Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

VISHOKA WANAOWATAPELI WAFANYABIASHARA ACHENI MARA MOJA:TRA

$
0
0
Irene Donald Meneja msaidizi wa mkoa wa kikodi wa Arusha,Upande wa ukusanyaji wa madeni na ridhaa ya ulipaji kodi.
Mkuu wa wiaya Arumeru Jerry Muro akizungumza katika wiki ya Elimu ya mlipa kodi iliyoandaliwa na TRA Mkoni Arusha.


Na Vero Ignatus,Arusha.

Onyo kali limetolewa kwa Vishoka wanaowatapeli wafanyabiashara kupitia mgongo wa Mamlaka ya Mapato TRA mkoani Arusha waache kufanya hivyo mara moja kwani Mamlaka hiyo itawatachukulia hatua kali za kisheria kwani wanakwamisha ulipaji kodi kwa hiari.

Irene Donald ni Kaimu Meneja wa TRA amesema hayo katika soko la Tengeru alipo alizungumza na walipa kodi katika wiki ya mlipa kodi ,ambapo amesema kuwa kuna baadhi ya watu wanaofahamika kama vishoka ambao hufika TRA na kufanya udanganyifu kwa wafanyabiashara kwa lengo la kujipatia faida huku wakiwaumiza wafanyabiashara.

Jerry Muro ni Mkuu wa Wilaya ya Meru amesema kuwa wafanyabiashara wanapaswa kulipa kodi kwa hiari ili kuchangaia maendeleo ya nchi na kuiwezesha serikali kutekeleza miradi ya maendeleo kwa wananchi wake.

Baadhi ya wafanyabiashara waliofika kupata elimu ya mlipa kodi Magreth Pallangyo amelalamikia uchafu wa soko la tengeru licha ya kulipa ushuru kwa Halmashauri hiyo hivyo wameiomba serikali itatue changamoto hiyo ili waweze kulipa kodi stahiki.

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI MEI 16,2019

DAWASA WAANZA USAJILI MAGARI YANAYOTOA HUDUMA YA KUUZA MAJISAFI DAR NA PWANI

$
0
0
Afisa Mawasiliano wa DAWASA Joseph Mkonyi (kulia) akibandika moja ya magari ambayo yaliletwa kwenye usajili ili kuweza kuendelea kutoa huduma ya kuuza majisafi jijini Dar es Salaam. Zoezi hilo limefanyika kituo cha Chuo Kikuu Ardhi nyenye matanki ya DAWASA maarufu kama Terminal. Anayeshuhudia ni dereva wa gari hilo. 
Afisa Mawasiliano wa DAWASA Joseph Mkonyi (kulia) akitoa maelekezo kwa dereva mara baada ya kumaliza zoezi la ubandikaji wa stika ili kuweza kuendelea kutoa huduma ya kuuza majisafi jijini Dar es Salaam. 
Afisa Mawasiliano wa DAWASA Joseph Mkonyi (kulia) akitoa maelekezo cheti cha utambuzi kwa kwa dereva mara baada ya kumaliza zoezi la ubandikaji wa stika ili kuweza kuendelea kutoa huduma ya kuuza majisafi jijini Dar es Salaam. 
Magari yakipata yakijaziwa maji tayari kwenda kuuza. Picha zote na Cathbert Kajuna - 

Kajunason/MMG. Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.

 Mamlaka ya Majisafi na MajiTaka Dar es Salaam (DAWASA) limeanza kutekeleza zoezi la usajili na utoaji wa vibali kwa magari ya kusambaza majisafi (water Bowsers) katika jiji la Dar es Salaam na Pwani. Zoezi hilo la Usajili litaendeshwa kwa wiki mbili kuanzia Mei 15 litadumu kwa wiki mbili mpaka Mei 29, 2019 eneo la kituo cha Chuo Kikuu Ardhi nyenye matanki ya DAWASA maarufu kama Terminal, Tegeta na Bagamoyo.

 Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati akisimamia zoezi hilo Afisa Mawasiliano wa DAWASA Joseph Mkonyi amesema kuwa zoezi hilo linalengo la kuwatambua wauzaji wote wa majisafi ikiwa na kuangalia usalama wa vyombo wanavyotumia kuwauzia maji wananchi.

 "Niwaombe wote wenye kufanyabiashara ya majisafi kujitokeza ili tuweze kuwatambua na kuwapa leseni na kuwapa mikakati yenye lengo la kujenga ili watoe huduma salama," amesema Mkonyi. Zoezi hilo la usajili linamtaka mwenye gari kuja na vielelezo ikiwemo picha moja ya rangi ya mmiliki wa gari na nakala ya kitambulisho chake (KURA, UTAIFA au HATI YA KUSAFIRIA). Kingine ni Nakala ya kasi ya gari, nakala ya bima ya gari na nakala ya leseni ya dereva vyote viwe vimethibitishwa na mwanasheria.

Amesema kuwa matenki yatakayokuwa yamekidhi vigezo vya kupata usajili yatasafishwa na dawa maalumu ya kuua wadudu kwenye mantenki na kubandikwa stika ya DAWASA. Amesisitiza kuwa baada ya zoezi hilo kuisha Mei 29, 2019 gari litakalokuwa halijasajiliwa halitaruhusiwa kuendesha biashara ya kutoa huduma ya kuuza maji na wananchi wanashauriwa kutoa taarifa kwa endapo watayaona magari hayo yakitoa huduma bila kuwa na vibali ili wachukuliwe hatua kali za kisheria.

Tigo yasajili laini za watumishi wa Umma Dodoma

$
0
0
 Afisa usajili laini za simu kutoka kampuni ya  Tigo Regan  Emmanuel (wa kwanza kulia), akisajili laini ya mteja wa kampuni hiyo kupitia utaratibu mpya ya usajili wa laini za simu kwa njia ya alama za vidole katika mji wa Kiserikali wa Mtumba mjijini Dodoma jana. Kushoto ni afisa mwingine wa Tigo Jackson Jerry akimsajili mteja.

 Afisa usajili laini za simu kutoka kampuni ya  Tigo Regan  Emmanuel (wa kwanza kulia), akisajili laini ya mteja wa kampuni hiyo kupitia utaratibu mpya ya usajili wa laini za simu kwa njia ya alama za vidole katika mji wa Kiserikali wa Mtumba mjijini Dodoma jana. Kulia kwake ni afisa  mwingine wa Tigo Jackson Jerry.

 Afisa usajili laini za simu kutoka kampuni ya  Tigo Regan  Emmanuel (kushoto), akisajili laini ya mteja wa kampuni hiyo kupitia utaratibu mpya ya usajili wa laini za simu kwa njia ya alama za vidole katika mji wa Kiserikali wa Mtumba mjijini Dodoma jana. Kulia ni afisa mwingine wa Tigo Placida Jamson 


Maafisa wa Kampuni ya Tigo wakisajili laini za simu za watumishi wa Umma kupitia  utaratibu mpya ya usajili wa laini za simu kwa njia ya alama za vidole katika mji wa Kiserikali wa Mtumba mjijini Dodoma jana.

JIJI LA TANGA LAELEZA NAMNA VITAMBULISHO VYA WAJASIRIAMALI VILIVYOSABABISHA KUKOSA MAPATO

$
0
0
  Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Mustapha Selebosi akisisitiza jambo wakati wa kikao cha baraza la Madiwani cha kuwasilisha taarifa ya utendaji wa kata kulia niKaimu Mkurugenzi Ramadhani Possi
 Kaimu Mkurugenzi Ramadhani Possi akizungumza wakati wa kikao hicho
 Diwani wa Kata ya Maweni Jijini Tanga Calvas akizungumza katika kikao hicho kushoto ni Diwani wa Kata ya Pongwe Mbaraka Sadi
 DIWANI wa Kata ya Mswambweni (CUF) Abdulrahamani  akizungumza katika kikao hicho kushoto ni Diwani wa Kata ya Chumbageni (CCM) Saida Gadafi
 Baadhi ya madiwani wakipitia makabrasha wakati wa kikao hicho
HALMASHAURI ya Jiji la Tanga imeeleza namna vitambulisho vya wajasiriamali vilivyotolewa na Rais John Magufuli vilivyowasababishia kukosa mapato huku vyanzo vyake vya mapato 15 kufutika na hivyo kushindwa kutekeleza miradi ya maendeleo.
Kauli hiyo aliitoa na Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Mustapha Selebosi wakati wa kikao cha baraza la Madiwani cha kuwasilisha taarifa ya utendaji wa kata kilichofanyika Jijini hapa na kusema hali ya Halmashauri imekuwa mbaya kutokana na vitambulisho hivyo kugawiwa kwa wafanyabiashara wasi walengwa.
Alisema kuwa Jiji hilo lilikuwa na jumla ya vyanzo vya mapato 38 ambavyo vilikuwa vinatarajiwa kuliingiza Halimashauri hiyo bajeti ya Bil 15 lakini ugawaji wa vitambulisho kwa wafanyabiashara wasio stahiki imesababisha kasoro hiyo.
Alidai chanzo cha kupelekea hali hiyo kimesababishwa na Watendaji wa kata na Mitaa kwa kushindwa kusimamia kwa ukaribu ugawaji wa vitambulishi hivyo kwa watu wanaostahili na badala yake wamewagawiwa hata wafanyabiashara wasihusika.
“Watendaji mmetuangusha mmegawa vitambulisho hata kwa wafanyabiashara wasiostahili na mmefanya hivyo ili kuvimaliza lakini ni athari kwetu hasa Halmashauri hatuna fedha na miradi mingi itakwama”Alisema Seleboss.
Aidha alisema watendaji  wamechangia kukwamisha ukusanyaji wa mapato ambapo yamefikia asilimia 65% huku ikiwa bado mwezi mmoja kumalizika kwa mwaka wa serikali uishe ilihali angalau ukusanyaji huo ulitakiwa ufikie 80%.
Alisema kuwa ukosefu huo wa mapato umesababisha Halimashauri hiyo kushindwa kutekeleza shughuli za kijamii kama usafi wa masoko pamoja na marekebisho ya taa za barabarani.
“Watendaji wameshindwa kutafsiri nia ya Rais kwani vitambulisho vimetolewa hadi kwa wavuvi pamoja na wafanyabiashara wakubwa wenye maduka sasa wote wamegeuka na kuwa wajasiriamali”alisema Mustafa.
Hata hivyo akiongelea upande wa leseni za biashara Meya Mustafa alisema kuwa wamepoteza mapato ya kiasi cha sh Mil 700 zilizokuwa zikusanywe kutokana na maombi ya leseni hizo lakini sasa wafanyabiashara wengi wamerudisha leseni hizo na kukata vitambulisho vya wajasiriamali.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Ramadhani Possi alisema kuwa ufinyu wa bajeti umesababisha miradi mingi ambayo walikuwa wamepanga kuitekeleza kushindwa kutekelezwa kwa wakati .
“Kwa sasa tunajipanga kuboresha miundombinu ya shule zetu kwa kujenga madarasa mapya ukarabati ya vyoo pamoja na madawati ambapo tunafanya kila pale tunapopata fedha japo kidogo”alisema Possi.
Kaimu Mkuu wa wilaya ya Tanga Selemani Zumo aliwataka watendaji wa Jiji kuhakikisha wanafanyakazi kwa uwadilifu na kujituma pamoja na kujua mipaka ya kazi zao.
Alisema kuwa haiwezekani watendaji hao wakawa ni sehemu ya migogoro baina yao na viongozi wa kisiasa ambao wao wapo kwa ajili ya kuhakikisha wanasimami maslahi ya wananchi ambao ni wapiga kura wao.
Awali akichangia mada katika baraza hilo Diwani wa kata ya Mabawa Mwasabu Ngare alisema baadhi ya taa za barabarani haziwaki na hali hiyo inaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la vibaka na wananchi kupoteza mali zao.
Mwisho. 

WAKALA WA VIPIMO (WMA) WAHAKIKI PAMPU KITUO CHA MAFUTA TOTAL MLIMANI CITY JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

Kaimu Meneja Wakala wa Vipimo (WMA) Mkoa wa Kinondoni Bw. Charles Mavunde akifanya ukaguzi wa Seal kwenye pampu katika kituo cha mafuta cha Total Mlimani City jijini Dar es salaam leo ili kujiridhisha kama upimaji mafuta wa Pampu ni sahihi wakati wateja wanapofanya manunuzi, Maadhimisho ya vipimo duniani yanatarajiwa kufanyika Mei 20, 2019 jijini Dar es salaam.

  
 Kaimu Meneja Wakala wa Vipimo (WMA) Mkoa wa Kinondoni Bw. Charles Mavunde akishuhudia wakati mafuta yakijazwa kwenye kipimo maalum cha mafuta wakati maofisa hao walipofanya ukaguzi wa Seal kwenye pampu  kituo cha mafuta cha Total Mlimani City jijini Dar es salaam leo, kushoto ni Ally Mohamed Meneja wa kituo cha Total Mlimani City.

  
Kaimu Meneja Wakala wa Vipimo (WMA) Mkoa wa Kinondoni Bw. Charles Mavunde akitoa maelezo kwa waandishi wa habari  wakati wakifanya  ukaguzi wa Seal kwenye pampu katika kituo cha mafuta cha Total Mlimani City jijini Dar es salaam leo ili kujiridhisha kama upimaji mafuta wa Pampu ni sahihi wakati wateja wanapofanya manunuzi anayejaza mafuta ni Mbaningo Mselem Afisa Vipimo.
  

Kaimu Meneja Wakala wa Vipimo (WMA) Mkoa wa Kinondoni Bw. Charles Mavunde akionyesha Stika ya uthibitisho kuwa pampu hizo zimekaguliwa wakati maofisa hao waliofanya ukaguzi kituo cha mafuta cha Total Mlimani City jijini Dar es salaam leo.

  
 Ally Mohamed Meneja wa kituo cha mafuta Total Mlimani City akihojiwa na  waandishi wa habari kwenye kituo hicho jijini Dar es salaam leo baada ya wakala wa vipimo kukagua pampu na kujiridhisha kuhusu ubora wake wa vipimo.


  

 Kaimu Meneja Wakala wa Vipimo (WMA) Mkoa wa Kinondoni Bw. Charles Mavunde akihojiwa na waandishi wa habari wa ITV mara baada ya  maofisa hao kufanya ukaguzi katika kituo cha mafuta cha Total Mlimani City jijini Dar es salaam leo.kushoto ni Irene John Meneja Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma Wakala wa Vipimo (WMA)
  
Kituo cha Mafuta cha Total Mlimani City jijini Dar es salaam.
 Kaimu Meneja Wakala wa Vipimo (WMA) Mkoa wa Kinondoni Bw. Charles Mavunde akifanya ukaguzi wa Seal kwenye pampu katika kituo cha mafuta cha Total Mlimani City jijini Dar es salaam leo ili kujiridhisha kama upimaji mafuta wa Pampu ni sahihi wakati wateja wanapofanya manunuzi, Maadhimisho ya vipimo duniani yanatarajiwa kufanyika Mei 20, 2019 jijini Dar es salaam.

  
 Kaimu Meneja Wakala wa Vipimo (WMA) Mkoa wa Kinondoni Bw. Charles Mavunde akishuhudia wakati mafuta yakijazwa kwenye kipimo maalum cha mafuta wakati maofisa hao walipofanya ukaguzi wa Seal kwenye pampu  kituo cha mafuta cha Total Mlimani City jijini Dar es salaam leo, kushoto ni Ally Mohamed Meneja wa kituo cha Total Mlimani City.

  
Kaimu Meneja Wakala wa Vipimo (WMA) Mkoa wa Kinondoni Bw. Charles Mavunde akitoa maelezo kwa waandishi wa habari  wakati wakifanya  ukaguzi wa Seal kwenye pampu katika kituo cha mafuta cha Total Mlimani City jijini Dar es salaam leo ili kujiridhisha kama upimaji mafuta wa Pampu ni sahihi wakati wateja wanapofanya manunuzi anayejaza mafuta ni Mbaningo Mselem Afisa Vipimo.
  

Kaimu Meneja Wakala wa Vipimo (WMA) Mkoa wa Kinondoni Bw. Charles Mavunde akionyesha Stika ya uthibitisho kuwa pampu hizo zimekaguliwa wakati maofisa hao waliofanya ukaguzi kituo cha mafuta cha Total Mlimani City jijini Dar es salaam leo.

  
 Ally Mohamed Meneja wa kituo cha mafuta Total Mlimani City akihojiwa na  waandishi wa habari kwenye kituo hicho jijini Dar es salaam leo baada ya wakala wa vipimo kukagua pampu na kujiridhisha kuhusu ubora wake wa vipimo.


  
 Kaimu Meneja Wakala wa Vipimo (WMA) Mkoa wa Kinondoni Bw. Charles Mavunde akihojiwa na waandishi wa habari wa ITV mara baada ya  maofisa hao kufanya ukaguzi katika kituo cha mafuta cha Total Mlimani City jijini Dar es salaam leo.kushoto ni Irene John Meneja Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma Wakala wa Vipimo (WMA)
  
Kituo cha Mafuta cha Total Mlimani City jijini Dar es salaam. 

UGONJWA WA DENGUE TISHIO DAR,WAGONJWA WAZIDI KUONGEZEKA,WANANCHI WASHAURIWA KUCHUKUA HATUA

$
0
0
Takwimu zinaonesha kuwa idadi ya wagonjwa wa Ugonjwa wa Dengue imeongezeka ambapo kwa sasa wamegundulika wagonjwa wapya 674 huku kata ya Ilala ikiongoza kwa kuwa na wagonjwa 235.

Akizungumza na waandishi wahabari Jijini Dar es Salaam Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhammad Kambi amesema kuwa Ugonjwa wa Dengue kwa sasa wameongeza vituo kwa mkoa wa Dar es Salaam na Tanga hadi vituo 19 tofauti na awali ambapo vilikuwa 7.

Amezitaja  baadhi ya vituo vya Serikali vinavyopima Ugonjwa huo kuwa ni pamoja na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Amana, Temeke, Tumbi, Mkuranga  huku uhamasishaji wa upatikanaji wa vipimo zaidi vya Ugonjwa huo ukiendelea.

Aidha ameongeza kuwa dalili za ugonjwa huo ni pamoja na homa ya ghafla, Kuumwa kichwa hususani sehemu za macho, maumivu ya viungo na uchovu ambapo dalili hizo huanza kujitokeza kati ya siku 3 hadi 14 tangu siku mtu alipoambukizwa virusi vya Ugonjwa huo.

Sambamba na hayo amewakumbusha viongozi wa mikoa, Wilaya,  Halmashauri, Kata, Tarafa, Vijiji, mitaa na vitongoji  pamoja na Maafisa wa Afya nchini kuchukua hatua kwa dhati kwani Ugonjwa huo haupo ukanda wa Pwani tu bali unaweza ukatokea pia katika maeneo yao.

Hata hivyo amesema tangu kutokea kwa Ugonjwa huo January watu 1901 wamethibitishwa kuwa na virusi au walikwishapata ugua Ugonjwa huo ambapo kati ya hao 1809 wanatoka Dar es Salaam, 89 kutoka Tanga na mkoa wa Pwani, Singida na Kilimanjaro kukiripotiwa mgonjwa mmojammoja.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Serikali Yudas Ndungile amesema wanaendelea na jitihada ya kuangamiza mazalia ya mbu ikiwemo kufukia kupulizia dawa  na wanamkakati wa kupata mashine ya kupuliza dawa angani.

Hata hivyo wito umetolewa kwa wananchi kwenda kupima pindi wanapoona dalili za ugonjwa huo na vipimo vinatolewa bure kwenye vituo vya Afya vya  Serikali huku akisisitiza kujikinga kwa kuangamiza  mazalia ya mbu kwa kufukia madimbwi, kufyeka vichaka na kuvaa nguo ndefu kwani mbu huyo hungata majira ya asubuhi mchana na jioni.

TANZANIA KUFIKIA ASILIMIA 70 YA KUONDOA UHABA WA WATUMISHI KATIKA SEKTA YA AFYA

$
0
0


waziri wa afya Ummy Mwalimu akifungua kikao cha kujadili changamoto za rasiliamali watu katika sekta ya afya kilichofanyika leo jijini Dodoma

Dkt.Dan Brun Peterson mshauri mwelekezi masuala ya afya idara ya sera ya mipango wizara ya afya akiwasilisha mada katika kikao hicho
waziri wa afya pamoja na katibu mkuu wake Dkt.Zainab Chaula(kulia)wakifuatilia mada iliyokuwa ikiwasilishwa
Viongozi mbalimbali wakifuatilia uwasilishaji wa mada kwenye kikao hicho ambacho kitaweka mikakati ya kuboresha uzalishaji,kuajiri watoa huduma za afya nchini
Baadhi ya viongozi wa wizara ya afya,Tamisemi pamoja wadau wa maendeleo wakifuatilia kikao hicho chenye kujadili changamoto.za.uhaba wa watumishi wa sekta ya afya ambapo pengo ni asilimia 52

Na.WAMJW,Dodoma

Tanzania imeazimia kufikia asilimia sabini kutoka arobaini na nane ya uhaba wa watoa huduma za afya kwa nchi za Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika ifikapo mwaka 2022.

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati akifungua kikao cha kujadili changamoto za rasilimali watu katika sekta ya afya kati ya viongozi kutoka Wizara ya Afya, Tamisemi pamoja na washirika wa maendeleo nchini.

Waziri Ummy amesema lengo la kikao hicho ni kujadili changamoto mbalimbali zinazohusu rasilimali watu ikiwemo ya upungufu wa watumishi, ajira, mafunzo pamoja na mahitaji ya watumishi kuanzia ngazi za zahanati hadi hospitali za wilaya nchini.

Amesema upungufu huo umetokana na ongezeko la miundombinu ambayo imewekwa na serikali ya awamu ya tano licha ya kazi kubwa iliyofanyika ya kuimarisha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba.

”ingawa bado ipo changamoto ya rasilimali watu katika sehemu za kutoa huduma za afya nchini ambapo pengo ni takribani asilimia 52 kwa kila watumishi wa afya mia moja tunawahitaji watumishi arobaini na mbili”. Amesisitiza Waziri Ummy.

Aidha, etaja sababu nyingine ya upungufu wa watumishi wa sekta ya afya kuwa ni pamoja na ongezeko la magonjwa yasiyo ya kuambukiza hivyo inahitajika watoa huduma wa afya wengi katika kuwahudumia wananchi wenye matatizo hayo.

Hata hivyo Waziri Ummy amesema kikao hicho kitaweka mikakati ya pamoja na ya ubunifu ya kuona kunakuwa na maboresho ya uzalishaji wa wataalam wa afya na wale wanaozalishwa ni kiasi gani wanaweza kuajiriwa na kuwekwa kwenye utumishi wa umma hususan kwenye ngazi ya zahanati na hospitali za wilaya.

“Tutaweka ubunifu ambao utawawezesha mfano wauguzi kupatiwa mafunzo ya kutoa dawa za usingizi na hii ni kuona wanao uwezo wa kufanya kazi nyingine tofauti, kwa ujumla sekta ya afya nchini inaenda vizuri na nina amini kwa pamoja tunaweza kutatua uhaba wa watumishi katika sekta ya afya.

JWTZ WATUMIA NDEGE YA ATCL KUSAFIRISHA WAPIGANAJI KUISHIRIKI ULINZI WA AMANI DARFUR

$
0
0
Na Luteni Selemani Semunyu

Maafisa na Askari wa jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania (JWTZ), wanaoshiriki Ulinzi wa Amani katika  Jimbo la Darfur nchini Sudan kwa Mara ya kwanza  kwa kipindi cha Miaka 10 ya Ulinzi wa Amani Jimboni humo wametumia Ndege ya Shirika la Ndege ya  Serikali ya ATCL ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Mhe Rais wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu katika  kulifanya Shirika hilo linapiga hatua zaidi kwa maslahi ya Shirika na Taifa kwa ujumla.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Mkuu wa Mafunzo na Utendaji Kivita wa JWTZ Meja Jenerali Alfred Kapinga amesema Jeshi ni Taasisi inayoongozwa na Uzalendo,uadilifu, uhodari  hivyo ni faraja kubwa kwa Jeshi  na wapiganaji kuunga mkono jitihada za Serikali katika Kuboresha Uchumi  ikiwa ni  sehemu ya mchango wao katika kuonesha  uzalendo kwa vitendo kwa  kutumia vitu vya nyumbani kwa maslahi mapana ya Taifa.

“ Tumekuwa tukitumia Ndege zetu za Jeshi lakini tumekuwa tukitumia Ndege za mataifa mengine kwa Mikataba kutoka Umoja wa Mataifa lakini sasa ni faraja kwani tumefanikiwa kuwashawishi Umoja wa Mataifa kutumia Ndege zetu” Alisema Meja Jenerali Kapinga.

Aidha,Meja Jenerali kapinga alisema   mbali na kutumia Ndege hiyo lakini aliwaasa Maafisa na Askari hao kuhakikisha wanapeperusha vema Bendera ya Nchi na kuendelea kuitangaza kwa  sifa nzuri za Utendaji Kimataifa.

Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Ndege la la Tanzania (ATCL),  Mhandisi Ladislaus Matindi  Alisema ni Fursa Nzuri kwa ATCL na wanalishukuru Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kupitia kwa mkuu wa majeshi ya Ulinzi  kwa Mchango mkubwa   kufanikisha kupata tenda hiyo.

“ Namshukuru Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi  Jenerali Venance Mabeyo na watendaji wake kwa Uzalendo wake na kuhakikisha anafanikisha ATCL kupata fursa kwa mara ya kwanza na hii itakuwa mwanzo mzuri na tutahakikisha tunaitumia vizuri  fursa hii kujitangaza zaidi Kimataifa kwa maslahi  ya Nchi “ Alisema Mhandisi Matindi.

Vilevile  Mhandisi Matindi aliongeza kuwa Ndege ya Dream Liner ina uwezo wa kusafiri kwa saa 12 bila kusimama, hivyo kwa  kutumia saa tatu kusafiri kutoka hapa mpaka nchini Sudan  ni sehemu ndogo ya Uwezo wake na ni nafasi ya kuwajaribisha watendaji wa Ndege wa ATCL katika kuhudumia safari Ndefu.

Naye Kamanda wa Kikosi cha TANZBATT- 13,  Luteni Kanali Khalfan Kayage  anayekwenda na  Kikosi hicho  alisema kuwa  inawapa nguvu kupeperusha Bendera yetu kupitia Ndege na ameahidi kufanya kazi kwa Bidii kuendeleza jina na sifa nzuri ya Tanzania Kimataifa.
Baadhi ya Maafisa na Askari wa JWTZ  Kundi la 13 wakijiandaa  kuondoka kwa Ndege ya ATCL leo Mei 16 2019 katika Uwanja wa Ndege wa Jeshi Jijini Dar es Salaam kwenda kushiriki Ulinzi wa Amani Jimboni Darfur Nchini Sudan  . Picha  na Luteni Selemani Semunyu.
 Mkuu wa Mafunzo na Utendaji Kivita wa JWTZ Meja Jenerali Alfred Kapinga  ( Kushoto ) akiagana na Kamanda Kikosi  Kundi la 13  Luteni kanali Khalfan Kayage (Kulia ) kinachoenda kushiriki Ulinzi wa Amani Jimboni Darfur Nchini Sudan leo mei 16 wakati wakiondoka kwa Ndege ya ATCL (Haipo pichani )  katika Uwanja wa Ndege wa Jeshi Jijini Dar es Salaam katikati ni Mkurugenzi wa ATCL Mhandisi Ladislaus Matindi. Picha na Luteni Selemani Semunyu
 Mkuu wa Mafunzo na Utendaji Kivita wa JWTZ Meja Jenerali Alfred Kapinga Akiagana na  Maafisa na Askari wa  JWTZ   Kundi la 13 linalokwenda kushiriki Ulinzi wa Amani Jimboni Darfur Nchini Sudan wakati wakiondoka kwa Ndege ya ATCL (haipo Pichani) leo Mei 16  katika Uwanja wa Ndege wa Jeshi Jijini Dar es Salaam Picha na Luteni Selemani Semunyu

Kakunda Akanusha Profesa Kabudi Kuhusika na Mkataba wa Kampuni ya Indo Power Solution

$
0
0
Waziri wa Viwanda na Biashara, Joseph Kakunda akifafanua jambo kuhusu taarifa za kumuhusisha Profesa Kabudi na sakata la Kampuni ya Indo Power Solution alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo jijini Dodoma.[/caption] 

Na: Frank Shija – MAELEZO, Dodoma

Waziri wa Viwanda na Biashara, Joseph Kakunda amekanusha shutuma zilizotolewa kuhusu ushiriki wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania katika mchakato wa kumpata mzabuni wa ununuzi wa Korosho ambaye ni Kampuni ya Indo Power Solution ya nchini Kenya.

Waziri Kakunda amesema kuwa anashanga kuona Profesa Kabudi anatupiwa lawama kuwa ameingiza Serikali mkenge jambo ambalo si kweli kwani wahusika wakuu ni timu ya wataalam kutoa Ofisi ya Wizara ya Viwanda na Biashara na kwamba upatikanaji wa zabuni hiyo ulipitia mchakato yote halali kilichotoke ni Serikali kuvunja mkataba baada ya mzabuni kutotimiza masharti yaliyomtaka kulipa ndani ya siku 10 na hata alipoongezewa muda haikutimiza.

“Kumuweka mtu ambaye hana makosa yeyote kwenye suala hili na bahati mbaya sana maagazeti karibu yote yakawa yanaandika yakimlaumu kushauri vibaya Serikalijambo ambalo halina ukweli wowote, Kabudi ambaye wakati huo alikuwa Waziri wa Katiba na Sheria alikuwa mualikwa tu wa kushuhudia hafla ya utiwaji saini mkataba wa Makubaliano baina ya Wizara ya Viwanda na Biashara na Kampuni ya Indo Power Solution,” Alisema Waziri Kakunda.

Kakunda alisema kuwa ni ajabu kwa kumlaumu mtu aliyealikwa na kuongeza kuwa timu ya wataalam iliyohusika inaongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa anayeshughulikia Viwanda hivyo kumuhusisha Profesa Kabudi ni jambo hili si sawa ni bora hata wangemuhusisha yeye kwa kuwa ndiye Waziri mwenye dhamana na Biashara.

Aidha Waziri Kakunda amesema kuwa ni vyema Watanzania wakaelewa na kutokubali kupotoshwa juu ya hatua iliyochukuliwa na Serikali kuvunja mkataba na Kampuni ya Indo Power Solution ya nchini Kenya iliyokuwa imepewa zabuni ya kununua Korosho tani 100 kwa kutofuata masharti ya mkataba.

Alisema kuwa mchakato wa Kuipatia zabuni Kampuni hiyo ulipitia njia mbalimbali zilizohusisha wataalam kutoka pande mbili na kujiridhisha kuwa Kampuni hiyo inavigezo vyote vya vya kupewa zabuni hiyo ya kununua Korosho nchini na kuongeza kuwa pamoja na kuwa imeshindwa kutimiza masharti ya mkataba uliopelekea Serikali kusitisha mkabata bado inabaki kuwa ni Kampuni halali.

Waziri Kakunda ametoa ufafanuzi huu kufuatia kauli iliyotolewa Bungeni jana na Mbunge wa Moshi Vijijini, Anthony Komu akimtuhumu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashari, Profesa Paramagamba Kabudi kuitia hasara Serikali kwa kumuhusisha na mkabata wa makubaliano ya ununuzi wa Korosho tani 100 na kampuni ya Indo Power Solution ya nchini Kenya ambayo baadae Serikali iliamua kusitisha mkataba wake baada ya Kampuni hiyo kutofuata masharti.

TAARIFA MBALIMBALI ZA UHALIFU KUTOKA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA

$
0
0
 Bidhaa mbalimbali vikiwemo vipodozi na pombe kali zilizopigwa marufuku nchini
 Gari aina ya Toyota Mark II iliyokamatwa ikiwa na bidhaa zilizopigwa marufuku nchini
 Watuhumiwa NASIBU JUMA na BRIGHT THOMAS
Watuhumiwa wa matukio ya wizi na utapeli, kutoka kushoto OMARY, HAMIS, ARTHA na PILI

KUKAMATWA KWA WATUHUMIWA WANNE KWA TUHUMA ZA WIZI NA KUGHUSHI NYARAKA MBALIMBALI.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa wanne [04] ambao ni:-
1.     PILI OMARI [30] Mkazi wa Mbezi – Dar es Salaam
2.     M HAMIS NGOWI [40] Mkazi wa Dar es salaama na
3.     OMARY MOHAMED [41] Mwalimu na Mkazi wa Nzovwe
4.     ARTHA KASMIRI [34] Mkazi wa Dar es salaam - Mbezi kwa tuhuma ya wizi katika Benki.

Mnamo tarehe 13.05.2019 saa 14:00 mchana huko katika Benki ya Posta tawi la Mwanjelwa iliyopo Kata ya Ruanda, Tarafa ya Iyunga, Jiji na Mkoa wa Mbeya. Askari Polisi kwa kushirikiana na maafisa wa benki hiyo waliwakamata PILI OMARI [30] na MARTHA KASMIRI [34] wote wakazi wa Dar es salaam - Mbezi wakiwa na nyaraka ‘salary slip’ zenye majina ya watu wengine ambao ni watumishi wa idara ya elimu, vitambulisho vya mpiga kura, fomu za utambulisho kutoka Jiji, fomu za mikopo kutoka benki ya Posta na barua za uthibitisho kutoka kwa mwajiri ambazo ni za kughushi.
Watuhumiwa wengine ambao ni HAMIS NGOWI [40] mfanyabiashara na mkazi wa Dar es salaama na OMARY MOHAMED [41] mwalimu na mkazi wa Nzovwe wamekamatwa wakati mtuhumiwa HAMIS NGOWI @ OPTATI NGOWI alipopekuliwa alikutwa na:-
1.     Mihuri 6 ya idara tofauti za serikali.
2.     Laini 10 za mitandao ya simu Vodacom, Tigo na Halotel,
3.     Picha ndogo 3 za watu tofauti ya jinsia ya kike,
4.     Funguo 2 za gari,
5.     Fomu za utambulisho kutoka Jiji,
6.     Fomu za mikopo kutoka benki ya Posta,
7.     ‘Salary slip’ pamoja na barua za uthibitisho kutoka kwa waajiri. Upelelezi wa shauri hili unaendelea.
KUKAMATWA KWA WATUHUMIWA WAWILI WANAOJIHUSISHA NA MATUKIO YA UNYANG’ANYI, WIZI NA UBAKAJI.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia vijana wawili ambao ni:-
1.     NASIBU JUMA [20] Mkazi wa Nzovwe Mbeya
2.     BRIGHT THOMAS [19] Mkazi wa Mtaa wa Ndanyella Mbeya
Kwa tuhuma ya kujihusisha na matukio ya unyang’anyi, wizi na ubakaji katika maeneo ya Nzovwe, Iyunga na Iwambi Jijini Mbeya.
Watuhumiwa walikamatwa mnamo tarehe 14/05/2019 huko Iyunga katika Klabu cha Pombe cha London kilichopo Jijini Mbeya na katika upekuzi watuhumiwa walikutwa na :-
1.     Mapanga mawili [02]
2.     Mizula miwili [02]
3.     Makoti meusi mawili [02]
Katika mahojiana na watuhumiwa wamekiri kuhusika katika matukio mbalimbali kama ifuatavyo:-
Mnamo tarehe 26/03/2019 saa 22:00 usiku huko Mtaa wa Inyala uliopo Kata ya Iyunga na Tarafa ya Iyunga ambapo walivamia nyumbani kwa Mwalimu wa Chuo MUST aitwaye WILLIAM MBATTA na kumjeruhi kwa mapanga sehemu ya kichwani na kisha kutoweka.
Mnamo tarehe 30/03/2019 saa 22:00 usiku katika viwanja vya MUST walimjeruhi ALLEN NYITTI kwa kumkata panga kichwani, kiunoni na tumboni na kupora simu aina ya Samsung Galaxy na pesa taslimu Shiling 21,000/=
Mnamo tarehe 05/04/2019 saa 02:00 usiku huko katika Mtaa wa Ndanyella, Kata ya Nzovwe, Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya walimvamia FATUMA HAJI [21] walimbaka na kupora pesa taslimu shilingi 3,280,000/= pia waliiba TV aina ya LG na Redio Sub Woofer, Deck na simu ya mkononi aina ya Samsung J7. Mali zote zikiwa na thamani ya shilingi 4,120,000/=
Mnamo tarehe 04/05/2019 saa 02:45 usiku huko Kota za Tazara zilizopo Iyunga Mbeya walivamia nyumbani  kwa FRANK CHARLES na kumjeruhi kwa kumkata na mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake yeye na mke wake aitwaye VICTORIA SAMWEL pamoja na kupora TV aina ya Boss yenye ukubwa wa inchi 55.


KUKAMATA BIDHAA ZILIZOPIGWA MARUFUKU NCHINI.

Mnamo tarehe 16/05/2019 saa 05:00 Alfajiri huko maeneo ya Block “T”, Kata ya Ruanda, Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya, Askari Polisi wakiwa doria katika maeneo hayo waliliona gari lenye namba ya usajili T.937 CKD aina ya Toyota Mark II Blit na kulitilia mashaka na ndipo kukuta limebeba bidhaa mbalimbali zilizopigwa marufuku nchini ambazo:-
1.     Pombe kali aina ya PRINCE katoni sita @ chupa 20 sawa na chupa 120
2.     Pombe kali aina ya Officer”s Verve katoni 24 @ chupa 20 sawa na chupa 480 
3.     Condom aina ya Ultimate Assured Protection katoni 63 ambazo zilitolewa na Serikali ya Marekani kwa nchi ya Zambia.
4.     Panga moja.
5.     Carolight 120ml pcs 36
6.     Citrolight 120ml pcs 84
7.     Coco Pulp 150mls pcs 24
8.     Coco Pulp 500mls pcs 06
9.     Coco Pulp 300mls pcs 36
10. Coco Pulp Lightening oil 50mls pcs 72
11. Coco Pulp 50g pcs 06
12. Carotone Crème ndogo 65mls pcs 24
13. Cocoderm pcs 06
14. Clinic Clear pcs 06
15. Extra Clair 120mls pcs 54
16. Elle 5 Crème pcs 3
17. Diproson tube 30g pcs 74
18. Diproson lotion 30mls pcs 48
19. Top Lemon Plus 170mls pcs 84
20. Carotone black spot corrector pcs 06
21. Dermotyl tube 15g pcs 10
22. Dermotyl lotion 30mls pcs 90
23. Dodo Crème ndogo pcs 06
24. Clairmen pcs 12
25. Bronz tone crème 125ml pcs 15
26. Miki Clair 160ml pcs 48
27. Movate Cream 30g pcs 50
28. Oranvate gel 30g pcs 50
29. Beaution Cream 330mls pcs 12
30. Miss Caroline 150mls pcs 12
31. Carolight Cream 120mls pcs 78
32. Diana lotion 30mls dozen 03 sawa na pcs 36
33. Teint Clair 150mls pcs 48
34. Betasol lotion 30mls pcs 36
35. Betasol tube 15g pcs 40
36. Perfect white cream 150mls pcs 12
37. Perfect white lotion 30mls pcs 06
38. Lemon vate cream 30g pcs 40
39. Mont Claire 30g pcs 10
40. Neoprosone Gel 30g pcs 10
41. Epiderm Creme 15g pcs 41
42. Epiderm Crème 30g pcs 24
Gari hilo lilikuwa likitokea Tunduma kuja Mbeya likiwa na bidhaa hizo. Gari pamoja na vielelezo vipo kituo cha Polisi. Msako mkali wa kuwatafuta watuhumiwa waliokuwa wakisafirisha bidhaa hizo unaendelea.

KUPATIKANA NA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU NCHINI.
Mnamo tarehe 13.05.2019 majira ya saa 21:00 usiku huko maeneo ya Iwambi, Kata ya Iwambi, Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya. Polisi walimkamata kijana mmoja aitwaye ELIA MWAKALIKWE [25] Mkazi wa Iwambi akiwa na Pombe Kali zilizopigwa marufuku nchini aina ya Verve katoni 27 zikitokea nchini Zambia.

Imetolewa na;
[ULRICH O. MATEI – SACP]
   KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

JPM atengua uteuzi wa Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya wawili.

Wafanyabiashara Jijini Dodoma Waunga Mkono Katazo la Matumizi ya Mifuko ya Plastiki

$
0
0

Baadhi ya wafanyabiasha katika Jiji la Dodoma wametoa maoni yao kuhusu katazo la matumizi na biashara ya mifuko ya plastiki ifikapo tarehe 1 Juni 2019 nakusema kuwa katazo hilo limekuja wakati sahihi.

Akizungumza na mwandishi wetu Katibu Mkuu wa Soko Kuu la Majengo, Jijini Dodoma, Eliamani Mollel amesema kuwa wao kama viongozi wamepokea na kuunga mkono marufuku ya kutotumia na kufanya biashara ya mifuko ya plastiki, Serikali ina nia ya dhati kabisa kukataza hii mifuko kutokana na uharibifu wa mazingira, sisi wenyewe ni mashuhuda tunaona mifuko inaleta uharibifu wa mazingira, kuziba kwa mitaro ya maji na adha zingine nyingi zinazofanana na hizo, kwa hiyo sisi kama viongozi kwa kushirikiana na Afisa Mtendaji , jiji kwa ujumla tunaunga mkono hili la Wazari Mkuu la kukataza matumizi ya mifuko ya plastiki.

Akichangia maoni hayo Mfanyabiashara wa Vifungashio vya biadhaa ikiwemo mifuko ya plastiki katika Soko la Majengo Jijini Dodoma, Isack amesema kuwa licha ya mud uliotolewa kuwa mfinyu lakini yupo tayari kuhakikisha ifikapo tarehe 1 Juni 2019 anakuwa amekwisha acha kuuza mifuko ya plastiki baadala yake atakuwa anauza mifuku ambayo inakubalika kwa mujibu wa katazo hilo lililotolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa hivi karibuni.

Naye Evarist Korneli Sanzi, Mfanyabiashara wa Soko la Changombe Jijini Dodoma amesema kuwa binafsi amefurahishwa sana na katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki lililotolewa na Waziri Mkuu kwani mifuko hiyo imekuwa ikiharibu mazingiora na uchafu na kuongeza kuwa kama angekuwa na uwezo angekuwa amekemea siku nyingi sana kwa sababu imekuwa ni kero, lakini aliposikia tamko la Waziri Mkuu amefurahi sana.

Mfanyabiashara mwingine aliyechangia maoni yake, Badiliko Ally Ndudi, ambaye ni mfanyabiashara wa vifungashio katika Soko la Majengo jijini Dodoma amesema kuwa pamoja na changamoto zitakazojitokeza lakini katazo la matumizi ya plastiki amesema kuwa mifuko ya plastiki ina athari kwa afya ya binadamu kwa mujibu wa wanasayansi walivyodai.

Mfanyabiashara wa Soko Kuu la Majengo Jijini Dodoma, Urban Munishi anasema kuwa katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki kwake ni fursa kutokana na aina ya bidhaa anayouza ikiwa ni nafaka pamoja na vikapu. Anasema kuwa wateja wa vikapu wameongezeka na mifuko ya sandarusi wameongezeka mara baada ya tangazo la marufuku ya matumizi ya mifuko ya plastiki ifikapo Juni Mosi 2019.

Kwa upande wake mnunuzi wa bidhaa katika Soko la Majengo jijini Dodoma, Bi. Josinah Leornad amesema kuwa amefurahishwa sana na katazo hili la matumizi ya mifuko ya plastiki kwani imekuwa kero kwani ulikuwa kila ukinunua kitu kidogo unafungiwa kwenye mifuko hiyo unajikuta nyumbani unakuwa na mifuko mingi sana na baadae ukiichoma moshi wake ni hatari kwa afya kwa hiyo nimefurahi kusikia wanaleta mifuko mbadala ambayo pia itakuwa rafiki kwa mazingira kwasabubu mifuko ya plastiki imekuwa ikisababisha vyanzo vya maji kuharibika, mitaro kuziba hivyo kusitishwa kwake kuta okoa mazingira.

Mwenyekiti wa Soko la Chang’ombe jijini Dodoma anasema kuwa katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki wanaliunga mkono kwani kwao ni kama limepiga ndege wawili kwa jiwe moja kwanza kulinda mazingira ambayo mifuko imekuwa ikizagaa zagaa lakini pili linawapa ahueni wafanyabiasha kwakuwa wamekuwa wakipata hasara kutokana na kugawa mifuko bure kwa wateja wao.

Amesema kuwa vifungashio mbadala ni rafiki kwa mazingira kutokana na malighafi iliyotumika kutengenezea mifuko hiyo, ameipongeza Serikali kwa uhamasishaji mkubwa ilioufanya hasa kwa kuhakikisha wananchi wote wanapata ujumbe mfupi wa kwa njia ya simu kuhusu katazo hilo hivyo anaimani kuwa ifikapo tarehe 1 Juni 2019 hakuna mwananchi atakayekuwa anatumia mifuko ya plastiki labda awe ameau kukaidi kwa makusudi tu.

Hassan Ramadhan Kikoro, mfanyabiashara wa nafaka na vifungashio Soko la Chang’ombe Jijini Dodoma amesema kuwa kutokana katazo hili la matumizi ya mifuko ya plastiki ameanza kuuza mifuko mbadala ambapo amesema kuwa ifikapo tarehe 31 Juni 2019 kama bado atakuwa na bidhaa ya mifuko ya plastiki ataichoma moto ili kuendana na amri iliyotolewa na Serikali, na kuongeza kuwa anafahamu athari zitokanazo na mifuko ya plastiki ila wamekuwa wakiiuza kwakuwa hakukuwa na mifuko mbadala wala katazo lolote.

Kwa upande wake mfanyabiashara wa Soko la Chang’ombe, Bibi. Elizabeth Boniphace Risasi ameishukuru Serikali kwa kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki kwa kuwa kwake binafsi imemcheleweshea maendeleo kwakuwa bidhaa zake anazouza (vikapu) kutonunuliwa kutokana na uwepo wa mifuko hiyo licha ya ukweli kwamba inachangia kwa kiasi kikubwa uharibifu wa mazingira.A

Rais Magufuli afanya kikao cha kazi na RC, RAS, DC, DAS na DED wote

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Magufuli amewataka Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji kujenga ushirikiano na uhusiano mzuri baina yao ili kurahisisha utekelezaji wa majukumu yao.

Mhe. Rais Magufuli ametoa maelekezo hayo leo tarehe 16 Mei, 2019 katika kikao cha kazi kati yake na viongozi hao kilichofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam, na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, baadhi ya Mawaziri na Makatibu Wakuu.

Mhe. Rais Magufuli amewaonya baadhi ya viongozi hao ambao wamekuwa na migogoro baina yao na hivyo kuathiri utendaji kazi na amesema endapo vitendo hivyo vitaendelea hatasita kuchukua hatua ikiwa ni pamoja kuwaondoa katika nyadhifa zao.
Pamoja na kuwataka kuwa waadilifu na wenye nidhamu kazini, Mhe. Rais Magufuli amewataka kusimamia kwa ukaribu miradi yote ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao, kusimamia ukusanyaji wa mapato yote ya Serikali, kusimamia ulinzi na usalama na kusimamia rasimali za umma.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli amewapongeza viongozi hao kwa kazi nzuri wanazozifanya zinazowezesha mipango na mikakati mbalimbali ya Serikali kwenda vizuri na amewahakikishia kuwa anawaamini na anatarajia wataendelea kufanya vizuri katika utekelezaji wa majukumu yao.

“Ni matumaini yangu baada ya kikao hiki cha leo sote tutakwenda kwa mwelekeo mzuri zaidi, nendeni mkachape kazi, mimi ndiye niliyewaweka kwenye nafasi hizo na ninafuatilia utendaji kazi wa kila mmoja wenu, sitarajii kusikia tena hamuelewani miongoni mwenu” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.

Katika kikao hicho Mhe. Rais Magufuli amesikiliza kero na changamoto mbalimbali ambazo zinawakabili viongozi hao katika maeneo yao ya kazi na ameahidi kwenda kuzishughulikia.
Kabla ya kuanza kwa kikao hicho, Mhe. Rais Magufuli amemuapisha Mhe. Juma Zuberi Homera kuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi.

Mhe. Homera pia amekula kiapo cha uadilifu kwa viongozi wa umma kilichoongozwa na Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji Mstaafu Harold Nsekela.

Baada ya kikao hicho, viongozi hao wamekula futari na Mhe. Rais Magufuli aliyoiandaa kwa ajili yao.
  
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
16 Mei, 2019

 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri na Makatibu Tawala wa Wilaya Ikulu jijini Dar es Salaam
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri na Makatibu Tawala wa Wilaya Ikulu jijini Dar es Salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri na Makatibu Tawala wa Wilaya Ikulu jijini Dar es Salaam. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi pamoja na Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi pamoja na Wakuu wa Wilaya Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri na Makatibu Tawala wa Wilaya Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU 

SAVE THE CHILDREN,KIWOHEDE WAENDESHA TAMASHA LA MWANAUME JASIRI KAHAMA

$
0
0
Mashirika yasiyo ya kiserikali mkoani Shinyanga Save The Children na KIWOHEDE, yameendesha Tamasha Mwanaume Jasiri la Kupinga Mila na Desturi kandamizi katika Kata ya Ulowa halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama, kwa lengo la kutokomeza mimba na ndoa za utotoni.

Tamasha hilo limefanyika Alhamis Mei 16, 2019 katika kijiji cha Kangeme Kata ya Ulowa, ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Afisa Maendeleo Jamii wa halmashauri ya Ushetu Aminael John akimwakilisha mkuu wa wilaya ya Kahama Anamringi Macha. Tamasha hilo liliambatana na kauli mbiu isemayo “Mwanaume Jasiri ana mlinda mtoto wa kike dhidi ya mimba na ndoa za utoton”.

 Akizungumza kwenye Tamasha hilo mgeni rasmi Afisa Maendeleo wa halmashauri ya Ushetu Aminael John, amewataka wanaume kuacha kuendekeza mila na desturi kandamizi zilizopitwa na wakati, ambazo zimekuwa zikichangia kuendelea kuwepo kwa tatizo la mimba na ndoa za utotoni. Amesema wanaume wanatakiwa kubadilika na kutambua umuhimu wa elimu, kwa kumlinda mtoto wa kike dhidi ya matukio hayo ya kupewa ujauzito na kuolewa ndoa za utotoni, ili waweze kutimiza malengo yao na kuja kuwasaidia hapo baadae.

 “Natoa wito kwa wanaume wa kata hii ya Ulowa na Ushetu kwa ujumla, acheni kuendekeza mila na desturi kandamizi ambazo zimekuwa zikiwanyima haki watoto wa kike kuweza kutimiza malengo yao, na kuishia kupewa ujauzito ama kuolewa ndoa za utotoni na kuacha shule,”amesema John.

 “Tambueni kuwa mtoto anapopata elimu ataweza kuja kuwa kiongozi mkubwa hapa nchini au kupata ajira yake nzuri, ambapo atawasaidia katika maisha yenu kuliko hata hao ng’ombe mnawategemea na kuona wa thamani sana, na kuamua kuwaozesha ndoa hizo za utotoni kwa tamaa ya kupata mifugo,”ameongeza.

 Naye Mtendaji wa kata ya Ulowa Geofrey Philip, ametaja takwimu za wanafunzi ambao walikatishwa masomo mwaka jana (2018) kwa sababu ya kupewa ujauzito kuwa walikuwa 10, ambapo kwa mwaka huu (2019) tayari wameshapewa mimba wanafunzi wawili. Aidha Kaimu Mkurugenzi wa shirika la Save The Children mkoa wa Shinyanga Alex Enock, amesema wameanzisha mradi huo katika kata nane za halmashauri hiyo ya Ushetu, kwa lengo la kutokomeza mila na desturi kandamizi, ambazo zimekuwa kikwazo katika kumaliza tatizo la mimba na ndoa za utotoni. 

Amezitaja kata hizo kuwa ni Ulowa, Ushetu, Ukune, Kisuke, Uyogo,Kimampula, Bulungwa, na Ulewe, kwa kutoa elimu mbalimbali ambazo zinahusu malezi bora kwa watoto, kwa kushiriki wazazi wa pande zote mbili baba na mama na siyo kumwachia mzazi mmoja, likiwamo pia na suala la kutokomeza mila na desturi kandamizi.

 Kwa upande wake, Mratibu wa mradi huo wa kupinga mila na desturi kandamizi kutoka Shirika la KIWOHEDE Victor Reveta, ambao ndiyo wanatekeleza mradi huo kwenye kata nane za halmashauri ya Ushetu, amesema ulianza mwaka 2017 na unatarajiwa kukoma mwaka huu 2019, ambapo pia wamewajengea uwezo wanaume 25 kwa ajili ya kuendelea kutoa elimu kwa wanaume wenzao dhidi ya kutokomeza tamaduni hizo ambazo zimeshapitwa na wakati. TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI


 Afisa Maendeleo wa halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama Aminael John akizungumza kwenye Tamasha la Mwanaume Jasiri la Kupinga Mila na Desturi Kandamizi ambazo zimekuwa zikichangia mimba na ndoa za utotoni kuendelea kuwepo kwenye kata ya Ulowa na kuwaasa wanaume waachane na mila hizo. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog  Afisa maendeleo wa halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama Aminael John, akielezea madhara ya mimba na ndoa za utotoni kuwa athari zake kuwa ni ongezeko la vifo vitokanavyo na uzazi, kuugua fistula, pamoja na magonjwa mengine ya ikiwa via vyao vya uzazi vinakuwa bado havijakomaa.  Kaimu Mkurugenzi kutoka shirika la Save The Children mkoani Shinyanga Alex Enock akielezea malengo ya mradi huo wa kutokomeza mila na desturi kandamizi kwenye halmashauri hiyo ya Ushetu wilayani Kahama, kuwa ni kutokomeza tatizo la mimba na ndoa za utotoni.  Mratibu wa Mradi wa Kutokomeza Mila na Desturi Kandamizi kutoka Shirika la KIWOHEDE wilayani Kahama Victor Reveta akielezea namna wanavyoutekeleza mradi huo katika halmashauri ya Ushetu katika kata nane, kuwa ni utoaji wa elimu wa kupinga mila hizo, elimu ya malezi pamoja na kuunda vikundi vya Wanaume Jasiri ambao watakuwa mabalozi wa kutoa elimu ya kutokomeza mila kwa wanaume wenzao.  Lenard Mboje akisoma risala kwa niaba ya Wanaume Jasiri 25 ambao wamejengewa uwezo wa kutoa elimu ya kupinga mila na desturi kandamizi kwa wanaume wenzao ,amebainisha kuwa kwa sasa kumeibuka mbinu mpya ya kuozesha wanafunzi ndoa za utotoni kwa kuweka ma Bibi harusi bandia ambao wemetimiza umri wa miaka 18, lakini kumbe muolewaji ni chini ya umri huo.  Wananchi wakiendelea kusikiliza elimu ya kupinga mila na desturi kandamizi ili kutokomeza mimba na ndoa za utotoni na kuweza kutimiza ndoto za mtoto wa kike kielimu.  Wananchi wakiendelea kusikiliza elimu ya kupinga mila na desturi Kandamizi, ili kumuokoa mtoto wa kike kielimu kwa kutokomeza tatizo la mimba na ndoa za utotoni.  Burudani ya uvutaji kamba ikitolewa kwenye tamasha hilo la mwanaume jasiri la kupinga mila na desturi kandamizi ili kutokomeza tatizo la mimba na ndoa za utotoni.  Burudani ikiendelea kutolewa kwenye Tamasha hilo kwa kukimbia mbio za kwenye magunia.  Burudani ya kukimbia mbio na mayayi nayo ikitolewa kwenye Tamasha hilo la Mwanaume Jasiri katika kata ya Ulowa.  Mchezo wa kukimbiza kuku nao ulikuwepo ambao washindi walipewa zawadi zao.  Mchezo wa kukimbiza kuku ukiendelea.  Wasanii nao walikuwepo kwenye Tamasha hilo la Mwanaume Jasiri la kupinga mila na desrturi Kandamizi, ili kutokomeza mimba na ndoa za utotoni.  Washindi walioshiriki michezo mbalimbali kwenye Tamasha hilo la Mwanaume Jasiri wakiondoka na zawadi zao.  Washindi walioshiriki michezo mbalimbali kwenye Tamasha hilo la Mwanaume Jasiri wakiondoka na zawadi zao. Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU USAJILI WA MAGARI YANAYOSAMBAZA MAJISAFI

DKT. ABBASI- SERIKALI INAENDELEA NA MAJADILIANO BANDARI YA BAGAMOYO

$
0
0
Na Grace Semfuko,MAELEZO,
DAR ES SALAAM,

MKURUGENZI na Msemaji Mkuu wa, Dkt. Hassan Abbasi amesema Serikali inaendelea na majadiliano kuhusu kuendelea na ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo Mkoani Pwani ili kuona kama inaweza kuwa na tija kiuchumi kwa upande wa Tanzania.

Dkt. Abbasi alisema Serikali ina uwezo wa kujenga bandari nyingi na kwa kuwa Tanzania ina ukanda mkubwa wa ufukwe wa bahari na kwamba bado majadiliano yenye tija kwa Taifa yanaendelea kufanywa baina ya Serikali ya Tanzania na wawekezaji wa mradi huo.

“Serikali haijasema kuwa Mradi wa Bandari ya Bagamoyo ni hatari, tunaendelea na majadiliano ya utekelezaji wa mradi huo, nchi yetu imejaliwa ukanda mkubwa wa ufukwe wa bahari kwa hiyo tuna uwezo wa kujenga Bandari nyingi tu, hii ya Bagamoyo si kweli kuwa imeachwa kuna mambo ya msingi tunayajadili na tusipofikia maamuzi tutaachana nayo” alisema Dkt Abbasi.

Kuhusu suala la uwekezaji wa vitu aliloulizwa kwenye kipindi hicho Dr Abbasi alisema Serikali haitaacha kuwekeza kwenye vitu kwa sababu vitu husaidia maendeleo ya watu, mfano afya, elimu na miundombinu mingine.

“Kwenye sekta ya madini tumekuachia fedha, dawa hospitalini tumeongeza na bei zimepungua, tumekuletea yote hayo lakini bado unasema huna pesa mfukoni, Serikali inafanya yote haya kuhakikisha kuwa uchumi wetu unaleta manufaa mapana kwa Taifa” alisema Dkt. Abbasi.

Kuhusu uhuru wa Habari na kufungia magazeti yasiyofuata sheria za uchapishaji Msemaji huyo wa Serikali alisema kuwa ofisi yake haikurupuki kufungia magazeti, na kusema kuwa ni magazeti mitatu tu yalifungiwa kati ya 266 yaliyosajiliwa nchini na kuwataka wamiliki wa magazeti hayo kufuata sheria.

Kuhusu malamiko ya wafanyabiashara kwenye maeneo mbalimbali nchini ya kufunga biashara hizo kwa kisingizio cha kodi na tozo mbalimbali, Dkt. Abbasi alisema ni muhimu wakaelewa kwamba kwa sasa Serikali inapita katika kipindi cha mabadiliko na hakuna siku serikali haitadai kodi huku akieleza kuwa kodi nyingi zimepunguzwa hususan kwenye sekta za Kilimo, Mifugo na uvuvi.

“kwanza tukubali tunapita kwenye kipindi cha mabadiliko, hakuna siku serikali haitadai kodi kwa sababu ndio msingi wa maendeleo ya nchi hii, kuna dhana ilijengeka kuwa unaweza kufanya biashara bila kulipa kodi hiyo sasa haipo, lazima tuangalie changamoto ambazo zinakumba sekta mbalimbali mfano sekta ya kilimo, miufgo na uvubvi kulikuwa na kodi zaidi ya 150, serikali imefuta zaidi ya kodi 80 hadi 100” alisema Dkt Abbasi.

MEMBE AMTOLEA UVIVU ROSTAM AZIZ , AMWAMBIA WAMEKATWA MIKIA

$
0
0
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

ALIYEKUWA Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe amesema yeye na Kada wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Rostam Aziz wamekatwa mikia huku akimshauri ajikite katika kujadili masuala ya uchumi wa nchi.

Membe amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati anazungumza na waaandishi wa habari ambapo ametumia nafasi hiyo kumjibu Rostam baada ya siku za karibuni kumshambulia.

"Kwanza niseme hivi, napata kigugumizi kumjibu rafiki yangu Rostam , lakini Rostam ni mchumi na nikikutana naye nitamshauri kwamba anafanya vizuri katika jamii ya Watanzania anapozungumzia uchumi.

"Rostam inabidi awe anazungumzia masuala ya nchi na sio kujikita kuzungumza mambo binafsi. Kwa levo yetu tunatakiwa kuzungumzia masuala ya kitaifa. "Kwa kuwa Rostam ni mchumi mzuri sana , tunapaswa kujadili kwanini uchumi wetu uko hapa ulipo.Kwanini wafanyabiashara wadogo na wakubwa wanafunga biashara zao,"amesema Membe.

Amesisitiza kuwa "Rostam ni mchumi, sasa huu ndio ushauri wangu kwake, ajielekeze kwenye uchumi. Rostam wewe ni mwenzetu, sisi tumekatwa mikia, hata ukijitahidi vipi mkia wako ni mfupi". Ameongeza anamshauri wawe wanazungumza vitu ambavyo wakizungumza binadamu wanawaheshimu.

"Asijifanye mtoto mzawa badala ya kukubali Rostam na mimi ni watoto wakambo,"amesema Membe huku akimsisitiza ajikite kwenye masuala ya uchumi.

Inadaiwa kuwa Rostam alitoa kauli ya kumzungumzia Membe kuhusu uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika mwakani huku akimhusisha na masuala ya kugombea urais.

RAIS DKT. MAGUFULI ASALI IBADA YA DOMINIKA YA TANO YA PASAKA KANISA KATOLIKI LA MTAKATIFU PETRO PAROKIA YA OYSTERBAY JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na waumini wengine wa Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay wakishiriki Ibada ya Dominika ya Tano ya Pasaka katika Kanisa hilo jijini Dar es Salaam leo tarehe 19 Mei 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mtoto ambaye ni muumini wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam mara baada ya Ibada Kanisani hapo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mtoto ambaye ni muumini wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam mara baada ya Ibada Kanisani hapo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Paroko wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay Padre Dkt. Alister Makubi pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro mara baada ya Ibada katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU.

RAIS DKT MAGUFULI MGENI RASMI KWENYE MASHINDANO MAALUMU YA 20 YA QUR-AAN TUKUFU AFRIKA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameipongeza Taasisi ya Al-Hikma kwa kuandaa mashindano ya Qur’aan Tukufu yaliyojumuisha nchi mbalimbali za Afrika, na kwa kushirikiana na Serikali katika utoaji wa huduma mbalimbali za kijamii.

Mhe. Rais Magufuli ametoa pongezi hizo leo tarehe 19 Mei, 2019 wakati akihutubia katika Mashindano Maalum ya 20 ya Qur’aan Tukufu Afrika yaliyohusisha washiriki kutoka nchi 18 za Afrika na kufanyika katika Uwanja Mkubwa wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Mhe. Rais Magufuli amesema pamoja na kujenga Misikiti 50 hapa nchini, Serikali inatambua kuwa Taasisi ya Al-Hikma imesaidia jamii kwa kuchimba visima vya maji 110, imejenga shule 1 ya msingi na shule 2 za Sekondari na inawasomesha watoto yatima 400.

Kutokana na mchango huo, Mhe. Rais Magufuli ameishukuru taasisi hiyo pamoja na taasisi zingine mbalimbali zinazomilikiwa na Madhehebu ya Dini ambazo zimekuwa zikitoa mchango mkubwa katika kuhudumia jamii kwenye sekta za elimu, afya na kutoa misaada ya kibinadamu.

Kufuatia maombi yaliyotolewa na Taasisi ya Al-Hikma, Mhe. Rais Magufuli amemuagiza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo kuhakikisha taasisi hiyo inapatiwa hati ya umiliki wa eneo ililoomba libadilishiwe matumizi kwa ajili ya kujenga Kituo cha Afya kitakachotoa huduma kwa wananchi wote ifikapo Ijumaa (24 Mei, 2019).

Aidha, Mhe. Rais Magufuli amewapongeza washiriki wote wa mashindano hayo ya Qur’aan Tukufu, Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Serikali ya Saudi Arabia na wadau mbalimbali kwa kufanikisha mashindano hayo ambayo licha ya kuimarisha misingi ya kumcha Mwenyezi Mungu, yanaimarisha uhusiano baina ya Tanzania na Saudia Arabia pamoja na Mataifa yote yanayoshiriki.

Amemtaka Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa wa Saudi Arabia Mhe. Dkt. Swalehe Al-Sheikh (ambaye amehudhuria katika mashindano hayo) kufikisha salamu zake kwa Mfalme wa Saudi Arabia, ambapo pamoja na shukrani kwa uhusiano mzuri wa Tanzania na Saudia Arabia ameomba nchi hiyo ijenge Msikiti mkubwa hapa nchini kwa ajili ya Waislamu kufanya Ibada zao.

Mhe. Rais Magufuli amewatakia heri Waislamu wote katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na amezitaka mamlaka za Serikali kuchukua hatua dhidi ya wafanyabiashara wenye tabia ya kupandisha bei za vyakula wakati wa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaji Dkt. Ali Hassan Mwinyi amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kuungana na Waislamu katika mashindano hayo na amewataka Watanzania kuendelea kumuombea kutokana na kazi nzuri anazozifanya za kusukuma mbele gurudumu la maendeleo kwa kasi kubwa na kudumisha umoja wa Watanzania.

Nae Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amesema uwepo wa Mhe. Rais Magufuli katika mashindano hayo na hotuba aliyoitoa imedhihirisha dhamira yake ya kuimarisha umoja na mshikamano kwa Watanzania wote na kwamba Waislamu wote wamefarijika sana.
Mhe. Rais Magufuli amekabidhi zawadi kwa washindi wa mashindano hayo ambapo aliyeibuka mshindi wa kwanza ni Mouhamed Diallo (Senegal), wa pili ni Faruq Kabiru Yakubu (Nigeria), wa tatu ni Shamsuddin Hussein Ally (Zanzibar), wa nne ni Idrissa Ousmane (Niger) na wa tano ni Sumaiya Juma Abdallah (Pwani, Tanzania).

Pamoja na viongozi hao, mashindano hayo yamehudhuriwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma, Makamu wa Rais Mstaafu Mhe. Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Mawaziri, Mabalozi wa nchi mbalimbali na viongozi mbalimbali wa Madhehebu ya Dini na vyama vya siasa.
  
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
19 Mei, 2019 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimzawadia Bw. Mohamed El Moujabba Diallo wa Senegal baada ya kuzoa Alama 99.88 na kuibuka mshindi wa Kwanza wa Washindi wa Kuhifadhi Juzuu 30 katika mashindano maalumu ya 20 ya Qur’aan Tukufu Afrika
yaliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo Jumapili Mei 19, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimzawadia Bi. Sumayyah Juma Abdallah wa Tanzania baada ya kupata alama 98.66 na kuibuka mshindi wa tano wa Washindi wa Kuhifadhi Juzuu 30 katika mashindano maalum ya 20 ya Qur’aan Tukufu Afrika yaliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo Jumapili Mei 19, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimzawadia Bw. Idrissa Ousmane wa Niger baada ya kupata Alama 98.67 na kunyakua ushindi wa nne wa Washindi wa Kuhifadhi Juzuu 30 katika mashindano maalumuya 20 ya Qur’aan Tukufu Afrika yaliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo Jumapili Mei 19, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimzawadia Bw. Shamshuddin Hussein Ali wa Zanzibar baada ya kuzoa Alama 98.83 na kuibuka mshindi wa tatu wa Washindi wa Kuhifadhi Juzuu 30 katika mashindano maalumuya 20 ya Qur’aan Tukufu Afrika
yaliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo Jumapili Mei 19, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia maelfu ya waumini wa Kiislamu na wadau wengine wakati akihitimisha mashindano maalumuya 20 ya Qur’aan Tukufu Afrika yaliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo Jumapili Mei
19, 2019.PICHA NA IKULU

Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images