Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1861 | 1862 | (Page 1863) | 1864 | 1865 | .... | 1897 | newer

  0 0


  Mkurugenzi wa Ansaf bw. Audax Rukonge, akiwasilisha mapendekezo ya mabadiliko ya kisera kutoka kwa wanachama na wadau mbalimbali kutoka taasisi binafsi zinazoshughulika na maendeleo ya sekta ya kilimo nchini
  Mkurugenzi wa Ansaf bw. Audax Rukonge, akiwasilisha mapendekezo ya mabadiliko ya kisera mbele ya waandishi wa habari morogoro


  Jukwaa huru la wadau wa kilimo nchini(ANSAF) limewasilisha mapendekezo ya mabadiliko ya kisera kutoka kwa wanachama na wadau mbalimbali kutoka taasisi binafsi zinazoshughulika na maendeleo ya sekta ya kilimo nchini. Zoezi la uwasilishaji wa mapendekezo ya mabadiliko ya sera ya kilimo nchini lilitangazwa na Wizara ya kilimo kupitia tangazo la Katibu mkuu Mhandisi Mathew John Mtigumwe tarehe 04.06.2019

  Akiwasilisha mapendekezo hayo katika mkoani Morogoro, Mkurugenzi wa Ansaf bw. Audax Rukonge ameipongeza serikali ya awamu ya 5 kupitia wizara ya kilimo kuweza kushirikisha wadau katika utoaji wa maoni kwa lengo la kuboresha sera ya taifa ya kilimo ya mwaka 2013.

  “sera ya kilimo inatambua umuhimu wa miundombinu katika maendeleo ya kilimo na ili kukuza kilimo kunahitajika kuwekeza kwenye miundombinu ya nishati, umwagiliaji, usafirishaji wa mazao kutoka vijijini masoko na uhifadhi wa mazao” alisema bw. Rukonge

  Baada ya hapo bw. Rukonge aliwasilisha mapendekezo yafuatayo:

  0 0

  Mabel Masasi ni Afisa mwandamizi wa habari na mahusiano kutoka TCRA amefafanua kwawaandishi wahabari kuwa Zoezi hilo limeenda sambamba na utoaji wa elimu  juu ya matumizisahihi ya vifaa vya mawasiliano.Picha na habari naVero Ignatus ,Michuz blog.
   Abubakari Kakinga Afisa wa NIDA mkoa wa kilimanjaro amesema kuwa wataendelea kutoa hudumakwa wananchi na kama vitambulisho vitakuwa vimechelewa wananchi wanawezakutumia namba za vitambulisho vyao kupata huduma malimbali kama usaajili wa simu zao.
   Calistus Mhode ni Mkaguzi msaidizi wa Polisi kitengo cha makosa ya mtandaoni,amewataka wananchi wenye changamoto za kipolisi waende wao wapo tayari kuwasikiliza na kuwapatia suluhu
   Julius Felix Afisa Mwandamizi TCRA Kanda ya Kaskazini amesema TCRA inarataibu zoezi hilo na zoezi kama hilo litafanyika pia Tanga na Mkoa wa Mnyara,amesema zoezi hilo ni bure kabisa hivyo wananchi wawe huru
   Afisa Uhamiaji kutoka Ofisi ya Mkoa waKiimanjaro Nicholaus Meela


  Wananchi wakiwa kwenye foleni kwaajili ya kupatiwa huduma eneo la stendi kuu ya mabasi Moshi mjini.
  Wananachi wakiwa kwenye foleni kwaajili ya kupatiwa huduma
  Mmoja wawatumishi kutoka mamlaka ya vitambuliudho vya Taifa akiwapa Wananchi wafomu kwaajili ya kuanza mchakato wa kujisajili kupata kitambulisho cha kitaifa

  Vero Ignatus,Kilimanjaro.

  Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania imeendesha zoezi la kusajili laini za simu kwa mfumo wa alama za vidole ikishirikiana na Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA) Jeshi la Polisi Kitengo cha makosa ya mtandaoni,Uhamiaji pamoja na watoa huduma za mawasiliano, stendi kuu ya mabasi mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro.

  Mabel Masasi ni Afisa mwandamizi wa habari na mahusiano kutoka TCRA ambapo amesema kuwa Zoezi hilo limeenda sambamba na utoaji wa elimu  juu ya matumizisahihi ya vifaa vya mawasiliano,ambapo NIDA wanawasaidia wananchi kupata vitambulisho vya Taifa ambapo mzunguko huo umekuwa ukifanyika nchi nzima ambapo Kilimanjaro ni mkoawa 10.

  Amesema kuwa wataendelea kuzunguka mikoa yote lengo kuu likiwa ni kufanya uhamasishaji wa kusajili kwa namba za vitambulisho vya Taifa na kwa alama za vidole na  ili kurahisisha huduma kwa wananchi ambao wamejitokeza katika zoezi hilo.

  Masasi amesema kuwa zipo changamoto malimbali walizokutana nazo na wamejaribu kuyatatua kadiri wanavyozidi kwenda mikoani,amesema kubwa zaidi ni vile amabavyo wananchi wengi wamekuwa wakilalamika hawazijui namba zao za vitambulksho ambapo tumewasihi NIDA waweze kutatua changamoto hiyo kwa wananchi.

  Calistus Mhode ni Mkaguzi maidizi kutoka Jeshi la Polisi kitengo cha makosa ya mtandaoni amesema amesema zoezi hilo linaendelea nchi nzima la mnada kwa mnada ambapo wanashirikiana na Taasisi nyingine za serikali katika kuielimisha jamii na kuwafikia wananchi juu ya matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii,na matumizi ya teknolojia kwa ujumla .

  "Tunawataka wananchi wote wanaokuwa na changamoto zakipolisi sisi tupo  tayari kuwaelimisha na kutafuta suluhu za changamoto mbalimbali amabazo zimewakumba "alisema Calistus.

  Abubakari Kakinga Afisa wa NIDA mkoa wa kilimanjaro amesema kuwa wataendelea kutoa hudumakwa wananchi na kama vitambulisho vitakuwa vimechelewa wananchi wanawezakutumia namba za vitambulisho vyao kupata huduma malimbali kama usaajili wa simu zao. 

  Amewahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi na kwa wakati kujisajili ya kupata kitambulisho cha Taifa wasisubirie hadi pale zoezi litakapofungwa.

  0 0

  Nyakati za usiku inaelezwa korongo hili ni hatari kwa wakazi wanaokatisha hapa kwani baadhi ya wahalifu hulitumia kufanya uhalifu kama vile ukabaji.
  Baadhi ya watoto walionaswa na kamera ya BMG wakicheza katika korongo hatari la Bolelo lililopo Kata ya Kumsenga, Halmashauri ya Mji wa Kasulu mkoani Kigoma ambapo korongo hilo linaelezwa kuwa uwanja wa vitendo viovu ikiwemo ushirikina.
  Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
  Pia korongo la Bolelo licha ya kwamba ni hatari kwa jinsi lilivyo, bado linapendwa na watoto wakiwemo wanafunzi wa shule za msingi zilizopo jirani ambapo wamekuwa wakilitumia kwa kucheza/ kujificha wanapotoroka shuleni.

  Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mwenge wilayani Kasulu, Mwl. John Edson akieleza mbele ya wanahabari namna uwepo wa korongo la Bolelo jirani na shule hiyo unavyoathiri masomo kwa wanafunzi ambao wamekuwa wakitoroka na kwenda kujifisha humo.
  Mkurugenzi wa Shirika la Kutetea Haki za Watoto na Wanawake KIVULINI, Yassin Ally (kushoto) akizungumza na Mkuu wa Shule ya Msingi Mwenge, Mwl. John Edson kuhusiana na mathara ya korongo ya Bolelo kwa wanafunzi.
  Tazama BMG Online TV hapa chini


  0 0

   Afisa Bima wa Shirika la  Bima la Taifa (NIC) Honest Valence kulia akitoa maelezo ya huduma mbalimbali zinazotolewa na NIC kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam ambao walitembelea banda hilo jana wakati wa maonyesho ya 43 ya biashara ya Kimataifa  yaliyoanza jana kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere Barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.

  Afisa Bima wa Shirika la  Bima la Taifa (NIC) Honest Valence kulia akifurahia jambo na mmoja wa wakazi wa Dar es Salaam waliotembelea banda la shirika hilo jana wakati wa maonyesho ya 43 ya biashara ya Kimataifa  yaliyoanza jana kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere Barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.

   Baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Bima la Taifa NIC wakiwa kwenye picha ya pamoja  wakati wa maonyesho ya 43 ya biashara ya Kimataifa  yaliyoanza jana kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere Barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.
   Wafanyakazi wa Shirika la Bima la Taifa NIC wakiwa kwenye ‘pozi’ wakati wa maonyesho ya 43 ya biashara ya Kimataifa  yaliyoanza jana kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere Barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.  0 0

  *Ni yale yaliyokuwa yanatoroshwa na kusafirishwa bila kibali
  *Yamo madini ya dhahabu, Tanzanite, mawaziri watatu wafunguka


  Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

  JUMLA ya madini yenye thamani ya Sh.3,125, 704,456.12 yamekabidhiwa kwa Serikali kupitia Hazina baada ya kutaifishwa kutokana na kubainika yalikuwa yanatoroshwa nchini.

  Mbali na kukabidhiwa madini na vito, pia Serikali imekabidhiwa fedha za kigeni ambazo nazo zimetaifishwa.

  Akizungumza wakati wa kukabidhi madini, vito na fedha hizo kwa Katibu Mkuu Hazina Dotto James, Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) Biswalo Mganga amefananua kuwa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (NPS) katika vipindi tofauti kati ya mwaka 2017 na mwaka 2018 imeendesha kesi mbalimbali.

  Amesema kesi hizo zilikuwa zinahusiasana na utoroshaji au kukutwa na madini bila kuwa na kibali na katika uendeshaji wa kesi hizo washtakwa walitiwa hatiani na kuamriwa kulipa faini au kutumikia kifungo gerezani pamoja na amri ya kutaifishwa madini na fedha walizokutwa nazo wakati wakisafirisha madini hayo.

  "Madini yaliyotaifishwa ni kilo 25.546 za dhahabu ,zaidi ya kilo 76,020.20(tani 76) za Colored gemstone, Tanzanite pamoja na fedha za kigeni za mataifa mbalimbali 15 zenye thamani ya Sh.1,023,608, 515.12.

  "Kwa kuwa madini hayo yametunzwa sehemu mbalimbali kiasi kwamba uwezekano wa kupotea au kumbukumbu zake kupotea na kwa kuwa mali zote zinazotaifishwa zinakuwa mali za Serikali na Katibu Mkuu Hazina ndiye msimamizi wa mali hizo" ameeleza.

  "Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) anakabidhi kilo 25.5 za dhahabu zenye thamani ya Dola za Marekani 913,954.72 sawa na Sh.bilioni 2,102,095,941,"amesema Mganga.

  Akifafanua madini na vito, amesema kuna tani 76 na Carrats 2849 zenye thamani ya Dola za Marekani 2,638,349.95 sawa na Sh.bilioni 6,068,204.885 na Carrats 2,849 zenye thamani ya Dola za Marekani 3,803.32 sawa na Sh. milioni 888,409,000.

  Pia Tanzanite gramu 888 zenye thamani ya Dola 3,197 sawa na Sh.bilioni 7,353,348 na fedha za kigeni za mataifa 15 ambazo ni sawa na Sh.1,023,608,515.12.

  Hata hivyo Mganga baada ya kukabidhi madini hayo na fedha kwa Katibu Mkuu Hazina ametumia nafasi hiyo kutoa onyo kwa watumishi wa madini ambao wanashindwa kutoa taarifa kwa wakati kuhusu madini na kuwataka kufanya hivyo ili awe nafasi ya kufuatilia na kuchukua hatua mapema.

  Akizungumza baada ya kukadhiwa madini na fedha hizo, Katibu Mkuu Hazina Dotto James amewahakikishia Watanzania wote kuwa mali yao iko salama na itatumika kufanya maendeleo kulingana na uamuzi wa Serikali kuhusu mali hizo.

  "Tunaamini Benki Kuu ya Tanzania(BoT) itatunza mali hizi bila wasiwasi wowote kama ambavyo wamekuwa wakitunza kwa siku zote na pale ambapo Serikali itaamua namna ya kuzitumia kwa lengo la kuimarisha huduma kwa wananchi wake basi itazichukua,"amesema James.

  Wakati huo huo Waziri wa Fedha na Mipango Dk.Philip Mpango amesema inasikitisha kuona watu wasiokuwa na nia njema wakitorosha madini wakati wananchi wakiendelea kuteseka."Kwa kweli inasikitisha sana kuona watu wanaendelea kutorosha madini wakati wananchi wanakabiliwa na changamoto mbalimbali.Bungeni wabunge kila siku wanalalamika maji! maji! halafu kuna watu wanatorosha madini." ameeleza.

  "Ni aibu Waziri wa Fedha kuendelea kuomba misaada wakati mali tunazo za kutosha...tena misaada mingine masharti yake ni magumu. Nitoe rai kwa Watanzania tuwe macho na wote ambao wanatabia ya kupora mali zetu na kuzitorosha,"amesema Waziri Mpango.

  Waziri wa Madini Dotto Biteko ametumia nafasi hiyo kutoa shukrani kwa wote ambao wamefanikisha kupatikana kwa madini na fedha hizo huku akitumia nafasi hiyo kueleza kuwa wachimbaji madini ambao wenye tabia ya wizi wa kutosha madini watambue kwa sasa hawana nafasi tena.

  Pia amesema kuna baadhi ya watanzania ambao wamekuwa wakifanya utapeli kwa njia mbalimbali ikiwemo mitandao ya kijamii kwa kujifanya wana madini na kisha kuchukua fedha za raia wa mataifa mengine, ambapo amesema wenye tabia hiyo wajue siku zao zinahesabika kwani Serikali haiko tayari kuendelea kuwavumilia wenye tabia hiyo.

  Kwa upande wake Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Augustino Mahiga amesema Tanzania kuna madini mengi ambayo hayawezi kuisha leo wala kesho na vema Watanzania wakawa macho kwa kuhakikisha madini hayo yanatunzwa kwa maslahi ya vizazi vya sasa na vijavyo.
  Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) Biswalo Mganga akimkabidhi Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James kwa niaba ya Serikali sehemu ya vipande vya Madini ya Dhahabu ambayo ilikamatwa na kuitaifishwa kwa mujibu wa Sheria zilizotokana na Kesi mbalimbali za Uhujumu Uchumi katika ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam Juni 29, 2019 
  Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akiwa na Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Dkt.Agustine Mahiga, Waziri wa Madini Dotto Biteko pamoja na Kamishina wa Madini Profesa Abdukalim Mruma wakiwa wamishika vipande vya madini ya dhahabu ambayo Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) Biswalo Mganga amezikabidhi kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James kwa niaba ya Serikali Madini, vito na Fedha za mataifa mbalimbali zilizokamatwa na kuitaifishwa kwa mujibu wa Sheria zilizotokana na Kesi mbalimbali za Uhujumu Uchumi nchini, katika ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam Juni 29, 2019 
  Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) Biswalo Mganga akionyesha juu kwa Mawaziri na Wanahabari Fedha za Kimarekani (Dollar) kabla ya kumkabidhi Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James kwa niaba ya Serikali Fedha hizo pamoja na Madini na Vito ambavyo vilikamatwa na kuitaifishwa kwa mujibu wa Sheria zilizotokana na Kesi mbalimbali za Uhujumu Uchumi nchini, katika ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam Juni 29, 2019 
  Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) Biswalo Mganga akimkabidhi Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James kwa niaba ya Serikali sehemu ya Fedha za Mataifa mbalimbali pamoja na Madini na Vito ambavyo vilikamatwa na kutaifishwa kwa mujibu wa Sheria zilizotokana na Kesi mbalimbali za Uhujumu Uchumi nchini, katika ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam Juni 29, 2019 
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James akikagua sehemu ya fedha za mataifa mbalimbali mara baada ya kukabidhiwa kwa niaba ya Serikali Fedha na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) Biswalo Mganga amabazo zilikamatwa na kuitaifishwa kwa mujibu wa Sheria zilizotokana na Kesi mbalimbali za Uhujumu Uchumi nchini vikiwemo pia Madini na vito mbalimbali, katika ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam Juni 29, 2019 
  Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) Biswalo Mganga akionyesha juu kwa Mawaziri na Wanahabari moja kipande cha madini ya Pie light kabla ya kumkabidhi Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James kwa niaba ya Serikali Madini, Vito na Fedha za mataifa mbalimbali ambavyo vilikamatwa na kuitaifishwa kwa mujibu wa Sheria zilizotokana na Kesi mbalimbali za Uhujumu Uchumi nchini, katika ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam Juni 29, 2019 

  Masanduku yaliyoifadhiwa Madini,Vito pamoja na fedha za Mataifa mbalimbali zilizotokana na Kesi mbalimbali za Uhujumu Uchumi zikiingizwa Ukumbini tayari kwa Mkurugenzi wa Mashtaka(DPP) Biswalo Mganga kukabidhi kwa Serikali kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BOT). 
   
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James akizungumza na wanahabari mara baada ya kukabidhiwa kwa niaba ya Serikali Madini, vito mbalimbali na Fedha kutoka kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) Biswalo Mganga ambazo zilikamatwa na kuitaifishwa kwa mujibu wa Sheria zilizotokana na Kesi mbalimbali za Uhujumu Uchumi nchini, katika ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam Juni 29, 2019 
  Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Dkt.Agustine Mahiga akizungumza na wanahabari katika hafla ya kukabidhi Madini, vito mbalimbali na Fedha kwa Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango kutoka kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) Biswalo Mganga ambazo zilikamatwa na kuitaifishwa kwa mujibu wa Sheria zilizotokana na Kesi mbalimbali za Uhujumu Uchumi nchini, katika ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam Juni 29, 2019 
  Waziri wa Madini Dotto Biteko akizungumza na wanahabari katika hafla ya kukabidhi Madini, vito mbalimbali na Fedha kwa Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango kutoka kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) Biswalo Mganga ambazo zilikamatwa na kuitaifishwa kwa mujibu wa Sheria zilizotokana na Kesi mbalimbali za Uhujumu Uchumi nchini, katika ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam Juni 29, 2019 

  PICHA NA IKULU

  0 0

  Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (kulia), akipeana mkono na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), baada ya uzinduzi wa Jengo la Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), jijini Dodoma. 
  Muonekano wa Jengo la Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Jijini Dodoma, lililozinduliwa na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa. 
  Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (kulia), akimkabidhi Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), kitabu cha matokeo ya viashiria muhimu vya utafiti wa mapato na matumizi ya Kaya binafsi kwa Tanzania Bara wa mwaka 2017/18, jijini Dodoma. 
  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (wa sita kulia) na viongozi wengine wakiwa wamenyanyua kitabu cha matokeo ya viashiria muhimu vya utafiti wa mapato na matumizi ya Kaya binafsi kwa Tanzania Bara wa mwaka 2017/18, jijini Dodoma 

  ******************* 

  Na. Josephine Majura na Peter Haule, WFM, Dodoma 

  Kiwango cha umaskini nchini Tanzania kimepungua kwa asilimia mbili, ikiwa ni matokeo ya juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano ya kupunguza umasikini kwa wananchi hasa wa hali ya chini. 

  Hayo yamebainishwa wakati Waziri Mkuu Mhe. Kassimu Majaliwa, akizindua ripoti ya matokeo ya viashiria muhimu vya utafiti wa mapato na matumizi ya mwaka 2017-18 na jengo la Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Mkoani Dodoma. 

  Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa, amewataka Watakwimu nchini kufanya kazi kwa weledi kwa kuzingatia sheria, taratibu na miongozo mbalimbali wakati wa kutekeleza majukumu yao hususan kuzalisha na kusambaza takwimu zenye viwango vya kitaifa na kimataifa ili kuisaidia Serikali kujua mahitaji yaliyopo. 

  “Serikali inayoongozwa na Mhe. Rais, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, inatambua umuhimu wa takwimu zenye ubora, kwa kuwa ndiyo macho na masikio ya Serikali katika kufuatilia na kutathmini mipango ya maendeleo ya nchi”, alieleza Mhe. Majaliwa. 

  Mhe. Majaliwa, alisema kuwa takwimu bora hutoa fursa kwa Serikali kufanya mapitio ya sera, mipango na mikakati kulingana na hali ilivyo kwa wakati husika na pia kupima ilikotoka, ilipo na kutabiri inakoelekea hivyo kupima mwenendo wa jitihada za Serikali. 

  Aidha aliiagiza Ofisi ya Taifa ya Takwimu Nchini (NBS), kuhakikisha Halmashauri zote nchini zinakuwa na Afisa Takwimu ili kurahisisha upatikanaji wa takwimu kwa wakati ili kuweza kusaidia maendeleo nchini. 

  Kwa upande wake Naibu wa Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji, amesema kuwa Wizara yake imepewa jukumu la kusimamia Uchumi wa Taifa, lakini haiwezi kusimamia uchumi bila kuwa na takwimu rasmi na sahihi. 

  “Katika kipindi cha takribani miaka mitatu na nusu tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani, umaskini nchini umepungua hadi kufikia takribani asilimia 26 kutoka asilimia 28, ikiwa ni sawa na kupungua kwa asilimia mbili”, alisisitiza Dkt. Kijaji. 

  Dkt. Kijaji alisema kuwa matokeo ya tafiti yaliyozinduliwa na Mhe. Kassim Majaliwa, yameonesha kupungua kwa umaskini wa watanzania waishio vijijini kwa asilimia 3.1 kati ya mwaka 2011/12 na mwaka 2017/18. 

  Alieleza kuwa hayo ni matunda ya uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano, chini ya Kiongozi wake, Mhe. Rais, Dkt. Magufuli. Kwa upande wake Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dkt. Albina Chuwa, alisema kuwa utafiti wa mwaka 2017/2018 umetumia teknolojia ya kisasa inayojulikana kama Survey Solution ambayo ni tofauti na njia ya awali ya kutumia madodoso yaliyochapishwa hivyo kupunguza gharama za kufanya tafiti za kijamii. 

  Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa akiwemo Mwakilishi wa Benki ya Dunia Bw. Denis Biseko, wameipongeza Serikali kwa kupunguza kiwango cha umasikini kwa takribani asilimia 2, na pia wamepongeza matokeo ya utafiti huo ambao umezingatia usawa wa kijinsia hivyo kuwa chachu ya maendeleo kwa kuwa ni moja ya lengo la mashirika hayo.

  0 0

  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
  MAONESHO ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, tayari yamepamba moto ambapo Mkurugenzi wa Banda la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma, (PSSSF), Bi. Eunice Chiume, ametoa wito kwa Wanachama wa Mfuko huo pamoja na Wananchi kufika kwenye banda hilo ili kupata elimu kuhusu huduma mbalimbali zitolewazo na Mfuko.

  Bi. Chiume amesema, banda la PSSSF liko jengo namba 13 mkabala na jengo la matangazo ndani ya viwanja vya Maonesho Sabasaba barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
  "Mfuko wa PSSSF umeundwa baada ya kuunganishwa kwa mifuko minne ya Hifadhi ya Jamii ya GEPF, PSPF, LAPF na PPF na kwa sababu hiyo bado ni mpya na wanachama wanahitaji kuelimishwa kuhusu majukumu mapya ya Mfuko huo kwa wanachama ambao ni watumishi wa Umma." Alifafanua Bi. Chiume.

  Alisema uduma za PSSSF zitatolewa kwenye jingo moja ambalo pia linatumiwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).

  Maonesho hayo yameanza Juni 28 na yatafikia kilele Julai 13, 2019 na kauli mbiu ya mwaka huu ni "Usindikaji wa Mazao ya Kilimo kwa maendeleo endelevu ya viwanda."
   Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bw. William Erio (kushoto), akizungumza na Mkurugenzi wa Banda la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bi. Eunice Chiume (wapili kushoto), pamoja na Afisa Matekelezo wa NSSF, Bi.Diogi Janguo, (wapili kulia) na Mtaalamu wa mifumo ya computer, NSSF Bi.Grace Magigile wakati Bw. Erio alipofika kwenye jengo namba 13 ambalo Mifuko yote miwili ya PSSSF na NSSF inatoa huduma kwa ushirikiano katika jengo hilo. Itakumbukwa kuwa PSSSF ni Mfuko ulioundwa kuhudumia Watumishi wa Umma na NSSF kuhudumia Sekta binasi.
   Afisa Matekelezo Mwandamizi wa PSSSF, Bw. Donald P. Maeda (kushoto), akimuhudumia Mwanachama wa Mfuko huo.
   Afisa Mwandamizi wa Malipo, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma,(PSSSF), Bi.Nyangi Masalu (kulia), akiwahudumia wanachama wa Mfuko huo waliotembelea banda la PSSSF kwenye viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam Juni 30, 2019.
   Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSSSF, Bw. Abdul Njaidi (kushoto), akiwahudumia wananchi hawa waliofika kwenye banda hilo.
  Jengo namba 13 ambalo ndipo ilipo Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya PSSSF na NSSF.
  Timu ya PSSSF ikiongozwa na Mkurugenzi wa Banda la Mfuko huo Bi. Eunice Chiume ikiwa tayari kutoa huduma bora kwa wanachama na wananchi watakaofika kwenye banda hilo.

  0 0

  Tanzania na Nchi ya Falme za Kiarabu zimekubaliana kuendelea kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia na kiuchumi ikiwa ni pamoja na kushirikiana katika masuala ya usalama wa eneo la Ghuba na bahari ya Hindi pia kusaidia kuimarisha hali ya usalama katika nchi za Somalia na Sudan.

  Hayo yamebainika wakati wa ziara ya Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi alipomtembelea na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Serikali ya Umoja wa Falme za kiarabu Sheikh Abdullah bin Zayed Al Nahyan.

  Katika Mazungumzo hayo wawili hao wamekubaliana kuendelea kuimarisha udugu wa muda mrefu baina ya mataifa hayo mawili ikiwa ni pamoja na kufufua mazungumzo ya Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano (JPC) ambayo kwa mara ya mwisho yalifanyika katika Mji wa Abu Dhabikatika Umoja wa Falme za Kiarabu ili kufufua na kutekeleza makubaliano ikiwa ni pamoja na kuangalia fursa za kiuchumi kwa faida ya pande zote mbili.

  Akizungumza mara baada ya mazungumzo hayo Waziri Palamgamba John Kabudi amesema pamoja na masuala mbalimbali waliyokubaliana pia Waziri wa Mambo ya Nje wa Serikali ya Umoja wa Falme za kiarabu Sheikh Abdullah bin Zayed Al Nahyan ameahidi kufanya mazungumzo na Ubalozi wa Falme za Kiarabu uliopo Nchini Tanzania ili kuharakisha matayarisho ya Ubalozi huo kuhamia Dodoma baada ya serikali ya Tanzania kuupatia ubalozi huo eneo la kujenga ubalozi wa Nchi hiyo mjini Dodoma bure.

  Waziri Kabudi ameongeza kuwa mazungumzo hayo yamekuwa ya manufaa kwa pande zote mbili na kwamba yataendelea kuimarisha mahusiano baina ya Nchi hizo mbili ikiwa ni pamoja na kufungua fursa za kibiashara kwa ajili ya maendeleo ya mataifa hayo.

  Katika hatua nyingine Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof Palamagamba John Kabudi akizungumza wakati akihitimisha ziara yake Nchini China,amesema ziara hiyo imekuwa ya manufaa kiuchumi kwa Tanzania ambapo tayari wawekezaji takribani 150 wanatarajiwa kuwasili nchini Tanzania kwa nia ya kuangalia maeneo mbalimbali ya uwekezaji mapema mwezi septemba wakitanguliwa na ujumbe wa watu 10 mwezi Julai 2019,hii ikiwa ni kipindi kifupi sana mara baada ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kuhudhuria mkutano wa kwanza wa maonesho ya uchumi na biashara kati ya China na Afrika uliofanyika katika mji wa Chanshang katika jimbo la Hunan,Nchini China.

  Aidha ametanabaisha kuwa tayari wamepatikana wawekezaji wanaotaka kujenga nyumba ya kulala wageni yenye vyumba mia tatu katika mji wa Karatu ulioko mkoani Manyara kwa nia ya kuhamasisha watalii hususani kutoka China ambao wanatarajiwa kuongezeka maradufu kufuatia hatua ya Tanzania kuweka msisitizo katika kutangaza vivutio vyake vya Utalii.

  Pia Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Beijing kimekubali ombi la Waziri Kabudi la kutaka kuongeza idadi ya wanafunzi watakaokwenda kusoma chuoni hapo kutoka 20 hadi kufikia idadi 40 nafasi zitakazotolewa kwa ufadhili wa chuo hicho kila mwaka ili kuandaa nguvu kazi ya kutosha wakati Tanzania ikijiandaa kuingia katika uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
   Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akisalimiana na mwenyeji wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Serikali ya Umoja wa Falme za kiarabu Sheikh Abdullah bin Zayed Al Nahyan,Abu Dhabi,Umoja wa Falme za Kiarabu. June 30,2019. Tanzania na Nchi ya Falme za Kiarabu zimekubaliana kuendelea kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia na kiuchumi ikiwa ni pamoja na kushirikiana katika masuala ya usalama wa eneo la Ghuba na bahari ya Hindi pia kusaidia kuimarisha hali ya usalama katika nchi za Somalia na Sudan. 
   Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi,akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Wizara ya Mambo ya Nje wa Umoja wa Falme za Kiarabu, Abu Dhabi. June 30,2019. 
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akiwa katika mazungumzo na mwenyeji wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Serikali ya Umoja wa Falme za kiarabu Sheikh Abdullah bin Zayed Al Nahyan,Abu Dhabi,Umoja wa Falme za Kiarabu. June 30,2019.  0 0

  Meneja wa Kanda wa NMB, Badru Idd (kushoto) akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari kuelezea namna Benki ya NMB ilivyojipanga kukidhi mahitaji ya wateja wao ndani ya Maonesho ya 43 ya kimataifa ya Biashara yanayoendelea viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere, Barabara ya Pugu, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja Msimamizi wa Banda la NMB ndani ya Viwanja vya Sabasaba, Bi. Kidawa Masoud.
  Meneja wa Kanda wa NMB, Badru Idd (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kuelezea namna Benki ya NMB ilivyojipanga kukidhi mahitaji ya wateja wao ndani ya Maonesho ya 43 ya kimataifa ya Biashara yanayoendelea viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere, Barabara ya Pugu, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja Msimamizi wa Banda la NMB ndani ya Viwanja vya Sabasaba, Bi. Kidawa Masoud.

  Meneja Msimamizi wa Banda la NMB ndani ya Viwanja vya Sabasaba, Bi. Kidawa Masoud (kulia) akizungumza na waandishi wa habari kuelezea namna Benki ya NMB ilivyojipanga kukidhi mahitaji ya wateja wao ndani ya Maonesho ya 43 ya kimataifa ya Biashara yanayoendelea viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere, Barabara ya Pugu, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja wa Kanda wa NMB, Badru Idd akiwa katika mkutano huo.
  Meneja Msimamizi wa Banda la NMB ndani ya Viwanja vya Sabasaba, Bi. Kidawa Masoud (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuelezea namna Benki ya NMB ilivyojipanga kukidhi mahitaji ya wateja wao ndani ya Maonesho ya 43 ya kimataifa ya Biashara yanayoendelea viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere, Barabara ya Pugu, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja wa Kanda wa NMB, Badru Idd akiwa katika mkutano na wanahabari.

  Meneja wa Kanda wa NMB, Badru Idd (kulia) akizungumza na waandishi wa habari kuelezea namna Benki ya NMB ilivyojipanga kukidhi mahitaji ya wateja wao ndani ya Maonesho ya 43 ya kimataifa ya Biashara yanayoendelea viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere, Barabara ya Pugu, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Benki ya NMB, Vicent Mnyanyika akiwa katika mkutano huo.

  Mmoja wa wateja wa Benki ya NMB (kushoto) akipata huduma ndani ya Banda la Benki ya NMB alipotembelea banda hilo.  BENKI ya NMB imejipanga kutoa huduma zote za kibenki wa washiriki na wananchi wanaotembelea maonesho ya 43 ya kimataifa ya biashara yanayoendelea viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara ya Pugu jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza na wanahabari leo ndani ya Banda la Benki ya NMB, Meneja wa Kanda wa NMB, Badru Idd alisema benki hiyo imejipanga kutoa huduma zote muhimu za kibenki ili kuhakikisha wanakidhi mahitaji yote kwa washiriki wa maonesho hayo.

  Aliwataka washiriki na wananchi wengine kutoumiza vichwa pindi watakapo hitaji huduma za kibendi ndani ya viwanja hivyo kwani benki hiyo imejipanga kutoa huduma zote muhimu za kibenki.Aidha aliwaomba wananchi kutembelea Banda la NMB kujipatia huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupata maelezo ya huduma mpya na bora kwa wateja wake.

  Kwa upande wake Meneja Msimamizi wa Banda la NMB ndani ya viwanja vya Sabasaba, Bi. Kidawa Masoud aliongeza kuwa huduma za NMB ndani ya maonesho ya 43 ya Biashara Kimataifa ni sawa na huduma zinazotolewa na tawi lolote kubwa la NMB hivyo kuwashauri wananchi kutembelea kipata huduma zote muhimu ndani ya viwanja hivyo.

  "...Huduma za NMB zinazotolewa katika maonesho ya 43 ya kimataifa ya biashara yanayoendelea viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere ni sawa na huduma zinazotolewa na tawi letu lolote...tuna mambo mengi mazuri kwa wateja na watakaotutembelea waje kwa wingi wafurahiye huduma zetu," alisema Bi. Masoud.

  0 0

  MWANARIADHA Magdalena Shauri akipokea zawadi kutoka kwa mgeni rasmi kwa niaba ya mkuu wa wilaya Monduli Meneja wa benki ya NMB Monduli Rebecca Lobulu mara baada ya kun'gara katika mashindano ya riadha ya Monduli Maasai Marathon yaliyofanyika juzi wilayani hapo.(Habari Picha na Pamela Mollel,Arusha)
  MWANARIADHA Marco Joseph akipokea zawadi kutoka kwa mgeni rasmi kwa niaba ya mkuu wa wilaya Monduli Meneja wa benki ya NMB Monduli Rebecca Lobulu mara baada ya kun'gara katika mashindano ya riadha ya Monduli Maasai Marathon yaliyofanyika juzi wilayani hapo.
  MWANARIADHA Asha Samwe akipokea zawadi kutoka kwa mgeni rasmi kwa niaba ya mkuu wa wilaya Monduli Meneja wa benki ya NMB Monduli Rebecca Lobulu mara baada ya kun'gara katika mashindano ya riadha ya Monduli Maasai Marathon nafasi ya pili yaliyofanyika juzi wilayani hapo.
  MWANARIADHA Josephat Joshua akipokea zawadi kutoka kwa mgeni rasmi kwa niaba ya mkuu wa wilaya Monduli Meneja wa benki ya NMB Monduli Rebecca Lobulu mara baada ya kun'gara katika mashindano ya riadha ya Monduli Maasai Marathon nafasi ya pili yaliyofanyika juzi wilayani hapo
  MWANARIADHA Mayselina Mbua akipokea zawadi kutoka kwa mgeni rasmi kwa niaba ya mkuu wa wilaya Monduli Meneja wa benki ya NMB Monduli Rebecca Lobulu mara baada ya kun'gara katika mashindano ya riadha ya Monduli Maasai Marathon nafasi ya tatu yaliyofanyika juzi wilayani hapo
  MWANARIADHA Fabiano Joseph akipokea zawadi kutoka kwa mgeni rasmi kwa niaba ya mkuu wa wilaya Monduli Meneja wa benki ya NMB Monduli Rebecca Lobulu mara baada ya kun'gara katika mashindano ya riadha ya Monduli Maasai Marathon nafasi ya tatu yaliyofanyika juzi wilayani hapo
  Mgeni rasmi kwa niaba ya mkuu wa wilaya Monduli Meneja wa benki ya NMB Monduli Rebecca Lobulu akizungumza katika mashindano hayo mara baada ya kukabidhi zawadi washindi walioongoza katika mashindano ya riadha 
  Mmoja wa waandaaji wa Monduli Maasai Marathon Meja Humphrey Nyuchi ambaye ni mkurugenzi mwenza alisema lengo hasa za mbio hizo kuimarisha michezo ,elimu na afya na mbio hizo zililenga katika kutangaza vivutio na fursa zilizopo Monduli.
  Kikundi cha ngoma kabila maarufu la kimaasai kikitoa burudani katika mashindano hayo,
  Mkurugenzi wa shule ya Upendo Friends Isabella Mwampamba akitoa zawadi shilingi elfu ishirini kwa mama aliyeshiriki mashindano hayo ya riadha huku akiwasii wanawake kujitokeza kwa wingi kushiriki michezo
  Mkurugenzi wa shule ya Upendo Friends Isabella Mwampamba akiwa katika picha ya pamoja na watoto walioshiriki mashindano hayo,amabapo alidhamini Zawadi za watoto zenye thamani ya shilingi laki tatu
  Kikundi cha Arusha runners wakishangilia zawadi ya mbuzi (2)walizokabidhiwa mara baada ya kutajwa kuwa wahamasishaji wa zuri wa shindano hilo  Na PamelaMollel,Monduli

  Mashindano ya riadha maarufu kwa jina la Monduli Maasai Maradhon imekuwa kivutio kikubwa kwa wananachi waliojitokeza kuangalia shindano hilo lililowashirikisha wadau mbalimbali 

  Mashindano hayo ya riadha yaliyofanyika juzi yanatajwa kuwa mashindano ya kwanza kufanyika Monduli na kufanya washiriki mbalimbali walioshinda kujinyakulia zawadi 

  Wanariadha Marco Joseph na Magdalena Shauri wamefanikiwa kushika nafasi ya kwanza katika mashindano ya riadha ya Monduli Maasai Marathon 

  Kwa wanaume waliokimbia kilomita 21 Joseph Kutoka talenti alitumia Muda wa saa 1:19:27 akifuatiwa na Josephat Joshua Kutoka Polisi kwa muda wa 1:05:54 huku nafasi ya tatu akishilia Fabiano Joseph kutoka JWTZ kwa muda wa saa 1:06:13.

  Kwa wanawake Magdalena Shauri aliongoza kwa muda wa saa 1:19:27 akifuatiwa na Asha Samwe kwa muda wa saa 1:20:16 huku nafasi ya tatu ikimwendea Mayselina Mbua kwa muda wa 1:20:32.

  Zaidi ya wanariadha 200 walishiriki mbio hizo za km 21,km 5 na km 2.5 ambazo ziliongozwa na mkuu wa wilaya Monduli Idd Kimanta ambapo washindi walikabidhiwa Zawadi za fedha na medali na tishirt.

  Washindi kwa kilomita 21 kwa wanaume na wanawake ,Mshindi wa kwanza Alipata shilingi laki 500,000 na ,mshindi wa pili 300,000 na Mshindi wa tatu 200,000, Mshindi wa nne 150,000 na Mshindi wa Tano 100,000 pamoja na katoni za vinywaji huku Zawadi za mbuzi mnyama zilitolewa kwa baadhi ya washindi wengine.

  Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa wilaya Monduli Meneja wa benki ya NMB Monduli Rebecca Lobulu aliwapongeza waandaaji na washiriki,huku akisistiza kuwa michezo ni fursa ya ajira na pia inaimarisha mwili

  Alitoa wito kwa wazazi kuwahimiza wototo michezo na badala yake waache kubeza watoto wanaofanya vizuri katika michezo.Mmoja wa waandaaji wa Monduli Maasai Marathon Meja Humphrey Nyuchi ambaye ni mkurugenzi mwenza alisema lengo la mashindano hayo kuibua fursa zilizopo katika eneo hilo pamoja na kuimarisha michezo

  Alisema ni Mara ya Kwanza mbio hizo zinazinduliwa na matarajio mbio hizo zitakuwa endelevu kwa ila maana ya kuwa zitafanyika kila mwaka mwishoni mwa mwezi Juni .Naye mkurugenzi wa shule ya Upendo Friends Isabella Mwampamba ambaye walidhamini Zawadi za watoto zenye thamani ya shilingi laki tatu alisema kupitia michezo watotonwanaweza kufanya vizuri zaidi

  Alisema serikali iweke mkazo zaidi kuwekeza katika michezo kuanzia ngazi za chini ili kuweza kuwa na vijana watakaofanya vizuri baadae na kuliwakilisha taifa vyema.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga (kushoto) akizungumza na wageni na wafanyakazi wa kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania Plc baada ya uzinduzi wa duka jipya la kampuni hiyo lililopo Kigoma mjini hivi karibuni. Kampuni ya Vodacom ina maduka takribani 100 na madawati ya huduma (Service desks) 350 na inaendelea kupanua upatikanaji wa huduma ili kuwawezesha wateja wake kupata huduma kirahisi zaidi. Kulia ni Mkuu wa mauzo wa Vodacom Kanda ya Ziwa Domician Mkama, wengine ni watoa huduma wa duka hilo jipya.   


   Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga (kushoto) akisaidiwa kuweka alama ya kidole na Mkuu wa mauzo wa Vodacom Kanda ya Ziwa, Domician Mkama kwa ajili ya kusajili laini ya mtandao huo wakati wa hafla ya uzinduzi wa duka jipya la Vodacom Kigoma mjini hivi karibuni. 

   Mkuu wa Mauzo wa Vodacom Kanda ya Ziwa, Domician Mkama (kushoto) akizungungumza na wateja wa kampuni hiyo waliohudhuria uzinduzi wa duka jipya la Vodacom  lililopo kigoma mjini hivi karibuni. Kampuni ya Vodacom ina maduka takribani 100 na madawati ya huduma 350 (Service Desks) na inaendelea kupanua upatikanaji wa huduma ili kuwawezesha wateja wake kupata huduma kirahisi zaidi.  Kushoto ni  Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga  na  wengine pichani ni watoa huduma wa duka hilo duka hilo jipya.


  0 0  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akitoa hotuba kwa maelfu ya wakazi wa jiji la Dar Es salaam waliojitokeza kwenye matembezi ya hisani yalioandaliwa na Shirika la Kimataifa la Amref Heath Africa limeshirikiana na Benki ya Azania (ABL) kuandaa matembezi chini ya mpango wa 'Stand up for African Mothers’, maarufu kama SU4AM, ambayo ni kampeni ya Amref Health Africa yenye lengo la kuhamasisha watu duniani kote kuhakikisha kuwa kina mama wanapata huduma ya msingi za matibabu wanayohitaji wakati wa ujauzito na vilevile wakati wa kujifungua. Matembezi yalifanyika jijini Dar es salaam ,mapema mwishoni wa wiki .

  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akimkabidhi zawadi ya cheti Mkurungezi wa Azania Bank Charles Itembe kwa mchango mkubwa waliotoa kufanikisha matembezi hayo ya hisani yanayolenga kuwezesha uwepo wa wakunga kwa uzazi salama nchini.

  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu na waziri wa afya na ustawi wa jamii Zanzibar,Mh. Hamad Rashid Mohamed wakiongoza matembezi ya hisani yalioandaliwa na Shirika la Kimataifa la Amref Heath Africa limeshirikiana na Benki ya Azania (ABL) kuandaa matembezi chini ya mpango wa 'Stand up for African Mothers’, maarufu kama SU4AM, ambayo ni kampeni ya Amref Health Africa yenye lengo la kuhamasisha watu duniani kote kuhakikisha kuwa kina mama wanapata huduma ya msingi za matibabu wanayohitaji wakati wa ujauzito na vilevile wakati wa kujifungua. Matembezi yalifanyika jijini Dar es salaam ,mapema mwishoni wa wiki .

  Mkurugenzi Mkaazi wa Amref Health Africa Tanzania, Dkt. Florence Temu akitoa hotuba mara baada ya matembezi ya hisani matembezi ya hisani yalioandaliwa na Shirika la Kimataifa la Amref Heath Africa limeshirikiana na Benki ya Azania (ABL) kuandaa matembezi chini ya mpango wa 'Stand up for African Mothers’, maarufu kama SU4AM, ambayo ni kampeni ya Amref Health Africa yenye lengo la kuhamasisha watu duniani kote kuhakikisha kuwa kina mama wanapata huduma ya msingi za matibabu wanayohitaji wakati wa ujauzito na vilevile wakati wa kujifungua. Matembezi yalifanyika jijini Dar es salaam ,mapema mwishoni wa wiki 
   
   
   Shirika la Kimataifa la Amref Heath Africa limeshirikiana na Benki ya Azania (ABL) kuandaa matembezi chini ya mpango wa 'Stand up for African Mothers’, maarufu kama SU4AM, ambayo ni kampeni ya Amref Health Africa yenye lengo la kuhamasisha watu duniani kote kuhakikisha kuwa kina mama wanapata huduma ya msingi za matibabu wanayohitaji wakati wa ujauzito na vilevile wakati wa kujifungua.

  Kufuatia kauli mbiu ya ‘Wezesha Uwepo wa Wakunga Zaidi kwa Uzazi Salama”, matembezi ya hisani ya SU4AM yaliyoongozwa na Mheshimiwa. Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto katika kumuakilisha Makamu wa Raisi Mama Samia Suluhu Hassan, aliongozana na Mheshimiwa. Hamad Rashid Mohamed, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii kwa Zanzibar katika viwanja vya Green Grounds, Oysterbay jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza na maelfu ya washiriki waliojitokeza katika viwanja vya green ground, Mkurugenzi Mkaazi wa Amref Health Africa Tanzania, Dkt. Florence Temu alisema kuwa kwa mwaka huu mpango huu wa SU4AM imelenga (i) kuendelea kuhabarisha na kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa uwepo wa wakunga wenye ujuzi ili kuwezesha uzazi salama na kuepusha vifo ambavyo vingeweza kutokea hasa wakati wa kujifungua. (ii) lengo kubwa ni kukusanya fedha kwa ajili ya kuwezesha uwepo wa wakunga katika vituo vya afya ambapo matembezi haya yanalenga kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 1 za kitanzania kwa muda wa miaka mitatu ( 2019-2021) (iii) kuhamisha na kuwezesha uwepo wa wakunga zaidi kwa uzazi salama katika vituo vya afya.

  Wakunga hawa ni kiungo muhimu katika kutoa huduma stahiki za afya hasa ya uzazi na wakati wa kujifungua na baada ya kujifungua, hivyo basi tunaomba na kuwasihi wananchi wote na kupitia makundi mbalimbali pamoja na mashirika na makampuni binafsi na washiriki wa maendeleo, waendelee kuchangia ili kukidhi lengo hili ili tuokoe maisha ya mama na mtoto katika maeneo yenye uhitaji Tanzania.

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa ABL, Ndg. Charles Itembe , aliongea na umati uliojitokeza katika matembezi haya na kusisitizia lengo la benki hiyo katika kusaidia sekta ya afya, hasa katika afya ya uzazi kama moja ya nguzo za msingi za sera ya uwajibikaji wa kijamii wa kampuni ya ABL. "Wanawake wa Kiafrika ni nguzo ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi," alisema Itembe, akibainisha kuwa bila ya huduma za msingi za afya, wanawake katika nchi zinazoendelea kama Tanzania, wataathririka kwa vifo vya uzazi kwa kiwango cha juu ambacho kitasababisha upungufu wa maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

  Ndg. Itembe aliongeza kuwa ABL imetambua uhitaji wa kuunga mkono washikadau wengine kama Amref Health Africa katika suala la kuchangia mabadiliko chanya ya maisha katika sekta ya afya, elimu na uchumi. Katika matembezi hayo, ABL ilichangia kwa hali na mali kwa kutoa fedha pamoja na kuwadhamini wakunga-wanafunzi watakaotoa huduma ya afya ya uzazi katika maeneo mbalimbali nchini.

  Tafiti zinaonyesha kuwa kina mama zaidi ya 200,000 wa Bara la Afrika hufariki kila mwaka kutokana na ukosefu wa huduma za matibabu. Aidha, asilimia 40 ya wanawake wa Afrika hawapati huduma za kliniki kabla ya kujifungua, na zaidi ya nusu yao hujIfungulia nyumbani. Vile vile, watoto milioni 1.5 wanaachwa bila mama kila mwaka kutokana na viwango vya juu vya vifo vya uzazi.

  Kwa upande mwingine, utafiti wa Kidemografia na Afya wa mwaka 2015-16, ulibaini vifo vya mama vilivyosabishwa na uzazi kuwa 556 kwa kila vizazi hai 100,000– idadi hii inamaanisha kuwa takriban kina mama 30 wa kitanzania hufariki kila siku kutokana na matatizo ya ujauzito. Hata hivyo tunaamini kutokana na Juhudi kubwa zinazoendelea katika awamu hii, ya kuongeza vituo vya afya, vitendea kazi na madawa, elimu ya huduma za dharura za wakati wa kujifungua

  ikiwemo na kuweka vyumba vya upasuaji katika vituo vya afya, elimu kwa jamii.. ushirikiswaji wa wadau na wafadhili mbalimbali, kiwango hicho cha vifo kitapungua kwa kiasi kikubwa.

  Kwa kuunga mkono na programu ya Amref Health Africa. Itembe alisema, ABL inalenga kuchangania kwa kiwango kikubwa kupunguza idadi ya vifo visababishwavywo na uzazi Tanzania na kuhamasisha kauli mbiu ya Amref Health Africa ya; “Wezesha Uwepo wa Wakunga Zaidi kwa Uzazi Salama”.

  0 0
  0 0


  Meneja KIongozi wa Uhusiano na Elimu kwa Umma wa NSSF Bi Lulu Mengele akitoa elimu kuhusu huduma mbalimbali zitolewazo na NSSF katika banda la NSSF na PSSSF katika maonesho ya kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa.
  Afisa Uhusuano wa NSSF Bi Aisha Sango akitoa ufafanuzi kwa mgeni alietembelea banda la NSSF na PSSSF katika maonesho yanayoendelea ya kimataifa ya Sabasaba katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa.
  Meneja KIongozi wa Uhusiano na Elimu kwa Umma wa NSSF Bi Lulu Mengele akitoa elimu kuhusu huduma mbalimbali zitolewazo na NSSF katika banda la NSSF na PSSSF katika maonesho ya kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa.
  Afisa matekelezo wa NSSF Ndugu Abdulaziz Abeid akitoa ufafanuzi kwa mgeni alietembelea banda la NSSF na PSSSF katika maonesho yanayoendelea ya kimataifa ya Sabasaba katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa.
  Maafisa Uhusiano wa NSSF (Aisha Sango, Kushoto na Amani Marcel, Katikati) na wa PSSSF (Coleta Mnyamani) wakitoa elimu kwa wageni mbalimbali kuhusu huduma mbalimbali zitolewazo na Mifuko hiyo katika maonesho ya kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa.
  Afisa Uhusuano wa PSSSF ndugu Abdul Njaidi akitoa ufafanuzi kwa mgeni alietembelea banda la NSSF na PSSSF katika maonesho yanayoendelea ya kimataifa ya Sabasaba katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa

  0 0

   Mkuu wa Kitengo cha Habari wa Mwananchi Communications Limited (MCL), Frank Sanga, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Francis Nanai, Afisa Mwandamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Jehud Ngolo na Meneja Masoko wa MCL, Sarah Munema wakiwa katika  waliazindua promosheni ya Shinda Mchongo wa Mwanaspoti ilifanyika  leo jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Francis Nanai, akionesha gazeti la Mwanaspoti  katika uzinduzi wa  promosheni ya Shinda Mchongo wa Mwanaspoti leo jijini Dar es Salaam.
  Afisa Mwandamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Jehud Ngolo kushoto akizungumza mara baada ya kuzinduzi  promosheni ya Shinda Mchongo wa Mwanaspoti ilifanyika  leo jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Kikundi/ Chama cha kusaidiana cha Familia Yenye Upendo (Family with Passion-FAWIPA) kilichopo Nyegezi jijini Mwanza, kimetimiza mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwake ambapo hafla ya kusherehekea mafanikio yake imefanyika jana jumapili Juni 30, 2019 ndani ya Passion Hotel.

  Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
  Mwenyekiti wa FAWIPA, Twalib Mafele akizungumza kwenye hafla ya chama hicho iliyofanyika jana ukumbi wa Passion Hotel ikiambatana na harambee kabambe ya kuimarisha chama.
  Mgeni rasmi kwenye hafla hioyo alikuwa Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Dkt. Philis Nyimbi ambaye aliwakilishwa na Afisa Mtendaji Kata ya Nyegezi, Shaaban Mpuya (katikati).
  Mwakilishi wa Mbunge wa Jimbo la Nyamagana akitoa salamu zake kwenye hafla hiyo.
  Mmoja wa wageni waalikwa akitoa nasaha zake kwenye hafla hiyo.
  Baadhi ya wageni waalikwa wakitoa salamu zo kwenye hafla hiyo.
  Mgeni rasmi akikabidhi zawadi kwa mmoja wa wanachama wa FAWIPA ambaye alionesha ushiriki mzuri wa shughuli mbalimbali za chama.
  FAWIPA ilitoa motisha kwa wanachama wanne walioonyesha ushiriki mzuri wa shughuli mbalimbali za chama.
  Washiriki kutoka vyama vingine rafiki pia walialiwa kwenye hafla hiyo.
  Wanachama wa FAWIPA pamoja na wageni waalikwa walisimama kwa dakika moja kama ishara ya kumkumbuka mmoja wa waasisi wa chama hiki, mwanahabari Cathbert Japhet ambaye pia ndiye aliyependekeza jina la chama kuitwa Familia yenye Upendo, aliyefariki dunia usiku wa kuamkia Mei 13, 2019.

  Wanachama na wageni waalikwa wakiwa ukumbini.
  Wanachama na waalikwa mbalimbali wakiwa ukumbini.
  Wasaa wa maakuli pia ulikuwepo.
  Wasaa wa kusakata rhumba pia ukawadia.
  Katibu wa FAWIPA, Innocent Alloyce (kushoto) akiweka kumbukumbu na baadhi ya waalikwa kwenye hafla hiyo.
  Tazama Video hapa chini

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza na Wajumbe  wa Tume ya Utumishi ya Polisi, Uhamiaji na Magereza wakati wa kikao cha kujadili utendaji wa vyombo vilivyopo chini ya wizara.Kikao hicho kimefanyika Ukumbi wa wizara jijini Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza na Wajumbe  wa Tume ya Utumishi ya Polisi, Uhamiaji na Magereza (hawapo pichani), kikao cha kujadili utendaji wa vyombo vilivyopo chini ya wizara.Kulia ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo Meja Jenerali Jacob Kingu.Kikao hicho kimefanyika Ukumbi wa wizara jijini Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu,akifafanua jambo mbele ya Wajumbe  wa Tume ya Utumishi ya Polisi, Uhamiaji na Magereza (hawapo pichani), wakati  wa  kikao cha kujadili utendaji wa vyombo vilivyopo chini ya wizara. Kulia  ni Waziri wa wizara hiyo Kangi Lugola. Kikao hicho kimefanyika Ukumbi wa wizara jijini Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia),Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,Meja Jenerali Jacob Kingu na Kamishna wa Polisi Benedict  Wakulyamba, wakipitia vitabu wakati wa kikao cha kujadili utendaji wa vyombo vilivyopo chini ya wizara.Kikao hicho kimefanyika Ukumbi wa wizara jijini Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
  Kamishna wa Magereza, Faustine Kasike  akizungumza wakati wa Kikao cha kujadili utendaji wa vyombo vilivyopo chini ya wizara.Kulia ni Kamishna wa Uhamiaji Dk. Anna Makakala.Kikao hicho kimefanyika Ukumbi wa wizara jijini Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
  Kamishna wa Uhamiaji ,Dk. Anna Makakala akizungumza wakati wa kikao cha kujadili utendaji wa vyombo vilivyopo chini ya wizara.Kushoto  ni Kamishna wa Magereza  Faustine Kasike.Kikao hicho kimefanyika Ukumbi wa wizara jijini Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
  Kamishna wa Polisi, Benedict Wakulyamba akizungumza wakati wa kikao cha kujadili utendaji wa vyombo vilivyopo chini ya wizara.Kikao hicho kimefanyika Ukumbi wa wizara jijini Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

  0 0


  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

  Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) wamewasogezea karibu huduma Wanachama wa Mifuko hiyo katika msimu huu wa Maonesho ya 43 ya Bishara ya Kimataifa ya Dar es Salaam maarufu Sabasaba.

  Wakizungumza leo Julai 2, 2019 kwa nyakati tofauti Wakurugenzi Wakuu wa Mifuko hiyo, Bw. Hoseah E. Kashimba (PSSSF) na Bw. William Erio (NSSF) wamesema kuwa wameamua kufanya maonesho hayo kwa kushrikiana ili kuwarahisishia Wanachama kupata huduma wanazohitaji wote wakiwa kwenye banda namba 13 lililo mkabala na jingo la matangazo ndani ya viwanja vya Sabasaba.

  “Tukiwa katika banda hili kwa kushirikiana na wenzetu wa NSSF ambao wao wanashughulika na wafanyakazi kutoka Sekta Binafsi na sisi PSSSF tunahudumia wafanyakazi kutoka Sekta ya Umma.”

  Tumeona tufanye maonesho haya pamoja kwa sababu ya kutoa elimu kwa wanachama kwa urahisi zaidi hasa kwa vile hatuko katika ushindani kama ilivyokuwa hapo awali, hii itasaidia kama Mwanachama anataka kujua taarifa kuhusu Mafao yake kama anatoka Sekta binafsi ataelekezwa aende NSSF na kama anatoka Sekta ya Umma ataelekezwa aende PSSSF, amefafanua Bw. Kashimba.

  Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Bw. William Erio alisema “Baada ya kuunganishwa Mifuko hapo mwaka jana bado watu hawajaelewa vema tofauti zilizopo kwa hiyo wanakuja hapa kama banda pekee linalotoa huduma ya Hifadhi ya Jamii na wakifika basi wanaelekezwa katika sehemu husika na kupata huduma wanayohitaji.” Alisisitiza Bw. Erio.

  Alisema ni sehemu ambayo watu wanaweza kuja na kujibiwa maswali yote waliyonayo na kutatuliwa kero zao. Maonesho hayo ya kila mwaka yamefunhguliwa rasmi leo Julai 2, 2019 na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan na yanatarajiwa kufikia kilele Jlai 13, 2019.
  Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF Bw. Hoseah E. Kashimba (wapili kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bw. William Erio (wapili kushoto) wakiwa na Mameneja Kiongozi Uhusiano na Elimu Kwa Umma, Bi. Eunice Chiume (kushoto) ambaye yuko PSSSF na Bi. Lulu Mengele (kulia) ambaye yuko NSSF.
  Bw. Erio (kushoto) na Bw. Kashimba wakibadilishana mawazo ndani ya banda hilo. Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Bw. Hoseah E. Kashimba, (kushoto), akimuhudumia Mwanachama wa Mfuko huo aliyetembelea banda namba 13 la Mfuko huo na ule wa NSSF.
  Picha ya pamoja ya wafanyakazi wa PSSSF na NSSF katika banda namba 13 viwanja vya Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam.

  0 0

  Tuzo ya “Best Logistics and Transportation Exhibitor” ambayo Shirika la Posta Tanzania limeshinda katika maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba 2019. Shirika la Posta Tanzania wamenyakua Tuzo ya washindi wa kwanza katika kipengele cha BEST LOGISTICS AND TRASPORTATION EXHIBITOR iliyofanyika katika maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba 2019 iliyotolewa na Makamu wa Raisi Mama Samia Suluhu Hassan wakati akifungua maonyesho hayo.   Baadhi ya wafanyakazi wakishika tuzo waliyoiopata baada ya Shirika kushinda tuzo ya Best Logistics and Transportation Exhibitor. Maonesho haya ya 43 ya Sabasaba yenye kauli mbiu “ Usindikaji wa mazao ya kilimo kwa maendeleo endelevu ya viwanda” yalianza rasmi Juni 28 na yatamalizika Julai 13 mwaka huu ambapo Shirika la Posta Tanzania ni mmoja wa washiriki kwa mwaka huu. Unapoingia kwenye Geti kuu la viwanja vya maonesho, Shirika la Posta tupo kwenye barabara ya kwanza kushoto mita chache kutoka geti hilo. Na 1ni jengo la pili kulia unapoingia Geti la mizigo (Geti 2).  Duka la kiamtandao lililoko ndani ya viwanja vya sabasaba. Usajili kwa wafanyabiashara na wenye bidhaa ni bure, kujisajili pitia wesite yetu ya www.postashoptz.post Huduma zinazotolewa ni kubadisha fedha za kigeni, kusajili bure kwa makampuni, wakulima, wafanyabiashara wakubwa na wadogo, pamoja na sekta ya usafirishaji kujiunga na huduma yetu ya E-commerce na kufanya biashara kupitia mtandao wetu wa Posta online. Pia wana duka la kubadilishia fedha ndani ya viwanja vya Sabasaba ambapo mteja ataweza kubadili fedha yake ya kigeni ndani ya viwanja. Wanahuduma ya EMS, kusajili masanduku mapya na huduma ya kulipia masanduku, tunatoa maelezo juu ya huduma yetu mpya ya Posta mlangoni, ambapo mteja anaweza kupelekewa vifurushi na barua zake mpaka mlangoni kupitia wahudumu wetu wa Posta walioko nchi nzima. 
  Tunatoa huduma ya posta mlangoni na virtual Box, na kusajili masanduka mapya ya barua. 

   Watoa huduma wakiwa na nyuso za furaha kukukaribisha katika banda la Shirika la Posta Tanzania ili kuweza kujipatia huduma mbali mbali.

  0 0
older | 1 | .... | 1861 | 1862 | (Page 1863) | 1864 | 1865 | .... | 1897 | newer