Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1849 | 1850 | (Page 1851) | 1852 | 1853 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dk Jones Kilimbe (kushoto) akipongezwa na Mjumbe wa Kamati ya Maudhui ya TCRA, Derek Murusuri, baada ya kumalizika kwa hafla ya kuzindua Mkataba wa Huduma kwa Mteja (Client Service Charter) wa Mamlaka hiyo jijini Dodoma leo.

  Akizindua Mkataba huo, Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Eng. Isack Kamwelwe (hayuko pichani), ameipongeza Bodi na Menejimenti ya TCRA kwa kuwa mfano bora kwa taasisi nyingine za umma kuandaa Mkataba wenye lengo last kuboresha huduma.

  Waziri Kamwelwe amempongeza Mkurugenzi mkuu wa TCRA, Eng. James Kilaba (katikati) kwa ubunifu na umakini mkubwa katika kufanikisha uandaaji wa mkataba huo utakaowafanya watanzania wajivunie huduma bora na kujaliwa katika taifa lao.

  Waziri Kamwelwe amesema kuwa uboreshaji wa huduma za Mawasiliano nchini pia utasaidia kuondoa rushwa kabisa kwani katika e-government, mteja atahudumiwa pasipo kuonana na mtoa huduma uso kwa uso.

  "Ni katika kuonana uso kwa uso vitendo vya rushwa vinafanyika, katika simu ukioomba rushwa utamulikwa tu," alisema.Tanzania chini ya Rais Magufuli, inapigiwa mfano katika bara la Afrika kwenye vita dhidi ya rushwa.

  Akiongea katika hafla hiyo kubwa iliyofanyika katika ukumbi ya Jakaya Kikwete, jijini Dodoma, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe George Mkuchika, amezitaka taasisi nyingine zote za umma kuiga mfano wa TCRA na kuandaa mikataba ya wateja.

  Ameitaka Mamlaka hiyo kuutekeleza Mkataba huo ili kusaidia kuharakisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini, hasa ukizingatia unyeti wa sekta ya Mawasiliano.

  Naye Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza, mbali na kuipongeza TCRA kwa kazi nzuri ya kuwahudumia watanzania, ameishukuru Mamlaka kwa mahusiano mazuri ya kikazi baina yao.

  Hafla hiyo imehudhuriwa viongozi mbalimbali wakiwemo Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Eng. Atashasta Nditiye na Naibu mwingine katika Wizara hiyo, anayeshughulikia sekta ya Ujenzi, Eng. Elias Kuandikwa.

  Wengine ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Eng. Mary Sassabo, Naibu Katibu Mkuu katika Wizara hiyo, Dk Jim Yonazi pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.

  0 0

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.

  Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako ameupongeza uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) kwa kutenga sh. bilioni moja kwa ajili ya kuwawezesha wanataaluma kufanya tafiti zaidi hasa zinazogusa matatizo ya jamii moja kwa moja.

  Waziri Ndalichako ametoa pongezi hizo jijini Dar es Salaam wakati akifunga maadhimisho ya tano ya Wiki ya Utafiti ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo amesema tafiti ni muhimu katika kuleta maendeleo kwa kujenga na kukuza uchumi wa viwanda nchini.

  Prof. Nalochako amesema serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kujenga uchumi wa viwanda lengo likiwa kuhakikisha kunakuwa na viwanda ambavyo vinatumika kuzalisha bidhaa na kutoa huduma zitakazotosheleza jamii ya Kitanzania na kusaidia kuongeza ajira kwa vijana.

  Akizungumzia Wiki ya Utafiti Waziri Ndalichako amesema inawapa wadau wa utafiti na ubunifu jukwaa la kufahamu shughuli za utafiti zinazofanyika; sehemu gani kuna mapengo na changamoto; na mikakati gani ya kimipango inahitajika ili kuziba mapengo pamoja na kutatua changamoto zilizobainika.

  "kama taifa, tuna wajibu mkubwa na fursa nyingi za kuweza kutumia utafiti, ubunifu na ujasiriamali hususan kupitia sekta ya elimu ili kuongeza kasi ya maendeleo ya viwanda nchini. Kufanya hivyo, kutawezesha kutekeleza azma ya Serikali ya awamu ya tano ya Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Dira ya Taifa ya 2015, ya kuhakikisha kuwa Tanzania inafikia uchumi wa kati kupitia viwanda." Amesisitiza Waziri Ndalichako.

  Nae Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa William Anangisye amesema kuwa tafiti zinazofanyika zinafanya Chuo kuweza kutambulika kimataifa.

  Amesema wanataraji kutenga sh.bilioni moja kwa ajili ya kazi za utafiti ili kuweza matokeo katika maendeleo katika utengenezaji sera mbalimbali.
  Makamu Mkuu wa Chuo hicho amesema kuwa tafiti ndizo kiungo na serikali katika kusaidia wananchi kutatua changamoto mbalimbali.

   Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akipata maelezo katika maonesho ya Utafiti katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.
  Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akifunga wiki ya Tano ya Utafiti wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM) uliofanyika katika ukumbi wa Nkrumah wa Chuo hicho.
   Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam -Profesa William Anangisye akitoa maelezo kuhusiana na Wiki ya Tano ya Utafiti wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.
   

   Baadhi ya wadau katika wiki ya Tano ya Utafiti wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.

  0 0

  Mkurugenzi wa Mashtaka nchini, (DPP) Biswalo Mganga ameziasa benki zote nchini, zilizotumika kuweka sh. Bilioni 14 za kampuni ya kusimamia shughuli za upatu (DECI), kwa mtindo wa kupanda mbegu na kuvuna fedha kutozigusa fedha zozote zilizoamriwa kutaifishwa na mahakama na wakibainika kufanya hivyo hatua Kali zitachukuliwa dhidi yao ikiwemo kupelekwa mahakamani

  DPP amesema hayo leo Mei 8, 2019 alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake kufuatia amri ya Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam iliyotolewa jana na kuamuru mali zote za Deci zitaifishwe na kuwa mali ya serikali.

  Amesema, mameneja wa benki hizo wanapaswa kuwa makini na kutambua kuwa mahakama tayari imeshatoa agizo na wasiruhusu kurubuniwa kuzihamisha kwenda kwenye akaunti nyingine.

  Akieleza sababu za kutoa onyo hilo, Dpp amesema, Januari 10, mwaka huu kulikuwa na kesi inayowahusu wakurugenzi wa Kampuni ya Rifaro Afrika ambayo inajihusisha na kuchezesha upatu ambao walikiri makosa na mahakama iliwaamuru fedha zilizokuwa benki ya biashara ya Kenya (KCB) sh milioni 149 zitaifishwe na kuwa mali ya serikali.

  Amesema, hatua hiyo ilikuja baada ya mahakama kuwaachiwa kwa kulipa faini ya zaidi ya Sh milioni 204, ambapo baada ya kulipa faini hiyo, fedha zilizokuwemo kwenye account KCB, benki walihamisha Sh milioni 109 na kuziweka kwenye akaunti maalum na kuacha Sh milioni 40 pekee.

  Amesema kufuatia kitendo hicho, ameshatoa maagizo kwa Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI) kufanya uchunguzi kwa meneja wa benki hiyo ya KCB na wahakikishe kwamba fedha hizo zinarudi mapema iwezekanavyo na waende mahakamani akaeleze kwa nini fedha hizo walieza kuziamisha kutoka kwenye akaunti husika huku wakijua zilikuwa zimezuiwa kwa amri ya mahakama kwa kutaifishwa.

  Aimezitaja mali zilizotokana na DECI ambazo ni nyumba nne, viwanja vitano na magari 11 na fedha hizo zilizoko kwenye akaunti za Benki ya NMB, DCB na KCB, ambazo Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam iliamuru mali hizo zitaifishwe na kuwa za serikali.

  Aidha DPP amewaasa wananchi wanaojishughulisha na upatu kuacha mara moja kwa sababu ni kosa la jinai na kwamba watakapokamatwa watashitakiwa na watapoteza mali na fedha zao kwa sababu zitataifishwa.

  "Ninafahamu kuna watu ambao bado wanajishughulisha na upatu, niwaombe waache, tulianza na Deci 2009, ikaja Rifaro ambayo tayari fedha zao zimetaifishwa na zote huko wataendelea kupoteza fedha, ninafahamu kuna watu walijiingiza kwenye upatu katika kampuni nyingine tuko kwenye upelelezi muda ukifika tutasema, lakini yeyote anayejiingiza kwenye upatu kwa kutafuta fedha za haraka haraka atapoteza fedha sake"amesema Mganga.

  Amesema watu watafute biashara halali ya kufanya uwekezaji kuliko kujiingiza kwenye upatu. Kwani sheria inasema yeyote anayejiingiza kwenye upatu anafanya kosa la jinai na akikamatwa atashtakiwa.

  Mganga alizitaja mali ambazo zimetaifishwa kuwa ni nyumba namba UKMMD/1237 iliyoko Mwembe Madafu, Ukonga, Dar es Salaam, kiwanja namba 651, kitalu ‘M’ kilichopo Forest area, Mbeya, nyumba iliyoko kiwanja namba 7, kitalu ‘P’ ikiwa na hati namba 033004/23 kilichopo mtaa wa Rufiji, Manispaa ya Mwanza.

  Pia mali nyingine ni kiwanja namba 2/283/2 kitalu “E” Mabibo, Kinondoni, Dar es Salaam, kipande cha ardhi ambacho hakijapimwa kilichopo kijiji cha Manyinga, Turiani, Mvomero, Morogoro, kiwanja namba 467 kilichopo kitalu “H” kikiwa na hati ya usajil;i namba 48170 kilichopo eneo la Tegeta, Dar es Salaam, nyumba iliyoko kiwanja namba MM/19/P kilichopo Manzese karibu na barabara ya Morogoro, Dar es Salaam na nyumba iliyoko katika kiwanja namba KND/MXS/MNM/Z ikiwa na leseni ya makazi namba KND 008337 Kinondoni, Dar es Salaam.

  Magari yaliyotaifishwa ni Toyota Premio lenye namba T 132 AWJ, Toyota Land Cruiser namba T 480 AUP, Toyota Rav 4 namba T 274 ATQ, Toyota Mark II namba T 676 AYP, Subaru Legacy namba T 682 AUT, Toyota Ipsum namba T 850 AXY, Toyota Ipsum T455 ADM, Toyota Mark II T 186 AYX, Mitsubishi Pajero T 852 AAV, Toyota Land Cruiser T 789 AUX, Nissan Terrano namba T 899 AYU.

  Aidha, Mganga alisema fedha zilizotaifishwa na kuwa mali za serikali ni Sh 12,503,068,647.89 zilizopo NMB, tawi la Msasani, Sh 1,457,700,462.49 zilizoko benki ya Dar es Salaam Community Bank (DCB), tawi la Uhuru na Sh 57,933,304.10 zilizoko KCB, tawi la Samora, Dar es Salaam.

  Alisisitiza kuwa mahakama hiyo iliamuru magari hayo yabadilishwe umiliki na kubadilishwa matumizi kwa namna serikali itakavyopenda na kiwanja ambacho hakijapimwa kinatakiwa kusajiliwa kwa jina la Katibu Mkuu hazina.

  Pia mahakama iliagiza DPP kupeleka maombi mahakamani hapo kuomba watu wanaoishi kwenye nyumba hizo watolewe kupitia kampuni ya udalali.

  0 0

  Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
  Shirika la AGPAHI (Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative) linalojishughulisha na mapambano dhidi ya Virusi vya Ukimwi na Ukimwi nchini Tanzania, limetoa huduma ya upimaji afya bure kwa wananchi mkoani Simiyu ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani 2019 ambayo kilele chake ni Mei 05 kila mwaka.

  Huduma hiyo imetolewa katika uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi yalikofanyika maadhimisho hayo ambapo wananchi hususani akina mama walipata fursa ya kufanya uchunguzi wa Saratani ya Mlango wa Kizazi pamoja na VVU kuanzia Mei 02, 2019.

  Akitoa takwimu za awali jana kabla hatujaenda mitamboni, Mratibu wa Shirika la AGPAHI mkoani Simiyu, Dafrosa Shiluka alisema zaidi ya akina mama 200 walifanyiwa uchunguzi na kati hao, mmoja aligundulika kuwa na dalili za awali za Saratani ya Mlango wa Kizazi na kuanzishiwa huduma ya mgandisho katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Simiyu, Somanda huku wengine wawili wakipewa rufaa.

  “Lakini pia akina mama wawili walikutwa na Saratani ya Mlango wa Kizazi ambapo tuliwapa rufaa ya kwenda Bugando (Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Ziwa) kwa ajili ya matibabu zaidi” alieleza Shiluka.

  Shiluka pia aliongeza kwamba akina mama 166 walikubali kupima maambukizi ya VVU ambapo kati yao, mmoja alikundulika kuwa na maambukizi ya VVU na kuanzishiwa dawa kupitia Kituo cha Afya Muungano.

  “AGPAHI tunatoa huduma za tiba na matunzo kwa wanaoishi na maambukizi ya VVU katika Wilaya zote za Mkoa Simiyu ambapo tuna jumla ya Vituo 73 ambavyo tunavihudumia kwa ajili ya huduma hiyo na Vituo vinane kati ya 73 vinatoa huduma ya uchunguzi wa Saratani ya Mlango wa Kizazi” alisema Shiluka.

  Shiluka alitoa rai kwa wananchi hususani akina mama kuwa na desturi ya kujitokeza kupima saratani ya mlango wa kizazi kwenye Vituo vya Afya na Hospitali zinazotoa huduma hiyo tofauti na ilivyo sasa ambapo wengi hujitokeza tu kwenye makongamano mbalimbali mkoani Simiyu.

  Baadhi ya akina mama waliojitokeza kufanya uchunguzi kwenye maadhimisho hayo walitoa shukrani kwa Shirika la AGPAHI kwa kutoa huduma hiyo na kuahidi kuitumia vyema elimu waliyoipata ikiwemo kuhamasisha wenzao kwenda katika Vituo vya Afya na Hospitali kufanya uchunguzi wa Saratani ya Mlango wa Kizazi na Matiti.

  “Tumefundishwa jinsi ya kuambukizwa na jinsi ya kujikinga, ukikutwa hauna Saratani ya Mlango wa Kizazi hautakiwi uwe na wanaume wengi, tujikinge, tuwe watulivu na tupime mara kwa mara” alisema Pendo Mboje.

  Mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo yaliyoandaliwa na Chama cha Wakunga Tanzania (TAMA) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, Dkt. Faustine Ndungulile ambaye ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto aliwahamasisha wananchi kupima afya zao ikiwemo VVU na Saratani ya Mlango wa Kizazi huku akiongeza kwamba Serikali itaendelea kuboresha huduma za afya nchini ili kuwaondolea wananchi adha ya kupata matibabu.
  Mratibu wa Shirika la AGPAHI mkoani Simiyu, Dafrosa Shiluka akizungumza na BMG kwenye maadhimisho hayo.
  Pendo Mboje ambaye ni Mkazi wa Bariadi akizungumza na BMG kuhusu huduma ya upimaji iliyotolewa na Shirika la AGPAHI.
  Mkuu wa Wilaya Busega, Festo Kiswaga akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani 2019 kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Simiyu, Antony Mtaka.
  Mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile akizungumza kwenye maadhimisho hayo kwa niaba ya Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan.
  Washiriki wa Siku ya Wakunga Duniani 2019 yaliyofanyika kitaifa Bariaadi mkoani Simiyu wakiwasili uwanjani.
  Viongozi mbalimbali kwenye maadhimisho hayo akiwemo Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile (wa tatu kushoto), Mkuu wa Wilaya Busega Festo Kiswaga (wa pili kulia),  Rais wa TAMA Feddy Mwanza (wa tatu kulia), Makamu Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu (UNFPA) nchini Tanzania, Dkt. Hashina Begum (wa pili kulia) pamoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa Simiyu (wa kwanza kushoto).
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile akisikiliza ufafanuzi alipotembelea banda la Shirika la AGPAHI.
  Mratibu wa Shirika la AGPAHI mkoani Simiyu, Dafrosa Shiluka (kushoto) akitoa ufafanuzi wa huduma zinazotolewa na Shirika hilo kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile  (kulia).
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile akipokea kipeperusha chenye elimu kuhusu Saratani ya Mlango wa Kizazi alipotembelea banda la Shirika la AGPAHI.
  Sehemu ya akina mama waliojitokeza kupata huduma ya uchunguzi kwenye banda la Shirika la AGPAHI.
  Mratibu wa Shirika la AGPAHI mkoani Simiyu, Dafrosa Shiluka akitoa ufafanuzi kwa mmoja wa wananchi waliofika kwenye banda la Shirika hilo.
  Sehemu ya akina mama waliojitokeza kupata huduma ya uchunguzi kwenye banda la Shirika la AGPAHI.
  Baadhi ya Wakunga waliohudhuria maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani 2019 kitaifa mjini Bariadi.
  Tazama BMG Online TV hapa chini
  Attachments area

  0 0

  Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

  KWANZA kabisa naomba nitumie fursa hii kukusabahi na natumai uko poa na mambo yanasonga.

  Pia sote tunafahamu Taifa letu lipo katika majonzi kutokana na kifo cha mpendwa wetu Dk.Reginald Mengi aliyefariki dunia usiku wa kuamkia Mei 2, 12019 akiwa Dubai. Mungu ilaze roho yake mahala pema peponi.Amina.

  Baada ya hapo sasa tuendelee iko hivi ukweli uliopo wasanii nchini Tanzania na hasa wa muziki wa kizazi kipya a.k.a Bongo Fleva wamekuwa wakitumia fedha nyingi sana pindi wanapohitaji kurekodi video za nyimbo zao.

  Ni mara kadhaa tumeshuhudia wakifunga safari kwenda nje ya Tanzania ili kupata maeneo ya kurekodi nyimbo zao. Wanamini nje ndiko kuzuri kwa kurekodi video zao kuliko nyumbani.Jamani sio kweli, ninao ushahidi.

  Nikiri Watanzania walio wengi tunayo kasumba nikiwemo mimi kasoro wewe tu unayesoma hapa ya kuamini vya nje ni bora zaidi kuliko vya kwetu.Na ndicho kinachowasumbua wasanii wetu.Si wote ila wengi wao wako hivyo.Usikatae ndio ukweli.

  Sasa umefika wakati kwa wasanii kubadili matazamo na fikra kwasababu katika ardhi ya Tanzania ambayo Mungu ameipagilia na ikapangika kuliko mahali popote tuna kila kitu.

  Ndio maana Wazungu wanafunga safari kuja nchini kwetu kutalii.Tunavyo ambavyo wao hawana.Mungu ametupendelea Watanzania.Tunayo sababu ya kumshukuru kwa kusema Ahsante Mungu.

  Chonde chonde wasanii wa Tanzania.Narudia tena chonde chonde, nyumbani kuna maeneo mazuri ya kurekodi video zenu.Niwahakikishie hamtajuta kutumia mazingira ya nyumbani kwa ajili ya video zenu.

  Nashukuru Mungu baadhi ya wasanii wameona haja ya kubadili mtazamo wao na sasa wameamua kubaki na Tanzania yao katika kufanya kazi zao za muziki.

  Wasanii Amini Mwinyimkuu na Linna Sanga wameonesha njia kwa wasanii wenzao.Unajua ambacho wamekifanya? Nikukumbushe wasanii hao wametoa nyimbo yao mpya inayofahamika kwa jina la Nimenasa.Nyimbo tamu balaa.

  Katika kuhakikisha video ya wimbo huo inakuwa bora na ya kuvuta wakaona isiwe taabu, wakafunga safari hadi kwa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) kwa ajili ya kuomba eneo la kurekodi video yao.  Kwa moyo wa upendo walionao TFS kwa wasanii wa nchi yetu, wala wahakujiuliza mara mbili, walikubali ombi la wasanii hao. Na sio kukubali tu bali waliamua kufadhili na gharama ya video yenyewe kwa asilimia 80.Hongereni TFS.

  Kwa dhamira njema ya TFS kwa wasanii, ni wajibu wa kila msanii iwe wa Bongo Fleva,Bongo Movie na hata wale wa filamu za 'Action' kuhakikisha mnakuwa karibu nao.Wameamua kutoa maeneo yao kwa ajili yenu pale mnapotaka kufanya kazi zenu.

  Wapo tayari kusaidia hata kama isiwe fedha basi hata kutoa watalaam wao ili kushauri sehemu nzuri itakayofaa kwa msanii kurekodi kazi yake kulingana na mahitaji yake. Mnataka nini tena?

  Kaimu Meneja Mawasiliano wa TFS Tulizo Kilaga amefafanua kwa kina sababu za kuamua kuwawezesha wasanii Amini na Linna kurekodi video yao ambapo amesema msingi mkubwa ulitokana na ombi la wasanii hao la kuomba eneo lenye mazingira asili zaidi ili kupata muonekana wanaouhitaji.

  "Walikuja kwetu kuomba maeneo ya kwenda kurekodi video ya Nimenasa.Kwetu TFS tukaona hii ni fursa kwa umaarufu wa wasanii haoa na kampeni yetu ya kuhamasisha utalii wa ndani basi tunaamini ujio wao utatusaidia kuongeza idadi ya watalii wa ndani.

  "Hivyo tuliwaelekeza video yao wakaifanyie Hifadhi ya Msitu wa Asili wa Magamba ulikopo wilayani Lushoto mkoani Tanga. Kuna maeneo mengi mazuri yakiwemo maporomoko ya maji , wanyama , mimea , ndege, pango la Mjerumani na kila aina ya kivutio kilingana na mashairi ya wimbo wao,"amesema Kilaga.

  Amefafanua kwa kuwa wasanii hao walionesha nia TFS imeona ni jukumu lake kuhakikisha kila ambacho wanakihitaji kinapatikana na uzuri wao wanasimamia hifadhi za misitu 17 nchini kote.

  "Sababu za kufanya hivyo tunataka wasanii hawa baada ya kwenda Magamba wawe mabalozi kwa wasanii wengine kwa kuwaambia hakuna sababu ya kuumiza kichwa kwa ajili ya maeneo ya kufanya video zao kwani hapa nyumbani yapo.TFS tunasimamia hifadhi ya misitu 17 na kote huko kuna kila kitu ambacho msanii anahitaji.

  "Kikubwa wasanii wanatakiwa kufika katika ofisi za TFS na kisha kueleza tu wanataka maeneo ya aina gani na sisi tutawapa maelekezo ya mahali pa kwenda na si kwa wanamuziki wa kizazi kipya hata wale ambao wanarekodi video za ngumi,"anasema.

  Ameongeza kuna maeneo mengi ambayo wasanii wanaweza kutayatumia kurekodi na kazi zao zikapendwa na msanii haitaji kutumia nguvu kutafuta maeneo, bali wao wafike tu TFS.

  Ameongeza wasanii wanapaswa kujivunia uwepo wa misitu iliyopo nchini Tanzania, kwani ina kila kitu ambacho kinaweza kuwepo kwenye kazi zao na kwamba TFS ipo tayari kutoa ushauri kwa wasanii.

  Amesisitiza " Tupo katika kipindi cha kufanya promosheni hasa kwa kuzingatia tunaelekea kwenye msimu wa utalii.Hivyo ujio wa Linna na Amini ni sehemu ya kufanya hamasa ya kuvuta Watanzania wengine kwenda maeneo ya utalii".

  Pamoja na mambo mengine, Tulizo anasema msanii anaweza kwenda katika Istagram ya TFS na kisha akatoa mawazo na ushauri wake na baada ya hapo wao wataufanyia kazi.

  Kwa upande wake Amini anasema anatoa rai kwa wasanii nchini kuhakikisha wanaitumia hifadhi za misitu ya asili kwa ajili ya kufanya kazi zao za sanii kwani hakuna ambacho kinakosekana huku akieleza kuwa anao ushahidi kwani yeye amepata nafasi ya kurekodi video ya Nimenasa katika msitu wa Magamba.

  Wakati Linna anasema hakuwahi kufikiria kama nchini kwetu kuna maeneo mazuri ya asili ambayo yaaweza kutumiwa na wasanii kurekodi kazi zao, hivyo naye amesema ni wakati muafaka kwa wasanii kutumia mazingira ya nyumbani kufanya kazi zao za muziki.

   Msanii Linna Sanga akiwa amekanyaga mgongo wa Kaimu Meneja Mawasiliano wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS)Tulizo Kilaga ili kumsaidia kupita aende kurekodi kipande cha video kitakachokuwemo kwenye wimbo wa Nimenasa.Aliyeshika mkono ni msanii Amini Mwinyimkuuu.
   Amini Mwinyimkuu na Linna Sanga wakiwa katika Msitu wa Magamba baada ya kupewa kibali na TFS warekodi video yao ya wimbo unaofahamika kwa jina la Nimenasa.
  0 0


   Mke wa Marehemu Jacline akiwa pamoja na watoto katika katisa la KKKT usharika wa moshi mjini
   Mtoto wa Marehemu Regina Mengi akiwa kanisani tayari kwa ibada katika Kanisa la KKKT usharika wa Moshi mjini Mkoani Kilimanjaro
   Waombolezaji wakiwa kanisani tayari kwa ibada
  Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini Usharika wa Moshi mjini mahali ambapo wenyeji wa Mkoa wa kilimanjaro,wageni mbalimbali wanapouaga Mwili wa Dkt.Regnald Mengi 
  Watu mbalimbali wakiendelea kuuaga Mwili wa Dkt.Regnald Mengi KKKT Usharika wa Moshi Mjij
   Waombolezaji wakiwa kwenye foleni kwaajili ya kuagana na mpendwa wao Regnald Mengi
   Waombolezaji wakiwa kwenye foleni
   Waombolezaji wakiingia kanisani
   Lango kuu la Kanisa kama linavyoonekana
   Wakazi wa Mkoa wa Kilimanjaro wakiwa katika foleni kwaajili ya kuingia kanisani kuuagana na mpendwa wao Regnald Mengi leo.
  Na Vero Ignatus,Moshi

  MAELFU ya wakazi wa  mikoa ya Kilimanjaro,Arusha,Manyara na maeneo jirani wamejitokeza kuaga mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Kampuni tanzu za IPP Regnald Mengi,kwenye ibada ya mazishi katika kanisa la kiinjili la Kilutheri usharika wa Moshi Mjini.

  Mwili wa marehemu Dkt Regnald Mengi,umewasili katika kanisa Hilo majira ya saa 2:00 asubuhi,ambapo ulipokelewa na na baadhi ya viongozi mbalimbali ambao ni wabunge Nape Mnauye,Godbles Lema,Freeman Mbowe,Luhaga Mpina,Anna Kilango na James Mbatia.

  Hata hivyo Mara baada ya mwili huo kuwasili pia ulipokewa na vilio,simanzi na majonzi kwa wanachi ambao walionekana wamefurika katika maeno yote ya viunga vya kanisa hilo.

  Kutokana na umati wa watu kuzidi skauti ambao walikuwa katika lango kuu la kuingilia watu  polisi walilazimika kuingilia katika ili kunisuru Hali iliyokuwepo ambayo ilihatarisha usalama.

  Hata hivyo baada ya zoezi la kutoa heshima za mwisho,Mwili wa Mengi,safari ya kuelekea machame Kijiji Nkuu Sinde kuulaza mwili huo utaanza,ambapo Waziri Mkuu anatarajiwa kuongoza maelfu ya wanachi katika mazishi hayo.


  0 0


  Mnamo Mei 04, 2019 majira kati ya saa 19:00 na 20:00 usiku huko Vwawa, Wilaya ya Mbozi na Mkoa wa Songwe, Mtu mmoja aitwaye MDUDE MPALUKE NYAGALI [31] ilibainika kuwa amechukuliwa na watu ambao hakuweza kuwatambua na kupelekwa mahali pasipojulikana.

  Taarifa zilifikishwa Polisi Mkoa wa Songwe na ufuatiliaji ulianza mara moja na mnamo tarehe 08 Mei, 2019 majira ya saa 21:00 usiku huko Inyala katika Kijiji cha Mtakuja kilichopo Mkoa wa Mbeya alionekana mtu anaomba msaada, ndipo Dereva wa Pikipiki @ Bodaboda aitwaye EMMANUEL KANAMGONDE na mwenzake AYUB WILSON walimbeba na Pikipiki hadi kwa uongozi wa serikali wa Kijiji cha Mtakuja. 

  Mhanga wa tukio hili baada ya kufikishwa kwa viongozi wa Kijiji hicho alijitambulisha kuwa yeye anaitwa MDUDE MPALUKE NYAGALI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo na akaomba wajulishwe viongozi wake. Kisha Mhanga alipelekwa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya kwa uchunguzi zaidi wa kitabibu. 

  Upelelezi wa shauri hili unaendelea ikiwa ni pamoja na msako mkali wa kuwatafuta waliohusika katika tukio hili. 

  Imetolewa na: 

  [ULRICH O. MATEI – SACP] 

  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA

  0 0

  NA WAJMW-DODOMA

  Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imezidi kutoa tahadhari ya  kuwepo kwa ugonjwa wa homa ya Dengue nchini hususani katika Jiji la Dar Es Salaam na Tanga.

  Tahadhari hiyo imetolewa leo na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhammad Kambi wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za wizara hiyo zilizoko jijini Dodoma.

  Prof. kambi amesema hadi kufikia tarehe 6 Mei 2019, kati ya watu waliopimwa, wagonjwa 1237 wamethibitishwa kuwa na virusi au walikwishapata ugonjwa wa Dengue na kati yao 1150 ni kutoka Dar Es Salaam, 86 ni kutoka Tanga na mtu mmoja kutoka Singida.

  Aidha, Prof Kambi amesema takwimu za ugonjwa wa Dengue kwa kipindi cha Januari hadi Aprili 2019 zinaonesha mwenendo wa ugonjwa huu kuwa na idadi ya wagonjwa 1237, vifo vya watu wawili na kuongeza kuwa waliofariki walikua na maradhi mengine.

  Pamoja na hayo Mganga Mkuu huyo wa Serikali amelipongeza jiji la Dar Es Salaam kwa kuanza kunyunyizia dawa viuadudu (Biolarvicides) kwa ajili ya kuangamiza mazalia ya mbu ili kupambana na ugonjwa huu.

  Vile vile amesema Wizara inaelekeza Mikoa na Halmashauri zote nchini kuendelea kuchukua hatua katika kudhibiti ugonjwa huu ikiwa ni pamoja na kufukia madimbwi ya maji, kunyunyizia dawa ya kuua viluwiluwi, kuondoa vitu vinavyosababisha mazalia ya mbu, kufyeka vichaka, kufunika mashimo ya maji taka kwa mifuniko pamoja kusafisha gata za paa la nyumba na kutoruhusu maji kusimama.

  Prof. Kambi amesema Wizara kwa kushirikiana na Mikoa na Halmashauri zote nchini itaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kudhibiti ugonjwa huu ikiwa ni pamoja na kuendelea kuangamiza mazalia ya mbu na viluwiluwi, kuweka mpango wa dharura wa miezi sita kuanzia Mei mpaka Oktoba ili kukabiliana na ugonjwa huu. Pia amesema Serikali imenunua Vitendanishi vyenye uwezo wa kupima wagonjwa 1870 na vimesambazwa kwenye vituo maalum vya ufuatiliaji wa ugonjwa huu nchini kote.

  Mwisho Prof. Kambi amewataka wananchi kuendelea kuchukua hatua za kujikinga kuumwa na mbu kwa kuvaa nguo ndefu, kutumia vyandarua vyenye viuatilifu, kutumia dawa za kufukuza mbu na kuweka nyavu kwenye madirisha na milango ya nyumba za kuishi ili kukabiliana na ugonjwa huu.
  Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhammad Kambi (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu kuwepo kuendelea kuwepo kwa ugonjwa wa Homa ya Dengue nchini.
   Baadhi ya waandishi wa habari waliojitokeza kusikiliza tamko la kuhusu kuwepo kwa ugonjwa wa Homa ya Dengue nchini wakati likitolewa na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhammad Kambi Jijini Dodoma.

  0 0

  Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

  FORUM CC kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya wameamua kuwatanisha wadau kutoka mashirika mbalimbali kwa lengo la kuwa na jukwaa ambalo litatumika kujadili masuala yanayohusu hali ya mabadiliko ya tabianchi.

  Pamoja na mambo mengine Forum CC na mashirika hayo wamejadili kwa kina namna bora ya kufanya kazi kwa karibu na mamlaka za Serikali kwa lengo la kuhakikisha jamii ya Watanzania inakuwa na uelewa wa kutosha kuhusu mabadiliko ya tabia nchi ambayo athari zake zinagusa kila mahali.

  Akizungumza leo Mei 9, 2019 wakati majadiliano hayo yaliyofanyika Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Forum CC Rebecca Muna amefafanua wao kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya wameamua kuwakutanisha wadau hao waliopo kwenye mashirika na asasi za kiraia kujadili kwa kina namna bora ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

  "Sababu iliyotufanya tukutane hapa leo tunataka tuwe na ushirikiano wa karibu na Serikali.Tunataka kufanya kazi na viongozi, hivyo wadau wote wa maendeleo tutakuwa na jukwaa litakalotupa fursa ya kufanya kazi kwa pamoja hasa za kutatua changamoto za athari za tabianchi,"amesema Muna.

  Amefafanua hali ya mabadiliko ya tabianchi yamesababisha nchi kuwa na ukame, mafuriko, kina cha bahari kuongezeka, kupanda kwa joto na magonjwa ya mazao , hivyo kusababisha madhara ya aina mbalimbali kwa jamii.

  Amesisitiza kupitia jukwaa la majadiliano ambalo litaanzishwa na wadau maana yake watakuwa na eneo maalumu ambalo litawakutanisha na kujadili kwa kina hali ya mabadiliko ya tabianchi.

  "Lengo letu ni kuwa na jukwaa la pamoja ambalo hilo litatuwezesha sote kwa umoja wetu kupata fursa ya kujadili na kupata ufumbuzi wa namna sahihi ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi,"amesema Muna.

  Hata hivyo amesema umefika wakati wa kuwepo kwa mfumo sahihi ambao utawawezesha mashirika, asasi za kiraia na wadau wa maendeleo kushirikishwa kikamilifu na Serikali katika kuleta maendeleo.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Forum CC Euster Kibona amesema kuwa pamoja na kuweka mikakati ya kujadili kuhusua mabadiliko ya tabianchi wamekumbusha kuhusu uwajibika ambapo kupitia mada yake iliyohusu dhana ya uwajibika alifafanua kwa kina huku akisisitiza uwajibikaji ni ushirikiano baina ya pande mbili.

  "Uwajibikaji ni muhimu katika kufuatilia masuala mbalimbali ya kimaendeleo na hata hili la mabadiliko ya tabianchi nalo lazima tujadiliane kuhusu namna bora ya kuwajibika kwani eneo hilo limekuwa na changamoto kubwa.

  "Katika kuwajibika lazima ufahamu nani anawajibika katika lipi na anawajibika kwani.Hata hivyo ili kufanikiwa ni jambo linalohusu uhusiano wa zaidi ya mtu mmoja.Hivyo ni wakati wetu kuweka mikakati ya namna bora itakayowezesha kila mmoja kwa nafasi yake kuwajibika,"amesema Kibona. 

  Awali Ofisa Programu,Ushawishi na Utetezi kutoka TGNP Deogratius Temba amesema mabadiliko ya tabianchi yanagusa maeneo mbalimbali yakiwemo ya jinsia na athari zake zinakwenda moja kwa moja kwa mtoto wa kike.

  "Athari za mabadiliko ya tabianchi ni nyingi ikiwemo ya ukame ambayo inasababisha hata maeneo ambayo wananchi walikuwa wanateka maji yakauka na kusababisha wanawake kuanza kufuata maji umbali mrefu na hivyo kusababisha hata matukio ya ukatili wa kijinsi.

  "Hivyo eneo hili linagusa maeneo mengi na hivyo kila mmoja wa nafasi yake anayo nafasi ya kujadili na kuweka mipango na hasa ambayo inatokana na maoni ya wananchi katika maeneo husika.

  "TGNP tumekuwa tukishirikiana na wananchi kuibua ajenda na kisha wananchi kuzipeleka katika mamlaka husika na hivyo hata haya masuala ya tabianchi ni vema wananchi wakajengewa uwezo ili kuwa na uelewa,"amesema Temba

  Mwenyekiti wa Bodi ya Forum CC Euster Kibona akizungumza jambo wakati wa kikao cha mashirika ya kirai kujadili hali ya mabadiliko ya tabianchi na mchango wa mashirika hayo katika kutafuta ufumbuzi wake kwa kushirikiana na Serikali.
  Mkurugenzi Mkuu wa Forum CC akizungumza na wadau wa maendeleo kupitia mashirika ya kiraia ambauo yamekutana kujadili namna bora ya kujadili changamoto za mabadiliko ya tabia nchi kwa kushirikiana na vongozi wa serikali.

  Ofisa Programu,Ushawishi na Utetezi kutoka TGNP Deogratius Temba akifafanua jambo kuhusu mabadiliko ya tabianchi yanavyoarithi moja kwa moja masuala ya kijinsia nchini Tanzania wakati wa kikao kati ya Forum CC na mashirika ya kiraia ambayo yamekutana kwa malengo mbalimbali likiwemo la kuwepo kwa jukwaa la pamoja na wadau hao 

  Sehemu ya washiriki wa mkutano uliondaliwa na Forum CC kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya wenye lengo la kuangalia namna bora ya mashirika ya kiraia kushirikiana na Serikali kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

  0 0

  Na.Vero Ignatus,Machame ,Kilimanjaro

  Waziri mkuu wa Tanzania Kasimu Majaaliwa, ameongoza maelfu ya watanzania katika mazishi ya aliyekuwa mfanyabiashara maarufu  ukanda wa Afrika mashariki, Dr. Regnald Mengi, ambaye amezikwa leo katika makaburi ya familia nyumbani kwa wazazi wake kijiji cha Kisereni Machame mkoani Kilimanjaro Km 35 kutoka Moshi mjini.

  Akitoa salamu za rambi rambi kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Waziri Mkuu Kassim Majaaliwa amesema kuwa taifa litamkumbuka Dkt. Mengi kwa mchango wake mkubwa wa kukuza uchumi nchini hasa katika sekta ya madini, habari, viwanda na mazingira, kwani amewahi kuwa mwenyekiti wa abaraza la mazingira Taifa.

   Waziri mkuu Majaaliwa amesema mchango wa Dkt.Mengi katika kuwakumbuka watu wenye mahitaji maalumu utaendelea kukumbukwa daima kuindokewa na mtu mzalendo katika historia ya Tanzania

  "Hakuna Mtanzania asiyejua mchango alioutoa kwa Taifa hili,kwa namna alivyoguswa katika nyanja mbalimbali kwa jamii na hata kwa serikali, tunatambua mchango wake"alisema Majaliwa.

  Amesema kuwa kama Taifa la Tanzania  msiba huo wa Dkt Reginald Mengi alikuwa ni mtu wa upendo na hakuwa na ubaguzi hivyo pigo na wameondokewa na mtu aliyekuwa muhimu maishani na Mungu alimbariki na yeye akawa baraka kwa wengine.

   Akitoa mahubiri katika ibada ya mazishi hayo iliyofanyika katika kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania KKKT Usharika wa Moshi mjini, Askofu mkuu wa Kanisa hilo Dkt. Fredrick Shoo, amewaasa viongozi wa serikali hasa wale wenye umri mdogo kuacha kiburi cha madaraka na badala yake watende haki kwa wananchi wote bila upendeleo na watapata za Mungu.

  Dkt Shoo amemtaja Marehemu Mengi kuwa  hakuwabagua maskini japo alikuwa na tajiri na tabia hiyo inapaswa kuigwa na watu wote wenye nafasi za uongozi serikalini, wenye madaraka na wenye pesa.

  Askofu Dkt. Shoo ameendelea kusisitiza kuwa kama Taifa la Tanzania linahitaji kupokea baraka kutoka kwa Mungu ni muhimu kuacha  ubaguzi,  kiburi na kujikweza,amekemea baadhi ya tabia ya kauli za viongozi ambazo zinaweza kuleta migogoro katika jamii.

  Kwa upande wake mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzania nchini Tanzania Freeman Mbowe, amekemea tabia ya ubaguzi wa ukabila unaooneshwa na baadhi ya viongozi na kwamba ili kumuenzi Mengi ni muhimu kuyaacha matendo hayo kwani alikuwa ni mtu wa kujishusha japo alikuwa Bilione.

  Katika hatua nyingine Askofu Dkt.Shoo amewataka Watanzania kuacha tabia ya kubaguana kwani ni dhambi mbele za Mungu ,wenye nafasi kuwakandamiza wale walio wa hali ya chini,amewataka kuacha kiburi 

  "Hivi nyie viongozi haswa vijana mnapopata cheo mnajisahau wanaojitutumua kama chatu wakumbuke kuwa kila siku tunamuomba Mungu na lazima Mungu  atawashusaha"

  Kwa upande wake Waziri mkuu Kassimu Majaliwa ametoa pole kwa familia ya Marehemu Dkt.Regnald Mengi kwa kuondokewa na mpendwa wao,amesema amepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa ya msiba wa Mengi

  Tujifunze kuwathamini  watu wasio na uwezo katika jamii na Taifa kwa ujumla msikivu ,mpenda amani,na mwenye kuwasaidia wengine 1990 alianza kupata chakula cha pamoja na watu wenye ulemavu.

  Kwa upande wake Mkuu CCM Taifa  Bashiru Ally amesema mchango wa Dkt. Mengi katika Taifa haswa katika mazingira  alisisitiza kupanda na kuotesha mingi tumuenzi na kupanda miti ya kutosha

  "Baba Askofu hatujafanya kazi ya kuwaandaa vijana wetu kuwa Viongozi bora, sasa tunavuna matunda yake, naomba nimuombe msamaha kijana wangu Makonda, nilimsema Simiyu mara ya kwanza, akaja ofisini analia, ameanza kujirekebisha" alisema Bashiru

  Akitoa salamu kwa niaba ya Bunge Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai amesema kuwa ameonyesha kwa hali na mali alikuwa na mali ila mkarimu na amefanya mengi ya heshima kubwa,alijitoa bila kujali alipanda miti zaidi ya milioni ishirini siyo jambo la kawaida.

  "Nawaomba wananchi wenzangu msiamini kila kitu kinachoandikwa  kwenye mitandao ya kijamii ,vingine vya  uongo sana.alisema Ndugai

  Kwa zaidi ya mzee mmengu ameshatangulia mbele za haki haitajalisha tutazungumza maneno mazuri kiasi gani ,tutakachoweza ni kuyaishi ya mema aliyotenda,alikuwa mnyenyekevu,kauli zake zilikuwa za kujenga,kupatanisha,mamlaka,fedha zinajenga kiburi zisipotumika vizuri,hakuwa kiongozi wa serikali 

  Na hatimaye msafara ukafika katika kijiji cha Kisereni Machame mkoani Kilimanjaro,  ambapo ndipo mwili wa mfanyabiashara huyo maarufu umehifadhiwa katika nyumba yake ya milele. Eneo alilozikwa Dkt. Mengi ni eneo la makaburi ya familia ambapo pia wamezikwa wazazi wake na ndugu wengine.

   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiweka shada la Maua kwenye Kaburi la Marehemu Dkt Reginald Mengi wakati wa mazishi,Machame mkoani Kilimanjaro

  0 0

  Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) akijibu swali bungeni leo tarehe 10 Mei 2019 wakati wa mkutano wa kumi na tano wa Bunge la Bajeti Jijini Dodoma. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
  Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akifatilia kipindi cha maswali na majibu wakati wa mkutano wa kumi na tano wa Bunge la Bajeti Jijini Dodoma leo tarehe 10 Mei 2019.
  Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) akijibu swali bungeni leo tarehe 10 Mei 2019 wakati wa mkutano wa kumi na tano wa Bunge la Bajeti Jijini Dodoma.
  Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) pamoja na Naibu waziri wa Nishati Mhe Subira Mgalu (Mb) wakifatilia mkutano wa kumi na tano wa Bunge la Bajeti Jijini Dodoma leo tarehe 10 Mei 2019.

  Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma

  Serikali kupitia Wizara ya Kilimo imeyaagiza makampuni ya Premium Agrochem, OCP na Export Trading Group (ETG) kuhakikisha kwamba ifikapo Julai, 2019 kampuni hizo ziwe na ghala za kuhifadhia mbolea na mawakala wa kusambaza katika mikoa inayotumia mbolea kwa wingi ukiwemo mkoa wa Katavi ili kuondoa changamoto ya upungufu wa mbolea kwa wakulima katika maeneo hayo.

  Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) ameyasema hayo leo tarehe 10 Mei 2019 wakati akijibu swali la Mbunge wa viti maalumu Mhe Taska Restituta Mbogo aliyetaka kufahamu kuwa serikali ina mpango gani wa kusambaza mbolea kwa wakati katika mkoa wa Katavi.

  Alisema kuwa Serikali inatumia Mfumo wa Ununuzi wa mbolea kwa pamoja Bulk Procurement System - BPS kuagiza mbolea ya kupandia (DAP) na mbolea ya kukuzia (UREA), Mfumo huo unawezesha upatikanaji wa mbolea kwa wakati na kwa bei nafuu na kudhibiti upandishaji wa bei za mbolea kiholela.

  Mhe Mgumba aliongerza kuwa Serikali inakamilisha zabuni ya kuingiza mbolea tani 280,000 ambapo tani 170,000 ni mbolea ya kupandia na tani 110,000 ni mbolea ya kukuzia kwa ajili ya msimu wa 2019/2020 kupitia mfumo wa BPS.

  Alisema, Mbolea hiyo inatarajiwa kufikishwa hapa nchini mwezi Agosti, 2019 na kusambazwa kwa wakulima wa mkoa wa katavi na maeneo mengine nchini kabla ya mwezi Septemba 2019. Vile vile, ziada ya mbolea iliyopo nchini inaendelea kusambazwa katika maeneo mbalimbali kulingana na msimu ambapo hadi tarehe 30 Machi, 2019 kulikuwa na tani 147,913 za mbolea.

  Aidha, Serikali inatumia Mfumo wa Ununuzi wa mbolea kwa pamoja Bulk Procurement System - BPS kuagiza mbolea ya kupandia (DAP) na mbolea ya kukuzia (UREA). Mfumo huo unawezesha upatikanaji wa mbolea kwa wakati na kwa bei nafuu na kudhibiti upandishaji wa bei za mbolea kiholela.

  Serikali inakamilisha zabuni ya kuingiza mbolea tani 280,000 ambapo tani 170,000 ni mbolea ya kupandia na tani 110,000 ni mbolea ya kukuzia kwa ajili ya msimu wa 2019/2020 kupitia mfumo wa BPS. Mbolea hiyo inatarajiwa kufikishwa hapa nchini mwezi Agosti, 2019 na kusambazwa kwa wakulima wa mkoa wa katavi na maeneo mengine nchini kabla ya mwezi Septemba 2019.

  Kadhalika, Mhe Mgumba alisema kuwa ziada ya mbolea iliyopo nchini inaendelea kusambazwa katika maeneo mbalimbali kulingana na msimu ambapo hadi tarehe 30 Machi, 2019 kulikuwa na tani 147,913 za mbolea.

  “Serikali imelielekeza Shirika la Reli Tanzania kutoa kipaumbele cha kusafirisha mbolea ili kusafirisha mbolea nyingi kwa wakati mmoja na gharama nafuu ili kumfikia mkulima kwa wakati na bei nafuu” Alikaririwa Mhe Mgumba na kuongeza kuwa

  Serikali inakusanya mahitaji ya mbegu bora na viuatilifu kutoka katika mikoa ili kuhamashisha kampuni na wafanya biashara kupeleka pembejeo hizo kwa wakulima kabla ya msimu wa kilimo kuanza na wakati wa mauzo ya mazao.

  0 0

  Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako ameupongeza Uongozi wa shule ya Dar es Salaam International Academy kwa kuwajengea uwezo na kuona umuhimu wa kuwafundisha na kuwapa nafasi wanafunzi kujifunza wenyewe.

  Prof. Ndalichako ametoa pongezi hizo jijini Dar es Salaam aliposhiriki katika maonesho mbalimbali ya wanafunzi wa darasa la tano katika shule hiyo ambapo amesema wanafunzi hao wamefundishwa kutafuta taarifa mbalimbali kutokana na mada walizopewa.

  “Nimefurahi kuona wanafunzi wa darasa la tano wanaonesha ubunifu katika kuangalia matatizo ya jamii kwani hata mada walizoangalia zinaendana na hali halisi ya sasa ambayo serikali imekuwa ikiwekea msisitizo kama masuala ya jinsia, magonjwa ya homa ya ini na Ebola, dawa za kulevya pamoja na Teknolojia,” amesema Ndalichako.

  Waziri Ndalichako amesema katika kutafuta taarifa wanafunzi hao wameonyesha vipaji vya hali ya juu wakati wa kuandaa mada za maonyesho kwani wametumia mitandao pamoja na kuwahoji watu waliowaona muhimu kuwapatia taarifa zilizowawezesha kukamilisha mada zao kwa ajili ya maonyesho hayo.

  Aidha, Waziri Ndalichako ametoa wito kwa walimu kuwawezesha na kuwapa nafasi wanafunzi katika kuwa na ubunifu, kujiamini na kuweza kutafuta taarifa mbalimbali katika kujifunza kwani wanafunzi wa kitanzania wana uwezo wa kufanya mambo makubwa sana lakini wanakwama kutokana na kushindwa kujiamini na uoga wakati shuleni ni sehemu ambayo vipaji hivyo vinaweza kuendelezwa.

  “Suala la kujiamini ni changamoto kubwa kwa watanzania wengi, wana uwezo, akili na vipaji lakini wanakuwa hawajiamini hili ni tatizo, kwa hiyo tuendelee kuwa na maonyesho kama haya ambayo yatawajengea wanafunzi wetu uwezo, kujiamini, kuonyesha yale wanayoweza na kutoogopa kusema mbele za watu,” amesisitiza Waziri Ndalichako.

  Aidha, Waziri Ndalichako amesema hata katika shule za serikali maonyesho kama hayo yanafanyika katika ngazi ya shule za sekondari ambayo yanaanza katika ngazi ya shule, wilaya na kilele inakuwa katika ngazi ya Kitaifa hata hivyo wameahidi kuangalia namna ya kuanza kushirikisha wanafunzi wa shule za msingi kwani kufanya hivyo inawezesha kuwaandaa wabunifu tangu wakiwa katika umri mdogo.

  Akizungmzia mkakati wa serikali wa kutambua na kukuza ubunifu nchini Waziri Ndalichako amesema kupitia Tume ya Sayansi na Teknolojia inazo atamizi ambazo zinatumika kuendeleza ubunifu lakini pia imeona si rahisi kila mtu kuweza kufika katika Tume hiyo hivyo imeanza utaratibu wa kuanzisha katika ngazi za Halmashauri ambapo mwaka huu mwongozo umetoka wa kuangalia namna gani wabunifu wakitambulika wanaweza kuendelezwa.

  “Pia katika vyuo vikuu vyetu kuna hatamizi kwa mfano Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Nelson Mandela kuna atamizi ambazo zinafanya vizuri sana na wao wamejikita katika mazao na kuangalia vitu ambavyo vinaweza kuweka sumu katika mazao lengo ni kuhakikisha tunaongeza wigo ili vipaji wa watanzania viweze kuendelezwa,” amesema Ndalichako.

  Naye Mkuu wa Shule hiyo, Fawzya Hirji amesema shule hiyo imejipanga kuhakikisha kunakuwa na ushirikiano kati ya walimu, wanafunzi na wazazi katika kuwawezesha wanafunzi hao kuwa na uwezo wa ubunifu, kujiamini na kutumia mitandao katika kutafuta taarifa mbalimbali zinazowapatia maarifa ya kujua mambo mbalimbali duniani.

  Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akipata maelezo kwa wanafunzi wa darasa la tano wa Shule ya Dar es Salaam International Academy.

  Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akipewa maelezo na wanafunzi wa Shule ya Dar es Salaam International Academy jijini Dar es Salaam.
   Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akipata maelezo kwa wanafunzi wa darasa la tano wa Shule ya Dar es Salaam International Academy.
  Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akipewa maelezo na wanafunzi wa Shule ya Dar es Salaam International Academy jijini Dar es Salaam.

  0 0


  MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella katikati akikata utepe wakati wa sherehe ya ufunguzi wa soko la madini ya vito wilayani Mkinga kulia ni Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Tanga Zabibu Napacho kushoto ni Mkurugenzi wa madini wa shirika la Pact Cristina Villegas akifuatiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake wachimba Madini Tanzania (Tawoma) Eunice Negelo  MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza wakati wa uzinduzi huo kulia Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Tanga Zabibu Napacho kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake wachimba Madini Tanzania (Tawoma) Eunice Negelo  Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Tanga Zabibu Napacho akizungumza wakati wa halfa hiyo kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akifuatiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake wachimba Madini Tanzania (Tawoma) Eunice Negelo  Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake wachimba Madini Tanzania (Tawoma) Eunice Negelo akizungumza kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Mkinga Mark Yona  Mkuu wa wilaya ya Mkinga Mark Yona akizungumza kulia Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake wachimba Madini Tanzania (Tawoma) Eunice Negelo  Mkurugenzi wa madini wa shirika la Pact Cristina Villegas akizungumza wakati wa ufunguzi huo ambapo aliipongeza Serikali ya awamu ya tano  MENEJA wa (TRA) Mkoa wa Tanga Specioza Owure akizungumza wakati wa ufunguzi huo  Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake wachimba Madini Tanzania (Tawoma) Eunice Negelo kushoto akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella wakati wa ufunguzi wa soko la Madini wilayani Mkinga kulia ni Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Tanga Zabibu Napacho kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Mkinga Mark Yonna  Sehemu ya wadau wa madini na wachimbaji wakiwa kwenye ufunguzi huo  Sehemu ya wadau wa madini na wachimbaji wakiwa kwenye ufunguzi huo  Sehemu ya wadau wa madini na wachimbaji wakiwa kwenye ufunguzi huo  MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akionyeshwa aina ya madini  Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake wachimba Madini Tanzania (Tawoma) Eunice Negelo katikati akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kulia na Mkuu wa wilaya ya Mkinga Mark Yonna kushoto na kulia ni Katibu wa Tawoma Salma Kundi mara baada ya kufanya ufunguzi wa soko la madini wilayani humo  Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake wachimba Madini Tanzania (Tawoma) Eunice Negelo kushoto akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella  Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake wachimba Madini Tanzania (Tawoma) Eunice Negeloakiwa na Katibu wake kushoto Salma Kundi wakiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kulia na anayefiuatia ni Mkuu wa wilaya ya Mkinga Mark Yonna  Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake wachimba Madini Tanzania (Tawoma) Eunice Negelo kushoto akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella  MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya sherehe ya ufunguzi wa soko la madini ya vito wilayani Mkinga .  MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella amesema Serikali itahakikisha inaendelea kuzipatia ufumbuzi wa kudumu changamoto zinazowakabili wachimbaji wadogo wadogo nchini ambazo zimekuwa ni kikwazo cha maendeleo yao


  Hayo yamesemwa na Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigela wakati wa sherehe ya ufunguzi wa soko la madini ya vito wilayani Mkinga .


  Alisema kuwa licha ya wachimbaji hao kufanya kazi nzuri ya uchmbaji lakini wamekuwa wakikabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo uduni wa vifaa ,masoko pamoja na mitaji .


  “Ufunguzi wa soko hili ni kielelezo cha kuonyesha namna ambavyo serikali yenu ipo tayari katika kuanza kushughulikia changamoto zenu kwani uwepo wa soko hili tayari ni mkombozi kwenu”alisema Mkuu wa mkoa huyo.


  Alisema kuwa changamoto nyingine ni namna ambavyo wataweza kuongeza thamani madini hayo ili yaweze kupata soko la uhakika na kwa haraka.


  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake wachimba Madini Tanzania (Tawoma) Eunice Negelo alisema kuwa uwepo wa soko hilo utasaidia kudhibiti utoroshwaji wa madini.


  Vile vile alisema kuwa uwepo wa soko hilo utaweza kuwasaidia wachimbaji wadogo kupata fursa ya masoko ambapo hapo awali ilikuwa ni changamoto kubwa kwao.


  “Tunaimani sasa serikali itaweza kupata mapato yake vizuri na wachimbaji wataweza kuuza madini yao kwa uhakika bila ya hofu ya kuweza kutapeliwa na wajanja wachache”alisema Mwenyekiti huyo.


  Hata hivyo Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Tanga Zabibu Napacho alisema kuwa soko hilo ndilo ambalo litaweza kutoa dira ya uanzishaji wa masoko mengine mkoani humo.


  Alisema kuwa mkoa huo unautajiri wa madini lakini wachimbaji wadogo waliowengi walikuwa hajaweza kunufaika biashara hiyo kutokana na ukosefu wa masoko ya uhakika.


  Mkurugenzi wa madini wa shirika la Pact Cristina Villegas aliipongeza serikali kwa kuja na uamuzi wa masoko hayo kwani utasaidia kuzui utoroshwaji wa madini kwa kiasi kikubwa.


  “kwa uwamuzi wa serikali utasaidia kudhibiti mapato yake lakini na mchimbaji mdogo ataweza kuona manufaa ya shughuli ya uchimbaji anayoifanya’alisema Villegas.

  0 0

  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiagana na Balozi Mdogo wa China anayefanyia Kazi zake Zanzibar Mhe. Xie Xiaowu, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)
   RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapiunduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Profesa Robert .C,Spear, wa Chuo Kikuu cha California, alipowasili katika ukumbi wakati wa hafla ya kuzungumza na Ujumbe wa WHO na Madaktari wa Kichina waliosimamia Mradi wa Kupambana na Kichocho Zanzibar.(Picha na Ikulu).

   RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Kiongozi wa Ujumbe wa WHO Dr. Dirk Engels, wakati walipofika na Ujumbe wa Madaktari wa Kichina Waliosimamia Mradi wa Kupambana na Kichocho Zanzibar, kushoto kwa Rais Balozi Mdogo wa China anayefanyia kazi zake Zanzibar Mhe. Xie Xiaowu, (Picha na Ikulu)
    BAADHI ya Madaktari wa Kichina waliosimamia Mradi wa Kupambana na Kichocho Zanzibar, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, walipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo leo,10-5-2019.(Picha na Ikulu)
   RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Ujumbe wa WHO na Madaktari wa Kichina Waliosimamia Mradi wa Majaribio ya Kupambana na Kichocho Zanzibar, kushoto Balozi Mdogo wa Chini Zanzibar Mhe. Xie Xiaowu walipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo.(Picha na Ikulu). 
   RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa WHO na Madaktari wa Kichina waliosimamia Mradi wa kupambana na Kichocho Zanzibar, waliofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo leo.10-5-2019.(Picha na Ikulu)

  0 0

  Na Seif Mangwangi, Arusha
  KIWANDA cha A to Z cha jijini hapa kimeingia mkataba wa bilioni 3.5 wa kuzalisha dawa aina ya AFLASAFE ya kutibia mazao yanayosababisha sumukuvu inayopatikana kwenye mahindi na karanga na ambayo imekuwa ikisababisha maradhi ya saratani ya ini.
  Mbali ya saratani ya ini, Sumukuvu (AFLATOX), inaelezwa kusababisha kudumaa kwa watoto ambao wamekuwa wakinywa uji unaotumia unga unaotengenezwa kwa zao la mahindi pamoja na karanga kwaajili ya lishe
  Mtendaji Mkuu wa A to Z, Kalpesh Shah na Kaimu Mkurugenzi wa taasisi ya kimataifa ya utafiti wa mazao ya kilimo (IITA) yenye makao yake makuu nchini Nigeria, Dkt Kenton Dashell walisema dawa hiyo itakuwa ni suluhu ya maradhi ya saratani kwa kuwa yamekuwa yakisababisha vifo vingi kwa wananchi wa Afrika.
  DKT Dashell alisema kila mwaka maelfu ya waafrika wamekuwa wakipoteza maisha kwa maradhi yanayosababishwa na sumukuvu na kupoteza nguvu kazi ya mataifa mengi ya Afrika, hivyo kuzalishwa kwa dawa hiyo kutapunguza vifo na kukuza uchumi wa Afrika.
  “ Kati ya kampuni nyingi zilizotenda kuomba mradi wa kuzalisha dawa hii, ni A to Z pekee ndio iliyoonekana kuwa na sifa na uwezo wa kuizalisha, kwa hiyo nipende tu kuwapongeza  sana kwa kushinda tendaII H,”alisema.
  Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa A to Z, Kalpesh Shah alisema kampuni yake itatumia Bilioni 3.5 katika mradi huo na kwamba dawa  hiyo itakayokuwa ikijulikana kama Aflasafe TZ01, itaanza kutumika nchini Novemba mwaka huu baada ya uzalishaji kuanza rasmi.
  Alisema kwa miaka mingi A to Z imekuwa ikifanya utafiti wa kugundua dawa ya kutibu Sumukuvu kupitia taasisi yake ya utafiti ya ATRC, kwa kuwa sumu hiyo imekuwa ikiwasababishia wakulima hasara kubwa pamoja na kupoteza soko la mazao yao nje ya nchi, hivyo kugunduliwa kwa dawa hiyo na wao kupata fursa ya kuizalisha ni jitihada za muda mrefu za kuokoa vifo na kukuza uchumi wa Tanzania na Afrika.
    Mtendaji Mkuu wa A TO Z Kalpesh Shah akitambulisha dawa aina ya Aflasafe ambayo itatumika kunyunyiziwa kwenye mahindi na karanga kwaajili ya kuua sumukuvu ambayo imekuwa ikisababisha maradhi ya saratani ya ini.

  Kaimu Mkurugenzi wa taasisi ya kimataifa ya utafiti wa mazao ya kilimo (IITA), Dkt Kenton Dashell pamoja na Mtendaji Mkuu wa ATOZ Kalpesh Shah wakibadilishana nyaraka za makubaliano ya kuanza uzalishaji wa sawa aina ya Aflasafe kwaajili ya kuua sumukuvu.

  0 0

  Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (wa pili kutoka kushoto) pamoja na Balozi wa Afrika Kusini nchini, Mhe. Thamsanga Dennis Msekelu pamoja na Balozi wa Algeria Mhe. Saad Belabed wakikata keki iliyoandaliwa kwenye hafla hiyo.
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.)akihutubia kwenye hafla ya maadhimisho ya miaka 25 ya Uhuru wa Taifa la Afrika Kusini iliyofanyika kwenye Hoteli ya Coral Beach jijini Dar es Salaam tarehe 09 Mei, 2019. 
  Juu na Chini ni sehemu ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo
  Prof. Palamagamba John Kabudi akiendelea kuzungumza kwenye hafla hiyo huku Balozi wa Afrika Kusini nchini, Mhe. Thamsanga Dennis Msekelu (aliyeketi) akimsikiliza.
  Sehemu nyingine ya wageni wakimsikiliza Prof. Kabudi hayupo pichani.
  Juu na chini ni sehemu nyingine ya wageni waalikwa aliohudhuria maadhimisho hayo wakisikiliza hotuba hiyo ya Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Hayupo pichani).

  0 0

  * Yasaidia wajasiriamali wadogo kwa kuwatengea sh. milioni 200 kila mwaka


  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameipongeza kampuni ya TOTAL Tanzania kwa kuwekeza hapa nchini mtaji wa dola za Marekani milioni 200 (sawa na sh. bilioni 460) ndani ya miaka mitatu.

  Alitoa pongezi hizo jana usiku (Alhamisi, Mei 9, 2019) kwenye sherehe za kutimiza miaka 50 kwa kampuni ya TOTAL hapa nchini, zilizofanyika jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani, mabalozi, Rais wa TOTAL Africa, wakandarasi na wafanyabiashara mbalimbali.

  “Tangu mwaka 2015, kampuni ya TOTAL imewekeza hapa nchini mtaji mkubwa wa zaidi ya dola za Marekani milioni 200 ili kutoa huduma za uagizaji, uuzaji na usambazaji wa bidhaa za mafuta ikiwemo mafuta ya dizeli, petrol, vilainishi mbalimbali pamoja na bidhaa za nishasti mbadala (solar products),” alisema.

  Sambamba na uwekezaji huo, Waziri Mkuu alisema, Watanzania zaidi ya 800 wamenufaika na ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja kutoka TOTAL ambapo kampuni hiyo imekuwa ikichangia sh. milioni 25 kila mwaka kwa ajili ya masuala ya usalama barabarani.

  Shughuli nyingine za kijamii ambazo zimenufaika na uwepo wa kamuni hiyo nchini ni ujenzi wa madarasa (sh. milioni 45), ujenzi wa vituo vya afya (sh. milioni 80) na uchangiaji wa madawati 3,000 kwa baadhi ya shule za mkoa wa Dar es Salaam.

  “Serikali ya awamu ya tano inaipongeza kampuni ya TOTAL kwa kuendelea kuwekeza nchini katika kipindi hicho cha miaka 50. Hongereni sana kwa ubunifu wenu na uwekezaji wa zaidi ya shilingi milioni 200 ili kusaidia wajasiriamali kupitia mpango ujulikanao kama The African Start Upper Challenge.”

  “Nimearifiwa kuwa tayari Watanzania sita wamenufaika na mpango huo kwa kupatiwa zaidi ya shilingi milioni 25 za kuanzisha shughuli mbalimbali za ujasiriamali,” alisema Waziri Mkuu akielezea mpango huo ulioanzishwa mwaka 2016.

  Kuhusu uwekezaji, Waziri Mkuu alisema Rais Dkt. John Pombe Magufuli kupitia Baraza la Biashara nchini amekuwa akikutana na jumuiya ya wafanyabiashara ili kujadili na kuzipatia ufumbuzi changamoto mbalimbali zinazowakabili.

  Alisema Rais Magufuli alianzisha Wizara ya Uwekezaji na kuiweka chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu ili iwe rahisi kwake kukutana na wawekezaji na kuzungumza nao moja kwa moja kuhusu vikwazo vya kibiashara wanavyokutana navyo.

  “Tumeanza utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Kuboresha Mazingira ya Uwekezaji na Biashara nchini (blueprint) na tunafanya mapitio ya vivutio mbalimbali vya uwekezaji ikiwemo vivutio vya kikodi, kupitia timu maalumu,” alisema.

  Aliwataka wawekezaji waliohudhuria sherehe hizo, waangalie Jiji la Dodoma kama fursa nyingine ya uwekezaji na njia ya kuunga mkono mkakati wa Serikali kuhamia Dodoma. “Sasa hivi Serikali tumetengeneza fursa nyingine ya uwekezaji, nayo ni Dodoma. Milango ya uwekezaji iko wazi na fursa za uwekezaji zipo. Ukitaka kujenga viwanda, majumba, mahoteli, njoo Dodoma. Ardhi tunayo, tutakupa,” alisisitiza.

  Mapema, akielezea utendaji wa kampuni hiyo, Rais kampuni ya TOTAL Africa anayeshughulikia masoko na huduma, Bw. Stanislas Mittelman alisema kampuni hiyo ilianzishwa mwaka 1969 na siku zote wamekuwa wakiamini kuwa uimara wa mahusiano yao na Serikali, utatokana na uvumilivu na uaminifu wao kwa jamii ya Watanzania.

  Alisema uwekezaji wanaoufanya ni sehemu ya ukuaji wao lakini pia ni njia yao ya kushiriki kuchangia azma ya Serikali ya ukuzaji wa viwanda ili kuelekea “Tanzania ya Viwanda”. “Tumeitikia wito wa Rais Magufuli wa kuongeza uwekezaji hapa nchini, tuliamua kuwa wabia Wakuu (leading partner) kwenye mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta litakalosafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima, Uganda kuja Tanga, Tanzania,” alisema.

  “Pia tumewekeza mtaji wa dola za marekani milioni 200 hasa kwenye ununuzi wa kampuni ya GAPCO, jambo ambalo limetusaidia tuongeze mtandao wetu mara tatu zaidi na kufikisha vituo zaidi ya 100 vya kuuzia mafuta hapa nchini. Pia tumezindua mtambo wa kisasa wa kusafishia mafuta ambao umetuwezesha kuingiza bidhaa mpya kwenye soko la Tanzania,” alisema.

  “Kampuni ya TOTAL itaendelea kuwashirikisha Watanzania ubunifu tunaoupata kwnye Nyanja za kimataifa na hii inadhihirishwa na mabadiliko tuliyoyafanya kwenye kituo chetu cha kuhifadhia mafuta (fuel storage terminal) na utoaji wa mafuta bora ya kusafishia injini ya TOTAL Excellium,” alisema.

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  IJUMAA, MEI 10, 2019.

  Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akiteta jambo na Rais wa TOTAL Africa, Stanislas Mittelman, katika sherehe za kutimiza miaka 50 kwa kampuni ya TOTAL Tanzania, zilizofanyika jijini Dar es Salaam Mei 9.2019
  Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza, katika sherehe za kutimiza miaka 50 kwa kampuni ya TOTAL Tanzania, zilizofanyika jijini Dar es Salaam Mei 9.2019.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
  Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Rais wa TOTAL Africa, Stanislas Mittelman, katika sherehe za kutimiza miaka 50 kwa kampuni ya TOTAL Tanzania, zilizofanyika jijini Dar es Salaam Mei 9.2019.
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Balozi wa wa Ufaransa nchini, kwenye sherehe za kutimiza miaka 50 kwa kampuni ya TOTAL Tanzania, zilizofanyika jijini Dar es Salaam Mei 9.2019.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

  0 0

   Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba (katikati) akizungumza na wazalishaji wa mifuko mbadala wa plastiki (hawapo pichani). Katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam, pamoja na mambo mengine wazalishaji hao wa mifuko mbadala wameihakikishia Serikali kuwa wako tayari kuongeza kasi ya usambazaji wa mifuko mbadala kote nchini. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira Nchini Dkt. Samuel Gwamaka. Kulia Dkt. Freddy Manyika Kaimu Mkurugenz Idara ya Mazingira.
   Sehemu ya wazalishaji wa mifuko mbdala wa plastiki kutoka Kampuni mbalimbali wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba (hayupo pichani) katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa  Karimjee Jijini Dar es Salaam, pamoja na mambo mengine wazalishaji hao wa mifuko mbadala wameihakikishia Serikali kuwa wako tayari kuongeza kasi ya usambazaji wa mifuko mbadala kote nchini ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Serikali la kusitisha matumizi ya mifuko ya plastiki hapa nchini ifikapo tarehe 1 Juni 2019.
  Bw. Heneriko Batamuzi kutoka Kampuni ya Kenwood Enterprise (T) Ltd akichangia mada katika kikao cha wadau cha kupitia Rasimu ya Kanuni  za kusimamia Taka Hatarishi hapa nchini. Ofisi ya Makamu wa Rais imeandaa rasimu ya Kanuni mpya za kusimamia Taka Hatarishi nchini ikiwa ni pamoja na ukusanyaji, urejelezaji, uteketezaji na usafirishaji wake ndani na nje ya nchi. Kikao hiki kimefanyika katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika ya Mashariki Martin Ngoga akizungumza na Wawakilishi wa wakulima wadogowadogo waliokutana leo Jijiji Arusha 
  Meneja Kampeni kutoka shirika la Oxfam Tanzania Jovitha Mlay akizungumza juhudi mbalimbali zinazofanywa ili kuwakwamua wakulima wadogo haswa wakina mama ambao ni wengi na wapo zaidi ya 60%duniani kote wanaojishughulisha na Kilimo.
  Elizabeth Ng'imo Katibu wa wakulima wadogo wanawake Afrika na mkulima kutoka Mkoa wa Kati Kenya
  Baadhi ya wawakilishi wa wakulima wadogowadogo kutoka katika Nchi wananchama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa katika ukumbi wa Bunge hilo leo walipokutana Jijini Arusha  Na.Vero Ignatus,Arusha.

  Wawakilishi Wakulima wadogowadogo wa Jumuiya ya Afrika ya mashariki wamekutana na wabunge wa Jumuiya hiyo lengo likiwa ni kujaribu kushwishi nchi wanachama kuongeza bajeti katika sekta ya kilimo

  Martin Ngoga Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika ya mashariki ambapo amesema azimio la Malabo lililosainiwa mwaka 2014 Guinea ya Ikweta kati ya nchi 47 linazitaka nchi za Afrika katika bajeti zake zitenge walau 10%zielekezwe kwenye kilimo

  Ngoga amesema kilimo ndiyo uti wa mgongo wa Nchi za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki na ndicho kinachotegemewa na wananchi walio wengi, hivyo wanajadiliana na wadau wengine kuona ni jinsi gani wanaweza kwenda haraka zaidi katika kutekeleza azimio hilo.


  ''Bado Bunge la Afrika ya Mashariki tunaamini kwamba azimio hilo bado ni muhimu japo kwa bahati mbaya Bunge halijafanya vizuri katika bajeti zao''alisema Ngoga.

  Jovitha Mlay ni Kampeni Meneja kutoka shirika la Oxfam Tanzania amesema wanaungana na wadau wengine kwaajili ya kudai ongezeko la bajeti katika kilimo,pamoja na kuwataka nchi wanachama kutekeleza makubaliano ambayo wamesaini kwenye maazimio ya Malabo. 

  Amesema ripoti iliyotoka inaonyesha nchi kadhaa katika Jumuiya ya Afrika ya mashariki hazijafikia kutenga hiyo 10% jambo ambalo lilitakiwa nchi wanachama ziwe tayari zimetenga na kusimamia ugawaji na matumizi ya fedha hizo katika sekta ya kilimo. 

  Amesema Oxfam lengo lake kubwa ni kuitisha nchi washirika kuhakikisha kwamba wanawekeza kwa wakulima wadogo kwani ndiyo wengi wanalisha,kuzalisha chakula kinacholisha jamii ya nchi wanachama.

  Amesema pia Oxfam inaangalia ushiriki wa wanawake katika utekelezaji na bajeti zinazotengwa kwani wapo zaidi ya 60%ya wakulima duniani kote,pia izingatie maswala ya utafiti,kutokana na mabadiliko ya tabia nchi,mbegu ,madawa na viwatilifu,pembejeo,miundombinu ya maji ambayo ni muhimu .

  Elizabeth Ng'imo Katibu wa wakulima wadogo wanawake Afrika na mkulima kutoka Mkoa wa Kati Kenya amesema kuwa changamoto kubwa katika sekta ya kilimo ni fedha hivyo wanaomba nchi wanachama kujitahidi kutenga hiyo bajeti kwaajili ya kuwasaidia wakulima wadogowadogo 

  Spika wa bunge la Afrika mashariki Martin Ngoga amesema kuwa agenda hiyo itakuwa ni miongoni mwa ajenda ambazo zitajadiliwa katika mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika mashariki unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni. Kikao hicho pia kimehudhuriwa na wadau wa kilimo yakiwepo mashirika yanayojihusisha na kilimo kama vile OXFAM, Action Aid na shirika la Trust Afrika.

  0 0


  Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Iringa, Stephen Mhapa akiwa na mkurugenzi wa halmashauri hiyo Robert Masunya wakati wa baraza la madiwani wakijadili kuhusu athari za wanyama Tembo na Boko
  Madiwani na wataalam wa halmashauri ya wilaya ya Iringa wakiwa kwenye baraza kujadili athari zitikanazo na wanyama Tembo na Boko  NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

  JUMLA ya wananchi saba wameuwawa na mnyama aina ya Boko ndani ya mwezi mmoja katika bwawa la Mtera lililopo katika tarafa ya Ismani halmashauri ya wilaya ya Iringa huku pia mnyama aina ya Tembo akiendelea kuharibu mazao ya wakulima wa halmashauri hiyo.

  Akizungumza katika baraza la madiwani ,diwani wa viti maalum kupitia chama cha mapinduzi kutoka katika tarafa ya Ismani Yusta Kinyanga alisema kuwa mnyama aina ya Boko wamezaliana kwa kasi kubwa na kuwa wengi katika bwawa la Mtera na kusababisha vifo vya wananchi kutoka na wingi wao.

  “Saizi Boko hao wapo wengi mno katika bwawa hili la Mtera na kusababisha vifo vya wananchi ambavyo havina tija yoyote na kupunguza nguvu kazi za taifa kwa kuuwawa na book hao” alisema Kinyanga

  Kinyanga alisema kuwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli aliagiza mamlaka zinazohusika kuhakikisaha wanavuna Boko hao ili kupunguza vifo vya wavuvi wanaofanya shughuli zake katika bwawa hilo.

  “Alipokuwaja Rais hapa nilimweleza juu ya swala hili la Boko na aliziagiza mamlaka husika kushughulikia swala hilo lakini toka alipoondoka Rais hadi sasa wananchi saba wameuuwawa kwa maana hiyo mamlaka husika zimepuuza tamko la Rais na kusababisha vifo hivyo vya wananchi” alisema Kinyanga

  Kinyanga ameiomba mamlaka zinazohusika kuhakikisha wanawavuna Boko hao ili kupunguza vifo vya wananchi vinavyosababisha kuacha wanawake wengi kuwa wajane kutokana na wanaume zao kuuwa na viboko hao.

  “Wanaofanya kazi ya uvuvi ni wanaume ambao kwa asilimia kubwa wameshaoa na wanafamilia hivyo kuuwawa kwa wanaume hao kuwanawacha wanawake kuishi bila wanaume zao hivyo kumpelekea mwanamke huyo kuwa mjane” alisema Kinyanga

  Naye diwani wa kata ya Ilolo mpya,Fundi Mihayo amesema kuwa wanyama wa aina ya tembo wamefanya uharibifu wa mazao wa wananchi wa kata hiyo kutokana na kuwepo kwa kundi kubwa na Tembo ambao wanafanya uharibifu wa mazao ya wananchi.

  “Mwaka huu kundi kubwa hili la tembo hatujui limetoka wapi na limekuja kuleta athari za mazao kwa wananchi wetu na mamlaka husika hakuna jitihada yoyote ile ambayo wanaifanya kuhakikisha wanakabiliana na tembo hao” alisema Mihayo

  Mihayo alisema athari nyingine ambayo imejitokezani kushindwa kwa wanafunzi kwenda shuleni kwa kuhofia kudhuliwa na Tembo ambao wamekuwa wakitembea katika maeneo hao ambao wanafunzi hao ndio njia kuu ya kuelekea shuleni.

  “Saizi wanafunzi wanaogopa hata kwenda shule maana njia zote ambazo wanafunzi huwa wanapita kwenda shule ndio njia ambazo kwa sasa tembo ndio maeneo ambayo wanashinda kutafuta chakula na wameweka makazi yao” alisema Mihayo

  Kwa ujumla mwaka huu hadi hivi sasa Tembo hao wameshafanya uharibifu wa mazao katika kata ya Ilolo Mpya,Nzihi na kata ya Kiwele na kuwaacha wananchi wasijue cha kufanya kutokana na kuwepo kwa Tembo hao.

  Kwa upande afisa maliasilia wa halmashauri ya wilaya ya Iringa Evidence Machenje alisema kuwa serikali imejipanga kuhakikisha wanawavuna Boko kutokana na taratibu na sheria za wanyama pori hivyo tayarai wamewasilisha taarifa hizo kwa wizara na wanasubiri majibu kutoka wizarani.

  “Ni kweli tunataarifa za athari zinazotokana na Boko hao hivyo sisi kama halmashauri hatuna mamlaka ya kuwavuna wanyama hao hivyo ni lazima tuwasiliane na mamlaka husika ili waje wafanyae utalamu wao ndipo lije swala la uvunaji wa Boko hao” alisema Machenje

  Aidha Machenje amekili kuwa Tembo na Boko wamefanya uharibifu mkubwa na kuleta madhara makubwa kwa wananchi lakini kila kitu kinaendeshwa kwa mujibu wa sheria na kanuni za nchi hivyo wananchi wanatakiwa kuwa na subira muda mfupi ujao kila kitu kitakuwa tayari kimefanyiwa kazi.

  Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Iringa, Stephen Mhapa alimwagiza mkurugenzi wa halmashauri hiyo kuhakikisha kuwa matatizo hayo ya wanyama hao yanatafutiwa ufumbuzi mapema iwezekanavyo ili kuokoa maisha ya wananchi

  Hata mimi ni mwadhirika kwenye kata yangu kwa Tembo kuaribu mazao ya wananchi hiki kitendo kinakera hivyo wataalam naombeni fanye haraka kuwasiliana na mamlaka husika kutatua tatizo hilo

older | 1 | .... | 1849 | 1850 | (Page 1851) | 1852 | 1853 | .... | 1898 | newer