Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1850 | 1851 | (Page 1852) | 1853 | 1854 | .... | 1898 | newer

  0 0


  Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde akizungumza na Mwakili wa UNICEF Tanzania Bi. Maniza Zaman alipokwenda kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kufanya kazi nchini Mei 10, 2019 Jijini Dodoma.
  Mwakilishi wa UNICEF Tanzania Bi. Maniza Zaman (kulia) akimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde. (katikati) ni Bi. Khadija Othman mwakilishi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
  Mwakilishi wa UNICEF Tanzania Bi. Maniza Zaman, akimweleza jambo Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde alipomtembelea Ofisini kwake Jijini Dodoma. (Kulia) ni Bi. Khadija Othman mwakilishi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
  Mkuu wa Ushauri na Sera za Kijamii Bw. Paul Van Lifford (kushoto), akieleza jambo kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde (kulia) kuhusu ushirikiano baina ya UNICEF na Serikali katika utekelezaji wa Sera ya Hifadhi ya Jamii (Social Security Policy).
  Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde akioneshwa picha ya Watoto na Mwakilishi wa UNICEF Tanzania Bi. Maniza Zaman, mara baada ya mazungumzo yao, Jijini Dodoma.
  Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde akijadili jambo Mwakilishi wa UNICEF Tanzania Bi. Maniza Zaman, mara baada ya mazungumzo yao, Jijini Dodoma.
  Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde akijadili jambo na Mkuu wa Ushauri na Sera za Kijamii Bw. Paul Van Lifford (kulia), (katikati) ni Mkurugenzi wa Hifadhi ya Jamii Bw. Daud Kaali. PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU) .

  Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde amekutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa UNICEF nchini Bi. Maniza Zaman ambaye amemaliza muda wake alipomtembelea Ofisi kwake iliyopo Jijini Dodoma. 

  Katika mazungumzo yao, Mhe. Mavunde amelipongeza Shirika la Umoja wa Mataifa la UNICEF kwa kushirikiana na Serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo na kwa kutoa misaada katika sekta mbalimbali nchini.

  “UNICEF imekuwa ikishirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu katika masuala mbalimbali yaliyolenga kuboresha na kuimarisha utekelezaji wa Sera ya Hifadhi ya Jamii (Social Security Policy of 2003), kuwapatia mafunzo watumishi katika masuala ya virutubishi na hifadhi ya jamii, pia kuwapatia vitendea kazi kama vile komputa na magari ambayo yanatumika kwenye miradi mbalimbali,” alieleza Mavunde.

  Aliongeza kuwa, Serikali imeguswa na jitihada za UNICEF na itaendeleza ushirikiano na shirika hilo katika kutekeleza jukumu la kuhudumia Watoto. Aidha, Naibu Waziri Mavunde alimpongeza Bi. Maniza Zaman kwa kazi nzuri aliyofanya kipindi cha muda wake na kumsihi kuendelea kuwa balozi mzuri wa masuala ya Watoto. “Tutakukumbuka kwa juhudi na ushauri uliokuwa ukitupatia katika masuala ya elimu na haki za Watoto,” alisema Mavunde.

  Kwa upande wake, Bi. Maniza Zaman amesema anaishukuru Serikali kwa ushirikiano iliompatia kwa kipindi chote alichokuwa hapa nchini.

  0 0

   Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Mwanza (MWAUWASA), Mhandisi. Anthony Sanga  (kushoto) na  Mkurugenzi wa Kampuni ya Bennet Contractors, Sabato Boaz  kutoka Jijini Mwanza  wakibadilishana  nakala za mkataba waliosaini Mei 10, 2019 wilayani Busega ,  kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa Maji wa Nyashimo na kushuhudiwa na viongozi wa Chama na Serikali wa Wilaya ya Busega na Mkoa wa Simiyu, wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa, Mhe. Anthony Mtaka (mwenye suti ya rangi ya kijivu)  ambao utakaogharimu zaidi ya shilingi bilioni 1.8
   Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Mwanza (MWAUWASA), Mhandisi. Anthony Sanga  (kushoto) na  Mkurugenzi wa  Kampuni ya Bennet Contractors Sabato Boaz  kutoka Jijini Mwanza  wakisaini  mkataba wa ujenzi wa mradi wa Maji wa Nyashimo Mei 10, 2019 wilayani Busega na kushuhudiwa na viongozi wa Chama na Serikali wa Wilaya ya Busega na Mkoa wa Simiyu, wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(mwenye suti ya rangi ya kijivu)  ambao utakaogharimu zaidi ya shilingi bilioni 1.8.
   Kutoka kushoto Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Mwanza(MWAUWASA), Mhandisi. Anthony Sanga,   Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka na Mbunge wa Busega, Dkt. Raphael  Chegeni wakielekea eneo maalum la utiaji saini mkataba wa ujenzi wa mradi wa maji wa Nyashimo wilayani Busega kati ya MWAUWASA na Mkandarasi Kampuni ya Bennet Contractors kutoka Jijini Mwanza.
   Baadhi ya wananchi wa kata ya Nyashimo wakifuatilia zoezi la  kusaini  mkataba wa ujenzi wa mradi wa maji wa Nyashimo wilayani Busega kati ya MWAUWASA na Mkandarasi Kampuni ya Bennet Contractors kutoka Jijini Mwanza, mradi utakaogharimu shilingi bilioni 1.8 na kuwanufaisha wananchi wa Kata ya Nyashimo.
   Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera akitoa neno la shukrani wakati wa  kusaini mkataba wa ujenzi wa mradi wa maji wa Nyashimo wilayani Busega kati ya MWAUWASA na Mkandarasi Kampuni ya Bennet Contractors kutoka Jijini Mwanza, mradi utakaogharimu shilingi bilioni 1.8 na kuwanufaisha wananchi wa Kata ya Nyashimo.
   Mbunge wa Busega, Dkt. Raphael  Chegeni akizungumza na wananchi wa Kata ya Nyashimo wakati wa kusaini mkataba wa ujenzi wa mradi wa maji wa Nyashimo wilayani Busega kati ya MWAUWASA na Mkandarasi Kampuni ya Bennet Contractors kutoka Jijini Mwanza, mradi utakaogharimu shilingi bilioni 1.8 na kuwanufaisha wananchi wa Kata ya Nyashimo.
   Mwananchi kutoka kata ya Nyashimo akifurahia jambo na Diwani wa Kata hiyo Mhe. Mickness Mahela wakati wa  zoezi la  kusaini mkataba wa ujenzi wa mradi wa maji wa Nyashimo wilayani Busega kati ya MWAUWASA na Mkandarasi Kampuni ya Bennet Contractors kutoka Jijini Mwanza, mradi utakaogharimu shilingi bilioni 1.8 na kuwanufaisha wananchi wa Kata ya Nyashimo.
  Baadhi ya Viongozi wa Serikali na Wajumbe wa Bodi ya MWAUWASA wakifuatilia mambo mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea kabla ya zoezi la kusaini mkataba wa ujenzi wa mradi wa maji wa Nyashimo wilayani Busega kati ya MWAUWASA na Mkandarasi Kampuni ya Bennet Contractors kutoka Jijini Mwanza, mradi utakaogharimu shilingi bilioni 1.8 na kuwanufaisha wananchi wa Kata ya Nyashimo.

  MWAUWASA, BENNET CONTRACTORS WASAINI MKATABA UJENZI WA MRADI WA MAJI WA BILIONI 1.8 BUSEGA
  Na Stella Kalinga, Simiyu
  Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Mwanza (MWAUWASA), Mhandisi. Anthony Sanga  na Mkurugenzi wa Kampuni ya  Bennet Contractors Sabato Boaz kutoka Mwanza, wamesaini mkataba wa ujenzi wa mradi wa Maji wa Nyashimo wilayani Busega utakaogharimu zaidi ya shilingi bilioni 1.8.

  Mkataba wa Mradi huo utakaonufaisha vijiji vya Bukabile, Mwagulanja na Bulima na kuhudumia wananchi 20,030 , umesainiwa Nyashimo wilayani Busega na kushuhudiwa na wananchi, viongozi wa Chama na Serikali wa Wilaya ya Busega na Mkoa wa Simiyu, wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka.

  Akizungumza na wananchi na viongozi waliofika kushuhudia zoezi hilo Mtaka amemtaka Mkandarasi Kampuni ya  Bennet Contractors kuzingatia muda na viwango katika utekelezaji wa mradi huo, huku akisisitiza kuhakikisha mradi huo unawanufaisha wananchi wanaozunguka eneo la mradi kwa kutoa ajira za muda na ununuzi wa vifaa vya ujenzi.

  “Mkataba unaonesha mradi huu ni wa miezi 15, nikuombe mkandarasi miezi 15ni mingi tungehitaji tunapoanza maandalizi ya kutengeneza ilani ya CCM mwaka 2020 tuzungumzie utekelezaji wa ilani siyo mpango; tunahitaji jamii yetu inufaike kupitia mradi huu, vijana wapate ajira, mama ntilie wapike chakula na baadhi ya vifaa vya ujenzi vinunuliwe kwenye maduka ya hapa” alisema Mtaka.

  Ameongeza kuwa Serikali imetoa zaidi ya shilingi bilioni 16.4  kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maji wilayani Busega, ikiwa ni pamoja na Mradi wa Lamadi, Kiloleli, Mwamanyili na ukarabati wa visima maeneo mbalimbali, ambayo itakapokamilika  itaongeza hali ya upatikanaji wa maji safi na salama Busega kutoka asilimia 39 ya sasa na kufikia asilimia 74.

  Naye Mbunge wa Busega, Dkt. Raphael Chegeni amesema pamoja na mradi wa Nyashimo Serikali inatekeleza miradi mingine ya maji wilayani Busega ukiwepo wa Kiloleri Mradi wa Lamadi, hivyo akasisitiza wananchi kulinda na kutunza miradi hiyo ili iwanufaishe.

  Nao wananchi wamesema“Tunashukuru kuletewa huu mradi tulikuwa tunapata adha ya maji tulikuwa tunanunua kwenye madumu na kufua ziwani, lakini endapo mradi huu uliosainiwa mkataba leo ukikamilika itakuwa ni neema kwetu hasa sisi wakina mama ambao ndiyo tunapata tabu zaidi na familia zetu” Sara Nanyori mkazi wa kijiji cha Bulima.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Mwanza (MWAUWASA), Mhandisi. Anthony Sanga  amesema mradi wa Nyashimo ni utekelezaji wa ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli aliyoitoa kwa wananchi na unafadhiliwa kwa asilimia 100 na fedha za Serikali ya Tanzania.
  Mkurugenzi wa Kampuni ya  Bennet Contractors(Mkandarasi) Sabato Boaz kutoka Mwanza, amesema pamoja na kwamba mkataba unaonesha utekelezaji ni miezi 15, kampuni yake inatarajia kutekeleza kwa ubora na kwa muda mfupi kadri itakavyowezekana ili kuleta  huduma ya maji safi na salama haraka kwa wananchi wa Nyashimo.

  0 0

  Ahadi ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa wakazi wa Kata ya Nyampande, Wilaya Sengerema mkoani Mwanza ya kuwaondolea adha ya upatikanaji wa maji imeanza kutekelezwa, baada ya Serikali kusaini mkataba na mkandarasi ili kutandaza mtandao wa maji ya bomba katika Kata hiyo.


  Mkataba huo wa zaidi ya shilingi bilioni moja umesainiwa Mei 09, 2019 baina ya Serikali kupitia Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira mkoani Mwanza (MWAUWASA) pamoja na mkandarasi kampuni ya HALEM ya jijini Dar es salaam mbele ya Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella.

  Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
  Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira mkoani Mwanza (MWAUWASA), Mhandisi Antony Sanga (kulia) pamoja na Mkurugenzi wa kampuni ya HALEM Construction ya jijini Dar es salaam, Mhandisi Happy Lebe (kushoto), wakisaini mkataba wa utekelezaji mradi wa maji Nyampande wilayani Sengerema. Aliyesimama upande wa kulia ni Mwanasheria wa MWAUWASA, Oscar Twakazi na kushoto ni Meneja Vifaa kampuni ya HALEM, Steven Malima.
  Mkurugenzi wa MWAUWASA, Mhandisi Antony Sanga (kulia) pamoja na Mkurugenzi wa kampuni ya HALEM, Mhandisi Happy Lebe wakikabidhiana mkataba wa utekelezaji wa mradi wa maji Nyampande wilayani Sengerema baada ya pande zote mbili kuusaini.
  Tazama Vidio hapa chini

  0 0

   Afisa Huduma kwa wateja kutoka Kampuni ya Tigo Regani Emmanuel, akimsajili Mbunge wa jimbo la Chwaka, Bhagwanji Meisuria (kulia), kupitia utaratibu mpya wa  usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole katika viwanja vya bunge mjini Dodoma mwishoni mwa wiki. 
   Afisa anayehusika na usajili wa laini za simu kutoka kampuni ya Tigo Tanzania, Atupiani Makweta, akimsajilia mbunge Tunduma Frank Mwakajoka kwa kutumia mfumo mpya wa usajili kwa kutumia alama za vidole mwishoni katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma.

   Afisa anayehusika na usajili wa laini za simu kutoka kampuni ya Tigo Tanzania, Atupiani Makweta, akimsajilia mbunge Tunduma Frank Mwakajoka kwa kutumia mfumo mpya wa usajili kwa kutumia alama za vidole mwishoni katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma.
  0 0


  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii.

  Mweyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa ,Jenerali (Mstaafu) George Waitara amezindua mfumo mpya wa utendaji kazi ndani ya Hifadhi za Taifa unaopeleka madaraka zaidi katika ngazi ya Kanda nne kuu zilizoundwa ili kuboresha utendaji kazi unaoendana na mfumo mpya wa jeshi -usu.

  Uzinduzi huo ulienda sambamba na zoezi la utoaji vyeo vipya vilivyoidhinishwa na bodi ya wadhamini kwa viongozi wa shirika ambao ni Naibu Kamishna wa Uhifadhi wawili,Makamishna wa Uhifadhi wa kanda wanne,Makamishna Wasaidizi Waandamizi 14,Makamishna wasaidizi 22 pamoja na Maafisa Wakuu na Waandamizi saba.

  Muundo mpya unahusisha Kanda ya Kaskazini yenye Hifadhi za Arusha,Tarangire ,Ziwa Manyara,Kilimanjaro na Mkomazi ,Kanda ya mashariki inayojumuisha Hifadhi za Saadan,Mikumi na Udzungwa ,Hifadhi za Ruaha na Kitulo na Katavi zitakuwa chini ya usimamizi wa  kanda ya Kusini ,

  Kanda ya Magharibi itasimamia Hifadhi za Taifa za Gombe,Mahale ,kisiwa cha Saanane ,Kisiwa cha Rubondo ,Serengeti pamoja na Hifadhi mpya za Burigi,Kimisi,Biharamulo,Ibanda na Rumanyika.

  Hafla hiyo pia imeendana na zoezi la kuwatunuku vyeti wahitimu 217 wa mafunzo yaliyochukua miezi sita kwa awamu mbili yakihusisha Maafisa wa Uhifadhi pamoja na waajiriwa wapya.

  Lengo kuu la mafunzo hayo ni kuwawezesha wahitimu kufanya kazi  kwa mfumo wa kijeshi -usu katika kuboresha utendaji kazi na majukumu ya usimamizi thabiti wa maliasili zilizopo hifadhini kwa kuwajengea wahitimu uwezo wa kimwili ,kisaikolojia,kimaadili na uzalendo

  0 0

  Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo akifungua kikao cha Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa cha kupitia rasimu ya Sera ya Taifa ya Ugatuaji wa Madaraka kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa St. Gasper Jijini Dodoma.
  Katibu Mkuu OR-TAMISEMI Mhandisi Joseph Nyamhanga akitoa taarifa ya utangulizi kwenye ufunguzi wa kikao cha Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa cha kupitia rasimu ya Sera ya Taifa ya ugatuaji wa madaraka kilichofanyika katika ukumbi wa St. Gasper Jijini Dodoma.
  Baadhi wa Wakuu wa Mikoa wakimsikiliza Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI Mhe. Seleman Jafo wakati akifungua kikao cha kupitia rasimu ya Sera ya Taifa ya Ugatuaji wa Madaraka kilichofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa St. Gasper Jijini Dodoma.
  Baadhi wa Makatibu Tawala wa Mikoa wakimsikiliza Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI Mhe. Seleman Jafo wakati akifungua kikao cha kupitia rasimu ya Sera ya Taifa ya Ugatuaji wa Madaraka kilichofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa St. Gasper Jijini Dodoma.

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo (watatu kutoka kushoto aliyekaa) akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Mikoa mara baada ya kufungua Kikao cha kupitia Sera ya Taifa ya Ugatuaji wa Madaraka kilichofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa St. Gasper Jijini Dodoma.


  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo (watatu kutoka kushoto aliyekaa) akiwa katika picha ya pamoja na Makatibu Tawala mara baada ya kufungua Kikao cha kupitia Sera ya Taifa ya Ugatuaji wa Madaraka kilichofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa St. Gasper Jijini Dodoma.

  ……………………………………………………………………………………………………..

  Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI

  Kutokuwepo kwa Sera ya Ugatuaji Madaraka iliyojengwa kwenye mfumo wa Sheria ni moja ya changamoto iliyofanya Serikali kufanya mapitio ya sera hiyo.

  Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Selemani Jafo(Mb) wakati wa kufungua kikoa kazi kilichokutanisha Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa kutoka Mikoa yote 26 kwa ajili ya kutoa maoni na mapendekezo kwenye Rasimu ya Sera ya Taifa ya Ugatuaji Madaraka ya 2019.

  Alisema kuwa changamoto moja wapo ni kutokuwepo kwa sera ya ugatuaji iliyojengwa kwenye mfumo wa kisheria inayoelekeza mipaka, majukumu na utaratibu wa utekelezaji wake, jambo ambalo linafanya ionekane kama ni hiari na utashi (Voluntary and Willingness).Jafo alisema changamoto nyingine ni kuwepo kwa mitazamo inayokinzana kati ya watendaji na viongozi wa kisiasa katika ngazi ya vijiji, kata na halmashauri katika kuweka vipaumbele na kutekeleza miradi ya maendeleo

  Aliongeza kuwa Mamlaka za Serikali za Mitaa zimekuwa zikitegemea fedha kwa kiasi kikubwa kutoka Serikali kuu na kutolea mfano kwa mwaka 2018 zilitegemea zaidi ya asilimia 88 ya mapato.“ Wizara za Kisekta kuandaa sera na sheria na kupeleka halmashauri kwa ajili ya utekelezaji bila kuambatanisha rasilimali fedha, vifaa na watu.”

  Waziri Jafo alibainisha kuwa uelewa mdogo wa dhana ya Ugatuaji wa Madaraka (D by D) kwa baadhi ya Wizara za Kisekta na hivyo Sera hii kuonekana kama ni suala ya OR-TAMISEMI kwa kiasi kikubwa imechangia kufanya Sera hii kutotekelezeka kwa kiwango kilichotegemewa.Jafo aliongeza: “Kwa ujumla hatujafikia kiwango cha mafanikio kilichotarajiwa kutokana na changamoto mbalimbali zilizojitokeaza na ndio maana Serikali imeamua kufanya mapitio ya Sera ya Taifa ya Ugatuaji ili kupata suluhisho la changamoto zilizojitokea.

  Aidha, Jafo amewataka wakuu wa mikoa na makatibu tawala kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika kutoa maoni na mapendekezo hayo ili kuboresha rasimu hiyo kwa maslahi mapana ya wananchi, wadau na taifa kwa ujumla.

  Aidha Mhe. Jafo alitumia fursa hiyo kuwahimiza wakuu wa mikoa na makatibu tawala wa mikoa kuhakikisha wanasimamia kwa ukabilifu fedha na utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwamo ujenzi wa vituo vya afya, ujenzi wa hospitali za wilata, ujenzi wa mabweni, madarasa, vyoo katika shule za msingi na sekondari ambayo tayari fedha zake zimeshatolewa na serikali.

  Naye Mwenyekiti wa wakuu wa mkoa ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Eng. Evarist Ndikilo aliahidi kushiriki mzuri wa wawakuu hao kwa kuwa wao ndio wanaotoka kwa wananchi.Pia alimhakikishia Waziri Jafo kuwa watasimamia kwa umakini utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuwa itakamilika katika muda uliopangwa na kwa ubora unaotakiwa.

  Naye Mwakilishi wa UNICEF, Pius Chaya alisema agenda ya mapitio ya Sera ya Taifa ya Ugatuaji Madaraka imekuja wakati muafaka, kwasababu Serikali inatakiwa kuhakikisha kwamba wananchi wanapata huduma wanazostahili na ambazo zinawafikia kwa wakati.

  Aidha, Chaya alisema wadau wa maendeo ambao pia wameshiriki katika machakto wa mapitio ya sera hiyo wameahidi kuendelea kushirikiana na serikali ya awamu ya tano katika kuwaletea wananchi wake maendeleo

  Sera ya Ugatuaji wa Madaraka ni dhana ya Kupeleka Madaraka, Majukumu na Rasilimali kutoka Serikali Kuu kwenda kwa Wananchi kupitia vyombo vya kidemokrasia na Kisiasa ambavyo, wajumbe wake huchaguliwa na kuwajibika kwa Wananchi na vimepewa Mamlaka ya kutoa Maamuzi na kusimamia rasilimali (yaani vina uhuru, vinajitawala, na vina hadhi ya kisheria).


  Sera hii ilianza kutekelezwa mwaka 1998 kupitia mpango wa maboresho ya Serikali za Mitaa ikiwa na lengo la kuwawezesha wananchi kushiriki shughuli za Maendeleo katika maeneo yao na kuongeza ufanisi katika uendeshaji wa shughuli za Serikali.

  0 0


  Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Dkt. Athumani Kihamia akizungumza an wafanyakazi wa NEC (hawapo pichani).
  Mkurugenzi wa Utawala na Menejimenti ya Rasilimali Watu wa NEC, Gerald Mwanilwa akifafanua jambo.
  Baadhi ya wafanyakazi wa NEC wakimsikiliza Dkt. Kihamia
  Baadhi ya wafanyakazi wa NEC wakimsikiliza Dkt. Kihamia
  Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Dkt. Athumani Kihamia (wa mbele katikati) akizungumza na wafanyakazi wa NEC


  kurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Dkt. Athumani Kihamia ameeleza kuridhishwa na utendaji kazi wa watumishi wa tume hiyo kutokana na kufanya kazi kwa bidii, ushirikiano, weledi na uzalendo.

  Dkt. Kihamia ameeleza hayo wakati alipokutana na wafanyakazi wa NEC kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kujadili mambo mbalimbali yanayohusu utekelezaji wa majukumu ya Tume.

  Alisema katika kipindi alichokaa Tume amegundua kuwa sasa utendaji kazi wa mazeoa umepungua na watumishi wengi wamekuwa wakitekeleza majukumu yao kwa wakati, kwa uaminifu, kutunza siri na kuepuka matumizi ya fedha yasiyo ya lazima.

  Mkurugenzi huyo wa NEC alifafanua kuwa katika kikao chake cha kwanza na watumishi wa Tume cha Agosti 7 mwaka 2018, alijadili changamoto zinazowakabili watumishi hao ambazo zilikuwa kikwazo cha utekelezaji wa majukumu yao kwa njia moja au nyingine.

  “Tuligundua kuwa changamoto nyingi zilitokana na tabia binafsi za baadhi ya watumishi, na baadhi yao kufanya kazi kwa kuigiza yaani kwa mazoea kwa kisingizio cha mchakato”, alisema Dkt. Kihamia na kufafanua kuwa:

  “Lakini sasa hivi jambo la kufurahisha asilimia kubwa ya watumishi wanafanya kazi sio kwa mazoea, lakini pia ufanisi wa kazi zao umeongezeka kwa kiwango kikubwa”.

  Alibainisha kuwa kwa sasa Tume imeimarika vya kutosha kwa kuwa wakati alipofika wastani wa utendaji kazi ulikuwa asilimia 52, ikimaanisha kuwa zaidi ya asilimia 48 ya watumishi walikuwa hawawajibiki ipasavyo, lakini sasa uwajibikaji umefikia wastani wa asilimia 65 baada ya kuwekeana malengo.

  “Kwa hiyo tulipo sasa tupo juu ila ni lazima tuendelee kuwa kitu kimoja, ingawa katika kuimarika huko wapo wenzetu wachache sana wenye matatizo madogo madogo, hivyo wanatakiwa warekebishwe” alisisitiza Dkt. Kihamia

  Alifafanua kuwa kuimarika kwa utendaji kazi ni jambo kubwa kwa maendeleo ya nchi kwa kuwa kutowajibika ipasavyo kwa watumishi wa umma katika nchi nyingi za Afrika kumesababisha udumavu wa maendeleo ya nchi hizo.

  Hivyo aliwataka watumishi wa NEC kuendeleza tabia ya uwajibikaji kwa mustakbali wa maendeleo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Tanzania kwa ujumla kwa kuacha kufanya kazi kwa mazoea ili kuwa chachu ya maendeleo ya nchi.Ili kuboresha zaidi utendaji kazi wa Tume, Dkt. Kihamia aliziagiza kila idara ziainishe vipaumbele (priorities) vitakavyotekelezwa na idara husika kwa kipindi chote kuanzia Julai 1 mwaka huu.

  Alisema baada ya kupata vipaumbele hivyo kutoka kila idara vitaunganishwa kupata vipaumbele vya Tume na aliwataka watumishi kutambua kuwa majukumu ya kila idara ni majukumu ya Tume hivyo ni muhimu kuwa kitu kimoja katika kuyatekeleza.

  “‘Checklist’ ni jambo kubwa sana kwa sababu kuna mtu ukienda kwenye idara yake ukimuuliza amefanya mambo gani, anaweza akawa amefanya mambo mazuri tu lakini hayakumbuki mpaka ayafikirie ndio akwambie” alisema Dkt. Kihamia na kufafanua kuwa:

  Alisema checklist ni mpango kazi ambao hata watafiti wanaofanya tafiti za kisasa wamegundua kwamba kampuni nyingi za kibiashara zinazofilisika ni zile ambazo hazina checklist za kisasa.Kwa hiyo checklist ni moja ya agenda ambayo nimekuja kuizungumzia leo kwa sababu tunafanya kazi kwa mipangokazi na unapokuwa na checklist unajua hili nimelifanya hili sijafanya” alisema Dkt. Kihamia.

  Alisema mtumishi asipokuwa na checklist ya kazi zake hawezi kuwa na muendelezo (consistency) mzuri wa majukumu ambayo mtumishi anataka kuyatekeleza na ukamilifu wa kazi zake hautakuwepo.Alisema wataalamu wanasema kwamba checklist ndio njia pekee kwa sasa inayoaminika katika kutekeleza majukumu kwa ufasaha.

  “Mtafiti mmoja aliwahi kusema checklist ni aina ya mpangilio wa majukumu ambao unapunguza kushindwa (failure)katika kazi, ina maana usipokuwa na checklist uwezekano wa kushindwa ni mkubwa” aliongeza Dkt. Kihamia.

  Kwa upande mwingine Dkt. Kihamia alimtaka kila mtumishi wa Tume atambue majukumu ya msingi ya NEC na ikiwemo kufahamu Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ni nini na kufahamu taratibu zote za uchaguzi.

  “Watu wajifunze kuwepo kwa nafasi wazi ni nini maana watu wanalalamika kwamba Serikali inatumia fedha nyingi kufanya chaguzi ndogo za mara kwa mara lakini wanasahau kwamba suala hilo lipo kwenye katiba na ni utarabu.” alisema Dkt. Kihamia.

  Dkt. Kihamia tangu alipoteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi amejiwekea utaratibu wa kukutana na watumishi wa tume hiyo huku hiki kikiwa ni kikao chake cha tatu.

  Katika kikao cha kwanza cha tarehe 7 Agosti mwaka 2018, Dkt. Kihamia aliainisha vipaumbele vyake 30 vya kuzingatia katika utekelezaji wa majukumu ya Tume na kuvifanyia tathmini kwenye kikao cha pili kilichofanyika mwezi Desemba mwaka 2018.

  Baadhi ya vipaumbele alivyosisitiza ni kuweka mpango kazi wa kila idara, kitengo na mtumishi na utekelezaji wake kwa kile mwezi, kuandaa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya kila idara, kutambua madeni ya kila idara na kitengo na kuonesha kama yamehakikiwa au la, sababu ya madeni hayo na kuwepo rejesta na mpango kazi wa malipo.

  Katika vikao hivyo wakuu wa Idara wamepewana nafasi ya kufafanua mambo mbalimbali katika idara zao na watumishi kuwepo nafasi ya kueleza mambo mbalimbali kuhusu utekelezaji wa majukumu yao.

  0 0

  Na. Peter Haule na Josephine Majura, WFM, Dodoma
  Serikali ya Tanzania inafanya mazungumzo na Serikali ya Cyprus ili kuweza kutatua changamoto za malipo kwa wateja walioweka amana zao katika Benki ya FBME ambayo ilifutiwa leseni ya kufanya shughuli za kibenki hapa nchini na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
  Hayo yameelezwa Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) alipokuwa akijibu swali la Msingi la Mbunge wa Viti maalaum  Mhe. Asha Abdullah Juma, alieuliza kuhusu hatua zilizochukuliwa na Serikali kuwasaidia wananchi walioweka amana zao katika Benki ya FBME.
  Dkt. Kijaji alisema kuwa zoezi la kukusanya mali na fedha zilizokuwa za Benki ya FBME katika taasisi mbalimbali za fedha hasa zilizopo nje ya nchi, limekumbwa na changamoto za kisheria kati ya Tanzania na Cyprus ambako benki ya FBME ilikuwa ikiendesha sehemu kubwa ya biashara zake hivyo kusababisha ucheleweshaji wa ukusanyaji na ugawaji wa fedha na ufilisi.
  “Hakuna tarehe rasmi ya kuanza kulipa fedha kwa sasa kutokana na uwepo wa kesi zinazokwamisha zoezi la ukusanyaji mali na madeni ya Benki ya FBME”, alieleza Dkt. Kijaji.
  Alisema kuwa, Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006 inaeleza kuwa amana au akiba za wateja katika Benki au Taasisi zina kinga ya Bima ya Amana ya kiasi kisichozidi Sh. milioni 1.5,  na iwapo mteja ana salio la amana la kiasi kisichozidi Sh. 1.5 atapata fidia ya asilimia 100.
  Aidha wateja walio na zaidi ya Sh. milioni 1.5 wanalipwa Sh. milioni 1.5 kama fidia ya bima ya amana na kiasi kinachobakia kinalipwa kwa mujibu wa Sheria na taratibu za Ufilisi.
  Hata hivyo malipo kwa mujibu wa Sheria na taratibu za ufilisi yanategemea makusanyo ya fedha kutoka kwenye mauzo ya mali pamoja na fedha zilizowekwa na benki katika taasisi mbalimbali za fedha za ndani na nje ya nchi.

   Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb).

  0 0
 • 05/13/19--05:59: International Mother's Day
 • Mothers across the country have been encouraged to endlessly pursue their careers without giving up while taking care of their families.

  Speaking during a mother’s day forum on Friday in Dar es Salaam organised by NMB to commemorate Mother’s day (celebrated internationally today) Head, Customer Experience at NMB Ms Abella Tarimo said that for people to achieve anything in life they need clarity on what they what to achieve, how to achieve and lastly a way to measure success.

  “As long as one has a clear vision and support system juggling between a career & family is manageable. Most women believe caring for a family and establishing a career at the same time is an impossible task for a mother to achieve,” she said.

  Themed ‘Glass Ceiling and Motherhood’, Ms Tarimo stressed that no one can accomplish things alone. “Working mothers should establish support systems no matter what they want to accomplish at home or work.”

  She pointed out that, “Mothers need to be there for their children, especially those who are still breastfeeding. It does cause challenge to careers but this is where as mothers we need to use our resourcefulness to be able to balance home and work, and this is where the support system comes in.”

  She explained that the support system can be members of the family, husband, maids; people that will be a helping hand for a mother or any person who has focused in achieving a targeted goal. “A mother just needs to realize the type of support system she needs.”

  On the other hand, Senior Relationship Manager; Business Liability, Business Banking Ms Beatrice Mwambije said that working mothers who are overwhelmed and think of quitting their career to take care of their children need to evaluate the situation first before doing so.

  The rigorous daily schedule of caring for an infant may tempt mothers to stay at home and care for their children. However, if you are a career person, there are ways you can strike a balance and achieve both successfully. Establish plans on how you can balance both career and family,” she commented.

  Adding that, “Mothers should think of the future in terms of financial security and their relevance as human beings after the children are grown up. Plan the future while putting all into consideration like sudden death or illness of a partner before deciding that quitting your job is the best option.” 
   Pauline Mohele, (center) NMB’s Manager Recovery, Special Asset Management, speaking during a panel discussion organised by NMB Bank Plc to commemorate World’s Mother’s Day themed ‘Glass Ceiling and Motherhood’. Right is Beatrice Mwambije, Senior Relationship Manager; Business Liability, Business Banking and NMB’s Head, Customer Experience, Abella Tarimo (left).
  Lillian Mwinula, (1ST right) NMB’s Senior Manager Special Projects, speaking during a panel discussion organized by NMB Bank Plc to commemorate World’s Mother’s Day themed ‘Glass Ceiling and Motherhood’. Left is NMB’s Head, Customer Experience, Abella Tarimo, Pauline Mohele, (centre ) NMB’s Manager Recovery, Special Asset Management and Right is Beatrice Mwambije, Senior Relationship Manager; Business Liability, Business Banking.  0 0

  Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NMB, mkoani Mwanza wakitoa msaada kwenye Kituo cha Afya cha Buzuruga wodi ya Mama na Watoto-Mwanza ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mama Duniani.


  WANAWAKE nchini wameshauriwa kutokata tamaa kufanyia kazi taaluma walizonazo huku wakizihudumia familia zao kwa mujibu wa majukumu yao nyumbani.

  Ushauri huo umetolewa jana jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Idara ya Huduma kwa Wateja wa Benki ya NMB, Abella Tarimo katika mjadaLa ulioandaliwa na benki hiyo kuadhimisha Siku ya Mama Duniani (Mother's Day).

  Alisema ili wanawake waweze kufanikiwa katika jambo lolote juhudi na uwazi juu ya suala wanalolifanya zinahitajika."Ili mradi mtu uwe na nia na unaungwa mkono huku ukiweka jitihada za dhati bila kusahau familia yako, utafanikiwa. Wapo baadhi ya wanawake ambao wamekuwa wakijikwamisha kwa kudhani kuwa hawawezi kufanyia kazi ujuzi waliousomea na kufanikiwa huku wakizihudumia familia zao ipasavyo, jambo ambalo si sawa," alisema Bi. Tarimo.

  Alisema kwa kuanzia mafanikio wanawake wafanyakazi hawana budi kujenga utamaduni wa kushirikiana pamoja na kuungana mkono bila kuathiri majukumu yao kifamilia.

  Kwa upande wake Meneja Uhusiano Mwandamizi, Amana na Biashara wa NMB, Beatrice Mwambije akichangia mada katika mjadala huo, aliwataka akina mama ambao wako kazini na wamekata tamaa na hata kufikiria kuacha kazi ili wakalee familia zao kutathmini mara mbilimbili kabla ya kufanya maamuzi yao."Ni kweli ukiangalia majukumu ya mama mwenye mtoto mchanga anaweza kubanwa akashindwa kutekeleza kazi zake ofisini...lakini hiki kisiwe kikwazo kuna namna unaweza kujipanga na kukabiliana na yote hayo na ukaendelea na kazi pasipo kuathiri pande zote," alisema Bi. Mwambije.

  Aidha aliwataka akinamama kuangalia usalama wa familia na watoto kwa maisha ya baadaye wanapokuwa wakubwa hivyo kuna kila sababu ya kuwajengea msingi imara.Mjadala huo ulioandaliwa na Benki ya NMB ulienda sambamba na maadhimisho ya 'Siku ya Mama Duniani’ huku ukisisitiza kutambuliwa kwa majukumu ya kinamama duniani kote kwani wanamchango mkubwa kimaendeleo.

  Benki ya NMB imeadhimisha siku hii kwa kualika wadau mbalimbali kujadili mada ya mama katika matawi yake yote nchi nzima pamoja na baadhi yao kutoa misaada kwa watoto na akina mama.
  Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NMB matawi mbalimbali, wakiwa katika picha za kumbukumbu mara baada ya maadhimisho ya Siku ya Mama Duniani. 
  Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NMB matawi mbalimbali, wakiwa katika picha za kumbukumbu mara baada ya maadhimisho ya Siku ya Mama Duniani. 
  Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NMB matawi mbalimbali, wakiwa katika picha za kumbukumbu mara baada ya maadhimisho ya Siku ya Mama Duniani. 

  0 0  KUKAMATWA KWA WATUHUMIWA WANNE WA TUKIO LA MAUAJI.


  Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watu wanne waliofahamika kwa majina ya:-

  1.      JAPHET YAHAYA NGUKU[37]Mkazi wa Msewe – Igurusi Wilaya ya Mbarali

  2.      AGATHA FRANCIS [30] Mkazi wa Mbalizi.

        3.ANDREW ANGANILE MWAMBULUMA [43] Mkazi wa Mapinduzi - Mbalizi

        4. MEJA JOTAM SANGA @ MESIA [48] Mkazi wa Ikonda Mkoa wa Njombekwa tuhuma za mauaji ya mtoto wa miaka sita [06] aitwaye ROSE JAPHET Mkazi wa Kijiji cha Msewe, Wilayani Mbarali.


  Ni kwamba mnamo tarehe 03.05.2019 majira ya saa 21:00 usiku huko Kijiji cha Msewe kilichopo Kata ya Igurusi, Tarafa ya Ilongo, Wilaya ya Mbarali, Mkoa wa Mbeya katika msitu wa hifadhi wa Chimala Mtoto aitwaye ROSE JAPHET [06] alikutwa ameuawa kwa kunyongwa shingo na kukatwa kanyagio la mguu wa kushoto pamoja na kiganja cha mkono wa kushoto ambapo kanyagio la marehemu limekutwa limefukiwa huko Mbalizi, Wilaya ya Mbeya Vijijini.


  Chanzo cha tukio hili ni tamaa ya kupata utajiri ambapo baba mzazi wa marehemu aitwaye JAPHET YAHAYA NGUKU alimtoa mwanae kwa ANDREW ANGANILE MWAMBULUMA ambaye ni mfanyabiashara kwa malipo ya Tshs5,000,000/= ili auwawe na kisha kukatwa kanyagio la mguu wa kushoto na kiganja cha mkono wa kushoto na kupatiwa mfanyabiashara huyo ili apeleke kwa mganga aitwaye MEJA JOTAM SANGA @ MESIA [48] ili amtengenezee ndagu (dawa ya utajiri) ili afanikiwe katika  biashara zake za Shule anayoimiliki iitwayo Shule ya Sekondari Ushindi iliyopo Mbalizi.

   

   

  KUPATIKANA NA MALI YA WIZI GARI.

  Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watu wawili waliofahamika kwa majina ya:-

  1.      ABRAHAM NSAJIGWA [37] Mkazi wa Forest

  2.      FESTO ZAKARIA [35] Mkazi wa Ilemi

  Kwa tuhuma ya kupatikana mali ya wizi gari lenye namba ya usajili T.899 DCW aina ya Noah rangi nyeusi.

  Watuhumiwa wamekamatwa mnamo tarehe 12.05.2019saa 02:00 usiku huko maeneo ya Isanga, Kata ya Isanga, Tarafa ya Sisimba, Jijini Mbeya. Gari hiyo iliibwa huko Temeke Mkoani Dar es Salaam ambapo baada ya tukio hilo, taarifa zililifikia Jeshi la Polisi na kuanza msako na jana kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa wakiwa na gari hilo.


  TAARIFA YA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA KATIKA MAENEO MBALIMBALI YA MKOA WA MBEYA.


  Kutokana na mvua zilizoanza kunyesha tangu tarehe 29/04/2019 hadi sasa Mkoani Mbeya zimesababisha uharibifu wa nyumba na mali yakiwemo mazao mbalimbali hasa katika Wilaya ya Rungwe na Kyela.


  Katika Wilaya ya Rungwe huko Mtaa wa Igamba, Kata ya Bulyaga, Tarafa ya Tukuyu Mjini mvua iliyonyesha usiku wa tarehe 12.05.2019 zimesababisha hatari ya kuweza kuleta majanga ikiwemo kubomoka kwa nyumba za wakazi wa maeneo hayo.


  Katika Wilaya ya Kyela mvua hizo zimesababisha uharibifu wa makazi ya watu na majengo hasa Shule ya Msingi Mwaya iliyopo Kata ya Mwaya kwani imezingirwa na maji. Pia maeneo ya Kata ya Mwaya na Tenende mvua zinazoendelea kunyesha zimesababisha nyumba zilizopo maeneo hayo kuzingirwa na maji.


             Imetolewa na:

   [ULRICH O. MATEI – SACP]

  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.  0 0

   Waziri wa Maliasili na Utalii,Dk Hamis Kigwangallah leo  amezindua mpango wa kuwafunga mikanda ya mawasiliano ya kijiographia(GPS) Tembo ambao wanapatikana hifadhi ya jamii ya wanyamapori ya Makao na Pori la Akiba la Maswa
   Maandalizi ya kumfunga tembo GPS 

   Waziri wa Maliasili na Utalii,Dk Hamis Kigwangallah (kushoto) na Mkuu wa Mmkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka wakiangalia tembo aliyefungwa GPS. 
  Mkurugenzi wa Friedkin Conservation Fund(FCF) Nicholas Negri akizungumza kuhusu mradi huo utasaidia sana uhifadhi nchini na kuvutia watalii zaidi.

  Mwandishi wetu,Arusha.

  Zaidi ya sh 800 milioni zinatarajiwa kutumika katika zoezi la kuwafunga mikanda ya mawasiliano ya kijiographia(GPS) Tembo ambao wanapatikana hifadhi ya jamii ya wanyamapori ya Makao na Pori la Akiba la Maswa.

  Waziri wa Maliasili na Utalii,Dk Hamis Kigwangallah leo  amezindua mpango huo katika eneo la Makao WMA ambalo imewekeza kampuni ya Mwiba Holding moja ya kampuni zilizochini ya Taasisi ya Friedkin Conservation Fund(FCF)

  Waziri Kigwangala alisemaVifaa hivyo il vya GPS vitawezesha Tembo kufatiliwa mienendo yao na kudhibitiwa matukio ya Tembo kuvamia mashamba na masuala ya ujangili.

  Alisema katika mpango huo pia kutakuwa na uzio wa technolojia ya kielekronik ambao utawezesha kuonekana Tembo ambao wanatoka maeneo ya hifadhi kabla ya kufanya madhara.

  Waziri Dk Kigwangallah alipongeza taasisi ya Friedkin Conservation Fund(FCF) kwa kufadhili mradi huo na kueleza wizara yake ilifanya utafiti na kubaini taasisi hiyo ni miongoni mwa taasisi safi zinazoendekeza uhifadhi.

  Waziri Kigwangallah pia alipongeza watafiti kutoka taasisi ya utafiti wa wanyamapori(TAWIRI) kwa kuendesha zoezi hilo.

  Mkurugenzi wa Friedkin Conservation Fund(FCF) Nicholas Negri alisema mradi huo utasaidia sana uhifadhi nchini na kuvutia watalii zaidi.

  Alisema FCF itaendelea kishirikiana na serikali katika kuendeleza uhifadhi kwani pia tayari wamefadhili mradi wa kuwafunga vifaa vya mawasiliano Faru ili kuwalinda na ujangili.

  Mtafiti Mkuu wa TAWIRI, Dk Edward Kohi amesema mradi huo,unatarajia kugharimu dola 300,000 ambazo ni zaidi ya sh 800 milioni.

  Amesema katika eneo la hifadhi ya jamii ya makao na pori la akiba la Maswa Tembo 18 watafungwa vifaa vya GPS na katika maeneo mengine tayari Tembo 95 wamefungwa GPS.

  Mtafiti wa Tawiri Dk Emmanuel Masenga amesema hadi sasa Tembo 95 wamefungwa mikanda ya GPS maeneo mbali mbali ya hifadhi nchini.

  Akizungumza wakati wa zoezi hilo ,Mkuu wa mkoa wa Simiyu,Anthony Mtaka alisema mpango huo wa kuwafunga Tembo GPS utasaidia kuondoa migogoro baina ya wa hifadhi na jamii.

  Alisema wananchi wamekuwa wakipiga simu mara kadhaa kuomba msaada pale Tembo wanapovamia mashamba yao.

  "Sasa Tembo kufungwa GPS ni faraja kwetu lakini pia tunapongeza mwekezaji wetu Mwiba Holdings kwa  mradi huo" alisema

  0 0  Mhe. Prof. Kabudi akimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya AICC, Balozi mstaafu, Ladis Komba (kulia) alipokuwa akimpatia taarifa fupi kuhus bodi hiyo. Kushoto ni Mjumbe wa Bodi, Balozi Brigedia Jenerali (mst.), Francis Mndolwa na Mkurugenzi Mwendeshaji wa AICC, Bw. Elishilia Kaaya.


  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi za Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) kwa ajili ya kukutana na Bodi ya Kituo hicho ikiwa ni mkutano wake wa kwanza tangu alipoteuliwa kushika wadhifa huo mwezi Machi 2019. Mkutano huo ulifanyika jijini Arusha tarehe 13 Mei 2019 


  0 0

  Mkurugenzi mtendaji wa Songas, Nigel Whittaker akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya milioni 47 Mwenyekiti wa mtaa wa Kibangu, Bw Desidery Ishengoma katika shule ya msingi Ubungo Kisiwani mapema leo, Kampuni hiyo ya uzalishaji wa gesi nchini Tanzania imetoa msada huo kama mchango wao katika kuisaidia serikali kuboresha miundombinu ya elimu nchini.
   PIC 3&2: Mkurugenzi mtendaji wa Songas, Nigel Whittaker akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya TZS milioni 47 kwa wanafunzi wa Ubungo Kisiwani mapema leo, Kampuni hiyo ya uzalishaji wa gesi nchini Tanzania imetoa msada huo kama mchango wao katika kuisaidia serikali kuboresha miundombinu ya elimu nchini.


  0 0  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.), akila kiapo cha utii mbele ya Bunge la Afrika Mashariki (EALA) ili kuwezesha kushiriki kwenye Bunge hilo kama Waziri anayeshughulikia masuala ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki kutoka Tanzania. Tukio hilo ambalo limefanyika kwenye Makao Makuu ya Bunge la Afrika Mashariki jijiji Arusha leo, limeshuhudiwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro na Spika wa Bunge hilo, Mhe. Martin Ngoga.
  Sehemu ya Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki wakishuhudia tukio la kuapishwa kwa Mhe. Prof. Kabudi
  Mhe. Prof. Kabudi akizungumza kwenye Bunge la Afrika Mashariki mara baada ya kula kiapo cha utii cha kushiriki Bunge hilo
  Sehemu nyingine ya Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki wakifurahia hotuba ya Mhe. Prof. Kabudi ambaye haonekani pichani
  Mhe. Prof. Kabudi akizungumza kwenye Bunge la Afrika Mashariki mara baada ya kula kiapo cha utii huku Spika wa Bunge hilo, Mhe. Martin Ngoga na wabunge wengine wakimsikiliza.

  0 0

  Watalii kutoka nchini China wakipata huduma ya kubadirisha fedha za kigeni katika Benki ya NMB kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro muda mfupi baada ya watalii Zaidi ya 345 kuwasili nchini kutokea China juzi jioni. Benki ya NMB ni wadau wa ugeni huu na imedhamini mikutano yao wakiwa hapa nchini.

  Watalii kutoka nchini China wakiondoka kwenye dirisha la Benki ya NMB baada ya kubadirisha fedha za kigeni kupitia Benki hiyo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro muda mfupi baada ya watalii Zaidi ya 345 waliowasili nchini kutokea China juzi jioni. Benki ya NMB ni wadau wa ugeni huu na imedhamini mikutano yao wakiwa hapa nchini.

  Watalii kutoka nchini China wakiondoka kwenye dirisha la Benki ya NMB baada ya kubadirisha fedha za kigeni kupitia Benki hiyo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro muda mfupi baada ya watalii Zaidi ya 345 waliowasili nchini kutokea China juzi jioni. Benki ya NMB ni wadau wa ugeni huu na imedhamini mikutano yao wakiwa hapa nchini.


  KATIKA kuhakikisha hali ya uchumi inazidi kuimarika kupitia sekta ya utalii, Tanzania imepokea watalii Zaidi ya 340 kutoka nchini China ikiwa ni wiki kadhaa toka watalii zaidi ya 1000 kuwasili nchini kutoka nchini Islael.


  Watalii hao kutoka nchini China walifika juzi jioni na kupokelewa na Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano waTanzania - Majaliwa Kasim Majaliwa, Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Hamis Kingwangala, Mwenyekiti wa bodi ya Utalii Thomas Mihayo na uongozi mzima wa Benk ya NMB ambao ndio wadhamini wa ugeni huo.

  Katika hatua nyingine Waziri mkuu aliipongeza sana Kampuni ya China ya TASH-ROAD INTERNATIONAL GROUP iliyoko chini ya M/Kiti, He Lei Hiu kwa upendo wa dhati aliouonyesha wa kukubali kuingia makubaliano na nchi ya Tanzania kwa kuwaleta watalii hao zaidi ya 300 ambapo itakuwa ni mwanzo mzuri wa kuendelea kujitanua zaidi na kuutangaza utalii katika anga zote za kimataifa.

  Meneja wa NMB anayeshughulikia Dawati la China – Agness Mulolele alisema kuwa, Benki ya NMB inaunga mkono jitihada za serikali katika kuendelea na kukuza utalii nchini hivyo wameamua kusogeza huduma karibu ili kuweza kuwahudumia watalii wote katika huduma zote za kifedha.

  Kama ambavyo unatuona leo tumevalia sare zetu kuonyesha ni jinsi gani tumeamua kuja kutoa huduma zetu hapa kama sehemu ya kusaidia nchi yetu kufikia malengo makubwa ya maendeleo ikiwemo kuweka mazingira bora kwa watalii wanapotembelea nchini ili waweze kupata huduma bora za kibenki ikiwemo kubadirisha fedha za kigeni.

  “Mkoa wowote watakao enda, wilaya yoyote watakayoenda, wajue sisi tupo na tutawahudumia bila tatizo lolote kwani tunapatikana katika wilaya zote nchini huku tukiwa na matawi 229 nchini kote.” Alisema Bi Mulolele.

  “Kama unavyofaham ndani ya watalii hawa kuna wafanyabiashara, wandishi wa habari, wamiliki wa makampuni ambao watahitaji huduma zetu na ndio maana tumeamua kuwa miongoni mwa watu wanaokuja kuwapokea,” aliongeza Bi. Mulolele.

  Wageni hawa kutoka china wametokea katika majimbo mawili ambayo ni HEJIAN’G na SHAN’GAI ambao jumla walikuwa ni 345 huku ndani yao wakiwemo wandishi wa habari 40, wamiliki wa makampuni 20 na wawekezaji 50 na wengine ambao wanatokea katika bodi tofauti za utalii nchini China, watakuwa nchini kwa siku nane kisha wataondoka kwenda nchi nyingine ambapo watakuwa katika zoezi lao zima la kuzizuru nchi tatu barani Afrika.

  0 0  Bw. Costantine Clement Afisa Vipimo Wakala wa Vipimo (WMA)Mkoa wa Ilala akihakiki mizani ya kupimia vyakula katika soko la Kisutu jijini Dar es salaam leo, kulia kwake ni Meneja wa Wakala wa Vipimo (WMA) Mkoa wa Ilala Bw. Evarist Masengo.

  .............................................................................

  Meneja wa Wakala wa Vipimo (WMA) Mkoa wa Ilala Bw. Evarist Masengo na maofisa wa Wakala huo wamefanya ukaguzi wa mizani za kupimia vyakula katika soko la vyakula Kisutu leo ili kujiridhisha kama walaji wanapata huduma zinazostahili wakati wanapofanya manunuzi kwa wafanyabiashara wa soko hilo.

  Akizungumza na waandishi wa habari katika soko hilo Bw.Evarist Masengo amesema ni kawaida ya Wakala wa Vipimo (WMA) kufanya ukaguzi mara kwa mara katika masoko, vituo vya mafuta, taasisi na maeneo mbalimbali ambayo Taasisi hiyo imekuwa ikisimamia katika masuala ya vipimo kwa ujumla.

  Ameongeza kwamba Soko la Kisutu ni soko ambalo wafanyabiashara wake wamekuwa wakizingatia masuala ya vipimo kwa kiwango kikubwa hivyo kuwafanya wanunuzi au walaji wa bidhaa zao kupata huduma za manunuzi zenye ubora wa vipimo uliozingatiwa.

  Amesema mnunuzi yeyote anayenunua bidhaa lazima awe makini kuangalia mizani kama imekaguliwa kwa sababu wao wanapokagua mizani wanaweka alama ya stika ya Wakala wa Vipimo (WMA) inayoonesha mwaka na tarehe ambayo mizani huo ulikaguliwa ili kumtambulisha mnunuzi kwamba huduma anayopata kutoka kwa mfanyabiashara imekidhi viwango.

  Amewaasa wafanyabiashara kuhakikisha mizani zao zinakaguliwa na kuwekewa stika ya Wakala wa Vipimo (WMA) ili kutoa huduma iliyohakikiwa na itakayompa mlaji mahitaji yake kwa ubora.

  Maofisa wa Wakala wa Vipimo (WMA) wanafanyika ukaguzi katika maeneo mbalimbali jijini Dar es salaam na maeneo mengine ikiwa ni maandalizi ya maadhimisho ya siku ya vipimo duniani yanayotarajiwa kufanyika Mei 20/ 2019 jijini Dar es salaam.
  Meneja wa Wakala wa Vipimo (WMA) Mkoa wa Ilala Bw. Evarist Masengo (kulia) na Bw. Costantine Clement Afisa Vipimo Wakala wa Vipimo (WMA)Mkoa wa Ilala wa pili kutoka (kulia) wakihakiki mizani ya kupimia vyakula katika soko la Kisutu jijini Dar es salaam leo.
  Meneja wa Wakala wa Vipimo (WMA) Mkoa wa Ilala Bw. Evarist Masengo akifafanua jambo kwa mwandishi wa habari wa TBC Stanley Ganzel wakati akigfafanua mambo mbalimbali katika soko la vyakula la kisutu katikati ni Bw. Costantine Clement Afisa Vipimo Wakala wa Vipimo (WMA)Mkoa wa Ilala.

  Picha mbalimbali zkionyesha baadhi ya vyakula , mbogamboga na matunda vinavyopatikana katika soko la Kisutu jijini Dar es salaam.


  Bi Mary Lazaro Mfanyabiashara wa matunda katika soko la Kisutu akihojiwa na waandishi wa habari katika soko hilo.
  Afisa Vipimo Wakala wa Vipimo (WMA) Mkoa wa Ilala Bw.Malaki Nyangasi akimsikiliza Irene John Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Umma Wakala wa Vipimo (WMA) wakati alipokuwa akimueleza jambo.
  Afisa Vipimo Wakala wa Vipimo (WMA) Mkoa wa Ilala Bw.Malaki Nyangasi akihakiki mzani mkubwa katika soko la Kisutu kulia ni Meneja wa Wakala wa Vipimo (WMA) Mkoa wa Ilala Bw. Evarist Masengo
  Meneja wa Wakala wa Vipimo (WMA) Mkoa wa Ilala Bw. Evarist Masengo wa pili kutoka kulia akiwa na maafisa wenzake kulia ni Contantine Clement Afisa Vipimo (WMA) mkoa wa Ilala kutoka kushoto ni Afisa Vipimo Wakala wa Vipimo (WMA) Mkoa wa Ilala Bw.Malaki Nyangasi na Irene John Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Umma Wakala wa Vipimo (WMA)
  Afisa Vipimo Wakala wa Vipimo (WMA) Mkoa wa Ilala Bw. Malaki Nyangasi akihakiki mzani mkubwa wakati maofisa wa MAOFISA WA WAKALA WA VIPIMO (WMA) WAFANYA UKAGUZI WA MIZANI KATIKA SOKO LA KISUTU LEO Wakala wa Vipimo (WMA) walipokagua mizani katika soko la vyakula la Kisutu leo.
  Afisa Vipimo Wakala wa Vipimo (WMA) Mkoa wa Ilala Bw.Malaki Nyangasi akifafanua jambo kwa waandishi wa habari.
  Makamu Mwenyekiti wa Soko la Kisutu Bw. Laurent Magali akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ukaguzi huo uliofanywa na Wakala wa Vipimo (WMA) katika soko hilo katikati ni Afisa Vipimo Wakala wa Vipimo (WMA) Mkoa wa Ilala Bw.Malaki Nyangasi na kushoto ni Meneja wa Wakala wa Vipimo (WMA) Mkoa wa Ilala Bw. Evarist Masengo

  0 0  0 0  0 0  Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna P. Makakala (katikati) akisisitiza jambo kwa timu za Mshauri Mwelekezi na Wajenzi wa Mradi wa Ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Uhamiaji eneo la NCC, Kitalu na 18 na 19, jijini Dodoma. Walioketi, kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Meja Jenerali Martin Busungu na kushoto kwake ni Mkuu wa Timu ya washauri waelekezi wa Mradi, Dkt. Msanifu Majenzi, Isabela Mtani kutoka Chuo Kikuu cha Ardhi, Dar es Salaam wakati wa makabidhiano ya Mradi huo wa Ujenzi kati ya Idara ya Uhamiaji ambayo ni mmiliki na SUMAJKT ambayo ni Mkandarasi.
  Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna P. Makakala (katikati) na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Meja Jenerali Martin Busungu (kulia) kwa pamoja wakisikiliza maelezo ya vipengele vya utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Uhamiaji eneo la NCC, Kitalu na 18 na 19, jijini Dodoma toka kwa Mshauri Mwelekezi wa Mradi, Dkt. Msanifu Majenzi, Isabela Mtani wa Chuo Kikuu cha Ardhi , Dar es Salaam (kushoto ) wakati wa tukio la makabidhiano ya Mradi huo wa Ujenzi kati ya Idara ya Uhamiaji ambayo ni mmiliki na SUMAJKT ambayo ni Mkandarasi. Walioketi mbele, kulia ni Kamishna wa Uhamiaji (Utawala na Fedha), Kamishna Peter Chogero na kushota ni Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT, Kanali Mabele.

  …………………..

  Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna P. Makakala jana alikabidhi Mradi wa Ujenzi wa jengo la ghorofa nane ambalo litakuwa Makao Makuu mpya ya Uhamiaji eneo la NCC, Kitalu na 18 na 19, jijini Dodoma kwa wakandarasi wa SUMAJKT.

  Kamishna Jenerali alisema ” tunaijua sifa ya SUMAJKT kupitia mifano mbalimbali ya majengo bora ambayo wameyakamilisha kwa wakati, na kwa ukweli huu nina imani kubwa nao ya kwamba jengo letu litajengwa kwa ustadi wa hali ya juu na hivyo kuwa ni moja ya majengo ya kisasa yanayovutia hapa jijini Dodoma”.

  Kwa upande mwingine tukio hili lilihudhuliwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Meja Jenerali Martin Busungu na Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT, Kanali Mabele ambaye aliahidi kuwa shirika lake litajenga jengo ambalo litakuwa ni kioo cha ubora wa kazi zao na kwamba watu hawata hitaji kwenda jijini Dar es Salaam kuona mifano ya kazi zao bali hapa Dodoma tu.

  Aidha, tukio hili lilishuhudiwaa na Mkuu wa Timu ya washauri waelekezi wa Mradi, Dkt. Msanifu Majenzi, Isabela Mtani kutoka Chuo Kikuu cha Ardhi, Dar es Salaam ambaye alisema kuwa makabidhiano ya Mradi huo wa Ujenzi kati ya Idara ya Uhamiaji ambayo ni mmiliki na SUMAJKT ambayo ni Mkandarasi yatafuatiwa na shughuli nyingi ambazo zimepangwa kwenda kwa haraka sana na bila kuathili ubora wa kazi yenyewe na jengo linalojengwa.

  Mradi wa jengo hilo ambalo litakuwa kubwa kuliko lile la Kurasini, Dar es Salaam na ambalo lilikuwa Makao Makuu ya zamani linatarajiwa kukamilika ndani ya kipindi cha miezi 18, na kuiwezesha Idara ya Uhamiaji kuanza kutumia jengo bora lenye hadhi ya kimataifa jijini Dodoma.

older | 1 | .... | 1850 | 1851 | (Page 1852) | 1853 | 1854 | .... | 1898 | newer