Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1831 | 1832 | (Page 1833) | 1834 | 1835 | .... | 1904 | newer

  0 0


  PMO_2292AAA
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na wabunge wakifurahia katika mazungumzo na Peter Mollel maarufu kwa jina la Pierre Konki Liquid (katikati) kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Aprili 3, 2019. Wengine kutoka kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum, Mariamu Ditopile, Mbunge wa Viti Maalum, Munde Tambwe, Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais na Mbunge wa Singida Mjini, Mussa Sima, Mbunge wa Kiembesamaki, Ibrahim Raza na Mbunge wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Bi. Neema Mtemvu, Afisa Uhusiano (TBS), akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari Kibaoni wakati TBS ilipotembela shuleni hapo kutoa elimu juu bidhaa hafifu.
  Wanafunzi wa shule ya sekondari Kwashungu, wakisikiliza elimu juu ya masuala yahusuyo viwango vya ubora, kutoka kwa maafisa Wa TBS.
  Bi.Amina Yasin, Afisa Udhibiti ubora Mwandamizi (TBS), akizungumza na wajasiriamali wilayani kilombero kuhusiana na utaratibu wa kupata alama ya ubora ya TBS.
  Bi Amina Yasin, Afisa Udhibiti Ubora Mwandamizi(TBS) akizungumza na wananchi wa soko kuu la Ifakara, wilayani Kilombero, juu ya umuhimu wa kununua bidhaa zilizothibitishwa ubora wake na TBS.

  ……………………………..

  Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limetembelea shule ya sekondari Kibaoni pamoja na Shule ya sekondari ya Kwashungu wakati wa Kampeni yake ya kuelimisha umma juu ya umuhimu wa kununua bidhaa zilizo na ubora katika Wilaya ya Kilombero. 

  Bi. Gladness Kaseka, Afisa Masoko Mwandamizi (TBS) akizungumza na wanafunzi pamoja na walimu, amefafanua umuhimu wa viwango katika maisha yao ya kila siku vilevile kuwafahamisha fursa ya huduma bure kwa wajasiriamali wadogo.

  Bi Gradness amesisitiza kuwa jukumu la kupiga vita bidhaa hafifu katika Taifa ni la kila mtu, hivyo aliwaasa wawe mabalozi wazuri wa kuhamasisha ubora katika jamii wanazoishi.

  Kwa upande wake, Mwalimu mkuu wa Shule ya Sekondari Kibaoni, Bw. Kalinga aliwapongeza TBS kwa kufika shuleni hapo kwani ni mkakati mzuri ukizingatia shule huwa na wanafunzi wengi na wanaoishi maeneo mbalimbali hivyo ikiwa kila mmoja atasambaza ujumbe huo kwa ndugu jamaa na marafiki utakuwa umewafikia watu wengi kwa muda mfupi. Mwalimu Kalinga pia hakuacha kutoa wito kwa TBS kuendelea na zoezi hilo kwani linajenga msingi mzuri kwa vizazi vijavyo na kutengeneza jamii yenye tamaduni ya kujali ubora.

  Kampeni hiyo ya Elimu kwa umma pia ilifanyika katika Soko kuu la Ifakara lenye viunga 515 na maduka 105, pamoja na maeneo ya madukani Ifakara mjini, huku jumla ya wanafunzi 2,089 na walimu 78 wakipata elimu juu ya masuala mbalimbali yahusuyo Ubora .

  Sambamba na hayo, TBS ilitoa semina kwa wajasiriamali wapatao 23 katika ukumbi wa halmashauri ya mji Ifakara, ambapo Bi.Amina Yasin, Afisa Udhibiti Ubora Mwandamizi (TBS), aliwasisitiza wajasiriamali kufuata utaratibu waliolekezwa ili kupata leseni ya kutumia alama ya ubora ya TBS bure bila gharama yoyote, kwani ni fursa ambayo inamlenga kumwinua mzalishaji kuweza kushindana na kuuza ndani na nje ya nchi . Vilevile wasisite kutuma maombi TBS kwa ajili ya kupata mafunzo maalum yatolewayo kwa wajasiriamali.

  0 0

  Mwanasheria mkuu wa kwanza Tanzania Jaji Mstaafu Mark Bomani amewataka watanzania kuchangamkia fursa ya mabadiliko ya sheria katika sekta za maliasili na madini yaliyofanyika hivi karibuni,kutokana na sheria hizo kuweka mazingira ya usawa (win - win situation)tofauti na sheria zilizokuwepo awali kutoa kipaumbele kwa wawekezaji kutoka Nje ya nchi.

  Jji Mstaafu Mark Bomani ameyasema hayo alipomtembelea ofisini kwake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi kwa lengo la kubadilishana mawazo kuhusu sekta ya madini nchini na kuongeza kuwa Tanzania ina utajiri mkubwa wa madini unaotosha kuendesha Nchi ukiachilia mbali maliasili nyingine zilizopo tatizo ni kuwa madini hayo hayakulinufaisha Taifa.

  “Mabadiliko ya sheria waliyoyafanya yatasaidia sana,sasa ni jukumu letu sisi Watanzania kuichangamkia fursa hiyo na tusisubiri kulalamika kama ilivyo kawaida yetu,tfanye kazi kwa bidii maana utajiri huu wa madini tuutumie na kujiletea maendeleo binafsi na yanchi kwa ujumla kwa kuwa sasa sheria hizi mpya zimeweka uwanja sawa”

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi mbali na kumshukuru Jaji Mstaafu Mark Bomani kumtembelea ofisini kwake ameongeza kuwa mabadiliko yaliyofanyika katika sheria za madini yametokana kwa kiasi kikubwa na ripoti ya tume iliyoundwa kuchunguza sekta ya madini ikiongozwa na Jaji Mstaafu Mark Bomani.

  “Haya yoote tuliyoyabaini na kuyaeleza kama upungufu yamo kwenye ripoti ya Bomani ingawa kuna mengine tuliyoyaongeza kama vile mrahaba ulio chini,kutolipa kodi na mengine mengi na kwakuwa Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ameutangaza mwaka 2019 kuwa mwaka wa uwekezaji,Mzee Bomani amekuja ili tubadilishane mawazo tuone namna ya kuuboresha mwaka huu wa uwekezaji” 
   
  Ameongeza kuwa wamezungumzia namna ya kuweka mikakati ya kuwavutia wawekezaji wenye tija kuja nchini kuwekeza ili Taifa liweze kunufaika na madini kupitia kodi,ajira kwa vijana na kwamba ujio wa Jaji Mstaafu Mark Bomani ofisini kwake umemjengea ari na nia ya kuonana na viongozi wengine waliolitumikia Taifa kwa tija ili aweze kupata maoni yao ya namna ya kuendesha shughuli za serikali katika wizara aliyopangiwa kazi na Rais Dkt John Pombe Magufuli.
   Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi (kushoto) akimsikiliza kwa makini mgeni wake Jaji Mstaafu Mark Bomani alipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es salaam.
  PICHA 2: Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi (kushoto) akiwa na mgeni wake Jaji Mstaafu Mark Bomani alipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es salaam.

  0 0  Meneja Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Nyanza Bottlers, Samwel Makenge (wa pili kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa Promosheni inayoendelea ya ‘Kunywaaah na Ushinde’ ambao wamejishindia zawadi mbalimbali zikiwemo TV na fedha taslim wote wakiwa ni wakazi wa Mwanza. Hafla ya makabidhiano ya zawadi hiyo ilifanyika jana jijini humo. Kunywaah na Ushinde ni Promosheni ya miezi mitatu inayoenda sambamba na msimu huu wa Coke Studio ambayo imedhamiria kuwatunuku wateja wake pendwa ambapo watu mbalimbali wanajinyakulia fedha taslimu, runinga na bidhaa nyingine nyingi kutoka Coca Cola.
  Meneja Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Nyanza Bottlers, Samwel Makenge (kushoto) akikabidhi zawadi ya Runinga kwa Mkazi wa Mwanza, Shaban Ismail wakati wa hafla ya kuwakabidhi washindi wa Promosheni hiyo inayoendelea ya ‘Kunywaaah na Ushinde’ ambayo ilifanyika jana jijini humo. Promosheni hiyo ya miezi mitatu inaenda sambamba na msimu huu wa Coke Studio ambayo imedhamiria kuwatunuku wateja wake pendwa ambapo watu mbalimbali wanajinyakulia fedha taslimu, runinga na bidhaa nyingine nyingi kutoka Coca Cola.

  Meneja Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Nyanza Bottlers, Samwel Makenge (kushoto) akikabidhi zawadi ya fedha taslimu kiasi cha shilingi laki moja 100,000/= kwa Mkazi wa Mwanza, Carolyne Ngowi wakati wa hafla ya kuwakabidhi washindi wa Promosheni inayoendelea ya ‘Kunywaaah na Ushinde’ ambayo ilifanyika jana jijini humo. Promosheni hiyo ya miezi mitatu inaenda sambamba na msimu huu wa Coke Studio ambayo imedhamiria kuwatunuku wateja wake pendwa ambapo watu mbalimbali wanajinyakulia fedha taslimu, runinga na bidhaa nyingine nyingi kutoka Coca Cola.
  Meneja Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Nyanza Bottlers, Samwel Makenge (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa fedha taslimu kiasi cha shilingi laki moja 100,000/= wa Promosheni inayoendelea ya ‘Kunywaaah na Ushinde’, Marco Msaba (kushoto) na Carolyne Ngowi (kulia) ambao wote ni wakazi wa Mwanza. Hafla ya makabidhiano ya zawadi hiyo ilifanyika jana jijini humo. Kunywaah na Ushinde ni Promosheni ya miezi mitatu inayoenda sambamba na msimu huu wa Coke Studio ambayo imedhamiria kuwatunuku wateja wake pendwa ambapo watu mbalimbali wanajinyakulia fedha taslimu, runinga na bidhaa nyingine nyingi kutoka Coca Cola.

  0 0  0 0

  On the 2nd of April, 2019, BANK OF AFRICA- TANZANIA introduced the bank’s new Managing Director and CEO Mr. Joseph Iha together with two other members in the managerial level, Deputy Managing Director Mr. Samir Yassine and General Managing Credit & Control Mr. Ellis Katwebaze.

  Addressing the bank’s staff members, clients and Bank of Tanzania Deputy Governor, Dr. Bernard Kibesse in Dar es salaam, Iha said digitization is the only way BOA under his management will consider as priority.

  “We will focus on digitization to enhance self- service solutions especially for corporate customers. We will continue to invest in innovation and alignment of our products and services to make them relevant to meet specific needs of clients,” said Iha while acknowledging that he has inherited a health bank.

  He promised to stay the course by improving service delivery, productivity while reducing cost and risk facing the bank’s products and services. “We will also focus on increasing value for business in the East African region,” the new BOA chief executive added.


  BANK of Africa Tanzania Limited Board Chairperson, Ambassador Mwanaidi Maajar (left), BANK of Tanzania Deputy Governor, Dr. Bernard Kibesse (Center) and the new Managing Director, Mr. Joseph Iha at a Cocktail party in Dar es salaam.


  BANK of Africa Tanzania Limited Board Chairperson, Ambassador Mwanaidi Maajar shaking hands with the newly appointed Managing Director, Joseph Iha at Serena Hotel, Dar es salaam.


  BANK of Africa Tanzania Limited Board Chairperson, Mwanaidi Maajar (Centre) together with the high ranking officers of the bank introduced to customers the new Managing Director, Joseph Iha, Deputy Managing Director Samir Yassine and the General Manager, Credit and Control, Mr. Ellis Katwebaze at Cocktail party organized by the bank.


  Bank of Africa newly appointed Managing Director, Joseph Iha introducing his management team to the clients, board members and Bank of Tanzania Deputy Governor, Dr. Bernard Kibese during his inauguration in Serena Hotel, Dar es salaam.


  BANK of Africa Tanzania Limited Board Chairperson, Mwanaidi Maajar sharing a light moment with the Ambassador of Kenya Embassy, Ambassador (Hon). Dan Kazungu.


  Bank of Africa Tanzania Limited Board Chairperson, Ambassador Mwanaidi Maajar addressing the invited guests at the introduction of the newly appointed Managing Director & CEO of the bank.


  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud (kulia) wakati akiwasili kwenye ufunguzi wa Kongamano la Pili la Maadhimisho ya kumbukumbu ya Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Kwanza wa Baraza la Mapinduzi Hayati Sheikh Abeid Amani Karume linalofanyika kwenye Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kampasi ya Zanzibar Bubu. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Ndugu Stephen Wasira (kushoto)wakati akiwasili kwenye ufunguzi wa Kongamano la Pili la Maadhimisho ya kumbukumbu ya Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Kwanza wa Baraza la Mapinduzi Hayati Sheikh Abeid Amani Karume linalofanyika kwenye Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kampasi ya Zanzibar Bubu. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
   :Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mwenyekiti wa Kongamano Spika Mstaafu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Pandu Amiri Kificho wakati akiwasili kwenye ufunguzi wa Kongamano la Pili la Maadhimisho ya kumbukumbu ya Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Kwanza wa Baraza la Mapinduzi Hayati Sheikh Abeid Amani Karume linalofanyika kwenye Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kampasi ya Zanzibar Bubu. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)


  0 0

  Na Shushu Joel.

  KATIKA uendelezaji wa sekta ya utalii nchini serikali ipo katika mchakato wa kuanzisha ujenzi wa terminal ya cruise katika Bandari ya jiji la Dar es salaam.

  Ujenzi wa Bandari hiyo katika bahari ya hindi utasaidia kupokea watalii kutoka nchi mbalimbali.

  Hayo yalielezwa leo na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk. Aloyce Nzuki,alipokuwa akipokea watalii zaidi ya 350 kutoka nchi za ulaya walikuja kwa kutumia meli aina ya Silver whisper.

  Alisema kuwa kutokana na ujio wa watalii hao kupitia meli imetuongezea motisha kama serikali,hivyo ujenzi wa terminal maalum utafanyika katika upanuzi wa unaoendelea kwenye cruise maalum ili kuepusha shughuli zingine za kushughulikia meli za cargo katika Bandari hiyo.

  "Watalii watakapo anza kuja kwa wingi kupitia bahari itasaidia taifa kujiongezea kipato kupitia idara hiyo" alisema Nzuki.

  Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi ya utalii (TTB) Jaji Thomas Mihayo alisema kuwa bodi hiyo itahakikisha inajadiliana na mamlaka husika ili kuona jinsi gani wanaweza wakatoa viza za muda mrefu kwa watalii ambao watakao penda kukaa nchini zaidi ya mwezi.

  Aidha aliongeza kuwa watanzania wanatakiwa kuongeza ukalimu kwa wageni wetu wanaofika nchini kwa lengo la utalii ili taifa liweze kujiongezea kipato kupitia nyanja ya utalii.
  Watalii zaidi ya 350 kutoka nchi za ulaya walikuja kwa kutumia meli aina ya Silver whisper wakishuka na kuelekea mbalimbali ya utalii leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)
  Muonekano wa meli ya Silver whisper.
  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk. Aloyce Nzuki, aikizungumza na waandishi wa habari alipokuwa akipokea watalii zaidi ya 350 kutoka nchi za ulaya walikuja kwa kutumia meli aina ya Silver whisper leo jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania, Bi. Devota Mdachi akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari leo alipo kuwa akipokea watalii zaidi ya 350 kutoka nchi za ulaya walikuja kwa kutumia meli aina ya Silver whisper leo jijini Dar es Salaam.
  Viongozi mbalimbali wakiwa katika bandari ya Dar esSalaam wakijadili mambo mbalimbali leo wakati wa kuwapokea watalii zaidi ya 350 kutoka nchi za ulaya walikuja kwa kutumia meli aina ya Silver whisper leo.

  0 0

  Na Woinde Shizza Globu ya jamii

  msaada wa mabati 50 yenye thamani ya shilingi milioni 1.5 kwa shule ya
  msingi ya Mkonoo ,ambayo iliezuliwa Marchi 30 mwaka huu kutokana na
  mvua iliyoambatana na upepo.

  Akikabidhi msaada huo jana kwa mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel
  Dacqaro, Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni mornaban Dk Philemon Mollel,
  aliesema akiwa ni mdau wa elimu ameguswa sana na tukio hilo la
  kuezuliwa kwa paa la shule na hivyo ametoa mabati hayo ili kuharakisha
  kuezekwa kwa vyumba vya madarasa na kuwezesha wanafunzi kuendelea na
  masomo yao.

  Amesema mara baada ya kupata taarifa hiyo amejitoa kuchangia mabati
  hayo geji 28 kutokana na kutambua umuhimu wa elimu kwa wanafunzi hivyo msaada huo utawezesha madarasa hayo matatu kuezekwa kwa haraka.

  Akipokea msaada huo mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqaro,
  amempongeza mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo, Dakta Phileoni
  Mollel, kwa moyo wake huo wa kujali wanafunzi .

  Amesema serikali kwa upande wake itaendelera kushirikisha wadau
  wengine wa maendeleo kutoa misaada ya vifaa vya jenzi ili kuwezesha
  wanafunzi wanasoma kwenye mazingira mazuri na salama..

  Aidha amesema katika tukio hilo pia shule ya sekondari Mkoo nayo
  imeathiriwa na mvua hiyo na kuezuliwa paa kwenye chumba kimoja cha
  maabara na baadhi ya nyumba zilizopo jirani na shule hiyo..Ameongeza kwamba licha ya msaada huo bado shule hizo zote mbili zina
  uhitaji wa bati 90 za geji 28 .

  Akipokea msaada huo kutoka kwa mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel
  Daqaro, mwalimu wa vifaa wa shule hiyo ya msingi Mkonoo,
  mwalimu,Ndeningwalanga Kaaya, amesema shule hiyo ya msingi ina jumla
  ya wanafunzi 990 kuanzia darasa la kwanza hadi la saba .

  Ameongeza kuwa kutokana na tukio hilo wanafunzi wa darasa la saba
  ambao wapo kwenye mikondo miwili wanalazimika kusomea chumba kimoja.
  Mkuu wa wilaya ya Arusha GabrielDaqaro, akipokea msaada wa mabati hayo kutoka kwa Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni mornaban Dk Philemon Mollel
   Mkuu wa wilaya ya Arusha GabrielDaqaro, akipokea msaada wa mabati hayo kutoka kwa Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni mornaban Dk Philemon Mollel


  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Kigamboni, Sara Msafiri ameagiza kumuweka ndani mkandarasi  anayejenga ukuta wa eneo la Kampuni ya Afroil iliyopo Vijibweni jijini Dar es salaam baada ya kukaidi agizo alilotoa jana la kusitisha ujenzi wa ukuta huo mpaka pale atakapojiridhisha kwani eneo hilo ni la barabara.
  Mhandisi wa Umeme wa kampuni ya Mihani,Kelvn Lubagula  wa (kwanza kulia)akimwelezea Mkuu wa wilaya ya Kigamboni,Sara Msafiri (wapili kulia) mtambo kusafirisha gesi kwenda kwnye matenki mbalimbali  unavyo fanya kazi leo katika ziara ya kukagua vituo vya kuhifadhi gesi leo jijini Dar es Salaam. 
   Mkuu wa wilaya ya Kigamboni,Sara Msafiri akiwa ameongozana na kamati ya ulinzi ya wilaya hiyo wakikagua mitambo mbalimbali ya kampuni ya gesi ya Mihani ya  katika ziara ya kukagua vituo vyakuhifadhi gesi leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)

  Mkandarasi  anayejenga ukuta wa eneo la Kampuni ya Afroil iliyopo Vijibweni jijini Dar es salaam akiwa chini ya ulinzi badaada ya Mkuu wa wilaya ya Kigamboni,Sara Msafiri kugiza kumuweka nanda msaa 12. kwakosa la kukaidi agizo alilotoa jana la kusitisha ujenzi wa ukuta huo mpaka pale atakapojiridhisha.Mafundi wakiendelea na ujenzi  katika eneo  la Kampuni ya Afroil iliyopo Vijibweni jijini Dar es salaam alilotoa jana la kusitisha ujenzi wa ukuta huo mpaka pale atakapojiridhisha.

  0 0

  Serikali imeonya kuwa haitakuwa na msalie mtume na mtu,chama cha siasa ama kikundi chochote kitakachojihusisha na rushwa kabla,wakati na baada ya uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka huu 2019 pamoja na Uchaguzi mkuu wa 2020.

  Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi wakati akifungua mkutano wa kujadili namna ya kudhibiti rushwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 jijini Dar es Salaam, na kuongeza kuwa Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli inataka wananchi watambue kuwa serikali yao imedhamiria kupambana na rushwa katika nyakati zake zote na sura zake zote.

  “Sote tunafahamu mwaka 2019 tutakuwa na Uchaguzi katika ngazi za Serikali za Mitaa hivyo basi,chaguzi hizi zinapaswa kuendeshwa na kusimamiwa kwa uadilifu na umakini mkubwa kwa kuzingatia sheria,kanuni na taratibu ili haki,usawa,uhuru na demokrasia viweze kustawi,kuendelezwa na kudumishwa hivyo Takukuru kamwe isiwe na Msalie Mtume kwa yeyote atakayejihusisha na masuala ya rushwa”

  Profesa Palamagamba John Kabudi ameongeza kuwa rushwa katika uchaguzi ni zaidi ya udanganyifu wa hesabu za kura,kwakuwa una madhara kadha wa kadha ikiwemo viongozi kukosa uwajibikaji,kukosa viongozi waadilifu,kukosa viongozi wazalendo,uwepo wa vitendo vya uvunjifu wa Amani kutokana na migogoro ya mara kwa mara ya kisiasa,uchumi wa Taifa kudidimia kwa kukosa mipango ya maendeleo na viongozi kufanya maamuzi ya kisera yenye maslahi kwa wachache.

  Aidha,amewapongeza TAKUKURU kwa kuandaa Warsha hiyo katika wakati muafaka na kusisitiza,pamoja na sheria na kanuni zilizopo bado kuna wajibu mkubwa wa kuhakikisha jamii inashirikishwa na kuelimishwa kuhusu madhara ya rushwa katika Uchaguzi.

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini TAKUKURU Kamishna wa Polisi Diwani Athumani amesema rushwa katika Uchaguzi ni hatari na inaweza kuleta madhara kwa Taifa kwani viongozi wala rushwa au watoa rushwa hawataweza kuisimamia nchi kwa misingi ya haki,usawa,uwazi,uwajibikaji na uzalendo na vilevile wananchi wapokea au watoa rushwa hawawezi kuhoji masuala mbalimbali kwa viongozi wao.

  Amewataka wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha na kutoa taarifa bila woga kwa wale wote watakaojihusiha na masuala ya utoaji ama upokeaji rushwa ili sheria ziweze kufuata mkondo wake na baadae kuwa na Taifa lenye usawa katika nyanja zote.

  Warsha hiyo ya wadau kujadili namna ya kudhibiti rushwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa imehudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wadini,vyama vya siasa,vyama vya kiraia na vyombo vya ulinzi na usalama.


  0 0

  Na. Andrew Chimesela - Morogoro
  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe amerudia kauli yake aliyoitoa Februari 11 mwaka huu alipoongea na wajumbe wa Kamati Tendaji ya chama cha madini Mkoa wa Morogoro– MOREMA  ya kutaka Maeneo ya uchimbaji wa madini ambayo hayaendelezwi, leseni husika zifutwe na maeneo hayo kupatiwa wachimbaji wadogo.
  Kauli hiyo ameirudia mwanzoni mwa wiki hii wakati akiufungua Mkutano wa Wadau wa Madini Mkoa wa Morogoro uliofanyika Ukumbi wa Chuo cha Ualimu Kigurunyembe katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro ambao unalenga kuboresha Sekta ya madini Mkoani humo ili kufikia malengo ya Serikali ya awamu ya tano ya kuwaletea wananchi maendeleo.
  Dkt. Kebwe amesema hakuna maana ya wachimbaji hao kuwa na maeneo makubwa lakini hawayafanyii kazi huku akiongeza kuwa fedha wanazolipa wachimbaji kwa mwaka katika maeneo yao ni kidogo ukilinganisha na fedha ambazo wangelipa wachimbaji wadogo endepo wangepewa maeneo hayo.
  “Mimi Mkuu wa Mkoa napendekeza  wanyang’anwe kwa sababu kwa upande wa utaratibu wa kisheria kwanza hawajaendeleza kwa hiyo utakuwa hujakosea, wanyang’anywe wapewe wachimbaji wadogo” alisema Dkt. Kebwe
  Sambamba na hilo amemuagiza Afisa Madini Mkoa wa Morogoro kushirikiana na Katibu Tawala wa Mkoa huo Clifford Tandari kuratibu zoezi la kufungua masoko ya madini kabla au ifikapo Mei 30 mwaka huu ili wachimbaji wasipate changamoto ya mahali pa kuuzia madini yao lakini pia Serikali kufaidika na madini hayo na kudhibiti utoroshwaji.
  Aidha, Dkt. Kebwe ametumia fursa hiyo kuagiza chama cha Madini Mkoa wa Morogoro, Morogoro Region Mining Association – MOREMA kusajili wachimbaji wote wa madini waliopo Mkoani humo ili wafahamike huku akitaka MOREMA kusimamia sheria hususan utoroshwaji wa madini na kutofanya kazi hiyo kwa kificho na wale watakaokwenda kinyume na sheria wachukuliwe hatua za kisheria.

  Naye Rais wa Shirikisho la vyama vya Wachimbaji madini Tanzania (FEMATA) Bw. John Bina, pamoja na kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kufuta utitiri wa kodi ambazo zilikuwa kero kwa wachimbaji madini amewataka wachimba hao kulipa kodi kwa Serikali  kama walivyomwahidi  Rais kwenye kikao chao cha mwezi Januari mwaka huu.

  Sambamba  na maagizo hayo, Bw. Bina ametumia fursa hiyo kulaani vitendo vilivyotokea katika Mikoa ya Mbeya na Shinyanga ambapo baadhi ya wachimbaji wametorosha madini hivyo kwenda kinyume na ahadi waliyoitoa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.       “kwa niaba ya wachimbaji wote napenda kulaani wale ambao jana katika Mkoa wa Mbeya na Kahama waliohusika kwenye wizi wa dhahabu … wale tunasema sisi sio wenzetu” alisisitiza John Bina.

  Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa FEMATA Kamishna Haroun Kinega amesema Serikali imesikia kilio cha wachimbaji wadogo wa madini cha uwepo wa maeneo makubwa kuhodhiwa kwa muda mrefu bila kufanyiwa kazi, tayari Tume ya madini inaendelea kufuta leseni za maeneo hayo na kutoa kwa wachimbaji wadogo.

  Akihitimisha kikao hicho Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Clifford Tandari aliwataka wachimbaji wadogo kufanya kazi zao kwa kushirikiana badala ya kufanya kazi hizo kwa mashindano kwa kuwa mara zote Umoja ni nguvu.

  kikao hicho cha wadau wa madini kilimalizika kwa wadau kujiwekea maazimio 17 ikiwa ni pamoja na Maeneo ambayo hayaendelezwi, leseni husika zifutwe na kupatiwa wachimbaji wadogo, Serikali kutoa bei elekezi ya madini yote ili kuwawezesha wachimbaji kupata faida na wachimbaji watambulike kwenye taasisi za kibenki ili kupatiwa mikopo.

  Maazimio mengine ni pamoja na Serikali kuombwa kuazisha benki za kuwakopesha wachimbaji wadogo wa madini kama ilivyo kwa wakulima na wanawake, Elimu ya sheria ya madini itolewe katika ngazi za Mkoa, wilaya, kata na vijiji ili kupunguza vikwazo katika shughuli za uchimbaji na MOREMA kutakiwa kushirikiana na viongozi wa serikali kutatua migogoro inayohusu Sekta ya madini.
  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa Madini mara baada ya kufungua Mkutano wa Wadau wa Uchimbaji katika Mkoa wa Morogoro. Wa tatu kutoka kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro Clifford Tandari na Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Madini hapa nchini Bw. John Bina. Na kutoka watatu kutoka kushoto ni Mtendaji Mkuu wa FEMATA Kamishna Haroun Kinega na Mhe. Regina Chonjo Mkuu wa Wilaya ya Morogoro.

  0 0

  Na Karama Kenyunko, globu ya janii.

  WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amempa muda wa mwezi mmoja Kamishna wa Idara ya Uhamiaji nchini, Dk. Anna Makakala, kuhakikishia kuwa anamkabidhi orodha ya mapapa wa biashara ya kuingiza na kusafirisha wahamiaji haramu nchini.

  Waziri Lugola ametoa maagizo hayo leo Aprili 4, 2019 jijini Dar es Salaam alipokuwa akifungua mkutano wa ngazi ya juu uliohusisha nchi za Kenya, Ethiopia na Tanzania kwa ajili ya kutafuta namna ya kupata ufumbuzi juu ya tatizo la wahamijia Haramu (EU-IOM).

  Mkutano huo wa siku mbili unalengo la kutafuta mwarobaini wa tatizo la wahamiaji.Lugola amesema, wahamiaji haramu wasingeweza kufanikiwa kuingia nchini kwa njia yoyote kama miongoni mwa watanzania hawatawasaidia, hivyo amewaasa waache kabisa kiwapokea na kuwasaidia kwa namna yoyote ile iwe kwa kuwapa chakula kuwasafirisha au kuwahifadhi katika jengo lolote ambapo hilo likifanyika, tatizo lotakwisha.

  Aidha amemtaka, kamishna Generali, sasa akae na timu yake ili walifanyie kazi hili tatizo ili ndani ya mwezi mmoja aje na orodha ya madalali wanaosaidia wahamiaji haramu hata kama wako nje ya nchi wanasakwa na kukamatwa ili kuvunja mtandao.

  "Tunataka hao madalali wenyewe kabisa wasakwe na wakamatwe maana tunaishia kukamata dereva wa fuso ambae amewapakia hao wahamiaji na tunawaacha wahusika wenyewe wakitembea angalau basi kwa uchache uje na orodha ya hawa madalali, wawili watatu hata kama tunaambiwa wako nchi nyinginie za jirani na ni wenzetu tuweze kutumia sheria tulizonazo za kuwakamata na kuwaleta tuhakikishe kwamba mtandao huu tunaumaliza" amesema Lugola

  Aidha amesema katika kupamba na tatizo la wahamiaji Haramu wamependekeza kuwa, wahamiaji haramu sasa wasiwe wanapelekwa mahakamani na kufungwa magerezani, badala yake wakikamatwa kuwe na njia mbadala, ya kuwarudisha kwao baada siku chache. Ambapo shirika la kimataifa la Uhamiaji limeahidi kuwa linatoa garama za kuwaaafirisha.

  Kwa upande wake, Kamishna Generali wa Uhamiaji, Dk. Anna Makakala, amesema, mkutano huo unalengo la kusaka suluhu juu ya changamoto hiyo ya wahamiaji haramu kwenye nchi hizo tatu kwa kushirikiana na mashirika ya kimataifa.

  Amesema, changamoto ni kubwa na inahitajika kupata suluhu ya kudumu, ndiyo maana tumekutana hapa kwa kushirikiana na wenzetu wa wa nchi hizi tatu ili tuweze kupata ufumbuzi wa kudumu jambo ambalo tunaamini kuwa tutafanikiwa," amesema Dk. Makakala.

  Naye, Balozi wa Wizara ya mambo ya Nje Kenya, Michael Oyugi amesema, nchi yake imeongeza idadi ya maafisa usalama wa Uhamiaji mipakani Ili wahamiaji haramu wanaoingia Kenya na kukimbia nchi zingine wanamalizika kabisa. 

  Amesema, Mipaka kati ya nchi ya Kenya name Ethiopia ni mirefu sana, ni kama mita 700 hivyo siyo rahisi kuweka maafisa usalama wa Uhamiaji katika mipaka hiyo yote hivyo Wengi wa hawa wahamiaji haramu hupita njia zisizohalali 'njia za panya' ambazo hazina maafisa wa Uhamiaji hivyo ni ngumu sana kuwakamata. 

  Amesema, makubaliano hayo yote yatasaidia sana kupunguza wahamiaji haramu, lakini inatupasa kwenda taratibu kwani jambo hili ni ngumu na hatuwezi kulisuluhisha Mara moja.

  "Tumeishakuwa na mikutano Kadhaa, ambayo inashughulikia namna ya kutatua tatizo hili pole pole na sasa tunatafuta njia ya kumaliza tatizo hili na haya makibaliano ambayo tunatoka nayo hapa tunayachukua na kwenda kuyafanyia kazi.
  Waziri wa Mbamo ya Ndani nchini,Kangi Lugola akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaa ambapo alimuagiza Kamishna Mkuu wa Uhamiaji kuhakikisha ndani ya mwezi mmoja anakuwa na orodha ya majina ya madalali wanouhusika kuwaingiza wahamiaji haramu nchini (Picha na Emmanuel Massaka,MMG)
  Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dk. Anna P. Makakala (kulia) akizungumz na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,mara baada ya kufunguliwa mkutano wa ngazi ya juu uliohusisha nchi za Kenya, Ethiopia na Tanzania kwa ajili ya kutafuta namna ya kupata ufumbuzi kuhusu tatizo la wahamijia Haramu (EU-IOM).
  Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dk. Anna P. Makakala (wapili kushoto) akiwa pamoja na vingonzi wa nchi mbalimbali wakisani hati za makubaliano ya uliohusisha nchi za Kenya, Ethiopia na Tanzania kwa ajili ya kutafuta namna ya kupata ufumbuzi kuhusu tatizo la wahamijia Haramu (EU-IOM).
  Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dk. Anna P. Makakala katikati akibadilisha hati zilizohusisha nchi za Kenya, Ethiopia na Tanzania kwa ajili ya kutafuta namna ya kupata ufumbuzi kuhusu kukomesha tatizo la wahamijia Haramu (EU-IOM).
  Picha ya pamoja

  0 0

  *Ni katika kufanikisha ujenzi wa shule ya sekondari ya wasichana Kisarawe ...
  Kauli ya DC Jocate yawakuna wananchi eneo ambalo shule inajengwa


  Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

  MKUU wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani Jokate Mwegelo, ameeleza kuwa harambee ya kuchangia ujenzi wa shule ya sekondari ya wasichana wilayani humo imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwani hadi sasa wamefanikiwa kukusanya Sh.milioni 915 kati ya Sh.Bilioni 1.3 ambazo zinahitajika kufanikisha ujenzi huo.

  Uchangiaji wa shule hiyo ya sekondari ambayo itajengwa katika Kata ya Kibuta ,ni muendelezo wa kampeni ya tokomeza ziro wilayani Kisarawe iliyoanzishwa na Jocate kwa kushirikiana na viongozi wengine.

  Akizungumza jana na waandishi wa habari Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mwegelo amesema baada ya kuzindua harambee ya kuchangisha fedha za ujenzi huo wameamua leo kutoa mrejesho kwa Watanzania wa nini ambacho kimepatikana.

  ",Tumefanikiwa kukusanya Sh. milioni 915 kati ya Sh. bilioni 1.3 tulizolenga kukusanya.Fedha taslimu ambazo zimeshawekwa benki hadi jana ni Sh. milioni 80 na bado tumeendelea kupokea ahadi za wadau mbalimbali wanaotaka kuchagia.

  " Mbali na michango ya fedha tuliyopokea, Chama cha Wahandisi Wanawake, wamejitokeza kutoa ushauri wa namna ya kujenga mabweni hayo.Pia amesema wapo wadau waliochangia mabweni mawili yanayochukua wanafunzi 80 kila moja na lengo ni kujenga mabweni sita,"amesema Jocate.

  Amesema anawashukuru wananchi wa Tanzania na wadau wa maendeleo waliojetokeza kuchangia kampeni hiyo ya kuwakomboa watoto wa kike kwa kuwawekea mazingira wezeshi ya kupata elimu, ingawa kwa siku za usoni watajenga na ya watoto wa kiume kwani kupanga ni kuchagua.

  “Kama mnavyojua Machi ulikuwa mwezi wa wanawake, Wilaya ya Kisarawe tukaona badala ya kuvaa sare na kusherehekea ni bora tuwe na kampeni itakayoinua wanawake wengi wa kesho ambao ni wanafunzi wa wilaya yetu wanaokabiliwa na changamoto mbalimbali zinazowafanya kushindwa kufikia malengo yao,"amesema.

  Pia amesema Kampuni ya Sao Hill wamejitolea kutoa mbao za kuezeka mabweni hayo zenye gharama ya Sh. milioni 10 na kutoa mafunzo ya ufundi wa kutengeneza samani kwa mgambo 40 wa wilaya hiyo.Ameitaja misaada mingine waliyopokea ni mifuko 1,890 ya saruji na tayari 1,050 imeshapokelewa ofisini kwake na kontena moja la marumaru.

  “Pamoja na kampeni hii iliyowezesha upatikanaji wa fedha pia kampeni hii imeenda sambamba na mafunzo ya walimu 220 ambao wafundishwa namna ya kutoa elimu inayoenda na karne ya 21 ya kuwawezesha wanafunzi wanaohitimu kujitegemea na kuwa viongozi wanaojitambua,” amesema Mkuu huyo wa Wilaya.

  Ameongeza kupitia kampeni ya kuwaweka wanafunzi kambini kwa ajili ya kujisomea wanapokaribia kufanya mitihani ya kidato cha nne, imesaidia kuongeza ufaulu daraja la kwanza kutoka wanafunzi saba hadi 37 na waliopata sifuri kupungua kutoka wanafunzi 257 hadi wanafunzi 175.

  Joketi pia ameeleza kuwa sababu ya kufanya kapeni hizo ni kupunguza idadi ya wanafunzi wanaoshindwa kufika kidato cha sita ambapo katika kipindi cha mwaka 2014 hadi 2017 jumla ya wanafunzi 4,880 walimaliza kidato cha nne lakini wanafunzi 66 ndio waliofika kidato cha sita.

  Wakati huo huo Jokate amepanda mti kwenye eneo ambalo ujenzi wa shule hiyo ya kisasa na ya mfano itajengwa huku akitumia nafasi hiyo kuwashukuru wananchi wa Kibuta kwa kukubali kufanyika kwa ujenzi huo ambapo wamekubali kutoa eneo bure.

  Amewaomba kuwa bado michango ya wananchi hao inahitajika hasa kwa kuzingatia wakati wa ujenzi kutachimbwa mitaro ,utachimbwa mchanga na maji na kwamba hayo yote yanahitaji nguvu kazi ya wananchi ili kufanikisha ujenzi.

  Amewaomba wananchi hao kuendelea kushirikiana na viongozi wa wilaya hiyo katika kufanikisha jambo hilo jema na lenye tija kwa Wana Kisarawe na Watanzania kwa ujumla.

  Pamoja na mambo mengine wananchi wilayani humo wamesema wamefurahishwa na namna ambavyo Mkuu wa Wilaya hiyo ambavyo amekuwa akishirikiana nao katika kufanya maendeleo ambapo wameahidi watatumia muda,nguvu na maarifa yao kufanikisha ujenzi wa shule hiyo unafanikiwa.


  Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo akipanda mti kwenye eneo ambalo ujenzi wa shule hiyo ya kisasa na ya mfano itajengwa huku akitumia nafasi hiyo kuwashukuru wananchi wa Kibuta kwa kukubali kufanyika kwa ujenzi huo ambapo wamekubali kutoa eneo bure.
  Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo akizungumza jambo mbele ya Waananchi na Wanafunzi kabla ya kupanda mti kwenye eneo ambalo ujenzi wa shule hiyo ya kisasa na ya mfano itajengwa huku akitumia nafasi hiyo kuwashukuru wananchi wa Kibuta kwa kukubali kufanyika kwa ujenzi huo ambapo wamekubali kutoa eneo bure.
  Mkuu wa Wilaya ya Kisarawa Jokate Mwegelo akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) jana ofisini kwake alipokuwa akieleza mafanikio makubwa yaliyopatikana kwenye kampeni ya kuhamasisha harambee ya kuchangia Tokomeza Zero Kisarawe ,Jakate akionekana mwenye bashasha na furaha muda wote alieleza kuwa kampeni hiyo ilifanikiwa kwa kiasi kikubwa kwani hadi sasa wamefanikiwa kukusanya kiasi cha Sh.milioni 915 kati ya Sh.Bilioni 1.3 ambazo zinahitajika kufanikisha ujenzi huo.Joketi alisema kuwa uchangiaji wa shule hiyo ya sekondari ambayo itajengwa katika Kata ya Kibuta ,ni muendelezo wa kampeni ya tokomeza ziro wilayani Kisarawe iliyoanzishwa na yeye mwenyewe kwa kushirikiana na viongozi wengine.
  Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Mh. Jokate Mwegelo akizungumza na waandishi wa habari jana alipokuwa akitoa mrejesho kwa Waandishi wa Habari Ofisini kwakwe Kisarawe,fedha na ahadi zilizopatikana wakati wa hafla ya kuchangia kampeni ya Tokomeza Zero Kisarawe iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam wiki iliyopita.
  Mkuu wa Wilaya ya Kisarawa Jokate Mwegelo akiwashukuru Waandishi wa habari pamoja na Watanzania kwa ujumla kwa kazi kubwa walioifanya wakati wa kuhamasisha harambee ya kuchangia kampeni ya Tokomeza Zero Kisarawe ,ambapo alieleza kuwa kampeni hiyo ilifanikiwa kwa kiasi kikubwa kwani hadi sasa wamefanikiwa kukusanya kiasi cha Sh.milioni 915 kati ya Sh.Bilioni 1.3 ambazo zinahitajika kufanikisha ujenzi huo.Joketi alisema kuwa uchangiaji wa shule hiyo ya sekondari ambayo itajengwa katika Kata ya Kibuta ,ni muendelezo wa kampeni ya tokomeza ziro wilayani Kisarawe iliyoanzishwa na yeye mwenyewe kwa kushirikiana na viongozi wengine.
  MKUU wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani Joketi Mwegelo, sambamba na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo wakitoa mrejesho wa harambee ya kuchangia ujenzi wa shule ya sekondari ya wasichana wilayani humo iliyojulikana kwa jina la Tokomeza Zero Kisarawe,iliyofanyika wiki iliopita ndani ya Mlimani City,Kinondoni jijini Dar na kuhudhuriwa na watu mbalimbali

  Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Mkoa wa Pwani,Mh. Jokate Mwegelo akitoa ufafanuzi mbele ya waandishi wa habari jana alipokutana na jana wakati akitoa mrejesho wa fedha na ahadi zilizopatikana kwenye hafla ya kuchangia kampeni ya Tokomeza Zero Kisarawe iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam wiki iliyopita.
  Pichani kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri Kisarawe,Musa Gama akieleza namna fedha hizo zilizopataikana katika harambee hiyo,zitakavyosaidia kutokomeza zero wilayani hummo, amesema shule itakayojengwa itakuwa na kidato cha kwanza hadi cha sita,na kwamba itakuwa ya mfano na itasaidia kuongeza ufaulu wa Wanafanzi kwa kiwango kikubwa. ''Jambo tunaloenda kulifanya ni shirikishi ndio maana tunaungwa mkono na wadau mbalimbali ikiwemo wananchi waliojitolea ardhi kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo ili kuongeza kiwango cha ufaulu”alisema Gama huku DC Jokate akimtazama kwa tabasamu zuri la mafanikio hayo.
  DC Jokate akimsikiliza kwa makini mmoja wa Waandishi kutoka Chanell Ten,Said Makalla (aliyenyoosha mikono kulia),alipoulizwa moja ya swali kuhusiana na mafanikio makubwa ya Harambee hiyo ya kutokomeza zero wilani humo.
  Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Mkoa wa Pwani,Mh. Jokate Mwegelo akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa Habari Ofisini kwake jana,wakati alipokuwa akitoa mrejesho kuhusu fedha na ahadi zilizopatikana wakati wa hafla ya kuchangia kampeni ya Tokomeza Zero Kisarawe iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam wiki iliyopita. Pichani kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri Kisarawe,Musa Gama


  Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Mh. Jokate Mwegelo akiwa amelinyanyua tofali la saruji na kulitupa chini kuhakiki ubora wake wakati akiwaonesha waandishi wa habari mradi huo ambao unaendeshwa na halmashauri hiyo kwa ajili ya ujenzi wa shule mbalimbali na miundombinu mingine katika wilaya hiyo.

  Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Mh. Jokate Mwegelo akionesha mradi wa matofali unaoendelea kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari ya bweni kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha sita na shule zingine.PICHA NA MICHUZI JR.

  0 0

  Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya imeendelea kuiunga mkono Serikali katika sera ya viwanda vya dawa kwa kutekeleza maelekezo ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuanzisha kiwanda cha kuzalisha maji tiba ‘Dripu’ za IV (Intravenous Fluids) kwa kutumia wataalamu wake wenye.

  Dripu hizo zenye ujazo wa mil’s 250 na Mil’s 500 zimeanza kutumika kwaajili ya kuhudumia wagonjwa wenye uhitaji hali inayosababisha kuondokana na adha ya kununua\kuagiza dripu nje ya nchi.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali Dkt Godlove Mbwanji amesema “Tunayo furaha kubwa kuanza uzalishaji wa maji tiba kwa ajili ya mahitaji ya hospitali yetu na kwa kufanya hivi, napenda kutoa shukrani nyingi kwa Serikali ya Awamu ya Tano kwa kutuunga mkono na kutusaidia. Uko mpango wa kuhakikisha tunazalisha maji tiba kwa kiwango kikubwa ili kutoa huduma hiyo kwa wengine ukanda wa Nyanda za Juu Kusini”.

  Amesema uanzishwaji wa kiwanda cha kutengeneza Maji Tiba (Dripu) umetekelezwa kwa kutumia mapato ya ndani na katika hatua inayofwata imeanza maandalizi ya mpango wa kutengeneza dawa ya macho.

  Hadi sasa Hospitali ya Rufaa ya kanda Mbeya imeendelea kutoa huduma za kibingwa kwa kutumia vipimo vya kisasa kama Endoscopy, Digital X-Ray, ECG Ultra sound, Echo-cardiogram na siku za karibuni huduma ya CT Scan, Digital Radiography na Digital Mammography zitaanza kutolewa.
   Baadhi ya maji tiba Drip yanayozalishwa na Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya
   Muonekano wa maji tiba Drip

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, Viongozi wa Mkoa wa Mtwara, wakati akikagua moja ya Wodi ya Wazazi katika  Kituo cha Afya cha Mbonde mara baada ya kukifungua Masasi mkoani Mtwara.
   Sehemu ya Wodi ya Wazazi katika  Kituo cha Afya cha Mbonde mara baada ya kufunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Masasi mkoani Mtwara.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, Viongozi wa Mkoa wa Mtwara, wakati akikagua chumba cha upasuaji katika wodi ya Wazazi katika  Kituo cha Afya cha Mbonde Masasi mkoani Mtwara.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, Viongozi wa Mkoa wa Mtwara akiangalia mashine ya kutoa dawa ya usingizi kkwa wagonjwa katika chumba cha upasuaji kwa wa mama wajawazito.
   Sehemu ya wakazi wa Masasi wakisikiliza hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati akihutubia mara baada ya kufungua kituo cha afya cha Mbonde.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungua mkono wananchi hawaonekani pichani wakati akiondoka eneo la kituo cha Afya cha Mbonde.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Kituo cha Afya cha Mbonde mara baada ya kukifungua.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mikangaula iliyopo Nanyumbu mkoani Mtwara wakati akielekea Mangaka kwenda kufungua barabara.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi wa Nanyumbu mara baada ya kuwasili kutoka Masasi kwa ajili ya kufungua barabara ya Tunduru-Mangaka-Mtambaswala yenye jumla ya km202.5.PICHA NA IKULU

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Masasi mara baada ya kufungua kituo cha Afya cha Mbonde kilichopo Masasi mkoani Mtwara.
  0 0

  * Miradi mipya ya kisekta yatarajiwa kuzalisha ajira mpya 15,491

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Tanzania inaongoza kwa uwekezaji katika Afrika Mashariki na imeweza kuvutia uwekezaji wenye thamani ya dola za Marekani bilioni 1.18, ikifuatiwa na Uganda dola za Marekani bilioni 0.7 na Kenya dola za Marekani bilioni 0.67.

  “Kutokana na hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali kuvutia uwekezaji nchini, hali ya uwekezaji imeimarika ikilinganishwa na nchi nyingine za Afrika Mashariki. Ripoti mbalimbali za uwekezaji duniani zinaonesha kuwa Tanzania imeongoza kwa kuvutia uwekezaji miongoni mwa nchi za Afrika Mashariki,” amesema.

  Ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Aprili 4, 2019) Bungeni jijini Dodoma, wakati akiwasilisha taarifa ya mapitio na mwelekeo wa kazi za Serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2019/2020 kwenye mkutano wa 15 wa Bunge.

  Amesema Taarifa ya Uwekezaji ya Dunia (World Investment Report) ya mwaka 2018 inayotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Biashara na Maendeleo (UNCTAD) imebainisha kiasi hicho kikubwa cha uwekezaji.

  “Taarifa nyingine ya“The Africa Investment Index (AII) 2018” inaonesha kuwa Tanzania imeshika nafasi ya 13 kati ya nchi 54 za Afrika katika kutoa fursa za masoko na vivutio vya uwekezaji.”

  Vilevile, Waziri Mkuu amesema kuwa taarifa ya “Where to Invest in Africa” ya mwaka 2018, nayo imeonesha kuwa Tanzania imeshika nafasi ya saba kati ya nchi 52 zinazovutia zaidi kwa uwekezaji barani Afrika.

  Kutokana na uwekezaji huo mkubwa, Waziri Mkuu amewataka Watanzania wachangamkie fursa zinazojitokeza kutokana na ukuaji wa uchumi, maendeleo ya kijamii na pia uwekezaji wa sekta ya umma kwenye miundombinu kwa kuthubutu kuwekeza kwenye uzalishaji wa bidhaa na utoaji wa huduma.

  Amesema katika mwaka wa fedha wa 2019/2020, Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara ikiwemo kutekeleza mapendekezo ya Mpango Kazi Jumuishi wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji nchini. Pia itakamilisha mapitio ya Sera ya Taifa ya Uwekezaji na Sheria ya Uwekezaji.

  Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema uhamasishaji wa miradi ya kisekta ndani na nje ya nchi, umefanikisha kuvutia uwekezaji kwenye sekta mbalimbali za kimkakati na unatarajia kuwekeza mitaji ya jumla ya dola za Marekani bilioni 1.84 na kuzalisha ajira mpya 15,491.

  “Hadi kufikia Februari, 2019 jumla ya miradi mipya 145 ilisajiliwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC). Kati ya miradi hiyo, miradi 104 sawa na asilimia 72 inamilikiwa na wawekezaji wa ndani; miradi 38 sawa na asilimia 26 inamilikiwa na wawekezaji kutoka nje na miradi mitatu sawa na asilimia 2.01 ni ya ubia,” amesema.

  Akizungumzia kuhusu zoezi la utoaji wa vitambulisho kwa wajasiriamali wadogo nchini, Waziri Mkuu amesema Serikali imekusanya shilingi bilioni 9.9 tangu kuanzishwa kwa utaratibu huo Desemba, 2018.

  “Hadi tarehe 10 Machi 2019, jumla ya vitambulisho 496,221 sawa na asilimia 74 vilikuwa vimegawiwa kwa wajasiriamali wadogo katika mikoa yote nchini.” Amesema hatua hiyo ilichukuliwa ikiwa ni kutambua umuhimu wa wajasiriamali wadogo nchini katika kuchangia pato la Taifa na kukuza uchumi

  “Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alitoa vitambulisho 670,000 kwa ajili ya wajasiriamali wadogo ambao mitaji yao haizidi shilingi milioni nne. Lengo la kutoa vitambulisho hivyo vyenye kugharimu shilingi 20,000 kwa kila kimoja ni kuwatambua, kuwaandalia maeneo ya kufanya biashara bila usumbufu wowote na kuziwezesha Mamlaka za Serikali za Mitaa kuongeza mapato ya ndani,” amesema.

  0 0

  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea taarifa ya utendaji ya Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kimataifa (CPA - INERNTIONAL) ya mwaka 2018 kutoka kwa Naibu Spika wa Bunge la Cameroon na Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya CPA,  Emilia Monjowa Lifaka, baada ya mazungumzo yao, ofisini kwa Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma Aprili 4, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Naibu Spika wa Bunge la Cameroon na Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kimatifa (CPA-INTERNATIONAL), Emilia Monjowa Lifaka, ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dodoma, Aprili 4, 2019. 
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Spika wa Bunge la Cameroon na Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kimatifa (CPA-INTERNATIONAL), Emilia Monjowa Lifaka (wa pili kushoto) baada ya mazungumzo yao, ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dodoma, Aprili 4, 2019. Wa tatu kulia ni Mbunge wa Babati Vijijni, Vrajilal Jitu Son na wa pili kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum na Mwakilishi wa CPA tawi la Tanzania, Maria Kangoye.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimwonyesha mandhari ya jiji la Dodoma, Naibu Spika wa Bunge la Cameroon na Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kimatifa (CPA-INTERNATIONAL), Emilia Monjowa Lifaka baada ya mazungumzo yao ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dodoma, Aprili 4, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
  SERIKALI ITAENDELEA KUSHIRIKIANA NA CPA-MAJALIWA


  WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema Serikali itatoa ushirikiano kwa Maspika wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika (CPA – Africa)

  wanaotarajia kufanya mkutano wao Novemba 2019, nchini Tanzania.

  Ametoa kauli hiyo jana (Alhamisi, Aprili 4, 2019) alipokutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya Chama cha Mabunge ya Madola Kanda ya Afrika, Mheshimiwa Emilia Monjolwa Lifaka.

  Waziri Mkuu alisema Bunge na Serikali nchini wanafanya kazi kwa kushirikiana, hivyo amemuhakikishia Mhe. Emilia ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge la Cameroon kuwa Serikali itatoa ushirikiano unaohitajika kwa CPA ili kufanikisha malengo tarajiwa

  Pia, Waziri Mkuu alisema Serikali inaushukuru uongozi wa CPA kwa kutoa ushirikiano stahiki kwa wabunge wa Bunge la Tanzania ambao ni wanachama wa CPA 

  Kwa upande wake, Mhe. Emilia aliipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuzingatia usawa wa kijinsia na kutoa fursa kwa wanawake katika nafasi za uongozi ikiwa ni pamoja na idadi kubwa ya wabunge wanawake kufikia asilimia zaidi ya 30 ya wabunge wote.

  Kadhalika, Mwenyekiti huyo alisema Maspika wa CPA – Afrikawanaotarajia kufanya mkutano Novemba 2019, katika jiji la Arusha nchini Tanzania wameridhika sana kwa ahadi ya Serikali ya Tanzania kuhusu ushirikiano na maandalizi mazuri.

  Mkutano huo wa Maspika wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika utajadili ajenda mbalimbali pamoja na kuimarisha ushirikiano uliopo kati ya nchi hizo kwa maslahi ya vizazi vya sasa na vijavyo.

  0 0

  Mkufunzi kutoka Mradi wa Boresha Habari ukiendeshwa chini ya uratibu wa mashirika yasiyo ya Kiserikali ya Internews na FHI 360 unaofadhiliwa na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID),Temigunga Mahondo wakati akitoa elimu kwa waandishi wa habari wa kituo cha redio Nuru Fm Iringa juu ya kusaidia kupaza sauti za wanyonge kupitia kalamu zao, hususani wale ambao wanaishi maeneo ya vijijini. 
  Mkufunzi kutoka Mradi wa Boresha Habari ukiendeshwa chini ya uratibu wa mashirika yasiyo ya Kiserikali ya Internews na FHI 360 unaofadhiliwa na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID),Temigunga Mahondo akiwaeleza waandishi wa habari wa kituo cha redio Nuru Fm Iringa juu ya kusaidia kupaza sauti za wanyonge kupitia kalamu zao, hususani wale ambao wanaishi maeneo ya vijijini. 
  Baadhi ya waandishi wa habari wa kituo cha redio Nuru Fm Iringa wakimsikiliza mkufunzi kutoka Mradi wa Boresha Habari ukiendeshwa chini ya uratibu wa mashirika yasiyo ya Kiserikali ya Internews na FHI 360 unaofadhiliwa na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID),Temigunga Mahondo wakati akitoa elimu kwa juu ya kusaidia kupaza sauti za wanyonge kupitia kalamu zao, hususani wale ambao wanaishi maeneo ya vijijini. 
  NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

  Waandishi wa habari wa kituo cha redio Nuru fm 93.5 mkoani Iringa wametakiwa kujikita kuandika habari za uchunguzi kwa kuibua matatizo ndani ya jamii, ambayo yamekuwa yakifichika na kutopaziwa sauti, jambo ambalo litawasaidia wananchi kutatulia kero ambazo zimekuwa zikiwakabili sababu ya kukosa sehemu pa kuzisemea.

  Hayo yamebainishwa na mkufunzi kutoka Mradi wa Boresha Habari ukiendeshwa chini ya uratibu wa mashirika yasiyo ya Kiserikali ya Internews na FHI 360 unaofadhiliwa na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID),Temigunga Mahondo wakati akitoa elimu kwa waandishi wa habari wa kituo cha redio Nuru Fm Iringa juu ya kusaidia kupaza sauti za wanyonge kupitia kalamu zao, hususani wale ambao wanaishi maeneo ya vijijini. 

  Alisema waandishi wa habari wanamsaada mkubwa sana ndani ya jamii kwa kupaza sauti za wanyonge kupitia kalamu zao, kwa kuibua matatizo ambayo yamekuwa yakiwakabili wananchi, na hasa kwa kuandika habari za uchunguzi ili jamii ipate kutatuliwa kero zao.

  “Naombeni waandishi wa habari mjikite zaidi kuandika habari za uchunguzi kwa kuibua matatizo ambayo yamekuwa yakijificha ndani ya jamii, hususani kwa wale wananchi wanaoishi maeneo ya vijijini, ambao wamekuwa wakikosa wa kuwapazia sauti na kuendelea kuishi maisha ya shida,”Alisema Mahondo

  Mahondo alisema kuwa waandishi wa habari mkijikita kwenye habari hizi mtakuwa mnaisaidia jamii ya wananchi wale wale wanyonge kwa kuwa tayari mtakuwa ninyi ndio sauti yao kwa kipindi chote ambacho mtakuwa mnaandika habari hiz.

  “Kuandika habari hizi zinanafasisi kubwa wa kuzifanya kwa kuangalia changamoto na manufaa katika sekta ya Afya,sekta elimu,sekta ya miundombi,sekta ya kilimo na mazingira na utapata uwanda mpana sana wa kufanya habari zenye tija kwa jamii” alisema Mahondo 

  Aidha Mahondo alisema,licha ya jamii kuhitaji kupata habari za kiburudani ambazo zimekuwa zikiwaburudisha kwa muda mfupi tu lakini kubwa zile habari ambazo zinasaidia kutatua changamoto za wananchi ndio zinatija hasa kwenye jamii kwa kufanikisha kutatua matatizo yao.

  “Hakuna wananchi ambaye hapendi kupata burudani hivyo tunaangalia aina gani ya burudani ambayo inawapa zaidi furaha jamii kwa kipindi kirefu ambayo itawasaidia kufanya shughuli za kimaendeleo ambazo zitawaletea faida wananchi” alisema Mahondo

  Naye mwaandishi wa habari na mtangazaji wa kipindi cha Sunrise Power cha Nuru fm Godfrey Mengele aliwatupia lawama wananchi hususani wa maeneo ya vijijini, ambapo wamekuwa waoga kutoa ushirikiano kwa waandishi wa habari kwa kushindwa kuzungumza matatizo yanayowakabili.

  alisema kuwa waandishi wa habari hawezi kuchunguza habari bila ya kupewa taarifa (Tipu) juu ya tatizo linalo wakabili wananchi, pamoja na kutozungumza na wahusika waliofanyiwa matukio hayo ya ukatili ama ndugu, ambapo wananchi hao hua hawapo tayari kuzungumza na kuwakimbia waandishi.

  Mengele aliwataka wananchi kuachana na tabia za uoga pale wanapotaka kusemewa matatizo yanayo wakabili kupitia vyombo vya habari, bali wawe karibu na media ambazo ndio msaada mkubwa kwao.

  “Wananchi wamekuwa waoga sana kutupa habari ambazo zinawagusa wao kwa kuhofia kufikishwa polisi,kwenye ofisi za serikali za mitaa hata mahakamani kutoa ushaidi ndio maana waandishi tunapata wakati mgumu pia kuandika habari hizi” alisema Mengele

  Lakini alitoa rai kwa waandishi wa habari kujikita kuandika habari za kichunguzi ambazo ndio zimekuwa zikiibua matatizo ya wananchi na kutafutia ufumbuzi wa kutatua changamoto zao.Kwa upande wake mtangazaji wa kipindi Street Bamiza Roger Magoha alisema mafunzo aliyopata yatamsaidia kukuza vipaji halisi vya wasanii wanaopenda kutoa burudani na kujua aina gani ya burudani wasikilizaji wanapenda kusikiliza.

  “Sasa nitafanya uchunguzi kujua wasikilizaji wangu wanapenda aina gani ya burudani kwa kuwa nimeshapata mbinu za kufanya uchuzi huo kutoka kwa mkufunzi wa Mradi wa Boresha Habari ukiendeshwa chini ya uratibu wa mashirika yasiyo ya Kiserikali ya Internews na FHI 360 unaofadhiliwa na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID),Temigunga Mahondo” alisema Magoha

  Magoha aliongeza kwa kusema kuwa amejifunza kufanya mahojiano bora na wasanii mbalimbali pamoja na viongozi hivyo mafunzo hayo yamemwogezea kitu kipya kichwani mwake ambacho hapo awali hakuwa nacho.

  Tarehe 17 Januari 2018, Serikali ya Marekani kwa kupitia Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID), ilizindua mradi wa kuimarisha asasi za kiraia na vyombo vya habari uitwao Boresha Habari Katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam, mradi huo ukiendeshwa chini ya uratibu wa mashirika yasiyo ya Kiserikali ya Internews na FHI 360, mradi wa Boresha Habari utashirikiana na wabia wa Kitanzania, ikiwa ni pamoja na: Baraza la Habari Tanzania, Tanzania Bora Initiative, na Jamii Media; ili kuboresha weledi miongoni mwa waandishi wa habari na kusaidia kuweka mazingira yaliyo wazi kwa vyombo vya habari. 

  “Serikali ya Marekani imedhamiria kwa dhati kusaidia kuinua ujuzi na weledi wa vyombo vya habari na asasi zisizo za kiserikali za Kitanzania hususan katika kuwawezesha wanawake na vijana kupaza sauti zao na kueleza dukuduku zao kwa ufanisi,” 

  Katika kipindi cha miaka mitano ijayo, mradi wa Boresha Habari unalenga kufanya kazi na wadau wa vyombo vya habari katika mikoa ya Dar es Salaam, Zanzibar, Iringa, Mbeya, Morogoro, Arusha, Manyara, Dodoma, Tanga, Mtwara, Mwanza na Kigoma. 

  Aidha, mradi wa Boresha Habari utatoa mafunzo na msaada wa kitaalamu kwa vyombo vya habari vya humu nchini ukivisaidia kuanza kutumia teknolojia za kidijitali na kuimarisha uwezo wao wa kiusimamizi na kifedha. 

  Hali kadhalika, mradi huu utatoa mafunzo kwa asasi za kiraia ili ziweze kushirikiana vyema na vyombo vya habari katika kusukuma mbele jitihada zao. Kwa kuzingatia umuhimu wa redio za jamii kama vyanzo maarufu vya habari za maeneo husika, mradi wa Boresha Habari utafanya kazi na vituo mbalimbali vya redio nchini kote ili kuboresha uwezo wao wa kitaalamu na uendelevu katika masuala ya kifedha.

  Kwa taarifa zaidi, tafadhali wasiliana na Ofisi ya Habari ya Ubalozi wa Marekani Dar es Salaam kwa simu namba: +255 22 229-4000 au kwa barua pepe: DPO@state.gov.

older | 1 | .... | 1831 | 1832 | (Page 1833) | 1834 | 1835 | .... | 1904 | newer