Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1838 | 1839 | (Page 1840) | 1841 | 1842 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akipongezana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na baadhi ya viongozi wengine mara baada ya kufunga jiwe la msingi kuashiria uzinduzi rasmi wa Mji wa Serikali katika eneo la Mtumba leo jijini Dodoma.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo mara baada ya kukata utepe kwenye jengo la Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora kuashiria uzinduzi wa Mji wa Serikali katika eneo la Mtumba leo jijini Dodoma. Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi, Mhadisi Balozi John Kijazi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, George Mkuchika, Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais Mstaafu, Mzee Samwel Malecela, Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli,Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Salma Kikwete, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Bashiru Ally.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mji wa Serikali ulijengwa katika eneo la Mtumba jijini Dodoma leo.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia Mkuu wa Majeshi na Ulinzi, CDF, Venance Mabeyo akimbadilishia cheo kutoka Kanali hadi kuwa Brigedia Jenerali wa Jeshi la Wananchi Tanzania(JWTZ), Brigedia Jenerali Charles Mbuge wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mji wa Serikali ulijengwa katika eneo la Mtumba jijini Dodoma leo. Wengine wanaoshuhudia zoezi hilo ni Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, Simon Sirro. Brigedia huyo amepewa cheo hicho na Mhe. Rais kufuatia uchapakazi wake katika kusimamia miradi ya ujenzi mbalimbali inayotekelezwa na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kwa kushirikiana na JKT. Baadhi ya wananchi na wabunge wakifuatila hafla ya uzinduzi wa Mji wa Serkali uliojengwa katika eneo la Mtumba jijini Dodo leo. Mkurugenzi wa Idara ya Habari - MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akiteta jambo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Adeladius Kilangi, Waziri wa Madini, Doto Biteko, na Waziri wa Nishati, Selemani Jaffo walipokutana katika hafla ya hafla ya uzinduzi wa Mji wa Serikali ulijengwa katika eneo la Mtumba jijini Dodoma leo.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kikosi Kazi kilichoratibu zoezi la Serikali Kuhania Dodoma mara baada ya uzinduzi wa Mji wa Serikali katika eneo la Mtumba leo jijini Dodoma.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Baadhi ya Mawaziri na Manaibu Waziri wa Wizara mbalimbali mara baada ya uzinduzi rasmi wa Mji wa Serikali katika eneo la Mtumba leo jijini Dodoma. .(Picha na Frank Shija - MAELEZO).

  0 0

  Na Immaculate Makilika- MAELEZO 

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa ni lazima kutekeleza masuala mbalimbali aliyoyaahidi Watanzania wakati akiingia madarakani mwaka 2015, ambayo yanalenga kuwaletea wananchi maendeleo. 

  wakati alipokuwa akizindua mji wa Serikali uliopo katika kata ya Mtumba jijini Dodoma, Rais Magufuli alisema kuwa aliamua kutimiza ahadi ya Rais wa Awamu ya Kwanza, Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere aliyoitoa mwaka 1973 ya kulifanya jiji la Dodoma kuwa makao makuu ya nchi. 

  Rais Magufuli alisema “Nataka yote tuliyoyaahidi tuyatekeleze, nataka ofisi hizi nzuri tulizojenga ziwe na watu, na zianze kutoa huduma kwa wananchi” 

  Alisisitiza, “ jukumu langu lilikuwa kutekeleza ahadi ya Mwalimu Nyerere, na nilipata nguvu baada ya kukumbuka kuwa ziko nchi nyingi tu duniani ikiwemo nchi za Afrika kama Nigeria na Cote d’Ivoire ambazo zilihamisha makao makuu ya nchi yao katika kipindi kifupi, nataka kuwahakikishia na mimi nakuja Dodoma kwa sababu hakuna kinachonichelewesha” 

  Aidha, Rais Magufuli alisema kuwa Serikali inaendelea kukamilisha mifumo na ujenzi wa miradi mbalimbali kwa ajili ya kutoa huduma kwa watumishi wa umma ambao watahamia na kufanya kazi katika majengo hayo ikiwa ni pamoja na kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi wanaofika katika mji huo wa Serikali, ikiwa ni sambamba na kuboresha jiji la Dodoma. 

  Alitaja miradi hiyo kuwa ni ujenzi wa barabara itakayogharimu bilioni 500 kwa mkopo wa fedha kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) itakayojengwa kutokea Mtumba, Veyula na Nala ambayo ina urefu wa kilomita 4. 

  Vile vile amesema, serikali inaendelea na ujenzi wa uwanja wa ndege mkubwa na wa kimataifa unaogharimu bilioni 400 pia inafanya maandalizi ya ujenzi wa Bandari kavu kwa vile jiji la Dodoma lina kituo kikuu cha reli ya kisasa (SGR). 

  Katika jitihada za Serikali za kuliboresha jiji la Dodoma ambalo ni Makao Makuu ya nchi, Serikali imepanga kujenga shule ya sekondari ya kisasa itakayogharimu shilingi bilioni 13na Chuo cha mafuzo (VETA) kitakachogharimu shilingi bilioni 18. Ikiwa ni pamoja na kuendelea kuimarisha hospitali ya Benjamini Mkapa ambayo imeanza kutoa matibabu ya kibingwa. 

  Aidha, Rais Magufuli alilipongeza Jeshi la Wananchi kwa kujenga majengo hayo ya mji wa Serikali, pamoja na kushiriki katika ujenzi wa miradi mbalimbali ya Serikali ikiwemo ukuta wa Mererani uliopo Arusha, ambapo amempandisha cheo msimamizi wa miradi hiyo ya ujenzi Kanali Charles Mbuge pamoja na kutoa ajira kwa vijana walioshiriki katika ujenzi huo. 

  Rais Magufuli, “Kanali Mbuge atakuwa Brigedia kuanzia leo, nataka ufanyike utaratibu wa kumuongezea vyeo ufanyike na aendelee na hii kazi. Tuwe na kikosi cha ujenzi na kiongozwe na Mbuge ili kusaidia kufanya maajabu katika nchi hii, nawapongeza Jeshi la Wananchi, kwani mnafanyakazi nzuri” 

  Kwa upande wake, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amempongeza RaisMagufuli kwa uamuzi wake wa kuhamishia makao makuu ya nchi Dodoma kwani uamuzi huo utasaidia kusogeza huduma kwa wananchi, pamoja na kusaidia ukuaji wa uchumi katika mikoa iliyopo katikati ya nchi. 

  Naye, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu Jenista Mhagama, alisema kuwa katika uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano miradi mbalimbali imetekelezwa katika jiji la Dodoma ikiwemo uzalishaji umeme megawati 48, huku mahitaji halisi yakiwa megawati 28. 

  Akitaja baadhi ya miradi mingine inayoendelea kutekelezwa kuwa ni pamoja na ujenzi wa barabara za mzunguko ndani ya Dodoma yenye urefuwa kilomita 39 pamoja na kituo cha afya katika mji wa Serikali kitakachogharimu bilioni 4.5. 

  Awali Rais Magufuli alizindua jengo la ofisi zake, pamoja na nyumba 41 za wafanyakazi wa Ikulu vilivyopo Chamwino jijini Dodoma. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mji wa Serikali ulijengwa katika eneo la Mtumba jijini Dodoma leo.

  0 0  Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro akikabidhi kikombe kwa Mshindi wa kuvuta kamba kitengo cha Mita Tanesco katika bonanza la michezo liloandaliwa na shirika hilo na kufanyika katika viwanja vya General Tyre ,kulia ni Nahodha wa timu hiyo Innocent Pascal.
  Nahodha wa Timu ya Mpira wa pete ya RAS ,Grace Kija akipokea zawadi wa kombe kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro.
  Nahodha wa Timu ya mpira ya Ras akipokea zawadi ya kikombe ,baada ya kuifunga timu ya Tanesco goli 2 kwa 1.
  Wachezaji wa timu ya mpira wa miguu ya RAS wakiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa mpira wa pete baada ya kukabidhiwa zawadiWachezaji wakisakata kabumbu kati ya Timu ya TANESCO na timu ya RAS
  Mashindano ya kuvuta kamba kati ya Timu ya Tanesco na RAS ambapo TANESCO iliibuka na ushindi katika viwanja vya General tyre Njiro Jijini Arusha
  Michezo ikiendelea hapa timu zote wakivuta kamba katika viwanja vya General tyre Njiro Jijini Arusha


  Na Vero Ignatus, Arusha.


  Shirika la Umeme Tanesco mkoani Arusha limefanya bonanza kubwa la michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu,mpira wa pete,kuvuta kamba na kukimbiza kuku huku wadau wengi wakijitokeza kwenye viwanja vya General tyre kushughudia michezo hiyo.

  Akifungua Bonanza hilo Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro amesema kuwa michezo ni afya ,ajira na furaha katika jamii hivyo bonanza hilo la Tanesco linalenga kuhamasisha wananchi kuunga mkono timu ya Vijana ya Taifa ya Serengeti ambayo inashiriki katika michuano ya Afcon.

  Daqqaro amesisitiza kuwa michezo inasaidia kupunguza uwezekano wa kupata magonjwa yasiyoambukiza kama presha,kisukari na saratani ambayo husababishwa na aina ya maisha isiyozingatia mazoezi na lishe.

  Kaimu Meneja wa Tanesco mkoa wa Arusha Donasiano Shamba amesema kuwa bonanza hilo linahusisha michuano mikali kati ya timu ya Tanesco na RAS arusha ambao walichuana katika mpira wa miguu na mpira wa pete.

  Shamba amesema kuwa michezo hilo inalenga na kujenga na kudumisha ushirikiano kati ya wadau mbalimbali ili kuleta maendeleo na pia kuunga mkono juhudi za Timu zinazoiwakilisha Tanzania katika michuano ya kimataifa ikiwemo Serengeti.

  Mmoja kati ya washiriki wa Bonanza hilo Innocent Pascal ameshauri waandaaji kuandaa michezo hiyo mara kwa mara ili kuibua vipaji vya michezo ambavyo vinaweza kuleta medani za heshima za kitaifa na kimataifa.

  0 0

  Akizungumza na wafanyabiashara wa Soko la Mahakama ya ndizi Wilaya ya Ubungo Mkoa wa Dar es salaam ikiwa ni sehemu ya kukagua na kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015 – 2020 Ndg. Humphrey Polepole Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi amesema CCM inatoa muda wa mwezi mmoja kwa Halmashauri ya Wilaya ya Ubungo kushughulika na changamoto za wafanyabiashara wa soko la Mahakama ya ndizi.

  Ndg. Polepole ameyasema haya baada ya kupokea Malalamiko kutoka kwa wafanyabiashara wa soko hilo ya kukosekana kwa miundombinu rafiki katika soko, uchakavu wa vibanda vya kufanyia biashara, vyoo vichache, dhulma kutoka kwa baadhi ya madalali na vitisho kutoka kwa wamiliki wa kiwanda cha urafiki.

  Ndg. Mkurugenzi tengenezeni mpango kazi hapa ni aibu soko la mahakama ya ndizi kuwa hivi, mnaweza kuwa na mabanda mazuri hapa, miundombinu mizuri hapa na wafanyabiashara wapo tayari kuchangia serikali vizuri bila matatizo yoyote” Ndg. Polepole

  Aidha Ndg. Polepole amewahakikishia wafanyabiashara katika soko la Mahakama ya ndizi kuwa changamoto zingine za vifungashio, tuhuma za rushwa kwenye mizani ya uloye, tanangozi na kibaha na mabadiliko katika matumizi ya ardhi katika soko hilo Chama kimepokea, kitazingatia na kuleta majibu ndani ya mwezi mmoja.

  Huu ni muendelezo wa ziara za kukagua na kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015 – 2020.

  0 0

  Shirika la Agape ACP limetoa elimu ya kutambua haki za binadamu ili kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na wasichana wafanyabiashara katika soko la Ngokolo Mitumbani Manispaa ya Shinyanga. 

  Elimu hiyo imetolewa leo Jumamosi Aprili 13,2019 wakati Mnada wa Jumamosi katika Soko la Ngokolo Mitumbani ukiendelea hivyo kufanikiwa kuwafikia watu mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara na wananchi waliofika mnadani hapo kujipatia mahitaji yao. 

  Agape ACP wanatoa elimu ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake na wasichana wafanyabiashara sokoni ikiwa ni utekelezaji wa mradi wa “Mpe Riziki Si Matusi” unaofadhiliwa na shirika la UN WOMEN kupitia Shirika la kitaifa la Equality for Growth (EfG). 

  Akitoa elimu, Meneja Miradi wa shirika la Agape, Mustapha Isabuda aliwataka wanawake na wasichana wanaofanyiwa vitendo vya kikatili kwenye masoko na katika jamii kwa ujumla kuacha tabia ya kuwa wakimya na badala yake watoe taarifa kwa viongozi mbalimbali ikiwemo Dawati la Jinsia katika kituo cha polisi. 

  “Acheni kukaa kimya mnapofanyiwa ukatili,msikubali kukaa na makovu ya ukatili kwenye masoko,pazeni sauti zetu,nanyi wanaume acheni kunyanyasa wanawake,msiwatukane na msiwadhulumu mama lishe,wapeni riziki si matusi”,alieleza Isabuda. 

  Isabuda alitumia fursa hiyo kuikumbusha jamii kuthamini wanawake na wasichana wafanyabiashara sokoni huku akiwatahadhalisha wanaume kuwa waaminifu katika ndoa zao na kuacha tabia ya kutongoza na kufanya mapenzi na wanafunzi kwani matokeo yake ni kufungwa jela miaka 30. 

  Naye Afisa Mradi wa 'Mpe Riziki Si Matusi' kutoka Agape,Helena Daudi alisema Agape imeendelea kutoa elimu katika masoko mbalimbali katika Manispaa ya Shinyanga ikiwemo Soko Kuu,Kambarage,Nguzo Nane Ngokolo Mitumbani na Majengo Mapya ili jamii iachane na tabia ya kuwafanyia ukatili wanawake na wasichana wafanyabiashara 

  Alisema tayari wamewajengea uwezo wasimamizi wa sheria ili wakaosaidia kutokomeza ukatili wa kijinsia unaotokea kwenye masoko. 

  Naye Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Soko la Ngokolo Mitumbani,Tracy Leonard alisema wafanyabiashara wanaofanyiwa zaidi ukatili sokoni akina mama hususani mama lishe ambao wanatolewa lugha chafu,wanadhulumiwa na kufanyiwa mashambulio ya aibu ikiwemo kushikwa shikwa bila idhini yao. 

  Alizitaja hatua ambazo wamekuwa wakizichukua pindi panapotokea ukatili sokoni kuwa ni kusuluhisha,kuwapiga faini ya shilingi 5000 wanaotukana na kama ni mfanyabiashara basi akirudia kutukana basi hufungiwa biashara yake kwa muda wa wiki mbili.
  Meneja Miradi wa shirika la Agape, Mustapha Isabuda akitoa elimu ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na wasichana wafanyabiashara katika soko la Ngokolo Mitumbani leo - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
  Meneja Miradi wa shirika la Agape, Mustapha Isabuda akielezea madhara ya kuwafanyia ukatili wanawake na wasichana wafanyabiashara sokoni.
  Wananchi wakimsikiliza Isabuda.
  Meneja Miradi wa shirika la Agape, Mustapha Isabuda akiwasisitiza wanaume na wanawake kuacha kuwafanyia ukatili wanawake na wasichana wafanyabiashara sokoni.
  Wananchi wakimsikiliza Isabuda.
  Afisa Mradi wa Mpe Riziki Si Matusi kutoka Agape,Helena Daudi akiwahamasisha wananchi kuwapenda wanawake na wasichana wafanyabiashara sokoni badala ya kuwanyanyasa na kuwanyima haki zao.
  Afisa Mradi wa Mpe Riziki Si Matusi kutoka Agape,Helena Daudi akiwataka wanawake kutoa taarifa pale wanapofanyiwa ukatili.
  Wananchi wakisoma vipeperushi mbalimbali vya kupinga ukatili dhidi ya wanawake na wasichana wafanyabiashara sokoni.
  Wananchi wakiwa eneo la tukio.
  Kikundi cha burudani cha 'Shinyanga Arts Group' kinachoongoza na Msanii ChapChap kikitoa burudani.
  Burudani inaendelea.
  Wasaidizi wa Kisheria kwenye masoko waliopewa mafunzo na Agape ACP wakitoa eimu ya kukabiliana na ukatili dhidi ya wanawake na wasichana wafanyabiashara kwenye masoko. Aliyeshikilia kipaza sauti kulia ni Shangwe Omary.
  Msaidizi wa Kisheria sokoni, Asha Jumanne akitoa elimu kwa jamii namna ya kutokomeza ukatili wa kijinsia kwenye masoko.
  Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Soko la Ngokolo Mitumbani,Tracy Leonard akielezea jinsi wanavyokabiliana na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na wasichana wafanyabiashara sokoni ambapo wamekuwa wakipiga faini ya shilingi 5000 wanaotukana na kufunga biashara za wafanyabiashara wanaofanya ukatili sokoni.
  Katibu wa Wafanyabiashara Soko la Ngokolo Mitumbani,Tracy Leonard akielezea namna wanavyowatetea akina mama wanaofanyiwa ukatili sokoni.
  Mfanyabiashara Soko la Ngokolo Mitumbani,Zuhura Athuman akielezea changamoto wanazokutana nazo sokoni ikiwemo kutolewa lugha chafu.


  Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

  0 0  Na Hussein Stambuli, Morogoro

  Mabehewa matano kati ya ishirini yaliyokuwa yakisafirisha shehena ya ngano kupitia reli ya kati kutoka jijini dar-es-salaam kuelekea jijini mwanza yameanguka eneo la kola manispaa ya morogoro na kusababisha uharibifu wa miundombinu ya reli eneo hilo huku baadhi ya abiria waliokuwa wakisafiri kutumia njia hiyo kukwama kwa muda. 

  Akizungumzia tukio hilo mkuu wa stesheni ya morogoro salvatory kimaro amesema ajali hiyo iliyotokea majira ya saa mbili usiku na hadi sasa chanzo chake hakijfahamika na tayari wataalamu wanaendelea na kazi za kurejesha mawasiliano ya njia hiyo..

  “taratibu nyingine ikiwemo mafundi wameshafika eneo la tukio kuweza kufanya tathmini za ujenzi na tunasafisha njia kwa kwa kutengeneza tuta ili zitakapo fika reli tuta liwelimeshaimarika na kumalizika kwa kazi hiyo kutatarajia mwenendo wa kazi za mafundi na tunatarajia kazi itafanyika haraka na kwa uhakika kupunguza usumbufu zaidi” amesema kimaro.

  Aidha kimaro amefafanua kuwa kuhusu treni za abiria zilizokuwa zikitokea dar es salaam kuelekea kigoma, mpanda na mwanza zilifika mapema morogoro jambo ambalo limesaidia kubadilishwa kwa abiria waliotoka dar wakaingia iliyokuwa inatoka mwanza na wale wa mwanza wameeendelea kwenye treni iliyokuwa ikitokea dar es salaam kuelekea mwanza.

  wananchi wanoishi jirani na eneo hilo wameiomba serikali kutafuta njia mbadala ya kudhibiti ajali katika eneo hilo ambalo linaonekana kuwa na kona kali na mara kwa mara limekuwa likisababisha ajali.

  “leo hii imetokea ajali ya treni ya mizigo ni vyema eneo hili likatazamwa vyema kabla haijatokea ajali ya treni yenye watu itakuwa hatari Zaidi” amesema Jackson isack mwananchi 

  Mmabehewa matano kati ya ishirini yaliyokuwa yakisafirisha  shehena ya ngano  kupitia reli ya kati  kutoka jijini dar-es-salaam  kuelekea  jijini  mwanza yakiwa yameanguka eneo la kola  manispaa ya morogoro ....
   Mabehewa matano kati ya ishirini yaliyokuwa yakisafirisha  shehena ya ngano  kupitia reli ya kati  kutoka jijini dar-es-salaam  kuelekea  jijini  mwanza yakiwa yameanguka eneo la kola  manispaa ya morogoro
  Reli ikiwa imeharibika vibaya mara baada ya mabehewa kuacha njia

  0 0


  Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Tunu Juma Kondo akikabidhiwa zawadi ya akina mama wa UWT Jimbo la Mwanakwerekwe.
  Kaimu Katibu wa UWT Wilaya ya Dimani Fatma Ramadhan akisoma risala ya UWT mbele ya Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Tunu Juma kondo katika ziara yake Wilayani humo.
  Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Tunu Juma Kondo akimkabidhi kadi ya uanachama wa UWT mwanachama mpya aliyejiuynga na umoja huo kutoka Chama cha ADA-TADEA ndugu Asha Juma Ali.
  -Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Tunu Juma Kondo akimkabidhi kadi ya uanachama wa UWT mwanachama mpya kutoka ADA-TADEA ndugu Dalila Hassan Sharif.
  Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Tunu Juma Kondo akizungumza na Wanawake wa UWT pamoja na viongozi mbali mbali wa CCM na jumuiya zake.
  ????????????????????????????????????
  VIJANA wa Kikundi Maalum cha UVCCM wakimvisha sikafu Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Tunu Juma Kondo mara baada ya kuwasili katika Ofisi ya UWT Wilaya ya Dimani Unguja,kwa ajili ya mwendelezo wa ziara yake ya kujitambulisha kwa Kamati ya Utekelezaji na Wanawake wa Wilaya hiyo.

  Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Tunu Juma Kondo akikagua Gwaride la Kikundi Maalum cha UVCCM mara baada ya kuwasili UWT Wilaya Dimani kwa ajili ya ziara yake Wilayani humo(PICHA NA IS-HAKA OMAR-AFISI KUU YA CCM ZANZIBAR).
  ………………….
   
  NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR. 

  WAZAZI na walezi nchini wametakiwa kufuatilia mienendo ya watoto wa kike ili wapate malezi bora yatakayowaepusha na changamoto za udhalilishwaji wa kijinsia. 

  Rai hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania(UWT) anayefanyia kazi zake Zanzibar Ndugu Tunu Juma Kondo katika mwendelezo wa ziara yake ya kujitambulisha kwa Kamati tekelezaji ya UWT Wilaya ya Dimani kichama. 

  Alisema wazazi,walezi na jamii kwa ujumla inatakiwa kuwa karibu na watoto wa kile ambao kwa sasa wanaishi katika mazingira hatarishi ya kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji vinavyopelekea kuwakosesha haki zao za msingi zikiwemo elimu,uongozi na haki ya kuishi huru. 

  Alisema wazazi wahakikishe watoto kila wanapotoka kwenda skuli na sehemu zingine za kijamii wakaguliwe mikoba yao kwani wengine wanaondoka na nguo za ziada na kwenda sehemu za starehe hali inayopelekea kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji. 

  Alieleza kuwa jukumu la malezi ya watoto ni jukumu la kila mtu hivyo pindi watoto wakionekana katika mazingira hatari wananchi wa mtaa husika wanatakiwa kuchukua hatua za kutoa taarifa kwa vyombo vya ulinzi ama kwa wazazi husika. Alibainisha kwamba kuna baadhi ya wanaume wasiokuwa na maadili mazuri wamekuwa ni chanzo cha kuwadanganya na kuwafanyia vitendo vya udhalilishaji watoto wa kike hasa wanaosoma shule za maandalizi na msingi,jambo ambalo ni kinyume na mila,desturi na utamaduni wa kizanzibar. 

  Naibu Katibu Mkuu huyo Tunu, aliweka wazi kuwa CCM kupitia UWT Zanzibar itaendelea kulaani vitendo vyote visivyofaa vinavyokatisha malengo ya maendeleo ya wanawake nchini na kuishauri serikali ichukue hatua stahiki kwa wahalifu wote wa matukio ya udhalilishaji. 

  Akizungumzia uimarishaji wa CCM Tunu, aliwataka Wanawake hao kulipa ada za uanachama kwa wakati ili kurahisisha mipango ya kiutendaji ya Chama na Jumuiya kwa ujumla. 

  ” Katubu Mkuu wetu juzi alininongoneza kuwa kuna mpango wa kuwapatia zawadi ya shilingi milioni moja (Sh.1,000,000),Katibu yeyote wa jumuiya ambaye Wilaya yake itaongoza kwa kulipa ada na kuongeza wanachama wapya kwa hiyo kazi kwenu”, aliwambia akina mama hao. 

  Akizungumzia maandalizi ya uchaguzi mkuu ujao,aliwasihi kuendelea kuongeza wanachama wapya na waliotimiza umri wa kupiga kura kisheria kwa lengo la kuongeza Jeshi la ushindi la CCM, litakalopambana vita ya kisiasaa na kukiletea ushindi Chama mwaka 2020. 

  Pamoja na hayo aliwataka akina mama hao kuitumia vizuri fursa ya ujasiriamali kwa kuanzisha na kuendeleza vikundi mbali mbali vya kuzalisha bidhaa za ujasiriamali ili kwenda sambamba na malengo ya serikali ya kupiga vita wimbi la umaskini na utegemezi. 

  “Wanawake tutaweza kufikia malengo yetu ya 50 kwa 50 endapo tutakuwa na uwezo mkubwa wa kumiliki mali na miradi mbali mbali ya kimaendeleo, wito wangu tuitumie vizuri fursa ya ujasiria mali itatukomboa kiuchumi”,alisisitiza.
  Katika maelezo yake Tunu, aliwasihi akina mama hao kuwakaribisha wanawake waliopo katika vyama vya upinzani ambao mpaka sasa wamekosa muelekeo wajiunge na CCM ili wanufaike na siasa na demokrasia iliyotukuka. 

  Aliwapongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza
  la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli kwa kasi yao ya usimamizi imara wa utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2015/2020. 

  Amewapongeza akina mama hao kwa mapokezi mazuri yaliyoambatana na zawadi mbali mbali ambazo ni sehemu ya kuimarisha ushirikiano na umoja ndani na nje ya Chama na jumuiya. 

  Akizungumza Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Magharibi, Zainab Ali Maulid alieleza kuwa akina mama ndani ya Mkoa huo wanaendelea kufanya kazi za kuimarisha CCM ili itimize malengo yake ya kuendelea kuongoza dola. 

  Naye Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Dimani ndugu Hussein Ali Mjema ‘Kimti’ alisema Chama kitaendelea kuwa karibu na jumuiya zote kwa lengo la kuongeza nguvu ya kuleta mabadiliko ya kweli ya kimaendeleo. 

  Katika risala yao iliyosomwa na Kaimu Katibu wa UWT Wilaya ya Dimani Fatma Ramadhan Mandoba, alisema wanawake katika wilaya hiyo wameendelea kujikusanya pamoja na kuanzisha vikundi vya ujasiriamali ili kujikwamua kiuchumi. 

  kupitia risala hiyo waliwashukuru baadhi ya Wabunge na Wawakilishi wa viti Maalum Wilaya hiyo waliotoa vitendea kazi mbali mbali vya kusaidia shughuli za kiutendaji za UWT.

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya Dkt. Godlove Mbwanji amesema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli imedhamiria kuiwezesha Sekta ya Afya nchini ili kuimarisha huduma ya afya kwa mama na mtoto.

  Dkt Godlove Mbwanji ametoa kauli hiyo mara baada ya utiaji saini Mkataba wa Ujenzi wa Jengo la wazazi kitengo cha META uliofanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya.

  Alisema Mradi huo wa upanuzi kwa kiasi kikubwa utasaidia kuongeza kwa upatikanaji wa huduma za kina mama wajawazito na watoto wachanga na kuwapunguzia akina mama shida ya kufuata huduma hiyo sehem nyingine.

  “Ukamilifu wa ujenzi huu itakuwa ni neema kwa akina mama wajawazito wanaohitaji huduma ya uzazi kwa Ukanda huu wa Nyanda za Juu Kusini.

  Tunategemea kukamilika kwa jengo hili tutakuwa na ongezeko la vitanda 200, wataalamu na huduma za kisasa, lengo ikiwa ni kumfanya huyu mama kuwa salama na kupunguza idadi ya vifo vya wajawazito na watoto wachanga". Alisema Dkt Mbwanji.

  Mradi huu unatarajia kukamilika ndani ya miezi 18 na utakagharimu chini ya shilingi Bilion 8.4 kwa kuwa unateklezwa kwa kutumia mfumo wa Force Account.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda, Mbeya Dkt. Godlove Mbwanji pamoja na Mhandisi Juma Mvumbo(Kutoka ZM SUMA JKT), katika utiaji saini Mkataba wa ujenzi wa Jengo jipya la gorofa tano Kitengo cha Meta katika Hospitali Rufaa ya kanda, Mbeya. Utiaji saini huo umeshuhudiwa na Viongozi mbalimbali wa Hospitali akiwemo Mhasibu Mkuu wa Hospitali Bi. Proce Gabone wa kwanza kutoka kushoto mbele na Mshauri elekezi Dkt. Duwa Chenguza (kutoka MCB MUST) wa tatu kutoka Kulia mbele.
  Mhandisi Bw. Juma Mvumbo kutoka SUMA JKT akimpatia maelezo Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya na viongozi mbalimbali wa Hospitali juu ya Ujenzi wa Jengo la jipya la Mama na mtoto katika Kitengo cha Meta Hospitali ya Rufaa ya Nyanda za Juu Kusini Mbeya baada ya utiaji saini Mkataba wa uanzaji wa ujenzi huo.
  Muonekano wa Jengo litakavyokuwa baada ya kumalizika kwa mradi, Matarajio ni ongezeko la utoaji huduma za kulaza vitanda 200, vyumba 2 vya upasuaji mkubwa na chumba maalum cha huduma za watoto wadogo ndani ya mwezi mmoja (Neonatal Intensive Care Unit) katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya linalotarajiwa kugharimu chini ya shilingi bilioni 8.4 litakapokamilika kwa kutumia mfumo wa Force account.
  Mkurugenzi Mtendaji Dkt Godlove Mbwanji, Akimkabidhi mkataba wa ujenzi wa mradi wa Jengo la wazazi Kitengo cha META kwa Mhandisi Juma Mvumbo kutoka SUMA JKT. Ujenzi wa Mradi unategemea kuanza hivi karibuni.

  0 0


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifunua kitambaa na Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan,Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa pamoja na Viongozi wengine kuashiria Ufunguzi rasmi wa majengo mapya ya Ikulu Chamwino Jijini Dodoma.Aprili 13,2019.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipongezana na Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan mara baada ya kufungua rasmi wa majengo mapya ya Ikulu Chamwino Jijini Dodoma. Aprili 13,2019.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipongezana na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa mara baada ya kufungua rasmi wa majengo mapya ya Ikulu Chamwino Jijini Dodoma. Aprili 13,2019.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe na Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan,Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli,Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa Dkt.Modestus Kipilimba kuashiria Ufunguzi rasmi wa majengo mapya ya Ikulu Chamwino Jijini Dodoma.Aprili 13,2019.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua majengo mapya ya Ikulu Chamwino akiwa ameambatana na Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan,Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli,Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa Dkt.Modestus Kipilimba pamoja na Katibu Mkuu Ikulu Dkt. Moses Kusiluka mara baada ya kufungua majengo hayo .Ikulu Chamwino Jijini Dodoma.Aprili 13,2019.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Katibu Mkuu Ikulu Dkt. Moses Kusiluka akielezea kuhusu mradi wa ujenzi wa majengo mapya ya Ikulu Chamwino huku akiwa ameambatana na Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan,Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli,Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi na Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa Dkt.Modestus Kipilimba, mara baada ya kufungua majengo hayo .Ikulu Chamwino Jijini Dodoma.Aprili 13,2019.
  Sehemu ya majengo mapya ya Ikulu Chamwino Jijini Dodoma. Ambayo yamefunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. Aprili 13,2019.

  PICHA NA IKULU

  0 0


  Naibu Waziri wa Ujenzi Mhe. Elias John Kwandikwa akitembezwa na wahandisi na viongozi wa TBA kukagua maendeleo ya mradi wa Ujenzi wa Nyumba za kisasa wa Magomeni Kota jijini Dar es Salaam alipofanya ziara yake leo.
  Naibu Waziri wa Ujenzi Mhe. Elias John Kwandikwa (kulia) akipata maelezo kwenye chumba cha kuendeshea mtambo wa kuchakata zege katika mradi wa Ujenzi wa Nyumba za kisasa wa Magomeni Kota jijini Dar es Salaam alipofanya ziara yake leo.
  Kaimu Mtendaji Mkuu wa TBA, Eng. Jasper Lugemarila (katikati) akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri wa Ujenzi Mhe. Elias John Kwandikwa (kushoto) alipofanya ziara leo kukagua maendeleo ya mradi wa Ujenzi wa Nyumba za kisasa wa Magomeni Kota.
  Kaimu Mtendaji Mkuu wa TBA, Eng. Jasper Lugemarila (kushoto) akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri wa Ujenzi Mhe. Elias John Kwandikwa (wa pili kulia) alipofanya ziara leo kukagua maendeleo ya mradi wa Ujenzi wa Nyumba za kisasa wa Magomeni Kota. Wengine ni wahandisi wa mradi huo.
  Naibu Waziri wa Ujenzi Mhe. Elias John Kwandikwa (kushoto) akitoka katika moja ya majengo ya mradi wa Ujenzi wa Nyumba za kisasa wa Magomeni Kota jijini Dar es Salaam alipofanya ziara yake leo.

  ……………………

  NAIBU Waziri wa Ujenzi Mhe. Elias John Kwandikwa ameagiza Wakala wa Majengo Nchini (TBA) kuhakikisha wanamaliza Mradi wa Nyumba za Kisasa wa Magomeni Kota jijini Dar es Salaam unamalizika kufikia mwezi Desemba mwaka huu.

  Naibu Waziri wa Ujenzi Mhe. Kwandikwa ametoa msisitizo huo leo jijini Dar es Salaam alipofanya ziara kukagua maendeleo ya mradi huo.

  Amesema kuanzia sasa atakuwa akiutembelea mradi huo kila mwezi ili kuhakikisha mambo yanakwenda sawa na hatimaye mradi ukamilike Desemba kama ilivyoagizwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli alipoutembelea mradi huo hivi karibuni.

  “…Kuanzia leo nitahakikisha nawatembelea hapa kama sio kila wiki basi kila mwezi, lengo langu ni kuhakikisha mradi huu mkubwa unakamilika kwa wakati na wananchi hawa wapatao 656 waliokuwa wakiishi hapa wanaingia na kuanza kuzitumia nyumba hizi,” alisema Naibu Waziri.

  Aidha aliongeza kuwa wizara yake itahakikisha inafika eneo hilo kila mara kutatua changamoto zote ambazo zitakuwa zikihitaji kutatuliwa na wizara hiyo, huku akionya itakuwa ni jambo la kushangaza endapo mradi huo utasimama tena na kumlazimu Rais Dk. Magufuli arudi tena eneo hilo.

  “…Sisi kama wizara tunataka endapo Mh. Rais Dk. John Pombe Magufuli akija tena eneo la Magomeni Kota ni kufanya uzinduzi wa nyumba zikiwa zimekamilika na si vinginevyo,” alisisitiza Naibu Waziri Kwandikwa akizungumza na viongozi na waandisi wa TBA wanaosimamia mradi huo.

  Aliipongeza TBA kwa kitendo cha kuanza kutumia mitambo ya kisasa ya kufyatua matofali, kuchanganya na kubeba zege hadi gorofani jambo ambalo litaongeza kasi ya ujenzi na ufanisi katika mradi huo.

  Aliwataka kuangalia namna ya kuanza haraka kufanya kazi usiku na mchana kutokana na ujio wa mitambo hiyo. Alisema wazo la kuanza kufanya kazi usiku na mchana licha ya kuongeza kasi ya ujenzi wa mradi linatoa fursa kwa vijana wengi sasa kuja kufanya kazi na kujipatia kipato.

  Kwa upande wake, Kaimu Mtendaji Mkuu wa TBA, Eng. Jasper Lugemarila akizungumzia changamoto zilizokwamisha mradi huo awali, alisema ilikuwa ni kupanda kwa bei ya zege ambayo walikuwa wakinunua pamoja na bidhaa nyingine kama simenti, kokoto na nondo.

  Alisema kwa sasa wamekwisha tatua changamoto hizo baadha ya kuanza kutengeneza zege wenyewe kwa kutumia mitambo ya kisasa inayoendeshwa na kompyuta.

  “…Mwanzoni tulikuwa tunamimina zege kwa kununua kutoka kwa wafanyabiashara hiyo, lakini walipoona mradi huu umeanza na ni mkubwa wakatupandishia bei sana wakijua lazima twende kwao,” alisema Eng. Jasper Lugemarila

  0 0  Na Tulizo Kilaga, TFS

  Mlele. Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Costantine Kanyasu amewataka askari wa misitu waliohitimu mafunzo ya kijeshi kuhakikisha wanarejesha katika uoto wake wa asili maeneo yote ya misitu ambayo yameharibiwa.

  Mhe. Kanyasu, aliyasema hayo jana alipokuwa akifunga mafunzo ya kijeshi kwa askari 140 wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) katika kambi ya mafunzo ya kijeshi Mlele mkoani Katavi.

  “Leo mmehitimu na tumewaapisha, mmekuwa askari kweli wa TFS lakini tambueni kuwa kazi za kiuchumi zinapelekea uharibifu mkubwa sana wa mazingira, na hatuwezi kusema zisiendelee, zinatakiwa kuendelea katika namna ambayo haitaifanya nchi yetu kuwa jangwa.

  “Kuhitimu kwenu hakumaanisha mnakwenda kuzuia maendeleo, kunamaanisha mnakwenda kushirikiana na wanaotaka maendeleo kwa kufanya kazi wakifikiria maendeleo endelevu,” alisema.

  Mhe. Kanyasu alisema hivi sasa nchi inakabiliwa na mabadiliko makubwa ya tabia nchi yanayosababishwa na uharibifu wa mazingira ikiwemo ukataji wa miti, ukame, mvua nyingi na mafuriko ambapo vyote hivyo husababishwa na matumizi mabaya ya kazi za kiuchumi.

  Alisema ni matarajio ya Serikali kuwa baada ya askari hao kuhitimu pamoja na kazi yao ya msingi ya ulizi watafanya kazi ya kuhakikisha wanarejesha uoto wa asili uliopotea.

  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo katika hotuba yake alisema Taifa limekuwa likikumbwa na changamoto mbalimbali za kiuhifadhi ikiwemo shughuli za kibinadamu pamoja na mmomonyoko wa maadili kwa watumishi na mambo hayo yote yanasababisha mafunzo hayo kuwa muhimu katika uhifadhi wa mapori na misitu ya hifadhi nchini.

  Prof. Silayo alisema pamoja na mafunzo hayo yanayofanyika, TFS inaimarisha vikosi vyake vya kufuatilia taarifa ambapo ina kitengo cha intelijensia ambacho wanakiimarisha ili kiweze kutoa taarifa sahihi kwa askari wa misitu na kuchukua hatua bila kupoteza wakati.

  Zoezi hilo limehudhuriwa na viongozi wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii, Wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Wizara kwa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Maliasili, Ardhi na Mazingira pamoja na wananchi.

  Wizara ya Maliasili na Utalii imebadili mfumo wake wa usimamizi wa maliasili toka ule wa kiraia kwenda mfumo wa kijeshi (Paramilitary). TFS imekuwa mstari wa mbele kwenda na mabadiliko hayo kwa kuanza kutekeleza mafunzo ya watumishi katika ngazi mbalimbali wakati ikisubiri mabadiliko ya muundo wa utumishi utakaotambua mabadiliko ya vyeo na majukumu ya kila siku.
   Askari wa misitu wakionesha umahiri wao kwenye kutembea mwendo wa haraka na taratibu huku wakiwa na silaha wakati wakionesha kwa vitendo mafunzo ya kijeshi waliyopata katika kambi ya jeshi ya Mlele mkoani Katavi ikiwa ni sehemu ya kubadili utendaji kazi wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii kuendeshwa katika mfumo wa jeshi usu.
   Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Costantine Kanyasu na viongozi wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii, wajumbe wawili wa bodi, Wajumbe 19 wa Kamati ya Bunge ya Maliasili, Ardhi na Mazingira wakiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wa mafunzo ya kijeshi yaliyofanyika katika kambi ya Mlele mkoani Katavi.

   Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Costantine Kanyasu akikagua gwaride wakati wa kufunga mafunzo ya kijeshi kwa askari wa misitu 140 wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) yaliyofanyika katika kambi ya mafunzo ya Mlele mkoani Katavi.
    Askari wa misitu wakionesha umahiri katika matumizi ya silaha wakati wakionesha kwa vitendo mafunzo ya kijeshi waliyopata katika kambi ya jeshi ya Mlele mkoani Katavi ikiwa ni sehemu ya kubadili utendaji kazi wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii kuendeshwa katika mfumo wa jeshi usu.
   Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Costantine Kanyasu akitunuku vyeti kwa askari wa misitu waliohitimu mafunzo ya kijeshi katika kambi ya Mlele mkoani Katavi.
   Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo (anayepiga makofi), viongozi wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii, wajumbe wa bodi na Wajumbe  wa Kamati ya Bunge ya Maliasili, Ardhi na Mazingira wakifurahia jambo baada ya askari wake kuonhyesha umahiri katika matumizi ya silaha wakati wakiomnyesha kwa vitendo jinsi wanavyoweza kupambana na adui kwa kutumia mbinu za kijeshi kama walivyofunzwa katika mafunzo ya kijeshi katika kambi ya Mlele mkoani Katavi.
   

  0 0

  Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (kushoto) akizungumza na Balozi wa China nchini Wang KE mapema leo Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.
  Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (kushoto) akimsikiliza Balozi wa China nchini Wang KE mapema leo Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.
  Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (kushoto) akizungumza na Balozi wa China nchini Wang KE mapema leo Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.
  Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (kulia) akiagana na Balozi wa China nchini Wang KE mara baada ya kuzungumza naye mapema leo Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.PICHA NA BUNGE

  0 0

  *Amwambia aache kuliita Bunge dhaifu na kama.analipenda basi ajiite yeye

  *Amshauri ajipime,ajitafakari na ikiwezekana aende kwa Rais kujieleza...kisha ajiuzulu
  *Asisitiza Bunge halitafanya kazi naye ila ripoti ya CAG sawa...amshangaa kuwaona wengine Mbuzi


  Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

  SPIKA wa Bunge Job Ndugai amesema hawana tatizo na ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) na kwamba wataifanyia kazi lakini msimamo wao Bunge halitakuwa tayari kufanya kazi na Profesa Mussa Assad.

  Ameongeza kuwa amemsikia Profesa Assad akisema ataendelea kutumia kauli ya Bunge dhaifu,hivyo amemtaka afahamu kuwa hawataki kusikia Bunge linaitwa dhaifu na kama analipenda basi ajiite yeye dhaifu na sio Bunge.

  Spika Ndugai amesema hayo leo Aprili 14,2019 wakati anazungumza na waandishi jijini Dar es Salaam ambapo pamoja ametumia nafasi hiyo kuelezea hawana tatizo na ripoti ya CAG lakini tatizo ni mtu ambaye ni Profesa Assad ,hivyo amemtaka ajitafakari,ajipime na ikiwezekana aende kwa Rais.

  "Anapokwenda kwa Rais wala asione tabu kumwambia anajiuzulu.kama Bunge hatutafanya kazi na Profesa Assad atafanya kazi na nani?Aniambie au niambieni waandishi wa habari kama yupo anayeweza kufanya naye kazi,"amsema Spika Ndugai.

  Ambapo amefafanua katika nchi nyingine Bunge likiadhimia kuhusu mtu hakuna njia nyingine zaidi ya kujiuzulu na kuchelewa kwake kujiuzulu anampa kazi Rais.

  Spika Ndugai amesema kwamba Rais ni sehemu ya Bunge kwani yeye ndio kila kitu na hata bajeti zinazojadiliwa vipi na zikakosa saini ya Rais bado haijawa bajeti.

  Amesisitiza Profesa Assad ameahidi kuendelea kutumia kauli ya kwamba Bunge dhaifu lakini amemtaka afahamu akiendelea watamuita na kumhoji tena na hiyo itakuwa mbaya zaidi kwake.

  " Ujue kama mtu anakwambia usimuite hilo jina halafu wewe unang'ang'ania kumuita,kama analipenda asijiite yeye mwenyewe.Sisi hatutaki kuitwa dhaifu,halafu sijui alifikiria ,mule ndani kuna viongozi wa ngazi mbalimbali hadi Waziri Mkuu na mawaziri.Kuisema Bunge dhaifu maana yake anataka kuiambia Serikali ni dhaifu.Yaani hapa ni sawa na kumtukana mtu anayekupa chakula,"amesema Spika Ndugai.

  Hata hivyo amesema yeye amesoma Norway na juzi hapa alikuwa Sweden ambapo mmoja ya marafiki zake alimwambia tatizo la Watanzania akisoma anajiona yeye ni ndio yeye na kuona wengine si chochote ,kumbe sio sawa.

  Amesema kuwa Profesa sio kigezo cha kuona wengine ambao si maprofesa ni sawa na mbuzi,hivyo anatakiwa kutambua wabunge walioko Bungeni ni wawakilishi wa wananchi,wanao uwezo wa kuchuja,kuchambua na kujadili mambo kwa maslahi mapana ya nchi.

  " Profesa Assad amefanya kosa na hapaswi kutukana Bunge kwa lugha za reja reja kwani Bunge linafanya mambo yake kwa mujibu wa kanuni za kibunge na si vinginevyo.Neno dhaifu linatumiwa na mhasibu anapofanya ukaguzi wake na baada ya hapo anakabidhi ripoti ambayo mwisho itakwenda kwadau.Na Bunge sasa ndio wanajadili kupitia kamati za Bunge kisha inaandaliwa taarifa na baada ya hapo ndipo yanapotolewa maagizo ya kuishauri Serikali.

  "Ieleweke Bunge ndio chombo pekee ambacho kinaweza maagizo au mapendekezo ya kuishauri Serikali kuhusu ripoti ya CAG.Ndugu zangu waandishi katika hili neno analilotamka rafiki Assad hata alipoitwa kwenye kamati alishindwa kuthibitisha kwani Bunge lilitoa kamusi zote hadi za Kenya na neno dhaifu halina maana hiyo ambayo yeye amekuwa akitoa kwa Bunge.

  Pamoja na hayo.ametumia nafasi hiyo kuwahakikishia Watanzania kwamba Bunge lao liko imara na litaendelea kufanya kazi,huku akifafanua ripoti ya CAG ambayo tayari iko mezani kwao itafanyiwa kazi chini ya kamati na baadae kujadiliwa.

  Alipoulizwa kuhusu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto kutumia fedha nyingi na sehemu kubwa zikionesha kutumiwa katika matibabu ya Spika ,amejibu kuwa kupanga matibabu sio jukumu lake ila tatizo litakuja iwapo fedha zimetumika vibaya.

  Hata hivyo amesema yeye kama Mtanzania haoni tatizo Serikali kumtibu kwa lengo la kuokoa maisha yake kwani inafanya hivyo kwa watanzania wengi ambao ni malofa kama yeye(Ndugai)."Kosa langu ni kutibiwa au ilitakiwa ndio waseme.

  "Kwanza kinachoonekana ni kitafuta sababu tu,hayo matumizi ya fedha kwa ajili ya Spika ziko ukurasa wa ngapi? niambieni?Tena mimi nilianza kuumwa mwaka 2015-2016 baada tu ya kuwaapisha wabunge.Hii ripoti ambayo imewasilishwa ni ya mwaka 2017-2018.Haya niambieni na bora nimeeleza maana wanataka kuaminisha watu uongo,"amesema.
  Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisi Ndogo ya Bunge Jijini Dar es Salaam kuhusu ripoti ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2017/18 .

  0 0


  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu amezindua taarifa ya utafiti wa viashiria na matokeo ya ukimwi wa mwaka 2016 – 2017 (Tanzania HIV Impact Survey) tarehe 13 Aprili, 2019 Jijini Dodoma.

  Akizungumza wakati wa hafla hiyo alieleza kuwa utafiti huo ni kielelezo tosha kuwa Serikali imeendelea kupambana na ugonjwa wa Ukimwi kwa kuonesha juhudi za kupungua kwa kiwango cha maambukizi mapya na kupungua kwa vifo vinavyotokana na Ukimwi. 

  “Tafiti zinaonesha maambukizi mapya ya VVU yamepungua kutoka watu 80,000 mwaka 2012 hadi kufikia watu 72,000 kwa mwaka katika mwaka 2017, vilevile takimu zinaonesha kupungua kwa vifo vinavyotokana na Ukimwi kutoka watu elfu 70 kwa mwaka katika 2010 hadi kufikia vifo elfu 32 kwa mwaka katika kipindi cha mwaka 2017,” alieleza Mhagama

  Alisema kuwa katika kuthibitisha hilo, kiwango cha maambukizi ya Ukimwi nchini kinazidi kupungua ambapo mwaka 2012 matokeo ya utafiti kama huo yalionesha kuwa kiwango cha maambukizi kilikuwa ni asilimia 5.1 kwa watu wenye umri kati ya miaka 15 hadi 49 na matokeo ya mwaka 2016 – 2017 kiwango cha maambukizi kwa watu wenye umri wa miaka 15 hadi 49 ni asilimia 4.7.

  Waziri Mhagama alieleza kuwa matokeo ya utafiti huo yanaonesha kuwa watu waliopima afya zao kwa hiari wanaongezeka kutoka tafiti moja hadi nyingine, kati ya watu hao wanawake waliopima ni wengi kuliko wanaume.

  Sambamba na hilo, amewapongeza wanawake kwa ujasiri na moyo wa kujali afya zao, pia kuwahimiza wanaume kujitokeza kwa wingi kupima ili wafahamu hali zao za kiafya.

  Hata hivyo, Waziri Mhagama ametaka kila Mkoa na Halmashauri zote nchini kujadili matokeo ya utafiti huo kwa undani katika kamati za VVU na Ukimwi kuanzia ngazi ya Mkoa, Wilaya, Kata na Vijiji ili kuelewa hali ilivyo katika maeneo yao na kuandaa mipango madhubuti ya kudhibiti ongezeko la maambukizi mapya ikiwemo kuongeza upatikanaji wa huduma stahiki kwa watu wanaoishi na VVU (WAVIU).

  Aidha, alitoa wito kwa watanzania kujitokeza kwa wingi na kupima afya zao, pia jamii kuelimishwa na kuhamasishwa juu ya umuhimu wa kutumia dawa za kufubaza Virusi vya Ukimwi kwa watu wanaoishi na VVU (WAVIU).

  Aliongeza kwa kuagiza TACAIDS na Baraza la Watu wanaoishi na Ukimwi (NACOPHA) kuongeza jitihada dhidi ya unyanyapaa na ubaguzi.

  Kwa Upande wake Naibu Waziri wa Afya, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Harusi Said Suleiman alisema kuwa taarifa ya utafiti huo itasaidia watunga sera na waratibu wa miradi kufuatilia na kufanya tathmini ya miradi iliyopo kuandaa mikakati mipya kuhusiana na masuala ya Ukimwi hapa nchini.

  Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania Bara (TACAIDS), Dkt. Leonard Maboko alisema kuwa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania imekuwa ikiratibu zoezi hilo la utafiti kila baada ya miaka mine na tafiti tatu zimeshafanyika mwaka 2003 – 2004, 2007 – 2008 na 2011 – 2012.

  Pia, Kaimu Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dkt. Albina Chuwa alisema kuwa malengo ya msingi ya utafiti utafiti huo yalikuwa ni kutoa makadirio ya mwaka ya Kitaifa ya maambukizi mapya ya VVU miongoni mwa watu wenye umri wa miaka 15 hadi 64, na kutoa makadirio ya hali halisi ya upimaji wa VVU Kitaifa na Kimkoa.

  “Utafiti wa aina hii ni wa kwanza kufanyika hapa nchini kwa kuwa umeangalia vitu vingi na umeshirikisha watu wa rika lote na viashiria vingine tofauti na tafiti nyingine zilizofanyika hapo awali,” alisema Chuwa.

  Utafiti wa Viashiria vya Ukimwi na Matokeo yake wa Mwaka 2016 – 2017, ulitekelezwa kwa kushirikiana baina ya Ofisi ya Takwimu (NBS), Ofisi ya Mtakwimu Mkuu Zanzibar na ICAP Tanzania, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Wizara ya Afya – Zanzibar na Tume ya Kudhibiti Ukimwi Zanzibar (ZAC), Maabara ya Taifa ya Afya za Jamii, Uhakiki, Ubora na Mafunzo, Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi (NACP), na Kitengo Shirikishicha Ukimwi, Kifua Kikuu na Ukoma, Zanzibar (ZIHTLP) kwa kushirikiana na wadau kutoka shirika lisilo la Kiserikali Centers for Disease Control and Prevention (CDC).
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akizindua Taarifa ya Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya Ukimwi wa Mwaka 2016 – 2017 (Tanzania HIV Impact Survey). (Kushoto) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania Bara (TACAIDS), Dkt. Leonard Maboko, Naibu Waziri wa Afya, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Harusi Said Suleiman. (Kulia) ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi na Dawa za Kulevya, Mhe. Osca Mukaza

   Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza wakati wa hafla ya kuzindua Taarifa ya Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya Ukimwi wa Mwaka 2016 – 2017 (Tanzania HIV Impact Survey) iliyofanyika Jengo la Takwimu tarehe 13 Aprili, 2019 Jijini Dodoma.
   Naibu Waziri wa Afya, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Harusi Said Suleiman akieleza namna Serikali ya Tanzania Bara na Zanzibar zimekuwa zikishirikiana katika kukabiliana na Ugonjwa wa Ukimwi nchini.

   Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania Bara (TACAIDS), Dkt. Leonard Maboko akitoa maelezo mafupi kuhusu utafiti huo uliofanyika juu ya Viashiria na Matokeo ya Ukimwi wa Mwaka 2016 – 2017.

   Baadhi ya washiriki wakisikiliza hotuba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa Taarifa ya Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya Ukimwi wa Mwaka 2016 – 2017 (Tanzania HIV Impact Survey) iliyofanyika Jengo la Takwimu tarehe 13 Aprili, 2019 Jijini Dodoma.

   Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akiwa pamoja na viongozi wengine wakifuatilia ripoti fupi iliyokuwa ikiwasilishwa na mwakilishi kutoka Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) hayupo pichani. (Wa pili kutoka kushoto) ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri anayeshughulika masuala ya Watu wenye Ulemavu Mhe. Stalla Ikupa.

   Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akionesha kitabu cha Taarifa ya Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya Ukimwi wa Mwaka 2016 – 2017 (Tanzania HIV Impact Survey) baada ya kuzindua taarifa hiyo, Jijini Dodoma

   Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akimkabidhi kitabu cha Taarifa ya Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya Ukimwi wa Mwaka 2016 – 2017 (Tanzania HIV Impact Survey) Bi. Dorothy Mwaluko mara baada ya Kuzindua taarifa hiyo, Aprili 13, 2019 Jijini Dodoma.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi na wadau wa maendeleo mara baada ya kuzindua Taarifa ya Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya Ukimwi wa Mwaka 2016 – 2017 (Tanzania HIV Impact Survey) Jijini Dodoma.PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)


  0 0

  Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imeanza kuendesha programu za elimu kwa wanafunzi wa shule za sekondari waliopo mikoani ili kuwaelimisha kuhusu sifa na taratibu za kuomba mikopo kwa usahihi.

  Akizungumza wilayani Maswa, mkoani Simiyu jana (Jumamosi, Aprili 13, 2019) na wanafunzi 1,166 wa kidato cha sita kutoka shule zote 12 za mkoa huo, Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Abdul-Razaq Badru amesema uendeshaji wa programu hizo unalenga kuondokana na changamoto wanazopata wanafunzi wakati wa kuomba mikopo ya elimu ya juu.

  HESLB ilianza kuendesha programu hizo katika mkoa wa Dar es salaam.

  Wanafunzi hao wapo katika kambi iliyoandaliwa na uongozi wa mkoa wa Simiyu kwa ajili ya maandalizi ya mitihani ya kidato cha sita inayotarajiwa kufanyika mwezi ujao wa Mei. Kambi hiyo ipo katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa.

  “Uzoefu wetu na maoni ya wadau wetu umetufanya tuanzishe programu hizi nchini kote ili wakati wa kuomba mikopo, muombe kwa usahihi na wale wenye sifa wapate na hatimaye kutimiza ndoto zao,” aliwaambia wanafunzi hao na kueleza kuwa kuanzia kesho (Aprili 15, 2019) maafisa wa HESLB watakua katika shule mbalimbali mikoani kutoa elimu hiyo.

  Katika mikutano hiyo, wanafunzi wanaelezwa kuhusu sifa, nyaraka muhimu zinazotakiwa, namna ya kuomba na kuwasilisha kwa usahihi kwa njia ya mtandao na utaratibu na umuhimu wa kurejesha mkopo mara wamalizapo masomo. Katika programu hizi, wanafunzi pia hupata fursa ya kuuliza maswali na kupata ufafanuzi.

  Kwa mujibu wa Badru, katika mwaka wa masomo 2018/2019, kati ya waombaji wa mikopo zaidi ya 57,000 ambao walipata udahili vyuoni, maombi zaidi ya 9,000 yalikua na upungufu mkubwa ikiwemo kukosa nyaraka kama vyeti vya kuzaliwa, vitambulisho sahihi vya wadhamini, kutosainiwa na waombaji, wadhamini au serikali za mitaa au vijiji.

  Akizungumza na wanafunzi hao, Afisa Mikopo Mwandamizi kutoka HESLB Daudi Elisha aliwasihi wanafunzi hao kusoma kwa makini mwongozo utakaotolewa na HESLB mwezi ujao ambao utaeleza hatua kwa hatua kuhusu uombaji wa mkopo.

  “Kuna baadhi ya waombaji wa mikopo huwa na haraka, mwezi ujao tukianza kupokea maombi, tutatoa mwongozo kwa lugha ya kiswahili na kiingereza, ninawasihi mtulie na msome kwa makini, msiwe na haraka kwa kuwa mtakuwa na miezi zaidi ya miwli ya kuomba,” alisema Elisha na kuongeza:

  “Hivi vipeperushi tunavyowapa vina maswali na majibu 21 ambayo nayo yanawaeleza hatua kwa hatua, mkisoma na kuzingatia, naamini wale wenye sifa watafanikiwa,” alisema Elisha.Akizungumza katika mkutano huo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka, Mkuu wa Wilaya ya Maswa Dkt. Seif Shekalaghe aliishukuru HESLB kwa kutambua changamoto wanazokutana nazo wanafunzi na kuamua kuzitatua.

  “Sisi kama mkoa, tunawashukuru sana kwa kuwa jitihada zetu za kuongeza ufaulu hazitakua na faida kubwa kama vijana masikini watafaulu halafu wakashindwa kutimiza ndoto zao kwa kukosa mkopo … hii ni programu nzuri sana,” amesema Dkt. Shekalaghe.

  HESLB ilianzishwa mwaka 2004 na kuanza kazi rasmi mwezi Julai 2005 ili kutoa mikopo ya elimu ya juu kwa wanafunzi watanzania wasio na uwezo na pia kukusanya mikopo iliyoiva iliyotolewa na Serikali tangu mwaka 1994/1995.
   Mkuu wa Wilaya ya Maswa, mkoani Simiyu Dkt. Seif Shekalaghe akiongea jana (Jumamosi, Aprili 13, 2019) wilayani Maswa katika mkutano kati ya HESLB na wanafunzi 1,166 wa kidato cha sita kutoka mkoa wa Simiyu. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Abdul-Razaq Badru. HESLB inaendesha programu za elimu ya uombaji mikopo ya elimu ya juu kwa wanafunzi wa kidato cha sita nchini kote(Picha: HESLB)
   Mwanafunzi Casto Nyakalungu wa kidato cha sita katika Shule ya Sekondari Binza, mkoani Simiyu akiuliza katika mkutano kati ya wanafunzi wa kidato cha sita kutoka shule 12 za mkoani humo na maafisa wa HESLB waliofika kutoa elimu kuhusu sifa na utaratibu wa kuomba mkopo (Picha: HESLB).
  Mwanafunzi wa kidato cha sita katika Shule ya Sekondari Mwenge, mjini Singida Victor Masimo akiuliza swali katika mkutano kati ya wanafunzi wa shule hiyo na maafisa wa HESLB waliofika shuleni hapo kutoa elimu kuhusu sifa na utaratibu wa kuomba mkopo (Picha: HESLB).

  0 0

  Na. OWM, MOROGORO.

  Mtandao wa Afya moja kwa nchi za Afrika mashariki, Kati na Magharibi (OHCEA) umeendesha mafunzo ya Dhana ya Afya moja kwa wanafunzi wa ngazi ya Stashahada na Astashahada kutoka vyuo vya kwenye sekta za Afya ya Binadamu, Mifungo, Wanyamapori na Mazingira. Tanzania imekuwa nchi ya kwanza Duniani kufundisha Dhana hiyo katika ngazi hizo za taaluma, kwa kuwa nchi nyingine duniani hufundisha tu kwa ngazi ya Shahada na Shahada ya Uzamivu masuala ya Afya moja.

  Dhana ya Afya moja ambayo ni ushirikishwaji wa pamoja sekta ya Afya ya Binadamu, Wanyamapori, Mfugo, Kilimo na mazingira katika kujiandaa, kufuatilia na kukabili magonjwa yatokayo kwa wanyama kwenda kwa binadamu ama kinyume chake. Wataalamu hao wamepata mafunzo hayo kwakuwa wapo karibu sana na jamii na pindi utokeapo mlipuko wa ugonjwa ndio huwa kikosi kazi cha kwanza na mstari wa mbele kuwa eneo la tukio katika kufuatilia na kukabili milipuko, kabla ya wataalamu wengine kushiriki kikamilifu.

  Akiongea wakati wa kufunga Warsha ya kufanya tathmini ya namna wakufunzi wanavyotumia mitaala ya Afya Moja katika kuwafundisha wanafunzi wao wa ngazi ya Stashahada na Astashahada, tarehe 13 Aprili, Mjini Morogoro, Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Shughuli za Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe alifafanua kuwa mafunzo hayo yanajenga kikosi kazi imara chenye kuchagiza shughuli za Afya moja hapa nchini.

  “Katika kuimarisha Afya ya Binadamu pamoja na Afya ya mifugo na wanyamapori, kwa kutumia Dhana ya Afya moja, ninafarijika kwa jitihada hizi za kuwajengea uwezo Wataalamu wa sekta za Afya katika ngazi ya Stashahada na Astashahada pamoja na wakufunzi wao, kwa kuwa tunaandaa rasilimali watu ya kuweza kuwa na uwezo wa kujiandaa, kufuatilia na kukabili magonjwa kwa Dhana ya Afya moja. Alisema Matamwe.

  Wakiongea kwa nyakati tofauti waratibu wa mafunzo hayo Profesa; Japheti Killewo na Profesa. Robinson Mdegela walifafanua kuwa tayari mitaala ya Afya moja kwa ngazi ya stashahada na astashahada imekamilika, lakini wakati taratibu za kuingiza masuala ya Afya moja zitakamilika hivi karibuni katika mitaala ya ngazi ya stashahada na Astashahada wameamua kufanya mafunzo hayo ili wakufunzi kujifunza kwa vitendo juu ya kufundisha masuala ya Afya moja lakini pia na kuwaandaa wanafunzi watakao fundishwa kwa kutumia mitaala hiyo.

  Aidha waratibu hao walibainisha kuwa wanafunzi hao wakiweza kuielewa vizuri dhana ya Afya moja watatumika vyema kuielimisha jamii juu ya masuala ya Afya Moja, na nchi yetu itaweza kuzuia maambukizi ya magonjwa ya mlipuko hususani yale yatokayo kwa wanyama kwenda kwa binadamu na pia kupunguza usugu wa madawa kwa sababu wataweza kuongeza ushirikiano, mawasiliano na uratibu baina ya sekta husika.

  Mafunzo hayo yaliyowajumuisha zaidi ya wanafunzi 210, wa ngazi ya astashahada na ngazi ya cheti kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi, Muhimbili, SUA, Wakala wa Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo Morogoro, Chuo cha Afya cha Kilosa, Chuo cha Wanyamapori Pasiansi na Chuo cha Wanyamapori Mweka,

  Aidha, wakufunzi zaidi ya 30 wameshiriki kutoka Chuo Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili, Chuo kikuu cha Kilimo Sokoine, Vyuo vya Afya Lindi, Mafinga, Kilosa, Mtwara, Singida, Kagemu, Mirembe, Wakala wa Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo Morogoro, Temeke, Tengeru, Buhuri, pamoja na Vyuo vya Taaluma ya Wanyamapori , Pasiansi na Mweka.

  Mafunzo hayo yameratibiwa na Chuo Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili na Chuo kikuu cha Kilimo Sokoine kwa kushirikiana na USAID, kupitia vyuo vikikuu vya MINNESOTA na Tufs vya nchini Marekani
  Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Shughuli za Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe akimkabidhi cheti mmoja wa washiriki wa mafunzo ya  Afya Moja katika kuwafundisha wanafunzi wa ngazi ya Stashahada na  Astashahada, mjini Morogoro tarehe 13 Aprili.
   Baadhi ya wanafunzi wa ngazi ya Stashahada na  Astashahada wa sekta za Afya ya Binadamu , wanyamapori, mifugo, kilimo na Mazingira wakifuatilia warsha ya kufunga mafunzo hayo ya  Afya Moja, mjini Morogoro tarehe 13 Aprili.
    Mratibu kutoka  Chuo Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili,  Profesa Japhet Killewo akisisitiza jambo wakati wa kufunga Warsha ya kufanya tathmini ya namna wakufunzi wanavyotumia mitaala ya Afya Moja katika kuwafundisha wanafunzi wao wa ngazi ya Stashahada na  Astashahada, mjini Morogoro tarehe 13 Aprili.
   Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Shughuli za Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe akimkabidhi cheti mmoja wa washiriki wa mafunzo ya  Afya Moja katika kuwafundisha wanafunzi wa ngazi ya Stashahada na  Astashahada, mjini Morogoro tarehe 13 Aprili.
   Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Shughuli za Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe akisistiza jambo wakati wa kufunga Warsha ya kufanya tathmini ya namna wakufunzi wanavyotumia mitaala ya Afya Moja katika kuwafundisha wanafunzi wao wa ngazi ya Stashahada na  Astashahada, mjini Morogoro tarehe 13 Aprili
   Baadhi ya Waratibu wa Warsha ya kufanya tathmini ya namna wakufunzi wanavyotumia mitaala ya Afya Moja katika kuwafundisha wanafunzi wao wa ngazi ya Stashahada na  Astashahada, mjini Morogoro tarehe 13 Aprili, kulia ni Mratibu kutoka  Chuo Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili,  Profesa Japhet Killewo na kushoto ni Mratibu kutoka Chuo kikuu cha Kilimo Sokoine, Profesa. Robinson Mdegela, katikati ni Rasi wa Ndaki ya Tiba za Wanyama na Sayansi za Afya Chuo kikuu Sokoine.  
   Baadhi ya wanafunzi wakimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Shughuli za Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe (hayupo pichani) wakati wa kufunga Warsha ya kufanya tathmini ya namna wakufunzi wanavyotumia mitaala ya Afya Moja katika kuwafundisha wanafunzi wao wa ngazi ya Stashahada na  Astashahada, mjini Morogoro tarehe 13 Aprili.
  Mratibu kutoka  Chuo Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine,  Profesa Robinson Mdegela akisisitiza jambo wakati wa kufunga Warsha ya kufanya tathmini ya namna wakufunzi wanavyotumia mitaala ya Afya Moja katika kuwafundisha wanafunzi wao wa ngazi ya Stashahada na  Astashahada, mjini Morogoro tarehe 13 Aprili.

  0 0

  Kamishna wa Tume ya Madini Dkt. Athanas Machiyeke mwenye kofia ya blue na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama na viongozi mbalimbali wakifanya jitihada ya kuinasua Gari ya polisi iliyokuwa imenaswa kwenye maji katikati ya mto wakati wakielekea mgodini


  amishna wa Tume ya Madini Dkt. Athanas Machiyeke akifukia shimo barabari ili kuwezesha magari yapite yaliyo kuwa yanaelekea mgodini kwa kwa lengo la kwenda kukagua shuguli za uchimbaji, mwenye sakafu ni mkuu wa wilaya ya Gairo na mwenye sare nyeupe ni askari wa usalama barabarani wilaya ya Gairo Sarehe Rajabu Mkambaku.
  Mkuu wa wilaya ya Gairo, Mwenyekiti wa Tume ya Madini na Kamishna wa Tume ya Madini na mjumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wakiangalia aina ya mawe yenye asili ya madini ambayo yameokotwa juu ya ardhi kwenye shamba la mahindi kandokando ya mto. 
  Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Kikula wa kwanza kushoto akiangalia madini ya Rubi Nut yaliyotelekezwa na mchimbaji wa madini hayo Sadick Athuman maarufu kwa jina la Saadam alie kimbia baada ya kuona msafara wa tume ya Madini na Mkuu wa Wilaya Gairo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya Gairo Siriel Shaid Mchembe na Kamishna wa Tume ya Madini Dkt. Athanas Machiyeke.
  Msafara wa tume ya Madini na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wakiwa kwenye eneo la mgodi Kijiji cha Kirama walipotembelea kukagua shuguli za uchimbaji katika eneo hilo wa mbele ni Athumani anae uongoza msafara kwenda kuonyesha anapochimba Sadick Athuan baada ya kukimbia
  Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Kikula wa pili kulia akiwa na kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya gairo ikiongozwa na mwenyekiti wake Siriel Shaid Mchembe wa tatu kushoto na wa kwanza kulia ni Kamishna wa Tume ya Madini Dkt. Athanas Machiyeke wakionyesha baadhi ya vifaa ikiwemo pikipiki iliyo telekezwa na mchimbaji wa madini Sadick Athuman maarufu kwa jina la Saadam alie kimbia baada ya kuona msafara wa tume ya Madini. 
  Kamanda wa jeshi la wananchi “Sajenti” Mkongwa akijaribu kuiwasha pikipiki iliyotelekezwa na mchimbaji wa madini Sadick Athumani baada ya kuona msafara wa tume ya madini na kamati ya ulinzi na usalama.  Na Issa Mtuwa (Wizara ya Madini) Gairo 

  Wachimbaji wa Madini ya Rubi wilaya ya Gairo kata ya Iyombe kijiji cha Kirama, wamekimbia na kutelekeza Madini ya viwandani aina ya Rubi Nut, Pikipiki na vifaa mbalimbali vya kuchimbia baada ya kuona msafara wa Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idris Kikula na Mwenyekiti wa ulinzi na usalama ambae pia ni Mkuu wa Wilaya (DC) ya Gairo Seriel Shaid Mchembe waliokuwa wanatembelea mgodi huo kuona shuguli za uchimbaji kwa lengo la kwenda kutatua kero zinazowakabili. 

  Msafara wa mwenyekiti wa Tume ya madini akiwa ameambatana na Kamishna wa Tume hiyo Dkt. Athanas Machiyeke na mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ulianza majira ya saa tatu asubuhi kuelekea kwenye eneo la mgodi. 

  Wakiwa njiani msafara huo ulikubwa na changamoto baada ya gari ya Polisi iliyokuwa inaongoza msafara huo kukwama kwenye maji katikati ya mto kwa muda wa saa moja kitendo kilichopelekea kuchelewa kufika kwenye eneo la mgodi. 

  Hata hivyo mara baada ya kufika kwenye nyumba ya mchimbaji mmoja alie tambuliwa kwa jina la Sadick Athuman maarufa kwa jina la (Saadam) alikutwa kijana mmoja aliejitambulisha kwa jina la Athumani mkazi wa Gairo mjini akilinda mahali apo ndipo mkuu wa Wilaya na vyombo vyake vya ulinzi na Mwenyekiti wa Tume na Kamishna waliingia ndani na kufanya msako na kukuta madini aina ya Rubi Nut yakiwa kwenye mifuko, Pikipiki moja na vifaa mbalimbali vya kuchimbia. 

  Alipo ulizwa bwana Athumani, nani anae miliki madini hayo, alisema ni madini ya bwana Saadam. Alipo ulizwa yeye anafanya nini alisema yeye ni kibarua tuu na mwenyewe Saadam yupo mgodini anaendelea na uchimbaji ndipo Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama akamuamuru Athumani kwenda nae mpaka anakochimba bwana Saadam na mara baada ya kufika eneo la mgodi wachimbaji wote wakakimbia na kuelekea vichakani akiwemo bwa Saadam huku vifaa vya uchimbaji vikiwa vimetelekezwa sambamba na madini yale ya kwenye mfuko na pikipiki. 

  Kufuatia kitendo hicho mwenyekiti wa tume ya Madini Prof. Kikula amesikitishwa na kitendo hicho ambacho kinaashiria uchimbaji wa mgodi huo unafanyika bila kufuata sheria. 

  Kutokana na hali hiyoo, mwenyekiti wa tume amemuagiza afisa Madini Mkazi mkoa wa Morogoro Mhandisi Emmanuel Shija kufuatilia uhalali wa eneo hilo (Leseni na Codinates) na mwenendo mzima wa uchimbaji wake, endapo eneo hilo litakuwa na leseni mmiliki wake alipe maduhuli yote anayotakiwa kulipa tangu alipoanza na kama eneo hilo halijakatiwa leseni mgodi huo ufungwe mara moja na shuguli za uchimbaji zisitishwe mara moja. 

  Aidha, amesikitishwa na wachimbaji na wawekezaji katika eneo hilo kushindwa kusaidia shuguli za maendelo ya kijiji kinacho zunguka migodi hiyo ambapo ofisi yake haikumridhisha mwenyekiti wa tume. 

  Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Gairo amesikitishwa na wachimbaji hao kwa kukiuka sheria zinazo ongoza shuguli za uchimbaji madini, amesema amekuwa akiwahimizi mara kadhaa wachimbaji wote wilayani humo kuzingatia na kufuata taratibu kabla hawajanza kazi za uchimbaji ikiwemo kukata leseni na kulipa maduhuli ya serikali. 

  Kufuatia kwa tukio hilo Mchembe amepiga marufuku kwa mtu yeyote katika wilaya ya Gairo kufanya shuguli za madini bila kuwa na kibali kutoka tume ya madini. 

  Wakati huo huo Mchembe amemuagiza Kamanda wa Polisi wilaya ya Gairo Lugano Piter Mwakisunga kuhakikisha anamkamata Sadick Athumani ndani ya siku saba na kumfikisha kwenye vyombo vya sheria. 

  Wakiwa kwenye mgodi wa eneo la mwekezaji wa kampuni ya Mofar Holdings (T) Ltd Kamishna wa Tume ya Madini Dkt. Machiyeke amemsisitiza mwekezaji huyo kuzingatia taratibu na sheria katika hatua ya kuajiri wafanyakazi na vibarua na manunuzi ya bidhaa kama muongozo unavyo sema. 

  Dkt. Machiyeke amesema, sheria inasisitiza kutoa kipaumbele kwa wananchi waozunguka mgodi na taifa kwa nafasi kubwa kabla ya kufikiria nje ya eneo hilo na nje ya nchi. 

  Mwenyekiti wa Tume ya Madini na Kamishna walikuwa wanahitimisha ziara yao ya siku tano katika mkoa wa Morogoro baada ya kutembelea wilaya ya Morogoro mjini, Ulanga, Mvomero na Gairo ambapo ujumbe wake mkubwa kwa wafanyakazi wa tume na wachimbaji madini ulikuwa ni uadilifu katika kazi zaona kuepuka rushwa+. 

  0 0

  Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Dr. Augustine Mahiga amewataka Viongozi wa Tanzania hasa Viongozi Vijana kuiga mfano wa UZALENDO na UTUMISHI ULIOTUKUKA wa Hayati Edward Moringe Sokoine ambaye aliitumikia nchi hii kwa nafasi mbalimbali za Uongozi mpaka katika Ngazi ya Uwaziri Mkuu.

  Hayo yamesemwa Wilayani Monduli,Arusha Tarehe 12.04.2019 wakati wa Ibada ya maadhimisho ya miaka 35 ya kifo cha Hayati Edward Moringe Sokoine,Ibada iliyoongozwa na Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo.

  “Sokoine aliipenda nchi yake,aliweka uzalendo mbele.Alikuwa ni mchapakazi asiyechoka,kuna siku aliniita nyumbani kwake saa 8 usiku kujadili masuala nyeti ya Taifa akanionea huruma akasema nikapumzike ila nirudi saa 11 Alfajiri, na nilivyorudi nilimkuta yeye bado yupo macho mezani pale pale ananisubiri.Viongozi tuna la kujifunza kwa aina hii ya maisha ya utumishi na kujitoa”Alisema Balozi Mahiga

  Akishukuru kwa niaba ya Familia,Mtoto wa Kiume wa Hayati Sokoine Balozi Joseph Sokoine amewashukuru watu wote waliojumuika nao katika siku hiyo muhimu na kuwataka Watanzania wayaenzi mambo mema yaliyofanywa na Baba yake na kwa kuwa Hayati Sokoine aliwapenda sana watanzania katika kumuenzi katika hilo Sokoine Memorial Foundation ilikabidhi madawa yenye Thamani ya Tsh 2.5m kwa kituo cha Afya Monduli na kadi 100 za Bima ya Afya kwa kaya maskini.

  Ibada hiyo pia ilihudhuriwa na Waziri Mkuu Mstaafu wa Serikali ya awamu ya nne Mh Mizengo Kayanza Peter Pinda,Naibu Waziri wa Kilimo Mh William Ole Nasha,Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Mh Anthony Mavunde,Mwenyekiti wa CCM Mkoa Arusha na Viongozi mbalimbali wa Siasa na Dini.


  0 0

  UNICEF NA TEF WATOA TUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI ZA WATOTO

  Na mwandishi wetu wa blog ya jamii,Tanga

  VYOMBO vya habari nchini vimekumbushwa juu ya wajibu wa kuendelea kuzipa kipaumbele habari zinazohusu masuala ya watoto na kufichua vitendo vyote vya ukatili wanavyotendewa ili mamlaka husika ziweze kuchukua hatua za kukabiliana na vitendo hivyo.

  Hayo jana Mkoani Tanga, na kaimu mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile  wakati wa hafla ya utoaji Tuzo za uandishi wa habari za watoto zinazoandaliwa na TEF kwa ushirikiano na Shirika la watoto ulimwenguni (UNICEF) Tawi la Tanzania.

  Balile alisema iwapo vyombo vya habari nchini vitajenga utamaduni wa kutoa kipaumbele kwa habari za watoto ni wazi serikali na wadau wengine wa watoto wataweza kuchukua hatua madhubuni za kuhakikisha mtoto wa Tanzania analindwa na kupata haki zake za msingi.

  “Lengo letu tukiwa waandishi wa habari ni kuangalia ni jinsi gani habari za watoto zinazoandikwa zitawasaidia watoto hapa nchini kuwaondolea ugumu wa maisha ya katika sehemu mbalimbali kwa kuwashirikisha kiuchumi, ili tuwasaidie kuondokana na ugumu walionao hivi sasa na waishi maisha bora zaidi,” alieleza Balile.

  Pia Balile alilishukuru shirika la UNICEF kwa ushirikiano mkubwa ambao linautoa kwa Jukwaa la wahariri hapa nchini ikiwemo kusaidia mafunzo mbalimbali kwa waandishi wa habari ambayo yameweza kuwajengea uwezo wa kuandika habari za watoto ambazo zimeanza kuleta matokeo mazuri kwa hivi sasa.

   Mwakilishi wa UNICEF Tanzania, Manisha Mashira aliwapongeza washindi wote 10 walioshinda tuzo hiyo kwa mwaka huu wa 2019 ambapo alisema wao binafsi wamefurahishwa na kazi nzuri zilizofanywa na waandishi hao na kuwataka waongeze bidii zaidi.

  “Nichukue fursa hii kuwapongeza waandishi wote mlioshinda kwa mwaka huu na kupewa Tuzo ya uandishi wa habari za masuala ya uchumi kwa watoto, tuzo hizi zimeonesha jinsi gani mnavyoandika habari kwa ajili ya kuwasaidia watoto,”

  “Niwapongeze pia viongozi wa Jukwaa la wahariri Tanzania (TEF) kwa juhudi wanazozifanya kwa lengo la kuwasaidia waandishi wa habari hapa nchini na niombe tuendelee kujitahidi katika kuijenga Tanzania, kwa upande wetu UNICEF tutaendelea kuwaunga mkono katika masuala yanayohusu watoto,” alieleza Manisha.

  Awali mmoja wa wajumbe wa baraza la TEF, Absalom Kibanda alitoa historia fupi ya jinsi kundi la wahariri lilivyoanzishwa mnamo mwaka 2017  likiwa na wahariri 15 ambapo moja ya malengo yake ni kuangalia jinsi gani waandishi watatumia kalamu zao kutetea haki za watoto.

  Kibanda pia aliwapongeza washindi wa tuzo hiyo kwa mwaka huu ambapo alisema TEF iliamua kubeba dhima ya kuielimisha jamii na kutetea haki za mtoto kama msingi wa kuweka msukumo kwa serikali na taasisi nyingine za umma na binafsi kuweza kutambua masuala ya haki za msingi za mtoto.

  Akitangaza rasmi majina ya washindi, katibu wa TEF, Neville Meena aliwakumbusha waandishi wote umuhimu wa kuendelea kuandika habari zinazohusu watoto kwa kuangalia pia katika halmashauri zao ni kiasi gani cha fedha kinatengwa katika bajeti za kila mwaka kwa ajili ya utekelezaji wa masuala ya watoto.

  Washindi waliotangazwa na kupewa Tuzo kwa mwaka huu wa 2019 ni pamoja na mwandishi wa gazeti la Majira, Suleiman Abeid kutoka Shinyanga, Lilian Lugakingira (Nipashe), Rehema Matowo (Mwananchi) na Sifa Lubasi (Habari Leo).

  Wengine ni Anne Robi (Daily News) ambaye pia alikuwa mshindi wa Tuzo ya jumla, Tumaini Msowoya (Mwananchi), John Kabambala (TKT Morogoro), Mwanzani Kiembe (ABM Dodoma), Arnold Jovin (Radio Kwizera) na Angelina Lukindo (Upendo Radio) huku Anne Rhobi(Daily News)akiibuka mshindi wa Jumla katika tuzo hizo.

   Mshindi wa jumla tunzo za kuandika habari za watoto Anne Rhobi kutoka gazeti la Daily News akipokea zawadi yake kutoka kwa mwakilishi wa UNICEF Tanzania Manisha Mashira.
   Baadhi ya waandishi washindi wa tunzo za habari za uandishi.wa watoto wakiwa na vyeti vyao vya ushindi.
   Picha ya pamoja

  0 0


  *Asema kuanzia kesho hakuna kiingilio kwa Watanzania

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefungua mashindano ya AFCON U17 na kutangaza kuwa kuanzia kesho Watanzania wataingia bila kulipia.

  Ametoa kauli hiyo leo jioni (Jumapili, Aprili 14, 2019) kwenye ufunguzi wa michuano hiyo iliyoanza leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. 

  Waziri Mkuu ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa michuano hiyo, aliambatana na Rais wa Shirikisho la Soka na barani Afrika (CAF), Ahmad Ahmad kukagua timu zilizofungua dimba na kisha akatangaza uamuzi huo wa Serikali. 

  Timu zilizofungua dimba leo ni Serengeti Boys ya Tanzania na Nigeria. Katika mchezo wa leo Nigeria imeibuka kidedea baada ya kuifunga Tanzania mabao 5-4. Hadi mapumziko timu ya Nigeria ilikuwa ikiongoza kwa mabao 3-1.

  Mabao ya Nigeria yalipatikana dakika ya 20, 29, 36, 71 na 78 wakati mabao ya Tanzania yalipatikana dakika ya 21, 51, 56 na 60 ambapo magoli mawili kati ya hayo, yalipatikana kwa njia ya penati.

  Bao la kwanza la Tanzania lililofungwa na Alphonce Mabula Msanga lilitinga kimiani dakika ya 21. Bao la pili, lilipatikana dakika ya sita ya kipindi cha pili na lilifungwa na Kelvin Pius John.

  Dakika tano baadaye, Morice Michael Abraham aliipatia Tanzania bao la tatu lililofungwa kwa njia ya penati. Kabla vijana wa Nigeria hawajakaa sawa, dakika nne nyingine, Edmund Godfrey John alitinga kimiani bao la nne, ambalo pia lililifungwa kwa penati.

  Timu ya Tanzania iko kundi A na imepangwa na timu za Nigeria, Uganda na Angola. Michuano hii inatarajiwa kumalizika Aprili 28. Endapo timu hiyo ya Taifa ya vijana ya Serengeti Boys itaibuka na ushindi katika michezo yake miwili, itakuwa imekata tiketi ya kushiriki mashindano ya dunia kwa vijana wa umri wa miaka 17 yatakayofanyika mwakani huko Brazil.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiikagua Timu ya Tanzania ya Serengeti Boys iliyopamba na Nigeria katika mechi ya Ufunguzi wa Michuano ya AFCON U17 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Aprili 17, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua Mashindano ya AFCON U17 kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam Aprili 14, 2019. Wenye Jezi za Bluu ni Timu ya Tanzania – Serengeti Boys na kulia ni Timu ya Nigeria. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi katika mechi ya ufunguzi wa Michuano ya AFCON U17 ambapo Tanzania ilipambana na Nigeria kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Aprili 14, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Rais wa Shirikisho ya Soka Barani Afrika (CAF), Ahmad Ahmad katika mechi ya ufunguzi ya Mashindano ya AFCON U17 kati ya Tanzania na Nigeria kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Aprili 14, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

older | 1 | .... | 1838 | 1839 | (Page 1840) | 1841 | 1842 | .... | 1897 | newer