Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live

Yaliyowasilishwa na Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo kwenye kongamano la rasilimali na madini UDASA

0
0


==============  ==========  ============
Mwishoni mwa wiki Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo alialikwa kwenye kongamano lililojadili  rasilimali za taifa ikiwa ni pamoja na ushirikishwaji wa wananchi lililofanyika katika  ukumbi wa Nkuruma, chuo kikuu cha Dar es Salaam. Kongamano hilo lilihusisha wadau wengine ikiwa ni pamoja na Mbunge wa Ubungo (Chadema) John Mnyika, Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Dkt Reginald Mengi na wadau wengine.

Nawasilisha presentation  za Mhe. Waziri kwa ajili ya kuhabarisha umma. Pia nimeambatisha na video iliyowasilishwa siku ya kongamano hilo.

TAMASHA LA UJASIRIAMALI KURINDIMA MWANZA IJUMAA HADI JUMAPILI

0
0
Mratibu wa Tamasha la Ujasiriamali, Abdallah Mrisho (wa pili kulia) akiongea jambo na waandishi wa habari leo ndani ya ukumbi wa The Atriums Hotel iliyoko Sinza, Afrika Sana jijini Dar es Salaam.
Meneja Mawasiliano wa Tigo, John Wanyancha (wa pili kushoto) akiongea na wanahabari (hawapo pichani). Kulia ni mratibu wa tamasha hilo, Abdallah Mrisho na kushoto ni H. Baba.
Abdallah Mrisho akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani).
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Bongo, Fid Q naye akielezea namna atakavyolitumia tamasha hilo kuwajenga vijana wa Mwanza katika maisha yao kupitia fani yake ya muziki.
Msanii kutoka jijini Mwanza, H. Baba, akielezea namna alivyojipanga kuwafikishia somo la ujasiriamali wakazi wa Mwanza.
Baadhi ya waandishi na wapiga picha (kulia) wakichukua matukio ya habari kuhusu tamasha hilo.

MENEJA Mkuu wa kampuni ya Global Publishers Ltd, ambaye pia ni mratibu mkuu wa Tamasha la Ujasiriamali linalotarajiwa kufanyika Ijumaa hii hadi Jumapili jijini Mwanza, Abdallah Mrisho, leo ameongea na baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali nchini na kuwaleleza kuhusu tamasha litakalofanyika siku ya Ijumaa katika Viwanja vya CCM Kirumba jijini Mwanza ambapo mikakati yote imekamilika.

Mrisho alisema tamasha hilo lililodhaminiwa na Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Benki ya NMB na Street University, limeandaliwa kuwawezesha vijana na wakazi wa Jiji la Mwanza kutambua mbinu mbalimbali za kujikwamua kimaisha. Watoa mada watakuwa ni Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers Ltd, Eric James Shigongo, James Mwang’amba, Emmanuel Mgaya (Masanja Mkandamizaji) na Mbunge wa Mbeya mjini Mh. Joseph Mbilinyi ‘Sugu’.

Kwa upande wa burudani kutakuwa na wasanii Fid Q, H. Baba, Young Killer, Jitta Man na Sugu. Pia kutakuwa na wasanii wa muziki wa Injili ambao ni Martha Mwaipaja atakayeimba sambamba na Masanja Makandamizaji na Edson Mwasabwite.
(Habari/Picha: Musa Mateja / GPL)

RAIS KIKWETE ALIPOSHIRIKI HAFLA YA KUMBUKUMBU YA MZEE NELSON MANDELA UWANJA WA FNB JIJIN JOHANNESBURG.

0
0
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Mama Salma Kikwete wakati wa hafla ya Kumbukumbu ya Mzee Nelson Mandela Uwanja wa FNB jijini Johannesburg Jumanne Novemba 10, 2013.
  Pichani juu na chini ni  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha Rais Barack Obama wa Marekani kwa viongozi mbalimbali wa Afrika wakati wa hafla ya Kumbukumbu ya Mzee Nelson Mandela Uwanja wa FNB jijini Johannesburg Jumanne Novemba 10, 2013.PICHA NA IKULU.

Shirika la Posta Tanzania lakusanya kiasi cha shilingi Bilioni 44.5 kufikia Mwaka 2012

0
0
Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta nchini Bw. Deus Mndeme akielezea kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya mpango kabambe wa miaka 10 wa shirika hilo kupitia utekelezaji wa sera na mipango mbalimbali pamoja na dira ya maendeleo ya Taifa ya 2025, kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari bi. Zamaradi Kawawa.

Meneja Mkuu Uendeshaji wa Biashara toka Shirika la Posta Bw. Fortunatus Kapinga akielezea kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya matumizi ya TEHAMA katika ofisi zake zipatazo 86 hapa nchini ili kutoa huduma kwa ufanisi.


Baadhi ya waandishi wa habari wakimfuatilia kwa karibu Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Bw. Deus Mndeme wakati akielezea mpango kabambe wa miaka 10 wa shirika hilo kupitia utekelezaji wa sera na mipango mbalimbali pamoja na dira ya maendeleo ya Taifa ya 2025.

Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta nchini Bw. Deus Mndeme akielezea kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya mpango kabambe wa miaka 10 wa shirika hilo kupitia utekelezaji wa sera na mipango mbalimbali pamoja na dira ya maendeleo ya Taifa ya 2025, Kushoto ni Meneja Mkazi Posta Zanzibar Bi. Mwanaisha Said. 
(Picha na Eliphace Marwa)


Na Frank Mvungi

Shirika la Posta Tanzania limefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi Bilioni 44.5 kufikia mwaka 2012 ikiwa ni matokeo ya kuboreshwa kwa huduma zake hapa nchini.

Hayo yamesemwa na Posta Masta Mkuu Bw. Deos Mndeme wakati alizungumza na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es salaam kuhusu mafaniko yaliyofikiwa na shirika hilo tangu kuanzishwa kwake.

Mndeme amesema kuwa mafanikio hayo yametokana na huduma bora zenye hadhi ya kimataifa zinazotolewa na shirika hilo kwa wananchi hali itakayosaidia kuongeza mapato ya Serikali.

“Shirika limejipanga zaidi kutumia TEHAMA katika kuboresha huduma zake ikiwa ni moja ya mkakati utakaosaidia serikali kuongeza mapato na kufikia malengo ya muda mrefu yaliyowekwa na shirika pia tumejipanga kuendelea kuboresha huduma tunazozitoa ili kuendana na mahitaji ya wakati” alisema Mndeme.

Mndeme aliongeza kuwa kwa sasa shirika limeunganisha Ofisi 86 kwenye Wilaya na Miji kote nchini na mfumo wa mawasiliano ili kuongeza idadi ya wateja wanaohudumiwa,kuondoa ucheleweshaji na kuondoa  malalamiko ya wateja.

Katika kuhakikisha shirika linashiriki kikamilifu katika shughuli za kitaifa Mndeme alisema shirika litafanya uzinduzi wa toleo jipya la stempu ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar katika sherehe hizo zitakazofanyika Disemba 28 mwaka huu.
  

Shirika la Posta ni mwanachama wa Umoja wa Posta Duniani (UPU) ambalo Tanzania ilijiunga mwaka 1963 na kwa hivi sasa idadi ya nchi wanachama wa umoja huo ni 192 malengo ya Umoja huo ni pamoja na kuisimamia,utumiaji wa barua,Vipeto,Vifurushi katika nchi mbalimbali duniani,kutoa ushauri,usuluhishi,kuunganisha ushirikiano baina ya nchi wanachama na kutoa misaada ya kiufundi.

MUME AMFYEKA MKEWE MIGUU NA MIKONO.

0
0

  

Heshima za mwisho kwa mwili wa Mandela

0
0
Viongozi mbali mbali pamoja na raia wa Afrika Kusini wanaendelea kutoa heshma za mwisho kwenye mwili wa aliyekuwa rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini Marehemu Nelson Mandela ambao umelazwa kwenye ikulu ya Afrika Kusini mji Mkuu wa Pretoria, ambapo utalala hapo kwa siku tatu.
Mwili ulichukuliwa katika msafara kutoka chumba cha maiti cha hosptali hadi kwenye jengo la Muungano. Msafara wenye jeneza la Marehemu uliondoka mjini katika Hosptali ya jeshi muda mfupi siku ya jumatano. Jeneza lilibebwa kwenye gari maalum na kufunikwa bendera ya Afrika Kusini.
Wananchi walijipanga kando kando ya barabara lilipopitishwa jeneza kama ishara ya kutoa heshma za mwisho kwa mwili wa marehemu. Msafara ulipita katika mitaa huku baadhi ya raia wakikimbia pembeni kwenye mstari wa askari wa wanajeshi Mwandishi BBC's Joseph Winter katika mji wa Pretoria amesema.
Wanajeshi waliobeba jeneza hilo walisonga hatua kwa hatua hadi katika Majengo ya Muungano eneo alikoapishwa kuwa rais wa kwanza mzalendo wa Afrika kusini 1994. Wanachi, wakuu wa nchi walioalikwa na wageni wengine wa kimataifa watapata nafasi ya kutoa heshima za mwisho kwenye mwili wa marehemu aliyefariki alhamisi akiwa na umri wa miaka 95. Wageni hata hivyo hawaruhusiwa kupiga picha.
Leo jioni wasanii mbali mbali wa Afrika Kusini watashiriki katika tamasha maalum la kumuenzi Mandela na ambalo wananchji wataruhusiwa kuhudhuria bila malipo. Marehemu Mandela atazikwa nyumbani kwake katika kijiji Qunu katika jimbo la Cape Mashariki siku ya jumapili.
Maelfu ya raia wa Afrika ya kusini hapa jana waliungana na viongozi mbali mbali duniani katika ibada ya kumbu kumbu siku ya jumanne kama sehemu ya mfululizo wa maombolezo kifo chicho.SOURCE BBC

Mkwere aula ubalozi wa kampuni ya simu bila jina

0
0
Kampuni inayoleta pamoja ubunifu na malengo kwa kuwa pekee kuzinduliwa bila jina.
 Muigizaji wa vichekesho  kwenye kundi la Mizengwe Hemedi Khalida maarufu kama Mkwere ameangukiwa na neema ya ubalozi wa kuhamasisha upatikanaji wa jina la  kampuni ya simu iliyoziduliwa bila jina. 
Kampeni hiyo itafanyika kupitia simu na mitandao mbalimbali ambapo wananchi wanatakiwa kuipatia jina kampuni hiyo. Mbali na hayo Mkwere atapata nafasi ya kupita mitaa mbalimbali akiwahimiza wananchi kupiga kura.
Sekta ya mawasiliano ya simu Tanzania na Afrika Mashariki imepata matumaini mapya kufuatia kuingia kwa kampuni mpya ya simu ya kipekee, ya ubunifu, yenye kuamini jamii, na yenye ushindani kuliko zote, kuzinduliwa bila jina.  
Pamoja na ahadi yake ya kuongeza idadi ya watumiaji wa mawasiliano ya mtandao wa simu, kampuni hiyo mpya kwa wakati mmoja imezindua pia kampeni ya kiubunifu inayotambulika kwa jina la “Tupe Jina” itakayofanyika kwa njia ya mtandao na ujumbe mfupi katika simu kwa lengo la kuipa fursa Afrika Mashariki kuichagulia jina bora kampuni hii kwa kupiga kura.  
Hii ni kampuni ya kwanza ya simu Afrika Mashariki ambayo kweli inajali na haigopi kuamini watu, na hakuna kampuni nyingine inaweza kuthubutu kufanya hivyo. Hakuna kampuni yoyote duniani iliyoweza kuzinduliwa bila jina na kutoa jukwaa kwa kampeni ya kusisimua kabla ya jina kuwekwa hadharani.
“Tupe Jina” ni kampeni itafanyika  kwa awamu mbili katika mtandao, ujumbe wa simu na mtandao wa kijamii wa facebook. Katika awamu ya kwanza, Afrika Mashariki inapaswa kuteua majina ambayo wanapenda hii kampuni mpya iitwe.
Mshirki anaweza kuchagua jina kwa kuingia katika mtandao wa Unaweza kuteua jina  kwa njia ya magogo kwenye mtandao wawww.giveusaname.net au kutuma ujumbe wa simu ukiambatanishwa na jina analopendekeza kwenda namba  15678 au aingie katika mtandao wa www.facebook.com/giveusaname. Katika awamu ya pili ya kampeni, jopo litatathmini majina yote na itatoa majina matano ambayo yamependekezwa mara nyingi zaidi, ya kipekee na yenye ubunifu.
 Baada ya hapo Afrika Mashariki watapiga kura kwa ajili ya kupata jina bora moja ambalo hatimaye litakuwa jina la kwanza la kampuni hii ya mawasiliano ya simu ambayo daima itakuwa ya kwanza ya Kiafrika Mashariki. Mshindi katika kampeni hii, mtu ambaye atakuwa amechagua jina ambalo hatimaye litakuwa la kampuni atajishindia muda wa bure wa kupiga simu za ndani na SMS bure kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Zawadi zingine zitakuwa simu za kisasa za ‘smartphone’ na kompyuta za kiganjani (tablets) kwa washiriki wa kampeni hii ya “Tupe Jina”.
Kutokana na wataalam kutabiri kuongezeka kwa pato la taifa la Tanzania kutoka asilimia 4 hivi sasa hadi asilimia 7 mwaka 2015, sekta ya mawasiliano ina nafasi kubwa ya katika ukuaji wa uchumi katika miaka ijayo na kampuni hii mpya ya mawasiliano ya inawakilisha sura ya kasi hii kubwa ya ukuaji.
Tanzania inabaki kuwa ni moja ya nchi zenye kiwango cha kuingiza simu chini ya asilimia 50 kufikia Juni 2013, jumla ya matumizi ya mawasiliano ya simu nchini humo ni chini ya wastani kwa nchi za Afrika.
Hii kampuni mpya ya simu kwa umuhimu mkubwa itawekeza kiasi kikubwa cha fedha kutoka kwa wateja wake kwa ajili ya maendeleo ya muda mrefu kwa watu wa Tanzania katika sekta ya afya na hasa katika tiba za kimtandao na vituo vya elimu ya masafa.
Hii tafsiri yake ni kwamba kuwekeza idadi kubwa ya faida katika kuwezesha Afrika Mpya kuzingatia ongezeko la watumiaji wa mawasiliano ya simu, na zawadi bora ambayo kampuni hii inatarajia katika miaka ijayo ni kukuza sekta ya afya.
Baada ya kampeni ya “Tupe Jina” wananchi wa Tanzania watapata nafasi ya kupeleka namba zao wanazopendekeza kabla ya kutangazwa na kuwekwa hadharani kwa jina la kampuni.

FM Academia kuzindua albam mpya Dec 21, Mashujaa kupamba

0
0

BENDI ya muziki wa dansi ya Mashujaa Musica 'Wazee wa Kibega'
inatarajia kupamba uzinduzi wa albamu ya 'Chuki ya Nini' ya bendi ya
FM Academia utakaofanyika Desemba 21 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Hayo yalisemwa jana Rais wa bendi hiyo, Nyoshi El-Saadat alipokuwa
akizungumza na waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari kuhusu
maandalizi ya uzinduzi huo aliodai kuwa utakuwa wa kishindo.
"Hii ni albamu yetu ya kumi ambayo imeandaliwa kwa ubora wa kimataifa
na sasa iko tayari kuzinduliwa Desemba 21 tukisindikizwa na bendi ya
Mashujaa Musica," alisema Nyoshi.



Nyoshi alitaja nyimbo za albamu hiyo kuwa ni 'Fataki', 'Otilia', 'Ndoa
ya Kisasa', 'Neema', 'Dai Chako Ulaumiwe', 'Maisha', 'Madudu',
'Miraessa' na 'Intro' ambazo zote zimeshaingizwa kwenye video.
Aliongeza kusema kuwa katika uzinduzi huo watawakumbuka pia kwa
kuwaombea watu wawili maarufu waliofariki dunia ambao ni Rais wa
zamani wa Afrika Kusini mzee Nelson Mandela na mwanamuziki mkongwe wa  Kongo, Tabu Ley.



Bendi ya FM Academia ilizindua albamu ya kwanza ya 'Hadija' mwaka 1998
kisha ikafuatia ya pili iitwayo 'Atomic' iliyozinduliwa mwaka 1999 na
baadaye mwaka uliofuata wa 2000 bendi hiyo ilizindua albamu ya tatu
iliyopewa jina la 'Prison'.



'Wazee wa Ngwasuma' hawakuishia hapo, mwaka 2001 walizindua albamu ya  nne iitwayo Freedom na kufuatiwa na ya tano ya 'Mpambe Nuksi'


iliyozinduliwa mwaka 2001 na kisha ikafuata ya sita iitwayo 'Dotnata'
mwaka 2003 kabla ya 'Dunia Kigeugeu' iliyozinduliwa mwaka 2006.
Baada ya hapo bendi hiyo ilikaa kidogo hadi mwaka 2010 ilipozindua
albamu mbili kwa mpigo ambazo ni 'Vuta Nikuvute' na 'Heshima kwa
Wanawake' na sasa mwaka huu wa 2013 unaumalizia kwa kuzindua albamu
ya 'Chuki ya Nini'.

SABC's Live Coverage

0
0

TAARIFA KUTOKA MKOA WA RUKWA

0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA WAZIRI MKUU

TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA




MKOA WA RUKWA

Telegraphic: “REGCOM”

Simu.  No:0252802137/2802138/2802144

Fax No. (025) 2802217/2802318

E-mail:rasrukwa@yahoo.com

            OFISI YA MKUU WA MKOA,

     P. O.  Box 128,

     SUMBAWANGA.

            

               


TAARIFA KWA UMMA.


Serikali Mkoani Rukwa inapenda kukanusha taarifa iliyotolewa na gazeti la Jambo Leo toleo namba 1546 la tarehe 3, Disemba 2013 iliyoandikwa na Mwandishi Gurian Adolf katika ukurasa wa 10 iliyokuwa na kichwa cha habari "TCCIA Rukwa yaomba mbolea ya DAP".


Sehemu ya taarifa hiyo ilieleza kuwa; Nanukuu "Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo (TCCIA) Mkoa wa Rukwa, Shadrack Malila ameiomba Serikali kuwashauri wakulima wa Mkoa huo kutumia mbolea nyingine ya kupandia mahindi badala ya mbolea ya minjingu ambayo haijafanyiwa utafiti katika Mkoa huo."


Kwa mujibu wa gazeti hilo taarifa hiyo aliitoa mbele ya waandishi wa habari Ofisini kwake mjini Sumbawanga ambapo aliongeza kuwa "Tangu awali wakulima hao walikataa mbolea hiyo, baada ya kuitumia kupandia na kushindwa kustawisha vizuri mazao yao ya mahindi, tofauti na mbolea ya DAP ambayo husaidia kupatikana kwa mazao mengi”. Mwisho wa kunukuu.


Serikali Mkoani Rukwa inapenda kukanusha kuwa sio kweli kwamba mbolea ya minjingu haijafanyiwa utafiti kufaa kutumika katika Mkoa huu na kwamba haijapokea malalamiko yeyote yaliyo rasmi kutoka kwa wananchi (wakulima) juu ya ubora na ufanisi wa mbolea hiyo. Matokeo yake yameonekana kuwa ni mazuri hususani baada ya mbolea hiyo kuboreshwa zaidi na sasa inaitwa "Minjingu Mazao".


Napenda ifahamike wazi kuwa tafiti mbalimbali za udongo zimefanyika Mkoani Rukwa mfano, taarifa ya  BRALUP, 1977, Tafiti za udongo zilizofanywa na Kituo cha Utafiti cha Uyole na Sampuli mbalimbali zilizopelekwa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) kutoka Halmashauri ya wilaya ya Nkasi miaka ya 2008-2010 na kuonesha sehemu kubwa ya udongo wa maeneo ya Uwanda wa juu wa Ufipa (Ufipa Plateau) kuna upungufu mkubwa wa kirutubisho cha aina ya Naitrojeni kulingana na mahitaji yake kwa mimea jamii ya nafaka, hasa mahindi chotara.


Aidha, majaribio ya kutumia aina na viwango mbalimbali vya mbolea kwa zao la mahindi ikiwemo Minjingu yamefanywa kupitia Kituo Kidogo cha Utafiti cha Uyole kilichokuwa wataalam huko Nkundi na mashamba ya majaribio sehemu mbalimbali na kutoa matokeo yaliyofanyiwakazi. Kufuatia majaribio hayo, Mkoa wa Rukwa ulitoa mapendekezo kwa kampuni ya Minjingu Mines & Fertilizer ya kubadilishwa kwa umbile la mbolea ya Minjingu kutoka katika umbile la unga (powder form) na kuwa katika umbile la sasa la chengachenga ili kuwa rahisi wakati wa kuweka mbolea shambani. Pia Mkoa ulipendekeza mbolea hiyo iwekewe kirutubisho aina ya Nitrojeni ili kukidhi mahitaji ya udongo wa sehemu kubwa ya Ukanda wa juu wa Ufipa, mapendekezo ambayo yamezingatiwa zimefanywa na matokeo yake kuonekanika.


Mashamba Darasa yanayohusisha mbolea ya Minjingu Mazao yameanzishwa na kuendeshwa sehemu mbalimbali za Mkoa katika msimu uliopita wa 2012/2013 na kukaguliwa na Viongozi kuona ufanisi wake. Yapo mashamba yaliyofanya vizuri na yapo ambayo hayakufanya vizuri. Hali ya tofauti kama hiyo hutokea kwa aina zote za mbolea zinapotumika katika maeneo tofauti. Ikumbukwe kuwa ardhi ipo hai na hutofautiana kutoka sehemu moja na nyingine!


Tafiti nyingi zimeonesha kuwa wakulima wengi wameshindwa kupata matokeo mazuri katika kilimo kwa kushindwa kufuata masharti ya wataalam wa kilimo hata kama wakitumia mbolea ya aina yeyote. Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Profesa Kauzeni na wenzake katika vijiji vya Ntendo na Mtimbwa mwaka 1998, pamoja na mambo mengine ilibainika kuwa wakulima wachache waliomudu kutumia mbolea au mbegu bora hawakuzingatia viwango vilivyopendekezwa na wataalam. Walitumia karibu nusu tu ya mapendekezo, Mfano Hekta moja iliyopandwa mahindi zilitakiwa kutumia kilo 125 za TSP Triple Super Phosphate ( P2O5 )18%  na kilo 250 za UREA (N) 46%, ili kuvuna tani sita za mahindi sawa na kilo 6,000 au wastani wa magunia 60 kwa hekta. Waliofanya vizuri kidogo walitumia kilo 100 tu za TSP na kilo 100 za UREA.


Kufuatia taarifa hiyo, Uongozi wa Mkoa wa Rukwa haupendi kuingilia uhuru wa mtu wa kupata na kutoa habari kama Mtanzania mwingine yeyote. Ni vema mtu akatoa taarifa anazozifahamu vizuri/zilizofanyiwa utafiti, zisizoleta mtafaruku au kuipotosha jamii na zisizolenga kuvutia maslahi binafsi kwa namna yeyote ile.


Serikali ya Mkoa imesikitishwa na taarifa aliyoitoa Bwana Malila. Ni dhahiri kuwa ametumia vibaya nafasi yake ya uenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Rukwa kuwashawishi wakulima wa Mkoa huu kuwa mbolea ya Minjingu haifai na haitowapa mavuno mazuri. Ikumbukwe kuwa Bwana Malila ambae ni msambazaji wa pembejeo zenye ruzuku ya Serikali katika Manispaa ya Sumbawanga kwa mwaka huu 2013/14 pia ni mfanyabiashara wa pembejeo za kilimo ikiwemo mbolea anayoipigia chapuo ya Diammonium Phosphate maarufu kama DAP.


Ifahamike pia kuwa Bwana Malila aliwahi kuwa na Mkataba na Kampuni ya Minjungu Mines & Fertilizer Ltd katika msimu wa kilimo wa mwaka 2009/2010. Kama kweli mbolea hiyo haifai mbona aliwahi kuwa wakala na akaisambaza kwa wakulima bila kutoa matamko kama haya? Ni dhahiri kuwa taarifa yake hiyo ina mgongano wa kimaslahi na hailengi katika kuboresha kilimo kwa wananchi wa Mkoa wa Rukwa.

Imetolewa na:

Albinus Mugonya,

Kaimu Katibu Tawala Mkoa,

RUKWA.


10 Disemba, 2013





TASAF yaanza kazi ya kutambua kaya masikini na zinazoishi katika mazingira hatarishi nchini

0
0
 Mtaalamu Mshauri wa  Mpango wa kunusuru kaya masikini unaoendeshwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii nchni TASAF  Rogelio Gomez Hermosillo akiwa katika kikao cha kujadili zoezi la utambuzi wa kaya masikini katika wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara.


Mfuko wa Maendeleo ya Jamii  TASAF umeanza kazi ya kutambua kaya masikini na zinazoishi katika mazingira hatarishi nchini kazi iliyoanza katika mikoa ya Mtwara na Lindi baada ya majaribio kufanyika katika wilaya za Bagamoyo,Kibaha,Chamwino na Bunda kuonyesha mafanikio makubwa,  zifuatazo ni baadhi ya shughuli zilizofanywa na Mtaalamu Mshauri wa Mpango huo kutoka Benki ya Dunia  ROGELIO GOMEZ HERMOSILLO aliyefanya ziara ya kuona namna kazi hiyo inavyoendelea mkoani Mtwara.

 Baadhi ya wawezeshaji katika mpango wa kunusuru kaya masikini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF  wakiwa katika kikao cha pamoja na Mtaalamu Mwelekezi kutoka Banki ya Dunia  Rogelio Gomez Hermosillo ( hayupo pichan)ikatika hafmashauri ya Masasi Mikindani.
 Mtaalamu Mshauri wa Mpango wa kunusuru Kaya Masikini unaoendeshwa na TASAF  Awamu ya TATU Rogelio  Gomez Hermosillo akizungumza na walengwa wa mpango huo katika mtaa wa Chuno  Manispaa ya Mtwara Mikindani juu ya umuhimu wa kutekeleza zoezi la utambuzi wa kaya masikini kwa uangalifu mkubwa. 

 Mtaalam wa Mafunzo na Ushiriki wa TASAF  Bi.Mercy  Mandao Mariki akifafana jambo kwa  walengwa  wa Mpango wa kunusuru kaya masikini katika Manispaa ya Mtwara Mikindani.

 Mtaalamu wa Mafunzo kutoka TASAF Bi Mercy Mandao Mariki akifafanua jambo kwa Mtaalamu Mwelekezi wa Mpango wa kunusuru kaya masikini  kutoka  Benki ya Dunia Rogello Gomez Hermosillo walipotembelea walengwa wa Mpango huo latika halmashauri ya wilaya ya Masasi mkoani Mtwara kuona namna kazi ya kutambua kaya masikini inavyoendelea.

Baadhi ya walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya masikini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF wakishiriki kazi ya utambuzi katika eneo la Chuno  Manispaa ya Mtwara Mikindani Mkoani Mtwara..

Wawezeshaji Ngazi ya halmashauri ya wilaya ya Masasi mkoani Mtwara wakimsikiliza Mtaalamu Mwelekezi wa Mpango wa kunusuru kaya masikini kutoka Benki ya Dunia Rogello Gomez Hermosillo (hayupo pichani) juu ya namna  ya kutambua kaya za walengwa wa mpango huo ulioanza kutekelezwa katika mikoa ya Lindi na Mtwara.

Mtaalam Mshauri wa Mpango wa kunusuu kaya masikini kupitia Mafuko wa Maendeleo ya Jamii nchini TASAF  Rogelio lGomez Hesmosillo  aliyeshika tama akisikiliza mchango wa mmoja wa  wawezeshaji wa mpango huo(hayupo pichani) wakati wa mjadala wa  namna zoezi la utambuzi wa kaya masikini katika halmashauri ya Mtwara Mkindani mkoani Mtwara linavyoendelea.

SALE SALE SALE @AK CLASSIC COSMETICS!!

0
0

 ILE CLEARENCE SALE YA MWISHO WA MWAKA NDANI YA @AK CLASSIC COSMETICS SASA IMEWADIA..JIPATIE MADINI YAO YAKIWA YAMESHUSHWA KWA KIASI KIKUBWA..MPAKA 50% . JIPATIE BIDHAA ZA VICTORIAS SECRETS,SIGNATURE COLLECTION,OTENTIKA,AVON NA VINGINE KIBAO KWA BEI YA SALE SALE!!
 SALE KUANZA 12/12/13 MPAKA MWISHO WA BIDHAA!!

 KWA MAELEZO NA PICHA ZAIDI WATEMBELEE www.akclassic.blogspot.com
 KUWEKA ODA NA KUFIKISHIWA BIDHAA MPAKA ULIPO PIGA  0753-482909/0713-468393

Ana kwa Ana na Mhe. January Makamba

0
0
Karibu katika mahojianokati ya Jamii Production na Mhe January Makamba. Mbunge wa Bumbuli na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Ameeleza mengi na kujibu maswali ya wasikilizaji wetu waliyouliza kupitia ukurasa wetu wa Facebook.
KARIBU

Watoto wanaoishi katika mazingira magumu Mtwara wakosa mahali pa kuishi

0
0
Meneja wa Vodacom kanda ya Kusini, Henry Tzamburakis akikabidhi msaada wa chakula kwa kituo cha wa watoto yatima cha EAGT Rahaleo Manispaa ya Mtwara Mikindani. Wanaopokea msaada huo kutoka (kushoto) ni watoto wanaoishi katika mazingira magumu Yasunta Rawland,  Boniface Seleman, Mkurugenzi wa kituo cha kulelea watoto cha EAGT Mtwara, Caroline Mkwele, Askofu wa kanisa la EAGT Rahaleo Mtwara pia (mwasisi wa kituo) George Mrope. Vodacom kanda ya kusini inatarajia kutumia Tsh.Milioni 3 kusaidia watu wenye matatizo mbalimbali katika jamii ya kanda ya kusini.
=========  =======  =========
MTWARA, Mkurugenzi wa kituo cha Kanisa la Evangelist Assemblies of God Tanzania (EAGT)  la Rahaleo Mtwara, Bi. Caroline Mkwele amesema kituo chake hakina majengo ya kuwalelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu takribani hamsini na tatu wanaolelewa na kituo hicho, hatua inayowalazimu watoto kuishi na walezi wao majumbani  nakupelekea  ugumu katika kuwalea katika maadili. 

Mkurugenzi huyo ameyasema hayo wakati wafanyakazi wa  kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania walipo watembelea kituoni hapo na kukabidhi msaada wa chakula, fedha na vitu mbalimbali ambavyo vinatoka katika michango ya wafanyakazi kupitia mpango wa Pamoja na Vodacom unaolenga kutatua changamoto za ugumu wa maisha zinazoikabili jamii.

“Changamoto tulizo nazo ni nyingi lakini zaidi ni hili la kukosa kituo rasmi kwa maana ya majengo ya kuwahifadhi watoto hawa kwa pamoja, kwa sababu usipowaweka hawa watoto pamoja uwezekano wa kuwa na tabia tofauti ni mkubwa. 

Hivyo kutokana na ukosefu wa kituo inatulazimu kukutana na watoto hawa kila siku ya Jumamosi. Nawashukuru Vodacom kupitia Taasisi yao ya Vodacom Foundation kwa msaada huu, pia natoa wito kwa wafadhili wengine watusaidie watoto hawa, wasilifumbie macho tatizo hili.” Alisema Bi. Mkwele.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo Meneja wa Vodacom Tanzania kanda ya kusini Henry Tzamburakis  amesema watoto yatima wanahitaji kupata elimu na mahitaji muhimu kama walivyo watu wengine hivyo  kampuni  yake  itaendelea kutoa msaada ili kuwapunguzia watoto hao ugumu wa maisha.

“Watoto hawa naweza kusema kwamba ni watoto wetu, wadogo zetu na ndugu zetu hivyo yatupasa kuwajali kwa kusikiliza mahitaji yao. Mimi binafsi ningependa kutoa wito tusingojee mpaka kampuni ijikusanye ndio tuje kutoa msaada, mtu yeyote anaweza kufanya hivi kwani haihitaji mpaka uwe tajiri sana, ukiwa na chakula, nguo, chochote kile ambacho unaona kitawafaa watoto hawa usisite kuwaletea.” Alisema Tzamburakis.

Kwa upande wao watoto wanaolelewa na kituo hicho walibainisha kwamba si kupenda kwao kuwa yatima hali hiyo inaweza kumkuta yeyote yule ndani ya jamii, wanawasihi watu wenye uwezo wa aina yeyote kuwasaidia.

“Tunashukuru kwa msaada huu, kwa kweli utatusaidia siku zote za maisha yetu, nawaomba msife moyo kutusaidia kwani bado tunahitaji sana na pia tunathamini kwa kile mnachokifanya.” Alisema Boniface Seleman mmoja wa watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha EAGT Rahaleo Mtwara.

Naye mtoto wa kituoni hapo, Sofia Said alisisitiza kuwa “tunashukuru kwa msaada huu, nawasihi na wengine kuiga mfano waliouonesha kampuni ya Vodacom, zaidi ya hayo ningependa kusema asanteni sana.”

“Napenda kuwaambia wanajamii wenzetu kama unamuona mtoto yatima na wewe una uwezo hata kidogo, sio lazima iwe pesa hata chakula unamsaidia tu.” Alimalizia Yasunta Rawland ambaye pia ni mtoto yatima wa kituoni hapo.

Kwa zaidi ya miaka kumi kampuni ya simu za mkononi Vodacom  imekuwa mstari wa mbele kusaidia makundi ya watu wenye mahitaji maalumu ambapo katika kipindi hiki watoto zaidi ya 53 wanaolelewa na kituo EAGT Mtwara wamenufaika na msaada huo. Ongezeko la watoto yatima limekuwa ni janga la kitaifa kwa muda mrefu nchini Tanzania huku serikali, taasisi, mashirika, makampuni binafsi na jamii kwa ujumla zikifanya jitihada mbalimbali za kupambana na kuondokana na changamoto hiyo inayotukabili.

Taasisi ya Vodacom Foundation imekuwa mstari wa mbele kushirkiana na serikali, mashirika, taasisi na wadau mbali mbali wa sekta za maendeleo nchini katika kuisaidia jamii ambayo kwa kiasi kikubwa ni wateja wake. Taasisi hiyo imejidhatiti kufanya kazi na kutoa ushirikiano wa aina yeyote kuhakikisha gurudumu la maendeleo la watanzania linasonga mbele kwa kasi inayotakiwa.

GAZETI LAKO LA PATA HABARI KILA ALHAMISI KWA SH. 500 TU

0
0



Solly Mahlangu ‘Obrigado’ Kuombeleza kifo cha Mandela uwanja wa Taifa.

0
0
Na Makuburi Ally.

WAKATI siku za Tamasha la Krismasi zikikaribia, Muimbaji mahiri  anayeshika kasi katika anga la muziki wa Injili barani Afrika, Solly Mahlangu anatarajia kuombeleza   kifo cha aliyekuwa rais wa nchi hiyo Nelson Mandela  anayetarajia kuzikwa keshokutwa kijijini Qunu nchini humo. 

 Baadhi ya waumini watajiuliza maswali mengi kwamba baada ya kifo cha Mandela labda muimbaji huyo hatoweza kushiriki katika Tamasha hilo la kumtukuza na kumuimbia Mungu, lakini ukweli ni kwamba wamtarajie muimbaji huyo ambaye ataimba baadhi ya nyimbo zake kwa lugha ya Kiswahili.  

Kwa mujibu wa Mkurugenzi  wa Kampuni ya Msama Promotions ambao ni waandaaji wa Tamasha hilo, Alex Msama, muimbaji huyo  ni mmoja wa waimbaji kutoka nje ya Tanzania ambao watashiriki, hivyo waumini watarajie kumuona jukwaani akifikisha neno la Mungu kwa njia ya nyimbo.
   
“Ni muimbaji ambaye anashika kasi katika anga ya muziki wa injili barani Afrika ambaye pia anamudu kuimba Kiswahili kizuri kwa  baadhi ya nyimbo zake, hivyo  anafaa zaidi kwenye tamasha la kumtukuza Mungu,” alisema Msama. Msama anatoa wito kwa waumini kujiandaa na Tamasha hilo ambalo litakuwa na viingilio vya shilingi 2000 kwa watoto, 5000 kwa viti vya kawaida, VIP B shilingi 10,000 na VIP A shilingi 20,000.

Msama anasema kwa mikoani viingilio vitakuwa ni shilingi  5000  kwa  wakubwa  na watoto shilingi 2000. Alizaliwa miaka 40 iliyopita na aliingia kwenye muziki wa kulipwa miaka minne iliyopita ambaye ameutangaza vilivyo muziki wa injili na kuuweka katika ramani ya muziki wa kumtukuza Mungu nchini Afrika Kusini. Mbali ya kuwa maarufu katika nyimbo za injili nchini humo ni Mchungaji  ambaye ana uwezo wa kufanikisha muziki wa injili na kanisa lake ambalo ni Word Praise Christian Centre Intenational lililoko Tembisa.

Muimbaji huyo mwenye utajiri wa tuzo mwaka  2009 alipata tuzo ya albam bora ya SABC Gospel Crown, albamu hiyo iliyokuwa kwenye mfumo wa DVD  aliuza kopi 15,000 na CD zaidi ya 20,0000. Mahlangu kabla ya kuja Tanzania kwenye Tamasha la Krismas hivi karibuni ametokea Harare Zimbabwe ambako alipeleka wimbo wake wa Kiswahili wa ‘Mwamba Mwamba’  ambapo kwenye tamasha hilo aliimba na muimbaji nguli Afrika Oliver Mutukudzi. Mahlangu  alikuwa  na waimbaji wake wanne ambao wanalitawala vilivyo jukwaa ambao ni Sebastian Magacha, Mathias Mhere, the Charambas na Shiloh.

Mahlangu  amefanikiwa kupata tuzo  nne Afrika Kusini  na moja  Uingereza ambapo tuzo hizo alizipata mwaka 2012. Mahlangu Obrigado anakuja Tanzania na msafara wa watu 14 ambaye atatoa zawadi ya Krismas kwa watanzania kwa kuimbva nyimbo 14 mfululizo, zikiwemo nyimbo za Kiswahili kama Mwamba mwamba na Eee Baba  ambazo zitafikisha ujumbe wa neno la Mungu kupitia uimbaji katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. 

Krismas litakalofanyika hapa nchini katika mikoa mitano, litawakutanisha waimbaji kutoka nje ya Tanzania ambao ni pamoja na Liliane Kabaganza (Rwanda), Solomon Mukubwa (Kenya), Ephraim Sekeleti (Zambia) na Solly Mahlangu (Afrika Kusini). Tamasha hilo ambalo litaanzia uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam (Desemba 25), Morogoro ( Desemba 26), Tanga ( Desemba 28), Arusha (Desemba 29) na Dodoma ( Januari 1 mwaka 2014).

 Waimbaji waliothibitisha kushiriki katika tamasha hilo ni pamoja na Obrogado, Liliane Kabaganza (Rwanda), Solomon Mukubwa (Kenya) na Eiphraim Sekeleti (Zambia) huku kwa waimbaji wa Tanzania ni pamoja na Rose Muhando, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Edson Mwasabwite, John Lissu na New Life Band. 

Airtel Tanzania kumleta Andy Cole Dar es Salaam kushiriki promosheni ya Mimi ni Bingwa

0
0
MCHEZAJI wa zamani wa klabu ya Manchester United Andy Cole anatarajia kutua jijini Dar es Salaam Ijumaa hii, imethibishwa.

Ziara ya Cole nchini inalenga kuwapatia uzoefu washindi wa tiketi za promosheni ya Airtel ya 'Mimi ni Bingwa' ambao watasafiri kwenda kuangalia mechi za klabu ya Manchester United moja kwa moja (live) katika uwanja wa Old Trafford pamoja na kukabidhi vifaa vya mazoezi  kwa wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania ya chini ya umri wa miaka 17.

Hii ni ziara ya pili Tanzania kwa mchezaji Cole baada ya kutembelea Tanzania mwaka 2011 alipozindua mpango wa kutafuta vipaji wa Airtel Rising Star.

Akizungumza na waandishi wa habari juu ya ziara hiyo, Meneja Uhusiano wa kampuni ya mawasiliano ya Airtel Tanzania, Bw Jackson Mmbando alisema kuwa mchezaji huyo mkubwa wa zamani wa Man U atakuwa na wakati wa kuzungumza na kushiriki mazoezi na wachezaji wa timu ya Tanzania chini ya miaka 17, timu ambayo wengi wao ni matunda ya mpango wa kuvumbua vipaji wa Airtel Rising Star.

"Andy Cole ataongea na nyota hao wanaochipukia, na kuwashawishi kuongeza jitihada zaidi katika michezo pamoja na kuwapatia mbinu za jinsi gani ya kufikia mafanikio katika fani yao ya michezo.

"Mbali na kuwaonyesha wachezaji hao njia ya mafanikio, mchezaji huyo mkubwa wa zamani wa Manchester United pia atakabidhi vifaa vya mazoezi kwa timu hiyo," alisema Mmbando.

Alisema kuwa Cole pia atahudhuria droo ya moja kwa moja (live) ya kuwatafuta na kuwatangaza washindi wa tiketi tatu za kwenda Old Trafford, kabla ya kuungana na washabiki wa Man U kuangalia mechi moja kwa moja (live) itakayoonyeshwa Coco beach kati ya Manchester United na Aston Villa itakayochezwa jumapili.

Rashid Jacob Kagomola na Dickson Lyatuu ni washindi wa kwanza wawili wa promosheni ya Mimi ni Bingwa waliojishindia tiketi za kwenda Old Trafford, ambapo zawadi zaidi ya shilingi milioni 40 tayari imetolewa kwa ajili ya washindi wa kila siku na kila wiki.

Mmbando alisema kuwa bado kuna zawadi nyingi zaidi kushindaniwa katika promosheni, na kuongeza kuwa ili mteja kushiriki anatakiwa kutuma ujumbe mfupi (SMS) wa neno "BINGWA" kwenda namba 15656.

Aidha, alisema Airtel imeweka vituo mbali mbali ambavyo washabiki wa Man U wataweza kuangalia mechi za Manchester United moja kwa moja (live) kupitia luninga kubwa, na kutaja vituo hivyo kuwa ni Mbeya - Shaba Pub, Mwanza - Shooters Pub, Dodoma - Four ways, Dar es Salaam - Coco Beach, Morogoro - Nyumbani Lounge na Arusha - Empire Sports bar.

Mwaka 2011 kampuni ya mawasiliano ya Airtel Tanzania ilizindua mpango wa kuvumbua vipaji katika soka kwa ushirikiano na klabu ya Manchester United, uliolenga kuvumbua vipaji na kuviendeleza katika mpira wa miguu Tanzania.
Cole amekuwa na dhamira ya kuonyesha uzoefu wake kwa wachezaji nyota wanaochipukia ikiwa ni kama njia ya kuunga mkono maendeleo ya mchezo wa mpira wa miguu duniani.

TANGAZO LA MUALIKO.

0
0
ASASI YA CULTURAL HARMONY AND REFORM FORUM (CHRF) INAYOSHUGHULIKA NA KUKUZA AMANI, UMOJA, UPENDO NA MAADILI MEMA MIONGONI MWA JAMII, INAKUALIKA KATIKA UZINDUZI WAKE SIKU YA JUMATATU TAREHE 16/12/2013 SAA 3.00 ASUBUHI.KATIKA UKUMBI WA KARIMJEE- AMBAPO MGENI RASMI NI RAISI WA AWAMU YA PILI MHE.ALI HASSAN MWINYI . WOTE MNAKARIBISHWA.

UTEUZI WA WAJUMBE WA BARAZA LA CHUO KIKUU CHA SAYANSI NA TEKNOLOJIA MBEYA

0
0

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

 WIZARA YA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA










 


TAARIFA KWA UMMA



UTEUZI WA WAJUMBE WA BARAZA LA CHUO KIKUU CHA SAYANSI NA TEKNOLOJIA MBEYA


               Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemteua Prof. Penina Mlama kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya. Uteuzi huo ni kwa mujibu wa Sheria ya Vyuo Vikuu ya mwaka 2005 na hati idhini ya Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya. Uteuzi huo ni wa kipindi cha miaka mitatu kuanzia tarehe 10 Desemba, 2013.


               Aidha, kufuatia uteuzi wa Mwenyekiti wa Baraza hilo, Prof. Makame M. Mbarawa (Mb), Waziri mwenye dhamana ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, ambaye kwa mujibu wa hati idhini ya Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya na mamlaka aliyonayo amewateua wafuatao kuwa wajumbe wa Baraza la Chuo:


1.   Mhe. Dkt. Pindi Chana, Mbunge wa Viti Maalum-Njombe na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge na Sheria, Mwakilishi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;


2.   Eng. Peter Chisawilo, Rais wa Chemba ya Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo, Mjumbe wa Bodi ya Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania, Mwakilishi wa Sekta Binafsi;


3.   Dkt. Haji Mwevura Haji, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo-Taaluma, Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar, Mwakilishi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar;


4.   Bw. Bernard T. D. Mbonde, Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya, Mwakilishi wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya;


5.   Prof. Evelyne Mbede, Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu, Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia;


6.   Bw. Mapunda Erick Chrisantus, Mhadhiri na Rais wa Chama cha Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya, Mwakilishi wa Chama cha Wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya; na


7.   Bw. Augustine K. Olal, Kamishna Msaidizi wa Sera za Uchumi Mpana, Mwakilishi wa Wizara ya Fedha.


 Uteuzi wa wajumbe wa Baraza la Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya ni wa kipindi cha miaka mitatu kuanzia tarehe 10 Desemba, 2013.


Imetolewa na;

Prof. Patrick J. Makungu,


Katibu Mkuu,


Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.


Diagnostic Review for Increasing Consumer Awareness and Protection and Financial Services in Tanzania

0
0


DAR ES SALAAM, December 11, 2013--The World Bank today presented at a Bank of Tanzania Dissemination Workshop the findings of the Diagnostic Review for Increasing Consumer Awareness and Protection and Financial Services in Tanzania conducted in January 2013. The study is in line with the revised standard framework of Consumer Protection Financial Literacy (CPFL) published in 2012, based on in-depth country-level reviews of good practices of consumer protection and financial literacy.

The CPFL review considered consumer protection issues in the banking, microfinance and pensions sectors with a particular focus on issues related to institutional structures, the legal and regulatory framework, transparency and disclosure, business practices and dispute resolution. A review was also undertaken of initiatives related to financial literacy.

The World Bank is supporting countries all around the world in their efforts to strengthen consumer protection and financial literacy frameworks. The Good Practices are a compilation of the most frequently used practices that have been successfully carried out in the field. They represent a summary of useful approaches for the improvement of conduct of financial institutions when dealing with retail customers and aim to provide a reference for policymakers in designing their financial consumer awareness and protection.

“We are pleased by the steps and activities that have been undertaken so far in Tanzania aiming a strengthening consumer protection and financial literacy levels of the Tanzanian  population” says Andrea Dall’Olio, the World Bank Sector Leader covering Finance and Private Sector Development for Tanzania, Uganda and Burundi. “The Team has been very impressed by the drive, determination and enthusiasm of the key stakeholders working on these issues and we hope to continue this very fruitful partnership with Bank of Tanzania in the implementation of key recommendations. Going forward, the World Bank look forward to working with key stakeholders on important issues associated with the CPFL framework in Tanzania.”

Notwithstanding these positive developments the report highlights further areas of reform in order to address institutional arrangements and the limited requirements concerning disclosure, dispute resolution and fair business practices. The report also notes the need to accelerate implementation of Tanzania’s financial education framework.

In the context of Tanzania the following challenges seem to be particularly relevant when designing and strengthening the existing CPFL framework: (i) the increased usage of delivery channels, in particular financial services delivered via mobile phones, have filled a critical need for consumers in Tanzania but raised important issues of consumer protection; (ii) the large share of the population is living in rural areas and with prevailing low levels of financial literacy which limits the use of formal financial services and increases the risk of consumer rights abuses.
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live




Latest Images