Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1870 | 1871 | (Page 1872) | 1873 | 1874 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusine na mkewe Dkt. Tshepo Motsepe wakiwasili
  katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius  Nyerere jijini Dar es
  salaam usiku huu. Rais Ramaphosa amewasili kwa ziara rasmi ya siku
  mbili nchini kabla ya kuhudhuria Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Nchi
  Wanachama za Jumuiya ya Maendeleo  ya Kusini kwa Afrika SADC
   Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusine akipokewa na Waziri wa Mambo ya Nje naUshirikiano wa Afrika Mashariki katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
  Julius  Nyerere jijini Dar es salaam usiku huu. Rais Ramaphosa
  amewasili kwa ziara rasmi ya siku mbili nchini kabla ya kuhudhuria
  Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Nchi Wanachama za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini kwa Afrika SADC
   Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini akipeana mikono  na Mkuu wa Wilaya ya
  Ubungo Mhe. Kisare Makori alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa
  Kimataifa wa Julius  Nyerere jijini Dar es salaam usiku huu. Wengine
  kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo,
  Mkuu wa Wiklaya ya Kigamboni Mhe. Mhe. Sarah Misafiri na Mkuu wa
  Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema. Rais Ramaphosa amewasili kwa ziara
  rasmi ya siku mbili nchini kabla ya kuhudhuria Mkutano wa Viongozi
  Wakuu wa Nchi Wanachama za Jumuiya ya Maendeleo  ya Kusini kwa Afrika SADC
  Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini akipeana mikono  na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa
  Kimataifa wa Julius  Nyerere jijini Dar es salaam usiku huu. Kushoto
  ni Kamanda wa Kanda Mazlumu ya Kipolisi ya Dar es salaam Lazaro
  Mambosasa. Rais Ramaphosa amewasili kwa ziara rasmi ya siku mbili
  nchini kabla ya kuhudhuria Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Nchi Wanachama
  za Jumuiya ya Maendeleo  ya Kusini kwa Afrika SADC 
   Rais Cyril Ramaphosa akiongozana na Waziri wa Mambo ya Nje na
  Ushirikiano wa Afrika Mashariki baada ya kupokewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa waJulius  Nyerere jijini Dar es salaam usiku huu. Rais Ramaphosa
  amewasili kwa ziara rasmi ya siku mbili nchini kabla ya kuhudhuria
  Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Nchi Wanachama za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini kwa Afrika SADC

  0 0

   Umoja wa wazazi CCM mkoa Shinyanga umetoa tamko la kumpongeza Rais John Magufuli kutokana na kutekeleza ipasavyo ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa kutetea haki za wanyonge pamoja na kuiletea nchi mafanikio makubwa ya kimaendeleo.

  Tamko la umoja huo wa wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga, limetolewa leo Agosti 14, 2019 kwenye kongamano la umoja huo, ambao limehudhuriwa na wajumbe kutoka wilaya ya Kishapu, Kahama, Shinyanga vijijini, na manispaa ya Shinyanga, ambalo limefanyika kwenye ukumbi wa CCM mkoa, huku mgeni rasmi akiwa mjumbe wa NEC Gaspar Kileo. 

  Akisoma tamko hilo, Katibu wa Umoja wa Wazazi mkoa wa Shinyanga Masanja Salu, amesema wanampongeza Rais John Magufuli kwa kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM ipasavyo, ambapo ndani ya miaka minne tangu alipoingia madarakani amefanya mambo makubwa ikiwamo kuiletea nchi maendeleo.

   “Sisi Umoja wa Wazazi mkoa wa Shinyanga tunatoa tamko la kupongeza Rais John Magufuli kwa kutekeleza ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi kwa asilimia 100, ambapo ndani ya miaka yake minne tu akiwa madarakani amefanya mambo makubwa sana katika nchi yetu, hivyo lazima tumpongeze na kumuombea pia,”amesema Salu. 

  “Mambo ambayo ameyafanya Rais wetu na anapaswa kupongezwa ni pamoja na kudhibiti mafisadi, rushwa, mishahara hewa, utoroshwaji wa makinikia, upotevu wa mapato, kaboresha mikataba mibovu ya madini, elimu bure, ujenzi wa madaraja, miundombinu ya barabara, reli ,huduma za afya, ununuaji wa ndege, na makazi ya watumishi,”amefafanua Salu. 

  Naye mgeni rasmi kwenye kongamano hilo la kumpongeza Rais John Magufuli mjumbe wa halmashauri kuu Taifa mkoani Shinyanga (NEC) Gaspar Kileo, akipokea tamko la pongezi hizo kwa niaba ya Rais Magufuli, ameupongeza umoja huo wa wazazi CCM mkoani humo kwa kutambua kazi kubwa ambayo anaifanya rais Magufuli.

  Amesema mbali na pongezi hizo, lakini zawadi pekee ambayo wanapaswa kumpa Rais John Magufuli, ni kumpatia ushindi wa kishindo kwa asilimia 100 kwenye changuzi zote kuanzia serikali za mitaa mwaka huu, pamoja na uchaguzi mkuu ujao mwaka 2020,wapinzani wasiweze kupata hata kiti kimoja cha ushindi waambulie zero.

   Aidha amesema ushindi huo ndiyo itakuwa zawadi kubwa kwa Rais John Magufuli ikisindikiza tamko lao la pongezi, huku akiwataka pia wajitokeze kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la mpiga kura, na kuhamasisha majirani zao, ndugu, jamaa na marafiki, ili waweze kupiga kura na kuipatia ushindi huo mnono CCM.  Mwenyekiti wa Umoja wa Wazazi CCM mkoa wa Shinyanga Salum Abdalah Simba akizungumza wakati Umoja huo ukitoa tamko la kumpongeza rais John Pombe Magufuli kwa kutekeleza kikamilifu ilani ya CCM. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog  Katibu wa Umoja wa Wazazi CCM mkoa wa Shinyanga Masanja Salu akisoma Tamko la umoja wa wazazi mkoa wa Shinyanga la kumpongeza Rais John Magufuli kwa uchapakazi wake wa kutekeleza ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi kwa asilimia 100. Katibu wa Umoja wa wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga Masanja Salu, mkono wa kulia akimkabidhi tamko la kumpongeza Rais John Magufuli, mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM Taifa NEC mkoani Shinyanga Gaspar Kileo kwa niaba ya Rais ambapo atamfikishia tamko lao.  Kitabu chenye tamko la Umoja wa Wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga la kumpongeza Rais John Magufuli kwa kutekeleza ipasavyo ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).  Mjumbe wa halmashauri kuu taifa (NEC) Gaspar Kileo akiteta jambo na mwenyekiti wa umoja wa wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga Salum Abdala Simba,kwenye kongamano la kupongeza utendaji kazi wa Rais John Magufuli kwa kutekeleza ilani ya CCM kwa asilimia 100.  Mjumbe wa halmashauri kuu Taifa (NEC) Gaspar Kileo, akizungumza mara baada ya kupokea Tamko la umoja wa wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga la kumpongeza Rais John Magufuli kwa kutekeleza Ilani ya uchaguzi ya CCM kwa asilimia 100 ndani ya miaka minne tu.  Mjumbe wa halmashauri kuu Taifa (NEC) Gaspal Kileo, akiwa asa wajumbe wa umoja huo wa wazazi CCM mkoa wa Shinyanga kuwa licha ya pongezi hizo, bali wanatakiwa wampatie zawadi Rais John Magufuli ya ushindi wa kishindo kwenye chaguzi zote kuanzia Serikali za mitaa hadi uchaguzi mkuu ujao mwaka 2020.  Mchungaji Elias Madoshi kutoka kanisa la FPCT Shinyanga akipongeza utendaji kazi wa Rais John Magufuli.  Shekhe Alhaji Ibrahimu Ramadhani akipongeza utendaji kazi wa Rais John Magufuli.  Wajumbe wa Umoja wa wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye Kongamano la kumpongeza Rais John Magufuli la kutekeleza ipasavyo ilani ya uchaguzi ya CCM ndani ya miaka yake Minne akiwa madarakani.  Wajumbe wakiwa kwenye Kongamano la kumpongeza Rais John Magufuli.  Wajumbe wa umoja wa wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye Kongamano la kumpongeza Rais John Magufuli la kutekeleza ipasavyo ilani ya CCM ndani ya miaka yake Minne akiwa madarakani.  Wajumbe wakiwa kwenye Kongamano la kumpongeza Rais John Magufuli.  Wajumbe wa umoja wa wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye Kongamano lao la kumpongeza Rais John Magufuli la kutekeleza ipasavyo ilani ya CCM.  Wajumbe wakiwa kwenye Kongamano la kumpongeza Rais John Magufuli.  Wajumbe wa umoja wa wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye Kongamano lao la kumpongeza Rais John Magufuli la kutekeleza ipasavyo ilani ya CCM.  Wajumbe wakiwa kwenye Kongamano la kumpongeza Rais John Magufuli.  Wajumbe wa umoja wa wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga wakipiga picha na MNEC Gaspar Kileo mara baada ya kupokea tamko lao la kumpongeza Rais John Magufuli.  wajumbe wakiendelea kupiga picha.  Wajumbe wa umoja wa wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga wakiserebuka huku wakibeba tamko lao la kumpongeza Rais John Magufuli.  Wajumbe wakendelea kuserebuka.Awali mjumbe wa halmashauri kuu Taifa (NEC) Gaspal Kileo mkono wa kulia akiingia ukumbini kwenye Kongamano la umoja wa wazazi CCM mkoa wa Shinyanga la kumpongeza Rais John Magufuli, kushoto ni mwenyekiti wa wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga Salum Abdala Simba.  Mjumbe wa halmashauri kuu Taifa (NEC) Gaspar Kileo akiwasili kwenye ukumbi wa CCM Mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kupokea Tamko la kumpongeza Rais John Magufuli lililoandaliwa na umoja wa wazazi CCM Mkoani humo, ambapo amepokelewa na viongozi wa umoja huo, huku akiwa ameshikana mkono na katibu wa umoja wa wazazi mkoa wa Shinyanga Masanja Salu.  Askofu Josephat Musira wa kanisa la TMRC- Ndembezi Shinyanga mjini, akimwombea Rais John Magufuli, pamoja na makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, na waziri mkuu Kassim Majaliwa na wateule wake wote wakiwamo mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya, Mungu awajalie afya njema na kuendelea kuchapa kazi ya kutumikia wananchi na kuleta maendeleo ya taifa. Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog

  0 0

  President Cyril Ramaphosa and Spouse Dr Tshepo Motsepe arrive at the State House received by President of the United Republic of Tanzania, President John Pombe Magufuli for the State Visit held today, 15 August 2019, in Dar es Salaam in the United Republic of Tanzania. 

  This is the first State Visit by President Ramaphosa since assuming office in May 2019. The visit will allow the two leaders to discuss bilateral, continental and global issues, and to reaffirm their commitment to further cooperate closely on multilateral issues between the two countries.

  South Africa and Tanzania enjoy strong fraternal, historical as well as excellent political, economic and social relations which were cemented during the period of the liberation struggle. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akizungumza jambo na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mh. Cyril Ramaphosa,mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam leo.Rais Ramaphosa amewasili hapa nchini jana jioni kwa Ziara ya Kitaifa ya siku 3 na baada ya hapo atahudhuria Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaofanyika Jijini Dar es Salaam. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwakaribisha wageni wao Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mh. Cyril Ramaphosa na mkewe Dkt. Dk Tshepo Motsepe, Ikulu Jijini Dar es Salaam leo. Rais Ramaphosa amewasili hapa nchini jana jioni kwa Ziara ya Kitaifa ya siku 3 na baada ya hapo atahudhuria Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaofanyika Jijini Dar es Salaam. 
  Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mh. Cyril Ramaphosa na mkewe Dkt. Tshepo Motsepe wakikabidhiwa maua ikiwa ni ishara ya upendo ya kuwakaribisha nchini,mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar na kupokewa na Rais Dkt John Pome Magufuli .
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama pamoja na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mh. Cyril Ramaphosa wakati nyimbo za Mataifa hayo mawili zikipigwa katika hafla fupi ya mapokezi kwenye viunga vya Ikulu leo jijini Dar.
  Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mh. Cyril Ramaphosa akikagua gwaride la heshima mara baada ya kuwasili katika viunga vya Ikulu,leo jijini Dar .

  0 0  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akimkabidhi tuzo Mkuu wa mauzo wa kanda ya Kaskazini wa Vodacom Tanzania, Brigita Stephen baada ya kampuni hiyo kuibuka mshindi wa kampuni bora upande wa mawasiliano kanda ya kaskazini katika maonyesho ya Nane Nane yaliyofanyika jijini Arusha, hivi karibuni, kushoto kwa Ulega ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (mwenye kofia). Kampuni ya Vodacom Tanzania inaendelea kuboresha huduma zake kuwa za kidijitali ili kuwawezesha Watanzania kwenda sambamba na maendeleo ya ulimwengu.
  Mtaalamu wa mauzo wa Vodacom Tanzania Mandela Seth, akiwapa maelezo ya kutumia kifaa cha intaneti (modem) wateja waliotembelea banda la Vodacom katika viwanja vya nane nane Nyakabindi mkoani Simiyu hapo jana. katika maonyesho ya nane nane mwaka huu kampuni ya Vodacom imewandalia wateja wao huduma za kidigatili ikiwemo vifaa mbali mbali vya intaneti na simu.
  Wakazi wa Bariadi mkoani Simiyu wakipatiwa huduma mbalimbali kwenye banda la Vodacom katika viwanja vya nane nane Nyakabindi mkoani Simiyu hapo jana. katika maonyesho ya nane nane mwaka huu kampuni ya Vodacom imewandalia wateja wao huduma za kidigatili ikiwemo vifaa mbali mbali vya intaneti na simu.

  0 0

  Kamishina wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa nchini Tanzania,Mhe. Balozi Omari Ramadhani Mapuri amefungua mkutano wa wa Tume na Wadau wa Uchaguzi katika mkoa wa Shinyanga kwa lengo la kupeana taarifa kuhusu uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura.

  Mkutano huo umefanyika leo Alhamis Agosti 15,2019 katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga na kuhudhuriwa na mkurugenzi wa uchaguzi,mratibu wa uandikishaji wa mkoa,viongozi wa dini,vyama vya siasa,wawakilishi wa watu wenye ulemavu,vijana,wanawake,asasi za kiraia,watendaji wa tume na waandishi wa habari.

  Balozi Mapuri alisema lengo la mkutano huo ni kupeana taarifa kuhusu uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura ulioanza kwa awamu ya kwanza tarehe 18 Julai,2019 katika mikoa ya Kilimanjaro na Arusha.

  Alisema uzinduzi rasmi wa zoezi la uboreshaji wa daftari la wapiga kura ulifanyika Mjini Moshi Julai 18 ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa na kwamba katika mkoa wa Shinyanga uboreshaji wa daftari la wapiga kura utafanyika Agosti 26 hadi Septemba 1,2019.

  "Lengo la kukutana nanyi leo ni kuwafahamisha kuwa tume imekamilisha maandalizi ya zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura,ikiwemo uhakiki wa vituo vya kujiandikisha,uandikishaji wa majaribio,maandalizi ya vifaa vya uboreshaji wa daftari,maandalizi ya vifaa vya uboreshaji na mkakati wa elimu ya mpiga kura naamini mafanikio ya zoezi hili yanategemea nyinyi wadau",alieleza.

  "Tume inatarajia kuanza uboreshaji wa daftari la wapiga kura kwa awamu ya nne katika mikoa ya Mwanza (halmashauri ya wilaya Kwimba),mkoa wa Shinyanga na mkoani Geita (Halmashauri ya Mji wa Geita,Nyang'wale,Bukombe na Mbogwe) kuanzia Agosti 26 hadi Septemba 1,2019",aliongeza.

  Alifafanua kuwa uboreshaji wa daftari la wapiga kura unafanyika kwa kutumia teknolojia ya kielektroniki ya Biometriki (BVR) ambayo huchukua taarifa za kibaiolojia za mtu na kuzihifadhi katika Kanzidata(Database) kwa ajili ya utambuzi.

  "Uboreshaji wa daftari la wapiga kura wa safari hii hautahusisha wapiga kura walioandikishwa kwenye daftari la kudumu la wapiga kura mwaka 2015 ambao kadi zao hazihitaji marekebisho yoyote ya taarifa.Uboreshaji huu utawahusu wapiga kura wapya ambao wametimiza umri wa miaka 18 na wale ambao watatimiza umri wa miaka 18 siku ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.",alisema Balozi Mapuri.

  Alisema uboreshaji huo pia utahusisha watu ambao wamehama kutoka maeneo yao ya awali na kuhamia maeneo mengine ya uchaguzi na wale ambao kadi zao zimeharibika au kupotea na wale ambao wanatakiwa kufutwa kwenye daftari baada ya kupoteza sifa wakiwemo waliofariki dunia.

  Kwa upande wake, Afisa Tehama Mwandamizi kutoka Tume ya Uchaguzi ya Taifa, Frank Mhando aliwataka watu wenye sifa ya kujiandikisha wajitokeze kwa wingi ili waandikishwe na wanaohitaji kuboresha taarifa zao wakati ndiyo huu.

  Alisema kila chama cha siasa kina wajibu wa kuweka wakala kwenye kituo cha uandikishaji daftari la wapiga kura huku akikisisitiza kuwa wakala hapaswi kuingilia majukumu ya tume ya uchaguzi na kwamba yeyote atakayeleta masuala ya siasa kwenye vituo atachukulia hatua.

  Aliwataka wanasiasa kuepuka kufanya siasa kwenye vituo bali majukumu yao yawe ni kuwatambua wenye sifa ya kujiandikisha wapate sifa ya kupiga kura wakati wa uchaguzi.

  "Hakuna uchaguzi bila wapiga kura,hakuna kupiga kura bila kujiandikisha,niwaombe wanasiasa mhamasishe watu wajitokeze kwenda kujiandikisha ili wawe na sifa ya kupiga kura",aliongeza.
  Kamishina wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa nchini Tanzania,Mhe. Balozi Omari Ramadhani Mapuri akifungua mkutano wa Tume na Wadau wa Uchaguzi katika mkoa wa Shinyanga kwa lengo la kupeana taarifa kuhusu uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura leo katika ukumbi wa halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
  Kamishina wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa nchini Tanzania,Mhe. Balozi Omari Ramadhani Mapuri akifungua mkutano wa Tume na Wadau wa Uchaguzi katika mkoa wa Shinyanga.
  Afisa Tehama Mwandamizi kutoka Tume ya Uchaguzi ya Taifa, Frank Mhando akiwataka watu wenye sifa ya kujiandikisha wajitokeze kwa wingi ili waandikishwe kwenye daftari la wapiga kura.
  Katibu Mwenezi wa CHADEMA wilaya ya Shinyanga Mjini,Charles Shigino akiiomba Tume ya uchaguzi kuruhusu mikutano ya hadhara ili wanasiasa waelimishe/wahamasishe wananchi kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura.
  Katibu wa Chama cha ACT-Wazalendo mkoa wa Shinyanga Sebastian Tafuta akichangia hoja wakati wa mkutano huo. 
  Wadau wa uchaguzi wakiwa ukumbini.
  Wadau wa uchaguzi wakiwa ukumbini.

  0 0


  Mkurugenzi wa Tigo, Nyanda za juu Kusini, Henry Kinabo(katikati), akikaribishwa katika chumba cha kufundishia kompyuta katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) na Rasi Kampasi ya Rukwa, Dkt. Duncan Mwakipesile(Kushoto) baada ya makabidhiano ya komputa 20 zenye thamani ya 48m/- zilizotolewa na Tigo kwaajili ya kuchangia katika masomo ya TEHAMA katika chuo hicho mkoani Mbeya.
  Mkurugenzi wa Tigo, Nyanda za juu Kusini, Henry Kinabo(katikati) akimkabidhi Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST), Profesa Aloys Mvuma, moja ya kompyuta 20 zenye thamani ya 48m/- zilizotolewa na Tigo kwaajili ya kuchangia katika masomo ya TEHAMA katika chuo hicho mkoani Mbeya.Pembeni yao ni Naibu wa makamu mkuu wa chuo Taaluma, Ushauri na Utafiti, Profesa Godliving Mtui.
  Wafanyakazi wa Tigo, kutoka Nyanda za juu Kusini, wakiwa katika ya pamoja na wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST baada ya makabidhiano ya kompyuta 20 katika chuo hicho zenye thamani ya 48m/- zilizotolewa na Tigo kwaajili ya kuchangia katika masomo ya TEHAMA katika chuo hicho mkoani Mbeya.

  Katika juhudi za kuchangia malengo ya Serikali ya kuboresha na kuinua viwango vya elimu katika taasisi za elimu ya juu, kampuni inayoongoza katika maisha ya kidigitali nchini Tanzania, Tigo, leo wamekabidhi kompyuta za mezani 20, zitakazo wanufaisha wanafunzi 4,630 katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya(MUST).

  Alipokuwa anakabidhi kompyuta hizo katika chuo hicho, Mkurugenzi wa Tigo, Nyanda za juu Kusini, Henry Kinabo alisema: “Tunaamini ya kwamba kompyuta tunazozitoa hapa leo, zitachangia sehemu kubwa katika kubadilisha jinsi wanafunzi wanavyosoma na pia zitaleta nafasi kwao kubuni teknolojia mpya na kuchangia katika ukuaji wa uchumi nchini Tanzania. Tigo ipo mstari wa mbele kwaajili ya kuboresha viwango vya elimu katika vyuo vikuu kwa kuleta nyenzo za kusomea na kuwasaidia wanafunzi na walimu kukuza vipengee muhimu vinavyohitajika katika karne hii ya 21.”

  Aliendelea kuelezea zaidi kwamba kupitia mchango huo, Tigo imeunga mkono juhudi za Serikali ya Tanzania katika mtazamo wake wa kubadilisha nchi kuwa ya viwanda na uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 ambapo TEHAMA ndio chachu ya maendelea hayo.

  Mnamo mwaka 2017, Tigo ilichangia kompyuta 47 katika Chuo kikuu cha Dodoma, zilizo wanufaisha wanafunzi takriban 36,150. Mpaka leo jumla ya wanafunzi 40,780 katika vyuo vikuu nchini wamenufaika na msaada wa kompyuta kutoka Tigo kwa kipindi cha miaka miwili sasa.

  Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia(MUST), Profesa Aloys Mvuma, aliipongeza kwa mchango wao kwa kusema, “Ni kupitia ushirikiano huu ndio tutaweza kutoa stadi za kisasa za TEHAMA za kisasa pamoja na maarifa kwa kizazi kijacho cha wataalam, ili nchi iweze kukidhi mahitaji ya taarifa zinazobadilika mara kwa mara na mitindo ya kidigitali katika jamii na uchumi wa dunia.”

  Rasi wa ndaki ya Sayansi na Elimu za Ufundi, Dkt. John.P.John, aliwashukuru Tigo kwa usaidizi wao mkubwa sana na alisema kompyuta hizo zitasaidia kuboresha kiwango cha elimu mkoani Mbeya. “Tunawashukuru Tigo kwa kusaidia juhudi za serikali kwa kutoa mchango wa vifaa vya kufundishia masomo ya TEHAMA katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia(MUST). Tunaamini ya kwamba hizi kompyuta zitaboresha jinsi wanafunzi wanavyosoma na pia itaongeza ueledi katika elimu ya kidigitali hapa Chuoni.”

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akihotubia mbele ya mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Cyril Ramaphosa katika mkutano baina ya Wafanyabiashara wa Tanzania na Ujumbe wa Wafanyabiashara toka Afrika kusini uliofanyika katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Cyril Ramaphosa akihotubia mbele ya mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano baina ya Wafanyabiashara wa Tanzania na Ujumbe wa Wafanyabiashara toka Afrika kusini uliofanyika katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Cyril Ramaphosa na Mawaziri wa Serikali ya Tanzania na Afrika kusini mara baada ya kumalizika kwa mkutano baina ya Wafanyabiashara wa Tanzania na Ujumbe wa Wafanyabiashara toka Afrika kusini uliofanyika katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Cyril Ramaphosa wakisalimiana mwenyekiti wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere Mzee Joseph Butiku mara baada ya kumalizika kwa mkutano baina ya Wafanyabiashara wa Tanzania na Ujumbe wa Wafanyabiashara toka Afrika kusini uliofanyika katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam. . PICHA NA IKULU
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimpongeza Rais wa Afrika kusini, Cyril Ramaphosa mara baada kukamilisha kusoma hotuba yake katika kongamano la biashara la Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) lililofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo.Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv.
   
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza wakati wa kikao cha wafanyabiashara na wawekezaji wa Tanzania na Afrika Kusini leo Agosti 15, 2019 jijini Dar es Salaam. Ambapo Mkutano huo umeudhuriwa na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ambaye yupo nchini kwa ziara ya Siku mbili huku akisubiri kuhudhuria mkutano wa 39 wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) unaotarajia kufanyika Agosti 17 na 18, 2019.
  Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa (wa tatu kutoka kushoto) akipiga makofi. 
  Wageni waliofika katika mkutano wa wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Tanzania na Afrika Kusini.
  Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa akihutubia katika wakati wa kikao cha wafanyabiashara na wawekezaji wa Tanzania na Afrika Kusini leo Agosti 15, 2019 jijini Dar es Salaam. Ambapo Mkutano huo umeudhuriwa na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ambaye yupo nchini kwa ziara ya Siku mbili huku akisubiri kuhudhuria mkutano wa 39 wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) unaotarajia kufanyika Agosti 17 na 18, 2019.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mkono na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi mara baada ya kumaliza kuhutubia kikao cha wafanyabiashara na wawekezaji wa Tanzania na Afrika Kusini leo Agosti 15, 2019 jijini Dar es Salaam.
  Wageni waliofika katika mkutano wa wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Tanzania na Afrika Kusini.

  0 0


  NMB MOVES TO PROVIDE LACTACTING MOTHERS A NURSING & FIRST AID ROOM


  NMB Bank has established a lactation room that will provide space for nursing mothers working with the Bank to breast feed their babies.

  The room will among other things help working moms at the bank pump and preserve breast milk for their babies during working hours. 

  The move, according to the NMB management, is to help mothers to transition well after maternity leave. 

  Speaking during the launching ceremony of the nursing room at NMB headquarters in Dar es Salaam, the Chairperson of NMB Women Arise Network and the bank’s head of Trade Finance Ms Linda Tegisa, said the establishment of the room is an initiative set by the bank to support women in carrying up their roles at the workplace and nursing their babies. 

  We are very grateful to the management of the bank for setting up the initiative to support women especially those with babies; she said adding that the move expresses strong commitment by the employer to support women in nursing their babies without missing at the workplace. 

  Ms Tegisa urged other financial institutions and others to establish nursing rooms and help the working mothers express breast milk for their babies in order to avoid unnecessary misunderstandings that may arise between the working moms and their employer. 

  Many working mothers face many challenges when it comes to balancing breastfeeding with tackling their job requirements; having a nursing room at the workplace is an important initiative to break the challenges; she said. 

  On the other hand, the Head of Innovation of the Bank Ms Josina Njambi, said the launched nursing rooms contain all important facilities to enable moms at the bank meet and breastfeed their babies, pump and preserve milk. 

  The rooms contains comfortable chairs that allow working mothers to sit up straight to pump milk, a refrigerator for storing breast milk and a sink to rinse out parts with soaps and towel among other necessities.
   Wafanyakazi wa NMB wakizundua chumba za huduma ya kwanza kwa wajawazito na wanaonyonyesha. 
   Afisa Mkuu wa wateja wadogo na wa kati wa benki ya NMB, Filbert Mponzi  na Meneja biashara, Abamwesiga Beneth  wakiwa chumba cha mapumziko kwa wagonjwa baada ya benki ya NMB kuzindua huduma ya kwanza.  0 0

  Rais wa Afrika Kusini, Cyril Matamela Ramaphosa, akiangalia moja ya kaburi la Wapigania Uhuru wa Afrika Kusini, katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), Mazimbu Campus mjini Morogoro. Agosti 16.2019.
  Rais wa Afrika Kusini, Cyril Matamela Ramaphosa, akiwa na mwenyeji wake, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, wakiangalia makaburi ya Wapigania Uhuru wa Afrika Kusini, katika kambi ya Mazimbu mjini Morogoro. Agosti 16.201
  Rais wa Afrika Kusini, Cyril Matamela Ramaphosa, akipanda mti, wakati alipotembelea Kambi ya iliyotumika na Wapigania Uhuru wa Afrika Kusini, iliyopo Mazimbu mjini Morogoro. Agosti 16.2019
  Rais wa Afrika Kusini, Cyril Matamela Ramaphosa, akiweka shada la mauwa, katika mnara wa kumbukumbu ya Wapigania Uhuru wa Afrika Kusini, wakati alipotembelea Kambi ya iliyotumika na Wapigania Uhuru hao, iliyopo Mazimbu mjini Morogoro. Agosti 16.2019.
  Rais wa Afrika Kusini, Cyril Matamela Ramaphosa, akiwa na mwenyeji wake, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, baada ya kutembelea Kambi ya Mazimbu, mkoani Morogoro, akiwa kwenye ziara ya Kiserikali nchini. Agosti 16.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).. Agosti 16.2019.
  Rais wa Afrika Kusini, Cyril Matamela Ramaphosa, akizungumza na wananchi katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), Mazimbu Campus mjini Morogoro,alipotembelea Kampasi hiyo. Agosti 16.2019.
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na wananchi katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), Mazimbu Campus mjini Morogoro, kabla ya kumkaribishaRais wa Afrika Kusini, Cyril Matamela Ramaphosa kuzungumza. Agosti 16.2019.
  Rais wa Afrika Kusini, Cyril Matamela Ramaphosa, akiwa amesimama katika moja ya picha ya wapigania uhuru wa Afrika Kusini, kwenye Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), Mazimbu Campus mjini Morogoro. Agosti 16.2019.
  Rais wa Afrika Kusini, Cyril Matamela Ramaphosa, akizungumza na mwenyeji wake Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, wakati akiwasili katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), Mazimbu Campus mjini Morogoro. Agosti 16.2019.
  Rais wa Afrika Kusini, Cyril Matamela Ramaphosa, akiwa kwenye picha ya pamoja, kwenye ofisi ya Utawala, iliyotumika na Wapigania Uhuru wa Afrika Kusini, katikaChuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), Mazimbu Campus mjini Morogoro. Agosti 16.2019.
  Rais wa Afrika Kusini, Cyril Matamela Ramaphosa, akiangalia moja ya kaburi la Wapigania Uhuru wa Afrika Kusini, katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), Mazimbu Campus mjini Morogoro. Agosti 16.2019.
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Rais wa Afrika Kusini, Cyril Matamela Ramaphosa, wakati alipowasili katika Mkoa wa Morogoro, akiwa kwenye ziara ya Kiserikali nchini. Agosti 16.2019.

  0 0
  · Innovation and technology contributed to the award


   NMB Bank PLC has for the 7th consecutive year scooped the Best Bank in Tanzania 2019 award by Euromoney Magazine outshining over 40 other banks operating in Tanzania. This is a top award issued by the leading global financial markets magazine based in London.

  NMB Bank being one of the key players in financial inclusion in the country, has consistently strived to provide innovative financial solutions to Tanzania’s banked and unbanked. Supporting the nation’s financial inclusion agenda, NMB Bank has pioneered revolutionary products and services, maximizing on technology to enhance customer experience through the bank’s branches, NMB Wakala network and digital platforms such as NMB Mastercard, NMB Mobile, NMB KLiK and Internet Banking.

  This award reflects the progress NMB Bank has made in delivering a banking experience that captures what customers need today and tomorrow, making it the best for financial inclusion.

  NMB’s Interim Managing Director Jonkergouw said in a statement: “We are today the bank that works, rather than one which exists. Tough decisions around capital, businesses and people have been made. Throughout that process, we have continued to deliver strong financials and pay industry-leading dividends to shareholders.”

  He added: “We are leveraging on the best of technology in digital banking, innovative products and our extensive branch network and Wakalas add real value to our customers’ lives.

  Winning the Best Bank in Tanzania award is a clear indication that our efforts are recognized not only in Tanzania but across the region. We acknowledge the dedication of our staff, and thank our valued customers for being part of this digital journey.”

  The Euromoney Award confirms the bank’s investment in digital transformation and technology has further strengthened its ability to deliver innovative solutions to the market.

  Describing the selection criteria and reliability of the results, Euromoney’s editor explained: “We have received almost 1000 submissions from banks in our awards programme which covers 20 global awards, more than 50 regional awards, and best bank awards in close to 100 countries. This year our most successful banks have clearly defined what their core strengths are, and built their businesses around them."

  This year’s Euromoney Awards for Excellence 2019, doubles Euromoney’s 50th anniversary as the most prestigious awards in the global banking industry, welcoming over 500 senior bankers around the world at the Tower of London recently where banks based in developing markets made a greater impact in the awards than ever before highlighted with NMB Bank being named the Best Bank in Tanzania.

  0 0

  Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Majaliwa Khasim Majaliwa na Mke wa Rais wa Afrika Kusni Dkt. Tshepo Motsepe-Ramaphosa wakipatiwa maelezo mbali mbali wakati wakitembelea makaburi ya wapiganaji wa ANC walikuwa wakikaa na kupatiwa mafunzo na serikali ya Tanzania. Ziara ya Ramaphosa inakuja siku chache kabla ya Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa SADC utakaofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Picha zote na Team Matokeo Chanya+.
  Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa akipanda mti wa kumbukumbu wakati alipotembelea makaburi ya wapiganaji wa ANC walikuwa wakikaa na kupatiwa mafunzo na serikali ya Tanzania.
  Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa na mkewe Dkt. Tshepo Motsepe-Ramaphosa akiweka shada la maua mara baada ya kutembelea makaburi ya wapiganaji wa ANC walikuwa wakikaa na kupatiwa mafunzo na serikali ya Tanzania.
  Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa  akizungumza machache mara baada ya kutembea makaburi ya wapiganaji wa ANC walikuwa wakikaa na kupatiwa mafunzo na serikali ya Tanzania.
  Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa akihutubia mara baada ya kutembelea kambi ya Mazimbu mjini Morogoro mapema leo Agosti 16, 2019 ambapo wapiganaji wa ANC walikuwa wakikaa na kupatiwa mafunzo na serikali ya Tanzania.  Ziara ya Ramaphosa inakuja siku chache kabla ya Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa SADC utakaofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Picha zote na Team Matokeo Chanya+.
  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Majaliwa Khasim Majaliwa akizungumza wakati wa hafla ya kumkaribisha Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa mara baada ya kutembelea kambi ya Mazimbu mjini Morogoro mapema leo Agosti 16, 2019 ambapo wapiganaji wa ANC walikuwa wakikaa na kupatiwa mafunzo na serikali ya Tanzania.  Ziara ya Ramaphosa inakuja siku chache kabla ya Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa SADC utakaofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Palamagamba Kabudi akizungumza wakati wa hafla ya kumkaribisha Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa mara baada ya kutembelea kambi ya Mazimbu mjini Morogoro mapema leo Agosti 16, 2019 ambapo wapiganaji wa ANC walikuwa wakikaa na kupatiwa mafunzo na serikali ya Tanzania.  Ziara ya Ramaphosa inakuja siku chache kabla ya Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa SADC utakaofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
  Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa (kulia) na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Palamagamba Kabudi (kushoto) wakimsikiliza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Majaliwa Khasim Majaliwa (hayupo pichani) akihutubia hafla ya kumkaribisha Rais Ramaphosa kutembelea kambi ya Mazimbu mjini Morogoro mapema leo Agosti 16, 2019 ambapo wapiganaji wa ANC walikuwa wakikaa na kupatiwa mafunzo na serikali ya Tanzania.
  Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa (kulia) na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Palamagamba Kabudi (kushoto) pamoja na Waziri wa Utalii wa Afrika Kusini Mmamoloko Kubayi-Ngubane wakimsikiliza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Majaliwa Khasim Majaliwa (hayupo pichani) akihutubia hafla ya kumkaribisha Rais Ramaphosa kutembelea kambi ya Mazimbu mjini Morogoro mapema leo Agosti 16, 2019 ambapo wapiganaji wa ANC walikuwa wakikaa na kupatiwa mafunzo na serikali ya Tanzania.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (kushoto) wakimsikiliza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Majaliwa Khasim Majaliwa (hayupo pichani) akihutubia hafla ya kumkaribisha Rais Ramaphosa kutembelea kambi ya Mazimbu mjini Morogoro mapema leo Agosti 16, 2019 ambapo wapiganaji wa ANC walikuwa wakikaa na kupatiwa mafunzo na serikali ya Tanzania.
  Wageni waalikwa wakifuatilia hotuba za viongozi.
  Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa akipatiwa zawadi ya picha na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Majaliwa Khasim Majaliwa mara baada ya kutembelea kambi ya Mazimbu mjini Morogoro mapema leo Agosti 16, 2019 ambapo wapiganaji wa ANC walikuwa wakikaa na kupatiwa mafunzo na serikali ya Tanzania.
  Wageni waalikwa.
  Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa na mkewe Dkt. Tshepo Motsepe-Ramaphosa wakipatiwa maelezo mbali mbali wakati wakitembelea makaburi ya wapiganaji wa ANC walikuwa wakikaa na kupatiwa mafunzo na serikali ya Tanzania.
  Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa na mkewe Dkt. Tshepo Motsepe-Ramaphosa wakipatiwa maelezo mbali mbali wakati wakitembelea makaburi ya wapiganaji wa ANC walikuwa wakikaa na kupatiwa mafunzo na serikali ya Tanzania.

  0 0


  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas D. Ndumbaro (Mb.) kuhudhuria Ufunguzi wa Mkutano wa SADC, unaotarajiwa kufanyika kesho katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijinin Dar es Salaam.
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Issa Haji Gavu, alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jiji Dar es Salaam, kuhudhuria Ufunguzi wa Mkutano wa SADC unaotarajiwa kufanyika kesho katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, kulia Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt.Damas D. Ndumbaro, na kushoto Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, wakielekea katika chumba cha mapumziko Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.(Picha na Ikulu)

  0 0  Rosemary Mroso kutoka kitengo cha huduma kwa wateja Kampuni ya simu za mkononi Tigo Tanzania akimhudumia mteja wa kampuni hiyo Emmanuel Liwimbi Ofisa Huduma za Mikutano Mwandamizi kutoka Sekretarieti ya SADC alipotembelea banda hilo kwenye mkutano wa SADC unaoendelea katika ukumbi wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam. Tigo ni mdhamini wa huduma za intaneti katika Mkutano huo.  Mfanyakazi wa Tigo akitoa huduma ya kusajili kwa alama za vidole kwa wateja waliofika katika banda lake lililopo ndani ya Ukumbi wa JNICC jijini Dar es Salaam ambapo Mkutano Mkuu wa 39 wa marais wa Jumuiya ya Maendeleo kwa Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) unafanyika. Tigo ni mdhamini mkuu wa Huduma ya inteneti katika mkutano huo.
  Mtaalam wa Mifumo ya Mtandao Kampuni ya Tigo Bw. Kundasen Simon akiwasikiliza wateja wa kampuni hiyo waliotembelea banda la kampuni ya Tigo lililopo kwenye ukumbi wa mikutano wa Julius Nyerere JNICC jijini Dar es salaam ambako Mkutano wa Wakuu wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaoendelea , Tigo ni miongoni mwa wadhamini wa intaneti ya bure katika mkutano huo.
  Mtaalam wa Mifumo ya Mtandao Kampuni ya Tigo Bw. Kundasen Simon akiwasikiliza wateja wa kampuni hiyo waliotembelea banda la kampuni ya Tigo lililopo kwenye ukumbi wa mikutano wa Julius Nyerere JNICC jijini Dar es salaam ambako Mkutano wa Wakuu wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaoendelea , Tigo ni miongoni mwa wadhamini wa intaneti ya bure katika mkutano huo.

  Mtaalam wa Mifumo ya Mtandao Kampuni ya Tigo Bw. Kundasen Simon akimsikiliza mteja wa kampuni hiyo Bw. Selemani Kifyoga aliyefika kwenye banda hilo kwa ajili ya kusajili laini yake ya simu kwa mfumo wa kutumia vidole. Tigo ni miongoni mwa wadhamini katika mkutano unaondelea wa SADC
  Mtaalam wa Mifumo ya Mtandao Kampuni ya Tigo Bw. Kundasen Simon akiwasikiliza wateja wa kampuni hiyo waliotembelea banda la kampuni ya Tigo lililopo kwenye ukumbi wa mikutano wa Julius Nyerere JNICC jijini Dar es salaam ambako Mkutano wa Wakuu wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaoendelea , Tigo ni miongoni mwa wadhamini wa intaneti ya bure katika mkutano huo.

  Mfanyakazi wa Tigo akitoa huduma kwa wateja waliofika katika banda lake lililopo ndani ya Ukumbi wa JNICC jijini Dar es Salaam ambapo Mkutano Mkuu wa 39 wa marais wa Jumuiya ya Maendeleo kwa Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) unafanyika. Tigo ni mdhamini mkuu wa Huduma ya intaneti katika mkutano huo.

  0 0

  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifunga rasmi mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere leo Jumapili Agosti 18, 2019 
  Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein na viongozi wengine wakimpigia makofi Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati akifunga rasmi mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere leo Jumapili Agosti 18, 2019 
  Katibu Mtendaji wa SADC Dkt. Stergomena Tax akitoa majumuisho kabla ya kufungwa rasmi kwa mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere leo Jumapili Agosti 18, 2019
  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Katibu Mtendaji wa SADC Dkt. Stergomena Tax kwa maandalizi mazuri baada ya kufunga mkutano huo wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere leo Jumapili Agosti 18, 2019 
  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Angola Mhe Joao Manuel Goncalves Lourenco baada ya kufunga rasmi mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere leo Jumapili Agosti 18, 2019 
  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Namibia Dkt. Hage Geingob na Rais wa Afrika Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa baada ya kufunga rasmi mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere leo Jumapili Agosti 18, 2019 
  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsidikiza Rais wa Andry Nirina Rajoelina baada ya kufunga rasmi mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere leo Jumapili Agosti 18, 2019 
  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Comorro Mhe Azali Assoumani na mkewe Mama Assoumani baada ya kufunga rasmi mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere leo Jumapili Agosti 18, 2019 
  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Waziri Mkuu wa Lesotho Mhe. Tom Thabane baada ya kufunga rasmi mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere leo Jumapili Agosti 18, 2019 
  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Rais wa Ushelisheli Mhe. Danny Faure baada ya kufunga rasmi mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere leo Jumapili Agosti 18, 2019 
  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika naRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpatia zawadi Rais wa Ushelisheli Mhe. Danny Faure walipomaliza mazungumzo yao baada ya kufunga rasmi mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere leo Jumapili Agosti 18, 2019

  0 0

  Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza na Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Magharibi Idrissa Kayera (Kulia) na Msajili wa Hati wa Kanda hiyo Julian Ngonyani (katikati) alipotembelea Ofisi ya Ardhi ya Kanda ya Magharibi akiwa katika ziara yake mkoani Tabora mwishoni mwa wiki. Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiwasili Ofisi ya Msajili wa Hati Kanda ya Magharibi zilizopo mkoani Tabora wakati wa ziara yake mkoani humo mwishoni mwa wiki. Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi akiangalia baadhi ya Hati za Ardhi zilizopo Ofisi ya Msajili wa Hati Kanda ya Magharibi wakati wa ziara yake mkoani Tabora mwishoni mwa wiki. Kulia ni Msajili wa Hati Kanda ya Magharibi Julian Ngonyani. Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akikabidhi Hati ya Kiwanja cha Chama cha Mapinduzi wilaya ya Tabora kilichopo eneo la Kanyenye Tabora kwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ora Mohamed Katete wakati wa ziara yake mkoani Tabora mwishoni mwa wiki. Kulia ni Katibu wa CCM mkoa wa Tabora Solomon Kasaba na kushoto ni Katibu wa Umoja wa Wanawake mkoa wa Tabora Rehema Mohamed. Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza baada ya kukabidhi Hati ya Kiwanja kwa Chama cha Mapinduzi wilaya Tabora mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Katibu wa UWT mkoa wa Tabora Rehema Mohamed na wa pili kulia ni Katibu wa CCM mkoa wa Tabora Solomon Kasaba (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)   ………………… 

  Na Munir Shemweta, WANMM TABORA 

  Idadi kubwa ya Hati za Ardhi takriban12,000 katika Ofisi ya Msajili wa Hati imemshtua Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula alipofanya ziara Ofisi ya Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Magharibi. 

  Mwishoni mwa wiki Dkt Mabula akiwa katika ziara yake ya kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi sambamba na kukagua masijala ya ardhi katika halmashauri za mkoa wa Tabora alitembelea Ofisi ya Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Magharibi kujionea utendaji kazi wa kanda inayojumuisha mikoa ya Tabora, Katavi na Kigoma. 

  Akiwa Ofisi ya Msajili wa Hati, Dkt Mabula alielezwa na Msajili wa Hati wa Kanda ya Magharibi Julian Ngonyani kuwa ofisi yake ina takriban hati 12,000 ambazo ziko tayari kwa ajili ya kukabidhiwa kwa waombaji lakini wahusika hawajajitokeza kuchukua kwa sababu ambazo hazijulikani. 

  Naibu Waziri Dkt Mabula alishangazwa na idadi kubwa ya Hati hizo na kubainisha kuwa Hati zilizopo Ofisi ya Msajili wa Hati kama zingechukuliwa basi wahusika wangekuwa na nyaraka zinazoonesha umiliki halali wa maeneo yao sambamba na hati hizo kuwasaidia katika shughuli za maendeleo kama vile kukopa pesa katika mabenki mbalimbali. 

  Alisema, Halmashauri katika mikoa ya Kanda hiyo ya Magharibi zinapaswa kuwajibika kwa kuhakikisha waombaji wanapata hati ambapo alizitaka kuandaa utaratibu maalum utakaowezesha Hati kupelekwa kwenye halmashauri husika na waombaji kuzichukua. 

  Kwa mujibu wa Dkt Mabula, utaratibu huo utawawezesha wananchi kuchukua hati zao kwa urahisi bila ya usumbufu ambapo hivi sasa waombaji hulazimika kuzifuata Ofisi ya Kamishna wa Kanda jambo alilolieleza kuwa ni usumbufu kwani baadhi ya waombaji hulazimika kutembea umbali mrefu hasa kwa wale wanaokaa maeneo yaliyo mbali na Ofisi ya Kanda. 

  ‘’Halmashauri inaweza ikandaa utaratibu wa kupelekewa Hati za Ardhi katika maeneo yao na Ofisi ya Kamishna wa Kanda na jukumu la halmashauri litakuwa kugharamia pesa ya kujikimu kwa watumishi wa Kanda watakaopeleka hati na kuzikabidhi kwa waombaji, hiyo itasaidia kuwapunguzia mzigo wananchi’’ alisema Dkt Mabula. 

  Katika Hatua Nyingine, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameikabidhi Hati ya Kiwanja No 47 Block A Chama cha Mapinduzi wilaya ya Tabora kilichopo eneo la Kanyenye Manispaa ya Tabora mkoni Tabora baada ya kiwanja hicho kuwa na mgogoro wa muda mrefu Kati ya ofisi ya CCM na Shirika la Utangazaji (TBC). 

  Dkt Mabula alimkabidhi hati hiyo Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Tabora Mohamed Katete ambapo makabidhiano hayo yalishuhudiwa na Katibu wa CCM mkoa wa Tabora Solomon Kasaba, Katibu UWT mkoa Rehema Mohamed, Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Magharbi Idrissa Kayera na Msajili wa Hati wa Kanda Julian Ngonyani. 

  Katika Makabidhiano hayo, Dkt Mabula alisema Chama cha Mapinduzi kina maeneo mengi inayomiliki lakini siyo yote yenye hati na kubainisha kuwa kukabidhiwa hati hiyo iwe chachu kwa chama kuhakikisha maeneo yake yote yanakuwa na hati kuepuka migogoro. 

  Ametoa wito kwa CCM kuhakikisha maeneo ya Kata yanayomilikiwa na chama hicho yasiyopimwa yanapimwa na kupatiwa hati na hata yale yasiyo pimwa basi yawe na mipaka na kubainisha kuwa kwa kufanya hivyo kutaondoa migogoro na kukifanya chama kuwa na miliki halali ya maeneo yake.

  0 0

  KAMPUNI ya Mafuta ya Puma Tanzania imempongeza Rais Dk. John Magufuli kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), na lugha ya Kiswahili kukubalika kuwa lugha ya nne kwenye jumuiya hiyo.

  Pongezi hizo zimetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Puma Tanzania, Dominic Dhanah wakati wa hafla ya kufunga mkutano wa 39 wa SADC ulioshirikisha nchi 16 za jumuiya hiyo.Mkutano huo umefungwa leo na Mwenyekiti wa jumuiya hiyo Dk.Magufuli.

  Akizungumza baada ya kufungwa kwa mkutano huo, Dominic Dhanah amesema Tanzania ni moja ya nchi ambayo wanafanya vizuri katika soko la mafuta na vimiminika, hivyo kitendo cha Rais Magufuli kuwa mwenyekiti kitawaongezea nguvu ya kufanya kazi kwa upana mkubwa.

  “Puma Energy Tanzania tunampongeza Rais Magufuli kuwa Mwenyekiti wa SADC, lakini pia hili la Kiswahili kuwa lugha rasmi ya jumuiya hii ni la kupongezwa na kuungwa mkono kwani ni wazi Kiswahili kitasambaa kwa kasi,” alisema Dhanah.

  Amesema Kampuni ya Puma inafanya kazi kwenye nchi 13 wanachama wa SADC hivyo ni imani yao kuwa juhudi anazozionesha Rais Magufuli kujenga uchumi na maendeleo ya nchi zitasambaa kwa nchi nyingine.

  Ameongeza mikakati yao ni kuhakikisha kuwa wanafikia nchi nyingine zilizobaki ili kushika koso zima la kanda hiyo ya jumuiya ya SADC.

  Mkurugenzi huyo amesema katika kuonesha mchango wao kwa SADC walitoa shilingi milioni 300 kwa ajili ya kugharamia mkutano huo wa 39.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya mafuta ya Puma Energy Tanzania akizungumza na vyombo ya habari wakati akitoa pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).Pongezi hizo amezito baada ya Rais Dkt Magufuli kufunga mkutano wa Jumuiya hiyo Agosti 18,2019 uliofanyika katika kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere,jijini Dar es Salaam.

  0 0

    Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Dan Kazungu akiteta jambo na Mama Maria Nyerere wakati wa ziara ya kihistoria yaliyofanywa na  kikundi cha  Kenya Maendeleo ya Wanawake Organization (MYWO) ambacho kilianzishwa mwaka 1952 kwa ajili ya kuhamasisha umoja na maendeleo ya wanawake, nyumbani kwa Mama Maria Nyerere, jijini Dar es Salaam, hivi karibuni. Aliyeketi kulia ni mwanasiasa mkongwe kutoka kenya, Muthoni Likimani, na wa kwanza kushoto ni mwanasiasa mkongwe wa Tanzania na Rais wa kwanza wa Pan-African Parliament (2004-2009),Gertrude Mongella.  
   Mwenyekiti wa shirika la Maendeleo ya Wanawake (MYWO), Rahabu Mwikali, akimkabidhi zawadi ya picha Mama Maria Nyerere wakati wa ziara ya kihistoria yaliyofanywa na  kikundi cha  Kenya Maendeleo ya Wanawake Organization (MYWO) ambacho kilianzishwa mwaka 1952 kwa ajili ya kuhamasisha umoja na maendeleo ya wanawake, nyumbani kwa Mama Maria Nyerere, jijini Dar es Salaam, hivi karibuni.
   Mama Maria Nyerere (Katikati) akipeana mkono na mwanasiasa mkongwe kutoka kenya, Muthoni Likimani kama ishara ya kumshukuru kwa zawadi walizoleta kutoka Kenya, wakati wa ziara ya kihistoria yaliyofanywa na  kikundi cha  Kenya Maendeleo ya Wanawake Organization (MYWO) ambacho kilianzishwa mwaka 1952 kwa ajili ya kuhamasisha umoja na maendeleo ya wanawake, nyumbani kwa Mama Maria Nyerere, jijini Dar es Salaam, hivi karibuni. Wa kwanza kushoto ni mwanasiasa mkongwe wa Tanzania na Rais wa kwanza wa Pan-African Parliament (2004-2009),Gertrude Mongella.
  Mwanaharakati na Mpigania uhuru wa Kenya Muthoni Likimani (94) akiwa na Mama Maria Nyerere (kushoto) baada ya kumkabidhi zawadi ya kikoi wakati wa ziara ya kihistoria yaliyofanywa na  kikundi cha  Kenya Maendeleo ya Wanawake Organization (MYWO) ambacho kilianzishwa mwaka 1952 kwa ajili ya kuhamasisha umoja na maendeleo ya wanawake, nyumbani kwa Mama Maria Nyerere, jijini Dar es Salaam, hivi karibuni.
   Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu, akisalimiana na Mama Maria Nyerere wakati wa ziara ya kihistoria yaliyofanywa na  kikundi cha  Kenya Maendeleo ya Wanawake Organization (MYWO) ambacho kilianzishwa mwaka 1952 kwa ajili ya kuhamasisha umoja na maendeleo ya wanawake, nyumbani kwa Mama Maria Nyerere, jijini Dar es Salaam, hivi karibuni. Aliyeketi kulia ni mwanasiasa mkongwe kutoka kenya, Muthoni Likimani, na wa kwanza kushoto ni mwanasiasa mkongwe wa Tanzania na Rais wa kwanza wa Pan-African Parliament (2004-2009),Gertrude Mongella. 

  0 0  Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri la Jumuia ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushikiano wa Afrika ya Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi, akisajili laini yeke kwa kutumia alama za vidole katika banda la kampuni ya simu ya Tigo ambapo Tigo alikuwa mdhamini mkuu wa intaneti ya bure katika Mkutano wa 39 wa wakuu wa Nchi za SADC jijini Dar es Salaam.

  Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri la Jumuia ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushikiano wa Afrika ya Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi, akisajili laini yeke kwa kutumia alama za vidole katika banda la kampuni ya simu ya Tigo ambapo Tigo alikuwa mdhamini mkuu wa intaneti ya bure katika Mkutano wa 39 wa wakuu wa Nchi za SADC jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Waziri wa Madini Dotto Biteko akizungumza na wadau wa madini, wapili kulia ni Rais wa FEMATA, John Bina
  Ofisa habari na mawasiliano wa shirikisho la vyama vya wachimbaji madini nchini FEMATA, Dk Bernard Joseph akizungumza na wadau wa madini ya dhahabu eneo la Bassotu Wilayani Hanang’ Mkoani Manyara.
  Waziri wa Madini Dotto Biteko (katikati) akiwa na Rais wa FEMATA, John Bina (kushoto) na Kamishna wa Tume ya madini wa FEMATA, Haroun Kinega.

  ……………………..
  SHIRIKISHO la vyama vya wachimbaji madini nchini (FEMATA) wakiongozwa na Rais wao John Bina wanatarajia kufanya mkutano mkuu wa sita jijini Tanga. 

  Kwa mujibu wa afisa habari na mawasiliano wa FEMATA, Dkt Bernard Joseph mkutano huo mkuu wa sita unatarajia kufanyika Agosti 31 mwaka huu kwenye hotel ya kitalii ya Tanga Beach Resort jijini Tanga. 

  Dkt Joseph alisema mgeni rasmi siku ya ufunguzi wa mkutano huo anatarajiwa kuwa Waziri wa Madini, Dotto Mashaka Biteko. 

  Alisema mambo mbalimbali yenye manufaa ya wadau wa madini yatajadiliwa na kupitishwa kwenye mkutano huo ambapo washiriki wanapaswa kuwasiliana na wenyeviti wa vyama vya wachimbaji madini wa mikoa au Mtendaji Mkuu wa FEMATA. 

  Alisema FEMATA ni shirikisho la vyama vya wachimbaji madini nchini linalowaunganisha wachimbaji madini, wafanyabiashara na wadau wa madini na Serikali. 

  “FEMATA huendesha mafunzo ya elimu na ujuzi wa madini, biashara ya madini, changamoto na athari za mazingira kwa kushirikiana na wataalamu wa Wizara ya Madini,” alisema Dkt Joseph.

  Alisema FEMATA imeundwa na vyama vya mikoa vya madini na Wadau mbalimbali vikiwemo vyama vya wafanyabiashara na wadau wa Madini.

  Alisema FEMATA ni uwakilishi katika vyama vya mikoa vya madini (REMAs) kwenye masuala mbalimbali ya madini.

  Alisema FEMATA ni chombo cha utetezi wa wachimbaji madini katika kuongeza ufanisi na masilahi ya wachimbaji na haki zao.

  Alisema FEMATA ni 
  shirikisho linalowakilisha vyama vya kimkoa vya wachimba madini (REMAs) katika kuwaunganisha wachimbaji madini na wadau wa uchimbaji madini na Serikali pamoja na wadau mbalimbali wa kimaendeleo.

  Alisema dira na malengo ya FEMATA ni kutengeneza mazingira rafiki kwa wachimbaji madini, wadau na serikali ili kuleta ufanisi katika sekta ya madini na ukuzaji wa pato la taifa.

  “Sisi FEMATA dira yetu ni kuhakikisha nchi na wachimbaji madini wananufaika na madini yaliyopo,” alisema Dkt Joseph.

  Dkt Joseph alisema wanachama wao ni wachimbaji au wamiliki wa migodi kutoka katika mikoa yote nchini, wafanyabiashara na wadau mbalimbali na wanaotaka kujiunga wanapaswa kuwasiliana kupitia info@femata.co.tz

  Alisema faida za kujiunga na FEMATA,  zipo nyingi ikiwemo kupata mafunzo mbalimbali yanayohusu madini, biashara ya madini, utatuzi wa changamoto mbalimbali, uwakilishi na utetezi kwa wanachama katika maeneo ya madini. 

  Alisema FEMATA ni kiungo muhimu katika kuwaunganisha wachimbaji madini na serikali ili kuhakikisha shughuli zao zinakwenda vizuri kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu.

  “FEMATA Ni Shirikisho linalowakilisha vyama vya kimkoa vya wachimba madini katika kuwaunganisha na serikali,” alisema Dkt Joseph.

  0 0

  WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mheshimiwa Ummy Mwalimu anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Chama cha Urembo na Vipodozi Tanzania (TCA) Agosti 26 mwaka 2019.

  Akizungumza leo Agosti 19,2019 jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Chama hicho Shekha Nasser amesema sekta ya urembo na vipodozi inakua kwa kasi na kutoa ajira nyingi kwa watanzania walio wengi.

  "Tukio hilo la kihistoria la kuzindua chombo hiki muhimu ndani ya nchi yetu litafanyika Agosti 26, 2019 katika jengo la PSSSF –KISENGA, Kijitonyama . Mgeni rasmi ni Waziri wa Afya Ummy Mwalimu,"amesema.

  Amefafanua wamekuwa wakishuhudia ongezeko la warembaji, wenye salons, watengeneza kucha, watengenezaji na wanaoingiza bidhaa za urembo na vipodozi,hivyo ni wakati muafaka kuwa na chama chao ambacho kitaaunganisha wadau wote.

  Amesisitiza TCA ni chama kinachoanzishwa mahsusi kwa ajili ya kuhudumia na kuunganisha wadau wote katika sekta ya urembo na vipodozi nchini."Chama hiki kitahusisha wadau wote kuanzia waelimishaji, wajasiriamali wakubwa na wadogo, wazalishaji wa viwanda vidogo na vikubwa.

  "Pia watengenezaji wa bidhaa asilia, watoa huduma, wasambazaji na watabibu wa ngozi katika sekta nzima hii ya urembo na vipodozi,"amesema.
  Amesema kupitia ndani ya ya TCA kutakua na mafanikio ya kukuza sekta ya urembo na vipodozi baada ya kuona changamoto nyingi wanazozipitia washikadau.

  Ametoa mfano pamoja na Wizara ya Elimu kupitia NACTE kupitisha mtaala wa kwanza wa elimu ya Stashahada hivi karibuni, lakini vyuo vya kutoa NTA Level 4, 5 na 6 bado havipo. 

  Ameongeza pamoja na VETA kuwa na mtaaala wa kozi ya cheti cha Cosmetology lakini changamoto kubwa ni walimu wenye sifa ya Diploma wa kufundisha wanafunzi ili wafanye mtihani wa Taifa na kupata walimu wenye Weledi na sifa nchini. 

  Amesema kuwa ukosefu huo wa walimu wa Cosmetology nchini unasababishwa na mambo mengi yakiwemo ya sekta hiyo kutotambulika rasmi na kujengewa heshima yake inayostahili kama ilivyo katika nchi za jirani Kenya, Uganda na South Afrika.

  "Watanzania wengi huenda kwenye nchi hizo kwa ajili ya kujifunza na kupata elimu ya Cosmetology ngazi ya Stashahada,"amesema Nasser na kuongeza kutokana na muamko huo wameona ni wakati muafaka wa kuanzisha chombo kitakachowaunganisha wadau wote wa sekta hiyo.

  Mwenyekiti huyo wa TCA ametumia fyrsa hiyo kuwakaribisha wadau wote wa sekta ya urembo nchini Tanzania kufika ili kushuhudia tukio hilo la kipekee kwa mara ya kwanza Tanzania lenye kauli mbiu " Urembo na vipodozi katika uchumi wa Viwanda". 
   Mwenyekiti wa Chama cha Urembo na Vipodozi Tanzania (TCA) ,Shekha Nasser  akizungumza na Waandishi wa habari leo jijini Dar kuhusu  uzinduzi  wa chama hicho, Agosti 26,mwaka 2019, ambapo Waziri wa  Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe.Ummy Mwalimu anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.Kulia ni Katibu wa TCA Braison Makena na kushoto ni Meneja Utawala TCA,Judy Charles  
  Baadhi ya Wageni waalikwa mbalimbali wakifuatilia mkutano huo.


older | 1 | .... | 1870 | 1871 | (Page 1872) | 1873 | 1874 | .... | 1898 | newer