Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1869 | 1870 | (Page 1871) | 1872 | 1873 | .... | 1904 | newer

  0 0

   SERIKALI imewataka wakandarasi na watu wote walioshiriki katika ujenzi mkubwa wa tangi la maji katika kata ya Makoko Bhalima Mjini Musoma mkoani Mara, na kutumia vibaya fedha za mradi huo kuhakikisha wanakamilisha haraka ujenzi huo.

  Naibu Waziri wa Maji Juma Aweso amesema hayo wakati akifungua ziara yake ya kikazi ya siku nne mkoani humo ya kukagua maendeleo ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi hususani wale waishio vijijini na kubaini matumizi halali  ya fedha zinazotolewa na serikali ambazo lengo lake kubwa ni kumtua mama ndoo ya kichwani.

  Amesema, mwaka 2017 Serikali ilitoa zaidi ya Sh. milioni 923 ili zitumike katika ujenzi wa tangi hilo ambalo ujenzi huo bado unasua sua,  hivyo Serikali haitatoa fedha nyingine katika kukamilisha ujenzi huo na kuwaasa wakandarasi na wananchi wanaoshiriki kazi hiyo kumalizia ujenzi  huo mara moja.

  ‘’Sisi kama viongozi wa Wizara hatutatoa fedha nyingine haiwezekani serikali inatoa fedha kwa ajili ya kutatua matatizo ya wananchi wa Musoma lakini zinalipwa ovyo ovyo kwa wajanja wachache ambao utekelezaji wao hauonekani  tutafanya kikao cha wazi kuzungumzia mustakabali wa pesa hizo ili tubaini zilipopelekwa,"ameongeza.

  Ameongeza viongozi watakuwa wakali  kuwabaini watendaji wa kazi za umma wasiokuwa waaminifu ambao baada ya kutoa kauli alitoa agizo kwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mhandisi, Robert Lupoja kuwaalika wakandarasi hao kushiriki mjadala wa ubadhilifu wa fedha hizo kesho.

  Aidha Aweso amezindua magari manne yenye gharama ya sh.bilioni 400  yaliyotengenezwa katika mfumo wa majitaka na yatakayozunguka kubeba maji machafu ambayo yatatumiwa na wananchi kwa gharama nafuu katika mtaa wa mradi huo.

   Naye, Muwakilishi wa mradi huo Mponeja John amesema mradi huo umefadhiliwa na kampuni ya Uholanzi, ulianza kutekelezwa Oktoba ,20128 ambapo tayari umekamilika kwa gharama ya Sh.bilioni 27.5 na utakusanya maji taka katika kata za kitaji,Mwigobero na Nyakato mjini hapa.
  Naibu waziri wa Maji, Juma Aweso akikata utepe kuzindua magari manne yenye thamani ya sh.bilioni 400. Magari hayo  yametengenezwa katika mfumo wa majitaka yatakayozunguka kubeba maji machafu ambayo yatatumiwa na wananchi kwa gharama nafuu katika mradi wa  Baruti kata ya Nyakato mjini hapa.
  Naibu waziri wa Maji, Juma Aweso akikata utepe kuzindua magari manne yenye thamani ya sh.bilioni 400. Magari hayo  yametengenezwa katika mfumo wa majitaka yatakayozunguka kubeba maji machafu ambayo yatatumiwa na wananchi kwa gharama nafuu katika mradi wa  Baruti kata ya Nyakato mjini hapa.
   Naibu waziri wa Maji, Juma Aweso akikagua Tangi la Nyamiongo lenye ujazo wa lita Milioni Tano  ambapo karibu na tangi hilo  patajengwa Kituo cha Kuongeza Nguvu ya Maji (Booster Station) kwenda kwenye tangi linalotarajiwa kujengwa katika kilele cha Mlima Bharima.

  0 0

  Meneja Uhusiano wa benki ya CRDB , Godwin Semunyu na Nuru Kilasa Afisa Uhusiano Mwandamizi Benki ya CRDB wakitoa maelezo kwa baadhi ya wateja waliotembelea katika banda la benki hiyo kwenye maonesho ya 4 ya Wiki ya Viwanda kwa nchi za SADC yanayoendelea kwenye viwanja vya Julius Nyerere jijini Dar es salaam.

  0 0

  Waziri Mkuu kasim Majaliwa akizungumza na baadhi ya watoa huduma wa Kampuni ya Airtel Tanzania inayomilikiwa na Serikali kwa asilimia 49 wakati alipotembelea banda la Airtel lililopo JNICC katika mkutano wa SADC unaondelea jijini DSM #SADC2019 #TZTUNATEKELEZA
  Baadhi ya wateja wa Airtel tanzania wakihudumiwa kusajili laini zao kwa alama za vidole katika banda la Airtel lililoko JNICC wakat wakati wa mkutano wa SADC unaondelea jijini DSM #SADC2019 #TZTUNATEKELEZA

  *Airtel yapeleka huduma za usajili kwa alama za vidole SADC.

  Kampuni ya simu za mkononi Airtel Tanzania Plc kupitia Meneja Mawasiliano wake bw, Jackson Mmbando imesema kuwa wateja wote wanaoingia katika naonesho na mkutano wa SADC unaoenselea wanatoa huduma zote za kampuni katika bada lao ikiwemo kukamilisha usajili wa SIM Card kwa wateja wao wote kwa njia ya alama za vidole yaani Beometric Registration.

  "sisi Kama watoa huduma tayari tumeweka kambia hapa tunatoa huduma za usajili kwa alama za visole hapa kwa kuwa tunafaham watu wengi wanatembelea hapa hivyo ni jukumu letu kuwasaidia kuokoa muda wao" alisema Mmbando

  Airtel ina mabanda mawili katika viwanja vya JULIUS NYERERE INTERNATINAL CONFERENCE CENTRE (JINCC) ,ambapo maonesho na mkutano wa SADC unaendelea katika ukumbi huo jijini DSM.

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa heshima za mwisho kwa Natalia Bahati Kilangi, Mke wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi katika mazishi yaliyofanyika Luchelele jijini Mwanza, Agosti 7, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitupa udongo kwenye kaburi la Natalia Bahati Kilangi, Mke wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi, katika mazishi yaliyofanyika Luchelele jijini Mwanza, Agosti 7, 2019. 
  Mwanasheria Mkuu wa Serikali Serikali, Profesa Adelardus Kilangi (wa pili kushoto) na familia yake wakishiriki katika Ibada ya mazishi ya Natalia Bahati Kilangi, Mke wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali yaliyofanyika Luchelele jijini Mwanaza Agosti 7, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu). 

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka shada la maua kwenye kaburi la Natalia Bahati Kilangi, Mke wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi katika mazishi yaliyofanyika nyumbani kwa Profesa Kilangi, Luchelele jijini Mwanza, Agosti 7, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu). 
  Waziri Mkuui, Kassim Majaliwa akisalimiana na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Mwanza, Renatus Nkwande na Askofu wa Jimbo la Geita, Flavian Kassala katika mazishi ya Natalia Bahati Kilangi, Mke wa mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi yaliyofanyika Luchelele jijini Mwanza, Agosti 7, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi wakati alipoiwakilisha serikali katika mazishi ya Mke wa mwanasheria Mkuu wa Serikali, Natalia Bahati Kilangi yaliyofanyika Luchelele jijini Mwanza, Agosti 7, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza katika mazishi ya Natalia Bahati Kilangi, Mke wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi yaliyofanyika Luchelele jijini Mwanza, Agosti 7, 2019. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai (kulia kwa Waziri Mkuu) wakishiriki katika ibada ya mazishi ya Natalia Bahati Kilangi, Mke wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi yaliyoanyika Luchelele jijini Mwanza, Agosti 7, 2019. Wengine pichani kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally, Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana,Ajira, na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama na kulia ni Waziri wa Madini, Doto Biteko. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha

  Naibu waziri wa Wizara ya mifugo na uvuvi Abdalla Ulega amesema kuwa Elimu na ujuzi Wa vitendo ipelekwe kwa wakulima wa vijijini pamoja na wafugaji ili kuwa na wafugaji wenye kufuga kisasa na hatimaye kuchangia katika kufikia uchumi Wa viwanda kama kauli mbiu ya maonyesho ya mwaka huu ya nane nane inavyosema Kilimo ,mifugo na uvuvi kwa ukuaji Wa uchumi Wa nchi.

  Naibu waziri Ameyasema hayo Leo wakati akifunga maonyesho ya 26 ya kilimo na mifugo (nanenane )kwa Kanda ya kaskazini yalikuwa yakifanyika katika viwanja vya Themi Njiro ambapo alisema kuwa kwakuzingatia kauli mbiu maarifa haya yaliotolewa katika maonyesho haya yasipoishia hapa nchi yetu itajitosheleza kwa chakula na mifugo na hatutakuwa na haja ya kuitaji chakula cha msaada bali tutakuwa na chakula cha kutosha .

  Alibainisha kuwa tukichukuwa ujuzi huu tulioupa hapa tutapata mazao bora na mifugo ambapo tutauza mazao ya kilimo na mifugo kibiashara ndani ya nchi na nje ya nchi pia tutaacha kuwa wazalishaji Wa malighafi kwa nchi zingine pia tutaacha kuhamasisha Elimu za viwandani kwenda nchi zingine endapo tutawekeza katika viwanda badala yake tutavuta wawekeza kutoka nchi zingine na kuja kuwekeza katika viwanda ndani ya mikoa hii ya Kanda ya kaskazini ambapo watakuwa na uhakika Wa kupata malighafi bora za Kilimo mifugo na uvuvi

  Aidha alitoa wito kwa wakuu Wa mikoa ya Kanda ya kaskazini ,Wakuu Wa wilaya pamoja na wakurugenzi wa halmashauri kuhakikisha wanatoa huduma staiki kwa maofisa ugani ili waweze kuwahudumia vyema wakulima na kuwajengea uwezo waweze kufikia dhamira ya kuongeza uzalishaji ,kuongeza dhamani,pamoja na kipato katika familia na hatimaye kuuza kibiashara .

  "Napenda kuwasisitizia wakuu Wa mikoa kuwasimamia vyema wakurugenzi Wa halmashauri na wakurugenzi Wa halmashauri kusimamia vyema wakulima kulima Kilimo chenye tija pamoja na wafugaji ili kuleta chachu ya maendeleo ili wanapo uza bidhaa zao waweze kuongeza pato lao na pato la Taifa kwa ujumla "alisema Ulega

  Alisema kuwa maafisa ugani wamekuwa Wanatumika zaidi kuonyesha uwezo wao Wa nadharia zaidi katika viwanja vya maonyesho badala ya kuonyesha ujuzi wao Wanadhari kwa wakulima Wa vijijini .

  Kwa upande wake Mkuu wa mikoa wa Arusha Mrisho Gambo ambaye mi mwenyeki wa maonyesho haya alisema kuwa mwitikio kwa mwaka huu umekuwa mkubwa hususa ni kwa wafugaji tofauti na miaka ya nyuma na hata ongezeko la uongezwaji thamani mazao ya mifugo umeongezeka .
    Naibu waziri wa Wizara ya mifugo na uvuvi  Abdalla Ulega akihutubia wananchi wakati akifunga sherehe za maonyesho ya nanenane  Kanda ya kaskazini yaliofanyika jijini Arusha
   bendi ya Polisi Moshi ikitumbuiza mbele ya mgeni rasmi wakati wa kilele cha maonyesho ya nanenane Kanda ya kaskazini yaliyofanyika njiro Themi jijini hapa.
   Naibu waziri wa Wizara ya mifugo na uvuvi  Abdalla Ulega akimkabidhi kombe la ushindi mkurugenzi wa TAHA Jacqueline Mkindi Mara baada ya kushinda katika sherehe za wakulima Kanda ya kaskazini.


   

  0 0


  *Wengine wasifu teknolojia ya hali ya juu walioyoina kwenye viwanda vya Tanzania
    
  *Wakiri Tanzania inaweza kuliteka solo la Jumuiya ya SADC ,waona fursa lukuki


   Na Ripota, Michuzi TV 

  WAJUMBE wa Mkutano wa 39 wa Jumuiya ya Maendeleo kwa  Nchi za Kusini mwa Afrika(SADC) wametapa nafasi ya kutembelea  viwanda 21vinavyofanya uzalishaji kwa ajili ya kuangalia ubora wa bidhaa na mazingira ya uzalishaji kwa Tanzania Bara na Zanzibar.

  Wakiwa katika viwanda hivyo wajumbe hao wamekiri na kuridhishwa na ambavyo  Serikali ya Tanzania namna ilivyodhamiria katika Uwekezaji katika viwanda huku wakieleza wazi Tanzania wanayo nafasi kubwa ya kumiliki soko la Jumuiya hiyo kwani kuna kila.kitu zikiwemo malighafi za uhakika.

   Baadhi ya wajumbe wa SADC wameiambia Michuzi TV na Michuzi Blog kuwa Tanzania ipo katika nafasi nzuri ya kulimiliki soko la jumuiya hiyo kwa kuwa kuna nguvu kazi ya kutosha na malighafi za uhakika.
    
  Mjumbe kutoka nchini Afrika Kusini wa Kampuni ya Flexion Renatus Joseph amesema kwamba yeye yupo katika sekta ya viwanda vya chuma jijini Johannesburg, Afrika Kusini na kwamba aliyoyashuhudia   katika kiwanda cha Lodha Group of Companies yamenifanya abadili fikra zake kuhusu uwezo wa viwanda kwa nchi ya Tanzania.

  Amesema amethibitisha kwa macho yake kuna matumizi makubwa ya teknolojia katika utengenezaji bidhaa za nondo na vifaa vingine vitokanavyo na chuma. "Hakika vikipatikana viwanda vingi vya namna hii SADC tutapiga hatua na tutakuwa na bidhaa zinazoleta ushindani ndani na nje ya Afrika,” amesema.
    
  Wajumbe hao wakiwa kiwandani hapo yameelezwa kiwanda hicho cha chuma kilichopo Mkuranga mkoani Pwani  ni miongoni mwa viwanda vilivyoitikia  mwito wa Rais Dk. John Magufuli kwa vitendo kuhusu Tanzania ya viwanda.
    
  Akizungumza mbele ya ujumbe wa SADC waliotembelea kiwandani hapo Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Mhandisi Kamara Gombe amesema Tanzania kwa sasa inazalisha tani 200,000 za bidhaa za viwanda huku mahitaji ni tani 300,000.
    
  "Hii maana yake kuna uhaba wa tani laki moja kwenye soko. Hivyo, Kampuni ya Lodhia ni miongoni mwa wadau wa viwanda wanaohakikisha Tanzania inajitegemea katika sekta ya viwanda.Hata hivyo, mbali ya uhitaji huo wa tani laki moja bado kuna tatizo la uhaba wa soko kwa kuwa wanazalisha tani 3000 kwa mwezi
    
  "Lakini  uwezo wao ni kuzalisha tani 10,000. Kazi yetu viwanda ni kulinda viwanda vya ndani, tutahakikisha tatizo hili tunalitafutia ufumbuzi ili hizi tani 7,000 zilizobaki ziweze kuzalishwa,” amesema Gombe.
    
  Wakati Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Toni Filbert amesema wilaya hiyo pamoja na Mkoa wa Pwani kwa ujumla wanazo fursa nyingi za uwekezaji kutokana na ardhi kubwa yenye rutuba. Vilevile, kuna bidhaa nyingi za kimkakati zinazozalishwa na wazawa.

  Akitoa maelezo kuhusu  uwezo wa kiwanda hicho, Mkurugenzi Mkuu wa Lodhia Group of Companies,Sailesh Pandit alisema kampuni hiyo ilianzishwa mwaka 1996 wakiwa wanafanya biashara ya jumla ya kuuza vyuma ambapo mwaka 2004 ndio walianza kuzalisha vyuma katika kiwanda kilichopo mkoani Arusha.
    
  “Vilevile tuligeukia bidhaa nyingine ikiwemo mabomba ya maji, Gypsum Board, mapipa ya kuhifadhia maji na bidhaa nyingine za ujenzi kwa kuhakikisha Tanzania inajitosheleza katika vifaa vya ujenzi bila kuagiza nje ya nchi,” amesema  Pandit  na kufafanua wanamshukuru Rais Magufuli kwa kuwahamasisha kuwekeza kwa nguvu na pia amesaidia kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji kwa kila kampuni bila kupendelea.
    
  Hata hivyo katika ziara hiyo, wajumbe wa SADC pia walipata fursa kutembelea kiwanda cha kusindika matunda cha Bakhresa Group of Companies kilichopo Mwandege Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.
    
  Wajumbe walivutiwa na namna ya kipekee waliyoonyesha wafanyakazi wa kiwanda hicho katika usindikaji matunda, mitambo ya kisasa na usafi wa hali ya juu pia ulionyesha ni namna gani kampuni hiyo ilivyo tayari kuliteka soko la SADC.

  Akielezea uwekezaji huo mkubwa uliogharimu Dola za Kimarekani Milioni 210, Mkurugenzi wa Mahusiano Bakhresa Group, Hussein Sufian alisema kampuni hiyo ina viwanda mbalimbali vipatavyo vinne ambavyo vinasindika bidhaa za chakula.
    
  “Soko letu baada ya kujitosheleza ndani tulijipanua katika mataifa mbalimbali ya kiafrika, kwenye muktadha wa SADC tunafikisha bidhaa zetu katika nchi saba ukiondoa Tanzania, ambazo ni DRC, Angola, Comoro, Msumbiji, Malawi, Zimbabwe na Afrika Kuisini.
    
  “Katika kuhakikisha tunakuza ajira na kuongeza tija katika uzalishaji, kwa asilimia kubwa malighafi zetu zinatoka Tanzania. Tuna ardhi kubwa inayotuwezesha kukusanya matunda kila kona ya nchi, tunayasindika na kuuza nje ya nchi kwa kiwango cha kutosha. Asilimia 15 ya bidhaa zetu tunazisafirisha nje ya Tanzania hasa hizi nchi za SADC,” ameeleza.
    
  Akizungumza katika kiwanda hiki, Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga amesema watahakikisha wanasimamia haki za msingi za kampuni hiyo kwa sababu imewapa heshima kubwa katika Mkoa wa Pwani kutokana na kupata ajira nyingi za vijana.
    
  Pamoja  na mambo mengine wajumbe wametembelea pia kiwanda cha kusindika korosho cha Biotan kilichopo wilayani Mkuranga ambapo  Katika kiwanda hiko wajumbe walijionea hatua kwa hatua namna korosho zinavyopokewa kutoka kwa wakulima, zinavyopangwa kwa daraja, zinavyochemshwa kwa kutumia mvuke hadi hatua ya kuzibangua zikiwa tayari kwa kuwekwa kwenye mifuko.
    
  Akizungumza kiwandani hapo Bahati Mayoma ambaye ni  Mkurugenzi wa Biotan Group Limited amefafanua kampuni yao kwa kiasi kikubwa kinamilikiwa na raia kutoka Australia, ndiyo maana hata bidhaa zao zinazingatia viwango vya hali ya juu kwa kuwa wanazisafirisha katika nchi za Ulaya.
    
  Ameongeza kuwa wanaliona soko la SADC muhimu kwao kwa kuwa kitu muhimu kinachotakiwa katika kulifikia soko hilo ni kuwa na bidhaa zenye ubora ambazo zinaandaliwa katika mazingira safi na salama kwa kutumia teknolijia za hali ya juu.

  “Bidhaa zetu tunazipeleka Denmark, Sweden, Ujerumani, Australia na nchi nyingine nyingi za kiafrika. Lakini kwa sasa soko letu jipya tunaangalia hizi nchi za SADC,” amesema Mayoma.

   Amesema kwamba kwa mwaka uwezo wao wa kuzalisha ni tani 1500 hadi 2000, lakini wanatarajia baada ya kuliteka soko la SADC ikifika mwaka 2021 uwezo wa uzalishaji utafikia tani 5000 kwa mwaka.
    
  Kwa kukumbusha tu SADC ni jumuiya ya kimaendeleo ya kiuchumi inayohusisha nchi wanachama 16 ambazo ni Tanzania, Msumbiji, Zambia, Zimbabwe, Malawi, Angola, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Ushelisheli, Comoro, Botswana, Eswatini, Lesotho, Madagascar, Afrika Kusini, Mauritius na Namibia. Kwa mwaka huu mkutano wa wakuu wa nchi wanachama utafanyika Tanzania kuanzia Agosti 17 hadi 18 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Julius Nyerere (JNICC).

    Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC walioshiriki wiki ya nne ya viwanda  wakiangalia namna nondo zinavyotengenezwa hatua kwa hatua ndani ya kiwanda cha Lodhia Group of Companies kilichopo MKuranga mkoani Pwani.Wajumbe hao wameembelea kiwanda hicho kwa ajili ya kuangalia ubora wa bidhaa na mazingira ya uzalishaji kwa Tanzania. 
  Mkurugenzi Mkuu wa Lodhia Group of Companies, Sailesh Pandit (kulia) akiwa na Meneja wa kiwanda hicho Harminder Bhachu wakiwaongoza Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC waliofika kutembelea kiwanda hicho
   Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC  wakipewa maelezo namna ya uzalishaji wa Nondo unavyofika
  Mkurugenzi Mkuu wa Lodhia Group of Companies, Sailesh Pandit  akieleza kuhusu namna Nondo zinavyotengenezwa hatua kwa hatua na hatimaye kupelekwa sokoni kwa kuuzwa,mbele ya Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC walioshiriki wiki ya nne ya viwanda  waliotembelea kiwanda hicho kwa ajili ya kuangalia ubora wa bidhaa na mazingira ya uzalishaji kwa Tanzania. 

  Pandit  alisema kampuni hiyo ilianzishwa mwaka 1996 wakiwa wanafanya biashara ya jumla ya kuuza vyuma ambapo mwaka 2004 ndio walianza kuzalisha vyuma katika kiwanda kilichopo mkoani Arusha.“Vilevile tuligeukia bidhaa nyingine ikiwemo mabomba ya maji, Gypsum Board, mapipa ya kuhifadhia maji na bidhaa nyingine za ujenzi kwa kuhakikisha Tanzania inajitosheleza katika vifaa vya ujenzi bila kuagiza nje ya nchi,” alisema Bhachu na kuongeza.

  Mkurugeni Mkuu wa Kampuni ya Lodhia Group of Companies Sailesh Pandit akiwaongoza Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC walioshiriki wiki ya nne ya viwanda  waliotembelea kiwanda hicho leo kwa ajili ya kuangalia ubora wa bidhaa na mazingira ya uzalishaji kwa Tanzania. 
  Meneja wa Kampuni ya  Lodhia Group of Companies, Harminder Bhachu akiwaonesha Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC nondo zikiwa tayari kusafirishwa maeneo mbalimbali kwa matumizi.
   Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC walioshiriki wiki ya nne ya viwanda  wakiangalia namna mabomba ya Platic yanavyotengenezwa  ndani ya kiwanda cha Lodhia Group of Companies, hatua kwa hatua na hatimaye tayari kwa matumizi
  Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Toni Filbert akizungumza mbele ya Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC walioshiriki wiki ya nne ya viwanda (hawapo pichani) mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea kiwanda cha Lodhia Group of Companies,kilichopo wilayani humo mkoani Pwani,Mh.Filbert alisema wilaya hiyo pamoja na Mkoa wa Pwani kwa ujumla wanazo fursa nyingi za uwekezaji kutokana na ardhi kubwa yenye rutuba. Vilevile, kuna bidhaa nyingi za kimkakati zinazozalishwa na wazawa. 

  “Tunaihakikishia serikali kuwa kazi tunaiweza, tutatoa fursa za ajira na kuzifanyia kazi rasilimali tulizonazo kwa ajili ya Tanzania mpya ya viwanda. Tunaomba, kampuni kama hizi za kimkakati zipewe fursa katika kushiriki ujenzi wa miradi mikubwa ikiwemo SGR na miradi mingine ikiwemo madaraja na barabara,” alisema Filbert.
  Mkurugeni Mkuu wa Kampuni ya Lodhia Group of Companies , Sailesh Pandit akisoma hotuba yake fupi mbele ya Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC walioshiriki wiki ya nne ya viwanda,ambao wametembelea kiwanda hicho leo kwa ajili ya kuangalia ubora wa bidhaa na mazingira ya uzalishaji kwa Tanzania. 
  Mkurugeni Mkuu wa Kampuni ya Lodhia Group of Companies Sailesh Pandit ,akizungumza na baadhi ya Waandishi wa habari walioambatana na Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC walioshiriki wiki ya nne ya viwanda,ambao wametembelea kiwanda hicho leo kwa ajili ya kuangalia ubora wa bidhaa na mazingira ya uzalishaji kwa Tanzania. 
  Mkurugenzi wa Mahusiano Bakharesa Group, Hussein Sufian akitoa ufafanuzi wa jambo mbele ya wajumbe wa SADC waliopata fursa ya kutembelea kiwanda hicho  cha kusindika matunda cha Bakhresa Group of Companies kilichopo Mwandege Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.Katika ziara hiyo Wajumbe walivutiwa na namna ya kipekee waliyoonesha wafanyakazi wa kiwanda hicho katika usindikaji matunda, mitambo ya kisasa na usafi wa hali ya juu,huku ikionesha pia ni namna gani kampuni hiyo ilivyo tayari kuliteka soko la SADC.

  Akielezea uwekezaji huo mkubwa uliogharimu Dola za Kimarekani Milioni 210, Mkurugenzi wa Mahusiano Bakharesa Group, Hussein Sufian alisema kampuni hiyo ina viwanda mbalimbali vipatavyo vinne ambavyo vinasindika bidhaa za chakula.“Soko letu baada ya kujitosheleza ndani tulijipanua katika mataifa mbalimbali ya kiafrika, kwenye muktadha wa SADC tunafikisha bidhaa zetu katika nchi saba ukiondoa Tanzania, ambazo ni DRC, Angola, Comoro, Msumbiji, Malawi, Zimbabwe na Afrika Kuisini.
  Mkurugenzi wa Mahusiano Bakharesa Group, Hussein Sufian akitoa ufafanuzi wa jambo mbele ya wajumbe wa SADC waliopata fursa ya kutembelea kiwanda hicho  cha kusindika matunda cha Bakharesa Group of Companies kilichopo Mwandege Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.
  Mkurugenzi wa Biotan Group Limited,Bahati Mayoma akizungumza mbele ya Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC walioshiriki wiki ya nne ya viwanda  na baadaye walitembelea kiwanda hicho cha kusindika Korosho kilichopo Mkuranga mkoani Pwani , Wajumbe hao walijionea hatua kwa hatua namna korosho zinavyopokewa kutoka kwa wakulima, zinavyopangwa kwa daraja, zinavyochemshwa kwa kutumia mvuke hadi hatua ya kuzibangua zikiwa tayari kwa kuwekwa kwenye mifuko.

  Akizungumzia kuhusu soko,Mayoma alibainisha kuwa wanaliona soko la SADC muhimu kwao kwa kuwa kitu muhimu kinachotakiwa katika kulifikia soko hilo ni kuwa na bidhaa zenye ubora ambazo zinaandaliwa katika mazingira safi na salama kwa kutumia teknolijia za hali ya juu.Alisema kwa mwaka uwezo wao wa kuzalisha ni tani 1500 hadi 2000, lakini wanatarajia baada ya kuliteka soko la SADC ikifika mwaka 2021 uwezo wa uzalishaji utafikia tani 5000 kwa mwaka. 
  Baadhi akina mama wakibangua korosho ndani ya kiwanda cha BIOTAN,kilichopo Mkuranga mkoani Pwani,Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC walioshiriki wiki ya nne ya viwanda na baadaye walitembelea kiwanda hicho cha kusindika Korosho kilichopo Mkuranga mkoani Pwani , Wajumbe hao walijionea hatua kwa hatua namna korosho zinavyopokewa kutoka kwa wakulima, zinavyopangwa kwa daraja, zinavyochemshwa kwa kutumia mvuke hadi hatua ya kuzibangua zikiwa tayari kwa kuwekwa kwenye mifuko.Picha na Michuzi JR.

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola aliyekaa kwenye Pikipiki akifurahia jambo na Mbunge wa Kilolo (CCM), Venance Mwamoto mara baada ya Munge huyo kukabidhi msaada wa Pikipiki mbili ili zitumike na Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa. Katikati ni Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa, ACP Juma Bwire(Picha na Datus Mahendeka, Jeshi la Polisi)  Na Datus Mahendeka, Jeshi la Polisi

  WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Polisi, Kangi Lugola amepokea msaada wa Pikipiki amanbazo zitatumika kwa ajili ya doria ili kupunguza uhalifu Mkoa wa Iringa.

  Aidha, amelitaka Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa kutotumia Pikipiki hizo kwa ajili ya kazi za kihalifu ikiwemo kusingikiza mirungi na badala yake zitumike kwa kazi iliyokusudiwa.

  Lugola alitoa kauli hiyo jana, wakati akipokea msaada wa Pikipiki mbili zenye thamani ya Tsh 2.8 zilizotolewa na Mbunge wa Kilolo, Venance Mwamoto kwa ajili ya kituo cha Ikokoto Iringa.

  “Tumepokea Pikipiki hizi…wazitunze ili zidumu.. zitumike kwa ajili ya kufanya doria kwenye maeneo korofi hususani maeneo ya mlima Kitonga”alisisitiza.

  Hata hivyo alitoa wito kwa wananchi na wadau werevu kuendelea kulisaidia jeshi la polisi kamwe wasichoke kutoa misaada kwa Jeshi la polisi.

  0 0

  Mjumbe kutoka ubalozi wa Uingereza nchini Tanzania akishiriki zoezi la upandaji miti lililondaliwa na kampuni ya Serengeti Breweries Ltd mkoani Kilimanjaro. 
  Ujumbe kutoka ubalozi wa Uingereza ukifurahia jambo ulipofanya ziara katika kiwanda cha SBL mjini Moshi.
  Mkurugenzi mtendaji wa SBL, Mark Ocitti (wa pili kushoto) akitoa maelezo juu namna kiwanda kinavyofanya kazi kwa ujumbe kutoka nchini Uingereza uliotembelea kiwanda hicho.
  Ujumbe kutoka ubalozi wa Uingereza nchini Tanzania ukishriki zoezi la upandaji miti liliondaliwa na kampuni ya Serengeti Breweries Ltd mkoani Kilimanjaro.


  Kama hatua ya kuchangia katika jitihada za utunzaji wa mazingira pamoja na vyanzo vya maji mkoani Kilimanjaro, kampuni ya bia ya Serengeti, Serengeti Breweries Limited (SBL) kwa kushirikiana na taasisi ya The Kilimanjaro Project imezindua kampeni ya kupanda miti elfu moja mkoani humo.

  Miti hiyo imepandwa katika kiwanda cha SBL kilichopo Pasua katika wilaya ya Moshi na mingine imepandwa katika wilaya ya Mwanga.

  Akizungumza wakati wa zoezi la upandaji miti, Mkurugenzi Mtendaji wa SBL, Mark Ocitti, amesema SBL imeamua kuongeza jitihada za uhifadhi wa mazingira si tu katika maeneo yaliyo chini ya SBL bali katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania.“Huu ni udhihirisho tosha kwamba SBL imejidhatiti na iko tayari kushirikiana na wadau wengine katika kutekeleza miradi yenye kuleta tija kwa jamii zetu,” amesema Ocitti.

  Zoezi la upandaji miti linakuja huku kukiwa na wito kutoka jumuiya ya kimataifa juu kupunguza uzalishaji wa hewa ya ukaa kwa kuongeza juhudi za uhifadhi wa misitu ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi na hivyo kuyaweka mazingira katika hali ya usalama kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

  Mpango huu wa SBL unaenda sambamba na sera ya kampuni katika kurudisha kwa jamii sehemu ya faida, na umejikita zaidi katika utoaji wa huduma bora ya maji safi kupitia mradi uitwao Water of Life (WOL); mpango kwa ajili kuwasaidia wanafunzi kupata ufadhili wa masomo ya elimu ya juu, kuwasaidia wakulima wa ndani hususani wa vijijini pamoja na mpango wa kuhamasisha unywaji pombe kistaarabu.

  Zoezi la upandaji miti limehudhuriwa na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Sara Cooke pamoja na Mwakilishi wa Waziri Mkuu wa Uingereza kitengo cha biashara, Andrew Rosindell, ambao walikuwa ziarani kiwandani hapo.

  0 0


  *Wengine wasifu teknolojia ya hali ya juu walioyoina kwenye viwanda vya Tanzania

  *Wakiri Tanzania inaweza kuliteka solo la Jumuiya ya SADC ,waona fursa lukuki

  WAJUMBE wa Mkutano wa 39 wa Jumuiya ya Maendeleo kwa Nchi za Kusini mwa Afrika(SADC) wametapa nafasi ya kutembelea viwanda 21vinavyofanya  uzalishaji kwa ajili ya kuangalia ubora wa bidhaa na mazingira ya uzalishaji kwa Tanzania Bara na Zanzibar.

  Wakiwa katika viwanda hivyo wajumbe hao wamekiri na kuridhishwa na ambavyo Serikali ya Tanzania namna ilivyodhamiria katika Uwekezaji katika viwanda huku wakieleza wazi Tanzania wanayo nafasi kubwa ya kumiliki soko la Jumuiya hiyo kwani kuna kila.kitu zikiwemo malighafi za uhakika.

  Baadhi ya wajumbe wa SADC wameiambia Michuzi TV na Michuzi Blog kuwa Tanzania ipo katika nafasi nzuri ya kulimiliki soko la jumuiya hiyo kwa kuwa kuna nguvu kazi ya kutosha na malighafi za uhakika.

  Mjumbe kutoka nchini Afrika Kusini wa Kampuni ya Flexion Renatus Joseph amesema kwamba yeye yupo katika sekta ya viwanda vya chuma jijini Johannesburg, Afrika Kusini na kwamba aliyoyashuhudia katika kiwanda cha Lodha Group of Companies yamenifanya abadili fikra zake kuhusu uwezo wa viwanda kwa nchi ya Tanzania.

  Amesema amethibitisha kwa macho yake kuna matumizi makubwa ya teknolojia katika utengenezaji bidhaa za nondo na vifaa vingine vitokanavyo na chuma. "Hakika vikipatikana viwanda vingi vya namna hii SADC tutapiga hatua na tutakuwa na bidhaa zinazoleta ushindani ndani na nje ya Afrika,” amesema.

  Wajumbe hao wakiwa kiwandani hapo yameelezwa kiwanda hicho cha chuma kilichopo Mkuranga mkoani Pwani ni miongoni mwa viwanda vilivyoitikia mwito wa Rais Dk. John Magufuli kwa vitendo kuhusu Tanzania ya viwanda.

  Akizungumza mbele ya ujumbe wa SADC waliotembelea kiwandani hapo Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Mhandisi Kamara Gombe amesema Tanzania kwa sasa inazalisha tani 200,000 za bidhaa za viwanda huku mahitaji ni tani 300,000.

  "Hii maana yake kuna uhaba wa tani laki moja kwenye soko. Hivyo, Kampuni ya Lodhia ni miongoni mwa wadau wa viwanda wanaohakikisha Tanzania inajitegemea katika sekta ya viwanda.Hata hivyo, mbali ya uhitaji huo wa tani laki moja bado kuna tatizo la uhaba wa soko kwa kuwa wanazalisha tani 3000 kwa mwezi

  "Lakini uwezo wao ni kuzalisha tani 10,000. Kazi yetu viwanda ni kulinda viwanda vya ndani, tutahakikisha tatizo hili tunalitafutia ufumbuzi ili hizi tani 7,000 zilizobaki ziweze kuzalishwa,” amesema Gombe.

  Wakati Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Toni Filbert amesema wilaya hiyo pamoja na Mkoa wa Pwani kwa ujumla wanazo fursa nyingi za uwekezaji kutokana na ardhi kubwa yenye rutuba. Vilevile, kuna bidhaa nyingi za kimkakati zinazozalishwa na wazawa.

  Akitoa maelezo kuhusu uwezo wa kiwanda hicho, Mkurugenzi Mkuu wa Lodhia Group of Companies,Sailesh Pandit alisema kampuni hiyo ilianzishwa mwaka 1996 wakiwa wanafanya biashara ya jumla ya kuuza vyuma ambapo mwaka 2004 ndio walianza kuzalisha vyuma katika kiwanda kilichopo mkoani Arusha.

  “Vilevile tuligeukia bidhaa nyingine ikiwemo mabomba ya maji, Gypsum Board, matenki ya ya kuhifadhia maji na bidhaa nyingine za ujenzi kwa kuhakikisha Tanzania ina

  jitosheleza katika vifaa vya ujenzi bila kuagiza nje ya nchi,” amesema Pandit na kufafanua wanamshukuru Rais Magufuli kwa kuwahamasisha kuwekeza kwa nguvu na pia amesaidia kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji kwa kila kampuni bila kupendelea.

  Mkurugenzi huyo pia aliiomba serikali kuangalia uwezekano wa kuweka “kodi kinzani” kwa asilimia kati ya 30/40 kwa bidhaa za chuma kutoka nje ili  kuvilinda viwanda vya ndani ambavyo kwa pamoja vina uwezo wa kuzalisha  zaidi ya tani 400,000 kwa mwaka iwapo viwanda hivyo vitafanya kazi kwa asilimia 100.

  “kwasasa sisi tunafanya kazi kwa massaa nane tu badala ya masaa 24 na sababu kubwa ni kukosekana kwa soko la ndani la uhakika la bidhaa za chuma kutokana na hatua ya serikali kuruhusu chuma kutoka nje kuingizwa bila ya kulipiwa ushuru hasa kutoka nchi za SADC”alisema Mkurugenzi huyo.

  Pandit aliongeza kuwa hatua ya serikali kuweka kodi kinzani italeta manufaa makubwa ya kiuchumi kwa kuongeza ajira kwa watanzania na serikali kuongeza mapato yake.
  Mkurugenzi Mkuu wa Lodhia Group of Companies, Sailesh Pandit  (pili kushoto) akionesha kipande cha nondo huku akieleza namna ambavyo hutengenezwa hatua kwa hatua na hatimaye kupelekwa sokoni kwa kuuzwa,mbele ya Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC walioshiriki wiki ya nne ya viwanda  waliotembelea kiwanda hicho kwa ajili ya kuangalia ubora wa bidhaa na mazingira ya uzalishaji kwa Tanzania. 
    Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC walioshiriki wiki ya nne ya viwanda  wakiangalia namna nondo zinavyotengenezwa hatua kwa hatua ndani ya kiwanda cha Lodhia Group of Companies kilichopo MKuranga mkoani Pwani.Wajumbe hao wametembelea kiwanda hicho kwa ajili ya kuangalia ubora wa bidhaa na mazingira ya uzalishaji kwa Tanzania. 
  Mkurugenzi Mkuu wa Lodhia Group of Companies, Sailesh Pandit (kulia) akiwa na Meneja wa kiwanda hicho Harminder Bhachu wakiwaongoza Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC waliofika kutembelea kiwanda hicho.
  Mkurugenzi Mkuu wa Lodhia Group of Companies, Sailesh Pandit  akieleza kuhusu namna Nondo zinavyotengenezwa hatua kwa hatua na hatimaye kupelekwa sokoni kwa kuuzwa,mbele ya Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC walioshiriki wiki ya nne ya viwanda  waliotembelea kiwanda hicho kwa ajili ya kuangalia ubora wa bidhaa na mazingira ya uzalishaji kwa Tanzania. 

  Pandit  alisema kampuni hiyo ilianzishwa mwaka 1996 wakiwa wanafanya biashara ya jumla ya kuuza vyuma ambapo mwaka 2004 ndio walianza kuzalisha vyuma katika kiwanda kilichopo mkoani Arusha.“Vilevile tuligeukia bidhaa nyingine ikiwemo mabomba ya maji, Gypsum Board, mapipa ya kuhifadhia maji na bidhaa nyingine za ujenzi kwa kuhakikisha Tanzania inajitosheleza katika vifaa vya ujenzi bila kuagiza nje ya nchi,” alisema Bhachu na kuongeza.
   Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC  wakipewa maelezo namna ya uzalishaji wa Nondo unavyofika
  Mkurugeni Mkuu wa Kampuni ya Lodhia Group of Companies Sailesh Pandit akiwaongoza Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC walioshiriki wiki ya nne ya viwanda  waliotembelea kiwanda hicho leo kwa ajili ya kuangalia ubora wa bidhaa na mazingira ya uzalishaji kwa Tanzania. 
  Meneja wa Kampuni ya  Lodhia Group of Companies, Harminder Bhachu akiwaonesha Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC nondo zikiwa tayari kusafirishwa maeneo mbalimbali kwa matumizi.
   Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC walioshiriki wiki ya nne ya viwanda  wakiangalia namna mabomba ya Platic yanavyotengenezwa  ndani ya kiwanda cha Lodhia Group of Companies, hatua kwa hatua na hatimaye tayari kwa matumizi
  Mkurugeni Mkuu wa Kampuni ya Lodhia Group of Companies , Sailesh Pandit akisoma hotuba yake fupi mbele ya Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC walioshiriki wiki ya nne ya viwanda,ambao wametembelea kiwanda hicho leo kwa ajili ya kuangalia ubora wa bidhaa na mazingira ya uzalishaji kwa Tanzania. 
  Mkurugeni Mkuu wa Kampuni ya Lodhia Group of Companies Sailesh Pandit ,akizungumza na baadhi ya Waandishi wa habari walioambatana na Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC walioshiriki wiki ya nne ya viwanda,ambao wametembelea kiwanda hicho leo kwa ajili ya kuangalia ubora wa bidhaa na mazingira ya uzalishaji kwa Tanzania.
  Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Toni Filbert akizungumza mbele ya Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC walioshiriki wiki ya nne ya viwanda (hawapo pichani) mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea kiwanda cha Lodhia Group of Companies,kilichopo wilayani humo mkoani Pwani,Mh.Filbert alisema wilaya hiyo pamoja na Mkoa wa Pwani kwa ujumla wanazo fursa nyingi za uwekezaji kutokana na ardhi kubwa yenye rutuba. Vilevile, kuna bidhaa nyingi za kimkakati zinazozalishwa na wazawa. 

  “Tunaihakikishia serikali kuwa kazi tunaiweza, tutatoa fursa za ajira na kuzifanyia kazi rasilimali tulizonazo kwa ajili ya Tanzania mpya ya viwanda. Tunaomba, kampuni kama hizi za kimkakati zipewe fursa katika kushiriki ujenzi wa miradi mikubwa ikiwemo SGR na miradi mingine ikiwemo madaraja na barabara,” alisema Filbert.

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia wakati alipofungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu (TAHLISO) katika Ukumbi wa Nkrumah uliopo Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Agosti 10, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisoma hati ya kiwanja ambacho kitajengwa Ofisi ya Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO) kilichopo eneo la Mtumba jijini Dodoma kilichotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi (kushoto) Agosti 10, 2019 wakati Waziri Mkuu alipofungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa TAHLISO katika Ukumbi wa Nkuruma uliopo Chuo Kikuu cha Dar es salaam. Kulia ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce Ndalichako na wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa TAHLISO, Peter Niboye.
  Baadhi ya washiriki wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu (TAHLISO) wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipofungua Mkutano huo katika Ukumbi wa Nkrumah uliopo Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Agosti 10, 2019.  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce Ndalichako wakati alipowasili katika Ukumbi wa Nkrumah uliopo Chuo Kikuu cha Dar es salaam kufungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO), Agosti 10, 2019.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozana na Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa, Joyce Ndalichako (kulia) na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salam, Utawala, Profesa David Mfinanga (kushoto) wakati alipoingia katika Ukumbi wa Nkrumah uliopo Chuo Kikuu cha Dar es salaam kufungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO), Agosti 10, 2019. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa TAHLISO, Peter Niboye

  ………………

  WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameutaka uongozi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kutafakari namna ya kurekebisha baadhi ya dosari zilizopo likiwemo suala la kuwanyima mikopo wanafunzi kwa kutumia kigezo cha kusoma katika shule binafsi.

  Amesema kuna baadhi ya wanafunzi ambao wamefaulu vizuri kidato cha nne na wamekosa nafasi katika shule za Serikali na wanatoka katika familia zisizokuwa na uwezo, hivyo wanatafuta wafadhili ambao wanawasomesha kwenye shule binafsi.

  Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumamosi, Agosti 10, 2019) wakati akifungua mkutano Mkuu wa Mwaka wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO) kwenye ukumbi wa Nkrumah, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

  Amesema kitendo cha bodi hiyo kuwanyima mikopo baadhi ya wanafunzi kwa kigezo cha kusoma katika shule binafsi bila ya kujiridhisha kama wanatoka kwenye familia zenye uwezo au zisizokuwa na uwezo kinawanyima wanafunzi hao fursa za kuendelea na masomo.

  Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwaonya wakuu wa vyuo vikuu ambao wanatumia vibaya fedha za mikopo ya wanafunzi kwa kuzipeleka katika miradi mbalimbali baada ya kuzipokea kutoka HESLB na kuwacheleweshea wanafunzi stahiki yao.

  Wakati huo huo, Waziri Mkuu amewaagiza viongozi wa vyuo vikuu kuimarisha mafunzo kwa njia ya vitendo kwani tafiti nyingi zinazohusu mambo ya ajira zimebainisha umuhimu wa mafunzo ya vitendo katika kumuwezesha mhitimu kuwa na uelewa na ujuzi mpana wa kile alichokisoma kwa njia ya nadharia.

  “Vyuo viongeze umakini na ufuatiliaji wa karibu wa vijana wetu wanapokuwa kwenye elimu kwa vitendo ili kuhakikisha kwamba wanapata maarifa na ujuzi uliokusudiwa katika mitaala yao. Pia natoa wito kwa waajiri wa sekta ya umma na binafsi watoe ushirikiano wa dhati kwa wanafunzi wanaotafuta nafasi za kufanya mafunzo kwa njia ya vitendo kwenye taasisi zao.” 

  Kwa upande wake, Mwenyekiti wa TAHLISO, Bw. Peter Niboye amesema miongoni mwa changamoto zinazowakabili wanafunzi wa elimu ya juu ni ucheleweshwaji wa mikopo kwa baadhi ya vyuo licha ya HESLB kuwasilisha fedha hizo mapema, hivyo ameiomba Serikali kuwasaidia katika kutatua tatizo hilo.

  Kadhalika, Mwenyekiti huyo wa TAHLISO, ameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli kwa ushirikiano mkubwa inaoipatia jumuiya hiyo hivyo kurahisisha utendaji wake.

  Awali, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Bw. Patrobas Katambi alimkabidhi Waziri Mkuu hati ya kiwanja kilichoko katika eneo la Mtumba jijini Dodoma kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za TAHLISO, ambapo baada ya kupokea hati hiyo, Waziri Mkuu aliikabidhi kwa Mkwenyekiti wa jumuiya hiyo Bw. Niboye.

  Mkutano huo umehudhuriwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Paul Makonda, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Bw. Godfrey Chongolo, Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Bw. Kisare Makori pamoja na viongozi kutoka vyuo mbalimbali nchini vinavyounda TAHLISO.

  0 0


  KAMISHNA Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini (CPG) Phaustine Kasike wa kwanza kushoto akiwa ameshika matofali wakati wa ziara ya kukagua mradi wa Ujenzi huo katika Magereza ya Isanga na Msalato yaliyopo jijini hapa (katikati) ni Mkuu wa Magereza mkoani Dodoma Kenneth Mwambije
  …………….
   
  Na.Alex Sonna,Dodoma

  KAMISHNA Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini (CPG) Phaustine Kasike amewaagiza maofisa wa jeshi hilo nchini kote kuhakikisha wanatekeleza agizo la Rais Dk John Magufuli la kujenga nyumba za gharama nafuu kwa ajili ya stafu wa jeshi hilo kupitia nguvu Kazi walionayo ili kuipunguzia mzigo Serikali.
  Jeshi hilo linakabiliwa na tatizo la uhaba wa nyumba za maofisa hao katika mikoa mbalimbali hapa nchini.

  Hayo aliyasema wakati wa ziara ya kukagua mradi wa Ujenzi huo katika Magereza ya Isanga na Msalato yaliyopo jijini hapa Kamishna Jenerali Kasike amesema kuwa jumla ya nyumba 9000 zinatakiwa kwa ajili ya kumaliza changamoto hiyo ambapo kila mkoa kupitia nguvu Kazi walionayo katika Magereza wanatekeleza mradi huo.

  Amesema kuwa upande wa mkoa wa Dodoma zinatakiwa nyumba 340 katika gereza la Isanga lakini hadi sasa tayari nyumba 137 zipo katika hatua ya mwisho ya Ujenzi huku zikisalia 203 ambazo nazo zinatakiwa kukamilika ndani ya muda ili ziweze kuanza kutumika kwa maofisa hao.

  “Nawapongeza sana maofisa wa Magereza kwa jitihada wanazofanya katika kusimamia Ujenzi huo nimeona Dodoma wako vizuri na mikoa mingine fanyeni hivyo ili tufikie lengo ikiwemo kutekeleza agizo la Rais,” amesema Kamishna Jenerali Kasike.Hata hivyo amesema kuwa jitihada wanazofanya kupitia nguvu Kazi,wanaimani Serikali itaweka nguvu ya ziada jambo ambalo watafanikiwa kumaliza tatizo hilo kabisa.

  “Nahakika hadi sasa tumepunguza gharama za Ujenzi ambazo Serikali ingetoa bila Jeshi hilo kubuni mradi huo,zikikamilika gharama halisi ya ujenzi itajulikana kiasi gani kimetumika na kipi kimeokolewa kama wangetumia wakandarasi “, amesisitiza Kamishna Jenerali Kasike.

  Akitolea mfano Gereza la Isanga lililopo jijini hapa amesema nyumba 20 tayari msingi imeshawekwa huku nyumba 14 zimefikia katika hatua ya lenta na sita zilizosalia katika gereza hilo zinaendelea kujengwa.

  Alisema Magereza hayo wamefanya vizuri kwa sababu wametumia muda na nguvu Kazi iliopo kuhakikisha wanafanikiwa kumaliza tatizo la uhaba wa nyumba za maofisa wa jeshi hilo.Alisema kutokana na kutumia vyanzo vyao bado wanaimani watakamilisha ndani ya muda waliojiwekea.

  Naye Mkuu wa Magereza mkoani Dodoma Kenneth Mwambije alisema Jeshi hilo mkoani Dodoma wako mstari wa mbele katika usimamizi wa mradi huo ili kutimiza lengo la kukamilisha Ujenzi huo pamoja na kutatua changamoto ya tatizo hilo.

  Mwambije alisema lengo ni kuona idadi ya nyumba zinazotakiwa katika mkoa wa Dodoma kwenye Magereza husika zinakamilika kwa wakati ili kurahisha ufanyaji Kazi wa askari wa jeshi hilo.“Tunashkuru Kamishna Jenerali kutembelea mradi huu wa Ujenzi tutahakikisha usimamizi unafanyika kifasaha na nyumba zitaendelea kukamilika,” alisema Mwambije.

  Kwa upande wa wakuu wa Gereza la Isanga na Msalato jijini Dodoma kwa nyakati tofauti walimshkuru Kamishna Jenerali kwa kutembelea mradi wa Ujenzi na kumuhakikishia wataendelea kusimamia ili kuhakikisha nyumba hizo zinakamilika kwa wakati.

  Huruma Mwalije ambaye ni Mkuu wa gereza la Msalato alisema lengo lao ni kuona idadi ya nyumba walizopangiwa zinakamilika.Kwa upande wa Mkuu wa gereza la Isanga John Daud alisema Kamishna asiwe na wasiwasi Kazi aliyowakabidhi itafanyika kwa mujibu wa sheria Na maelekezo waliopewa.

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dkt. Juma Mfinanga kuhusu hali za majeruhi 43 ambao wanapatiwa matibabu mara baada ya kuungua miili yao katika ajali ya moto iliyotokea mkoani Morogoro baada ya Lori la Mafuta kupinduka na kuteketea kwa moto. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dkt. Juma Mfinanga kuhusu hali za majeruhi 43 ambao wanapatiwa matibabu mara baada ya kuungua miili yao katika ajali ya moto iliyotokea mkoani Morogoro baada ya Lori la Mafuta kupinduka na kuteketea kwa moto.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwajulia hali majeruhi wa ajali ya moto ambao wamelazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili mara baada ya kusafirishwa kutokea mkoani Morogoro.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi mbalimbali katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili mara baada ya kutoka kuwajulia hali majeruhi 43 wa ajali ya moto ambao wanapatiwa matibabu katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam. wakwanza kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Profesa Lawrence Museru na wa kwanza kulia ni Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali Dkt. Juma Mfinanga. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dkt. Juma Mfinanga kuhusu hali za majeruhi 43 ambao wanapatiwa matibabu mara baada ya kuungua miili yao katika ajali ya moto iliyotokea mkoani Morogoro. Wakwanza kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Profesa Lawrence Museru
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akitoka katika kitengo cha Dharura na kuelekea katika Wodi za Wagonjwa kwa ajili ya kuwajulia hali majeruhi wa ajali ya moto.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akitoka katika wodi ya Sewahaji mara baada ya kuwajulia hali majeruhi wa ajali ya moto. PICHA NA IKULU

  0 0

   
  QNET, kampuni ya mauzo ya moja kwa moja ambayo ni mshirika rasmi wa Timu ya mpira wa miguu ya Manchester City, Ikiwa kama sehemu ya ahadi yake ya kuendeleza vipaji na kama namna ya kampuni kurudisha kwa jamii, imedhamini wachezaji watatu chipukizi wa kiafrika kuhudhuria mafunzo ya mpira wa miguu ya jijini Manchester (City Football Language School in Manchester) .

   Shule ya Lugha ya Mpira wa Miguu ya Manchester ni kozi ya wiki mbili ya mpira wa miguu na mafunzo ya lugha ya kiingereza kwa wachezaji chipukizi (vijana). Kozi hii ilianza tarehe 28 Julai na itakamilika tarehe 12 August mwaka 2019. 

  Wachezaji hao chipukizi walichaguliwa kutoka katika mchakato wenye ushindani mkubwa nchini Ghana, Cameroun na Ivory Coast, na ni kozi ambayo haina gharama yoyote kwa wachezaji hawa walio chaguliwa. 

  Shule ya Lugha ya Mpira wa Miguu ni kozi ya lugha ya kiingereza na mpira wa miguu yenye hamasha kwa wachezaji chipukizi wenye umri wa kati ya miaka 12-17, ambayo inafanyika katika viwanja vya mafunzo vilivyoko huko katika jiji la Manchester. Wachezaji chipukizi waliochaguliwa wanapata fursa ya kupata falsafa ya mafunzo na mbinu za mpira wa miguu za manchester city kupitia katika vipindi vya mafunzo ambavyo vinaongozwa na makocha wa mpira wa miguu wa jiji la manchester. 

   Vile vile wanapata fursa ya kuendeleza uwezo na ujuzi wao wa kutumia lugha ya kiingereza kupitia majadiliano katika vipindi vya ulimwengu wa mpira (the world of football) kutoka kwa walimu wa vituo vya mafunzo ya lugha vya British Study Centres 

  Wachezaji hao chipukizi wanajifunza na kupata mafunzo nyumbani au katika makao makuu ya machester city katika kitovu cha campus ya Etihad, sehemu ambayo watakuwa na nafasi ya kutumia miundombinu bora. Mafunzo ya Mpira wa miguu yenye ubunifu wa kiwango cha juu na Mtaala wa Lugha ya Kiingereza vimeandaliwa kwa lengo la kuhakikisha wanaongeza uwezo wa kujifunza nje na ndani ya uwanja, ikiwa inagusa maeneo ya msingi ya maisha ya mtaalamu wa mpira wa miguu. 

  Zaidi ya kutambuliwa na Shule ya Lugha ya kiingereza ya British Council, kozi hii vile vile inatambuliwa na Eaquals ambao lengo lao ni kuthibitisha kwamba viwango vya juu katika kufundisha lugha na mafunzo vinafikiwa duniani kote. 

  Akiongelea kuhusu fursa hiyo, Bwana Biram Fall; Meneja Mkuu wa QNET wa kanda ya Kusini mwa Jangwa la Sahara alisema: "QNET inaendelea kuwekeza katika kuendeleza na kukuza vipaji katika ngazi zote. Udhamini wa Klabu ya mpira wa miguu ya Manchester City kama mshirika wa mauzo ya moja kwa moja ni moja kati ya majukumu yetu katika mpira wa miguu na ari ambayo mpira huo unaambatana nao duniani kote. 

  Mchezo wa mpira wa miguu unaunganisha watu kutoka katika asili na maeneo mbalimbali. Mpira wa miguu vile vile unahamasisha kufanya kazi kwa pamoja kama timu, kuwa na ari ya timu, kufanya kazi kwa nguvu na hamasa. Hizi ni baadhi ya tunu za msingi za QNET kama biashara." 

  Katika Afrika, QNET ni mshirika wa mauzo ya moja kwa moja Ligi ya mabingwa CAF, Kombe la Shirikisho la Total CAF na Kombe la Total CAF Supa Cup (Total CAF Champions League, Total CAF Confederation Cup and the Total CAF Super Cup) 

  QNET inaendelea kupanua uwepo wake katika sehemu mbalimbali katika bara la Afrika, huku ikiwa inatoa fursa za ujasiriamali kwa watu na kuwasaidia kubadilisha maisha yao kuwa bora zaidi. Mbali na ushirika katika michezo, QNET vile vile ni kampuni ambayo imewekeza katika kuwajibika kwa jamii, kurudisha na kutoa kwaajili ya manufaa ya jamii na jambo hili linafanyika katika maeneo yote ambako QNET inaendesha shughuli zake. 

   Katika mwezi Novemba mwaka 2018, Kampuni ya QNET ilitunukiwa tuzo ya e-Commerce CSR Company kuwa ni kampuni bora ya biashara ya mtandao kwa mwaka huo, ambayo ilitolewa na Kituo cha Uwajibikaji wa Mashirka kwa Jamii cha Afrika Magharibi (Centre for Corporate Social Responsibility West Africa.)


  0 0

  Mkurugenzi wa Miundo mbinu katika Sekretarieti ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini Mwa Afrika ( SADC), Mapolao Makoena akizungumza wakati wa mkutano na Waandishi wa habari za SADC katika kituo cha mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC),kuhusu uboreshaji wa miundombinu hasa kwa nchi wanachama wa SADC,Makoena amempongeza Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kuzindua ujenzi wa mradi mkubwa uzalishaji wa umeme mtoto Rufiji,amesema mradi huo ni wa kujivunia sana na kwamba ukikamilika utasaidia kuondoa changamoto ya nishati hiyo katika nchi wanachama wa SADC na nchi Wanachama wa Afrika Mashariki. Picha na Michuzi Jr.
  Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara na Viwanda katika Sekretarieti ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini Mwa Afrika ( SADC), ,Calicious Tutalife akizungumza wakati wa mkutano na Waandishi wa habari za SADC katika kituo cha mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC),Kuhusu uwezeshaji wa biashara huria sambamba na uwepo wa upatikanaji wa ushindani na maendeleo ya Viwanda anuai,kuongezeka kwa uwekezaji wa viwanda na tija,kufuata ubora na viwango vilivyowekwa Kimataifa katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini Mwa Afrika ( SADC),
  Kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara na Viwanda katika Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini Mwa Afrika ( SADC),Calicious Tutalife,Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano- SADC Barbara Lopi na Mkurugenzi wa Miundo mbinu katika Sekretarieti ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini Mwa Afrika ( SADC), Mapolao Makoena .
   
  Wanahabari wakisikiliza yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo   Ujenzi wa mradi wa umeme katika Mto Rufiji umetajwa kuwa wa mfano katika nchi za SADC na nchi wanachama wa Afrika Mashariki wa EAC, kutokana na namna Serikali ilivyoamua kuusimamia. 

  Akizungumza katika kituo cha mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar  leo na Wanahabari , Mkurugenzi wa Miundo mbinu katika Sekretarieti ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini Mwa Afrika ( SADC), Mapolao Makoena  amesema mradi huo mkubwa unaojengwa nchini ni wa kipekee, ambao unasimamiwa moja kwa moja na Serikali na unagharamiwa na fedha za ndani. 

  “Mradi huu mkubwa wa Rufiji ni jambo la kujivunia, sisi SADC tunajivunia na si kwa SADC tu, lakini pia kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), amesema mradi huo ni wa kujivunia sana na kwamba ukikamilika utasaidia kuondoa changamoto ya nishati hiyo katika nchi wanachama wa SADC na nchi Wanachama wa Afrika Mashariki.

  Mokoena amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa uthubutu wake wa kutekeleza mradi huo mkubwa wa umeme, ambao utasaidia kupunguza tatizo la umeme katika nchi za SADC huku akisema SADC inamuunga mkono katika utekelezaji wa mradi huo mkubwa wa umeme. 

  Amesema mradi huo unaonesha unatoa funzo kwamba uongozi unahusika katika kuhakikisha miradi yenye tija inasimamiwa kwa nguvu zote ili kuzinasua nchi zetu katika matatizo ambayo yanaweza kutatuliwa kwa uwezo wa ndani. 

  Mokoena amesema kutokana na uhaba wa nishati unaozikabili nchi nyingi wanachama wa SADC, juhudi za ziada zinahitajika kuboresha upatikanaji wa nishati, ambayo ni muhimu katika kutimiza malengo ya uwekzaji katika viwanda na uzalishaji wa bidhaa. 

  Amesema miongoni mwa mikakati muhimu ya SADC kwa sasa ni kuhakikisha kuwa na uhakika wa nishati rahisi, yenye uhakika, gharama ya chini, kupitia mpango maalumu uliowekewa ukomo wa mwaka 2027.


  0 0

  Benki ya NMB imetoa msaada wenye thamani ya zaidi ya sh 50 milioni kwaajili ya kusaidia sekta za afya na elimu katika wilaya za Musoma na Butiama mkoani Mara. 

  Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo meneja wa NMB kanda ya ziwa Agustino Abraham alisema kuwa lengo la kutoa msaada huo nikutaka kuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha huduma za kijamii hususan katika sekta ya elimu na afya. 

  Alisema kuwa benki yake imeamua kusaidia sekta hizo hasa ikizingatiwa kuwa serikali ya awamu ya tano ina sera ya uchumi wa viwanda na kwamba sera hiyo haiwezi kufanikiwa endapo sekta za afya na elimu hazitakuwa imara. 

  Alisema kuwa kutokana na umuhimu wa sekta hizo katika ukuaji wa uchumi wa taifa na jamii kwa ujumla benki yake imekwisha tumia zaidi ya sh 550 milioni kuboresha sekta hizo nchini kati ya sh 1 bilioni ambazo zimetengwa na NMB kwaajili ya kutoa msaada katika sekta hizo mwaka huu. 

  Alisema kuwa msaada uliokabidhiwa ni pamoja na madawati , vitanda kwaajili ya wagonjwa na vingine kwaajili ya akinamama kujifungulia pamoja na mabati huku akisema kuwa msaada huo itanufaisha shule tatu za Msingi na tatu za sek9dari pamoja n.a. vituo vitatatu vya afya katika wilayani Musoma na Butiama.

  Akipokea msaada huo, Mkuu wa mkoa wa Mara Adam Malima aliishukuru benki hiyo ambapo alisema kuwa serikali imepanga kuboresha sekta za afya na elimu lakini juhudi hizi zinahitaji ushirikiano kutoka kwa wadau mbalimbali zikiwemo taasisi za kifedha. 

  Malima alisema kuwa pamoja na kupokea msaada huo lakini serikali mkoani Mara bado inahitaji msaada na ushirikiano mkubwa kutoka kwa benki hiyo ili kuweza kuboresha mazingira ya elimu hususuan kwa watoto wa kike.

  Alisema kuwa kutokana na mkoa wa Mara kuwa miongoni mwa mikoa inayoongoza kwa vitendo vya ukatili , serikali mkoani humo imepanga kujenga makambi maalum maarufu kwa jina la nyumba salama kwa ajili ya kuwahifadhi watoto wa kike Ile waweze kuepukana na vitendo vya ukatili ambavyo kwa namna moja ama nyingine vimekuwa vikisababisha watoto wengi wa kike kuacha masomo na hivyo kushindwa kutimiza ndoto zao za elimu.

  Malima pia ameitaka benki hiyo kusaidia katika kuboresha sekta ya kilimo kupitia mfumo wa NMB foundation kwa maelezo kuwa sekta ya kilimo ikiimarika ni dhahiri kuwa umasikini katika jamii utakuwa umetokomezwa na hivyo kufikia lengo la serikali la kuboresha maisha ya watanzania.

  Akizungumza is niaba ya walimu walionufaika na msaada huo, Mkuu wa shule ya Sekondari ya Buhare iliyopo manispaa ya Musoma, Jonas Zakayo alishukuru NMB kwa msaada huo ambao alismea kuwa uatsaid8a katika kuboresha elimu na taaluma katika shule hizo.

  Alisema kuwa pamoja na jitihada zinazofanywa na serikali katika kuboresha elimu lakini bado zipo changamoto mbalimbali ambazo zinatakiwa kutatuliwa kwa kushirikiana na wadau ili.elimu iweze kutolewa katika mazingira mazuri kwa manufaa ya kizazi kilichopo na kijacho.

  Mkuu wa Mkoa wa Mara Adam Malima (kulia) akipokea moja ya vitanda vya kawaida vya hospitali kutoka kwa Meneja wa Kanda ya Ziwa wa NMB Abraham Augustino, kwenye hafla iliyofanyika katika Shule ya Sekondari Buhare. Benki hiyo imetoa msaada wa Sh 50Milioni ikijumuisha viti na meza 300 kwa ajili ya Shule sita, mabati 222 kwa ajili ya shule moja, vitanda vya kujifungulia, mashuka na vitanda vya kawaida vya hospitali kwa ajili ya vituo vya afya vitatu vyote mkoani Mara.
  Mkuu wa Mkoa wa Mara Adam Malima (wa pili kulia),Katibu Tawala wa mkoa huo Caroline Mthapula (kulia) wakipokea moja ya madawati zilizotolewa na NMB kutoka kwa Meneja wa Kanda ya Ziwa wa NMB Abraham Augustino (wa pili kushoto) na Meneja wa tawi la NMB Musoma Sebastian Kayaga (kushoto) , kwenye hafla iliyofanyika katika Shule ya Sekondari Buhare. Benki hiyo imetoa msaada wa Sh 50Milioni ikijumuisha viti na meza 300 kwa ajili ya Shule sita, mabati 222 kwa ajili ya shule moja, vitanda vya kujifungulia, mashuka na vitanda vya kawaida vya hospitali kwa ajili ya vituo vya afya vitatu mkoani Mara.
  Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Buhare, wakibeba viti baada ya kukabidhiwa na Benki ya NMB, katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika shuleni hapo. Benki hiyo imetoa msaada wa Sh50 milioni ikijumuisha viti na meza 300 kwa ajili ya Shule sita, mabati 222 kwa ajili ya shule moja, vitanda vya kujifungulia, mashuka na vitanda vya kawaida vya hospitali kwa ajili ya vituo vya afya vitatu vyote mkoani Mara

  Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Buhare wakijisomea kipeperushi cha Benki ya NMB shuleni hapo wakati wa hafla ya kupokea msaada. Benki hiyo imetoa msaada wa Sh 50Milioni ikijumuisha viti na meza 300 kwa ajili ya Shule sita, mabati 222 kwa ajili ya shule moja, vitanda vya kujifungulia, mashuka na vitanda vya kawaida vya hospitali kwa ajili ya vituo vya afya vitatu vyote mkoani Mara   0 0

  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mshauri wa Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Abdalla Mwinyi alipowasili katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Taifa Kampasi ya Bertras, kuhudhuria Sala ya Eid El Hajj.(Picha na Ikulu)
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,.Dk.Ali Mohamed Shein, akijumuika na Waumini wa Dini ya Kiislam katika Sala ya Eid El Hajj iliofanyika katika viwanja Chuo Cha Taifa SUZA Kampasi ya Bertars Wilaya ya Magharibi A Unguja, (Picha na Ikulu).

  BAADHI ya Waumini wa Dini ya Kiislam wakifuatilia hutba ya Sala ya Eid El Hajj iliofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Taifa SUZA Kampasi ya Betras Wilaya ya Magharibi A Unguja.(Picha Ikulu).
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi, wakifuatilia hutba ya Sala ya Eid El Hajj katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar Kampasi ya Betras Wilaya ya Magharibi Unguyja ikisomwa na Sheikh Tawaha Huein Twaha baada ya kumalizika kwa Sala hiyo.
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein na kulia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi na Viongozi wa Dini na Serikali wakiitikia dua ikisomwa na Kadhi Dhamana wa Wilaya ya Magharibi A Unguja Sheikh Othman Haji Chum.(Picha na Ikulu)
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Alhajj Ali Mohamed Shein, akihutubia Baraza la Eid El Hajj katika viwanja vya Dole Wilaya ya Magharibi A Unguja.
  KADHI Dhamana wa Wiliya ya Magharibi A Unguja Sheikh Othman Haji Chum akisoma dua baada ya kumalizika kwa Sala ya Eid El Hajj iliofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Taifa SUZA Kampasi ya Bertras Wilaya ya Magharibi A Unguja.(Picha na Ikulu).


  0 0

  Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wakiwa katika picha ya pamoja.Picha na Michuzi JR.

  ====  =====  =====  =====

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi amekabidhiwa uenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa jumuiya hiyo na Naibu Waziri Mkuu wa Namibia na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Mhe. Netumbo Nandi- Naitwah aliyemaliza muda wake ikiwa ni sehemu ya mkutano huo utakaohitimishwa na wakuu wa nchi wanachama Agosti 17 na 18, 2019.
  Naibu Waziri Mkuu wa Namibia na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Mhe. Netumbo Nandi- Naitwah (kulia) akimkabidhi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi kijiti cha uenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) iliyofanyika mapema leo Agosti 13, 2019 wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mawaziri wa Nchi za SADC unaondelea jijini Dar es Salaam, Tanzania. Ambapo Tanzania ni mwenyeji wa Mkutano huo wa 39.
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi (kushoto) akipokea ngao ikiwa ni ishara ya kuupokea uenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi (kushoto) akipokea ngao ikiwa ni ishara ya kuupokea Uenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
  Naibu Waziri Mkuu wa Namibia na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Mhe. Netumbo Nandi- Naitwah akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Mawaziri wa Nchi za SADC unaondelea jijini Dar es Salaam, Tanzania. Ambapo Tanzania ni mwenyeji wa Mkutano huo wa 39.
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi akitoa hotuba yake mara baada ya kukabidhiwa uenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) iliyofanyika mapema leo Agosti 13, 2019 wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mawaziri wa Nchi za SADC unaondelea jijini Dar es Salaam, Tanzania. Ambapo Tanzania ni mwenyeji wa Mkutano huo wa 39.
  Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC),Dkt.Stergomena Tax akizungumza katika Mkutano wa baraza la Mawaziri wa jumuiya hiyo jijini Dar leo.
  Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wakifuatilia kwa makini ufunguzi huo.
  Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo.
  Meza kuu ikifuatilia jambo
  Meza kuu ikifuatilia moja ya video maalum iliondaliwa katika mkutano huo
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) akitoka nje ya Ukumbi kwa ajili ya tukio la kupiga picha. 
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi akizungumza na Waandishi wa Habari nje ya ukumbi mara baada ya kukabidhiwa uenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliyofanyika mapema leo Agosti 13, 2019 jijini Dar es Salaam, Tanzania. Ambapo Tanzania ni mwenyeji wa Mkutano huo wa 39.Picha na Michuzi JR.

  0 0


  Na Said Mwishehe,Michuzi TV

  WAZIRI wa Nishati Dk.Medard Kalemani ameeleza kwa kina mkakati wa Serikali ya Tanzania kuhusu namna ambavyo imejipanga kuhakikisha kunakuwa na umeme wa kutosha, uhakika , gharama nafuu na unaotabirika huku akitumia nafasi hiyo kueleza kwa kina namna ambavyo wamejipanga kuuza umeme kwa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika(SADC).

  Dk.Kalemani amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati anazungumza na waandishi wa habari waliohudhuria uzinduzi wa machapisho matano yaliyotayarishwa na Kituo cha Utafiti kwa nchi za SADC ambapo moja ya machapisho hayo yanazungumzia mkakati wa nishati ya meme wa uhakika kwa nchi za jumuiya hiyo katika kuleta maendeleo.

  Akifafanua zaidi ,Waziri Kalemani amesema kuwa katika eneo la nishati ya umeme kuna mambo manne makubwa na kwamba jambo la kwanza kama nchi ni kujihakikishia kuwa na umeme wa kutosha kwa ajili ya kuleta maendeleo kupitia uchumi wa viwanda.Mbili umeme unaotabirika, tatu wa uhakika na nne wa bei nauu.

  "Kwa sasa upande wa Tanzania kuna mambo matatu likiwemo la makubaliano ya nchi za SADC kwamba kila nchi ijenge miundombinu ya umeme ambayo itaunganisha kati ya nchi na nchi. Kama nchi kwa upande wetu Tanzania tumeweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha tunakuwa na umeme wa kutosha lakini wakati huo huo tumeangalia na malengo ya nchi za SADC na katika eneo hilo tumeweka majukumu ya kuzalisha umeme megawati 10,000 ifikapo mwaka 2025,"amesema Waziri Kalemani.

  Amefafanua katika kuhakikisha kunakuwa na umeme wa kutosha kwa ajili ya kuuza kwa nchi za jumuiya hiyo Serikali imeweka mkakati wa kutumia umeme mchanganyiko ukiwemo wa gesi asili na umeme unatokana na maji."Katika eneo la gesi asilia pamoja na gesi iliyopo , pia tunaendelea kuvumbua gesi na tunazo futi za ujazo trilioni 57 .54 na kati hizo futi za ujazo trilioni 8.8 zitatumika kuzalisha umeme.

  " Pia kuna chanzo cha maji na kupitia utafiti ambao umefanyika kwa miaka mitano imeonekana tunaweza kuzalisha mpaka megwati 4,000 na tayari tumeanza na maporomoko ya mto Rufiji ambapo tutatalisha mgewati 2,115.Mradi wa umeme wa maporomoko ya Mto Rufiji ni wa kwanza na wa kihistoria kwa ukubwa nchini Tanzania, ni bwawa la kwanza la kuzalisha umeme Afrika Mashariki, ni bwawa la nne kwa Bara la Afrika na kwa dunia ni kati ya mabwawa 70 makubwa ya kuzalisha umeme mwingi,"amesema Dk.Kaleman.

  Ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa kwa mara ya kwanza katika nchi za SADC zimeingia kwenye historia ya kuwa na mabwawa makubwa ya kuzalisha umeme."Tumeanza na mradi huu wa umeme wa maporomoko ya bonde la mto Rufiji kwasababu tunakwenda kuleta mambo manne ambayo ni ya umeme wa umeme, unaotosheleza, unbaotabirika na gharama nafuu,".

  Amefafanua kuwa sehemu ya pili ni kwamba unapokuwa na umeme wa kutosha na gharama na fuu unaweza kusambaza sehemu nyingi na kwa gharama nafuu, hivyo mkakati ulipo ni kujenga miundombinu ya kuusafirisha .

  "Kwa sasa katika nchi yetu tunajenga miundombinu ya kusafirisha umeme kwenye kona zote nne za nchi yetu.Tunafahamu ajenda hapa ni kuzalisha umeme wa uhakika na kusambaza, hivyo ni muhimu kujenga miundomboni ya kusambaza umeme huo,"amesema Dk.Kalemani huku akitaja baadhi ya kona hizo ni ile ya kutoka Dar es salaam kwenda Kaskanini.

  Wakati kona ya pili amesema ni kuutoa umeme kutoka Iringa, Mbeya, Sumbawanga, Kigoma mpaka Nyakanazi.Pia amesema kuna mradi wa umeme wa kilovoti 400 ambao unatoka Mkoa wa Iringa kwenda Mbeya ambao unaweza kwenda mpaka nchini Malawi na tayari wamepata fedha kutoka Benki ya Dunia."Makubaliano ya nchi za SADC ni kuuziana umeme kulingaa na mahitaji".

  Amesisitiza kuna mkakati wa mradi wa kusafirisha umeme kati ya Zambia ,Tanzania na Kenya na tayari umeshaanza. "Na huu mradi ni muhimu katika kuunganisha umeme kwa nchi za SADC, hivyo mradi wa umeme bonde la Rufuji unatakapokamilika tutauuza kwa nchi nyingine za jumuiya ikiwemo nchi ya Malawi,Zambia na Congo DRC".

  Hata hivyo amefafanua kukiwa na umeme wa kutosha maana yake maeneo mengi ya vijiji yatakuwa na umeme wa uhakika na hivyo kutaisaidia kupunguza uharibifu wa mazingira huku akieleza kuna mikakati mbalimbali ya kuhakikisha nishati ya umeme na gesi asili inatumika katika maeneo yote nchini.

  Ametumia nafasi hiyo kutoa rai kwa nchi za SADC kuhakikisha zinaweka mikakati madhubuti ya kuunganisha umeme kwenye maeneo ya vijiji ili kuondoa changamoto ya uharibifu wa mazingira.

  WAZIRI wa Nishati Dk.Medard Kalemani akizungumza na waandishi wa habari waliohudhuria uzinduzi wa machapisho matano yaliyotayarishwa na Kituo cha Utafiti kwa nchi za SADC ,ambapo moja ya machapisho hayo yanazungumzia mkakati wa nishati ya meme wa uhakika kwa nchi za jumuiya hiyo katika kuleta maendeleo.

  Kalemani ameeleza kwa kina mkakati wa Serikali ya Tanzania kuhusu namna ambavyo imejipanga kuhakikisha kunakuwa na umeme wa kutosha, uhakika , gharama nafuu na unaotabirika huku akitumia nafasi hiyo kueleza kwa kina namna ambavyo wamejipanga kuuza umeme kwa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika(SADC).
  WAZIRI wa Nishati Dk.Medard Kalemani akisalimiana na Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya SADC,Dkt . Stragomena Tax kabla ya uzinduzi wa machapisho  matano yaliyotayarishwa na Kituo cha Utafiti kwa nchi za SADC 
  WAZIRI wa Nishati Dk.Medard Kalemani (kulia) pamoja na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakiyasoma baadhi ya majarida kabla uzinduzi wa machapisho matano yaliyotayarishwa na Kituo cha Utafiti kwa nchi za SADC  
    WAZIRI wa Nishati Dk.Medard Kalemani (kulia) akimsikiliza wakati akimueleza jambo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kabla ya uzinduzi wa machapisho matano yaliyotayarishwa na Kituo cha Utafiti kwa nchi za SADC

  Baadhi ya Wageni waalikwa wakiwemo wanahabari wakiwa ukumbini humo kushuhudia uzinduzi wa machapisho matano yaliyotayarishwa na Kituo cha Utafiti kwa nchi za SADC .Picha na Michuzi JR.

  0 0

  Mamia ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam hii leo Jumatano Agosti 14, wamejitokeza kwa wingi ili kuungana na Benki ya Exim Tanzania ambayo kwa kushirikiana na Mpango wa Taifa wa Damu Salama (NBTS) waliendesha zoezi la uchangiaji damu kwa ajili kuwasaidia majeruhi wa ajali ya moto iliyosababishwa na lori la mafuta lililopinduka na kulipuka eneo la Msamvu Mkoani Morogoro ambapo watu zaidi ya 70 walifariki dunia na wengine kujeruhiwa.

  Zoezi hilo litakalodumu kwa siku tatu mfululizo limefanyika kwenye viunga vya Stendi ya mabasi ya Mbagala jijini Dar es Salaam ambapo imeshuhudiwa idadi kubwa ya wakazi wa jiji hilo wakijitokeza kwa wingi ili kujitolea damu huku wadai kuwa muitikio huo umetokana na kuguswa kwao na tukio hilo la kusikitisha lililotokea mkoani Morogoro.

  Meneja Masoko na Mahusiano ya jamii wa Benki ya Exim, Bw Abdulrahman Nkondo (alievaa kofia nyeupe) akiwagawia vinywaji baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliojitokeza kwa wingi kwenye viunga vya Stendi ya mabasi ya Mbagala jijini Dar es Salaam ili kuchangia damu kwa ajili ya majeruhi wa ajali ya moto iliyosababishwa na lori la mafuta lililopinduka na kulipuka eneo la Msamvu Mkoani Morogoro ambapo watu zaidi ya 70 walifariki dunia na wengine kujeruhiwa. Zoezi hilo la siku tatu limeratibiwa na benki hiyo kwa kushirikiana na Mpango wa Taifa wa Damu Salama (NBTS)na linatarajiwa kukamilika Agosti 16.  Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliojitokeza kwenye viunga vya Stendi ya mabasi ya Mbagala jijini Dar es Salaam wakifuata taratibu ili kuchangia damu kwa ajili ya majeruhi wa ajali ya moto iliyosababishwa na lori la mafuta lililopinduka na kulipuka eneo la Msamvu Mkoani Morogoro ambapo watu zaidi ya 70 walifariki dunia na wengine kujeruhiwa. Zoezi hilo la siku tatu limeratibiwa na benki ya Exim Tanzania kwa kushirikiana na Mpango wa Taifa wa Damu Salama (NBTS)na linatarajiwa kukamilika Agosti 16.
   

  0 0


  Charles James, Michuzi TV

  WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka 20 ya siku ya kimataifa ya vijana kwa mwaka 2019 ambayo yatafanyika Jijini Dodoma.

  Akitoa taarifa kwa wanahabari Meneja program ya vijana na maendeleo kutoka UNFPA- Tanzania Dkt Majaliwa Marwa, amesema katika maadhimisho hayo yanayowezeshwa na UNFPA, UNESCO, ILO na UNIC yana lengo la kuhakikisha vijana wanajengewa uwezo na kuwa na ubunifu mbalimbali.

  Amesema maadhimisho hayo yatashirikisha vijana zaidi ya mia tano kutoka Tanzania bara na visiwani na kwa mwaka huu wamejikita zaidi katika kutilia mkazo kuhusu elimu kwa vijana.

  “Mwaka huu ni maadhimisho ya 20 ya siku ya vijana kimataifa na mwaka huu tumejikita katika elimu ili kuwajengea vijana uwezo na kuwa wabunifu kuweza kujitegemea, dhamira Tanzania iliyopendekezwa kuelekea 2030 ni Tanzania ya viwanda boresha elimu kwa ajili ya maendeleo ya vijana.

  “Tarehe 15 tutakuwa na kongamano litakuwa na mada mabalimbali ikihusisha ubunifu na afya ya uzazi kwa vijana, na siku ya pili kutakuwa na tamasha litakuwa katika eneo la Chang’ombe eneo lenye mkusanyiko wa vijana wengi na kutakuwa na burudani nyingi” amesema.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Shirika la RESLESS DEVELOPMENT, chini ya mradi wa Kijana wajibika kwa mkoa wa Dodoma, Ridhiwani Juma amesema wao kama wenyeji wameweza kuratibu na kuhakikisha hata vijana wenye mahitaji maalumu nao wanakuwa sehemu ya mmaadhimisho hayo.

  Muwakilishi wa vijana ambaye ni katibu Afriyan Tanzania, Seif Ibrahimu amesema kundi la vijana linakabiliwa na tatizo la ukosefu wa ajira kwa kiasi kikubwa.
  Meneja Program Maalum ya vijana kutoka Umoja wa Mataifa, Dk Majaliwa Marwa akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dodoma leo kuhusiana na kongamano la vijana litakalofanyika kesho ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu, Mhe Kassim Majaliwa

older | 1 | .... | 1869 | 1870 | (Page 1871) | 1872 | 1873 | .... | 1904 | newer