Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1847 | 1848 | (Page 1849) | 1850 | 1851 | .... | 1897 | newer

  0 0


  Kamati ya uongozi ya Bunge la Afrika ‘The Pan African Parliament Bureau’ imekutana na Mabalozi ‘Ambassadors’ wanaowakilisha mataifa mbalimbali barani Afrika katika nchi ya Afrika Kusini kujadili masuala kadha wa kadha kuhusu bara la Afrika. 

  Mkutano huo ukiongozwa na Rais wa Bunge la Afrika,Mheshimiwa Roger Nkodo Dang kutoka Cameroon, umefanyika leo Ijumaa Mei 3,2019 katika Ukumbi wa Makao Makuu ya Bunge la Afrika kama sehemu ya mkutano wa maandalizi ya Mkutano wa Pili wa Bunge la Tano la Bunge la Afrika jijini Johannesburg Afrika Kusini.

  Akizungumza wakati wa mkutano huo wa Mabalozi wa Afrika walioidhinishwa na Jamhuri ya Afrika Kusini, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika Mheshimiwa Stephen Masele ambaye ni mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini na Naibu Waziri wa zamani nchini Tanzania alisema Bunge la Afrika litajadiliana na kutoa Azimio juu ya tabia ya Xenophobic nchini Afrika Kusini.

  “Suala hili linapaswa kuchukuliwa kwa umakini, kuna vitendo vya uhalifu vinavyofanywa na vikundi tofauti kutoka nje inaonekana kama Afrika Kusini haitaki wageni katika nchi yao… La hasha lakini kwa undani kuna matendo ya uharifu kwa kivuli cha Xenophobia”,alisema Mhe. Masele.

  “Ninafurahi na kuhamasishwa na hatua zilizochukuliwa na serikali ya Afrika Kusini ili kukabiliana na mambo yote ya uhalifu.Tutakuwa makini sana wakati tunajadiliana jambo hili kwa sababu hatutaki kuingilia kati mambo ya ndani ya Afrika Kusini au kuingilia kati vyombo vya usalama kutekeleza majukumu yao”,aliongeza.

  Masele aliomba mamlaka ya Afrika Kusini kushughulikia suala la tabia ya Xenophobic katika Afrika kwani haikubaliki.

  “Sisi kama Wabunge wa Afrika tunatarajia kuona hatua kali zikichukuliwa dhidi ya waharifu wote, wanaharibu sifa nzuri ya Afrika Kusini na Afrika. Bunge la Afrika litapaza sauti na kukemea suala hili..Vikwazo vya hali yoyote dhidi ya watu binafsi au nchi huumiza watu wasiokuwa na hatia hususani wanawake na watoto na huzuia jitihada za maendeleo za watu wetu na nchi ambazo zina vikwazo”,aliongeza.

  Kikao cha Pili cha kawaida cha Bunge la Tano la Afrika kinatarajiwa kuanza mnamo Mei 6, 2019 huko Midrand - jijini Johannesburg Afrika Kusini.

  Pamoja na mambo mengine , watajadiliana juu ya Kauli mbiu ya Umoja wa Afrika ya mwaka huu "Mwaka wa Wakimbizi na Watu Waliopotea",ambapo pia Bunge la Afrika litajadili Suluhisho la Kudumu juu ya tatizo la wakimbizi barani Afrika.

  Hali kadhalika Bunge hilo, litajadili taarifa juu ya amani na usalama katika bara la Afrika ikiwa ni pamoja na maendeleo ya hivi karibuni na hali ya kisiasa Libya, Sudan, Algeria na mchakato wa amani nchini Sudan Kusini.

  Masele anahimiza pande zote zinazohusika katika majadiliano ya amani zisiwe na upendeleo kwa lengo la kutimiza ahadi zilizotolewa kwa watu wa Afrika. Angalia picha za matukio wakati wa mkutano Wajumbe wa Kamati ya uongozi ya Bunge la Afrika na Mabalozi wanaowakilisha mataifa mbalimbali barani Afrika katika nchi ya Afrika Kusini wakiwa kwenye mkutano leo Ijumaa Mei 3,2019 jijini Johanesburg Afrika Kusini. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika Mheshimiwa Stephen Masele akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Makao Makuu ya Bunge la Afrika,Midrand,Johanesburg,Afrika Kusini. Rais wa Bunge la Afrika,Mheshimiwa Roger Nkodo Dang kutoka nchi ya Cameroon akizungumza wakati wa mkutano wa Kamati ya uongozi ya Bunge la Afrika na Mabalozi wa nchi za Afrika nchini Afrika Kusini. Kulia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika Mheshimiwa Stephen Masele akiandika dondoo muhimu wakati wa mkutano wa Kamati ya uongozi ya Bunge la Afrika na Mabalozi wa nchi za Afrika nchini Afrika Kusini. Wajumbe wa Kamati ya uongozi ya Bunge la Afrika na Mabalozi wanaowakilisha mataifa mbalimbali barani Afrika katika nchi ya Afrika Kusini wakiendelea na mkutano. Wajumbe wa Kamati ya uongozi ya Bunge la Afrika na Mabalozi wanaowakilisha mataifa mbalimbali barani Afrika katika nchi ya Afrika Kusini wakiwa wamesimama kuwakumbuka watu waliofariki dunia kutokana na majanga yaliyotokea katika baadhi ya nchi za Afrika yakiwemo mafuriko na Kimbunga Keneth. Mkutano ukiendelea. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

  0 0

  Waziri Mkuu Mstaafu Mzee John Malecela na mkewe Mhe Anna Kilango-Malecela wakiwa wamemtembelea kumjulia hali mwana wao William Malecela maarufu kama Le Mutuzu Super Brand aliyelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete jijini Dar es salaam kwa matibabu leo Jumapili Mei 5, 2019

  0 0

  Na Woinde Shizza Michuzi Tv, Arusha

  Mkuu Wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo wakishirikiana na mkuu wilaya ya Arumeru jana wamegawa vitambulisho vya kufanya biashara kwa wafanya biashara wadogo wadogo (machinga) hii ikiwa ni awamu ya pili yaugawaji.

  Mkuu wa mkoa huyo pia alikabidhi wilaya ya Arumeru vitambulisho vya machinga Elfu kumi ambavyo vitagawiwa kwa halmashauri mbili zilizopo ndani ya wilaya ya Arumeru ambapo kila halmashauri imekabidhiwa vitambulisho 5000.

  Akizungumza kuhusiana na ugawaji huo, Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro alisema kuwa hii ni awamu ya pili ya ugawaji wa vitambulisho ,
  awamu ya kwanza waligawa nahii ni awamu yapili wamepokea vitambulisho elfu 10 kutoka kwa mkuu wa mkoa kwaajili ya kuwapatia wafanyabiashara wadogo wadogo.

  Alisema kwa jana tu katika soko la Tengeru wamegawa vitambulisho 1000 kwa wafanyabiashara na wataendelea kuvigawa Hadi wafanyabiashara wote wavipate

  "kama mnavyoona mimi na timu yangu yote tumeingia sokoni na tumefanyakazi mmeona watendaji wangu wa kata wafanyakazi wa halmashauri wote bila kujali cheo tumeingia kugawa vitambulisho vya machinga na tumegawa vitambulisho 1000 natunaendelea kugawa katika masoko yote"alisema Muro

  Alimshukiru mkuu wa mkoa wa Arusha kwenda kuwapa ushirikiano katika zoezi hilo kwani amewapa motisha ya kutosha.

  Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Ariana Mrisho Gambo alisema ameamua kuwapamotisha ya ugawaji wa vitambulisho wafanyakazi wa wawilaya hiyo.
  Picha ikionesha Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro wa kwanza kulia akimkabidhi mkurugenzi wa halmashauri ya Arusha Dr. Wilson  Mahera vitambulisho 2500 Kwa ajili ya kuwagawia wafanyabiashara wadogo wa halmashauri yake

  0 0

   Mwenyekiti wa Tasisi ya Tushikamane Foundation, Rosemary Mwapachu, akizungumza na wadau na Marafiki wa Taasisi hiyo waliofika katika hafla fupi ya kuchangia gharama za Wazee wanaohudumiwa na taasisi hiyo
   Jaji Mstaafu Mark Bomani akieleza na kutoa ushuhuda juu ya taasisi hiyo ilivyokuwa msaada kwa wazee na kutaja kuwa kitu wanachokifanya ni kikubwa zaidi kuliko watu wengine
   Balozi Juma Mwapachu akimpongeza Mkewe Bi Rose Mwapachu kwa kufanya vizuri katika ujenzi wa nyumba ya Wazee na kufanikisha Harambee kwa ajili ya mahitaji ya wazee hao kwa mwezi
   Sehemu ya Washiriki wa Harambee hiyo wakifuatilia kwa makini namna mambo yanavyoenedelea

  0 0

  Na Ripota Wetu,Michuzi TV.

  ALIYEKUWA Katibu Kata wa Chama cha Wananchi (CUF) kata ya Makurumla, Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam, Chahasi Shomari amekihama chama hicho na kuhamia Chama Cha Mapinduzi(CCM).

  Chahasi amerudisha kadi ya CUF na kukabidhiwa ya CCM leo na Katibu wa Siasa na Oganaizesheni wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, Cholaje Mohamed katika mafunzo ya viongozi wa jumuiya hiyo ngazi ya kata.

  Akizungumza baada ya kukabidhiwa kadi hiyo, Chahasi amesema amefanya uamuzi wa kuhamia CCM kutokana na haki walizokuwa wakizipigania akiwa CUF kuanza kutekelezwa na Rais Dk. John Magufuli pamoja na mshikamano uliopo ndani ya chama hicho tawala.

  Amesema Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahimu Lipumba amekuwa akipigania haki za kiuchumi hasa kwa wafanya biashara wadogo ambapo sasa wametambulika na serikali.

  “Kwa sasa machinga tumeanza kupata neema ya kutekeleza shughuli zetu bila kubughudhiwa na sasa tumepatiwa vitambulisho vya kutambua shughuli zetu,” amesema Chahasi. Ameongeza kuwa Mungu amemteua Rais Magufuli kuwakomboa wanyonge hivyo Watanzania hawana budi kumuunga mkono.

  Aidha aliwataka kundi alilokuwa anafanya nalo kazi maarufu kama Mungiki kumuunga mkono uamuzi wake kwa kuwa siasa zinabadilika na kila mmoja anahitaji maisha bora, uchumi na maendeleo kwa Taifa.

  Kwa upande wake Cholaje amesema wanaamini Chahasi atakuwa na msaada mkubwa katika CCM kwa kuwa ataonesha mapungufu waliyonayo vyama vya upinzani kwa kusaidia kuyaeleza kwa wananchi.

  “Ni siku ya neema kwa ngazi zote za chama kuanzia tawi hadi taifa kwa kuwa tumemchukua mpiganaji wa CUF ambaye alikuwa msaada mkubwa kwa Lipumba,” amesema Cholaje.

  Aliongeza kuwa wanatarajia Chahasi atakuwa sehemu ya Kampeni kuanzia kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa. Chahasi amekuwa mwanachama wa CUF tangu mwaka 1999 na anatajwa kuwa alikuwa ni sehemu ya wanamkakati wa waliofanikisha ushindi wa udiwani wa sasa kupitia CUF katika Kata ya Makurumla, Omari Kombo ‘Kijiko’.


  Aliyekuwa Katibu wa Chama cha Wananchi (CUF), Kata ya Makurumla, Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam, Chahasi Shomari, akikabidhi kadi ya chama hicho kwa Katibu wa Siasa na Oganaizesheni wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, Cholaje Mohamed.
  Aliyekuwa Katibu wa Chama cha Wananchi (CUF), Kata ya Makurumla, Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam, Chahasi Shomari, akipa kiapo cha uaminifu kwa chama pamoja na viongozi wa CCM.
  Aliyekuwa Katibu wa Chama cha Wananchi (CUF), Kata ya Makurumla, Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam, Chahasi Shomari, akisindikizwa kuingia ukumbini na mmoja wa viongozi wa CCM.
  Katibu wa Siasa na Oganaizesheni wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, Cholaje Mohamed, akizungumza na wana CCM baada ya kukabidhi kadi kwa aliyekuwa Katibu wa CUF Makurumla, Shomari Chahasi.

  0 0

   Basi la Kilimanjaro lenye namba za usajili  T 983 AWY limepinduka jioni ya leo mbele ya eneo la MKATA, Tanga. Basi hilo lilikuwa likitokea  jijini Arusha kuelekea jijini Dar es Salaam. Kwa mujibu wa mashuhuda walioshuhudia ajali hiyo wameeleza kuwa katika ajali hiyo hakuna aliyepoteza maisha eneo la tukio zaidi ya majeruhi kadhaa,Wakielezea zaidi mbele ye Michuzi TV kuhusu chanzo cha ajali hiyo,wakabainisha kuwa chanzo ni mwendo kasi wa basi hilo.

  Tutawaletea zaidi  taarifa kamili kutoka Mamlaka husika.
  Baadhi ya Abiria waakiangalia baadhi ya majeruhi na ukaguzi wa mizigo yao kufuatia basi hilo kupinduka maeneo ya Mkata,likiwa linatoka  Mkoani Arusha kuelekea jijini Arusha.
  Baadhi ya abiria walionusurika katika ajali hiyo wakitoa msaada kwa majeruhi
  Baadhi ya Abiria waakiangalia baadhi ya majeruhi na ukaguzi wa mizigo yao kufuatia basi hilo kupinduka maeneo ya Mkata,likiwa linatoka  Mkoani Arusha kuelekea jijini Arusha.
  Basi la Kilimanjaro lenye namba za usajili T 983 AWY likiwa limepinduka mbele ya eneo la MKATA, Tanga,hakuna aliyepoteza Maisha.


  0 0

  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamiii

  Wito umetolewa kwa Serikali na watunga sera kuhakikisha wanapitia upya na kufanya mabadiliko katika sheria ya usalama barabarani hili kuweza kudhibiti ajali zinazotokana na uzembe wa watu kwa makusudi.

  Wito huo umetolewa jijini Dar es Salaam leo na Kaimu Mkurugenzi wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania(TAWLA),Mary Richard alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari juu ya maadhimisho ya wiki ya usalama barabarani kwa umoja wa mataifa.

   "sheria hiyo kwa sasa ina mapungufu mengi kiasi mtu akikutwa na kosa adhabu zake ni za kawaida na makosa mengi yamebainishwa katika kanuni badal aya sheria yenyewe ametaja sheria hii inamtaja mtu aliyekaa siti ya mbele na Dereva ndio wanapaswa kufunga mkanda wakati kanuni inataja abiria wote wafunge mkanda jambo ambalo lina ukakasi kidogo"amesema Mary.

  Mary ametaja kuwa sheria hii ya Sasa inaseama Dereva wa pikipiki ndio anapswa kuvaa kofia ngumu peke yake wakati sasa jeshi la Polisi ketengo usalama barabarani wameweka kanuni Dereva na abairia ndio wanapaswa kuvaa kofia hivyo ni bora vitu vyote hivi vingewekwa kwenye sheria hivyo tunaomba mamlaka zinazousika pamoja na Wizara ya Mambo ya ndani waangalie utaratibu wa kubadilisha sheria hii.

  kwa upande wake Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma , Fatma Toufiq amesema kuwa ajali za barabarani zinaepikika kama watanzania wote wataweza kufata sheria na kuwa makini pindi wanapoendesha vyombo vya moto.

  amesema kuwa yeye kama mbunge anayeshiriki katika kutunga sheria atasimama kidete kuhakikisha sheria hii mpya ya usalama barabarani inapatikana hli tuweze kupunguza takwimu za ajali na walemavu wakudumu wanaotokana na ajali za barabarani
   Kaimu Mkurugenzi wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania(TAWLA),Mary Richard akizungumza na Waandishi juu wiki ya usalama barabarani 
  Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma , Fatma Toufiq, akieleza ushuhuda wake kwa waandishi wa habari juu ya ajali ilivyoweza kumletea cahangamoto ya utendaji katika kazi

  Mratibu wa Usalama Barabarani kutoka shirika la umoja wa Mataifa la WHO,Mary Kessy akizungumza mpango wa shirika lake katika kudhibiti usalama barabarani
   
  Muwakilishi wa Mabalozi wa Usalama Barabarani(RSA),John Seka akieleza namna taasisi yao ilivyojipanga na inavyoshirikiana na jeshi la Polisi kutoa taharifa za watu wanaokiuka sheria za Usalama Barabarani
  Sehemu ya Waandishi wa habari walioshiriki Mkutano kuhusu Masuala ya Usalama barabarani leo jijini Dar es Salaam uliofanyika katika ukumbi wa Tamwa


  0 0


  0 0

  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein amewanasihi wafanyabiashara kuwa waadilifu katika kuwafanyia wanunuzi tahafifu za bei za bidhaa na huduma nyenginezo hasa katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

  Alhaj Dk. Shein aliyasema hayo katika risala maalum aliyoitoa kwa wananchi kupitia vyombo vya habari katika kuukaribisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani katika mwaka huu wa 1440 Hijria sawa na mwaka 2019 Miladia.

  Katika risala yake hiyo, Alhaj Dk. Shein aliwataka wafanyabiashara kukumbuka kwamba kwa kufanya hivyo hawatokula hasara bali watazidi kupata fadhila mbali mbali za Mola wao Mlezi zinazoambatana na Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

  Aidha, aliwataka wakulima waendelee na ustaarabu pamoja na utamaduni wao ule ule wa ustahamilivu na uadilifu kwa kujiepusha na tabia ya uvunaji na uuzaji wa mazao machanga.

  Rais Dk. Shein aliongeza kuwa lengo la Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar si kumkomoa mtu kwa sababu Serikali huwa haiwakomoi wananchi wake bali dhamira yake ni kuwalinda na kuona kwamba hawafikwi na matatizo ambayo yanaweza kuepukika na kujikinga nayo. 

  Pamoja na hayo, Alhaj Dk. Shein alitoa nasaha zake kwa wale ambao si Waislamu na wale ambao watakuwa na dharura zinazowazuwia wasifunge kuwa wasifanye vitendo vitakavyoathiri wanaofunga.

  Alhaj Dk. Shein alisisitiza haja ya kuhimizana zaidi kuisoma Qur-an kwa wingi ndani ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani pamoja na kujitahidi kufahamu mantiki ya maelekezo yake.

  Aliwataka waumini kuhimizana kuhudhuria darsa katika misikiti ndani ya mwezi wa Ramadhani na kuepuka kutumia muda kwa kufanya mambo yasiyo na manufaa katika mwezi huo ambayo yanapingana na mafunzo ya Uislamu na silka zao.

  Sambamba na hayo, Rais Dk. Shein aliwatakia kila la heri Wajumbe wote wa Baraza la Wawakilishi wakiongozwa na Spika Zubeir Ali Maulid katika Mkutano wao wa 14 wa Baraza la Tisa la Wawakilishi utakaojadili Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa Fedha wa 2019-2020.
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein

  0 0  0 0

   Hivi ndivyo hali ilivyokuwa katika maeneo mengi hapa jijini Dar es Salaam na mkoa wa Pwani kutokana na Mvua  kubwa iliyonyesha jana, ambapo  barabara nyingi za Dar zilijaa maji hali iliyosababisha baadhi ya magari  kuharibika na pia kusabaisa foleni kubwa ya magari,lakini pia inaonesha mitaro mingi ya kupitisha maji machafu kati kati ya jiji imeziba,hali inayochangia pia kutuama kwa maji.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi  Tv)


  Limezima anasubiriwa fundi
   Gari likiwa limehariika katikati ya barabara ya Kilwa kata ya Mandege mkoa wa Pwani.
   Kama ionekanavyo pichani hapa wananchi  wakisukuma gari baada ya kukwama kwenye matope kufuatia Mvua zilizoanza kunyesha wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi  Tv)

  0 0

  Makamu wa Rais wa Kwanza wa Bunge la Afrika,Mheshimiwa Stephen Masele akipokelewa na mwenyeji wake,Balozi wa UAE,nchini Afrika Kusini Mahash Saeed Alhameli kabla ya kikao cha majadiliano ya ushirikiano baina ya ujumbe wa Bunge la Afrika na ujumbe kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu (United Arab Emirates- UAE) jana Mei 5,2019 jijini Pretoria,Afrika Kusini.
  Kushoto ni Makamu wa Rais wa Kwanza wa Bunge la Afrika,Mheshimiwa Stephen Masele akizungumza tete-a-tete na Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (United Arab Emirates- UAE),nchini Afrika Kusini Mahash Saeed Alhameli.
  Makamu wa Rais wa Kwanza wa Bunge la Afrika,Mheshimiwa Stephen Masele akiongoza kikao cha majadiliano kuhusu ushirikiano wa bunge la Afrika na Bunge la Umoja wa Falme za Kiarabu (United Arab Emirates- UAE) ambapo Ujumbe wa Bunge la UAE umeongozwa na Spika wa Bunge la Umoja wa Falme za Kiarabu (United Arab Emirates- UAE), Dk. Amal Abdulla Al Qubaisi ,kwa pamoja wamekubaliana mambo ya msingi ya kushirikiana baina ya mabunge hayo.
  Makamu wa Rais wa Kwanza wa Bunge la Afrika,Mheshimiwa Stephen Masele akiagana na mwenyeji wake,Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (United Arab Emirates- UAE),nchini Afrika Kusini Mahash Saeed Alhameli.

  0 0

   Shirika lisilokuwa la kiserikali Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) limeshiriki maadhimisho ya siku ya mkunga duniani kwa kutoa huduma ya uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi kwa akina mama pamoja na upimaji wa Virusi Vya Ukimwi (VVU) mkoani Simiyu.


  Maadhimisho hayo kitaifa yamefanyika Mei 5, 2019 kwenye uwanja wa michezo wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt Faustine Ndugulile akimwakilisha Makamu wa Rais,Mhe. Samia Suluhu Hassan. 

  Mratibu wa Shirika la AGPAHI mkoa wa Simiyu Dafrosa Charles,alisema shirika la AGPAHI limeshiriki maadhimisho ya siku ya mkunga duniani kwa kutoa huduma ya uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi kwa akina mama pamoja na upimaji wa Virusi Vya Ukimwi (VVU). 

  Amesema kati ya akina mama 205 waliowafanyia uchunguzi wa saratani hiyo ya mlango wa kizazi, wawili waligundulika kuwa na tatizo hilo na wamepatiwa rufaa ya kwenda kutibiwa kwenye hospitali ya rufaa Bugando Jijini Mwanza, huku 166 waliowapima VVU, mmoja kati yao amebainika kuwa ana maambukizi ya VVU na ameanzishia huduma ya dawa za kupunguza makali ya VVU. 

  Aliongeza kuwa Saratani hiyo ya mlango wa kizazi kwa sasa ndiyo imekuwa ikisababisha vifo vingi vya akina mama wakati wa kujifungua kutokana na kuvuja damu kwa wingi na kuwataka akina mama wajenge tabia ya kupima afya zao mara kwa mara ili waweze kupata matibabu mapema na ili kumaliza vifo hivyo. Baadhi ya akina mama waliopatiwa huduma kwenye banda la Shirika la AGPAHI akiwemo Pendo Mboje, wamelipongeza Shirika hilo kwa kuwapelekea huduma hiyo, ambapo walikuwa hawajui visababishi vya kuugua saratani ya mlango wa kizazi pamoja na athari zake na kuahidi kujilinda zaidi na kwenda kutoa elimu kwa wenzao.

  Maadhimisho hayo ya siku ya mkunga dunia kitaifa hapa nchini yamefayika mkoani Simiyu yakiwa na kaulimbiu isemayo,”Wakunga watetezi wa haki za wanawake”. Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile alimewataka wakunga kuendelea kutoa huduma nzuri kwa akina mama wajawazito na kuwaasa kuacha tabia ya kuwatolea lugha chafu ili kuongeza idadi kubwa ya wanawake kupenda kujifungulia kwenye vituo vya afya hali ambayo itapunguza tatizo la vifo vitokanavyo na uzazi.

   “Licha ya Serikali kupunguza tatizo la vifo vya mama na mtoto vitokanavyo na uzazi bado hali siyo ya kuridhisha ambapo awamu hii ya tano tumedhamiria kabisa kumaliza changamoto hiyo kwa kuhakikisha tunaendelea kuboresha huduma za afya hasa za mama na mtoto,”aliongeza. Rais wa Chama cha Wakunga Tanzania (TAMA) Feddy Mwanga, alisema kilianzishwa mwaka 1992 kwa lengo la kuunganisha wakunga wasajiliwa nchini ili kuwa na nguvu moja katika kupambana kumaliza tatizo la vifo vya mama na mtoto vitokanavyo na uzazi wakati wa kujifugua. 

  “Hapa mkoani Simiyu Chama cha Wakunga Tanzania kimeadhimisha siku hii kuanzia Mei 3 hadi leo Mei 5,2019 kwa kushirikiana na wadau wenzetu ambao wametoa huduma mbalimbali za afya ukiwamo upimaji wa VVU, huduma za uzazi wa mpango na uchuguzi wa saratani ya mlango wa kizazi na matiti,”alisema Mwanga. Naye katibu tawala wa mkoa wa Simiyu Jumanne Sagini alisema takwimu za vifo vya mama na mtoto vitokanavyo na uzazi kuwa vimepungua ambapo mwaka 2017 vilikuwa 48 ambapo mwaka 2018 vilitokea vifo 40 na kubainisha kuwa tatizo ni kuwapo kwa upungufu wa wakunga .
   Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Faustine Ndugulile akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya mkunga duniani yaliyofanyika kitaifa mkoani Simiyu na kuwataka wakunga kufanya kazi kwa kuzingatia maadili na kuacha lugha za matusi kwa wajawazito ili kuhamasisha kujifungulia kwenye huduma za kiafya na ili kumaliza vifo vitokanavyo na uzazi.Picha na Marco Maduhu- Malunde 1 blog  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt Faustine Ndugulile (wa pili kulia) akiwa na viongozi wa mkoa wa Simiyu kwenda kukagua mabanda ya wadau wa sekta ya afya likiwemo shirika la AGPAHI ambao wametoa huduma mbalimbali za kiafya kwenye maadhimisho hayo ya siku ya mkunga duniani yaliyofanyika kitaifa mkoani Simiyu.  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt Faustine Ndugulile akiwa kwenye banda la Shirika la AGPAHI akipewa maelezo na Mratibu wa AGPAHI mkoa Simiyu Dafrosa Chalres namna linavyotoa huduma ya uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi kwa akina mama pamoja na kuwapima maambukizi ya VVU na kuanza kuwapatia huduma wale ambao wanagundulika kuwa na magonjwa hayo.  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt Faustine Ndugulile , akipokea kijizuu kwenye banda la Shirika la AGPAHI.  Muuguzi mkunga Conchesta Alexander kutoka kituo cha afya Muungano Bariadi mkoani Simiyu, akitoa elimu kwa akina mama mkoani humo juu ya kujikinga na saratani ya mlango wa kizazi ugonjwa ambao unaua akina mama wengi wakati wa kujifungua.  Muunguzi mkunga kutoka kituo cha afya muungano Bariadi , Elizabeth Holela akitoa elimu kwa akina mama juu ya saratani ya mlango wa kizazi, madhara yake pamoja na namna ya kujikinga.  Muuguzi mkunga kutoka hospitali ya mkoa wa Simiyu Conchesta Alexander akiendelea kutoa elimu kwa akina mama mkoani humo kwenye Banda la AGPAHI namna ya kujiepusha na magonjwa ya saratani ya mlango wa kizazi.  Akina mama mkoani Simiyu wakiwa kwenye Banda la Shirika la AAGPAHI kupewa elimu ya saratani ya mlango wa kizazi, ili kutokomeza vifo vya mama na mtoto vitokanavyo na uzazi.  Akina mama mkoani Simiyu wakiwa kwenye Banda la Shirika la AGPAHI kupewa elimu ya saratani ya mlango wa kizazi, ili kutokomeza vifo vya mama na mtoto vitokanavyo na uzazi.  Mratibu wa Shirika la AGPAHI mkoani Simiyu Dafrosa Charles akitoa elimu kwa mmoja wa wanaume mkoani Simiyu namna ya kumkinga mke wake kutopata saratani ya mlango wa kizazi.  Muuguzi mkunga Mwaisha Yoma kutoka kituo cha afya Muungano Bariadi akichukua maelezo kwa mmoja wa akina mama ambaye amejitokeza kufanyiwa uchuguzi wa saratani ya mlango wa kizazi kutoka kwenye Banda la AGPAHI.  Pendo Mbonje ambaye ni mmoja wa akina mama mkoani Simiyu ambao wamejitokeza kufanyiwa uchunguzi wa Saratani ya mlango wa kizazi katika banda la AGPAHI, wakati wa maadhimisho ya ukunga duniani yaliyofanyika kitaifa mkoani humo Simiyu.  Seke Ndongo akielezea namna alivyofanyiwa uchuguzi wa Saratani ya mlango wa kizazi na alivyopewa elimu ya kujikinga na saratani hiyo. 
   Katibu tawala wa mkoa wa Simiyu Jummane Sagini akiiomba wiraza ya afya impatie wauguzi wakunga ili kukabiliana na tatizo la vifo vya uzazi mkoani humo, ambapo kwa mwaka jana walipoteza maisha akina mama 40.  Rais wa Chama cha Wakunga Tanzania Feddy Mwanga akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya mkunga duniani kitaifa mkoani Simiyu, na kuelezea malengo ya maadhimisho hayo kufanyika mkoani Simiyu kuwa ni kuunganisha nguvu za pamoja kupambana kumaliza tatizo la vifo vya mama na mtoto vitokanavyo na uzazi.  Wakunga wakiwa kwenye maadhimisho yao kitaifa mkoani Simiyu wakisikiliza nasaha za Naibu waziri wa afya ,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Faustine Ndugulile namna ya kuzingatia maadili ya kazi yao kiufasaha ili kutokomeza vifo vya uzazi.  Wananchi mkoani Simiyu wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya mkunga duniani mkoani humo.  Awali naibu waziri wa afya maendeleo ya jamiim jinsia wazee na watoto Dkt Faustine Ndugulile mwenye kaunda suti akipokea maandamano ya wakunga kwenye maadhimisho hayo kitaifa mkoani Simiyu.  Wakunga wakiingia kwa maandamano kwenye uwanja wa michezo wa halmashauri ya mji wa Bariadi wakitokea kwenye kituo cha afya cha Muungano mjini Bariadi.  Wauguzi wakunga nao hawakuwa nyuma kutoa burudani kwenye maadhimisho yao ya siku ya mkunga duniani, yaliyofanyika kitaifa mkoani Simiyu.  Wakunga wakiendelea kutoa burudani. Picha na Marco Maduhu- Malunde 1 blog

  0 0

   Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Hosiptali ya CCBRT, Brenda Msangi akitoa mada yake wakati wa kongamano la mwanamke kwenye ushawishi kufikia ndoto ya  mafanikio kimaendeleo jijini Dar es Salaam.HABARI PICHA/NA PHILEMON SOLOMON
  ............................................................
  WANAWAKE nchini wametakiwa kujitambua jambo litakalo wasaidia kujiepusha na vitendo vya ngono maofisini.

  Ombi hilo limetolewa na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Brenda Msangi wakati akitoa mada katika kongamano la mwanamke kwenye ushawishi kufikia ndoto ya  mafanikio kimaendeleo lililofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

  Alisema masuala ya unyanyasi wa kingono maofisi yapo lakini yanashindwa kuweka hadharani kwa kuwa yanafanyika kisiri na walengwa wakubwa wakiwa ni wanawake.

  "Wanawake tunatakiwa kujitambua kuanzia uvaaji wetu, jinsi tunavyozungumza hali hiyo itaondoa dhana ya kuwa sisi wenyewe tunapenda kufanyiwa vitendo hivyo.

  Alisema kumekuwa na vitendo vya unyanyasaji wa kingono maofisini lakini kupitia kongamano ili tunaweza kupiga hatua ya kukabiliana na changamoto hiyo na ndio maana baadhi ya washiriki, wakurugenzi kutoka katika makampuni.

  Msangi alisema kukiwepo na mifumo mizuri maofisini itasaidia kujua namna ya kumsaidia muathirika wa vitendo hivyo na hatua za kuchukua.

  "Mwanamke akijengwa kifikra na kuwa na uthubutu anaweza kuwa na maendeleo makubwa kiuchumi kuanzia ngazi ya familia na Taifa kwa ujumla.

  Mmoja wa wakurugenzi wa shirika hilo, Emelda Mwamanga alisema kwa zaidi ya miaka 10 tangu waanzishe shirika hilo mwaka 2008 wamekuwa wakitoa mafunzo ya kuwajengea uwezo wanawake wa kibiashara na kufanya matamasha mbalimbali kwa ajili ya kuibua vipaji ili  kuwainua kiuchumi.

  Kongamano hilo liliandaliwa na Shirika la Woman of Influence la jijini Dar es Salaam.
   Meneja Mipango na Usimamizi wa Utendaji Afrika Mashariki kutoka Kampuni TBL,Nancey Riwa  (kushoto) akichangia mada wakati wa kongamano hilo (katika) Mkurugenzi wa Uhusiano kutoka VodaCom, Rosalynn Mworsia, na kulia Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Hosiptali ya CCBRT, Brenda Msangi.
   Program Meneja Mwandamizi kutoka Kampuni ya Trade Mark, Monica Hangi (aliyesimama kushoto) akifurahia jambo wakati akichangia mada.
   Kongamano likiendelea.

  0 0

  Na Editha Edward- Michuzi TV,Tabora

  Kamati ya Ulinzi na usalama kupitia jeshi la polisi mkoa wa Tabora limeahidi Kuongeza nguvu ya Ulinzi na usalama katika Soko kuu la Madini mkoa wa Tabora kwa kutumia mbinu za kiteknolojia na kuimarisha Ushirikiano dhidi ya Wachimbaji wadogo na Serikali lengo ikiwa ni kuhakikisha wauzaji na wanunuzi wa Madini wote wanakuwa na Ulinzi na usalama dhidi ya biashara hiyo

  Yamesemwa hayo hii leo mjini Nzega Mkoani Tabora katika Ufunguzi wa soko la Madini ambalo limejengwa kisasa huku likizingatia Weledi wa juu pamoja na kutekeleza agizo la Serikali ya Awamu ya Tano

  Kamanda wa polisi mkoa wa Tabora Kamishina Msaidizi Mwandamizi Emmanuel Nley amesema biashara hiyo itakuwa safi na salama Kamati ya Ulinzi imejipanga kuimarisha suala hilo kwa vitendo zaidi

  "Soko kuu la kununua na kuuza dhahabu litaimarishwa sana kutakuwa na Askari wa aina mbili Askari wanaovaa Uniform watakuwa hapa na Askari wanaovaa kiraia watakuwa hapa katika jengo hili na zitafungwa teknolojia zilizoimatishwa kutakuwa na CCTV Camera na vyombo vya moto kwa hiyo katika jengo hili kutakuwa na Usalama "Amesema Nley

  Kwa upande wake katibu Tawala mkoa wa Tabora Robert Makungu amesema soko hilo limezingatia vigezo vya kibiashara kwani huduma za kifedha zinapatika bila usumbufu wowote

  Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amesema hatarajii kusikia watu wanatorosha Madini ."Sitaki kusikia mtu anakamatwa kwa kosa la kutorosha Madini atakayekamatwa atachukuliwa hatua za sheria na mtu huyo atakayefanya hivyo ujue hataki maendeleo ya nchi "Amesema Mwanri

  Aidha Serikali ya mkoa wa Tabora imeendelea kuwatoa hofu wauzaji na Wafanyabiashara wa kuwauzia Madini katika soko hilo ambapo imesema bei itakuwa ni rafiki na hakutakuwa na ubabaishaji na soko hilo litawasaidia Wafanyabiashara wa Madini kutokwenda nje ya mkoa kuuza madini yao kwani soko hilo limekidhi kila kitu.
  Pichani ni Soko kuu la madini la  Mkoani Tabora lililopo Mjini Nzega  Tabor.

  0 0

  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, MOROGORO

  MKUU wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Steven Kebwe, amewaasa madaktari kufanya tathmini ya magonjwa na ajali zitokanazo na kazi kwa kuzingatia miongozo iliyopo.

  Dkt. Kebwe alitoa wito huo leo Mei 6, 2019 wakati akifungua mafunzo ya siku tano kwa madaktari na watoa huduma za afya kuhusu namna ya kufanya tathmini ya magonjwa na ajali zitokanazo na kazi mjini Morogoro.

  Mafunzo hayo yameandaliwa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) na zaidi ya madaktari 100 kutoka mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani, Dar es Salaam na Morogoro wanashiriki mafunzo hayo.

  “Mnapofanya tathmini vizuri mnausaidia Mfuko kulipa fidia stahiki, mfanye tathmini kwa haki, msije mkaingia kwenye mtego msikubali kurubuniwa na huu ndio wito wangu kwenu.” Alisema

  Dkt. Kebwe aliupongeza Mfuko kwa hatua iliyofikia hususan katika eneo la kutoa elimu kwa wadau kama madaktari ambao ndio huuwezesha Mfuko kutekeleza wajibu wake wa ulipaji Fidia kwa usahihi.“Kwa sasa tayari mmetoa mafunzo kwa madaktari 764 kote nchini na leo hii idadi nyingine inaongezeka hili ni jambo ambalo mnastahili pongezi kwa kufikia hatua hii katika muda mfupi wa uhai wa Mfuko.” Alisema Dkt. Kebwe.

  Alisema Mfuko huu ni muhimu katika nchi yetu katika kipindi hiki ambacho taifa linajenga uchumi wa viwanda.Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba alisema licha ya kutoa mafunzo hayo, lakini pia Mfuko hutumia fursa hiyo kuwaelimisha kuhusu shughuli za Mfuko.

  Alisema mafunzo hayo yatatolewa na wataalamu kutoka Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi kwa kushirikiana na watalamu kutoka Taasisi ya Mifupa MOI na MUHAS.

  Aidha Bw. Mshomba alimpongeza Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuona umuhimu wa kipekee katika kujenga uchumi wa viwanda kwa kuweka kipaumbele kwa nchi yetu kama namna ya kutufikisha kwenye uchumi wa kati ifikapo 2020-2025 kwani ni ukweli ulio wazi kwamba hakuna nchi iliyoendelea Duniani bila ya kuwa na uchumi wa viwanda na nilazima wote kama watanzania tusimame pamoja kumsaidia Mhe. Rais.

  “Sisi kama Mfuko tutamsaidia Mhe. Rais katika azama yake kwa kuahkikisha kwamba, tunafanya kazi kwa ufanisi ikiwa ni pamoja na kuwaelimisha na kuwakinga wafanyakazi kwa kutoa elimu ili kuhakikisha kwamba tunalinda nguvu kazi ya taifa kwa kuzuia ajali makazini au kuzipunguza na hata zinapotokea basi malipo ya Fidia yanafanyika kwa haraka”. Alisema.
  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Steven Kebwe, akitoa hotuba ya ufunguzi wa mafunzo ya siku tano kwa madaktarina watoa huduma za afya kuhusu namna ya kufanya tathmini ya magonjwa na ajali zitokanazo na kazi mjini Morogoro leo Mei 6, 2019. Mafunzo hayo ambayo yamewaleta pamoja madaktari kutoka hospitali na umma na binafsi kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Lindi na Mtwara yameandaliwa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF).
  Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, akitoa neon la utangulizi.
  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Steven Kebwe (wapili kulia), akipeana mikono na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Masha Mshomba, mara baada ya kufungua mafunzo ya siku tano kwa madaktari n a watoa huduma za afya kuhusu namna ya kufanya tathmini ya magonjwa na ajali zitokanazo na kazi. Mafunzo hayo yaliypowaleta pamoja Zaidi ya madaktari 100 kutoka mikoa mitano imeanza leo Mei 6, 2019 mjini Morogoro. Wakwanza kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Ttahmjni wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omary.Mkurugenzi wa Uendeshaji WCF, Bw. Anselim Peter, akitoa mada kuhusu kazi za Mfuko
  Mkuu wa Kitengo cha Sheria, WCF, Bw.Abraham Siyovelwa, akitoa mada kuhusu masuala ya kisheria katika kutekeleza majukumu ya Mfuko.
  Mkurugenzi Mkuu, Bw. Mshomba (wapili kushoto), akibadilishana mawazo na wataalamu (wawezeshaji), Daktari bingwa mbobezi wa mifupa na viungo nchini, Dkt. Robert Mhina(watatu kushoto), Dkt. Hussein Mwanga na Bw. Yahya Kishashu.

  0 0

  Kampuni inayotoa huduma za usafiri kwa njia ya mtandaoni nchini - Bolt imezindua kitufe cha dharura (SOS)  kwa lengo la kuimarisha usalama wa madereva kipindi wanapokutana na hatari yoyote.

  Akizungunza na waandishi wa  habari jana jijini Dar es Salamaam Meneja wa Bolt Tanzania Remmy Eseka alisema madereva wanaotumia programu hiyo ya Bolt sasa wanaweza kutumia huduma hiyo mpya ya usalama muda wowote watakapo hisi kuwa wapo hatarini au eneo ambalo si salama. 

  Alisema matumizi hayo ya kitufe cha dharura dharura (SOS) yamekuwa kama muendelezo wa Bolt kutumia teknolojia kuimarisha usalama wa madereva wanapokuwa barabarani.

  "Usalama wa dereva na abiria ni swala la muhimu sana kwetu. Tunaongeza safu ya usalama wa dereva zaidi ya ule uliopo tayari wa kufutalia mubashara safari kwa kutumia GPS na mfumo wa thathmini.

  "Kitufe cha dharura (SOS) kilichopo kwenye programu ya Bolt ya dereva, huwezesha taarifa kuwafikia kampuni ya ulinzi ya SGA Tanzania Limited, kampuni inayoongoza kwa kutoa huduma hizi Afrika Mashariki" alisema meneja kampuni hiyo ambayo zamani ilifahamika kwa jina la Taxify

  Aidha, Meneja wa mauzo na masoko kutoka SGA, Faustina Shoo akisem kitufe cha dharura (SOS) kilichowekwa kwenye programu ya madereva kinapotumika, simu hupelekwa kwenye kituo cha dharura cha SGA, ambao baada ya kuhakiki uhalali wa dereva, wanapeleka gari la wagonjwa au timu ya askari kuelekea alipo dereva kuweza kumsaidia kama watoa huduma wa kwanza. 

  "Bolt italipia gharama hizi pamoja na gharama zitakazo pitishwa kwa kila  tukio.
  Tunaendeleza nia yetu ya kujibu mahitaji ya wateja/wabia kwa kutoa huduma ya uokoaji wa dharura kwa madereva wa Bolt kutokana na ubia huu. "Madereva wa Bolt wanahakikishiwa kupata huduma ya masaa 24 kupitia kitengo chetu cha dharura iwapo watapata tatizo wakiwa safarini.” alisema.
  Mmoja wa abiria wanaotumia programu ya Bolt, akipata huduma kutoka kwa dereva bodaboda baada ya Bolt zamani Taxify inayotoa huduma za usafiri kwa njia ya mtandaoni nchini kuzindua kitufe cha dharura (SOS) jijini Dar es salaam jana  kwa lengo la kuimarisha usalama wa madereva kipindi wanapokutana na hatari yoyote.
   

  0 0

  Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma Fatma Toufiq akizungumza na Washiriki wa Mkutano wa kujadili masuala ya usalama barabarani ulioandaliwa na Chama Cha Wanasheria wanawake TAWLA

  Mratibuwa Masula ya Uslama barabra kutoka Umoja wa Mataifa Marry Kessy akizungumzia malengo mawili ya milenia ambayo yamegusia usalama barabarani na muda uliongezwa wa maalengo ya milenia kufikia 2030
  Mkurugenzi wa Chama Cha Wanasheria Wanawake TAWLA, Tike Mwambipile akizungumza na Washiriki wa Semina hiyo juu ya masuala ya usalama barabarani
  Mmoja wa Washiriki wa Semina hiyo na Mdau wa Masuala ya Usalama Barabrani Mzee Hamza Kasongo akichangia katika mjadala wa nini kifanyike kupunguza ajali nchini
  Sehemu ya Washiriki wa Semina juu ya Masuala ya Usalama Barabarani yaliyoandaliwa na TAWLA Kwa kushirikiana na Azaki nyingine za kiraia

  0 0


  *Kukutanisha wajasiriamali 5,000 wa Bara la Afrika

  Na Ripota wa Michuzi TV -Abuja, Nigeria

  Taasisi ya Tony Elumelu Foundation (TEF) ambayo inapambania wajasiriamali kutoka Afrika itakuwa mwenyeji wa awamu ya 5 ya mkusanyiko mkubwa wa wajasiriamali kutoka Afrika itakayofanyika Julai 26 na 27, 2019, ambapo mkutano huo wa siku mbili utafanyika Hoteli ya Transcorp Hilton, Abuja nchini Nigeria.

  Mkutano huo wa kila mwaka  huandaliwa kupitia Programu ya Tony Elumelu Foundation Entrepreneurship ambayo imewapa mafunzo Waafrika chipukizi 3,000 ambao walichaguliwa kutoka zaidi ya waombaji 216,000. 

  Tukio hilo linawapa nafasi wanawake na wanaume chipukizi kutoka nchi zote 54 za Afrika kukutana, kujifunza na kubadilishana mawazo yenye mlengo wa kuwa wawekezaji bora Afrika na duniani.

  Pia ni fursa muhimu kwa viongozi wanasiasa na watunga sera kukutana uso kwa uso na kizazi kipya cha wafanyabiashara viongozi Wafrika ambao wanabadilisha uchumi wa Afrika.

  Wazungumzaji wakuu katika warsga hiyo muhimu ni Rais wa Rwanda, Paul Kagame, na Rais wa Senegal, Macky Sall, ambao wataungana na Mwanzilishi wa TEF ambaye pia ni Mwenyekiti wa Heirs Holdings na United Bank for Africa (UBA), Tony O. Elumelu, katika majadiliano ya wazi.

  Uwepo wa marais hao unawapa fursa wajasiriamali kutoka Afrika wanaohudhuria kuwa na mjadala wa kina na kutoa ushuhuda namna serikali inavyoweza kufanya kuchochea ukuwaji wa biashara.

  Ajenda ya mkutano huo inahusisha majadiliano na wataalamu kutoka Afrika na duniani ambao watawapa mafunzo washiriki kuongeza ujuzi katika biashara yao. Aidha warsha hiyo itawapa fursa baadhi wajasiriamali wateuli kuelezea bidhaa na huduma wanazotoa mbele ya jopo la majaji.

  Kwa mara ya kwanza, warsha hiyo itafanyika Abuja, Nigeria na kuwaleta pamoja watunga sera wakubwa, wafanyabiashara wakubwa na wale waliowahi kufaidi Programu hiyo.

  Mwaka jana, tukio muhimu lilikuwa uzinduzi wa TEFConnect ambayo ni sehemu ya wajasiriamali kutoka Afrika kubadilishana mawazo kupitia mfumo wa digitali.

  Mikutano hiyo imewahi kuhudhuriwa  na marais kadhaa wakiwamo Rais wa Ghana, Nana Akufo-Addo, Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, Rais wa Mstaafu wa Nigeria, Olusegun Obasanjo, Waziri Mkuu wa mstaafu wa Benin na Mjumbe wa Bodi ya Ushauri, Lionel Zinsou na Makamu wa Rais wa Nigeria, Profesa Yemi Osinbajo.

  Taasisi ya Tony Elumelu imedhamiria kuleta mabadiliko Afrika nzima kupitia ujasiriamali kwa kutaka zaidi Waafrika kujitegemea, Africapitalism, chini ya mwanzilishi huku akitambua zaidi kuwawezesha vijana wa Afrika kiuchumi hususan karne hii ya 21.

  Mwaka 2015, taasisi hiyo ilijitolea dola za Marekani milioni 100 million kuwawezesha wajasiriamali 10,000 kutoka kote barani kwa zaidi ya miaka 10 ambapo kwa sasa inakwenda kutimiza miaka mitano.

  Pia Tony Elumelu Foundation imetoa mchango wa  kushauri na kutoka mafunzo ya menejementi kwa zaidi ya watu 7,500 wanaoanzisha na wenye biashara ndogo kwa nchi zote 54 za Afrika.

  “Warsha ya TEF Entrepreneurship haitaleta tu watu wadau muhimu katika mabadiliko ya ujasiriamali wa Afrika lakini pia kumpa nafasi kila mtu kupanua biashara yake kwa nia ya kuleta maendeleo barani.

  “Tunafarijika kupokea habari kutoka kwa wajasiriamali wetu ambao wanatengeneza ajira, wanaajiri watu na kubadilisha maisha ya jamii inayowazunguka barani Afrika. Tunaamini hawa wajasiriamali ni tegemeo wetu wa baadaye. Wekezeni kwao sasa na kuvuna ndoto ya kesho ya Afrika,” alisema Mkurugenzi Mtendaji wa TEF.Ifeyinwa Ugochukwu.

  Manzilishi wa Taasisi ya Tony Elumelu Foundation, Tony Elumelu, akiwa katika moja ya mikutano ya wajasiriamali wa Afrika nchini Nigeria.
  Washiriki wa moja ya mikutano iliyopita wakiwa katika picha ya pamoja na mwasisi wa Tony Elumelu Foundation.

  0 0


   Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Bw. Abebe Aemro Selassie alipokutana na kufanya mazungumzo naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu Mei 6, 2019
   Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Bw. Abebe Aemro Selassie alipokutana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu Mei 6, 2019
   Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimtambulisha  Mkurugenzi wa Idara ya Afrika wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Bw. Abebe Aemro Selassie kwa Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango na Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi alipokutana na kufanya mazungumzo naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu Mei 6, 2019

  Rais Dkt. John Pombe Magufuli akipata picha ya kumbukumbu na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Bw. Abebe Aemro Selassie na ujumbe wake pamoja na  Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpang, Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa palamagamba Kabudi na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto james na maofisa wa Wizara alipokutana na kufanya mazungumzo naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu Mei 6, 2019

   Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiagana  na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Bw. Abebe Aemro Selassie baada ya kukutana na kufanya mazungumzo naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu Mei 6, 2019
   Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Afrika wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Bw. Abebe Aemro Selassie akiongea na wanahabari akiwa na  Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpang, Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James na maofisa wa Wizara baada ya kukutana na kufanya mazungumzo naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu Mei 6, 2019
  PICHA NA IKULU
older | 1 | .... | 1847 | 1848 | (Page 1849) | 1850 | 1851 | .... | 1897 | newer