Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46327 articles
Browse latest View live

RAIS WA ZANZIBAR MHE.DK.SHEIN AZUNGUMZA NA UONGOZI WA WIZARA YA BIASHARA NA VIWANDA ZANZIBAR IKULU NDOGO KIBWENI ZANZIBAR

$
0
0


 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akifungua wa Utekelezaji wa Mpango Kazi Wiizara ya Biashara Viwanda Zanzibar, katika Ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar.(Picha na Ikulu)
IMG_6629
WAZIRI wa Biashara na Viwanda Zanzibar Mhe. Balozi Amina Salum Ali kulia na kushoto Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Biashara na Viwanda Zanzibar Ndg. Ali Khamis wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzu Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akifungua Mkutano wa Utekelezaji wa Mpango wa Wizara ya Biashara na Viwanda kwa mwezi wa Julai 2018 na Marchi 2019, uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar, wakiwa na Maofisa wa Idara za Wizara hiyo.(Picha na Ikulu)
IMG_6632
WAZIRI wa Biashara na Viwanda Zanzibar Mhe Balozi Amina Salum Ali akisoma taarifa ya Wizara yake wakati wa mkutano wa Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Wizara hiyo, uliofanyika Ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar kulia Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee na kushoto Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Biashara na Viwanda Ndg. Ali Khamis.(Picha na Ikulu)
IMG_6660
BAADHI ya Watendaji wa Idara za Wizara ya Biashara na Viwanda Zanzibar ,wakifuatilia mkutano huo wa Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Wizara ya Biashara na Viwanda Zanzibar, uliofanyika katika Ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar.(Picha na Ikulu)
IMG_6663
MKURUGENZI wa Idara ya Biashara Ndg.Khamis Ahmada Shauri, akichangia wakati wa mkutano huo wa Utekelezaji wa Mpango Kazi, katika ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar(Picha na Ikulu)
IMG_6670
MKURUGENZI wa Idara ya Masoko Dkt. Abdallah Rashid Abdallah akichangia wakati wa mkutano huo wa Utekelezaji wa Mpango Kazi , uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar.(Picha na Ikulu)
IMG_6678
NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Biashara na Viwanda Ndh Ali Khamis, akisoma taarifa ya Matumizi na Mapato ya Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Wizatra ya Biashara na Viwanda Zanzibar, wakati wa mkutano huo uliofanyika Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar.(Picha na Ikulu)
IMG_6750
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiongoza Mkutano wa Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Wizara ya Biashara na Viwanda Zanzibar, uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar.(Picha na Ikulu)
IMG_6783
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiongoza Mkutano wa Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Wizara ya Biashara na Viwanda Zanzibar, uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar.(Picha na Ikulu)
IMG_6818
MKURUGENZI Mtendaji wa Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC) Dkt. ,Said Seif Mzee, akichangia wakati wa mkutano huo wea Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Wizara ya Biashara na Viwanda katika ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar.(Picha na Ikulu)

PROF JANABI AZUNGUMZA NA WANACHAMA WA OYSTER BAY ROTARY CLUB KUHUSU HUDUMA ZA MATIBABU YA MOYO ZINAZOTOLEWA NA JKCI

$
0
0


Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiwaelezea wanachama wa Oyster Bay Rotary Klabu huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa na Taasisi hiyo wakati wa kikao cha wanachama wa klabu hiyo kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam katika Hoteli ya Oster Bay.


Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiwaelezea wanachama wa Oyster Bay Rotary Klabu huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa na Taasisi hiyo wakati wa kikao cha wanachama wa klabu hiyo kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam katika Hoteli ya Oster Bay.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiwaelezea wanachama wa Oyster Bay Rotary Klabu huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa na Taasisi hiyo wakati wa kikao cha wanachama wa klabu hiyo kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam katika Hoteli ya Oster Bay.

RC MAKONDA AWAPA POLE WATHIRIKA WA MAFURIKO, ASEMA SERIKALI INAKARABATI MIUNDOMBINU YOTE ILIYOATHIRIWA NA MVUA.

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo amefanya ziara ya ukaguzi wa athari za mafuriko ambapo amesema serikali imeanza kukarabati miundombinu iliyoathiriwa na mvua zinazoendelea kunyesha ikiwemo Madaraja,Barabara,Mito na Mifereji.

RC Makonda amesema miongoni mwa maeneo yanayoboreshwa na pesa ipo tayari ni mto msimbazi wenye urefu wa Km 19 na eneo la Jangwani ambalo maboresho yake yatagharimu zaidi ya shilingi Bilioni 200 ikiwa ni mkopo kutoka Bank ya Dunia.

Aidha RC Makonda amesema hadi sasa jumla ya watu wawili wamefariki kutokana na mvua ambapo amewapa pole wananchi waliokumbwa na athari za mafuriko ikiwemo wale ambao mali zao zimeharibiwa na wengine kulazimika kuyaama makazi yao.

Pamoja na hayo RC Makonda amewataka wananchi wanaoishi maeneo hatarishi kuhama huku akiwataka wakazi wa jiji hilo kufanya usafi katika mazingira yao ili kuepuka magonjwa ya mlipuko.

Katika hatua nyingie RC Makonda amewataka wananchi kuchukuwa tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Dengue kwa kuhakikisha wanatokomeza mazalia ya mbu na kuhakikisha wanawahi vituo vya afya pindi wanapoona dalili za homa.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akizungumza na baadhi ya watu waliothiriwa na na mafuriko kufuatia mvua kubwa zilizonyesha hivi karibuni jijini Dar. RC Makonda amefanya ziara ya yake ya ukaguzi wa athari za mafuriko, ambapo amesema serikali imeanza kukarabati miundombinu iliyoathiriwa na mvua zinazoendelea kunyesha ikiwemo Madaraja,Barabara,Mito na Mifereji.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akikatiza kwenye moja ya nyumba iliyozingirwa na maji,wakati wa ziara yake ukaguzi wa athari za mafuriko, ambapo amesema serikali imeanza kukarabati miundombinu iliyoathiriwa na mvua zinazoendelea kunyesha ikiwemo Madaraja,Barabara,Mito na Mifereji.

Muhimbili yapokea vifaa tiba vya kutibu saratani ya macho

$
0
0

Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imepokea msaada wa mashine za kutoa tiba ya saratani ya macho kwa watoto bila kuyaondoa zenye thamani ya shilingi milioni 170 kutoka Rotary Club Oyster bay jijini Dar es Salaam.

Msaada huu utawanufaisha watoto wengi wanaofikishwa hapa Muhimbili kwa ajili ya kupatiwa huduma ya saratani ya macho kutoka mikoa mbalimbali nchini.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa msaada, Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Prof. Lawrence Museru ameishukuru Rotary Club kwa kuwa vifaa hivi vitatoa tiba sahihi kwa watoto mwenye saratani ya macho bila kufanyiwa upasuaji wa kuyaondoa.

Prof. Museru amesema watoto wenye seratani ya macho watakuwa wakipatiwa huduma ya mionzi baridi na moto.

“Huu ni msaada mkubwa kwani vifaa vitasaidia kutoa tiba sahihi kwa watoto wenye matatizo ya saratani ya macho. Muhimbili tuna zaidi ya watoto 100 wanaougua saratani mbalimbali, hivyo tuna kazi kubwa ya kuwapatia huduma bora ya afya,” amesema Prof. Museru.

Pia, Mkurugenzi ameipongeza shirika lisilo la kiserikali la Tumaini la Maisha Tanzania (TLM) kwa kutoa huduma bure ya matibabu,malazi na chakula kwa watoto wenye saratani ya aina mbalimbali.

Mkurugenzi wa Mradi wa Rotary Club ya Oyster bay, Kripa amesema wametoa msaada kwa ajili ya kuboresha huduma ya matibabu kwa watoto wenye saratani ya macho.

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Macho, Dkt. Anna Sanyiwa wa Muhimbili amesema vifaa hivi ni vya kisasa na kwamba vinatumiwa na nchi mbalimbali duniani kutoa tiba ya saratani ya macho.

“Ni vifaa muhimu kwa tiba ya saratani ya jicho. Vifaa hivi vinatusaidia kuondoa vivimbe kwenye macho au jicho bila kufanya upasuaji wa kuondoa jicho la mgonjwa mwenye saratani. Kabla ya kupata vifaa, tulikuwa tunalazimika kuondoa jicho kwa mgonjwa,” amefafanua Dkt. Anna.

Amesema endapo watoto wenye saratani ya macho wakifikishwa hospitali mapema watatibiwa bila macho au jicho kuondolewa kwa kutumia vifaa vilivyokabidhiwa leo. Vifaa vilivyopokelewa leo ni mashini mbili ya mionzi ya moto, mashini moja ya mionzi baridi na kamera mbili.
 Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru akizungumza baada kupokea msaada wa vifaa vinavyotumika kutoa huduma ya saratani ya macho kutoka Rotary Club Oyster bay jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto kwake ni  Rais wa Rotary Club Oyster bay ya Dar es Salaam, Vikash Shah na Mkurugenzi wa Mradi, Kripa. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji wa Muhimbili, Dkt. Baruani Sufiani na Dkt. Anna Sanjiwa wa Muhimbili.
 Prof. Lawrence Museru akikabidhiwa bango leo na Rais wa Rotary Club Oyster bay jijini Dar es Salaam, Vikash Shah.
 Prof. Museru wa Muhimbili na Rais wa Rotary Club, Vikash Shah wakiwa katika picha ya pamoja na wataalam wa MNH na wawakilishi wa Rotary Club ya Oyster bay jijini Dar es Salaam.

UVCCM WILAYA YA ARUSHA MJINI WAWAJIA JUU VIJANA WANAOTAPELI WAFANYABIASHARA.

$
0
0
Katibu wa Umoja wa UVCCM Wilaya Arusha akizungumza na vyombo vya habari leo Ofisini kwake.
Mwenyekiti wa umoja wa was Vijana wa chama cha apinduzi(Uvccm)wilaya ya Arusha Mjini akiwa na katibu wa Hamasa Abdi na Marijani na Mjumbe wa kamati ya utekelezaji Mohamed Khalifa wakizungumza na Vyombo vya habari

Na mwandishi wetu -Michuzi TV,ARUSHA

Umoja wa Vijana wa chama cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Arusha Mjini umelaani vikali baadhi ya vijana ambao wanajiita Viongozi wa Umoja huo kujipatia fedha isivyohalali kwa wafanyabiashara wa madini na wengine jijini Arusha.

Wakizungumza na waandishi wa habari Katibu wa Umoja huo Idd Ntonga alisema kuwa jambo hilo sio la kufumbiw macho kwa kuwa limekuwa likitia doa umoja huo.

Aidha alisema kuwa swala hilo linazidi kushika kasi kutokana na vitendo hivyo kukithiri na kupelekea wafanyabishara kutoa malalamiko yao pamoja na ushahidi kwakundi hilo.

“Pamoja na baadhi ya wafanyabiashara kuja kwetu na kulalamika ni kwamba tumeshachukua hatua kwa kupeleka majina ya wahusika katika vyombo vya sheria lakini pia tumeamua kuwaita waandishi wa habari ili pia kufahamisha umma wa watanzania juu ya utapeli huo ambao Uvccm hatuhusiki nao”alisema ntonga

Pia alisema kuwa chama cha mapinduzi kinaongozwa kwa taratibu na kanuni mbali mbali ambapo amesema ikiwa kama kuna mchango wowote unahitajika upo utaratibu wa viongozi kufanya hivyo na sio kila mtu kujiendea kwa wafanyabiashara.

Kwa upande wake katibu Hamasa wa Uvccm wilaya ya Arusha Mjini Abdi Marijani alisema kuwa pamoja na malalamiko hayo wapo baadhi ya vijana wamekuwa wakianzisha makundi katika mitandao wa (Whatsap) yenye jina la umoja huo ambao ameyataka kuacha mara moja.

Marijani alisema kuwa Makundi hayo yamedaiwa kutumika vibaya kwa kuwaunga viongozi wakubwa wa serikali na kuwahoji badala ya kutumia vikao halali ambavyo vinatumika na chama hicho.

Nae mjumbe wa chama hicho Mohamed Kalifa amewatoa hofu wafanyabiashara jijini Arusha kuendelea na shughuli zao kwa kuwaserikali ya awamu ya tano imekuwa imeweka mazingira mazuri ya kufanya shughuli zao.

Viongozi hao wamechukua hatua hiyo ya kuzungumza na vyombo vya habari baada ya kupokea malalamiko mengi kutoka kwa wafanyabiashara kupeleka malalamiko kwa viongozi wa chama hicho.

NAIBU WAZIRI IKUPA AIPIGA JEKI UWT DODOMA MIFUKO 30 YA SARUJI

$
0
0

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia watu wenye ulemavu Mhe.Stella Ikupa akikabidhi Mifuko 30 ya Saruji kwa UWT Mkoa wa Dodoma wa kwanza kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya UWT Rehema Mwendamaka (katikati) mwenye T.shirt nyeupe ni Kaimu katibu wa UWT Diana Madukwa na mwingine ni Mwenyekiti wa UWT Neema Majule wakipokea mifuko hiyo.
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya UWT Mkoa wa Dodoma,Rehema Mwendamaka akimpongeza kwa moyo wa dhati Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia watu wenye ulemavu Mhe.Stella Ikupa mara baada ya kuwakabidhi Mifuko 30 ya Saruji kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha watoto.
Kaimu katibu wa UWT Mkoa wa Dodoma,Diana Madukwa akimshukuru Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia watu wenye ulemavu Mhe.Stella Ikupa mara baada ya kuwakabidhi Mifuko 30 ya Saruji kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha watoto.
Mwenyekiti wa a UWT Mkoa wa Dodoma,Neema Majule akimpongeza na kumshukuru kwa Moyo wa dhati aliouonesha Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia watu wenye ulemavu Mhe.Stella Ikupa mara baada ya kuwakabidhi Mifuko 30 ya Saruji kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha watoto.


Mwenyekiti wa a UWT Mkoa wa Dodoma,Neema Majule akimsisitiza jambo Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia watu wenye ulemavu Mhe.Stella Ikupa mara baada ya kuwakabidhi Mifuko 30 ya Saruji kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha watoto.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia watu wenye ulemavu Mhe.Stella Ikupa akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa UWT Mkoa wa Dodoma mara baada ya kuwakabidhi Mifuko 30 ya Saruji kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha watoto.
Sehemu ya ujenzi wa kituo cha watoto kinachojengwa ambapo Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia watu wenye ulemavu Mhe.Stella Ikupa amekabidhi mifuko 30 ya saruji
Mwenyekiti wa a UWT Mkoa wa Dodoma,Neema Majule pamoja na baadhi ya viongozi wakiagana na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia watu wenye ulemavu Mhe.Stella Ikupa mara baada ya kuwakabidhi Mifuko 30 ya Saruji kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha watoto.


Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Dodoma Neema Majule akisalimiana na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia watu wenye ulemavu Mhe.Stella Ikupa alipowasili katika ofisi za chama kukabidhi Saruji Mifuko 30 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha watoto.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia watu wenye ulemavu Mhe.Stella Ikupa akisalimiana na Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya UWT Mkoa wa Dodoma Rehema Mwendamaka.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia watu wenye ulemavu Mhe.Stella Ikupa akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya chama cha CCM mkoa wa Dodoma alipowasili kutoa mchango wake wa saruji mifuko 30 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha watoto kushoto kwake ni Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Dodoma Neema Majule.
Picha na Alex Sonna-Fullshangwe blog,Dodoma

...........................

Na.Alex Sonna,Dodoma

NAIBU Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia watu wenye ulemavu Mhe.Stella Ikupa ametoa mifuko ya Saruji 30 kwa Umoja wa Wanawake Tanzania mkoa wa Dodoma (UWT) ikiwa ni katika kuunga mkono jitihada zinazofanywa na jumuiya hiyo za kujenga kituo cha kulelea watoto jijini hapa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana baada ya kukabidhi saruji hiyo Naibu Waziri huyo amesema kuwa anaupongeza uongozi wa UWT Mkoa w Dodoma kwa ubunifu mkubwa ambao wameendelea kuufanya ikiwemo wa kujenga kituo cha kulelea watoto ambacho sasa ni mardi ambao utakuwa mkubwa sana.

“Nampongeza sana Mwenyekiti pamoja na wale ambao anaambatana nao ,hivyo kutokanana na mradi huu naamini wataondokana na utegemezi”alisisitiza Mhe.Ikupa

Aidha amesema kuwa Saruji hiyo itawasaidia kuwasogeza ,lakini pia amewaomba wadau mbalimbali waweze kujitokeza kusaidia kwani bado UWT wanahitaji vifaa mbalimbli vya ujenzi kama vile Mabati,Mbao ,na vifaa vingine.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dodoma Neema Majule alisema kuwa wanamshukuru Waziri Ikupa kwa kuwa na moyo wa kipekee kwa kuwaletea mifuko ya sumenti 30 kwaajili ya kukamilisha ujenzi wa madarasa 3.

“Kiukweli ametushangaza sana wanawake wa Dodoma kwa upendo wake wa dhati maana sikila mtu aliyenacho anatoa,hivyo mimi na mjumbe wangu wa kamati ya utekelezaji, bado tunaendelea kuwaomba wale wote wenye mapenzi mema na uwt waweze kujitokeza kuchangai kwani bado tunahitaji,Mabati,Malumalu,Madirisha na milango ili ujenzi uweze kukamilika”amesema Majule.

Hata hivyo Mwenyekiti huyo alisema kuwa Mradi huo ni wa ccm mkoa lakini utasaidia wilaya zote saba zilizopo Dodoma. “Na lengo letu mara baada ya mradi huu kuanza ambao utakuwa na thamani ya shilingi mil.200,utaweza kabisa kufanya UWT DODOMA kuwa endelevu na utasaidia kuweza kuweka miradi mingine kila wilaya ili wanawake waweze kupata vitega uchumi kila wilaya kwa kujitegemea.

MKUU WA WILAYA KOROGWE AHIMIZA WANANCHI KULIPA KODI KWA WAKATI

$
0
0

Na Veronica Kazimoto,Tanga

Mkuu wa Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga Kissa Kasongwa amewahimiza wananchi kulipa kodi kwa wakati ili kuiwezesha Serikali kutekeleza miradi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuboresha huduma za jamii kwa lengo la kuleta maendeleo nchini.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Wiki ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi inayofanyika wilayani humo, Mkuu huyo wa Wilaya amesema kuna miradi ya huduma za jamii inayojengwa katika Wilaya ya Korogwe ikiwemo Hospitali ya Wilaya, miradi ya barabara, maji, umeme na elimu ambayo yote inategemea kodi ili iweze kukamilika.

“Bado Korogwe kiwango chetu cha kulipa kodi ni kidogo kwani kati ya wananchi 303,000 wa wilaya hii, ni wananchi 2,800 ndiyo wanalipa kodi na tumeshaelekeza kwamba wale wasiokuwemo kwenye mfumo wa TRA ambao mauzo ghafi yao ni chini ya sh. 4,000,000 wanatakiwa kuwa na vitambulisho vya wajasiriamali.

“Sote tunatakiwa tutambue kwamba, tusipolipa kodi, tunajidhoofisha wenyewe kimaendeleo. Hivyo, tujitahidi kulipa kodi kwa hiari na kwa wakati ili tuweze kutekeleza miradi inayoendelea hapa wilayani kwetu,” alisema Kasongwa.

Naye Mkurugenzi wa Sheria wa Sekretariati ya Bodi na Huduma za Kisheria wa TRA Makao Makuu Salim Beleko, amesema kuwa kodi ni sawa na damu kwenye mwili wa binadamu, hivyo kama Serikali itashindwa kupata kodi itashindwa kufanya jambo lolote la maendeleo kwa wananchi wake.

Aidha, Beleko ameongeza kuwa wananchi hawatakiwi kulalamika kwasababu wanayo fursa ya kukata rufaa endapo hawataridhika na makadirio ya kodi waliyokadiriwa na malalamiko yao tatafanyiwa kazi Mamlaka ya Mapato Tanzania huku akisisitiza kuwa Tanzania ni moja ya nchi chache ambazo wananchi wake wanalipa kodi kwa hiari tofauti na nyingine ambapo wanalipa kwa nguvu.

Kwa upande wa Kaimu Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Lucas Kaigarula amesema lengo la wiki hiyo ya huduma na elimu kwa mlipakodi ni kutoa elimu ya kodi, kusikiliza malalamiko, changamoto pamoja na kupokea maoni mbalimbali kutoka kwa walipakodi.
Wiki ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi inafanyika nchi nzima ambapo kwa Mkoa wa Tanga inafanyika wilayani Korogwe. Wiki hii ya elimu kwa mlipakodi imeanza tarehe 13 na itamalizika tarehe 17 Mei, 2019 ikiongozwa na kaulimbiu isemayo “Karibu tukuhudumie na tukuelimishe”.
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga Kissa Kasongwa akizungumza kwenye ufunguzi wa Wiki ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi katika Mkoa wa Tanga inayofanyika katika Stendi ya zamani ya mabasi, Manundu. Wengine ni Mkurugenzi wa Sheria wa Sekretariati ya Bodi na Huduma za Kisheria wa TRA Makao Makuu Salim Beleko (kulia) na Kushoto ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Korogwe Rehema Bwasi

Mkurugenzi wa Sheria wa Sekretariati ya Bodi na Huduma za Kisheria wa TRA Makao Makuu Salim Beleko akizungumza kwenye ufunguzi wa Wiki ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi inayofanyika katika Stendi ya zamani ya mabasi, Manundu mkoani Tanga. Wengine ni Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Kissa Kasongwa (kushoto) na Kulia ni Kaimu Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Lucas Kaigarula.
Mkurugenzi wa Sheria wa Sekretariati ya Bodi na Huduma za Kisheria wa TRA Makao Makuu Salim Beleko akizungumza kwenye ufunguzi wa Wiki ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi inayofanyika katika Stendi ya zamani ya mabasi, Manundu mkoani Tanga. Wengine ni Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Kissa Kasongwa (kushoto) na Kulia ni Kaimu Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Lucas Kaigarula. 

RAIS DKT MAGUFULI AMTUMBU RC KATAVI,AMOSS MAKALLA


TRA YATAKIWA KUIMARISHA UKAGUZI WA MASHINE ZA EFD

$
0
0
Afisa Elimu kwa Walipakodi TRA Kanda ya Kaskazini Eugenia Mkumbo amesema kuwa Mamlaka hiyo inatoa fursa kwa wafanyabiashara wanaolalamikia kukadiriwa kodi ya juu kuliko kipato chao.
Mkui wa Wilaya ya Arusha Gabriakizindua wiki ya mlipa kodi iliyofanyika eneo la stendi kuu ya Mabasi ya mikoani,ambapo ameitaka TRA 
Baadhi ya wananchi waliojitokezankatika uzinduzi wa wiki ya Elimu kwa mpiga kodi iliyoansaliwa na Mamlaka ya Matapo nchini TRA Jijini Arusha



Na Vero Ignatus ,Arusha.

Mamlaka ya Mapato TRA mkoa wa Arusha imetakiwa kuimarisha ukaguzi wa mashine za kielektroniki ili kuwabaini wafanyabiashara wanaokwepa kodi na kuikosesha serikali mapato ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua Kali za kisheria. 

Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro amesema hayo wakati akizindua wiki ya mlipa kodi iliyofanyika eneo la stendi kuu ya Mabasi ya mikoani,ambapo ameitaka TRA kuhakikisha kuwa wanakagua na kuwabaini wafanyabiashara wasiotoa risiti na kuikosesha serikali mapato jambo ambalo ni uhujumu uchumi.

Aidha amewataka Wafanyabiashara kutoa taarifa za siri juu ya baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu wanaokwepa kodi ili hatua Kali zichukuliwe juu yao.
Kaimu Meneja wa TRA mkoa wa Arusha Irine Donald amesema kuwa wataendelea kushirikiana n wafanyabiashara katika kutatua changamoto na kero zao ili waweze kufurahia kulipa kodi ya serikali.

Kwa upande wao wafanyabiashara Elisante Mungure na Winifrida Massawe Wafanyabiashara. wamelalamikia uwepo wa wamachinga mbele ya maduka yao huku wakiuza bidhaa zinazofanana hivyo kukosa soko la bidhaa zao.

WABUNGE WA BUNGE LA UGANDA WATEMBELEA BUNGE LA AFRIKA

$
0
0
Wabunge wa Bunge la Uganda wametembelea Bunge la Afrika ‘Pan - African Parliament’ katika makao yake makuu Jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini ili kujifunza namna bunge hilo linavyofanya kazi. 

Ujumbe huo wa wabunge nane kutoka Uganda ukiongozwa na Mheshimiwa,Ongalo Obote Kenneth umepokelewa leo Jumanne Mei,14 2019 na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika,Mheshimiwa Stephen Masele ambaye anatoka Tanzania,Kanda ya Mashariki ya Afrika.

Mhe. Kenneth alisema lengo la kufika katika Bunge la Afrika ambalo wabunge wake wanaendelea na Mkutano wa pili wa kawaida wa bunge la tano la tano ni kujifunza namna bunge hilo linavyofanya kazi.

“Tumefurahi kufika hapa kuona na kujifunza mambo kadha wa kadha kuhusu Bunge la Afrika, ikiwemo historia yake,muundo wake na namna wanavyoendesha shughuli zao na kuzungumzia masuala ya Afrika,kwa kweli bunge hili ni imara kupitia viongozi wake akiwemo,Mheshimiwa Masele ambaye ni kijana lakini ana uwezo mkubwa wa kuongoza taasisi hiyo kubwa Afrika”,alisema Mhe. Kenneth.

Kwa upande wake, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika, Mhe. Stephen Masele amewapongeza wabunge hao kwa kuona umuhimu wa kutembelea bunge hilo kujifunza kuhusu bunge na siasa za Afrika.

“Nimefurahi kupokea ujumbe wa wabunge wa bunge la Uganda wanaotoka katika kamati mbalimbali,mmejionea jinsi tunavyoendesha shughuli za bunge la Afrika,wamefahamu kuhusu historia ya bunge,historia ya Umoja wa Afrika (AU),ukombozi Afrika na mambo mengine”,alisema Mhe. Masele.

“Bunge la Afrika lina wabunge kutoka nchi mbalimbali barani Afrika,wenye tamaduni na lugha tofauti tofauti,ninaamini kwa siku zote mtakazokuwa hapa bungeni,mtafaidika vya kutosha kuhusu siasa za Afrika”,aliongeza Mhe. Masele.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika,Mheshimiwa Stephen Masele akiwa ofisini kwake katika Makao Makuu ya Bunge la Afrika,Midrand,Johannesburg, Afrika Kusini akizungumza na Ujumbe wa wabunge kutoka Bunge la Uganda waliotembelea Bunge la Afrika leo Mei 14,2019. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog.
Kushoto ni Mhe. Masele akizungumza na Ujumbe wa wabunge kutoka Bunge la Uganda (kulia) waliotembelea Bunge la Afrika.
Wabunge wa Bunge la Uganda wakimsikiliza Mhe. Masele. 
Kiongozi wa Ujumbe huo wa wabunge kutoka Uganda Mhe. Ongalo Obote Kenneth akielezea lengo la ziara yao kutembelea Bunge la Afrika.
Picha ya pamoja,Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika,Mheshimiwa Stephen Masele na wabunge wa bunge la Uganda.
Mbunge kutoka Uganda,Mhe. Mugoya Kyawa(kulia) akiteta jambo na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika,Mhe.Stephen Masele.Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog

SERIKALI KUVUTIA UWEKEZAJI KUPITIA SEKTA YA UTALII Inbox x

$
0
0
Na Ahmed Mahmoud Arusha

Serikali imeeleza kuwa itatumia sekta ya utalii na watalii wanaokuja kutembelea nchini kushawishi uwekezaji mkubwa na kutangaza kufungua milango ya fursa ya uwekezaji nchini kwa lengo la kuinua uchumi na kuongeza fursa za ajira kwa vijana.

Hayo yameelezwa na Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu Uwekezaji Angela Kairuki kwenye Kongamano la kuvutia wawekezaji lililofanyika Jijini hapa ambapo alibainisha mkakati huo wa serikali ya awamu ya tano kuongeza wigo mpana wa wawekezaji wakubwa kuvutiwa kuja kuwekeza nchini.

Amesema kuwa Tanzania itaendelea kupokea wageni wengi wanaokuja kwa ajili ya utalii na kuwatumia kutangaza fursa za utalii kama walivyofanya kwa wageni kutoka China ambao wapo nchini kwa siku nne kutembelea vivutio vya utalii ikiwemo Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro na Serengeti sanjari na Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara.

Amebainisha kuwa huu ni mkakati wa serikali ya awamu ya tano katika kupanua ushirikiano kwa lengo la kukuza biashara hususani ya madini na utalii kuongeza wigo wa mapato ya nchini na kutumia fursa ya rasilimali tulizojaaliwa

“Niombe ndugu zangu watanzania tuweze kuitangaza vizuri nchi yetu hususani nyinyi waandishi wa habari mmeona waandishi wenzenu kutoka China wanaitangaza nchi yetu hii itasaidia kuongeza watalii na kuitangaza Tanzania na rasilimali ilizonazo kwa manufaa ya sasa na baadae”

Awali akiongea kwenye kongamano hilo Naibu waziri wa nchi sera bunge ajira vijana na watu wenye ulemavu Anthony Mavunde ameishukuru wizara ya uwekezaji kwa kuja na mkakati huo wa kuongeza na kutangaza kuvutia uwekezaji nchini kwani anaona kupitia uwekezaji wataweza kupambana na changamoto ya mfumuko wa ongezeko la ajiri kwa vijana wanaomaliza vyuoni.

Amesema kuwa uwekezaji mkubwa utafungua fursa pana ya kuweza kuongeza wafanyakazi kwenye kada mbali mbali na sasa serikali kupitia watalii itafungua milango kwa wawekezaji wanaotaka kuja kuwekeza nchini kwani miongoni mwa watalii wengi wanaokuja wano fursa nzuri za kuwekeza nchini.

“Serikali inapenda wafanyakazi kutoka nje ya nchi kuja kufanyakazi nchini kwa kufuata sheria zilizopo na si kwamba inakataa wafanyakazi hao kwani wanaleta ujuzi mpya na kuongeza ufanisi kazini ila wafuate taratibu za kupata vibali tena sasa upatikanaji wake umeboreshwa”

Nae Mkurugenzi wa Taasisi ya uwekezaji nchini TIC Jofrey Mwambe amesema kuwa mpango wao ni kuweka mkakati wa kuongeza wawekezaji kuwekeza nchini na mkutano huo umeonyesha mafanikio makubwa kwa kampuni iliyowaleta wageni hao italeta wageni wengine mwaka huu takribani 10 elfu kutoka nchini China.

Amesema kuwa hiyo ni faida kwa watalii hao wanaokuja kutembelea vivutio vya utalii nasi tukaitumia nafasi hiyo kutangaza fursa za uwekezaji ikiwa ni mkakati wa kuongeza wigo wa uwekezaji nchini kusaidia kuinua pato la taifa.

Aidha kwa Mujibu wa Mkurugenzi wa taasisi ya sekta Binafsi Godfrey Simbeye amesema kuwa ujio wa wageni hao na wawekezaji kutoka taifa la China kwao ni faraja kwa ukuaji wa sekta binafsi kuongeza wigo wa pato la taifa na uchumi kwa ujumla.

Amesema uendeshaji wa uchumi ni muhimu sana kwani serikali ikiweka mazingira mazuri kwa kuvutia wawekezaji watanzania watapata mitaji kutokana na wawekezaji hao kuja kuweza ila serikali zao nazo ziliweka mazingira maziru ya kibiashara kwa wananchi wa mataifa hayo, “Tunaiomba serikali kuona umuhimu wa mazingira mazuri ya kuwekeza kwa wananchi wa Tanzania tunaishukuru serikali yetu ya awamu ya tano kuanza kuona umuhimu huo na kuiga mataifa kama ya wenzetu kutoka nje”

Tanzania Tunao Uwezo Mkubwa wa Kuzalisha Mifuko Mbadala - Makamba Inbox x

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba akielezea mbele ya Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa katika kikao chao leo Jijini Dodoma. Waziri Makamba alisisitiza umuhimu wa ushirikiano baina ya viongozi wakati wa utekelezaji wa Operesheni ya Marufuku ya Matumizi ya Mifuko ya Plastiki nchini inayotarajiwa kuanza tarehe 1/6/2019.[/caption]

Na: Mwandishi Wetu

Tanzania inao uwezo mkubwa wa kuzalisha mifuko mbadala ambayo itatosheleza kufanikisha azma yake ya kupiga marufuku biashara na matumizi ya mifuko ya plastiki.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, mhe. Januari Makamba wakati akizungumza na Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa leo Jijini Dodoma.

Makamba amesema kuwa ni jambo la kushangaza kuona asilimia 100 ya mifuko ya karatasi inayotumika nchini Rwanda na asilimia hamsini nchini Kenya inazalishwa Tanzania huku Tanzania ikitumia zaidi ya asilimia 80 ya mifuko ya plastiki inayozalishwa nje ya nchi jambo linalokinzana na dhana ya kukuza uchumi wa viwanda. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba akielezea mbele ya Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa katika kikao chao leo Jijini Dodoma. Waziri Makamba alisisitiza umuhimu wa ushirikiano baina ya viongozi wakati wa utekelezaji wa Operesheni ya Marufuku ya Matumizi ya Mifuko ya Plastiki nchini inayotarajiwa kuanza tarehe 1/6/2019. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo akizungumza wakati wa kikako baina yake na Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa katika kikao chao leo Jijini Dodoma

“ Tunao uwezo mkubwa wa kuzalisha mifuko mbadala, wazalishaji wa mifuko hiyo wameithibitishia Serikali kuwa wanao uwezo mkubwa wa kuzalisha mifuko hiyo ambapo Kiwanda cha Karatasi cha Mufindi kimesema kitaongeza uzarishaji zaidi ya maratatu huku wawezkezaji zaidi ya 50 wakiwa wameagiza mashine za kuzalishia mifuko hiyo,”Alisema Waziri Makamba.

Makamba aliongeza kuwa nchi ya Tanzania inaweza kufanikiwa katika zoezi hili kwa kuwa inazalisha mifuko mbadala ya karatasi ambayo hutumiwa kwa kiasi kikubwa na nchi jirani za Rwanda huku kenya wakitumia asilimia kubwa ya mifuko kutoka Kiwanda cha Karatasi cha Mufindi cha hapa nchini, Kenya ikitumia asilimia 50, jambo linalotoa tafsiri kuwa tunaouwezo wa kuzalisha mifuko mbadala itakayotosheleza,” Alisema Januari Makamba.

Waziri Makamba amesema kuwa wazalishaji wa mifuko mbadala wameithibitishia Serikali kuwa wanao uwezo mkubwa wa kuzalisha mifuko hiyo ambapo Kiwanda cha Karatasi Mufindi kitaongeza uzalishaji zaidi ya mara tatu kinavyozalisha sasa huku wawekezaji zaidi ya 50 wakiwa wameagiza mashine kwa ajili ya kuzalishia mifuko hiyo. Baadhi ya Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa wakifuatilia maelezo ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba(hayupo pichani) alipokuwa akiwaeleza kuhusu utekelezaji wa Operesheni ya Marufuku ya Matumizi ya Mifuko ya Plastiki nchini inayotarajiwa kuanza tarehe 1/6/2019 Baadhi ya Watendaji wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira wakifuatilia maelezo ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba (hayupo pichani) alipokuwa akiwaeleza kuhusu utekelezaji wa Operesheni ya Marufuku ya Matumizi ya Mifuko ya Plastiki nchini inayotarajiwa kuanza tarehe 1/6/2019. (Na: Ofisi ya Makamu wa Rais)

Katika hatua nyingine Waziri Makamba alitumia fursa hiyo kutoa rai kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa kushirikiana kwa karibu na mamlaka zingine zitakazo husika katika zoezi la kutokomeza biashara na matumizi ya bidhaa za Plastiki zilizopigwa marufuku.

Akizungumzia marufuku hiyo Makamba amesema kuwa katika awamu ya kwanza marufuku hiyo inahusisha mifuko ya plastiki tu huku bidhaa zingine zinazotumia plastiki vifungashio vya plastiki kuendelea kutumika wakati utaratibu ukiendelea. Alizitaja bidhaa hizo kuwa ni bidhaa za chakula, kilimo na dawa.

Utekelezaji wa katazo hilo la matumizi ya bidhaa za plastiki nchini linafuatia utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyotoa tarehe 26, April, 2019 katika maadhimisho ya Muungano jijini Dodoma.

BEI ZA MCHELE SOKO LA BUGURUNI

$
0
0
  Bei za mchele katika soko la Buguruni wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam  kama inavyo onekana katika picha.
 Bei za bidhaa mbalimbali katika soko Buguruni wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam,kamazinavyo onekana katika picha.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)



JESHI LA POLISI MOROGORO LAWASHIKILIA WATUHUMIWA 8 KWA KUCHOMA NYUMBA YA MFUGAJI

$
0
0
Na Hussein Stambuli, Morogoro.

Jeshi la polisi mkoani morogoro limewakamata na kuwashikilia watuhumiwa 8 walio jihusisha na tukio la kuchoma nyumba ya mfugaji kwa sababu ya migogoro ya wakulima na wafugaji sambamba na kufunga barabara kuu ya dar-es salamu –morogoro maeneo ya maseyu mikese katika kushinikiza kuachiwa kwa watuhumiwa waliokamatwa kwa kitendo hicho cha kuchoma nyumba.

Kamanda wa polisi mkoani hapa Wilbroad  Mutafungwa amesema chanzo cha mgogoro huo ni kutokana na wananchi siku ya jana tarehe 13,5,2019 kuvamia nyumba ya mfugaji aliyefahamika kwa jina la mbega sultani boy kwa kudaiwa kulisha mifugo kwenye mashamba ya wakulima kwa muda mrefu.
Ambapo wanakijiji hao wakaivamia nyumba yake na kuchoma moto jumla ya nyumba tano baada ya kumkosa mfugaji huyo anayedaiwa kwa muda huo kuwepo mahakamani kukabiliana na kesi nyingine zinazo mkabili za kulisha mifugo mazao ya wakulima na kusababisha nyumba hizo kuteketea vibaya huku wake wa 2 na watoto 19 akiwemo mtoto mmoja mlemavu wakinusurika kifo.

“kufuatia tukio hilo tumefanikiwa kuwatia mbaroni watuhumiwa wane kwa kosa la kufanya fujo na kufunga barabara ambao ni ernest mkandula (25), machemba samiki (40), juma shabani (40) shaban ally (45) wakazi wa kijiji cha maseyu na misako mikali inaendelea katika kijiji hicho na tumefanikiwa kuyaondosha magogo yaliyokuwa yamewekwa barabara na safari zinaendelea. Amesema mutafungwa

Kamanda wa polisi akatoa wito kwa wananchi kutii sheria na kuacha kujichukulia sheria mkononi kwani husababisha kukosa haki zao za msingi kwa kujiingiza kwenye makosa mengine..
 Kamanda  wa polisi mkoani morogoro wilbroad Mutafungwa na watuhumiwa 8 walio jihusisha na tukio la kuchoma nyumba ya mfugaji sambamba na kufunga barabara kuu ya dar-es salamu –morogoro maeneo ya maseyu mikese
 magari yakiwa yamesimama kutokana na kufungwa barabara kuu ya dar-es salamu –morogoro maeneo ya maseyu mikese.
 watuhumiwa 8 walio jihusisha na tukio la kuchoma nyumba ya mfugaji sambamba na kufunga barabara kuu ya dar-es salamu –morogoro maeneo ya maseyu mikese
wilbroad mutafungwa kamada wa polisi mkoa wa morogoro, akizungumza na waandishi wa habari mkoani morogoro

MPINA ATOBOA SIRI YA ONGEZO LA GHAFLA LA VIWANDA VYA NYAMA Inbox x

$
0
0
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina  (mwenye kizibao chekundu) akitoa maelekezo kwa  mmiliki wa kiwanda cha nyama cha Eliya Foods Overseas LTD kilichopo Longido  ndugu Shabbir Virjee(mwenye shati jeupe), kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Longido Frank Mwaisumbe

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina (Mwenye nguo nyeusi) akishuka kwenye gari maalum ya kubebea maziwa baada ya kulikagua gari hilo la kiwanda cha maziwa cha Kilimanjaro Fresh alipotembelea kiwanda hicho kuangalia utendaji wake hivi karibuni.

Na John Mapepele

Serikali imewahakikishia wawekezaji wa viwanda vya mazao ya mifugo nchini kuwa hakuna atakayechezea masoko yao kwa kuingiiza bidhaa hizo sokoni kwa njia isiyo halali na badala yake serikali imetaka jitihada zinazofanywa na wawekezaji lazima zilenge kuwainua wafugaji kote nchini na kutoa majawabu ya changamoto zinazowakabili wafugaji ikiwa ni pamoja na ajira, masoko na nyama bora ili uwekezaji huo uwe wenye tija na endelevu.

Hayo amesemwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa Luhaga Joelson Mpina alipofanya ziara ya kikazi mkoani Arusha leo kukagua shughuli mbalimbali za sekta ya mifugo ambapo amesema Serikali ya awamu ya tano imejipanga kikamilifu  kuhakikisha  kuwa  hakuna mtu atakayekwepa kufuata taratibu za  biashara ya mazao ya mifugo kutoka ndani na nje ya nchi ili kuwa na ushindani wa halali.

Amesema  kutokana na udhibiti uliofanywa na serikali wa kuzuia ukwepaji wa kodi, uingizaji wa mazao ya mifugo na kwa udanganyifu na utoroshaji mkubwa mifugo kwenda nje ya nchi kwa njia za panya umesaidia kuwavutia wawekezaji wengi kuwekeza katika ujenzi wa viwanda vikubwa vya nyama na maziwa  kwa wingi kuliko kipindi chochote kuanzia nchi yetu ilivyopata uhuru hadi sasa.

“Mheshimiwa Waziri, tumekuwa tukitorosha  mifugo kwenda kuuza nchi za jirani kwa kuwa hapa kwetu  palikuwa hakuna soko la uhakika la kuuzia lakini sasa tunaishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kutusaidia kupata kiwanda hiki hapa Longido ambacho kitakuwa mkombozi wa soko la uhakika la mifugo yetu” alisisitiza  Mzee maarufu wa kimasai, Olesiyanda Sidala wakati Waziri Mpina alipomaliza kukagua kiwanda cha kusindika  nyama cha Eliya Foods Overseas LTD kilichopo eneo la Longido mkoani Arusha.

Mkurugezi Mtendaji wa Kiwanda hicho Shabbir Virjee alisema Kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wa kuchinja ng’ombe 500 hadi 1000 na  mbuzi na kondoo 2000 hadi 5000 kwa siku na kinatarajia kutoa zaidi ya ajira 300,ambapo pia aliiomba serikali eneo la ekari  100 kwa ajili ya kupumzishia mifugo kabla ya kuchinjwa na kuahidi kuwa ifikapo Oktoba mwaka huu kiwanda kitakuwa kimekamilika na kuanza kufanya kazi.

Aidha Waziri Mpina aliongeza kwamba hivi sasa wananchi na wawekezaji wengi wanajitokeza kuwekeza kwenye sekta ya mifugo baada ya muda mrefu kukimbia uwekezaji kwa sababu walikuwa wanafika mahala  wanachinja na kukosa masoko ya kuuza nyama hizo.

Amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kuwalinda wawekezaji wote kwa sheria na kwamba  Wizara itaendelea na operesheni muda wote kila mahali kuanzia  bandarini,mipakani, viwandani, kwenye  maduka na katika  vya ndege  kukagua na kuona kama kuna mtu ameingiza  bidhaa kwa kufuata sheria na ubora wake.

Aliongeza kuwa Tanzania ni nchi ya pili barani Afrika kwa kuwa na mifugo mingi hivyo inaweza kutoa malighafi ya kutosha kwa viwanda  vya mifugo vinavyoanzishwa na kwamba asilimia 1.4 ya mifugo yote duniani ipo Tanzania na asilimia 11 kwa Afrika, ambapo ina jumla ya Ngombe milioni 30.5, Mbuzi milioni 18.8 na Kondoo milioni 5.3.

Mkuu wa Wilaya ya Longido, Frank Mwaisumbe  amepongeza jitihada zinazofanywa na Wizara ya mifugo ambapo amesema  Wizara  imeonyesha kuwa siyo ya kupokea misaada kama ilivyokuwa inatazamwa awali bali inayoweza hata kusaidia wizara nyingine zisizozalisha na kuifanya nchi yetu isonge mbele.

“Mheshimiwa Waziri naomba kusema wazi kuwa umekuwa bega kwa bega kudhibiti utoroshaji na ukwepaji wa kodi na umeonyesha uwezo mkubwa wa kuitendea haki sera ya viwanda kwa kuweka mazingira mazuri ya kuvutia viwanda vingi kujengwa  naamini wizara nyingine zige mfano kutoka wizara ya Mifugo na Uvuvi “ aliongeza Mwaisumbi.

Mpina aliongeza kuwa Serikali inaendelea na mikakati mbalimbali ya kuboresha kosaafu za mifugo ili kupata mifugo bora itakayoweza kushindana na mifugo mingine katika masoko ya kimataifa ambapo alisema  tayari madume bora ya ngombe yanayozalisha  mbegu bora yameletwa na serikali kwenye Kituo cha Uhimilishaji cha Taifa  Usariver jijini Arusha ambayo yanauwezo wa kutosha kwa nchi nzima.

Katika kuhamasisha wafugaji wanawapeleka watoto wao kwenye mafunzo maalum ya ufugaji, Waziri Mpina alitoa nafasi kwa mtoto mmoja wa mfugaji anayeongoza kwa mifugo mingi kuweza kusomeshwa  bure na serikali kwenye Wakala wa Mafunzo ya Mifugo Tengeru na Kituo cha Uhimilishaji cha Taifa  Usariver jijini Arusha.

Katika ziara hiyo Waziri Mpina alitembelea  bwawa lililobomoka la Kimokowa  na kuelekeza kuwa Wizara na Halmashauri ya Longido  kukarabati bwawa hilo mara moja pia alimwelekeza katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo kukarabati majosho 8 kati ya 16 ya Wilaya ya Londigo kabla ya Julai mwaka huu, ambapo pia alisema tayari Wizara imeshatoa kiasi cha Shilingi milioni 150 kwa ajili ya kukarabati soko la kimataifa la mnada wa mpaka wa Longido.

Kaimu Msajiri wa Bodi ya Nyama nchini Imani Sichalwe alimhakikishia Waziri Mpina kuwa Bodi ya nyama itaendelea kushirikiana na wawekezaji katika kuwatafutia masoko ya bidhaa zao ndani na nje ya nchi.

Katika hatua nyingine  Waziri Mpina alitembelea kiwanda cha maziwa  cha Kilimanjaro Fresh chenye uwezo wa kuzalisha  lita 5000 hadi 50000 kwa siku ambapo kwa sasa kimeanza kuzalisha lita 5000 baada ya kuanza rasmi uzalishaji Februari 2, mwaka  huu,ambapo aliwahakikishi kuwapa ushirikiano na aliwataka  wamiliki kuangalia bei wanaonunua maziwa kwa wafugaji zisiwe kandamizi.

Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda hicho Irfhan Virjee amesema kuwa kiwanda hicho kimekuwa kikiuza jumla ya lita 4000 kwa siku na kwamba kiwanda kinatarajia kuongeza uzalishaji wa mazao mengine ya maziwa ikiwa ni pamoja na jibini na siagi ndani ya miezi miwili ijayo, ambapo kwa sasa kinaendelea kutoa maziwa yenye radha tofauti za matunda.

Kwa upande wake Kaimu Katibu Mkuu Mifugo, Daktari  Asimwe Lovince alimshukuru Waziri Mpina na kumhakikishia kuwa amepokea maelekezo yote na kwamba atayafanyia kazi kikamilifu katika kipindi kifupi ili sekta ya mifugo iweze kukua kwa kasi  na kuleta mapinduzi yanayohitajika kwa sasa. 

Aidha alisema kufanya kazi kwa viwanda vya nyama na maziwa nchini kutasaidia kuliingizia taifa fedha za kigeni ambapo kwa upande wa viwanda vya nyama  vitasaidia kutoa mazao mengi zaidi kwenye damu(vyakula vya mifugo),pembe na ngozi.

Katika kipindi cha  miaka miwili sasa wizara ya Mifugo na Uvuvi imekuwa  na mikakati mbalimbali ya kuleta  mageuzi ya sekta kuanzia mapato, kutafuta ufumbuzi wa migogoro baina ya wafugaji wa watumiaji wengine wa ardhi, kudhibiti magonjwa, kuboresha kosaafu za mifugo kwa njia mbalimbali.

BALOZI AMINA SALUM ALI AFANYA MAZUNGUMZO NA WANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA HARBAD

$
0
0
Na Ali Issa Maelezo -Zanzibar 

Ujumbe wa wanafunzi sita kutka Chuo Kikuu cha Harvad umefanya mazungumzo na Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Balozi Amina Salum Ali Ofisini kwake Migombani.

Ujumbe huo upo Zanzibar kuangalia ubora wa chumvi inayozalishwa hapa nchini ukilinganisha na mataifa mengine ili hatimae iweze kutambulika na kuingia katika soko la kimataifa.

Akizungumza na Ujumbe huo Balozi Amina Salum Ali amesema Chumvi inayozalishwa Zanzibar ina ubora wa hali ya juu kutokana na mfumo unaotumika wakati wa uzalishaji na inaweza kutumika katika nchi yoyote duniani.

Amsema kufika kwa ujumbe huo ni mafanikio kwa mradi wa chumvi ya Zanzibar na ameeleza matarajio yake kuwa utasaidia kuhakikisha chumvi ya Zanzibar inaingia katika soko la kimataifa.

Aliutaka ujumbe huo kufanya uchunguzi wa kina kujua ubora wa chumvi ya Zanzibar na kuona tofauti iliyopo na chumvi inayozalishwa n nchi nyengine duniani.

Mbali na kuangalia ubora wa chumvi inayozalishwa Zanzibar, pia ujumbe huo utakagua kilimo cha pilipili na kilimo cha mwani ambacho kimekuwa maarufu sana katika maeneo mbali mbali ya pwani ya Zanzibar.

Wanafunzi hao kutoka Marekani wametawanywa katika mataifa mbali mbali na kwa hapa Tanzania wamekuja kumi ambapo wanne wamebakia Tanzania Bara.
Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Balozi Amina Salum Ali akizungumza na Ujumbe wa wanafunzi sita kutoka Chuo Kikuu cha Harvad cha Marekani Ofisini kwake Migombani, wanafunzi hao wapo nchini kuangali ubora wa Chumvi inayotengenezwa Zanzibar.
Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Balozi Amina Salum Ali na ujumbe wa wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Harvad wakiangalia Paketi za Chumvi iliyotengenezwa Zanzibar Ofisini kwake Migombani.Picha Na Miza Othman –Maelezo Zanzibar

RAIS MAGUFULI NA USHINDI WA KULINDA RASILIMALI ZA MADINI

$
0
0

Na Judith Mhina -Maelezo

Adhima ya Tanzania kuwa kinara uuzaji wa dhahabu Afrika Mashariki na kuzuia utoroshaji ya madini yake imetimia.

Hii imetokana na kutekelezwa kwa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli katika kuratibu na kutambua madini yote, kuanzishwa kwa masoko ya ununuzi ya dhahabu ndani na uuzwaji wa madini nje ya nchi.

Kuzinduliwa kwa soko kuu la kimataifa la uuzaji wa madini ya dhahabu Mkoa wa Mwanza, lililopo katika jengo la Rock City Mall, kumedhihirisha nia ya Tanzania kuhakikisha inalinda rasilimali za madini ya Tanzania. Hii inawahakikishia wachimbaji wadogo kunufaika na kazi yao, pamoja kuchangia pato la Taifa.

Akiongoza utekelezaji wa agizo la Rais Magufuli mapema mwezi Machi Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa alizindua mnada wa dhahabu katika Mkoa wa Geita, yenye masoko mawili, ili kuondoa changamoto ya wachimbaji wadogo kuhangaika kutafuta mahali pa kuuzia madini yao.

Baadhi ya Mikoa iliyotekeleza agizo la ujenzi vituo vya kuuzia dhahabu ni pampja na Geita, Mwanza, Shinyanga, Chunya (Mbeya) Mpanda, (Katavi), Mara, Arusha, Singida, Iringa, Mkinga (Tanga) na Manyara ambao wanajenga vituo viwili vya kuuzia madini ya Tanzanite na vito vingine.

Aidha, ujenzi huo utajengwa katika miji midogo ya Mererani maalum kwa ajili ya uuzwaji wa madini ya Tanzanite na vito, wakati soko la pilli linajengwa mji mdogo wa Orkesumet kwa ajili ya uuzwaji wa ruby, green tourmaline na vito vingine.

Jitihada za Rais Magufuli za kulinda na kupigania rasilimali za Watanzania zimemfanya Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni kutuma ujumbe ulioongozwa na Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini Peter Crolies, kukiri kuwa uwekezaji nchini Tanzania katika sekta ya madini ni mfano wa kuigwa na nchi nyingine za Afrika.

Waziri Crories amesema hayo katika ziara ya siku nne mkoani Mwanza na Geita ambapo lengo ni kujifunza, jinsi Tanzania inavyoendesha sekta ya madini na kufanikiwa kuwa na uhusiano mzuri baina ya serikali, wachimbaji wadogo na wakubwa kwa kudumisha amani.

“Tanzania na Uganda zitaendelea kushirikiana katika Nyanja za kitekinolojia na taarifa za kiolojia Tumekuja hapa kujifunza jinsi ya usimamizi wa rasilimali ya madini ili nasi kupata ujuzi kutoka TZ ambao tutakwenda kufikisha jatika serikali yetu na kuwafundisha wananchi wetu wanaojihusisha na uchimbaji” Amesema Waziri Clories.

Amesema ziara hiyo imekuwa na mafanikio kwao kwa kuwa hajawahi kushuhudia na kujifunza rasilimali za madini zinavyotakiwa kuendeshwa na kutunzwa hadi kufikia hatua ya jamii na serikali wa kupata uchumi mzuri.

Katika ziara hiyo Naibu Waziri wa Madini Stansilaus Nyongo amesema wachimbaji wadogo ndio watoroshaji wakubwa wa madini hususan dhahabu lakini Tanzania imejipanga kuthibiti na kupunguza namna ya utoroshwaji wa huo kwa kuanzisha masoko hayo ya kuuzia madini.

Watanzania wamekuwa na utamaduni au desturi ya kudharau na kubeza jambo lolote jema linaloanzishwa hapa nchini na kupenda kusifia na kuona mambo yanayofanyika nje ya Tanzania ndio mema tu. Waswahili husema “Mdharau kwao ni mtumwa”.

Lakini ubora wa Tanzania umethibitishwa na Waganda walioona ni vizuri kuja kujifunza kuhusu madini kutokana na nchi yetu kutunza vizuri rasilimali za madini hasa kwa wachimbaji wadogo. Ambapo imekuwa vigumu kwa nchi nyingine kufanya kazi kwa ushirikiano na kudumisha amani. Amesema Waziri Nyongo.

Ujumbe wa Uganda ulikuwa na maafisa waandamizi wa serikali pamoja na wachimbaji wadogo 35 ulitembelea maeneo yanayochibwa dhahabu katika migodi ya Geita Gold Mine- GGM Rwangwa Busonwa Mine, Msagano na maeneo ya kuchengulia dhahabu ya Rich Hill na Genge tatu.

Zoezi hili la uazishwaji wa vituo vya kuuzia madini ni utekelezaji wa maagizo kadhaa ya Rais Magufuli ambapo, itarahisisha serikali kuratibu wanunuzi wa madini na wanunuzi hao kujulikana wanapoyauza madini hayo, ndani na nje ya nchi, na kutambua kiasi cha fedha nchi ilizopata kutokana na mauzo hayo.

Aidha, kurejeshwa kwa utaratibu wa zamani wa Benki Kuu ya Tanzania-BOT, kuhusika na ununuaji na uuzaji wa dhahabu, iliyochenguliwa nje ya nchi na kuratibu mapato yatokanayo na uuzwaji wa dhahabu na madini mengine ambayo yanapatikana hapa nchini Tanzania. Itadhihirisha dhahiri kama nchi tunaongoza katika uuzaji wa dhahabu Afrika Mashariki.

Kulingana na taarifa ya mwezi April ya BOT kuna ongezeko la uuzwaji wa dhahabu nje ya nchi. Ongezeko hilo lililotokana na ulinzi na uangalizi sahihi wa uuzwaji wa madini ambapo watoroshaji walikuwa na mwanya wa kuiba katika migodi na kutorosha nje ya Tanzania.

Umakini wa serikali wa Awamu ya Tano umaezaa matunda katika migodi miwili mikubwa hapa Tanzannia ukiwemo Geita Gold Mining na North Mara Gold Mining baada ya kuzalisha kiasi kikubwa zaidi cha madini hayo na kuuzwa nje ya nchi .

Ongezeko hilo ni la Dolla za Marekani milioni 100 kuanzia Julai 2018, mpaka kuishia Machi 2019 ambapo ni sawa na fedha za Tanzania Bilioni 223. Ongezeko hilo ni la fedha za Marekeni ni sawa na bilioni 1.68 ikilinganishwa na mwaka 2018 mwezi Machi.

Pia, Mkoa wa Geita kilo 198 za dhahabu zimeuzwa kwa kipindi cha mwezi mmoja tangu soko hilo limeanzishwa tarehe 22 Machi mpaka April 2019. Vilevile Mkoa wa Mbeya Wilaya ya Chunya ndani ya siku nne tangu soko kuanzishwa, kilo 22 zimeuzwa wakati hapo nyuma zilirekosiwa kuuzwa kilo 12 tu kwa mwaka mzima.

Ongezeko hili la dhahabu kuuzwa nje ya nchi, imesababisha kukuza pato la bidhaa na huduma zitolewazo na nchi ya Tanzania zilizotolewa kuishia Machi 2019 kufikia Dola za marakani Milioni 8.5 kutoka milioni 8.4 dola za marekani kwa mwezi Machi 2018.

Soko la dhahabu la Wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya lilofunguliwa tarehe 05 Mei 2019 na Katibu Mkuu Wizara ya Madini Profesa Simon Msanjila akifungua soko hilo amesema “ Serikali imejipanga kuhakikisha soko a madini linatatua changamoto kubwa zinazowakabili wadau wa sekta ya madini”

Ameongeza kwa kusema “Kwa kuanzia serikali imeanzisha soko la pamoja la madini ambalo litatoa fursa kuanzia mchimbaji mdogo mpaka mkubwa na kuuza dhahabu yake sambamba na kuwatafutia wanunuzi”

Aidha, wafanyabiashara wa Chunya waliomba serikali kuwahakikishia usalama wa mali zao –madini na fedha zao katika soko hilo lililofunguliwa mjini Chunya, lakini bado wana wasiwasi kuhusu usalama wao. Hivyo ni vema serikali kuimarisha ulinzi na usalama kwenye eneo la soko na kwenye migodi.

Pia wanaipongeza serikali kwa kuweka soko la pamoja la madini ambalo litatoa nafasi kila mfanyabiashara wa dhahabu kuwa kwenye ushindani wa bidhaa yake.

Akitoa kasoro kadhaa zilizokuwepo kwenye sheria ya madini ya mwaka 2007 na kanuni zake Rais Magufuli aliagiza kufanya marekebisho ya sheria ambayo yalifanyika mwaka 2018 na kuagiza kurekebisha kanuni zake wakati wa Mkutano Mkuu na Wadau wa Sekta ya Madini mapema Januari 2019.

Marekebisho hayo yalihusu utaratibu wa uchimbaji wa dhahabu ikiwemo kuweka kumbukumbu ya dhahabu inayopatikana na mauzo yake, na kusaidia kupata takwimiu sahihi. Vilevile kujua ukweli katika Afrika Mashariki nchi ipi inayoongoza kwa uuzwaji wa dhahabu na madini mengine.

Maagizo hayo ya Rais Magufuli yalitolewa wakati wa mkutano wa wadau wa madini uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Julius Nyerere-JNCC uliofanyika kuanzia tarehe 22 Januari mpaka 24, Januari 2019 Jijini Dar-es-salaam.

Hata hivyo, zipo changamoto mbalimbali za madini ambazo zinahitaji kufanyiwa kazi kwa kutoa elimu ya kutosha kwa wadau ili serikali iweze kufanya kazi kwa pamoja na wananchi – wachimbaji wadogo wadogo na migodi mikubwa ya wawekezaji.

Mfano hivi karibuni Wilaya ya Gairo Mkoa wa Morogoro wachimbaji wa madini kadhaa na mmliiliki wa madini wamewakimbia viongozi ambao ni Mwenyekiti wa Tume ya Madini Profesa Idris Kikula ambaye alifatana na Mkuu wa Wilaya ya Gairo Seriel Mchembe na Kamishina wa Tume ya Madini Dkt. Athanas Machiyeke.

Wadau hao waliacha madini aina ya Ruby, Nut, pikipiki na vitendea kazi baada ya kuona wanamiliki madini hayo kinyume cha sheria bila kuwa na kubali cha kumiliki. Hii ni uthibitisho kuwa sekta ya madini bado inahitaji ushirikishaji wa karibu wa wadau ili wajue wajibu wao wa kufata sheria, taratibu, kanuni na miongozo ya sekta husika.

RAIS DKT MAGUFULI AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUAGA MWILI WA RAFIKI YAKE MAREHEMU FESTO RUTAMIGWA ISOKOZA KATIKA HOSPITALI KUU YA JWTZ YA LUGALO JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakitoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa marehemu Festo Rutamigwa Isokoza alipoongoza waombolezaji kuaaga mwili huo katika Hospitali kuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania ya Lugalo jijini Dar es salaam leo Jumatano Mei 15, 2019. Marehemu, aliyekuwa mtaalamu wa kilimo alifanya kazi katika JWTZ na taasisi zake za kilimo kama vile JKT Itende na Mgambo kabla ya kustaafu akiwa Shirika la Elimu Kibaha, alikuwa rafiki mkubwa wa Rais Dkt Magufuli ambaye walisoma pamoja tokea darasa la kwanza hadi la saba katika Shule ya Msingi ya Chato mkoani Geita na baadaye elimu ya sekondary katika Seminari ya Katoke, Biharamulo mkoani Kagera.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakitoa mkono wa pole kwa mjane Mama Anna Isokoza kuifariji familia ya marehemu Festo Rutamigwa Isokoza alipoongoza waombolezaji kuaaga mwili wa marehemu katika Hospitali kuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania ya Lugalo jijini Dar es salaam leo Jumatano Mei 15, 2019. Marehemu, aliyekuwa mtaalamu wa kilimo aliyefanya kazi katika JWTZ na taasisi zake za kilimo kama vile makambi ya JKT ya Itende na Mgambo kabla ya kustaafu akiwa Shirika la Elimu Kibaha, alikuwa rafiki mkubwa wa Rais Dkt Magufuli ambaye walisoma pamoja tokea darasa la kwanza hadi la saba katika Shule ya Msingi ya Chato mkoani Geita na baadaye elimu ya sekondary katika Seminari ya Katoke, Biharamulo mkoani Kagera.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwasindikiza mjane Mama Anna Isokoza na familia ya marehemu Festo Rutamigwa Isokoza baada ya kuongoza waombolezaji kuaaga mwili marehemu katika Hospitali kuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania ya Lugalo jijini Dar es salaam leo Jumatano Mei 15, 2019. Marehemu, aliyekuwa mtaalamu wa kilimo aliyefanya kazi katika JWTZ na taasisi zake za kilimo kama vile makambi ya JKT ya Itende na Mgambo kabla ya kustaafu akiwa Shirika la Elimu Kibaha, alikuwa rafiki mkubwa wa Rais Dkt Magufuli ambaye walisoma pamoja tokea darasa la kwanza hadi la saba katika Shule ya Msingi ya Chato mkoani Geita na baadaye elimu ya secondary katika Seminari ya Katoke mjini Biharamulo mkoani Kagera.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli akiagana na familia ya marehemu Festo Rutamigwa Isokoza baada ya kuongoza waombolezaji kuaaga mwili marehemu katika Hospitali kuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania ya Lugalo jijini Dar es salaam leo Jumatano Mei 15, 2019. Marehemu, aliyekuwa mtaalamu wa kilimo aliyefanya kazi katika JWTZ na taasisi zake za kilimo kama vile makambi ya JKT ya Itende na Mgambo kabla ya kustaafu akiwa Shirika la Elimu Kibaha, alikuwa rafiki mkubwa wa Rais Dkt Magufuli ambaye walisoma pamoja tokea darasa la kwanza hadi la saba katika Shule ya Msingi ya Chato mkoani Geita na baadaye elimu ya secondary katika Seminari ya Katoke mjini Biharamulo mkoani Kagera.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea machache baada ya kuongoza waombolezaji kuaaga mwili marehemu marehemu Festo Rutamigwa Isokoza katika Hospitali kuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania ya Lugalo jijini Dar es salaam leo Jumatano Mei 15, 2019. Marehemu, aliyekuwa mtaalamu wa kilimo aliyefanya kazi katika JWTZ na taasisi zake za kilimo kama vile makambi ya JKT ya Itende na Mgambo kabla ya kustaafu akiwa Shirika la Elimu Kibaha, alikuwa rafiki mkubwa wa Rais Dkt Magufuli ambaye walisoma pamoja tokea darasa la kwanza hadi la saba katika Shule ya Msingi ya Chato mkoani Geita na baadaye elimu ya secondary katika Seminari ya Katoke mjini Biharamulo mkoani Kagera.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na waombolezaji baada ya kuongoza hafla ya kuaaga mwili marehemu marehemu Festo Rutamigwa Isokoza katika Hospitali kuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania ya Lugalo jijini Dar es salaam leo Jumatano Mei 15, 2019. Marehemu, aliyekuwa mtaalamu wa kilimo aliyefanya kazi katika JWTZ na taasisi zake za kilimo kama vile makambi ya JKT ya Itende na Mgambo kabla ya kustaafu akiwa Shirika la Elimu Kibaha, alikuwa rafiki mkubwa wa Rais Dkt Magufuli ambaye walisoma pamoja tokea darasa la kwanza hadi la saba katika Shule ya Msingi ya Chato mkoani Geita na baadaye elimu ya secondary katika Seminari ya Katoke mjini Biharamulo mkoani Kagera.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa zamani Mhe. Edgar Maokola Majogo aliyekuwa miongoni mwa waombolezaji baada ya kuongoza hafla ya kuaaga mwili marehemu marehemu Festo Rutamigwa Isokoza katika Hospitali kuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania ya Lugalo jijini Dar es salaam leo Jumatano Mei 15, 2019. Marehemu, aliyekuwa mtaalamu wa kilimo aliyefanya kazi katika JWTZ na taasisi zake za kilimo kama vile makambi ya JKT ya Itende na Mgambo kabla ya kustaafu akiwa Shirika la Elimu Kibaha, alikuwa rafiki mkubwa wa Rais Dkt Magufuli ambaye walisoma pamoja tokea darasa la kwanza hadi la saba katika Shule ya Msingi ya Chato mkoani Geita na baadaye elimu ya secondary katika Seminari ya Katoke mjini Biharamulo mkoani Kagera.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na askari baada ya kuongoza hafla ya kuaaga mwili marehemu marehemu Festo Rutamigwa Isokoza katika Hospitali kuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania ya Lugalo jijini Dar es salaam leo Jumatano Mei 15, 2019. Marehemu, aliyekuwa mtaalamu wa kilimo aliyefanya kazi katika JWTZ na taasisi zake za kilimo kama vile makambi ya JKT ya Itende na Mgambo kabla ya kustaafu akiwa Shirika la Elimu Kibaha, alikuwa rafiki mkubwa wa Rais Dkt Magufuli ambaye walisoma pamoja tokea darasa la kwanza hadi la saba katika Shule ya Msingi ya Chato mkoani Geita na baadaye elimu ya secondary katika Seminari ya Katoke mjini Biharamulo mkoani Kagera. PICHA NA IKULU

KILWA WASAINI MKATABA WA BIL 1.2 UJENZI WA KITUO CHA AFYA Inbox x

$
0
0
 Na  David Langa Afisa afisa habari  Kilwa .
 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa imesaini mkataba wa ujenzi wa Kituo cha Afya Somanga na upanuzi wa hospitali ya Wilaya Kinyonga.

Mkataba huo wenye thamani ya shilingi bilioni moja na milioni mia mbili (1.2bilion) umesainiwa kati viongozi wa Halmashauri  ya Wilaya ya Kilwa na kampuni ya Pan African Energy ambao ni wadau wa maendeleo katika Wilaya ya Kilwa. Utiaji saini huo umeshuhudiwa na wawakilishi wa kampuni ya Pan African na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa.

 Mkurugenzi wa Wilaya ya Kilwa Ndg. Renatus Mchau ameishukuru kampuni hiyo kwa msaada huo uliokuja kwa wakati na kueleza kuwa kwa muda mrefu Wilaya ya kilwa ilikuwa na changamoto katika sekta ya Afya
lakini kwa sasa changamoto hizo zinakaribia kwisha kutokana na halamshauri yake kuweka nguvu katika kuzitatu.

‘ Tangu mwaka 2017 tumepokea zaidi ya shilingi bilioni moja na milioni mia nane kutoka ofisi ya Rais TAMISEMI katika mpango wa uboreshaji wa Miundo mbinu ya sekta ya Afya ambapo vituo vinne vya Afya vya Masoko, Tingi, Pande na Nanjilinji, na sasa mchango wa hawa wadau wametuongezea nguvu nyingine katika kuendeleza sekta ya Afya. 

Alisema msaada huo wa Pan African utaongeza idadi ya vituo vya Afya kutoka vitano vya sasa hadi sita ambapo kati ya hivyo vituo vinne vitakuwa na uwezo wa kufanya upasuaji  na kuongeza damu kwa wanawake wajawazito.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Mhe.Abuu Mjaka amewashukuru kwa mara nyingine kampuni hiyo kwa msaada huo kwani ni mara ya pili wanatoa msaada mkubwa baada ya ujenzi wa awali wa kituo cha Afya cha Nangurukuru. ‘Nyie sasa tunawatambua rasmi si kama wadau tu bali familia ya Kilwa’’ aliongeza Mhe.Mjaka.

Ujenzi Kituo cha Afya cha Somanga ulianza kwa Mchango wa  nguvu za wananchi ambapo mpaka sasa jengo la mapokezi lipo katika hatua ya linta  ambapo zaidi ya shilingi  milioni sabini  kutokana na mchango wa wananchi , halmashauri pamoja mchango binafsi toka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Dkt.John Pombe Magufuli wa shiingi milioni ishirini(20,000,000) aliyoitoa mwaka 2017 akiwa katika ziara mkoani Lindi. Mhe.Rais alitoa msaada huo baada ya kuombwa na wananchi waliomsimamisha katika kata ya Somanga, msaada huo ulikuwa chachu kwa wanachi wa kata hiyo na hivyo wakaanda kuchangia nguvu  zao.

Upanuzi huo utahusisha ujenzi wa Jengo la mapokezi,Jengo la wazazi, Upasuaji , chumba cha kuhifadhia maiti na chumba cha kufulia nguo vyote kwa pamoja vikiwa na thamani ya milioni mia nane na thelathini.

Katika hospitali ya Wilaya ya Kinyonga upanuzi utahusisha chumba cha kuhifadhia maiti na Bohari ya dawa thamani ya shilingi milioni mia nne.

Baada ya kukamilika kwa ujenzi Kituo cha Afya cha Somanga, Wilaya ya Kilwa itakuwa na vituo vya Afya sita ambavyo ni Somanga, Tingi, Masoko,Nanjilinji , Pande na Njinjo.

Mkurugenzi wa Wilaya ya Kilwa,Renatus Mchau (kulia) Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa,Abuu Mjaka wakisani mkataba wa ujenzi wa kituo cha Afya Somanga na upanuzi wa hospitali ya Wilaya Kinyonga kushoto ni Mwanasheria Pan African,Rita Mahel.

 Mkurugenzi wa Wilaya ya Kilwa,Renatus Mchau (kulia) Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa,Abuu Mjaka (katikati) wapili kutoka kushoto ni Mwanasheria Pan African,Rita Mahele na Meneja uhusiano Pana African Andrew Kashangaki wakibadilisha hati leo mara baada ya kusaini  mkataba wa ujenzi wa kituo cha Afya Somanga na upanuzi wa hospitali ya Wilaya Kinyonga.
Picha ya pamoja

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS WA BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA (AFRICAN DEVELOPMENT BANK (AfDB) DKT. AKINWUMI ADESINA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na mgeni wake Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB Dkt. Akinwumi Adesina mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na mgeni wake Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB Dkt. Akinwumi Adesina mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi zawadi ya picha ya Wanyama Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB Dkt. Akinwumi Adesina mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi zawadi ya picha ya Wanyama Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB Dkt. Akinwumi Adesina mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza mgeni wake Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB Dkt. Akinwumi Adesina mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza mgeni wake Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB Dkt. Akinwumi Adesina mara baada ya kupiga picha ya pamoja na viongozi wengine kutoka nchini  na ujumbe kutoka benki hiyo ya AfDB.


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanahabari pamoja na mgeni wake Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB Dkt. Akinwumi Adesina mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB Dkt. Akinwumi Adesina mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam akizungumza na wanahabari. PICHA NA IKULU




Viewing all 46327 articles
Browse latest View live




Latest Images