengine katika Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania-UTPC uliofanyika leo katika ukumbi Idris Abdul Wakili, Vuga Mjini Zanzibar,(wa tatu kulia) Rais wa UTPC Deogratias Nsokolo
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akitoa hutuba yake katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania-UTPC uliofanyika leo katika ukumbi wa Idris AbdulWakil,Vuga Mjini Zanzibar.
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Rais wa UTPC Deogratias Nsokolo alipowasili katika viwanja vya ukumbi Idris Abdul Wakili Vuga Mjini Zanzibar katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania-UTPC uliofanyika leo.
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Balozi wa Sweden Nchini Tanzania Anders Sjøberg alipowasili katika viwanja vya ukumbi Idris Abdul Wakili Vuga Mjini Zanzibar leo katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania-UTPC

  0 0

  Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa akifunga kongamano la Biashara kati ya Tanzania na Uganda lililofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania Septemba 6-7, 2019 ambapo Kongamano hilo liliwahusisha wafanyabishara wa nchi zote mbili na yalifunguliwa Septemba 6, 2019 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na Rais wa Uganda Yoweri Museveni. Picha zote  na Matokeo Chanya+
  Wafanyabiashara wa Tanzani na Uganda wakifuatilia.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade), Edwin Rutageruka akielezea mambo machache wakati wa kongamano la Biashara kati ya Tanzania na Uganda lililofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania Septemba 6-7, 2019.
  Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa (kulia) akiwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro (kushoto) wakifuatilia kwa makini. 
   Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro  (kulia) akiwa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) Bwana Godfrey Simbeye.
  Wafanyabiashara wa Tanzania na Uganda wakifuatilia tukio hilo.
  Mkurugenzi wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) Bwana Godfrey Simbeye akihutubia wakati wa ufungaji wa kongamano la Biashara kati ya Tanzania na Uganda lililofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania Septemba 6-7, 2019 ambapo Kongamano hilo liliwahusisha wafanyabishara wa nchi zote mbili na yalifunguliwa Septemba 6, 2019 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na Rais wa Uganda Yoweri Museveni.  
  Wafanyabiashara wa Tanzania na Uganda wakifuatilia tukio hilo.  0 0  Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa wa Tigo Pesa, James Sumari (kulia) akimkabidhi mfano wa hundi ya Sh. Milioni mbili, Mshindi wa Promosheni ya Mawakala wa Tigo Pesa iliyokuwa inajulikana kama ‘Cash In Promotion’, Said Khatibu kutoka Zanzibar. Promosheni hii ilifanyika mwezi wa nne, mwaka huu.

  Bwana Said Issa Khatib,alianza safari yake ya kuelekea kwenye mafanikio kwa kutumia kadi ya simu ya kuazima kutoka kwa jirani yake mwaka 2014, kwa sasa ni moja kati ya mawakala wakubwa zaidi wa Tigo Pesa, mjini Zanzibar. Biashara imekua kutoka ilivyokuwa mwanzoni na kufikia kufanikiwa kukuza biashara yake katika kipindi cha miaka mitano iliyopita kufikia kuwa biashara ya mamilioni, jambo ambalo liliwezeshwa na idadi ya wateja inayoongezeka kila siku ya wateja wa Tigo Pesa.

  Bwana Khatib ambaye pia ni mshindi wa tuzo nyingi za Tigo Pesa zenye jumla ya milioni 15/- katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, alisema kwamba alianza biashara yake kwa kutumia line ya simu aliyoazima kutoka kwa jirani yake. Kama ilivyo kwa maelfu ya mawakala wengine waliosambaa nchi nzima, Khatib aliona fursa kubwa katika biashara ya kampuni ya simu ya Tigo ya kuhamisha pesa baada ya kujipatia line yake mwenyewe ya Till ya Tigo Pesa miaka mitano iliyopita.

  "Nilitumia line ya jirani yangu kwa muda wakati huo nikiwa natunza pesa kwa ajili ya kuweza kupata line yangu mwenyewe. Nilikuwa nampa jirani yangu asilimia 70 ya mapato ya siku wakati mimi nakibakiwa na asilimia 30", bwana Khatib ambaye ni baba wa watoto watatu alisema wakati akibainisha kwamba mpango wake ulikuwa ni kuwa super dealer wa kampuni ya Tigo mjini Zanzibar, kampuni ya huduma za simu za mkononi inayokua kwa kasi zaidi.

  0 0


  Mwenyekiti wa Klabu ya Golf ya Lugalo, Brigedia Jenerali mstaafu, Michael Luwongo akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuanza rasmi kwa Mashindano ya Mchezo wa Golf ya Mkuu wa Majeshi yanayofanyika kwa siku mbili viwanja vya mchezo huo Lugalo jijini Dar es Salaam. Benki ya NMB imedhamini Mashindano maalum ya Mchezo wa Golf ya Kombe la Mkuu wa Majeshi nchini "NMB CDF TROPHY".
  Baadhi ya wachezaji wa Golf wakipokea sehemu ya vifaa vya kucheza mchezo huo toka kwa mdhamini mkuu wa mashindano hayo, Benki ya NMB kabla ya kuanza kucheza. Benki ya NMB imedhamini Mashindano maalum ya Mchezo wa Golf ya Kombe la Mkuu wa Majeshi nchini "NMB CDF TROPHY".
  Kushoto ni baadhi ya wachezaji wa Golf wakipokea sehemu ya vifaa vya kucheza mchezo huo toka kwa mdhamini mkuu wa mashindano hayo, Benki ya NMB kabla ya kuanza kucheza.

  Mchezaji wa Golf, Tumwesige Mujwauzi toka Benki ya NMB akiendelea na Mashindano maalum ya Mchezo wa Golf ya Kombe la Mkuu wa Majeshi nchini "NMB CDF TROPHY" katika viwanja vya Club ya Golf Lugalo jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Majeshi, Mstaafu Jenerali George Waitara akishiriki Mashindano ya Mchezo wa Golf ya Kombe la Mkuu wa Majeshi nchini "NMB CDF TROPHY" katika viwanja vya Club ya Golf Lugalo.
  Nahodha wa Timu ya NMB inayoshiriki Mashindano ya Mchezo wa Golf ya Kombe la Mkuu wa Majeshi nchini yaani "NMB CDF TROPHY" akizungumza na wanahabari kuelezea walivyojiandaa kushiriki mchezo huo.
  Baadhi ya wachezaji wa Golf katika Mashindano maalum ya Mchezo wa Golf ya Kombe la Mkuu wa Majeshi nchini "NMB CDF TROPHY" linalofanyika viwanja vya TPDF Lugalo Golf Club wakiendelea na mchezo.
  Baadhi ya wachezaji wa Golf katika Mashindano maalum ya Mchezo wa Golf ya Kombe la Mkuu wa Majeshi nchini "NMB CDF TROPHY" linalofanyika viwanja vya TPDF Lugalo Golf Club wakiendelea na mchezo.
  Mchezaji wa Golf kutoka Benki ya NMB akiendelea na Mashindano ya Mchezo wa Golf ya Kombe la Mkuu wa Majeshi nchini "NMB CDF TROPHY" linalofanyika viwanja vya TPDF Lugalo Golf Club.
  Mchezaji wa Golf kutoka Benki ya NMB akiendelea na Mashindano ya Mchezo wa Golf ya Kombe la Mkuu wa Majeshi nchini "NMB CDF TROPHY" linalofanyika viwanja vya TPDF Lugalo Golf Club.
  Uzinduzi Mashindano ya Mchezo wa Golf ya Kombe la Mkuu wa Majeshi nchini "NMB CDF TROPHY" katika viwanja vya Golf Lugalo.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akiangalia pamba iliyochambuliwa na kufungwa kwenye robota katika kiwanda cha kuchambua pamba cha Alliance Ginneries Ltd, wakati wa ziara ya viongozi wa mkoa huo ya kukagua mwenendo wa ununuzi wa pamba, iliyofanyika Septemba 08, 2019.
  Katibu wa Chama cha Wanunuzi wa Pamba nchini , Bw. Boaz Ogola ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kiwanda cha kuchambua pamba cha Alliance Ginneries Limited kilichopo Bariadi Mkoani Simiyu, akimweleza jambo viongozi wa Mkoa huo walipotembeelea kiwandani hapo kwa lengo la kujionea namna kiwanda hicho kinavyonunua pamba kutoka kwa wakulima katika ziara iliyofanyika Septemba 08, 2019.
  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akiangalia pamba iliyochambuliwa na kufungwa kwenye robota katika kiwanda cha kuchambua pamba cha Alliance Ginneries Ltd, wakati wa ziara ya viongozi wa mkoa huo ya kukagua mwenendo wa ununuzi wa pamba, iliyofanyika Septemba 08, 2019.

  *******************


  Na Stella Kalinga, Simiyu RS

  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amewakikishia wakulima wa pamba mkoani Simiyu kuwa Serikali itahakikisha mwezi huu wa Septemba pamba yote inanunuliwa kwa bei elekezi ya shilingi 1200 kwa kilo na wakulima kulipwa fedha zao, ambapo amesema hadi sasa zaidi ya kilo milioni 54 zenye thamani ya shilingi bilioni 65.1 zimenunuliwa na wakulima wamelipwa fedha zao.

  Mtaka ameyasema hayo wakati wa ziara ya Viongozi wa Mkoa wa Simiyu katika vyama vya ushirika vya msingi (AMCOS) na Kiwanda cha Kuchambua pamba cha Alliance Ginneries Limited wilayani Bariadi, iliyofanyika Septemba 08, 2019 kwa lengo la kujionea mwenendo wa ununuzi wa pamba, ambapo amewataka wanunuzi kutumia fedha walizopewa dhamana na Serikali kwa ajili ya kununua pamba zitumike kuwalipa wananchi badala ya kuzielekeza mahali pengine au kufanya tofauti na makubaliano.

  Amesema makisio ya mkoa ya mavuno yalikuwa ni kuvuna kilo milioni 180 ambapo hadi sasa pamba iliyokusanywa ni kilo milioni 132.7 ambayo thamani yake ni shilingi bilioni 159.3 na kati ya hizo kilo milioni 54.2 zenye thamani ya shilingi bilioni 65.1 zimelipiwa na ambazo bado hazijalipiwa ni kilo milioni 78.5 ambayo thamani yake ni zaidi ya shilingi milioni 94.2.

  Ameongeza kuwa kuelekea katika kipindi cha mvua za vuli Mtaka ni vema wakulima kutoa pamba majumbani na kupeleka kwenye vyama vya ushirika ili iweze kununuliwa na kutunzwa mahali salama, huku akitoa wito pia kwa wanunuzi kujielekeza kwenye maeneo ambayo ni magumu kufikika kipindi cha mvua na maeneo ambayo maghala yake si salama sana.

  Aidha, Mtaka amewakata viongozi wa vyama vya ushirika kuwa waadilifu badala ya kushirikiana na machinga kuwanyonya wakulima kwa kuuza pamba chini ya bei elekezi ya shilingi 1200 na kuwataka wanunuzi kununua pamba kwa mujibu wa utaratibu kwa kuwa watakaobainika kufanya umachinga watachukuliwa hatua na pamba hiyo itapigwa mnada kama ilivyofanyika hivi karibuni Wilayani Bariadi.

  “Ujumbe huu uwafikie wanunuzi wote wa pamba wanaokuja kununua pamba Simiyu , pamba itanunuliwa kwenye vyama vya ushirika vya msingi (AMCOS)kwa bei elekezi ya shilingi 1200 kwa kilo, pamba haitanunuliwa kienyeji kwenye nyumba za watu usiku wa manane kwa bei ndogo, atakayekamatwa asije akalaumu vyombo vya sheria”alisema Mtaka.

  Naye Mwenyekiti wa CCM, Mhe. Enock Yakobo amewataka wanunuzi wa pamba mkoani Simiyu kuhakikisha kuwa wanawalipa wakulima fedha zao kwa wakati ili waweze kujikimu na mahitaji yao na kujiandaa na msimu ujao wa kilimo.

  Katibu wa Chama cha Wanunuzi wa Pamba nchini, Bw. Boaz Ogola amesema Serikali imewahakikishia wanunuzi wote kuwa itakuwa tayari kufidia hasara itakayopatikana endapo watapata hasara wakiuza kwenye soko la dunia baada ya kununua pamba kwa shilingi 1200, hivyo mwenendo wa ununuzi wa pamba nchini ni mzuri ambapo hadi tarehe 01/09/2019 kilo milioni 210 zimeshanunuliwa nchi nzima.

  Kwa upande wao Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga na Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe. Dkt. Seif Shelakaghe wamesema pamba inaendelea kununuliwa katika maeneo yao huku wakisema wataendelea kusimamia na kuhakikisha pamba inanunuliwa kwa kufuata utaratibu uliowekwa na wananchi wanapata fedha zao.

  Awali wakulima wamesema kuwa baadhi ya makampuni ya ununuzi pamba hayajawalipa fedha zao hivyo wakaomba Serikali kuwasaidia kuongea na wanunuzi wa zao hilo ili fedha zao zipatikane kwa wakati waweze kununua chakula na mahitaji mengine na kujiandaa na msimu ujao.

  “Sisi tunaitegemea pamba na hapa kuna makampuni tunawadai fedha zetu tunaiomba serikali itusaidie tupate fedha zetu tuna mambo mengi ya kufanya,tunataka tununue chakula kabla bei haijapanda sasa hivi kila mara bei ya mahindi inapanda”alisema Charles Ng’andwe kutoka Kijiji cha Ibulyu Bariadi.

  0 0

  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

  KASI ya ujenzi wa mradi wa umeme wa maji wa Julius Nyerere (JNHPP) kwenye Mto Rufiji Mkoani Pwani “imemkuna” Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani baada ya kutembelea eneo la mradi huo leo Jumapili Septemba 8, 2019 na kukuta hatua muhimu ya ujenzi wa ADIT (njia ya kufika kwenye handaki la kuchepusha maji) (diversion tunnel), pamoja na miundombinu wezeshi ikiwa imekamilika.
  Sambamba na kupigwa kwa hatua hizo muhimu katika utekelezaji wa mradi huo uliozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Dkt. John Pomba Magufuli Julai 26, 2019 na ambao utazalisha Megawati 2115, pia amepongeza usimamizi na utawala katika mradi huo.

  “Hii ni mara yangu ya nane kutembeela mradi huu tangu uanze, leo nimetembelea ili kuangalia masuala makubwa matatu, kasi ya ujenzi, usimamizi na utawala na masuala yote ya ujenzi wa miundombinu wezeshi ili kuona kama imekaa sawasawa.” Alisema Dkt. Kalemani.
  Alisema baada ya kuangalia masuala hayo amefurahishwa na hatua iliyofikiwa ambapo amewapongeza wasimamizi wa mradi huo TANESCO na TANROADS ambao Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alitoa maelekezo kuwa lazima ujenzi huo usimamiwe na Watanzania wenyewe na ukamilike katika muda uliopangwa ambao ni miezi 42, ambapo miezi 36 ni ya ujenzi na miezi 6 ya mobilization kwa maana ya maandalizi ya vifaa na watumishi ambapo kazi ilianza Juni 15, 2019 na kazi inakwenda vizuri.” Alifafanmua Dkt. Kalemani.
  Akifafanua zaidi Dkt. Kalemani alisema hadi sasa tayari wakandarasi wamekwishatumia miezi nane 8 kati ya 42 na kazi ambazpo zilikuwa zinaendelea kufanyika ni ujenzi wa njia za kuchepusha maji (diversion tunnel), nilikuja Julai 22, 2019 na nikaelekeza kazi hii ifanyike ndani ya siku 45 na ikamilike umbali wa Mita147.6 nashukuru wamemaliza na wameokoa siku 7 kabla ya muda niliotoa.
  Mheshimiwa Dkt. Kalemani pia alisisitiza kuwa  ni matumaini ya serikali wakandarasi watamaliza kazi ya ujenzi ndani ya muda na kwamba hakuna muda utakaoongezwa. 
  “Nimatarajio yetu mkataba unaisha Juni 14, 2022 na nimatumaini yetu kwamba watatukabidhi mradi huo siku hiyo saa 9;30 alasiri wataukab idhi na mimi niukabidhi kwa Watanzania na asitokee mtu atakaejaribu kuuchelkewesha mradi huo, sisi kama serikali tutahakikisha tunaanza kumchelewesha yeye kwanza kabla hajatuchelewesha sisi kukamilisha mradi huo.” Alionya.

  Alisema mradi huo wa bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere (JNHPP) ni muhimu, bwawa hilo ni kubwa sana litahitaji kilomita za ujazo Aliwataka Watanzania kutunza vyanzo vya maji yanayoelekea kwenye mto Rufiji ili kuwepo uhakika wa upatikanaji wa maji ya kutosha ni bwawa kubwa litahitaji maji kwenye ujazo wa mita za ujazo bilioni 33.2 hivyo maji ya kutosha yatahitajika.
  "Bwawa hili ni kubwa kati ya mabwawa 70 duniani bwawa la JNHPP ni bwawa mojawapo, kati ya mabwawa manne makubwa Afrika bwawa hili ni mojawapo na ni la kwanza kwa ukubwa Afrika Mashariki kwa hivyo Watanzania wanayo kila sababu ya kujivunia na ni wajibu wetu kuyinza na kuhifadhi vyanzo vuya maji." Alisisitiza.

  Alisema manufaa ya mradi huo ni pamoja na kuongeza umeme kwenye gridi ya taifa, kusambaza umeme vijijini na kwenye viwanda, pia utasaidia sana kupunguza uharibifu wa mazingira.
  Awali akitoa taarifa ya mafanikio ya utekelezaji wa mradi huo yaliyofikiwa hadi sasa, Mratibu wa Mradi huo Mhandisi Steven Manda ambaye pia ni Meneja Miradi wa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) alisema, pamoja na kukamilika kwa ujenzi wa handaki la kuchepusha maji, pia daraja namba mbili kwa maana ya miundombinu wezeshi nalo limekamilika na sasa mashine kubwa na vifaa vya ujenzi vinavushwa kutoka upande mmoja wa mto kwenda upande wa pili kupitia daraja hilo.
   WAZIRI wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, akitoa tathmini yake mbele ya sehemu ya kuingilia kwenye handaki la kuchepusha maji (diversion channel) la ujenzi wa mradi wa umeme wa maji wa Julius Nyerere kwenye mto Rufiji Mkoani Pwani leo Jumapili Septemba 8, 2019 wakati alipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo ambao ukikamilika utazalisha umeme wa Megawati 2115.
   Daraja namba mbili  la kukatisha mto Rufiji eneo la ujenzi wa mradi wa umeme wa maji wa Julius Nyerere (JNHPP) likiwa limekamilika leo Jumapili Septemba 8, 2019.
   Kijiko kikitoka kwenye handaki la kuchepusha maji leo Septemba 8, 2019.
   Waziri Dkt. Kalemani akiwa na viongozi mbalimbali kwenye eneo la mradi
  Msafara wa magari ya Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani ukipita kwenye daraja namba mbili linalokatisha mto Rufiji leo Septemba 8, 2019.
  Waziri Mhe. Dkt. Kalemani (katikati) akipatiwa maelezo na Mratibu wa mradi huo Mhandisi Steven Manda wakati wa ziara 
  Ujenzi wa nguzo za daraja namba moja litakalounganisha pande mbili za mto Rufiji ukiwa unaendelea. Daraja hilo litasaidia kuvusha vifaa vya ujenzi (mashine) kutoka upande mmoja wa mto kwenda upande wa pili ili kusaidiana na daraja namba mbili ambalo tayari linafanya kazi.
  Eneo la kuingilia ADIT (njia ya kufika kwenye handaki la kuchepusha maji) (diversion tunnel).
  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Dkt. Kebwe Stephene Kebwe akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara hiyo.
  Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Mheshimiwa Juma Abdallah Njwayo akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara hiyo.
  Dkt. Kalemani akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephene Kebwe na Kamanda wa Polisi Wilaya ya Rufiji (OCD) Lepold Fungu, akipatiwa maelezo na Mmoja wa wasimamizi wa mradi huo.


  Mhe. Dkt. Kalemani akimsikilzia Meneja Mradi kutoka kampuni ya Arab Contractor ya Misri, Mhandisi Mohammad Samaha.(kushoto). 
  Daraja namba mbili likiwa limekamilika na kufanya kazi
  Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Medard Kalemani akimsikiliza Mratibu wa ujenzi wa Mradi wa bwawa la kufua umeme la Nyerere (JNHPP), ambaye pia ni Meneja Miradi wa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO), Mhandisi Steven Manda, mara baada ya kutembelea maeneo kadhaa ya utekelezaji wa mradi huo Jumapili Septemba 8, 2019.

  0 0

  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harison Mwakyembe akikabidhi cheti kwa mwanafunzi Abdulkadri Shayo, wakati wa Mahafali ya 15 ya darasa la saba ya Shule za Bethel Mission ya Ubungo Makuburi na Mahafali ya kwanza ya darasa hilo shule ya Bethel Mission Mbezi Msakuzi, yaliyofanyika kwa pamoja kwenye Shule ya Bethel Mission Ubungo Makuburi, Dar es Salaam, leo, Septemba 8, 2019. Katika Mahafali hayo Wanafunzi 33 wa Bethel School Ubungo na 19 wa Msakuzi walikabidhiwa vyeti. Wanafunzi hao wanatarajiwa kufanya mtihani wa kuhitimu darasa la saba na wenzao wa darasa hilo nchini kote Jumatano ijayo. Wapili kulia ni Meneja wa Bethel Mission School Emmanuel Mshana.Meneja wa Bethel Mission School Emmanuel Mshana (Wapili kulia) akimpatia maelezo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harison Mwakyembe (kushoto) baada ya kumpokea ofisini kwake, Waziri huyo alipowasili kuwa mgeni rasmi kwenye Mahafali ya 15 ya darasa la saba  ya Shule za Bethel Mission ya Ubungo Makuburi na Mahafali ya kwanza ya darasa hilo shule ya Bethel Mission Mbezi Msakuzi, yaliyofanyika kwa pamoja kwenye Shule ya Bethel Mission Ubungo Makuburi, Dar es Salaam, jana. Katika Mahafali hayo Wanafunzi 33 wa Bethel School Ubungo na 19 wa Msakuzi walikabidhiwa vyeti. Wanafunzi hao wanatarajiwa kufanya mtihani wa kuhitimu darasa la saba na wenzao wa darasa hilo nchini kote, Jumatano ijayo. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Shule hiyo Justine Sangu.Meneja wa Bethel Mission School Emmanuel Mshana. akimpa kitabu cha wageni Waziri Dk. Harison Mwakyembe kwa ajili ya kusaini baada ya kuwasili.Meneja wa Bethel Mission School Emmanuel Mshana (kulia) akimwongoza Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harison Mwakyembe kwenda eneo la tukio, baada ya kumpokea waziri huyo alipowasili kuwa mgeni rasmi kwenye Mahafali ya 15 ya darasa la saba ya Shule za Bethel Mission ya Ubungo Makuburi na Mahafali ya kwanza ya darasa hilo shule ya  Bethel Mission Mbezi Msakuzi, yaliyofanyika kwa pamoja kwenye Shule ya Bethel Mission Ubungo Makuburi, Dar es Salaam, jana. Wanafunzi hao wanatarajiwa kufanya mtihani wa kuhitimu darasa la saba na wenzao wa darasa hilo nchini kote, Jumatano ijayo.Meneja wa Bethel Mission School Emmanuel Mshana (kulia) akimwongoza Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harison Mwakyembe kwenda eneo la tukio, baada ya kumpokea waziri huyo alipowasili kuwa mgeni rasmi kwenye Mahafali ya 15 ya darasa la saba ya Shule za Bethel Mission ya Ubungo Makuburi na Mahafali ya kwanza ya darasa hilo shule ya  Bethel Mission Mbezi Msakuzi, yaliyofanyika kwa pamoja kwenye Shule ya Bethel Mission Ubungo Makuburi, Dar es Salaam,jana.Meneja wa Bethel Mission School Emmanuel Mshana (Kulia) akimpatia maelezo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harison Mwakyembe kabla ya kuzindua jiwe la msingi la ujenzi wa Bwalo la chakula la Wanafunzi wa Bethel International School, waziri huyo alipowasili kuwa mgeni rasmi kwenye Mahafali ya 15 ya darasa la saba ya Shule za Bethel Mission ya Ubungo Makuburi na Mahafali ya kwanza ya darasa hilo shule ya Bethel Mission Mbezi Msakuzi, yaliyofanyika kwa pamoja kwenye Shule ya Bethel Mission Ubungo Makuburi, Dar es Salaam, jana.Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harison Mwakyembe akizindua jiwe la msingi la ujenzi wa Bwalo la chakula la Wanafunzi wa Bethel International School, waziri huyo alipowasili kuwa mgeni rasmi kwenye Mahafali ya 15 ya darasa la saba ya Shule za Bethel Mission ya Ubungo Makuburi na Mahafali ya kwanza ya darasa hilo shule ya Bethel Mission Mbezi Msakuzi, yaliyofanyika kwa pamoja kwenye Shule ya Bethel Mission Ubungo Makuburi, Dar es Salaam,jana .Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harison Mwakyembe akizungumza baada ya kuzindua jiwe la msingi la ujenzi wa Bwalo la chakula la Wanafunzi wa Bethel International School, waziri huyo alipowasili kuwa mgeni rasmi kwenye Mahafali ya 15 ya darasa la saba ya Shule za Bethel Mission ya Ubungo Makuburi na Mahafali ya kwanza ya darasa hilo shule ya Bethel Mission Mbezi Msakuzi, yaliyofanyika kwa pamoja kwenye Shule ya Bethel Mission Ubungo Makuburi, Dar es Salaam, jana .Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harison Mwakyembe akitazama eneo ambalo ujenzi wa Bwalo hilo la chakula la Wanafunzi wa Bethel International School unafanyika, waziri huyo alipowasili kuwa mgeni rasmi kwenye Mahafali ya 15 ya darasa la saba ya Shule za Bethel Mission ya Ubungo Makuburi na Mahafali ya kwanza ya darasa hilo shule ya Bethel Mission Mbezi Msakuzi, yaliyofanyika kwa pamoja kwenye Shule ya Bethel Mission Ubungo Makuburi, Dar es Salaam, jana Meneja wa Bethel Mission School Emmanuel Mshana (kulia) akimwongoza Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harison Mwakyembe kwenda eneo la tukio la sherehe za mahafali, , baada ya kumpokea waziri huyo alipowasili kuwa mgeni rasmi kwenye Mahafali ya 15 ya darasa la saba ya Shule za Bethel Mission ya Ubungo Makuburi na Mahafali ya kwanza ya darasa hilo shule ya Bethel Mission Mbezi Msakuzi, yaliyofanyika kwa pamoja kwenye Shule ya Bethel Mission Ubungo Makuburi, Dar es Salaam,jana Meneja wa Bethel Mission School Emmanuel Mshana (kulia) akimwongoza Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harison Mwakyembe kwenda eneo la tukio la sherehe za mahafali, , baada ya kumpokea waziri huyo alipowasili kuwa mgeni rasmi kwenye Mahafali ya 15 ya darasa la saba ya Shule za Bethel Mission ya Ubungo Makuburi na Mahafali ya kwanza ya darasa hilo shule ya Bethel Mission Mbezi Msakuzi, yaliyofanyika kwa pamoja kwenye Shule ya Bethel Mission Ubungo Makuburi, Dar es Salaam,jana "Hawa ndiyo wahitimu wenyewe?" Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harison Mwakyembe akiuliza alipowaona wanafunzi wa darasa la saba alipowasili kwenye Mahafali ya 15 ya darasa la saba ya Shule za Bethel Mission ya Ubungo Makuburi na Mahafali ya kwanza ya darasa hilo shule ya Bethel Mission Mbezi Msakuzi, yaliyofanyika kwa pamoja kwenye Shule ya Bethel Mission Ubungo Makuburi, Dar es Salaam, jana  "Watoto hamjambo?" Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harison Mwakyembe akiwasalimia wanafunzi haoWanafunzi wa darasa la saba na chekechea wakimlaki kwa nyimbo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harison Mwakyembe alipowasili kwenye Mahafali ya 15 ya darasa la saba ya Shule za Bethel Mission ya Ubungo Makuburi na Mahafali ya kwanza ya darasa hilo shule ya Bethel Mission Mbezi Msakuzi, yaliyofanyika kwa pamoja kwenye Shule ya Bethel Mission Ubungo Makuburi, Dar es Salaam, jana Wanafunzi wa darasa la saba na Chekechea wakimlaki kwa nyimbo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harison Mwakyembe alipowasili kwenye Mahafali ya 15 ya darasa la saba ya Shule za Bethel Mission ya Ubungo Makuburi na Mahafali ya kwanza ya darasa hilo shule ya Bethel Mission Mbezi Msakuzi, yaliyofanyika kwa pamoja kwenye Shule ya Bethel Mission Ubungo Makuburi, Dar es Salaam, jana  Waziri Dk. Mwakyembe akifuatana na Ndugu Mshana wakati akiwasili eneo la shughuli ya mahafali hayo. Kulia ni Ndugu Sangu. Wazazi na wageni waalikwa wakishangilia wakati Waziri Dk. Mwakyembe akiwasili eneo la shughuli ya Mahafali. Wazazi na wageni waalikwa wakiwa wamesimama wakati Waziri Dk. Mwakyembe akiwasili eneo la shughuli ya Mahafali.Wanafunzi wa darasa la saba Shule za Bethel Mission ya Ubungo Makuburi na Bethel Mission Mbezi Msakuzi, wakiingia ukumbini tayari kwa shughuli za mahafali yao yaliyofanyika kwa pamoja kwenye Shule ya Bethel Mission Ubungo Makuburi, Dar es Salaam,jana. Waziri Dk. Mwakyembe akiwa amesimama pamoja na meza kuu kuwalaki ukumbini wanafunzi hao.
  Waziri Dk. Mwakyembe akishiriki kuimba wimbo wa Taifa mwanzoni wa shughuli za mahafali hayo.Meneja wa Bethel Mission School Emmanuel Mshana akimsikiliza kwa makini Waziri Dk. Mwakyembe wakati akielezwa jambo wakati wa mahafali hayo. Baadhi ya Wazazi wakiwa kwenye mahafali hayoWanafunzi wa darasa la saba Shule za Bethel Mission ya Ubungo Makuburi na Bethel Mission Mbezi Msakuzi, wakitoa burudani ya wimbo wakati wamahafali yao yaliyofanyika kwa pamoja kwenye Shule ya Bethel Mission Ubungo Makuburi, Dar es Salaam,janaWanafunzi wa darasa la saba Shule za Bethel Mission ya Ubungo Makuburi na Bethel Mission Mbezi Msakuzi, wakitoa burudani ya wimbo wakati wamahafali yao yaliyofanyika kwa pamoja kwenye Shule ya Bethel Mission Ubungo Makuburi, Dar es Salaam,jana Meneja wa Bethel Mission School Emmanuel Mshana akizungumzaWanafunzi wa darasa la saba Shule za Bethel Mission ya Ubungo Makuburi na Bethel Mission Mbezi Msakuzi, wakitoa burudani ya wimbo wakati wamahafali yao yaliyofanyika kwa pamoja kwenye Shule ya Bethel Mission Ubungo Makuburi, Dar es Salaam,jana  Wawakilishi wa wanafunzi wa darasa la saba wakisoma risala wakati wa mahafali hayo. Wanafunzi hao wakimkabidhi risala yao waziri Dk. Mwakyembe baada ya kuisoma.Wanafunzi wa darasa la saba Shule za Bethel Mission ya Ubungo Makuburi na Bethel Mission Mbezi Msakuzi, wakitoa burudani ya wimbo wakati wamahafali yao yaliyofanyika kwa pamoja kwenye Shule ya Bethel Mission Ubungo Makuburi, Dar es Salaam, janaWaziri Dk. Mwakyembe na viongozi wa meza kuu wakishangilia bada ya kuvutiwa na namna wahitimu wa tarajiwa wa darasa la saba Shule za Bethel  Mission ya Ubungo Makuburi na Bethel Mission Mbezi Msakuzi, walivyokuwa wakitoa burudani ya wimbo wakati wamahafali yao yaliyofanyika kwa pamoja kwenye Shule ya Bethel Mission Ubungo Makuburi, Dar es Salaam, janaMeneja wa Bethel Mission School akitoa hotuba wakati wa mahafali hayo. Kushoto ni Waziri Dk. Mwakyembe na kulia ni Mtunza hazina wa Kanisa la International Mission Society of Seventy Adventist Church Kanda ya Afrika Mchungaji Perminar Shirima.Kiongozi wa Kanisa la International Mission Society of Seventy Adventist Church Mchungaji Bright Fue akimkaribisha Dk. Mwakyembe kuzungumza.Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Mwakyembe akihyutubia kwenye mahafali hayo. Dk. Mwakyembe alionyesha kuvutiwa na wanafunzi wa darasa la saba kwa namna walivyoonyesha vipaji na weledi mkubwa katika kuzungumza kiingereza. Aliipongeza shule hiyo kwa kazi nzuri ya kueleimisha watoto huku ikijikita pia katika kuwalea vizuri kimaadili. Kutokana na kukunwa na shule hiyo aliahidi Wizara yake kutoa sh. milioni 5 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa Bwalo la wanafunzi kwenye shule ya Bethel Mission Ubungo.Waziri Dk. Mwakyembge akishauriana jambo na Kiongozi wa Kanisa la International Mission Society of Seventy Adventist Church Mchungaji Bright Fue 

  KUKABIDHI VYETI KWA WAHITIMU⇓

  Waziri Dk. Mwakyembe akionyesha zawaidi baada ya kukabidhiwa na Meneja wa Bethel Mission School Emmanuel Mshana wakati wa mahafali hayoWaziri Dk. Mwakyembe akipokea zawaidi ya shati baada ya kukabidhiwa na Meneja wa Bethel Mission School Emmanuel Mshana wakati wa mahafali hayoWaziri Dk. Mwakyembe akipokea zawaidi ya kitabu cha tiba kutoka kwa Kiongozi wa Kanisa la International Mission Society of Seventy Adventist Church Mchungaji Bright Fue Waziri Dk. Mwakenye na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wa Chekechea wa Bethel Mission School Ubungo wakati wa mahafali hayoWaziri Dk. Mwakenye na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na wahitimu watarajiwa wa Darasa la saba wa Bethel Mission School Ubungo na Mbezi Msakuzi, wakati wa mahafali hayoWaziri Dk. Mwakenye akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Bethel Mission School na baadhi ya wageni waalikwa mwishoni wa shughuli za mahafali hayo.

  0 0


  Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania(JWTZ), Mohamed Yacoub (wa tatu kushoto) akimkabidhi kikombe na zawadi ya Mshindi wa Jumla wa Mashindano ya Mchezo wa Golf ya Kombe la Mkuu wa Majeshi 'NMB CDF trophy 2019', Bw. A. Mcharo (kulia). Wa pili kushoto ni Mkuu wa Idara ya Wateja Wakubwa na Serikali wa Benki ya NMB- Filbert Mponzi ambao ni wadhamini wakuu wa mashindano hayo.
  Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania(JWTZ), Mohamed Yacoub (wa tatu kushoto) akimkabidhi kikombe na zawadi ya Mshindi wa Jumla wa Mashindano ya Mchezo wa Golf ya Kombe la Mkuu wa Majeshi 'NMB CDF trophy 2019', Bw. A. Mcharo (kulia). Wa pili kushoto ni Mkuu wa Idara ya Wateja Wakubwa na Serikali wa Benki ya NMB- Filbert Mponzi ambao ni wadhamini wakuu wa mashindano hayo.
  Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania(JWTZ), Mohamed Yacoub (kulia) akimkabidhi cheti cha shukrani Mkuu wa Idara ya Wateja Wakubwa na Serikali wa Benki ya NMB- Filbert Mponzi aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa NMB katika hafla ya ufungaji Mashindano ya Mchezo wa Golf ya Mkuu wa Majeshi 'NMB CDF trophy 2019'.
  Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania(JWTZ), Mohamed Yacoub akifunga rasmi Mashindano ya Mchezo wa Golf ya Mkuu wa Majeshi 'NMB CDF trophy 2019' kwa niaba ya Mkuu wa Majeshi jana jijini Dar es Salaam.
  Mwenyekiti wa Klabu ya Golf ya Lugalo, Brigedia Jenerali mstaafu, Michael Luwongo akimshukuru, Mkuu wa Idara ya Wateja Wakubwa na Serikali wa Benki ya NMB- Filbert Mponzi aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa NMB katika hafla hiyo. Benki ya NMB ni mdhamini mkuu wa Mashindano ya Mchezo wa Golf ya Mkuu wa Majeshi 'NMB CDF trophy 2019'.
  Mkuu wa Idara ya Wateja Wakubwa na Serikali wa Benki ya NMB- Filbert Mponzi aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa NMB katika hafla ya ufungaji Mashindano ya Mchezo wa Golf ya Mkuu wa Majeshi 'NMB CDF trophy 2019' akizungumza katika hafla hiyo.  Mkuu wa Idara ya Wateja Wakubwa na Serikali wa Benki ya NMB- Filbert Mponzi akimkabidhi mmoja wa washindi (kushoto) katika hafla ya ufungaji Mashindano ya Mchezo wa Golf ya Mkuu wa Majeshi 'NMB CDF trophy 2019'.
  Mkuu wa Idara ya Wateja Wakubwa na Serikali wa Benki ya NMB- Filbert Mponzi akimkabidhi mmoja wa washindi (kushoto) katika hafla ya ufungaji Mashindano ya Mchezo wa Golf ya Mkuu wa Majeshi 'NMB CDF trophy 2019'.  MNADHIMU Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Mohamed Yacoub amefunga rasmi Mashindano ya Mchezo wa Golf ya Mkuu wa Majeshi 'NMB CDF trophy 2019' kwa niaba ya Mkuu wa Majeshi, huku Benki ya NMB ikiahidi kuendelea kudhamini mashindano hayo.

  Akizungumza jana katika viwanja vya Club ya Golf Lugalo jijini Dar es Salaam, Mnadhimu Mkuu JWTZ, Luteni Jenerali Yacoub ameishukuru Benki ya NMB kwa kuendelea kudhamini mashindano hayo, hivyo jeshi litaendelea kushirikiana na benki hiyo.

  Aliwataka majenerali wa jeshi na wananchi wengine kuupenda na kuucheza mchezo wa golf na kuachana na mawazo ya baadhi ya watu wanaoamini kwamba mchezo huo ni wa matajiri pekee.

  Awali akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa Idara ya Wateja Wakubwa na Serikali wa Benki ya NMB- Filbert Mponzi alisema NMB ni wadau wakubwa wa Jeshi la Wananchi hivyo, itaendelea kusaidia mchezo wa golf hasa mashindano ya Club ya Mchezo wa Golf Lugalo ya jijini Dar es Salaam.

  Alisema katika udhamini wa mwaka huu Benki ya NMB imetoa udhamini wa pesa ya kununua vifaa mbalimbali pamoja na zawadi za washindi kunogesha mashindano hayo na itaendelea kufanya hivyo.

  Aidha aliongeza kuwa, NMB ni wadau wa Serikali na wabia pia kibiashara na Serikali hivyo inaamini inastahili kulihudumia Jeshi. "Mtandao tulionao ni mkubwa zaidi nchini nzima, tuna matawi zaidi 220, mashine za ATM zaidi ya 800 ambazo zingine zipo karibu na kambi za Jeshi la Wananchi na sasa tunaendelea kutanuka kupitia mtandao wa mawakala ambapo tuna zaidi ya mawakala 7000 maeneo mbalimbali ya nchini." Alisema Bw. Mponzi.

  Katika mashindano ya 'NMB CDF trophy 2019' mwaka huu yalioshirikisha makundi mbalimbali ya wachezaji nchini wakiwemo wa kulipwa takribani washindi 22 wamejinyakulia vikombe na zawadi anuai kulingana na nafasi walizoshinda.

older | 1 | .... | 1875 | 1876 | (Page 1877) | 1878 | 1879 | .... | 1903 | newer