Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live

MAGAZETI YA LEO IJUMAA MEI 3,2019

0
0














HUU SIO UBINADAMU, MNAHATARISHA AFYA ZA WATOTO- RC MWANGELA

0
0

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. (Mst) Nicodemus Mwangela akitazama makazi ya wananchi wa Mtaa wa Shule ulioko jirani na Shule ya Msingi Mlowo, Wilayani Mbozi ambapo takataka zimemwaga katikati ya makazi ya wananchi kabla ya kuagiza kufungwa kwa dampo hilo.
Wananchi wa Mtaa wa Shule wakitazama takataka zilizomwagwa jirani na makazi yao mara baada ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. (Mst) Nicodemus Mwangela kupita mtaani hapo na kuagiza dampo hilo lifungwe.

……………………

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. (Mst) Nicodemus Mwangela ameagiza kushikiliwa na polisi kwa masaa 24 Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mlowo Seriadi Mbugi kutokana na kurundika takataka jirani na makazi ya wananchi pamoja na shule ya Msingi Mlowo na hivyo kuhatarisha maisha yao.

Brig. Jen. (Mst) Mwangela amefikia uamuzi huo mapema leo wakati akifanya ukaguzi wa hali ya usafi katika Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mlowo na kukuta takataka zimemwagwa katikati ya makazi ya wananchi ikiwa ni siku saba tangu amuelekeze Kaimu Mkurugenzi huyo kuhakikisha mji huo unakuwa Msafi.

“Nilifanya Mkutano na wananchi wa Mji wa Mlowo na malalamiko yao makubwa yalikuwa mrundikano wa takataka na madampo katikati ya miji yao, nilimuagiza na kumpa siku saba Mkurugenzi wa Mji mdogo wa Mlowo kuhakikisha anausafisha mji huu lakini leo siku saba zimepita ninakagua na kukuta takataka zimemwaga katikati ya makazi ya watu, naambiwa watoto wanacheza na kuokota taka hapa, huu sio ubinadamu”, amesema Brig. Jen. (Mst) Mwangela

Ameongeza kuwa Mkurugenzi huyo amekiuka agizo lake na hivyo kuhatarisha maisha ya wananchi hao kwa kuwawekea takakata wananchi katikati ya makazi yao kinyume na taratibu za kiafya zinavyoelekeza.

“Huu sio utendaji wa serikali kabisa, licha ya Kaimu Mkurugenzi wa Mji Mdogo kukaa ndani, namuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi kuhakikisha ndani ya masaa manne takataka hizo ziwe zimetolewa na dampo hilo lifutwe”, amesisitiza Brig. Jen. (Mst) Mwangela

Kwa upande wake mkazi wa mtaa wa shule Bi Salehemu Filimon Mwaihojo amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kutembelea eneo hilo na kutatua kero hiyo kwakuwa wamekuwa wakipata hofu ya magonjwa kutokana na uwepo wa takataka hizo

“Hii ni wiki ya pili wanamwaga matakataka hapa, watoto wanachezea na kuokota makopo wanachota maji machafu na kunywa kwenye makopo hayo machafu wengine unakuta wanaokota kondomu zinazomwaga hapa wanapuliza wao wanajua mipira, kwakweli tulikuwa na hali mbaya, kwakuwa tuliona wametumwagia magonjwa hapa”, amesema Mwaihojo

Ameongeza kuwa dampo hilo lipo pia jirani na Shule ya Msingi Mlowo na hivyo wanafunzi hupita na kuchezea hapo hali ambayo wangeweza kudhuriwa na vipande vya chupa na taka ngumu zinazo mwagwa hapo huku wengine wakiokota na kula mabaki ya vyakula yanayotupwa hapo na hivyo kuhatarisha afya zao.

Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Azindua Soko la Madini Chunya

0
0

Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Soko la Madini Chunya. Kulia ni Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula.
Kutoka kushoto Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila, Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Mary-Prisca Mahundi na Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula wakifungua kitambaa kama ishara ya uzinduzi wa Soko la Madini Chunya.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila, (katikati waliokaa mbele) Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula (wa pili kushoto waliokaa mbele) na Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Mary-Prisca Mahundi ( wa nne kushoto waliokaa mbele) wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji kutoka Wizara ya Madini, Tume ya Madini na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Chunya mara baada ya uzinduzi wa soko hilo
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila, (katikati waliokaa mbele) Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula (wa pili kushoto waliokaa mbele) na Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Mary-Prisca Mahundi ( wa nne kushoto waliokaa mbele) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyabiashara wa madini ya dhahabu Chunya mara baada ya uzinduzi wa soko hilo
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Mary-Prisca Mahundi (katikati) mara baada ya kuzindua Soko la Madini la Chunya lililopo Mjini Chunya Mkoani Mbeya tarehe 02 Mei, 2019.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila akisoma hotuba ya uzinduzi kabla ya kuzindua Soko la Madini Chunya.
Watendaji kutoka Wizara ya Madini, Tume ya Madini na Idara nyingine za Serikali wakifuatilia hotuba ya uzinduzi wa Soko la Madini Chunya iliyokuwa inatolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila. (hayupo pichani).
Sehemu ya wananchi waliofika kushuhudia uzinduzi wa Soko la Madini Chunya wakifuatilia hotuba ya uzinduzi iliyokuwa inatolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila. (hayupo pichani).

……………………

Na Greyson Mwase, Chunya

Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila amezindua Soko la Madini Chunya ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ya kutaka Wilaya ya Chunya kuhakikisha imekamilisha na kuzindua soko la madini ndani ya kipindi cha siku saba. Rais Magufuli alitoa agizo hilo tarehe 27 Aprili, 2019 wilayani Chunya katika mkutano wake na wachimbaji na wachenjuaji wa madini.

Uzinduzi huo ulishirikisha Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula, Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Mary-Prisca Mahundi, Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu kutoka Wizara ya Madini, Issa Nchasi, Mhasibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Anthony Tarimo na Kamishna Msaidizi- Uendelezaji wa Migodi kutoka Wizara ya Madini, Ali Ali.

Wengine walioshiriki katika uzinduzi huo ni pamoja na Mkurugenzi wa Ukaguzi na Biashara ya Madini kutoka Tume ya Madini, Dk. Venance Mwase, wawakilishi wa wachimbaji na wafanyabiashara wa madini, viongozi wa dini pamoja na vyombo vya habari.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Profesa Msanjila alisema kuwa, tangu kuingia madarakani kwa Serikali ya Awamu ya Tano, imekuwa ikisisitiza dhamira yake ya kuhakikisha Sekta ya Madini inakua, inanufaisha watanzania pamoja na kuchangia ukuaji wa Pato la Taifa.

Akielezea mafanikio ya Serikali kupitia Wizara ya Madini kwenye usimamizi wa rasilimali za madini, Profesa Msanjila alisema kuwa, ili kuhakikisha kuwa wananchi wote wananufahika na rasilimali za madini, Serikali ilitunga Sheria ya Mamlaka ya Nchi Kuhusiana na Umiliki wa Maliasili Namba 5 ya Mwaka 2017; Sheria ya Mapitio na Majadiliano Kuhusu Masharti Hasi katika Mikataba ya Maliasili za Nchi Namba 6 ya mwaka 2017 pamoja na kufanya marekebisho ya Sheria ya Madini Sura ya 123.

Aliendelea kueleza kuwa Serikali pia imefuta baadhi ya tozo ambazo zilikuwa kero kwa wafanyabiashara wa madini hususan wachimbaji wadogo na kufafanua kuwa tozo hizo kuwa ni pamoja na kodi ya ongezeko la thamani (VAT) asilimia 18 na kodi ya zuio ya asilimia tano kwa wachimbaji wadogo.

Alisema kuwa, kuwekwa kwa mazingira mazuri ya kibiashara kwenye sekta ya madini pamoja na kufuta kodi na tozo mbalimbali zinazofikia asilimia 23 kutaondoa utoroshwaji wa madini na kusaidia wachimbaji wadogo kutambuliwa kupitia uanzishwaji wa masoko ya madini.

Alieleza manufaa mengine kuwa ni pamoja na kupunguza gharama za uendeshaji wa shughuli za wachimbaji wadogo na kuongeza wigo wa mapato ya nchi.

Katika hatua nyingine, Profesa Msanjila aliwataka wachimbaji wote wadogo na wafanyabiashara wa madini kuendelea kushirikiana na mamlaka mbalimbali za Serikali katika kutekeleza majukumu yao kwa kufuata sheria, kanuni, taratibu na miongozo mbalimbali inayotolewa na Serikali.

Akielezea manufaa ya soko jipya la madini Chunya, Profesa Msanjila alisema soko litaziba mianya ambayo imekuwa chanzo cha utoroshwaji wa madini, ukwepaji kodi na hivyo kusababisha biashara nzima ya madini kufanyika kiholela katika maeneo mengi ya nchi.

Aliongeza kuwa kuanzishwa kwa Soko la Madini Chunya kutawezesha na kurahisisha biashara nzima ya madini na kuwa kiungo muhimu cha kuwakutanisha wachimbaji na wafanyabiashara kwa lengo la kuuza na kununua madini.

Profesa Msanjila aliendelea kufafanua manufaa mengine ya soko kuwa ni pamoja na kuwa suluhisho la tatizo la kupunjwa na kudhulumiwa na kuondoa vitendo vya dhuluma ambavyo vimekuwa vikiwahusisha wafanyabiashara wa madini wasiokuwa waaminifu kwa baadhi ya wachimbaji wadogo.

“Soko hili litaondoa uwezekano wa wanunuzi wa madini kuibiwa na wajanja wachache wanaojifanya kuwa na madini wakati hawana, nawasihi wanunuzi wa madini kulitumia soko kikamilifu ili kuepuka udanganyifu na matapeli tu” alisema Profesa Msanjila.

Katika hatua nyingine Profesa Msanjila aliupongeza uongozi wa Wilaya ya Chunya, wafanyabiashara wa madini kwa kuhakikisha Soko la Madini Chunya limezinduliwa ndani ya muda uliopangwa.

Wakati huo huo akizungumzia hali ya uanzishwaji wa masoko ya madini nchini, Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula alisema kuwa, hadi kufikia sasa masoko matano ya madini yameshafunguliwa katika mikoa ya Geita, Singida, Kahama, Arusha – Namanga na Chunya.

Aliongeza kuwa masoko mengine ya madini yanatarajiwa kufunguliwa kabla ya tarehe 05 Mei, 2019 ikiwa ni pamoja na Soko la Madini ya Dhahabu na Vito vya Thamani Ruvuma, Soko la Madini Shinyanga, Soko la Madini Dodoma na Soko la Madini Mbeya. Profesa Kikula alitaja masoko mengine ambayo yanatarajiwa kufunguliwa hivi karibuni kuwa ni pamoja na Soko la Madini ya Bati (tin) na Soko la Madini ya Dhahabu Handeni.

Alisisitiza kuwa mikoa mingine ipo katika hatua za mwisho kukamilisha vigezo mbalimbali vikiwemo vya kiusalama na miundombinu.

TUMIENI HATI ZA HAKI MILIKI ZA KIMILA KUTAFUTA MIKOPO YA UWEKEZAJI–DC UYUI

0
0
Mkuu wa Wilaya ya Uyui mkoani Tabora Gift Msuya akisisitiza umuhimu wa wananchi kutumia hati milki za kimila za kumiliki ardhi kujiletea maendeleo jana katika Kijiji cha Miyenze.

Meneja Urasimishaji ardhi Vijijini kutoka Mpango wa kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanynge Tanzania(MKURABITA) Antony Temu akieleza faida za mafunzo kwa wakulima zaidi ya 100 wa Kijiji cha Miyenze Wilayani Uyui Mkoani Tabora wakati wa hafla ya kufungua mafunzo hayo jana katika Kijiji cha Miyenze.


Kikundi cha Ngoma kutoka Kijiji cha Miyenze Wilayani Uyui mkoani Tabora kikitoa burudani wakati wa hafla ya kufungua mafunzo kwa wakulima wa Kijiji ya Miyenze yaliyoandaliwa na Kuratibiwa na Ofisi ya Rais MKURABITA ili kuwawezesha wakulima hao kuwa na kilimo chenye tija.
Mkuu wa Wilaya ya Uyui Gift Msuya akiwa kwenye picha ya pamoja na sehemu ya wazee maarufu wa kijiji cha Miyenze Wilayani humo jana baada ya kukabidhi hati 100 kwa wakazi wa eneo hilo.



Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora Mhe Gift Msuya akiwa kwenye picha ya pamoja na sehemu ya wakulima waliopata hati miliki za kimila za kumiliki ardhi wa kijiji cha Miyenze Wilayani humo.
Baadhi ya Wakazi wa Kijiji cha Miyenze wakimsikiliza jana Mkuu wa Wilaya ya Uyui Gift Msuya wakati wa hafla ya ugawaji wa hati za hakimiliki za kimila za ardhi kwa wakazi 100.
Mkuu wa Wilaya ya Uyui Gift Msuya akitoa hati ya hatimiliki ya kimila jana kwa Mkazi wa Kijiji cha Miyenzi Masele Makonda.
Mkuu wa Wilaya ya Uyui Gift Msuya akitoa hati ya hatimiliki ya kimila jana kwa Mkazi wa Kijiji cha Miyenzi Rufunga Maguki. Picha na WHUSM

………………….
NA TIGANYA VINCENT ,TABORA

WAKAZI wa Kijiji cha Miyenze wilayani Uyui wametakiwa kutumia hati za hakimiliki za kimila walizopewa kuomba mikopo kwa ajili ya uwekezaji katika kilimo na shughuli nyingine za kiuchumi ili kujiletea maendeleo.


Kauli hiyo imetolewa jana na Mkuu wa Wilaya ya Uyui Gift Msuya wakati wa kufungua mafunzo ya kuwajengea uwezo wakulima wa Kijiji cha Miyenze na kukabidhi hati za hakimiliki ya ardhi za kimila kwa wakazi 100.

Alisema wakazi walipata hati za haki miliki hizo za kimila wanao usalama wa zao za ardhi na wameiongezea thamani ambayo inawafanya kuwa na fursa za kupata pesa. Msuya aliongeza kuwa hati hizo zitawasaidia kupata dhamana hata kwenye vyombo vya kisheria kama vile Mahakama pindi wanatakiwa kuweka mali isiyo hamishika.

Alisema hati walizopata ni fursa pia ya kuwawezesha kuingia ubia na wawekezaji mbalimbali ambao wanatafuta ardhi inayotambulika kisheria kwa ajili ya kuwekeza katika sekta za viwanda, hoteli, maduka na shughuli mbalimbali za kiuchumi.

Aidha Mkuu huyo wa Wilaya aliwataka wakazi wa Kijiji hicho na maeneo mengine katika wilaya hiyo ambao mashamba yao hayajapimwa kuhakikisha wanaypima ili kuyaongezea thamani na kuwaondoa katika umaskini na kupunguza migogoro.

Alisema hakuna haja ya wananchi kukumbatia maeneo makubwa ambayo hayajapimwa kwa kuwa hayawezi kuwasaidia kupata maendeleo yao na nchi kwa ujumla kwa kuwa ni sawa na mali mfu.

Kwa upande wa Meneja Urasimishaji ardhi Vijijini kutoka Mpango wa kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanynge Tanzania(MKURABITA) Antony Temu alisema kuwa pamoja na kutoa hati hizo watawajengea uwezo wakulima 100 na viongozi 10 jinsi ya kuendesha kilimo bora na utunzaji wa kumbukumbu za hesabu za kilimo na biashara.

Alisema maeneo mengine ni jinsi ya kutafuta fursa na kuzitumia na ufugaji wa kuku wa kienyeji kibiashara na uandishiwa mpango wa biashara na uundaji wa vikundi vya uchumi.

Naye mmoja wa wakulima wa Kijiji cha Miyenze William Mauye aliishukuru Serikali kwa kuwawezesha kupima mashamba yao na hatimaye kuwapatia hati za haki miliki za kimila kwa kuwa zitawasaidia kuinua kipato chao kwa kuwa watakuwa na fursa ya kupata mikopo ya benki.

Alisema mkopo atakaochukua utamwezesha kununuza zana za kilimo za kisasa kwa ajili ya kuboresha kilicho chake cha mpunga na mahindi na hivyo kuongeza uzalishaji.

Mauye aliiomba Serikali kupitia MKURABITA kuendelea kuwasaidia wananchi wa vijiji ili wapimie ardhi yao na kuepuka baadhi ya watu ambao wakuwa wakichukua fedha zao bila hata kuwapimia maeneo yao.

IGP SIRRO AFANYA ZIARA YA KIKAZI KATIKA WILAYA ZA RUNGWE NA KYELA MKOANI MBEYA

0
0


 Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akizungumza na baadhi ya wananchi wa eneo la Ushirika, Tukuyu mkoani Mbeya leo, wakati akiwa katika ziara ya ukaguzi katika wilaya za Rungwe na Kyela mkoani humo ambapo IGP Sirro aliwataka wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kuwafichua wahalifu.
2
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akinunua matunda kutoka kwa mmoja wa wajasiliamali katika eneo la Ushirika, Tukuyu mkoani Mbeya leo, wakati akiwa katika ziara ya ukaguzi katika wilaya za Rungwe na Kyela mkoani humo kwa lengo la kuona utendajikazi unaofanywa na askari wa Jeshi hilo.
3
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akizungumza jambo na mmoja kati ya wajasiliamali ndogo ndogo katika eneo la Ushirika, Tukuyu mkoani Mbeya leo, IGP Sirro yupo mkoani hapa kwa ziara ya kikazi.
5
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Kyela Mhe. Claudia Kitta, wakati alipowasilia wilayani humo kwa ziara ya kikazi yeye lengo la kuona utendajikazi unaofanywa na askari wa Jeshi hilo. Picha na Jeshi la Polisi.

RAIS DKT. SHEIN AFUNGUA MAJENGO YA OFISI ZA SMZ PEMBA

0
0

MAJENGO ya Wizara Tatu za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar yaliojengwa katika eneo la Gombani Kisiwani Pemba Wilaya ya Chakechake yaliofunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiondoa kipazia kuashiria kuweka Jiwe la Msingi la Magengo Matatu ya Wizara za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar zilioko katika eneo la Gombani Wilaya ya Chakechake Pemba, kulia Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe. Balozi Mohammed Ramia Abdulwawa.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akikata utepe kuashiria kufungua majengo ya Wizara Tatu za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, kushoto Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe.Balozi Mohammed Ramia Abdulwawa na kulia Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto Zanzibar Mhe. Maudline Castico na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Khamis Juma Maalim, wakishiriki katika ukataji wa utepe huo wakati hafla ya ufunguzi wa majengo hayo.(Picha na Ikulu)


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mshauri wa Ujenzi wa Majengo Matatu ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Ndg. Mbarouk Juma, wakati wa hafla hiyo ya ufunguzi wa Majengo hayo eneo la Gombani Pemba.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiuliza mswali wakati wa hafla hiyo ya ufunguzi wa majengo hayo katika eneo la Gombani Pemba.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mjenzi wa Majengo ya Wizara za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Ndg. Khamish Ali Khamis, ( na kushoto Mshauri Elekezi wa Mradi wa Ujenzi huo Ndg. Mbarouk Juma.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Kaimu Afisa Mdhamini Wizara ya Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto Pemba Ndg. Hakim Vuai Shein, kulia, wakati akitembelea jingo la Wizara hiyo.(Picha na Ikulu)

WAZIRI wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe. Balozi Mohammed Ramia Abdulwawa, akitowa maelezo kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akitembelea majengo hayo baada ya kuyafungua rasmin leo kisiwani Pemba katika eneo la Gombani.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mjenzi wa Majengo hayo wakati alitembelea majengo hayo baada ya kuyafungua rasmin leo.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, amesema kuwa miongoni mwa malengo makuu ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni kuona kwamba watumishi wa umma wanafanya kazi zao wakiwa katika mazingira yaliyo bora na salama zaidi.

Dk. Shein aliayasema hayo leo katika hafla ya uzinduzi wa Jengo la Ofisi za Serikali huko Gombani Chake Chake Pemba, Mkoa wa Kusini Pemba, ambapo viongozi mbali mbali wa vyama na serikali pamoja na wananchi na wafanyakazi walihudhuria.

Rais Dk. Shein alisema kuwa uzinduzi wa jengo hilo ni miongoni mwa vielelezo muhimu vya utekelezaji wa lengo hilo kwani majengo ya ofisi ndio mahali pa kufanyia kazi ambapo hutumia muda mwingi ambayo ni theluthi moja ya siku nzima baada ya kutoka nyumbani.

Alieleza kuwa kuwa na mahala pazuri pa kufanyia kazi kunampelekea mtendaji afanye kazi kwa furaha, umakini na kujiamini Zaidi na ndio maana Serikali imeamua kujenga.

Aliongeza kuwa ujenzi wa jengo hilo ni jitihada za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia maamuzi ya Baraza la Mapinduzi ambapo hatua yote hiyo ni kuwawwzesha wafanyakazi katika mazingira mazuri.

Alieleza kuwa ujenzi huo unatokana na baadhi ya ofisi kuchakaa, nyengine hazina nafasi ya kutosha kwa ajili ya watumishi pamoja na wananchi wanaofika kwa ajili ya kupatiwa huduma.

Hata hivyo, Rais Dk. Shein alisema kuwa baadhi ya Wizara na Taasisi nyengine za Serikali zililazimika kukodi nyumba kutokana na uhaba wa majengo halisi ya kiofisi hali ambayo haipendezi hivyo Serikali itaendelea kujenga majengo ya Ofisi Unguja na Pemba.

Rais Dk. Shein alisema kuwa Serikali imejenga ofisi hizo ili kurahisisha utoaji wa huduma hivyo, kila mfanyakazi ahakikishe kwamba anawajibika ipasavyo kulingana na dhamana na majukumu ya kazi aliyopangiwa. Hivyo, aliwataka wafanyakazi wahakikishe wanatumia vizuri muda wa kazi kwa kufanya mambo yanayopaswa kufanywa katika sehemu za kazi.

Alisema kuwa Serikali itaongeza mshahara kwa kima cha chini na juupale mapato yatakapoongezeka kwa wafanyakazi kuzidi kujituma na kuendelea kufanya kazi kwa ari, taratibu na nidhamu za kazi.

Alisisitiza wafanyakazi kufanya kazi kwa masaa manane ya kazi kwa siku kwani hatua hiyo itaongeza ufanisi na kuongeza mapato huku akisisitiza haja kwa wafanyakazi kutunza siri za kazi kwani nyenzo kubwa katika Utawala Bora sambamba na kujiepusha na malumbano.

Aliongeza kuwa kuna haja ya kutafuta namna itakayowezesha kudhibiti matumizi ya simu za mikononi wakati wa saa za kazi kwani kumekuwa na malalamiko mengi kwa wananchi katika sehemu mbali mbali juu ya suala matumizi mabaya ya simu.

“Wafanyakazi wanatumia muda mwingi kazini kuchati na kuperuzi katika mitandao ya kijamii vile vile natoa indhari kwa wale wanaotega kazi kwamba kuwepo kwa ofisi hizi ndani ya jengo moja kusichukuliwe kuwa ni ukaribu wa marafiki kuonana kirahisi kwa ajili ya mazungumzo”,alisisitiza Dk. Shein.

Aidha, Dk. Shein aliwahimiza viongozi na wafanyakazi wote watakaotumia jengo hilo wahakikishe kwamba wanalitumia vizuri pamoja na vifaa na miundombinu mengine ili viweze kudumu Zaidi.

Pia, alieleza kuwa ofisi hizo mpya zitaongeza ari na hamasa ya wafanyakazi ili waweze kufikia malengo yaliyowekwa ya kutoa huduma bora Zaidi kwa wananchi huku akisisitiza kuwa jengo hilo litasaidia hata zile taasisi ambazo zimechakaa huku taratibu zikiandaliwa kujenga ofisi nyengine Zaidi.

“Na zile taasisi ambazo hazina pa kukaa zitaletwa hapa hapa huku Serikali ikiendelea kujenga majengo mapya”,alisema Dk. Shein. Sambamba na hayo, Rais Dk. Shein alisema kuwa utekelezaji wa miradi hiyo mikubwa ya maendeleo ni kielelezo cha juhudi za kuendeleza fikra, falsafa na malemgo ya Mapinduzi ya mwaka 1964 kwa kuzingatia miongozo ya viongozi na wazee waliotangulia.

Alisisitiza kwamba Waasisi wa Mapinduzi chini ya Marehemu Mzee Abeid Amani Karume walihakikisha kwamba panakuwa na uwiano wa kasi ya maendeleo baina ya Unguja na Pemba. Alieleza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Awamu ya Saba na Awamu zote zilizotangulia zimekuwa zikiyaendeleza haya kwa kasi na ari ile ile ya Kimapinduzi licha ya kwamba wapo wanayoyabeza.

Alisema kuwa kuimarika kwa uchumi kumeiwezesha Awamu hii kuyafanya maslahi ya wafanyakazi yawe bora kwa mara nne pamoja na kuubadilisha mshahara wa kima cha chini kwa asilimia mia moja. Rais Dk. Shein alisema kuwa mambo yote yanayofanywa ikiwa ni pamoja na ujenzi wa majengo hayo ni kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar Ibara ya 10.

Alitumia fursa hiyo kuipongeza Kampuni za ndani za Zanzibar za “Quality Building Contract” iliyojenga ofisi hizo pamoja na Kampuni ya “ZANCON”iliyokuwa Mshauri elekezi na msimamizi wa ujenzi huo.

Nae Waziri wa Fedha na Mipango Mohamed Ramia Abdiwawa alieleza kuwa juhudi hizo za ujenzi zinatokana na utekelezaji wa Ilani ya CCM sambamba na azma ya Mapinduzi Matukufu ya Januari 12, 1964 na kutoa pongezi kwa Mawaziri wawili waliomtangulia ambao ni Omar Yussuf Mzee na Dk. Khalid Salim kwaa kusimamia vyema mchakato wa ujenzi huo.

Nae Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Khamis Mussa alisema kuwa ujenzi wa jengo hilo lenye vyumba 145 umegharimu jumla ya TZS Bilioni 13.6 ambazo ni fedha za mapato ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Alisema kuwa miongoni mwa Wizara ambazo zina ofisi katika majengo hayo ni sita kwa hivi sasa ambazo ni Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Katiba na Sheria, Wizara ya Kazi Uwezeshaji Wazee, Wanawake na Watoto, Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Wizara ya Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati na Wizara ya Vijana, Utamaduni na Michezo.

Mapema baada ya kulizindua jingo hilo Rais Dk. Shein alipata fursa ya kulitembelea jengo hilo katika Ofisi za Wizara zote ndani ya jengo hilo na kupata maelezo.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

FAINALI YA MAVUNDE CUP KIKUYU KASKAZINI YAIBUA VIPAJI,MBUNGE MAVUNDE AAHIDI MAKUBWA

0
0
Fainali ya Mavunde Cup kata ya Kikuyu Kaskazini imemalizika jana kwa kishindo kikubwa kwa Timu ya Kikuyu Football Club kuibuka kidedea na kunyakua ubingwa huo baada ya kuitandika Timu ya St John’s University kwa bao moja kwa bila katika Mchezo uliochezwa katika Viwanja vya Chuo kikuu cha St John’s na kuhushuriwa na maelfu ya wananchi wa Dodoma.

Akihitimisha mashindano hayo,Mfadhili wa mashindano hayo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde amezipongeza timu zote kwa ushiriki wao na kuonesha uwezo mkubwa wa vipaji vikubwa kwa muda wote wa mashindano na kuahidi kwamba atahakikisha anaendelea kuvikuza na kuvilea vipaji hivyo ili Vijana hao pia waweze kufikia malengo yao katika mchezo wa mpira wa miguu ambao sasa umekuwa ni fursa ya Ajira kwa Vijana wengi.

Akishukuru kwa niaba ya Vijana wenzake,Mratibu wa mashindano hayo *Comrade Elibariki **alimshukuru Mbunge Mavunde kwa Ufadhili wa mashindano hayo na vifaa vya michezo kwa Timu *10 ambazo zimeshiriki katika mashindano haya lakini pia na namna ambavyo amekuwa mstari wa mbele katika kushirikiana na Vijana katika Jimbo la Dodoma Mjini katika nyanja mbalimbali.



 

KAIMU RPC TANGA AWATAKA WANAHABARI KUTUMIA KALAMU ZAO VEMA KUHABARISHA UMMA

0
0

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Daudi Mafwimbo akizungumza leo wakati wa siku ya maadhimisho ya siku ya uhuru wa habari Duniani ambapo kwa mkoa wa Tanga ilifanyika ukumbi wa Regal Naivera kushoto ni Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Tanga (UTPC) Hassani Hashim anayefuatia ni Makamu Mwenyekiti wa UTPC Lulu George
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Tanga (UTPC) Hassani Hashim akizungumza wakati wa maadhimisho hayo kulia ni Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Daudi Mafwimbo kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa UTPC Lulu George
Katibu wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani hapa Alex Abraham akiwasilisha taarifa kwenye maadhimisho hayo
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Tanga (UTPC) Hassani Hashim kulia akiteta jambo na Makamu Mwenyekiti wa UTPC Tanga Lulu George
AFISA Uhisiano wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Dorrah Killo akizungumza wakati wa maadhimisho hayo

Waandishi wa Habari kushoto ni Amina Omari kutoka Gazeti la Mtanzania na Raisa Saidi wa gazeti la Mwananchi wakifuatilia kwa umakini hotuba ya mgeni rasmi wakati wa maadhimisho hayo
Kamishna wa NCCR Mageuzi Mkoani Tanga Ramadhani Manyeko kulia akiwa na Mwandishi Mwandamizi wa gazeti la Citizen mkoani Tanga George Sembony kwenye maadhimisho hayo
Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Tanga Lupaksyo Kapange akiwa kwenye maadhimisho hayo
Sehemu ya waandishi kutoka vyombo mbalimbali mkoani Tanga wakifuatilia maadhimisho hayo


NA MWANDISHI WETU, TANGA. 

WAANDISHI wa Habari mkoani Tanga wametakiwa kutumia vema kalamu zao katika kuhabarisha umma kwani wakiitumia vibaya kwa kutokuzingatia maadili inaweza kuibomoa jamii na kuleta madhara.

Hayo yalisemwa leo na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi mkoani hapa Daudi Mafwimbo wakati wa siku ya maadhimisho ya siku ya uhuru wa habari Duniani ambapo kwa mkoa wa Tanga ilifanyika ukumbi wa Regal Naivera.

Alisema kama waandishi wa habari wakishindwa kuzingatia suala hilo licha ya kuibomoa jamii lakini pia inaweza kuleta madhara yanayoweza kuwa histoiria kwa jamii zinazowazunguka

“Ndugu zangu leo hii tunaadhimisha siku ya Uhuru wa vyombo vya habari lazima tuzingatie miiko na maadili yenu kwa lengo usalama na mustakabali wa jamii kwani muandishi wa habari bila jamii sawa na samaki bila maji wanategemeana lakini kubwa tujikite kurudi kukumbuka miiko ya uandishi wa habari “Alisema Kaimu RPC

“Lakini pia wakati tunaadhimisha siku hii muhimu leo kwa waandishi wa habari na wadau wa habari tuwakumbuke ndugu zetu wana habari na wana jamii waliopoteza uhai wao kwa lengo la kuhakikisha jamii inapata habari au kuelimishwa”Alisema .Hata hivyo aliwataka kuhakikisha wanajikita kwenye kuandika habari ambazo zitakuwa zitachochea ukuaji wa maendeleo kwa jamii ikiwemo kuibua changamoto zilizopo.

Awali akiwasilisha Taarifa ya Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Tanga (TPC) Katibu wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani hapa Alex Abraham alisema wamekuwa na mahusiano mazuri na Baraza la Habari Tanzania (MCT) na umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) ambao wamekuwa wakiwapa mafunzo mbalimbali ya kitaaluma kwa wanachama chini ya udhamini wa SIDA.

Alisema siku ya leo waandisi na tasnia ya habari kwa ujumla huitumia kwa kuwakumbuka na kuwapa heshima waandishi ambao wamepata matatizo mbalimbali wakiwa kazini na hata wengine kufikia hatua ya kupoteza maisha.

“Kwa uhuru wa kujieleza ni haki ya msingi na muhimu kuweza kufikia haki nyenginezo ambazo zimo katika matamko mbalimbali ya kimataifa ya haki za binadamu, miaka miwili baadaye baada ya azimio la Windhoek yaani mwaka 1993 Baraza la Umoja wa Mataifa (United Nations General Assembly) likaitambua rasmi na kuitangaza Mei 3 kuwa siku ya Uhuru wa Habari Duniani “Alisema

Kauli mbiu ya siku ya Uhuru wa vyombo vya habari Duniani inasema “Jukumu la UTPC na klabu za waandishi wa habari kuchangia uchaguzi huru na haki”

MBUNGE JUMANNE KISHIMBA AJITOSA KUUCHAMBUA MFUMO WA ELIMU,ATAKA UANGALIWE UPYA

0
0
*Asisitiza  wenye digrii ni kama viazi vilivyoshindwa kuiva...aeleza changamoto ya ajira kwa waliosoma

*Aweka wazi elimu ya sasa haina tofauti na kifungo cha maisha, ambacho wanafunga wazazi na watoto


Na Ripota Wetu,Michuzi TV

HATIMAYE Mbunge wa Jimbo la Kahama Mjini, mkoani Shinyanga Jumanne Kishimba (CCM), ameamua kujitosa kwa kuzungumzia mfumo wa elimu uliopo sasa ambao umeshindwa kumwandaa mwanafunzi kujitegemea na kwamba hiyo ni dalili mbaya kwa Taifa la Tanzania.

Kishimba amesema umefika wakati l kwa Serikali kupitia Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako kuangalia namna bora ya kutoa elimu ya kumwandaa mwanafunzi pamoja na kuangalia mitaala ya elimu kama inakidhi vigezo vya elimu na ikiwezekana ifanyiwe maboresho.

Amefafanua ni bora akazungumzia mfumo wa elimu kwani wengi wamekuwa wakiogopa kueleza ukweli,lakini kwake anaona ni wakati wa mfumo wetu wa elimu kuangaliwa upya kama ambavyo amewahi kushauri Rais mstaafu Benjamin Mkapa.

Akizungumza bungeni Mjini  Dodoma, wakati anachangia mjadala wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Kishimba amesema kuwa alishtushwa na taarifa ya watu 40,000 kuwasilisha maombi ya ajira 70 zilizotangazwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) hivi karibuni.

Amesema suala hilo linapaswa kuisikitisha, kuiogofya na kuishangaza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na vyuo vikuu kwa sababu kama waombaji ni 40,000 na wanaopata kazi ni 50 hawa wengine wanakwenda wapi.

“Elimu yetu hii tulirithi kutoka kwa wakoloni Waingereza, haina pingamizi. Waingereza wakistaafu watu 900,000, watakaomaliza shule au ‘University’ (chuo kikuu) watakuwa milioni moja, kwa hiyo 900,000 watapata kazi hawa 100,000, Serikali inaweza kuwatunza na kuwahifadhi, lakini kwetu wanaomaliza shule wanaweza kuwa milioni moja wanaopata kazi ni 50,000, "amesema.

Ameongeza kuwa “Kwahiyo tukiendelea na utaratibu huu mwenyekiti tunatengeneza bomu kubwa, kwenye suala hili naona kila mtu anaogopa kupasema, lakini ukweli mwenyekiti ni vizuri tukubaliane na Wizara ya Elimu ambao wao ndio watunga sera za elimu, iundwe kamati au tume ambayo itachunguza suala la elimu kwa Tanzania".

Kishimba ameongeza kuwa “Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, amejaribu kuliongelea hili suala mara mbili mara tatu, lakini naona watu hawalichukulii uzito, lakini mwenyekiti watu 40,000 kama wangekuwa Uwanja wa Taifa wakasema hawatoki mle uwanjani, utakuwa na kazi ngumu ya kuwatoa." 

Mbunge huyo aliyekuwa anachambua mfumo wa elimu kwa kujiamini huku wabunge wakionesha kuguswa na mchango wake ili kuboresha elimu ya Tanzania, ametoa ushauri kutungwa sera mpya ya elimu itakayowawezesha kujifunza shughuli za biashara, kilimo na ufugaji badala mfumo uliopo sasa ambao mwanafunzi anahitimu elimu ya juu kwa kupewa cheti ambacho hakimwezeshi kupata ajira popote.

Kishimba amesema mfumo huo unapaswa kuhakikisha kuwa asilimia 50 ya maksi wanafunzi wazipate katika masomo hayo na asilimia 50 zitokane na masomo ya darasani.

Aeeleza kwamba  mfumo huo utamsaidia mwanafunzi pale anapohitimu masomo yake ya sekondari au chuo kikuu, akiambiwa akajitegemee anakuwa na sababu ya msingi ya kufanya hivyo kwa sababu atakuwa akifahamu akajitegemee vipi.

“Lakini leo kumwambia mtu mwenyekiti aende akajitegemee, wewe umechukua fedha zake za ‘University’ alafu wewe ukampa unayosema ni digrii, lakini kiukweli umempa karatasi, ni sawa sawa na mtu amecheza Deci, hii digrii hakuna mahala inapotambuliwa popote, hata kama unaumwa huwezi kuiweka dhamana famasi, huwezi kuiweka dhamana benki, sasa inawezekana kweli?

“Binafsi  nimesomesha mtoto wangu, nimeuza mifugo yangu, nimelipa milioni 10, wewe umenipa digrii halafu wewe unaniacha mimi nikazunguke mtaani na ile digrii. Mimi mwenyewe ni mwathirika wa hizo digrii, ninao watoto sita wana digrii, kwa kweli mwenyetiki inahuzunisha sana, ingekuwa bora watunga sera tukubaliane kwamba vyuo vikuu kabla havijatangaza nafasi za shule zikatafute ajira zenyewe.

"Zieleze na mishahara, ziseme tumepata NBC mshahara ni Sh 800,000, tumepata NSSF Sh 500,000, sasa tunaanza kusajili, leta milioni tano nikupe digrii kazi hii hapa,” amesema na kuongeza suala hilo linaweza kuonekana kama la kuchekesha, lakini hali ni mbaya mitaani kwa sababu watu wanazo digrii kila kona, hawana ajira.

Pia amesema  muda wa kusoma vilevile watunga sera waangalie ni nani alifanya ‘research’ kwamba ubongo wa binadamu unahitaji kila mwaka darasa moja, kama yupo atwambie. "Wakati huu nafasi za ajira hakuna unachukuliwa mtoto wako miaka 17, unarudishiwa ana miaka 25 mnaambiwa katafuteni kazi ya kujitegemea, mnajitegemeaje mwenyekiti?

“Kama watakubali watunga sera mwaka mmoja wasome madarasa matatu au manne ili watu wamalize shule mapema, itatusaidia sana ili mtu akimaliza shule arudi huku tuje tuendelee na maisha kijana akiwa bado mdogo. Leo wanakaa naye muda wote wanakuja kukurudishia wewe ana miaka 25," amesema.

Kishimba amesema ukienda kwenye familia zilizoathirika kwenye suala hilo la elimu ukasema elimu ni ufunguo wa maisha watasema hapana elimu ya Tanzania ni kifungo cha maisha, maana ni kifungo kigumu, umefungwa wewe, amefungwa mtoto, amefungwa mama na fedha zimeenda, wote mna vyeti viko ukutani na majoho ya siku ya ‘graduation’, cha kufanya hamna mnatazamana.

Amesema kuwa lengo lake si kubeza elimu, lakini ni lazima yafanyike mabadiliko makubwa na kwamba nchi nyingi duniani zina matatizo kama hayo ikiwamo Afrika Kusini kwa sababu wao pia wamefuata mfumo huo wa elimu wa Uingereza ambao unakwenda kwa mfumo wa sukuma, sukuma, sukuma na kupewa cheti, lakini hakuna kitu wanachokipata.l

Pia kwa sasa wanapokwenda kwenye majimbo vijijini wakiuliza ni mtoto gani ana faida kati ya aliyesoma na ambaye hajasoma, wanajibu kuwa ambaye hajasoma ndiye mwenye faida kijijini, anayefuata wa darasa la saba, kisha wa kidato cha nne ndiyo anafuata wa chuo kikuu.

Ameongeza  kuwa wananchi wanasema mhitimu wa chuo kikuu ni kama viazi vilivyoshindwa kuiva kwa sababu hawezi kufanya kazi yoyote ikiwamo kulima, anabaki kusubiri ajira ambazo hazipo.

“Kama zimetangazwa nafasi 50 walioomba ni 40,000 na hawa ndio wana e-mail na internet, je ambao hawana e-mail na internet na walioghairi. Je, watu hawa wako wapi sasa hivi na wanafanya nini?” alihoji.

Alisema kuwa waziri amekuwa akisema anaboresha elimu, lakini hajui ni elimu ipi inayoboreshwa kwa sababu waliohitimu hawajapata kazi.

“Bidhaa inaboreshwa pale ambapo bidhaa uliyopeleka sokoni wateja wamesema tunataka bidhaa ya aina fulani. Ukisema unataka kuboresha elimu, unaboresha ipi kama watu walio bora hawajapata kazi,” amesema.

MWILI WA DKT. REGINALD MENGI KUWASILI NCHINI JUMATATU MEI 6, 2019

0
0
Mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Dkt. Reginald Mengi utawasili nchini Jumatatu 6, 2019 na ndege ya Shirika la ndege la Emirate ukitokea Dubai, Falme za Kiarabu, Mwanasheria wa familia ya Dkt. Mengi, Bw. Michael Ngalo amewaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Mei 3, 2019. 

Mwili wa Dkt. Mengi ambaye alifariki dunia akiwa huko Dubai usiku wa kuamkia Mei 2, 2019, ukishawasili jijini Dar es Salaam, utahifadhiwa kwenye hospitali Kuu ya Jeshi, Lugalo na siku inayofuata yaani Jumanne Mei 7, 2019, shughuli ya kuaga mwili huo itafanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar. 

Taarifa hiyo imeendelea kusema kuwa baada ya shughuli hiyo ya kutoa salamu za mwisho, mwili wa Dkt. Mengi utasafirishwa Jumatano Mei 8, 2019 kuelekea mahala alikozaliwa Machame, Mkoani Kilimanjaro ambapo shughuli za mazishi zitafanyika Alhamisi Mei 9, 2019.

TANZANIA YASHIKA NAFASI YA NNE KWA WATU WANAOAMINI UMILIKI WA ARDHI NA MAKAZI UKO SALAMA

0
0
Na Munir Shemweta, DODOMA

Tanzania imeshika nafasi ya nne kati ya nchi tisa za Kusini na Mashariki mwa Afrika zilizofanyiwa utafiti kwa kuwa na asilimia 64 ya watu wanaoamini kuwa hali ya umiliki wa ardhi na makazi ni salama.

Hayo yalibainika leo tarehe 3 Mei 2019 wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya Matokeo ya Utafiti wa Msingi kuhusu Haki na Usalama wa Umiliki wa Rasilimali Ardhi na Makazi Tanzania uliofanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu, uzinduzi ulifanyika jijini Dodoma.

Akizungumza wakati wa kuzindua Ripoti hiyo, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula alisema kiwango hicho ni kikubwa zaidi ya wastani wa asilimia 61 kwa nchi tisa zilizofanyiwa utafiti katika Afrika ya Magharibi.

Aidha, Utafiti wa Ripoti hiyo unaonesha Tanzania imeshika nafasi ya kumi kati ya nchi 33 zilizoshiriki katika Utafiti huo kwa kuwa na asilimia zaidi ya hamsini ya watu wanaomiliki makazi yao wenyewe.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alisema, matokeo ya utafiti huo yametokana na hatua mbalimbali ambazo serikali imeendelea kuzichukua ili kuhakikisha wananchi wake wanakuwa na usalama wa umiliki wa ardhi na makazi.

Kawa mujibu wa Dkt Mabula, kama ungefanyika utafiti mwingine leo basi huenda matokeo yake yangekuwa tofauti kutokana na Serikali kudhamiria kupanga , kupima na kumilikisha kila kipande cha ardhi na kutolea mfano katika mwaka wa fedha 2018/2019 Serikali ilipanga kupima na kumilikisha vipande vya ardhi.

Dkt Mabula alibainisha kuwa, takwimu zinaonesha kati ya mwezi Agosti 2018 na Machi 2019 Hatimiliki 36,428 zimeandaliwa kwa wamiliki wa viwanja na mashamba na Hatimili za kimila 286472 ziliandaliwa kwa ajili ya wamiliki wa ardhi walioko vijijini.

Dkt Mabula alisema, hatua nyingine ambazo serikali imechukua ni pamoja na kuanza kutumia mifumo ya kielektroniki katika utoaji huduma za ardhi ambapo Mfumo Unganishi wa Kumbukumbu za Sekta ya Ardhi (ILMIS) umeendelea kufanyiwa majaribio katika wilaya za Ubungo na Kinondoni na kusisistizia kuwa mfumo huo utasaidia kuongeza kasi ya umilikishaji ardhi na kupunguza gharama kwa kiasi kikubwa..

Kwa upande wake Mtakwimu Mkuu wa Serikali kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt Albina Chuwa alisema utafiti uliofanyika ulishirikisha sekta zote muhimu na kuzitaja baadhi yake kuwa ni pamoja na Wizara ya Ardhi, Global Land Allience, DFID sambamba na wananchi wote wakiwemo wakuu wa kaya za Tanzania Bara na Zanzibar.

Alisema, Tanzania ni nchi ya kwanza kutoa ripoti yake mwenyewe kati ya nchi 33 na ripoti hiyo itatumiwa na Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika kupanga mipango yake na kuzitaka taasisi za vyuo kutumia ripoti hiyo kufanyia utafiti ili kuisaidia sekta ya ardhi.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizindua Ripoti ya Matokeo ya Utafiti wa Msingi kuhusu Haki na Usalama wa Umiliki wa Rasilimali Ardhi na Makazi Tanzania jijini Dodoma leo tarehe 3 Mei 2019. Kushoto ni Mwakilishi wa kutoka Taasisi ya Prindex David Ameyaw na wa pili kulia ni Mtakwimu Mkuu Serikali Dkt Albina Chuwa.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akionesha Ripoti ya Matokeo ya Utafiti wa Msingi kuhusu Haki na Usalama wa Umiliki wa Rasilimali Ardhi na Makazi Tanzania baada ya kuizindua jijini Dodoma leo tarehe 3 Mei 2019. Kushoto ni Mwakilishi wa kutoka Taasisi ya Prindex David Ameyaw na wa pili kulia ni Mtakwimu Mkuu Serikali Dkt Albina Chuwa.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wawakilishi wa taasisi wakati wa uzindua Ripoti ya Matokeo ya Utafiti wa Msingi kuhusu Haki na Usalama wa Umiliki wa Rasilimali Ardhi na Makazi Tanzania jijini Dodoma leo tarehe 3 Mei 2019. Wa pili kushoto waliokaa ni Mwakilishi wa kutoka Taasisi ya Prindex David Ameyaw na wa pili kulia waliokaa ni Mtakwimu Mkuu Serikali Dkt Albina Chuwa.(PICHA NA WIZARA YA ARDHI)

WAZALISHAJI WA MAZAO YA NAFAKA NCHINI WAHIMIZWA KUONGEZA THAMANI BIDHAA ZAO

0
0
Wazalishaji wa mazao ya nafaka nchini wahimizwa kuongeza thamani bidhaa wanazozalisha nchini na sio kuuza mazao ghafi ili soko liweze kuongezeka na kuleta faida katika sekta ya kilimo inayochangia katika ukuaji wa uchumi nchini. 

Hayo yamesemwa na Mheshimiwa Richard Kasesela, Mkuu wa Wilaya wa Iringa alipokuwa akifungua mkutano wa wadau wa wazalishaji wa mazao ya nafaka nchini uliofanyika tarehe 3 Mei, 2019 mkoani Iringa uliondaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade). 

Akiongea na washiriki zaidi ya 150 amesema sekta ya kilimo inaajiri watanzania zaidi ya asilimia 67 na kuchangia katika pato la Taifa kwa asilimia 30 na kuingiza dola bilioni 1.2 ambazo ni chache ukilinganisha na ardhi tuliyonayo na inalisha asilimia 65 ya malighafi katika sekta ya viwanda na zaidi ya asilimia100 katika chakula. 

“Kuna bidhaa hatujaziendeleza hadi sasa na zina fursa nzuri sana kwenye masoko nje ya nchi kama vile cornflakes na zinaliwa nchi nzima na hadi sasa Watanzania hawajaamua kuwekeza kwenye viwanda vinavyozalisha bidhaa hizi” alisema Mhe Kasesela 

Aliongeza kwa kusema kuwa msingi wa ustawi wa kilimo ni upatikanaji wa soko la uhakika, katika kutekeleza hilo serikali ya awamu ya tano imetengeneza mazingira rafiki kupitia uwekezaji wa viwanda kwa kutumia malighafi zake nchini 

Ameiomba TanTrade isaidie wafanyabiashara nchini katika kufundisha mikakati mbalimbali ya biashara hasa kwa kuendana na mabadiliko ya kiteknolojia ili kuweza kufanya biashara kupitia simu za viganjani kupitia mifumo mbalimbali ya tehama. 

Alihitimisha kwa kutoa wito kuwa katika mkutano huo maazimio yajikite kwenye kutoa majibu ya ubora wa mbegu, namna ya uhifadhi bora wa mazao, kuondokana na kilimo cha kutegemea mvua hasa katika maeneo yanayopitiwa na mito kwa kutumia maji machache, kuboresha mifumo mizuri ya kupata takwimu sahihi, masoko na pia kufanya mkutano huu uwe endelevu kila mwaka na katika kila maazimio yanayotolewa kwenye mkutano maafisa biashara, kilimo na ushirika wa serikali lazima washiriki ili kuweza kusaidia katika kusimamia na kutekeleza maazimio ya kila mkutano 

Bw Edwin Rutageruka, Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade aliongeza kwa kusema kuwa mkutano huu utakuwa chachu kwa wazalishaji ili kuleta matokeo ya kuongeza uzalishaji, kuweza kutosheleza soko la ndani na kuangalia masoko katika nchi zinazotuzunguka katika ukanda wa Afrika Mashariki na nchi katika nchi wanachama wa jumuiya ya SADC 

Na amewasisitiza wazalishaji wa mazao ya nafaka nchini kushiriki katika Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam ambapo kutakuwa na mikutano ya wafanyabiashara (B2B) ili kuweza kupata masoko endelevu. 

Bw Ledis Kigala, Afisa Programu kutoka Baraza la Nafaka la Afrika Mashariki aliongeza kwa kusema kuwa, Tanzania inauza mazao ya nafaka kama vile mchele, mahindi na maharage katika nchi jirani. Wakulima wameweka nguvu zaidi kwenye uzalishaji wa mahindi meupe wakati asilimia 90 ya mahindi yanayozalishwa duniani ni ya Njano. 

Pia alisema kuwa kuna fursa kubwa ya masoko kwa mazao ya nafaka hasa mahindi na mtama kwaajili ya matumizi ya viwanda vya bia ingawa hadi sasa changamoto kubwa katika sekta ya mazao haya ni uwepo wa sumu kuvu na uhifadhi bora wa mazao. 

Nae Bi Karungi Gotifrid, Afisa Ubora kutoka Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko amewahimiza wakulima wa mazao ya nafaka kujiunga katika vikundi ili waweze kupewa elimu na alitoa vigezo vya mahindi yanayonunuliwa na Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko kama ifuatavyo unyevunyevu chini ya asilimia 13, mahindi yasiyokomaa chini asilimia 1, uchafu chini ya asilimia 1, mahindi yaliyooza na yenye ugonjwa hayatakiwi kuwepo ili kuepusha sumu kuvu, mahindi yaliyoliwa na wadudu hayatakiwi kuwepo kwasababu yanaondoa kiini ambacho kinahitajika kwa bianadamu vilevile mdudu hai haitajiki ndani ya magunia ya mahindi na pia mahindi yaliyovunjika yawe chini ya asilimia 1

TEN/MET, YAWASIMAMISHA WANAHABARI KUMKUMBUKA DK MENGI

0
0

Na Joachim Mushi

MTANDAO wa Elimu Tanzania (TEN/MET) jana uliwasimamisha waandishi wa habari mbalimbali kwa dakika moja kabla ya kuanza mkutano nao, ikiwa ni ishara ya kumkumbuka Marehemu Dk. Reginald Mengi Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP ambaye amefariki dunia.

Akizungumza kabla ya tukio hilo, Mratibu wa Taifa wa TEN/MET, Bw. Ochola Wayoga alisema Marehemu Mengi alikuwa mmoja wa wadau wa elimu na amefanya mambo mengi kuchangia mafanikio ya sekta hiyo hivyo wanakila sababu ya kumkumbuka.

"...TEN/MET imeguswa na msiba wa Marehemu Dk. Mengi kwa kuwa alikuwa mdau mzuri katika kuchangia elimu, amefanya mambo mengi kuchangia na kusaidia wahitaji katika elimu...naomba tusimame kwa dakika moja kumkumbuka," aliwaambia wanahabari.

Jana  TEN/MET ilikutana na waandishi wa habari mbalimbali jijini Dar es Salam kuzungumzia shughuli za maadhimisho ya Juma la ELimu (GAWE) linalo tarajia kufanyika mkoani Tanga katika Wilaya ya Handeni.

Mratibu wa Taifa wa TEN/MET, Bw. Wayoga akizungumzia maadhimisho hayo alisema mwaka huu yataanza Mei 6 hadi 10, 2019 katika Viwanja vya Shule ya Msingi Chanika, huku yakiambatana na mikutano vijiji mbalimbali kwa madhumuni ya kuhamasisha wanajamii kuhusu ushiriki wa pamoja na serikali katika kuboresha elimu iliyojumishi na endelevu.

"...Tarehe 10 Mei itakuwa ni kilele cha wiki ya uhamasishaji wa Elimu. Mgeni na mgeni wa Heshima atakuwa Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa. Kamati ya Maandalizi ya TEN/MET imeamua Kauli mbiu kwa Tanzania iwe ni: “ELimu Bora, Haki Yangu”.

Aidha alisema maadhimisho ya juma la elimu yatazinduliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mh. Suleman Jafo mkoani Tanga yatakayofanyika  Wilayani Handeni.

"...Tarehe 10 Mei itakuwa ni kilele cha wiki ya uhamasishaji wa Elimu. Mgeni na mgeni wa Heshima atakuwa Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa. Kamati ya Maandalizi ya TEN/MET imeamua Kauli mbiu kwa Tanzania iwe ni: “ELimu Bora, Haki Yangu”. Alisema Mratibu huyo.
Mratibu wa Taifa wa TEN/MET, Bw. Ochola Wayoga (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumzia maadhimisho ya Juma la Elimu (GAWE) linalotarajia kufanyika katika Wilaya ya Handeni, Mkoani Tanga. Kulia ni Mwenyekiti wa GAWE, James Ogondick na Ofisa Utetezi TEN/MET, Bw. David Sizya (kushoto). 
Sehemu ya waandishi wa hahabari kulia wakiwa wamesimama kwa dakika moja kabla ya kuanza mkutano wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET) na wanahabari kuzungumzia shughuli za maadhimisho ya Juma la ELimu (GAWE) linalo tarajia kufanyika mkoani Tanga katika Wilaya ya Handeni. 

Mratibu wa Taifa wa TEN/MET, Bw. Ochola Wayoga pamoja na meza kuu wakiwa wamesimama kwa dakika moja kabla ya kuanza mkutano wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET) na wanahabari kuzungumzia shughuli za maadhimisho ya Juma la ELimu (GAWE) linalo tarajia kufanyika mkoani Tanga katika Wilaya ya Handeni. 

WAANDISHI WA HABARI,WADAU WA HABARI SHINYANGA WAADHIMISHA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI

0
0

 Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Shinyanga 'Shinyanga Press Club - SPC) imeadhimisha siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari duniani na kutaka usalama wao uzingatiwe kwenye kipindi cha uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu pamoja na uchaguzi mkuu ujao mwaka 2020.

Maadhimisho hayo yamefanyika leo, Mei 3, 2019 kwenye ukumbi wa mikutano wa Liga Hoteli Mjini Shinyanga ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akimwakilisha mkuu wa mkoa huo Zainab Telack na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa habari mkoani Shinyanga wakiwemo viongozi wa kidini, siasa, makampuni,serikali na taasisi zisizo za kiserikali. 

Akizungumza kwenye maadhimisho hayo, Mkuu huyo wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko amewataka wanahabari mkoani Shinyanga kutumia kalamu zao vizuri kuhamasisha amani na utulivu vitawale kwenye kipindi cha uchaguzi wa Serikai za mitaa na uchaguzi mkuu ujao, ili wananchi waweze kuchagua viongozi wanaowataka kuwaletea maendeleo bila ya kubughuziwa. “Kauli mbiu yenu ya maadhimisho ya uhuru wa habari mwaka huu 2019 'ya “Jukumu la UTPC na Klabu za Waandishi wa habari kuchangia uchaguzi huru na haki”, 

imekuja kwa muda muafaka, ikiwa tunaelekea kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa ambapo waandishi wa habari ni kiungo muhimu kwenye uchaguzi huu ikiwamo kutoa taarifa kwa wananchi pamoja na kudumisha amani,”amesema Mboneko. “Hivyo nawaomba waandishi wa habari muitumie kalamu yenu vizuri sana kwenye kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa ili kutoa taarifa kwa wananchi juu ya umuhimu wa kupiga kura, pamoja na kulinda amani kwenye uchaguzi,”ameongeza Mboneko. 

Pia amewataka waandishi wa habari kujikita kuandika habari kwa wingi zenye kuhamasisha wawekezaji wa viwanda kwenda kuwekeza mkoani Shinyanga ili kuchochea ukuaji wa uchumi wa mkoa wa Shinyanga. Kwa upande wake Kaimu kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Lutusyo Mwakyusa, amewatoa wasiwasi waandishi wa habari na kuhusu usalama wa waandishi wa habari wakati wa uchaguzi akibainisha kuwa usalama utakuwepo juu yao kwenye kipindi hicho cha uchaguzi wa Serikali za mitaa na kutoa wito kwao huku akiwakumbusha kuwa kutokiuka miiko na maadili na taaluma zao. 

Naye Kaimu Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoani Shinyanga Shabani Alley, akisoma hotuba ya Klabu hiyo, amewaomba viongozi wa Serikali kufanya kazi kwa ukaribu na waandishi wa habari, ili kuutangaza mkoa huo pamoja na kudumisha amani na utulivu ili upate kukua kimaendeleo. 

"Waandishi wa habari mkoani Shinyanga tumejipanga vyema kushirikiana na serikali, wanasiasa na wadau mbalimbali katika kuhakikisha kuwa uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu ujao unakuwa wa haki,tunaomba tuendelee kushirikiana ili kuhakikisha mkoa wetu unakuwa salama na kukua kimaendeleo",aliongeza Alley.


Maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari mwaka huu 2019 yana kauli mbiu isemayo “Jukumu la UTPC na Klabu za waandishi wa habari kuchagia uchaguzi huru na haki” ambapo wadau wa habari na waandishi wa habari mkoani Shinyanga pia wamejadili pia kuhusu usalama wa mwandishi wa habari katika kipindi cha uchaguzi wa Serikali za mitaa na uchaguzi mkuu na umuhimu wa vyombo vya habari katika uchumi wa viwanda.  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Vyombo vya habari mkoa wa Shinyanga yaliyoandaliwa na Shinyanga Press Club. Mboneko aliwataka waandishi wa habari mkoani humo kutumia kalamu zao kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kupiga kura ili kuchagua viongozi sahihi pamoja na kudumisha amani. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga ,Shaban Alley,kulia ni Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga Lutusyo Mwakyusa. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akiwataka waandishi wa habari mkuano Shinyanga kujikita pia kuandika habari za kuchochea uwekezaji wa viwanda ili kukuza uchumi wa mkoa.  Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari mkoani Shinyanga Shabani Alley akisoma hotuba ya Klabu hiyo siku ya maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari duniani mwaka 2019.  Awali kabla ya kuanza kwa maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari mkoani Shinyanga, mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akiongoza Sala ya kumuombea Mmiliki na Mwanzilishi wa Makampuni ya IPP MEDIA Dkt. Reginald Mengi ambaye amefariki dunia jana akiwa Dubai kwa matibabu.Dkt. Mengi ni miongoni mwa watu ambao wana mchango mkubwa sana kwenye Tasnia ya Habari.  Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga Lutusyo Mwakyusa akiwahakikishia usalama wao waandishi wa habari kwenye kipindi cha uchaguzi wa viongozi wa Serikali za mitaa na uchaguzi mkuu ujao 2020.  Mkurugenzi msaidizi wa Radio Faraja FM Stereo Mjini Shinyanga Anikazi Kumbemba ambaye pia ni Mwandishi Mwandamizi akielezea dhumuni la maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari duniani.  Waandishi wa habari Mkoani Shinyanga wakiwa kwenye maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari.  Waandishi wa habari mkoani Shinyanga pamoja na wadau wakiwa kwenye maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari.  Wadau wa habari Mkoani Shinyanga wakiwa kwenye maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari duniani.  Maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari mkoani Shinyanga yakiendelea.  Waandishi wa habari na wadau wakiwa kwenye maadhimisho siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani.  Shabani Katambi ambaye ni mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini akichangia mada kwenye maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani mkoani Shinyanga.  Afisa maendeleo ya jamii manispaa ya Shinyanga Octavina Kiwone akichangia mada kwenye maadhimisho siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani na kuwataka waandishi mkoani Sinyanga wakijikite pia kuandika habari za kuhamasisha utalii ili Serikali iweze kupata mapato.  Diwani wa Kata ya Ngokolo manispaa ya Shinyanga Emmanuel Ntobi (CHADEMA)akichangia mada kwenye maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari duniani mkoani Shinyanga na kuwataka waandishi wa habari mkoani humo, waandike pia habari ya kufufua kiwanda cha Nyama ambacho hakifanyi kazi katika manispaa hiyo.  Waandishi wa habari na wadau wa habari wakiendelea kusikiliza uchangiaji wa mada kwenye maadhimisho hayo ya uhuru wa vyombo vya habari.  Kaimu Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt. Daniel Maguja akichangia mada kwenye maadhimisho ya uhuru wa habari na kuwataka wanahabari wajikite pia kwenye maadili pale wanapokuwa wakiandika habari zao ili kuepuka kujiingiza kwenye matatizo.  Mdau wa habari Chief Abdala Sube naye akichangia mada kwenye maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari na kuvipongeza vyombo hivyo namna vinavyofanya kazi ya kutetea maslahi ya wananchi kwa kutatua kero zao.  Mwenyekiti wa mtaa wa Dome manispaa ya Shinyanga Solomoni Najulwa 'Cheupe', akivipongeza vyombo vya habari namna vilivyosaidia kuunyosha mtaa huo ambapo ulikuwa ukikabiliwa na changamoto nyingi.  Waandishi wa habari wakiwa na wadau wa habari kwenye maadhimisho ya uhuru wa habari wakisikiliza uchagiaji wa mada mbalimbali.  Mwandishi wa habari wa Gazeti la Uhuru Chibura Makorongo akizungumza kwenye maadhimisho hayo ya uhuru wa vyombo vya habari, na kuwataka viongozi wa Serikali waboreshe mahusiano mazuri na wana habari ili kutangaza fursa za mkoa.  Wadau wa habari Mkoani Shinyanga wakiwa kwenye maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari duniani.  Waandishi wa habari mkoani Shinyanga wakipiga picha ya pamoja na wadau wa habari mara baada ya kumaliza kuadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani. Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog

WAANDISHI WALIA KUFANYA KAZI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU,BILA MIKATABA,BILA MISHAHARA/IKIWEPO NI FINYU

0
0

Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Jonathan Shana akizungumza na waadhishi wa habari mkoani Arusha katika siku ya Maadhimisho ya Uhuru wa vyombo vya habari Duniani yanayofanyika kila mwaka 3 .Mei
Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa Habari Mkoani Arusha Cloud Gwandu katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Golden Rose Hotel
Victor Maleko Meneja programu kutoka Umoja wa Vilabu vilabu vya waandishi wa habari Tanzania UTPC.amesema bado hawatanyamaza hadi tujue hatma ya waandishi wa habari,bora tuendelee kupiga kelele tu.
Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa(Utawala)wa Arusha David Lyamongi akizungumza na waandishi akimuwakilisha RAC Richard Kwitega.

Baadhi ya waandishi kushoto Lilian Joel wa gazeti la uhuru na Cythia Mwilolezi kutoka gazeti la Nipashe ,wakifuatilia mambo kwa makini
Waandishi wa vyombo mbalimbali Jijini Arusha.
Waandishi wa habari wakiwa kwenye mkutano ,wa kuadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani.
Waandishi wakifuatilia mada kwa makini
Waandishi wakifuatilia kinachoende
Waandishi wakiwa katika ukumbi wa mkutano tayari kwa kuanza kongamano la maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo ya habari duniani.
Mwandishi Abraham Gwandu akifuatilia jambo kwa makini katika kongamano la siku moja la maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari Jijini Arusha,akiwa na Seif Mangwangwi
Grace Macha mwandishi wa Tanzania Daima akiwa katika kongamano la siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani Jiji Arusha.
Kutoka kushoto ni Shaban Mdoe Katibu mwenezi wilaya ya Arumeru,Katikati Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari Jijini Arusha Cloud Gwandu na Afisa programu Victor Maleko kutoka UTPC.


Na.Vero Ignatus ,Arusha.

Katika kuadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani,waandishi wa habari mkoani arusha wamekutana kwa pamoja ili kujadili na kuangalia changamoto mbalimbali wanazokutana nazo katika utekelezaji wao wa ukusanyaji wa habari wa kila siku na namna yavkupata ufumbuzi.

Akizungumza mwenyekiti wa Klabu ya waandishi mkoani hapo Claud Gwandu amesema kwa sasa kilio kikubwa cha waandishi ni kufanya kazi katika vyombo vya habari bila malipo,kukosa mikataba sambamba na kutopewa ushirikiano wakati wa utafutaji wa habari.

Gwandu amesema wanahabari wengi wanafanya kazi bila mikataba,malipo yanakuwa duni sana au hakuna kabisa, amesema, kinakosekana chama cha wafanyakazi waandishi wa habari,jambo ambalo inapelekea kutoonekana dalili za matatizo ya waandishi hayatatuliwi kwa haraka.

"Tunakosa chama cha wafanyakazi waandishi wa habari ,jambo ambalo linatupa wasiwasi kutoona wapi matatizo yetu yanashughulikuwa kwa haraka ukizingatia sisi ndiyo tunahabarisha umma,tunaelimisha,na tunaonya pia.alisema Gwandu"

Amesema waandishi wanafanya kazi katika mazingira magumu bila kuwa na mikataba,bila mishahara,ameviomba vyama vya utetezi wa haki za binadamu kuangalia upya swala hili dhidi ya wanahabari kufanya kazi bila kulipwa maana huo ni sawa na utumwa wa aina fulani.

Kwa upande wake Meneja Programu kutoka Umoja wa vilabu vya waandishi wa habari nchini (UTPC) Victor Maleko amesema kuwa hawajachoka kufanya kazi ambayo zitahakikisha kila mwandishi atakuwa sawa na kupata stahiki zake.

Ni kweli waandishi wanafanya kazi katika mazingira magumu,ya vitisho,kupotea katika mazingira ya kutatanisha,kupoteza maisha , ila hatutakaa kimya tunaendelea kupiga kelele hadi tutakapojua hatma ya waandishinwa habari alisema."UTPC kuna utaratibu tunmalizia kuuweka wa kuhakikisha kila mwanahabari anapata stahiki zake kulingana na kazi zake"

Kwa upande wake mgeni rasmi katika maadhimisho hayo Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Jonathan Shana amewataka waandishi amewataka kuzingatia utanaduni,uzalendo,

kutumia kalamu zao vizuri,kutetea uhuru wa watu binafsi na ziwalinde wao wenyewe,na kuzilinda habari walizoziandika."Kalamu za waandishi wa habari ni silaha, zinaweza kuua, kujeruhi na kuokoa,zitumieni vizuri kwa kuilinda Amani ya nchi,uzalendo na utamaduni wa nchi yenu'' akisema Shana.

Kamanda Shana amezungumzia pia kuhusiana na haki za watoto haswa katika mkoa wa Arusha kumekuwa na wimbi la kulawitiwa na kubakwa kwa watoto ambapo kesi zake wazazi wanamalizana na wanaukoo,amesema swala hilo halitafumbiwa macho akibainika mazazi au mlezi amepewa hongo Jeshi la polisi litashughulika nae ipasavyo.

Pia amewataka waandishi kuwa mstari wa mbele kwa kutumia kalamu zao vizuri kupinga ndoa za jinsia moja ambayo ni kinyume na maadili na utamaduni wa Taifa la Tanzania kwani hata vitabu vya dini vinapinga swala hilo.

Pia amewahakikishia waandishi ulinzi na usalama wakati wa Uchaguzi wa serikali za mitaa pamoja na ule wa 2020. Kwa upande wake Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa(Utawala)wa,Arusha David Lyamongi ambae alimuwakilisha Katibu Tawala mkoa Richard Kwitega amesema wanatambua umuhimu na thamani ya waandishi wa habari na utendaji kazi wao.

Akijibu swali lililoulizwa na mmoja wa waandishi kuhusiana na vitisho kutoka kwa baadhi ya viongozi amesema kuwa mkoa wa Arusha hawapo katika muundo huo bali wameendelea kushirikiana na vyombo vya habari kwa hali mzuri

Amesema swala hilo la kamatakamata la waaandishi wa habari halijawekwa wazi linafanywa na uongozi wa mkoa,wilaya ,kata,amesema wataendelea kulinda haki za waandishi,amesema atapeleka taarifa hizo kwa uongozi wa mkoa kama kuna chombo chochote kile kinachoonea waandishi wa habari atoe maelekezo yake kudhibiti hali.

Maadhimisho hayo yamebeba kauli mbiu isemayo jukumu la UTPC na klabu za waandishi wa habari kuchangia uchaguzi huru na wa haki.

UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM) WAPEWA MAELEKEZO YA KUJIZATITI KATIKA MAPAMBANO YA KUJIKOMBOA KIUCHUMI

0
0
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeweka bayana msimamo na mwelekeo wake katika masuala ya Kilimo na Viwanda, Ulinzi na Usalama na Sayansi na Teknolojia katika muktadha wa mapambano ya kujikomboa kiuchumi na mwelekeo wa siasa za kidunia.

Akizungumza katika Mkutano Maalum wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Ndg. Bashiru Ally Katibu Mkuu wa CCM amesema katika mazingira ya sasa ya kidunia mapambano ya kiuchumi yamejikita katika namna ambavyo nchi masikini zinasimamia ipasavyo sekta ya kilimo, uzalishaji wa kilimo wenye tija sambamba na viwanda vitakavyochakata bidhaa za kilimo na kujenga uwezo wa kuzalisha chakula, kujitosheleza ndani na ziada.

Ndg. Bashiru Ally amefafanua unyeti wa suala la ulinzi na usalama na kwamba vijana ndio walinzi wa mwanzo na wananchi kwa ujumla, hivyo uzalendo, nidhamu, kufanya kazi, utii na kujitoa ni misingi muhimu kwa vijana wa CCM. Aidha, ameeleza jitihada zetu za kujikomboa kiuchumi hazitapokelewa vizuri na wasiotutakia mema na maadui zetu ambao wako ndani na nje ya nchi, na kwa mantiki hii vijana wa kitanzania wana jukumu ya kuilinda nchi yetu, kutetea msimamo wetu, kuyasemea mazuri yanayofanywa na Serikali yetu.

Akizungumzia kuhusu Sayansi na Teknolojia Ndg. Bashiru Ally Katibu Mkuu wa CCM ameeleza wigo wa Sayansi na Teknolojia ndio ulipo uwanja wa mapambano na ni muhimu kujihami mapema na kuwa tayari kukabiliana mashambulizi ya kimtandao, wanaotumia mitandao kupotosha kazi nzuri inayofanyika katika nchi yetu lazima wajibiwe kwa hoja na kwa ushahidi wakati wote.

Ndugu Bashiru Ally amewataka wajumbe wa Mkutano Maalum wa Baraza Kuu la UVCCM kutupatia aina ya Kiongozi (Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa kutoka vijana) ambaye anaelewa mazingira tuliyomo na awe tayari kusimama imara kuulinda Muungano wetu, kujenga umoja, kulinda uhuru wetu, mtu mwenye msimamo usioyumba, atakayelinda heshima ya viongozi wetu na anayeakisi maono na mwelekeo wa Ndg. John Pombe Joseph Magufuli Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Vitendo vya ukabila, udini, ubaguzi wa rangi, vitendo vya rushwa, kila jambo linalokwenda kinyume na Katiba, Kanuni na desturi nzuri za Chama Cha Mapinduzi (CCM) havina nafasi katika Umoja wa Vijana wa CCM amesema Ndg. Bashiru Ally akihitimisha hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano Maalum wa Baraza Kuu ya UVCCM.

Mkutano Maalum wa Baraza Kuu la UVCCM unaketi kuchagua Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa anayewakilisha Umoja wa Vijana baada ya nafasi hiyo kuwa wazi, umehudhuriwa na Ndg. Humphrey Polepole Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi na Mzee Kombo Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM pamoja na Viongozi wa UVCCM wakiongozwa na Ndg. Kheri James Mwenyekiti wa UVCCM.

Imetolewa na,

*IDARA YA ITIKADI NA UENEZI*
*CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)*

WATANZANIA WAISHIO UK WAKUBALI KUUNGA MKONO JITIHADA ZA RAIS MAGUFULI

0
0
 Mbunge wa Busega Dkt Raphael Chegeni akiwa na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Dk.AshaRose Migiro mara baada ya kufanya mazungumzo na watanzania wanaokaa na kufanya kazi Uingereza katika fani mbalimbali za afya na biashara. 

Watanzania hao wamekubali kupitia umoja wao kuunga jitihada za  Rais Dk.John Magufuli katika kusaidia upatikanaji wa vifaa muhimu vya kisasa, kuchangia fedha na watalaam wa afya ili kuboresha huduma za afya nchini. 

Watanzania hao wamepongeza jitihada za serikali ya awamu ya tano katika ujenzi na uboreshaji wa huduma za afya mijini na vijijini ambapo serikali imekuwa ikijenga Hospitali, vituo vya afya na Zahanati katika kila Kata.
 Mbunge wa Busega, Dk. Raphael Chegeni akizungumza na Baadhi ya maofisa wa Ubolozi wa Tanzania nchini Uingereza. Kulia kwake ni Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Dk.AshaRose Migiro.
Picha ya pamoja 

Serikali yasisitiza majadiliano kuboresha sekta ya habari

0
0
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Serikali imesema haina mpango wa kuendelea kuvifungia vyombo vya habari vinavyokiuka kisheria kwenye utekelezaji wa majukumu na badala yake itaendelea kutumia njia ya majadiliano pale inapotokea changamoto ya kiutendaji.


Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas aliyasema hayo jana jijini Dodoma wakati akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwenye kilele cha maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2019.


Dkt. Abbas alisema ni vyema wadau wa habari wakaunda kamati maalum itakayoketi na kujadiliana na Serikali kuhusiana na changamoto mbalimbali wanazodhani ni vikwazo kwenye utekelezaji wa majukumu yao ikiwemo vifungu na sheria za habari.


Aidha Dkt. Abbas aliwahimiza wadau wa habari kuzisoma na kuzielewa vyema sheria hususani Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari ya mwaka 2016 ili wanapokutana na Serikali kwenye majadiliano wawe na uelewa wa kutosha kuelezea vifungu vyenye changamoto tofauti na hivi sasa ambapo baadhi wanalalamika bila kuweka wazi vifungu gani vina mapungufu.


Katika maadhimisho hayo, washiriki walipendekeza maazimio 16 ikiwemo kuunda kamati itakayoketi na Serikali kujadiliana baadhi ya changamoto zinazokwamisha uhuru wa habari kama vile kufungia vyombo vya habari pamoja na kanuni zenye vikwazo kwenye Sheria ya Huduma za Huduma za Vyombo vya Habari ya mwaka 2016.


Taasisi mbalimbali zilishiriki kufanikisha maadhimisho hayo ikiwemo MISA Tanzania, Ubalozi wa Marekani, Internews, FES, IMS, Umoja wa Mataifa, UTPC, TMF, TEF, UK Aid, TAMWA, MCT, Unesco na Serikali ya Tanzania huku kauli mbiu ikiwa ni “wajibu wa vyombo vya habari kwa demokrasia, tasnia ya habari na uchaguzi nyakati za upotoshaji wa taarifa”.

Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Dkt. Inmi Patterson akizungumza kwenye maadhimisho hayo ambapo alisisitiza juu ya uhuru wa vyombo vya habari katika kutimiza majukumu yake bila kuingiliwa.
Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Mhe. Sarah Cooke akitoa salamu zake kwenye maadhmisho hayo.
Mkurugenzi wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Abubakary Karsan akichangia mada kwenye maadhimisho hayo.
Afisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa ofisi ya Tanzania, Stella Vuzo akitoa salamu za Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres kwenye maadhimisho hayo.
Washiriki wa maadhimisho hayo wakifuatilia ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres kwa njia ya vidio.
Fuatilia matukio katika picha kwenye maadhimisho hayo.
Washiriki wa maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2019 kitaifa jijini Dodoma wamesimama kwa muda kama ishara ya kumuombea aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT) na pia mmiliki wa makampuni ya IPP, Dkt. Reginald Mengi aliyefariki usiku wa kuamkia jana nchini Dubai akiwa na miaka 77.
Washiriki wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Washiriki wakifuatia mada kwenye maadhimisho hayo.
Mkurugenzi wa Misa Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Dkt. Hassan Abbas (kushoto) baada ya kuwasili kwenye maadhimisho hayo.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Dkt. Hassan Abbas akiwa na Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Dkt. Inmi Patterson pamoja na viongozi kutoka taasisi mbalimbali kutembelea mabanda ya maonyesho ya kitaaluma kwenye maadhimisho hayo.
Wachezaji wa ngoma za asili kutoka kabila la Wagogo walinogesha mapokezi ya washiriki na viongozi mbalimbali.
SOMA>>> MISA Tanzania yasisitiza umoja ili kupambana na ukiukwaji wa uhuru wa habari.Picha na KD Mula

Serikali yasisitiza majadiliano kuboresha sekta ya habari

0
0
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Serikali imesema haina mpango wa kuendelea kuvifungia vyombo vya habari vinavyokiuka kisheria kwenye utekelezaji wa majukumu na badala yake itaendelea kutumia njia ya majadiliano pale inapotokea changamoto ya kiutendaji.


Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas aliyasema hayo jana jijini Dodoma wakati akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwenye kilele cha maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2019.


Dkt. Abbas alisema ni vyema wadau wa habari wakaunda kamati maalum itakayoketi na kujadiliana na Serikali kuhusiana na changamoto mbalimbali wanazodhani ni vikwazo kwenye utekelezaji wa majukumu yao ikiwemo vifungu na sheria za habari.


Aidha Dkt. Abbas aliwahimiza wadau wa habari kuzisoma na kuzielewa vyema sheria hususani Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari ya mwaka 2016 ili wanapokutana na Serikali kwenye majadiliano wawe na uelewa wa kutosha kuelezea vifungu vyenye changamoto tofauti na hivi sasa ambapo baadhi wanalalamika bila kuweka wazi vifungu gani vina mapungufu.


Katika maadhimisho hayo, washiriki walipendekeza maazimio 16 ikiwemo kuunda kamati itakayoketi na Serikali kujadiliana baadhi ya changamoto zinazokwamisha uhuru wa habari kama vile kufungia vyombo vya habari pamoja na kanuni zenye vikwazo kwenye Sheria ya Huduma za Huduma za Vyombo vya Habari ya mwaka 2016.


Taasisi mbalimbali zilishiriki kufanikisha maadhimisho hayo ikiwemo MISA Tanzania, Ubalozi wa Marekani, Internews, FES, IMS, Umoja wa Mataifa, UTPC, TMF, TEF, UK Aid, TAMWA, MCT, Unesco na Serikali ya Tanzania huku kauli mbiu ikiwa ni “wajibu wa vyombo vya habari kwa demokrasia, tasnia ya habari na uchaguzi nyakati za upotoshaji wa taarifa”.

Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Dkt. Inmi Patterson akizungumza kwenye maadhimisho hayo ambapo alisisitiza juu ya uhuru wa vyombo vya habari katika kutimiza majukumu yake bila kuingiliwa.
Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Mhe. Sarah Cooke akitoa salamu zake kwenye maadhmisho hayo.
Mkurugenzi wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Abubakary Karsan akichangia mada kwenye maadhimisho hayo.
Afisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa ofisi ya Tanzania, Stella Vuzo akitoa salamu za Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres kwenye maadhimisho hayo.
Washiriki wa maadhimisho hayo wakifuatilia ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres kwa njia ya vidio.
Fuatilia matukio katika picha kwenye maadhimisho hayo.
Washiriki wa maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2019 kitaifa jijini Dodoma wamesimama kwa muda kama ishara ya kumuombea aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT) na pia mmiliki wa makampuni ya IPP, Dkt. Reginald Mengi aliyefariki usiku wa kuamkia jana nchini Dubai akiwa na miaka 77.
Washiriki wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Washiriki wakifuatia mada kwenye maadhimisho hayo.
Mkurugenzi wa Misa Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Dkt. Hassan Abbas (kushoto) baada ya kuwasili kwenye maadhimisho hayo.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Dkt. Hassan Abbas akiwa na Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Dkt. Inmi Patterson pamoja na viongozi kutoka taasisi mbalimbali kutembelea mabanda ya maonyesho ya kitaaluma kwenye maadhimisho hayo.
Wachezaji wa ngoma za asili kutoka kabila la Wagogo walinogesha mapokezi ya washiriki na viongozi mbalimbali.
SOMA>>> MISA Tanzania yasisitiza umoja ili kupambana na ukiukwaji wa uhuru wa habari.Picha na KD Mula

Shule za Serikali Zaongoza Uandishi wa Insha, EAC na SADC

0
0
Na Lilian Lundo - MAELEZO, Dodoma
Wanafunzi Innocent Shirima na Sada Kimangale kutoka shule za Sekondari Moshi (Kilimanjaro) na shule ya Sekondari Kwemnabara (Tanga) wameshinda nafasi ya kwanza ya uandishi wa insha wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) kwa mwaka 2018.
Wanafunzi hao wamepewa vyeti na zawadi kwa ngazi ya kitaifa, leo Jijini Dodoma na Kaimu Katibu Mkuu ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Dkt. Ave Maria Semakafu.
Akitoa hotuba wakati wa utoaji wa vyeti kwa wanafunzi hao, Dkt. Semakafu amesema Watanzania waache kujizalilisha kwa kusema shule za Serikali sio bora, kwani watoto hao wanaozalilishwa wakienda kwenye ngazi ya Kimataifa wanafanya vizuri.
"Tukio la leo linatuma ujumbe kwa wale wote wanaoiponda elimu ya Tanzania, kwani washidi wa kwanza wa insha za EAC na SADC wote wanatoka katika shule za Serikali  ambazo zinapondwa kila siku," amesema Dkt. Semakafu.
Ameeleza kuwa, walioifikisha Tanzania hapa ilipo ni Watanzania waliosoma hapahapa Tanzania na wala sio watu waliosoma nje ya Tanzania.
Aidha amempongeza Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kufungua na kupaanua wigo wa elimu kwa Serikali kulipa gharama za wanafunzi hivyo kuwezesha watoto wote wa Tanzania kupata fursa kupata elimu.
Kwa upande wake, Mratibu wa mashindano hayo kutoka Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Sylivia Chinguwile amesema mashindano ya uandishi wa insha yamekuwa chachu kwa vijana kufanya utafiti, kujifunza na kufahamu vizuri mchakato na hatua mbalimbali za uimarishaji mahusiano kwa nchi wanachama.
"Mada zinazoshindaniwa huzingatia makubaliano ya wakuu wa nchi, baada ya hapo kila nchi wanachama huwajibika kutangaza na kubainisha vigezo vya ushiriki kama inavyoelekezwa na sekretarieti za jumuiya husika," ameeleza Sylivia.
Amesema, insha hizo huwasilishwa wizarani baada ya kuteuliwa insha bora katika ngazi ya shule na kusahihishwa na jopo la wataalam, ambapo insha bora za SADC hupelekwa Botswana, makao makuu ya SADC ili kushindanishwa na mataifa wanachama wa Jumuiya hiyo.
Kwa upande wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, insha tano bora hupelekwa Arusha makao makuu ya Jumuiya kwa ajili ya kushindanishwa na mataifa wanachama wa Jumuiya hiyo.
Naye, Mshindi wa insha za Jumuiya ya Afrika Mashariki, Innocent Shirima ambaye pia ni mlemavu wa macho, amesema mashindano yamewapa fursa ya kujifunza masuala ya jumuiya hiyo.
Hata hivyo, ameomba waratibu wa mashindano hayo kuweka kipaumbele  matumizi ya lugha ya kiswahili katika uandishi wa insha ili kuangaza zaidi lugha ya Kiswahili nje ya mipaka ya Tanzania.
Washindi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Kitaifa ni Paschal Thomas kutoka Shule ya Sekondari Kibaha (Pwani), Lazarius Yamawasa kutoka Shule ya Sekondari Mzumbe (Morogoro),  Innocent Shirima kutoka Shule ya Sekondari Moshi (Kilimanjaro), Nasra Kondo kutoka Shule ya Sekondari Kifungilo (Tanga), Hanifa Gunter Harms kutoka Shule ya Sekondari Heritage (Pwani), Mwanaisha Mwalimba kutoka Shule ya Sekondari Kwemkabala (Tanga), Asha Pazi kutoka Shule ya Sekondari Kilangalanga Sekondari (Pwani), Jacquiline Kassian kutoka Shule ya Sekondari Harrison UWATA (Mbeya), Samweli Chale kutoka Mbagala Sekondari (Dar es Salaam) na Coloniel Jishosha kutoka Shule ya Sekondari Shinyanga (Shinyanga).
Washindi wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika ni Sada Kimangale kutoka Shule ya Sekondari Kwemnabara  (Tanga), David Mkinga kutoka Shule ya Sekondari St. Augustine Tagaste (Dar es Salaam) na Alex Paul kutoka Shule ya Sekondari Longido (Arusha).
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Ave Maria Semakafu akizungumza wakati wa hafla fupi ya kutoa zawadi kwa wanafunzi walioshinda mashindano hayo kwa mwaka 2018 leo jijini Dodoma.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Ave Maria Semakafu akizungumza wakati wa hafla fupi ya kutoa zawadi kwa wanafunzi walioshinda mashindano hayo kwa mwaka 2018 leo jijini Dodoma.
 Mratibu wa Mashindano ya Insha kwa wanafunzi wa Shule za Sekondari toka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Bi.Sylivia Chinguwile akizungumza wakati wa hafla fupi ya kutoa zawadi kwa wanafunzi walioshinda mashindano hayo kwa mwaka 2018 leo jijini Dodoma. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Ave Maria Semakafu na kushoto ni Kaimu Kamishna wa Elimu Tanzania.

 Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu na Huduma za Jamii toka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Eliabi Chodata akielezea namna ushiriki wa mashindano hayo kwa upande wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakati wa hafla fupi ya kutoa zawadi kwa wanafunzi walioshinda mashindano hayo kwa mwaka 2018 leo jijini Dodoma.
 Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Moshi ya Watu wenye mahitaji maalum, Innocent Shirima  Akitoa neon la shukrani kwa niaba ya wenzake wakati wa hafla fupi ya kutoa zawadi kwa wanafunzi walioshinda mashindano hayo kwa mwaka 2018 leo jijini Dodoma.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Ave Maria Semakafu akimkabidhi Cheti cha Pongezi Mshindi wa Mashindano ya Insha kwa Wanafunzi wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Sada  Kimangale kutoka Shule ya Sekondari Kwemkabara ya wilayani Muheza mkoani Tanga leo wakati wa hafla ya kuwapa zawadi washindi wa mashindano hayo kwa mwaka 2018 leo jijini Dodoma.Kulia ni Mzazi wa mwanafunzi huyo.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Ave Maria Semakafu akimkabidhi Cheti cha Pongezi na fedha taslimu shilingi Laki Tano Mshindi wa Mashindano ya Insha kwa Wanafunzi wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Innocent Shirima kutoka Shule ya Sekondari Moshi ya Watu wenye mahitaji Maalum. Kulia ni Mkuu wa Shule hiyo hiyo  leo wakati wa hafla ya kuwapa zawadi washindi wa mashindano hayo kwa mwaka 2018 leo jijini Dodoma.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Ave Maria Semakafu akimkabidhi zawadi ya fedha Dola za Kimarekani 500 Mshindi wa Mashindano ya Insha kwa Wanafunzi wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Sada  Kimangale kutoka Shule ya Sekondari Kwemkabara ya wilayani Muheza mkoani Tanga leo wakati wa hafla ya kuwapa zawadi washindi wa mashindano hayo kwa mwaka 2018 leo jijini Dodoma.Kulia ni Mzazi wa mwanafunzi huyo.Kushoto ni Bibi. Agnesi Kayola Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda toka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Ave Maria Semakafu akimkabidhi Cheti cha Pongezi Mshiriki wa Mashindano ya Insha kwa Wanafunzi wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), na Jumuiya ya Afrika Mashariki, Hanifa Harms kutoka Shule ya Sekondari Heritage ya Kibaha Pwani wakati wa hafla ya kuwapa zawadi washindi wa mashindano hayo kwa mwaka 2018 leo jijini Dodoma.Kulia ni Mzazi wa mwanafunzi huyo. Bi. Shamim Yunga.
 Baadhi ya wanafunzi walioshinda Mashindano ya Insha kwa Wanafunzi wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki wakifuatilia zoezi la utoaji zawadi wakati wa hafla fupi ya kuwapa zawadi washindi wa mashindano hayo kwa mwaka 2018 leo jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Ave Maria Semakafu akiwa katika picha ya pamoja na Washindi wa Mashindano ya Insha kwa Wanafunzi wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na wazazi wao mara baada ya kumaliza hafla fupi ya kuwapa zawadi washindi wa mashindano hayo kwa mwaka 2018 leo jijini Dodoma. (Picha na Idara ya Habari –MAELEZO).
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live




Latest Images