Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1865 | 1866 | (Page 1867) | 1868 | 1869 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Meneja Mwandamizi wa Benki ya NMB Idara ya Biashara Makao Makuu, Bw. Wogofya Mfalamagoha akimkabidhi cheti maalum cha pongezi kwa kufanya biashara kwa uaminifu, Bi. Salome Shayo kilichotolewa na Benki ya NMB kwenye Kongamano la Klabu ya Biashara ya NMB wilayani Kibaha jana. 
  Meneja wa NMB Kanda ya Mashariki, Baraka Ladislaus (wa pili kushoto) akimkabidhi cheti maalum cha pongezi kwa kufanya biashara kwa uaminifu, mmoja wa wafanyabiashara kilichotolewa na Benki ya NMB kwenye Kongamano la Klabu ya Biashara ya NMB wilayani Kibaha jana.
   
  Meneja wa NMB Kanda ya Mashariki, Baraka Ladislaus (katikati) akizungumza na wafanyabiashara kwenye Kongamano la Klabu ya Biashara ya NMB wilayani Kibaha jana. Kushoto ni Meneja Mwandamizi wa Benki ya NMB Idara ya Biashara Makao Makuu, Bw. Wogofya Mfalamagoha pamoja na Meneja wa Benki ya NMB Kibaha, Hosea Lyatou (wa kwanza kulia) wakifuatilia warsha hiyo. 
  Meneja Mwandamizi wa Benki ya NMB Idara ya Biashara Makao Makuu, Bw. Wogofya Mfalamagoha (kulia) akizungumza na wafanyabiashara hao(hawapo pichani). 
  Meneja Mahusiano Biashara wa Benki ya NMB, Kanda ya Mashariki, Bi. Prisca Lius (kushoto) akijibu baadhi ya maswali ya wafanyabiashara (hawapo pichani) kwenye Kongamano la Klabu ya Biashara ya NMB wilayani Kibaha. Kongamano hilo lililokuwa na kaulu mbiu ya 'Habaki Mtu...tunasonga Mbele Paamoja' liliandaliwa na Benki ya NMB. 
  Meneja wa Benki ya NMB Kibaha, Hosea Lyatou (kulia) akimpongeza mmoja wa wafanyabiashara (kushoto) mara baada ya kutunukiwa cheti maalum na Benki ya NMB kwa kufanya vizuri zaidi katika biashara yake. 
  Mkurugenzi Mtendaji wa True Maisha Training Company, Erick Chrispin aakiwasilisha mada kwenye Kongamano la Wafanyabiashara lililoandaliwa na Benki ya NMB Wilayani Kibaha. 
  Mmoja wa washiriki katika Kongamano la Klabu ya Biashara ya NMB wilayani Kibaha akiuliza swali jana mara baada ya kupata mafunzo namna ya kukuza biashara zao. Kongamano hilo lililokuwa na kaulu mbiu ya 'Habaki Mtu...tunasonga Mbele Paamoja' liliandaliwa na Benki ya NMB. 
  Baadhi ya washiriki katika Kongamano la Klabu ya Biashara ya NMB wilayani Kibaha wakiuliza maswali mara baada ya kupata mafunzo namna ya kukuza biashara zao. Kongamano hilo lililokuwa na kauli mbiu ya 'Habaki Mtu...Tunasonga Mbele Pamoja' liliandaliwa na Benki ya NMB. 
  Meneja Mikopo NMB Kibaha, Alfred Matovelo akizungumza na wafanyabiashara katika kongamano hilo. 
  Sehemu ya washiriki katika Kongamano la Klabu ya Biashara ya NMB wilayani Kibaha wakifuatilia mada mbalimbali kwenye Kongamano hilo lililokuwa na kauli mbiu ya 'Habaki Mtu...Tunasonga Mbele Pamoja' liliandaliwa na Benki ya NMB.

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na wafanyabiashara wa nyama katika eneo la Mbande mkoani Dodoma mara baada ya kuzungumza nao.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wafanyabiashara pamoja na Wananchi wa Mbande hawaonekani (pichani) katika Njiapanda ya Kongwa mara baada ya kusimama wakati akitokea Kongwa mkoani Dodoma.
  Wafanyabiashara pamoja na Wananchi wa Mbande mkoani Dodoma wakishangilia wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli wakati aliposimama na kuzungumza nao katika eneo hilo la Mbande.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akicheza mziki kwenye gari wakati akiondoka eneo la Mbande mara baada ya kuwasalimia wananchi wa eneo hilo.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na wafanyabiashara wa nyama katika eneo la Mbande mkoani Dodoma mara baada ya kuzungumza nao.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi pamoja na wafanyabiashara wadogo wadogo Wamachinga katika eneo la Mbande mnadani wakati akitokea Kongwa mkoani Dodoma.
  Mfanyabiashara ndogondogo Lukas Chanzi akimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli wakati akizungumza katika eneo hilo la mnadani Mbande mkoani Dodoma. PICHA NA IKULU 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi pamoja na wafanyabiashara wadogo wadogo Wamachinga katika eneo la Mbande mnadani wakati akitokea Kongwa mkoani Dodoma.


  0 0  Benki ya TPB imetoa msaada wa rangi ndoo 50 katika shule ya Sekondari Buluba iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga kwa ajili ya kupendezesha mandhari ya shule hiyo na kuiweka katika mazingira mazuri ili wanafunzi wajisomee kwa bidii na kupata ufaulu mzuri.Msaada wa ndoo za rangi umetolewa leo Julai 18,2019 shuleni hapo na Mkurugenzi wa Masoko kutoka makao makuu ya benki ya TPB, Deogratius Kwiyuka akimwakilisha Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo Sabasaba Moshigi na kuhudhuriwa pia na Uongozi wa Chama Kikuu cha Ushirika (SHIRECU) ambao ndiyo wamiliki wa shule hiyo. Akizungumza kwenye hafla hiyo fupi ya makabidhiano hayo,Mkurugenzi wa Masoko wa Benki hiyo Kwiyuka, amesema wanaunga Juhudi za serikali ya awamu ya tano ya kuboresha elimu hapa nchini, hivyo wao kama wadau wakubwa wa elimu wakaona ni vyema kutoa msaada huo wa rangi ili kuboresha mandhari nzuri ya shule hiyo ya sekondari Buluba. Amesema shule inapokuwa katika mandhari nzuri inaleta ari ya wanafunzi kufanya vizuri kwenye masomo yao na kupata ufaulu mkubwa, huku akitoa wito kwa wanafunzi wa shule hiyo ya Sekondari Buluba kujituma kwenye masomo ili waje kuwa tegemezi katika familia zao na taifa kwa ujumla. “Benki ya TPB huwa tunahusika na masuala ya Ustawi wa Jamii, Afya pamoja na Elimu, hivyo kutokana na sisi kuwa wadau wakubwa wa elimu tumetoa sehemu ya faida ya beki ili kutoa msaada huu wa rangi kwa ajili ya kupendezesha shule ya Sekondari Buluba na kuiweka katika mandhari nzuri,”amesema Kwiyuka. Naye Mwalimu wa Shule hiyo, Emmanuel Kazyoba akisoma risala ya shule hiyo, amesema ina miaka 50 ambapo inakabiliwa na changamoto ya uchakavu wa miundombinu na kupongeza msaada huo wa rangi ambao utasaidia kuipendezesha shule hiyo. Amesema licha ya kukabiliwa na uchakavu wamekuwa wakifanya vizuri kwenye masomo ambapo matokeo ya kidato cha sita mwaka huu (2019), daraja wa kwanza wamefaulisha wanafunzi 4, daraja la pili 24, la tatu 46, la nne 10 pamoja na zero moja, Kwa upande Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika mkoani Shinyanga (SHIRECU) Richard Luhende ambaye pia ni mwenyekiti wa bodi wa shule hiyo, amepongeza msaada huo wa rangi na kuahidi kuendelea kusimamia ufaulu wa shule ambapo wametoka kwenye zero saba mwaka jana hadi moja. Na Marco Maduhu - Malunde 1 blog


  TAZAMA PICHA HAPA CHINI Mkurugenzi wa Masoko kutoka Benki ya TPB Makao makuu Deogratius Kwiyuka, akizungumza wakati wa kukabidhi ndoo za rangi 50 kwenye shule ya sekondari Buluba Shinyanga Mjini kwa ajili ya kupendezesha shule hiyo na kuwa katika mazingira mazuri na kuongeza ufaulu kwa wanafunzi. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog Meneja wa Benki ya TPB tawi la Shinyanga, Faraji Basu, akizungumza kwenye kukabidhi ndoo za rangi 50 katika shule hiyo ya sekondari Buluba. Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika mkoani Shinyanga (SHIRECU), Richard Luhende ambaye pia ni mwenyekiti wa bodi wa shule ya sekondari Buluba, akishukuru kwa msaada huo wa ndoo za rangi, na kuahidi kuendelea kuboresha miundombinu ya shule hiyo. Ndoo za rangi 50 zikiandaliwa kwa ajili ya kukabidhiwa kwenye shule ya Sekondari Buluba. Mkurugenzi masoko kutoka Benki ya TPB Makao makuu Deogratius Kwiyuka (kulia) akikabidhi ndoo za rangi 50 kwa ajili ya kupendezesha shule ya Sekondari Buluba, katikati ni Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika mkoani Shinyanga (SHIRECU) Richardi Luhende ambaye pia ni mwenyekiti wa bodi wa shule hiyo na Meneja wa (SHIRECU) Ramadhani Kato wakipokea rangi hizo. Mkurugenzi wa masoko kutoka benki ya TPB Deogratius Kwiyuka katikati akikabidhi ndoo za rangi 50 katika shule ya Sekondari Buluba kama sehemu ya faida kwenye benk hiyo, wa kwanza kulia ni mwanafunzi Thomas Majuto,na mwisho kushoto ni meneja wa (SHIRECU) Ramadhani Kato, akifuatiwa na mwenyekiti wa SHIRECU Richard Luhende. Mkurugenzi wa masoko kutoka benk ya TPB makao makuu Deogratius Kwiyuka, akizungumza jambo wakati wa hafla fupi ya kukabidhi rangi ndoo 50 katika shule ya Ssekondari Buluba. Meneja wa Chama Kikuu cha Ushirika (SHIRECU) Mkoani Shinyanga Ramadhani Kato akishukuru kwa kupokea msaada huo wa ndoo za rangi zilizotolewa na benki ya TPB kwa ajili ya kuweka mandhari nzuri ya shule hiyo. Awali Mwalimu wa shule ya Sekondari Buluba Emmanuel Kazyoba, akisoma taarifa ya shule hiyo na kuelezea kuwepo na changamoto ya uchakavu wa majengo ambapo rangi hizo zitasaidia kuiweka shule katika mandhari nzuri. Mwanafunzi Thomas Majuto akishukuru kwa niaba ya wanafunzi wa shule ya sekondari Buluba kuhusu msaada huo wa rangi na kuahidi kujituma kusoma kwa bidii ilikuongeza ufaulu katika shule hiyo. Wanafunzi wa shule ya Sekondari Buluba wakiwa kwenye hafla ya makabidhiano ya msaada wa rangi ndoo 50 kutoka benki ya TPB. Wanafunzi wa shule ya Sekondari Buluba wakisikiliza nasaha za kusoma kwa bidii ili waje wasaidie familia pamoja na taifa kwa ujumla. Wafanyakazi wa (SHIRECU) wakiwa kwenye hafla fupi ya kukabidhiwa rangi ndoo 50 kutoka Benki ya TPB. Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchiwa Kongwa mara baada ya kuwasili wakati akitokea Chamwino mkoaniDodoma
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi waKongwa mkoani Dodoma mara baada ya kuwasili wakati akitokeaChamwino mkoani Dodoma.
  Sehemu ya Wananchi wa Kongwa wakisikiliza kwamakini hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli wakati alipokuwa akiwahutubia.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na viongozi wakidini wakati akiondoka katika eneo la Makaburi ya Ukoo wa Ndugaikatika eneo hilo la Kongwa mara baada ya kuweka shada la maua.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza katika eneo laMakaburi ya Ukoo wa Ndugai mara baada ya sala fupi iliyofanyika katikaeneo hilo.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiweka shada la maua katikakaburi la Baba mzazi wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai katika eneo la Makaburi ya Ukoo wa Ndugaiyaliyopo Chimotolo Kongwa mkoani Dodoma. PICHA NA IKULU

  0 0

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia vitabu katika maktaba iliyokarabatiwa ya Shule Kongwe ya Same Sekondari, katika mradi wa ukarabati wa shule hiyo kongwe mkoani Kilimanjaro, Julai 19.2019. Kushoto ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Same Sekondari Hoza Mgonja. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizindua mradi wa ukarabati wa shule kongwe ya Same Sekondari, iliyoko wilayani Same katika mkoa wa Kilimanjaro, Julai 19.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na wanafunzi wa Same Sekondari mara baada ya kuzindua mradi wa ukarabati wa shule hiyo kongwe, iliyoko wilayani Same katika mkoa wa Kilimanjaro, Julai 19.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akimsikiliza mwanafunzi wa Same Sekondari, Omari Pundugu, akielezea changamoto mafanikio na changamoto za shule hiyo mara baada ya uzinduzi wa mradi wa ukarabati wa shule hiyo kongwe, iliyoko wilayani Same katika mkoa wa Kilimanjaro, Julai 19.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwasalimia wananchi, baada ya kuzindua mradi wa ukarabati wa shule kongwe ya Same Sekondari, mkoani Kilimanjaro Julai 19.2019.

  *************

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka watumishi wa umma wawe na mipango ya kazi ambayo itaweza kupimika na kutoa matokeo.

  “Kila mtumishi anapaswa awe na mpango kazi katika sekta yake na ni lazima aende kupima matokeo. Awamu hii, tunataka kuona matokeo ya kazi zenu.” Ametoa kauli hiyo leo asubuhi (Ijumaa, Julai 19, 2019) wakati akizungumza na watumishi wa wilaya ya Same kwenye ukumbi wa Halmashauri ya wilaya hiyo, mjini Same. 

  “Watumishi mmeletwa kwenye wilaya hii ili muwahudumie wananchi. Tulioajiriwa, kazi yetu kubwa ni kuwatumikia wananchi bila ubaguzi wowote uwe ni wa kabila, itikadi au rangi.” 

  Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwakumbusha watumishi hao kwamba baada ya mchujo wa watumishi hewa, waliobakia wanapaswa kufanya kazi kwa bidii. “Fanyeni kazi kwa bidii, msimamo wa Serikali hii ni kwamba hatumvumilii mtumishi ambaye si mwajibikaji, ni mwizi, mzembe au anaomba rushwa. Serikali hii hatuna muda wa kujadili matatizo ya watumishi, tunamalizana hapo hapo,” amesema. 

  Amewataka watumishi hao wasimamie utekelezaji wa ahadi zilizotolewa kwenye Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi kwa sababu ndiyo chama tawala. “Mtumishi angalia sekta yako inasema nini, ifanyie kazi. Kama ni maji, tafuta ni wapi yanapatikana, changanua zinahitajika shilingi ngapi, tafuta njia ya kupata hizo fedha ili wananchi wapate maji.” 

  Kuhusu tabia ya kukaa ofisini, Waziri Mkuu amekemea tabia hiyo na kuwataka watumishi wote nchini waache tabia ya kukaa ofisini na badala yake waende vijijini kuwasikiliza wananchi. 

  “Watumishi wa umma msikae ofisini. Nendeni vijijini walau kwa siku nne za juma. Hizo mbili zinazobakia, zitumieni kuandaa taarifa. Nendeni huko ili wananchi wasipate usumbufu wa kuja hapa mjini kuwatafuta,” amesisitiza. 

  “Mkuu wa Wilaya simamia zoezi la wakuu wa idara na wasaidizi wao kwenda vijijini. Wakienda vijijini ni lazima waonane na waheshimiwa madiwani, washirikiane kusikiliza kero na kutafuta majibu kwa wananchi. Huo ndiyo mshikamano wenyewe unaohitajika,” amesema. 

  Wakati huohuo, Waziri Mkuu amewataka watumishi wa umma watambue mipaka yao na wajenge mahusiano baina yao na wengine. Alitoa kauli hiyo jana jioni (Alhamisi, Julai 18, 2019) wakati akizungumza na watumishi wa Manispaa ya Moshi, kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa. 

  “Kila mmoja lazima atambue mipaka yake na mamlaka baina yake na wengine. Hapa mko wateuliwa, waajiriwa na wachaguliwa. Kila mtu ana nafasi yake ya kuwatumikia wananchi.Aliwataka watumishi hao watambue falsafa ya Kiongozi mkuu wa nchi ambayo inahimiza uchapakazi. “Kwa hiyo tunaposema Hapa Kazi Tu, maana yake chapa kazi na tuone matokeo. Tunasisitiza kazi na tunataka kazi unayoifanya, itoe matokeo,” alisema.


  0 0

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwa ameshika jani la katani, wakati alipotembelea shamba la katani la Hassan Sisal Estate Makanya, wilayani Same katika mkoa Kilimanjaro Julai 19.2019. Anayetoa maelezo ni Meneja Mshauri wa shamba hilo, Ndekirwa Nyari.
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwa ameshika katani iliyokua imeanikwa, wakati alipotembelea shamba la katani la Hassan Sisal Estate Makanya, wilayani Same katika mkoa Kilimanjaro Julai 19.2019. Anayetoa maelezo ni Meneja Mshauri wa shamba hilo, Ndekirwa Nyari.
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwa anakagua marobota ya katani, wakati alipotembelea shamba la katani la Hassan Sisal Estate Makanya, wilayani Same katika mkoa Kilimanjaro Julai 19.2019. Kushoto ni Meneja Mshauri wa shamba hilo, Ndekirwa Nyari.
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na wafanyakazi wa shamba la katani la Hassan Sisal Estate Makanya pamoja na wananchi, wakati alipotembelea shamba hilo, wilayani Same Julai 19.2019.
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akimsikiliza Meneja Mshauri wa shamba wa shamba la katani la Hassan Sisal Estate Makanya, Ndekirwa Nyari pamoja, baada ya kutembelea shamba hilo, wilayani Same Julai 19.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

  0 0

   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akipokea treni ya mizigo, iliyowasili tokea Tanga, kwenye uzinduzi wa treni hiyo katika reli ya Kaskazini Julai 20.2019.

   Wananchi wa Moshi, wakipokea treni ya mizigo kwa furaha kubwa, wakati ikiwasili tokea TangaJulai 20.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akikata utepe kuzindua treni ya mizigo katika reli ya Kaskazini Julai 20.2019. Uzinduzi huo umefanyika katika stesheni ya reli Moshi. 
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwapungia mikono wananchi waliyofika kushuhudia uzinduzi wa treni ya mizigo katika reli ya Kaskazini uliyofanyika katika stesheni ya reli Moshi, Julai 20.2019. 
   Wananchi wa Moshi, wakishangilia kwa furaha kubwa  baada ya kupokea treni ya mizigo katika reli ya Kaskazini, wakati ikiwasili tokea TangaJulai 20.2019.


  *Apokea treni ya kwanza yenye tani 800 za saruji

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea treni ya kwanza ya mizigo kutoka Tanga ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa reli ya kutoka Tanga hadi Moshi.

  Waziri Mkuu amepokea treni hiyo leo (Jumamosi, Julai 20, 2019) ambayo iliwasili saa 4:30 asubuhi kwenye stesheni ya Moshi na kukata utepe wa uzinduzi saa 4:32, kisha akapanda kwenye treni hiyo saa 4:33.

  Akizungumza na mamia ya wakazi wa mji wa Moshi na wengine kutoka mkoa jirani wa Tanga, Waziri Mkuu amesema amefurahi kupokea treni hiyo yenye mabehewa 20 yaliyokuwa na mzigo wa tani 800 za saruji kutoka kampuni ya Saruji ya Tanga. 

  Amesema kukamilika kwa kipande cha reli ya Tanga - Moshi na kuanza kutoa huduma leo hii, ni mwendelezo wa utekelezaji wa dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano kuhakikisha miundombinu ya usafiri na usafirishaji inafaidika na fursa ya kijiografia iliyopo nchini kwa kutoa huduma za usafiri na uchukuzi wa reli kwa uhakika, usalama na kwa gharama nafuu.

  “Wataalamu wa masuala ya usafirishaji duniani wanaeleza kuwa matumizi ya reli kwa ajili ya usafirishaji wa shehena, hupunguza gharama za bidhaa kwa asilimia kati ya 30 na 40. Vilevile, matumizi ya reli huwa ni kichocheo kikubwa cha ukuaji wa uchumi kutokana na ukweli kwamba, kupitia usafiri wa reli unaweza kusafirisha mizigo mingi kwa haraka na kwa wakati mmoja kwenda kwa mlaji,” amesema.

  Amesema kama ilivyo kwa mradi wa SGR, njia ya reli ya Tanga - Moshi yenye urefu wa km. 353, ukarabati wake unagharamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na umetekelezwa na wataalamu wazawa.

  “Kwa msingi huo, naagiza viongozi na watendaji wa mikoa na maeneo ambayo yanapitiwa na reli hii, kwa kushirikiana na Shirika la Reli Tanzania, waanze mara moja kampeni ya kutoa elimu kwa umma kuhusu usalama lakini pia kuwakumbusha wananchi kuwa walinzi wa miundombinu hii muhimu ya reli,” amesema.

  Akitoa salamu kwa niaba ya makatibu wakuu wa vyama 19 vya siasa nchini, Katibu Mkuu wa ADC, Bw. Hassan Doyo alisema kufufuliwa kwa treni hiyo ya mizigo kutawasaidia wachimbaji wa madini walioko Makanya, Same ambao walikuwa wakipata taabu ya kukodisha malori na kusafirisha bidhaa zao hadi kiwanda cha saruji cha Tanga.

  Alisema reli hiyo itawanufaisha pia wachimbaji wa Kabuku, wilayani Handeni. "Wachimbaji wa madini ya chuma walioko Kabuku, walikuwa wanapata shida ya kusafirisha mizigo yao kwa barabara hadi Mtwara, gharama ziko juu mno. Lakini sasa watapata ufumbuzi baada ya reli hii kufufuliwa," alisema.

  Mapema, akitoa taarifa kuhusu mradi huo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Bw. Masanja Kadogosa alisema makadirio ya gharama za kufufua reli hiyo kutoka Korogwe hadi Arusha yalikuwa sh. bilioni 14 lakini mpaka sasa wametumia sh. bilioni 5.7.

  Alisema ujenzi huo ulifanywa na wafanyakazi wazawa 525 kutoka TRC wakiwemo vibarua 466, wahandisi 12 na mafundi wa reli na nyanja nyingine 47. "Hawa watapata ajira ya kudumu na ndiyo wataisimamia hii reli," alisema. Alisema reli ya mizigo ilikuwa haifanyi kazi kwa miaka 12 iliyopita na huduma ya kusafirisha abiria ilisitishwa tangu mwaka 1994.

  Hafla huyo ilihudhuriwa na Naibu Mawaziri wa Uchukuzi, TAMISEMI, Wabunge, watendaji wa Serikali, wawakilishi wa vyama vya siasa na wananchi mbalimbali.

  0 0  0 0

  Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe . Kassim Majaliwa amefanya ufunguzi wa njia ya reli ya Tanga mpaka Moshi / Kilimanjaro katika hafla iliyofanyika mjini Moshi , Kilimanjaro Julai 20, 2019, iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, wa vyama pamoja na wa dini.

  Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amelipongeza Shirika la Reli Tanzania -TRC kwa Kurejesha njia ya Tanga-Moshi ambayo takribani zaidi ya miaka 12 ilikuwa haifanyi kazi. Waziri Mkuu amesema kuwa mafanikio haya ni utekelezaji wa sera ya kitaifa na Mkakati wa Nchi kuinua sekta mbalimbali za kimkakati ili inchi ya Tanzania ifikie Uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

  Waziri mkuu aliongeza kuwa juhudi na kujitoa kulikofanyika kurejesha njia ya reli kuanzia Dar es Salaam hadi Tanga na kisha kuelekea Moshi ,Kilimanjaro ni uamuzi wa busara uliokuja kwa wakati na unaoshamirisha azima yetu ya kuchochea ukuaji wa uchumi lakini na kuyabadili maisha ya wananchi kupitia huduma bora za usafiri na uchukuzi .

  “ Kamwe hatuwezi kufikia hadhi hiyo muhimu kiuchumi bila kuwa na miundombinu imara ikiwemo ya reli “ amesema Mhe. Kassim Majaliwa.

  Aidha Waziri Mkuu amebainisha kuwa Tanzania inapakana na nchi zaidi ya tano ambazo zinategemea sana miundombinu ya nchi ya Tanzania ya usafirishaji na uchukuzi ndani ya nchi ili kupitisha bidhaa. Pia aligusia juu ya mradi mkubwa wa kihistoria wa SGR unaoendelea kuanzia Dar es Salaam hadi Mokutopola na kusema kuwa Serikali ya awamu ya tano imewekeza takribani Shilingi Bilioni 7.2 fedha za walipa kodi kutekeleza mradi huo .

  Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Atashasta Nditiye ameipongeza Serikali ya awamu ya tano kwa kutoa fedha pia amepongeza bodi na uongozi wa Shirika la Reli Tanzania katika ufuatiliaji na utekelezaji wa miradi ya kimkakati ya ufufuaji wa Shirika na njia mbalimbali za reli zilizokufa kwa miaka mingi hapa nchini. Hata hivyo Naibu Waziri ametoa rai kwa wafanyazi wa Shirika la Reli na watanzania kwa ujumla kuwa walizi wa miundombinu ya reli ambayo ni kichocheo kikubwa cha uchumi wa nchi yetu.

  “TRC limepewa dhamana na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kusimamia uhuishaji na utendaji wa shirika pamoja na kuboresha huduma za reli “ amesema Mhe . Nditiye .

  Naye Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania ndugu Masanja Kungu Kadogosa ametoa Shukrani za dhati kwa Waziri Mkuu kuitikia wito wa ufunguzi wa reli hiyo ya Tanga hadi Moshi / Kilimanjaro ulioambatana na uzinduzi wa safari za treni za mizigo kutoka bandari za Dar es Salaam na Tanga kuelekea Moshi Kilimanjaro. Ndugu Kadogosa aliwapongeza wafanyakazi wa Shirika la Reli kwa uzalendo na juhudi kubwa walizofanya katika mradi wa ufufuaji wa njia ya reli kutoka Tanga hadi Moshi.

  “Timu ya kutekeleza mradi huu ilijumuisha wafanyakazi wapatao 525 kutoka TRC , kati ya hao vibarua ni 466, wahandisi 12 na mafundi wa reli na nyanja nyingine 47 “ amesema Ndugu Masanja Kungu Kadogosa.

  Hata hivyo Mkurugenzi Mkuu alibainisha kua juhudi za Serikali na kujituma kwa wafanyakazi wa TRC kutafungua fursa mpya katika usafirishaji na uchukuzi katika ukanda wa Kilimanjaro ambapo historia inaonesha 12 iliyopita Shirika lilikuwa na uwezo wa kusafirisha mazao mbalimbali tani elfu 70 kwa mwaka kutoka Tanga, tani Laki moja za mbolea kwa mwaka na maharage mabehewa 144 kwa mwaka.

  “ Ningependa kuihakikishia serikali kuwa Shirika la Reli Tanzania litaendelea kusimamia miradi yote ya kuboresha huduma za Shirika, utendaji na miundombinu kwa kasi na ubunifu unaopaswa ili kufikia malengo ya Serikali ya awamu ya tano” alizungumza Mkurugenzi Mkuu.


  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza mbele ya Wageni waalikwa mbalimbali (hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa treni ya mizigo katika reli ya Kaskazini uliyofanyika katika stesheni ya reli Moshi, Julai 20.2019.
  Muonekano wa Treni ya Mizigo iliyozinduliwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

  Wananchi wa Moshi, wakipokea treni ya mizigo kwa furaha kubwa, wakati ikiwasili tokea Tanga, Julai 20.2019.
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwapungia mikono wananchi waliyofika kushuhudia uzinduzi wa treni ya mizigo katika reli ya Kaskazini uliyofanyika katika stesheni ya reli Moshi, Julai 20.2019.

  0 0


  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akifafanuliwa jambo na Kiongozi wa Mradi, Richard Magwizi, wakati akikagua mradi wa maji wa Same, Mwanga, Korogwe (SMK) ,uliyopo katika kijiji cha Kinya-Nyumba ya Mungu, Julai 20.2019. Katikati ni Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu). 
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akikagua mradi wa maji wa Same, Mwanga, Korogwe (SMK) ,uliyopo katika kijiji cha Kinya-Nyumba ya Mungu, Julai 20.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu). 
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na wananchi, baada ya kukagua mradi wa maji wa Same, Mwanga, Korogwe (SMK) katika kijiji cha Kinya-Nyumba ya Mungu, Julai 20.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na viongozi pamoja na watumishi wa Wilaya ya Mwanga, katika ukumbi wa Green Bird, wilayani hapo, Julai 20.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso, wakati alipowasili kukagua mradi wa maji wa Same, Mwanga, Korogwe (SMK) na kuongea na wananchi, katika kijiji cha Kinya-Nyumba ya Mungu, Julai 20.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia mashine za kusukumia maji, kwenye mradi wa maji wa Same, Mwanga, Korogwe (SMK) ,uliyopo katika kijiji cha Kinya-Nyumba ya Mungu, Julai 20.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia chanzo cha maji, katika mradi wa maji wa Same, Mwanga, Korogwe (SMK) ,uliyopo katika kijiji cha Kinya-Nyumba ya Mungu, Julai 20.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu). 

  …………………………………………………. 

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea mradi wa maji wa Same-Mwanga-Korogwe ulioko Kirya, wilayani Mwanga, na kukagua hatua mbalimbali za ujenzi wa mradi huo. 

  Waziri Mkuu amekagua ujenzi huo jana (Jumamosi, Julai 20, 2019) na kutoa maelekezo kadhaa ili kuharakisha ujenzi wa mradi ambao umekuwa ukiendelea kwa muda mrefu sasa. 

  Akizungumza na wakazi wa Kirya, Nyumba ya Mungu na vijiji vilivyo jirani na eneo la mradi, Waziri Mkuu alisema Serikali itaendelea kutoa fedha hatua kwa hatua ili kukamilisha mradi huo. 

  Waziri Mkuu amewataka wakazi hao waache kutumia uvuvi haramu na badala yake, wavue samaki kwa kutumia njia halali. “Bwawa la Nyumba ya Mungu linagusa wilaya tatu za Mwanga, Simanjiro na Moshi Vijijini. Ninataka Serikali za wilaya husika zisimamie jambo hilo,” alisisitiza. 

  Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amemwagiza Afisa Elimu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Bibi Pauline Nkwama amsimamie Afisa Elimu wa Wilaya hiyo anayeshughulikia elimu ya msingi, Bibi Mariana Mgonja na kuhakikisha kuwa anawahamishia walimu kwenye shule mbili za Kirya ambazo zilikuwa na walimu wawili wakati zina wanafunzi zaidi ya 400 kila moja. 

  “Afisa Elimu Mkoa hakikisha Afisa Elimu wa elimu ya msingi katika wilaya hii anahamisha walimu kutoka pale mjini na kuwaleta huku ili huku vijijini kuwe na walimu sita katika kila shule. Kesho Jumapili (leo) andika barua za uhamisho, Jumatatu wapewe ili Jumanne waje kuripoti huku,” alisema. 

  Alimwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mwanga, Bw. Zephrin Lubuva awatafutie gari walimu watakaohamishiwa huko ili wafike mapema. 

  Amechukua hatua hiyo, baada ya kuelelezwa na mbunge wa jimno hilo, Profesa Jumanne Maghembe kwamba katika eneo hilo kuna shule mbili ambazo zina walimu wawili wakati kuna madarasa nane, yaani la awali moja na ya msingi saba, na wanafunzi zaidi ya 400. Alizitaja shule hizo kuwa ni Kiti cha Mungu na Emangulai. 

  Mapema, akitoa taarifa kuhusu mradi huo, msimamizi wa mradi huo Mhandisi Richard Magwizi alimweleza Waziri Mkuu kwamba Serikali inatekeleza mradi huo ili kuondoa kero ya maji inayowakabili wakazi wa miji ya Same na Mwanga na vijiji 38 vilivyo katika eneo la mradi. 

  Alisema mradi huo utakapokamilika, unatarajiwa kunufaisha wananchi 438,931 katika Wilaya za Same (246,793), Mwanga (177,085) na Korogwe (15,053). Alisema mradi huo umegawanywa katika awamu mbili za utekelezaji na unakadiriwa kugharimu dola za Marekani milioni 300. 

  “Awamu ya kwanza inahusisha ujenzi wa miundombinu ya uzalishaji wa maji safi na kusambaza maji kwa wakazi wa Mji wa Same na Mji wa Mwanga na vijiji 9 vilivyo kandokando ya chanzo cha maji ambapo awamu ya pili itahusisha ujenzi wa miundombinu ya usambazaji wa maji katika vijiji 29,” alisema. 

  Akielezea changamoto zinazowakabili, Mhandisi huyo alisema wana changamoto ya kuchelewa kwa malipo ya mkandarasi kutokana na uwiano wa uchangiaji ambapo Serikali inagharimia asilimia 50.18. “Malipo yanapochelewa, yanaathiri kasi ya utekelezaji,” alisema.

  0 0


  *Yapangua hoja potofu za UNESCO, WWF kuhusu uamuzi wa Rais Dk. Magufuli  TIMU ya wataalamu bingwa watano wa kitanzania waliobobea katika masuala ya uhifadhi, mazingira na uchumi, juzi ilizindua ripoti yake ya utafiti wa kitalaamu kuhusu faida na madhara ya ujenzi wa mradi mkubwa wa kufua umeme wa Mto Rufiji, unaofahamika zaidi kama Stiegler’s Gorge Hydropower Project.

  Ripoti hiyo imezinduliwa zikiwa zimesalia takriban siku saba kabla ya kuzinduliwa rasmi kwa ujenzi wa mradi huo unaotekelezwa na Kampuni inayomilikiwa na Serikali ya Misri,inayofahamika kwa jina la Arab Contractors.

  Akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliofanyika katika Hotel ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam, kiongozi wa timu hiyo wa wataalamu, Saleh Pamba alisema utafiti wao ulilenga kuangalia madhara na faida za ujenzi wa mradi baada ya mashirika mawili ya umoja wa mataifa kujitokeza hadharani kupinga azma ya Rais Dk. John Pombe Magufuli, kuutekeleza.

  Pamoja na Pamba, wataalamu wengine katika timu hiyo ni Dk. Abubakar Rajab, Abdulkarim Shah, Dk. Magnus Ngoile na Dk. Thomas Kashililah.Pamba aliyataja mashirika ya umoja wa mataifa yaliyojitokeza kuupinga mradi huo na kusambaza taarifa zake duniani kote zikieleza athari zitakazojitokeza iwapo utatekelezwa kuwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na Shirika la Kimataifa la Uhifadhi wa Mazingira na Wanyamapori (WWF).

  Alisema hoja za upinzani huo dhidi ya uamuzi wa Rais Dk. Magufuli zilizosambazwa duniani kote kwa njia ya maandishi kwenye vyombo vya habari na mitandao mbalimbali ya kijamii kabla ya kubebwa na baadhi ya wapinzani wa maendeleo wa ndani ya Tanzania zilianza kujenga taswira mbaya dhidi ya mradi wenyewe na Rais Magufuli ambaye aliapa kuutekeleza.

  “UNESCO na WWF walitushtua sana baada ya kusoma maandiko yao yaliyokuwa yakipinga mradi wa Stiegler’s, waliandika hoja nyingi zilizokuwa zikipinga uamuzi wa rais kutekeleza ujenzi wa mradi huo wakitaka jumuiya ya kimataifa ipaze sauti kwa pamoja ili usitekelezwe. Sisi tulishtuka kwa sababu hizo hoja zao nyingine zilikuwa haziingii akili lakini nyingine zilikuwa zinafikirisha.

  “Tukaona kama wasomi wa kitanzania ni wajibu wetu kujiridhisha ili kama kuna hizo hatari walizozianisha tuishauri serikali ifanye vinginevyo, tumefanya utafiti wa kina kweli kweli, tumegusa kila kipengele walichopigia kelele lakini sasa ajabu tulichogundua ni kwamba kelele zote za hao wazungu ni uongo mtupu. Wanatishwa na kasi ya Rais Dk. Magufuli kuliletea maendeleo taifa letu,” alisema Pamba.

  Alisema, haina shaka hata kidogo kuwa mataifa ya Magharibi yanajaribu kutumia kisingizio kuwa Hifadhi ya Selous ambayo inatambulika kama eneo la urithi wa dunia na mahali unapojengwa mradi wa Stiegler’s, serikali imekusudia kupaharibu lakini ukweli ni kwamba hofu kubwa ya Magharibi ni kasi ya Tanzania kuelekea kwenye uchumi wa kati na kujitoa kwenye utegemezi wa mataifa hayo na taasisi zake za misaada.

  Pamba alisema katika utafiti wao wamebaini kuwa eneo la hifadhi la Selous litakalotumika kujenga mradi ni asimilia mbili tu ya kilomita za mraba 50,000 hivyo sehemu kubwa ya hifadhi haitaguswa na kwamba hata eneo ambalo mradi utatekezwa halitaathirika na uharibifu wa mazingira au kuhatarisha ustawi a wanyama.

  “Kama UNESCO na WWF wana wasomi wasiokuwa na uwezo wa kufanya utafiti wa kiwango kile basi tafiti zao hasipaswi kupewa kipaumbele hata siku moja. Lakini sisi katika utafiti wetu tulibaini kuwa hawa jamaa ajenda yao ni kuhakikisha Tanzania haifikia malengo ya kuwa na uchumi wa kati ifikapo 2025.

  “Umeme wa Stiegler’s utawezesha kukua haraka kwa sekta za viwanda, madini, uendeshaji wa treni za kisasa ya umeme, upatikanaji wa umeme vijijini na wafanyabiashara wadogo watakuwa na uhakika wa kupata umeme wa bei nafuu, uchumi wetu utapaa kwa kasi ya ajabu.

  “Ripoti yetu hii ambayo tunaitoa kwenu waandishi wa habari nendeni mkaisome na mtakubaliana na sisi kuwa uamuzi wa ujenzi wa mradi huo ulifikiwa miaka 60 na 70 huko lakini uamuzi wa kuifanya Selous kuwa eneo la urithi wa duniani ulichukuliwa mwaka 1982. Hizi taasisi za kimataifa zilikuwa na taarifa kuhusu uamuzi wetu huo.

  “Sasa katika hoja zao za sasa wanasema ujenzi wa mradi huo utahatarisha hali ya usalama na utasababisha uharibifu mkubwa wa mazingira, siyo kweli hata kidogo. Sisi tumebaini katika utafiti kuwa utekeklezaji wa mradi utalinda mazingira na tumefafanua vizuri sana katika ripoti kuwa hali ya usalama itamaarika mno kwa sababu kutakuwa na ulinzi wa kutosha katika eneo zima la mradi hivyo hata wawindaji haramu hawatasogolea huko.

  “Hawa wazungu wanasema wakati wa utekelezaji wa mradi kutakuwa na kelele na uchafuzi wa hewa, hoja za kitoto kabisa kwa sababu sisi katika uchunguzi wetu tumebaini kuwa kabla ya mradi kuanza kutekelezwa, hivi sasa kuna viwanja vya ndege vidogo, hizi Airstrips 38 na kati za hizo 33 zinafanya kazi kila uchao kusafirisha watalii, hapo hawaoni kelele hizo za ndege kupaa na kutua.

  “Sasa utafiti hupingwa kwa utafiti, ripoti ya utafiti wetu tumeiweka mezani kama wao wanayo yao mpya ya utafiti wa kweli kweli siyo ya kuchafua nchi au rais nao waiweke mezani. Wapeni watanzania ripoti yetu wajue kuwa mradi huu una manufaa makubwa kwa nchi yetu na hawa wazungu lengo lao tusiutekeleze ili tuendelee kuwategemea wao.

  “Kwetu sisi tunaiomba serikali ichukue hatua madhubuti za ujenzi wa vyanzo vipya vya uzalishaji umeme wa uhakika ili iepuka kushindwa kufikia malengo ya kuwa taifa lenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.“Pia Tanzania inapaswa kuwa na vyanzo vipya vya umeme wa uhakika ili kuepuka hatari ya maeneo ya misitu kugeuka jangwa na kuepuka athari za mabadiliko ya tabia ya nchi, alisema Pamba.

  Alisema kupatikana kwa umeme wa uhakika kutaepusha uteketezwaji wa kilimota za mraba 412,000 za misitu kila mwaka kwa ajili ya shughuli za kibinadamu na hivyo kuongeza ustawi wa maeneo ya uoto wa asili na mapori mengi zaidi.
  Mmoja wa TIMU ya wataalamu bingwa watano wa kitanzania waliobobea katika masuala ya uhifadhi, mazingira na uchumi,Saleh pamba

  0 0

  Na Ripota Wetu,Michuzi TV

  KUMEKUCHA Sherehe za Siku ya Urembo wa asili Tanzania!ndivyo unavyoweza kuelezea sherehe hizo ambazo zinatarajia kufanyika Julai 27 na 28 mwaka huu.

  Taarifa ya Mratibu na muandaaji wa sherehe hizo Antu Mandoza ni kwamba zitafanyika eneo la Life Park Mwenge-Dar es salaam na hakutakuwa na kiingilio.Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Juliana Shonza.

  Mandoza amesema katika siku hiyo pia watawafundisha wanawake kutengeneza vipodozi vya asili na visivyo na kemikali na watatoa kipaumbele kwa wanawake wajasiriamali wa kundi maalumu kama vile watu wenye ulemavu kushiriki katika maonesho hayo bure.

  "Mgeni rasmi atakuwa Juliana Shonza na kutakuwa na maonesho ya Wajasiriamali wa kutengeneza bidhaa mbalimbali za asili zisizo na madhara kwa ngozi na nywele , urembo na wajasiriamali wengine watashiriki.Pia kutakuwa na upimaji wa kansa ya shingo ya uzazi na ya titi bure , pamoja na burudani ya muziki, fashion shows ya wasichana naturalist na watoto,"amesema.

  Tamasha hilo linalofanyika kwa mara ya pili sasa ambalo limeandaliwa na kuratibiwa na Antu Mandoza @missmandoza lengo kubwa ni kusaidia jamii kuepukana na matumizi ya vipodozi hatarishi vinavyosababisha madhara makubwa kiafya kama vile Kansa na pia kuwapa wanawake hasa wasichana ujasiri wa kujiamini na kujipenda walivyo." Naomba kwa wale ambao wanahitaji ufafanua na maelezo mengine ya ziada tuwasiliane kupitia mawasiliano ya namba za simu 0783324787,"amesema Mandoza.


  0 0

  Mwenyekiti wa ALAT Taifa - Mh Gulamhafeez Mukadam akiondoka kwa mbwembwe na cheki ya mfano ya shilingi Milioni 150 aliyopewa na Afisa Mkuu wa Wateja Wadogo na wa Kati – filbert Mponzi kama ishara ya udhamini wa Mkutano Mkuu wa ALAT Taifa unaotegemewa kuanza leo jijini Mwanza na unaotarajiwa kufunguliwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania – John Magufuli. Wanaoangalia ni Katibu Mkuu wa ALAT - Elirehema Kaaya wa pili na Mjumbe wa Kamati Tendaji ya ALAT Mh Zaynab Vulu. NMB ndiye Mdhamini Mkuu wa Mkutano Mkuu wa ALAT Taifa. 

  Afisa Mkuu wa Wateja Wadogo na wa Kati – filbert Mponzi (Kushoto) akikabidhi mfano wa Hundi kwa Mwenyekiti wa ALAT Taifa – Mh Gulamhafeez Mukadam ikiwa ni ishara ya udhamini wa Mkutano Mkuu wa ALAT Taifa unaotegemewa kuanza leo jijini Mwanza na unaotarajiwa kufunguliwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania – John Magufuli. Wa pili kushoto ni Mkuu wa KItengo cha Huduma za Serikali – NMB – Vicky Bishubo na Katibu Mkuu wa ALAT – Elirehema Kaaya. NMB ndiye Mdhamini Mkuu wa Mkutano Mkuu wa ALAT Taifa.

  Benki ya NMB imesaidia Zaidi ya shilingi Milioni 150 kwaajili ya Mikutano Mikuu ya Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa (ALAT) kwa miaka mitano mfululizo huku wakiahidi kuendelea kushirikiana na serikali za mitaa nchini kutatua changamotoimbalimbali.

  Afisa Mkuu wa Wateja Wadogo na wa Kati – Filbert Mponzi aliyasema hayo juzijijini Mwanza wakati akikabidhi udhamini wa Benki hiyo kama mdhamini Mkuu wawa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa ALAT unaoanza leo katika Hoteli ya MalaikaBeach jijini Mwanza.

  Mponzi alisema kuwa Benki hiyo inatambua mahusiano ya kibiashara yaliyopokati ya NMB na ALAT kupitia Zaidi ya halmashauri 180 ambapo Benki inashirianakukusanya mapato ya Serikali huku akisema kusema kuwa taasisi hiyo ni mmbiawa karibu na serikali, hivyo mahusiano ya NMB na ALAT yameanza mudamrefu uliopita.

  “Tunaishukuru sekretariet ya Alat pamoja na wajumbe wote kwa kuendelea
  kutoa ushirikiano, kufanya biashara pamoja na sisi kama benki tumekuwa
  tukiendelea kuboresha huduma zetu ili kuweza kuhudumia serikali kuu
  pamoja na serikali za mitaa,” alisema Mponzi.

  “Tumepeleka huduma zetu nchi nzima huku tukizifikia Zaidi ya halmashauri 180tukiwahudumia katika Nyanja mbalimbali za kibenki kuanzia wafanyakazi,wafanyabiashara na wajasiliamari na pia madiwani nah ii inaonyesha utayariwetu wa kuhudumia Serikali za mitaa.” Alisema Mponzi.

  Mwenyekiti wa ALAT taifa – Gulamhafeez Mukadam ameishukuru Benki ya NMBkwa kuonyesha kujali Serikali za mitaa na mchango wa mwaka huu unaonyeshadhamira na ushirikiano wa kweli kati ya taasisi mbili.

  Mheshimiwa Mukadam aliongeza kuwa jamii za Serikali za mitaa na mamlaka zakebado zinakabiliwa na changamoto nyingi ambazo zinahitaji kushikwa mkono nataasisi kama NMB kwaajili ya kusaidiana kutatua changamoto hizo.

  Aliiomba pia Benki ya NMB kuangalia namna ya kuangalia upya misaada yakeinayotolewa kwa jamii kupitia uwajibikaji kwa jamii (CSR) akiomba Benki kuanzakusaidia jambo ambalo mwisho linakuwa kubwa kuliko misaada midogo midogoambayo inaweza ikawa na mchango mdogo kwenye jamii.

  Mukadam alitoa mfano wa misaada ya vifaa vya ujenzi mashuleni na
  mahospitalini na kusema kuliko kusaidia vifaa vya kuezekea, ichukue mradi mzimakama ni ujenzi wa darasa mpaka unakamilika kwa manufaa ya jamii.

  “Nafikiria Benki inaweza sasa ikabadiri muelekeo wake kuhusu misaada
  mbalimbali kwa jamii, kwa kuhakikisha wanachukua mradi hata mmoja mkubwakwenye wilaya na kuhakikisha wanaukamilisha kwa usimamizi wao ambao utaletaile thamani halisi ya fedha wanazotoa.” Alisema.

  Mjumbe wa Kamatiu Tendaji ya ALAT na Meya wa SUmbawanga – Justine
  Malisawa aliishukuru Benki ya NMB kwa kuleta mfumo wa ukusanyaji mapato yahalmashauri kielektroniki na kuisifia kuwa imeleta mafanikio makubwa kwamapato ya Serikali kuongezeka tofauti na ilivyokuwa zamani hasa ndani ya miakahii mitatu.

  Maneno ya Bwana Malisawa yaliungwa mkono na Mbunge wa Viti Maalumu waKisarawe na Mjumbe wa Kamati tendaji ya ALAT – Mh Zaynab Vuli huku akisemaBenki hiyo imejipambanua kwa kufika maeneo ambayo Benki zingine hazijafika.

  Mh Vulu aliiomba Benki hiyo kupunguza riba na kutoa mikopo nafuu kwa wafanyabiashara wadogo hasa wale wanaofanya biashara zao vijijini ili kusaidiamaendeleo ya mtu mmoja mmoja nchini.

  0 0  Umati wa watu uliojitokeza katika Ibada ya kuadhimisha miaka 80 ya Kanisa la TAG Tanzania iliyofanyika kitaifa Jijini Arusha katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid Karume Jijini Arusha ambapo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kasimu Majaliwa.Picha na Habari na Vero Ignatus Michuzi Blog.


  Maandamano ya maandhimishonya mika 80 ya Kanisa la TAG na miaka 10 ya mpango mkakati wa mavuno 2009-2019
  Maandamano yakiingia uwanjani kwaajili ya sherehe ya maadhimisho ya miaka 80 ya Kanisa la Tanzania Asaemblies of God nchini Tanzania.
  Maandamano yakiingia uwanja wa Shekh Amri Abeid Karume.
  Wamishionari wa ww kanisa la TAG wakiwa katika maadhimisho ya miaka 80 ya Kanisa hilo .
  Baadhibyavwachungaji wakiwa katika ibada ya kuadhimisha miaka 80 ya kanisa la TAG iliyofanyika kitaifa Jijini Arusha.
  Baadhi ya wachungaji wakimuomba Mungu katika maadhimisho ya miaka 80 ya kanisa la TAG leo Jijini Arusha.
  Vijana wa CAS kama wanavyoonekana katika picha wakicheza kwa furaha katika maadhimisho ya miaka 80 ya kanisa lao la TAG yaliyofanyika kitaifa Jijini.Arusha.
  Umati wa watu waliojitokeza katika maadhimisho ya miaka 80 ya kanisa la TAG tangia kuanzishwa kwake mwaka.1939 mkoani Mbeya.
  Baadhi ya wamishionari wa Kanisa la TAG wakiwa katika maadhimisho ya miaka 80 ya kanisa hilo yaliyofanyika Jijini Arusha katika uwanja wa makumbusho ya Sheikh Amri Abeid Karume leo.
  Mass Preise Team wakiwa wanaimba katika maadhimisho ya miaka 80 ya kanisa la TAG na Mpango utekelezaji wa mkakati wa mika 10 ya mavuno  Na.Vero Ignatus,Arusha.

  Maadhimisho ya miaka 80 ya TAG na miaka 10 ya mpango mkakati wa mavuno 2009-2019 yamefanyika jijii Arusha na kuhuduhriwa na viongozi mbalimbali wa dini na waumini wa kanisa hilo.

  Dkt.Barnabas Mtokambaki ni Askofu mkuu wa Kanisa la TAG nchini Tanzania ambapo pia ni Rais wa kanisa hilo Afrika, Maadhimisho hayo Askofu mkuu wa amemshukuru Rais wa Jamuhuri ya Tanzania kwa kulipenda Kanisa hilo na kuwajali.

  Mpango mkakati wa awamu ya kwanza ya mafanikio ya kanisa la TAG kwa mujibu wa Dkt.Mtokambali wameyapata katika miaka 10 ya mavuno kwani majimbo yameongezeka kutoka 10-69,makanisa 2,619-9,986,wachungaji 2,616-10,085,washirika kuongezeka 200,069-13,326,vyuo vya Biblia 4-8 ambapo Idara ya kujenga shule za sekondari na nyingine zitaanza kuandikisha wanafunzi mwezi Januari 2020.

  Ameeleza changamoto kubwa waliyonayo ni eneo la kujenga ofisi kwani makao makuu ya kanisa hilo yaliyopoubungoba limekuwa na nafasi ni ndogo ukilinganisha na wingi wa idadi ya waumini waliopo hivyo wamemuomba Dkt.Magufuli kuwatazama upya na kuwapa eneo kwaajili ya ujenzi sambamba na kuondolewa kodi ya vifaa ambavyo vipo bandarini.

  Vile vile Dkt.Mtokambali ameweza kukabidhi mifuko 1000 ya saruji kwa mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo kwaajili ya kumalizia ujenzi katika shule zilizopo mkoani huko ambapo awali alishawahi kutoa mifuko mingine 5000 ya saruji.

  Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo ni Rais wa Jamuhuri ya Tanzania ambapo amewakilishwa na waziri mkuu Kasimu Majaliwa ambapo amesema kuwa serikali imedhamiria kuwatumikia watanzania wote bila kujali dini wala siasa.

  Amesemaserikalivya awamu ya tano itaendekea kudumisha umoja na ushirikiano na Taasisi za kidini Mungu katika utekelezaji wa majukumu yake yote wakati wanasheherehekea mpango mkakati wa mavuni ni vyema wakakumbuka mchango wa waanzilishi wote wa Kanisa hilo na kuwapongeza kwa kazi nzuri waliyoifanya hadi kufikia,walipo sasa.

  Mhe.Waziri Mkuu amewataka viongozi hao kuendelea kuendelea kuimarisha kitengo chao cha kuinua miradi itakayowafaidisha na kuwainua kiuchumi.

  Akijibu ombi la lililoletwa na Askofu mkuu wa Kanisa la TAG Dkt.Barnabas Mtokambali kuhusu eneo la kanisa lililopo Ubungo kitalu namba 434 G unamilikiwa na TTCL,Waziri Mkuu amesema ombi hilo limepokelewa na atalifanyia kazi.

  Vile vile Mhe. Waziri Mkuu alitolea ufafanuzi kuhusiana na msamaha wa kodi kwa vifaaa na kusema kuna baadhi ya Taasisi za kidini zilitumia vibaya msamaha huo wa kodi ndiyo walisababisha eneo hilo kuwekewa sheria ila ameahidi swala hilo atalifikisha kwa Mhe.Rais wa Tanzania Dkt.Magufuli.

  Serikali inaendelea kusimamia swala la Amani na utulivu sambamba na kudhibiti matukio yote yanayovunja Amani ambaposerikali inawategemea sana viongozi wa dini.

  "Endeleeni kuliombea taifa na viongozi wake ili kuliombea taifa na viongozi wake mnajua fika kuwa Mhe.Rais anahitaji kuombewa sana na nyie viongozi wa dini" ili aweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi"alisema Waziri Mkuu.

  Amehitimisha kwa kusema kuwa Seririkali inaendekea kuliongoza taifa la Tanzania kwa kufuata miongozo mbalimbali kama Katiba na sheria katika katika kila nyanja na kwa maslalahi ya Taifa.Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema Viongozi wa dini kichocheo cha usalama na Amani katika mkoa wa Arusha .

  "Hata mimi nilipoteuliwa kuwa kiongozi mahali pa kwanza nilipokwenda kuripoti ni kwa viongozi wa dini na kuwaambia mimi ni kijana wenu naomva ushirikiano wenu na popote nitakapotetereka mnirekebishe"

  Kanisa hilo la TAG lilianza kazi nchini mwaka 1939, Igale Mbeya,Askofu wa kwanza akiwa Emmanuel Lazaro,Mwanisongile,na awamu ya tatu Dkt.Barnabas Mtokambali, ambapo hivi sasa yapo makanisa 9,986, vyuo vya Biblia 8 vyuo vya kupanda makanisa ,shule za sekondari,vyuo vya ualimu ambavyo vinakaribia kukamilika,vituo vya Radio,vyuo vya ualimu,vituo vya Afya na vituo vya huduma za jamii kwa watoto yatima.

  0 0   Kamanda wa polisi mkoani Ruvuma Simon Maigwa Marwa akionesha Bunduki mbili aina ya AK 47 kwa waandishi wa Habari zilizokamatwa katika kijiji cha Nambendo Songea vijijini ambazo zimeingizwa kutoka Nchi jirani ya MSUMBUJI ambapo watu wanne wanashikiliwa na kuhusiana na  tukio hilo.
  Mkazi wa kijiji cha Nambendo tarafa ya Muhukuru Issa Millanzi akiwa na  meno mawili ya tembo yenye thamani ya zaidi ya Ml 50 baada ya kukamatwa na Polisi kufuatia msako mkali unaofanywa na Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma kuwasaka watu wanaojihusisha na matukio ya uharifu na ujangili katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo hasa maeneo yanayopakana na Nchi jirani ya MSUMBUJI,

  0 0

   Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbasi Kulia, na Mhariri Mkuu wa shirika la Xinhua Tanzania Si Sibo Li Kushoto, wakisaini mkataba wa Ushirikiano ,  waliosimama kutoka kulia  ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe, Katikati ni Bw.He Ping Mhariri Mkuu wa Xinhua na mjumbe wa Kamati Kuu ya  Chama cha CPC na Kushoto Wang Ke balozi wa China nchini Tanzania, wakishuhudia tukio hilo. (Picha na Idara ya Habari MAELEZO)
   Kutoka Kushoto Balozi wa China nchini Tanzania Wang Ke, Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe, Mhariri Mkuu wa Xinhua na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha CPC He Ping, Dkt.Hassan Abbassi Mkurugenzi wa Idara ya Habari na MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, pamoja na Si Sibo Li Mhariri Mkuu wa Xinhua Tanzania , wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kusaini makubaliano Jijiji Dar es Salaam. (Picha na Idara ya Habari MAELEZO)


  Na Mwandishi Wetu-MAELEZO. 

  Ofisi ya Idara ya Habari MAELEZO chini ya Wizara ya Habari Utanaduni Sanaa na Michezo, imesaini Mkataba wa Ushirikiano kati yake na Shirika la Habari la Serikali ya China Xinhua ili kuimarisha na kukuza ushirikiano kati ya Tanzania na China ulioasisiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Mao Tse Tung. 

  Akizungumza katika hafla ya utiaji saini Mkataba huo iliyofanyika Jijini Dar es Salaam jana, Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe alisema ushirikiano wa Tanzania na China umekuwepo kwa miaka mingi katika Nyanja mbalimbali na sasa nchi hizo zimekua kama ndugu. 

  Waziri Mwakyembe alisema yapo mambo mengi yalioacha alama kwenye ushirikiano wa kindugu kati ya China na Tanzania, ikiwemo reli ya Tazara pamoja na uwanja mkubwa wa Taifa Jijini Dar es Salaam pamoja na majengo mbalimbali makubwa. 

  “Nafurahi kuona leo wenzetu wa Idara ya Habari Maelezo wanatiliana saini mkataba wa ushirikiano kati yao na Xinhua, hii inadhihirisha kukomaa kwa urafiki kati ya Tanzania na China na imeongeza wigo wa maeneo ambayo nchi hizi mbili zinashirikiana” Alisema Waziri Mwakyembe. 

  Alisema licha ya kwamba kuna mashirika ya Habari ya China ambayo yanafanya kazi hapa nchini kama CCTV,CGTN, XNHUA pamoja na baadhi ya magazeti, ushirikiano mpya uliosainiwa kati ya Xinhua na Idara ya Habari Maelezo utaimarisha zaidi sekta ya habari hapa nchini , na pia utasaidia kubadilishana uzoefu katika masuala ya habari na mawasiliano kwa ujumla. 

  Kwa upande wake mhariri Mkuu wa Shirika la Xinhua ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya chama cha ukombozi cha watu wa China CPC Bwana He Ping, alisema amekuja Tanzania kuimarisha uhusiano wa kindugu ulioasisiwa na waanzilishi wa mataifa haya mawili, na pia kushuhudia utiaji saini wa makubaliano ya ushirikiano kati ya Idara ya Habari Maelezo na shirika la Habari la Xinhua. 

  Alisema tangu mwaka 1969 Xinhua imekua ikileta wanahabari wake kufanya kazi hapa nchini, lakini ushirikiano mahsusi kama ulioanzishwa kati ya Shirika hilo na Idara ya Habari, utasaidia katika upatikanaji wa habari nyingi za maendeleo kwani nchi yake inahangaika usiku na mchana kuendelea kuwaletea wananachi wake maendeleo. 

  “Lengo letu kama taasisi ya Serikali ni moja tu kuhakikisha kwamba habari tunazoandika na kusambaza zinachangia katika kuboresha maisha ya wananchi kwa kujikita hasa katika habari za maendeleo, hili linatakiwa kusisitizwa sana kwani katika miaka 40 iliyopita China ilikua ni nchi inayoendelea lakini kwa sasa imepiga hatua kubwa za maendeleo duniani” Alisema Bwana Ping. 

  Naye Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbasi, alisema habari ni maendeleo na ushirikiano huo ulioanzishwa utaendelea kuleta chachu ya maendeleo baina ya Tanzania na China hasa katika kipindi hiki ambacho Tanzania inafanya mageuzi makubwa. 

  “Sisi tuko tayari kuwapa habari za kina na zenye takwimu sahihi ili mtusaidie kuieleza dunia kwamba Tanzania sasa tunapiga hatua, kama mlivyofanya mageuzi makubwa ya kiuchumi huko China na sisi tunajitahidi kuhakikisha tunakua Taifa lenye maendeleo makubwa na lenye nguvu kiuchumi” Alisema Dkt Abbasi. 

  Mkataba uliosainiwa kati ya Idara ya Habari MAELEZO na Shirika la Xinhua una lengo la kuimarisha uhusiano katika kubadilishana habari na taarifa mbalimbali, kupitia magazeti na majarida lakini pia kupitia mitandao ya kijamii. 

  Aidha katika Ushirikiano huo Idara ya Habari Maelezo italisaidia shirika la Xinhua katika kupanga na kufanya mahojiano na viongozi wa serikali, Taasisi na wakala mbalimbali pamoja na kuwawezesha waandishi wa Shirika hilo kufanya kazi zao kwa wepesi zaidi hapa nchini. 

  Katika mkataba huo wa ushirikiano Idara ya habari pia itawasaidia waandishi wa habari wa Xinhua katika kupata vibali vya kufanyia kazi hapa nchini pamoja na kuwapatia vitambulisho vya wanahabari (Press cards). 

  Kwa upande wa shirikala Xinhua watasaidia kwenye kutafiti,kuandika na kutoa habari ambazo zinaisaidia Serikali kupitia Ofisi ya Msenaji Mkuu, pia watahakikisha habari wanazotoa zinz viwango vinavyokubalika na Idara ya Habari, pamoja na kusaidia ujenzi wa kituo cha wanahabari (press Center) Jijini Dodoma. 

  Utiaji saini wa mkataba huo wa ushirikiano, ulifanywa na Dkt.Hassan Abbasi Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali na Bwana Si Sibo Li ambaye ni mhariri Mkuu wa shirika la Xinhua hapa nchini. 

  Hafla ya utiaji saini mkataba huo wa ushirikiano, ulihudhuriwa pia na Balozi wa China hapa nchini Wang Ke, wawakilishi wa Xinhua kutoka Nairobi Kenya, wawakilishi kutoka Makao Makuu China, wawakilishi wa Idara ya habari Maelezo, Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo pamona na mwakilishi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

  0 0  0 0

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza wakati alipotembelea mnara wa fuvu la binadamu wa kale (Zinjanthropus Boisei), uliliyopo katika bonde la Olduvai-Ngorongoro, Julai 22.2019. Tokea kushoto ni Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamis Kigwangala. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Balozi wa Marekani Tanzania, Dkt. Inmi Patterson, baada kutembelea mnara wa fuvu la binadamu wa kale (Zinjanthropus Boisei), uliyopo katika bonde la Olduvai-Ngorongoro, Julai 22.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwa ameshika fuvu la binadamu wa kale (Zinjanthropus Boisei), katika eneo alipo gunduliwa binadamu huyo wa kale na Dkt. Mary Leakey, kwenye bonde la Olduvai-Ngorongoro, Julai 22.2019, kabla ya kufungua maadhimisho ya miaka 60 ya kumbukizi ya ugunduzi wa fuvu la binadamu wa kale (Zinjanthropus Boisei). Katikati ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamis Kigwangala na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwa ameshika fuvu la binadamu wa kale (Zinjanthropus Boisei), katika eneo alipo gunduliwa binadamu huyo wa kale na Dkt. Mary Leakey, kwenye bonde la Olduvai-Ngorongoro, Julai 22.2019, kabla ya kufungua maadhimisho ya miaka 60 ya kumbukizi ya ugunduzi wa fuvu la Zinjanthropus Boisei. Tokea kushoto ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamis Kigwangala, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Profesa Audax Mabula. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

  *******************

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii isimamie uboreshaji wa eneo la mnara wa Zinjathropus ili paweze kuvutia zaidi.

  Ametoa agizo hilo leo mchana (Jumatatu, Julai 22, 2019) wakati akizungumza na wananchi na viongozi waliohudhuria maadhimisho ya miaka 60 ya kumbukizi ya ugunduzi wa fuvu la Zinjathropus Bosei, eneo la bonde la Olduvai, wilayani Ngorongoro, mkoani Arusha.

  Maadhimisho hayo yamefanyika ndani ya hifadhi ya Ngorongoro sambamba na uzinduzi wa makumbusho ya Dkt. Mary Leakey. Mnara wa Zinjathropus na Homo habilis umejengwa kwenye hifadhi ya Ngorongoro karibu na njia panda ya kuelekea bonde la Olduvai.

  “Kwenye mnara wa Zinjathropus na Homo habilis pasiachwe kama palivyo. Pajengwe seng’eng’e kuzunguka eneo lile lakini pia paweke kibanda cha mlinzi ambaye pia atakuwa anatoa taarifa kwa wageni wanaopita hapo.”

  “Mtafute vijana kadhaa ambao ni wenyeji wa eneo hili, wafundishwe historia kamili kisha wapewe ajira hizo. Kibanda kikijengwa kwa juu kiwe na vioo ili anayelinda aweze kuona pande zote na pia muweze kumkinga na vumbi na upepo mkali wa eneo lile.”

  Waziri Mkuu pia alitembelea korongo la Frida Leakey, (mahali ambapo zinjathropous aligunduliwa) na kupata maelezo juu ya kugunduliwa kwa fuvu la mtu wa kale duniani yapata miaka milioni mbili iliyopita.

  Akigusia kuhusu uhifadhi wa eneo hilo, Waziri Mkuu alisema nako pia pajengwe kibanda cha mlinzi mwenye uwezo wa kutoa taarifa kwa watalii na akasisitiza pia ajira hizo ziwahusu wenyeji wa eneo hilo.

  “Kwenye korongo la Frida, pawekwe bango lenye maelezo ya Kiswahili, nako pia wapatikane vijana sita au nane, waeleweshwe hiyo historia, wakifuzu, Wizara iwawezeshe, wapangiane zamu ya kushinda hapo. Pia pajengwe kibanda cha wageni kupumzikia wakifika eneo hilo.

  Kuhusu makumbusho ya Dkt. Leakey, Waziri Mkuu alisema makumbusho hayo ni lulu kwa Taifa. “Ninawapongeza viongozi na watumishi wa Mamlaka ya Ngorongoro kwa kuendeleza na kutunza makumbusho haya.”

  Kwa upande wake, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangallah alisema kwa sasa dunia inatambua kuwa chimbuko la binadamu ni Afrika. “Hata kama tunatofautiana sura na rangi, watu wote duniani wana asili ya Afrika. “Kwetu sisi Tanzania, tunaadhimisha uvumbuzi huu kwa sababu fuvu la Zinjanthropus ni alama na nembo ya Tanzania na dunia.”

  Alisema maadhimisho hayo yataendelea kwa kufanya maonesho ya fuvu la Zinjanthropus boisei na malikale zingine katika mikoa sita ya Arusha, Dar es Salaam, Mwanza, Iringa, Mtwara na Dodoma.

  Alisema wizara yake imebaini fursa zilizopo kwenye sekta ya urithi wa utamaduni yaani malikale au utamaduni tuli (static cultural heritage) na utamaduni hai (dynamic culture) ili kuvutia watilii na hivyo kuongeza idadi yao na kuwafanya waongeze muda wa kukaa nchini (length of stay) na hatimaye kuongeza pato la Taifa litokanalo na utalii.

  “Wizara yangu imeanza kuiboresha na kuendeleza sekta ya malikale na urithi wa utamaduni ili izalishe mazao ya utalii na kuvutia watalii kwa kuhamisha vituo vya Idara ya Mambo ya Kale na kuvipeleka TANAPA, TAWA, NCAA, TFS na Makumbusho ya Taifa ili viendelezwe na kuwa vivutio vya utalii.

  “Pia tumehamishia Makumbusho ya Taifa kazi zote za uhifadhi wa urithi wa utamaduni tuli au malikale na kuanzisha tamasha la urithi wa utamaduni wa Mtanzania (Urithi Festival: Celebrating Our Heritage). Tamasha hili litasherehekewa Septemba, kila mwaka.

  Naye Balozi wa Marekani hapa nchini, Dk. Inmi Patterson ameipongeza Serikali kwa kukuza na kuendeleza utalii wa kitamaduni.

  Pia alisifu utajiri wa rasilmali misitu na wa nyama ambao Tanzania imejaliwa kuwa nao. “Uamuzi wa Rais Magufuli wa kuanzisha hifadhi ya Burigi, unazidi kunogesha sifa ya Tanzania katika suala la hifadhi za maliasili na utalii na katika kukuza urithi na utajiri wa nchi,” alisema kwa Kiswahili fasaha.

  Alisema maadhimisho hayo ni siku muhimu kwake kwani yamewakutanisha watu wa kaliba tofauti wakiwemo wanasiasa, wanasayansi, maprofesa kutoka Uingereza, Marekani na Ujerumani, wanafunzi kutoka shule za Tanzania na wenyeji wa Ngorongoro.

  0 0


  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa  akimweleza Afisa Mkuu wa Wateja Wadogo na wa Kati wa NMB – Filbert Mponzi jinsi Serikali inavyothamini Benki ya NMB kama Benki ya Serikali alipotembelea banda la Benki ya NMB kwenye Mkutano wa ALAT unaoendelea jijini Mwanza. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Serikali cha NMB – Vicky Bishubo na Meneja wa NMB Kanda ya Ziwa – Abraham Augustino.
  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa akipata maelezo ya huduma za kibenki kutoka kwa Afisa Mkuu wa Wateja Wadogo na wa Kati – Filbert Mponzi alipotembelea kwenye banda la Benki ya NMB kwenye Mkutano wa ALAT unaoendelea jijini Mwanza. Wengine ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Serikali cha NMB – Vicky Bishubo (Kushoto).
   

  0 0

  Na.Khadija seif, Michuzi tv.

  WAFANYABIASHARA wametakiwa kuona kama tunu na kuupa kipaumbele Mkutano
  kwa nchi wanachama wa  Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), unaotarajiwa kufanyika nchini mwaka huu.

  Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions na Auction Mart Alex Msama amesema Mkutano huo unatarajiwa kuhudhuriwa na zaidi ya watu 1,000 kutoka nchi mbalimbali.

  "Mkutano huo wa 39 unatarajiwa kuhudhuriwa na wakuu wa nchi 16 wanachama wa jumuiya hiyo hivyo ni fursa pekee kufanyika ndani ya ardhi ya Tanzania na tutaweza kuongeza pato la taifa katika kila sekta hapa nchini,"

  Aidha, Msama amesema mbali na kuongeza pato la taifa kupitia sekta mbalimbali bali pia tutaweza kupata fursa ya kufanya biashara mbalimbali ikiwemo mahoteli,vyakula pamoja na usafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine kupitia wageni watakaokuwepo nchini katika Mkutano huo.

  "Ni wakati wa wafanyabiashara wenzangu kuzikimbilia fursa kwa kipindi hicho wageni watakapowasili kwenye Mkutano huo ambapo Rais wetu John Pombe Magufuli amekishika kijiti Cha kuendesha Mkutano huo akiwa kama Mwenyeji ,"

  Pia Msama amesema kutokana na juhudi zinazoendelea kufanywa na serikali ya Mapinduzi chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hakuna ambae ataweza kumuangusha chini Rais huyo ifikapo 202o katika uchaguzi Mkuu.

  "Katika kipindi chote alichokua Madarakani Rais Magufuli ameboresha kila sekta kuanzia elimu,usafiri,ajira, pamoja na Miundombinu mbalimbali na kwa wiki hii tunategemea kupokea umeme wa Rufiji ikiwa ni ishara tosha ya kuendelea kupokea wawekezaji kwa wingi bila kuwepo kwa kikwazo cha kukosa na kukatisha shughuli za uzalishaji viwandani kwa wawekezaji wetu,"
   Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promosheni na Msama Auction Mart, Alex Msama akizungumza na Waandishi wa habari mapema leo Ofisini kwake,jijini Dar kuhusu mambo mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujio wa mkutano mkubwa wa SADC.

older | 1 | .... | 1865 | 1866 | (Page 1867) | 1868 | 1869 | .... | 1897 | newer