Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46201 articles
Browse latest View live

WAFANYABIASHARA WA TANZANIA WAHAMASISHWA KUSHIRIKI KONGAMANO LA BIASHARA KATI YA TANZANIA NA UGANDA

0
0
Dkt John Pombe Magufuli Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania amemualika Mhe Yoweri Kaguta Museveni Rais wa Jamhuri ya Uganda kuzindua kongamano la kwanza la biashara kati ya Tanzania na Uganda linalotarajiwa kufanyika tarehe 6-7 Septemba, 2019 katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam. 

Hayo yamesemwa na Mhe Innocent Bashungwa, Waziri wa Viwanda na Biashara wakati akizungumza na waandishi wa habari na kuwaeleza kuwa Mhe Yoweri Kaguta Museveni Rais wa Jamhuri ya Uganda ataambatana na wafanayabiashara kutoka nchini kwake ili kukutana na wafanyabaishara wa Tanzania. 

Mhe Bashungwa ameeleza kuwa lengo la kongamano hilo ni kutangaza fursa na kuhamasisha biashara na uwekezaji zilizoko Tanzania na Uganda. Pia Serikali itapata fursa ya kuongea na wafanyabiashara hao ili kuangalia changamoto za kufanya biashara katika nchi hizo mbili. Vilevile Serikali zetu zitashirikiana kuzitatua, kuangalia fursa zilizopo, kuongeza biashara katika nchi hizo mbili na kuhamasisha uwekezaji. 

“Sisi Tanzania tumekuwa tunawauzia chakula na vifaa vya viwandani, kwakuwa tunajenga uchumi wa viwanda ni fursa kwa watanzania kushiriki kwenye kongamano hilo ambalo litakuwa na tija kubwa kwetu kama nchi. Rais wetu analeta wakuu wa nchi mbalimbali ikiwemo Uganda ili kuwaonesha fursa tulizonazo pamoja na kujenga mtandao mpana wa biashara”, amesema Mhe Bashungwa 

Mhe Bashungwa ameeleza kuwa kutakuwa na Maonesho ya bidhaa za Tanzania ambapo Watanzania watapata fursa ya kuonesha bidhaa za kilimo na za viwandani, taasisi za umma na sekta binafsi zinazosaidia katika mnyororo wa thamani za biashara. Ujio wa Rais wa Jamhuri ya Uganda pamoja na wafanyabiashara toka nchini humo itakuwa ni fursa ya kuunganisha wafanyabiashara wetu na wafanyabiashara wa Uganda kukuza wigo wa biashara, kupata masoko mapya pamoja na kutatua changamoto na kujenga mazingira mazuri zaidi ya kufanya biashara. Amewahamasisha wazalishaji wa bidhaa za kilimo, wafanyabaishara na wamiliki wa viwanda kutoka Mikoa yote ya nchini kujitokeza kushiriki. 

“Wafanyabaishara waelewe kuwa ni mwanzo mzuri wa kupenya katika soko la Sudani ya Kusini kwasababu wapo wafanyabiashara wa Uganda wanafanya biashara nchini Sudani ya Kusini” amesema Mhe Bashungwa. 

Ameendelea kusema kuwa mwelekeo wa Serikali ya Tanzania ni kujenga uchumi wa viwanda hivyo ni fursa kwa Watanzania kutumia kongamano hili kwasababu Serikali inazidi kuweka mazingira wezeshi ya kufanya biashara nchini, kujenga viwanda na kufuatilia masoko mbalimbali lengo ni kutaka uuzaji wa bidhaa nchini Uganda uongezeke. 

Imetolewa na: 
Theresa Chilambo 

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano-TanTrade

Rais Dkt. Magufuli azungumza na Watendaji Kata Ikulu Jijini Dar es Salaam

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Watendaji wa Kata zote za mikoa ya Tanzania Bara Ikulu jijini Dar es Salaam.
Watendaji wa Kata zote za mikoa ya Tanzania Bara wakiimba Wimbo wa Taifa kabla ya kuanza kwa Mkutano wao na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.
Watendaji wa Kata zote za mikoa ya Tanzania Bara wakifurahia jambo wakati walipokuwa wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Watendaji Kata wakiwa katika mkutano wao na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.

PICHA NA IKULU

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA MAAFISA WATENDAJI WA KATA WA NCHI NZIMA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli,Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora) Mhe. George Mkuchika, Rais wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Suleiman Jaffo, Katibu Mkuu Ikulu Dkt. Moses Kusiluka, Katibu Mkuu Utumishi Dkt. Laurian Ndumbaro,Katibu Mkuu TAMISEMI Mhandisi Nyamhanga na Naibu Katibu Mkuu Utumishi Dkt. Francis Michael katika picha ya pamoja na Maafisa Watendaji wa Kata baada ya kukutana na kuzungumza nao Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 2, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata chakula cha mchana na Maafisa Watendaji wa Kata wa nchi nzima baada ya kukutana na kuzungumza nao Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 2, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Maafisa Watendaji wa Kata wa nchi nzima wakati wa chakula cha mchana baada ya kukutana na kuzungumza nao Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 2, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Maafisa Watendaji wa Kata wa nchi nzima alipokutana nao Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 2, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Maafisa Watendaji wa Kata wa nchi nzima baada ya kukutana na kuzungumza nao Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 2, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora) Mhe. George
Mkuchika, Rais wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Suleiman Jaffo,Katibu Mkuu Ikulu Dkt. Moses Kusiluka, Katibu Mkuu Utumishi Dkt.Laurian Ndumbaro, Katibu Mkuu TAMISEMI Mhandisi Nyamhanga na Naibu Katibu Mkuu Utumishi Dkt. Francis Michael katika picha ya pamoja na Maafisa Watendaji wa Kata wa Mkoa wa Lindi baada ya mkutano wao Ikulu ijini Dar es salaam leo Septemba 2, 2019

PICHA NA IKULU

DC ARUSHA AZINDUA AWAMU YA NNE YA MAFUNZO KUHUSU MATUMIZI YA MFUMO WA MANUNUZI YA UMMA KWA NJIA YA MTANDAO (TANePS)

0
0
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mh. Gabriel Daqqaro, amefungua awamu ya nne ya mafunzo kuhusu matumizi ya Mfumo wa Manunuzi ya Umma kwa Njia ya Mtandao (TANePS) kwa wataalam wa manunuzi na Tehama kutoka taasisi nunuzi. 

Akizungumza na washiriki wa mafunzo hayo wapatao 172 kutoka taasisi nunuzi 65, Mh. Daqqaro alipongeza jitihada za Serikali kwa kuanzisha mfumo huo mpya wa TANePS unaosimamiwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma - PPRA kwa kuwa utasaidia kupunguza malalamiko na kero zilizokuwa zinaelekezwa kwenye sekta ya manunuzi ya umma ikiwemo kukabiliana na vitendo vya rushwa,  kupunguza gharama na muda wa michakato ya manunuzi.

Mkuu huyo wa Wilaya aliongeza kuwa Mfumo huo utaisaidia Serikali kuokoa fedha nyingi ambazo zinaelekezwa kwenye sekta hiyo ya manunuzi, na kutoa wito kwa wadau wote wa manunuzi ya umma kutoa ushirikiano wa dhati ili mfumo huo ufanye kazi. 

 Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA, Mhandisi Leonard Kapongo akifafanua jambo kwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Mh. Gabriel Daqqaro, kabla ya Ufunguzi wa awamu ya nne ya mafunzo ya TANePS, jijini Arusha
Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Mh. Gabriel Daqqaro, akizungumza wakati wa ufunguzi wa awamu ya nne ya mafunzo kuhusu Mfumo wa TANePS jijini Arusha.
 Baadhi ya washiriki wakiwa kwenye mafunzo kwa vitendo kuhusu matumizi ya mfumo wa TANePS

Dkt. Kalemani: Mwanakijiji kuweka umeme ni lazima si hiari

0
0
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani,( katikati) akikata utepe kushiria
kuwasha umeme katika moja ya shule za msingi katika Kijiji cha Saja,
wilayani ya Wanging’ombe mkoani Njombe.

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani,( kulia) akiwa ameshika mkuki
huku amevaa mavazi maalum baada ya kusimikwa kuwa Chifu wa Kijiji
cha Ihalula, kutoka kwa mmoja wa wazee wa kimila( aliyesimama kulia),
baada kuwasha umeme katika kijiji hicho kilichopo Halmashauri ya Wilaya
ya Njombe mkoani Njombe.


Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani,( wa pili kulia) akitoa maelekezo
baada ya kutembelea chumba kujifungulia akina mama wajawazito katika
Kituo cha Afya cha Ihalula, katika halmashauri ya wilaya ya Njombe,
mkoani njombe,baada ya kuwasha umeme katika zahanati hiyo.


Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani,( kushoto) akigana na Mbunge
wa Wanging’ombe, Gerson LWENGE( kulia) baada ya kuwasha umeme
katika Kijiji cha Itombololo, wilayani Wanging’ombe mkoani Njombe.
***************

Na Zuena Msuya, Njombe

Waziri wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani, amesema zoezi la mwakijiji
yeyote kuunganishiwa umeme ni lazima siyo hiari kwa kuwa kila mtanzania
hasa walio vijijini wanamudu gharama ya kuunganishiwa umeme kutokana
na kiwango cha gharama kilichopangwa na serikali.

Dkt.Kalemani alisema serikali imetumia fedha nyingi kugharamia
utekelezaji wa Mradi wa Usambazaji wa Umeme vijijini(REA) ili uweze
kuwafikia wananchi wote walioko vijijini ambao wanatakiwa kuchangia kiasi
kidogo cha fedha ili kuunganishwa na huduma hiyo.

Dkt.Kalemani alisema hayo wakati akiwasha umeme katika vijijini vinne
ambavyo ni Ihalula, Itombololo, Itowo na Saja vilivyopo katika Halmashauri
ya Wilaya Njombe na Wanging’ombe mkoani Njombe, Septemba 2,2019.

Kwa mujibu wa Dkt.Kalemani, Serikali iliangalia hali ya uchumi kwa
wananchi wake wote hasa wanaoishi Vijijini na kujiridhisha kuwa kila
mlengwa anauwezo kwa kuchangia shilingi 27,000/= ikiwa ni gharama
nafuu ya kuunganishiwa umeme kwa kuwa gharama zingine za kutekeleza
mradi huo zinalipwa na serikali.

Alifafanua kuwa zoezi kuunganisha umeme kwa kila nyumba ya mwanakijiji
anaeishi kijijini ni lazima kwa sababu Mradi wa Usambaji Umeme Vijijini(
REA) unaunganisha nyumba za aina zote na maeneo yote ya vijijini bila
kujali itikadi za Kisiasa, Imani za Dini, wala Kabila.

Aliendelea kusisitiza kuwa, hapo baadaye serikali itafanya zoezi la kukagua
nyumba moja baada ya nyingine zilizopo vijijini kufuatilia zoezi la
uunganishwaji wa umeme kwa wanavijiji, na endapo watabaini kuwa
mwakijiji ameshindwa kuunganisha huduma hiyo bila sababu ya msingi,
basi itamlazimu kuuza mifugo au mazao ili kupata shilingi 27,000/= ikiwa ni
gharama ya kunganisha umeme kwa lazima.

“Zoezi la kuweka umeme katika kila nyumba vijijini ni lazima siyo hiari
kama mnavyodhani, serikali imetumia fedha nyingi kutekeleza mradi wa (
REA),pia ni nia ya kuwasogezea huduma bora na za msingi kwa
maendeleo ya wananchi wake, ambao na wao watachangia gharama
ndogo: Sasa usipoweka umeme tutakuja kuuza chochote unachozalisha
nyumbani kwako tukulipie huduma hii”. Alisema Dkt.Kalemani.

MAKAMU WA RAIS SAMIA AMUWAKILISHA RAIS MAGUFULI KUAGA MWILI WA KADUMA

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo Sept 03,2019 amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe magufuli kwenye Shuhuli ya kuaga Mwili wa Mwanasiasa Mkongwe Nchini Marehemu Ibrahim kaduma.

Katika salam zake za pole kwa Wanafamilia, wafiwa na Watanzania wote kwa Ujumla, Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan amewaomba kuwa na Subira na Uvumilivu katika kipindi hiki cha Maombolezo na kumuomba Mwenyezi Mungu kuwapa nguvu na Moyo wa Subira.

Wakati wa Uhai wake Marehemu Ibrahim Kaduma aliwahi kuwa Mwanasiasa pamoja na kupitia ngazi mbali mbali za Uongozi hapa nchini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa Heshima za Mwisho mbele ya Jeneza lenye Mwili wa Mwanasiasa Mkongwe Nchini Marehemu Ibrahim Kaduma katika Kanisa la KKKT Makongo Juu leo Sept 03,2019 ambapo Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwenye Msiba huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisani kitabu cha kumbukumbu ya maombolezo kufuatia kifo cha Mwanasiasa Mkongwe nchini Marehemu Ibrahim Kaduma alipowasili katika Kanisa la KKKT Makongo Juu kwa ajili ya kumuwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwenye Shuhuli ya kuaga Mwili wa Mwanasiasa huyo leo Sept 03,2019. Kushoto ni Dkt. Alex Malasusa Askofu wa KKKT Dayosis ya Mashariki na Pwani.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimfariji, Mjane wa Marehemu Marehemu IBrahim Kaduma katika Kanisa la KKKT Makongo Juu, jijini Dar es salaam leo Sept 03,2019.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Dkt. Alex Malasusa Askofu wa KKKT Dayosis ya Mashariki na Pwani alipowasili katika Kanisa la KKKT Makongo Juu kwa ajili ya kumuwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwenye Shuhuli ya kuaga Mwili wa Mwanasiasa Mkongwe Marehemu IBrahim Kaduma leo Sept 03,2019.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na kuwapa pole Baadhi ya Wajukuu na Vitukuu vya Mwanasiasa Mkongwe Nchini Marehemu IBrahim Kaduma wakati wa shuhuli ya kuaga Mwili wa Mwanasiasa huyo leo Sept 03,2019 katika kanisa la KKKT Makongo Juu, Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwenye Msiba huo.

RC MAKONDA ATIMIZA NDOTO ZA WAJANE,AKABIDHI MUSWADA WA SHERIA YA MIRATHI KWA WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA.

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo September 03 ametimiza ndoto za Wajane kwa kukabidhi Muswada wa Mapendekezo ya Mabadiliko ya Sheria ya Mirathi kwa Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Dkt. Augustine Mahiga kwaajili ya Kufanyiwa maboresho na kufikishwa Bungeni.

Akikabidhi Muswada huo mapema leo Mjini Dodoma RC Makonda amesema ndani ya Muswada huo ameainisha mapendekezo ya kubadilishwa kwa Sheria kandamizi ambazo zimekuwa mwiba na Mateso kwa Wajane kwa muda wa miaka mingi.

Aidha RC Makonda amesema Miongoni mwa Sheria kandamizi anazopendekeza zifanyiwe mabadiliko ni Sheria ya Kiserikali ya Mirathi ya Mwaka 1865, Sheria ya Mirathi ya Kimila ya Mwaka 1963 na Sheria ya Mirathi ya Kidini ya Mwaka 1963 kwakuwa zimepitwa na Wakati na zimekuwa na Mapungufu mengi ya Kisheria.

RC Makonda amevitaja baadhi ya vipengele anavyopendekeza vifanyiwe maboresho ni pamoja na kipengele cha kumpa uhalali Mke wa marehemu kushiriki katika vikao vya mgawanyo wa mali, mjane kupewa haki ya kurithi na kusimamia mali za marehemu, Mjane kutoondolewa kwenye nyumba wala Mali kuhamishwa, Usawa wa watoto katika kumiliki mali za marehemu bila kujali jinsia pamoja haki ya mtoto wa nje ya Ndoa kurithi Mali.

Vifungu vingine ambavyo RC Makonda ameeleza kuwa ni kandambizi kwa Mjane ni pamoja na kipengele kinachoruhusu Mjane kurithiwa na kile kinachomnyima Mwanamke haki ya kurithi ardhi ya ukoo.

Pamoja na hayo RC Makonda amesema chimbuko la muswada huo ni mapendekezo yaliyotokana na Kongamano la Wajane zaidi ya 5,181 alilohitisha mwezi April Ukumbi wa Mlimani City ambapo katika kongamano hilo alipokea Kero na Malalamiko yaliyomlazimu kuunda kamati iliyoshirikisha Wadau na Wataalamu mbalimbali kutoka Serikalini na Asasi za Kiraia.

Kwa upande wake Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Dkt. Augustine Mahiga amesema kuwa alichokifanya RC Makonda kupigania haki za wajane ni Ushujaa wa hali ya Juu na ameweka historia ya Jambo ambalo halijawahi kufanyika ambapo amemuahidi kufanyia maboresho ya haraka na kuwasilisha Bungeni.

Tigo yazindua huduma ya kwanza na ya kipekee ya Home Internet

0
0

Mkuu wa Bidhaa na Huduma kutoka Tigo, David Umoh akimkabidhi Home Internet Router Mtangazaji wa Clouds Tv, Abdallah Kamelo, katika uzinduzi wa huduma ya kwanza na ya kipekee ya Home Internet kutoka Tigo, Katikati ni Afisa Mkuu wa Biashara, Tarik Boudiaf


Wateja wa Kampuni ya mawasiliano,Tigo, kwa mara ya kwanza watapata fursa ya kufurahia huduma Home Internet yenye kasi ya 4G+ majumbani mwao. Huduma hii ni ya kwanza na ya kipekee Tanzania, yenye ubunifu wa hali ya juu itakayowafanya wateja wafurahie intaneti ya 4G+ kwa kutumia vifaa vya Router au Modem.

Kampuni ya simu ya Tigo imezindua rasmi huduma hiyo ambayo itatatua changamoto ambazo watumiaji wa mitandao ya simu hususan wale wa majumbani wamekuwa wakikabiliana nazo.

Kupitia huduma hiyo, wateja wa kampuni ya Tigo sasa watapata fursa ya kupanga na kuchagua ni jinsi gani watatumia huduma ya intaneti, ikiwemo kununua vifurushi, kuongeza na kuangalia salio kupitia simu zao za mkononi.

“Mrejesho kutoka kwa wateja wetu umeonyesha kwamba kuna umuhimu wa uwepo wa huduma rahisi na ya uhakika ya mtandao wa intaneti majumbani. Hata hivyo, uzoefu katika matumizi ya huduma ya mtandao wa intaneti majumbani kwa wateja ni jambo lenye umuhimu mkubwa sana kwetu,” ameeleza Mkuu wa kitengo cha Biashara cha Kampuni ya Tigo, Tarik Boudiaf.

“Zama zile za mteja kusumbuka kutumia simu yake ya mkononi kama modem au kuhamisha line inayotumika kwenye modem au router ili kupata huduma ya intanet zimekwisha pita kitambo. Zama za kununua kifurushi ama kuongeza au kuangalia salio la laini inayotumika kwenye modem au router kwa kutumia kifaa kingine, ni jambo ambalo humpa mteja usumbufu, nazo zimekwisha pita kitambo,” ameongeza Boudiaf.

Kupitia huduma hii iliyozinduliwa na Tigo, wateja sasa wanaweza kupangilia matumizi yao ya huduma ya intaneti kwa kuunganisha vifaa vya modem na router kutumia Tigo Pesa App.

“Lengo letu ni kuhakikisha kuwa kila mteja wa Tigo nchini ambaye atahitaji kutumia huduma yetu ya Home Internet anaunganishwa muda wote bila vikwazo vyovyote,” ameongeza Boudiaf.
Kwa mujibu wa Boudiaf, huduma hii mpya iliyozinduliwa kwa mara ya kwanza nchini ni sehemu tu ya jitihada za kampuni ya Tigo ya kutoa huduma zinazojali maslahi ya wateja katika kuwapa uzoefu endelevu wa kijiditali kupitia mtandao wenye kasi zaidi wa 4G+.

Uzinduzi wa huduma hii mpya umeshuhudiwa pia na Meneja huduma za intaneti wa kampuni ya Tigo, Mkumbo Myonga, ambaye amewahakikishia wateja kupata huduma bora na rahisi wanapojuanga na huduma ya Home Internet.

Ili kujiunga na kufurahia huduma hiyo ya Home Internet, wateja wa Tigo wanaweza kununua modem au router katika maduka ya Tigo yaliyopo nchi nzima. Wateja wa Home internet wanaweza kuwasiliana na kitengo cha huduma kwa wateja wakati wowote, yani masaa 24 kwa siku.

Ili kufurahia huduma hiyo, wateja wa kampuni ya mawasiliano Tigo wanaweza kununua kwa urahisi vifurushi vya Home Internet kwa kutumia Tigo Pesa App, au kwa kutembelea tovuti ya; internet.tigo.co.tzau pia kwa kupiga *147*00# ili kujiunga mwenyewe au kununulia ndugu, jamaa na marafiki kifurushi cha Home Internet.

Wateja wa Tigo watapata huduma hiyo ya Home Internet kulingana na thamani ya fedha zao kwa kununua kifurushi cha wiki au mwezi, kwa kuanzia Tsh15,000 kwa GB12 kwa siku 7 hadi Tshs120,000 kwa GB200 kwa mwezi mmoja.

Vifaa hivyo vitapatikana kwa urahisi kwa bei ya rejareja ya Sh150,000 kwa Modem na Sh250,000 kwa Routers, ambapo mteja wa Tigo akinunua atapata na kifurushi cha bure cha intaneti cha mwezi mmoja cha GB40 na GB100.
Meneja Huduma za Intaneti Mkumbo Myonga akiwaelezea waandishi wa habari,jinsi gani Mteja anaweza kuangalia salio, kununua kifurushi kwa kupitia Tigo Pesa App katika uzinduzi wa huduma ya kipekee ya Home Internet, Kushoto kwake ni Afisa Mkuu wa Biashara, Tarik Boudiaf.

TCRA YAVITAKA VYOMBO VIWILI VYA HABARI KUOMBA RADHI SIKU 7 MFULULIZO KWA MAKOSA YA MAUDHUI MTANDAO

0
0
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imevitaka vyombo vya habari viwili viombe radhi kwa siku saba mfululizo kutokana na makosa mbalimbali ya ukiukwaji wa Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (Maudhui Mtandaoni) ikiwemo kuonesha na kuchapisha picha mbalimbali za ajali ya gari la mafuta, iliyotokea Msamvu, Morogoro.

Kamati ya Maudhui ilitoa onyo hilo kwa Lemutuz Online Tv na Global Tv ambapo wametakiwa kuomba radhi kuanzia Septemba 4 mwaka huu.

Akisoma uamuzi huo, mwenyekiti wa kamati hiyo, Valeria Msoka alisema katika ajali iliyotokea Agosti 10 mwaka huu baadhi ya vyombo vya habari hususan Online TV zaidi ya 15 zilichapisha na kuonesha picha za miili ya watu wakiofariki katika ajali hiyo kinyume cha sheria, kanuni na maadili ya uandishi na utangazaji wa habari.

Alisema baadhi ya vyombo hivyo viligundua makosa yao na kuziondoa picha hizo na kwamba Lemutuz Online Tv na Global Tv walishindwa kujirekebisha na Agosti 28 mwaka huu walifika mbele ya kamati hiyo na kujieleza.

"Katika utetezi wao Lemutuz Online Tv ilieleza kuwa kosa hilo lilisababishwa na uzembe wa msimamizi wao wa maudhui ambaye hakutumia busara na kuzingatia weredi katika uchapishaji video ile,Global Tv ilisema ilichukua tahadhari kubwa ya kuziziba picha za miili ya watu waliokuwa wameungua katika ajali ile kwa kuweka vivuli lakini ilitokea tatizo la kiufundi na kuonesha picha hizo chini ya kivuli,"amesema Msoka

Ameongeza kuwa vyombo vyote hivyo vya habari vilikiri makosa yao na kuomba radhi na kuahidi kutorudia tena na baada ya kusikiliza kwa kina maelezo ya utetezi wao, kamati imeona imekiuka kanuni za mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (maudhui mtandaoni) ya mwaka 2018.

Msoka amesema, kutokana na hilo kamati ya maudhui imeamua kutoa onyo kali na kuamuru chaneli hizo mbili kuomba radhi kwa watazamaji kupitia chaneli zao kwa siku saba mfululizo kuanzia Septemba 4 mwaka huu.

Amesema imeshauri chaneli zote mbili kuimarisha usimamzi makini wa chaneli zao ili kuhakikisha maudhui yao ni salama kisheria na kimaadili kabla ya ya kuwekwa mtandaoni.

Katika hatua nyingine, kamati hiyo imetoa onyo kali kwa Televisheni ya East Africa (EATV) kwa kurusha maudhui yasiyo na maadili Julai 2 mwaka huu kupitia kipindi chake cha 'Dadaz' kipengele cha Mtukati.

Pia ilitoa onyo kali kwa kituo cha TBC FM Radio , kwa kukiuka agizo la serikali la kutosoma habari za magazeti kwa undani.

Alisema radio hiyo ilitenda kosa hilo kupitia kipindi chake cha 'Busati' kipengele cha magazeti ambapo mtangazaji wa kipindi alisoma kwa undani habari mbalimbali zilizoandikwa katika magazeti ya uhuru na Habari Leo.

Alisema vyombo vyote vya habari viligundua nakukiri makosa yao na kuomba radhi ambapo kamati imevishauri kuimarisha na kuboresha usimamizi, utayarishaji na utangazaji wa vipindi vyao.

WAZIRI HASUNGA; TUTAFANYA MABADILIKO MAKUBWA KWENYE SEKTA YA KILIMO

0
0


Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Katikati) akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Israel Mhe Job Daud Masima (Kulia) katika Ofisi za Ubalozi huo zilizopo katika mtaa wa 12, Abba Hillel Silver Jijini Tel Aviv nchini Israel. Mwingine ni Mwambata Jeshi Brigedia Jenerali Kahema Juni Mziray, Leo Tarehe 3 Septemba 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Kulia) akizungumza na Mkuu wa Mradi wa Umwagiji Afrika kampuni ya Netafim Ndg Shay Haxter mara baada ya kutembelea katika shamba la utafiti wa kilimo wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku sita nchini Israel. Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Israel Mhe Job Daud Masima Leo Tarehe 3 Septemba 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa Tanzania walioshiriki mafunzo ya Kilimo nchini Israel kwenye shamba la mifugo la Jacob's Farm, Mwingine pichani ni Balozi wa Tanzania nchini Israel Mhe Job Daud Masima (Kulia), Leo Tarehe 3 Septemba 2019.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Israel zilizopo katika mtaa wa 12, Abba Hillel Silver Jijini Telaviv nchini Israel, Leo Tarehe 3 Septemba 2019.



Na Mathias Canal, Telaviv-Israel

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) amesema kuwa serikali YA Tanzania imejipanga kuikabili sekta ya kilimo ikiwa ni pamoja na kuona umuhimu wa kuwaandaa watanzania katika kubadilisha kilimo chao kutoka kwenye kilimo cha kujikimu na kuwa kilimo cha kibiashara.

Waziri Hasunga ameyasema hayo leo tarehe 3 Septemba 2019 wakati akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Israel Mhe Job Daud Masima katika Ofisi za Ubalozi huo zilizopo katika mtaa wa 12, Abba Hillel Silver Jijini Tel Aviv nchini Israel.

Alisema kuwa katika ziara yake hiyo amejifunza namna ambavyo nchi ya Israel imepiga hatua ya ujuzi katika sekta ya kilimo hivyo kuona umuhimu wa serikali ya Tanzania kuwekeza katika skimu za umwagiliaji.

Alisema kuwa asilimia kubwa ya wakulima nchini Tanzania wanatumia majembe ya mkono katika kilimo jambo ambalo haliwezi kuongeza tija na uzalishaji. “Tunatumia majembe ya mkono mbaya zaidi kilimo chetu kinategemea msimu wa mvua, hivyo kilimo cha namna hiyo bado kinatuchelewesha, tuna wajibu wa kujifunza kwa wenzetu walioendelea” Alisema Mhe Hasunga

Alisema kwa kuanza serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na wadau wa kilimo inaweza kujenga mabwawa kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji ili kuongeza uwezo wa kilimo cha umwagiliaji kitakachofanya kazi msimu mzima badala ya kilimo cha kutegemea mvua.

Mhe Hasunga alisema kuwa Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kadhalika wizara ya Viwanda na Biashara zitafanya kazi kwa pamoja ili kuona namna ya kuzalisha kwa tija mazao ya kilimo na kutoa malighafi nyingi zitakazochangia katika kuinua na kuchagiza matakwa ya serikali ya kuwa na serikali ya viwanda.

Kuhusu masoko ya mazao yanayozalishwa nchini Tanzania Mhe Hasunga alisema kuwa serikali inaendelea na mkakati maalumu wa kuimarisha masoko kwani imeanzisha kitengo maalumu katika wizara ya kilimo kitakachokuwa na wajibu wa kushughulikia masoko ya mazao ya wakulima.

Katika hatua nyingine Waziri Hasunga ameyaalika makampuni mbalimbali ya Israel yanayojishughulisha na kilimo kutembelea nchini Tanzania kwa ajili ya kujionea fursa za uwekezaji zilizopo nchini Tanzania.

“Tanzania ni nchi yenye rutuba nzuri, eneo kubwa kwa ajili ya uwekezaji wa kilimo, hivyo nayaalika makampuni yote yanayohusika na kilimo hususani yanayojishughulisha na utafiti, kutembelea Tanzania kwani ni nchi yenye eneo zuri na kubwa kwa ajili ya uwekezaji hususani katika sekta ya kiliumo” Alikaririwa Mhe Hasunga

Mhe Hasunga amesema kuwa Israel ni nchi yenye eneo dogo kwa ajili ya kilimo lakini wanazalisha chakula kinachotosheleza wananchi wake sambamba na kuuza mazao yao nje ya nchi jambo ambalo linaimarisha pato la serikali ya nchi hiyo na kipato cha mtu mmoja mmoja.

Vilevile, waziri Hasunga ameupongeza Ubalozi wa Tanzania nchini Israel unaoongozwa na Mhe Balozi wa Tanzania nchini Israel Mhe Job Daud Masima na watendaji wengine wote kwa kazi nzuri wanayoifanya ya uwakilishi wa Tanzania, Aidha Mhe Hasunga amemuomba Balozi huyo kutafuta fursa zaidi za makampuni ya kilimo na viwanda kwa ajili ya kuwekeza nchini Tanzania.

Kwa upande wake Balozi wa Tanzania nchini Israel Mhe Job Daud Masima amesema kuwa miongoni mwa mambo muhimu ya kuyafanyia kazi ni pamoja na kutafuta namna ya kuongeza idadi ya vijana wanaoshiriki katika mafunzo ya kilimo ya Agro Studies ili izidi kuongezeka maradufu.

Kadhalika, alisema kuwa ofisi yake inaendelea kufanya kazi kubwa kuongeza idadi ya watalii wanaotembelea nchini Tanzania kwani idadi kubwa ya watalii inaongeza pato la kigeni la nchi.

Balozi Masima alisema kuwa nchi ya Israel ina mafanikio makubwa kwenye sekta ya teknolojia hivyo ni wajibu wa Tanzania kutumia fursa hiyo muhimu katika elimu ya ujuzi wa teknolojia za kilimo hususani umwagiliaji.

RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA MKUTANO WA MASHAURIANO WA MWAKA WA AQRB, ERB, CRB PAMOJA NA WADAU MBALIMBALI WA SEKTA YA UJENZI NCHINI, JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wadau mbalimbali kutoka Bodi ya Usajili Wabunifu na Wakadiriaji Majenzi (AQRB), Bodi ya Usajili Wakandarasi (CRB) Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB) pamoja na wadau wa  Sekta ya Ujenzi kabla ya kufungua mkutano huo wa Mwaka wa Mashauriano katika Bodi na Taasisi hiyo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua vifaa mbalimbali vya Mabomba ya Maji katika viwanja vya Diamond Jubilee mara baada ya kufungua mkutano wa Mashauriano wa Mwaka wa AQRB,CRB,ERB pamoja na Wadau wa Sekta ya Ujenzi nchini.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua moja wapo ya gari linalotumika katika ujenzi wa Miondombimbu mbalimbali katika viwanja vya Diamond Jubilee mara baada ya kufungua mkutano wa Mashauriano wa Mwaka wa AQRB,CRB,ERB pamoja na Wadau wa Sekta ya Ujenzi nchini.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia vitasa mbalimbali vya Milango wakati alipopita kukagua mabanda katika maonesho ya Wadau wa Sekta ya Ujenzi.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Charles Kitwanga Mbunge wa Misungwi mara baada ya kukagua mabanda  katika maonesho ya Wadau wa Sekta ya Ujenzi yaliyopo katika viwanja vya Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mchungaji Daniel Mgogo mara baada ya kufungua mkutano huo wa Mashauriano uliofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi wakati Mchungaji Daniel Mgogo alipokuwa akizungumza katika mkutano huo. PICHA NA IKULU

Huu Ndio Muonekano Wa Jengo Jipya la Mfuko wa Mwalimu Julius Nyerere

0
0
Muonekano wa jengo jipya la Mfuko wa Mwalimu Julius Nyerere linalojukana kama ‘Mwalimu Nyerere Foundation Square’ lililopo Barabara ya Sokoine/Morogoro jijini Dar es Salaam baada ya kukamilika kwa ujenzi. Jengo hilo lenye ghorofa 30 limejengwa na kampuni ya Kichina ya CRJE (East Africa) linatarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni.

Benki ya BancABC yatoa msaada wa mazishi wa mteja wake wa Mkopo Rahisi Dar es Salaam.

0
0
Benki ya BancABC ambayo ni kampuni tanzu ya Atlas Mara Tanzania imetoa msaada wa mazishi kwa Mke wa mmoja wa wateja wake wa Mkopo Rahisi wa jijini Dar es Salaam ambaye hivi karibuni alifiwa na mume wake. Mkopo Rahisi ni moja ya huduma ambayo hutolewa na BancABC kwa ajili ya kufariji familia ya mteja wake inapotokea kifo kwa kufuta mkopo uliokuwa umebaki pamoja na kutoa msaada wa Tzs500,000/- kwa familia. 

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati wa kukabidhi hundi ya fedha hizo kwa Maria Privatus ambaye mume wake alikuwa ni mteja wa BancABC Mkopo Rahisi kabla ya kufariki, Meneja wa BancABC Kanda ya Dar es Salaam Ferdinand Mgeni alisema kuwa benki hiyo imekuwa ikitoa msaada kwa familia ambayo mteja alikuwa na Mkopo Rahisi kutoka BancABC. ‘Kile ambacho mnaona tukifanya hapa leo ni jambo ambalo tulikuwa tukifanya siku zote. Sisi BancABC ambao ni kampuni tanzu ya Atlas Mara Tanzania tuliamua kuwa na kipengele cha aina hii kwenye mikopo yetu ya Mkopo Rahisi ili tuwe tofauti na wengine kwenye soko. Lakini zaidi ni kufanya familia ya wafiwa kuwa na amani kwani mbali na kutoa rambi rambi ra Tzs500,000/- lakini pia tunafuta deni la mkopo ambao marehemu alikuwa anadaiwa, Mgeni aliongeza. 

Mgeni aliongeza kuwa mkopo wa Mkopo Rahisi unao faida nyingi kwa mteja kwani una riba ya chini kwa mwezi. Nia yetu ni kupunguza mzigo kwa wateja wakati wa kulipa mikopo yao. Vile vile Mkopo Rahisi unatoa muda mrefu wa kulipa kwani muda wake ni miezi 72 (miaka 6) na wateja anaweza kupata mkopo hadi TZS40 milioni. 

Naomba nichukue fursa hii kuwaomba Watanzania kutembelea tawi lolote la BancABC na kupata mkopo wa Mkopo Rahisi ambao ni rahisi na haraka kupata. Wateja wetu wanao uhuru wa kutumia mkopo kwa uhuru wao iwe ni kulipa ada ya shule, kodi ya nyumba na mengineo lakini pia muda wowote mteja anaweza akiongezea kuchukua mkopo wake. 

Akizungumza baada ya kupokea rambi rambi hiyo ya Tzs500,000/-, Maria Privatus ambaye mume alifariki akiwa ni mwalimu wa shule ya wasichana ya Zanaki ya jijini Dar es Salaam alisema, ‘Nawashukuru sana BancaABC kwa kutoa muda wenu na kuja kunitembelea pamoja na kunipa rambi rambi hii. Nimekuwa nikifanya biashara ya kuuza chakula hapa shuleni ambapo mume wangu alikuwa ni mwalimu. Nitatumia pesa hii kwa ajili ya kukuza biashara yangu na hatimaye niweze kuendesha familia kwani kwa sasa nimebaki bila ya kuwa na mtu wa kunisaidia. 

Maria aliongeza, kwa sasa mimi nishahidi mzuri wa BancABC. Wakati kutangaza kwamba mteja wenu wa Mkopo Rahisi anapofariki, benki mara moja ufuta deni la mkopo wake pamoja na kusaidia familia ya marehemu kwa kiasi cha Tzs500,000/- sikuamini mpaka haya ya kwangu yalipotokea. Nitaendelea kuwa mteja wenu na nawaomba Watanzania wajiunge na BancABC kwani ni benki yenye bidhaa na huduma za uhakika kwa hapa nchini.

Meneja wa benki ya BancABC Tanzania Kanda ya Dar es Salaam Ferdinand Mgeni akikabidhi hundi ya Tzs500,000/- kwa Maria Privatus ambaye ni mkazi wa jijini Dar es Salaam baada ya kufiwa na mume wake. BancABC Tanzania kupitia Mkopo Rahisi ufuta deni la mkopo pamoja na kutoa pole kwa familia ya mteja wake pale anapofariki akiwa na na Mkopo Rahisi kutoka benki hiyo. Anayeangalia ni Ofisa Mikopo wa benki hiyo Ally Bendera.

Mnufaika wa Mkopo Rahisi Maria Privatus akionyesha hundi baada kukabidhiwa na BancABC leo jijini Dar es Salaam. Mkopo Rahisi ni mkopo ambao utolewa na BancABC ambapo mteja anapofariki benki hiyo ufuta deni la mkopo pamoja na kutoa rambi rambi ya Tzs500,000/- kwa familia ya marehemu.


Meneja wa benki BancABC Tanzania Kanda ya Dar es Salaam Ferdinand Mgeni (aliyesimama) akiongea wakati wa kukabidhi rambi rambi ya Tzs500,000/- kwa mke wa mmoja ya mteja wa Mkopo Rahisi ambaye alifariki kwenye tukio lilofanyika jana (leo) jijini Dar es Salaam. Mkopo Rahisi ni mkopo ambao utolewa na BancABC ambapo mteja anapofariki benki hiyo ufuta deni la mkopo pamoja na kutoa rambi rambi ya Tzs500,000/- kwa familia ya marehemu.

MABONDIA NA VIONGOZI WA NGUMI NCHINI WATEMBELEA BUNGE

0
0
Naibu Spika Mhe. Dkt Tulia Ackson akifurahia jambo na Mabondia na Viongozi wa Ngumi walipotembelea Bunge Jijini Dodoma leo. Kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe.

Naibu Spika Mhe. Dkt Tulia Ackson (wa pili kulia) katika picha ya pamoja na Bigwa wa Dunia wa WBO Asian Pacificc (wa tatu kulia) alipotembelea Bunge Jijini Dodoma leo. Kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe na Kushoto ni Rais wa Kamisheni ya Ngumi Bw. Joe Anea.
Naibu Spika Mhe. Dkt Tulia Ackson (wa tano kulia) katika picha ya pamoja na Mabondia na Viongozi wa Ngumi walipotembelea Bunge Jijini Dodoma leo. Watatu Kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe.
Naibu Spika Mhe. Dkt Tulia Ackson (katikati) akizungumza na Mabondia na Viongozi wa Ngumi walipotembelea Bunge Jijini Dodoma leo. Wakwanza kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe.

PICHA NA BUNGE

WATAALAM KUENDELEA KUSHAURI SERIKALI KUHUSU SEKTA YA MELI NCHINI

0
0
Bw. Julius Nguhulla akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam kulia ni Joel Uronu Katibu wa Chama cha Mawakala wa Meli (ASAA). 

............................................................

MBOBEZI wa Kimataifa katika shughuli za usafirishaji bidhaa kwa njia ya meli ambaye pia ni Mtanzania pekee kati ya wawili waliopo Tanzania wenye ubobezi wa aina yake aliyepo kwenye bodi ya watalaamu wa biashara ya usafirishaji wa mzigo kwa njia ya meli Duniani( ICS,) Julius Nguhulla(FICS) amesema ataendelea kumshauri Rais wetu mpendwa Dk.John Magufuli kuhusu sekta ya meli nchini kwa maslahi ya Watanzania wote.

Nguhulla amesema Juni 3 mwaka huu wa 2019 kwa nia njema alimuandikia barua ya kumpongeza Rais wetu kwa kazi nzuri anazofanya kuhusu sekta ya bandari na meli ikiwani pamoja na kuanzishwa kwa Shirika la Meli Tanzania(TASAC)ambapo pia aliomba Rais aishauri mamlaka husika kuhusu umuhimu watozo za delivery order na jinsi zilivyokuwa zikichangia pato kwa taifa yaani kodi.

Hata hivyo alitoa historia pamoja na umuhimu wa waraka huo na jinsi unavyopaswa kuzingatiwa kitaalamu ili kuendelea na ufanisi wa biashara ya meli na bandari.

Nguhulla ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam Salaam wakati akizungumza na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari nchini ambapo amesisitiza amewahi kumshauri Rais Magufuli kuhusu sekta ya meli kupitia barua yake hiyo aliyomuandikia .

"Tangu mwaka 2016 nimekuwa nikijishughulisha na kazi za usafirishaji bidhaa kwa njia ya meli.Mimi ni miongoni mwa watu Duniani waliokwenye Bodi ya wataalumu wa biashara ya usafiri wa mizigo kwa njia ya meli yaani shipping.

"Kutokana na ubobezi wangu katika usafiri wa mizigo kwa njia ya meli nimekuwa nikishiriki kutoa ushauri wa kitaalamu wa mambo ya meli na bandari ndani na nje ya Tanzania.Kupitia ubobezi wangu tarehe 03.06.2019 niliandika barua kumpongeza Rais wetu kwakazi nzuri anazofanya kuhusu sekta ya bandari na meli ikiwa ni pamoja na kuanzishwa kwa TASAC.

"Kadhalika , nilimwomba Rais aishauri mamlaka husika kuhusu umuhimu watozo za delivery order na jinsi zilivyokuwa zikichangia pato kwa taifa yaani kodi.

"Hata hivyo nilitoa historia pamoja na umuhimu wa waraka huo na jinsi unavyopaswa kuzingatiwa kitaalamu ili kuendelea na ufanisi wa biashara ya meli,"alisisitiza Nguhulla.

Alifafanua zaidi kwa kutumia ubobezi wake katika sekta ya bandari na meli hatasita kutoa ushauri kwa wakuu wa nchi na hasa Rais Magufuli ambaye amekuwa mzalendo kwa nchi yake,hivyo kuna kila sababu za Watanzania wa kada mbalimbali akiwemo yeye kumshauri kwa kufuata taratibu za nchi bila kuvunja sheria.

Hata hivyo alisema kuwa baada ya kumuandikia barua Rais, amesikitishwa na namna ambavyo mmoja ya wanaharakati kumtusi na kutoa maneno ya kejeli dhidi yake.

"Agosti 26, mwaka 2019 mtu mmoja alinitukana kwa kutumia moja ya televisheni nchini na kusema mimi nilimwandikia barua kumshauri Rais kuhusu waraka unaoitwa delivery order na tozo zake.Mtu huyo alinichafua na kunitukana kwa kutaja jina langu kwa kudai kwamba kwa uamuzi huo mimi nilioufanya mimi ni mjinga na mpuuzi kabisa na sijui chochote,.

"Waandishi wa habari ni kweli nilimwandikia barua Rais nikimshauri kuhusu mada kama nilivyotaja hapo juu nikiwa na haki ya kumshauri Rais wangu kwa lengo la maendeleo ya Taifa langu lakini, hata hivyo nimedhalilishwa kwa kutukanwa kama nilivyoainisha hapo juu huku nikitajwa Jina langu,"alisema.

Alifafanua kuwa ameambiwa amemdanganya Rais wetu kuwa shipping ni taaluma yake na kwamba hajawahi kufanya kazi ya aina hiyo popote.Hivyo alisema kwa sababu upotoshaji na udhalilishaji huu ulifanywa kwenye chombo cha habari umma wa watanzania ukasikia na yeye ameona atoe sikitiko lake la kutukanwa mbele ya Umma wa Watanzania.

Pia alisema amejitokeza hadharani kukanusha mbele ya umma wa watanzania kwamba yeye hakumdanganya Rais kwamba shipping ni taaluma yake,hivyo aliamua kutoa ufafanuzi hatua kwa hatua kuhusu shughuli ambazo amezifanya.

Nguhullla amewaambia waandishi wa habari kuwa anayo shahada ya heshima kutoka nchini Uingereza kuhusu mambo ya usafirishaji wa mizigo kwa njia ya meli yaani Shipping baada ya kusomea kwa miaka mitano na kuingia kwenye bodi ya wataalamu wa shiping wa dunia ambapo chao cha juu cha kitaalam kwenye masuala ya biashara ya meli ni cha mtu anayeitwa FICS ambapo kwa Tanzania imefanikiwa kumtoa mtu mmoja ambaye ni yeye kati ya watu 2000 duniani.

Pia anayo Masters ya Biashara ya meli yaani MBA in shipping aliyoisomea Cyprus na sasa anaendelea na utafiti( Global Business University).

Alisema anao uzoefu wa miaka 15 ya kazi za meli( uwakala wa meli) na amewahi kufanya kazi na Mkurugenzi Mkuu wa TASAC wa sasa kwa muda wa miaka mitatu akiwa mwajiri wake na kuongeza kila mwaka huwa anaenda nje ya Tanzania kwa ajili ya mikutano ya shipping pamoja na kufundisha.

"Sisemi haya kujisifu ila namshukuru Mungu maana yeye peke yake ndio wakusifiwa. Kadhalika , Serikali yangu ya Tanzania imekuwa ikinihusisha sana na shughuli mbalimbali ikiwemo mikutano ya kuelimisha kuhusu shipping na mengineyo. Ipo siku nilitoa somo nikiwa na CEO wa TICTS tulipoalikwa na serikali kueleza umuhimu wa Teknolojia katika Port Operations. Serikali imewahi kuniomba kuwafanyia interview wakurugenzi waliokuwa wanataka kuajiriwa kwenye ofisi ya Serikali inayohusika na shipping.

"Nimewahi kuombwa na TRA kufanya mafunzo kwa siku mbili katika kitengo cha enforcement kuhusu Bill of Lading. Pia Januari mwaka 2018 nilitoa Presentation Tanzania ikijumuisha watu wa Serikali , na wamiliki wa meli wa mataifa mbalimbali , idadi ya watu ikiwa ni 200 kuhusu matumizi ya bill of leading, manifest na mengine mengi,"alisema.

Alisisitiza bila uzoefu wake na taaluma aliyonayo Serikali yake isingempa heshima kama hiyo ambayo ameianisha na kumuomba mtu asitumie cheo chake ambacho amepewa na Mungu kuwatumikia watanzania kwa kutukana watu na taaluma zao.

"Namheshimu sana mtu huyu na nitaendelea kumheshimu na nina msamehe maana umri wake kwangu ni kama baba yangu. Na haya niliyosema si kwamba namshambulia ila naeleza ili Umma ufahamu kuhusu mimi na kupuuza upotoshaji uliofanywa dhidi yangu na heshima ya taaluma yan,"alisema Nguhulla.

Alisisitiza watanzania wanayofursa sawa ya kumshauri Rais pasipo kuvunja sheria na kwamba kama wameamua kuzungumzia maslahi yaTaifa ,basi waendelee na mtazamo huo huo badala ya kuhamia katika maslahi binafsi.

WAFANYABIASHARA WAIPONGEZA BENKI YA NMB KWA KUTOA HUDUMA ZA KIBENKI MAENEO MENGI MKOANI KIGOMA

0
0
Baadhi ya wananchi Wilayani Kasulu mkoani Kigoma wameziomba taasisi mbalimbali za kifedha kuongeza vituo vya kutolea huduma za kibenki katika maeneo ya vijijini ili kupunguza changamoto ya wafanyabiashara kuvamiwa na kuporwa fedha zao pale wanaposafiri na fedha kwenda kununua bidhaa
mbalimbali hasa nafaka.

Wakizungumza wakati wa mkutano wa biashara na wateja wa benki ya NMB wilayani Kasulu mkoani Kigoma, wananchi hao walisema kuwa kumekuwepo na matukio ya mara kwa mara ya wafanyabiashara kuvamiwa na kunyang’anywa fedha zao jambo walilodai kuwasababishia usumbufu na kushindwa kufanya biashara kutokana na kuwepo kwa vitendo hivyo.

Bi.Emmakulatha Mazina ambaye ni mfanyabiashara wilayani humo alisema uwepo wa taasisi za kifedha katika maeneo ya vijijini itasaidia pia kuongeza mzunguko wa fedha na kukuza biashara hasa kutokana na baadhi ya wakulima na wanunuzi wa mazao wakifanya biashara kwa hofu ya kuvamiwa, huku pia wakiomba serikali na wadau wengine wa maendeleo kutoa elimu kwa wananchi wa vijijini juu ya namna bora ya kuhifadhi fedha kwenye mabenki ili kuepuka hasara zisizokuwa za lazima zinazoweza kujitokeza.

“Wafanyabiashara kusafiri na pesa kwa sasa ni hatari sana katika maeneo yetu, unakuta mtu anaenda kijijini kununua mahindi au mihogo na hata mazao mengine akiwa na pesa mikononi, majambazi wakijua tu anatafuta bidhaa wanaanza kupanga njama za kumvami”alisema.

Aidha wafanyabiashara hao waliipongeza benki ya NMB kwa kutoa huduma za kibenki katika maeneo mengi ya mkoa wa Kigoma na kuomba benki hiyo kuendelea kuboresha huduma kwa wateja wake pamoja na kuona haja ya kutoza viwango vya riba za mikopo kwa kuzingatia hali ya kipato cha maeneohusika.

Pia waliiomba benki hiyo kuharakisha mchakato wa utoaji mikopo mikubwa kwa wateja kwa kuwaruhusu mameneja wa matawi kufanya tathimini na kumuidhinisha mteja kukopeshwa mkopo mkubwa tofauti na ilivyo sasa ambapo mteja hulazimika kusubiri majibu kutoka ngazi ya kanda na makao makuu ya ofisi za benki hiyo hali waliyosema imekuwa ikisababisha usumbufu mkubwa kwao.

Kwa pande wake Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi Sospeter Magesse alisema benki hiyo inaendelea kutatua changamoto zilizopo katika maeneo mbalimbali ili kuhakikisha malengo ya benki hiyo kuwahudumia wananchi yanafanikiwa kama ilivyokusudiwa.

Aidha alisema kuwa benki hiyo imeanza utaratibu wa kushusha madaraka ya kutoa mkopo hadi bilioni moja kwa mameneja wa benki ngazi ya tawi ili baada ya kupokea maoni kutoka kwa wateja wake katika maeneo mbalimbali nchini.

“Tunajaribu kuweka mambo sawa yakiwemo ya kisheria ili kujaribu kulegeza vigezo na masharti, lakini pia tuna mikopo ya aina nyingi mfano unahitaji kukopa milioni sitini za kujenga kiwanda, hapo lazima taratibu zifanyike hata kuanzia ngazi ya chini hadi kwenye bodi yetu ya wakurugenzi na wao ndio wenyemamlaka ya kuruhusu mkopo huo utolewe”alisema meneja huyo.

Awali akiwasilisha mada katika mkutano huo mshauri wa masuala ya kibiashara kutoka kampuni ya TRUEMAISHA TRAINING COMPANY Bwana Erick Chrispin ambaye pia ni mkurugenzi wa kampuni hiyo aliwapongeza wafanyabishara wa wilaya ya Kasulu kuwa na idadi kubwa ya wafanyabiashara wanaofanya vizuri katika biashara zao huku akiwashauri kuwa makini katika kufanya biashara kwa kutumia mbinu za kitaalamu ambazo zitawasaidia kuepuka kupata hasara na kuona biashara kama mzigo.

Bidhaa ya unga wa Ngano ya AZAM sasa kupatikana katika vifungashio vipya

0
0
Uongozi wa kampuni ya kutengeneza vyakula inayomikiliwa na makampuni ya Said Salim Bakhresa &Ltd, inayozalisha unga bora wa ngano wenye jina la kibiashara la Azam, imetangaza kubadilisha muonekano wa bidhaa yake maarufu ya unga wa ngano unaojulikana kwa chapa ya Ngano Bora.

Muonekano mpya wa kifungashio (mfuko) wa bidhaa hii umeboreshwa ili kuwapatia wateja wake kuitambua kwa urahisi na kuweza kuitofautisha na bidhaa zenye vifungashio vinavyofanana nayo.

Akiongea katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Mahusiano wa kampuni hiyo,Hussein Sufian , amesema kumekuwepo na wazalishaji ambao wanaiga na kubadilisha rangi za muonekano wa bidhaa zao zifanane na bidhaa za AZAM, hali ambayo imekuwa ikiwachanganya wateja kwenye masoko kutambua bidhaa za kampuni hiyo.

Alisema kutokana na kubadilisha vifungashio, wateja wa Ngano Bora, unaotengenezwa na AZAM kwa sasa wataweza kutambua bidhaa hizo kwa urahisi pia ametoa tahadhari kwa wazalishaji wasio waaminifu ambao wamekuwa wakiiga muonekano wa bidhaa za kampuni hiyo kuacha kufanya hivyo kwa kuwa wanavunja sharia na tayari wameishatoa taarifa kwa mamlaka mbalimbali,watakaokamatwa kwa kufanya udanganyifu huu watachukuliwa hatua za kisheria.

Aidha kampuni imetoa tahadhari kwa wafanyabiashara ambao wamekuwa wakitumia vifungashio vya bidhaa za kampuni hiyo zilizotumika na kujaza bidhaa nyingine na kuziuza kwa wateja kama bidhaa za kampuni ya AZAM.

Sufian alisema kampuni inapenda kuwahakikishia wateja wake kuwa itaendelea na ubunifu na uzalishaji wa bidhaa zenye kiwango cha juu ubora kukidhi matakwa ya wateja wote nchini na nje ya nchi.

Mkurugenzi wa Mahusiano wa kampuni ya Said Bakhresa Group, Hussein Sufian (kushoto) na Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni hiyo Ahmed Jaruan, wakionyesha waandishi wa habari muonekano mpya wa vifungashio vya unga wa ngano wa Azam ujulikanao kama Ngano Bora, ikiwa ni mkakati wa kulinda ubora na kutambulisha bidhaa zake kwa wateja.
Mkurugenzi wa Mahusiano wa kampuni ya Said Bakhresa Group, Hussein Sufian akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaaam (hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa muonekano mpya wa vifungashio vya unga wa ngano wa Azam ujulikanao kama Ngano Bora, ikiwa ni mkakati wa kulinda ubora na kutambulisha bidhaa zake kwa wateja.Wengine pichani ni Maofisa Waandamizi wa kampuni hiyo
 

Bolt yatanua wigo wa huduma zake katika miji mikubwa Tanzania

0
0
KAMPUNI inayokua kwa kasi katika utoaji wa huduma za usafiri kwa njia ya mtandaoni barani Ulaya na Afrika- BOLT, inatarajia kuzindua huduma zake katika miji mikubwa miwili nchini Tanzania ikiwa ni hatua mojawapo ya kuendelea kupanua huduma za usafiri katika soko lake la ndani ya nchi.

Huduma hiyo imeanza kupatikana jana Septemba 4, 2019 katika jiji la Arusha na kuanzia wiki ijayo itaanza kupatikana Visiwani Zanzibar.

Uzinduzi huo wa Bolt katika jiji la Arusha na Visiwani Zanzibar unaongeza idadi ya miji ya Kitanzania inayohudumiwa na kampuni hiyo kutoka mikoa mitatu hadi mitano, na kuifanya Bolt kuwa mtoaji huduma mkubwa wa usafiri kwa njia ya mtandao katika ukanda huu wa Afrika.

Meneja wa Bolt Tanzania, Remmy Eseka alisema kuwa dhamira ya Bolt ni kufanya usafirishaji wa mijini kuwa rahisi zaidi na wa bei nafuu kwa watu wote na hivyo kufikia malengo ya kampuni katika utoaji huduma za usafiri na ajira ikiwa ni moja ya mchango Bolt kwa jamii.

"Baada ya miji ya Dar es Salaam, Mwanza na Dodoma kama ilivyo ada Bolt imeendelea kukua kwa kasi nchini kote. Sasa tunakusudia kujenga jamii mpya Arusha na Zanzibar kutokana na uaminifu tunaoendelea kuupata kwa Watanzania," alisema Eseka.

Alisema huduma hiyo ni rahisi kutumi kwani abiria wanatakiwa kupakua programu ya Bolt kutoka kwenye maduka ya programu ya iOS au ya Android na kujaza wasifu wa mtumiaji. Wakati wapo tayari kusafiri, watumiaji hufungua program na kuweka eneo lao walilopo na mahali walipokusudia kufika.

Pia Programu itatoa makisio ya gharama kwa safari hiyo.

"Mara baada ya abiria kuomba safari, programu humwonesha madereva wa karibu ambao wanakubali safari hiyo.Mara tu dereva anapokubali safari hiyo, abiria wataweza kuona jina la dereva wao, picha, muundo wa gari na usajili, na kuweza kufuatilia dereva anayewafuata kwa wakati muafaka na wa kweli lakini pia program hiyo hufanya iwe rahisi kuwa na uhakika kuwa wanaingia salama kwenye gari sahihi na dereva sahihi.

"Abiria pia wanaweza kutoa maelezo ya safari yao kwa kutumia program ‘ETA’ iliyomo katika kipengele cha ziada kwenye suala la usalama.

"Wakati safari imekamilika, malipo hufanywa na pesa taslimu, au kupitia kadi ya deni ya mpandaji aliyejiunga kwenye program hiyo. Abiria na madereva wanaweza kupima kila mmoja kati ya nyota tano na kutoa maoni kuhusu umahiri wa utumiaji programu ya Bol," alisema.

Aidha, alisema Bolt tayari imewasajili madereva katika miji ya Arusha na Visiwani Zanzibar, ambao wote wanapokea asilimia 80 ya nauli zote zinazolipwa na abiria.Hata hivyo, madereva wanaotumia Bolt wanaweza kuchagua masaa mangapi wanaendesha na wanaweza kufanya kazi katika maeneo yoyote wanayotaka.

"Magari ya Madereva lazima yawe yamesajiliwa kuanzia mwaka 2000 au mapya zaidi. Gari lazima iwe na milango minne (Toyota Corolla, aina ya Hyundai, Kia Rio, nk). Hii inamaanisha kuwa kila mtu akipanda safari kupitia Bolt anaweza kuwa na hakika kwamba watafika salama kwao na kwa raha," alisema.
Mwisho

WAZIRI WA MAMBO YA NJE PROF. KABUDI AWAAGA WANAFUNZI WANAOKWENDA ISRAEL KUSHIRIKI MAFUNZO YA KILIMO

0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wanafunzi 44 kati ya 100 waliochaguliwa kwenda nchini Israel kushiriki program ya mafunzo ya kilimo kwa kipindi cha miezi tisa kuanzia mwezi Septemba 2019. Hafla hiyo imefanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam tarehe 4 Septemba 2019. Wengine katika picha kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati, Bw. Ayoub Mndeme na Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Bw. Emmanuel Buhohela. 
Prof. Kabudi akizungumza na wanafunzi hao 
Wanafunzi hao wakimsikiliza Prof. Kabudi (hayupo pichani) 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirkiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe naye akiwaasa wanafunzi hao kuzingatia maadili na kuwa wazalendo wanapokuwa kwenye mafunzo nchini Israel 
Dkt. Mnyepe akizungumza 
Mhe. Prof. Kabudi akimkabidhi tiketi na hati ya kusafiri, Bi. Janeth Barnaba ambaye ni mmoja wa wanafunzi wanaokwenda kushiriki mafunzo ya kilimo nchini Israel 
Mwanafunzi mwingine akipokea tiketi na hati yake ya kusafiria tayari kuelekea nchini Israel tarehe 5 Septemba 2019 kwa ajili ya kuanza program ya mafunzo ya kilimo 
Prof. Kabudi akiendelea na zoezi la kuwakabidhi wanafunzi hao tiketi na hati zao za kusafiria kama inavyoonekana pichani 
Zoezi la kukabidha tiketi na hati za kusafiria likiandelea 
Wanafunzi wakishuhuda mwenzao akikabidhiwa hati yake ya kusafiria na tiketi ya ndege 
Prof. Kabudi akikabidhi hati za kusafiria na tiketi za ndege kwa wanafunzi wanaokwenda Israel kushiriki program ya mafunzo ya kilimo kwa vitendo 
mwanafunzi akifurahia kukabidhiwa hati ya kusafiria na tiketi ya ndege vitakavyomwezesha kwenda Israel kushiriki mafunzo ya kilimo 
Prof. Kabudi akimkabidhi hati ya kusafiria na tiketi ya ndege mwanafunzi atakayeshiriki program ya mafunzo ya kilimo nchini Israel 
Wanafunzi wakiwa wameshikilia hati zao za kusafiria na tiketi za ndege zitakazowawezesha kusafiri kwenda Israel kushiriki program ya mafunzo ya kilimo 
Mhe. Prof. Kabudi akiwaasa wanafunzi hao mara baada ya kuwakabidhi tiketi zao na hati za kusafiria zitakazowawezesha kwenda Isarel kuanza mafunzo ya kilimo kwa vitendo. Prof. Kabudi aliwataka wanafunzi hao kuwa waadilifu, wasikivu, wachapakazi, wazalendo na warejee nyumbani wakiwa na ujuzi na maarifa kwa manufaa ya Taifa.
===============================================================

Serikali ya Tanzania inaungana na Serikali ya Afrika Kusini kulaani vikali vitendo vya ubaguzi na mashambulizi vinavyofanywa na raia wachache wa nchi hiyo dhidi ya raia wa nchi zingine za Afrika na kuziasa nchi zingine kutolipa kisasi kutokana na vitendo hivyo.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wanafunzi 100 kutoka Tanzania wanaokwenda Israel kushiriki mafunzo ya kilimo iliyofanyika leo tarehe 4 Septemba 2019 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Mhe. Prof. Kabudi amesema kuwa, vitendo vinavyofanywa na raia wachache wa Afrika Kusini vya kuwashambulia raia kutoka nchi zingine za Afrika na kuharibu mali zao vinasikitisha na kuivunjia heshima nchi hiyo. Hata hivyo, alisema kuwa Serikali ya Tanzania inaunga mkono kauli ya Rais wa Afrika Kusini, Mhe. Cyril Ramaphosa aliyoitoa hivi karibuni ya kukemea na kulaani vikali vitendo vinavyofanywa na raia hao wachache.

Aidha, ameongeza kuwa, vitendo hivyo ambavyo vinatokana na raia hao wengi kukosa ajira, ardhi na pia kutopenda kujishughulisha havihalalishi watu wengine wakiwemo watanzania kulipa kisasi kwa namna yoyote ile.

“Ni jambo la kusikitisha lakini Serikali ya Afrika Kusini inalisimamia kikamilifu na sisi tupo tayari kushirikiana nao ili kulitafutia ufumbuzi wa kudumu.Nawasihi Watanzania wenzangu tusilipize kisasi na tutaendelea kuwalinda raia wa Afrika Kusini waliopo Tanzania kwani tunaamini kuwa Afrika ni moja na waafrika ni ndugu zetu” alisema Prof. Kabudi.

Kadhalika, Prof. Kabudi alieleza kuwa hadi sasa hakuna taarifa kuhusu Mtanzania kuuawa, kujeruhiwa au kuharibiwa mali kutokana na vurugu hizo. Pia alisema kuwa Wizara itaendelea kutoa taarifa za uhakika kadri zinavyopatikana kutoka kwenye vyanzo vya uhakika ukiwemo Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini.

Wakati huohuo, Mhe. Prof. Kabudi amewaaga wanafunzi 44 kati ya 100 waliochaguliwa kwenda nchini Israel kushiriki mafunzo ya kilimo kwa vitendo kwa kipindi cha miezi tisa kuanzia mwezi Septemba 2019. Wanafunzi hao ambao wengi wamehitimu katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), Taasisi ya Kilimo ya Uyole ya Mbeya na Ukiriguru ya Mwanza wanakwenda kushiriki mafunzo hayo ya vitendo kwenye sekta mbalimbali za kilimo ikiwemo uzalishaji na teknolojia. Kati ya Wanafunzi hao, 16 wameondoka nchini tarehe 4 Septemba, 2019, kuelekea Israel, 44 wataondoka nchini tarehe 5 Septemba 2019 na idadi iliyosalia itaondoka tarehe 10 Septemba 2019.

Katika hotuba yake, Mhe. Prof. Kabudi amewataka wanafunzi hao vijana kuzingatia mafunzo hayo ili kuja kutoa mchango wao kwenye mapinduzi ya kilimo ambayo yatachochea mapinduzi ya viwanda nchini. Aidha aliwaasa kuwa waadilifu, kufanyakazi kwa bidii, kushikamana na kujiepusha na vitendo viovu. 

“Mnaenda Israel kutafuta ujuzi, uzoefu na ubunifu katika maeneo ya uzalishaji mazao. Hivyo tunaamini kuwa mna nafasi kubwa ya kuja kuibadilisha Tanzania katika eneo la kilimo na mtaleta mapinduzi ya kilimo kwani vijana mpo wengi nchini, mna ari na ni nguvu kazi ya Taifa” alisisitiza Prof. Kabudi.

Akiielezea Israel, Mhe.Prof. Kabudi amesema kuwa nchi hiyo ni nusu jangwa kama ilivyo baadhi ya mikoa hapa nchini. Hata hivyo Israel inaongoza kwa kuuza mazao ya mbogamboga na matunda kwenye nchi za Ulaya kutokana na watu wa nchi hiyo kutumia maarifa katika kugeuza ukame kuwa fursa. Hivyo aliwataka wanafunzi hao kuhakikisha wanapata maarifa na kujifunza mbinu bora na teknolojia za kisasa ili kuja kuendeleza kilimo kikiwemo kile cha umwagiliaji kwenye mikoa kama Singida, Manyara, Shinyanga na Dodoma.

Wanafunzi hao mia moja (100) wamechaguliwa kati ya wanafunzi 1,440 waliotuma maombi ya kwenda kushiriki program ya mafunzo ya kilimo nchini Israel ambayo hufanyika kwa kipindi cha miezi tisa. Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki iliratibu zoezi la upatikanaji wa wanafunzi hao kwa maelekezo ya Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyoyatoa mwezi Novemba 2018 alipofanya mazungumzo na Balozi wa Israel nchini, Mhe. Noah Gal Gendler.


Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dar es Salaam.

Azania Benki yatangaza washindi wapya wa promosheni ya ‘AMSHA NDOTO’

0
0
Meneja wa Mauzo ya Reja Reja wa Benki ya Azania, Thobias Samwel (kulia) akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kufanyika kwa droo ya kupata washindi iliyofanyika katika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Humud Semvua, mjumbe kutoka Bodi ya Taifa ya Michezo ya Kubahatisha

 Benki ya Azania (ABL) leo imewatangaza washindi wa awamu
ya pili ya promosheni yake ya ‘Amsha Ndoto’ ambayo ina lengo la kuwahamasisha wateja wake na umma wa watanzania kujenga utamaduni wa kuweka akiba itakayowasaidia kuwa na maishaya baadaye yaliyo imara kifedha.

Promosheni hii ambayo ni ya mizezi mitatu ilianza rasmi tarehe 27/06/2019 na inatarajia kufikiatamati tarehe 27/09/2019 huku ikihusisha wateja wa Azania Benki wa zamani na wale wapya naimejikita zaidi katika bidhaa mbili kuu za uwekaji akiba, ambazo ni: Ziada Akaunti pamoja naWatoto Akaunti.

Mwezi Agosti, droo ya kwanza ya promosheni hii ilifanyika ambapo jumla ya washindi watatuwalipatikana ambao wote kwa pamoja walijishindia jumla ya shilingi millioni 8.Akitangaza washindi kwenye droo ya mwezi huu ambayo imefanyika leo jijini Dar es Salaam,Meneja wa Mauzo ya Reja Reja wa Benki ya Azania, Thobias Samwel, amesema benki imetimizaahadi ya kuwapatia zawadi washindi walioshoriki kwenye promosheni na kwamba zawadi
wanazopewa zitawasaidia kutimiza ndoto zao.

 “Katika droo iliyopita tulipata washindi kutokaArusha, Tunduma paamoja na Dar es Salaam na wote walipewa zawadi zao kama walivyostahili,”
amesema Samwel.Kwa mujibu wa Samwel, washindi wa mwezi huu wa promosheni hii ambao wamepatikana baadaya droo kufanyika ni; (kiasi cha fedha walichojishindia kwenye mabano);
1. Lucas Brian Temu kutoka Mwanza (Sh milioni 3)
2. Amos Wankara Nyansada kutoka Geita (Sh milioni 3)
3. Alye Awadhi kutoka Geita (Sh milioni 2)

Huku ukiwa umebaki mwezi mmoja kampeni hii kufika tamati, Samwel amesema kuwa ili mtu aweze kushiriki kwenye promosheni ya Amsha Ndoto ni lazima kwanza awe mteja wa AzaniaBenki mwenye akiba ya kiasi kisichopungua TZS 1,000,000 ambaye anapewa tokenizinazomwezesha kufuzu kwa ajili ya droo ya mwisho inayowapata washindi. Wanaobahatikakushinda watafurahia riba ya 6% katika kipindi chote cha kampeni na mwaka mzima.

Akitoa pongezi kwa washindi wa promosheni, Samwel amewahasa wateja wa ABL kushiriki kwawingi na kwamba wana nafasi kubwa ya kujishindia zawadi lukuki katika droo inayofuata hukuPage 2 of 2wakijahakikishia kuwa na akiba ya kutosha kwenye akaunti zao kwa ajili ya matumizi yao ya siku za usoni.

Kwa mujibu wa Samwel, ‘Ziada Akaunti’ ni kwa ajili ya watu binafsi na wafanyabiashara wadogo (SMEs) wanaotaka kujivuna kiwango kizuri cha riba. Mmiliki anaweza kuweka akiba muda wowote na kuweza kutoa kila baada ya miezi mitatu. Na ‘Watoto Akaunti’ ni kwa ajili ya watoto, akaunti ambayo inafunguliwa na mzazi kwa ajili kumwekea akiba mtoto wake.

“Tunawahamasisha wazazi wote na walezi kuwafungulia Watoto wao ‘Watoto Akaunti’ ili kuwa na uhakika wa maisha yao ya baadaye yaliyo salama. Kwa namna hii hawatahangaika kutafuta namna gani ya kuwaandaa watoto wao kwa maisha ya baadaye kwani akaunti hii inaweka msingi wa kuwaandaa watoto kujifunza namna ya kuweka akiba kuanzia kwenye umri mdogo”, amesema Samwel.

Promosheni hii, yenye kaulimbiu: ‘Weka Akiba Ushinde Tumuwezeshe Ada ya Shule’, inawasilishwa kupitia mitandao ya kijamii na tovuti za ndani za benki. Benki pia imetengeneza tovuti ndogo, maalumu kwa wateja wapya kujiunga na inaweza kupatikana kupitia amshandoto.com

Viewing all 46201 articles
Browse latest View live




Latest Images