Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live

Diwani kata ya Lemara Profesa Raymond Mosha akabidhi baiskeli ya walemavu kwa mkazi wa kata hiyo George Makinda

0
0
Na Ahmed Mahmoud,Arusha.
Diwani wa Kata ya Lemara ,Profesa Raymond Mosha ameanzisha mpango wa kuwafikia watu wenye ulemavu na kuwapatia mahitaji yao pamoja na nyenzo wanazohitaji ikiwemo baiskeli maalumu za walemavu.
Akizungumza katika zoezi la kukabidhi baiskeli ya mlemavu mwenye umri wa miaka zaidia ya sitini mkazi anayeitwa Mzee George Makinda  wa kata ya Lemara katika eneo la Njiro jijini Arusha amesema kuwa  baiskeli  hiyo  itamsaidia kujishughulisha na kazi zake kama kawaida.
Msaada wa baiskeli hiyo  imetolewa na Professa Raymond Mosha ambae ni diwani wa kata hiyo ya Lemara baada ya kuona familia ya Mzee George Makinda haina uwezo wa ununuzi wa baiskeli hiyo,
Professa Mosha alisema kuwa alihuzunishwa sana na maisha ya mlemavu huyo kwani George Makinda  miaka ya nyuma alikua mzima lakini alikubwa na ugonjwa wa kupooza uliomfanya kua mlemavu wa kushindwa kuongea wala kutembea.
alisema hali hiyo ndio iliomgusa yeye na marafiki zake nakuamua kujitolea baiskel ambayo itamsaidia kwa namna moja au nyingine kutembelea na kujiona kama watu wengine.
Hata hivyo Mke wa Mzee George Makinda  Bi Estar Makinda  pamoja na kutoa shukurani  ya  msaada wa Baiskel hiyo ambayo anataja kua sababu ya kumfanya kumpa ahuweni kwakua ameteseka kwa muda mrefu katika kumlea mumewe,
Estar alisema hata muda mwingine alishindwa kujishughulisha na kazi za kiuchumi nakubaki kumhudumia mumewe  kutokana na  muda wote ni mtu wa kuhudumiwa kila kitu,
“ sasa amepatiwa msaada wa Baisekel itakayomsaidia kutembea naamini sasa mabadiliko ya familia yataonekana”  Alisema Estar Makinda.
Diwani wa kata ya Lemara Profesa  Raymond Mosha akikabidhi baiskeli ya walemavu kwa mkazi wa kata hiyo George Makinda ambaye ni mlemavu wa miguu baada ya kupata ugonjwa wa kupooza .picha zota na Mahmoud Ahmad Arusha


RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA MOROCCO HAPA NCHINI ALIYEAMBATANA NA UJUMBE KUTOKA NCHINI KWAO

0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Kiongozi wa Ujumbe kutoka nchini Morocco Balozi Mohamed Methqal ambaye ni Mkurugenzi mkuu wa Wakala wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Morocco  mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam. katikati  ni Balozi wa Morocco hapa nchini Abdelilah Benryane akishuhudia.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika kikao na Balozi wa Morocco hapa nchini Abdelilah Benryane ambaye aliambatana pamoja na Kiongozi wa Ujumbe kutoka nchini Morocco Balozi Mohamed Methqal ambaye ni Mkurugenzi mkuu wa Wakala wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Morocco,  Ikulu jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini Patrick Mfugale pamoja na wajumbe wengine.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo kuhusu ujenzi wa Uwanja wa Mpira wa Miguu utakaokuwa na uwezo wa kuingiza watazamaji zaidi ya  85,000 mkoani Dodoma huku Balozi wa Morocco hapa nchini Abdelilah Benryane wanne kutoka (kushoto) pamoja na Kiongozi wa Ujumbe kutoka nchini Morocco Balozi Mohamed Methqal watatu kutoka kushoto pamoja na ujumbe huo wakisikiliza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia mfano wa Uwanja mkubwa wa mpira wa miguu utakaojengwa jijini kwa ufadhili wa Mfalme wa Morocco Mohamed VI. Uwanja huo utakuwa  na uwezo wa kuchukua watazamaji 85,000 (normal capacity) waliokaa kwenye viti lakini pia utaweza kubeba washabiki  hadi105,000 kama walivyopanga. Kwa nje uwanja huo utakuwa na muonekano kama mlima Kilimanjaro hivyo kuzidi kupamba madhari ya mjii mkuu wa Tanzania mkoani Dodoma.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Morocco hapa nchini Abdelilah Benryane wasabi kutoka kushoto akifatiwa na Kiongozi wa Ujumbe kutoka nchini Morocco Balozi Mohamed Methqal ambaye ni  Mkurugenzi mkuu wa Wakala wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Morocco pamoja na Ujumbe wao. Wengine katika picha ni  ni Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi wasabi kutoka kulia, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale wasita kutoka kulia, Balozi Zuhuru Bundala wakwanza kulia  pamoja na wajumbe wengine Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

RC MAKONDA AZINDUA KAMPENI YA KUZUIA VIFO VITOKANAVYO NA UZAZI, AKABIDHI BILION 3 ZA UJENZI HOSPITAL ZA WILAYA.

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo amefanya tukio la kihistoria la uzinduzi wa Kampeni ya kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi pamoja na kukabidhi hundi ya Shilingi Bilioni 3 alizotoa Rais Dkt.John Magufuli kwaajili ya ujenzi wa Hospital za Wilaya ya Kigamboni na Ilala eneo la Kivule ambapo ametoa muda wa Miezi 3 kuhakikisha ujenzi umekamilika.

Akizungumza katika Uzinduzi huo RC Makonda amesema serikali imejidhatiti kuhakikisha inapunguza na ikiwezekana kumaliza kabisa vifo vya Mama na Mtoto kwa kujenga Hospital za kutosha, Zahanati, Vituo vya Afya, Ununuzi wa Magari ya kubebea Wagonjwa pamoja na vifaa tiba ili wananchi wasipate tabu.

RC Makonda amesema katika Fedha hizo Wilaya ya Kigamboni imepokea Shilingi Bilion 1.5 na Ilala Bilioni 1.5 ambapo Hospital zitakazojengwa zitakuwa na watumishi zaidi ya 500 na kuongeza kuwa mbali na Ujenzi wa Hospital hizo za Wilaya pia Serikali inaendelea na ujenzi wa Hospital nyingine ya kisasa eneo la Mabwepande.

Aidha RC Makonda amewataka wanaume kuwasindikiza wake zao Clinic ili kujua maendeleo ya Afya zao jambo litakalosaidia kuepusha vifo vya mama au mtoto wakati wa kujifungua.

Pamoja na hayo RC Makonda amewataka mabinti kuhakikisha wanaepuka Mimba za utotoni ambazo zimekuwa chanzo cha ongezeko la vifo na hata maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.

Uzinduzi wa Kampeni ya kuzuia Vifo vitokanavyo na Uzazi JIONGEZE TUWAVUSHE SALAMA inaenda na kaulimbiu isemayo kila mmoja anao wajibu wa kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi "MANENO BASI SASA NI VITENDO"

MATUKIO KATIKA PICHA WAZIRI MKUU ASHIRIKI IBADA YA KUMSALIA MAREHEMU KAKA YAKE MZEE SAID MAJALIWA

0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishiriki ibada ya kumsalia marehemu kaka yake Mzee Said Majaliwa aliyefariki Machi 12, 2019 katika kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa Machi 13.2019 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka udongo kwenye kaburi la marehemu kaka yake Mzee Said Majaliwa aliyefariki Machi 12, 2019, ambaye amezikwa machi 13.3.2019 katika makaburi ya familia, Nandagala Wilayani Ruangwa. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipewa mkono wa pole wa marehemu kaka yake Mzee Said Majaliwa aliyefariki Machi 12, 2019 na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa, kijijini kwake Nandagala Wilayani Ruangwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Shirika la chakula Duniani WFP waungana na TRC kusafirisha chakula nje ya nchi

0
0


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Issack Kamwele na Mkurugenzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya TRC Profesa John Kondoro wakishuhudia Meneja Mkazi wa WFP Tanzania , Bw. Michael Dunford (kulia) na Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania Bw. Masanja Kadogosa (kushoto) wakitia saini mkataba wa makubaliano ya ukarabati wa Mabehewa 40 ya treni yatakayofanya kazi ya kubeba mizigo ya WFP kwenda nchi mbalimbali za ukanda wa Afrika mashariki na Maziwa Makuu, Mkataba huo umetiwa saini leo katika Karakana ya TRC.


……………………………………………………………………

*Kwa mwaka huu wamejipanga kununua zaidi ya tani laki 1 za mahindi

*JPM atoa Bil 5/- kukarabati mabehewa 200, WFP kukarabati 40 kwa Bil 1.1/-

WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Issack Kamwele amesema hawezi kuwa tayari kuona baadhi ya masuala yanasshindwa kufanikiwa katika taasisi zilizo chini ya wizaaraa yake kwa kisingizio cha kubanwa na sheria.

Alisema hayo jana wakati wa hafla yaa kutiliaanaa saini mkaataba wa kutengenezaa mabehewa 40 kati ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) na Shirika la Mpango wa Chaakulaa Duniani (WFP) kwenye karakana ya treni jijini Dar es Salaam jana.

Mhandisi Kamwele alisema, uwiano wa mizigo inaayosafirishwaa hailingani na uwezo wa maamlaaka ya bandari na TRC kutokana na uwekezaji mkubwa uliowekwa na Serikali ya Awamu ya Tano na fursa ya kupakana na nchi zisizo na baahari.

“TRA (Mamlaka ya Mapato Tanzania), TPA (Mamlaka ya Bandari Tanzania) na TRC zinakwamisha uwezo wa bandari yetu kupakua naa kupakia mizigo. Tutafanya hiki kwa pamoja maaana nimebaini tatizo kubwa lipo TRA,” aalisema Mhandisi Kamwele na kuongezaa:

“Nimeshamwandikia baruaa Waziri wa Fedha na Mipango tukutane kwa ajili ya maazungumzo, maana sheria za fedha zipo lakini kama zinatukwamisha tuzifanyie marekebisho. Kwa mfano Uganda inazalisha tani laki 7.5 kwa mwaka lakini uwezo wa bandari yetu hadi sasa ni tani laki tatu kwa mwaka, tunakwama wapi. Tutataajana naani anakwamisha kupaata hii mizigo.”

Aidha, katika hafla hiyo TRC na WFP walikubaliana kusafirisha mizigo yaa chakula kutoka shirika hilo la kimataifa linalosambaza chakulaa ndani na nje ya nchi.

Ambapo katika kuimarisha uhussaano wao WFP wameamua kutoaa kiasi cha Dola za Kimarekani 600,000 sawa na Sh Bilioni 1.1 kwa ajili ya kukarabati mabehewa 40 ya shirika hilo.

“Napenda kutumia furssa hii kuwashukuru WFP kwa msaada huu ambao utaenda kukuza uwezo wa shirika la reli katika kuhudumia mizigo hususan unaopita bandari ya Dar es Salaam kwenda mikoa mingine na nchi jirani kama Uganda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Zambia, Rwanda na Burundi. Tunashukuru WFP kwa kuungaa mkono juhudi za serikali iliyojielekeza kuleta mageuzi ya kiuchumi chini kwa kukuza biashara na kujenga uchumi wa viwanda,” alisema Mhandisi Kamwele.

Kaatika kuimarisha shirika hilo, hivi karibuni Rais Dk. John Magufuli alitoaa kiasi cha Bil 4 kwa ajili ya ukarabati wa maabehewa ya mizigo, ambapo lengo ni kukarabati mabehewa 200 hadi kufikia sasa TRC wameshakarabati mabehewa 40.

Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa alisema kwa kiasi kikubwa mabadiliko yametokea ndani ya shirika hilo tangu kuingia madarakani Rais Magufuli, ambaye aliapa kuinua uchumi wa watanzania kupitia viwanda na miundombinu imara.

“Miaka 15 iliyopita TRC ilikuwa na uwezo wa kusafirisha hadi tani milioni 1.4 kwa mwaka, lakini katikati tulipata misukosuko tukapoteza uwezo wetu. Tulipolibinafsisha tulizifunga njia nyingi katika reli ya kati na ya Tazara.

“Tunafanya ukarabati mkubwa katika reli ya kati, tunakarabati kilomita 970. Tayari kipande cha Tanga hadi Mombo kimeshakamilika viwanda vya saruji vimeanza kusafirisha mizigo yao kwa njia ya reli,” alisema Kadogosa.

Alibainisha, uhusiano wao na WFP unafikia mwaka mmoja sasa na kwa kuwa hilo ni shirika la kimataifa kuna uwezekano mkubwa wakapata wateja wengi zaidi kwa kuwa vigezo wanavyotumia kutaka kusafirisha mizigo hadi vimekubaliwa maana yake TRC wanaweza kufanya kazi na shirika lolote duniani.

“Mkakati huu wa kukarabati mabehewa una lengo la kukarabati mabehewa zaidi ya 500, kwa sasa tunaanza na haya 200 kwa fedha iliyotolewa na Rais Magufuli. Tunafanya kazi usiku na mchana ili tumalize mapema, mpango huu utasaidia kutoa ajira za moja kwa moja 30 na za muda mfupi 32,” alisema Kadogosa.

Kwa upande wake Meneja Mkazi wa WFP, Michael Dunford alisema walianza kutoa kazi za muda mfupi ili kuangalia uwezo wa TRC lakini ndani ya kipindi kifupi wamevutiwa na uwezo wao na ndiyo maana wameamua kufanya nao makubaliano.

“Mpango wa chakula kazi yake si lishe tu bali kusafirisha mizigo pia, tangu mwaka 2010 katika ardhi ya Tanzania tumenunua kiasi cha tani 500,000 za chakula, kwa mwaka jana 2018 tumenunua zaidi yaa tani laki moja na mwaka huu tuna mpango wa kununua zaidi ya tani laki moja na nusu, hii mizigo yote inahitaji kusafirishwa.

“Ndiyo maana tukaamua kutoa fedha kwa ajili ya ukarabati wa mabehewa 40 yatakayosaidia kusafirisha mizigo yetu ndani na nje ya nchi kwenda DRC, Uganda hadi Sudan. Si tu tutaongeza ajira lakini pia tutachangamsha uchumi kwa masuala mbalimbali ya usafirishaji na miundombinu,” alisema
Dunford.

Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Deusdedith Kakoko ambaye pia alihudhuria hafla hiyo alisema kuimarika kwa shirika la reli kuna faida kubwa kwa TPA kwa sababu kazi zao zinategemeana.

“Hakuna reli bila bandari na hakuna bandari bila reli, lazima kazi zetu tuzifanye kwa pamoja. Nafikiria pia TPA tuingie mkataba kama huu na WFP kwa sababu ya kurahiisisha kuvusha mizigo mipakani. Na TRA vilevile wanahitaji kuhusishwa kwa kuwa yapo mambo mengi yanakwama au kuchelwa kwa kukosa maelewani,” alisema Kakoko.

Ushirikiano huu utaakuwa na tijaa kwa wakulima na wafanyakazi wa kubeba na kupakua mizigo kuanzia bandarini hadi kwenye maeneo ya reli, kwa kuwa WFP wamepanga kuwa watanunuaa chakula kutoka Tanzania ambayo ni faida kwa wakulima na watasafirisha kwa kutumia miundombinu ya reli na wakifika maeneo ya maziwa makuu watavusha kwa kutumia Ziwa Victoria kwenda nchi jirani.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Issack Kamwele na Mkurugenzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya TRC Profesa John Kondoro wakishuhudia wakati Meneja Mkazi wa WFP Tanzania , Bw. Michael Dunford wa pili (kulia) na Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania Bw. Masanja Kadogosa (kushoto) wakionyesha mkataba wa makubaliano ya ukarabati wa Mabehewa 40 ya treni yatakayofanya kazi ya kubeba mizigo ya WFP kwenda nchi mbalimbali za ukanda wa Afrika mashariki na Maziwa Makuu Mkataba huo umetiwa saini leo katika karakana ya TRC

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Issack Kamwele na Mkurugenzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya TRC Profesa John Kondoro wakishuhudia Meneja Mkazi wa WFP Tanzania , Bw. Michael Dunford (kulia) na Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania Bw. Masanja Kadogosa (Kushoto)wakibadilishana mkataba wa makubaliano ya ukarabati wa Mabehewa 40 ya treni yatakayofanya kazi ya kubeba mizigo ya WFP kwenda nchi mbalimbali za ukanda wa Afrika mashariki na Maziwa Makuu Mkataba huo umetiwa saini leo katika Karakana ya TRC.

Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania Bw. Masanja Kadogosa akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Issack Kamwele (kulia),Meneja Mkazi wa WFP Tanzania , Bw. Michael Dunford (katikati) na Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania Bw. Masanja Kadogosa Kushoto wakiwasili katika karakana ya TRC kwa ajili ya utiaji saini mkataba huo.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Issack Kamwele (kulia),Meneja Mkazi wa WFP Tanzania , Bw. Michael Dunford (katikati) na Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania Bw. Masanja Kadogosa Kushoto wakijadili machache kabla ya utiaji saini mkataba huo.
Meneja Mkazi wa WFP Tanzania , Bw. Michael Dunford akizungumza katika hafla hiyo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Issack Kamwele akitoa hotuba yake kabla ya utiaji saini wa mkataba huo.
Meneja Mawasiliano wa TRC Jamila Mbarouk akitoa ratiba fupi na kukaribisha wageni katika hafla hiyo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Issack Kamwele akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya TRC na wadau mbalimbali walioshiriki katika hafla hiyo.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI KUTOKA MKOA WA MBEYA LEO

0
0











AJALI YA MOTO KUUNGUZA NYUMBA NA KUSABABISHA MAJERUHI NA UHARIBIFU WA MALI.

Mnamo tarehe 12.03.2019 majira ya saa 20:00 usiku huko katika Kitongoji cha Mapogoro, Kijiji cha Kapunga, Kata ya Itamboleo, Tarafa ya Ilongo, Wilaya ya Mbarali, Mkoa wa Mbeya, CATHERINE MFIKWA [32] Mkazi wa Kapunga pamoja na mtoto wake aitwaye PRISCAN PIUS @ MWAFWALO [14] Mkazi wa Kapunga walijeruhiwa kwa kubabuliwa na moto sehemu za miguu yao kutokana na moto uliozuka ghafla kwenye duka lao.
Katika tukio hilo moto huo ulisababisha uharibifu wa bidhaa zilizokuwa zinauzwa kwenye maduka ya (1) PIUS AIDAN @ MWAFWALO [41] Mkazi wa Kapunga, aliyekuwa anauza vinywaji baridi (2) JOMBAA @ RAS aliyekuwa anauza vitu vya jumla (3) JUMA MWAMJINGA aliyekuwa anauza bidhaa za dukani na mahindi.
Majeruhi wamelazwa na wanapata matibabu katika Hospitali ya Misheni Chimala na wanaendelea vizuri. Bidhaa zote zilizokuwa zipo stoo zimeokolewa na zimekabidhiwa kwa wamiliki. Chanzo cha ajali hiyo ya moto ni kulipuka kwa jiko la gesi lililokuwa linatumiwa na CATHERINE MFIKWA (mke wa PIUS AIDAN @ MFIKWA) na kushika kwenye bidhaa za dukani na kusambaa kote. Moto huo umezimwa na kikosi cha zimamoto na uokoaji Wilaya ya Mbarali, Polisi na wananchi. Thamani ya mali iliyoungua bado kufahamika.











AJALI YA GARI KUGONGA UZIO NA NYUMBA NA KUSABABISHA MAJERUHI.

Mnamo tarehe 12.03.2019 majira ya saa 14:00 mchana huko maeneo ya Inyala, Wilaya ya Kipolisi Mbalizi, Mkoa wa Mbeya katika barabara ya Mbeya/Iringa, gari no. T. 608 DNP/T. 214 DNW aina ya FAW iliyokuwa ikitokea mkoa wa Songwe kuelekea Dar-es- Salaam ikiwa inaendeshwa na dereva asiyefahamika iliacha njia na kugonga uzio na nyumba inayotumika kwa huduma ya vipimo vya magonjwa mbalimbali ya binadamu [kliniki] na kusababisha majeruhi kwa 1. ZAKARIA CHINA [24] Mkazi wa Uyole ambaye ni mhudumu katika kliniki hiyo, 2. ELIUD FUNGO [38] Mkazi wa Inyala

ambaye ni Daktari wa kliniki hiyo 3. MAGRETHI HASSAN [32] Mkazi wa Inyala aliyekuwa anapata huduma 4. PILI MWANGAMBA [28] Mkazi wa Tunduma na alikuwa abiria kwenye gari hilo. Majeruhi wote wamepata majeraha ya kawaida mwilini na wamelazwa Kituo cha Afya Inyala. Chanzo cha ajali ni ubovu wa gari. Gari hiyo ilikuwa imebeba mzigo aina ya shaba. Msako mkali wa kumtafuta Dereva na mmiliki wa gari unaendelea.



KUFANYA SHUGHULI ZA UGANGA BILA KIBALI (LAMBALAMBA)

Mnamo tarehe 12.03.2019 majira ya saa 07:00 asubuhi huko katika Kijiji na Kata ya Sangambi, Tarafa ya Kiwanja, Wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya, Askari wakiwa katika msako waliwakamata 1. PETER DAUDI [37] Mkazi wa Mlimanjiwa 2. SIMON PAMBO [44] Mkazi wa Sangambi 3. AZOLE MWANAHELA [31] Mkazi wa Sangambi na 4. MASUMBUKO CHARLES @ MWANAHELA [36] Mkazi wa Sangambi wakiwa wanafanya shughuli za uganga wa lambalamba isivyo halali. Watuhumiwa walikamatwa wakiwa na madawa mbalimbali ya kienyeji, manyanga na ngoma mbili. Watuhumiwa wengine walitoroka kabla ya kutiwa nguvuni na juhudi za kuwasaka zinaendelea.

TAARIFA YA KIFO – RUNGWE.
Mnamo tarehe 07/03/2019 saa 12:30 mchana huko katika Mto Kiwira uliopo Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya Mwanafunzi wa Chuo cha Ualimu Tukuyu Mwaka wa Tatu aitwaye SAMWEL JAMES CHACHA [25] alikufa maji akiwa anaogelea kwenye Mto huo na mwili wake kutoonekana baada ya kusombwa na maji.
Kutokana na tukio hilo zilifanyika jitihada za kuutafuta mwili wa mwanafunzi huyo ambapo tarehe 11/03/2019 majira ya saa 16.00 jioni huko katika Kijiji cha Mboyo, Kata ya Lupepo, Tarafa ya Ukukwe, Wilaya ya Rungwe na Mkoa wa Mbeya kwenye mto kiwira mwili wa mwanafunzi huyo ulipatikana.
Chanzo cha tukio ni uzembe wa marehemu kutaka kuogelea kwenye mto huo bila kuchukua tahadhari. Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Rungwe – Makandana kusubiri uchunguzi wa kitabibu. Upelelezi unaendelea.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linatoa tahadhari kufuatia matukio ya kufa maji yanayosababishwa na uzembe wa kutovaa maboya wakati wanapoingia majini, mtoni au ziwani. Aidha kufuatia mvua zinazonyesha nawasihi wazazi kuwapeleka watoto wadogo shuleni na kuwapokea ili kuwalinda dhidi ya madhara ya kutumbukia katika maji.

KUZINI NA MAHARIMU.

Mnamo tarehe 09.03.2019 saa 21:00 usiku huko Mtaa wa Ghana, Tarafa ya Sisimba, Jiji na Mkoa wa Mbeya TUMAINI MWASOMI, Mkazi wa Mama John aligundua kubakwa kwa binti yake aitwaye CAREEN BONIPAHCE [14] Mkazi wa Ghana, Mwanafunzi wa Kidato cha Kwanza katika Shule ya Sekondari LEJIKO na baba yake mzazi aitwaye BONIPHACE JULIUS [42] Mkazi wa Ghana.

Aidha CAREEN BONIPHACE anaishi Ghana na baba mzazi baada ya kutengana na mama yake na ndipo baba yake akaanza kumbaka mara kwa mara tangu Septemba, 2018 bila kumwambia mtu yeyote na ndipo juzi tarehe 09.03.2019 majira ya saa 21:00 usiku baba yake alitaka kumbaka tena na ndipo binti huyo alikataa na baba yake alianza kumpiga na kumsababishia maumivu makali mwilini na hivyo kupelekea kumsimulia shangazi yake aitwaye LUCY MWASUMBULE juu ya vitendo vya kubakwa anavyofanyiwa na baba yake.
Chanzo cha tukio ni tamaa za kimapenzi. Mtuhumiwa amekamatwa na yupo mahabusu. Mhanga anaendelea na matibabu Hospitalini.



KUPATIKANA NA MICHE YA BHANGI.

Mnamo tarehe 10.03.2019 saa 07:00 asubuhi huko eneo la Mapanga, Kijiji cha Stamiko, Kata ya Mkola, Tarafa ya Kiwanja, Wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya. Askari Polisi walikamata miche 30 ya bhangi ikiwa imelimwa kwenye shamba la mahindi lenye ukubwa wa robo heka mali ya NDUSHI SHIJA. Mtuhumiwa alikimbia na juhudi za kumtafuta zinaendelea lakini GUMBA ZALA [32] mkazi wa mapanga-stamiko ambaye ni mke wa mtuhumiwa na LUHENDE SHIJA [18] ambaye ni mtoto wa mtuhumiwa wamekamatwa kwa mahojiano. Mtuhumiwa ni mkulima na muuzaji wa bhangi. Upelelezi unaendelea.

MALI YA KUOKOTA.

Mnamo tarehe 10.03.2019 saa 21:30 usiku huko Kitongoji cha Lubele, Kata ya Ikimba, Tarafa ya Unyakyusa, Wilaya ya Kyela, Mkoa wa Mbeya. Askari Polisi wakiwa doria pamoja na kikundi cha ulinzi shirikishi waliona gari aina ya Toyota Ractics rangi nyeupe ikiwa imeegeshwa maeneo ya uchochoroni kwenye pagala na watu wasiofahamika ambapo msako mkali wa kuwatafuta watuhumiwa unaendelea. Watuhumiwa waliacha gari hilo.
Baada ya kulikagua iligundulika kubomolewa kioo kidogo cha mbele upande wa dereva na pia kuharibika mfumo wa kuwashia gari, hivyo kuunganisha nyaya kwa urahisi wa kuliwasha. Gari hilo lilikuwa limebandikwa namba za kitanzania T 512 DCL na ndani ya gari hilo kumekutwa nyaraka zinazoonyesha kuwa ni IT iliyokuwa ikielekea Blantyre nchini Malawi. Ufuatiliaji unaendelea

KUPATIKANA NA MALI ZIDHANIWAZO ZA WIZI.

Mnamo tarehe 10.03.2019 saa 10:00 asubuhi huko maeneo ya ZZK Mbalizi na maeneo mbalimbali ya Mbalizi Wilaya ya Kipolisi Mbalizi. Askari Polisi wakiwa katika msako wa wahalifu na uhalifu na matukio ya uvunjaji walimkamata GOODLUCK JOSHUA [21] mkazi wa Nsalala akiwa na speaker mbili kubwa aina ya Dynamic Ailiong na Equalizers 1 aina media com na baada ya mahojiano alikiri kuhusika katika matukio mbalimbali ya uvunjaji na kutaja washiriki wenzake ambao ni JOHN MBEMBEJA, RAMADHANI, BONKE JIRANI na EMMANUEL MAPUNDA wote wakazi wa Mbalizi.

Makazi yao yamefanyiwa upekuzi na kupatikana mali mbali mbali ambazo ni:-
Mashine ya kuchezea bahati nasibu ya kichina 1,
Monitor aina ya dell 1,
CPU aina ya hp 1,
Radio za aina ya sub woofer zenye majina mbalimbali 5 na speaker zake 8,
King’amuzi cha kampuni ya startimes 1,
Mashine za kunyolea nywele aina home cut 2,
Cable ya umeme aina tronic 1,
Deck ya cd aina singsung 1,
Keyboard na mtungi mdogo wa gas kampuni ya Orexy,
Burner, pamaoja na stand yake mali zote zikidhaniwa kuwa za wizi.
Baadhi ya mali zimetambuliwa katika matukio ya uvunjaji. Mbinu ni kuvunja makufuri ya maduka na sehemu za biashara nyakati za usiku na kuiba.

Imesainiwa na:
[ULRICH O. MATEI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA

KUPATIKANA NA MALI ZIDHANIWAZO ZA WIZI.

Mnamo tarehe 10.03.2019 saa 10:00 asubuhi huko maeneo ya ZZK Mbalizi na maeneo mbalimbali ya Mbalizi Wilaya ya Kipolisi Mbalizi. Askari Polisi wakiwa katika msako wa wahalifu na uhalifu na matukio ya uvunjaji walimkamata GOODLUCK JOSHUA [21] mkazi wa Nsalala akiwa na speaker mbili kubwa aina ya Dynamic Ailiong na Equalizers 1 aina media com na baada ya mahojiano alikiri kuhusika katika matukio mbalimbali ya uvunjaji na kutaja washiriki wenzake ambao ni JOHN MBEMBEJA, RAMADHANI, BONKE JIRANI na EMMANUEL MAPUNDA wote wakazi wa Mbalizi.

Makazi yao yamefanyiwa upekuzi na kupatikana mali mbali mbali ambazo ni:-
Mashine ya kuchezea bahati nasibu ya kichina 1,
Monitor aina ya dell 1,
CPU aina ya hp 1,
Radio za aina ya sub woofer zenye majina mbalimbali 5 na speaker zake 8,
King’amuzi cha kampuni ya startimes 1,
Mashine za kunyolea nywele aina home cut 2,
Cable ya umeme aina tronic 1,
Deck ya cd aina singsung 1,
Keyboard na mtungi mdogo wa gas kampuni ya Orexy,
Burner, pamaoja na stand yake mali zote zikidhaniwa kuwa za wizi.
Baadhi ya mali zimetambuliwa katika matukio ya uvunjaji. Mbinu ni kuvunja makufuri ya maduka na sehemu za biashara nyakati za usiku na kuiba.

Imesainiwa na:
[ULRICH O. MATEI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS YOWERI MUSEVENI JIJINI KAMPALA

0
0
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa Africa Now Summit 2019 katika hoteli ya Munyonyo Commonwealth Resort mjini Kampala, Uganda. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI MACHI 14,2019

0
0
















SERIKALI YATOA ONYO KALI KUTANGAZA MILIPUKO YA MAGONJWA YA MIFUGO NCHINI

0
0

WAZIRI Mpina akishiriki katika zoezi la uogeshaji mifugo kwenye Josho la kwanza kujengwa na Wajerumani katika nchi za Afrika Mashariki liitwalo Nunge lililojengwa mwaka 1905 lililoko wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina wa kwanza kushoto mwenye koti jeupe kwenye picha ya pamoja na wadau mballimbali mara baada ya kutoa hotuba ya tathmini ya zoezi la uogeshaji kitaifa iliyofanyika kwenye josho la kwanza kujengwa na Wajerumani katika nchi za Afrika Mashariki liitwalo Nunge lililojengwa mwaka 1905 lililoko wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma.



NA JOHN MAPEPELE, MPWAPWA

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amepiga marufuku mtu yoyote kutangaza kuwepo magonjwa ya mifugo nchini isipokuwa yule aliyepewa mamlaka hayo kwa kuwa kufanya hivyo ni kinyume na taratibu za nchi na kwamba hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote atakayebainika.

Akizungumza hivi karibuni katika tathmini ya kampeni ya uogeshaji kitaifa iliyofanyika kwenye josho la kwanza kujengwa na Wajerumani katika nchi za Afrika Mashariki liitwalo Nunge lililojengwa mwaka 1905 lililoko wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina alisema Sheria za kimataifa na Sheria ya Magonjwa ya Mifugo Namba 17 ya mwaka 2003 inazuia kufanya hivyo.

Kwenye tathmini hiyo ya miezi mitatu kuanzia Novemba 2018 hadi Februari 2019 jumla ya Mifugo milioni 32 sawa na asilimia 56 ya mifugo milioni 57 iliyopo nchini iliogeshwa ambapo kati ya mifugo iliyoogeshwa ng’ombe milioni 19.9, mbuzi milioni 8.9, kondoo milioni 2.88, punda 224 na mbwa 229,000 huku majosho yanayofanya kazi nchini ni 1,197 kati ya majosho 2,300 lakini majosho 1,124 ni mabovu hayafanyi kazi vikundi 847 vimeundwa na kufungua akaunti vikundi 612


Aidha Mpina alisisitiza kuwa shabaha ya kuzuiwa kufanya hivyo kwa sababu baadhi ya watu wanaweza kujitokeza kupeleka hofu kwa wananchi na kusababisha kuharibu biashara hiyo na hivyo mwenye dhamana ya kufanya hivyo ni Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo na sio mtu mwingine yoyote yule.

Hivyo Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo ndiye aliyepewa dhamana ya kutangaza ugonjwa wowote wa mifugo kwa niaba ya watanzania na wala sio mtendaji yoyote yule wa Serikali

Alisema nchi yetu imejipanga vizuri kudhibiti magonjwa ya mifugo na ndio maana inazo kanda nane za uchunguzi wa magonjwa ya mifugo hivyo watanzania wako salama Tanzania iko huru na magonjwa na sasa tunazalisha chanjo 8 kufikia mwezi 9 hadi mwakani kutakuwa na chanjo 11 ili mifugo ichanjwe isipatwe tena na magonjwa.

Hivyo Waziri Mpina ilifakapo Julai mosi mwaka huu wizara yake itakuwa imeshatoa kanuni za namna ya uendeshaji wa zoezi la uogeshaji ili kila mmoja afahamu wajibu wake.

Pia Waziri Mpina alisisitiza agizo lake la ukarabati wa majosho na kwamba ifikapo Julai mosi mwaka huu halmashauri ambayo itakuwa hajakarabati majosho itazuiliwa kukusanya mapato huku akizindikia barua za kusudio la kuzizuia kukusanya mapato halmashauri hizo.

Majosho 132 kati ya majosho mabovu 1,124 yameshakarabatiwa ni asilimia 11 ya agizo hilo limetekelezwa leo miezi mitatu na kuupongeza Mkoa wa Kagera ambao wamekarabati majosho 34, Mkoa wa Mwanza wamekarabati majosho 19, Mkoa wa Arusha majosho 11 wengine hawajafanya hivyo

Mpina alisema halmashauri zote nchini zinakusanya zaidi ya shilingi bilioni 30 kwa mwaka mapato yanayotokana na sekta ya mifugo lakini ni halmashauri chache zinazotenga fedha kidogo za kusaidia mifugo huku Mkoa wa Dodoma hadi sasa umekarabati majosho mawili tu

Alisema mwongozo unaelekeza asilimia 15 ya mapato yanayokusanywa kutoka kwa wafugaji iende kutoa huduma kwa mifugo ikiwemo ukarabati wa majosho, malambo na chanjo hivyo lazima fedha zitengwe kwenda kwa wafugaji.

Hivyo Waziri Mpina aliziagiza Mamlaka zote zinazosimamia zoezi la uogeshaji kusimamia mwongozo uliotolewa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi ikiwa ni pamoja na kila josho kuwa na kikundi na kiwe kimefungua akaunti.

MATUKIO KATIKA PICHA ZIARA YA WAZIRI MWAKYEMBE MKOANI SINGIDA KUJIONEA MAENEO YA URITHI WA UKOMBOZI WA BARA LA AFRIKA

0
0

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akisoma moja ya kaburi la wakoloni wa Kijerumani eneo la Kilima Tindewakati akiwa katika ziara ya kikazi katika mkoa wa Singida kwa ajili ya kutembelea maeneo ya historia ya ukombozi wa Bara la Afrika ikiwa ni mikakati ya kuhamasisha viongozi na wananchi kutunza, kuhifadhi na kuyaendeleza maeneo hayo kwa matumizi ya kizazi cha sasa na kijacho.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akiangalia eneo lilotumiwa na wakoloni wa Kijerumani eneo la Kilima Tindewakati wa ukoloni akiwa katika ziara ya kikazi katika mkoa wa Singida kwa ajili ya kutembelea maeneo ya historia ya ukombozi wa Bara la Afrika ikiwa ni mikakati ya kuhamasisha viongozi na wananchi kutunza, kuhifadhi na kuyaendeleza maeneo hayo kwa matumizi ya kizazi cha sasa na kijacho.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akiangalia handaki lilotumiwa na wakoloni wa Kijerumani eneo la Kilima Tindewakati wa ukoloni akiwa katika ziara ya kikazi katika mkoa wa Singida kwa ajili ya kutembelea maeneo ya historia ya ukombozi wa Bara la Afrika ikiwa ni mikakati ya kuhamasisha viongozi na wananchi kutunza, kuhifadhi na kuyaendeleza maeneo hayo kwa matumizi ya kizazi cha sasa na kijacho.

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KATIBA NA SHERIA YATEMBELEA UJENZI WA MAJENGO YA MAHAKAMA MBEYA

0
0
 Jengo la Mahakama ya wilaya ya Rungwe na Mahakama ya Mwanzo ya Rungwe mjini likiwa katika hatua za awali za ujenzi. jengo hili linajengwa na Mkandarasi M/S Moladi Tanzania Ltd na kusimamiwa na Chuo Kikuu cha Ardhi kama Mtaalam Mshauri. Ujenzi ulianza kutekelezwa mwaka wa fedha 2017/2018 na unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Aprili 2019. Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria walitembelea na kukagua ujenzi wa jengo hili leo mkoani Mbeya.
 Mhandisi wa Mahakama ya Tanzania Bwn Khamadu Kitunzi akiwaelezea waheshimiwa wabunge kuhusu utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa majengo ya Mahakama.

  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akisikiliza ufafanuzi juu ya mradi wa ujenzi wa Mahakama kutoka kwa Mhandisi wa Mahakama ya Tanzania Bwn Khamadu Kitunzi (hayupo pichani) walipoongozana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria walipotembelea mradi huo.

 Jengo la Mahakama ya Mwanzo Uyole likiwa katika hatua za ukamilishwaji (finishing) Jengo hili linajengwa na Mkandarasi M/S PIM Innovators na kusimamiwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) mkoa wa Mbeya. Ujenzi ulianza Desemba mwaka jana na unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Aprili 2019. Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria walitembelea na kukagua ujenzi wa jengo hili leo mkoani Mbeya.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria walipotembelea mradi wa ujenzi wa Mahakama ya Mwanzo Uyole.Lydia Churi Ntambi.



Na Lydia Churi- Mahakama-Mbeya


Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wameanza ziara ya kukagua miradi ya ujenzi wa majengo ya Mahakama ya Tanzania inayoendelea nchini ambapo leo wajumbe hao wametembelea miradi iliyopo wilayani Rungwe pamoja na Uyole jijini Mbeya. 

Pamoja na wajumbe wa kamati hiyo, Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga pamoja na Katibu Mkuu wa wizara hiyo Prof. Sifuni Mchome pia walikuwa ni miongoni mwa watu walioshiriki kwenye ziara hiyo. 

Katika ziara hiyo mkoani Mbeya, wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya Katiba na Sheria walianza kwa kutembelea mradi wa ujenzi wa Mahakama ya wilaya ya Rungwe ambao bado uko katika hatua za awali. 

Mradi huu uliopangwa kutekelezwa mwaka 2017/2018 unahusisha huduma za mahakama ya wilaya na ya Mwanzo mjini Rungwe ambao unatekelezwa na Mkandarasi M/S Moladi Tanzania Ltd na kusimamiwa na Chuo kikuu cha Ardhi kama Mtaalamu Mshauri. 

Aidha, Mradi wa Ujenzi wa Mahakama ya wilaya na ya Mahakama ya Mwanzo Rungwe mjini ulianza kutekelezwa mwaka jana na unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Aprili mwaka huu. 

Baada ya kutembelea ujenzi wa Majengo ya Mahakama wilayani Rungwe, wajumbe wa Kamati hiyo pia walitembelea ujenzi wa Mahakama ya Mwanzo Uyole ulioanza kutekelezwa Desemba 2018 na unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi April mwaka huu. 

Mradi huu unatekelezwa na Mkandarasi M/S PIM Innovators na kusimamiwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) mkoa wa Mbeya kama Mtaalamu Mshauri. Hatua iliyofikiwa sasa ni kuezeka na kuanza kazi za umaliziaji( finishing) 

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria pia wanatarajia kutembelea na kukagua ujenzi wa Mahakama katika mkoa wa Arusha na Manyara.

RC KIGOMA ATOA ONYO KWA WEZI WA MIUNDOMBINU YA SERIKALI

0
0

Na Rhoda Ezekiel Kigoma,

MKUU wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emanuel Maganga amewataka vijana mkoani Kigoma kuacha wizi wa miundombinu ya Serikali na kwa atakayekamatwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Hayo aliyasema leo wakati wa uzinduzi wa Sanamu ya Samaki aina ya Mgebuka ambapo alisema kumekuwa na tabia ya vijana wengi kuiba taa za barabarani na wengine kuvamia majimbani na kuiba, na kuwataka waache tabia hiyo na kufanya kazi.

Aidha Mkuu huyo alisema kuanzia sasa wafanyabiashara mkoani Kigoma waanze kufanya hadi saa sita usiku tofauti na mwanzo ambapo walikuwa wakifunga maduka yao saa kumi na mbili jioni kwa kuwa ulinzi umeboreshwa mkoani Kigoma na Miundombinu imeboresha kwa kuwa Serikali imejipanga kuwasaidia Wananchi kuleta maendeleo.

Alisema Kwa yeyeto atakayekamatwa akijihusisha na ujambazi hawatamvumilia, na kutoa onyo kwa kikundi cha vijana kinacho jishughulisha na masuala ya ubakaji na wizi kuacha maramoja na endapo watakamatwa serikali itawachukulia hatua .

Kwa upande wake Meneja wa Wakala wa barabara was Barabara nchini Tanzania( TANROADS) Naris Choma alisema,ujenzi wa sanamu ya Samaki ni maagizo ya Serikali kwamba barabara zote zinazo hudumiwa na TANROADS kuboreshwa iliziweze kuwa na maadhari nzuri na ziweze kuwahudumia wananchi.

"Na leo wameanza na sanamu ya Mgebuka inaashiria ni samaki anaepatikana katika Ziwa Tanganyika na kwa heshima ya Wakazi wa Kigoma kuweka Sanamu hii kuonyesha vivutio vilivyopo mkoani Kigoma,", amesema.

Alisema ujenzi wa sanamu umegharimu kiasi cha shilingi milioni saba na laki moja na umeambatana na mzunguko ambao nao umeghalimu kiasi cha shilingi milioni 187 pamoja na taa.

Pia wanatarajia kufanya Upanuzi wa mifereji na upanuzi wa barabara, ujenzi wa daraja la waenda kwa miguu katika Soko la Kigoma kupunguza msongamano wa Watu na Magari.

Nao baadhi ya Wananchi akiwemo Alex Dackriss alisema hatua hiyo ni nzuri na wameipongeza Serikali kwa kujenga sanamu hiyo kwa kuwa walizoe kuona smaki Mwanza na wanaahidi kuitunza miundombinu hiyo kwa kuwafichua wote watakao baini wanafanya wizi wa miundombinu ya Serikali.

Juma Kizza nae ni mkazi wa Kigoma alisema Wamefarijika kuona mgebuka na maendeleo ya naendelea mkoani Kigoma na kuwaomba Vijana wafanye kazi na kuacha kuiba miundombinu ambayo inawasaidia wenyewe.

Alisema Suala la kufanya biashara hadi usiku wanampongeza Mkuu wa Mkoa wa uamuzi huo na kuomba ulinzi kuimalishwa na kuboresha miundombinu itakayo ruhusu biashara kufanyika.
 Picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi huo 
 
 Wanachi wakishngilia baada ya kufanyika uzinduzi huo
  Sanamu yasamaki aina  mgebuka baada ya kuzinduliwa rasmi
MKUU wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emanuel Maganga kwa pamoja wakikata utepe kuzindua  Sanamu ya Samaki aina ya Mgebuka ambapo alisema kumekuwa na tabia ya vijana wengi kuiba taa za barabarani na wengine kuvamia majumbani na kuiba, na kuwataka waache tabia hiyo na badala yake wajitume kufanya kazi.

MKOA WA KIGOMA WAZINDUA SANAMU YA PICHA YA MGEBUKA

0
0
Na Editha Karlo wa blog ya jamii Kigoma.

MKUU wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emanuel Maganga amewataka wakazi wa Kigoma kuacha tabia ya kuharibu miundombinu ya barabara ili Makao makuu ya Mkoa yasiwe kama kijiji.

Maganga ameyasema hayo leo round about ya Mwanga kwenye zoezi la uzinduzi wa picha ya sanamu ya samaki aina ya mgebuka kama utambulisho wa rasilimali kwa wageni kwa Mkoa wa Kigoma.

Alisema baadhi ya wakazi Kigoma siyo waaminifu wamekuwa wakifanya uhalifu wa kuharibu miundombinu ya barabara iliyowekwa na serekali kwa gharama kubwa hali inayofanya mji kushindwa kuendelea na kuwa wa kisasa.

"Serikali yetu imekuwa ikitumia fedha nyingi kuboresha miundombinu ya barabara lakini kuna wahalifu wachache wamekuwa wakiharibu miundombinu hiyo,tulifunga za sora za barabarani zikaibiwa mji ukawa giza,yeyote atakayekamatwa anaharibu miundombinu hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake."alisema Maganga

Maganga pia amewataka wakazi wa Kigoma kutunza mazingira kwa kuweka maeneo yao ya makazi na biashara kuwa safi,pia kuacha tabia ya kuacha mifugo inazagaa ovyo mitaani na barabarani.

"Mji wetu umekuwa kama kijiji ukipita mitaani mitaro ya maji machafu,mifugo inazagaa ovyo mitaani,tuutunze mji wetu uwe wa kisasa pia naagiza wafanyabiashara wote waache kufunga maduka saa 12,biashara zifanyike hadi saa sita ikiwezekana hadi asubuhi nina wahakikishia kuwepo kwa ulinzi wa kutosha"alisema

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Samson Hanga amewataka pia wakazi wa Kigoma kutunza picha ya rasilimali ya samaki aina ya mgebuka iliyozinduliwa leo kama alama ya utambulisho wa Mkoa wa Kigoma.

"Sanamu huyu amegharamiwa pesa nyingi kutengenezwa nawaomba sana tuitunze ili iweze kudumu,wakati ujenzi unaendelea hapa tuliifunika na turubai lakini kuna watu waliiba lile turubai tukiwakamata hatutawaoenea haya"alisema Mkuu wa Wilaya.

Meneja wa Tanroad wa Mkoa wa Kigoma Injinia Nalis Choma alisema mradi wa kujenga sanamu ya picha ya mgebuka umegharimu jumla ya shilingi za kitanzania milioni 7 huku milioni 187 zikigharimu ujenzi wa barabara mzunguko(round about)pamoja na mataa.

Choma alisema kuwa wanatekeleza maagizo ya serikali ya kuboresha barabara za Tanroad.

 Wakazi wa Kigoma wakiangalia Picha ya sanamu ya samaki aina ya Mgebuka iliyozinduliwa leo na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Emanuel Maganga kwenye mzunguko wa barabara(round about)ya Mwanga ikiwa kama ishara ya moja ya rasilimali zinazopatikana Mkoani humo
Wakazi wa Kigoma wakipiga picha ya sanamu ya picha ya samaki aina ya mgebuka baada ya kuzinduliwa leo


 Mkuu wa Mkoa wa Kigoma akikata utepe kuashiria uzinduzi wa sanamu ya picha ya Mgebuka kwenye round about ya Mwanga

NITAIPIMA NFRA KWA KUNUNUA TANI 500,000 ZA NAFAKA KWA WAKULIMA-HASUNGA

0
0
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) na Mwakilishi Mkazi wa Mpango wa Chakula Duniani (WFP) Bw Michael Dunford wakiwasha soketi ya mtambo wa kusafisha nafaka ikiwa ni ishara ya uzinduzi katika hafla iliyofanyika makao makuu ya NFRA, Jijini Dodoma leo tarehe 14 Machi 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe Patrobas Katambi wakikagua mtambo wa kusafisha nafaka katika hafla iliyofanyika makao makuu ya NFRA, Jijini Dodoma leo tarehe 14 Machi 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akihutubia katika hafla ya kukabidhi mtambo wa kusafisha nafaka kwa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kutoka kwa Mpango wa Chakula Duniani (WFP), makao makuu ya NFRA, Jijini Dodoma leo tarehe 14 Machi 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) na Mwakilishi Mkazi wa Mpango wa Chakula Duniani (WFP) Bw Michael Dunford wakizindua mtambo wa kusafisha nafaka katika hafla iliyofanyika makao makuu ya NFRA, Jijini Dodoma leo tarehe 14 Machi 2019.
Sehemu ya washiriki wakifatilia hotuba ya Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) wakati akizungumza katika hafla ya kukabidhi mtambo wa kusafisha nafaka kwa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kutoka kwa Mpango wa Chakula Duniani (WFP), makao makuu ya NFRA, Jijini Dodoma leo tarehe 14 Machi 2019.


Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma

Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) umetakiwa kuhakikisha kuwa katika msimu huu wa mwaka 2019/2020 unanunua mahindi kwa zaidi ya Tani 500,000 kwa wakulima ili kutimiza azma ya serikali ya kuimarisha masoko ya wakulima.

NFRA pia imetakiwa Kubadili mfumo wa ununuzi wa mahindi ili kupunguza gharama kubwa zinazojitokeza wakati wa msimu wa ununuzi. Hayo yamebainishwa na Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) leo tarehe 14 Machi 2019 katika hafla ya kukabidhi mtambo wa kusafisha nafaka kwa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kutoka kwa Mpango wa Chakula Duniani (WFP), makao makuu ya NFRA, Jijini Dodoma.

Hasunga alisema kuwa NFRA imekuwa ikinunua nafaka kidogo kwa wakulima kwa ajili ya kuhifadhi pekee badala yake wametakiwa kufanya biashara ya kununua na kuuza nafaka kwa wingi.

Alisema WFP imekuwa mdau mkubwa wa maendeleo nchini kwa muda mrefu na kwa upande wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula, ushirikiano huo umedumu tangu mwaka 2012. WFP na NFRA wamekuwa wakishirikiana kikamilifu katika kutekeleza majukumu yao kwa manufaa ya pande zote mbili.Mpango Mkakati wa WFP wa miaka mitano (Country Strategy Plan 2017-2021) unaendana na mipango ya Serikali inayolenga kufikia Maendeleo Endelevu ya Dunia (SDGs), hususani lengo la kutokomeza njaa (Zero Hunger) ifikapo mwaka 2030. 

Aliongeza kuwa, mkakati wa WFP wa kuwasaidia wakulima wadogo kupitia mpango wa Farm To Market Alliance (FTMA) unashabihiana na Mpango wa Kuendeleza Sekta ya Kilimo nchini (ASDP II), kwa kuwa mikakati yote imelenga katika kuwasaidia wakulima kuongeza uzalishaji, kupunguza upotevu wa mazao baada ya mavuno, kuongeza thamani ya mazao na kufikia masoko.

Mhe Hasunga alisema kuwa kutokana na mkakati huo, Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, inathamini na kuipongeza WFP katika kuimarisha usalama wa chakula na lishe hapa nchini. 

Aidha, alisema serikali inaishukuru WFP kwa kuichagua Tanzania kuwa moja wapo ya Kituo cha Usimamizi wa Bidhaa za Kimataifa (Global Commodity Managed Facility) ambacho kinasaidia kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa masoko ya mazao ya chakula kwa wakulima nchini.

Vivevile, Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) alimuhakikishia Mwakilishi Mkazi wa WFP Michael Dunford kuwa WFP haikukosea kuichagua Tanzania kuwa Kituo cha Usimamizi wa Bidhaa za Kimataifa (GCMF) kuwa, ukiacha faida za kijiografia, Tanzania inajivunia kuwa na kiwango kizuri cha utoshelevu wa chakula. Mfano, katika mwaka huu, nchi ina kiwango cha utoshelevu wa chakula kwa 124%, hivyo, nchi ina ziada ya chakula, hii inadhibitisha na kuwahakikishia kuwa Tanzania ina uwezo wa kuuza kwa WFP tani zaidi ya 200,000 wanazohitaji za chakula ambapo ni hitaji lao la kila mwaka.

WASHINDI 15 WAPATIKANA PROMOSHENI YA TIA KITU PATA VITUUZ NA DSTV

0
0




Mkuu wa kitengo cha thamani kwa wateja kampuni ya Multichoice kupitia king'amuzi cha Dstv Hilda nakajumo akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutangaza washindi 15 waliopatikana katika droo ya 3 ya promosheni ya tia kitu pata vituuz akiwa pamoja na Afisa Mwandamizi wa bodi ya michezo ya kubahatisha Humud Abdulhussein .


Na.Khadija seif,Globu ya jamii

KAMPUNI ya Multichoice nchini kupitia king'amuzi cha Dstv imechezesha droo ya 3 ya promosheni ya tia vitu upate vituuzi jijini Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa kitengo cha thamani kwa wateja Hilda nakajumo wakati wa kutangaza washindi hao 15 waliopatikana katika kila vifurushi kama Compart plus,family , premier pamoja na kifurushi cha bomba amesema ni wakati wa wateja kunufainika na kufaidika na kuendelea kuuwasha moto kiburudani zaidi.

"Leo tumefanikiwa kupata washindi 15 kutoka mikoa mbalimbali kama vile Arusha ,Kagera,Manyara pamoja na Dar es salaam inaonyesha wazi king'amuzi cha dstv kinaendelea kutoa huduma nzuri na gharama nafuu,alisema nakajumo"

Aidha amesema washindi hao wamezawadiwa malipo ya miezi miwili bure ili kuendelea kufaidika na vipindi mbalimbali kupitia King'amuzi cha dstv.

Hata hivyo kwa upande wake Afisa Mwandamizi wa bodi ya michezo ya kubahatisha Humud Abdulhussein amesema ni wakati wa wateja wa dstv kulipia ving'amuzi vyao kwa wakati ili kupata ofa hiyo ."Hakuna mtu ambae anapangwa droo inachezeshwa kwa haki bila janja yoyote pamoja na vigezo na masharti vinazingatiwa ipasavyo ," alisema Abdulhussein.

Na Mshindi wa kifurushi cha Compart mkazi wa jijini Mwanza Musa juma mwenye umri wa miaka 24 amewapongeza dstv kwa promosheni hiyo ya tia vitu pata vituuz."Sikutegemea kama ningeweza kushinda katika droo hii ya 3 mara nyingi nasikia tu wenzangu wakishinda nikajaribu bahati yangu na nikaamua kulipia kwa wakati king'amuzi changu hatimae nimeibuka mshindi," alisema juma

Pia amewapa ujasiri wateja wengine kulipa kwa wakati ili waweze kuingia kwenye droo hiyo na kushinda kabisa.

SERIKALI WILAYANI HAI ,KUBATILISHA UMILIKI WA VIWANJA 34 ,VIMO VIWANJA VYA VIGOGO.

0
0
Mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya akizungumza na wananchi waliofika kwa ajili ya kuwasilisha kero juu ya Ardhi katika ukumbi wa mikutano wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) usharika wa Hai mjini.
Katibu tawala wa wilaya ya Hai,Upendo Wella akizungumza wakati wa siku ya kwanza iliyotengwa na Wilaya ya Hai kushughulikia kero zinazohusua masuala ya migogoro ya Ardhi katika wilaya hiyo.
Badhi ya wananchi waliojitokeza kuwasilisha kero zao katika ukumbi wa KKKT usharika wa Hai mjini .
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,Yohana Sintoo akizungumza katika mkutano huo wa kushughulikia kero za Ardhi katika wilaya hiyo.
Badhi ya wananchi waliofika kuwasiliha kero zao.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,Yohana Sintoo (kushoto) akimueleza jambo mkuuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya (kulia)  wakati wa siku ya kusikiliza kero juu ya masuala ya Ardhi inayofanyika katika mji wa Bomang'ombe.
Katibu tawala wa wilaya ya Hai,Upendo Wella akimueleza jambo mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya wakati wa usikilizaji wa keo juu ya masula ya ardhi katika wilaya ya Hai.
Baadhi ya wakuu wa idara katika Halmashauri ya wilaya ya Hai wakisiliza malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusu masuala ya ardhi.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,Yohana Sintoo akisikiliza malalamiko juu ya masuala ya Ardhi kutoka kwa wananchi wa wilaya hiyo.
Katibu tawala wilaya ya Hai,Upendo Wella akiwa na Mkaguzi wa Polisi,Inspekta Shabo wakichukua maelezo kutoka kwa mmoja wa wananchi walowasilisha malalamiko yao juu ya masuala ya Ardhi.

Mkuu wa wilaya ya Hai.Lengai Ole Sabaya akimsikiliza mmja wa wananchi waliojitokeza kutoa malalamiko yake juu ya suala la Ardhi .
Mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,Yoahana Sintoo wakitizama moja ya malalamiko makubwa ya Ardhi ktaika wilaya hiyo ,lalamiko linalowahusu watu zaidi ya 300 wa eneo la Gezauleole . 

 Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
 
SERIKALI katika wilaya ya Hai imetangaza kubatilisha umiliki wa viwanja 34 kati  52 vilivyopo kwenye eneo la maendelezo ya viwanda la Weruweru katika Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro kutokana na madai mbalimbali ikiwemo kutoyaendeza.

Madai mengine ya kuandikwa kwa ilani hiyo kwa Waziri wa Ardhi, , Nyumba na Maendeleo ya Makazi, imetajwa kuwa ni wamiliki wa maeneo hayo  ni deni la fedha za Pango la Ardhi kwa zaidi ya miaka 20.

Wanaotajwa kumiliki maeneo hayo wamo pia viongozi wa vyama vya siasa,viongozi wa serikali wastaafu,wafanyabiashara ,kampuni zinazo miliki mashamba makubwa pamoja na taasisi zisizo za kiserikali.

Akizungumza katika mkutano wa kwanza wa kushughulikia kero zinazohusu masuala ya Ardhi ,Mkuu wa wilaya ya Hai ,Lengai Ole Sabaya amesema tayari Halmashauri imewasilisha barua kwa Waziri wa Ardhi ili kumfikishia rais wa Jamhuri ya muungano Tanzania kwa ajili ya utiaji saini. 

Idadi hiyo ya watu 34, inafanya jumla ya kiasi cha fedha kinachodaiwa kutokana na pango la ardhi kufikia Sh. 1, 828, 166, 096.

Waliotajwa katika orodha ya wamiliki wa viwanja hivyo ni pamoja na Mbunge w jimbo la Hai, Freeman Mbowe ,Mkuu wa mkoa wa zamani wa Kilimanjaro, Cynthia Hilda Ngoye, Kiwanda cha Kutengeneza Vipuri cha Kilimanjaro Mashine Tools Manufacturing Company Ltd kilichopo chini ya Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) na wafanyabiashara maarufu wa mji wa Moshi na wamiliki wa shule binafsi na makampuni ya utalii.

Sabaya alisema watu hao wamo katika orodha ndefu ya wamiliki ambao viwanja vyao vimeombewa kibali cha kufutwa na kwamba kwa mujibu wa orodha hiyo, Kiwanda cha Mashine Tools kina deni la Sh. milioni 315,720,720 ambalo inadaiwa kati ya mwaka 2010 hadi 2018.

“Huko nyuma watu walipewa viwanja mashine tools, viwanja 52 vikubwa wakaambiwa waendeleze kwa sababu ni eneo la viwanda, wana miaka mingapi? Afisa Ardhi yuko wapi, njoo, nini kimetokea pale.

“Sasa sikilizeni huo mziki, unapewa shamba (eneo la kiwanja) mwaka 1984, mmesikia? kabla mimi sijazaliwa, hajawahi kufanya lolote, akapewa na halmashauri ili waendeleze kujenga viwanda. Sasa Afisa Ardhi ameshaandika barua ya kubatilisha hivyo viwanja…Niwaambie hapa hapa wako watu mnaowaheshimu na hawalipi kodi na leo ntawataja humu.”

Katika mkutano huo, Mkuu huyo wa Wilaya alipokea malalamiko 266 yanayohusu ardhi na kuahidi ndani ya siku mbili yatakuwa yamepata majibu.

Katika mkutano huo, Kaimu Kamishna wa Ardhi Msaidizi wa Mikoa ya Kanda ya Kaskazini, Alphonce Lekule, aliwaeleza wananchi wa Hai kwamba kuwapo idadi kubwa ya malalamiko ni kwa ni changamoto kwa watendaji wa ardhi.

TANZANIA YAPIGA HATUA UWEZESHAJI WANAWAKE

0
0
Na Mwandishi Wetu – New York Marekani

Tanzania ni nchi mmojawapo duniani iliyofanikiwa kupiga hatua katika kuwawezesha wanawake kijikwamua kiuchumi kwa kuwasaidia kupata mikopo isiyo na riba inayowawezesha kuanzisha miradi mbalimbali ya kiuchumi.

Hayo yamesemwa leo na Mh Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, katika Mkutano Mkuu wa 63 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani unaoendelea New York, Marekani.

Waziri Ummy alieleza kuwa Tanzania imepiga hatua katika uwezeshaji wa wanawake kiuchumi kwa kuwapatia fursa za mikopo na kufanyia marekebisho Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa ya mwaka 2018 ambayo imefuta Riba kwa mikopo yote inayotolewa kwa wanawake kupitia Halmashauri.

Alisema Halmashauri zimekuwa zikichangia asilimia 5 ya mapato yao ya ndani kwa ajili ya mikopo kwa wanawake, matokeo yake kiwango cha fedha zinazotolewa na Halmashauri kwa ajili ya mikopo ya wanawake kimeongezeka kutoka bilioni 3.4 mwaka 2015/16 kufikia bilioni 16 mwaka 2017/18. 

Waziri Ummy alieleza kuwa tangu mwaka 2015 Tanzania imepiga hatua kubwa kwa kutoa elimu bure ya Msingi na Sekondari na kufanya ongezeko la asilimia 80 katika uandikishaji wa watoto wa shule za msingi na ongezoko la asilimia 20 kwa Sekondari. 

Ameongeza kuwa katika kuhakikisha watoto wa kike wanapata elimu bila vikwazo vyovyote mwaka 2018 Serikali imefuta tozo ya kodi katika taulo za kike (pads) na hivyo kupelekea upatikanaji wake kuwa rahisi na kwa gharama nafuu ambapo mwanzo watoto wengi wa kike walikuwa wanakosa vipindi madarasani kutokana na kukosa taulo hizo.

Katika huduma za afya, Tanzania imepiga hatua kubwa katika utoaji wa huduma za afya hususan huduma za afya ya mama na mtoto pamoja na maboresho ya miundombinu ya afya na chanjo. Kwa mwaka 2018/19 Kati ya vituo vya afya 518, vituo 304 vimekarabatiwa ili kuboresha huduma za afya ya mama na mtoto ikiwa ni pamoja na huduma za upasuaji na hivyo kuwa na jumla ya vituo 459 nchi nzima vinavyotoa huduma za dhalura na uzazi ukilinganisha na vituo 109 mwaka 2015.

Na katika sekta ya nishati Waziri Ummy alieleza kuwa Tanzania kupitia mradi wa umeme vijijini (REA) imeweza kusambaza umeme katika vijiji zaidi ya 7000 kati ya vijiji 15000 sawa na asilimia 46 ya vijiji vyote nchini hili limesaidia sana kuwawezesha wanawake kupata fursa mablimbali kutokana na upatikanaji wa nishati hiyo kwa urahisi kuanzisha miradi ya kiuchumi ikiwemo viwanda vidogo vidogo.

Ameongeza kuwa kwa mujibu wa Taarifa ya Utafiti wa Upatikanaji wa Nishati Tanzania ya mwaka 2016 asilimia 32.8 ya kaya Tanzania bara zina Umeme, na asilimia 44.2 Zanzibar. Upatikanaji wa umeme umewezesha huduma za afya kupatikana kwa wepesi hasa huduma za uzazi, upatikanaji wa maji na kurahisisha shughuli zingine za uzalishaji mali kwa wanawake.

Mkutano wa 63 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa wa Hali ya Wanawake Duniani kwa mwaka 2019 unaendelea jijini New York Nchini Marekani ukiwa na Kaulimbiu inayosema "Mifumo ya Hifadhi ya Jamii, Huduma za Umma na Miundombinu Endelevu kwa Usawa wa Kijinsia na Uwezeshaji wa Wanawake na Wasichana".
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (Kushoto) akiwa katika katika Mkutano Mkuu wa 63 Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani unaoendelea katika jiji la New York nchini Marekani.

MISA TAN YAENDESHA MAFUNZO KWA WATUMISHI WA MAHAKAMA KILIMANJARO.

0
0
  Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Moshi, Patricia Fikirini,akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu kwa watumishi wa Mahakama,mafunzo yanayoendeshwa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika-Misa tan katika Hotel Ya Leopard mjini Moshi.
Baadhi ya Watumishi wa Mahakama mbalimbali katika mkoa wa Kilimanjaro wanaoshiriki mafunzo hayo  .
  Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (Misa Tan),Salome Kitomary akizungumza wakati wa mafunzo kwa watumishi wa mahakama za mkoa wa Kilimanjaro.
Baadhi ya Watumishi wa mahakama wakishiriki mafunzo hayo yanayofanyika katika Hoteli ya Leopard mjini Moshi.
  Mkurugenzi wa Misa Tan, Gasirugwa Sengiyumva,akiwaleza washiriki wa mafunzo hayo shughuli mbalimbali ambazoo taasisi ya Misa Tan imekuwa ikifanya .
Baadhi ya washiriki katika mafunzo hayo.
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi ,Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu kanda ya Moshi ,Patricia Fikirini pamoja na wakufunzi wakati wa ufunguzi rasimi wa mafunzo hayo .


Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.

KAIMU Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Moshi, Patricia Fikirini,amesema kuwa mafunzo ya huduma kwa wateja na upatikanaji wa taarifa kwa watumishi wa Mahakama ni muhimu kwa kuwa yatapunguza malalamiko kwa watumiaji wa mahakama.

Akizungumza  wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa watumishi wa mahakama za mkoa wa Kilimanjaro, Jaji Fikirini alisema mafunzo hayo yamekuja kwa wakati muafaka kwa kuwa limekuwa ni hitaji la muda mrefu.

Mafunzo hayo yameendeshwa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika-Misa tan, kwa kushirikiana na Taasisi ya Kijerumani ya Friedrich Ebert Stiftung, yanahusu huduma kwa wateja, upatikanaji wa taarifa na maadili kwa utumishi wa umma.

“Mafunzo haya ni msingi wa mabadiliko kwa kilio kwa wateja kutoridhishwa na huduma za mahakama.Natarajia yatazingatiwa na kusaidia kuleta mabadiliko katika kuwahudumia wateja.”alisema Jaji Fikirini.

Aidha, aliwataka watumishi hao kuunda kukosi kazi cha ufuatiliaji wa utekelezaji wa mafunzo hayo ya jinsi wanavyowahudumia wateja wanaofika mahakamani, ili kupunguza malalamiko ambayo yanatoa taswira isiyo sahihi kwa mahakama.

Awali akimkaribisha Jaji Mfawidhi Kanda ya Moshi, Patricia Fikirini, kufungua mafunzo hayo, Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (Misa Tan),Salome Kitomary alisema Misa Tan imepanga kutoa mafunzo mbalimbali kwa watumishi hao wa mahakama.

Alisema mafunzo yatakayotolewa ni pamoja na huduma kwa wateja, upatikanaji wa taarifa na maadili kwa watumishi wa mahakama kwa Mahakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi, Mahakimu wa Mahakama za Wilaya, Mwanzo pamoja na watumishi wa mahakama na watunza kumbukubu 36 wa mkoa wa Kilimanjaro.

Kitomary alisema washiriki hao watafundishwa nini maana ya uhuru wa kujieleza (mambo muhimu na misingi yake), huduma kwa wateja na ujuzi wa mawasiliano kwa watumishi wa umma.

Kadhalika, washiriki watajifunza mifano ya utekelezaji wa uhuru wa kujieleza, Tanzania, Afrika na Duniani, Matakwa ya kisheria ya uhuru wa upatikanaji wa taarifa, muundo wa vyombo/ taasisi za umma na upatikanaji wa taarifa.

Aidha, washiriki hao pia watajifunza jinsi ya kutoa taarifa na kuomba taarifa, ujuzi wa misingi na sifa za kushughulikia malalamiko ndani yake ikiwa ni muundo wa kushughulikia malalamiko,manufaa ya kushughulikia malalamiko kwa wakati, kukabiliana na tabia za ndani na jinsi ya kwuahudumia wateja wenye hulka tofauti na kukabiliana na malalamiko kiufundi katika kukabiliana na hasira na majibu yenye mhemko.

Mada nyingine zinazotarajiwa kuwasilishwa ni pamoja na kukabiliana na kazi zenye malalamiko ambayo ndani yake ina kukubaliana na hatua inayofaa kwa wateja, kuwa wazi juu ya mamlaka/nguvu ulizonazo, kuongezeka kwa malalamiko na mchakato wa usimamizi wa malalamiko, kutoka maoni na kuheshimu ahadi.

Kwa siku ya tatu washiriki watafundishwa au kukumbushwa juu ya kanuni za maadili na maadili kwa watumishi wa umma, utaratibu wa mahakama katika kushughulikia malalamiko.

Mkurugenzi wa Misa Tan, Gasirugwa Sengiyumva, alisema  chanzo cha mafunzo haya ni mwaka 2004 baada ya Mahakama kupata kufuli kwa kutofunguka kutoa taarifa kwa wananchi, utafiti huo ulifanywa na Misa Tan, ukiangalia taasisi za umma ambazo zimefungaka zaidi na ambazo hazikufunguka kutoa taarifa kwa wananchi wa kawaida kabisa.

TPDC YAKABIDHI KAMBI NAMBA 8 KWA SERIKALI YA KIJIJI CHA NJIA NNE WILAYA YA KILWA

0
0
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limeendelea kuimarisha huduma mbalimbali za kijamii kwa Vijiji na Mitaa inayoguswa na miundombinu ya bomba la gesi asilia kutoka Mtwara hadi Dar es salaam. Katika kufikia azma hii TPDC imekabidhi kambi Namba 8 kwa kijiji cha Njia nne Wilayani Kilwa ili Kijiji kiweze kupanga matumizi sahihi ya Kambi hiyo.

Kukabidhiwa kwa majengo ya Kambi hayo kunatokana na kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa miundombinu ya bomba la gesi asilia kutoka Madimba-Mtwara na Songosongo hadi Dar es Salaam, hivyo kufanya majengo hayo kutotumika tena kwa shughuli za ujenzi. 

Akikabidhi rasmi kambi hiyo kwa uongozi wa Serikali ya Kijiji cha Njia nne hivi karibuni, Meneja Mawasiliano na Mahusiano wa TPDC Bi. Marie Msellemu alisema kuwa “Mikoa ya Lindi na Mtwara ni wadau wakubwa katika ustawi wa miundomibinu ya bomba la gesi asilia na tumekuwa tukishirikiana katika mambo mbalimbali ya kimaendeleo na ya kijamii ikiwemo afya, michezo, utawala bora na maji lengo ikiwa ni kudumisha mahusiano mema na kuboresha huduma muhimu za kijamii, na hivyo kuwataka wananchi wa mikoa hii ya kusini kushirikiana na TPDC katika kuilinda miundombinu ya gesi asilia na kwa pamoja kuboresha huduma za jamii’’.
Muonekano wa sehemu ya jengo la Kambi ya Kijiji cha Njia nne Wilaya ya Kilwa
Meneja Mawasiliano na Mahusiano wa TPDC Bi. Marie Msellemu akikabidhi hati ya makabidhiano ya Kambi Namba 8 kwa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kilwa Dr. Khalfan Ilekizemba.
Hati ya Makabidhiano ya Kambi Namba 8 kati ya TPDC na Kijiji cha Njia nne, Wilayani Kilwa.

Akiongea katika hafla ya kukabidhi Kambi hiyo, Kaimu Mkurugezi wa Wilaya ya Kilwa Dr. Khalfani alitoa shukrani za dhati kwa TPDC kwa kuwa mdau mkubwa na wa karibu katika shughuli mbalimbali za maendeleo Wilayani Kilwa hasa katika kuboresha sekta ya elimu na afya.

‘Tunalishukuru Shirika la TPDC kwa kutupatia kambi hii ambayo itasaidia Halmashauri na Kijiji kupanga matumizi sahihi katika nyanja ya afya, Shule au nyumba za watumishi wa umma’’. Pia, alisema kuwa tayari kambi hiyo yenye uwezo wa kuchukua kaya/familia 25 imeshaanza kutumika kwa kusaidia makazi kwa waajiriwa wapya wa Halmashauri. 
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Daktari Khalfani akiwa na jopo la wadau wa maendeleo katika hafla ya kukabidhi kambi. 

Mheshimiwa Diwani wa Kata ya Tingi Bw. Bayani Saidi Mtenda katika kutoa shukrani zake alisema sambamba na TPDC kutoa Kambi hiyo , Serikali ya Kijjji na wananchi kwa ujumla wanawajibu wa kuilinda na kuhakikisha usafi wa mazingira unaimarishwa ili iweze kudumu na kuwa na tija kwa manufaa ya Kijiji. 

Aidha, alisema kwamba Mkutano Mkuu wa Halmashauri ya Kijiji ndiyo utakaoamua na kupanga matumizi ya kambi hiyo ikiwa ni pamoja na kupanga Kodi/tozo kwa watakaobahatika kuyatumia majengo ya Kambi hiyo. 

Bw Bayana alitoa wito kwa TPDC na wadau wengine wa maendeleo kuendelea kusaidia shughuli za maendeleo kijijini hapo kwani Kijiji kinachangamoto kubwa hasa katika Sekta ya elimu na kuweka bayana mapungufu ya vyumba vya madarasa hali inayopelekea wanafunzi kusomea chini ya miti.

UJUMBE WA SHIRIKA LA NGUVU ZA ATOMIKI DUNIANI KANDA YA AFRIKA WAKUTANA NA VIONGOZI WA WIZARA YA AFYA ZANZIBAR

0
0

Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika, Shirika la nguvu za Atomiki Duniani (IAEA) Prof. Shaukat Abdulrazak akizungumza na uongozi wa Wizara ya Afya Zanzibar ulioongozwa na Katibu Mkuu Wizara hiyo Asha Ali Abdalla (kushotoni kwake).

Mkurugenzi Mkuu, Tume ya Nguvu Atomu Tanzania (TAEC) Prof. Lazaro Busagala akisisitiza jambo katika mkutano uliowashirikisha viongozi wa Wizara ya Afya na Ujumbe wa Shirika hilo uliofanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja.

Baadhi ya wakuu wa vitengo mbali mbali vya Wizara ya Afya wakimikiliza Mkurugenzi wa Shirika la nguvu za Atomiki Duniani (hayupo pichani) Profesa Shaukat Abdulrazak.Picha na Makame Mshenga.



Na Ramadhani Ali – Maelezo Zanzibar


Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki Duniani (IAEA) Kanda ya Afrika Profesa Shaukat Abdulrazak amesema Shirika hilo litaongeza ushirikiano na Zanzibar ili kuona linatoa mchango mkubwa zaidi katika kukuza maendeleo ya sekta mbali mbali.

Profesa Shaukat alieleza hayo alipofanya mazungumzo na uongozi wa Wizara ya Afya Zanzibar ulioongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Asha Ali Abdalla ofisini kwake Mnazimmoja.

Alisema lengo kuu la kufika Zanzibar kwa ziara ya kutwa moja ni kukutana na watendaji wa sekta mbali mbali ili kuwaeleza juu ya nafasi kubwa iliyopo ya kuongeza ushirikiano kwa ajili ya maendeleo ya Zanzibar.

Alisema ushirikiano baina ya Shirika la IAEA na Tanzania ulianza tokea mwaka 1976 na linatoa ufadhili katika miradi mbalimbali inayohusisha sekta za Afya, Kilimo, Maji, Mifugo, Rasilimaliwatu, Nishati na Viwanda.

Kwa upande wa Zanzibar Profesa Shaukat alisema Shirika hilo limesaidia katika kupambana na changamoto ya kuteketeza magonjwa yote yanayoambukizwa na Mbung’o na hivi sasa magonjwa hayo sio tatizo kubwa.

Alisema pamoja na kufadhili sekta mbali mbali, Shirika hilo limeweka kipaumbele katika kuwajengea uwezo watendaji kwa kuwapa mafunzo ili kupata uelewa mpana zaidi katika kutekeleza majukumu yao.

Aliweka wazi kuwa Shirika la IAEA limeandaa mpango wa kuimarisha vitengo vinavyoshughulikia maradhi ya Saratani katika Hospitali zinazoshughulikia maradhi hayo baada ya kuonekana yanaongeza kwa kasi katika nchi nyingi zinazoendelea.

Alisema kwa mujibu wa idadi ya Watanzania kunahitajika kuwa na mashine 55 zinazotoa huduma ya mionzi kwa wagonjwa wa Saratani hata hivyo utafiti waliofanya wamegundua zipo mashine tano tu katika Hospitali tatu zinazotoa matibabu hayo ikiwemo Ocean Road na Bugando.

Alisema kuwa mradi wa nguvu za Atomiki Duniani katika Kanda ya Afrika unahusisha nchi 45 ambapo unajikita katika uhusiano wa ushirikiano katika nyanja tofauti.

Mkurugenzi Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Dk. Jamala Adam Taib aliueleza ujumbe huo kuwa Serikali itajenga Hospitali kubwa katika eneo la Binguni na Kitengo maalum cha maradhi ya Saratani kimepewa kipaumbele.

Alilishauri Shirika la IAEA kutoa msukumo zaidi suala la rasilimaliwatu na mafunzo kwa watendaji wa Kitengo cha Saratani ili baada ya kukamilika Hospitali ya Binguni kuwe na nguvukazi ya kutosha.

Akizungumza katika kikao hicho Daktari wa huduma za Saratani Hospitali kuu ya Mnazimmoja Dk. Abdulrahaman Said alisema Kitengo kinachoshughulikia maradhi hayo hivi sasa kina madaktari wawili na wengine watatu wapo masomoni na miaka michache ijayo kitaimarika kufikia madaktari watano.

Alisema hivi sasa Kitengo Saratani kinatoa huduma ya dawa na upasuaji tu kwa vile hawana mashine ya mionzi kwa wagonjwa wa maradhi hayo na hulazimika kwapeleka Hospitali ya Ocean Road Dar es salaam.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Bi. Asha Ali Abdalla alimshukuru Profesa Shaukat Abdulrazak kufika Zanzibar akiambatana na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania Profesa Lazaro Busagala na kueleza matarajio yake kuwa ziara hiyo italeta manufaa makubwa kwa Zanzibar.
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live




Latest Images