Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 180 | 181 | (Page 182) | 183 | 184 | .... | 1897 | newer

  0 0


  0 0
  0 0

  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wakazi wa Mbeya mjini, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jioni hii katika Uwanja wa Rwanda Nzovwe, wilaya ya Mbeya mjini, ikiwa ni mkutano wa kuhitimisha ziara yake katika mkoa huo, ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia ya kuzitatua.
   Katibu NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akihutubia maelfu ya wananchi wa Mbeya, katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo jioni katika Uwanja wa Rwanda Nzovwe, wilaya ya Mbeya mjini, ikiwa ni mkutano wa kuhitimisha ziara yake katika mkoa huo, ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia ya kuzitatua.

   Sehemu ya Wakazi wa jiji la Mbeya wakishangilia jambo wakati Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye alipokuwa akihutubia,katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo jioni katika Uwanja wa Rwanda Nzovwe, wilaya ya Mbeya mjini, ikiwa ni mkutano wa kuhitimisha ziara yao katika mkoa huo
   Wafuasi wa chama cha CCM,wakishangweka kwa nderemo na vifijo kabla ya kuwasili Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana katika  Uwanja wa Rwanda Nzovwe, wilaya ya Mbeya mjini, ikiwa ni mkutano wa kuhitimisha ziara katika mkoa huo
   Pichani kati ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana pamoja na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye wakiwapungia mikono wakazi wa jiji la Mbeya waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa hadhara wa CCM,uliofanyika katika uwanja wa Rwanda Nzovwe,nyuma ni Katibu wa NEC,Siasa na mahusiano ya Kimataifa Dkt.Asharose Migiro.
    Pichani kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa kwenye Bajaj huku akiwapungia mkono baadhi ya Wananchi na Wanachama wa CCM,waliokuwa wamejipanga barabarani kushuhudia tukio hilo la aina yake wakati Ndugu Kinana akiwa ameambatana na msululu wa Bajaji akielekea kwenye mkutano wa hadhara,anaekimbia pichani kulia ni Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi Nape Nnauye .
   Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt.Asharose Migiro akiwapungia mkono baadhi ya Wananchi na Wanachama wa CCM,waliokuwa wamejipanga barabarani kushuhudia tukio hilo la aina yake wakati Ndugu Kinana akiwa ameambatana na msululu wa Bajaji akielekea kwenye mkutano wa hadhara
  Baadhi ya Wadau wakifuatili mkutano huo wa hadhara.
   Sehemu ya umati wa wakazi wa jiji la Mbeya wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipokuwa akihutubia leo jioni kwenye uwanja wa Ruanda Nzovwe,mkoani Mbeya.


  0 0

  Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando, (Katikati) akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) baada ya kumtangazi Rashid Jacob Kagomola, mkaazi wa Bukoba mkoani Kagera, kama mshindi wa pili wa tiketi mbili na safari ya kwenda kuangalia mechi ya klabu ya Manchester United moja kwa moja (live) nchini Uingereza kwenye uwanja wa Old Trafford wakati wa droo ya wiki ya pili ya ‘Mimi Ni Bingwa’ iliyochezeshwa jana. Kulia ni Ofisa Huduma Kwa Wateja Airtel Pamela Marinyo na Emmanuel Ndaki, Msimamizi Mwandamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha ya Tanzania.
  Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando, (Katikati) akimpigia simu Rashid Jacob Kagomola, mkaazi wa Bukoba mkoani Kagera, aliyeibuka mshindi wa pili wa tiketi mbili na safari ya kwenda kuangalia mechi ya klabu ya Manchester United moja kwa moja (live) nchini Uingereza kwenye uwanja wa Old Trafford wakati wa droo ya wiki ya pili ya ‘Mimi Ni Bingwa’ iliyochezeshwa jana. Kulia ni Ofisa Huduma Kwa Wateja Airtel Pamela Marinyo na Emmanuel Ndaki, Msimamizi Mwandamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha ya Tanzania.

  KAMPUNI ya mawasiliano ya Airtel imemtangaza Rashid Kagomola, mkazi wa Bukoba mkoani Kagera kama mshindi wa tiketi mbili na safari iliyolipiwa ya kwenda kuangalia moja kwa moja (live) mechi ya Ligi Kuu ya Uingereza katika uwanja wa Old Trafford.

  Kagomola alishinda safari hiyo wakati wa droo ya kila wiki ya promosheni ya ‘Mimi Ni Bingwa’ inayolenga kuwazawadia wateja waaminifu, iliyoingia katika wiki ya pili.
  Anakuwa mshindi wa pili wa tiketi baada ya Dickson Lyatuu kutoka mkoani Arusha, kuibuka mshindi wa kwanza.

  Akitangaza mshindi wa tiketi hiyo katika wiki ya pili, washindi wawili wa shilingi milioni 5 na washindi wanne wa shilingi milioni moja kila mmoja, Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando alisema washindi wote wa tiketi watapewa nafasi ya kuchagua mtu mmoja watakaesafiri nae kwenda Uingereza, kuangalia mechi ya Manchester United katika uwanja wa Old Trafford.

  “Tunafuraha kutangaza kuwa mshindi wetu wa tiketi ya kweneda Old Trafford wa droo yetu ya pili ya promosheni ya ‘Mimi Ni Bingwa’ kuwa ni Rashid Jacob Kagomola atakaeungana na Bw. Dickson Lyatuu aliyeshinda tiketi ya kwanza na wengine 11 watakaojishindia tiketi baadae kwenda kuangalia mechi moja kwa moja (live) katika uwanja wa Old Trafford katika mwezi huu wa kwanza wa droo yetu.

  “Kagomola alichaguliwa baada ya namba ya mtu wa kwanza kujitokeza, kushindwa kupokea simu baada ya kumpigia mara tatu. Kwa maana hiyo napenda kumuasa kila aliyejisajili katika droo hii kujiweka tayari kupokea simu kutoka Airtel kwa sababu anaweza kuibuka mshindi,” alisema Mmbando.

  Aliwataja Godfrey David Msiu kutoka Arusha na Junior Ashery Pesambili, mkazi wa Arusha mjini kuwa washindi wa shilingi milioni tano kila mmoja wa wiki hii na wateja wengine wanne waliojishindia shilingi milioni moja kila mmoja. 

  Mmbando alisema kuwa bado zawadi nyingi zaidi kushindaniwa na kuongeza kuwa ili kushiriki katika promosheni hiyo mteja anatakiwa kutuma ujumbe mfupi (SMS) ukiwa na neon “BINGWA’ kwenda namba 15656.

  Alisema kuwa Airtel pia imeweka vituo maalum kwa ajili ya wapenzi wa Man U kuangalia mechi za Manchester United bure kupitia luninga kubwa, na kuyataja maeneo hayo kuwa, Mbeya – Shaba Pub, Mwanza – Shooters Pub, Dodoma – Four Ways, Dar es Salaam – Rose Garden, Morogoro – Nyumbani Lounge na mkoani Arusha ni Empire Sports Bar.

  Droo hiyo ilishuhudiwa na wawakilishi kutoka katika Bodi ya Michezo ya Kubahatisha ya Tanzania.

  0 0

  Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal akizindua rasmi kampeni ya mZinduka itakayowawezesha wananchi kujiunga na kupokea bure taarifa kuhusu Malaria kupitia simu za mkononi za mtandao wa Vodacom ambao pia ni wafadhali wa mradi huo kupitia Vodacom Foundation huku Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein Mwinyi (kushoto kwake) na Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim (wa kwanza kulia) wakishuhudia kwa karibu.Mbali na Vodacom kampeni hiyo inazihuisha pia Taasisi ya Malaria No More na Tanzania House of Talents(THT).
  Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein Mwinyi akiongea kwenye hafla ya uzinduzi wa kampeni ya mZinduka itakayowawezesha wananchi kujiunga na kupokea bure taarifa za Malaria kupitia simu za mkononi za mtandao wa Vodacom ambao pia ni wafadhali wa mradi huo kupitia Vodacom Foundation. Walioketi kutoka kulia ni Makamu wa Kwanza wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal, Mkurugenzi Mwanzilishi wa THTRuge Mutahaba na Ofisa Mkuu Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Georgia Mutagahywa. Kampeni hiyo inazihusisha pia Taasisi ya Malaria No More na THT.
  Makamu wa Rais Dk Mohamed Gharib Bilal akisalimiana na Mkuu wa Idara ya Miradi ya Kijamii wa Vodafone Laura Turkington wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni ya mZinduka itakayowawezesha wananchi kujiunga na kupokea bure taarifa za Malaria kupitia simu za mkononi za mtandao wa Vodacom ambao pia ni wafadhali wa mradi huo kupitia Vodacom Foundation.Kushoto ni Ofisa Mkuu Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Georgia Mutagahywa.
  Kundi la wasanii wa ngoma za kienyeji kutoka Nyumba ya Vipaji (THT) wakipamba hafla ya uzinduzi wa kampeni ya mZinduka itakayowawezesha wananchi kujiunga na kupokea bure taarifa za Malaria kupitia simu za mkononi za mtandao wa Vodacom ambao pia ni wafadhali wa mradi huo kupitia Vodacom Foundation. Mbali na Vodacom kampeni hiyo inahusisha pia Taasisi ya Malaria No More na THT.
  Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal(wa pili kushoto walioketi) na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein Mwinyi (wa pili kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Vodacom waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa kampeni ya mZinduka itakayowawezesha wananchi kujiunga na kupata bure taarifa za Malaria kupitia simu za mkononi za mtandao wa Vodacom ambao pia ni wafadhali wa mradi huo kupitia Vodacom Foundation. Wa kwanza kushoto ni Mwakilishi wa Malaria No More Lilian Madege na Mkurugenzi Mwanzilishi wa THT Ruge Mutahaba.

  0 0

  Leo tar 5 Dec ni siku ya hepi besdei ya kuzaliwa mai ankal Bahati a.k.a. Barbie ambaye anatimza miaka miwili. Mr & Mrs Bahati Singh pamoja na kaka na dada zake wanamtakia maisha marefu, afya njema, mafanikio mengi, mapenzi kwa wazazi wake na ibada kwa Allah. 
  Amen.

  0 0

  Rais Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na Ujumbe wa Wataalam kutoka Idara ya Afya ya Jimbo la Nanjing,nchini China,waliofika Ikulu Mjini Zanzibar,wakiongozwa na Kiongozi wao Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Afya Wang Hua,(wa pili kulia).Picha na REamadhan Othman Ikulu.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal katikati, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Kongamano la Kitaifa la Ajira kwa bara la Afrika mara baada ya kufungua kongamano hilo leo Disemba 5-2013 kwenye Ukumbi wa Mikutano ya Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Waziri wa kazi na Ajira Mhe. Gaudensia Kabaka mara baada ya kufungua kongamano la kitaifa la Ajira kwa bara la Afrika kwenye Ukumbi wa Mikutano ya Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam leo Disemba 5,2013. 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifungua Kongamano la Kitaifa la Ajira kwa bara la Afrika kwenye Ukumbi wa Mikutano ya Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam leo Disemba 5,2013.
  Baadhi ya washiriki wa kongamano la kitaifa la Ajira barani Afrika wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, alipokua akifungua Kongamano hilo leo Disemba 5,2013 katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalim Julius nyerere Dar es salaam. (Picha na OMR)

  0 0

  WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Krismasi Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, Desemba 25 mwaka huu.

  Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa Dar es Salaam leo na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama ilieleza kuwa maandalizi kuhusiana na tamasha hilo yanaenda vizuri.

  “Hamasa imekuwa kubwa pengine kuliko matamasha mengine ambayo Kampuni yangu ya Msama Promotions imewahi kuyaandaa. Waimbaji wanatamani siku ifike wafanye mambo, mashabiki nao wanatamani siku ifike waone mambo.

  “Pia nafurahi kuwajulisha kuwa Waziri Lukuvi amekubali kuwa mgeni rasmi Desemba 25 Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, naamini siku hiyo itakuwa burudani ya aina yake. Namshukuru sana kwa kuungana nasi,” alisema Msama, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi Tamasha la Pasaka.

  Alisema kiingilio cha chini katika tamasha hilo kwa upande wa Uwanja wa Taifa kitakuwa sh. 5000 na viingilio vingine vitakuwa sh 10,000 na sh.20,000 kwa majukwaa maalum A na B.

  “Pia watoto watachangia sh. 2,000, tumeweka viingilio vya kawaida ili wote tuweze kuhudhuria Uwanja wa Taifa,” alisema Msama na kuongeza kuwa kwa mikoani viingilio ni sh 5,000 kwa wakubwa na watoto itakuwa Sh 2,000.

  Waandaaji hao wamepanga tamasha hilo lifanyike Desemba 25 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na siku inayofuata Uwanja wa Jamhuri, Morogoro, kisha Desemba 28 Uwanja wa Mkwakwani Tanga na Desemba 29 Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.

  0 0

  Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Njombe, Sanga (katikati) akimtambulisha Katibu wa NEC wa Siasa na Uhusiano wa Kimataifa wa CCM, ambaye pia ameteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kuwa Mbunge, Dk. Asha Rose Migiro wakati msafara wa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia) ulipowasili katika Kijiji cha Mfumbi wilayani Makete, Njombe kuanza ziara baada ya jana kumaliza ziara katika mikoa ya Ruvuma na Mbeya ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM.
  Kinana (kulia) akiwasalimia wananchi baada ya kuwasili katika Kijiji cha Ifumbi, akitokea mkoani Mbeya na kuanza ziara ya kikazi wilayani Makete, Njombe. Katikati ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye,shoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe,Mh.Deo Sanga
  Kinana akimkabidhi Mwenyekiti wa Vijana wa Tarafa ya Ikuwo, Tunsume Shemgogo ufunguo ikiwa ni ishara ya kukabidhi Trekta kwa vijana wa Mkoa wa Njombe kwa ajili ya kusaidia Kilimo.Trekta hilo limetolewa na CCM kwa vijana wa mkoa huo,aidha makabidhiano hayo yamefanyika leo kwenye kambi ya vijana iliyopo kweneye kijiji cha Mlengu,kata ya Kiangala,tarafa ya Ikuwo wilayani Makete,mkoani Njombe,ambapo kambi hiyo ina eneo la ekari 300 za mashamba,Ndugu Kinana aliahidi kutoa Trekta hilo wakati alipofanya ziara ya kikazi mkoani humo mnamo Agosti mwaka huu,baada ya kuelezwa jinsi vijana hao walivyojiunga pamoja katika kikundi na kuamua kujishughulisha na kilimo ili kujikwamua na suala zima la umaskini.

  Mkuu wa Wilaya ya Makete, Josephine Matiro (katikati) akielezea kuhusu mradi wa kilimo wa vijana wa Tarafa ya Ikuwo, wilayani Makete, wakati Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia), alipokabidhi msaada wa Trekta  la kuwasaidia vijana wa Mkoa wa Njombe katika kilimo.
  Kinana akihutubia wananchi muda mfupi kabla ya kukabidhi msaada huo wa trekta ambapo alisema kuwa trekta hilo litawasaidia vijana katika kilimo bila kujali itikadi za vyama,na kuongeza kuwa lengo la kutoa msaada huo wa trekta ni kutaka kuwawezesha vijana kufanya kazi kwa kujitegemea n¨badala kusububiri ajira,ambalo ni tatizo kubwa kwa vijana.

  Kinana akilima shamba la vijana wa Tarafa ya Ikuwo kwa kutumia trekta wakati wa makabidhiano yaliyofanyika katika Kijiji cha Mlengo, wilayani Makete mkoani Njombe leo jioni.
  Kinana akilima kwa kutumia treka shamba la Vijana 252 wa Tarafa ya Ikuwo lenye ukubwa wa ekari 300 muda mfupi kabla ya kuwakabidhi msaada huo wa Trekta lenye thamani ya sh. mil 42.
  Kinana akiungana na wakazi wa Ikuwo kucheza ngoma ya asili ya kabila la Wawanji katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Mlengu, Kata ya Ikuwo, Makete-
  Kinana akihutubia mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Mlengu, Ikuwo, wilayani Makete.
  Kinana (kulia), Dk. Asha Rose Migiro wakiangalia vyerehani vya kisasa walipotembelea Chuo cha Ufundi Stadi cha Makete-VETA
  Kinana akiongozwa na Mkurugenzi VETA Nyanda za Juu Kusini, Monica Mbele (kulia), na Mkuu wa Wilaya ya Makete, Josephine Matiro (kushoto) kutembelea chuo hicho cha VETA.
  Kinana na Ujumbe wake wakipata maelezo mafupi kutoka kwa Injinia Asifiwe Swalo,kuhusiana na moja ya mashine ya mbao kama ionekavyo pichani,inavyofanya kazi
  Injinia Asifiwe Swalo akielezea mashine mojawapo ya mbao inayofanya kazi ya kuchana mbao katika mianguko mbalimbali ikiwemo na kuweka urembo mbele ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na ujumbe wake mara baada ya kutembelea karakana ya ufundi Selemara.
  Mmoja wa waatalamu kutoka chuo hicho cha VETA,Abel Mbilinyi akielezea nama ya upimaji wa kiasi cha mfinyanzi uliopo kwenye Udongo,mbele ya Ndugu Kinana na Ujumbe wake.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishiriki kupanda mti nje ya eneo la chuo hicho cha VETA,kushoto kwake anaeshuhudia ni Mkurugenzi wa VETA nyanda za juu kusini,Bi.Monica Mbele.
  Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt.Asharose Migiro akishiriki upandaji miti nje ya eneo la chuo hicho cha VETA,mapema leo Wialayani Makete mkoani Njombe.
  Picha ya pamoja
  Pichani katini katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt.Asharose Migiro akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Makete,Mh. Josephine Matiro (kushoto) na  Mkurugenzi wa VETA nyanda za juu kusini,Bi.Monica Mbele.

  0 0

   Mwinjilisti wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Usangi Mwanga akisoma misa ya Kumuombea Marehemu Penina Philipo Msuya aliyefariki mjini Dar Es Salaam Mnamo tarehe 1 Disemba 2013 kwa ugonjwa wa Moyo na hatimaye kusafirishwa Hadi Kijijini Kwao Usangi Mwanga mkoani Kilimanjaro Juzi Jumanne kwaajili ya Mazishi yaliyofanyika Jana Jumatano
   Mmoja wa Ndugu wa Marehemu Penina Philipo Msuya akisoma historia fupi ya marehemu Penina wakati wa Misa ya Kumuombea iliyofanyika nyumbani kwa marehemu Usangi Mwanga Mkoa wa Kilimanjaro
   Baadhi ya Watoto, Ndugu na Jamaa wa marehemu Penina Philipo Msuya wakiwa na majonzi ya kumpoteza mama yao mpendwa wakati wa Misa ya kumsalia marehemu iliyofanyika jana kijijini kwao Usangi Mwanga Mkoa wa Kilimanjaro
   Baadhi ya Ndugu, Jamaa na Marafiki wa Familia ya Marehemu Penina Philipo Msuya wakitoa heshima zao za mwisho kabla ya kwenda makaburini kwaajili ya kuupumzisha kwa amani mwili wa Marehemu Penina Msuya.


   Baadhi ya Ndugu, Jamaa na marafiki wakiweka jeneza lenye mwili wa Marehemu Penina kwaajili ya kuupumzisha Katika Nyumba yake ya Milele.
  Baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki wa familia ya marehemu Penina Msuya waliohudhuria katika mazishi yaliyofanyika jana Jumatano Usangi Mwanga Mkoani Kilimanjaro.
  Watoto wa Marehemu Penina Philipo Msuya wakiweka Shada la Maua Juu ya Kaburi la Marehemu mama yao mpendwa wakati wa mazishi ya Marehemu Penina Philipo Msuya yaliyofanyika jana Usangi Mwanga Mkoani Kilimanjaro
   Mchungaji wa kanisa la KKKT Usharika wa Usangi akiweka shada la maua juu ya kaburi la Marehemu Penina Philipo Msuya wakati wa Mazishi yaliyofanyika jana Jumatano huko Usangi Mwanga Mkoa wa Kilimanjaro
  Baadhi ya Watoto, Ndugu, jamaa na marafiki wa Marehemu wakiwa katika picha ya kumbukumbu mara baada ya kumaliza kuweka mashada ya maua juu ya kaburi la Marehemu Mpendwa wao Penina Philipo Msuya.Picha na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog

  0 0


  Lt. Col. Ludwino Mgumba, (left) Deputy Commissioner General, Fire and Rescue Force; Gabriel Nderumaki (centre) Acting Managing Editor, State-owned Tanzania Standard Newspapers, publishers of Daily News, Habari Leo and Sport Leo newspapers;  and Imani Lwinga (right), Communications Manager , Serengeti Breweries Limited shares a right moment after being conferred with MA degrees in Mass Communication at St. Augustine University of Tanzania, Mwanza on November 30, 2013.


  Serengeti Breweries Limited Communications Manager Imani Lwinga (left) in jovial mood with Shukuru Senkondo (2nd right), Joseph Jackson Gahima (2nd  left) and Paul Gyuna (left) after being conferred with degrees of Master of Arts in Mass Communicatio.
   Imani Lwinga of Serengeti Breweries (left) with Shukuru Senkondo, Christina Njovu, Paul Gyuna and Joseph Jackson after getting their MA in Mass Communications
   St. Augustine Alumni Christina Njovu of National Electoral Commission, Wilson Malosha of Ministry of Indutry and Trade, Lt. Col. Ludwino Mgumba of Fire and Rescue Force, Shukuru Senkondo and media editor/consultant, Joseph Jackson Gahima of Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) and Imani Lwinga of Serengeti Breweries Limited after getting their MA degrees in Mass Communications
   Imani Lwinga (right) of Serengeti Breweries Limited, Wilson Malosha (centre) of Ministry of Industry and Trade and Christina Njovu of National Electoral Commission pose for a photo after receiving their MA degrees in Mass Communications at St. Augustine University of Tanzania in Mwanza on 30th November 2013.

  Lulu Musa (left) Information Officer in the Vice President’s office – Environment; Gabriel Nderumaki  (centre), Acting Managing Editor, Tanzania Standard Newspapers and Hoyce Temu, Communication Analyst at United Nations office in Tanzania pose for souvenir photo after receiving their MA degrees in Mass Communicatio.

  0 0


  TANZANIANS THANKS FOR YOUR VOTES –3 DAYS TO GO TO THE FINALE!
  now
  HISIA is among the 6 finalists!

  3 DAYS to go before East Africa’s favorite music reality show produces an East African star for the 6th time through Tusker.
  You have a say on who takes the grand price home.  Our Tanzanian representative HISIA depends on your votes to win.

  EVERY SINGLE VOTE COUNTS!

  HOW TO VOTE
  a)      Create your account on https://tusker.mobi/register to have a say on who wins the grand price ( ONE VOTE PER DAY)

  Or

  b)      SMS the words Tusker12 to the number 15324 ( 5 SMS PER PERSON PER DAY)

  ITS YOUR TIME TO TAKE THE STAGE / UZALENDO MBELE!

  0 0

  Meneja Uhusiano wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI) Bw. Jumaa Almasi akieleza kwa waandishi wa Habari (hawapo pichani) Mipango mbalimbali ya Taasisi hiyo ikiwamo utekelezaji wa awamu ya tatu ya MOI (MOI Phase III) itakayosaidia kuboresha huduma za afya nchini,kulia ni Afisa Uhusiano wa Taasisi hiyo Bw. Patrick Mvungi na kushoto ni Afisa Habari wa Idara ya Habari(MAELEZO) Bw. Frank Mvungi.

  Meneja Uhusiano wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI) Bw. Jumaa Almasi akionesha kwa waandishi wa Habari (hawapo pichani) Picha ya sehemu ya kichwa iliyowekewa kifaa maalum(Mayfield Clamp). kulia ni Afisa Uhusiano wa Taasisi hiyo Bw. Patrick Mvungi.  Na Frank Mvungi
  Taasisi yaTiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI) imepanga kutumia zaidi ya Bilioni 17 katika ujenzi wa awamu ya Tatu ya Mradi wa Taasisi yaTiba ya Mifupa   na Mishipa ya Fahamu (MOI phase 111) hadi mradi huo utakapokamilika mapema mwakani.

  Hayo yamesemwa leo na Meneja Uhusiano wa Taasisi hiyo Bw. Jumaa Almasi wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.

  Almasi alisema kuwa Ujenzi wa jengo hilo jipya lenye ghorofa 7 ambao unaendelea ukikamilika utaongeza maeneo ya kutolea huduma,Vitanda vitafikia 380 kutoka 159 vilivyopo sasa hali ambayo itapanua wigo wa huduma zinazotolewa kwa sasa.

  “Mradi huu utasaidia kuongeza ufanisi na huduma zinazotolewa na taasisi kwani ukikamilika utaongeza maeneo ya kutolea huduma kwa kupunguza msongamano wa wagonjwa mawodini kutokana na kuongezeka kwa vitanda kutoka 159 hadi kufikia 380” Alisema Almasi.

  Aliongeza kuwa huduma nyingine zitakazotolewa  ni CT SCAN,MRI,huduma za Cybernife na Digital Antiograph ambazo kwa Sasa hazitolewi katika Taasi  hiyo .Alibainisha kuwa MOI ni moja ya Taasisi  zenye vifaa bora vya upasuaji pamoja na vyumba vya upasuaji vinavyokikidhi viwango vya kimataifa kusini mwa jangwa la Sahara baada ya Afrika ya kusini.

  Alisema kuwa hali hiyo ni matokeo ya juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali katika kuboresha huduma za afya nchini ambapo wameweza kupatiwa vifaa vya kisasa pamoja na wataalamu waliobobea katika  huduma za tiba ya mishipa ya fahamu na upasuaji wa uti wa mgongo.


  Bw. Almasi  alibainisha kuwaTaasisi ya MOI imeendelea kushirikiana na Taasisi za Kimataifa  zinazotoa huduma za afya kama SIGN GROUP  ya nchini Marekani  ambayo imekuwa ikitoa msaada wa vifaa tiba ikiwa ni alama ya ushirikano mzuri uliopo kati ya Taasisi hiyo na mashirika ya Kimataifa.

  0 0

   Mkuu wa Kitengo cha Affluent Banking wa benki ya Barclays Tanzania Ms
  Neema Rwehumbiza akiongea na waandishi wa habari waliofika katika ofisi za Benki hiyo katika tawi lililopo Alpha House barabara ya Ali hassan Mwinyi kwaajili ya kushuhudia washindi wa Droo ya Pili ya "Double your Saving"kutoka benki ya Barclays
   Mmoja wa Wafanyakazi wa Benki ya Barclays tawi la Alpha house Barabara  ya Ali Hassan Mwinyi akizungusha pipa lenye kuponi za washiriki wa droo ya pili ya  "Double Your Saving" kwaajili ya kupata washindi wa tano wa Mwezi November, huku  akiongozwa na afisa kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha
   Mkuu wa Kitengo cha Affluent Banking wa benki ya Barclays Tanzania Ms
  Neema Rwehumbiza akisoma jina la Mshindi wa Kwanza aliyepatikana mara baada ya  pipa hilo kuzungushwa katika droo ya pili ya "Double your saving' kutoka Benki ya Barclays Tanzania iliyochezeshwa leo katika Ofisi ya Benki hiyo katika tawi lililopo barabara ya Ali Hassani Mwinyi
  Mmoja wa Wafanyakazi wa Benki ya Barclays tawi la Alpha house Barabara
  ya Ali Hassan Mwinyi akichukua moja ya kuponi za washiriki wa droo ya pili ya "Double your Saving" kwaajili ya kumtaja mshindi wa Pili katika droo iliyochezeshwa leo na Kupelekea kupatikana kwa washindi watano ambao kila Mmoja ataondoka na Kitita Cha shilingi Milioni Moja

  0 0

  MUONGOZAJI bora wa filamu Swahiliwood Jackson Kabirigi ‘Jack’ anawashukru wadau wote wa tasnia ya filamu kwa ujumla wake kutokana na mchango wake ambao wamempa kupitia kazi zake ambazo ameshiriki katika kuigiza na kuongoza sambamba na filamu ya Mdundiko iliyomletea sifa baada kuchaguliwa nchini Marekani.

  Akiongea na wanahabari msanii huyo ambaye ana sifa za kimataifa amesema kuwa baada ya filamu yake ya Mdundiko kushinda tuzo nje ya nchi na si ndani ya nchi ambapo hata tuzo za ZIFF ilinyimwa, lakini Jack anasema kuwa amejifunza mengi na anatoa shukrani kwa wadau wa filamu ambao wamekuwa bega kwa bega katika kuhakikisha anasonga mbele kisanaa.

  “Nawashukru wote wanahabari jamaa zangu hata wale ambao wamekuwa wakinishauri kupitia njia mbalimbali, kila mtu kwangu ana mchango mkubwa sana naheshimu hilo kwa kila mtu kwa nafasi aliyo nayo na kuhakikisha wanafanya jambo kubwa kwa ajili yangu mimi Jack nasema Asanteni sana na Mungu awabariki,”anasema Jack.

  Aidha msanii huyo ameamua kuanzisha utaratibu wa kutoa taarifa za maendeleo ya kazi yoyote ambayo atakuwa akiifanya na taarifa kuwafikia wapenzi wa filamu nchini nzima na kuwa ndio njia ya wasanii kujenga mahusiano mema na watazamaji wao ambao kuna wanataka kujua maisha ya wasanii ya kawaida nje ya uigizaji lakini si rahisi.

  Jack pia anawashukru sana wapenzi wa filamu Swahiliwood baada ya kuipokea kazi yake vema ya Kisate filamu iliyoingia sokoni hivi karibuni na kufanya vizuri kwa kuteka soko la filamu Bongo, sinema hiyo kaongoza na kuigiza mwenyewe akishirikiana na wasanii wengine wakali kama Tino, Dino, Dennis, Mzee Magari, Hamis Korongo na wasanii wengine wanofanya vizuri.

  Msanii huyo ana filamu nyingi sana lakini yeye amechagua filamu kadhaa kuwatambulisha wanahabari na wadau wote kwa ujumla, sinema hizo ni  My Nephew, Money Transfer, filamu hizo kaigizia Afrika ya kusini, Born to Suffer, filamu ya Nunda, The Close, Home village,Ania.

  Filamu zingine  ambazo kaingiza na kuzingoza ni Filamu ya Hatia Nguvu ya Imani, CID, Single O, Kigodoro, Kisate na filamu bora ya Mdundiko hizi ni baadhi ya filamu ambazo zote zipo katika ubora wa juu na ameahaidi kufanya mambo makubwa mwaka ujao.

  Kazi nzuri ya Jack kutoka Bongo filamu yake aliyoongoza ya Mdundiko kuibuka kama filamu bora iliyofanikiwa katika kipengere cha mafanikio ya hadithi katika filamu (Achievement Narrative in Feature Film) ni ushindi mkubwa kwa mapinduzi ya filamu Bongo Movie. Huyu ndio Jackson Kabirigi muongozaji wa filamu wa Kimataifa 

  “NAWAPENDA SANA NAOMBA USHIRIKIANO HUU UENDELEE MIMI NI KIJANA WENU SITOWAANGUSHA KATIKA KULETA MAPINDUZI YA KWELI YA FILAMU TANZANIA MUNGU AWABARIKI NYOTE,” Jackson Kabirigi. 05.December. 2013

  0 0

  President Dr. Jakaya Mrisho Kikwete together with some heads of States from Africa who participated on the Roundtable meeting on Elephant and other endangered species held in Paris France this afternoon. 
  Others in the picture from left Commoro’s President Dr. Ikililou Dhoinine,(left), Cameroon President Paul Biya (Third left) The Host President Francois Hollande of France (fourth), Togolese President Faure Eyadema (fifth), Gabon’s President Ally Bongo (second right), and right is Ivory Coast’s President Allasane Ouatarra. President Kikwete is in Paris for a working visit. Photos by Freddy Maro.

  0 0

  MBU_0840

  Sasa imezinduliwa rasmi.......Gari aina ya JEEP Grand Cherokee 2014 ni FWD System, 8 Speed Automatic with Electronic Shift, na Engen yake ni 5.7 V8.
  IMG_4288
  Mkurugenzi wa Biashara wa CFAO Motors, Bw.Charles-Edouard CAMBOURNAC akifafanua jinsi jinsi gari hiyo mpya aina ya JEEP Grand Cherokee 2014 inavyoweza kufanya kazi kwa Balozi wa Canada Nchini Tanzania, Alexandre Leveque.
  IMG_4294
  Picha juu na chini ni muonekano wa mbele na nyuma wa gari aina ya JEEP Grand Cherokee 2014.
  IMG_4299
  IMG_4324
  Mmoja wa wageni waalikwa akipewa maelezo jinsi gari hiyo mpya inavyofanya kazi na Mkurugenzi Mtendaji wa CFAO Motors.
  MBU_0856
  Mkurugenzi Mtendaji wa CFAO Motors Wayne McIntsoh na Meneja Masoko wa kampuni hiyo Tharaia Ahmed wakikagua gari mpya aina ya JEEP Grand Cherokee 2014 wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa gari hiyo.


  MBU_0832
  Maendeleo Dance Group wakitoa burudani ya aina yake kwa wageni waalikwa.
  IMG_4341IMG_4349
  Models waliopendezesha uzinduzi wa gari mpya aina ya JEEP Grand Cherokee 2014 katika pozi.
  IMG_4188
  Mkurugenzi Mtendaji wa Coca-Cola Kwanza Basil Gadzios akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya CFAO Motors Wayne McIntosh wakati wa uzinduzi rasmi wa gari mpya aina ya JEEP Grand Cherokee 2014 jijini Dar.
  IMG_4181
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya CFAO Motors Wayne McIntosh akibadilishana mawazo na baadhi ya wageni waalikwa wakati wa uzinduzi rasmi wa gari aina Jeep Grand Cherokee 2014.
  IMG_4088
  Meneja Masoko wa CFAO Motors Tharaia Ahmed akizungumza na Wanenguaji wa Maendeleo Dansi Group wakati wa kusheherekea uzinduzi wa gari mpya Grand Cherokee (JEEP) 2014 jijini Dar.
  IMG_4094
  Meneja Masoko wa CFAO Motors Tharaia Ahmed akizungumza na mmoja wa wadau kutoka Stanbic Bank wakati halfa fupi ya uzinduzi wa gari aina ya JEEP Grand Cherokee 2014.
  IMG_4176
  Timu ya Jack Daniels ilikuwepo kutoa huduma bure kwa wageni waalikwa.
  IMG_4103
  IMG_4115
  Maendeleo Dance Group wakitumbuiza.
  IMG_4237
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya CFAO Motors Wayne McIntosh akizungumza kwenye utambulisho rasmi wa gari jipya la Grand Cherokee (JEEP) 2014 wakati wa uzinduzi rasmi.
  Bw. McIntosh amesema gari hiyo imezinduliwa wakati kampuni ya CFAO Motors ikitimiza miaka 10 ndani ya soko la Tanzania ni gari ambayo inatumika muda wote wa hali ya hewa na nzuri wakati wa foleni na Teknolojia yake ni rahisi kutumia wakati wote wa safari katika jiji la Dar es Salaam.
  MBU_0807
  Pichani juu na chini ni wanenguaji kutoka Maendeleo Dance Group ambao walikuwa wakiburudisha wageni waalikwa kwenye uzinduzi huo.

  0 0

  Na. M. M. Mwanakijiji .

  Mpigania haki za weusi na alama kuu ya udhalimu wa mfumo wa Ubaguzi wa Rangi nchini Afrika ya Kusini Mzee Nelson ‘Madiba’ Mandela amefariki dunia baada yakuugua kwa muda mrefu kufuatia maambukizi ya mapafu kushindwa kutengemaa kwa muda sasa. Mzee Mandela ambaye kwa miezi kadhaa sasa amekuwa akisumbuliwa na matatizo ya maambukizi kwenye mapafu yake amefariki dunia nyumbani kwake ambako alipelekewa toka hospitali ya Moyo ya Mediclinic mjini Pretoria, chini Afrika ya Kusini baada ya familia yake kuomba kufanya hivyo. 

  Mzee Mandela alipelekwa hospitali hiyo Jumamosi ya tarehe 8 Juni ikiwa ni baada ya kuanza tena kusumbuliwa na mapafu; miaka ya themanini akiwa kifungoni Mandela alipata ugonjwa wa Kifua Kifuu (TB) kutokana na kazi ngumu ya kupasua mawe kama sehemu ya adhabu ya kifungo chake. Aliondoka hospitali hapo Septemba 1, 2012 baada ya familia kuomba hivyo na kuahidiwa huduma nzuri ya kitabibu nyumbani. Wakati anaondoka hospitali hali yake bado ilikuwa ya utulivu kidogo lakini isiyo na mabadiliko makubwa. Mipango ya mazishi ambayo inatarajiwa kuvuta maelfu ya watu na mamia ya viongozi wa kimataifa inatarajiwa kutangazwa punde.


  Mandela akiwa na Walter Sisulu gerezeni Kisiwa cha Robben.

  Bw. Mandela (95) alikuwa Rais wa kwanza mweusi wa Afrika ya Kusini kufuatia kutokomezwa kwa utawala wa ubaguzi wa rangi uliofanywa na Makaburu kwa karibu miaka 400 ambapo watu weupe walijipa haki ya kuwatawala na kuwabagua watu weusi. Kabla ya kuwa Rais wa Afrika ya Kusini Mzee Mandela alitumikia kifungo cha miaka 27 jela ambako pamoja na kazi ngumu aliendelea kuongoza kundi la wapigania haki wengine kudai usawa, utu, na umoja wa Waafrika ya Kusini. Mandela alikuwa ni mfungwa maarufu zaidi wa kisiasa duniani ambapo harakati za kutaka afunguliwe zilipiganwa na wanaharakati sehemu mbalimbali duniani licha ya upinzani wa Serikali ya Afrika ya Kusini na Baadhi ya Nchi za Kimagharibi ambazo zilimuona Mandela kama Ghaidi na mchochezi.

  Maisha yake ya awali.

  Mzee Mandela alizaliwa Julai 18, 1918 katika kijiji cha Mvezo mji mdogo wa Umtatu Jimbo la Cape. Akiwa ni mmoja wa watoto wa Mzee Gadla Henry Mphakanyiswa Nelson Mandela alikulia kwa mamake – mke wa tatu wa Mzee Gadla – katika kijiji cha Qunu ambako pamoja na shughuli nyingine za nyumbani alikuwa mvulana mchunga ng’ombe. 


  Baadaye alianza masomo ya shule ya msingi na baadaye Sekondari ambapo aliamini kuwa alikuwa anaandaliwa kwa ajili ya utumishi katika nyumba ya Chifu wa Kabila lake la Xhosa kama mshauri. Hata hivyo baada ya kurudi nyumbani kutoka masomoni mwaka 1940 alikuta kuwa Chifu Jongintaba ameandaa ndoa Nelson Mandela pamoja mtoto wa kiume wa Chifu huyo aitwaye Justice walitoroka nyumbani na kwenda kwenye Jiji la Johannesburg. Alifanya kazi kama mlinzi katika Kampuni ya Madini ya Crown lakini alifukuzwa kazi na msimamizi wa pale baada ya kugunduliwa kuwa alikuwa ametoroka kwao. 


  Mandela akiwa amevaa mavazi ya kabila lake la Xhosa; alitoka katika familia ya kichifu.
  Kuingia Katika Siasa.

  Alipokuwa akiishi kwa muda na mmoja wa binamu zake Nelson Mandela alitambulishwa kwa mwanaharakati wa chama cha ANC Bw. Walter Sisulu ambaye baadaye walifungwa pamoja – Sisulu akitumikia miaka 25 jela. Walter Sisulu alimtafutia kazi ya ukarani katika kampuni ya Wanasheria ya Witkin, Sidelsky and Edelman. Akiwa hapo alifanya masomo ya elimu kwa njia ya Posta ambapo alikuwa anatafuta shahada yake ya kwanza. Mwaka 1943 alihitimu masomo yake ya sheria na kuanza kazi kama Mwanasheria badala ya kurudi kijijini kutumika kwa Chifu. 

  Akiwa ameanza kazi kama Mwanasheria Mandela aliendelea kuwa chini ya uangalizi wa Walter Sisulu ambaye alikuwa anaendeleza harakati za kudai haki za weusi. Akikutana mara kwa mara na wanaharakati wengine nyumbani kwa Sisulu Mandela alikutana tena na rafiki yake Oliver Tambo. Ilikuwa ni katika mikutano hiyo alikutana na mwanamama Evelyn Mase ambaye walianza uhusiano wa mapenzi na baadaye kufunga ndoa yake ya kwanza Oktoba , 1944. Walijaliwa watoto wawili wa kiume na wa kike; wa kiume Madiba “Thembi” Thembikile alizaliwa Februari 1946 na wa kike Makaziwe alizaliwa mwaka uliofuatia lakini alifariki miezi tisa baadaye baada ya kupata maambukizi ya ugonjwa uti wa mgongo.   Mandela na mtoto wake wa kwanza wa kiume Themi.

  Baada ya uchaguzi wa 1948 ambapo watu weupe peke yao walishirikia vyama vya Herenigle Nacionale Party na Afrikaner Party viliungana na kuunda chama cha National Party ambacho kilikuwa na sera ya wazi ya ubaguzi na kikapisha na kupanua ukali wa sera ya ubaguzi kupitia sheria mbalimbali za ubaguzi wa rangi. Serikali ya Kikaburu ikaja na mojawapo ya Sheria kali kabisa za kupambana na wanaharakati ambayo inajulikana kama Ukandamizaji wa Ukomunisti ya 1950. Sheria hii ilikuwa inashughulikia karibu mambo yote yanayohusiana na kuipinga serikali na ikiwahusu watu wote. 

  Migongano kati ya ANC na Serikali ya Kikaburu ilianza kupamba moto.

  Mwaka 1952 Nelson Mandela alikamatwa na utawala wa Makaburu kwa kile kilichodaiwa kujihusisha na vitendo vya Kikomunisti chini ya ile sheria iliyopitishwa miaka michache nyume. Alihukumiwa miezi tisa jela na “kazi ngumu” lakini utekelezaji wa hukumu hiyo ulisitishwa kwa miaka miwili. Lakini mwezi Disemba mwaka huo huo Mandela alipigwa marufuku kuzungumza na zaidi ya mtu mmoja kwa miezi sita. Akiwa kiongozi wa ANC hii ilimaanisha kuwa asingeweza kufanya mikutano na wanachama wake. Mwaka 1953 Mandela na rafiki yake Oliver Tambo walifungua kampuni yao ya Wanasheria katika Jiji la Johannesburg na kuifanya kuwa kampuni ya kwanza ya Wanasheria Weusi katika Afrika ya Kusini. Walijishughulisha na malalamiko mbalimbali ya wananchi hasa yanayohusiana na ukatili wa kisiasa. 

  Hata hivyo serikali ikitumia sheria nyingine ikalazimisha kufungwa kwa ofisi hiyo iliyokuwa na wateja wengi na kuihamisha sehemu nyingine ambapo ilikuwa ni vigumu kwa wateja kuifikia. Mwaka 1955 Mandela na wenzake walishirikiana kuandaa kongamano kubwa la watu wa Afrika Kusini ambao wanaamini katika taifa moja la watu wamoja japo wanatoka katika makabila na rangi mbalimbali. 

  Katika kongamano hili kulisainiwa kile kinachoaminika kama mojawapo ya nyaraka muhimu kabisa za kutetea usawa na utu wa watu wote ambayo ilijulikana kama Freedom Charter. Kufananisha hii ni sawasawa na Azimio la Uhuru la Marekani au ile nyaraka ya Waingereza ya Magna Carta. Kwa Tanzania tunaweza kufananisha kabisa na Azimio la Arusha. Freedom Charter ilitengeneza ramani ya kujenga taifa la watu walio huru na sawa katika Afrika Kusini. 

  Nelson Mandela na Oliver Tambo – wanasheria


  Marafiki wawili – miaka mingi toka Kisiwa cha Robben
  Hata hivyo kwa upande wa familia ndoa yake kwa Evelyn ilianza kuwa matatani. Kulikuwa na tuhuma za kukosa uaminifu ambapo alidaiwa kuwa na mahusiano ya mapenzi na baadhi ya kina dada wa ANC. Evelyn alijaribu watengane lakini pamoja na jitihahada mbalimbali za kupatana Nelson Mandela aliamua kupeana talaka na mke wake wa kwanza mwezi Machi 1958. Walikuwa wamejaliwa mtoto mwingine wa kike. Wakati huo wa mchakato wa talaka Nelson Mandela alikuwa ameanza mahusiano na Winnie Madikizela mmoja wa wafanyakazi wa mambo ya kijamii. Walifunga ndoa Mwezi Juni 1958.   Ndoa ya Madiba na Winnie.

  Migogoro na utawala wa kikaburu haikukoma. Na Mandela alizidi kuwa na siasa za mrengo wa kushoto. Njia za amani za kupata mabadiliko ya kisiasa zilionekana kutozaa matunda; Mandela na wenzake walianza kuamini katika njia za kimapinduzi na za kutumia silaha. Hili lilimletea matatizo zaidi na watawala wa Kikaburu. Hatimaye Augusti 2, 1962 Nelson Mandela alikamatwa na utawala wa Makaburu na kushtakiwa kwa kuchochea mgomo wa wafanyakazi na kuondoka nchini bila kibali. Mandela alijiwakilishi mwenyewe mbele ya mahakama huku akitumia nafasi hiyo kutoa hutuba motomoto za kisiasa dhidi ya utawala wa kibaguzi wa makaburu. Alikutwa na hatia na kuamuriwa kufungwa miaka mitano jela; wakati anatoka mahakamani mashabiki wake walisimama pembeni na kuimba wimbo wa Mungu Ibariki Afrika (Nkosi Sikeleli Afrika).

  Kesi ya Rivonia.

  Matatizo yake hayakufikia mwisho. Julai 11, 1963 polisi walivamia shamba la Lilliesleaf – mji mdogo wa Rivonia nje ya Johannesburg) ambapo pamoja na vitu mbalimbali waliamini walikuta ushahidi wa kutosha kumhusisha Mandela na mipango ya kuipindua serikali. Mandela na wenzake walitumia shamba hili kama sehemu yao ya kujificha huku Mandela akijifanya ni mtunza bustani. Kesi hii ilikuwa motomoto kwani Mandela na wenzake walishtakiwa kwa makosa manne yakiwa ni ya uhujumu wa miundo mbinu ya nchi (vitendo zaidi ya 200) pamoja na kutaka kupindua serikali; serikali ilikuwa inapendekeza kuwa wakikutwa na hatia basi wahukumiwe kifo. Mashahidi wengi wa serikali waliitwa pamoja na lundo la ushahidi wa picha na nyaraka kuthibitisha mashtaka ya serikali dhidi ya Mandela na 
  wenzake tisa. 


  Mara baada ya kuachiliwa mwaka 1990 Mandela alihakikisha anamtembelea rafiki yake mpenzi Oliver Tambo aliyekuwa anapata matibabu Sweden
  Wengine ambao walikuwa pamoja na Mandela ni pamoja na Walter Sisulu na Govan Mbeki (baba yake na Thabo Mbeki aliyemrithi Mandela kama Rais wa Afrika ya Kusini). Ilikuwa ni katika kesi hii ambapo Mandela alitoa mojawapo ya hotuba zinazosifiwa zaidi duniani na ambayo inasomwa na wanafunzi wa siasa sehemu mbalimbali duniani kwani ilielezea falsafa ya kupinga ubaguzi wa rangi. Inafanana sana kimaudhui na barua ya Martin Luther King Jr akiwa katika jela ya Birmingham huko Alabama ambapo alielezea kwanini alikuwa anapinga kubaguliwa na kwanini kila mpenda haki duniani anapaswa kufanya hivyo hivyo. Katika hotuba hii inayojulikana kama “I’m Prepared to Die Speech” Mandela alisema kuwa alikuwa anapigania haki ya watu weusi kuheshimiwa kutokana na utu wao na kuwa wao ni sawa kama binadamu wengine.
  Alisema kuwa hapiganii haki ya weusi kuwabagua weupe bali haki ya watu wote kuishi kwa pamoja kama watu wa jamii moja. Mandela alisema “This is the struggle of the African people, inspired by their own suffering and experience. It is a struggle for the right to live. I have cherished the ideal of a democratic and free society, in which all persons live together in harmony and with equal opportunity. It is an ideal which I hope to live for and achieve. But, if needs be, my Lord, it is an ideal for which I am prepared to die”. Yaani, “Haya ni mapambano ya watu wa Afrika yaliyotokana na mateso na mang’amuzi yao wenyewe. Haya ni mapambano ya kupigania haki ya kuishi. Nimelifurahia wazo la jamii ya kidemokrasia na huru, ambapo watu wote wanaishi katika amani na haki sawa. Ni wazo ambalo ninatumaini kuishi kwa ajili yake na kulitimiza. Lakini, ikibidi, mheshimiwa, ni wazo ambalo
  nimejiandaa kufa kwa ajili yake”
  Baada ya kuhukumiwa kifungo cha maisha Mandela na wenzake wakitoka Mahakamani
  Pamoja na utetezi wake wote timu ya Mandela ilishindwa kesi hii na wote wakakutwa na hatia isipokuwa mmoja. Kwa vile tayari kulikuwa na mwamko sehemu mbalimbali duniani kupinga adhabu ya kifo Mahakama ikawaamuru Mandela na wenzake kutumikia kifungo cha maisha na huo ndio ukawa mwanzo wa kifungo cha karibu miaka 30 jela (ikumbukwe kesi hii ilipoanza Mandela tayari alikuwa anatumikia ile hukumu ya miaka 5 jela). Mandela na wenzake walipelekwa katika jela ya Kisiwa cha Robben ambako pale peke yake alitumikia miaka 18. Maisha kifungoni Kisiwa cha Robben na kwingine


  Kisiwa cha Robben ambako Mandela alifungwa kwa miaka 18
  Mandela na wenzake walihukumiwa kazi ngumu vile vile na kweli ilikuwa ni kazi ngumu kwani pamoja na kuponda mawe walipewa baadaye kazi ya kuponda mawe ya chokaa. Kwa muda alikatazwa kuvaa miwani ya jua kitua mbacho kilimsababishia ubovu wa macho ambao hakuweza kupona kabisa. Akiwa kifungoni mamake alimtembelea mwaka 1968 na siku chache baadaye alifariki dunia, mwaka uliofuata mtoto wake wa kwanza Thembi alifariki katika ajali ya gari – Mandela hakuruhiswa kuhudhuria mazishi yao wote hao. Maisha kifungoni yalikuwa magumu kwa kila kipimo licha ya maisha baada ya miaka kuanza kuboreshwa kidogo kufuatia maandamano na harakati za kutaka Mandela afunguliwe. Utawala wa makaburu hawakusikia la mtu yeyote hasa kwa vile walikuwa wanaushirika wa karibu na serikali ya Marekani na Uingereza ambazo zote zilimuona Mandela kama Mkomunisti na Ghaidi. 
  Mwaka 1966 gerezani Mandela anaonekana akiitia viraka nguo yake ya jela
  Mandela alitumikia pia katika magereza ya Pollsmoor huko Cape Town na Gereza kati ya 1982 hadi 1988 na baadaye gereza la Victor Verster 1988-1990 ambako kwa kiasi kikubwa alikuwa amepewa maisha ya unafuu (hapa chini akiwa na mpishi na huduma mbalimbali) kulinganisha na alivyoishi katika gereza la Kisiwa cha Robben. 
  Akiwa gereza la Victor Verster alipewa nyumba na mtumishi. Hapa pichani na aliyekuwa mpishi wake kwenye gereza hilo.
  Ikumbukwe miaka aliyokuwa Robben ndiyo ilikuwa migumu zaidi kwani hakuruhusiwa kutembelewa na watu wengi na alipewa nafasi ya kutembelewa na kuandikwa barua moja tu kila baada ya miezi sita. Katika magereza hayo mengine Mandela alipata unafuu kidogo.
  Kuingia kwa F. W. de Clerk na kuachiliwa kwa Mandela
  Chini ya utawala wa Pieter Botha Afrika ya Kusini ilizama katika siasa na sera za ubaguzi wa rangi. Botha aliwachukia weusi na aliamini kabisa kuwa utawala wa kikaburu utadumu kwa muda mrefu. Botha anaweza kabisa kufananishwa na aliyekuwa Gavana wa Alabama George Wallace ambaye aliapa kuwa “ubaguzi sasa, ubaguzi kesho, ubaguzi milele”; japo aliishi na kuona Ubaguzi ukifumuliwa katika jimbo lake na katika Marekani sera hizo zikitupwa katika mifumo ya utawala. Hata hivyo alikuwa ni F. W. de Clerk mwanasiasa mwingine mzungu ambaye licha ya kutoka katika chama kilichoamini katika ubaguzi wa rangi yeye mwenyewe alijikuta akiukataa kifikra kwani aliona hauwezi kudumu.
  Kwa muda hivi tangu 1988 Mandela alikuwa na mazungumzo ya siri na baadhi ya viongozi wa serikali juu ya masharti ya yeye na wenzake kuachiwa huru na mwelekeo wa siasa za Afrika ya Kusini. Mazungumzo hayo yalikumbana na vikwazo vingi sana ikiwemo kutokukubaliana kwa masharti – kwa mfano serikali ilitaka Mandela asijiingize kwenye siasa na kuwa wasilazimishwe kuwa na utawala wa wengi (majority rule) masharti ambaye Mandela aliyakataa. 


  Baada ya Mdahalo mzito ambao de Klerk alionekana kushinda; Mandela alipompa mkono alionekana kushangaza umati wa watu na kujenga daraja kati yake na de Klerk kwa maisha.
  Matokeo yake ni kuwa Mandela na wenzake waliachiliwa huru na utawala lwa De Clerk Februari 2, 1990 na kuleta furaha wanaharakati pote duniani. Ikumbukwe kwa Tanzania wimbo maarufu wa “Kilicho cha Wapenda Haki Duniani Kote” ulivuma sana wakati huo katika kuhamasisha Mandela na wenzake waachiliwe huru. Baada ya kuachiliwa huru muda mrefu ulitumika kufanya mazungumzo na utawala wa kikaburu kuhusiana na mwelekeo wa siasa za Afrika ya Kusini na hata kuelekea uchaguzi mkuu. Hata hivyo kutokana na matukio mbalimbali ya vurugu na mauaji ya kisiasa yaliyokuwa yanaendelea na hata migongano ya chama cha Inkatha cha Chifu Buthelezi Mandela aliona hana jinsi isipokuwa kufikia makubaliano ya msingi. Baadhi ya makubaliano hayo yalihusisha kufunguliwa kwa wafungwa wa kisiasa, kuitishwa kwa uchaguzi mkuu, kuwa na Katiba ya Mpito na kuhakikishia kuwa kazi za weupe hazitafukuzwa kama ukiingia utawala wa weusi.Mandela na de Klerk walitunukiwa tuzo ya Nishani ya Amani ya Nobel mwaka 1993 
  Mandela na de Klerk wakionesha nishani ya Nobel

  Uchaguzi Mkuu wa 1994
  Hatimaye Afrika ya Kusini ikaingia katika uchaguzi mkuu wa kwanza huru na wawananchi wote mwaka 1994, Aprili 27. Kampeni ilikuwa na vurugu za hapa na pale lakini kwa ujumla wananchi wa Afrika ya Kusini hasa weusi walijikuta kwa mara ya kwanza wanapiga kura kumchagua kiongozi wanayemtaka. Mandela akiongoza ANC walishinda asilimia 62 ya kura na kushindwa kupata theluthi mbili ambayo ingewawezesha kuweza kubadili Katiba. Serikali yake ilikuwa ni ya umoja wa kitaifa ikitegemea kwa kiasi kikubwa baadhi ya maofis waliokuwa katika utawala wa kikaburu. De Clerk alikuwa Makamu wa kwanza wa Rais na Thabo Mbeki akiwa Makamu wa Pili wa Rais. 
  Mandela (katikati) akiwa na Makamu wake wawili

  Mandela alishaeleza toka awali kuwa atagombea kipindi kimoja tu na ndivyo alivyofanya na baadaye kumwachia Thabo Mbeki kama Rais wa Afrika ya Kusini. Baada ya kustaafu siasa Mandela aliamua kujishughulisha na program mbalimbali za ndani ya Afrika ya Kusini na kutembelea baadhi ya nchi. Hata hivyo udhaifu wa mwili uliotokana na magonjwa na uzee ulimzidia na kumfanya apunguze safari za nje. Kwa mara ya mwisho alionekana katika shughuli za hadhara katika mashindano ya Kombe la Dunia mwaka 2010 ambayo yalifanyika Nchini Afrika ya Kusini.
  Mandela na Tanzania
  Tanzania kama nchi imehusika kwa kiasi kikubwa sana katika kuuvunja vunja utawala wa kikaburu na katiak kuongoza harakati za kutaka Mandela aachiliwe huru. Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere na utawala wake mara baada ya Uhuru 1961 aliazimia kutoa msaada wote unaohitajika kwa wapigania uhuru wa Afrika ya Kusini. Kama ilivyodokezwa hapo juu kuwa mojawapo ya mashtaka dhidi ya Mandela ni lile la kwenda nje ya Afrika ya Kusini bila kibali. Mwaka 1962 Mandela akitumia njia za panya alitoroka Afrika ya Kusini na hatimaye kuingia Tanganyika na kukutana na Mwalimu Nyerere ambaye aliwapa ahadi ya ushirikiano mkubwa. Mandela mwenyewe akizungumza katika dhifa aliyomwandaliwa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere mwaka 1997 Oktoba 17; alisema “Inanyenyekesha kukumbuka mchango wa Mwalimu Nyerere katika ukombozi wa bara letu na Uhuru wa Afrika ya Kusini”.   Aliendelea na kumsifia Nyerere kwa kusema kuwa wakati watu wengine walikuja baadaye kuona ubaya wa utawala kikaburu Nyerere aliliona hili mwaka 1959 ambapo akishirikiana na Fr. Huddleston walianzisha harakati za kupinga ubaguzi wa rangi (anti-apartheid movement) ambao zilikuja kuwa maarufu sana baadaye – hasa baada ya kesi ya Rivonia. Mandela alisema kukutana na Mwalimu mwaka 1962 kulimuonesha jinsi Nyerere alivyokuwa anataka haki sehemu zote duniani na jinsi alivyojitoa yeye na taifa lake changa kuona kuwa Afrika yote inakuwa huru. 


  Wanaharakati – wakisherehekea miaka 80 ya Askofu Trevol Huddleston, Nyerere, Askofu Mkuu Desmond Tutu na aliyekuwa Katibu wa Jumuiya ya Madola Shirdath Ramphal
  Katika kuonesha hili Mandela alichagua Tanzania miongoni mwa nchi za kwanza kutembelea mara baada ya kuachiliwa huru mwaka 1990. Aliingia nchini Machi 7, 1990 na kupokelewa na maelfu ya watu wakiongozwa na baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere pamoja na Rais Ali Hassan Mwinyi. Wakati anatembelea nchini kama mtu huru Tanzania ilikuwa na wapiganaji karibu 10,000 wa Afrika ya Kusini waliokuwa wanaishi Tanzania na kujihusisha na mambo mbalimbali. Ikumbukwe ANC ilifungua ofisi yake ya kwanza nje ya Afrika ya Kusini Jijini Dar-es-Saalam mwaka 1961 na hii ilichangia baadaye pia kwa ofisi za vyama vingine vya ukombozi kuchagua Dar kama makao yao makuu. Yote haya yalisaidia kuifanya Tanzania kuwa makao makuu ya Kamati ya Ukombozi ya Nchi Zilizo Mstari wa Mbele ambayo kwa muda mrefu iliongozwa na Brig. Hashim Mbita. Uhusiano huu wa karibu wa Tanzania na Wapigania Uhuru ulithibitika zaidi baada ya Tanzania kuwapatia wapigania uhuru hao maeneo ya mafunzo ya kijeshi na taaluma mbalimbali huko Morogoro eneo la Mazimbu na maeneo mengine Mtwara na sehemu nyingine nchini. Pamoja na vyuo wapigania uhuru hao walipewa maeneo ya shule za msingi na sekondari vile vile.
  Wakufunzi wa chuo cha ANC Mazimbu Morogoro enzi hizo

  Uhusiano huu wa karibu wa Tanzania na wapigania uhuru wa Afrika ya Kusini ulionekana pia wakati wa Mkutano wa Mawaziri Wakuu wa Nchi za Jumuiya za Madola uliofanyika London, Uingereza . Katika makala yake aliyoandika kwenye gazeti la The Observer Machi 7, 1961 Nyerere aliweka msimamo wa Tanganyika mapema kabisa kuhusiana na uanachama wa Afrika ya Kusini kwenye Jumuiya hiyo (Afrika ya Kusini iliomba kuwa mwanachama na mawaziri wakuu walitakiwa kuchukua uamuzi). Katika makala hiyo Nyerere alisema mojawapo ya mistari inayokumbukwa sana kuwa “kuipigia kura Afrika Kusini ijiunge ni kutupigia kura sisi kujitoa (To vote South Africa in, is to vote us out) na inaaminikuwa kuwa hoja aliyoijenga ilichangia sana kubadili upepo na kusababisha Afrika ya Kusini kutoa ombi lake la kujiunga. Uhusiano wa karibu wa Nyerere na Mandela haukushia wakati huo tu; hata baada ya kifo cha Mwalimu alikuwa ni Nelson Mandela aliyechukua jukumu la kusaidia kuleta amani Rwanda kama Mpatanishi. 

  Buriani
  Mandela ametutoka baada ya maisha ambayo ametumikia nchi yake, bara lake na dunia kwa namna ambayo ameacha alama ya kudumu ya kukumbukwa. Kwa mtu ambaye utawala wa kikaburu ulimnyima haki nyingi za msingi na kumchukulia miaka ishirini na saba ya maisha yake angeweza kuwa mtu mwenye kisasi pale aliposhika madaraka kama Rais wa nchi yake. Mtu ambaye alinyanyaswa, kuteswa, na kushindwa hata kuhudhuria mazishi ya mamake kwa namna ya kawaida angekuwa ni mtu mwenye kinyongo sana. Hata hivyo Mandela alionesha huruma na msamaha wa hali ya juu sana. Aliposhika madaraka alihakikisha kuwa watu weupe wanajihisi salama na kuondoa kabisa roho ya kulipiza kisasi hasa kwa watu weusi ambao waliumia sana mikononi mwa weupe kwa karibu miaka 400. Anapoitwa “Baba wa Taifa” la Afrika ya Kusini haitwi hivyo kirahisi. Mchango wake wa pekee kwa nchi yake unamuweka katika nafasi ya pekee kukumbukwa na vizazi vingi vijavyo. Hali hii ya msamaha iligusa hata maisha yake binafsi. Pamoja na kupata habari za mkewe Winnie Mandela kukosa uaminifu Mandela bado alihakikishia kuwa anapatiwa uwakilishi wa kutosha kujitetea kwenye kesi iliyomkabili ya utekaji na mauaji. Hata baada ya kuachana naye Mandela na mkewe mpya Graca Machel – aliyekuwa mke wa marehemu Samora Machel – Mandelea amekuwa na mahusiano mazuri nay a utulivu. Dunia imepoteza shujaa wa haki za binadamu, nyota ya Afrika na mfano wa viongozi ambao waliweka maslahi ya watu wao mbele zaidi kuliko furaha zao binafsi na za familia zao. Wananchi wa Afrika ya Kusini wanapomlilia wanaungana na mamilioni zaidi katika bara la Afrika na Dunia ambao wanakumbuka nafasi ya Mandela katika maisha yao. Kwa Watanzania wengi hasa waliokua miaka ya sabini na themanini harakati za kutaka Mandela afunguliwe na kukomeshwa kwa utawala wa kikaburu zilikuwa ni sehemu ya maisha yao. Hawa pia wanamshukuru Mungu kwa maisha ya Mandela na wanaungana kutoa rambirambi na pole kwa familia ya Mandela na kumwombea pumziko la amani baada ya maisha ya uchovu na kazi ngumu. Watanzania wanaungana na ndugu zao wa Afrika ya Kusini katika maombolezo haya; wao wenyewe wanakumbuka vile vile jinsi walivyoondokewa na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere na jinsi akili ya jumla ya Taifa ilivyoguswa lakini pia kuonekana kwa kubadilika kwa taifa kwa kutokuwepo Mwalimu. Ni wazi kuwa hata Afrika ya Kusini nayo itapita huku ambapo ile Dhamira ya Taifa (Consciousness of a Nation) yaani Mandela atakuwa hayupo. Njia pekee ya kuhakikisha kuwa Afrika ya Kusini inazidi kujijenga katika maisha ya kisasa na kuinua watu wake kuelekea maendeleo ni lazima kukumbuka umoja na udugu ambao Mandela alipigania.
  youtube video
  MUNGU AILAZE ROHO YAKE PEMA PEPONI
  (Haki zote za picha na vielelezo vingine zinabakia kwa wenye nazo)

  0 0


older | 1 | .... | 180 | 181 | (Page 182) | 183 | 184 | .... | 1897 | newer