Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1824 | 1825 | (Page 1826) | 1827 | 1828 | .... | 1896 | newer

  0 0

  Mkuu wa Mkoa Iringa Ally Hapi akimsikiliza Mkuu wa Wilaya Mh Richard Kasesela. Ziara ya mkuu wa mkoa akishirikiana kwa karibu na Mkuu Wa Wilaya Iringa Mh Richard Kasesela wameendelea kutatua kero za wananchi ikiwemo migogoro ya ardhi. Ziara hizi zimekuwa na mafanikio makubwa Kwa wanainchi, pia imekuwa ikileta changamoto Kwa watumishi wa serikali ambao hawawatendei haki wanainchi. 
  Mkuu wa MKoa wa Iringa Ally Hapi akizungumza mbele ya Wananchi wakati wa ziara yake ya kusikiliza na kutatua kero za Wananchi ikiwemo migogoro ya Ardhi,Pichani kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela.
  Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela akimsikiliza mmoja wa Wananchi alipokuwa akiwasilisha kero yake kwa Mkuu wa Mkoa Mh Ally Hapi
  Ziara ya mkuu wa mkoa akishirikiana kwa karibu na Mkuu Wa Wilaya Iringa Mh Richard Kasesela wameendelea kutatua kero za wananchi ikiwemo migogoro ya ardhi. Ziara hizi zimekuwa na mafanikio makubwa Kwa wanainchi, pia imekuwa ikileta changamoto Kwa watumishi wa serikali ambao hawawatendei haki wanainchi

  0 0

  SERIKALI imeendelea kuboresha huduma za matibabu ya kifua Kikuu kwa kuongeza vituo vya kutolea huduma za matibabu sambamba na kuongeza vifaa tiba, ikiwa ni jitihada za Serikali kutokomeza ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB) nchini.

  Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu leo wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za kifua Kikuu na kutoa tamko kuhusiana na ugonjwa huo katika Hospitali ya Mbagala Jijini Dar es salaam.

  "Huduma za matibabu ya Kifua Kikuu (TB) sugu zimesogezwa karibu kwa wananchi, ambapo kwa sasa tunazo hospitali 93 za kutibu Kifua Kikuu sugu ikilinganishwa na mwaka 2015 ambapo, huduma za matibabu zilikuwa zinapatikana katika Hospitali ya Kibong'oto pekee " amesema Waziri Ummy.

  Pia, Waziri Ummy amesema katika kila Watanzania 100,000 Watanzania 269 wanahisiwa kuwa na ugonjwa wa Kifua Kikuu, huku watu 70 wanafariki kila siku kutokana ugonjwa wa Kifua Kikuu ambapo ni sawa na watu watatu hufariki kila saa.

  "watu 70 kila siku kutokana na ugonjwa wa Kifua Kikuu, kwahiyo kila saa ni sawa na watu watatu wanafariki kutokana na ugonjwa wa Kifua Kikuu ambao unatibika " alisema Waziri Ummy.

  Waziri Ummy amesema takribani wagonjwa 154,000 wanaokadiriwa kuugua ugonjwa wa Kifua Kikuu wanapaswa kufikiwa na kuingizwa katika mpango wa matibabu kila mwaka ili kuutokomeza ugonjwa huu nchini.

  Waziri Ummy ameendelea kusema kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi 30 Duniani zenye kiwango kikubwa cha wagonjwa wa Kifua Kikuu, inakadiriwa kuwa wapo wagonjwa takribani 154,000 ambao huugua ugonjwa wa kifua Kikuu kila mwaka.

  Aidha, Waziri Ummy amesema kuwa Mgonjwa wa Kifua Kikuu ambae hajaanza matibabu anaweza kuambkiza Kati ya watu kumi hadi watu 20 kwa mwaka, hivyo jitihada za makusudi zinatakiwa kuendelea kuchukuliwa ili kutokomeza ugonjwa huu nchini.

  "ifahamike kuwa mgonjwa wa kifua Kikuu ambae hajaanza matibabu anaweza kuambukiza kati ya watu kumi hadi watu ishirini kwa mwaka, hivyo tunalojukumu kubwa lakuhakikisha tunawafikia wote wanaougua ili tuweze kuzuia maambukizi mapya ya Kifua Kikuu" alisema Waziri Ummy

  Mbali na hayo, Waziri Ummy amesema kuwa kitaifa tunakadiliwa kuwa wapo wagonjwa wa Kifua Kikuu sugu takribani 200 na kati yao, wagonjwa 167 sawa na 84% walianzishiwa matibabu, huku akitoa wito kwa wagonjwa wengine kujitokeza kupata matibabu.

  Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaviva amemuomba Waziri Ummy kuona ulazima wa kuipanua Hospitali ya Mbagala, ili kurahisisha utoaji huduma za Afya, kwani takribani wanawake 67 mpaka 70 hujifungua kwa siku.

  "Wakina mama wanaojifungua hapa ni wengi sana, kwa Mfano jana tu wakina mama 67 wamejifungua, siku nyingine wanafika 70 mpaka 80, hivyo tunahitaji ipanuliwe hospitali hiyo " alisema Mhe. Felix Lyaviva

  Nae Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Mbagala Dkt. Dk Ally Mussa amesema kuwa kutokana na maboresho makubwa ya hospitali kumekuwa na ongezeko kubwa la wagonjwa hadi kufikia wagonjwa 1700 kwa siku, kumekuwa na maboresho makubwa ya huduma za mama na mtoto, maboresho ya huduma za uchunguzi wa magonjwa (maabara za kisasa)

  "kumekuwa na ongezeko kubwa la wagonjwa baada ya maboresho mengi katika huduma za Afya za hospitali, kumekuwa na ongezeko kubwa la wagonjwa hadi kufikia wagonjwa 1700 kwa siku" alisema Dkt. Dk Ally Mussa.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wa (kushooto) akisema jambo na wananchi wa Mbagala alipotembea Hospitali ya Mbagala Jijini Dar Es Salaam na kutoa tamko la Siku ya Kifua Kikuu duniani.(wapili kushoto),Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (kushoto) akitoa dawa za Kifua Kikuu kwa Bw. Abbas Sudi alipotembelea Hospitali ya Mbagala Jijini Dar Es Salaam kujionea hali ya utoaji huduma za matibabu ya Ugonjwa wa Kifua Kikuu na kutoa Tamko la Serikali katikabkuadhimisha Siku ya Kifua Kikuu Duniani amnayo huadhimishwa Tarehe 24 Machi kila Mwaka.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (kushoto) akitoa dawa za Kifua Kikuu kwa Bi. Aisha Rashid alipotembelea Hospitali ya Mbagala Jijini Dar Es Salaam kujionea hali ya utoaji huduma za matibabu ya Ugonjwa wa Kifua Kikuu na kutoa Tamko la Serikali katikabkuadhimisha Siku ya Kifua Kikuu Duniani amnayo huadhimishwa Tarehe 24 Machi kila Mwaka.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (kushoto) akiangalia zawadi ya nguo aliyopewa na Taasisi ya Mukukite inayojishughulisha kutoa huduma za matibabu ya ugonjwa wa kifua kikuu.
  Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Felix Lyaviva akizungumza na wanachi wa Mbagala leo jijini Dar es Salaa ambapo amewaomba wananchi wanapoona dalili za (TB) waende mapema Hospitali watatibuwa bure.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (kulia) akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Felix Lyaviva pindi alipofanya ziara na kujionea huduma za matibabu ya ugonjwa wa Kifua Kikuu katika Hospitali ya Mbagala leo jijini Dar Es Salaam.picha zote na (Emmanuel Maasaka,MMG)
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (wapili kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Felix Lyaviva (wa kwanza kushoto) pamoja na wadau mbalimbali wa afya wakiwasili katika Hospitali ya Mbagala leo jijini Dar Es Salaam.picha zote na (Emmanuel Maasaka,MMG)
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (kushoto) akipokea maelezo kutoka kwa mtaalam kuhusu uchugnguzi wa ugonjwa wa Kifua Kikuu alipotembelea Hospitali ya Mbagala leo jijini Dar Es Salaam.
  Picha ya pamoja.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa mh. Joachim Wangabo amemuagiza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa ACP Mathias Nyangi kuhakikisha anafanya msako wa waganga wa kienyeji katika mkoa na kuwakamata wale wote wanaofanya uganga wa kienyeji bila ya kuwa na leseni halali za kuwaruhusu kufanya shughuli hizo.

  Ametoa agizo hilo baada ya kusikiliza vilio vya wananchi wakati wa mkutano ulifanyika mtaa wa Vuta, Kata ya Kizwite, mjini Sumbawanga, wananchi waliokuwa wakiomboleza vifo vya watoto wawili na mmoja kubaki mahututi katika hospitali ya rufaa ya mkoa baada ya mganga wa kienyeji kuwateka na kuwaficha katika gari lake chakavu tangu watoto hao kupotea tarehe 21.3.2019 na wawili kupatikana wakiwa wamefariki tarehe 23.3.2019 baada ya mmoja aliyepona kutoroka na kuwajulisha wananchi kilichotokea.

  Amesema kuwa msako huo wa waganga wa kienyeji ufanyike katika wilaya zote tatu za mkoa ili kuwahakikishia wananchi amani na utulivu ambayo imekuwepo kwa miaka yote na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano katika kuhakikisha wanawafagia waganga hao wanaonyesha dalili za kuvuruga utulivu uliopo katika mkoa.

  “RPC fanya Operesheni kali ya waganga wa Kienyeji ndani ya Mkoa huu, wale ambao wana leseni tutajua hukohuko kwamba huyu ana leseni n ani halai au siyo halali na kama sio halali basi huyo ni halali yako, na kama kuna mganga wa kienyeji asiye na leseni, huyo ndio kabisa halali yako zaidi, kuanzia sasa hivi bonde la ziwa Rukwa kule Nkasi, Kalambo, Sumbawanga yenyewe hapa kote, opresheni ipite ya kamatakamata waganga wa kienyeji, tumechoka,” Alisisitiza.

  Wakati wakitoa malalamiko yao kwa mkuu huyo wa mkoa, wananchi hao walisema kuwa vifo vya watoto hao vinahusishwa na Imani za kishirikina ambapo kumekuwa na wimbi la vijana wanaoonekana wakila, wakinywa na kuvaa vizuri bila ya kujulikana shughuli zao maalum wanazofanya jambo mbalo limekuwa likiwaumiza kichwa wananchi hao na kukosa majibu.

  Mmoja wa wananchi hao Debora Maenge alisema “ Nasikitika kwa tukio hili lililotokea mtaa wa Vuta, huyu mtu tunaishi nae jirani sana, tunajua ni mtu mwema, kumbe ni mtu ambae sio mwema na hafai kabisa katika jamii, cha kushanga alikuwa na vibali ambavyo alikuwa akijitambulisha kuwa yeye ni mganga wa jadi, vibali hivi vinatolewa serikalini, Je serikali yetu mtaendelea kutoa vibali hivi ili watu waendelee kuuawa kiasi hiki? serikali angalieni mnapotoa vibali je ni waganga Kweli?” Aliuliza.

  Mh. Wangabo alitembelea eneo la nyumba ya mganga huyo wa kienyeji ambayo gari alilowafichia watoto ilikuwamo na kukuta nyumba hiyo ikiwa imevunjwa na gari la mganga huyo kuchomwa moto na wananchi wenye hasira kali.

  Watuhumiwa James Kapyela (52) pamoja na mtoto wake Michael Martin (14) wa tukio hilo la mauaji ya watoto Nicolous Mwambage (7) pamoja na Emanuel Juma (4) hivi sasa wanashikiliwa na polisi huku uchunguzi wa awali ukionyesha watoto hao walifariki kwa kukosa hewa baada ya kufungiwa ndani ya gari chakavu aina ya Chaser Saloon iliyokuwa haitumiki na vioo vya gari hiyo kufungwa. 
   Eneo la Nyumba ya mtuhumiwa ambaye ni Mganga wa Kienyeji wa mtaa wa Vuta, Kata ya Kizwite mjini Sumbawanga baada ya nyumba hiyo kuchomwa moto na wananchi wenye hasira kali baada ya kubaini kuwa mganga huyo amesababisha vifo vya watoto wawili na mmoja kuwa mahututi. 
    Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Mtaa wa Vuta Sangu Sokoni juu ya tukio la kupotea kwa watoto watatu na hatimae kupatikana wawili wakiwa wamefariki na mmoja kuwa mahututi akiendelea na matibabu.
   Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akionyesha eneo katika nyumba iliyokuwa haijamalizika ambapo maiti za watoto hao zilipatikana baada ya kutupwa na mtuhumiwa James Kapyela ambae ni mganga wa kienyeji. 
    Diwani wa Kata ya Kizwite ambae pia ni mchungaji Felician Mavazi (alipiga magoti) akiomba muda mfupi kabla ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa  Mh. Joachim Wangabo kuongea na wananchi wa mtaa huo wa Vuta kata ya Kizwite juu ya tukio la mauaji ya watoto wawili. 
  -Mkuu wa Mkoa wa Rukwa  Mh. Joachim Wangabo alipokuwa akiongea na wananchi wa mtaa wa Vuta, Kata ya Kizwite Sumbawanga mjini. 

    Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akitoa pole kwa wazazi waliofiwa na watoto wao alipotembelea hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Rukwa mara tu baada ya kupata taarifa ya vifo vya watoto wawili na mmoja kuwa mahututi baada ya kupatikana tangu kupotea kwao tarehe 21.3.2019.

  0 0   
  0 0

  Na Ripota Wetu -ABUJA, NIGERIA 

  WATANZANIA 52 ni miongoni mwa waliofanikiwa kushinda katika programu ya wajariamali Afrika, inayoratibiwa na na Taasisi ya Tony Elumelu ya nchini Nigeria. 

  Kuchaguliwa kwao sasa kunawafanya kuwa miongozi mwa wajariamali 1,000 ambao watanufaika kwa kuwezeshwa zaidi ya Sh milioni 10 ili kuimarisha biashara zao na kuzalisha ajira kwa vijana hususani kwa nchi za Afrika. 

  Hatua hiyo inatokana na matokeo yaliyotanganzwa mwishoni mwa wiki na Taasisi ya Tony Elumelu (TEF) ambayo ni ya Kiafrika inayoongoza kutoa ushauri na kuwawezesha wajasiriamali kutoka Afrika. 

  Pamoja na hali hiyo pia ilitangaza wajasiriamali wa Afrika 3,050 kutoka nchi 54 za Afrika ambao wamejiunga kwenye mzunguko wa tano wa dola za Marekani milioni 100 katika programu ya Ujasiriamali wa TEF. 

  Matokeo hayo yalitangazwa jijini Abuja baada ya washauri wa maendeleo kuwasilisha mchakato wa uteuzi huo, ambapo kwa mwaka huu zaidi ya watu 216,000 waliwasilisha maombi ikiwa ni ongezeko ya watu 151,000 kutoka mwaka jana. 

  “Takribani maombi 90,000 yaliwasilishwa na wajasiriamali wanawake ikiwa ni ongezeko la asilimia 45, hii ni ishara ya mkakati wa Taasisi hiyo kufikia usawa wa jinisia. Wajasiriamali waliochaguliwa kila moja atapokea dola za Marekani 5,000 za mitaji ambayo haitarudishwa, upatikanaji wa washauri na wiki 12 ya mafunzo ya biashara yanayohusisha moja kwa moja mahitaji ya wajasiriamali kutoka Afrika. 

  “Julai 26 – 27, 2019, watakusanyika kwenye Mkutano wa Biashara wa TEF, mkusanyiko mkubwa wa kila mwaka wa wajasiriamali wa Kiafrika na mazingira ya ujasiriamali katika Bara hili la Afrika 

  “Kila mwaka, tunakabiliwa na kazi ngumu – kuchagua wajasiriamali 1,000 kutoka maelfu ya waliyoomba. Wajasiriamali wetu wananjaa ya kuchochoea mabadiliko. Lazima tushirikiana kuwawezesha ili kuchochea mabadiliko tunayotaka katika bara letu,” alisema muasisi wa TEF, Tony Elumelu. 

  Katika hotuba yake, Mke wa Rais wa Nigeria, Aisha Buhari, alipongeza jitihada za programu na kuwasisitizia wajasiriamali waliochaguliwa kuchangia maandeleo ya bara la Afrika. 

  “Nina imani hawa wajasiriamali wa Tony Elumelu watakuwa na msaada mkubwa sio tu Nigeria lakini bara nzima,” alisema. 

  Akizungumza kuhusu mchakato huo Ofisa Mtendaji Mkuu ajaye Ifeyinwa Ugochukwu, alisema “Programu ya Ujasiriamali wa Taasisi ya Tony Elumelu, imewawezesha kwa mafanikio wajasiriamali 7,520 katika miaka yake mitano ya kwanza kati ya miaka 10 ya programu. Ikitimiza miaka mitano kati ya miaka 10 ya programu, uteuzi wa mwaka huu umehusisha wajasiriamali 2,050 wakisaidiwa na washirika wa Taasisi. 

  “Mwaka jana, tulizindua TEFConnect - jukwaa la mitandao ya digital kwa wajasiriamali wa Kiafrika na kufunguliwa kwa wote - kuendeleza demokrasia ufikiaji wa fursa kwa maelfu ya wajasiriamali ambao hawawezi kufaidika moja kwa moja na Programu ya Wajasiriamali. Hii inaonyesha zaidi dhamira yetu ya kuwawezesha wajasiriamali wetu na imani yetu kuwa ujasiriamali una ufunguo wa kufuta uwezo wa kweli wa bara la Afrika,” alisema. 
   
  Alisema washirika wa taasisi hiyo kwa sasa wanazidi kuongezeka ni Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC), United Nations Development Programme (UNDP), Serikali ya Benin (Seme City), Anambra State Government, Indorama, Serikali ya Botswana na Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB).

  Mwanzilishi wa Taasisi ya Tony Elumelu, Tony Elumelu (Kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na na mke wa Rais wa Nigeria, Aisha Buhari (katikati) na kulia ni Mwasisi Msaidizi Dk. Awele Elumelu. Hafla ya kutangaza majina ya wajariamali 1,000 wa Afrika wataowezeshwa na Taasisi ya TEF ilifanyika jana jijini Abuja nchini Nigeria


  Kutokana kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tony Elumelu anayeingia, Ifeyinwa Ugochukwu, Mkurugenzi anayemaliza muda wake Parminder Vir, Balozi WA Israel nchini Nigeria, Shimon Ben-Shoshan, Mwasisi wa Taasisi ya Tony Elumelu, Mke wa Rais wa Nigeria Aisha Buhari, Mwasisi Msaidizi wa TEF, Dk. Awele Elumelu, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutangazwa kwa majina ya wajasiriamali 1,000 watakaonufaika kwa kuwezeshwa na taasisi hiyo.


  0 0


  Muonekano wa Jengo la Wizara ya Madini linalojengwa katika Mji wa Serikali eneo la Ihumwa.

  Waziri wa Madini Doto Biteko, (mwenye koti) Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo (wa tatu kushoto) na Prof. Simon Msanjila (mwenye tisheti nyekundu) wakikagua maeneo maeneo mbalimbali ya jengo la Wizara

  Waziri wa Madini Doto Biteko ( wa kwanza kushoto), Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo (wa pili kushoto ) na Katibu Mkuu wa Madini Prof. Simon Msanjila, wakijadiliana jambo wakati wakikagua maeneo mbalimbali ya jengo la Wizara, eneo la Ihumwa.

  Waziri wa Madini Doto Biteko katikati na Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo wakiangalia kitu wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Wizara, Ihumwa.
  …………………….  *Viongozi Waandamizi Madini watembelea jengo la Wizara, Ihumwa
  *Waziri Biteko asema wizara iko tayari kuwahudumia watanzania kutokea Ihumwa
  *Mkandarasi aahidi kukamilisha ujenzi ndani ya siku Tano

  Viongozi Waandamizi wa Wizara ya Madini, wakiongozwa na Waziri wa Madini, Doto Biteko leo Machi 23, wametembelea Jengo la Wizara ya Madini lililopo mji wa Serikali eneo la Ihumwa, Jijini Dodoma kwa lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi huo.

  Akizungumza baada ya kukagua jengo hilo, Waziri wa Madini Doto Biteko amewahakikishia watanzania wote pamoja na wadau wa madini kuwa, wizara iko tayari kuwahudumia kutokea eneo hilo la Ihumwa pindi itakapohamia na kuwataka watumishi kujiandaa kuhamia eneo hilo mara baada ya mkandarasi kukabidhi jengo kwa wizara. Vilevile, Waziri Biteko amezitaka taasisi nyingine zenye uhitaji wa kutumia madini ya mawe yanayopatikana nchini ikiwa ni pamoja na mable, kuwa wizara iko tayari kuwasaidia kwa kuwaunganisha na wajeta wake.

  Pia, amemshukuru Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa kutokana na msukumo alioutoa kuhakikisha ujenzi wa majengo ya serikali unakamilika kwa wakati. Aidha, amempongeza Mkandarasi kampuni ya Mzinga Holding Co. Ltd kutokana na kuongeza kasi ya ujenzi ikiwemo kuzingatia ubora nakuongeza kwamba, wizara imeridhika na ujenzi.

  Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo, ameeleza kuwa, wizara imepanga kulifanya eneo la ofisi hiyo kuwa kijani kwa kuhakikisha inapanda miti ya aina mbalimbali na kuhakikisha kwamba eneo hilo linawekewa mazingira mazuri ya kuvutia. 

  Naye, Katibu Mkuu wa Madini, Prof. Simon Msanjila Amesema Mkandarasi Kampuni ya Mzinga Holding Co. Ltd imeahidi kuikabidhi Wizara jengo hilo ndani ya kipindi cha siku Tano zijazo “awali ujenzi ulianza kwa kusuasua lakini sasa uko katika hatua nzuri na mkandarasi amezingatia ubora,” amesema Prof. Msanjila. 

  Akizungumzia mahitaji ya ofisi na idadi ya watumishi, amemsema kwa idadi ya watumishi wa wizara Makao Makuu ofisi zilizopo katika jego hilo zinatosheleza mahitaji na kuongeza kuwa, kwa kuanza Idara zote na Vitengo vya Wizara vinatarajia kuhamia katika eneo hilo isipokuwa Idara ya fedha kutokana na masuala ya mfumo wa kifedha. Pia, ameeleza kuwa, wizara imetumia malighafi inayopatikana nchini yakiwemo madini ya mable ambayo yamepatikana kutoka kwa wachimbaji wadogo wa madini nchini.

  Kwa upande wake, Mkandarasi wa kampuni hiyo Hamisi Msangi ameihakikishia wizara kuwa , ndani ya siku tano zijazo, jengo hilo litakabidhiwa rasmi kwa wizara hiyo.

  0 0


  Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

  MAGOLI matatu ya timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' dhidi ya timu ya Taifa ya Uganda ' The Cranes' yametosha kuwapelekeaWatanzania nchini Misri kwenye michuano ya AFCON mwaka 2019.

  Mbele ya mashabiki  zaidi ya 60,000 ambao walikuwa na jukumu la kuhakikisha wanaishangalia Taifa Stars yalikuwa chachu tosha kwa wachezaji ambapo waliokuwa wanacheza kwa uwezo wa hali ya juu.

  Taifa Stars ilipata goli la kwanza kupitia kwa Mshambuliaji wake Simon Msuva ambalo liliduma hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza, hadi wanakwenda mapumziko Taifa Stars ilikuwa inaongoza kwa goli 1-0 dhidi ya The Crains.

  Wakati wachezaji wa timu ya Taifa Stars wakicheza kwa jihadi huku wakitambua kaulimbiu inayosema ' Ni zamu yetu', kipindi cha pili walirudi uwanjani wakiwa na nguvu zaidi na kufanya mashambulizi ya mara kwa mara golini kwa 'The Cranes'.

  Mashambulizi ya Taifa Stars yalisababisha kupatikana kwa penalti kwa upande wa Tanzania ambapo mchezaji aliyekuonesha umahiri wa hali ya juu kumiliki mpira Erasto Nyoni aliifunga goli la pili.

  Kasi ya Taifa Stars ilisababisha kupatikana kwa goli la tatu kupitia kwa mchezaji Agrey Morris.

  Hata hivyo wachezaji wa Uganda walionekana kusuka mipango ya kutafuta bao lakini Taifa Stars waliziba njia zote na kuharibu mipango na kuifanya kushindwa kupata goli.

  Watanzani waliokuwa uwanjani wakiongozwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa walikuwa na furaha isiyo kifani huku wachezaji wa Taifa Stars wakionesha kuwa kichwani wanaiwaza AFCON na sio kitu tofauti na hicho.

  Magoli ya Taifa Stars yalisababisha mashabiki kushindwa kukaa kwenye viti ambapo karibu muda wote wa mchezo walikuwa wakishangilia.

  Hata hivyo wakati Taifa Stars na Uganda wakiendelea kuchezaji,mashabiki walitangaziwa kuwa mechi kati ya Lesotho na Cape Verde yalikuwa ni sare .Matokeo hayo yameipeleka Taifa Stars na Uganda Misri hasa kwa kuzingatia Uganda walishafuzu kwa kuwa na alama 13 kabla ya mchezo wa leo.

  Hata hivyo mashabiki wa Uganda waliokuwa uwanjani hapo walionekana nao wakishangilia ushindi wa Taifa Stars.Kabla ya kuanza kwa mechi ya leo iliyofanyika Uwanja Mkuu wa Taifa mashabiki wa Uganda walikuwa na matumaini ya kushinda.  0 0

  Msimamizi msaidizi wa mradi wa maji wenye thamani ya Shs. 152 milioni, Baltazar Mtenga (kushoto) kutoka kampuni ya Ifango General Enterprises, akielezea changamoto za kukwama kwa mradi huo mbele ya Mwenyekiti wa CCM Tawi la Mbagala Charambe Machinjioni, Shaibu Omari Naputa (kulia) na Mwenyekiti wa Mtaa wa Machinjioni A, Mkonge Hassan Katani (wa pili kulia) wakati Halmashauri Kuu ya tawi hilo ilipofanya ziara kukagua miradi ya maendeleo mwishoni mwa wiki.  HALMASHAURI ya Chama cha Mapinduzi (CCM) tawi la Charambe Machinjioni katika Jimbo la Mbagala mkoani Dar es Salaam imeonyesha kukerwa na ucheleweshaji wa utekelezaji wa miradi miwili ya maji yenye thamani ya zaidi ya Shs. 170 milioni.

  Akizungumza mwishoni mwa wiki katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo iliyoko katika Mtaa wa Machinjioni A, Mwenyekiti wa CCM wa tawi hilo, Shaibu Omari Naputa, alisema kutokamilika kwa miradi hiyo muhimu kunaitia doa Serikali ya CCM, ambayo imedhamiria kuwaletea wananchi maendeleo.

  Miradi hiyo ya maji, mmoja ukitekelezwa na Halmashauri ya Wilaya na mwingine ukiwa umefadhiliwa na Ofisi ya Jimbo, ingeweza kuwahudumia wakazi zaidi ya 30,000 jimboni humo, ambao kwa sasa wanapata shida kubwa ya kupata huduma hiyo.

  “Miradi hii ilikuwa ikamilike zaidi ya mwaka mmoja ulipita, lakini mpaka sasa ujenzi unasuasua huku mradi unaofadhiliwa na Ofisi ya Jimbo ukiwa umekwama na vifaa kung’olewa,” alisema Naputa.

  Katika mradi wa kwanza ambao ulikuwa chini ya taasisi ya CHADEA kabla ya Halmashauri ya Manispaa ya Temeke kuuchukua, ulitengewa takriban Shs. 152 milioni ili kuupanua kwa kujenga tenki kubwa na vituo vitano vya kusambazia maji pamoja na pampu, lakini badala ya kukamilika Mei mwaka 2018, mpaka sasa hata ujenzi wa tenki haujakamilika.

  Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo, Mkonge Hassan Katani ambaye aliongoza ziara hiyo, alisema kwamba, kwa vile wasimamizi wakubwa ni Halmashauri ya Manispaa yeye hana mamlaka ya moja kwa moja ya kuwahimiza wakandarasi wamalize haraka ujenzi, kwani licha ya mradi huo kuwepo mtaani kwake, hajui hata mikataba yao ikoje.

  “Nimekuwa nikiwaulizia tu wakandarasi, lakini wanatoa sababu kwamba hawajapatiwa fedha kutoka halmashauri, sasa kwa sababu halmashauri wenyewe ndio wasimamizi, inakuwa vigumu kwangu kuwahimiza," alisema.

  Msimamizi msaidizi wa mradi huo kutoka kampuni ya Ifango General Enterprises, Baltazar Mtenga, alisema kinachokwamisha ni fungu la fedha kuchelewa kutoka halmashauri.Alikiri kwamba, mradi huo ulikuwa ukamilike tangu Mei 2018, lakini mkandarasi akaomba kuongezewa muda kutokana na sababu mbalimbali, ikiwemo kuchelewa kupewa fedha na halmashauri.

  “Fedha zinatolewa kwa awamu, kila tunapojenga lazima waje wakague halafu waidhinishe fungu jingine, lakini kuna kipindi tulisubiri kwa karibu miezi mitatu bila kupata fedha, jambo ambalo linakwamisha utekelezaji.

  “Tukipata fedha tunaweza kukamilisha ujenzi ndani ya mwezi mmoja,” alisema Mtenga wakati ujenzi wa tenki lenye uwezo wa kujaza lita 45,000 za maji ukiendelea.Kwa upande wake, Naputa amemuagiza mkandarasi kuhakikisha anakamilisha mradi huo ndani ya mwezi mmoja kwani mpaka sasa ni mwaka mzima tangu mradi huo ulipokuwa ukamilike.

  Aidha, amemuomba Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa kuhakikisha anaidhinisha fedha kwa wakati ili wananchi wasiendelee kuteseka kutafuta huduma ya maji.

  Kuhusu mradi wa maji uliokuwa utekelezwe na Ofisi ya Jimbo, Mwenyekiti wa Mtaa Bw. Katani alisema kwamba, ulitumia kiasi cha Shs. 24 milioni, lakini tangu kisima kilipochimbwa miaka mitatu iliyopita hakikuweza kutumika hadi Mei 2018 walipofunga pampu.

  “Pampu ilipofungwa ikaanza kuvuta tope badala ya maji, kwahiyo hapa maji hayajatoka ingawa miundombinu yote ilikuwa imekamilika ikiwemo tenki na kituo cha kutolea maji.“Baada ya kuona hivyo, Mbunge wa Jimbo la Mbagala, Ally Mangungu, aliamua kuja kung’oa pampu na nyaya za umeme kwa kuhofia zingeweza kuibiwa, lakini mpaka sasa sijui vifaa hivyo vilivyong’olewa viko wapi japokuwa alisema angeibadilisha pampu,” alisema Katani.

  Kwa upande wake, Naputa alisema kwamba, anaamini fedha hizo za Mfuko wa Jimbo hazijawasaidia wananchi wa Mbagala, akaitaka Ofisi ya Jimbo iwajibike kwa sababu hasara iliyotokea imetokana na uzembe.

  Miradi mingine iliyokaguliwa ni pamoja na ujenzi wa Ofisi ya Serikali ya Mtaa na Barabara ya Charambe-Buza ambao haujaanza licha ya kwamba tayari wakazi wote wamekwishalipwa fidia kupisha barabara hiyo.

  Katani alisema, ikiwa barabara hiyo yenye urefu wa takriban kilometa 3 itakamilika basi itakuwa mkombozi kwa wananchi wengi na kupunguza msongamano, kwani magari, hasa yanayokwenda Tandika, Buza na Uwanja wa Ndege hayatalazimika kuzungukia Temeke.

  Kuhusu ujenzi wa Ofisi ya Serikali ya Mtaa, wana-CCM hao wameonyesha mashaka ya matumizi ya Shs. 8 milioni zilizotolewa na Halmashauri ya Manispaa na kusimamiwa na Ofisi ya Kata, kwani gharama zilizotumika zinaonekana kuwa ndogo kuliko fedha zilizotolewa.

  Naputa amesema watamwandikia barua Katibu wa CCM wa Kata ili kumtaka Ofisa Mtendaji wa Kata aeleze mchanganuo wa matumizi ya fedha hizo kwa kuwa wanahisi kuna ufisadi mahali.Mwenyekiti wa Mtaa, Bw. Katani, alisema mpaka kuezekwa jengo la ofisi hiyo zimetumika Shs. 13 milioni na kwamba kuna upungufu wa Shs. 7 milioni ili ofisi hiyo ikamilike pamoja na miundombinu yake.
  Mwenyekiti wa CCM Tawi la Mbagala Charambe Machinjioni, Shaibu Omari Naputa (katikati) na Mwenyekiti wa Mtaa wa Machinjioni A, Mkonge Hassan Katani (kushoto) wakiwa katika kituo cha kutolea maji katika mradi wa maji uliofadhiliwa na Mfuko wa Jimbo la Mbagala ambao umekwama. 
  Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM ya tawi la Charambe Machinjioni katika Jimbo la Mbagala wakiwa katika Ofisi wa Serikali ya Mtaa wa Mmachinjioni A ambayo haijakamilika.

  0 0


  Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania kwa kushirikiana na umoja wa Ulaya (EU) inafanya warsha na wadau mbalimbali kwa lengo la kujadiliana namna ya kuboresha sheria na kanuni mbalimbali kwenye uchimbaji wa madini ya Urani hapa nchini. 

  Wadau kutoka Wizara ya Madini, Tume ya madini, Wizara ya Elimu ,Sayansi na Teknolojia ,Wizara ya Mali Asili na Utalii na Baraza la Mazingira nchini (NEMC) wote kwa pamoja wanajadiliana namna ya kuboresha sheria na taratibu za uchimbaji wa madini yenye mionzi. 

  Akizungumza kwenye warsha Kaimu Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Teknolojia na huduma za Ufundi wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania Dennis Mwalongo amesema kuwa wadau kwa pamoja wataweza kusaidia kuboresha kanuni za uchimbaji wa madini yenye mionzi kwa lengo la kuondoa muingiliano wa sheria hizo katika sekta ya madini. 

  “Majadiliano haya yatatuwezesha kutoka na kanuni ambazo zitasaidia kwa namna moja ama nyingine katika kuweka mfumo mzuri utakaowezesha uchimbaji madini yenye mionzi kuwa katika utaratibu mzuri na usio na muingiliano kwenye sekta ya madini na mazingira kwa ujumla” alisema Mwalongo. 

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Migodi na Mazingira wa Tume ya Madini Nchini Dkt. Abdul Rahaman Mwanga ameeleza kuwa wanatarajia kupata utaratibu na mfumo mzuri wa usimamiaji wa madini yatokanayo na mionzi hapa nchini. 

  Amesema kuwa Sheria zipo lakini kumekuwa na muingiliano wa sheria ambapo kwa kukaa pamoja wadau watawezesha kuimarisha taratibu za madini na kuwa taratibu hizo ambazo zimeboreshwa zitasaidia katika usalama wa mazingira na afya kwa viumbe mbali mbali vinavyozunguka maeneo ya uchimbaji ya madini ya Urani. 

  “Tuna imani kuwa taratibu tutaziweka sawa ili kuwezesha uchimbaji wa madini ya Urani hapa nchini na matarajio yetu kuwa madini hayo yatakapoanza kuchimbwa hakutakuwa tena na na muingiliano wowote” alisema Mwanga. 

  Pia ameeleza kuwa sheria na kanuni hizo na uboreshaji wake utakapokamilika kurekebishwa kutawezesha utaoji bora wa huduma kwa wawekezaji ambao wataamua kuwekeza katika uchimbaji wa madini ya Urani hapa nchini. 

  Naye mshiriki mwingine kwenye warsha hiyo Dkt. Justin Ngaile amesema mfumo mzuri wa usimamizi wa madini ya Urani utawekwa jambo ambalo litasaidia kurahisisha uwekezaji mkubwa hapa nchini. 

  Umoja wa Ulaya ndio mdhamini katika warsha hii ambapo kupitia wataalamu wake wanasaidia uboreshaji wa sheria na kanuni mbali mbali za uchimbaji wa madini yenye Mionzi ambazo zimeingiliana na uchimbaji wa madini na masuala yamazingira. 

  Baadhi ya maeneo hapa nchini yanapopatikana madini ya Urani ni pamoja na Bahi Mkoani Dodoma na Mkuju Mkoani Ruvuma. 

  Imetolewa na; 


  Peter G. Ngamilo 
  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano 
  Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania 
  Namba ya Simu 0755496515

  0 0

   Meneja wa Mawasiliano na Matukio wa Vodacom Tanzania (plc), Christina Murimi (kulia) akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi 500,000/-mmoja wa washiriki wa kampeni ya M-Pesa Tuzo Points, Christian Myamba, fundi cherahani na mkazi wa Sinza, Dar es Salaam. Kupitia kampeni hii wateja 140 wa Vodacom walizawadiwa shilingi 25,000/-kila mmoja na baada ya kampeni kumalizika wateja 10 wa Vodacom nchi nzima watazawadiwa shilingi 500,000/-kila mmoja
   Meneja wa Mawasiliano na Matukio wa Vodacom Tanzania (PLC), Christina Murimi (kulia) akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi 500,000/-mmoja wa washiriki wa kampeni ya M-Pesa Tuzo Points,Regina Mwampinga,mkazi wa Tegeta, Dar es Salaam. Kupitia kampeni hii wateja 140 wa Vodacom walizawadiwa shilingi 25,000/-kila mmoja na baada ya kampeni kumalizika wateja 10 wa Vodacom nchi nzima watazawadiwa shilingi 500,000/-kila mmoja
   Meneja wa Mawasiliano na Matukio wa Vodacom Tanzania (plc), Christina Murimi (kulia) akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi 500,000/-mmoja wa washiriki wa kampeni ya M-Pesa Tuzo Points, Christian Myamba, fundi cherahani na mkazi wa Sinza, Dar es Salaam. Kupitia kampeni hii wateja 140 wa Vodacom walizawadiwa shilingi 25,000/-kila mmoja na baada ya kampeni kumalizika wateja 10 wa Vodacom nchi nzima watazawadiwa shilingi 500,000/-kila mmoja
  Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania PLC, Alex Bitekeye na Meneja mawasiliano na Matukio wa kampuni hiyo ,Christana Murimi (kulia) mara baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi 500,000/- wakati wa hafla hiyo ilifanyika katika ofisi yake ya Vanessa Hair Beuaty Salon iliyopo Tabata Chama jijini Dar es Salaam

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wachezaji wa timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu Taifa Stars ambao walifika Ikulu mara baada ya kufanikiwa kufuzu kushiriki Fainali za michuano ya Mataifa ya Africa AFCON baada ya kuifunga Timu ya Taifa ya Uganda The Cranes magoli 3-0 jijini Dar es Salaam.
   Wachezaji wa timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu Taifa Stars waliopo upande wa kulia pamoja na viongozi wengine wakionesha ishara ya magoli matatu ambayo timu ya Taifa iliupata siku ya jumapili zidi ya Timu ya Taifa ya Uganda The Craines na kufanikiwa kufuzu kucheza Fainali za michuano ya Mataifa ya Africa AFCON nchini Misri baadae mwaka huu.

   Sehemu ya Wachezaji wa  wa timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu Taifa Stars waliopo upande wa kulia pamoja na viongozi wengine wakiwa katika ukumbi wa Mkutano Ikulu jijini Dar es Salaam.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mchezaji wa Timu ya Taifa Taifa Stars Shabani Iddi Chilunda mara baada ya kumaliza kuzungumza na wachezaji hao.
   Mwenyekiti wa Kamati ya Uhamasishaji ya Timu ya Taifa Stars ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda wanne kutoka kushoto waliokaa pamoja na wachezaji Wachezaji wa  wa timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu Taifa Stars waliopo upande wa kulia pamoja na viongozi wengine wakiwa katika ukumbi wa Mkutano Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Bondia wa Ngumi za kulipwa Hassan Mwakinyo kutoka Tanga akijitambulisha Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya kupewa nafasi ya kuzungumza kuhusiana na mafanikio yake makubwa aliyoyapata katika ngumi za kulipwa pamoja na kuitangaza nchi kimataifa.
   Mfungaji wa goli la pila la Taifa Stars zidi ya Uganda Erasto Nyoni akijitambulisha Ikulu jijini Dar es Salaam.
    Bondia wa Ngumi za kulipwa Hassan Mwakinyo kutoka Tanga akizungumza mara baada ya kupewa nafasi Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi wakati Bondia Hassan Mwakinyo alipokuwa akizungumza.
   Mchezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars Jonas Mkude akifurahia jambo wakati wakiwa Ikulu jijini Dar es Salaam pamoja na wachezaji wenzake.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Kocha wa Taifa Stars Emanuel Amunike mara baada ya kumaliza kuzungumza na wachezaji wa Timu ya Taifa.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mchezaji wa zamani wa  Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars Peter Tino ambaye alifunga goli moja lililoipeleka Tanzania kwa mara ya kwanza katika michuano ya AFCON mwaka 1980 iliyofanyika nchini Nigeria. Pia Rais Dkt. Magufuli amemsaidia mchezaji huyo wa zamani kiasi cha Shilingi milioni tano. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa anapata chakula cha mchana na viongozi pamoja na Wachezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars Ikulu jijini Dar es Salaam.

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Juliana Shonza, Rais wa TFF Walace Karia, Bondia wa Ngumi za kulipwa Hassan Mwakinyo wapili kutoka kushoto katika picha ya pamoja na  Wachezaji wa timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu Taifa Stars ambao walifika Ikulu mara baada ya kufanikiwa kufuzu kushiriki Fainali za michuano ya Mataifa ya Africa AFCON baada ya kuifunga Timu ya Taifa ya Uganda The Cranes magoli 3-0 jijini Dar es Salaam. PICHA  NA IKULU


  =======  =========   =========  ==========

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 25 Machi, 2019 amekutana na kuwapongeza wachezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kwa kufanikiwa kufuzu kucheza fainali za michuano ya soka Barani Afrika kwa mwaka 2019 (AFCON-2019) na pia amempongeza bondia Hassan Mwakinyo ambaye juzi alishinda pambano lake dhidi ya bondia Sergio Gonzalez wa Argentina lililofanyika Jijini Nairobi nchini Kenya.

  Hafla ya kuwapongeza wanamichezo hao imefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Kamisheni ya Ngumi Tanzania (TPBRC) na Kamati ya Ushindi ya Taifa Stars iliyoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda.

  Akizungumza katika hafla hiyo Mhe. Rais Magufuli ameelezea kufurahishwa kwake na matokeo ya mchezo wa jana ambapo Taifa Stars iliifunga Timu ya Taifa ya Uganda (The Cranes) katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kwa magoli 3-0 na ameahidi kuwa Serikali itaendelea kuunga mkono juhudi za wanamichezo wote kwa kuwa mafanikio yao yanaliletea Taifa sifa na heshima na pia yanatangaza fursa mbalimbali ikiwemo utalii, biashara na uwekezaji.

  Mhe. Rais Magufuli amewapongeza wachezaji wa Taifa Stars, viongozi wa TFF, Kamati ya Ushindi ya Taifa Stars na Watanzania wote kwa kuungana pamoja kuishangilia timu yao katika mchezo wa jana bila kujali tofauti zao za kidini, itikadi za kisiasa, makabila na kanda wanazotoka.

  “Kwa kweli jana nilifurahi sana jinsi mlivyokuwa mnacheza na jinsi mlivyofunga magoli, Watanzania wanataka furaha, sio kufungwafungwa kama mlivyofungwa kule Lesotho, ile iliniuma sana hadi nilipanga kuwa sitaita tena timu kuja hapa Ikulu, lakini sasa safi.

  Nataka niwahakikishie Serikali ipo na nyinyi na ni matarajio yangu kuwa mtajiandaa vizuri ili mkafanye vizuri katika michuano ya AFCON huko Misri, sasa vita imeanza” amesema Mhe. Rais Magufuli.

  Mhe. Rais Magufuli ametoa changamoto kwa wadau wote wa michezo kuhakikisha wanasimamia uboreshaji wa miundombinu ya michezo, wanajipanga vizuri kwa michezo mbalimbali ya kuiwakilisha nchi, wanarekebisha dosari zote zilizosababisha kusuasua kwa Tanzania katika michezo ya kimataifa na ameipongeza TFF kwa kufanikiwa kurejesha mgao wa fedha za maendeleo kutoka Shirikisho la Soka Duniani (FIFA).

  Aidha, ameiagiza Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kufuatilia uendeshaji wa uwanja wa Taifa ili kujiridhisha juu ya mapato na matumizi ya fedha za uwanja huo pamoja na kuangalia ubora wake kutokana na kuwepo kwa taarifa kuwa maeneo yanayoharibika hayafanyiwi matengenezo inavyopaswa.

  Mhe. Rais Magufuli amempongeza bondia Hassan Mwakinyo kwa ushindi alioupata hapo juzi baada ya kumpiga kwa knockout bondia Sergio Gonzalez wa Argentina katika pambano lisilo la ubingwa lilifanyika Jijini Nairobi nchini Kenya, pamoja na mapambano mengine ambayo alishinda na amemtaka kuendelea kufanya vizuri katika mapambano mengine ili kuipatia sifa Tanzania.

  “Nafahamu kuwa unazo changamoto nyingi ambazo hukusema hapa, lakini nakupongeza sana, juzi umemtandika yule jamaa mpaka akakaa chini na huwa nakuona unavyofanya mazoezi makali kwa kutumia matairi, wewe ni kijana safi sana” amesema Mhe. Rais Magufuli.

  Mhe. Rais Magufuli ameipongeza kampuni ya Serengeti Breweries Limited ambayo ni wadhamini wa timu ya Taifa Stars na SportPesa ambao ni wadhamini wa bondia Hassan Mwakinyo kwa mchango wao mkubwa wa kuendeleza michezo.

  Katika hafla hiyo Mhe. Rais Magufuli amekubali maombi yaliyotolewa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ya kusaidiwa maandalizi ya michuano ya AFCON kwa vijana wa chini ya miaka 17 iliyopangwa kuanza tarehe 14 Aprili, 2019 hadi tarehe 28 Aprili, 2019 Jijini Dar es Salaam huku Tanzania ikiwakilishwa na timu ya Serengeti Boys, ambapo amesema Serikali itatoa shilingi Bilioni 1 kusaidia maandalizi hayo.

  Halikadhalika Mhe. Rais Magufuli ametoa zawadi ya kiwanja kimoja cha kujenga nyumba Jijini Dodoma kwa kwa kila mchezaji wa Taifa Stars, Bondia Hassan Mwakinyo, mchezaji wa zamani na Nahodha wa Taifa Stars Leodgar Tenga na mchezaji wa zamani na mfungaji wa bao lililoiwezesha Tanzania kucheza robo fainali ya AFCON mwaka 1980 Peter Tino ambaye pia amezawadiwa shilingi Milioni 5.

  Kwa upande wao wachezaji wa Taifa Stars ambao wameongozwa na Nahodha Msaidizi Himid Mao na bondia Hassan Mwakinyo wamemshukuru Mhe. Rais Magufuli na Serikali kwa ushirikiano mkubwa walioupata hadi kufikia mafanikio hayo na wamemuahidi kuendelea kufanya vizuri katika michezo inayofuata.

  Rais wa TFF Bw. Wallace Karia na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bw. Leodgar Tenga wamesema baada ya kufuzu kucheza fainali za AFCON sasa Taifa Stars inaelekeza nguvu zake kujiandaa na michuano hiyo mikubwa Barani Afrika na pia wameelezea matumaini makubwa ya Tanzania kufanya vizuri katika michuano ya AFCON kwa vijana wa chini ya miaka 17 ambapo Tanzania itawakilishwa na timu ya Serengeti Boys, michuano ya AFCON kwa wanawake ambapo Tanzania inawakilishwa na Twiga Stars na kufanya vizuri kwa timu ya Taifa ya Soka chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heros) ambayo tarehe 31 Machi, 2019 itacheza na Eritrea Mjini Asmara. 


  Pamoja na kuwapongeza wachezaji wa Taifa Stars na Bondia Hassan Mwakinyo Mhe. Rais Magufuli amekula chakula cha mchana na wachezaji hao. 


  Gerson Msigwa 
  Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU 
  Dar es Salaam 
  25 Machi, 2019

  0 0


  0 0

  Operesheni Meneja wa Shamba Narayawan Krishna akifafanua jambo kwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF,William Erio akiwa na baadhi ya viongozi waandamizi kutoka shirika hilo,kuhusu maandalizi makubwa yanayotarajiwa kufanywa ndani ya shamba hilo ikiwemo na miundo mbinu mbalimbali namna itakavyojengwa,Uongozi wa NSSF jana Machi 25,2019 umetembelea shamba la sukari la Bagamoyo linalomilikiwa na Kampuni ya Bakharesa kwa lengo la kujifunza kilimo na uzalishaji wa bidhaa hiyo,ambapo shamba hilo lina ukubwa wa Ekari 25,000 .

  Operesheni Meneja wa Shamba Narayawan Krishna (mwenye kofia) akifafanua jambo kwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF,William Erio akiwa na baadhi ya viongozi waandamizi kutoka shirika hilo,namna ya kuandaa shamba la miwa,upandaji mbegu na utunzaji wake. Uongozi wa NSSF umetembelea shamba la sukari la Bagamoyo linalomilikiwa na Kampuni ya Bakharesa kwa lengo la kujifunza kilimo na uzalishaji wa bidhaa hiyo,ambapo shamba hilo lina ukubwa wa Ekari 25,000 .

  Muonekano wa shamba la Miwa akianza kuchipua

  Operesheni Meneja wa Shamba Narayawan Krishna akimueleza jambo Mkurugenzi Mkuu wa NSSF,William Erio (pichani kati) walipokuwa wakitembelea maeneo mbalimbali ya shamba hilo ikiwemo kujionea ujenzi wa miundo mbinu kama vile mabwawa ya maji,mabomba ya maji,barabara yote hiyo ikiwa ni sehemu ya maandalizi makubwa yanayotarajiwa kufamywa ndani ya shamba hilo lenye ukubwa wa Ekari elfu 25,000, kushoto ni Mkuu wa Mradi wa shamba hilo,Hosein Sufiani.

  Operesheni Meneja wa shamba la sukari la Bagamoyo linalomilikiwa na Kampuni ya Bakhresa, Narayawan Krishna (mwenye kofia) akieleza maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya kusambaza maji ndani ya shamba hilo kwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF,William Erio alieongozana na baadhi ya viongozi waandamizi kutoka shirika hilo. Uongozi wa NSSF umetembelea shamba la sukari la Bagamoyo linalomilikiwa na Kampuni ya Bakharesa kwa lengo la kujifunza kilimo na uzalishaji wa bidhaa hiyo,ambapo shamba hilo lina ukubwa wa Ekari 25,000 .

  Mkurugenzi Mkuu wa NSSF,William Erio (pichani kushoto) akiwa ameongozana na Wasimamizi wa shamba hilo wakitembelea kuona maendeleo ya ujenzi wa miundombinu katika shamba hilo,lililopo nje kidogo ya mji mkongwe wa Wilaya ya Bagamoyo,mkoani Pwani.


  Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bw. William Erio akiwa ameambatana na baadhi ya viongozi Waandamizi wa shirika hilo,walifika Ofisini kwa Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya Bakharesa, Bw. Said Salim Bakharesa (pichani kulia),kumshukuru mara baada ya kumaliza ziara yao walioifanya asubuhi Machi 25,2019 ya kutembelea shamba la sukari la Bagamoyo linalomilikiwa na Kampuni ya Bakharesa kwa lengo la kujifunza kilimo na uzalishaji wa bidhaa hiyo ya sukari.
  Mkurugenzi Mkuu wa NSSF,William Erio (pichani kulia ) akimsikiliza Mkuu wa Mradi wa shamba hilo,Hosein Sufiani alipokuwa akieleza namna mbegu za miwa zinavyooteshwa ndani ya Kitalu,jana Machi 25,2019,ambapo Uongozi wa NSSF ulietembelea shamba la sukari la Bagamoyo lenye ukubwa wa Ekari 25,000 linalomilikiwa na Kampuni ya Bakharesa kwa lengo la kujifunza kilimo na uzalishaji wa bidhaa hiyo.


  Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bw. William Erio akiagana na Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya Bakhresa, Bw. Said Salim Bakharesa ofisini kwake jana Machi 25,2019 jijini Dar,akiwa ameambatana na baadhi ya viongozi waandamizi wa shirika hilo (hawapo pichani),walipokwenda kumshukuru mara baada ya kumaliza ziara yao walioifanya leo asubuhi walipotembelea shamba la sukari la Bagamoyo linalomilikiwa na Kampuni ya Bakhresa kwa lengo la kujifunza kilimo na uzalishaji wa bidhaa hiyo ya sukari.

  Serikali kupitia Shirika la Hifadhi ya Jamii, NSSF na Jeshi la Magereza Tanzania, wapo katika hatua za mwisho za uanzishwaji wa mradi wa kiwanda cha sukari na shamba la miwa Morogoro Vijijini, eneo ambalo linamilikiwa na Jeshi la Magereza.NSSF kupitia kampuni yao tanzu ya Mkulazi imeamua kuliendeleza shamba hilo kwa kushirikiana na Jeshi la Magereza katika kujenga kiwanda kipya cha kuzalisha sukari, lengo likiwa ni kupunguza uhaba wa sukari nchini, pia kupunguza matumizi ya fedha za kigeni za kuagiza sukari nje ya nchi na kutoa ajira kwa wakazi wa eneo hilo.
  Picha ya Pamoja mara baada ya mazungumzo mafupi.
  Na Grace Semfuko-maelezo

  Serikali kupitia Shirika la Hifadhi ya Jamii, NSSF na Jeshi la Magereza Tanzania, wapo katika hatua za mwisho za uanzishwaji wa mradi wa kiwanda cha sukari na shamba la miwa Morogoro Vijijini, eneo ambalo linamilikiwa na Jeshi la Magereza

  NSSF kupitia kampuni yao tanzu ya Mkulazi imeamua kuliendeleza shamba hilo kwa kushirikiana na Jeshi la Magereza katika kujenga kiwanda kipya cha kuzalisha sukari, lengo likiwa ni kupunguza uhaba wa sukari nchini, pia kupunguza matumizi ya fedha za kigeni za kuagiza sukari nje ya nchi na kutoa ajira kwa wakazi wa eneo hilo.

  Akizungumza Wilayani Bagamoyo, Mkoani Pwani wakati alipotembelea shamba la sukari la Bagamoyo linalomilikiwa na Kampuni ya Bakharesa kwa lengo la kujifunza kilimo na uzalishaji wa bidhaa hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bw. William Erio, alisema mradi huo unalenga kuzalisha tani za sukari zisizopungua laki mbili kwa mwaka.

  Alisema pia katika mradi huo watazalisha umeme kwa kutumia mabaki ya miwa kiasi cha megawatt 20 kwa mwaka, kwa ajili ya matumizi ya kiwanda na kuuza TANESCO, kiasi hicho aliongezea kusema kitatokana na uzalisha wa miwa kwa tani milioni mbili kwa mwaka.

  “Sisi NSSF tunafahamu mahitaji makubwa ya sukari katika nchi yetu, Mradi huu mkubwa utaongeza sukari sokoni, lengo letu kubwa ni kuongeza ajira na kupunguza changamoto ya upatikanaji wa sukari nchini Tanzania,” alisema Bw. Erio.

  Kwa upande wake Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya Bakhresa, Bw. Said Salim Bakhresa, alizipongeza taasisi hizo za Serikali kwa hatua hizo na akawataka kuendelea kujifunza na kuonesha milango kuwa wazi wakati wowote.

  “Sisi Makampuni ya Bakhresa tupo wakati wote na tutawapa ushauri wa suala lolote mnalotaka kujifunza kwa kuwa tunajenga Taifa moja kiuchumi, milango ipo wazi” alisema, Bw. Bakhresa.

  Bw. Bakhresa ni mwendeshaji wa shamba la miwa ya kufua sukari la Bagamoyo, lenye Hekta elfu kumi lililopo katika eneo la Makurunge, nje kidogo ya mji mkongwe wa Bagamoyo, ambalo lilianza shughuli zake za kilimo cha miwa kwa majaribio mwaka 2018 na kufanikiwa kuvuna tani 864 za miwa kwa ajili ya uzalishaji wa sukari.

  Mwezi Oktoba 6, mwaka 2017, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli, mara baada ya kufungua kiwanda cha vinywaji baridi cha Bakhresa,aliipatia kampuni hiyo shamba hilo kwa ajili ya kuwekeza kwenye kilimo cha miwa, ili kuondokana na changamoto ya upatikanaji wa bidhaa hiyo.

  Katika kipindi cha mwaka 2016/2017 mahitaji ya sukari yalikuwa tani 590,000 na kati ya hizo tani 135,000 zilikuwa ni mahitaji ya viwandani na tani 455,000 mahitaji ya kawaida ya binaadamu, ambapo uzalishaji wa sukari nchini ulikuwa tani 350,846 na kuwepo na upungufu wa tani 259,156; hatua iliyoifanya Serikali kuwezesha sekta binafsi katika kuzalisha bidhaa hiyo, na hivyo kiwanda cha Bakhresa pekee kinatarajia kuzalisha tani laki moja za sukari ifikapo mwaka 2022.

  0 0

  Na Sultani Kipingo
  Mchezaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Peter Tino leo amekabidhiwa shilingi Milioni 5 alizopewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutambua mchango wake kwa Timu ya Taifa ya mwaka 1980 ambayo ilifuzu kuingia fainali Michuano ya Soka Barani Afrika (AFCON).

  Mchezaji Peter Tino ndiye aliyefunga goli lililoiwezesha Tanzania kuingia fainali hizo na tangu mwaka huo wa 1980 Tanzania haikuwahi kufanikiwa tena kuingia hatua hiyo mpaka mwaka 2019 ikiwa ni miaka 39 imepita.

  Peter Tino alialikwa Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 25 Machi, 2019 wakati Rais Magufuli alipokutana na kuwapongeza wachezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) ambao jana waliifunga Timu ya Taifa ya Uganda (The Cranes) na kufanikiwa kufuzu kucheza fainali za AFCON 2019 zitakazofanyika baadaye mwezi Juni 2019 huko Misri.

  Pamoja na kupatiwa shilingi Milioni 5, Peter Tino pia ameunganishwa katika zawadi ya kupatiwa kiwanja Jijini Dodoma kwa kila mchezaji wa Taifa Stars iliyotolewa na Rais Magufuli ambapo naye atapatiwa kiwanja cha kujenga nyumba.

  Peter Tino ameziweka pesa hizo katika akaunti yake ya Benki ya CRDB aliyoifungua mara tu baada ya kutoka Ikulu na kukabidhiwa kadi yenye taarifa zake za benki (ATM).

  “Hakika Mungu ni mkubwa” amesema Peter Tino baada ya kupokea kadi yake ya Benki kwa Meneja Biashara wa Tawi la CRDB la Azikiwe, Bw. George Yatera, akishuhudiwa na Afisa kutoka kutoka TFF Bw. John Michael Mashaka. “Hela hii sikuiota hata ndotoni na mradi Raisi wetu mpendwa John Pombe Magufuli kanikumbuka hakika sintomwangusha. Yaani nitakwenda kumalizia kibanda changu kule Morogoro, ” aliongezea.

  Afisa wa Benki hiyo Bi. Gloria Kaale ndiye aliyemsajili mchezaji huyo ambaye wadogo zake, Gebbo Peter na Emma Peter, nao walitikisa anga za soka nchini kwa nyakati tofauti siku za nyuma kabla ya na wao kustaafu. Familia yao kwa sasa inaishi Morogoro.

  Kwa mujibu wa kumbukumbu zilizopo, ilikuwa ni Agosti 26,1979 wakati timu ya soka ya Taifa, Taifa Stars ilipokuwa ikirudiana na timu ya soka ya Taifa ya Zambia katika mechi ya michuano ya kuwania kufuzu kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika za mwaka 1980 zilizofanyika nchini Nigeria.Pambano hilo lilichezwa mjini Ndola.

  Mechi hiyo ilikuwa na umuhimu mkubwa kwa Taifa Stars kwa vile ilikuwa ikihitaji sare ya aina yeyote ili iweke historia ya kufuzu kucheza fainali hizo kwa mara ya kwanza , tangu ilipoanza kushiriki michuano hiyo mwaka 1968. Katika mechi ya kwanza iliyochezwa wiki mbili nyuma kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Taifa Stars iliishinda Zambia bao 1-0. Bao hilo lilifungwa na kiungo Mohammed Rishard Adolph.

  Ushindi huo ulipatikana kwa mbinde kiasi kwamba mashabiki wengi hawakuwa na imani iwapo Taifa Stars ingeshinda ama kupata sare katika mechi ya marudiano. Na hivyo ndivyo ilivyokuwa kwani Wazambia walifanikiwa kupata bao la kuongoza dakika za mapema na kudumu nalo kwa takriban dakika 86.

  Zikiwa zimesalia dakika tatu pambano hilo kumalizika, mshambuliaji mrefu mwenye kasi na mashuti makali, Peter Tino alibadili sura ya mchezo na kufanya kile kilichokuwa kikisubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa mchezo huo nchini.

  Ilipigwa kona kwenye lango la Taifa Stars, kipa Juma Pondamali akaupangua mpira kwa ngumi, ukamkuta kiungo Leodegar Tenga, aliyetoa pasi ndefu kwa kiungo mwenzake, Hussein Ngulungu, ambaye naye alitoa pasi ndefu kwa Tino.

  Akiwa amezungukwa na mabeki watatu wa Zambia, Tino alilazimika kupiga hesabu za haraka haraka. Aliwachomoka mbio mabeki nao na kukimbia na mpira kwa kasi. Alipofika nje kidogo ya eneo la hatari la Zambia, alifumua shuti kali la mguu wa kulia, lililompita kipa Shileshi wa Zambia na mpira kutinga wavuni.Bao hilo lilipatikana baada ya pasi tatu.

  Katika mechi hiyo, Taifa Stars iliwakilishwa na kipa Juma Pondamali,mabeki ni Leopard Tasso, Mohammed Kajole/ Ahmed Amasha, Salim Amir, Jella Mtagwa, viungo ni Leodegar Tenga, Hussein Ngulungu na washambulaji ni Omari Hussein, Peter Tino, Mohamed Salim na Thuweni Ally.

  Kikosi hicho kilikuwa chini ya Kocha Slowmir Work kutoka Poland, akisaidiwa na Wazawa Joel Bendera na Ray Gama (ambao kwa sasa wote ni marehemu), ndicho kilichoiwakilisha Tanzania katika fainali za kombe hilo zilizofanyika nchini Nigeria.

  Katika fainali hizo, Taifa Stars ilichapwa mabao 3-1 na wenyeji Nigeria katika mechi ya ufunguzi, ilitoka sare ya mabao 2-2 na Ivory Coast kabla ya kuchapwa mabao 2-1 na Misri na kutolewa hatua ya makundi.

  Hiyo ilikuwa ni miaka 39 iliyopita ambapo hivi sasa, baada ya kuichapa Uganda mabao 3-0 Jumapili, kila Mtanzania ameweka matumaini kwenye kikosi hicho kipya kilicho chini ya kocha kutoka Nigeria, Emmanuel Amunike.
    Mchezaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Peter Tino akikamilisha kufungua akaunti ili aweke shilingi Milioni 5 leo alizopewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutambua mchango wake kwa Timu ya Taifa ya mwaka 1980 ambapo goli lake liliiwezesha Tanzania kufuzu fainali ya Michuano ya Soka Barani Afrika (AFCON). Wanaoshuhudia ni Meneja Biashara wa Tawi la CRDB la Azikiwe, George Yatera na Afisa kutoka kutoka TFF John Michael Mashaka. Kushoto ni Afisa wa Benki hiyo Bi. Gloria Kaale ambaye ndiye aliyemfungulia akaunti nyota huyo wa zamani.
   Mchezaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Peter Tino akielekezwa na Meneja Biashara wa Tawi la CRDB la Azikiwe, Bw. George Yatera namna na kutumia kadi yake ya ATM baada ya kukamilisha kufungua akaunti ili aweke shilingi Milioni 5 alizopewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutambua mchango wake kwa Timu ya Taifa ya mwaka 1980 ambapo goli lake liliiwezesha kufuzu fainali ya Michuano ya Soka Barani Afrika (AFCON). Kushoto ni Afisa wa Benki hiyo Gloria Kaale
   Mchezaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Peter Tino akikabidhiwa kadi yake ya ATM kutoka kwa Meneja Biashara wa Tawi la CRDB la Azikiwe, Bw. George Yatera baada ya kukamilisha kufungua akaunti ili aweke shilingi Milioni 5 alizopewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutambua mchango wake kwa Timu ya Taifa ya mwaka 1980 ambapo goli lake liliiwezesha kufuzu fainali ya Michuano ya Soka Barani Afrika (AFCON). Wanaoshihudia ni Afisa kutoka kutoka TFF Bw. John Michael Mashaka na Afisa wa Benki hiyo Bi. Gloria Kaale ambaye ndiye.
   Mchezaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Peter Tino akionesha kadi yake ya ATM baada ya kukamilisha kufungua akaunti ili aweke shilingi Milioni 5 alizopewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutambua mchango wake kwa Timu ya Taifa ya mwaka 1980 ambapo goli lake liliiwezesha kufuzu fainali ya Michuano ya Soka Barani Afrika (AFCON).
  Mchezaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Peter Tino akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kumzawadia shilingi Milioni 5 kwa kutambua mchango wake kwa Timu ya Taifa ya mwaka 1980 ambapo goli lake liliiwezesha Tanzania kufuzu fainali ya Michuano ya Soka Barani Afrika (AFCON) wakati Rais Magufuli alipokutana na kuwapongeza wachezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) ambao jana waliifunga Timu ya Taifa ya Uganda (The Cranes) na kufanikiwa kufuzu kucheza fainali za AFCON 2019 zitakazofanyika baadaye mwezi Juni 2019 huko Misri.

  0 0

   Mkulima wa mananasi mwenye maskani yake, Bagamoyo, mkoani Pwani, Ambari Zuberi Kingwamba, amekabidhiwa fedha zake alizoshinda kutoka Biko, bahati nasibu ya Watanzania inayotoa ushindi mkubwa, ambapo alinyakua sh milioni tano kutoka kwenye bahati nasibu hiyo ya aina yake. Kulia ni Mratibu Msaidizi wa Biko, Hassan Ahmed. P
   Mshindi wa sh milioni tano kutoka kwa waendeshaji wa mchezo wa kubahatisha wa Biko, Ambari Zuberi Kingwamba wa Bagamoyo mkoani Pwani, anayejihusisha na ukulima wa mananasi, amekabidhiwa fedha zake leo tayari kwa kuziingiza kwenye matumizi yake ya kila siku ili kuinua uchumi wake. Picha na Mpigapicha Wetu.


  0 0


  Shirika lisilo la Kiserikali The Voice of Marginalized Community (TVMC) Shinyanga kwa kushirikiana na Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo SIDO limeendesha mafunzo ye kutengeneza Batiki kwa vikundi vya wazazi kutoka kata ya Chamaguha Manispaa ya Shinyanga.

  Mafunzo hayo ya siku nne yalianza Machi 21 na kumalizika Machi 25,2019 katika ukumbi wa SIDO mkoa wa Shinyanga kwa kukutanisha washiriki 25 yakiwa na lengo la kuwakwamua kiuchumi,kuondokana na umaskini ili kuzuia mimba na ndoa za utotoni sambamba na kuanzisha viwanda vidogo vidogo.

  Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo,Mgeni Rasmi ambaye ni Afisa Maendeleo ya Jamii mkoa wa Shinyanga,Glory Mbia alilipongeza shirika la TVMC kumsaidia Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli kutengeneza viwanda.

  “TVMC mmeonesha kwa vitendo kuwa mnaunga mkono serikali ya Viwanda,tunawapongeza kwa kufanya kazi nzuri inayofuata matakwa ya serikali,tunaamini kuwa kupitia mafunzo haya,tutapata viwanda vidogo kutoka wajasiamali hawa na tunafurahi mmetoa mafunzo kwa kushirikiana na SIDO”,alieleza Mbia.Aidha alisema serikali itaendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo katika kuwainua kiuchumi wananchi huku akiwataka wajasiriamali kuomba mikopo kwenye halmashauri za wilaya ili kuendeleza shughuli zao.

  Kwa Upande wake,Mkurugenzi wa Shirika la TVMC, Musa Ngangala alisema mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa Kuzuia Mimba na Ndoa za Utotoni unaotekelezwa na TVMC kwa ufadhili wa shirika la Firelight Foundation la nchini Marekani.

  “Ili kufanikisha mradi huu,mwaka 2016 tulianzisha vikundi vya ujasiriamali kwa wazazi ili kuhakikisha tunawakwamua kiuchumi ili kuondokana na umaskini ambao huchangia kwa kiasi kikubwa mimba na ndoa za utotoni,na kwa muda wa siku nne tumetoa mafunzo ya kutengeneza batiki”,alieleza Ngangala.

  “Ili kuunga mkono kwa vitendo sera ya serikali ya Viwanda kupitia kwa Rais wetu Mpendwa Dkt. John Pombe Magufuli,Tunatarajia kuanzisha vyumba maalum kwa ajili ya shughuli ya utengenezaji batiki na tutatoa vitendea kazi vya kuanzia ili kuhakikisha vikundi hivi vinakuwa vya mfano katika Manispaa ya Shinyanga lakini mkoa kwa ujumla”,alisema Ngangala.

  Hata hivyo Ngangala alisema TVMC itaendelea kutoa mafunzo ya aina mbalimbali ili kuwapa ujuzi wananchi wafanye shughuli za ujasiriamali ikiwa ni katika kuwaletea maendeleo wananchi.Mara baada ya mafunzo ya Utengenezaji Batiki kumalizika,umefanyika uzinduzi wa batiki za kwanza kutengenezwa kata ya Chamaguha kupitia TVMC.

  Mgeni Rasmi ambaye ni Afisa Maendeleo ya Jamii mkoa wa Shinyanga,Glory Mbia akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya kutengeneza Batiki kwa vikundi vya wazazi kutoka kata ya Chamaguha Manispaa ya Shinyanga yaliyoendeshwa na SIDO kwa ufadhili wa Shirika lisilo la Kiserikali The Voice of Marginalized Community (TVMC). Kushoto ni Meneja wa SIDO mkoa wa Shinyanga,Hopeness Elia,kulia ni Mkurugenzi wa TVMC,Musa Ngangala. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
  Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali The Voice of Marginalized Community (TVMC),Musa Ngangala akielezea lengo la kutoa mafunzo ya utengenezaji batiki kwa vikundi vya wazazi katika kata ya Chamaguha. Meneja wa SIDO mkoa wa Shinyanga,Hopeness akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya kutengeneza batiki kwa vikundi vya wazazi kata ya Chamaguha katika manispaa ya Shinyanga.
  Kushoto ni Meneja wa SIDO mkoa wa Shinyanga,Hopeness na Afisa Maendeleo ya Jamii mkoa wa Shinyanga,Glory Mbia wakiwa wameshikilia batiki iliyotengenezwa na vikundi vya wazazi kutoka kata ya Chamaguha wakati wa uzinduzi wa batiki za kwanza kutengenezwa kata ya Chamaguha kupitia TVMC.Kulia ni Mkurugenzi wa TVMC ,Musa Ngangala akifurahia batiki ya ukweli.

  Uzinduzi wa batiki za kwanza kutengenezwa kata ya Chamaguha kupitia TVMC ukiendelea.
  Uzinduzi wa batiki za kwanza kutengenezwa kata ya Chamaguha kupitia TVMC.Pichani ni miongoni mwa batiki zilizotengenezwa na wajasiriamali kutoka Chamaguha.
  Uzinduzi wa batiki za kwanza kutengenezwa kata ya Chamaguha kupitia TVMC ukiendelea.Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa shirika la PACESH, Perpetua Magoke aliyealikwa kushuhudia kazi ya wajasiriamali wa Chamaguha.
  Zoezi la utoaji vyeti kushiriki na kufuzu mafunzo ya utengenezaji batiki likiendelea.
  Utoaji vyeti ukiendelea.
  Washiriki wa mafunzo hayo wakitengeneza batiki.
  Utengenezaji batiki ukiendelea.
  Zoezi la kuchanganya rangi likiendelea.
  Batiki ikitolewa kwenye rangi.
  Picha ya pamoja washiriki wa mafunzo ya utengenezaji batiki. Picha ya pamoja. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

  0 0

  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe (kushoto) akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Morocco, Mhe. Nasser Bourita, baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa mkutano.

  Dkt. Mnyepe amemwakilisha Mhe. Prof. Palamagamba John Aidan Kabudi (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwenye mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Afrika kuhusu maamuzi ya Umoja wa Afrika (AU) kuunga mkono jitihada za usuluhishi wa mgogoro wa eneo la Sahara Magharibi kati ya Morocco na Saharawi uliofanyika jijini Marrakech, Morocco tarehe 25 Machi, 2019. 
  Katibu Mkuu, Dkt. Mnyepe akifuatilia mazungumzo na michango ya wajumbe kutoka nchi mbalimbali wakati wa mkutano huo. 
  Katibu Mkuu, Dkt. Mnyepe wa tatu kutoka kushoto, mstari wa nyuma, akiwa katika picha ya pamoja ya Mawaziri na Wawakilishi wa Mawaziri walioshiriki mkutano huo.

  0 0

  Na Margareth Chambiri

  Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inatarajia kufanya zoezi la uandikishaji wa Wapiga Kura kwa majaribio katika Kata mbili za Kibuta iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, Mkoani Pwani na Kihonda katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, Mkoani Morogoro.
  Taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Tume Jaji (Rufaa) Semistocles Kaijage Jijini Dar es Salaam leo (Jumanne Tarehe 26. 03. 2019) imesema Uandikishaji huo wa Majaribio utakaoanza Machi 29, hadi Aprili 04, 2019 utafanyika katika vituo 20 vya kuandikisha Wapiga Kura ikiwa ni vituo 10 katika kila Kata. 

  Taarifa hiyo imeeleza kuwa uandikishaji huo unalenga katika kuvifanyia majaribio vifaa na mfumo wa Uandikishaji Wapiga Kura ili kubaini changamoto kabla ya kuanza rasmi kwa zoezi hilo.

  Imezitaja sifa za watu watakaoandikishwa katika uandikishaji huo kuwa ni raia wa Tanzania aliyetimiza umri wa miaka 18 au atakayetimiza umri wa miaka 18 siku ya Uchaguzi Mkuu ujao.

  Aidha uandikishaji huo hautawahusu raia walio chini ya kiapo cha utii wa nchi nyingine, aliyebainika kuwa hana akili timamu au yuko kizuizini kama mhalifu mwenye ugonjwa wa akili au yuko kizuizini kwa ridhaa ya Rais.

  Taarifa hiyo imeendelea kutaja watu ambao hawatahusika katika majaribio hayo ya uboreshaji kuwa ni mtu aliyehukumiwa adhabu ya kifo na mahakama au anatumikia kifungo kinachozidi miezi sita pamoja na mtu aliyepoteza sifa za kuandikishwa kuwa Mpiga Kura chini ya Sheria za Uchaguzi au Sheria nyingine yoyote inayohusu makosa ya uchaguzi.

  Tume ya Taifa ya Uchaguzi pia inawajulisha wakazi wa Kata hizo zinazofanya Uandikishaji wa Majaribio na ambao walijiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mwaka 2015 kuwa wanaweza kutumia fursa hiyo kuhakiki taarifa zao katika vituo walivyojiandikishia.

  Wakati huo huo Tume inatoa fursa kwa Vyama vya Siasa kuweka Wakala mmoja katika kila kituo cha Kuandikishia Wapiga Kura kwa lengo la kushuhudia na kujiridhisha juu ya taratibu zitakazotumika pamoja na changamoto zitakazojitokeza ili ziweze kupatiwa ufumbuzi kabla ya zoezi rasmi la Uandikishaji.

  Tume imevitaka Vyama vyenye nia ya kuweka Mawakala katika uandikishaji huu wa Majaribio kuwasilisha orodha ya majina ya Mawakala na vituo walivyopangiwa kwa Maafisa Waandikishaji wa Halmashauri za Kisarawe na Manispaa ya Morogoro.

  Kadhalika Vyama vimetakiwa kuwasilisha nakala mbili za barua za utambulisho zikiwa na picha mbili na nakala mojawapo kati ya Kitambulisho cha Taifa au Kadi ya Mpiga Kura, Pasi ya Kusafiria au Leseni ya Udereva na kwamba kila Chama kitagharamia Wakala wake.

  Kwa mujibu wa taarifa hiyo wakati wa uandikishaji huo wa majaribio Tume ya Taifa ya Uchaguzi itatumia runinga, redio, mitandao ya kijamii na magari ya matangazo kwa ajili ya kutoa Elimu ya Mpiga Kura ili kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi na kushiriki katika zoezi hilo.

  Mwenyekiti wa Tume Mheshimiwa Kaijage kupitia taarifa hiyo amewaomba wakazi wa Kata za Kibuta na Kihonda kujitokeza kwa wingi katika Uandikishaji huo wa majaribio na kutoa ushirikiano kwa Tume wakati wote wa utekelezaji wa jukumu hilo muhimu kwa mustakabali wa demokrasia ya Taifa.

  Tume ya Taifa ya Uchaguzi hufanya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa mujibu wa Ibara ya 74 (6) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoipa Tume mamlaka ya kusimamia na kuratibu uandikishaji wa Wapiga Kura katika Uchaguzi wa Rais na Wabunge wa Jamhuri ya Muungano pamoja na Madiwani kwa Tanzania Bara.

  Tume kwa mujibu wa Kifungu cha 15(5) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi Sura ya 343 na Kifungu cha 21(5) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa Sura ya 292 inapaswa kuboresha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mara mbili kati ya Uchaguzi Mkuu mmoja na unaofuata.

  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Iringa mjini Richard Kasesela ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye uzinduziwa duka jipya la Tigo lililopo mtaa wa Miomboni mjini Iringa, akikata utepe kuashiri uzinduzi rasmi wa duka hilo litakalokuwa na uweza wa kuwahudumia wateja wengi zaidi. 
   1Mkuu wa wilaya ya Iringa mjini Richard Kasesela ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa duka jipya la Tigo lililopo mtaa wa Miomboni mjini Iringa, akiwatubia wananchi waliofika katika uzinduzi wa tawi hilo linaloweza kuwahudumia wateja wengi Zaidi kwa wakati mmoja
   Mkuu wa wilaya ya Iringa mjini Richard Kasesela ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye uzinduziwa duka jipya la Tigo lililopo mtaa wa Miomboni mjini Iringa, akiwa na Abbas Abrahmani ambaye ni Meneja wa Tigo kanda ya Kusini pamoja na Laverty Khana ambaye ni Meneja Huduma kwa Wateja kanda ya Kusini  muda mfupi kabla ya uzinduzi rasmi wa duka hilo 
   : Mgeni rasmi kwenye tukio la uzinduzi wa duka jipya la Tigo lililipo mtaa wa Miomboni mjini Iringa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mjini Richard Kasesela (wa kwanza kulia) akipata maelekezo kutoka kwa wafanyakazi wa Tigo namna wanavyohudia wateja.
  Waandishi wa habari wakichukua matukio mbali mbali ikiwamo hotuba ya mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Iringa mjini Richard Kasesela kwenye uzinduzi wa duka jipya la Tigo lililopo mtaa wa Miomboni mjini Iringa.


  Kampuni ya Tigo leo imezindua duka jipya la huduma kwa wateja lililopo Iringa mjini ambalo litarahisisha upatikanaji wa huduma kwa wateja wake wa eneo la Iringa mjini na maeneo ya jirani.

  Akizungumza wakati wa uzinduzi wa tawi hilo Mkurungezi wa kanda ya Kusini wa Tigo, Henry Kinabo, amesema tawi hilo jipya lililopo mtaa wa Miyomboni, ni sehemu ya mkakati wa kampuni hiyo kuwafikishia wateja wake huduma zake karibu zaidi.

  Kinabo alisema duka hilo litahudumia wateja zaidi ya 100 kwa siku kwa kuwapa huduma mbalimbali za Tigo ikiwemo huduma ya kuunganishwa na intaneti, usajili wa laini za simu, Tigo Pesa na huduma za simu janja.

  “Duka hili lina manufaa makubwa kwa wateja kwa sababu imepeleka huduma zetu kuwa karibu zaidi na wao. Pia linapatikana sehemu nzuri inayofikika kirahisi kiasi kwamba litavutia wateja wengi kutoka maeneo jirani. Tumebadilisha pia muonekano wa duka letu kuwa mzuri zaidi, na kuongeza pia nafasi ili kuweza kuwahudumia wateja wengi zaidi kwa wakati mmoja,” alisema.

  Aliongeza, “Kupitia duka letu hili lililoboreshwa, wateja watapata pia promosheni zetu mbali mbali kama; 4G+, App ya Tigo Pesa, promosheni ya CASH IN kwa mawakala, pamoja na simu mpya za S10 na S10+.” 

  Duka hili limetenga pia sehemu maalum ya uuzaji wa bidhaa mbalimbali kama simu janja ambapo mteja anaruhusiwa kuzijaribu kabla ya kununua. “Hii inamuwezesha mteja kufanya uamuzi sahihi kabla ya kununua, hivyo huchagua na kununua aina ya simu inayokidhi mahitaji yake.”

older | 1 | .... | 1824 | 1825 | (Page 1826) | 1827 | 1828 | .... | 1896 | newer