Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live

SERIKALI IMEIMARISHA USIMAMIZI NA UDHIBITI WA MATUMIZI SALAMA YA TEKNOLOJIA YA NYUKLIA NCHINI.

$
0
0
Mkurugenzi wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania, Profesa Lazaro Busagala akitoa neon la ukaribisho kwa wajumbe wa mkutano wa kimataifa wa waratibu wa miradi ya sayansi na Teknolojia ya Nyuklia kutoka nchi wanachama 49 wa Shirika la Nguvu za Atomiki la kimataifaIAEA)
Naibu waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Mh William Ole Nasha (Kulia) akifurahia jambo na Mkurugenzi wa Shirika la nguvu za Atomiki duniani Profesa Shaukat Abdulrazak kwenye mkutano wa kimataifa unahusisha nchi 49 za kanda ya AFRIKA.
Naibu waziri Elimu,Sayansi na Teknolojia Mh William Ole Nasha wakati akifungua mkutano wa kimataifa unaohusisha waratibu wa miradi ya sayansi na teknolojia ya Nyuklia kutoka nchi za kanda ya AFRIKA

Picha ikimuonyesha Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Mh William Ole Nasha akiwanna washiriki wa mkutano wa kimataifa wa waratibu wa miradi ya sayansi na teknolojia ya nyuklia kutoka katika nchi wanachama 49 wa Shirika la Nguvu za Atomiki duniani

………………………………………………………………….

Serikali ya Tanzania kupitia Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) imefanikiwa kuimarisha usimamizi na udhibiti wa matumizi ya Teknolojia ya Nyuklia nchini. Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Tekenolojia Mheshimiwa William Ole Nasha wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa kimataifa wa waratibu wa miradi ya Sayansi na Teknolojia ya Nyuklia kutoka nchi 46 wanachama wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki ( IAEA ) unaofanyika jijini Arusha.

Naibu waziri Ole Nasha amesema Shirika hilo linafadhili miradi mingi katika sekta mbali mbali hapa nchini ikiwemo sekta ya afya ambapo imewezesha kupatikana kwa vifaa mbali mbali vya uchunguzi wa tiba na maradhi ya saratani ambavyo vimefungwa katika hospitali ya Rufaa ya kanda ya ziwa Bugando jijini Mwanza na Hospitali ya Ocean Road jijini Dar es salaam.

Pamoja na vifaa vya uchunguzi katika hospitali hizo mbili, pia taasisi nyingine mbalimbali zimepata vifaa vya maabara ambapo kwa ujumla wake vifaa vyote vina thamani ya kiasi cha shilingi za Tanzania bilioni 6.2 na pia kutoa mafunzo kwa wataalamu katika eneo la matumizi ya mionzi na Teknolojia ya Nyuklia mpango ambao uligharimu Shilingi za Tanzania Bilioni 3.3.

Mh Ole Nasha amelishukuru na kulipongeza shirika hilo kwa kuendelea kuimarisha ushirikiano baina ya mataifa wanachama hususan kwa utaratibu wake wa kuwa na mikutano inayowezesha kubadilishana uzoefu baina ya wanachama. Amewataka washiriki wa mkutano huo kuhakikisha wanafanya majadiliano yenye tija kwa lengo la kusaidia nchi zao kwenye udhibiti na matumizi salama ya teknolojia ya nyukulia. “ majadiliano yenu yalenge katika kuhakikisha mionzi na teknoljia ya Nyuklia katika Afrika inatumika vizuri kwa maendeleo”.Alisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Nguvu za Atomiki Duniani (IAEA ) Profesa Shaukat Abdulrazak amesema wataendeela kushirikiana na serikali ya Tanzania katika kuhakikisha matumizi salama ya teknolojia ya Nyukilia kwenye sekta mbali mbali ikiwemo sekta ya Afya , Kilimo,Mifugo,Maji ,Viwanda na Ujenzi.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Nguzu za Atomiki Tanzania , Profesa Lazaro Busagara amesema taasisis yake imeendelea udhibiti na kuwachukulia hatua za kuwafungia taasisi zinazokiuka taratibu za matumizi salama ya Mionzi na Teknolojia ya Nyuklia hapa nchini ikiwemo kutokuwa na leseni, kutokuwa na wafanyakazi wenye utaalamu wa matumizi ya mionzi na teknolojia ya Nyuklia na Mionzi.

Akitoa mfano wa Hospitali amesema mwaka 2018 walifungia hospitali 112 zilizoshindwa kufuata masharti hayo, katika hizi tayari hospitali 40 zimekidhi na kufunguliwa huku hospitali 72 zikiwa bado zimefungiwa kutumia vifaa vinavyotumia mionzi .
Mkutano huo wa Siku tano utamalizika tarehe 15 , Machi 2019.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano
Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC)
11/ 3/2019
Arusha, Tanzania

Wafanyakazi wanawake Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) watakiwa kushirikiana na kutengenezeana Fursa Mbalimbali za Maendeleo

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Idara kuu ya Afya Dkt. Zainab Chaula akizungumza na wanawake wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) (hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani iliyofanyika machi 8 mwaka huu katika ukumbi wa taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Tiba Shirikishi wa JKCI Dkt. Delila Kimambo
Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Agnes Kuhenga akielezea namna ambavyo wanawake wa taasisi hiyo walivyoanzisha kampeni ya kuwasaidia wanawake na watoto katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani wakati wa hafla fupi ya kuhitimisha siku ya wanawake duniani iliyofanyika machi 8 mwaka huu katika ukumbi wa taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam
Baadhi ya viongozi wanawake kutoka katika taasisi za afya wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokua yakiendelea wakati wa hafla fupi ya kuhitimisha siku ya wanawake duniani iliyofanywa na wanawake wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) machi 8 mwaka huu katika ukumbi wa taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Idara kuu ya Afya Dkt. Zainab Chaula akimkabidhi baba wa mtoto mwenye magonjwa ya moyo Richard Zaya kiasi cha shilingi 593,000 kilichotolewa na umoja wa wanawake wa JKCI kusaidia matibabu ya mtoto huyo wakati wa hafla fupi ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani iliyofanywa na wanawake wa JKCI machi 8 mwaka huu katika ukumbi wa Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam
Baadhi wa wanawake wa Taasisi ya moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Idara kuu ya Afya Dkt. Zainab Chaula (hayupo pichani) wakati wa hafla fupi ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani iliyofanywa na wanawake hao machi 8 mwaka huu katika ukumbi wa taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Tiba Shirikishi na Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Delila Kimambo akimshukuru mgeni ramsi kushirikiana na wanawake wa JKCI kuadhimisha siku ya wanawake duniani wakati wa hafla fupi ya kuadhimisha siku hiyo iliyofanyika machi 8 mwaka huu katika ukumbi wa taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Idara kuu ya Afya Dkt. Zainab Chaula akicheza mziki na wafanyakazi wanawake wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa hafla fupi ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani iliyofanywa na wanawake wa JKCI machi 8 mwaka huu katika ukumbi wa taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam

Baadhi ya wanawake wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) katika picha ya pamoja wakati wa hafla fupi ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani iliyofanywa na wanawake hao machi 8 mwaka huu katika ukumbi wa taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam

…………………………..

Na Anna Nkinda

Wafanyakazi wanawake wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wametakiwa kushirikiana na kutengenezeana fursa mbalimbali za maendeleo ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Rai hiyo imetolewa hivi karibuni na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Idara Kuu ya Afya Dkt. Zainab Chaula wakati akiongea na wafanyakazi wanawake wa Taasisi hiyo katika sherehe ya kuadhimisha siku ya mwanamke Duniani.

Dkt. Chaula alisema ni muhimu kwa kila mwanamke akahakikisha anatengeneza fursa ya mafanikio kwa mwenzake jambo la muhimu ni kupendana, kushikana mkono na kuhakikisha hakuna mtu atakayefukuzwa kazi na atakayetamani kustaafu kabla ya wakati.

“Hakikisheni mazingira ya kazi yanakuwa mazuri na salama kwenu ninyi wote, kushirikiana kwenu kutawawezesha kufika mbali zaidi katika utendaji wenu wa kazi kwani katika mafanikio yoyote yale mchango wa mwanamke ni mkubwa zaidi ukilinganisha na wa mwanaume”, alisema Dkt. Chaula.

Aliendelea kusema kuwa katika sehemu ya kazi kila mtu anamchango katika mafanikio ya mwenzake, ukiona umefanikiwa tambua nyuma yako kuna watu wamekufanya ukafika hapo ulipo hivyo basi ni muhimu kwa wafanyakazi hao kuwa karibu zaidi.

Dkt. Chaula alimalizia kwa kuwataka wanawake hao kumtanguliza Mungu katika kazi zao za kila siku kwani kwa kufanya hivyo watakuwa na familia njema zenye hofu ya Mungu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Tiba Shirikishi Dkt. Delila Kimambo alisema katika kuadhimisha siku ya wanawake Duniani wafanyakazi wanawake wa Taasisi hiyo walifanya upimaji wa viashiria vya magonjwa ya moyo pamoja na kutoa elimu kwa wanawake wa soko kuu la Kimataifa la Samaki la Feri pamoja na maeneo jirani.

Dkt. Delila ambaye ni daktari bingwa wa magonjwa ya moyo alisema waliamua kwenda kupima magonjwa ya moyo na kutoa elimu kwa wanawake wa Soko hilo kwa kuwa hawana muda wa kwenda kupima afya zao.

“Tuliwafundisha viashiria vya hatari vya magonjwa ya moyo kwa wanawake na kuwapima afya zao. Tafiti zinaonyesha kuwa ukitoa elimu ya magonjwa ya moyo kwa wanawake kwa asilimia 80 utapunguza uwezekano wa kupata magonjwa ya moyo katika jamii”, alisema Dkt. Delila.

Katika kuadhimisha siku hiyo wafanyakazi hao walichanga kiasi cha shilingi 593,000/= fedha ambazo walimkabidhi baba mzazi wa mtoto Yasinta Zaya (15) ambaye amelazwa katika Taasisi hiyo kwa ajili ya matibabu ya moyo.

Akizungumza kabla ya kuzikabidhi fedha hizo Daktari bingwa wa usingizi na wagonjwa walioko katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) Anjela Muhozya alisema waliamua kumsaidia mtoto huyo ambaye alianza kuumwa ugonjwa wa moyo akiwa na umri wa miaka sita.

“Mtoto huyu anasubiri kwenda kupatiwa matibabu nchini Israel, hivi sasa afya yake imebadilika amelazwa ICU anatakiwa kufanyiwa vipimo mbalimbali ikiwemo MRI (Magnetic Resonance Imaging – MRI. Tumeona tumsaidie kwani wazazi wake hawana uwezo”, alisema Dkt. Anjela.

Akiongea mara baada ya kupokea fedha hizo Baba mzazi wa mtoto huyo Richard Zaya ambaye ni mkazi wa Kalambo mkoani Rukwa aliwashukuru wafanyakazi hao kwa moyo wa upendo waliouonyesha kwa mtoto wake na kuomba waendee kufanya hivyo kwa watu wengine wenye uhitaji.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Dkt. Chaula alitoa kiasi cha shilingi milioni moja na elfu hamsini kati ya hizo shilingi milioni moja itatumika kwa ajili ya vipimo vya mtoto huyo.

GAVANA SHILATU ASHIRIKI UJENZI ZAHANATI ‘NI ULE ALIOAGIZA UENDELEZWE’

$
0
0
Na Mwandishi wetu Mihambwe 

Afisa Tarafa Mihambwe Gavana Emmanuel Shilatu ameshiriki ujenzi wa Zahanati ya Ngongo iliyopo Kijiji Cha Ngongo kilichopo kata ya Michenjele.
Gavana Shilatu alienda kufuatilia utekelezaji wa maagizo yake ya ujenzi wa mradi huo wa Zahanati alioagiza ndani ya siku mbili uanze kutokana na kutelekezwa tangu Mwaka jana. 

Gavana Shilatu alifurahishwa kukuta nyasi zimefyekwa na Mafundi wapo kazini Kama alivyoagiza na kuwasisitiza watangulize mbele uzalendo kwa kuhakikisha mradi unajengwa kwa kuzingatia ubora na viwango vinavyolingana na thamani ya pesa. 

Katika ushiriki wa ujenzi huo Gavana Shilatu aliambatana na Serikali ya Kijiji pamoja na kamati ya ujenzi.

ZOEZI LA UPIMAJI WA MARADHI YA MOYO LAANZA MKOANI ARUSHA

$
0
0
Daktari Bingwa wa magonjwa ya moyo Samwel Rweyemam kutoka JKCI akimpima Mwenyekiti wa Bodi AICC Dkt. Ladis Komba leo Jijini Arusha katika uzinduzi wa upimaji wa magonjwa yasiyoambukiza
Daktari Bingwa wa magonjwa ya moyo Samwel Rweyemam kutoka JKCI akimpima Kaimu mkurugenzi wa AICC Mkunde Senyagwa Mushi leo Jijini Arusha katika uzinduzi wa upimaji wa magonjwa yasiyoambukiza
 Baadhi ya wananchi waliojitokeza kuja kupima afya zao leo katika uzinduzi wa upimaji wa magonjwa yasiyoambukiza Jijini Arusha. Picha na Vero Ignatus


Na. Vero Ignatus, Arusha

Imeelezwa kuwa 75%ya vifo vinavyotokea katika mataifa yanayoendelea ukanda wa Afrika ikiwemo  Tanzania vinasababishwa na magonjwa yasiyoambukizwa kwa utafiti uliofanywa 2012 na shirika WHO

Hayo yamesemwa na Dkt Bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka  Taasisi ya inayojihusisha na magonjwa ya moyo ya JKCIA  Dkt Samwel Rweyemamu katika Uzinduzi wa zoezi la upimaji wa maradhi ya moyo mkoani Arusha. 

Amesema kuwa kutokana na takwimu zilizofanywa 2016 wilayani simanjiro mkoa wa Manyara zinaonyesha kuwa 30%ya wanaume wote waligundulika kuwa na shinikizo la damu, hiyo ikiwa ni data zinazofanana za watu wanaoishi mjini. 

'' Data zinaonyesha tukiweza kupambana shinikizo la damu, uzito uliokithiri, kuangalia sukari kwenye miili yetu na kupima mafuta kwenye mwili tutapunguza vifo kwa 80% '' alisema Dkt Rweyemamu

Kwa upande wa mwenyekiti wa Bodi Balozi Dkt. Ladis Komba amesema kuwa azma la AICC katika eneo la Afya lina shabiana na azma ya serikali katika kusogeza huduma bora kwa wananchi wengi zaidi 

Amesema AICC itaendelea kuwa mstari wa mbele kwenye kutoa huduma za Afya kwa wananchi ikiwa ni pamoja na huduma ya upimaji ili kufanikisha malengo ya hospitahi hiyo na kwa Taifa kwa ujumla. 

 Mkurugenzi wa AICC Elishilia Kaaya amesema kuwa kwa mujibu wa wataalam wa Afya magonjwa haya yanatokana na kubadilika kwa mtindo wa maisha ambapo watu wengi hawapati muda wa kufanya mazoezi kutokana na kuelemewa na ratiba za kazi za ofisini na kutokuwa na elimu ya kutosha juu ya magonjwa haya. 

''Magonjwa haya kwa bahati mbaya hayaonyeshi dalili za wazi na hivyo ni vigumu kwa mtu anayeugua maradhi haya kujitambua mapema hivyo kuchelewa kupata matibabu, na mara nyingi imepelekea watu wengi kupoteza maisha ghafla na wengine kupata ulemavu wa kudumu''alisema 

Zoezi hilo la upimaji wa Afya ya moyo linatarajia kuchukua wiki moja kuanzia tarehe 11-18 marchi, hivyo wananchi wameombwa kujitokeza kwa wingi kwaajili ya kupima afya ya moyo pamoja na shinikizo la damu.

BAADA YA KUREJEA CCM MGEJA AENDA MBUGA ZA WANYAMA KUONDOA 'STRESS'

$
0
0
Na Ripota Wetu, Globu ya jamii 

SIKU chache baada ya kurejea Chama Cha Mapinduzi(CCM) Hamisi Mgeja amesema ameamua kwenda kuondoa 'Stress' katika mbuga za wanyama za Ngorongoro na Serengeti.

 Mgeja aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga amerejea Chama hicho mwanzoni mwa wiki iliyopita akitokea Chadema ambapo alijiunga na chama hicho wakati wa mchakato wa kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka 2015.

 Akizungumza leo kwa njia ya simu Mgeja ameiambia Michuzi Blog kuwa kwa sasa wameamua kwenda kujipumzisha mbuga za wayama baada ya kurejea CCM na hiyo inatoa nafasi kwake na wenzake kutafakari maisha mapya ndani ya CCM baada ya kurejea tena.

"Baada ya kumaliza kazi ya kumsindikiza Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa  nyumbani Monduli na kupokelewa na maelfu ya Wananchi wa Mkoa wa Arusha na Wana-CCM katika tukio la kurejea kwake rasmi na kupewa kadi mpya.

"Tumeamua kuja mbuga za wanyama kupumzika kidogo, ni wakati sahihi kwetu kuondoa 'Stress' za Chadema wakati tunafakari namna ya kushirikiana na Mwenyekiti wetu wa Chama Rais Dk.John Magufuli katika kuleta maendeleo ya Taifa letu,"amesema Mgeja.

Amesisitiza kuwa baada ya kurejea CCM kwa sasa moyo wake umejaa amani tele na kueleza anajihisi mwenye furaha na ameutua mzigo uliokuwa kichwani hasa kutokana na aina ya maisha aliyokuwa anaishi Chadema.

 "Nimekaa Chadema , kuna mambo nimejifunza nikiwa huko.Ndio maana wakati narejea CCM niliamua kuwapa ushauri iwapo  wanataka kuwa Chama cha siasa lazima wabadilike tofauti na hapo watabaki kama walivyo,"amesema Mgeja.

Akizungumzia mwenendo wa siasa nchini Mgeja amesema anampongeza Rais Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo."Hakika Rais wetu mpendwa anafanya kazi kubwa sana ya kuleta maendeleo, ni jukumu letu kumuunga mkono kwa kila hatua."amesema Mgeja.
 Hamisi Mgeja (Katikati) akifafanua jambo wakati anazungumza na makada wenzake wa CCM ambao wameamua kwenda kujipumzisha mbuga ya  wanyama Ngorongoro baada ya kurejea katika Chama hicho akitokea Chadema
 Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Hamisi Mgeja ambaye aliamua kuhamia Chadema na sasa amerejea tena CCM akiwa katika moja ya jengo lililopo katika mbuga ya wanyama Ngorongoro ambako amekwenda kupumzika.
Hamisi Mgeja wa pili kushoto akiwa na Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa(mwenye nywele nyeupe) pamoja na baadhi ya Wana-CCM wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuwasili mkoani Arusha

UNESCO watembelea Mamlaka ya Hifadhi Ngorongoro

$
0
0
Na Ripota wetu ,Arusha

Timu ya Wataalamu kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), imetembelea Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro NCAA.

Wataalamu hao walitembelea eneo hilo la urithi wa dunia mchanganyiko kutokana na Tanzania kujiunga na kuwa mwanachama wa UNESCO tangu mwaka 1962.

Katika ziara yao timu hiyo ilifanikiwa kutembelea maeneo ya mradi wa ujenzi wa barabara unaotarajiwa kuanza kujengwa hivi karibuni na NCAA kwa kiwango cha tabaka gumu zege ili kurahisha shughuli za utalii, na masuala mengine ndani ya eneo hilo.

Ujio wa timu hiyo umetajwa kuwa ni utaratibu wa kawaida ambapo hutembelea maeneo ya urithi wa dunia kuangalia changamoto za uhifadhi na kutoa ushauri au mapendekezo.

Mkuu wa timu ya wataalamu wa Shirika la Umoja wa Mataifa inaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamduni (UNESCO), Edmound Moukala (katikati), akimsikiliza Kaimu Meneja Idara ya Urithi wa Utamaduni na Mratibu wa UNESCO eneo la NCCA Selestine Ummanuel.

Meneja wa Idara ya Utafiti na Ufuatliaji Mamlaka ya Hifadhi ya gorongoro(NCAA), Julius Kibebe akizungumza kwa niaba ya Kamishna wa Uhifadhi NCAA Dk. Fredy Manongi kwenye majumuisho ya ziara ya wataalamu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamduni (UNESCO), waliopo kushoto kwake.

Mkuu wa timu ya wataalamu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamduni (UNESCO), Edmound Moukala akisisitiza jambo kwenye kikao cha majumuisho baada ya kutembelea baadhi ya maeneo ndani ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorogoro.

Pix6. Mwakili wa Baraza la Wafugaji Tarafa ya Ngorongoro akichangia wakati wa majumuisho ya timu ya wataalamu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamduni (UNESCO), waliotembelea maeneo tofauti ndani ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro NCAA.

Mobile technology, an enabler of inclusive development and women empowerment.

$
0
0
The 21st century has been characterized by rapid technological advancement giving rise to breakthroughs that will affect our politics, economies, improve medicine and influence our culture. Technology has transformed social and economic activities, increased connectivity and created a global village. However, there has been an uneven distribution in mobile technology access and usage between men and women. 

 According to a GSMA report, 14% of women are less likely to own a phone, this equates to 200 million fewer women than men engaging in mobile technology. Sub-Saharan Africa is identified as the second leading region with the gender gap in mobile ownership and internet usage after South Asia. In Tanzania, various interventions in education, health and agriculture sectors such as CodeLikeAGirl, Wazazi Nipendeni and Women Farmer Network respectively, seek to address the gender imbalance in uptake of mobile technology. 

Social and economic factors contribute significantly to gender discrepancy in low and middle – income countries. Social norms and inequality between men and women in education have predominantly contributed to the gender gap in the tech space. The financial cost of possessing a phone coupled with not being tech savvy featured as a deterrent. Women also cited security and harassment in their respective communities as a hindrance to ownership of a mobile phone. 

In Tanzania, the government and various stakeholders in the public and private sector have incorporated mobile technology that will improve service delivery in key areas such as maternal health and education. 

The aspirations highlighted in the Second Five Year Development Plan (FYDPII), are expected to see a reduction in maternal mortality by 50%. Through the ‘Wazazi Nipendeni’ initiative, the Ministry of Health in partnership with public and private sector actors delivers a solution that dispenses pre and post-natal information. 

 Commenting on Vodacom Foundation’s commitment to improve maternal health, Rosalynn Mworia, Director Corporate Affairs and Vodacom Foundation said, “This program has reached nearly 40,000 women and significantly reduced maternal mortality rate in the lake zone as a result of mobile technology.” ‘At a minimum, women should be equipped with information that will allow them to deliver their babies safely. Mobile technology allows us to reach women in remote areas by sending informative text messages on their progress, providing them with peace of mind throughout their pregnancy.’

Removing impediments to learning include identifying and addressing factors such as that affect school attendance. UNESCO estimates that young girls miss 20% of school per year and according to a 2015 report issued by Tanzania Water and Sanitation Network (TAWASANET), about 75% of schoolgirls acknowledge that menstruation impacts their performance in school. By utilizing mobile technology to advice on menstrual hygiene management and sexual reproductive health education the ‘Hakuna Wasichoweza Project’ empowers girls with education on hygiene and selfcare. Additionally, the collaboration between T-MARC and Vodacom Foundation has equipped more than 10,000 schoolgirls in Mtwara and Lindi with sanitary pads that has resulted in an increase in school attendance. 

As the leading economic contributor in Tanzania, agriculture employs over 70% of the population and according to the Ministry of Health, women make up 52% of the labor force in the sector. Vodacom’s Women Farmer Networks has empowered women in the agriculture sector through skills development programs and providing access to capital and markets using mobile technology. 

The network reaches women’s cooperatives in nearly 300 projects in the Northern zone and have recorded remarkable success such as financial independence, awareness of best practices and unlocked opportunities to other economic activities such as livestock keeping and significantly triggered financial inclusion of women. 

Mobile technology has the muscle to substantially bring about the socio-economic transformation of communities. However, it is important for women to be included from the inception phase of these technologies and provide solutions that cater to their needs

NIC Bank Tanzania yaadhimisha siku ya wanawake duniani kwa kutoa msaada katika taasisi ya saratani ocean road

$
0
0

Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya NIC Tanzania, Margaret Karume, akihojiwa na waandishi wa habari.

Afisa Ustawi wa ORCI , Malkiory Niniko akipokea msaada kutoka kwa Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya NIC Tanzania, Margaret Karume.
Afisa Ustawi wa Taasisi ya Saratani Ocean Road, Malkiory Niniko akitoa shukrani.

wafanyakazi wakiwa katika picha ya pamoja.



Benki ya NIC Tanzania yatoa msaada katika Taasisi ya Saratini ya Ocean Road(ORCI)

Dar es Salaam, 8th Machi,2019, Benki ya NIC Tanzania leo imeadhimisha siku ya wanawake duniani inayosherehekewa kote duniani tarehe 8 Machi kwa kutembelea na kutoa msaada katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road(ORCI).

Akiongea katika tukio hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NIC Tanzania, Margaret Karume alisema, “Siku ya wanawake duniani ni siku kubwa katika kalenda ya wafanyakazi wa benki hii, kwa ajili ya kusaidia na kuyainua maisha ya wanawake wasiojiweza katika jamii iliyotuzunguka. Saratani ni ugonjwa ambao umeathiri na unaendelea kuathiri watanzania wengi sana, Zaidi kama haijagundulika mapema”.

Aliongeza kwa kusema, kila mmoja wetu ananafasi ya kucheza katika jamii, ambapo dunia inahitaji usawa. Katika uamuzi wetu wa kutoa msaada kwa wagonjwa wa saratani, tujenga usawa kwa ajili yakuwa na dunia iliyobora.

“Kama Benki, tumejikita kuhakikisha tunatoa mchango chanya, kwa jamii tunazo endesha shughli zetu. Ndio sababu kusaidia Taasisi kama hizi ipo katika mkakati maalum wa kusaidia jamii,” alisema Karume.

Akiongea katika hafla hiyo Afisa Ustaei wa Taasisi hiyo Malkiory Niniko alisema, “Tunaipongeza Benki ya NIC Tanzania, kwa kutoa msaada huu, na tunawaomba wadau mbalimbali waige mfano huu adhimu, na Taasisi inakaribisha usaidizi kutoka idara mbalimbali kwa sababu haiwezi kufanikisha malengo yake yote kwa mkupuo”

VISA, MABENKI 15 WAZINDUA HUDUMA YA VISA KWENYE SIMU YA MKONONI JIJINI DAR

$
0
0

Mkurugenzi Mkuu wa VISA Afrika Mashariki Kevin Langley akizungumza katika uzinduzi wa huduma ya Visa kwenye simu za mkononi iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Wageni waalikwa waliohudhuria katika uzinduzi wa huduma ya Visa kwenye simu za mkononi iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Rais wa Kampuni ya VISA kwa Sab-Sahara Afrika Aida Diara akizungumza katika katika uzinduzi wa huduma ya Visa kwenye simu za mkononi iliyofanyika jijini Dar es Salaam ambapo amesema lengo la kuzinduwa huduma hiyo ni kuhamasisha uboreshaji huduma na kupunguza makato kwa wateja, wafanyabiashara na sekta ya huduma ya fedha kwa ujumla.



Wageni waalikwa wakifuatilia kwa makini.
Mkurugenzi Mwandamizi wa Mauzo ya Biashara Kennedy Luhombo akitoa ufafanuzi juu ya huduma ya VISA inavyofanya kazi katika simu za mkononi katika uzinduzi uliofanyika jijini Dar es Salaam.



*BoT yasema Tanzania imepiga hatua kuongeza malipo ya kieletroniki *Yaelezwa Watanzania milioni 20 wana usajili au akaunti za fedha kwenye simu Na Said Mwishehe, Globu ya jamii. VISA na benki 15 nchini Tanzania wamezindua huduma ya kwanza ya malipo ya simu bure ambapo sasa wateja wanaofanya miamala watakuwa na uwezo wa kutuma au kupokea fedha ndani na nje ya nchi bila makato yoyote.
 
 Akizungumza leo Machi 12, 2019 jijini Dar es Salaam, Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Dk. Bernad Kibese amesema uzinduzi huo wa VISA kwenye simu ya mkononi ni hatua nzuri na Tanzania imepiga hatua kubwa katika kuongeza malipo ya kieletroniki na kukuza ushirikishwaji wa fedha. "Uzinduzi wa Visa kwa njia ya simu ya mkononi unaonesha hatua muhimu katika kuongeza kasi ya uhamaji kutoka fedha taslimu kwenda mfumo wa uchumi wa kidigitali Tanzania ambao ni mzuri kwa jamii zetu,"amesema Dk. Kibese. 
 
Kwa upande wake Rais wa Kampuni ya VISA kwa Sab-Sahara Afrika Aida Diara amesema lengo la kuzinduliwa kwa huduma hiyo ni kuhamasisha uboreshaji huduma na kupunguza makato kwa wateja, wafanyabiashara na sekta ya huduma ya fedha kwa ujumla. Amesema ili kutumia huduma hiyo , Diara amesema mteja wa benki anatakiwa kupakua programu ya simu ya benki husika, kisha atatafuta Visa kwenye programu na lipia bidhaa na huduma ama kwa kupiga picha alama ya QR au kwa kutumia USSD (Unstructed Supplimentary Service Data)katika sehemu ya biashara ulipo.
 
Huduma hiyo ni ya Visa na inapatikana bure na salama. "Matumizi ya malipo ya kieletroniki yanaongeza usalama na urahisi barani Afrika huku ikipunguza gharama na kuongeza uwazi katika shughuli za kifedha.Sehemu kubwa ya uchumi wa Afrika na usio rasmi, malipo hufanyika kwa kubadilishana fedha taslimu kwa zaidi ya asilimia 90.
 
 "Inatia moyo kuona Watanzania tayari wanafuata na kukubali teknolojia ya simu ikiwa na usajili wa watu zaidi ya milioni 41 na zaidi ya asilimia 80 ya waliosajiliwa hutumia mtandao kwa kutumia simu za mkononi.Ni ukweli unaofahamika kuwa zaidi ya Watanzania milioni 20 wana usajili au akaunti za fedha kwenye simu.Hizi zote ni ishara za matumaini kwa VISA,"amesema. 
 
Diara amesisitiza lengo la uzinduzi wa Visa kwa njia ya simu nchini Tanzania, lina msingi imara na kwamba wafanyabiashara watafurahia na kuthamini utamaduni huo mpya kabisa wa malipo ya fedha taslimu wa kulipa au kulipwa. Ameongeza kuwa uhamaji wa kutoa fedha taslimu kwenda kidigitali unapanua wigo wa juu na chini wa thamani .
 
Kwa mteja huduma za fedha za simu zinaleta usalama,urahisi, mazingira mazuri ya malipo kuliko fedha taslimu na inaokoa muda na gharama za safari. Kuhusu malengo yao kwa upande wa Kusini mwa Jangwa la Sahara, Diara amesema wameendelea kukuza mipango yao, biashara na teknolojia katika ukanda huo kwa kufungua mtandao wao kuunga mkono mahitaji ya taasisi za fedha, wauzaji , waendelezaji na washirika wa FinTech ili kujenga mazingira jumuishi ya kimazingira. 
 
Wakati huo huo Mkurugenzi Mkuu wa VISA Afrika Mashariki Kevin Langley amesema kulingana na jarida la TanzaniaInvest , eneo la biashara ya simu nchini Tanzania inashuhudia ukuaji wa haraka unaofikia zaidi ya Dola za Marekani bilioni 1.6 zilizofanyika kila mwezi mwaka 2018. Amezitaja baadhi ya benki ambazo zimeshirikiana na VISA kutoa huduma hiyo ni CRDB, NMB, NBC, benki ya Azania, TIB , benki ya Posta, DCB, benki ya Mkombozi, Mufindi Community Bank Limited, Benki ya Watu wa Zanzibar , Benki ya Uchumi,Benki ya Mwalimu,Benki ya Maendeleo na Yetu Microfinance Bank.

wafanyakazi Vodacom Tanzania watembelea shule ya Sangu, Mbeya na shule ya Arusha Day kuadhimisha siku ya wananwake Duniani,watoa msaada wa vifaa mashuleni.

$
0
0


 Mkuu wa mauzo wa Vodacom Tanzania Kanda ya Kaskazini, Brigita Stephen (kulia) akimkabidhi zawadi Mkuu wa shule ya sekondari Arusha Day, Joyce Gyunah katika hafla iliyofanyika jijini Arusha jana. Katika kuadhimisha wiki ya wanawake duniani, Wafanyakazi wa Vodacom wametembelea shule hiyo ya wasichana na kuwapatia vifaa kwa ajili ya mahitaji yao ya shule ikiwa ni jitihada za kuhakikisha watoto wa kike wanafanya vizuri katika masomo na wanatimiza ndoto na malengo yao.

Mkuu wa mauzo wa Vodacom Tanzania Kanda ya Kaskazini, Brigita Stephen akizungumza na wanafunzi wa kike wa shule ya sekondari Arusha Day na kuwahimiza kusoma kwa bidii, katika hafla iliyofanyika jijini Arusha jana. Katika kuadhimisha wiki ya wanawake duniani, kampuni ya Vodacom imetembelea shule hiyo ya wasichana na kuwapatia vifaa kwa ajili ya mahitaji yao ya shule ikiwa ni jitihada za kuhakikisha watoto wa kike wanafanya vizuri katika masomo na wanatimiza ndoto na malengo yao.

Meneja Masoko wa kampuni ya Vodacom Tanzania kanda ya Nyanda za juu kusini, Magreth Lawrence (kushoto) akimkabidhi daftari, Jackline Chaula, mwanafunzi wa kidato cha tano katika shule ya sekondari ya Sangu jijini Mbeya. Katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani, wafanyakazi wa kampuni hiyo wametembelea, kuongea na kutoa zawadi na vifaa mbalimbali kwa wasichana ili kuwasaidia mahitaji yao ya shule ikiwa ni jitihada za kuhakikisha watoto wa kike wanafanya vizuri katika masomo na wanatimiza ndoto na malengo yao.
Meneja Masoko wa kampuni ya Vodacom Tanzania kanda ya Nyanda za juu kusini, Magreth Lawrence, akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Sangu juu ya umuhimu wa elimu kwa watoto wa kike. Katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani, wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wametembelea shule hiyo na kuwapatia vifaa mbalimbali kwa ajili ya mahitaji yao ya shule ikiwa ni jitihada za kuhakikisha watoto wa kike wanafanya vizuri katika masomo na wanatimiza ndoto na malengo yao.

KILAVE -AWATAKA UWT KIGAMBONI KUJITOEZA KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI KATIKA CHAGUZI ZIJAZO

$
0
0
--
 Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam, Dorothy Kilave akizungumza na Wanawake wa UWT  Kata ya Kigamboni Katika ziara yake ya kikazi kuinua hari ya chama na kukumbushana mambo ya Msingi ikiwa pamoja na fursa za mikopo zinazopatikana katika Halmashauri zetu kwa Asilimia nne Wanawake,Asilimia Vijana na Mbili kwa ajili ya watu wenye ulemavu.
 Katibu wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam(UWT),Grace Haule akiwakumbusha majukumu watendaji wa chama ngazi ya kata mpaka matawi na kuwatka kudumisha umoja hili CCM iweze kuibuka na ushindi Mnono katika uchaguzi wa 2019 na 2020
 Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji Umoja wa Wanawake(UWT), Chokole Mohamed, akiwasalimia wakazi wa kata ya Kigamboni Katika Mkutano wa ziara ya Mwenyekiti wa UWT Mkoa.
 Diwani wa Viti Maalum Kata ya Kigamboni, Amina Yakub akisalimia wakazi wa Kigamboni wakati wa ziara ya Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Dar es Salaam.
 Diwani wa Kata ya Kigamboni, Dotto Msawa akiwasalimia Wajumbe wa Mkutano wa UWT Kata ya Kigamboni wakati wa Ziara ya Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Kigamboni, Mwajabu Mbwambo akitoa neno la ukaribisho kwa wageni Waalikwa na Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Dar es Salaam.
 Sehemu ya Wajumbe wa Mkutano wa UWT Kata ya Kigamboni wakifatilia hotuba kutoka kwa Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Dar es Salaam,Dorothy Kilave
Sehemu ya Wajumbe wa Mkutano wa UWT Kata ya Kigamboni wakifatilia hotuba kutoka kwa Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Dar es Salaam,Dorothy Kilave

Prof. Kabudi na Dkt. Mahiga wakabidhiana ofisi

$
0
0
Waziri wa Katiba na Sheria ambaye awali alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akikabidhi Taarifa ya Makabidhiano ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi ambaye awali alikuwa Waziri wa Katiba na Sheria. Makabidhiano hayo yalifanyika jijini Dodoma tarehe 12 Machi 2019. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi (kushoto) akimkabidhi Taarifa ya Makabidhiano ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akiweka saini Kitabu cha mahudhurio mara baada ya kukabidhiwa ofisi jijini Dodoma. 
Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akiongea na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi mara baada ya makabidhiano ya ofisi. 
Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakishuhudia makabidhiano ya ofisi kati ya Waziri wa Katiba na Sheria na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. 
Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akiongea na Wakuu wa Idara na Vitengo (hawapo pichani) baada ya kukabidhiwa ofisi na Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga. 
Wakuu wa Idara na Vitengo wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (hayupo pichani). 
Wakuu wa Idara na Vitengo wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akiongea na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. 
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Bi Savera Kazaura akitoa maelezo kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Waziri wa Katiba na Sheria kabla zoezi la makabidhiano kuanza. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akisalimiana na baadhi ya watumishi mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Anayemkaribisha ni mmoja wa watumishi hao, Bw. Shaban Mtambo. 
Bi. Chiku Kiguhe akisalimiana na Mhe. Prof. Kabudi. 
Bw. Habibu Ibrahim akisalimiana na Mhe. Waziri. 
Bw. Maulidi Mkenda akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akiongea na baadhi ya watumishi waliojitokeza kumpokea mara alipowasili kwa mara ya kwanza katika ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje jijini Dodoma. 
Bw. Caesar Waitara akisalimiana na Mhe. Prof. Kabudi

DC- KINONDONI AKAMATA BIDHAA ZINAZO INGIZWA KIMAGENDO KUPITIA BANDARI BUBU MBWENI.

$
0
0
*Ni baada ya Polisi, DC Kinondoni kufanya msako usiku wa manane
*Ng'ombe waliopewa mafunzo maalumu watumika kubeba magendo 
*Waliohusika wakimbia nyumba...sasa msako wa nyumba kwa nyumba kufanyika

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii 

SUKARI bandia kilo 350 na mafuta ya kupikia madumu 25 ambayo hayana ubora yamekamatwa katika eneo la Mbweni wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Sukari na mafuta hayo ya kupikia yamekamatwa usiku wa kuamkia leo, Machi 12.2019 eneo la Mbweni ambako kumebainika kuwepo kwa bandari bubu ambayo watu wasiowaaminifu wanatumia bandari hiyo kuingiza bidhaa za magendo na kibaya zaidi zisizokuwa na ubora.

Msako mkali uliofanyika usiku wa kuamkia leo, kupitia Jeshi la Polisi Kituo cha Polisi Mbweni kilichopo katika Wilaya ya Konondoni pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo wamefanikiwa kukamata bidhaa hizo za magendo.

Kwa mujibu wa Polisi Mbweni ni kwamba wanaopitisha bidhaa hizo za magendo wamekuwa wakitumia ufukwe wa Bahari ya Hindi katika eneo hilo na kisha baada ya kuingiza bidhaa hizo nchi kavu wanatumia ng'ombe ambao wamepata mafunzo maalumu kwa ajili ya kubeba mizigo hiyo na kukimbia nayo kwa ajili ya kufichwa.

Akizungumza akiwa katika Kituo cha Polisi Mbweni ambako ndiko bidhaa hizo za magendo zimehifadhiwa, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo amesema, kutokana na msako mkali ambao umefanywa na Polisi wamekamata bidhaa hizo ambapo kimsingi ni hujuma kubwa kwa Serikali kwani wanaopitisha wanakwepa kodi na kibaya zaidi wanahatarisha maisha ya wananchi.

"Baada ya kufanyika kwa msako huu usiku kucha tumekamata mifuko 70 ya sukari na kila mfuko una kilo 50, hivyo kwa ujumla tumekamata kilo za sukari 350 pamoja na mafuta madumu 25.Haifahamiki hii sukari na haya mafuta yanatoka nchi gani lakini wanaofaya biashara hii haramu wakifika nchi kavu wanachukua hiyo sukari na kisha kuijaza kwenye mifuko ya sukari ambayo inazalishwa nchini na kisha kwenda kuuza.

Hata hivyo amesema kuwa jahazi au boti ambayo imetumika kuleta sukari hiyo baada ya kuona Polisi wamefika eneo la tukio wahusika waliirudisha kwenye maji na hivyo haikufanikiwa kupatikana kwani iliondolewa.

Chongolo amesema Serikali haiko tayari kuona zinaingizwa bidhaa ambazo ziko chini ya ubora na wanaofanya hivyo watambue mwisho wao umefika na wote ambao wamehusika watachukuliwa hatua kwani majina yao yamefahamika.

Amefafanua kuwa kwa sasa sukari kutoka nje hairuhusiwi kuingizwa nchini kwani viwanda vilivyopo vinazalisha sukari ya kutosha huku akifafanua sukari ambayo wameikamata haijathibitishwa ubora wake wala inakotoka.

"Hatuwezi kukubali kuona wananchi wanadhuruka.Huu msako ambao tumeuanzisha ni endelevu na utaendelea kila siku, wale ambao wamezoea kufanya biashara kiujanja ujanja ikiwa pamoja na kukwepa kodi watambue mwisho wao umefika.

Amesema kitendo cha kuingiza sukari ambayo haina ubora inaweza kusababisha madhara makubwa ikiwemo kupata saratani ya tumbo au vidonda vya tumbo."Hii sukari ambayo tumeikamata haijulikani ni ya viwandani ama wapi? Wanaohusika na michezo hii wajue hatutawaacha."

Kwa upande wake Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Polisi Kawe Dk. Ezekiel Kyogo amesema bidhaa hizo zinapitishwa kupitia bandari bubu na matokeo yake kuikosesha Serikali mapato yatokanayo na kodi.Amefafanua baada ya kufanya uchunguzi wao wamebaini nyumba zinazotumika kuficha bidhaa za magendo pamoja na majina ya wahusika ambao wengine wamekimbia nyumba zao baada ya kufanyika msako.

Amesema kuwa watu wanne wanashikiliwa na Polisi kutokana na kutuhumiwa kuhusika kwenye kuingiza bidhaa hizo za magendo na sheria itachukua mkondo wake."Tutafanya msako nyumba hadi nyumba kuhakikisha wote ambao wamehusika wanachukuliwa hatua".

Kuhusu jahazi ambalo limetumika kuleta bidhaa hizo za magendo, Dk.Kyogo amesema wameshindwa kulipata kwani walikimbia eneo la tukio.
Mkuu wa Wilaya ya KInondoni Mh Daniel Chongolo akioneshwa bidhaa hizo za Magendo zilizokamatwa leo katika Bandari Bubu,Mbweni jijini Dar
Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya  Kipolisi Kawe ,Dkt Ezekiel Kyogo  akimuonesha Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,Daniel Chongolo (kulia) mashine iliyokuwa ikitumika  kwenye boti za kubebea mizingo ya magendo kutoka baharini katika Bandari Bubu ya Mbweni jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh.Daniel Chongolo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kukamatwa kukamatwa kwa bidhaa mbalimbali za magendo katika Bandari Bubu ya Mbweni,leo jijini Dar.
 Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya  Kipolisi Kawe ,Dkt Ezekiel Kyogo akitoa ufafanuzi namna bidhaa hizo za magendo zilivyokamatwa katika bandari bubu,Mbweni jijini Dar. 
Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya  Kipolisi Kawe ,Dkt Ezekiel Kyogo  akimuonesha Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,Daniel Chongolo (kulia) Ng'ombe wanaobeba mizingo ya magendo kutoka baharini katika  Bandari Bubu ya Mbweni jijini Dar es Salaam.
Bidhaa mbalimbali za magendo zilizokamatwa katika bandari Bubu ya Mbweni jijini Dar es Salaam .
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Daniel Chongolo akipewa maelezo na 
Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Kipolisi Kawe ,Dkt Ezekiel Kyogo mara baada ya kukamatwa bidhaa za magendo katika ufukwe wa Mbweni (bandari Bubu),leo jijini Dar
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh DaniellChongolo akizungumza jambo na vijana wanaodaiwa kutumika kubeba mizigo hiyo ya magendo inapofikishwa nchi kavi,Mbweni jijini Dar

MAGAZETI YA LEO JUMATANO MACHI 13,2019

MKUTANO WA AFRICA NOW WAFUNGULIWA LEO JIJINI KAMPALA

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye mkutano wa Africa Now Summit 2019 ulioanza leo kwenye hoteli ya Commonwealth Resort, Munyonyo jijini Kampala, Uganda. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).

Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni akihutubia wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Africa Now Summit 2019 ambapo viongozi wa Afrika wanakutana kujadili masuala mbalimbali ya utengamano katika kuleta maendeleo endelevu barani Afrika ambapo Tanzania imewakilishwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kushoto) akiwa na mwenyeji wa Mkutano wa Africa Now Summit 2019 Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni pamoja na Rais wa Somalia Mhe. Mohamed Abdullahi Mohamed (kulia) wakati wakielekea kwenye ukumbi wa mkutano katika hoteli ya Commonwealth Resort, Munyonyo jijini Kampala Uganda.

WAZIRI KAIRUKI AMKABIDHI RASMI WIZARA, BITEKO

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji Angellah Kairuki, amemkabidhi rasmi majukumu ya Uwaziri wa Wizara ya Madini, Doto Biteko katika kikao kilichohudhuriwa na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo. 

Waziri Kairuki amemshukuru Waziri Biteko kwa ushirikiano aliompatia kwa kipindi chote alichokuwa Waziri wa wizara hiyo na kueleza kwamba, kabla ya makabidhiano hayo, wamepata wasaa wa kupitia kwa pamoja majukumu na vipaumbele vya wizara ikiwemo maeneo muhimu yanayotakiwa kupewa msukumo. 

Naye, Waziri Biteko akizungumza mara baada ya kukabidhiwa majukumu hayo, amemshukuru Waziri Kairuki na kumwelezea kuwa ni Waziri aliyekuwa Mwalimu mzuri kwake kwa kipindi chote alichokuwa Naibu Waziri. 

Ameongeza, Waziri Kairuki hakuwahi kumnyima nafasi ya kujifunza ikiwemo kumtuma kuteleleza majukumu mbalimbali nafasi ambayo imemkomaza. 

” Waziri hakuwahi kuninyima nafasi ya kujifunza ikiwemo kutekeleza majukumu yangu na nitaendelea kuhitaji ushauri wake,”amesema Biteko. 

Makabidhiano hayo yamefanyika Machi 12, Ofisini kwa Waziri Biteko Jijini Dodoma. 

Waziri Biteko aliteuliwa Januari 8, 2019 kushika wadhifa huo baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli kufanya mabadiliko madogo katika Baraza la Mawaziri na kufanya uteuzi wa viongozi mbalimbali. 

Waziri Biteko alichukua nafasi ya aliyekuwa Waziri wa Madini Angellah Kairuki ambaye aliteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji.

WASANII WAUNGANA KUMSAIDIA HAMIS ALIYEVIMBA MIGUU,WAISHUKURU SERIKALI

$
0
0
WASANII wa fani mbalimbali nchini wameamua kumsaidia kijana Hamisi Salum anayesumbuliwa na tatizo la kuvimba miguu kwa kumpeleka Hospitali ya Taifa Muhimbili ili apate matibabu kwani wanaamini atapona na kutimiza ndoto zake. 

Akizungumza jana Machi 12, 2019 kwa niaba ya wasanii wenzake, Msanii maarufu nchini Steve Nyerere amesema wanamatumaini makubwa Hamis atapona, kikubwa ni Watanzania kumuombea kwa Mungu. 

Amefafanua Hamis alishapelekwa nchini India kwa matibabu na kisha akarejea nyumbani Tanzania na baadae tena alipelekwa Muhimbili. 

Ameongeza wasanii katika kuhakikisha Hamis anapona na kutimiza ndoto zake wameamua kumfuata tena nyumbani kwao na kisha kumpeleka Hospitali ya Taifa Muhimbili akatibiwe. 

Steve Nyerere amesema baada ya wao kupaza sauti zao Rais Dk.John Magufuli amesikia na kwa kupitia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda wameamua kumsaidia. 

"Tunaishukuru Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dk.John Magufuli kwa kujali wanyonge, wasanii tumepaza sauti zetu kuhakikisha Hamis anasaidiwa na Rais wetu amesikia na leo amepokelewa Muhimbili kwa ajili ya kupata matibabu.Pia tunamshukuru Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa jitihada zake za kumsaidia Hamis,"amesema Steve Nyerere. 

Amesisitiza kuna kila sababu ya kumsaidia Hamis kwani bado anayo matumaini na vijana wenzake wakiwamo wao wasanii wamejikusanya kumsaidia. 

Kuhusu gharama ya matibabu,Steve Nyerere amesema bado hajafahamu gharama halisi itakayotumika katika matibabu ya kijana huyo lakini wanachoamini nafasi ya kupona ipo, hivyo kikubwa ni watanzania kumsaidia. 

Ametoa onyo kuwa ugonjwa wa Hamis usitumike vibaya kwani wanaweza kujitokeza watu na wakatoa namba za simu ili wawe wanatumiwa fedha kumbe ni matapeli."Hamis anahitaji kusaidiwa na si kutumika kibiashara." 
Wasanii wakimsaidia kijana Hamis Salumu mwenye matatizo ya kuvimba miguu kumuingiza katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili kupatiwa matibabu baada ya Rais Dkt John Pombe Magufuli kujitolea kumpatia matibabu kwa kupitia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda na Wasanii wakiongozwa na Steve Nyerere. 
Wasanii wakiwa nje ya Chumba cha wagonjwa wa dharula katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili kushuhudia kijana Hamis Salumu akifikishwa kwa ajili ya matibabu. 
Wasanii wakimsanidia Kijana Hamis Salum kumtoa nyumbani kwao Temeke jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuelekea hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar.

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA NAIBU RAIS WA KENYA MH RUTO.

$
0
0





Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Rais wa Kenya Mhe. William Ruto katika hoteli ya Munyonyo Commonwealth Resort, Kampala nchini Uganda ambapo kuna mkutano wa Africa Now Summit 2019. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Naibu Rais wa Kenya Mhe. William Ruto kabla ya kufanya mazungumzo yao katika hoteli ya Munyonyo Commonwealth Resort, Kampala nchini Uganda ambapo kuna mkutano wa Africa Now Summit 2019. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Prof. Kabudi akutana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mheshimiwa Prof. Palamagamba J. Kabudi (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Mheshimiwa Mikhail Bogdanov, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Shirikisho la Urusi katika Ofisi Ndogo ya Wizara Jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo hayo, Waheshimiwa Mawaziri wamezungumzia masuala mbalimbali yaliyolenga kuboresha na kuimarisha uhusiano na ushirikiano baina ya mataifa haya mawili, hususan, katika Nyanja ya kidiplomasia, nishati, biashara na uwekezaji. Naibu Waziri huyo yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili. 
Waheshimiwa Mawaziri wanaendelea na mazungumzo hayo, huku ujumbe aliofuatana nao Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi ukifuatilia mazungumzo hayo .
Kutoka kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Urusi, Mej. Jenerali mstaafu Simon Mumwi, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Bw. Jestas Nyamanga, Balozi wa Urusi nchini Tanzania, Mhe. Yuri Popov na Afisa wa Ubalozi wa Urusi nchini Tanzania wakifuatilia mazungumzo ya Waheshimiwa Mawaziri.

Article 0

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI, PWANI 

WANANCHI zaidi ya 200 mkoani Pwani,wanadai kutapeliwa fedha milioni 185 ,kwa ajili ya kupatiwa viwanja na kujengewa nyumba kwa gharama nafuu kupitia kampuni ya Vicoba group union Tanzania (VIGUTA). 

Aidha Chamwino huko Dodoma wanadai kuidai kampuni hiyo milioni 61 huku wakikosa kupatiwa nyumba walizolipia kujengewa kwa gharama nafuu.

Aliyekuwa meneja wa Viguta mkoani Pwani,Iddi Kanyalu alikiri kuwepo kwa tetesi hizo na kudai taarifa hizo tayari amezifikisha kwenye vyombo vya sheria ili kufanya uchunguzi na sheria kufuata mkondo wake. 

Alisema,ni kweli walikuwa wananchi wanalipia viwanja kwa bei nafuu na nyumba walikuwa wakilipia kwa asilimia 25 mfano ukitaka kujengewa nyumba ya milioni 25 unalipia milioni 7.5 ambapo wengi walishalipia asilimia 25 na wengine fedha zote kisha kuingizwa mkenge. 

Kanyalu alieleza, utapeli huo umegusa watu ambao wameuziwa viwanja hewa na nyumba ambazo hawajakabidhiwa hadi sasa. 

"Wamenisababishia doa, kwanza mimi ni diwani wa kata ya Kongowe, kutokana na aibu hii na mimi kutohusika, nimeshachukua hatua ya kulifikisha suala hili polisi ili kuchukua hatua zaidi "alifafanua Kanyalu. 

Alipoulizwa kuwa kwanini asigutuke toka alipopewa kazi hiyo hadi kufikia hatua ya kuleta kero na ubabaishaji kwa jamii, Kanyalu alijitetea kuwa kama utapeli ulikuwa wa kimataifa hadi kufikia hatua ya kujitangaza kwa wabunge na kuingia mkataba na baadhi ya taasisi za kifedha hivyo haikuwa rahisi kwake kutambua ubabaishaji huo. 

Baadhi ya wananchi wa Kibaha akiwemo Aidan Mndewa na Kisaken ,walibainisha, kutokana na kudai fedha zao kutokana na kutopatiwa viwanja wala nyumba wanaiomba serikali ifuatilie kampuni hiyo na kuwasaidia kurejeshewa fedha zao. 

Wakati huo huo, msimamizi wa VIGUTA Chamwino huko Dodoma, Hilda Kadunda, ambae pia ni diwani viti maalum alisema wananchi walioingia katika mpango huo Dodoma wanadai milioni 300 na Chamwino wanadaiwa milioni 61 ambapo wapo watu waliouziwa viwanja mara mbili mbili. 

"Ninasimamia Chamwino pia kuna wakati nilikuwa katika mkoa wa Dodoma, mkurugenzi Christina na Mwenyekiti Salmin Dauda wao ndio watia saini lakini tukidaiwa wakipigiwa simu wanazima ama kudai hawapo wanashughulikia masuala mengine "

Kamanda wa polisi mkoani Pwani, ACP Wankyo Nyigesa alipoulizwa juu ya tuhuma hizo kama wahusika akiwemo Mkurugenzi wa VIGUTA Christina Rwebangila na mwenye kampuni hiyo Salmin Dauda kama hatua zozote zimeshachukuliwa kufuatia malalamiko hayo, amedai hajapata taarifa hizo. 

Wankyo alielezea, atafuatilia kwa watendaji wake ili kujua kama wamepata taarifa hizo ili waweze kufanya uchunguzi na kuchukua hatua .
Baadhi ya picha zikionyesha nyumba za sampo zilizokuwa zikidaiwa kujengewa wananchi kwa gharama nafuu
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live




Latest Images