Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1864 | 1865 | (Page 1866) | 1867 | 1868 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Wafanyakazi wa Benki ya Exim Tanzania wakiwahudumia wateja waliotembelea banda la huduma za benki hiyo kwenye Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Wadau wa Korosho uliofanyika mkoani Mtwara mwishoni mwa wiki. Benki hiyo ni miongoni mwa wadau wakubwa wa zao la korosho hapa nchini ambapo imekuwa ikitoa huduma mbalimbali za kifedha kwa wakulima na wafanyabaishara wa zao hilo.
  Wafanyakazi wa Benki ya Exim Tanzania wakiwahudumia wateja waliotembelea banda la huduma za benki hiyo kwenye Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Wadau wa Korosho uliofanyika mkoani Mtwara mwishoni mwa wiki. Benki hiyo ni miongoni mwa wadau wakubwa wa zao la korosho hapa nchini ambapo imekuwa ikitoa huduma mbalimbali za kifedha kwa wakulima na wafanyabaishara wa zao hilo

  0 0

  Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza na Mmiliki wa shule za Musabe zilizoko mkoani Mwanza Daniel Musabe wakati wa oporesheni ya kufuatilia wadaiwa sugu wa kodi ya pango la ardhi katika mkoa wa Mawanza mwishoni mwa wiki. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Kodi Wizarani Denis Masami na wa tatu kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa shule za Musabe Faustine Magabilo. 
  Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akihakiki deni la kodi ya pango la ardhi la kampuni ya Birchard Oil Limited pamoja na Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo Arshad Jetha (kushoto) wakati wa oporesheni za kuwatembelea wadaiwa sugu wa kodi ya pango la ardhi katika mkoa wa Mawanza mwishoni mwa wiki. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Kodi Wizarani Denis Masami. 
  Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Ziwa Makwasa Biswalo (wa tatu kulia) akifafanua jambo kwa Meneja wa Kampuni ya Ideal Development Ltd Burnanuddin Rajbhai (wa kwanza kushoto) wakati Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula alipoitembelea kampuni ya Ideal Development Limited katika operesheni ya kufuatilia wadaiwa sugu wa kodi ya pango la ardhi katika mkoa wa Mwanza mwishoni mwa wiki. Wa pili kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Dorothy Mwanyika na wa pili kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Kodi Wizarani Denis Masami. 
  Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akihakiki deni la kodi ya pango la ardhi la kampuni ya Jesse and Company Ltd wakati wa oporesheni ya kufuatilia madeni ya kodi ya pango la ardhi katika mkoa wa Mawanza mwishoni mwa wiki. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Jesse and Company ltd Sundeep Bachu. 
  Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiagana na Afisa Mfawidhi wa Maabara ya Taifa ya Udhibiti Samaki na Mazao ya Uvuvi Emanuel Mundoko wakati wa oporesheni ya kufuatilia madeni ya kodi ya pango la ardhi katika mkoa wa Mawanza mwishoni mwa wiki. 
  Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akimpa maelekezo Meneja Rasilimali Watu wa kapmuni ya Synergy Tanzania Ltd ( wa kwanza kulia) wakati wa oporesheni ya kufuatilia wadaiwa sugu wa kodi ya pango la ardhi katika mkoa wa Mawanza mwishoni mwa wiki. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Kodi Wizarani Denis Masami. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI). 
  ……………………… 
  Na Munir Shemweta, WANMM MWANZA 
  Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi amezidi kuzibana Taasisi na Makampuni yenye madeni makubwa ya kodi ya pango la ardhi ambapo ametua mkoani Mwanza na kuyabana makampuni na taasisi nane ambazo kwa ujumla wake zinadaiwa zaidi ya milioni 900. 

  Kampuni na taasisi alizotembelea Dkt Mabula ni Synergy Tanzania Ltd, Ideal Development Ltd, Birchard Oil Ltd, Shule za Musabe, Taasisi ya Taifa ya Utafiti Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Ndamavyo Auto Spares, Jesse & Company Ltd na Maabara ya Taifa ya Udhibiti Samaki na Mazao ya Uvuvi. 

  Akizungumza katika ziara yake hiyo ya kufuatilia madeni ya kodi ya pango la ardhi mwishoni mwa wiki, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alisema ziara hiyo anayoifanya ya kuwafikia wale wenye madeni makubwa inafuatia baadhi ya kampuni na taasisi zinazodaiwa kushindwa kulipa ama kurekebisha madeni yao baada ya kikao cha Juni 11, 2019 kilichowakutanisha wadaiwa zaidi ya 200 jijini Dodoma
   
  katika mwanzo wa ziara yake kwenye shule za Musabe, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alimueleza mmiliki wa shule hizo Daniel Musabe kulipa deni lake la kodi ya pango la ardhi linalofikia milioni 57.4 katika viwanja vyake vinne anavyomiliki kufikia tarehe 31 Julai 2019 ili kuepuka kufikishwa katika Baraza la Ardhi na Nyumba. 

  Hata hivyo, Mmiliki wa Shule hizo ambazo ni za Chekechea, Msingi na Sekondari alimueleza Dkt Mabula kuwa yuko tayari kulipa deni la kodi ya pango la ardhi lakini alishindwa kufanya hivyo kutokana na changamoto za kibiashara ambapo hata hivyo aliahidi kulipa kiasi anachodaiwa kuanzia Agosti 2019 na kumaliza deni lote ifikapo Desemba 2019. 

  Akiwa katika Kampuni ya Birchard Oil Limited, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Mabula ambaye aliambatana na Mkuu wa Kitengo cha Kodi Wizarani Denis Masami aliitaka kampuni hiyo kulipa kiasi inachodaiwa cha kodi ya pango la ardhi inayofikia milioni 85,235,050 ikiwa ni pamoja na malimbikizo ya kodi za miaka ya nyuma. 

  Meneja uhusiano wa Kampuni hiyo inayojishughulisha na uzalishaji Mafuta na Marobota ya Pamba Arshad Jetha alimueleza Naibu Waziri wa Ardhi kuwa kampuni yake pamoja na kudaiwa kodi ya pango la ardhi kwa baadhi ya viwanja inavyomiliki lakini baadhi yake alishalipia hivyo aliomba kuhakikiwa madeni yake ili kupata deni halisi. 

  Ideal Development Ltd kupitia Meneja wake Burnanuddin Rajbhai alikiri deni la kodi ya pango la ardhi linalofikia milioni 79 na kuomba kupewa muda wa kulipa katika awamu tatu tofauti. Hata hivyo, Naibu Waziri wa Ardhi alizitaka kampuni na Taasisi zilizokubali kulipa madeni kuandika barua ya kueleza namna zitakavyolipa na muda wa mwisho wa kulipa madeni yao katika ofisi za ardhi za halmashauri husika na nakala za barua hizo ziende ofisi ya Kamishna Msaidizi wa Ardhi wa Kanda ya Ziwa. 

  Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Ziwa Makwasa Biswalo aliionya kampuni ya Ideal Development Ltd kwa kushindwa kutekeleza makubaliano yaliyofikia ya kulipa deni lake na kuieleza kuwa hatua itakayofuata kwa kampuni hiyo ni kufikishwa katika Baraza la Ardhi na suala la kuingia makubaliano ya malipo haliwezi kufanyika kwa mara ya pili. 

  Kampuni ya Synergy Tanzania Ltd Kupitia kwa Meneja Utawala wake Florence Kivamba iliahidi kuandika barua ya makubaliano ya kulipa deni la milioni 43 inayodaiwa ingawa alioamba kufanya mawasiliano na uongozi wa juu kwa kuwa ziara ya Naibu Waziri wa Ardhi ilikuwa ya kushtukiza na uongozi haukuwepo. 

  Akiwa katika Taasisi ya Taifa ya Utafiti Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Naibu Waziri wa Ardhi Dkt Mabula aliueleza uongozi wa Taasisi hiyo kuwa inadaiwa jumla ya shilingi milioni 515,713,900 ya kodi ya pango la ardhi na taasisi hiyo haijawahi kulipa kodi hiyo tangu mwaka 1996. 

  Mkurugenzi wa NIMR mkoa wa Mwanza Safari Kinuhi alijitetea kwa kueleza kuwa taasisi yake inapaswa kusamehewa kulipa kodi ya pango la ardhi kwa kuwa haiko kibiashara bali inatoa huduma kwa wananchi na kuboresha afya ingawa aliahidi kuwasiliana na uongozi wa juu kuhusiana na suala hilo. 

  Hata hivyo, Dkt Mabula alimueleza kuwa Taasisi yake inapaswa kufuata sheria wakati wa kuomba kusamehewa kodi ya pango la ardhi huku Mkuu wa Kitengo cha Kodi Wizarani Denis Masami akisisitiza kuwa hata kama Taasisi hiyo itasamehewa kulipa kodi hiyo lakini deni la nyuma lazima lilipwe kwa kuwa sheria ya msamaha itaanza pale tamko la msamaha lilipotoka. 

  Maabara ya Taifa ya Udhibiti Samaki na Mazao ya Uvuvi iliyopo eneo la Nyegezi ilionekana kutokuwa na hati ya eneo inalomiliki ingawa Afisa Mfawidhi wa Taasisi hiyo Emanuel Mundoko alijitetea kwa kueleza kuwa awali Taasisi hiyo ilikuwa sehemu ya chuo cha Uvuvi na sasa inajitegemea hivyo hawajui madeni halisi wanayodaiwa.

  0 0

  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa mavazi ya kiraia), akiangalia moja ya bidhaa zinazotengenezwa na wafungwa katika Gereza la Butimba, jijini Mwanza ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Dkt. John Magufuli la kutaka wafungwa watumike katika shughuli za uzalishaji. 
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa mavazi ya kiraia), akiangalia moja ya bidhaa zinazotengenezwa na wafungwa katika Gereza la Butimba, jijini Mwanza ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Dkt. John Magufuli la kutaka wafungwa watumike katika shughuli za uzalishaji 
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa mavazi ya kiraia), akiangalia nguo inayoshonwa na wafungwa katika Gereza la Butimba, jijini Mwanza ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Dkt. John Magufuli la kutaka wafungwa watumike katika shughuli za uzalishaji 
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na Maafisa wa Jeshi la Magereza wakati wa ziara yake alipotembelea Kiwanda cha Gereza Butimba, jijini Mwanza 
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akiangalia moja ya mashine inayotumika kutengenezea vikoi wakati wa ziara yake alipotembelea Kiwanda cha Gereza Butimba, jijini Mwanza.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

  0 0

  KATIBU Mkuu wa Chama cha Maafisa Mawasiliano wa Serikali (TAGCO), Bw, Abdul Njaidi amewapongeza Maafisa hao kwa kazi nzuri waliyofanya katika kipindi chote cha Maonesho ya 43 ya biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam kwenye viwanja vya Mwalimu J.K Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

  Aliyasema hayo mwishoni mwa maonesho hayo yaliyoanza Juni 28, 2019 na kufikia kilele Julai 13, 2019.

  “Kipekee kabisa nimefarijika sana kuona kazi kubwa mliyoifanya ya kutangaza shughuli mbalimbali zinazofanywa na taasisi za umma ama kupitia vyombo vya habari au kwa kuwaelimisha wananchi moja kwa moja.” Alisema Bw. Njaidi wakati alipokuwa akiwatembelea maafisa hao kwenye mabanda waliyokuwa wakiyasimamia katika viwanja hivyo maarufu kama Viwanja vya Sabasaba.

  Bw. Njaidi ambaye alikuwa amefuatana na Mjumbe wa TAGCO, Bi. Lulu Mengele alisema. “Jukumu letu kubwa ni kuhakikisha wananchi wanapata taarifa muhimu zinazifanywa na Serikali yao kupitia taasisi mbalimbali za Umma na kwa hili nimeliona mimi binafsi wakati nikiwa hapa lakini pia kupitia vyombo mbalimbali vya habari.” Alisisitiza.

  Alisema wananchi wanayo haki ya kujua jinsi serikali yao ya awamu ya tano chini ya uongozi wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli inavyowatumikia katika Nyanja mbalimbali kama vile huduma za kijamii zikiwemo, Afya, Elimu, Maji, ujenzi wa miundombinu ambao ndio unaotupeleka kwenye nchi ya uchumi wa kati.

  Maonesho ya mwaka huu yalibeba kauli mbiu isemayo “"Usindikaji wa Mazao ya Kilimo kwa Maendeleo Endelevu ya Viwanda.
  KATIBU Mkuu wa Chama cha Maafisa Mawasiliano wa Serikali (TAGCO), Bw, Abdul Njaidi, (wapili kushoto), akiwa na Meneja Msaidizi Uhusiano na Itigfaki, Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bi. Vicky Msina (watatu kushoto), Meneja Kiongozi Uhusioano na Elimu kwa Umma, Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bi. Lulu Mengele (wane kushoto) na Afisa Uhusiano Mwandamizi kutoka Idara ya Uhusiano na Itifaki BoT. Bw. Lwaga Mwambande (wakwanza kushoto), wakati alipowatembelea kwenye banda la BoT, Mwishoni mwa maonesho hayo Julai 13, 2019.
  Bw. Njaidi alizungumza na Afisa Mawasiliano Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bw. Luhende Singu, alipomtembela kwenye banda la NHIF Mwishoni mwa maonesho hayo.
  Meneja Kiongozi Uhusioano na Elimu kwa Umma, Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bi. Lulu Mengele (kulia), akizungumza na Bw.Luhende Singu, Afisa Mawasiliano NHIF.
  Bw. Njaidi akisalimiana na fisa Mwandamizi wa Masiko na Uhusiano PSPTB, Bi. Shamim Ally Mdee huku Bi. Lulu Mengele akishuhudia.

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi wa CCM wa wilaya za Kigoma Mjini na Kigoma Vijijini kwenye ukumbi wa NSSF mjini Kigoma, Julai 14, 2019. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Kigoma, Amandus Nzamba. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Mlezi wa CCM Mkoa wa Kigoma, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimina na Mbunge wa Kigoma Vijijini, Peter Serukamba wakati aliopowasili kwenye ukumbi wa NSSF mjini Kigoma kuzungumza na Viongozi wa CCM kutoka wilaya za Kigoma Mjini na Kigoma Vijijini, Juni 14, 2019. Wa pili kushoto ni Mbunge wa Kasulu Mjini, Daniel Nsanzugwako.
  Baadhi ya viongozi wa CCM wa wilaya za Kigoma Mjini na Kigoma Vijijini wakimsikiliza Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Mlezi wa CCM Mkoa wa Kigoma, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa NSSF mjini Kigoma, Julai 14, 2019.

  0 0

  Jopo la majaji hao linamjumuisha Jeff Koinange, ambaye ni maarufu zaidi katika vyombo vya habari nchini Kenya ambaye pia amefanya kazi katika vyombo mbalimbali vya habari Duniani.

  Mwingine ni Gaetano Kagwa, mwigizaji wa Uganda na mtangazaji ambaye amejizolea umaarufu mkubwa zaidi katika eneo hilo ambaye pia anatangaza katika kituo cha Capital FM, akiongoza kipindi cha Tusker Project Fame na alikuwa mshiriki wa Big Brother Africa.

  Jaji mwingine ni Vanessa Mdee, mwimbaji wa Kitanzania na mtunzi wa nyimbo na Mtanzania wa kwanza MTV VJ, mwenyeji wa Epic Bongo Star Search na pia alishiriki kwenye shoo ya runinga ya Coke Studio Africa 2019 kati ya nyota wengine wa muziki wa Afrika.

  Pia yumo Makeda Mahadeo aliyebobea katika vyombo vya habari nchini Rwanda na DJ wa kwanza wa kike nchini Rwanda.

  Majaji watakuwa na jukumu muhimu katika kuidhinisha washiriki ambao wanatakiwa kuendelea kwa hatua inayofuata mwishoni mwa kila hatua na kutoa maoni au kukosoa juu ya waliyoshuhudia jukwaani. Washiriki wataondolewa ikiwa hawapati kura nyingi kutoka kwa majaji wanne.

  Hii ni shoo ambayo itakuwa kinyumbani zaidi kufuatana na soko ambapo itatangazwa katika nchi nne za Afrika Mashariki ikiwemo Kenya, Tanzania, Uganda na Rwanda. Vyombo vya habari vishiriki vitakuwa ni Citizen TV, Clouds Tv, NBS na RTV.

  Kampuni ya Coca-Cola pia itakuwa na jukumu la kutoa huduma mbalimbali zikiwemo ushauri wa ushiriki wa fursa katika kanda nne zilizoshiriki.

  "Mfumo wa Coca-Cola unaamini kusaidia sekta ya ubunifu nchini na kutoa jukwaa ambapo watu wanaweza kuonyesha na kuendeleza vipaji vyao katika kanda. Tunaamini kwamba majaji waliochaguliwa wana uwezo wa kuchagua vipaji bora kwa wasikilizaji wetu wa Afrika Mashariki, ili waweze kufahamu na kufurahia shoo, "alisema Beatrice Nyamari, Meneja Mwandamizi wa Mawasiliano wa Coca-Cola Kanda ya Biashara Kusini na Mashariki mwa Afrika (SEABU).

  Wanajiunga na Safaricom PLC ambao ni wadhamini wa shoo hiyo Kenya na moja wa wafadhili wa Afrika Mashariki kupitia huduma yao ya M-PESA; na Challenge Access, ambayo inaongoza Kampeni ya Moja kwa Moja, kwa msaada wa Programu ya Huduma za Afya Duniani na Mpango wa UHC wa Kenya, Afya Care.

  "Afrika ya Mashariki ina vipaji vya kuonyesha ambavyo vinatoa fursa kwa Waafrika Mashariki kuonyeshea talanta zao na kampuni yetu inaamini katika kutoa majukwaa ya watu kustawi, tunafurahi sana kuwa sehemu ya shoo,"alisema Sitoyo Lopokoiyit, Afisa Mkuu wa Huduma za Fedha, Safaricom.

  Jukwaa hilo litaonyesha vipaji mbalimbali kutoka kwa watu wote wa umri tofauti wa Afrika Mashariki, na litajumuisha vipaji vinavyotokana na kuimba, kucheza, maigizo na aina nyingine nyingi za vipaji.

  "Sisi tunafarijika kuleta msisimuko huu wa kidunia nyumbani. Tunaamini kuwa jukwaa hili litaamua wafuatiliaji wa kimataifa kwa vipaji vya kipekee vya Afrika Mashariki, "alisema Joseph Kusaga, Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media International na mmiliki wa Franchise.

  Majaji wanne watakuwa na vitufe vyao vyekundu ambavyo vinaweza tu kubonyezwa mara moja, pale jaji anapoona imetosha na inapotokea wakati mmoja, vikabonyezwa vyote basi kinachoendelea itapasa kisitishwe.

  Kila mshiriki anahitaji kupokea idhini tatu kutoka kwa majaji kwenda kwenye duru ijayo.

  Kutokana na kuanzia mwezi wa Agosti mwaka huu, kuonyesha EAGT itakuwa na vipindi 10, pamoja na nusu fainali na finali kubwa kuishi eneo moja nchini Kenya. Mshindi wa shooo atajinyakulia fedha za Kenya milioni tano (dola 50,000) kwa kupigiwa kura na watazamaji, ambayo itamuwezesha kuingia ubia wa kufanya kazi muda mrefu na mafunzo ya ujasiriamali.

  Vipindi vitahaririwa katika vipengele sita ambavyo vitaanza kurushwa kuanzia Jumapili ya Agosti 4 saa mbili usiku (saa moja usiku Rwanda) katika sehemu zote nne za ukanda.


  Meneja Mwandamizi wa chapa ya Coca-Cola nchini Tanzania, Kabula Nshimo akizungumza kuhusu ushirikiano baina ya Coca-Cola na mashindano makubwa ya kuibua vipaji kwa ukanda wa Afrika Mashariki ya East Africa’s Got Talent kwa Tanzania wakati wa hafla ya kuwatambulisha majaji wa mashindano hayo iliyofanyika katika makao makuu ya Coca-Cola jijini Nairobi hivi karibuni.
  Meneja Mwandamizi wa Chapa ya Coca-Cola nchini Tanzania, Kabula Nshimo (kushoto) akitambulishwa na mshereheshaji rasmi wa mashindano makubwa ya kuibua vipaji kwa ukanda wa Afrika Mashariki (East Africa’s Got Talent) Anne Kansime wakati hafla ya kuwatambulisha majaji wa mashindano hayo iliyofanyika katika makao makuu ya Coca-Cola jijini Nairobi hivi karibuni.

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugora watatu kutoka kulia, Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, Wabunge pamoja na Viongozi mbalimbali akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Nyumba za Makazi ya Askari Polisi katika eneo la Magogo mkoani wa Geita.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro wakati akitoka kukagua moja ya nyumba za makazi ya Askari wa Jeshi la Polisi katika eneo la Magogo mkoani Geita.
    Makamishna kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi nchini wakifurahia hotuba iliyokuwa ikitolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa sherehe za uzinduzi wa Nyumba za makazi ya Askari Polisi katika eneo la Magogo mkoani Geita.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza katika sherehe za uzinduzi wa nyumba za makazi ya Askari wa Jeshi la Polisi katika eneo la Magogo mkoani Geita.
   Bendi ya Jeshi la Polisi ikitumbuiza katika sherehe za uzinduzi wa nyumba za makazi ya Askari wa Jeshi la Polisi katika eneo la Magogo mkoani Geita.

   Sehemu ya Mradi wa  nyumba za makazi ya Askari wa Jeshi la Polisi katika eneo la Magogo mkoani Geita ambao umezinduliwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika eneo la Magogo mkoani Geita.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wakazi wa Geita mara baada ya  kuhutubia katika uzinduzi wa nyumba hizo za makazi ya Askari Polisi. 
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Geita wakati akielekea kuzindua nyumba za Askari wa Jeshi la Polisi mkoani humo.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Katoro na Buseresere hawaonekani pichani wakati akielekea Geita mjini.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Bwanga wakati akitokea Chato mkoani Geita. PICHA NA IKULU

  0 0

  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni,akipokea zawadi ya kitabu cha kuhifadhia kumbukumbu kutoka kw Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi ,Arthur Mgongo wakati Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilayani Kahama ilipotembelea mgodi huo ikiwa ni ziara ya kuimarisha Ulinzi katika wilaya hiyo.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni,akionesha zawadi ya kitabu cha kuhifadhia kumbukumbu alichopokea kutoka kwa Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi ,Arthur Mgongo(kushoto), wakati Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilayani Kahama ilipotembelea mgodi huo ikiwa ni ziara ya kuimarisha Ulinzi katika wilaya hiyo.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akiongozana na Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi , Arthur Mgongo (kulia) wakati Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilayani Kahama ilipotembelea mgodi huo ikiwa ni ziara ya kuimarisha Ulinzi katika wilaya hiyo.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza wakati Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilayani Kahama ilipotembelea mgodi huo ikiwa ni ziara ya kuimarisha Ulinzi katika wilaya hiyo.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
  Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi ,Arthur Mgongo akizungumza mbele ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), wakati Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilayani Kahama ilipotembelea mgodi huo ikiwa ni ziara ya kuimarisha Ulinzi katika wilaya hiyo.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

  0 0

  Makamu Mwenyekiti wa UVCCM, Tabia Mwita akiwa ameshika zawadi ya picha ya Rais Dk. John Magufuli. 
  Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam, Mussa Kilakala, akiendesha mnada wa keki ambayo ilinunuliwa kwa Sh milioni 1.8 Kulia ni mgeni rasmi Makamu Mwenyekiti wa UVCCM, Tabia Mwita.
  Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam, Mussa Kilakala, akizungumza katika uzinduzi wa Ilala ya Kijani. 


  UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), umesema kuwa sasa unajipanga kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 kwa kuhakikisha unampatia kura za heshima Rais Dk. John Magufuli. 

  Pamoja na hali hayo, UVCCM imesema ni vema chama kikatoa fursa kwa vijana kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kama njia ya kumuenzi Rais Magufuli ambaye ameamua kuwaamini katika nafasi mbalimbali za uongozi serikalini. 

  Akizungumza Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Ilala ya Kijani, Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam, Mussa Kilakala, amesema wao kama vijana kwa sasa wanatembea kifua mbele kutokana na kazi kubwa inayofanywa na Rais Magufuli pamoja na wasaidizi wake, wakiwamo Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na mawaziri. 

  Kilakala amesema viongozi hao wamekuwa wakijenga heshima kwa nchi na chama kwa kuhakikisha wanasimamia falsafa na misingi ya CCM kwa kuimarisha mshikamano kwa Watanzania. 

  “Ndugu Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa (Tabia Mwita), sisi vijana wa Dar es Salaam tunatembea kifua mbele kwani Rais Magufuli amekiheshimisha chama na taifa letu kwa ujumla na mwaka 2020 tutampatia kura za heshima. 

  “Lakini pia kama kiongozi wa nchi (Rais Magufuli), ameweza kuwaamini vijana basi na uchaguzi wa mwaka huu tunakiomba chama kitoe tamko la kutokata majina ya wagombea vijana ambao muda wote wamekuwa wakikijenga chama kwa kuimba ‘hiyena hiyena’ na sasa nao waweze kuingia katika uongozi wa Serikali za Mitaa, udiwani na hata ubunge,” amesema Kilakala. 

  Mgeni rasmi katika mkutano huo wa ndani, Makamu Mwenyekiti wa UVCCM, Tabia Mwita, amesema kuwa ili kijana aweze kutimiza wajibu wake, ni lazima ahahakikishe anajiandikisha na kuwa na kitambulisho cha kupigia kura. 

  Tabia alisema hatua hiyo itahakikisha ushindi mnono wa CCM kwa kushinda viti vya mitaa, vijiji na vitongoji pamoja na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020. 
  Amesema agizo la CCM ni kuhakikisha inashinda nafasi zote za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa pamoja na Serikali Kuu. 

  “Kama kuna mtendaji yeyote atakayekwamisha uandikishaji kwenye Daftari la Kudumu la Wapigakura toeni taarifa haraka ili tumpe taarifa Mwenyekiti wa CCM Rais John Magufuli,” amesema Tabia. 

  Pia ametoa onyo kwa mataifa yanayojaribu kuisemea demokrasia ya nchi na kuwataka watatue matatizo yanayowakabili badala ya kushughulika na Tanzania. Pia aliwataka viongozi wa chama hicho kushirikiana na kuepuka migogoro ya ndani inayokigawa chama hicho kipindi cha uchaguzi. 

  “Tuacheni tabia za kubomoana wenyewe kwa wenyewe, tunahitaji ushirikiano na muelekezane kwa utaratibu uliowekwa na chama,” amesema Tabia. Mwenyekiti wa UVCCM, Wilaya ya Ilala, Amani Pazi, amesema wamefanya uchunguzi na kubaini kwamba asilimia 80 ya wapigakura ni vijana, hivyo ili kuweza kushinda uchaguzi wagombea vijana wapewe kipaumbele zaidi. 

  Katika mkutano huo, wanachama 200 walijiunga na CCM akiwamo aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) upande wa Vyuo Vikuu, Jackson Nzinza.

  0 0

   Na Ripota, Michuzi TV-Morogoro
  HALMASHAURI ya Wilaya Mvomero mkoani Morogoro imesema asilimia 30 kati ya asilimia 33 ya bajeti ya halmashauri hiyo inategemea mazao ya kilimo na hasa cha umwagiliaji.
  Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Florent Kyombo mbele ya Mkurugenzi wa Uendelezaji Miundombinu -Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Mhandisi Senzia Maeda pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Marco Ndonde.
   Wakurugenzi hao wapo katika wilaya hiyo ya Mvomero kwa lengo la kuangalia shughuli za kilimo cha umwagiliaji kinachotokana na skimu zilizopo wilayani humo ikiwa ni jitihada za Serikali kuimarisha kilimo cha umwagiliaji.
  Akifafanua zaidi Kyombo amesema mchango wa kipato kinachotokana na kilimo cha umwagiliaji kwa halmashauri ni mkubwa na asilimia 33 ya bajeti ya halmashauri inategemea mazao ya kilimo na kati hizo 30 ni mazao ya umwagiliaji.
   "Hivyo tukiona skimu zinaendelezwa katika Wilaya yetu na zinafanya kazi kwa ufanisi tunaamini wananchi wetu watavuna sana na maana yake hata kwa halmashauri tunatajia mapato ya fedha za bajeti kuongezeka.
   "Hivyo kupitia fedha hizo halmashauri itajenga madarasa, zahanati, itaboresha miundombinu pamoja na kuendeleza miradi mingine ya maendeleo kwa ajili ya wananchi,"amesema Kyombo.
  Pia amesema kuimarika kwa miundombinu kumekuwa kukiongeza mzunguko wa fedha, kwani sehemu kubwa ya kipato cha wananchi kinategemea  kilimo na mifumo. "Hivyo wananchi wakivuna utaona mzunguko wa fedha unaongezeka na shughuli za uchumi zinachangamka ikiwemo watu kwenda minadani."
  Akizungumzia skimu katika Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Kyombo amesema kuna skimu 11 lakini zinazofanya kazi ni chache kwani nyingine bado hazijaendelezwa.
  "Ukiangalia hata maeneo yaliyowekwa miundombinu ni madogo ukilinganisha na ukubwa wa eneo la Skimu. Hata hivyo kupitia skimu hizo chache ukweli ni kwamba faida zake ni nyingi sana  kwani kwa sasa uzalishaji wa zao la mpunga umeongezeka na hiyo maana yake pato la mwananchi nalo limeongezeka,"amesema Kyombo.
  Amesisitiza  kutokana na kuboreshwa kwa skimu hizo wakulima wa zao la mpunga wanavuna kati ya gunia 40 hadi gunia 50 kwa ekari moja wakati huko nyuma kabla ya skimu walikuwa wnavuna kati ya gunia 10 hadi 15 tu.
   "Kuptia skimu ambazo tunazo , uzalishaji wa zao la mpunga umeongezeka.Pia imetoa fursa ya ajira kwa vijana, wanawake na wanaume na kubwa zaidi kila mmoja anaweza kujikwamua kiuchumi.
   "Hivyo Halmashauri tumeendelea kuwa na mikakati ya kuomba fedha ili skiku ambazo bado hazijaendelezwa nazo ziendelezwe.Kwa Dakawa tunayo skimu kubwa sana ambayo uwepo wapo umefanya kuwe kunazalishwaa mpunga kwa wingi sana,"amesema Kyombo.
   Pia amesema kwa halmashauri yao nao wamejipanga ili kuwa na Skimu ambayo wanaamini itasaidia kuongeza mapato na kuwa chachu kwa wakulima wa mpunga huku akitoa rai kuwa wananchi wanalo jukumu la kuhakikisha skimu ambazo miundombinu yake imeendelezwa inalindwa.Wakati huo huo ameipongeza Serikali kwa jitihada zake za kuendeleza skimu zilizopo Mvomero kwani imekuwa ikitumia fedha nyingi kuziendeleza ikiwemo skimu ya Dakawa.
   Pia amesema kuna skimu nyingi ambazo nazo miundombinu yake ipo hatua mbalimbali ya kuendelezwa na ni matumaini yao zitakapokamilika zitasaidia kuongeza upatikanaji wa mazao ya kilimo.
  "Wananchi wamehamasika sana kutokokana na uwepo wa skimu hizi.Tunafahamu skimu kongwe zote nazo zipo kwenye mchakato wa kuendelezwa ikiwemo skimu ya Mkenge ambayo imeshawekewa banio na itaanza kutumika siku za karibuni,"amesema Kyombo.
    Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mvomero,Mhe.Florent Kyombo akifafanua jambo ofisini kwake mbele ya Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji,Bwa.Marco Ndonde, Mkurugenzi wa Uendelezaji Miundombinu -Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Mhandisi Senzia Maeda wakiwa na Wataalamu pamoja na Wafanyakazi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji  (hawapo pichani),kuhusu Skimu ya Umwagiliaji wilayani humo mkoani Morogoro
  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mvomero,Mhe.Florent Kyombo akisoma moja ya kitabu (nyenzo) kinachohusu Skimu ya Umwagiliaji,alichokabidhiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji,Bwa.Marco Ndonde (pichani kulia) kwa ajili ya kuendelea kuimarisha Skimu ya Umwagiliaji Wilayani humo,mkoani Morogoro.

  Tume ya Taifa ya Umwagiliaji,Wataalamu wapo katika wilaya hiyo ya Mvomero kupata taarifa kuhusu Maendeleo na mafanikio waliyoyapata baada ya ukarabati mkubwa wa miundombinu kufanyika katika shamba la Ushirika la Wakulima Wadogowadogo Kilimo cha Umwagiliaji Mpunga Dakawa (UWAWADA),Wilayani humo,ambapo ukarabati wa miundominu hiyo umefadhiliwa na Serikali ya watu wa Marekani kupitia Shirika la Misaada la USAID-Tanzania,aidha gharama za ufadhili huo wa Ukarabati wa Miundombinu hiyo ya shamba imegharimu zaidi ya Shilingi bilioni 24.
   Pichani kulia Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji,Bwa.Marco Ndonde na kushoto ni Mkurugenzi wa Uendelezaji Miundombinu -Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Mhandisi Senzia Maeda wakiwa na Wataalamu pamoja na Wafanyakazi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji wakimsikiliza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mvomero,Mhe.Florent Kyombo kwa ajili ya kupata taarifa kuhusu Maendeleo na mafanikio waliyoyapata kufuatia ukarabati mkubwa wa miundombinu uliofanywa katika shamba la Ushirika la Wakulima Wadogowadogo Kilimo cha Umwagiliaji Mpunga Dakawa (UWAWADA),Wilayani humo,ambapo ukarabati wa miundominu hiyo umefadhiliwa na Serikali ya watu wa Marekani kupitia Shirika la Misaada la USAID-Tanzania,aidha gharama za ufadhili huo wa Ukarabati wa Miundombinu hiyo ya shamba imegharimu zaidi ya Shilingi bilioni 24. 
   Mkurugenzi wa Uendelezaji Miundombinu -Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Mhandisi Senzia Maeda  akiomba taarifa kutoka  kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mvomero,Mhe.Florent Kyombo kuhusu Skimu ya Umwagiliaji katika Wilaya ya Mvomero inavyofanya kazi na mafanikio yake mpaka sasa.
  Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji,Bwa.Marco Ndonde (kushoto) pamoja na Wataalamu kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji wakifuatilia taarifa iliyokuwa ikitolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mvomero,Mhe.Florent Kyombo kuhusu maendeleo na mafanikio ya Skimu ya Umwagiliaji wilayani humo.

  0 0

  Na Charles James, Michuzi TV

  Naibu Waziri wa Maji, Mhe Jumaa Aweso amewataka Mameneja wa Mikoa na Wilaya wa Wakala wa Majisafi, Usafi na Mazingira Vijijini kufanya kazi kwa weledi na kuhakikisha wanaondoa changamoto za Maji katika maeneo yao.

  Mhe Aweso ameyasema hayo wakati alipokutana na Mameneja hao jijini Dodoma ambapo amesema kwa sasa Wizara hiyo imeunda kitengo cha usanifu ambacho kitasaidia katika kuangalia upya usanifu, mikataba na gharama zinazowekwa na wakandarasi kabla ya ujenzi wa miradi.

  Amewataka Mameneja hao kutumia weledi na taaluma zao kuhakikisha wanamtua mama ndoo kichwani na kuwataka kuacha mambo ya hovyo yaliyokuepo awali.

  " Katika ziara zangu zote katika maeneo mbalimbali nimekua mkali sana kwa wahandisi na wakandarasi, baadhi ya wataalamu wametuangusha kwa kutumia miradi kujipatia fedha, nimejionea mwenyewe miradi mingi wakishindwa kuimaliza kwa wakati. Wakandarasi hawa hatuwezi kuwavumilia hata kidogo.

  " Mhe Rais ametuamini sana katika nafasi hizi tulizoteuliwa, ni jukumu letu kumsaidia kazi na kutumia taaluma zetu kuhakikisha upatikanaji wa maji kwa wananchi waliopo vijijini inafikiwa kwa asilimia 85 au zaidi ifikapo mwaka 2020," amesema Mhe Aweso.

  Amewataka Mameneja hao kutosubiri Waziri au Katibu Mkuu kufika katika maeneo yao ya kazi na kuwaonesha changamoto badala yake waunde mikakati ya kuwawezesha kufikia maeneo yenye changamoto ya Maji ili waweze kuitatua.

  Awali akimkaribisha Naibu Waziri, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Prof Kitila Mkumbo amesema malengo ya Wizara hiyo ni kuongeza upatikanaji wa Maji kufikia asilimia 84 kutoka asilimia 64 kwa maeneo ya Vijijini, lakini pia wakifikia asilimia 95 kutoka asilimia 84 kwa maeneo ya Mjini.

  " Tumekua tukiwekeza sana kwenye miradi mipya lakini kama tukiongeza nguvu na kumaliza miradi ambayo imekwishaanza na kuanza kufanya basi tungekua mbali sana hivyo katika bajeti zetu lazima tupange bajeti zetu Katika kukarabati miradi ya zamani.

  " Mhe Naibu Waziri kazi kubwa na ya haraka kufanywa na RUWASA ni kujenga imani kubwa kwa Mhe Rais na Wananchi, na imani hiyo itajengwa na wahandisi hawa kwa kuhakikisha miradi ya wananchi inafanya kazi lakini kubwa zaidi ni kumaliza tatizo la Maji," amesema Prof Mkumbo.
   Naibu Waziri wa Maji, Mhe Jumaa Aweso akizungumza na Mameneja wa RUWASA kwa ngazi ya Mikoa na Wilaya (hawapo pichani) katika mkutano uliofanyika jijini Dodoma.
   Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Prof Kitila Mkumbo akitoa neno katika kikao cha Mameneja wa RUWASA kwa ngazi ya Mikoa na Wilaya jijini Dodoma.
   Mameneja wa RUWASA kwa ngazi za Mikoa na Wilaya wakiwa katika ukumbi wa Chuo cha Mipango Jijini Dodoma walipokutana na Naibu Waziri wa Maji, Mhe Jumaa Aweso.
  Naibu Waziri wa Maji, Mhe Jumaa Aweso (katikati) akiwa Katika picha ya Pamoja na watendaji wa Wizara hiyo na Mameneja wa RUWASA kwa ngazi za Mikoa na Wilaya jijini Dodoma.

  0 0
  Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo (kulia) na Mkuu wa mauzo wa Vodacom Kanda ya Kaskazini, Brigita Stephen wakizindua duka la Vodacom litakalowahudumia wateja eneo la Kwamrombo jijini Arusha, wa tatu kushoto ni mdau wa Vodacom Bakari Fungo.
  Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (kulia), Mkuu wa mauzo wa Vodacom Kanda ya Kaskazini, Brigita Stephen (wa pili kulia), mdau wa Vodacom Bakari Fungo na mkewe wakifurahi baada ya kuzindua duka la Vodacom litakalowahudumia wateja eneo la Kwamrombo jijini Arusha.

  Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (kushoto) akiwa pamoja na Mkuu wa mauzo wa Vodacom Kanda ya Kaskazini Brigita Stephen(kulia) wakati wa uzinduzi wa duka la Vodacom eneo la Kwamrombo jijini Arusha.
  Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (katikati) akimsikiliza Mkuu Vodacom Kanda ya Kaskazini, Brigita Stephen (kushoto) wakati wa uzinduzi wa duka la Vodacom eneo la Kwamrombo jijini Arusha, kulia ni mdau wa Vodacom Bakari Fungo.


  Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (katikati) akifungua chupa ya Champagne wakati wa uzinduzi wa duka la Vodacom eneo la Kwamrombo jijini Arusha, wa pili kulia ni mdau wa duka hilo Bakari Fungo na kushoto ni Mkuu wa mauzo wa Vodacom Kanda ya Kaskazini, Brigita Stephen.  0 0

  MKURUGENZI wa Maendeleo ya jamii kutoka Wizara ya Afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto, Patrick Golwike,akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya tathimini khusu ndoa za utotoni iliyoitishwa na Shirika la Save the Children iliyofanyika jijini Dodoma. Mkurugenzi kutoka Save the Children Makao Makuu Dar es Salaam Bi.Angela Makota akitoa taarifa wakati wa ufunguzi wa warsha ya tathimini khusu ndoa za utotoni iliyoitishwa na Shirika la Save the Children iliyofanyika jijini Dodoma. Mkurugenzi Idara ya Watoto wizara ya Afya Sebastian Kitiku,akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya tathimini khusu ndoa za utotoni iliyoitishwa na Shirika la Save the Children iliyofanyika jijini Dodoma. Mratibu wa ufuatiliaji wa Shirika la Save the Children, Kanuty Munishi,akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani)wakati wa ufunguzi wa warsha ya tathimini khusu ndoa za utotoni iliyoitishwa na Shirika la Save the Children iliyofanyika jijini Dodoma. Sehemu ya wadau wakifatilia wakati wa ufunguzi wa warsha ya tathimini khusu ndoa za utotoni iliyoitishwa na Shirika la Save the Children iliyofanyika jijini Dodoma. MKURUGENZI wa Maendeleo ya jamii kutoka Wizara ya Afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto, Patrick Golwike,akiwa katika picha ya pamoja na viongozi kutoka Shirika la Save the Children na wadau mara baada ya kufungua warsha ya tathimini khusu ndoa za utotoni iliyoitishwa na Shirika la Save the Children iliyofanyika jijini Dodoma. 

   Warsha ya nne ya tathimini na kupinga mila na desturi za mimba na ndoa za utotoni kwa mkoa wa Shinyanga imefanyika leo Julai 16,2019 Makao makuu ya nchi,jijini Dodoma. Akizungumza katika warsha hiyo ya tathmini iliyokutanisha wadau mbalimbali wa kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto mkoani Shinyanga,Kaimu katibu mkuu wizara ya Afya,maendeleo ya jamii,jinsia Wazee na Watoto ,Idara kuu ya Maendeleo Patrick Golwike amesema lengo la warsha hiyo ni mpango mkakati wa kupashana habari na kupambana na mila potofu dhidi watoto .
   
   Golwike ambaye pia ni mkurugenzi idara ya Maendeleo ya Jamii ametaja baadhi ya mila na desturi potofu na zenye madhara ambazo zimeshamiri mkoani Shinyanga ni mimba za utotoni , kumwozesha mtoto wa kike mapema kwa tamaa ya kupata ng’ombe huku akibainisha kuwa mkoa wa Shinyanga ukishika nafasi ya kwanza hapa nchini kwa asilimia 59% .
   
   Aidha lengo la warsha hiyo ni kuelimisha jamii athari za ndoa Za Utotoni hususan Mkoani Shinyanga ambapo sheria mbalimbali zimewekwa katika kukabiliana na hilo. Bw.Golwike amesema katika utafiti mdogo uliofanywa na Shirika la Save The Children mkoani Shinyanga ulibaini kuwa 90% ya wananchi wanafahamu kuwa ni kosa kumwozesha mtoto wa kike huku ikiamini kuwa kumwozesha mtoto mdogo inachochea na kuvutia kupata mahari nyingi zaidi mfano ng,ombe 25 hadi ng,ombe 50. 
   
  Hata hivyo,Bw.Golwike amesema mradi wa kuelimisha jamii juu ya maddhara ya ndoa za utotoni mkoani Shinyanga umefikia jumla ya watu Themanini na nne elfu [84 ,000]kwa wilaya za Ushetu na Kishapu kati ya watu thamanini na tano elfu [85,000]waliokusudiwa . Kwa upande wake mdau wa elimu juu ya kupinga Mila potofu ,Paulo Robert kutoka Ukune Ushetu Mkoani Shinyanga amesema baada ya kupata elimu naye akaitumia vyema elimu hiyo kuelimisha watu wengine hususan Mimba na ndoa za utotoni. 
   
  Kwa Upande wao baadhi ya Wanafunzi waliohudhuria warsha hiyo wamesema wataendelea kupambana na ndoa za utotoni katika jamii wanayoishi. Warsha hiyo imekutanisha asasi mbalimbali za kiraia ikiwa ni pamoja na SAVE THE CHILDREN,KIWOHEDE ,Umoja wa Ulaya,ambapo dhumuni kuu ni kuangalia changamoto za mimba na ndoa za utotoni hususan katika mikoa 6 ya Shinyanga,Tabora,Dodoma,Rukwa ,Manyara, na Katavi ambayo ndiyo mikoa inayoongoza kwa mila na desturi za ndoa za utotoni.

  0 0

  Serikali mkoani Shinyanga kwa kushirikiana na Wadau wa afya (HPSS) wamezindua kampeni ya kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko wa afya ya jamii CHF iliyoboreshwa, ili waweze kupata huduma ya matibabu kwa gharama nafuu.

  Uzinduzi wa kampeni hiyo umefanyika leo Julai 16, 2019 kwenye kijiji cha Ilobashi kata ya Masengwa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa mkoa huo,Mhe. Zainab Telack, na kuhudhuriwa pia na Waziri wa Kilimo,Mhe. Japhet Hasunga.

  Akizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni hiyo ya CHF iliyoboreshwa ,Telack amewataka wananchi wa mkoa wa Shinyanga wajiunge kwa wingi, ili pale wanapotatwa na magonjwa na kukutwa hawana fedha,kadi hiyo ya CHF itawawezesha kuwapatia matibabu bure bila ya kutoa gharama yoyote ile.Amesema kadi hiyo ya bima ya afya CHF iliyoboreshwa inakatwa kwa bei ya Shilingi 30,000 kwa kila Kaya, ambapo watatibiwa watu sita kwenye kaya moja kwa muda wa mwaka mzima, ambapo matibabu watayapa kuanzia ngazi ya zahanati, kituo cha afya, wilaya, hadi hospitali ya mkoa.

  “Naomba wananchi wa mkoa wa Shinyanga mjitokeze kwa wingi kujiunga kwenye mfuko huu bima ya afya ya jamii CHF iliyoboreshwa kwani ni mkombozi kwetu , ambapo pale utakapougua japo atuombei kwani ugonjwa pia hua hauna hodi, utaweza kukusaidia kupata matibabu kwa gharama nafuu sawa na bure,”amesema Telack.

  “Naagiza pia kwenye huduma zote za kiafya mkoani hapa zihakikishe madirisha yanakuwepo ya wagonjwa ambao wana kadi za CHF iliyoboreshwa, wapewe kipaumbele, pamoja na kupewa huduma stahiki yakiwamo na madawa, ili waweze kupata tiba na kuimarisha afya zao,”ameongeza.

  Katika hatua nyingine amewataka wananchi kuachana na tabia ya kupenda kwenda kutibiwa kwa waganga wa kienyeji, bali waudhulrie kwenye vituo vya afya kupata tiba, ikiwa serikali imeboresha huduma hizo kwa kujenga vituo vya afya 11 pamoja na hospitali za wilaya mbili, sambamba na kuwepo kwa dawa za kutosha.

  Naye Waziri wa Kilimo,Mhe. Japhet Hasunga, amewataka wananchi wa mkoa wa Shinyanga hususani wakulima, pale watakapouza pamba yao wahakikishe wanatenga fedha kwa ajili ya kukata bima hiyo ya afya ya jamii CHF iliyoboreshwa, ambayo itaswaidia kwenye matibabu pale watakapougua.

  Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt. Rashidi Mfaume, ametaja takwimu za wananchi mkoani humo ambao wamejiunga na CHF iliyoboreshwa kuwa ni kaya 25,513 sawa na asilimi 9.8, kati ya kaya 261,608 idadi ambayo ni ndogo.

  Meneja mradi wa HPSS tuimarishe afya Mkoani Shinyanga Dkt. Harun Kasale, amesema kutokana kuwepo kwa idadi ndogo ya wananchi mkoani humo kujiunga CHF iliyoboreshwa, kwa kushirikiana na Serikali ya Uswizi wameona ni vyema kuzindua kampeni ya kuhamasisha wananchi kujiunga na bima hiyo ambayo itawasaidia kwenye matibabu.

  Na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog
  Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akizindua kampeni ya kuhamasisha wananchi wa mkoa huo kujiunga na mfuko wa bima ya afya ya jamii CHF iliyoboreshwa ili kuwasaidia kupata matibabu kwa gharama nafuu.
  Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mhe. Zainab Telack, akielezea namna Serikali inavyo boresha huduma za kiafya ambapo mpaka sasa vimeshajengwa vituo vya afya vipya 11 pamoja na hospitali za wilaya mbili, pamoja na kuwepo na madawa ya kutosha, na kuwataka wananchi wachangamkie fursa hiyo ya kukata bima ya afya CHF iliyoboreshwa ili waweze kufaidi huduma za matibabu kwa gharama nafuu. 
  Meneja mradi wa HPSS tuimarishe afya Mkoani Shinyanga Dkt Harun Kasale, akielezea kutokana kuwepo kwa idadi ndogo ya wananchi mkoani humo kujiunga na bima ya CHF iliyoboreshwa, kuwa kwa kushirikiana na serikali ya Uswizi ndipo wakaona ni vyema kuzindua kampeni hiyo ya kuhamasisha wananchi kujiunga na bima hiyo ambayo itawasaidia kwenye matibabu.
  Waziri wa Kilimo.Mhe. Japhet Hasunga, akiwataka wananchi wa mkoa wa Shinyanga pale watakapouza Pamba yao wahakikishe wanatenga fedha kwa ajili ya kukata kadi ya bima hiyo ya afya ya jamii CHF iliyoboreshwa ambayo itawasaidia kupata matibabu kwa gharama nafuu pale watakapougua na kukutwa hawana fedha za matibabu.

  Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa akisisitiza wananchi kujiunga na bima ya CHF iliyoboreshwa ambayo itakuwa msaada mkubwa kwenye upataji wa matibabu yao kwa gharama nafuu ambapo kaya wenye watu sita wataweza kutibiwa mwaka mzima kwa shilingi 30,000.
  Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt. Rashid Mfaume akitoa takwimu za mkoa huo kwa kaya ambazo zimejiunga na CHF iliyoboreshwa kuwa ni kaya 25,513 sawa na asilimia 9.8, kati ya kaya 261,608 idadi ambayo amebainisha kuwa ni ndogo.
  Awali mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko, akimkaribisha mgeni rasmi mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack, kuzungumza na wananchi kwenye uzinduzi wa kampeni hiyo ya kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko wa bima ya afya ya jamii CHF iliyoboreshwa.
  Wananchi wa kata ya Msengwa wakiwa kwenye uzinduzi wa kampeni ya hamasa ya kujiunga na mfuko wa bima ya afya ya jamii CHF iliyoboreshwa, wakisikiliza umuhimu wa bima hiyo ambayo itawasaidia kupata matibabu kwa gharama nafuu, kwa shilingi 30,000 ndani ya mwaka mzima kwa Kaya yenye watu sita.
  Uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha wananchi mkoani Shinyanga kujiunga na mfuko wa bima ya afya ya jamii CHF iliyoboreshwa ukiendelea katika kijiji cha Ilobashi kata ya Masengwa.
  Wananchi wa Kata ya Msengwa Shinyanga vijijini wakiwa kwenye uzinduzi wa kampeni ya hamasa ya kujiunga na mfuko wa bima ya afya ya jamii CHF iliyoboreshwa, wakisikiliza umuhimu wa bima hiyo.
  Wananchi wa Kata ya Msengwa Shinyanga vijijini wakiwa kwenye uzinduzi wa kampeni ya hamasa ya kujiunga na mfuko wa bima ya afya ya jamii CHF iliyoboreshwa.Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog

  0 0

  VIONGOZI mbalimbali Wastaafu na waliopo Madarakani wakiongozwa na Rais Mstaafu Alli Hassan Mwinyi wamepamba harusi ya Mtoto wa Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa, Robert Lowassa na mkewe Stephanie Kaaya. 

  Ndoa ya wawili hao ilifungwa katika Kanisa la KKKT Usharika wa Mjini Kati na baadae katika tafrija iliyofanyika ukumbi wa Kiringa Gardens, Burka jijini Arusha.

  Pichani juu ni Rais Mstaafu Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi akiwapongeza Maharusi hao.
   Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akiwapongeza maharusi Robert 'Bob' na Mkewe Stephanie
    Viongozi mbalimbali waliohudhuria Sherehe hiyo wakisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa. 
   Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa.
  Mke wa Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na Edward Lowassa.
   Maharusi, Robert Lowassa 'Bob' akifurahia jamabo na mkewe  Stephanie Kaaya.
   Maharusi, Robert Lowassa 'Bob' akifurahia jamabo na mkewe  Stephanie Kaaya.
   Maharusi, Robert Lowassa 'Bob' wakiwa katika upigaji picha  na mkewe  Stephanie Kaaya.
   Alama ya Ndoa ya Robert na Stephanie
   Mfanyabiashara Rostam Aziz akiwasili ukumbini
   Maharusi wakiingia ukumbini 
   Mama Mwinyi na Mama Lowassa wakiingia 


  0 0

  *Awataka wafanyabiashara kuwa na ushirikiano na kulitumia soko hilo vyema pamoja na kutowafumbia macho watakaotorosha madini na kufanya biashara kinyemela 

  Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

  MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo Julai 17 amezindua rasmi soko la kimataifa la madini na vito jijini Dar es salaam ikiwa utekelezaji wa agizo lililotolewa na Rais Dkt. John Magufuli kwa kutaka kila Mkoa kuwa na soko hilo.

  Akizungumza katika warsha hiyo Makonda amesema kuwa, uwepo wa soko hilo litasaidia Wananchi kununua madini na vito halali na kupunguza matapeli waliokuwa wakiuzia wananchi na raia wa kigeni madini na vito bandia.

  Makonda amesema kuwa, uzinduzi wa soko hilo umekuja wakati muafaka ambao Tanzania imechaguliwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa wakuu wa nchi za SADC ambapo wageni wataanza kuingia nchini mwezi ujao wakiambatana na wafanyabiashara ambapo pia anaamini watapata nafasi ya kutembelea soko hilo na kutengeneza fursa zaidi kwa wafanyabiashara nchini.

  Hata hivyo  Makonda amesema ndani ya soko hilo yanapatikana madini ya aina zote hivyo amewataka wananchi kulitumia kwakuwa ni halali na linatambulika na serikali.

  Kwa upande wake mwakilishi wa wafanyabiashara wa madini nchini Othman Tharia amemshukuru Rais Magufuli kwa kutoa wazo la kujenga masoko hayo ambapo hadi sasa Mikoa 28 imetekeleza kwa kujenga masoko hayo hali itakayopelekea kukoma kwa mianya ya utoroshaji na wakiwa wafanyabiashara wanahaidi  kuunga jitihadi za Rais katika utendaji kazi.

  Aidha amewataka wafanyabiashara hao kuwa na chama maalumu kitakachowatambulisha kote nchini na wameishukuru Wizara ya madini kwa kusimamia sheria katika usimamizi wa masoko hayo.

  Ikumbukwe kuwa Mkoa wa Dar es salaam ndio soko na lango kuu la biashara ikiwemo madini hivyo uwepo wa soko hili ni fursa kwa wachimbaji, wafanyabiashara na wananchi kupata madini na vito halali kwa bei halali.
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda (katikati) akikata utepe wakati wa uzinduzi wa soko la kimataifa la madini leo jijini Dar es Salaam.
   Mfanyabishara ya madini Othman Tharia (kushoto) akitoa maelezo kutoka sekta  ya madini mbele ya Mkuu was Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda (kulia) mara baada ya kuzindua soko la kimataifa la madini katika Mkoa wa Dar es Salaam.
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda (aliyeketi) akisikiliza maelezo kutoka kwa mfanyabishara wa madini Othman Tharia kuhusiana na namna wanavyoendesha biashara hiyo, leo jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo na Mabalozi wastaafu walioiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali duniani kwa nia ya kupata ushauri na maoni yao kuhusu maandalizi ya Mkutano wa 39 wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC). Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Julius Nyerere uliopo jijini Dar es Salaam. Katika mkutano huo Prof. Palamagamba John Kabudi ameongozana na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb.), Katibu Mkuu Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe (wa kwanza kushoto) na Naibu Katibu Mkuu Balozi Ramadhani Muombwa Mwinyi (wa kwanza kulia). 
  Juu na Chini ni sehemu ya Mabalozi wastaafu walioiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali duniani wakimsikiliza Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (hayupo pichani). 
  Sehemu ya watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakimsikiliza Prof. Palamagamba John Kabudi (hayupo pichani) 
  Mkutano ukiendelea
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.), Naibu Waziri Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb.), Katibu Mkuu Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe, Naibu Katibu Mkuu Balozi Ramadhani Mwinyi wakiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wastaafu walioiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali duniani

  0 0

  Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akipokea mabati yenye thaman ya takribani milioni.15 mkurugenzi mtendaji wa kutoka Kampuni ya Mount Kilimanjaro Safari Club George Ole Meing'arrai .
  Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akimkabidhi Afisa Tarafa Mabati mara baada ya kuyapokea kutoka ya Mount Kilimanjaro Safari Club.
  Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akikagua moja ya vyumba vya mahabara katika shule hiyo mpya inayotazamiwa iliyopo katika kata ya Olasiti mkoani hapa kuingiza wanafunzi kuanzia januari mwakani 2020.Picha/Habari na Vero Ignatus Michuzi Blog.
  Mkuu wa mkoa Mrisho Gambo akielekea kukagua msingi wa ujenzi wa nyumba xa Waalmu katika shule mpya ya sekondari ya Mrisho Gambo ambayo inatazamiwa kuanza kuingiza wanafunzi januari mwakani 2020.

  Msingi wa nyumba za Waalimu katika Shule mpya ya Sekondari ya Mrisho Gambo kama ubavyoonekana katika picha.
  Diwani wa Kata ya Olasiti Alex Marti akizungumza na cwasndishi.wa habari katiks eneo la shule mpya ya Sekondari ya Mrisho Gambo.
  Afisa Tarafa ya Elerai Titho Maulilyo Cholobi akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhiwa mabati ya kuezekea shule ya sekondari ya Mrisho
  Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Mount Kilimanjaro Safari Club George Ole Neing'arrai akizungumza na waandishi ww habari mara baada ya kukabidhi mabati yenye thamani ya takribani Mil.15 katika shule ya Sekondari ya Mrisho Gambo.
  Mkuu wa Arusha Mrisho Gambo akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua madarasa pamoja na ujenzi unaoendelea katika shule mpya ya Sekondari ya Mrisho Gambo iliyopo katika kata ya Olasiti mkoani hapo.

  Na.Vero Ignatus,Arusha.

  Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amepokea mabati yenye thamani ya takribani milioni 15 kutoka kwa Kampuni ya Mount Meru Kilimanjaro Safari Club ya Jijini Arusha.

  Akizungumza baada ya kupokea mabati hayo amesema mwaka jana 2018 Jiji la Arusha lilipata changamoto kubwa ya wanafunzi zaidi ya 10,000 kukosa madarasa ya kusoma katika hivyo mkoa ukadhamiria kushirikiana na wilaya zote kujenga shule ya hiyo ambayo itakayoweza kuwachukua wanafunzi watakaokaa sawasawa na matakwa ya serikali 

  Amesema kuwa hadi sasa wanajenga madarasa 8 yenye maabara 3 za sayansi ,kemia,bayolojia na Fizikia lengo likiwa ni kukabiliana na changamoto kwa waalimu wa sayansi katika nchi ya Tanzania.

  Mhe.Gambo amesema kuwa changamoto ya walimu wa sayansi ni kubwa hivyo wameona wanapojenga shule lazima watengeneze miundombinu kwa wanafunzi kusoma masomo ya sayansi kwa vitendo.

  Victoria Moshi ni Afisa ustawi wa jamii Kata ya Olasiti amesema kuwa ujenzi wa shule hiyo utasaidia sana katika kipengele cha ulinzi wa ntoto kwani hawataenda mbali kufuata elimu na wazazi pia watanufaika kwani hawatakuwa na hofu juu ya usalama wawatoto wao.

  Wameahidi kwamba wataendelea kuihamasisha jamii ili waendelee kushiriki katika kuchangia maendeleo ya shule katika nyanja mbalimbali na katika kuitunza shule hiyo ili kizazi kijacho nao wanufaike kwa kupitia shule hiyo. 

  Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji kutoka Kampuni ya Mount Kilimanjaro Safari Club amesema amemshukuru mkuu wa mkoa kwa.kuwashirikisha kama wakala wa utalii katika maendeleo ya jamii ikiwepo maswala ya Elimu .

  Amesema kuwa wataendelea kuwepo kushiriki ambapo ametoa wito kwa sekta mbalilimbali iki nyingine za kiraia kushiriki ikiwemo ya Madini utalii na sekta mbalimbali wajitokeze kushiriki katika swala la maendeleo haswa sekta ya elimu. 

  Amesema kuwa azma ya nchini ua Tanzania watoto wapate maeneo ya.kusoma na wapate elimu bora kwa kuboresha madarasa,mahabara na mazingira ya kumvutia mtoto.

  0 0

   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Injinia Isaack Kamwelwe akikata keki wakati wa hafla fupi ya uzinduzi rasmi wa safari ya Mumbai nchini India kwa ndege ya Air Tanzania ikiwa ni safari ya kwanza kwa ndege za Air Tanzania kutoka nje ya Bara la Afrika na ni safari ya moja kwa moja kutokea Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.Ndege ya kwanza ya Air Tanzania imeondoka Julai 17, 2019 kuelekea Mumbai, nchini India.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Injinia Isaack Kamwelwe akikata utepe wakati wa hafla fupi ya uzinduzi rasmi wa safari ya Mumbai nchini India kwa ndege ya Air Tanzania ikiwa ni
  safari ya kwanza kwa ndege za Air Tanzania kutoka nje ya Bara la Afrika na ni safari ya moja kwa moja kutokea Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam. Ndege ya kwanza ya Air Tanzania imeondoka Julai 17, 2019 kuelekea Mumbai, nchini India.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Air Tanzania, Ladislaus Matindi akizungumza wakati wa hafla fupi ya uzinduzi rasmi wa safari ya Mumbai nchini India kwa ndege ya Air Tanzania ikiwa ni safari ya kwanza kwa ndege za Air Tanzania kutoka nje ya Bara la Afrika na ni safari ya moja kwa moja kutokea Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam. Ndege ya kwanza ya Air Tanzania imeondoka Julai 17, 2019 kuelekea Mumbai, nchini India.
   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Injinia Isaack Kamwelwe akizungumza wakati wa hafla fupi ya uzinduzi rasmi wa safari ya Mumbai nchini India kwa ndege ya Air Tanzania ikiwa ni safari ya kwanza kwa ndege za Air Tanzania kutoka nje ya Bara la Afrika na ni safari ya moja kwa moja kutokea Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam. Ndege ya kwanza ya Air Tanzania imeondoka Julai 17, 2019 kuelekea Mumbai, nchini India.

  0 0

  Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania Plc kwa kushirikiana na Idara ya Uhamiaji nchini wamezindua huduma mpya iitwayo ‘Malipo ya Pasipoti kwa M-Pesa’ katika hafla fupi iliyofanyika ofisi za makao makuu ya Uhamiaji, kurasini, jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza katika uzinduzi huo Mkurugenzi wa M-Commerce, Epimack Mbeteni alisema huduma hii mpya inalenga kuwawezesha wateja wa kampuni hiyo kufanya malipo kwa haraka na urahisi zaidi. “Napenda kuwataarifu wateja wetu na Watanzania kwa ujumla kwamba, sasa wanaweza kulipia hati zao uhamiaji kwa kupitia M-Pesa”. 

  “Ili mteja aweze kulipia inabidi aingie kwenye menu ya M-Pesa na kufuata utaratibu wa kulipa malipo ya serikali au kupitia zana (app) M-Pesa. Lengo letu ni kuhamasisha Watanzania wapate hati mpya za kieletroniki lakini pia kuwasogezea huduma za malipo viganjani kwao, ndio maana tumeona umuhimu wa kushirikiana na Uhamiaji kufanikisha hili” Aliongeza Mbeteni 

  Huu ni mkakati wa kuwarahishia waombaji wa hati za kusafiria (Passport) ulipaji wa malipo kwa idara ya Uhamiaji, kwa vile walikuwa wakipanga foleni na kusubiria kwa muda mrefu ili kukamilisha malipo hayo 

  Kamishna wa Passport wa Uhamiaji Marry Palmer alisema “tuna furaha kuungana na Vodacom Tanzania Plc kuwawezesha wateja kufanya malipo kirahisi, vile vile kuiwezesha idara yetu kufanya kazi kwa urahisi zaidi. Nategemea kuona bunifu nyingi zaidi kutoka Vodacom”. 

  Vodacom imedhamiria kufikia idadi kubwa ya watu ambao hawapo kwenye mifumo rasmi ya kifedha, kuchochea ujumuishwaji, na uwezeshaji kupitia huduma rafiki na salama hivyo hii ni moja ya njia ya kufanikisha lengo hilo. 

  “Tunaendeleza nia ya kubadili Tanzania kuwa jamii inayofanya malipo kidijitali, tunawekeza katika teknolojia ya simu ambayo itaingiza watu wengi zaidi katika mifumo ya kifedha na hatimaye, kufikia malengo ya kijamii na kiuchumi ya nchi”, alisisitiza mbeteni. 

  Kampuni ya Vodacom imedhamiria kuipeleka Tanzania katika ulimwengu wa kidijitali ikiwa ni pamoja na kukuza matumizi ya pesa mtandao (E-money) kupitia mtandao wake ulioshamiri nchi nzima ambayo itasaidia wananchi kuepuka hatari mbalimbali zitokanazo na kubeba fedha kila wanapotaka kufanya manunuzi. 
  Mkurugenzi wa M-Commerce Vodacom Tanzania, Epimarck Mbeteni akishikana mkono Kamishna wa Vibali, Mary Palmer, kuashiria uzinduzi wa huduma ya ‘Malipo ya Uhamiaji kwa M-Pesa’ wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika hafla ya uzinduzi huo uliofanyika makao ya Idara ya Uhamiaji, Kurasini, jijini Dar es Salaam. Wateja wa Vodacom sasa wanaweza kufanya malipo ya huduma za Uhamiaji moja kwa moja kupitia menu ya M-Pesa na Vodacom App.
  Kamishna wa Vibali, Mary Palmer, (wa pili kushoto) akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari katika hafla ya uzinduzi wa huduma ya ‘Malipo ya Uhamiaji kwa M-Pesa’ iliyofanyika makao ya Idara ya Uhamiaji, Kurasini, jijini Dar es Salaam. Wateja wa Vodacom sasa wanaweza kufanya malipo ya huduma za Uhamiaji moja kwa moja kupitia menu ya M-Pesa na Vodacom App. Katikati ni Mkurugenzi wa M-Commerce, Epimarck Mbeteni, Mkurugenzi wa Wateja wa Mikataba (Business Enterprise Unit), Arjun Dhillon (wa pili kushoto) na Afisa Udhibiti wa Pasipoti, Peter Lucas Mwita (kushoto)

older | 1 | .... | 1864 | 1865 | (Page 1866) | 1867 | 1868 | .... | 1898 | newer